Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Huyu Denis anajiona ameiva mpaka kumvamia Roma kweli?
Swali ninalojiuliza Roma "The Hades" atamuweza Athena "The Don" kama Godstone ilichukuliwa mikononi mwake bila yeye kujua?!🤣🤔
Ijumaa sio mbali, wacha tusubiri
 
Huyu Denis anajiona ameiva mpaka kumvamia Roma kweli?
Swali ninalojiuliza Roma "The Hades" atamuweza Athena "The Don" kama Godstone ilichukuliwa mikononi mwake bila yeye kujua?![emoji1787][emoji848]
Ijumaa sio mbali, wacha tusubiri
Atapigwa busha huyo hajui Roma ni wizzy
 
Huyu Denis anajiona ameiva mpaka kumvamia Roma kweli?
Swali ninalojiuliza Roma "The Hades" atamuweza Athena "The Don" kama Godstone ilichukuliwa mikononi mwake bila yeye kujua?!🤣🤔
Ijumaa sio mbali, wacha tusubiri
Yaani mimi nimeona thread yako nikajua tayari mzigo umetua nilikuwa najiandaa kununua popcorn tyu 🤣🤣🤣
 
Nukta yangu imepigwa hapa.
 
SEHEMU YA 265

“Mr Deniss nadhani sio utaratibu kuingia kwenye nyumba za watu kwa namna ya kuruka ukuta , unataka tukufikirie vipi?”Aliuliza Roma baada ya kugundua mtu aliekuwa akisababisha mgandamzo wa hewani ni Denisi na ukweli alishangaa mno kwani aliona mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wa Denisi tofauti na alivyokutana nae kwa mara ya mwisho ndani ya familia ya Mzee Atanasi.

“Wewe muuaji huna haja ya kuniuliza maswali nimeingiaje hapa ndani, unachotakiwa kwasasasa ni kujisalimisha kwangu kabla sijakufanya kitu kibaya”Aliongea Denisi.

Denisi licha ya kwamba alivalia mavazi ya kawaida , lakini mwili wake na sauti yake viliogofya kwa wakati mmoja, kwani licha ya kwamba alikuwa akiongea kwa kejeli lakini aliongea kwa sauti kubwa kiasi kwamba hata Blandina aliekuwa ndani na eye alitoka nje kujua ni kipi kinaendelea akiwa Pamoja na Bi Wema na Sophia.

“Denisi kama haya yote ni kwa ajili yangu naomba uache mara moja Roma hausiki”Aliongea Sophia kwa kukaripia na Denisi alimgeukia Sophia na kumwangalia.

“Sophia mwanamke wa Maisha yangu ni kweli nipo hapa kwa ajili yako , lakini sio hilo tu , nadhani mpaka sasa hujafahamu kwamba mtu unaeishi nae ni katili kupitiliza”

“Kijana unaongea nini , hatukuelewei umeingia nyumbani kwetu na kuanza kuongea mambo yasioeleweka , unapaswa kujjitambulisha”Aliongea Blandina kwa namna ya kufoka. Na Denisi alimwangalia Blandina kwa dharau sana.

“Mama nadhani hujanifahamu mpaka sasa , mimi ni Denisi mtoto wa Raisi Senga , mwanaume ambaye ulimsaliti miaka ya nyuma na kumkimbia”Aliongea kwa kejeli na kumfanya Blandina kushangaa , hakuamini kama aliekuwa mbele yake ni mtoto wa Raisi Senga afahamikae kwa jina la Denisi , unajua licha ya kwamba Blandina alikuwa akijua Senga ana mtoto anaeitwa Denisi , lakini hakuwahi kumuona kwa macho yake.

“Kumbe wewe ndio Denisi mtoto wa raisi Senga? , unaonaje ukaeleza ni kipi ambacho kimekuleta nyumbani kwetu na kuanza fujo?”Aliongea Blandina huku akipotezea baadhi ya maneno ya Denisi kama vile usaliti na mengineyo ya mauzi.

“Kwa jinsi unavyonekana ni dhahiri haufahamu alichokifanya mtoto wako, basi ngoja nikuambie, Roma kamuua mtoto wa Maya Hubat afahamikae kwa jina Salah”Aliongea Denisi na kumfanya Blandina kutoa macho na sio kwake tu hata kwa wale wote ambao hawakufahamu tukio la Jana yake wlaionekana kuwa katika mshangao akiwemo Bi Wema.

“Denisi mimi namheshimu sana baba yako kwani ni kiongozi mkubwa wa nchi hii , lakini hili swala lakumsingizia mwanangu naomba uache mara moja na uondoke nyumbani kwetu”Aliongea Blandina , hakuamini kama Roma anaweza kumuua mtoto wa Tajiri mkubwa kama Maya Hubat

“Hehe…Bi Mkubwa nadhani unafahamu machache sana kuhusu mwanao Roma na muda si mrefu utafahamu kwamba mwanao ni shetani ambaya hapaswi kuishi akichangamana na binadamu”

“Naomba unyamaze Roma ni mwanangu mimi niliemzaa licha ya kwamba sijamlea haimaanishi kwamba simfahamu , Roma sio mkatili na hawezi kuua mtu”Aliongea Blandina na kumfanya Denisi kucheka kicheko cha juu cha dharau.

Wakati huu Mage na Magdalena ukweli hawakuelewa madhumuni haswa ya Denisi kuja hapo ndani, licha ya Magdalena kuhisi uwezo usio wa kawaida wa Denisi lakini bado hakuelewa swala la Salah na Denisi linaingia vipi , lakini hata hivyo Magdalena alikuwa kwenye wasiwasi mkubwa kwani aliamini kinaweza kumkuta kitu kibaya Denisi jambo ambalo lingeinua mtifautno mkali kwani Roma na Denisi ni kitu na kaka yake .

“Mr Denisi tafadhali naomba uondoke , swala la Salah sio kosa la Roma”Aliongea Magdalena.

“Mhmh .. Roma sijui hawa wanawake unawapaga nini , kwani kila mmoja anaonekana kuwa upande wako , si ajabu Ajenti Flamingo hapa na yeye anakupenda”Aliongea Denisi na kumfanya Roma amwangalia Magdalena kumsoma na kweli maneno yale yalimfanya Magdalena kukosa utulivu.

“Roma usijali hili nitakusaidia lipite mwanangu najua haujaua”Aliongea Blandina akitaka kupoza hali.

