Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 257

Edna hakutaka kumuachia kabisa Lanlan kuondoka na kwa Lanlan ilikuwa hivyo hivyo , hakupenda kuachiana na Edna na kurudi Bagamoyo na ilibidi Edna amshawishi Qiang mlezi wa Lanlan kukubali kubaki kwa siku kadhaa nyumbani kwake mpaka pale babu yake na Lanlan atakaporiudi.

Qiang licha ya mwanzo kumhofia Edna lakini aligudua Edna ni mtu mzuri hivyo ilibidi akubali.

“Mama , Lanlan anapenda bahari na anapenda na Wanyama”Aliongea Lanlan wakitoka kwenye mgahawa huu wa Best Bite na Edna alikuwa amemshikilia mkono 1anlan na walionekana mama na mwana kwa ukamili kabisa.

“Lanlan unataka nikupeleke ukaone bahari?”Aliuliza Edna na Lanlan alitingisha kichwa kuashiria ndio anataka kuona.

“Okey Lanlan bahari ipo upande wa pili nitakupeleka ukaone bahari”Aliongea Edna na Lanlan aliruka ruka kwa furaha mno.

“Lanlan anampenda sana mama yake”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kufurahi pia na walikuwa washasahau kama kuna watu wapo nyuma yao.

Roma na Qiang walikuwa wakiwaangalia na Roma haikueleweka alikuwa akiwaza nini , lakini kwa jinsi mke wake alivyoonekana kwenye macho yake alijiambia Edna atakuwa mama mzuri kama siku moja atakuja kupata mtoto wake.

Ukweli Roma licha ya kwamba Edna amefurahishwa na uwepo wa Lanlan lakini kwa upande wake ilikuwa tofuati ,kwake hakuwa sana mpenzi wa kucheza na Watoto , hususani wale ambao hakuwafahamu , lakini kwa upande wa Lanlan kuna kitu ambacho sio cha kawaida alikuwa akihisi kila anapomwangalia , lakini jambo lingine ni kwamba Lanlan hakuwa mtoto wa kawaida , kwani alikuwa na nguvu za ziada kwenye mwili wake.

“Roma nampeleka Lanlan kuona bahari , endesha kuelekea Coco”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuachama kwa kuchoka na Edna alimwangalia.

“Kama umechoka unaweza kurudi nyumbani nitaendesha mimi mwenyewe”Aliongea na Roma alifikiria kidogo.

“Okey wife wewe utaendesha mimi naenda nyumbani kupumzika”Aliongea Roma na kisha akampatia Edna ufunguo na yeye alianza kutembea kusonga mbele kuelekea nyumbani kwani hapakuwa mbali.

“Roma mbona uko mwenyewe wakati umetoka hapa ukiwa na Edna?”Aliuliza Blandina aliekuwa amekaa nje kwenye bustani akiangalia maji ya Swimming pool na Roma alisogea mpaka alipokaa mama yake na kuketi kivivu huku akivuta hewa nzuri iliokuwa ikipuliza pua zake.

Nyumba ya Edna haikuwa mbali na Baharini , ni kama nyumba ileile ya kule Kigamboni utofauti wa nyumba hii na ya kile ni kwamba eneo la Baharini linaonekana kwa ukubwa Zaidi kama utakaa juu ya ghorofa kwenye balconi.

“Kapata mtoto na kampeleka kuona maji ya baharini , nimechoka nimerudi kupumzika”Aliongea Roma.

Ukweli Roma sio kama alikuwa amechoka ila alikuwa akitaka atulie kidogo muda uende aende nyumbani kwa Nasra, kwani juzi yake aliachana nae akiwa mwenye hasira hivyo aliamini kwenda kumpeti peti mrembo huyo anaweza kushusha hasira zake n ahata kumtunuku kitumbua.

“Mtoto gani tena kampata?”

“Alisema wiki iliopita mlikutana na mtoto kwenye kituo cha kulelea Yatima , ndio huyo ambaye tumekutana nae eneo la Mwenge na wanaonekana kuzoeana sana kiasi kwamba anamuona kama mtoto wake , hivyo kamchukua na kumpeleka ufukweni”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kukumbuka.

“Ndio nakumbuka , kuna huyu mtoto alifanya mpaka akazimia”Roma alijikuta akishangaa baada ya kusikia neno kuzimia , hakuwa na taarifa ya Edna kuzimia.

“Unamaanisha nini kuzimia” Blandina alivuta pumzi na kisha akaanza kumuelezea tukio lilivyokuwa na Roma alijikuta akishangaa lakini pia hata kwake yeye alishindwa kujua sababu iliompelekea kuzimia ni nini , lakini pia akili yake ilianza kukumbuka jumapili ya wiki iliopita Edna alirudi nyumbani akiwa na mabadiliko makubwa kimwili.

“Mh! nini kimempata?”

“Hata mimi nilishindwa kuelewa na nilishangaa baada ya kushituka jina la kwanza kuuliza ni la huyo Lanlan , Roma jitahidini mpate mtoto na Edna, sipendi hivi nyie ni wanandoa na kulala vyumba tofauti”Aliongea Blandina.

“Mama hilo lisikuumize kichwa , Edna akiamua mwenyewe juu ya hilo mimi sina shida , kwasasa sitaku kumlazimisha kutokana na namna tulivyokutana”Aliongea Roma na kisha alinyanyuka kwa ajili ya kuelekea ndani , lakini muda huo huo geti la jumba lao lilifunguliwa na gari aina ya V8 ilionekana ikiingia na Roma baada ya kuangalia vizuri aligundua mmoja ya mwanamke aliekuwa ndani ya gari hilo, wa kwanza alikuwa ni Jestina na mwingine alikuwa ni mwanamke ambaye hakumfahamu vizuri , lakini mwanamke huyo alikuwa ni mdogo wake Raisi Senga afahamikae kwa jina la maarufu la Mama Theresia.

“Roma”Aliita Jestina huku akimsogelea Roma kwa furaha na kumsalimia.

“Roma huyu ni Shangazi yako anafahamika kwa jina maarufu la Mama Theresia”Aliongea Jesgtina na kumfanya Roma kutabasamu na kisha kumsailimia mwanamke ambaye ametambulishwa kwake kama Shangazi.

“Namkumbuka siku ambayo nilikuja kuonana na wewe ndani ya Landmark Hotel nilimuona akiwa nyuma yetu”Aliongea Roma na kumfanya Jestina kushangaa na kisha kucheka.

“Kwahio ulimuona?”

“Ndio nilimuona na nilifahamu siku ile alikuwa na wewe kwa namna yoyote ile kwani alikuwa akituangalia sana”

“Ni kweli , nisamehe mama yako , Roma unaweza usiamini ila mimi nilikufahamu tokea siku ya kwanza unafika ndani ya familia yetu kwenye ile sherehe nadhani unakumbuka hata baba alitaka kuongea na wewe ni kwasababu ulikuwa ukifanana kabisa na baba yako wakati akiwa katika ujana wake”Aliongea Jestina na Roma alitabasamu na kuona kumbe mama huyo kipindi kile alikuwa kwenye misheni yake , ila aliona sio jambo la kuzingaria sana.

“Mama Theresia!”Aliita Blandina na kusogeleana na Mama Theresia na kukumbatiana , ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuonana tokea Blandina arudi kutoka Kenya, walionekana kukumbukana sana na Roma aliona hilo na hakuona haja ya kuendelea kusimama , kwani alitembea na kuingia ndani na alikutana moja kwa moja na Sophia.

“Broo..!!”Aliita Sophia na kumshika mkono Roma na kupandisha nae juu na kumpekea kwenye sebule ya juu upande wa Balconi.

“Kuna nini Sophia mbona una mchecheto hivyo?”Aliuliza Roma na kumfanya Sophia kupumua.

“Siri yetu imefichuka”Aliongea Sophia na kumfanya Roma kushangaa hakumuelewa Sophia alikuwa akimaanisha nini.

“Siri gani hio sijakuelewa”

“Nimetoka kuongea na mama hapa , anasema aliongea na Sister Edna muda tu juu ya mimi kukaa nyumbani kwake”Aliongea Sophia na kumfanya sasa Roma kuelewa anachomaanisha ni nini.

“Kwahio unamaanisha Edna alikuwa akifahamu wewe sio mdogo wangu kama tulivyomdanganya?”

“Ndio na mama kasema Sister Edna anajua kila kitu na inaonekana aliamua kukaa kimya”Aliongea Sophia huku akionekana kuwa na hatia na kwa upande wa Roma licha ya kwamba swala hilo halikuwa likimsumbua sana , ila hakujua kwanini Edna alikaa kimya baada ya kugundua kama walimdanganya.

“Nilikuambiaga mimi , Mke wangu ana akili nyingi na ni ngumu sana kumdanganya”

“Acha kumsifia mbele yangu ,mama ndio kaharibu , yaani anapenda kuingilia mipango yangu sana”Aliongea huku akionekana kumlaani mama yake.

“Wewe nae una mipango gani?”

“Hupswi kujua nina mipango gani , hapa nawaza namna ya kumuomba msahamaha Sister Edna , sijawa muaminifu kwake toka mwanzo huenda ananichukia ndani kwa ndani”Aliongea Sophia

“Mimi sidhani Edna yuko hivyo naamini aliamua kukaa kimya kwasababu anakuchukulia kama mdogo wake na ndio maana hajaonyesha utofauti wowote , ila inapaswa kuongea nae”Aliongea Roma na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea kweney chumba chake kwa ajili ya kupumzika.

“Kwahio mimi ndio ninaepaswa kuongea nae peke yangu na hili halikuhusu?”Aliuliza Sophia.

“Hehe… kwani nani alilazmisha kuishi na mimi, wewe na baba yako ndio mlinifanya nikadanganya, hivyo Edna akinikasirikia nitamwambia tu ukweli kama unataka kuwa mke wangu wa pili simple”Aliongea Rsoma huku akitabasamu kifedhuli.

“Roma…!!!”Aliita kwa hasira Sophia huku akikunja ngumu , lakini Roma hakumjali na kupotea kwenye macho yake.

*********

Edna alionekana kufurahi kweli , yaani moyo wake ulikuwa mweupee na alijihisi dunia yote alikuwa akiimiliki , licha ya kwamba ni masaa machache sana ambayo aliweza kuonana na Lanlan lakini kwake ni kama miaka mingi.

Lanlan vilevile alionekana kufurahia uwepo Wa Edna alimuona Edna kama mama yake kamili na hakuona kabisa utofauti wa aina yoyote ile na ndio maana alijiachia atakavyo na kuomba kununuliwa anachotaka.

Takribani masaa mawili yote Edna , Qiang na Lanlan walikuwa wakifurahia upepo wa baharini .

Lanlan alikuwa akiogelea kiasi kwamba ilimfanya Edna kuwa na wasiwasi kumruhusu Lanlan kuingia kwenye maji , lakini Qiang alimtoa wasiwasi Edna na kumwambia Lanlan anaweza akaingia kwenye maji chini kabisa na kuzuia pumzi kwa takribani dakika nne.

“Unadanganya”Aliongea Edna huku akimwangalia Qiang.

“Ni kweli Miss , Lanlan sio mtoto wa kawaida na kadri unavyoishi nae ndio utagundua kuwa anaweza kufanya mambo mengi ambayo watu wa kawaida hawawezi kufanya , ndio maana hata Master hajawahi kufikiria kumpekea Shule kutokana na uwezo wake”Aliongea Qiang na kumfanya Edna kushangaa.

“Unataka kuniambia kuwa Lanlan hajawahi kusoma popote hata chekechea ,mbona anaonekana akili yake kukomaa tofauti na umri wake?”

“Ndio maana nakuambia Lanlan ana mambo mengi ya kukushangaza Miss Edna”Aliongea Qiang lakini muda huo huo Lanlan alitoka kwenye maji na kuwakimbilia.

“Mama , Aunt Qiang , Grandpaa amerudi”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kushangaa.

“U?nasema kweli Lanlan?”

“Ndio Grandpaa karudi , yule kule…”Kabla hajamaliza Sentesi yake alitoka nduki akiwa na kijichupi tu na kufanya watu wamshangae na Edna aligeuka na kumwambia asikimbie lakini Qiang alimzuia.

“Ni master”Aliongea Qiang na kumfanya Edna kushangaa na moyo wake kuuma maana alijua ujio wa babu wa Lanlan ndio kumkosa hivyo Lanlan, aliangalia upande wa kushoto kwake na kweli Lanlan alimkubaria kwa kumrukia mwanaume mmoja mweupe asiemfahamu ambaye alikuwa ni mchina.

“Yule ndio babu yake Lanlan?”Aliuliza Edna na Qiang alitingisha kichwa nayeye kuanza kukimbia kwa kutabasamu kuelekea upande wa kushoto alipo Lanlan na babu yake.















SEHEMU YA 258

“Linda unamaanisha nini kwamba ulikuwa ni mpango wako?”Aliuliza Raisi Senga kwani hata yeye alikuwa akimjua Linda na tena sio kumjua tu kama msaidizi wa karibu na mtu wa kuaminika kwa Senior , lakini pia alikuwa akimfahamu Linda kama mchepuko wa raisi Jeremy.

