Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Leo mzigo naamini unatupiwa kama wote
Bila shaka yupo hatua za mwisho..anauweka sawa piga lip, plaster, nilu, na weekend hii naamini kutakuwa na mi epsode ya kutosha.
 
SEHEMU YA 271

Ilikuwa ni siku ya Linda kufahamu ukweli juu ya mtu ambaye alijitambulisha miaka ya nyuma kwa kujiita X , Linda ambaye siku zote alikuwa akiamini huenda X akawa The Doni alijikuta akishangaa mno baada ya kupewa maelezo na Pastor Cohen , mshangao ambao kwa wengine walichukulia kawaida tu kwani hata wao pia walikuwa wamepitia kwenye sintofahamu kama aliokuwa nayo Linda.

Ni siku ya Jumamosi ndio siku ambayo kikao kilikuwa kikifanyika ndani ya nyumba ya Afande Kweka , kikao ambacho kilihudhuriwa na Ally Assad moja ya mgeni ambae Pastor Cohen aliwaahidi Mellisa na wenzake juu ya kukutana nae , mgeni ambaye alikuwa rafiki wa karibu na Hades wa zamani.

Ally Assady alijitambulisha kwa wageni waliokuwa mbele yake , watu ambao hawakuwa wakimfahamu na alijitambulisha kwa kusema kuwa yeye ni moja ya watu waliokuwa karibu sana na Hades na alikutana nae miaka mingi kidogo na ni Hades wa zamani aliemwambia juu ya mipango yote ambayo inaandaliwa na Athena.

"Kati yenu hapa mimi pekee ndio nilikutana ana kwa ana na Hades wa zamani , naelewa Pastor Cohen umekuwa ukitimiza maagizo mbalimbali kutoka kwa Hades wa zamani toka siku ambayo amejitambulisha kwako kwa siku ya kwanza".

"Komredi nilifikiri ulishakutana tayari na Hades wa zamani mpaka sasa??"Aliuliza Afande kweka , ukweli mzee huyu aliamini Mchungaji alikuwa ashakutana na Hades wa zamani lakini anashangaa Assad akisema kwamba hajawahi kuonana nae.

"Ni kweli sijawahi kukutana na Hades wa zamani ana kwa ana licha ya kuwa na mawasiliano nae ya karibu na nimekuwa nikiomba sana ajitokeze kwangu , lakini aliniambia anayo sababu ya kutojitokeza na mpaka leo hii hakuwahi kuniambia ni sababu gani aliokuwa nayo"Aliongea Pastor Cohen.

"Cohen , Master anasababu kubwa ya kutojitambulisha kwako na juu ya sababu hio sitaizungumzia kwa siku ya leo , tumekutana hapa kuzungumza yale ambayo yamenifanya kuja hapa nchini" Aliongea Assad licha ya kwamba rafudhi yake iliathiriwa na lugha ya kiarabu lakini maneno yake yalikuwa yamenyooka na ya kueleweka.

"Wote mliopo hapa inamaanisha jambo kubwa sana na maneno ambayo ninakwenda kuongea ndio maneno ambayo Hades wa zamani alinieleza nianze nayo kuwaambia kwa niaba yake"Aliongea na akavuta pumzi na kisha akaendelea.

"Ni wapongeze kila mmoja kwa kazi nzuri , tumeweza kukutana kwasababu ya misheni tulizokuwa nazo , misheni ambazo Hades alitupatia na kuzitimiza" Alivuta pumzi na kisha akaendelea

"Mellisa una swali ??" Aliuklliza Cohen mara baada ya Mellisa kuonekana kutaka kuongea.

"Ndugu Sheikh Ally Assad nadhani kabla haujaendelea utuweke wazi kabla ya kukutana na Hades na baada ya kukutana nae ulikuwa ukifanya kazi gani, lakini pia unaonekana kufahamu vyema lugha ya kiswahili"

"Swali zuri Linda ni kweli naijua lugha ya kiswahili kutokana na kwamba niliishiTanzania kabla ya kuhamia Marekani kwa ajili ya huduma ya kidini, kama nilivyosema wote tupo hapa kutokana na kazia ambazo zilitukuta nyuma hivyo ndivyo ilivyo kwangu pia , nilipokuwa nchini Marekani nilipatwa na changamoto ambayo ndio hio iliionifanya kukutana na Hades"

*****

Ni takribani lisaa Roma bado alikuwa ndani ya chumba alicholazwa Denisi , Edna na Blandina walioketi nje sehemu ya kusubiria ndio ambao walikuwa na wasiwasi, licha ya kwamba walifurahi Roma kumsaidia Mdogo wake Denisi kupona lakini maneno ya Roma juu ya jambo hilo kuwa la hatari yaliwafanya kuwa na wasiwasi.

Upande wa Damasi pia alikuwa na wasiwsi tofauti ya kwake ma wengine ni kwamba alikuwa na hofu kwamba Denisi anaweza asipone huo ndio wasiwasi wake mkubwa , jambo ambalo hata kwa Ashley aliliona na ilibidi amsogelee mama yake na kumtoa wasiwasi kwa kumwambia kwamba anaamini Roma atamsaidia Denisi kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida .

Roma aliekubali kumsaidia Denisi alitoa ombi la kuachiwa uhuru wa kuwa yeye pamoja na Denisi pekee ili kufanya matibabu yake kwa namna ya siri , haikueleweka ni kwa namna gani anakwenda kumponya Denisi , lakini jambo hilo lilionekana kuchukua muda.

Baada ya kama dakika tano hivi kupita mlango wa chumba cha matibabu hatimae ulifunguliwa na mtaalamu Roma Ramoni huku akionekana kutokwa na Jasho jingi, Edna na Damasi ndio waliokuwa watu wa kwanza kuinuka na akafuatia Blandina.