“Mama hata usiwe na wasiwasi , ni kweli jana nilimuua kijana mmoja mpumbavu ambaye alikuwa akimdhalilisha mke wangu , ni adhabu ya kawaida sana ninayotoa kwa watu wenye makosa”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kubung`aa na kumwangalia Roma.

“Hapana Roma mwanangu huwezi kukubali kosa ambalo sio lako , kwa mwonekanao wako wa utulivu huonyeshi kabisa umeua”Aliongea Blandina.

Ni kweli Roma hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi kama ameua na ndio maana Blandina aliamini Roma hajafanya kosa kama hilo , kwani alikuwa akijua siku zote mtu mwenye hatia ya mauaji lazima aonyeshe wasiwasi kwenye macho yake, lakini asichokijua Blandina kwa upande wa Roma swala la kuua mtu halikuwa swala kubwa kwake , lilikuwa ni sehemu ya adhabu zake pale mtu akimkosea, Roma alijiambia mama yake hamfahamu bado na alifanya vyema kutomwabia historia yake ya nyuma , kama angesema kwamba ameua Zaidi ya watu elfu moja kwa wakati mmoja huenda mama yake angezimia palepale.

“Denisi kilichokuleta hapa ni uchokozi wa waziwazi juu yangu na familia yangu, mimi nimemuua huyo mpuuzi Salah kwa makosa yake sasa iweje wewe kuungana na watu wenye makosa?”

“Kifo sio adhabu pekee katika hii dunia na unawahakikishia vipi watu kama Salaha alikuwa na makosa?, Hata hivyo sijaja hapa kupoteza muda nimekuja kukuadhibu kwa niaba ya familia yaMzee Maya”Aliongea Denisi huku akisogea mbele na kumfanya hata Roma kutabasamu kifedhuli.

“Naona una mwili usio wa kawaida tokea mara ya mwisho nilivyokuona , sijui umefanyiwa nini lakini nikushauri kama hutaki wazazi wako watoe machozi kwa ajili yako ni bora ukaondoka”Aliongea Roma.

Ukweli upande wa Roma alihisi mwili wa Denisi ni kama mwili wa Depney tu kule Ufaransa.

“Unajigamba sana Roma lakini huu ndio mwisho wako “Aliongea Denisi na palepale alivyatuka kumfuata Roma aliposimama huku upande wa Roma hakuwa na wasiwasi kabisa, licha ya kumuona Denisi ana mwili ambao sio wa kawaida lakini bado alimuona wa kawaida sana.

“Puuuh”ni ngumi nzito iliotua kwenye kifua cha Roma kiasi kwamba ilisababisha mlio mkubwa , lakini ajabu ni kwamba licha ya Denisi kutumia uwezo wake wote kumpiga Roma , lakini hakukuwa na madhara ya aina yoyote na Roma alikuwa vilevile alivyosimama na hakusogea hata inchi moja.

“Kitendo cha kuja nyumbani kwangu na kusababisha fujo ni makosa ya wazi kabisa na leo hii siwezi kukusamehe”Aliongea Roma na kisha akampiga Denisi kibao.

“Romaa..!!!” Wa kwanza kutahamaki alikuwa ni Magdalena m, kibao alichopigwa Denisi kilikuwa cha kawaida sana lakini madhara yake yalionekana wazi , kwani Denisi alizunguka kama pia na kudondokea ngazi za kuingilia ndani ya nyumba yao.

Denisi alijikongoja na kusimama upya , mwanzoni alionekana kutumia uwezo wa kawaida sana kupambana na Roma na ndio maana kibao kilimpeleka chini lakini awamu hiii alinyanyuka akiwa na uwezo wake halisi.

“Magdalena muangalie ni .. nini kimemtokea?”Mage ndio aliekuwa wa kwanza kujawa na hofu mara baada ya kumuona Denisi akitanuka mwili huku macho yake yakiwa kama ya mbwa mwitu.

“Mh!!naona hiki ndio kimekupa ujasiri wa kuja kunijaribu”Aliogea Roma huku akimwangalia Denisi kwa macho ya dharau, lakini jambo ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba Denisi alionekana kama mtu ambaye ashakosa uwezo wake wa kuongoza akili yake na Roma alijiambia yoyote ambaye amehusika na sayansi ya mwili wa Denisi basi kuna makosa ambayo ameyafanya huenda ni kwa kudhamiria au hakuwa akielewa anachokifanya.

Denisi ni kama alikuwa akitafuta mtu wa kudhuru , alianza kukagua mtu mmoja mmoja , alianza kwa Sophia na kumwangalia kwa macho makali na kumfanya Sophia kutamani kujikojolea , Akahamia kwa Yezi aliekuwa ndio kwanza anatoka ndani baada ya kusikia mitafaruku na Yezi alijikuta mwili ukiota vipele , Denisi alimgeukia Mage na Magdalena na kumfanya Mage kurudi nyuma ya dada yake huku akiwa na hofu mno.

Kwa jinsi Denisi alivyoonekana ni kama hakuna ambaye anamfahamu na staili yake ya kuzungusha shingo ni kama ya roboti.

“Roma usipambane nae atakudhuru , anaonekana kuwa mnyama , masikini sijui nini kimetokea”Aliongea Blandina ambaye alipona kutoka kwenye mshituko na kuanza kumkagua Denisi lakini licha ya kuongea hivyo akujua namna ya kujihadhari nae.

“Mama unaweza kuingia ndani maana sitaki ukishuhudia nikiua mtu lakini kama haina tatizo kwa upande wako basi unaweza kuangalia”Aliongea Roma ,

Denisi aliekuwa kama kachanganyikiwa ni kama sasa amemtambua Roma kama moja ya mtu anatakiwa kupigana nae kwani aliruka juu kwa mikono yake yote Pamoja na miguu kumfuata Roma huku akidhamiria eneo la Shingon kumdhuru Roma.

“Paah!!!” Awamu hii Roma hakumpiga shavuni tena bali alimpiga Denisi upande wa utosini kwa kutumia mkono mmoja na hii nimara baada ya Denisi kumfikia na palepale Denisi alidondoka chini kwenye miguu ya Roma na mwili wake ukaanza kutetema,lilikuwa ni pigo la kawaida mno lakini lililoshangaza sana .

Magdalena ndio wa kwanza kusogea sehemu ambayo Denisi amelala chini huku akitetema kama kuku anaepoteza Maisha.

“Roma umemuua?”Aliongea Magdalena kwa wasiwasi.