Mheshimiwa Jeremy alikuwa haamini kama ni kweli Linda alikuwa akijua mpango LADO muda wote na kumkalia kimya, alitaka kusikiliza kila kitu ndio aamini kwani aliona Linda ni kama alikuwa akimtania.

Linda alivuta pumzi na kisha alitembea na kwenda moja kwa moja kukaa kwenye huku akimwangalia Jeremy kwa huruma.

“Jeremy najua naweza usinisamehe kwa kile nilichokifanya lakini naomba usikie kila kitu na baada ya hapo nitakuwa tayari kupokea adhabu ya aina yoyote ile”Aliongea mwanamama Linda kwa huzuni na kumfanya hata Raisi Jeremy kushindwa kuongea.

“Linda tunakusikiliza unaweza kuongea kila kitu”Aliongea Raisi Senga na Linda alivuta kumbukumbu kurudi nyuma.

“Kabla ya yote mnatakiwa kutambua kwamba mimi ni CIA undercover Ajent”Aliongea Linda na kumfanya Jeremy mwili wake kukaa kitako pasipo ya akili yake kuelewa.

“Linda niambie unadanganya?”Aliongea Jeremy lakini Linda hakumjali , Zaidi ya kuingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake na kutoa Flash Disk na kumkabidhi mheshimiwa Senga.

“Hii inanithibishia utambulisho wangu kama CIA , ni nyaraka kamili pia zinazotambulisha uraia wangu wa taifa la Marekani”Aliongea na Rasie Senga haraka haraka alisogelea Tablet na kuunganisha Flash ile.

“Password ni nini?”Aliuliza Mheshimiwa Raisi Senga baada ya kugundua Flash Disk inanywira.

“Oprah Fraklin”Aliongea Linda.

“Hili ndio jina lako halisi naamini , CIA hawajawah kutumia majina yao halisi”Aliongea Raisi Senga na kufungua faili moja lililokuwa kwa mfumo wa kama Software yaani ni faili ambalo baada ya kuligusa ni kama limeliwa na virusi kwani lilionyesha vijiboksi vidogo vidogo.

“This File is Corrupted Linda”Aliongea Senga na Linda alimpa ishara ya kumpatia hio Tablet na Senga alimkabidhi na jambo ambalo liliwashangaza ni kwamba Linda alianza kuandika kwa haraka haraka kwa kutumia ile Tablet na kila maneno ambayo anaandika vile vijiboksi vilianza kujikusanya kwa muundo falani hivi kama vile mchoro na ndani ya dakika tu vile vijiboksi vilitegeneza picha ‘ Logo’ ya shirika la kijasusi la CIA na chini kukaonekana ‘Form’ yaani hapa nikimaanisha fomu ya kilectroinics ambayo inamuhitaji Linda kuingiza jina lake halisi la kuzaliwa nalo , mwaka aliojiunga na CIA , pamoja na nywira ili kufungua akaunti yake.

“Kwa sheria za ma ajenti wote wa CIA tunapokuwa kazini hatubebi vitambilisho vinavyotuunganisha moja kwa moja na taifa la Marekani , bali tunabeba Flash Disk maalumu ambayo ukichomekwa na kifaa chochote huonekana kama Flash disk hio ina virusi ndani yake”Aliongea Linda na Senga aliitikia na kuona Yes hapa yupo na CIA mweyenyewe sio wa mchongo.

Linda aliingiza jina lake la Oprah Franklin na kisha palepale karatasi kama mfano wa vyeti unavyopewa shuleni au ukihitimu ilionekana kwenye Tablet na Linda alimpatia Raisi Jeremy.

“Huo ndio utambulisho wangu wa uraia wa Marekani , lakini pia nikionekana kama raia ninaelitumikia taifa langu nje na nyumbani”Aliongea Linda na Jeremy alipitia faili hilo na kisha hakuongea chchote na kumpatia Senga ambaye baada ya kusoma maelezo hayo aliamini maneno ya Linda na kuona ni kweli wapo na jasusi wa siri kutoka Idara ya CIA kutoka taifa la Marekani.

Ukute hata Kabwe anaweza kuwa CIA na ananichora tu, Damn it lazima niende kwenye ibada ya mpasuko wa mwezi, kwa namna hiikuna majasusi wa CIA wa ngapi ndani ya hili taifa”Aliwaza Raisi Senga mwenyewe huku akimuangalia raisi Jeremy.

“Mhmh ! Hehe Senior anaonekana na yeye kupitishwa ubatizo wa moto, huenda hisia alizokuwa nazo ni kama nilizopitia nilivyofahamu Blandina na Denisi wapo hai , namuonea huruma”Aliendelea kuwaza huku akimwangalia Rafiki yake.

“Jeremy nakumbuka mara ya mwisho ulivyogundua uwezo wangu usio wa kawaida uliniuliza niliupatia wapi na nikakujibu ni kutoka kwa kundi la Yamaguchi , ni kweli kabla ya kuja Rwanda nilikuwa chini ya taasisi ya kininja ya Yamaguchi na ndiko nilipopatia mbini na nguvu zangu za ziada za kimapigano ambazo mtu wa kawaida hawezi kuwa nazo”

“Yamaguchi , sijawahi kusikia hio taasisi”Aliongea Senga.

“Ndio huwezi kuifahamu kwani ni taasisi za siri sana”

“Linda tafadhari ongea kila kitu nielewe wewe ni nani na kazi yako ya kuwa ndani ya ikulu ya Rwanda ni ipi , weka kila kitu wazi kwani baada ya hapa utakuwa mfu labda unipe sababu ya kutofanya hivyo , nachukia sana usaliti kwenye Maisha yangu”Aliongea Jeremy kwa hasira.

“Niliingizwa ikulu ya Rwanda kwa maagizo ya The Doni mara baada ya kumaliza mafunzo yangu ya kininja kutoka Yamaguchi na kazi yangu kubwa ni kukulinda mpaka pale nitakapopewa maagizo mengine, kabla ya kufanya mafunzo na kundi la Yamaguchi nilikuwa ni CIA Agent., hata kuingizwa ndani ya kundi hilo ni maagizo maalumu niliopewa na taifa langu la Marekani”

“Linda nadhani kwanza unielezee hili kundi la Yamaguchi kazi yake ni nini haswa na kwanini wanafundisha watu kuwa maninja , hebu elezea kila kitu kwanza”Aliongea Raisi Senga kwa mchecheto , alihitaji kujua kila kitu.

Kwa maelezo ya Linda ni kwamba Yamaguchi ni taasisi ya siri kutoka China ambayo inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na serikali mbili yaani China na Japani, taasisi hii kazi yake kubwa ni kufundisha vijana wa kuanzia miaka kumi na moja mafunzo ya hali ya juu ya Uninja huku dhumuni kubwa ni kuua ndio wanachofundishwa.

Anaendelea kusema kwamba Yamaguchi baada ya kuwafundisha wanafunzi wake huko msituni na kufuzu mafunzo yote kuanzia ya kimapigano mpaka ya kichawi , maninja hao hufudishwa sheria maalumu ambazo zinawaongoza kufanya kazi zao baada ya kutoka mafunzoni na kuchangamana na watu wa kawaida na moja ya sheria hizo ni kutokutambuana na mwanafunzi mwingine wala kuwasiliana, Linda anasema kwamba baada ya wanafunzi kuhitimu mafunzo ya kimapigano moja kwa moja wanapangiwa majukumu(Target) kwa ajili ya kufanyia kazi, hivyo hata yeye baada ya kumaliza mafunzo alipangiwa Target yake ambayo ni Ikulu ya Rwanda.

“Kwahio wewe kazi yako uliopewa na Yamaguchi ni kumlinda Mheshimiwa Jeremy?”

“Hio ndio kazi yangu na sio kwa Jeremy tu , kama itatokea raisi mwingine akachaguliwa ndani ya Rwanda basi target yangu itabadilika”

“Hapo Yamaguchi walikuwa wakifahamu kama wew ni CIA?”

“Hawakua wakifahamu hilo kwani sikujitambulisha kwao kama CIA na pia niliingizwa kwenye mafunzo hayo kwa makusudi maalumu”

“Makusudi gani?”

“Misheni yangu ilikuwa ni kuingia kwenye kundi hilo na kutoa taarifa zote ya kile kinachoendelea na nilifanya hivyo na hata baada ya kumaliza mafunzo niliendelea kuwa chini ya Yamaguchi licha ya kutopokea maelekezo mengine kutoka CIA”Aliongea Linda.

“Sasa ilikuwaje ukahusika kwenye mpango LADO au Serikali ya Marekani walikuagiza kufanya hivyo”

“Serikali ya Marekani hawajawahi kunitafuta tokea nimalize mafunzo ndani ya Yamaguch na kuja hapa Rwanda kwasababu wanajua mpaka sasa hivi nimekufa”Aliongea Linda na kuwafanya waheshimiwa kuzidi kuchanganyikiwa Zaidi.

“Unamaanisha nini?” Aliuliza Jeremy na Linda alianza kushikwa na huzuni na kisha akanyamza na kuvuta kumbukumbu.

Kwa maelezo ya linda alisema kwamba baada ya kutoka kwenye kundi la Yamaguchi na kupangiwa tageti yake , serikali ya marekani ilitoa oda maalumu ya Linda kuuwawa mara moja , mpaka muda huo mwenyewe anashindwa kuelewa kwanini alikuwa akiwindwa na Serikali yake ilihali alikuwa amepewa misheni na aliifanya vizuri , ila alisema wakati akiwa katika harakati za kuingia Ikulu ya Rwanda ndipo alipoweza kupata taarifa iliokuwa ikihusu yeye kuuliwa kwa oda kutoka makao makuu.(Termination order)

“Nani alitoa hio oda ya wewe kuuliwa na kwanini na nani alikuletea taarifa hio”

“Mtu alieniambia hio taarifa simfahamu , ila ninachokumbuka ni kwamba nilikuwa kwenye nyumba yangu hapa Rwanda asubuhi na kwenye meza kulikuwa na karatasi iliokuwa ikithibitsha kwamba nawindwa na CIA , mwanzoni sikuamini karatasi hio na nilitumia marafiki zangu makao makuu kuthibitsha Ushahidi uliokuwa kwenye mikono yangu na walinithibitishia ni kweli na nikawauliza kwanini nawinda na serikali yangu ilihali nilikuwa kwenye misheni , ila hakukuwa na majibu maalumu na Rafiki yangu ndani ya CIA aliniambia nisije nikampigia tena na nijifiche kwa namna yoyote”

Ukweli raisi Senga bado alionekana kutokumuelewa kabisa Linda , kwanza mwanamke huyu alisema kwamba aliingia kwenye kundi la Yamaguachi akiwa kama CIA akiwa kwenye misheni maalumu huku akichukua mafunzo ya uninja ili kujifanyisha na yeye ni mwanfunzi na baada ya kumaliza mafunzo akapangiwa taget yake , sasa raisi Senga ambacho hajaelewa ni kwanini CIA hao hao ambao wamempa misheni kutoa oda ya kifo chake ilihali Linda bado alikuwa na umuhimu kwao, pili pia Linda anaeleza kwamba alijikuta akiwa nyumbani kwake asubuhi na alipoamka alikuta karatasi iliokuwa ikithibitisha oda ya kuuwawa kwake na mtu ambaye kamletea karatasi hio hakuwa akimfahamu, bado maelezo yake yalikuwa na maswali mengi.

Kwa upande wa Raisi Jeremy licha ya kwamba alikuwa na hasira na Linda lakini pia alikuwa akimuogoopa , alikuwa akijua uwezo wa kimapigano aliokuwa nao Linda , lakini pia uwezo wake wa kupotea kimazingara pia alikuwa akiufahamu na alijiambia kama Linda angekuwa mtu wa kawaida basi angemhoji akiwa chini ya chumba cha mateso kama ilivyokuwa kawaida yake na kwa muda huo alishiandwa hata kuuliza maswali kwani alikuwa kwenye hasira nyingi sana na ndio maana aliacha Rafiki yake Senga amuulize Linda maswali yote.

“Linda unayosayesma haya yote ni ya kweli au kuna jambo unatudanganya,?”

“Nimeamua leo kuweka ukweli wote wazi hivyo sina nia ya kuficha chochote, nitaeleza kile ninachofahamu kwa upande wangu”Aliongea Linda.

“Ilikuwaje ukahusika kwenye mpango LADO , tueleze hapo tuelewa kwanini nyaraka za mpango LADO zina sahihi yangu ya .senior na ya Rahel? Na kuonyesha kama sisi ndio wahusika wa mpango huo?”





SEHEMU YA 259

1997

Ni mwezi wa kumi na moja ndani ya ofisi ya mkuu wa majeshi , Jenerali Cammillius Kweka anaonekana Linda alievalia suti ya rangi nyeusi akiwa aneo la Mapokezi akiwa ameshikilia mkoba wake.