Edna alimshika Roma mkono kwa hiari yake kwa mara ya kwanza , haikueleweka mrembo huyu alikuwa akiwaza nini dakika kadhaa zilizopita lakini alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno , alijiambia yote hayo yalitokea kwasababu yake.

"Roma vipi hali yake??"Aliuliza Damasi na Roma alimpa ishara ya kwenda kumuona mtoto wake , Edna aliejisahau kamshika mkono Roma alijikuta akimwangalia Roma kwa wasiwasi hakuwahi kumuona akitokwa na jasho kwa namna hio .

Blandina , Mage na Magdalena pia walionekana kuwa na wasiwasi pia nakushangazwa na muonekano wa kichomvu wa Roma.

"Kazi yangu nimemaliza na sasa napaswa kuondoka sitaki kubaki hata sekunde moja hapa".Aliongea Roma na kisha alimwangalia Edna aliekuwa amemshika mkono huku macho ya wasiwasi yakimwangalia , kwa mara ya kwanza Roma anamuona Edna akimwangalia kwa macho ya wasiwasi.mno.

"Mnaweza kumuona mgonjwa mimi nitatangulia" Aliongea Roma .

"Tutaondoka wote"Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

Blandina alijikuta akiridhishwa na muonekano wa Edna , unajua siku zote mama atapenda mtoto wake kuwa na mtu ambaye ataijaza nafasi yake , kwa mfano mama atataka mtoto wake wa kiume apate mke ambaye atampenda kwa dhati na hivyo hivyo kwa mtoto wa kike atapenda mtoto kupata mume anaempenda kwa dhati ili hata kama hayupo duniani apumzike kwa amani na ndio maana siku zote wazazi wanapenda sana kuona watoto wao wakioa na kuolewa kabla ya wao kwenda mbele za haki na hiki ndio ambacho Blandina alikuwa akihisi kwenye moyo wake , Edna kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Roma ndio alichokiona na kujikuta akiridhika.

"Roma utaondoka na Edna mimi nitakuja na hawa mapacha " aliongea Blandina na Mage aliekuwa kimya muda wote alimwangalia Roma kwa kuibia na kuona wivu , alitamani nafasi ya Edna iwe yake na mama mkwe amwambie aondoke na Roma.

Roma hakuleta ubishi , kwasababu mke wake ndio alitaka waondoke wote hivyo alikubali na wakaongozana wakiwaacha Mage na Magdalena wakiingia chumba cha matibabu kuangalia hali ya Denisi.

"Wife utaendesha" Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kuzunguka upande wa dereva.

Roma baada ya kuingia ndani ya gari alijibwaga na kujiegemeza kwenye kiti na kufumba macho na kumfanya Edna amwangalie kwa sekunde kadhaa kabla ya kuwasha gari.

"Pole"Aliongea Edna kwa sauti ya chini na kumfanya Roma afumbue macho kivivu na kumwangalia.

"Babe Wife pole ya nini tena?"

"Sijawahi kukuona ukitoka jasho namna hio , inaonekana ilikuwa hatari kama ulivyongea , nilikuwa na wasiwasi"Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

"Hupaswi tena kuwa na wasiwasi ni kweli ilikuwa ni hatari lakini sio kwa upande wangu bali kwa Denisi"Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa kukubali huku akikaza macho barabarani.

Upande wa hospitalini Denisi afya yake iliwashangaza hata madaktari , kwanza kabisa alikuwa asharejewa na fahamu zake tofauti na mwanzo lakini pia viungo vyake vya mwili vilikuwa vikifanya kazi na kutoa ushirikiano kwa kiasi kikubwa jambo ambalo lilimfurahisha sana Damasi , ule wasiwasi uligeuka furaha , hawakujua ni namna gani Roma aliweza kumponya Denisi lakini yote hayo hawakujali tena , walijali uzima wa Denisi.

Blandina na mapacha yaani Mage na Magdalena walijawa na ahueni baada ya kuona hali ya Denisi inaimarika sana.

*****

Mheshimiwa Senga aliekuwa na hasira kila akikumbuka sura ya Blandina, alishituliwa na simu yake ya mkononi aina ya I phone iliokuwa inaita , aliangalia jina na kuvuta pumzi na kisha akapokea na kuweka sikioni, na muda huu alikuwa Ndani ya ofisi yake ya Ikulu kiendelea na majukumu yake ya kazi kama kawaida.

"Mheshimiwa za wakati huu ??"Ilisikika sauti upande wa pili

"Salama kabisa Askofu , vipi kwa upande wako?"

"Mambo sio mazuri sana Mheshimiwa kama tulivyopanga"Ilisikika sauti ya mwanaume upande wa pili.

"Kuna shida gani Askofu??"

"Mheshimiwa nadhani unataarifa juu ya kifo cha Salah ??"

"Ndio nimepata habari hizo leo , nimesikitishwa sana na jambo hilo"Sauti upande wa pili ilionekana kuwa kimya kwa Sekunde , ni kama mtu aliekuwa akiongea na mheshimiwa alikuwa akifikriia cha kusema.

"Mheshimiwa ni vyema kama.umesikia juu ya kifo chake ,swala ambalo limeleta mkanganyiko ni kutokana na Mzee Maya mwenyewe ambae ni mfiwa wa mtoto wake , kifo cha Salah kimesababishwa na Roma Ramoni na Mzee Maya anahusisha familia yako yote juu ya kifo cha mwanae , Mheshimiwa labda nikueleze swala ambalo hukulifahamu hapo kabla , Mzee Maya ndio mkuu wa Koneksheni na yule mtu" Sauti ilikoma na kumshangaza sana Raisi Senga hakuwa na taarifa hio na ndio kwanza anafahamu.