“Sijamuua ila napanga kumuua”Aliongea Roma na kisha aliinamana na kumshika tai Denisi na kumning`iza hewani na kitendo kile kilionekana kama tiba kwa Denisi kwani palepale mwili wake ulirudi kwenye hali ya kawaida huku akiacha kutetema.

“Naona ushatoka kwenye dunia ya Wanyama na sasa umerudi kwenye uhalisia”Aliongea Roma baada ya kumuona Denisi kasharejewa na akili zake timamu.

Denisi baada ya kujishtukia yupo kwenye mkono mmoja wa Roma alianza kujikakamua kutafuta uwezo wake ili kumzidi nguvu Roma lakini kila akijaribu mwili ulikosa nguvu.

“Huwezi tena kutumia uwezo wako wa kipuuzi tena mbele yangu , watu wa aina yako nishakutana nao kwenye Maisha yangu mara nyingi na wengi wao niliishia kuwatoa nguvu zao zote”Aliongea Roma na kumfanya Denisi azidi kutapatapa hewani kwa kukosa pumzi , alitamani kuongea lakini alishindwa.

“Roma utamuua?”Aliongea Blandina huku akihisi woga kweli na sio kwake tu hata kwa Magdalena hakuwa tayari kuona Roma anamuua mdogo wake.

“Roma tafadhari Denisi ni mdogo wako usimuue.. tafahdari”Aliongea Blandina tena kwa wasiwasi kwani aliona mwisho wa Denisi anauona, ila Roma hakujali Zaidi ya kuendelea kumkaba Zaidi na Zaidi Denisi..

Magdalena baada ya kuona Roma hana mpango wa kumuachia Denisi alijaribu kutumia uwezo wake kumsukuma Roma,lakini hakukuwa na mafanikio kabisa.

Ni dakika moja tu Denisi shingo yake ishalegea na kufanya Blandina kuanza kutoa machozi , hakuamini kabisa Roma kamuua mdogo wake.

Roma yeye hakujali, baada ya kuona kazi yake ya kunyonga ishakamilika alimtupa Denisi chini kama zigo na Magdalena ndio aliekuwa wa kwanza Kwenda kushika mwili wa Denisi kuupima na ulionekana kuanza kupoteza joto kwa kiasi kikubwa ikiashiria hakuwa hai tena...









SEHEMU YA 266.

Mtu wa kwanza kupokea taarifa za kifo cha Salah alikuwani raisi Kigombola , Raisi mstaafu huyu baada ya kusikia kifo cha Salah alijawa na wasiwasi kweli , kilichomfanya kugopa ni ukubwa wa tukio hilo kwani kifo cha Salah hakikuwa cha kuitwa na Mungu bali cha kutekelezwa na binadamu.

“Ilikuwaje Erick?”Aliuliza mheshimiwa Kigombola huku uso wake ukiwa umesawajika kwa wasiwasi.

“Mheshimiwa Abubakari Hamadi kanipigia simu na kuniambia kwamba Roma ndio kasababisha kifo chake kwa kitendo cha Salah kumdhalilisha Edna Adebayo, Boss wa Vexto”Aliongea Erick msaidizi wa raisi Kigombola na kumfanya Mheshimiwa kushangaa kwani taarifa hio hakuwa nayo. Alikuwa akifahamu Salah amekufa kwa kuuliwa lakini hakufahamu kwamba sababu ya kifo chake ilikuwa ni kumdhalilisha Boss Edna.

“Kwahio nani kamuua Salah?”Aliuliza Mheshimiwa

“Mheshimiwa sijafahamu nini kimetokea , lakini kwa maneno ya Abubakari aliehusika na kifo cha Salah ni Roma Ramoni mke wa Edna”Aliongea na kumfanya mheshiumiwa Kigombola kutoa macho ya mshangao.

“Romaa..!!!”Aliongea mheshimiwa kwa wasiwasi na palepale faili la Roma , Hades liliibuka kwenye kichwachake na jasho liliamza kumtirika.

“Kama kweli Roma ndio kahusika , hili swala sio dogo tunatakiwa kufanya maamuzi ya haraka kabla ya Mzee Maya hajalifahamu hili”.

“Mheshimiwa napaswa kufanya nini?”Aliuliza Erick na kumfanya Mheshimiwa asimame kutoka kwenye sofa alilokalia na kuwaza kidogo lakini kabla hajajua cha kufanya simu yake ilianza kuita mfululizo na Erick aliichukua na kumpatia mheshimiwa na baada ya kuangalia jina alishangaa kidogo, kwani jina lilisomeka 'First Lady’ alijishauri kupokea ama kutopokea ,lakini alijikuta akiona apokee.

“Za siku nyingi mheshimiwa?”Ilisikika suati upande wa pili ya kike.

“Salama Kizwe”

“Kigombola mpenzi, hilo jina nishakwambia silipendi”Ilisikika sauti ya madaha

“Kizwe kama unaanza mambo yako, naomba unipigie baadae nipo kwenye matatizo”

“Kigombola tangu lini matatizo yako yakawa peke yako mpenzi, nimekumiss sana Kigombola”Ilisikika sauti na kumfanya Kigombola amwangalie Erick.

“Unaweza Kwenda, ongea na Abubakari mwambie aje hapa mara moja atupe maelezo”Aliongea na Erick aliitikia na kisha akaondoka.

“Kizwe nimekuambia nipo kwenye matatizo kwa sasa kwanini hutaki kuelewa , halafu hata hivyo mahusiano yetu yaliishaga baada ya kazi yako kukamilika”Aliongea Mheshimiwa Kigombola kwa sauti ya chini sana , ni kama alikuwa akigopa mtu kumkamata.

“Mh! Ni kweli kazi ile iliisha lakini sikuwahi kusema hakuna kazi nyingine , nimesikia swala la kifo cha Salaha wa Mzee Maya”Aliuongea na kumfanya mheshimiwa kushangaa kidogo.

“Huyu mwanamke sitaki kuhusika nae tena , anaonekana kuwa wa hatari mno kwangu”Aliwaza mheshimiwa Kigombola.

“Kizwe niambie sababu yako ya kunipigia?”Aliongea Mheshimiwa Kigombola huku akiweka sauti ya kibesi kidogo.

“Kigombola nadhani unakumbuka tulichokifanya miaka ile kwa kushirikiana na Kampuni ya Maya?”