Linda alionekana kuwa na wasiwasi kweli licha ya kwamba yupo eneo ambalo lina ulinzi mkubwa sana nchini kutokana na maamuzi yote ya kijeshi kufanyikia hapo , lakini pia sehemu ambayo wafanyakazii wake wote ni wanajeshi.

Linda akiwa eneo la Mapokezi kwa takribani dakika kama kumi na tano hivi , huku akikagua kila mwanajeshi aliekuwa akiingia kwa wale waliokuwa na gwanda na wale ambao hawakuvaa gwanda , alifuatwa na mwanajeshi wa cheo cha Kapteni mwanaume mrefu mweusi wa umri mkubwa kuliko wake.

“Dada unaweza kunifuata , Jenerali ameridhia kuonana na wewe”Aliongea yule mwanajeshi na kumfanya Linda kutabasamu.

“Asante sana kaka kwa kunipelekea ombi langu”Aliongea Linda akiweka tabasamu na yule mwanajeshi alitabasamu pia na kupokea shukrani na kisha alianza kutembea kumpeleka Linda kwenye ofisi ya Afande Camllius Kweka.

“Nafikiri nimefanya maamuzi sahihi ya kuja ofisini kwake kuongelea hili swala”Aliwaza Linda huku akitembea kwa hali ya kujiamini.

Ukweli ni kwamba Linda kabla ya kuja hapa Tanzania kufanya maongezi na mkuu wa majeshi ya Tanzania , jana yake asubuhi kuna tukio ambalo lilimtokea na kumchanganya sana.

Jana yake mrembo huyu baada ya kurudi kutoka Ikulu ya Rwanda sehemu ambako anafanyia kazi kama katibu muhtasi wa raisi Jeremy , alivua nguo zake na kuzitundika vizuri kwenye kabati kama ilivyokuwa kawaida yake.

Linda ni moja ya wanawake ambao hawakuwa na mambo mengi na hii yote ni kutokana na mafunzo aliokuwa nayo ya kimapigano , alikuwa ni mwanamke ambaye hata mavazi yake karibia yote ni suti tupu na aina ya mavazi mengine ni kama tracksuit ambazo mara nyingi hutumia kuchukulia mazoezi ya kukimbia na pale anapokwenda Gym na ndio maana kwa mwaka huo wa tisini na saba katika moja ya nyumba za serikali alipokuwa akiishi , nyumba yake haikuwa na vitu vingi , kulikuwa na makochi ya mbao upande wa sebuleri na meza katikati ya mbao pia pamoja na Tv ya chogo , kwa upande wa chumbani kwake hakukuwa na vitu vingi Zaidi ya kabati la mbao analotumia kuhifadhia nguo na baadhi ya vitu vyake vya thamani.

Sasa siku ambayo mrembo huyu anaamka asubuhi nyumba yake ilikuwa sio ya kawaida kama alivyozoea , kwanza kabisa kwenye mwili wake kulikuwa na mabadiliko , katika paja lake kuna alama ambayo hata yeye mwenyewe hakujua alama hio imetoka wapi na alipoona hio alama ya tatoo ni kama vile yupo kwenye ndoto na atashituka na kuona alama hio kupotea , lakini hakukuwa na mabadiliko kwani mpaka inatimia saa mbili asubihi alama hio ipo , alijaribu kuifuta lakini haikuwezekana., alishangaa na kuogopa kwa wakati mmoja na kujiuliza alama hio imefikaje kwenye mwili wake , kwani jana alilala akiwa hana alama na hata kama kuna mtu aliingia nyumbani kwake na kumuwekea hio alama angetambua, kwani yeye alikuwa ni mwanajeshi na wanajeshi usingizi wao ni wa machale , lakini ajabu alilala fofofo na cha kushagnaza Zaidi anaamka asubuhi na kukuta ana alama kwenye mwili wake , alama ambayo haifutiki lakini pia hakujua inahusiana na nini.

Linda akiwa katika mawazo alitembea mpaka eneo la sebuleni huku akijihisi kuwa na uwoga wa ajabu kwa swala ambalo limemtokea na alikimbilia sebulni kwa ajili ya kuangalia usalama na ile anafika eneo la makochi ndipo alipoona bahasha ya khaki iliokuwa mezani na kumfanya kushangaa na kuanza kukagua nyumba nzima kuthibitisha usalama , lakini ajabu ni kwamba nyumba yake haikuonesha hali yoyote ya mtu kuingia kabisa kwani kama alivyofugna milango kabla ya kulala usiku wa jana , ndivyo alivyokuta asubuhi.

“So strange, what is happening , am I hallucinating”Aliongea mwenyewe huku akisogelea bahasha iliopo kwenye meza na kuiangalia juu yake.

“From X to Oprah Franklin”

Hayo ndio maneno yliosomeka juu ya bahasha hio na kumchangnya mno Linda , kwanza jina ambalo lipo juu ya Bahasha ni jina ambalo hajawahi kulitumia tokea afike nchini Rwanda na alishangaa imekuwaje fomu ikawekwa nyumbani kwake na ikawa na jina lake la utotoni , jina ambalo lipo kwenye database ya serikali ya Marekani tu , alishangaa na kujiuliza maswali na kutetemeka mikono kwa wakati mmoja.

“Itakuwa ni CIA hawa lazima tu, lakini hapana vipi kuhusu tatoo kwenye paja langu na yenyewe ni kutoka kwa CIA?”Aliwaza Linda huku akigeuza geuza bahasha ambayo ipo kwenye mikono yake.

Usalama wote upo vizuri , hakuna sehemu inayoashiria mtu kuingia ndani lakini naamka asubuhi nikiwa na alama kwenye paja langu la mguu wa kushoto na sasa nimeshikilia bahasha ambayo sijui ndani yake kuna kitu gani , mtu aliefanya haya yote ni nani , je ni kundi la Yamaguchi, lakini hapana Yamaguchi hawafahamu jina langu halisi , sio wao naamini kuna mtu mwingine anaenifahamu”Aliwaza Linda lakini alijikuta akiwaza ujinga kwani aliamini huenda majibu yote yapo kwenye bahasha alioshikilia kwenye mikono yake.

Linda alikaaa chini harakaharaka na kuanza kufungua ile bahasha kwa kuchana na kisha akatoa karatasi nne zilizopo ndani yake na kuzishika mkononi na kuanza kusoma , lakini ajabu ni kwamba juu ya karatasi ya kwanza kuna alama ambayo ni kama iliokuwa kwenye paja lake la mguu.

“Nimeingia nyumbani kwako pasipo kuacha alama yoyote ya namna nilivyoingia , lakini pia nimeweza kukuchora tatoo kwenye paja lako la kushoto na nikaacha nyaraka ambayo unazisoma , Amini kwamba mimi sio mtu wakawaida na naweza kukufanya jambo lolote kwa muda ninaotaka” ndio sentensi ya kwanza iliokuwa juu ya nyaraka ya kwanza , moyo ulipiga kite na kuogopa Zaidi.

“Unatakiwa kutimiza kila maelekezo nilioandika kwenye nyaraka nilizoacha kama unataka kunifahamu , kwasasa utanitambua kwa jina la X na alama kwenye paja lako ni ya utambulisho kwamba wewe ni mwanachama”Sentensi ya pili kwenye Nyaraka na kumfanya Linda kuzidi kuchanganyikiwa.

Mwanachama , X , Tatoo alijiuliza vyote kwa pamoja na Linda kwa papara Zaidi alifungua ukurasa wa pili na alijikuta akishangaa kwani aliona picha ya mtu anaemjua.

Raheli mpenzi wa siri wa Raisi Jeremy ndio picha alioshikilia na kumfanya kushangaa Zaidi lakini alichana na picha hio na kuhamia nyaraka ya ta tu na hii ilikuwa ni nyaraka ya maandishi ambayo ina malekezo.

Malekezo no 1: “Mtafute Cammilius Kweka kutoka Tanzania kipengele namba mbili ndio anaepaswa kukisoma na kukuambia cha kufanya.”

Malekezo No 2: “Kweka huyo ni mshirika wako zidi ya Mpango LADO na nyaraka hii inamtambulisha”

Maelekezo no 3: “Kiongozi yoyote lazima asaini aidha kwa kukubali au kulazimishwa ili kuidhinisha mpango LADO na mzazi mmoja wa mhusika katika mpangon asaini ili kulinda mpango husika”

Linda alisoma vipengele vyote viwili na kujikuta akishangaa Zaidi lakini aliachana na nnyaraka ya tatu na kufungua nyaraka ya nne ambayo ilikuwa ikijitegemea na Linda baada ya kuisoma jasho lilianza kumtoka.

“Termination Order , Ajenti Flower Rain”Alisoma Linda maelezo hayo na kuangalia sahihi na muhuli na alichoka kwani Ajent Flower rain ni jina la kodi ndani ya CIA.

“Director Powel From CIA” ndio sahihi ambayo Linda asingeshindwa kuitambua na alijiuliza kwanini CIA wanamtaka kufa ni kipi ambacho amekosea ni kweli yupo Rwanda pasipo kutoa taarifa kwa wakubwa wake , lakini hakuweza kufanya hivyo kwasababu wao wenyewe ndio wa kwanza kumtafuta kwa njia wanazozijua wao, lakini Linda bado alikuwa kwenye maswali na mshangao , alijiuliza kama kweli CIA wametoa oda yake ya kufa inakuwaje mpaka sasa hivi yupo hai kwani alikuwa akifahamu uwezo wa shirika la CIA wakitoa oda jihesabie tayari ni mfu.

Linda kwa hasira akaanza kukung`uta ile bahasha kuhakikisha karatasi zote zimetoka na matarajio yake yalikuwa kweli kwani kulidondoka kikaratasi cha njano mfano wa kimemo.

“You are already dead when you go along with plan , you will be alive and hunted when you refuse to go along with plan, this notes only for you , I am X till second phase of plan”

“Wewe ni mfu tayari kama utaenda na mpango , utakuwa unaishi na kuwindwa kama utakataa kwenda na mpango , hiko kijimemo ni kwa ajili yako , mimi ni X mpaka hatua ya pili ya mpango” kijimemo aliweza kukisoma hivyo na kujikuta akishangaa Zaidi lakini ghafla Linda yupo Tanzania ndani ya makao makuu ya Jeshi la Tanzania akikubali kila kitu kilichoachwa nyumbani kwake na kuamini ni ukweli.

Kwanza anaanza vipi kuona sio kweli , yeye ni ninja wa hatari kutoka kwenye kundi la Yamaguchi lakini mtu anakuja nyumbani kwake na kumchora tatoo kwenye paja na kuacha maelezo pasipo yeye kutambua, aliamini huyo m mtu ni wa hatari sana na hivyo dakika ambayo atafanya kinyume basi ndio dakika ambayo kifo chake kitamkuta.

“No I am Dead , I will go along with plan”Aliwaza Linda wakati akifika mbele ya ofisi ya mkuu wa majeshi , jenerali Cammilius Kweka na mlango ukafunguliwa na akaingia ndani ya ofisi yanye ubaridi wa kiyoyozi wa hali ya juu , ofisi ambayo mkuu wa majeshi hufanyia maamuzi.

“Karibu Binti, nimesikia unataka kuonana na mimi na unatokea Ikulu ya Rwanda karibu sana”Sauti nzito ilimkaribisha Linda na Linda alitabasamu.

*********

Senga alijikuta akishangaa na kukosa cha kusema , kwahio mpango wote ule wa mwanae Denisi kupanda ndege , lakini pia Lorraine mtoto wa Jeremhy na Raheli ulisukwa na Senga pamoja na Linda, alijikuta akikaa chini na kuanza kuona baba yake ni mtu hatari sana na asipokufa mapema anaweza kuleta shida zaidi kwa taifa.

“Kwahio huyo mtu aliekuja nyumbani kwako na kukuchora alama kwenye paja ndio aliekupa maelekezo ya kufanya kila kitu”

“Ndio nilifanya kila kitu kwa maelekezo yake”

“Vipi kuhusu sahihi yangu , lakini pia mhuli wa raisi iliwezekana vipi maana sikumbuki kutia Saini wala kugonga muhuli karatasi ya mpango Zero”

“Ulifanya kila kitu kwa maelekezo yangu ninao uwezo huo na sio kwako tu hata kwa Raheli alitia sahihi pasipo ya kujitambua na kwako Senga hivyo hivyo , mbinu hio ni sehemu ya mafunzo kutoka kwa kundi la Yamaguchi, I have ability to hypnotize anyone and do things according to my wishes”

“Kwahio Linda mpango na ushauri ulionipa wa kumpeleka Lorraine kwenda China kupitia Malaysia ulikuwa ni mpango wako na Afande Kweka , lakini kwa maneno marahisi ni kwamba wewe ndio uliemuua mwanangu , ulimchukua mwanangu kutoka kwangu mtoto ambaye alikuwa ni kama zawadi kutoka kwa Rahel?” Aliongea Jeremy huku akianza kupandwa na jazba mdogo mdogo.