"Askofu unamaanisha."

"Mheshimiwa kabla ya Ibada ya Mpasuko wa Mwezi nataka kwanza kusikia msimamo wako juu ya swala la uhusikaji wa Roma kwenye kifo cha Salah???" Mheshimiwa Senga ukweli mpaka hapo alishindwa kujua ajibu nini kwanza hakujua kwamba watu walikuwa wakifahanu swala la uhusiano wake na Roma na swali la mtu anaeitwa Askofu kwake aliliona kama la mtego.

"Askofu how much do you know about Roma Ramoni???"
 
SEHEMU YA 272

Mheshimiwa Senga licha ya kwamba aliuliza swali lake lakini kwenye akili yake alikuwa akiamini watu wanaohusika na ibada ya Mpasuko wa mwezi walikuwa ni hatari mno kutokana na kujipandikiza kila mahali , hivyo hata swali lake la juu ya Roma aliamini kabisa watu hao watakuwa na majibu , lakini kabla ya kuweka wazi kile alichokuwa akikifahamu kuhusu Roma hakutaka kukiweka wazi moja kwa moja , hakufanya hivyo kwa mapenzi kwa Roma bali ni kwa ajili yake na familia yake aliamini swala la Blandina kama litafahamika kwa watu wengi basi litaleta shida kisiasa na maadui zake wanaweza wakalichukulia kama fimbo ya kumchapia nayo na ndio maana hakupenda sana kulizungumzia , lakini hata hivyo aliamin kwa upande wa watu wanaohusika na Ibada ya mpasuko wa mwezi swala hilo ni tofauti kwani wana watu wengi mpaka serikalini ambao hata yeye mwenyewe hakuwa akiwafahamu , na hata atake kuwafahamu swala hilo lilikuwa gumu kwani ibada hizo zilikuwa zikifanyika kwa siri sana na pia mtu yoyote ambae ni mwanachama ni ngumu kumfahamu kwani siri ndio moja ya itifaki inayofuatwa na kila mwanachama.

"Mheshimiwa, Mzee Maya anafahamu Roma ni mtoto wako na Blandina , ndio maana nakuuliza msimamo wako juu ya hilo maana mpaka sasa swala hili linafahamika kuwa moja ya siri kubwa"Aliuliza.

"Ni kweli kabisa Roma ni damu yangu lakini hii haimaanishi kwamba nimemkubali kama mwanangu ,msimamo wangu kwasasa ni kwamba, haitotokea siku nikamtambua Roma kama mwanangu na mambo yote anayoyafanya sitaki yahusishwe na familia yangu , huo ndio msimamo wangu"

"Mheshimiwa una uhakika na haya maneno ??"

"Nipo na uhakika kwa asilimia mia moja na jambo hili , Sina uhusiano wowote na Roma"Aliongea mheshimiwa kwa sauti kavu kabisa na alionekana hakuwa na mapenzi kabisa na Roma na alijiambia hana cha kupoteza , hakujali uwezo mkubwa Roma tena licha ya kusoma faili lake , yeye alichoamini kwa muda huo ni hisia zake tu .

"Okey mheshimiwa hili swala nitawakilisha kama lilivyo kwa mzee Maya ili lisiathiri mipango yetu"Ilisikika sauti na kumfanya Mheshimiwa Senga kuvuta pumzi.

"Asante sana Askofu naamini ratiba haitobadilika??".

"Hakuna kitakachobadilika ili mradi nishasikia msimamo wako mengine niachie mimi" Aliongea na kisha akaaga na kukata simu.

********

Ilionekana Sheikh Ally Assad alikuwa pia na historia zinazofanana na ya kwake , kwa maelezo yake ni kwamba yeye alikuwa akiishi Tanzania na alihamia Marekani kwa makusudi ya kwenda kueneza dini ya kiislamu ndani ya nchi hio , jambo ambalo baada tu ya kulianza ndio msururu wa matatizo ulipoanzia , yeye nia yake ikikuwa ni thabiti katika kueneza dini lakini Serikali ya Marekani ilimchukulia kama mtu ambaye alikuwa akieneza ugaidi , mwanzoni alikuwa akifanyiwa uchunguzi tu wa kawaida pasipo kuzuiliwa kifungoni lakini mambo yaliharibika baada ya tukio la.Afshar Bahman kumiminia watu risasi ndani ya jimbo la Texas huko Marekani.

Kila mmoja alishangaa baada ya kusikia kwamba Ally Assad alikuwa akihusishwa na tukio hilo .kwani stori ya Phill ilikuwa ikihusiana kabisa na tukio la mauaji lililotokea miaka kadhaa nyuma huko Marekani , tukio la bwana Afshar Bahman kumiminja risasi waumini wa kanisa ka The Forgiven siku ya mkesha wa Christmass.

"Sheikh ilikuwaje na kwanini tukio lile likaunganishwa na wewe?"Aliuliza Mellisa kwa mshangao kwani hata yeye pia alikuwa akikumbuka vyema tukio hilo , kwani liliteka hisia za raia wengi kipindi hiko.

"Afshar Bahman ni moja ya waumini na wana harakati ambao tulikuwa pamoja katika swala la uenezaji wa dini , tofauti yangu na Afshar Bahman

ni kwamba mimi nilifika Marekani kwa ajili ya kueneza Dini na Afshar yeye alifika Marekani kwa ajili ya kutafuta maisha akiwa anatokea Irani"

"Shekh Ally una uhakika kwamba Afshar alikuwa nchini kwa ajili ya kutafuta maisha au alikuwa na Ajenda nyingine ??"