“Nakumbuka ndio , hivyo nenda moja kwamoja kwenye topic”

“Kama nilivyosema Salah nimesikia amekufa na aliehusika na kifo chake ni mume wa Edna , swala ambalo linatuweka kwenye wakati mgumu mimi na wewe, mpaka sasa ninawasiwasi na maneno ya Raheli wakati anakaribia kufariki juu ya Ushahidi alioacha”Aliongea Kizwe.

“Unataka kusema nini?”

“Fikiria vizuri Kigombola naongelea kuhusu swala la kifo cha Raheli, mimi na wewe ndio tulihusika lakini uongozi wa Maya ndio ulitekeleza mpango husika na sasa huyu mtoto mpumbavu Salah anatengeneza muunganiko kati yetu na familia ya Adebayo jambo ambalo sitaki litokee kwa sasa mpaka litakapokamilika”aliongea Kizwe na kumfanya mheshimiwa kigombola kuvuta pumzi.

“Kigombola fanya ufanyavyo, swala la kifo cha Salah halipelekei ufukunyuzi wa mambo yaliopita”

“Mbona unaongea kama unanipa amri wewe mwanamke?”

“Sio amri Kigombola hayo ni maagizo ya kawaida tu ,uhusiano wetu ulikufa mara baada ya ukamilishaji wa mpango , lakini haimaanishi kwamba hatukuwahi kuwa na mahusiano huwezi kuifuta historia Kigombola nafikiri unaelewa ninachomaanisha”Aliongea kizwe na simu ilikatwa palepale na kumfanya Mheshimiwa kutukana ndani kwa ndani.

“Mheshimiwa kuna mgeni anataka kuonana na wewe?”Aliongea Scorpion.

“Ni nani?”

“Yan Buwen ,mheshimiwa”Aliongea na kumfanya Kigombola kuvuta pumzi na kumpa ishara ya kumruhusu kuingia na Yan Buwena alionekana hapo ndani ila hakuwa peke yake bali alikuwa ametangulizana na Denisi, na Kigombola alikuwa akimfahamu vyema Denisi kama mtoto wa raisi Senga.

“Karibuni sana Mr Yan Buwen na Denisi”Aliongea mheshimiwa na Yan Buwen alitabasamu na kisha alijongea na Kwenda kuketi kwenye sofa na Denisi alienda kuketi pia.

Walisalimiana kwa muda mfupi huku Yan Buwen akimweleza mheshimiwa kwamba ndio karudi rasmi nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kazi na mheshimiwa aliweka tabasamu la kinafiki na kumkaribisha huku akimwahidi ushirikiano.

“Mr Yan Buwen licha ya kwamba namfahamu Denisi kama mtoto wa Raisi wetu wa Tanzania , lakini sijafahamu kwanini umetangulizana ane?”Aliuliza Mheshimiwa Kigombola na Yan Buwen alitabasam.

“Mheshimiwa nadhani unakumbuka ahadi yangu niliowekeana na wewe kabla ya kukubaliana na mpango wa kuingia kwenye maabara?”

“Ndio nakumbuka”Aliongea na kumfanya Yan Buwen kutabasamu..

“Kama ni hivyo ,mheshimiwa basi ni vyema , kwasasa nafahamu kabisa kwamba upo kweye matatizo juu ya kifo cha mtoto wa Mzee Maya , kifo ambacho kimesababishwa na adui yako namba moja”

“Ndio Mr Yan Buwen nipo kwenye matatizo ya aina hio kwasasa na swala la kifo cha Salah limenisikitisha sana ukijumlisha pia na nguvu ya Mzee Maya”

“Mheshimiwa swala la Mzee Maya lisikupe shida sana kwa sasa kwani nitakusaidia kulitatua”Aliongea na kumfanya Kigombola macho yake kuongezeka ukubwa kidogo.

“Kivipi Mr Yan Buwen , hili swala ni kubwa licha ya kwaba Salah sio mtoto pendwa wa Mzee Maya Hubat haimaanishi kwamba swala la kifo cha mtoto wake anaweza kukichukulia kawaida?”

“Ni kweli kabisa mheshimiwa na ndio maana nikaja na kijana wangu hapa Denisi , yeye atatusaidia kuanza kudili na Roma Ramoni kwani ana uwezo mkubwa sana wa kimapigano lakini pia naweza kusema anamkaribia kaka yake kwa nguvu za ziada”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa kushangaa mno na kumchunuza Denisi.

“Mr Yan unanitania ?”

“Mheshimiwa unaonekana kutokuniamini , lakini huo ndio ukweli , kabla sijaja hapa Tanzannia Denisi alikuwa anaishi kwenye maabara zangu nikiufanyia mwili wake sayansi ya kumfanya kuwa na uwezo mkubwa”

“Denisi ni kweli anayoongea mr Yan?”

“Ni kweli mheshimiwa sipo kama wengi wanavyonichukulia , ninao uwezo mkubwa sana wa kupambana na Hades”Mheshimiwa alikuna kichwa ,mpaka hapo swala lishakuwa zito maana Dneisi na Roma alisikia majuzi tu kwamba ni ndugu lakini swala la wao kupigana kama ndugu ni la aina yake.

“Kwanini unataka kupambana na kaka yako?”Aliuliza .

“Kwasababu ni tishio kwa nafasi yangu ya kifamilia , Babu yangu Mzee Kweka mpaka sasa hivi anapanga kumrithisha Roma kila kitu , jambo ambalo sipo tayari kulipokea , ni nashukuru tu baba hayupo tayari kumpekea Roma kama mtoto wake”Aliongea Denisi kwa kujiamini na kumfanya mheshimiwa Kigombola kuvuta pumzi.

“Mr Yan kama kweli uliosema ni sahihi basi sitaki kuweka kipingamizi , lakini kabla ya yote nataka kujua unamaliza vipi swala hili”

“Mheshimiw aswala ni rahisi tu , Roma kamuua mtoto wa Mzee Maya na sasa kaka yake anataka kuisaidia familia ya mzee Maya kulipa kisasi nadhani sio jambo baya na kama mzee Maya atafahamu juu ya Denisi kutaka kulipiza kisasi kwa niaba ya familia yake itakuwa rahisi kwasisi kumtuliza.”Aliongea Yan Buwen.

“Kwahio unataka Denisi akamuue Roma?”

“Hilo ndio jibu mheshimiwa hahaha.. au hutaki Roma akifa”Aliongea .