“Jeremy najua unahasira sana , lakini kumbuka kama isingekuwa mimi usingweza hata kufahamu kama una mtoto duniani , Raheli hakuwa na mpango wa kukuambia ila mimi nilikuambia kwa mapenzi yangu mwenyewe”

“Stupid woman!, you told me in order for your evil plan to work , umenifanya nimshawishi Rahel kuniachia mtoto mmoja kati ya mapacha ili iwe rahisi kwako”

“Hapana Jeremy huo haukua mpango wetu na nzee Kweka kwa mara ya kwanza , the plan was very simple na kama sio mimi usingesikia kabisa kuhusu Edna wala Lorraine, Jeremy tatizo lako uliamini Rahel anakupenda san ana hapo ndipo ulipokosea”

“How so, unataka kuniambia Rahel hanipendi?”Aliuliza kwa hasira mno kiasi cha misuli ya uso kusimama.

********

“Wewe ni miss Edna , mwanamke Tajiri ndani ya taifa hili?”Aliuliza Babu yake Lanlan.

“Ndio ni mimi” Alijibu Edna na hii ni baada ya kusalimiana na Babu yake Lanlan na Edna kushangazwa na babu hiyo kuwa wa umri mdogo.

“Nakiri kwamba unafanana kwa asilimia mia moja na mama yake Lanlan , lakini hio haikufanyi kuwa mama yake”

“Grandpa..”Aliingilia Lanlan kama vile alikuwa akielewa kinachoongelewa ila kwa upande wa Edna alijisikia vibaya ,mzee huyo alionyesha kuwa na maneno ya kuumiza lakini yanayoeleweka.

“Qiang mchukue mtoto na mnisubiri pale mbele”Aliongea kwa Kingereza na mlezi wa Lanlan alimchukua Lanlan.

“Hapana Lanlam anataka kuwa na mama yake”

“Lanlan nisikilize mimi babu yako huyu sio mama yako na nitakutafutia mama yako mwingine”Aliongea yule mzee na kumpa ishara Qiang kuondoka na Lanlan , lakini Lanlan alianza kulia na kumfanya Edna kukasirika .

“Huna haja ya kukasirika kwani huna haki yoyote ya kufanya hivyo”Aliongea yule mchina kwa maneno ya kejeli na Edna alijikuta akikasirika na kuumia lakini hakutaka kuonyesha aliona avumilie yapite kwa ajili ya Lanlan.

“Maneno yangu yanaweza kuonekana ya kejeli lakini huo ndio ukweli”

“Naomba uende moja kwa moja kwa ulichotaka kuongea”Aliongea Edna.

“Unaonekana kumpenda Lanlan sana na Lanlan pia anakupenda na tokea akuone amekuwa msumbufu na nikiri ni kweli Lanlan mama yake mpaka sasa hivi kashafariki hivyo hana mama, unaonaje kama utamlea kama utatimiza masharti yangu”Aliongea yule mzee na kumfanya Edna moyo wake kulipukwa na furaha.

“Kumlea , nipo tayari kumlea niambie masharti yako”Aliongea Edna pasipo hata ya kufikiria ukweli licha ya kwamba alikuwa akimpenda Lanlan lakini wazo la kumlea bado hakuwa nalo.

“Sidhani kama utayaweza masharti”Aliongea yule mwanaume na kutmbasamu kwa kejeli.

“Niambie ni masharti gani hayo unayoamini siyawezi?”

“Okey Miss Edna ukweli ni kwamba sharti ni moja tu na ukilitimiza unaweza kuondoka na Lanlan, kwanza mtoto wenyewe msumbufu kwangu na nina kazi nyingi kiasi cha kunifanya niondoke bila taarifa hivyo sifai kuwa mlezi wake”Alipumua na kisha akamwangalia Edna.

“Achana na mumeo kwa talaka na baada ya hapo nitakuruhusu umchukue Lanlan”

“Nini..!!”

“Ndio usishangae kama utaweza kuchanana Roma , basi Lanlan kuanzia leo atakuita mama , maamuzi unatakiwa kuyafanya sasa hivi , Je upo tayari kuachana na mume wako umchukue Lanlan au upo tayari kuendelea na mume wako umkose Lanlan? , kwa upande wa Lanlan naamini anaweza kuniacha mimi babu yake nilieteseka nae na kukuchagua wewe”Aliuliza yule mzee kwa Kingereza na kumfanya Edna kutoa macho , kwenye Maisha yake hajawahi kukutana na Dillema ya aina hio.

“Mama Lanlan anapenda kuishi na mama yake, usiniache tena”Aliongea LAnlana na kuanza kulia kilicho cha kwikwi huku akishika miguu ya Edna na Edna alimwangalia Lanlan na kuanza kutokwa na machozis.

“Miss Edna fanya maamuzi , Sharti ni dogo sana”Aliongea yule mwaume mchina na kuonyesha kejeli za waziwazi.

Unafikiri Edna atamuacha Roma na kumchukua Lanlan , nini kitendelea itaendelea kesho.


HAPPY WIKIEND KUTOKA KWA MWANDISHI SINGANO JR , NAMBA YANGU NI WATSAPP NI 0687151346 , USISITE KUNICHEKI UNAPOHITAJI MWENDELEZO

Great story
 
SEHEMU YA 76

Roma na Bi Wema wote walishangazwa na kuhuzunishwa na taariFa hio iliowafikia asubuhi hio,Edna alijikuta akijongea mpaka kwenye sofa na kukaa, hakuwa akitoa machozi lakini alionekana kuwa kwenye uchungu wa kumpoteza mzazi wake.

Ndio Edna na Baba yake hawakuwahi kuwa na ule ukaribu wa utoto na Ubaba na hii yote nikutokana na siri ambayo Edna hakuwa akiijua uu ya baba yake,Mzee Adebayo hakuwahi hata kumshika mkono Edna tokea anazaliwa mpaka kuwa mkubwa.

Na maisha ya Edna na Mzee Adebayo , yalikuwa ni ya kugombana ,kila siku jambo ambalo lilimfanya Edna asimpende kabisa baba yake , hata pale Edna alivyomshuhudia Roma kumdhuru baba yake hakuona hatia hata kidogo , kwake aliona anastahili , na tokea siku ile Edna hakuwahi kusikia habari yoyote kutoka kwa baba yake na pia hakujali kujua , hayo ndio maisha ya Edna na Mzee Adebayo , lakini licha ya hivyo Edna bado alimchukulia Mzee Adebayo kama baba yake mzazi na hakumpuuza.

“Kipi kimesababisha kifo chake?”Aliuliza Roma.

“Nadhani hamkuwa na taarifa , ila siku chache zilizopita mzee alipatwa na ukichaa wakati akiendelea na matibabu ndani ya hospitali ya Aghakani , na haikueleweka ilikuwa vipi , ila leo asubuhi tulimkuta akiwa amefariki pembeni ya jengo la hospitalini , na kwa uchunguzi uliofanyika inaonesha alijirusha gorofani”Aliongea Rasi.

“Mwili wake kwa sasa upo wapi?”

“Bado upo Hospitalini umehifadhiwa”Aliongea Rasi na kila kitu Edna alikisikia kwani Roma ndie aliekuwa akiuliza.

“Rasi wasiliana na Babu kuhusu taarifa za msiba, atakupa utaratibu”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae , hakuwa na taarifa ya uwepo wa Babu kwenye maisha ya Edna ndio maana alikuwa akishangaa ,lakini Roma hakujilaumu kwa kutokujua , kwani tokea aingie ndani ya familia ya Edna hakuwahi kumuuliza kuhusu baadhi ya ndugu zake.

“Sawa Madam”Aliongea Rasi na kisha akageuka na kutoka nje , kwani lililokuwa limemleta hapo ndani , lilikuwa limekwisha kufanyika.

“Edna sijawahi kusikia ukimtaja babu yako” Aliongea Roma akikaa kwenye masofa na Bi Wema alimuangalia Roma na kuona ngoja amjibu yeye.

“Mzee Adebayo baba yake yupo hai na ni Jenerali wa jeshi mstaafu, haujasikia kuhusu taarifa zake kutokana na kwamba MissEdna na babu yake hawajawahi kupatana kama ilivyokuwa kwa baba yake”

“Kunasababu gani ya Edna kutopatana na Babu yake?”Aliuliza Roma na Bi Wema akamwangalia Edna aliejinamia chini.

Kwa maelezo ya Bi Wema , Mzee Athumani ambaye ndie babu Yake Edna , alimtelekeza Mariam (jina la bibi yake Edna) wakati akiwa na ujauzito wa Adebayo , na hii ilimfanya bibi yake Edna kumchukia Mzee Athumani kwa kitendo cha kumtelekeza akiwa mjamzito na kwenda kuoa mke mwingine.

Bibi yake Edna licha ya Adebayo kuwa mtoto wa Athumani hakutaka kumuingiza kwenye familia ya Athumani na alichokifanya miaka hio ni kumuita jina la Jedi Adebayo na kwanzia hapo familia yao ikafahamika kama ya Adebayo.

Hivyo ni rahisi kusema kwamba Edna asingempenda mtu ambaye bibi yake alikuwa akimchukia , Edna na Bibi yake walikuwa wakipatana sana Enzi hizo za uhai wake na hii ilichangia pakubwa kwa Edna kumchukia Mzee Athumani.

Licha ya kwamba mzee huyu baada ya kustaafu katika jeshi , alijitahidi kuweka ukaribu na Edna ili amtambue kama babu yake , ila Edna hakutaka kabisa mazoea nae na aliweka mstari kabisa wa ukomo kati yake na Babu yake kindugu.

Mzee Adebayo baada ya kuona mama yake hampendi Mzee Athumani baba yake mzazi na pia kitendo cha kutomrithisha kampuni kama mtoto wake, aliweka ukaribu na Mzee Athumani kama kisasi cha kumkasirisha mama yake , na hii ndio ilioongeza ukaribu baina yao, hivyo ni rahisi kusema kwamba Adebayo anatambulika ndani ya familia ya Athumani na msiba ulikuwa ukiwahusu kwa asilimia kubwa.

Wakati Bi Wema akiendelea kumuelezea historia hio ya kuchanganya Roma, simu ya Edna ilianza kuita na jina lilisomeka ‘Mzee Athunani’, aliangalia simu yake na kisha akapokea kinyonge.

“Edna pole sana , nimepata sasa hivi taarifa ya kifo cha mwanangu Adebayo na nimeona utakuwa kwenye uchungu mkubwa kumppoteza baba yako na ndio maana nimeona nikupigie simu kukupa pole , na pia kukuambia tuko pamoja na Ramadhani atahakikisha taratibu zote za msiba zinafanyika”Aliongea Mzee huyu.

“Sawa nashukuru”Aliongea Edna na kisha kukata simu , alionekana hakutaka mazungumzo mengi.

“Anasemaje?”Aliuliza Bi Wema.

“Balozi Ramadhani atasimamia taratibu za msiba”alijibu Edna na kuendelea kumshangaza Romana kumwangalia Bi Wema.

“Ni yule ambaye aliomba muongee kwenye kusanyiko , ni balozi nchini Japani”Aliongea Edna kinyonge na kumfanya Roma ashangae Zaidi.

“Inamaana Edna na Sophia ni ndugu , sasa kwanini Balozi anataka nimuoe Sophia ilihali anajua Edna na Sophia ni ndugu”Aliwaza Roma hhuku akishindwa kuelewa kwa wakati mmoja , ila Roma aliona hayo ayaweke kiporo kwanza aangalie swala muhimu kwa wakati huo.

Edna na Roma walitoka kwa pamoja kwenye Gari moja kuelekea hospiali ya Aghakani, Edna alitaka kuona mwili wa baba yake kabla haujapelekwa nyumbani kwa ajili ya taratibu zingine za kuupumzisha.

“Za saa hizi ndugu?”Roma aliekuwa eneo la nje kwenye hospitali hii ya Aghakani alifuatwa na bwana mmoja hivi mhindi , ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kidaktari, wakati huu Edna alikuwa akiongea na baadhi ya wasaidizi wa Mzee Adebayo na Roma aliwapa nafasi ya wao kuongea.

“Salama”

“Niwape pole za msiba , numekuona ukiingia hapa na Miss Edna na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba wewe ni mume wake , nimeona nikufuate kwani kuna jambo ambalo nataka tuongee”Aliongea Dokta na kumfanya Roma ashangae.

“Lina husiana na nini Labda?”

“Ni swala nyeti kidogo na ndio maana nilivyokuana uko peke yako nikakusogelea , ni juu ya Mzee Adebayo”Aliongea.

“Okey , nimekuelewa , tunaongea wapi , hapa au ofisini”

“Ofisini itakuwa vyema Zaidi”aliongea Daktari huyu na kisha akageuza kuelekea ofisini kwake huku Roma akifuatia.

“Dokta nieleze , swala ambalo umesema ni nyeti?”Aliongea Roma mara baada ya kuketi na Dokta alivuta faili moja kwenye shelf na kulifungua na kisha akatoa karatasi na kumpatia Roma.