"Kama alikuwa na Ajenda nyingine basi ajenda hio iliibuka akiwa Marekani lakini mimi niliemfahamu Afshar kwa miaka mingi hakufika Marekani kwa ajili ya kushambulia waumini wa kanisa "

"Unamaanisha nini kusema kwamba kama ni Ajenda hio aliipatia hapo hapo Marekani na ni kwa kiasi gani ulikuwa ukimfahamu Afshar mpaka kufikia kwenye hitimisho la kuamini Afshar hakuwa mtuhumiwa"Aliuliza Phill knight moja ya mhangwa wa tukio hilo na mabadiliko yake yalionekana dhahiri kwa kila mmoja lakini Sheikh Assad alionekana kuwa mtulivu.

"Afshar hajawahi kunificha kitu na mimi ndio mtu niliempokea baada ya kufika Marekani na natambua kabisa alikuwa mwanajeshi wa jeshi la Irani kabla ya kuja Marekani , je Bwana Phill kwenye habari ya uchunguzi uliotolewa na FBI walitoa wasifu wa Afshar kuwa mwanajeshi wa Irani??"Aliuliza na Phill alitingisha kichwa akiashiria taarifa hio ni mpya na hata hao FBI hawakuwahi kuitoa.

"Hapo ndio walakini unapoanzia"

"Sheikh nini kilitokea mpaka ukaweza kuonana na Hades?"

"Swali zuri Miss Zoe Kovac ,licha ya swala hili sikutaka kulizungumzia kwenye kikao hiki lakini nawiwa kusema kwa uchache, kwanini niliweza kuonana na Hades wa zamani"

"Kwanza niseme Pastor Cohen ndio mtu wa kwanza kuonana na Hades kabla yangu na hata Hades mwenyewe alinieleza hilo ....."

Sheikh Assad anasema baada ya tukio la Texas kutokea alikamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani , masalani FBI kwa ajili ya mahojiano , moja ya sababu ya kuwa mshukiwa wa kwanza ni .kutokana na ukaribu aliokuwa nao na Afshar Bahman, hivyo FBI hawakumchukua Assad kama ndugu wa karibu wa Afshar bali walimchukulia kama mhalifu ambae ameshirikiana na Ashar Bahman , jambo ambalo halikuwa kweli kwani Yeye alikuwa akieneza dini , dini ambayo msingi wake ukikuwa ni unyenyekevu pamoja na Amani , lakini licha ya kujitetea wanausalama hawakutaka kumuelewa na walitaka taarifa inayomuhusu Afshar Bahman kuhusiana na tukio pamoja na kupotea kwake katika mazingira ya kutatanisha lakini licha ya kuhojiwa hakuwa na namna ya kujibu kwani hakuwa akifahamu chochote na hapo ndipo alipofaulishwa kutoka kwa FBI kwenda idara ya CIA na hapo ndio mahojiano ya mateso yalipoanza , Assad anaelezea hivyo kwa kusema kwamba hakumbuki ni mara ngapi aliweza kupoteza fahamu kutokana na maumivu , lakini jambo la uhakika analokumbuka ni kujishtukia akiwa Saudi Arabia na kwanzia hapo ndipo alipokutana na Hades wa Zamani.

"Sheikh tukio lako linafanana sana na la kila mmoja wetu lakini haujatueleza kwanini Hades aliamua kujionyesha kwako"Aliongea Mellisa ukweli mwanamke huyu alikuwa na uchungu mwingi wa kutokumfahamu Hades , kwake ilikuwa ni kama kwa wanawake wengi kutamani nikuonana na mtu aliewaokoa , hivyo ni kama Mellisa alikuwa ashatenegwneza hisia za kimapenzi na Hades wa Zamani.

********

Ni muda wa jioni, Roma aliweza kipata simu kutoka kwa Mheshimiwa Jeremy , kwanza alishangazwa sana na simu hio kutoka kwa mzee huyo lakini hata hivyo alishindwa kukataa wito.

Muda wa makutano ilikuwa jioni saa kumi kamili za jioni hivyo mchana baada ya kupata chakula kilichoandaliwa na Sophia pamoja na Bi Wema alipumzika mpaka muda wa saa tisa na nusu ndio alimuaga Edna kuwa anatoka na hata Edna hakuuliza anaenda wapi , mrembo huyo siku hio hakurudi tena kazini na alikuwa bize kwenye chumba chake.

Aya Sophia Kigamboni ndio mahali ambapo Roma aliahidiana na mheshimiwa wa Rwanda kwa ajili ya kukutana na Roma kwakua alishakuwa na uzoefu na Kigamboni hivyo kuendesha mpaka ndani ya hoteli hio haikumpa shida kabisa kwani ndani ya madakika kadhaa tu aliweza kuingia ndani ya eneo hilo.

Ulinzi ukikuwa mkubwa kuashiria kuwa siku hio kuna mtu mkubwa ndani ya hilo eneo , Roma alipokelewa na bwana mrefu alievalia suri ambaye kwa mwonekano wake tu ni wazi utajua kuwa alikuwa Mrwanda.

Roma alifuatishana na mwongizaji huyo ndani ya eneo hili zuri kabisa kwa ufahari mpaka kwenye moja ya nyumba kati ya nyumba nyingi ndani ya eneo hili.

Nje kabisa ya mlango walionekana walinzi waliosimama kikakamavu huku wakionyesha kutoa ulinzi mkubwa mno na hawakutaka Roma kupita tu pasipo ya kumkagua kama hana siraha na Roma hakuleta ubishi kwania alijua hizo ni taratibu za kawaida sana pale unapokutana na kiongizi mkubwa , hivyo baada ya kusachiwa na walinzi kuridhika, walimruhusu Roma kuingia ndani.