“Natamani sana kusikia kifo chake , lakini kutokana na uwezo wa Roma nashindwa kuamini kama Denisi atamshinda kaka yake”

“Mheshimiwa huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu mimi , licha ya kwamba nina uwezo mkubwa wa kupambana na Roma , lakini pia ninayo nia thabiti ya kumuua Roma , chuki niliokuwa nayo juu yake ni kubwa mno kiasi kwamba ninachokwenda kutimiza ni jambo ambalo nishalifanya mara nyingi katika akili yangu”Aliongea Denisi huku akionekana kuwa na mchecheto mno

Na Mheshimiwa Kigombola hakuona mbaya kwa wanafamilia wakipigana , kwanza aliamini ingekuwa rahisi kwake kufanya kile ambacho Kizwe kamwambia , aliamini ataepusha migongano ya moja kwa moja kati ya Familia ya Maya na ya Edna Adebayo hivyo siri yao isingeweza kufichuka.

“Mr Yan una uhakika Denisi anaweza kumshinda Roma?”Aliuliza Mheshimiwa kigombola baada ya Denisi kuruhusiwa kuondoka.

“Hehe.. Mheshimiwa unanionaje kwa mfano, Hades ni mtu mzito sana na itachukua muda kuweza kujua namna ya kumdhibiti, swala la kumruhusu Denisi akapigane na kaka yake ni kuibua fursa”

“Fursa gani tena?”

“Mheshimiwa wewe ni mwanasiasa , lakini mambo madogo kama haya yanakushinda , sehemu ambayo ina amani siku zote hakuna Fursa , hivi kwa mfano Roma akaungana na familia yake unafikiri ni nini kitatokea?”Aliuliza na kumfanya mheshimiwa Kigombola kutabasamu.

“Ni Dhahiri kwamba nitakosa nguvu na ni swala la muda tu Senga anaweza kumtumia Hades kuniadhibu?”

“Swadakta Mheshimiwa naona sasa akili yako inafanya kazi, najua Denisi licha ya kwamba nimeweka sayansi kwenye mwili wake lakini hana uwezo wa kumzidi Hades, na hii ndio fursa kwani kwa ninavyomjua Hades atamuua Denisi na hapo ndio mparanganyo wa kifamilia unapoanzia”Aliongea na kutabasamu kifedhuli.

“Hahaha… nimekubali mipango yako , kweli sehemu ikiwa na amani fursa zinakosekana, ila hujaniambia ni sayansi gani umemuingizia mpaka kujiamini kiasi kile”

“Sayansi ya kawaida tu nimeingiza damu yake na aina ya kirusi kinachomfanya kuwa na uwezo kama wa Wolverine , lakini haimaanishi kwamba ana nguvu , moja ya tabia kubwa ya kirusi hiki sio kumpa binadamu uwezo wa kimapigano ila ni kumuongezea kujiamini tu, kuhusu kushinda mapigano inategemea na uwezo wake mweyewe”Aliongea Yan Buwen huku akinywa kidogo Wine iliowekwa kwenye glass na muhudumu dakika kadhaa zilizopita.

“Huyu Yan Buwen anaonekana kuwa na roho ya kishetani asilimia miamoja halafu ana akili nyingi , watu hawa ni wazuri kwa mafanikio yangu , nitaendelea kumtumia mpaka nitakapo pata mbinu ya kumuangamiza”Aliwaza mheshimiwa huku akicheka kwa cheko kubwa la kinafiki mbele ya Yan Buwen.

Sasa haya maongezi wakati yanafanyika , ni kabla ya tukio la jumamosi asubuhi , yaani muda huo ilikuwa ni ijumaa usiku wa saa mbili.













SEHEMU YA 267

Kila mtu alikuwa kwenye mshituko mkubwa , ni kama hawaamini kama ni kweli Roma alikuwa ashaua, tena sio kuua mtu wa kawaida bali ni ndugu yake , Blandina ndio aliekuwa kwenye majonzi kuliko watu wote , kwani swala la Roma kumuua kaka yake likuwa ni swala kubwa sana na aliamini swala hilo litamuweka Zaidi mbali na baba yake , jambo ambalo hataki litokee kwani aliamini Roma asingeweza kuishi hapa Tanzania kwa kukosa sapoti kutoka kwa familia yake.

Wengine ilikuwa hivyo hviyo ,Mage na Magdalena walikuwa kwenye majonzi baada ya kushuhudia Denisi kufa kwa namna ya kunyongwa.

“Roma umefanya nini sasa mbona unazidi kujiingiza kwenye matatizo”Aliongea Magdalena huku akitaka kuushika mwili wa Denisi kwa mara ya pili.

“Usingumse tena”Aliongea Roma kwa sauti na kumfanya Magdalena kuacha alichokuwa akitaka kufanya na wote hawakuelewa kwanini anasema asiguswe,kwa upande wa Roma aliona kila mmoja yupo kwenye majonsi nza mshangao hivyo aliona awape maelezo.

“Kwa mwili wa Denisi unavyoonekana ameambukizwa na kirusi aina ya W-Virus, hiki ni kirusi kinachotengenezwa maabara na kirefu cha W ni Wolverine Virus , kimepewa jina hilo kutokana na kwamba wanasyansi wameweza kutengeneza kirusi hiko kwa kutumia vina saba vya damu vya mnyama anefahamika kwa jina la Wolverine”Aliongea Roma na kupumua.

“Wolverine ni jamii ya Wanyama wanaofanana sana na Dubu na sifa kubwa ya mnyama huyu ni ukali wake Pamoja na nguvu, ana uwezo wa kumdhuru binadamu muda wowote atakoonana nae na hio yote ni kutokana na kujiamini kwake., kama ilivyo sifa yake ya ukali , lakini pia kujiamini anapokutana na hatari ndio kilivyokwa kirusi hiki pale binadamu anapoambukizwa anakuwa kwa asilimia kubwa kama Wolverine , sasa namna ya kuongoza kirusi hiki kwenye mwili mpaka uingizwe maabara na kufaniwa utaalamu”Aliongea Roma na kufanya kila mmmoja kushangaa.

“Kwahio unamaanisha mabadiliko yake yametokeana na kirusi kilichopo kwenye mwili wake?”

“Ndio kama nilivyosema Magdalena , Denisi kaambukizwa na kirusi hiko na ndio maana alionekana kujiamini sana na kuonyesha tabia flani kama za mnyama na kushindwa kujiendesha kiakili, mara ya kwanza kirusi hiki kutumiwa kwa binadamu ni kwa wanajeshi mwaka 1999”

“Wanajeshi!!?”