Roma alijikuta akishangazwa na taarifa hio iliokuwa kwenye karatasi hio.

“Hii taarifa ni sahihi?”

“Ndio Mister , ni taarifa sahihi kabisa”

“Kwanini unanionesha hii taarifa?”Aliuliza Roma.

“Nadhani mpaka hapo ushaelewa taarifa hio kama ikijulikana italeta madhara gani kwa Mkeo”

“Ndio maana nikakuuliza kwanini umenionesha hii taarifa , unataka nini , ongea acha kuzunguka zunguka?”Aliongea Roma huku akianza kukosa utulivu na hasira kuanza kuonekana na huyu dokta wala hakutishwa na kupaniki kwa Roma alitabasamu.

“Napanga kuitunza hio taarifa na ibakie kuwa siri yangu mimi kama daktari ambaye nilikuwa nikimtibia Mzee Adebayo kwa kipindi chote , hivyo ili taarifa hii iwe siri nataka cha kuniziba mdomo”Aliongea akimaanisha kwamba anataka kiasi cha pesa ili kutoivujisha taarifa hio , Roma alijikuta akikasirika sana na swala hili , alichukia sana watu wa aina hio katika maisha yake, wanaotumia udhaitu wa wengine kwa ajili ya faida.

“Okey nishakuelewa unataka kitu cha kuziba mdomo, niambie ni kiasi gani unataka?”

“Bilioni moja na nusu tu itanitosha”Aliongea Mhindi huyu kwa kujiamini , alijua ni kiasi kidogo sana kwa Roma kutoa ukilinganisha na utajiri ambao Mke wake alikuwa akimiliki , lakini pia aliona Taarifa hio ni kubwa sana na ingeweza kuleta madhara makubwa kwa Edna kama jamii ingeifahamu.

Ilikuwa ni kitendo cha haraka sana alichofanya Roma , kwani tayari alikuwa amemshika Shingo daktari huyu wa kihindi na kumning`iniza hewani kwa mkono mmoja.

“Nachukia watu wa aina kama yako na siku zote nimekuwa wakutoa adhabu ya kifo kwa watu kama wewe,maana hamna mchango wowote kwa dunia”Aliongea Roma huku macho yake yakianza kubadilika Rangi na kuwa ya kijani na kumfanya Dokta azidi kutapatapa , alikuwa akinyongwa na mkono mmoja , na alijitahidi kujitoa kwenye mikono ya Roma lakini alishindwa kabisa kujitoa kwake ,na kifo alikiona kile kinakuja.

Roma alionekna leo hakudhamiria kuua , maana baada ya kuridhika na kumkaba dokta huyu mhindi alimtupa chini kama furhushi , na kisha akachukua ile karatasi na kuichanachana.

“Siku ukifungua mdomo wako na ukatoa hii taarifa , nitatekeleza kifo chako kwa Staili ambayo hata shetani mwenyewe atashangaa”

Aliongea Roma huku akiwa ameshika Kidevu cha Dokta huyu ambaye alikuwa akihema kwa shida kwenye Sakafu , na Roma hakuridhika , baada ya kumpiga biti Dokta Mhindi, alimpiga kibao cha uso kwa namna ya kumziba , na Dokta aliona nyota nyota , kwenye maisha yake hakuwahi kuwaza kukutana na aina hio ya mtu, harufu ya mkojo ilianza kusambaa ndani ya hiki chumba.

“Umenielewa?”Aliuliza Roma huku akimwangalia dokta huyu ambaye Pua zake zilikuwa zikitoa Damu mfululizo , na bwana huyu kinyonge alitingisha kichwa kuashiria ameelewa.

Muda huohuo ambao Roma alikuwa akimpiga Biti Dokta mpaka kupelekea mkojo ,mlango ulifunguliwa na Edna aliingia na kushangazwa na hali iliokuwa hapo ndani , aliinua macho yake kwa Roma na kuwaza ni jambo gani Roma anafanya.

“Edna umejuaje nipo humu?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Edna ambaye macho yake yalikuwa kwa Dokta Mhindi aliekuwa akitokwa na damu.

“Ni nini kunaendelea Roma ,Mbona dokta yupo hivyo?”

“Kuna jambo nilikuwa namuelekeza mke wangu , usiulize mengi ni maswala ya kawaida tu ,kama ushamaliza tuondoke”Aliongea Roma kwa sauti ya siriasi na kumfanya Edna amwangalie Roma machoni na alimuona macho yake yapo kawaida , alijua kuna jambo ambalo linaendelea hapa ndani ,lakini alishindwa kuuliza.

Roma alimsukumia Edna nje na alirudi ndani kwa spidi na kisha akamsogolea Dokta mhindi na kumpiga teke la tumbo na kumfanya Dokta huyu ajikunje kwa maumivu makali huku machozi yakimtoka.

“Onyo mara moja ukirudia ni kifo ,Ole Wako”

“Romaa..!!”Aliita Edna aliefungua mlango kwa mara nyingine akijiuliza ni nini tena Roma anafanya.
ITAENDELEA JUMAPILI MCHANA
UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 100 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
Leo hapa
 
Mkuu singanojr usitufanyie hivyo story yako ndefu sana unatuacha na arosto mpaka tumeahaanza kula methadone hamna ya story inapungua Kaka [emoji23][emoji23][emoji23]
 
SEHEMU YA 260

Edna alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu na kushindwa kujua ni maamuzi gani anapaswa kufanya , alijiona kaingia kikamilifu kwenye mtego wa mwanaume aliekuwa mbele yake.

Kwa upande wa mzee wa kichina ambaye ni babu yake Lanlan alionekana kumwangalia Edna kwa Kejeli, aliona kabisa mwanamke huyo hatokuwa na uwezo kabisa wa kumchukua Lanlan na kumucha Rom.

Mlezi pia wa Lanlan , Qiang hakujua ni maamuzi gani ambayo Edna atachukua na yeye macho yote yalikuwa kwa Edna.

Edna alichuchumaa na kisha akatoa nguo za Edna kwenye mkoba wake na kumvalisha.

“Lanlan Mama hawezi kukuacha tena, na usilie tena sawa?”Aliongea Edna na Lanlan alitabasamu baada ya kusikia maneno ya Faraja kutoka kwa mama yake.

“Lanlan anampenda sana mama yake”Alionea Lanlan na kumkumbatia Edna na Edna alijikuta akiguswa sana na maneno ya Lanlan.

“Kwahio ndio umeamua nini Miss Edna , muda unaenda?”Aliuliza yule mzee wakichina na kumwangalia Edna usoni.

“Hili swala limekuwa la ghafla sana kwangu, Lanlan nimefahamiana nae kwa siku chache lakini nahisi kabisa nina muunganiko nae ambaye siwezi kuelezea na inaniuma kumkosa hata kwa dakika”

“Huna haja ya kuelezea Zaidi , mpaka hapo nimeelewa kwamba unampenda sana mumeo kuliko Lanlan”Aliongea Yule mchina na kisha alimsogelea Lanlan.

“Lanlan twende nyumbani nimekuletea zawaidi ambayo utaipenda”Aliongea huku akimuweka begani Lanlna.

“Lakini Grandpa Lanlan anataka kukaa na mama yake , siwezi kuondoka”Aliongea huku akianza kulia akimwangalia mama yake.

“Lanlan niangalie usoni?”Aliongea yule mzee na Lanlan alitii na kumwangalia usoni babu yake , na haikueleweka mzee yule amemfanya nini lakini Lanlan alipitiwa na usingizi dakika ileile na kulaza kichwa chake kwenye kifua cha babu yake.

“Miss Edna nisamehe sana kama nimeongea maneno ya kukuuzi , usiwe na wasiwasi kabisa na Lanlan nitamtafutia mama yake ambaye yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yake”Aliongea na kisha akainamisha kichwa chake kwa namna ya heshima mbele ya Edna na kisha akampa ishara Qiang aondoke.

“Subiri..”Aliongea Edna huku akishikwa na huzuni lakini mzee yule hakuangalia nyuma na aliondoka na dakika nne mbele hawakuonekana tena kwenye macho yake.

“Hey mrembo huna haja ya kuwa huzuni, nina mbegu nzuri sana kama utanikubalia ninaweza kukupatia ujauzito na ukazaa mtoto kama yule”Ilisikika sauti ya mwanaume nyuma ya Edna na kumfanya ageuke.

“Kwa hadhi gani uliokuwa nayo ,potea kwenye macho yangu”

“Hehe.. acha kujifanyisha wewe Malaya , umepokonywa mtoto hapa na nikikuangalia tu unaonekna kuwa kahaba ndio maana , acha maringo na twende nikakupe mambo”Aliongea yule mwanaume jamii ya mhindi mchanganyiko na mwafrika akiwa kifua wazi na bukta ilioloa maji na alionekana alikuwa akiogelea.

“Paah!!!”Kilikuwa ni kibao cha nguvu kilichotoka kwa Edna Kwenda kwa yule mwanaume.

“Nishakuambia ondoka kabla sijakufanya kitu kibaya”Alionea Edna huku akiwa na hasira mno , alikuwa akiumia kwa kumkosa Lanlan lakini hakuwa tayari kuvumilia kejeli kutoa kwa mwanaume aliekuwa mbele yake.

Bwana yule baada ya kuona kapigwa kibao , alionekana kukasirika mno na palepale alimpiga Edna bonge la kibao na kumfanya kudondokea kwenye maji ya baharini.

“Haaaa……!!!”Watu waliokaribu walishangazwa

“Oya braza unachofanya sio sahihi acha uzalilishaji”Aliongea mwanaume mmoja akitaka kumzuia yule mhindi kwa kutaka kumshika , lakini aliambulia teke lililompiga tumboni na kusinyaa na yule mhindi baada ya kuona amemuadhibu mwanaume kiherehere alimsogelea Edna alieloa kwenye maji huku damu zikimtoka puani na kumshika kwa ajili ya kumpiga ngumi nyingine lakini mkono uliishia hewani na kukuta sura ambayo haifamu.

“Crack!!!”

Kilikuwa kitendo cha fasta sana kilichofanyika na yule mwanaume palepale jina lake lilibadilika kutoka kuwa mtu hai na kuwa hayati.

“Khaa… jamani … uwiiii … kaua”Ilisikika sauti ya mwanamke na kufanya hata watu ambao hawakuwa wakifahamu tukio la udhalilishaji kusogea sehemu ya tukio.

“Edna…!!!”Aliita Roma na kumsogelea Edna ambaye alikuwa kwenye maji na kumbeba juu kwa juu kama mtoto.

“Mamaaaa….!!!!” Kundi lote lililokuwa limekusanyika lilitawanyika.

“Kuna nini?”

“Jini … jini …”Aliongea moja ya mwanaume aliekuwa akihema baada ya kusimama mita kadhaa kutoka kwenye tukio.

Ukweli kilichowafanya kutawanyika ni baada ya Roma kupotea ndani ya eneo lile ,ndio maana watu walichanganyikiwa mno na kuamini Roma alikuwa ni jini, watanzania wengi maswali kama hayo ya kupotea walikuwa wakiyashuhudia kwenye filamu , kama vile filamu ya Shumileta sasa kupotea kwa Roma kuliwafanya waamini ni jini.

******

TURUDI NYUMA KIDOGO

Roma alipumzika chumbani kwake kwa taribani lisaa limoja na nusu ndipo aliposhituka kutoka usingizini na kitu cha kwanza alichoshika ilikuwa ni simu yake, aliangalia saa na kuona amelala kwa lisaa na nusu.

Aliamka kivivu na kuingia bafuni na kuoga huku akiwa na mpango wa Kwenda nyumbani kwa Nasra mapema , hakutaka kulala huko huko kwani pia alikuwa na mpango wa Kwenda kwa Mrembo Rose kwani ni muda kidogo alikuwa hajawasiliana nae , lakini pia alikuwa akienda kumueleza juu ya swala la uwekezaji kwenye kammpuni yake mpya , hivyo akili yake ilikuwa na mipango miwili , mpango wa kwanza ni Kwenda kwa Nasra na kuweka mambo sawa na mpango wa pili ni Kwenda Mbagala Maji matitu kwa ajili ya kuonana na Rose.

Alitumia dakika kumi na tano tu kumaliza mpaka kuvaa na alitoka na ufunguo wa gari yake na kushuka chini sebuleni kwa ajili ya kuaga kama anatoka.

“Mama natoka kidogo”Aliongea Roma.

“Unarudi saa ngapi, tulijua unabaki ili tupate chakula cha Pamoja na Shangazi yako?”Aliongea Blandina na Roma alifikiria kidogo.

“Kama unaondoka inabidi kwanza umsubirie Edna ndio umuage uondoke”Aliingilia Blandina , hakutaka kumzuia kuondoka , ila alitaka kumzoesha Roma kumuaga Edna kila anapotoka , aliamini hio ndio mbinu ambayo inaweza kupunguza umbali uliokuwa kati yao , aliamini kama Roma ataaga na Edna kumruhusu basi itapunguza makasiriko ya Edna kwani atakuwa amemruhusu mwenyewe.