"Mr Roma karibu sana"Sauti ya kiume ya Mheshimiwa Jeremy ilisikika kutoka eneo la Sebuleni na Roma alijongea kwa kujiamini mpaka kufika eneo la Sebule na kumuona Raisi Jeremy aliekuwa amesimama huku akiwa amevalia mavazi ya suti na kwa jinsi alivyoonekana ni kama ndani ua eneo hilo walichagua tu kwa ajili ya kufanyia mazungumzo , kwani hakuonekana kuwa amekuja muda mrefu kutokana na mpangilio .

"Nimekaribia mheshimiwa " Aliomgea Roma na kumpatia Mheshimiwa Jeremy mkono , na walisalimiana na kisba wakakaa.

"Mr Roma nashukuru sana kwa kutii wito wangu wa kuonana na mimi"

"Ni jambo la kawaida kwa mtu wa kutii wito , nadhani itakuwa jambo jema kwenda moja kwa moja kwenye mazungumzo" Aliongea Roma na Mheshimiwa Jeremy Alitabasamu na kisha akainua glass yake ya kinywaji , na pia muda ule alikuja muhudumu na glass nyingine na kinywaji.

"Hii wine ya Martel ni kinywaji bora ambacho naamini kila mmoja mnywaji anafurahia radha yake na ndio maana nimekiagiza kwa ajili yako kabka ya kufika hapa" Aliongea na kisha alimpa Ishara muhudumu kumimina kwenye Glass.

"Ni kweli kabisa ni moja ya kinywaji kizuri na nakipenda pia ,japo unywaji wangu wa Wine unategemena na taifa" Aliongea na mheshimiwa alitabasamu huku akiweka Glass yake chini na aliacha muhudumu kuondoka kabisa ndipo aanze mazungumzo.
 