“Ndio wanajeshi , haya ni maswala ambayo sitoongelea hapa ila mpaka sasa unatakiwa kuelewa kuwa kama Denisi angekuwa anapambana na wanajeshi wa kawaida basi angekuwa na uwezo wa kuua wanajeshi wengi Zaidi pasipo kufa”Aliongea na kumfanya Magdalena kushangaa na sio kwake tu hata kwa wengine.

“Lakini Roma umemuua kaka yako hata kama alikuwa ameambukizwa na kirusi dunia haitokuelewa”Aliongea Sophia kwa wasiwasi.

“ Nimemsaidia”

“Umemsaidia kwa kumuua?”

“Unafikiri ningemuacha hai nini kingemtokea?”Aliongea Roma.

“Sasa kwanini umeniambia nisimguse, ulikuwa ukinizuia kutokuambukizwa?”

“Hakiambukizi kwa njia ya hewa wala kugusana bali ni kwa njia ya damu moja kwa moja kwasababu sifa kuu ya kirusi cha Wolverine kinaathirika kwa asilimia kubwa na joto la mazingira ya kawaida ya dunia.”

“Unataka kumaanisha nini?

“Namaanisha kwamba Kirusi Wolverine kina uwezo wa kuishi kwenye mazingira yenye ubaridi sana wa nyuzi sifuri(Freezing point) au katika mazingira yenye joto kuanzia nyuzi 360C”Aliongea Roma na kisha alimsogelea Denisi alielala kwenye majani akiwa maiti na Roma aliingiza vidole kwenye masikio yake.

Roma alijiambia mara mwisho ya kuua mtu na kumfufua ni kipindi alichokuwa akimpa mateso kapteni Kisu mvunjiko kule Japani alipokuwa na Dorisi, wakati akimhoji.

Roma alitumia dakika kadhaa tu mwili wa Denisi ulirudi kawaida japo hakuwa amezinduka.

“Unaweza kumgusa sasa”Aliongea Roma na Magdalena alimgusa Denisi na alijikuta akishangaa kwani Denisi Joto lake limerudi kawaida.

“Jamani hajafa bado”Aliongea Magdalena na kumfanya Roma kutabasamu .

“Mpaka hapo hana tena maambukizi ya virusi , lakini hata kama akipona hawezi kutembea tena”Aliongea Roma.

“Unamaanisha nini Roma?”

“Atakwa na ugonjwa wa kiharusi upande wa chini kwa Maisha yake yote , hio ndio adhabu yangu kwake kwa kuja kuleta fujo nyumbani kwangu”Aliongea Roma na hakusubiria maongezi aliingia ndani ,kwanza alikuwa amechoka kwani alikuwa ndio anarudi kwa michepuko yake.

“Jamani tumpelekeni hospitalini”Aliongea Sophia na palepale wote walikubaliana na Denisi alitolewa na kupelekwa Hospitali ya TMJ kwani ndio iliokuwa karibu na alipokelewa haraka haraka sana.

********

Simu ndio iliovuruga maongezi kati ya Edna na Ashley.

“Kuna nini mama?”

“Uko wapi Ashley , kaka yako kapatwa na matatizo na kapelekwa hospitali ni TMJ”Sauti upande wa pili ilisikika kwenye simu ya Ashley.

“Nakuja sasa hivi”Aliongea Ashley a kisha kunyanyuka.

“Edna nitatafuta muda wa kuongea , kaka yangu kapatwa na matatizo”Aliongea Ashley.

“Unamaanisha Denisi?”

“Ndio Edna”Alijibu.

“Okey ngoja twende wote”Aliongea Edna na kunyanyuka haraka haraka na kuchukua mkoba wake na kisha alitoka wakitangulizana na Ashley.

Upande wa Hospitali ya TMJ alionekana Blandina akiwa na wasiwasi mno , hakujua namna ya kutoa maelezo ya kueleweka pindi familia ya Denisi ikifika hapo hospitalini lakini hata hivyo aliamini ni wajibu wake kufanya hivyo ndio maana hakuondoka.

Edna na Ashley ndio waliokuwa wa kwanza kufika hospitalini akiwaa ameambatana na Ashley na alishangazwa na uwepo wa watu anaowafahamu ndani ya eneo la kusubiria na kujiuliza ni nini kinaendelea.

“Mama nini kimetokea mbona wote mpo hapa?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi.

“Sisi ndio tumemleta Denisi Hospitalini”Aliongea Mage na kisha kuanza kuhadhithia kilichotokea na wote walishangazwa na jambo hilo na alieshangaa Zaidi ni Ashley.

“Hapana kaka yangu hawezi kuambukizwa kirusi cha Wolverine”Aliongea Ashley huku akikimbilia upande ambao alikuwa akiamini ndio chumba ambacho kaka yake anafanyiwa matibabu.

Dakika chache mbele wakati Edna akielewesha kilichotokea , ving`ora vya magari vilisikika vikiingia ndani ya hospitali hio kwa kasi sana na Kwenda kusimama.

Raisi Senga akiwa ametangulizana na mke wake Damasi, walionekana wakiingia mkuku mkuku na ujio wao ulifanya wafanyakazi wa hospitali hio kuhaha , kwani licha ya kwamba TMJ hospital ilikuwa ni binafsi lakini pia ilikuwa ikisimamiwa na serikali.

“Karibu sana mheshimiwa”Aliongea mganga mkuu wa hospitali akimsalimia kwa heshima Raisi Senga , aliekuwa amezungukwa na walinzi.

“Nimekuja kumuona mwanangu , nimepata taarifa yupo hapa hospitalini kwenu “Aliongea Mheshimiwa.

“Ni kweli mheshimiwa , nitakupeleka moja kwa moja kwenye chumba ambacho amelazwa , matibabu mpaka sasa yanaendelea kuhakikisha afya yake inarudi kwenye hali ya kawaida”Aliongea

“Okey ongoza njia “Aliongea na Dokta yule mweupe wa kihidi alitembea kuingia ndani ya jengo hilo kubwa la ghorofa akitangulizana na mheshimiwa raisi na dakika chache tu walikuwa kwenye Korido ya wagonjwa wa hadhi ya juu , sehemu ambayo Blandina , Mage ,Magdalena na Edna walikuwa wamekaa wakisubiria majibu kutoka kwa madokta waliokuwa ndani ya chumba cha matibabu.