“Ngoja nimpigie simu”Aliongea Roma huku akitoa simu yake.

“Yaani Roma unatumia simu ya aina hio mpaka sasa hivi , kwanini usinunue mpya?”Aliuliza Jestina na Roma alitabasamu.

“Ni salama Zaidi kutumia simu za aina hii kuliko hizo kubwa”Aliongea Roma na kuweka simu sikioni na simu ilianza kuita takribani kwa dakika moja na haikupokelewa, alipiga kwa mara ya pili na haikupokelewa tena.

“Sh***T”Aliongea Roma chini chini na kutoka nje.

Roma alikumbuka asubuhi wakati akitoka na Edna aliwapa ishara Chiara na John ya kupumzika kwa siku hio kwanni atakuwa na mke wake , sasa ndio Roma alikumbuka na kujiona amefanya makosa kumuacha Edna na Lanlan kuwa peke yao pasipo kuwa na ulinzi

Roma baada ya kuona simu sasa haipokelewi alijawa na wasiwasi na hakuwa na mpango wa kutmia kabisa gari kwani Fukwe ya Coco haikuwa mbali , alitumia mbinu ya kuteleport.

Baada ya kufika Coco alijikuta akipandwa na Jazba baada ya kuona Edna akidhalilishwa na mwanaume kwa kupigwa kibao ambacho kilimdumbukiza kwenye maji ,na ilikuwa bahati yake kwani kama angechelewa Edna angepigwa ngumi takatifu ya uso.

“Mtu kama huyu ni kifo tu haina haja ya kumueleza kosa lake “Aliwaza Roma na palepale alimvunja shingo mwanaume wa kihindi ambaye hakutaka hata kumfahamu ni nani.

*****

Roma aliibukia kwenye gari ya Roll Royce ambayo Edna alikuja nayo hapo ufukweni na alimlaza kwenye siti Edna ambaye alikuwa amelala pasipo ya kuwa na fahamu , huku damu zikiwa zimegandiana kwenye pua zake , lakini pia nguo zake kuloana na maji ya baharini.

Roma baada ya kumuweka vizuri aliinua viganja vyake vya mkono kwa sentimita kadhaa Kwenda juu akimlenga Edna tumboni kwa dakika kama mbili hivi na palepale nguo za Edna zilianza kukauka kwa Spidi ya ajabu sana , huku pia damu ambayo ilikuwa imeganda kwenye pua zake ikipotea, ndani ya dakika tano Edna alirudi kwenye hali yake ya kwaida na alimwamsha.

“Wife pole sana”Aliongea Roma baada ya Edna kunyanyuka na kuketi kwenye kiti huku akijishangaa, kwani dakika kadhaa nyuma alikuwa baharini , akiwa amezungukwa na watu , lakini pia akishuhudia kitendo cha Roma kumuua mtu mbele yake , alikumbuka kila kitu na alishangazwa pia kuona nguo zake zimekauka na pia hakuwa akitoka damu tena.

Alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa na Roma alimwangalia mke wake huku akijiuliza Edna anawaza nini.

“Kulikuwa na haja ya kumuua?”Aliuliza Edna kwa sauti ndogo yenye unyonge na kujutia.

“Wife kama unakumbuka maneno yangu ya asubuhi vizuri basi nilichokifanya ndio sheria yangu , mtu kama yule ambaye alitaka kukudhalilisha adhabu kwake ni kifo hakuna namna”Aliongea Roma na kisha alitoa ufunguo kwenye mkoba wa Edna na kuwasha gari kurudi nyumbani.

“Yule mtoto Lanlan yuko wapi?”Aliuliza Roma na kumfanya akili ya Edna ianze kufikiria upya.

“ Babu yake kamchukua”Aliongea Edna kinyonge na kumfanya Roma kushangaa.

*****

Upande wa barabarani muda huohuo inaonekana gari aina ya Toyota Camry rangi nyeusi ikiwa imeegeshwa mita kadhaa kutoka kwenye moja ya jumba la kifahari ndani ya eneo la Osterbay huku mziki kwa mbaali ukisikika kutoka kwenye gari hio.

Dakika chache mbele alionekana kijana alievalia suruali ya Track , akija kwa kuhema kusogelea gari hio huku mkononi akiwa ameshikilia Camera kampuni ya Sony.

“Mbona unahema hivyo?”Ilisikika sauti ya kiume kutoka kwenye gari baada ya kioo kushushwa.

“Boss misheni imefeli”Aliongea yule mwanaume na mlango ulifunguliwa na kijana akaingia ndani.

“Unamaanisha nini misheni imefeli?”

“Salah is dead”

“What!…Salaah is what “

“ I mean dead , ameuliwa na mwanaume jini”Aliongea yule kijana na kumfanya mwanaume aliekuwa kwenye gari kukosa utulivu.

“Elezea vizuri nikuelewe , unanichanganya wewe mpumbavu”Kijana alielezea kilichotokea na kumfanya boss wake kushangaa mno.

“Umechukua picha tukio zima?”

“Ndio boss , si ndio ilikuwa kazi yangu kwenye huu mpango , nimechukua pia video tena HD na Edna na muuaji wamenaswa vyema” Aliongea na kisha akashika Kamera yake kwa mikono miwili huku akionekana kwenye mchecheto na kuwasha.

“Mbona hunipi nikiona hizo video unahangaika tun a hio Kamera” Aliongea yule mwanaume na kumwangalia yule dogo akihangaika na kamera yake.

“Hakuna picha , boss , inawezekana vipi hii wakati nilisevu kila kitu”Aliongea huku akitafuta picha baada ya kamera yake kuwaka lakini hakukuwa na kitu na kumfanya kupagawa.

“Acha kuchachawa inaonekana yule mpuuzi alijua kabisa unachukua video”Aliongea yule mwanaume.

“Boss unamjua?”

“Acha maswali mengi maana hayakusaidii , chuku pesa hii hapa kama malipo na poteaa kwenye macho yangu”Aliongea yule mwanaume kwa hasira na dogo baada ya kuona boss wake kakasirika haraka haraka alichukua pes ana kushuka kwenye gari na kupotea.

“Hahaha… Roma umenirahisishia kazi , ungekuwa na akili usingemuua Salah , Edna nikiri ulikuwa na akili nyingi sana ya kuolewa na Shetani Roma , lakini awamu hii nitahakikisha unatoa machozi ya damu,nimezaliwa upya na sio Abubakari mpuuzi wa kupanga mipango na kufeli”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli , lakini muda uleule simu yake ilianza kuita na aliangalia jina na kuona ni Matilda.

Haikueleweka Abubakari karudi lini Tanzania, ila ashaanza kumchokoza Roma.





SHEMU YA 261.

Edna hakutaka kumueleza Roma juu ya sharti alilopewa na babu yake Lanlan kabisa , alijiambia itakuwa siri yake , licha ya kwamba swala hilo lilikuwa likimuuma sana lakini alijikaza mbele ya Roma.

Simu ya Roma ilianza kuita mfululizo baada ya kukaribia nyumbani na kuichukua huku akiendesha gari na mkono mmoja na baada ya kuangalia jina alijikuta akishangaa kwani jina lilikuwa la Magdalena.Alimwangalia Edna na kisha akapokea

“Roma usiniambie wewe ndio umemuua Salah?”Aliuliza Magalena kwa hasira.

“Salah ndio nani?”Aliuliza

“Niambie umeua au hujaua?”Aliongea Magdalena kwa sauti ya ukali.

“Ndio leo nimeua ila sijamuua Salah mimi unaemtaja”Aliongea Roma na kumfanya Edna aliekuwa ametulia kumwangalia Roma kwa wasiwasi.

“Umefanya nini Roma , kwanini unapenda kuua bila tahadhari unajua Salah ni nani wewe?”

“Magdalena usinipigie kelele , mimi nimemuua mtu alienikosea na kutaka kumdhalilisha mke wangu , Sijui kinachokufanya uogope ni nini lakini nimeshamwadhibu na alichostahili , na toa salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa”Aliongea Roma na kukata simu.

“Magdalena anasemaje, ni nani yule mwanaume”

“Sijajua na hata awe nani sijali, nilichofanya ni sahihi kwa mtazamo wangu”Aliongea Roma huku akiingiza gari getini na Kwenda kulisimamisha na giza lilikuwa lishaanza kutanda.

“Umeniweka kwenye nafasi mbaya , najua kuna watu waliokuwa wakirekodi kila kitu pale na picha zangu na zako zitasambaa mtandaoni”Aliongea Edna huku akianza kujawa na wasiwasi.

“Wife usijali mimi sio mjinga mpaka niruhusu watu kukurekodi , hakuna picha wala video kwenye kifaa chochote kimeweza kurekodi”Aliongea Roma na kisha akashuka kwenye gari.

“Unaenda wapi?”Aliuliza Edna baada ya kuona Roma anaingia kwenye gari yake nyingine.

“Ninaenda kumtembelea Nasra, nikitoka kwa Nasra nitaenda kwa Rose, Wife sitowahi kurudi leo”Aliongea Roma na hakusubiria hata jibu kutoka kwa Edna na aliwasha gari na kisha akashusha kioo.

“Wife nakupenda sana , najua una huzuni kwa Lanlan kuchukuliwa na babu yake, ila mimi mumeo nitajitahidi kuhakikisha unapata mtoto wa kwako, babe I love you and goodnight”Aliongea Roma na kisha akampa Edna busu la hewani na kutoa gari na Edna aliangalia mpaka inatoka nje ya geti na haikueleweka alikuwa akifikiria nini , ila alitoa mkoba wake kwenye gari na kisha kuanza kutembea kinyonge Kwenda ndani na akapokelewa na Blandina.

Blandina alimwangalia mke mwana na kujikuta moyo wake ukiwa kwenye majonzi , aliona mabadiliko aliokuwa nayo Edna.

“Edna umeonana na Roma?”Aliuliza Blandina na Edna aliitikia kwa kichwa na kisha alimsalimia Mama Theresa na Jestina na kisha alipiga hatua kuelekea juu kwenye chumba chake hku wote macho yakimwangalia Edna kwa chini alionekana kuwa mtu mwenye huzuni kwenye macho yao.

*******

Maongezi kati ya Pastor Cohen na Afande kweka yalisimama mara baada ya simu ya Afande kweka kuita na aliitoa kwenye mfuko wake wa koti na kumuomba msamaha Cohen kwa ajili ya kupokea simu hio.

Aliangalia jina juu ya kioo na lilisomeka Linda na Afande kweka alijikuta akishangaa kidogo na kisha akameza mate na kupokea.

“Za siku nyingi Afande” ilisikika sauti ya Linda kwenye simu.

“Salama Linda. Natumaini upo Tanzania?”

“Ndio Afande nipo hapa Tanzania na kabla sijarudi nchini Rwanda nataka muendelezo wa pale tulipoishia miaka ishirini iliopita, najua mpaka sasa una hasira na mimi kwa Kwenda nje ya mpango , lakini mpango ulifanikiwa licha ya njia tofauti, huna haja ya kunitenga ilihali mimi ni mshirika”Sauti ya Linda ilisikika na kumfanya afande Kweka avute pumzi.

“Unataka nini kutoka kwangu Lind?”

“Nahitaji kumjua X, lakini pia kuna kitu nilikuficha nahitaji pia kukueleza kabla sijarudi Rwanda”Aliongea na kumfanya Afande kweka kumwangalia Pastor Cohen.

“Linda kwasababu upo Tanzania litakuwa jambo la busara tuonane, naamini majibu yako yote ambayo nilishindwa kuyajibu miaka ile yanaweza kuwa na majibu sasa”Aliongea.

“Mheshimiwa kabla hatujaonana nataka kuweka kitu wazi”

“Ongea Linda”

“Mheshimiwa Jeremy amepata Ushahidi wa kila kitu juu ya ndege ya M Airline na awamu hii siwezi kabisa kuzuia swala hili lisiendelee na anapanga kuonana na vyombo vikubwa vya Habari kwa ajili ya swala hili kutangazwa na mheshimiwa kutoka Urusi ametoa ruhusa”Aliongea Linda na kumfanya Afande kweka kushangaa.

“Linda ngoja nakupigia muda huu”Aliongea Afande Kweka na kisha akakata simu.

“Kuna nini Komredi?”Aliuliza Cohen baada ya kufundua mabadiliko ya Afande kweka.

“Inaonekana Jeremy ashaanza kuchukua hatua juu ya kutangazia dunia kilichotokea mwaka 1998, hili litakuwa jambo la hatari kwa dunia na inaonekana Urusi wapo nyuma yake”Aliongea Afande Kwek ana kumfanya Pastor Cohen ashangazwe kidogo.

“Raisi wa Urusi mpango wake kwa sasa ni kuivamia Ukraine na nadhani anataka kutumia vyombo vya Habari kusambaza ukweli ili kutegeneza mtifuano kwa wanachama wote wa G20 ambao wanahusika na mpango LADO , huku akitumia mpango TASAC kwa mataifa ya Afrika kukaa kimya”Aliongea.