SEHEMU YA 273
Mheshimiwa Jeremy licha ya kumuita Roma kwa ajili ya mazungumzo lakini hakujua namna ya kuanza kwani swala la Lorraine ni kama lilikuwa siri sana na kuuliza maswali moja kwa moja ilikuwa ikimaanisha kwamba ni lazima atobie siri ya kile kilichotokea miaka ya nyuma, lakini hata hivyo siku hio aliamini lazima atapata kitu kutoka kwa Roma na ndio maana alikuwa tayari kwa lolote.
"Mr Roma nimekuitia hapa kwa ajili ya jambo muhimu sana , jambo ambalo linahusiana na maisha yangu muhimu , ni kama stori na Stori hio nimeweza kugundua na wewe unahusika"
"Mheshimiwa huna haja ya kuzunguka na kuongea kisiasa , mpaka kuja hapa nilikuwa najua unataka kufahamu kuhusu Seventeen"Aliongea Roma na kumfanya Jerrmy kushangaa kwani hakujua jina la Seventeen.
"Seventeen?? Ndio nani Mr Roma?"Haikueleweka kama ni kweli mheshimiwa hajawahi kusikia jina la Seventeen , lakini kwa muonekano wake kama ni kuigiza basi tungesema uigizaji wake ni wa asilimia mia moja , yaani hakukuwa na chembe ya Jeremy kumfahamu Seventeen.
"Namaanisha pacha wa Mke wangu Edna , ndio namzungumzia kwani ndio jina lake" Aliongea Roma huku akimimina wine yote kwenye glass na kunywa yote huku akimwangalia mheshimiwa.
Raisi Jeremy sasa anaelewa kuwa Lorraine jina lake lipya ni Seventeen na alijikuta akivuta pumzi maana alitegenea mazungumzo yake na Roma kuchukua mida mrefu kidogo , lakini aliona Roma kama ilivyo kwa jina lake la Hades alikuwa akijua ukweli wote juu ya yeye na Raheli lakini pia juu ya mtoto wake , Raisi Jeremy tumaini jipya lilianza kuchipua aliamini kama Roma anamfahamu Seventeen ambaye ndio Lorraine basi ni uhakika kwamba Lorraine hakufa kwa ajali ile ya ndege na yupo hai.
"Mheshimiwa naona sura ya wasiwasi imekutoka??"
"Mr Rona nikushukuru sana kwajua mtu wa kunyossha maelezo , umemtaja Seventeen ambaye mimi namjua kama Lorraine naomba unielezee kuhusu Seventeen kama yupo hai na maisha yake kwa jumla"
"Seventeen ashakufa mheshimiwa" Aliongea Roma pasipo kubadili mwonekano huku akichukua chupa ya wine nusu aliobakisha Raisi Jeremy na kuimimina yote kwenye glass yake.
"Mr Roma acha utani kama umemfahamu Seventeen basi yupo hai"
" Sina haja ya kuongea kwa mafumbo mafumbo napenda kuweka mambo wazi ili upambane na hali , kama ulikuwa unamtafuta Seventeen basi jibu ni kwamba ashakufa tayari na uache kumtafuta "
"Hapana Mr Roma ..How ?...no , She is alive"
"No she is dead"Aliongea Roma kwa hasira ni kama mtu baye hakuwa akitaka kusikia habari za Seventeen na alikuwa akitafuta kitu cha kumlewesha kwani chupa mbili za wine alizihakiki kwa kuzitingisha na kugundua zishaisha
Mheshimiwa Jeremy moyo wake ulikuwa na maumivu mno , licha ya kwamba alikuwa na hisia kwamba Lorraine amefariki kitambo ndio maana Roma akarudi Tanzania akiwa mwenyewe lakini hakukuzipa kipauambele hisia zake na hata pale siku zinapomjia mara nyingi amekuwa ni mwenye kuzipotezea na mawazo chanya.
Raisi Jeremy aliona hakuna namna ambayonRoma alikuwa akitania , moyo ulikuwa ukiuma baada ya kuthibitisha sasa mtoto wake kafa, Alichokifanya ni kutoa ishara kwa kijana wake aliekuwa mita kadhaa akitoa ulinzi na kumwambia aite muhudumu na pombe ziletwe na Roma alitabasamu.
"Mheshimiwa hupaswi kutumia kilevi kwasasa kwani una miadi na muwekezaji"
"Fanya hivyo leta vinywaji acha maneno mengi"Aliongea kwa Kirwanda na palepale msaidizi yule alitingisha kichwa na kuondoka na dakika chache mbele bia ziliwekwa mezani na mhudumu na kumiminia wateja na ile anamaliza tu kujaza mheshimiwa alichujua glass na kumeza bia yote.
"Mr Roma nataka unieleze kuhusu Loraine kwa kila kiru nataka kujua namna alivyoishi , alivyokuwa mkubwa alikuwa akifanania vipi , nieleze kila kitu kuhusu Seventeen" Aliongea huku macho yake yakianza kuwa mekundu na Roma aklitabasamu na kisha akaweka pombe kwenye glasa na yeye na kisha akashusha yote .
"Seventeen anafanana na mke wangu Edna kwa asilimia nyingi nadhani hilo linadhihirisha kuwa ni mapacha hivyo sina cha kukuambia kingine" Aliongea Roma na Jeremy aliendendwelea kushusha glass za bia mfululizo.
"Ni mwaka gani na tarehe ipi alikufa??
"Miaka kama minne iliopita mwezi wa saba tarhehe 20"Aliongea Roma na kumfanya Jeremy amwangalie kwa mshangao kidogo .
"Kwahio alikuwa mzima wa afya miaka yote hio pasipo mimi kufanikiwa kumtafuta .."Aliongea huku akionyesha hali ya kuwa na hatia.
"Hata kama ungejaribu usingefanikiwa"
"Unamaanisba nini?"
"Maisha ya Seventeen yalikuwa ya tofauti sana na raia wengine hivyo hata uwepo wake duniani unajukikana kwa watu wachache sana na kama ungemtafuta usingempata,mheshimiwa kwa sasa jikite kwenye kumueleza Edna ukweli, sidhani kama kuna haja ya kujificha zaidi"Aliongea Roma
"No!"Alijibu Jeremy
"What , usiniambie humtambui Edna kama mtoto wako"
"Hata kama namtambua siwezi kumpokea na kutangazia umma kama nina mtoto niliezaa nje ya ndoa, wananchi wangu hawatonielewa na inaweza nisababishia matatizo"Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
"Kwa maneno marahisi ni kwamba haupo tayari kumpokea Edna kama mtoto wako na haitakuja siku ukamueleza ukweli?"
"Mr Roma unaweza ukanifikiria kama mimi ni baba mbaya sana na sistahili kabisa kuitwa baba , lakini amini nakuambia Edna ni mtoto ninaempenda na nitaendelea kumpenda , lakini jambo moja tu ambalo ni kikwazo kwangu ni kwasababu mimi maisha yangu sio yangu bali ni ya wananchi wa Rwanda , as long as naendelea kua kiongozi basi jua haitokuja kutokea siku nikamtambulisha Edna kama mtoto wangu hadharani , mambo yatakuwa hivi hivi kama ilovyokuwa kila siku"Aliongea na kisha akameza pombe yote kwenye glass .
"Unaongea upuuzi"Aliongea Roma huku akimwangalia Jeremy kwa macho ya Dharau na tabasamu lake feki.
"Inawezekana Mr Roma ila ukweli ndio huo , Edna ataishi kwenye moyo wangu na nitamsapoti kwa siri kama nilivyokuwa nikifanya lakini sio kumtangaza kama mtoto wangu"
"Unaonekana kulewa madaraka , hivi unafikiri maneno haya Edna akiyasikia atajihisi vipj , ushawahi kufatilia maisha yake ya nyuma namna alivyoishi na baba yake , unajua ni kiasi gani na yeue anahitaji malezi ya baba lakini upo zako hapa na tumbo lako unaongea ujinga , stupidi kabisa"
"Mr Roma kuwa na heshima kwa mheshimiwa na punguza maneno yako ya kejeli"Aliongea bodigadi baada ya kusikia maneno ya juu.
"Naongea ukweli kumrekebisha huyu raisi wako mpumbavu ambaye anahisi madaraka ni bora zaidi kuliko familia yake" Aliongea Roma na palepale bodogadi alitoa siraha yake lakini Jeremy alimpa ishara ya kutulia.
Ukweli maneno ya Jeremy yalimuumiza sana Roma , hata yeye mwenyewe aliishi maisha ya kutokuwa na baba na mama kwenye maisha yake yote jambo ambalo limemfanya kutaka walau kuhisi inavyokuwa ukiwa na mzazi lakini yeye na ,Sevwnteen hawakuwahi kupata nafasi hio kwenye utoto wao kabisa , waliishi kama watoto yatima maisha yao yote , sasa jambo hilo anaona linaenda kujitokeza kwa Edna mke wake , alijua lazima Edna angeumia kama angefahamu baba yake hakuwa akimtaka na yeye kwake madaraka ni bora zaidi.
"Nasikita kuona nimekuja hapa kupoteza muda wangu kwa ajili ya kuongea na wewe , sidhani hata kama ni Seventeen ungemjali kuliko madaraka yako , ninaondoka"Aliongea Roma na kisha akanyanyuka na kuanza kupiga hatua kutoweka eneo hilo.
"Mr Roma naomba umjali sana Edna na kumlinda kwa niaba yang..."Kabla hajamaliza sentensi yake alijikuta akisimamishwa na nguvu ya ajabu na kukabwa shingo huku akining'ia jambo ambalo lilimfanya bodyguard kutoa Siraha yake lakini Roma alijikinga na mwili wa Raisi Jeremy huku akiendekea kumkaba shingoni.
Dakika mbili zilikuwa nyingi sana na ni kama chumba kilikuwa na Kamera kwani wana usalama waliingia na siraha zao zikiwa juu kuachia Shambulio.
 