Raisi Senga na mke wake Damasi waliokuwa kwenye wasiwasi mkubwa walitembea wakiongozwa na Mganga mkuu bwana Manyani Sepengo mpaka eneo la kusubiria kabla ya kuruhusiwa kuonana na mgonjwa.

Mtu wa kwanza kumtambua Senga alikuwa ni Blandina ,moyo wake ulipiga kite , ukweli hakufikiria kama atakuja kuonana na Raisi Senga kwenye wakati kama huo , licha ya mambo mengi yalitokea katikati yao , lakini hakupata nafasi ya kuonana kabisa na Senga tokea arudi Tanzania.

“Mheshimiwa kuna nini?”Aliuliza Dokta baada ya kugundua Raisi amesimama katikati ya korido.

Senga macho yake yalikuwa moja kwa moja kwa Blandina na Blandiina hhivyo hivyo alikuwa amemkodolea macho Senga , tofauti ni kwamba Blandina alianza kutoa machozi na Senga alianza kupandwa na jazba, Damasi aliekuwa pembeni alimuona sasa Blandina na hapo ndio alipogundua kinachoendelea ila kwake hakuwa na muda wa kujali alikuwa akifikirai hali ya mtoto wake tu.
 
SEHEMU YA 268.

Damasi baada ya kuona hali imebadilika ghafla kwa upande wa mume wake alichokifanya ni kumshika mheshimiwa Senga mkono.

“Senga not here please..” Aliongea Damasi kwa msisitizo na kumfanya Raisi Senga kukubaliana na mke wake na kujongea mbele.

Mabadiliko ya Blandina pia Edna aliyaona hivyo alichokifanya ni kumshika mama mkwe wake na kumpa kitambaa afute machozi na Blandina alifuta machozi na kuangalia pembeni.

“Mom, Dady”Aliita Ashley baada ya kutoka kwenye chumba cha matibabu.

“Ashley nini kinaendelea , vipi hali ya mdogo wako?”Aliuliza Damasi paispo kujali watu waliokuwa wapo ndani ya eneo hilo.

“Amepalalaizi”

“Nini..!!”Walihamaki huku Damasi akijikokota nyuma manusura kudondoka.

“What Happened to him , he was so fine just this morning?”Aliongea Meshimiwa Senga , alionekana alitaka maelekezo.

Ukweli ni kwamba Denisi licha ya kwamba aliwadanganya wazazi wake , lakini hakugombezwa sana ,ijapokuwa alikuwa na makosa lakini wazazi siku zote ni wazazi hivyo walimsamehe lakini pia waliridhishwa na kauli ya Denisi Mwenyewe baada ya Raisi Senga kumuuliza mtoto wake swali.

“Hey! Boy is this real what you want?”

“Hey kijana , hiki ndio kweli unachotaka?”

“Yes Dady , sijawahi kujutia kuchakua kuwa mwanajeshi”

“Denisi mwanngu kama kweli ndio unachotaka sisi hatuna kipingamizi , ila hakikisha siku nyingine hautufichi kitu sisi wazazi wako kwa namna yoyote ile , sisi ndio wenye jukumu kwa lolote litakalotokea kwako kama wanafamilia , we always Stick together , baba yako ni kiongozi mkubwa na ana maadui wengi na ni ngumu sana kujua yupi wa kumuamini na yupi asimwamini lakini sio kwa sisi wanafamilia hatokuwaminiana sisi wenyewe, mnafikiri kama sisi wanafamilia hatuaminiani raia na wenyewe wataweza kutuamini?”Aliongea Damasi kwa msisitizo

“Denisi alichoongea mama yako ni kweli kabisa na sio kwako tu hata kwa Ashley pia , yaliopita yashapita na kuanzia sasa tunapaswa kuwa wazi kwa kila mmoja”

“Sawa Dady , Sawa Dady”hivyo ndivyo Watoto wa Senga walivyokubaliana na wazazi wake.

Sasa hata asubuhi kulivyokucha baada ya Denisi kuondoka , kwa wanafamilia hao hawakuwa na wasiwasi kabisa kwani waliamini Denisi ni mtu mkubwa sana na ambaye anapaswa hata kuwa na nyumba yake ajitegemee ndio maana hawakumzuia , lakini cha ajabu baada ya masaa mawili ndio wanapata taarifa kwamba mtoto wao amepalalaizi , kwanini wasiwe na wasiwasi na kujiuliza maswali nini kilichotokea , kwani alikuwa na afya tele asubuhi tu.

Swali lile la Raisi Senga la kwamba nini kimemtokea Denisi kiliwafanya wanafamilia kuwa katika wakati mgumu wa kuelezea tukio zima na ni kama walikuwa wakitegeana.

“Saluti kwako mheshimiwa , Ajenti Flamingo kutoka kikosi cha wachawi naripoti kwako tukio zima”Aliongea Magdalena na kumfanya Mheshimiwa Senga kushangaa kwani hakuelewa kuhusu kikosi cha wachawi , mara nyingi yeye jeshi lake hakulifuatilia sana Zaidi ya kutoa maagizo tu kwa yale makubwa makubwa na kazi zote zilikuwa chini ya wizara Pamoja na mkuu wa majeshi.

“Ajenti Flamingo unaweza kuelezea nini kimetokea”Aliongea msaidizi wa Raisi Senga bwana kabwe na ndio Magdalena alipoanza kuelezea kila kitu kuanzia kifo cha Salah na alijikuta akishangaa mno kwani hakuwa na taarifa za kifo cha mtoto wa Mzee Maya.

Upande wa Damasi alijikuta moyo ukipiga kite , lile jambo ambalo hakutaka litokee hatimae ndio linatokea , siku zote mwanamama huyu alikuwa akiogopa swala la Roma kwa Senga kutolichukulia maamuzi na kulipotezea na matokeo yake ndio hayo ambayo yanaanza kuonekana , kwani Roma kamfanya mtoto wake kupalalaizi baada ya Denisi Kwenda kumshambulia.

“Haya yote ni makosa ya Blandina”Aliongea Senga kwa sauti huku akimwangalia Blandina kwa hasira na Blandina kwakua watu walikuwa wengi alishindwa kuongea chochote , lakini pia kwa mfano Dokta Majani hakumfahamu Blandina ni nani na wengine pia hakuna ambaye alikuwa akimfahamu Blandina ni nani , kwani historia ya Blandina na Senga ilikuwa ikifahamika kwa watu wachache sana.