“Afande lakini mrusi ni mshirika wetu na pia kama taifa tumekuwa na ushirikiano mkubwa sana”Aliongea Afande na kumfanya Cohen kutabasamu.

“Kweka nakumbuka nilikupatia mpango LADO peke yake , lakini sikukupatia nyaraka ambayo inahusiana na Zeros Organisation?”Aliongea

“Zeros Organisation!? Ndio Komredi”

“Najua unaelewa kwamba mpango LADO ulikuwa chini ya Zeros organisation na taifa la Marekani peke yake?”

“Ndio nyaraka ilivyoeleza”

“Okey Kweka kuna mambo mengine huyafahamu mpaka sasa labda nikusaidie kuyatambua kabla hatujaachia majukumu yetu yote kwa Hades”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kujawa na shauku.

“Zeros organisation ni taasisi ya siri sana ambayo imeundwa na mataifa yenye nguvu duniani, yaani G20 , hii Habari ushawahi kuisikia?”Aliuliza.

“Hapana ni jambo jipya kwangu Komredi”

“ Ndio hivyo unatakiwa kuelewa , kwamba Zeros ipo chini ya mataifa 20 hivyo mpango LADO pia ulikuwa chini ya mataifa 20, nadhani unakumbuka nilivyokupatia nyaraka ya mpango LADO nilikuambia kuwa nilizipata kwa kupitia njia zangu za siri?”

“Ndio nakumbuka”

“Unakumbuka pia nilipokupa picha ya Rahel Adebayo sikukupatia maelezo mengine licha ya kukuambia mtoto wake atakaemzaa ahusishwe kwenye mpango LADO?”

“Ndio pia nakumbuka , ulisema utanipatia maelezo baada ya mpango kukamilika”

“Basi muda huu lazima nikupatie maelezo yote , kiufupi miaka ile kabla sijakuambia mpango LADO na kukupatia nyaraka, Denisi mjukuu wako alikuwa ndani ya mpango tayari na nilitumia tu ugonjwa wake wa saratani kukushawishi , lakini ukweli ni kwamba Denisi alizaliwa na mwili wa tofauti sana katika mfumo wake wa vinasaba vya damu , swala ambalo lilimfanya Hades wa zamani kutaka aingie kwenye mpango LADO, hivyo hivyo kwa mtoto wa Raheli aliekuwa tumboni”Aliongea na kumfanya Afande kweka kushangaa.

“Kwahio miaka ile Komredi Denisi aliingia kwenye mpango LADO si kwasababu ya mimi kutaka apone uongjwa wake bali ni kwasababu ya damu yake na kila kitu kilikuwa kimepangwa hivyo na Hades wa Zamani?”

“Nadhani sasa unanipata , sikutaka kukudanganya lakini Hades wa zamani alinipatia maagizo nisikueleze chochote na nitumie ugonjwa wa Denisi kukushawishi, lakini hata hivyo Hades aliamini kama Roma angeshinda kwenye mpango basi ugonwa wake ungepona lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakupona kabisa ugonjwa wake , lakini sayansi iliukubali mwili wake na aliendelea kuishi licha ya kuwa na saratani ya ubongo”

“Unamaanisha Roma hakupona Saratani ya Ubongo?”

“Kwa maelezo ya Hades wa zamani Roma hakupona Saratani ya ubongo ila sayansi iliowekwa kwenye mwili wake ndio iliomuwezesha kuishi na ugonjwa wa Saratani na naamini mpaka sasa bado ana ugonjwa wake , hatahivyo jambo ambalo ninataka kukueleza Zaidi ni hili la raisi Jeremy”Alivuta pumzi na kuendelea.

“Zile nyaraka za mpango LADO walizosaini pasipo ya uelewa wao si bado unazo?”

“Ndio ninazo na nilimuonyesha Senga na kumuonya asije akamwambia Jeremy kwa namna yoyote ile”

“Basi ni vizuri , kwanza kabisa kabla sijakuelezea kuhusu namna tunavyokwenda kushirikiana na Urusi, huyu Linda tumuache kwanza amueleze Jeremy kilichotokea ili kumfunga miguu asiendelee na mpango wake”

“Lakini hili swala lina mkono wa mrusi huoni kwamba hata kama yeye asipofanya Urusi itafanya kwani Ushahidi wote wanao?”

“Sio kweli Urusi wana Ushahidi ambao The First Black aliruhusu wawe nao , Urusi linaweza kuwa taifa kubwa lakini kwenye intellijensia hawako vizuri kama ilivyokwa CIA na hiki ndio kinamfanya raisi Nipitu ashinwe kutekeleza mipango yake, kabla sijakueleza mpigie simu Linda aongee na Jeremy amueleze kila kitu kilichotokea na baada ya hapo atajumuika na wengine kwenye kikao chetu”Aliongea na Afande Kweka alimpigia Linda na kumpa ruhusa ya kumueleza Raisi Jeremy.

“Sasa Kweka inabidi nikuelezee kwanini kwa sasa hatupaswi kumhofia mrusi bali tunatakiwa kumhofia huyu mwanamke Athena na mpango wake wa kufufua Roho zilizolala”Aliongea.

“Nakusikiliza Komredi”

“Okey ni hivi..”
 
SEHEMU YA 264

Aliekuwa mlangoni hakuwa mwingine bali ni Ashley mtoto wa raisi Senga na Edna alishangaa kumuona Ashley kwenye ofisi yake asubuhi hio.

“Edna..!!!”Aliita Ashley na Edna alitabasamu na kutoka kwenye kiti chake na kumsogelea Ashley na kumkaribisha kwa kumkumbatia.

“Karibu sana Ashley , umerudi lini?”

“Nina siku mbili Tanzania”Aliongea Ashley kwa furaha kabisa

“Boss mimi nitaondoka kama hakuna maagizo mengine”

“Naomba uendelee kufatilia kinachoendelea ndani ya kampuni ya MAYA”Aliongea na Suzzane aliitikia na kisha alitoka kwenye ofisi akimwacha Profesa Ashley mtoto wa raisi Senga akiongea na Edna.

“Edna nadhani sasa hivi nikuite wifi”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kushangaa.

“Kwanini jamani”

“Edna usijifanye na wewe hupo tayari kutupokea kama wanafamilia ,mimi na Roma ni kaka na dada hivyo wewe ni mume wake na inakufanya kuwa wifi yangu haha..”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kucheka na kuona aibu kwa wataki mmoja.

Ashley na Edna wanafahamiana sana na sio kwasababu Raisi Senga alikuwa na ukaribu na familia ya Adebayo , bali Ashley na Edna walisoma shule moja ya IST kwanzia darasa la kwanza mpaka la saba, hivyo ni rahisi kusema kwamba Ashley , Mage , Magdalena na Edna walisoma shule moja na walikuwa marafiki wote kipindi cha utoto wao na ni Ashley ndio aliekuwa akiwaburuza darasani wanafunzi wote na nafasi ya pili ilikuwa ikishikiliwa na Edna.

“Edna nilikuja nyumbani nikaambiwa umekuja kazini ndio nikaona nije moja kwa moja kukuona kwani sina muda mrefu nataka kurejea Uingereza”Aliongea

“Mh! wewe nae na Uingereza yako , hujawahi kuipenda Tanzania wewe tokea uende masomoni”

“Sio kweli Tanzania naipenda , lakini mazingira yake na taaluma yangu ni vitu viwili tofauti , Serikali za wenzetu zinawapa sapoti sana wanasayansi kuliko hapa Tanzania”Aliongea na Edna alimuunga mkono.

“Sasa ni kipi ambacho unataka kuongea na mimi?”Aliuliza Edna.

“Hehe… kabla ya yote nilitaka kumuona mke wa kaka yangu kabla ya kurudi uingereza”Aliongea na kumfanya Edna kujisikia vizuri, kila mwanamke alieolewa mawifi wakikupenda basi unajiona kuwa na bahati ,na hio ndio ilikuwa kwa Edna , kupendwa na wifi yake Ashley hakuliona jambo baya, alijishangaa pia mambo yao na Roma yalivyoanza , lakini kadiri siku zinavyoenda mahusiano yao yanachukua sura mpya kila siku.

“Edna nimekuja kukuambia siri yangu ila nataka uniahidi kama hutomwambia Roma”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa.

“Niambie siri yako itakuwa siri yangu”

“Hehe. Umenikumbusha wakati tukiwa Watoto ulizoea kusema hivyohivyo lakini mwisho wa siku siri zangu ulimwambia mama yako”Aliongea Ashley na kumfanya Edna akumbuke na kuona aibu.

“Ule ulikuwa utoto , saivi mimi mkubwa na hata hivyo mama ndio mtu niliekuwa nikimwambia siri zangu na sasa hivi hayupo tena”Alionge akinyongea kidogo.

“Usijali Edna, mimi wifi yako nakupenda sana, Edna mimi nilijua kuwa wewe ni wifi yangu tokea siku uliokuja Ikulu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Unataka kumaanisha nini Ashley?”

“Namaanisha kwamba nilimfahamu Roma kabla yako hio ndio siri yangu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa Zaidi.

“Unasema kweli?”

“Ndio namfahamu Roma huenda kuliko unavyomfahamu wewe , mimi Roma nilimfahamu ni kaka yangu kabla hata hajaja huku Tanzania”Edna alishangazwana jambo hilo mno.

“Hebu nielezee vizuri”Aliongea.

“Usijali nipo hapa kukuelezea kila kitu ninachokijua kuhusu Roma”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kujawa na shauku Zaidi, ijapokuwa alikuwa akitaka Roma ndio amwambie mwenyewe historia yake ya nyuma lakini swala la Ashley kumjua Roma lilimgusa na kutamani kujua.

“Kwa muonekano wako unaonekana Roma hajakueleza Maisha yake ya nyuma?”

“Ndio Ashley najua ana historia ya kipekee lakini sijawahi kupata kuijua”

“Mh ! Basi mimi nitakuelezea kwa upande wangu nilivyomfahamu Roma”Aliongea Ashley na Edna alikaa kitako kutaka kusikiliza histori ya Roma , alikuwa na hamu ya kujua Maisha ya nyuma ya Roma , lakini alikuwa akisita sana kumuuliza Roma mwenyewe.

********

Roma jana yake alienda kwa Nasra lakini alivyofika hakumkuta na alijaribu kumpigia simu lakini pia haikuwa ikipatikana , lakini hata hivyo hakuwa na wasiwasi na aliamua Kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Dorisi ili kumsalimia kwani ni muda kidogo hakuwa ameonana nae na alivyofika alimkuta na Dorisi alifurahishwa na ujio wa Roma na Roma alidumu nyumbani kwa Dorisi kwa masaa matatu mpaka alipoaga kuelekea Mbagala kwa ajili ya Rose , alikuwa amemkumbuka Rose hivyo alijiambia hawezi kumaliza siku pasipo ya Kwenda kumuona.

Na usiku ndio aliumalizia huko na asubuhi ya saa tatu ndio alionekana akiingia ndani ya nyumba yake anayoishi Pamoja na familia yake.

Roma baada ya kumaliza kuegesha gari moja kwa moja alitembea mpaka ndani na kumkuta mama yake akiangalia Runinga Pamoja na Bi Wema , lakini jambo lililomshangaza pia Mage na Magdalena walikuwepo.

“Roma wageni wako wanakusubiria”Aliongea Blandina baada ya kusalimiana na mtoto wake.

“Mama tutaongelea hapo nje”Aliongea Magdalena na kisha alitoka wa kwanza akimuacha Mage anaemkagua Roma.

Roma aligeuza na kisha alianza kutembea mpaka nje huku nyuma akifuatia Mage na walikuja kusimama kwenye bustani.

Mapacha hao walionekana warembo kweli kiasi cha kumfanya Sophia kukaa juu ya balcony na kuchungulia chini kile kinachoendelea , kwani yeye dakika kadhaa zilizopita ndio aliwapokea Mage na Magdalena sasa baada ya kuona wamekuja kwa ajili ya Roma alifikiria ni lazima watakuwa sehemu ya michepuko yake na ndio maana alishindwa na wivu kiasi cha kumpekea kupanda juu ya Balconi kuangalia kinacheondelea.

Roma alimwangalia Mage na kisha akamkonyeza na kumfanya Mage kuona aibu.

“Hivi Roma kwanini huna wasiwasi na sisi ndio tunaonekana kuwa na wasiwasi?”Aliuliza Magdalena huku akiweka kibesi.

“Magdalena usiniambie ni yaleyale ya Salah , mimi swala lile niliachana nalo muda uleule ulionipigia”Aliongea Roma na kumfanya hata Mage amshangae.

“Yaani umeua halafu unasema umeachana nalo , unajua hata mtu uliemuua kweli”Aliongea Magdalena.

“Magdalena kama unaona huyu mwanaume niliemuua ni wa spesho sana ni bora ukaniweka wazi ni nani haswa na kwanini unaogopa kuniambia”Magdalena alivuta pumzi.