SEHEMU YA 274
Roma hakutaka kumdhuru Raisi Jeremy , alichokifanya ni kujaribu kumuonya tu na ndio maana baada ya walinzi kuingia alimwachia na kisha kutoka , walinzi walitaka kumzuia Roma , lakini Raisi Jeremy aliwapa ishara ya kumuacha aondoke zake.
Mazungumzo yalianza kwenye muda wa saa kumi na mbili hivyo mpaka Roma kumaliza kuongea na raisi Jeremy ilikuwa ni saa kumi na nusu ikimaanisha kwamba wametumia lisaa limoja kumaliza maongezi yao.
Roma hakutaka kurudi moja kwa moja nyumbani, mudi yake haikuwa nzuri kwani maongezi yanayomhusu Seventeen mara nyingi yanapozungumziwa huwa yanaharibu kabisa mudi yake na anakuwa mwenye mawazo na ndio maana alijiambia atafute sehemu tulivu kwa hapo Kigamboni kwa ajili ya kutuliza kichwa.
Mikadi Beach ndio sehemu ambayo aliona inamfaa kwa kupotezea muda, hakuwahi kufika ila alitumia uwezo wa gari yake kutafuta uelekeo na ndani ya dakika moja tu alikuwa ashakaribia.
“Kaka samahani nipo hapa kwa ajili ya kuwa peke yangu sihitaji kampani”Ilisikika sauti ya mwanamke mrembo ndani ya fukwe hii ya Mikadi, mwanamke ambaye kwa siku hio alionekana kama kivutio kwa wanaume wengi waliokuwepo hapo na kwa jinsi mwanadada huyu alivyokuwa akilalamika ni dhahiri kabisa kwamba amesumbuliwa na wanaume wengi sana tokea ajipumzishe, na hii lilidhihirika kwani alimkataa mwanaume aliehisi uwepo wake pembeni yake pasipo kumwangalia usoni , kwani muda huo mrembo huyu alikuwa amejifunika usoni na kofia yake aina ya Hat huku akiwa ameegamia kwenye viti vilivyojengwa ndani ya eneo hili kwa ajili ya mapumziko.
“Babe Nasra inaonekana Mungu ndio kanileta hili eneo”Aliongea Roma na kumfanya mrembo yule kutoa ile kofia na kumwangalia mwanaume eliekuwa mbele yake , mwaaume ambaye alimkataa sekunde kadhaa zilizopita kwa kumdhania kuwa ni walewale wanaume ambao walikuwa wakimsumbua , ndio alikuwa ni Nasra.
“Roma! , Unafanya nini hapa?”Nasra aliuliza kwa mshangao huku akimwangalia Roma aliekuwa mbele yake , ni kama hakutegemea kabisa kumuona na mapigo ya moyo wake yalienda mbio.
“Oya nadhani yule ndio mwenye mali wazee”Sauti upande wa pili ilisikika kwenye meza ambayo imekaliwa na vijana wanne ambao walikuwa wapo hapo Ufukweni kupunga upepo kwa siku hio ya Wikiend.
“Daah! Wanawake bwana , kama ni kweli basi hawa viumbe sio wa kueleweka kabisa yaani ananikataa mwanaume Hb kama mimi halafu awe na mwanaume kama yule”Aliongea mwanaume mmoja kuunga mada na alionekana alikuwa ametupia ndoano kwa Nasra na akachomolewa na sasa yupo kwenye mshangao baada ya kuona Nasra anatoka ushirikiano kwa mwanaume ambaye hakuwa na mwonekano mzuri kama wake.
“Haha.. hivi viumbe wewe achana navyo kabisa Abduli, kila mtu na bahati yake”Aliongea na kufanya wenzake kucheka na kisha waliendelea kuangaliia upande ambako mwanaume ambaye hawakumfahamu akiongea na mrembo waliemshindwa.
Upande wa Nasra alionekana kutomtegemea kabisa Roma eneo hilo na ndio maana alishangaa uwepo wake.
Nasra Baada ya kumsindikiza rafiki yake Najma kuondoka kuelekea masomoni nchini Marekani hakulala nyumbani kwake kabisa , akili yake haikuwa imetulia na alikuwa kwenye mawazo na ndio maana aliamua kutafuta sehemu ya kutulia na , sehemu ambayo aliona inafaa ni Mikadi Lodge na ndio maana hata Roma jana yake alivyoenda nyumbani kwa Nasra hakumkukuta.
“Babe Nasra unajua ni kwa kiasi gani nimekutafuta?”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kiti cha pembeni na Nasra muda wote alikuwa akimwangalia Roma , ni kama mambo mengi yalikuwa yakipita kwenye kichwa chake na hakuwa na namna ya kuelezea.
“Roma naomba uondoke”Aliongea Nasra kwa sauti ya chini na kumfanya Roma kutabasamu aliona mrembo huyu bado yupo na hasira na yeye na hilo hakujali hata kidogo na alijiambia huo ndio muda mzuri wa kuyajenga.
*******
Upande mwingine Edna alionekana akipitia karatasi zilizokuwa kwenye mikono yake , swala la Kampuni ya Maya bado lilikuwa likimuumiza sana kichwa na hii yote ni mara baada ya kugundua kuwa jina la kampuni hio lipo kwenye orodha ya kampuni zilizoorodheshwa kwenye nyaraka ambayo mama yake ameacha nyuma , orodha ya kampuni ambayo aliitafsiri kama sehemu ya malipizo ya kisasi ambacho alikuwa nacho mama yake Raheli na yeye mwenyewe hakufahamu ni kisasi juu ya nini.