“Senga hupaswi kusema hivyo, this was all your Fault , usimbebeshe mtu mizigo, Tunatakiwa kujua muafaka wa matibabu ya Denisi kwanza kabla ya mambo mengine”Aliongea Damasi akitetea , sifa kubwa ya Damasi ni busara licha ya kwamba alikuwa na wivu kama mwanamke lakini likija swala la kutumia akili kuliko hisia zake ,ndio kitu kikubwa alichojaaliwa , ukweli aliona ndio Blandina alikuwa na makosa lakini chanzo kilianza kwa nani? , aliona chanzo kilianza kwa familia ya Senga mwenyewe na sio kwa Blandina peke yake.

“Dokta kuna uwezekano wa mtoto wetu kupona?”Aliuliza Damasi.

“Kwasasa hatuwezi kuongea chochote Madam kwani uchunguzi wa kina katika mwili wake unafanyika”

“Dady I think there is Solution “Aliongea Ashley na kumfanya mama yake macho yake kuongezeka ukubwa.

“Tueleze, kuna njia gani unafikiria?”Aliuliza Senga kwa hamaki na Ashley kabla ya kuongea aliangalia baadhi ya wasaidizi wa raisi ni kama alikuwa akitaka waondoke ili waongee, na kabwe msaidizi wa Raisi alielewa hilo haraka na kuwapa ishara walinzi kusogea mita kadhaa nyuma.

“Baba inaonekana Denisi hakuwa jeshini tu iila kuna mengine”Aliongea Ashley na kumfanya Senga kutaka kujua Zaidi.

“Kwa maelezo ya Mage hapa ni kwmba Denisi alikuwa kama mnyama alipoenda kumshambulia Roma”

“Unaongea nini Ashley kaka yako tunamjua ni binadamu wa kawaida na mpole inakuwaje awe mnyama?”Aliuliza Damasi huku akikosa utulivu.

“Mom Calm Down and listen to my expalantion, Actualy my brother was infected with Wolverine Virus it`s not confirmed yet but somehow I can tell..”

“Mama tulia na usikilize maelezo yangu , ukweli kaka yangu alikuwa ameambukizwa na kirusi cha Wolverine , haijathibitika bado lakini ninaweza kufahamu”

“Ashley nyoosha maelezo hatuelewi maana ya Wolverine Virus?”Aliongea Senga na Ashley alimwangalia Magdalena na kumtaka aelezee namna alivyokuwa Denisi wakati akipigana na Roma na Magdalena alianza kuelezea kila kitu.

“So dady!, he was loosing control , na kama sio uwezo wa Roma huenda madhara kwa watu wa katibu yangekuwa makubwa Zaidi , hiki kirusi hakiingii kwenye mwili wa binadamu kwa bahati mbaya , hivyo naamini kabisa kaka yangu alipokuwa China mwili wake ulikuwa ukifanyiwa sayansi ya kuingiziwa hiki kirusi”Aliongea Ashley na kufanya Damasi aanze kutokwa na machozi , aliamini swala la Denisi lilikuwa lishaisha asubuhi yake lakini kumbe ni mwendelezo wa matatizo.

“Unachotaka kumaanisha Ashley ni kwamba mwanangu mimi, Denisi alikuwa China kwenye maabara akifanyiwa majaribio ya kisayansi na kufanywa mnyama?”Aliuliza Senga na Ashley kwa huzuni aliitikia kwa kichwa.

“Okey kabla haujatueleza hayo kwa kina , ni njia gani ambayo unaamini inaweza kumsaidia kupona , sipo tayari kuona mtoto wangu anaishi kitandani kwa Maisha yake yote”

“Kwa vipimo vya haraka haraka vlivyofanywa na madaktari inaonekana mwili wake virusi hauna tena zaidi ya chembe zilizobaki katika mwili wake , jambo ambalo ni ajabu sana kutokea kwa mtu ambaye ana virusi vya Wolverine , kwa maneno marahisi naweza kusema kwamba Roma amemponyesha na kumuadhibu kwa wakati mmoja”Aliongea Ashley lakini wazazi wake walionekana kutokuelewa , hivyo ilibidi awape shule juu ya kirusi Wolverine kinavyofanya kazi kwenye mwili wa binadamu.

“Hivyo Roma alimuua Denisi ili mwili wake upate baridi ambayo itaathiri moja kwa moja kirusi cha Wolverine , kwani ili kiweze kiishi kwenye mwili wa binadamu kinategemea joto kuanzia nyuzi 36 mpaka 42 na zikishuka Zaidi ya hapo u kuongezeka Zaidi ya hapo basi kirusi kinakufa moja kwa moja na hiko ndio kilichotokea kwenye mwili wa Denisi , Roma alishusha joto la mwili wake ili kukiua kirusi na kisha akamrudishia uhai wake”

“Ashley unatuchanganya , Roma anawezaje kurudishia mtu uhai baada ya kumuua , mimi baba yako licha ya kwamba sijasoma kama wewe lakini akili yangu ni timamu na ndio maana naongoza taifa hili”

“Dad this is not about politics , it`s about Science you never heard of , Baba kwenye huu ulimwengu, gunduzi za kisaynasi ambazo zinatangazwa ni kwa ajili ya makusudi maalumu ambayo mara nyingi hubebwa na uanasiasa ndani yake, lakini pia kuna sayansi ambazo zinafanywa kuwa siri sana na yote haya ni kwa ajili ya matumizi ya baadae kwenya ajenda za watu wanaosimamia wagunduzi wa sayansi hizo”Aliongea Ashley

“Ashley hujajibu swali Langu bado , nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kama yule mpuuzi Roma anaweza kufufua watu”

“Senga Roma sio mpuuzi ni mwanao na anajua anachokifanya”Sauti ya Blandina ilisikika hakupenda Senga alivyomwita mtoto wake Roma hivyo aliamua kumtetea.

“Wewe Malaya kaa kimya” Raisi Senga alifoka.

Unadhani nini kitaendelea itakujia juma nne jioni.

napatikana watsapp kwa anaehitaji kujiunga nasisi kwenye grupu letu , tupo sehemu ya 320 nicheki 0687151346 nikupe utaratibu, grupu hilo halina mambo ya kuchati ni simulizi tu.
 
Ok let's wait.
Mkuu singanojr naupate hui WhatsApp, na huko Kuna kusubiria subiria kama huku au ni mwendo wa "Weka bandua?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…