“Ushawahi kusikia makampuni ya MAYA hapa Tanzania au popote ndani ya Afrika?”Aliuliza Magdalena na Roma hakuwa akifahamu kampuni ya MAYA kwani hakuwa mtu wa kufatilia sana Habari za watu ambao hawamhusu.

“Unaonekana haumfahamu basi ni hivi ni hivi mtoto uliemuua jana baba yake ndio mmiliki wa Makapuni ya MAYA”Aliongea.

“Maya Hubat ndio mmiliki wa makampuni hayo”

“Okey Magdalena tusema huyu Maya Hubat ni mtu mzito hapa nchini , mnachotaka mimi kufanya ni nini maana mimi sio Mungu niweze kurudisha uhai mtoto wake , mnaonaje mkienda moja kwa moja kwenye swali mlilokuja nalo”Aliongea Roma.

“Unachukulia mambo kwa wepesi sana..”

“Roma tunachotaka ni wewe kukana kuhusika kuwa muuaji wa Salah”Aliongea Mage na kumfanya Roma kwanza atabasamu.

“Kwanini napaswa kufanya hivyo?”

“Roma tunakusaidia ili kuepuka swala hili, unaweza ukachukulia poa swala la Salah ila Mzee Maya hagusiki kwa namna yoyote ile na anao uwezo mkubwa wa kukuangamiza na hata raisi mwenyewe hana uwezo wa Kwenda nae kinyume”

“Afande Mage huu ni msimamo wangu “

“Mimi Roma Ramoni nimemuua Salah nikiwa na akili zangu timamu kwa kumkosea heshima mke wangu kwa kitendo chake cha kumdhalilisha hivyo sipo tayari kukana adhabu ambayo nimeitoa kwani nitakuwa naenda kinyume na sheria nilizojiwekea, Ukifanya jambo na nafsi yako ikakuhumu basi jua umetenda dhambi , mimi nafsi yangu hainihukumu licha ya kwamba nimemuua Salah , hivyo haina haja ya kuhangaika”Aliongea Roma na kisha aliwaacha Mage na Magdalena wasijue cha kufanya lakini kabla ya Roma hajakaribia mlango wa kuingia mara alijikuta akisimama na kisha akageuka na kutabasamu kifedhuli , alihisi msuguano wa hewa ambao sio wa kawaida na sio kwake tu hata kwa Magdalena ilikuwa hivyohivyo.

“Denisii.!!!”Aliiita Sophia aliekuwa juu baada ya kumuona Denisi akiruka ukuta kama vile fisi na kutua kwenye eneo la Bustani.

ITAENDELEA

Haya Denisi huyo hapo , nini kitatokea
Nicheki watsapp 0687151346
 
SEHEMU YA 264

Aliekuwa mlangoni hakuwa mwingine bali ni Ashley mtoto wa raisi Senga na Edna alishangaa kumuona Ashley kwenye ofisi yake asubuhi hio.

“Edna..!!!”Aliita Ashley na Edna alitabasamu na kutoka kwenye kiti chake na kumsogelea Ashley na kumkaribisha kwa kumkumbatia.

“Karibu sana Ashley , umerudi lini?”

“Nina siku mbili Tanzania”Aliongea Ashley kwa furaha kabisa

“Boss mimi nitaondoka kama hakuna maagizo mengine”

“Naomba uendelee kufatilia kinachoendelea ndani ya kampuni ya MAYA”Aliongea na Suzzane aliitikia na kisha alitoka kwenye ofisi akimwacha Profesa Ashley mtoto wa raisi Senga akiongea na Edna.

“Edna nadhani sasa hivi nikuite wifi”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kushangaa.

“Kwanini jamani”

“Edna usijifanye na wewe hupo tayari kutupokea kama wanafamilia ,mimi na Roma ni kaka na dada hivyo wewe ni mume wake na inakufanya kuwa wifi yangu haha..”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kucheka na kuona aibu kwa wataki mmoja.

Ashley na Edna wanafahamiana sana na sio kwasababu Raisi Senga alikuwa na ukaribu na familia ya Adebayo , bali Ashley na Edna walisoma shule moja ya IST kwanzia darasa la kwanza mpaka la saba, hivyo ni rahisi kusema kwamba Ashley , Mage , Magdalena na Edna walisoma shule moja na walikuwa marafiki wote kipindi cha utoto wao na ni Ashley ndio aliekuwa akiwaburuza darasani wanafunzi wote na nafasi ya pili ilikuwa ikishikiliwa na Edna.

“Edna nilikuja nyumbani nikaambiwa umekuja kazini ndio nikaona nije moja kwa moja kukuona kwani sina muda mrefu nataka kurejea Uingereza”Aliongea

“Mh! wewe nae na Uingereza yako , hujawahi kuipenda Tanzania wewe tokea uende masomoni”

“Sio kweli Tanzania naipenda , lakini mazingira yake na taaluma yangu ni vitu viwili tofauti , Serikali za wenzetu zinawapa sapoti sana wanasayansi kuliko hapa Tanzania”Aliongea na Edna alimuunga mkono.

“Sasa ni kipi ambacho unataka kuongea na mimi?”Aliuliza Edna.

“Hehe… kabla ya yote nilitaka kumuona mke wa kaka yangu kabla ya kurudi uingereza”Aliongea na kumfanya Edna kujisikia vizuri, kila mwanamke alieolewa mawifi wakikupenda basi unajiona kuwa na bahati ,na hio ndio ilikuwa kwa Edna , kupendwa na wifi yake Ashley hakuliona jambo baya, alijishangaa pia mambo yao na Roma yalivyoanza , lakini kadiri siku zinavyoenda mahusiano yao yanachukua sura mpya kila siku.

“Edna nimekuja kukuambia siri yangu ila nataka uniahidi kama hutomwambia Roma”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa.

“Niambie siri yako itakuwa siri yangu”

“Hehe. Umenikumbusha wakati tukiwa Watoto ulizoea kusema hivyohivyo lakini mwisho wa siku siri zangu ulimwambia mama yako”Aliongea Ashley na kumfanya Edna akumbuke na kuona aibu.

“Ule ulikuwa utoto , saivi mimi mkubwa na hata hivyo mama ndio mtu niliekuwa nikimwambia siri zangu na sasa hivi hayupo tena”Alionge akinyongea kidogo.

“Usijali Edna, mimi wifi yako nakupenda sana, Edna mimi nilijua kuwa wewe ni wifi yangu tokea siku uliokuja Ikulu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Unataka kumaanisha nini Ashley?”

“Namaanisha kwamba nilimfahamu Roma kabla yako hio ndio siri yangu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa Zaidi.

“Unasema kweli?”

“Ndio namfahamu Roma huenda kuliko unavyomfahamu wewe , mimi Roma nilimfahamu ni kaka yangu kabla hata hajaja huku Tanzania”Edna alishangazwana jambo hilo mno.

“Hebu nielezee vizuri”Aliongea.

“Usijali nipo hapa kukuelezea kila kitu ninachokijua kuhusu Roma”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kujawa na shauku Zaidi, ijapokuwa alikuwa akitaka Roma ndio amwambie mwenyewe historia yake ya nyuma lakini swala la Ashley kumjua Roma lilimgusa na kutamani kujua.

“Kwa muonekano wako unaonekana Roma hajakueleza Maisha yake ya nyuma?”

“Ndio Ashley najua ana historia ya kipekee lakini sijawahi kupata kuijua”

“Mh ! Basi mimi nitakuelezea kwa upande wangu nilivyomfahamu Roma”Aliongea Ashley na Edna alikaa kitako kutaka kusikiliza histori ya Roma , alikuwa na hamu ya kujua Maisha ya nyuma ya Roma , lakini alikuwa akisita sana kumuuliza Roma mwenyewe.

********

Roma jana yake alienda kwa Nasra lakini alivyofika hakumkuta na alijaribu kumpigia simu lakini pia haikuwa ikipatikana , lakini hata hivyo hakuwa na wasiwasi na aliamua Kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Dorisi ili kumsalimia kwani ni muda kidogo hakuwa ameonana nae na alivyofika alimkuta na Dorisi alifurahishwa na ujio wa Roma na Roma alidumu nyumbani kwa Dorisi kwa masaa matatu mpaka alipoaga kuelekea Mbagala kwa ajili ya Rose , alikuwa amemkumbuka Rose hivyo alijiambia hawezi kumaliza siku pasipo ya Kwenda kumuona.

Na usiku ndio aliumalizia huko na asubuhi ya saa tatu ndio alionekana akiingia ndani ya nyumba yake anayoishi Pamoja na familia yake.

Roma baada ya kumaliza kuegesha gari moja kwa moja alitembea mpaka ndani na kumkuta mama yake akiangalia Runinga Pamoja na Bi Wema , lakini jambo lililomshangaza pia Mage na Magdalena walikuwepo.

“Roma wageni wako wanakusubiria”Aliongea Blandina baada ya kusalimiana na mtoto wake.

“Mama tutaongelea hapo nje”Aliongea Magdalena na kisha alitoka wa kwanza akimuacha Mage anaemkagua Roma.

Roma aligeuza na kisha alianza kutembea mpaka nje huku nyuma akifuatia Mage na walikuja kusimama kwenye bustani.

Mapacha hao walionekana warembo kweli kiasi cha kumfanya Sophia kukaa juu ya balcony na kuchungulia chini kile kinachoendelea , kwani yeye dakika kadhaa zilizopita ndio aliwapokea Mage na Magdalena sasa baada ya kuona wamekuja kwa ajili ya Roma alifikiria ni lazima watakuwa sehemu ya michepuko yake na ndio maana alishindwa na wivu kiasi cha kumpekea kupanda juu ya Balconi kuangalia kinacheondelea.

Roma alimwangalia Mage na kisha akamkonyeza na kumfanya Mage kuona aibu.

“Hivi Roma kwanini huna wasiwasi na sisi ndio tunaonekana kuwa na wasiwasi?”Aliuliza Magdalena huku akiweka kibesi.

“Magdalena usiniambie ni yaleyale ya Salah , mimi swala lile niliachana nalo muda uleule ulionipigia”Aliongea Roma na kumfanya hata Mage amshangae.

“Yaani umeua halafu unasema umeachana nalo , unajua hata mtu uliemuua kweli”Aliongea Magdalena.

“Magdalena kama unaona huyu mwanaume niliemuua ni wa spesho sana ni bora ukaniweka wazi ni nani haswa na kwanini unaogopa kuniambia”Magdalena alivuta pumzi.

“Ushawahi kusikia makampuni ya MAYA hapa Tanzania au popote ndani ya Afrika?”Aliuliza Magdalena na Roma hakuwa akifahamu kampuni ya MAYA kwani hakuwa mtu wa kufatilia sana Habari za watu ambao hawamhusu.

“Unaonekana haumfahamu basi ni hivi ni hivi mtoto uliemuua jana baba yake ndio mmiliki wa Makapuni ya MAYA”Aliongea.

“Maya Hubat ndio mmiliki wa makampuni hayo”

“Okey Magdalena tusema huyu Maya Hubat ni mtu mzito hapa nchini , mnachotaka mimi kufanya ni nini maana mimi sio Mungu niweze kurudisha uhai mtoto wake , mnaonaje mkienda moja kwa moja kwenye swali mlilokuja nalo”Aliongea Roma.

“Unachukulia mambo kwa wepesi sana..”

“Roma tunachotaka ni wewe kukana kuhusika kuwa muuaji wa Salah”Aliongea Mage na kumfanya Roma kwanza atabasamu.

“Kwanini napaswa kufanya hivyo?”

“Roma tunakusaidia ili kuepuka swala hili, unaweza ukachukulia poa swala la Salah ila Mzee Maya hagusiki kwa namna yoyote ile na anao uwezo mkubwa wa kukuangamiza na hata raisi mwenyewe hana uwezo wa Kwenda nae kinyume”

“Afande Mage huu ni msimamo wangu “

“Mimi Roma Ramoni nimemuua Salah nikiwa na akili zangu timamu kwa kumkosea heshima mke wangu kwa kitendo chake cha kumdhalilisha hivyo sipo tayari kukana adhabu ambayo nimeitoa kwani nitakuwa naenda kinyume na sheria nilizojiwekea, Ukifanya jambo na nafsi yako ikakuhumu basi jua umetenda dhambi , mimi nafsi yangu hainihukumu licha ya kwamba nimemuua Salah , hivyo haina haja ya kuhangaika”Aliongea Roma na kisha aliwaacha Mage na Magdalena wasijue cha kufanya lakini kabla ya Roma hajakaribia mlango wa kuingia mara alijikuta akisimama na kisha akageuka na kutabasamu kifedhuli , alihisi msuguano wa hewa ambao sio wa kawaida na sio kwake tu hata kwa Magdalena ilikuwa hivyohivyo.

“Denisii.!!!”Aliiita Sophia aliekuwa juu baada ya kumuona Denisi akiruka ukuta kama vile fisi na kutua kwenye eneo la Bustani.

ITAENDELEA

Haya Denisi huyo hapo , nini kitatokea
Nicheki watsapp 0687151346

Daaah genius sana singano jr hata sijui lini tena
 
Back
Top Bottom