Alijiambia lazima kuna kitu kilitokea kati ya kampuni hii ya Maya na mama yake na ndio maana ilikuwa kwenye orodha , lakini mpaka muda huo hakuwa akifahamu ni muunganiko wa namna gani ambao upo na ndio maana alijiambia ni lazima atumie akili zake zote na rasilimali alizokuwa nazo kutafuta muunganiko huo.
Alijikuta akiangalia baadhi ya vitabu vilivyopangwa kwenye chumba hiki ambacho kilikuwa ni kama ofisi ya mama yake hapo kabla na kujikuta akiingia kwenye mawazo, ukweli akili yake ilikuwa imekwama kabisa kwani licha ya kwamba Suzzane amemtumia baadhi ya taarifa kwa kile kinachoendelea kwenye kampuni ya Maya lakini bado hakukuwa na muunganiko na kwa jinsi alivyokuawa akiangalia Shelf hizo zilizojaa vitabu ambavyo mama yake siku zte alikuwa akisoma ni kama alikuwa akitafuta wazo jipya.
Kampuni ya Maya ni kampuni ambayo inajihusiha na mambo mengi na hii ni kutokana na kuwa na ‘Subsidiaries’ nyingi ndani ya taifa la Afrika , ni kampuni ambayo ina makao makuu yake nchini India na inawekwa na majarida mbalimbali ulimwengu kama moja ya kampuni kubwa sana ambayo inaongoza katika maswala ya utafiti na utengenezaji wa madawa duniani na moja ya mafanikio yake makubwa yalitokana na kufanikiwa kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Ebola kupitia kituo chake cha utafiti kilichopo ndani ya taifa la Canada.
Mwaka 2001 ndio mwaka ambao walifungua tawi la kampuni yao hapa Tanzania na moja ya sababu kubwa ya mwanzilishi wa kampuni hii kupenda kufungua tawi hapa Tanzania ni kutokana na kwamba mke wake mkubwa alikuwa ni Mtanzania hivyo ni kama alifungua tawi hilo kwa heshima ya mke wake kuwa raia wa Tanzania.
Maya Hubat licha ya kwamba alikuwa mhindi , lakini pia alikuwa akilipenda sana Taifa la Tanzania na mara nyingi amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Tanzania hasa upande wa tiba , kwani mara nyingi alionekana akichangia sana michango katika hospitali nyingi lakini jambo kubwa pia kwa Kampuni ya Maya pia wanazo hospitali maarufu sana ambazo zimetapakaa kwenye mikoa yote mikubwa Tanzania.
Hivyo ni rahisi kusema kwamba heshima ya Mzee Maya imetokana na michango yake lakini pia uwekezaji wake hapa Tanzania,maswala hayo yote Edna alikuwa akiyafahamu na hata nyaraka zilizokuwa kwenye meza yake zilikuwa zikisema hivyo , alisoma kila kitu kilichokuwa kikihusiana na kampni ya Maya lakini hakuishia kwa kampuni ya Maya tu , lakini pia alisoma na mwanzilishi wa makampuni haya ya Maya na nia zake zote za kupendelea taifa la Tanzania katika maswala ya uwekezaji , lakini licha ya Edna kusoma nia halisi ya Mzee Maya kwa hapa Tanzania katika swala la uwekezaji , aliona kuna jambo ambalo bado halikai sawa, ni kweli kwamba Mzee Maya ameoa Tazania na mara nyingi amekuwa mtu wa kujinasibu kama moja ya watu wanaolipenda tafai la Tanzania kwani limempatia mke bora , lakini hata hivyo aliamini ni kama jambo la ziada kwa hayo yote , Edna alikuwa mfanyabiashara na siku zpte ukifikiria kibiashara Zaidi utajua kwamba kuna baadhi ya uwekezaji hata kama una mapenzi mengi na taifa husika huwezi kuufanya kwani hauwezi kukuletea faida Zaidi ya hasara na hili ndio aliliona kwa kampuni hii ya Maya , Mzee Hubati kuna uwekezaji ambao amefanya hakuona tija yake na kama yeye ndio mwamuzi mkuu basi asingejihangaisha kabisa katika kuwekeza hapa nchini na hili ndio lilimfanya aone kuna Zaidi ya sababu katika juhudi za kiuwekezaji kwa Mzee Hubati na alitaka kuzifahamu.
Edna wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo , akili yake ilikuja kutua kwene moja ya kitabu kilichokuwa kikionekana wazi upande w akushoto kwenye shelf , kitabu ambacho mara baada ya kukiona alikumbuka mama yake mara nyingi alimuona akiwa amekishikilia akikisioma enzi za uhai wake, alikiangalia kwa dakika kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kunyanyuka alipokuwa amekaa na kukisogelea na kukitoa kwenye shelfu na kurudi nacho kwenye meza yake na kuketi kwa ajili ya kukifungua na kuanza kukisoma , alikuwa akitamani kujua ni kitu gani ambacho mama yake alikuwa akikisoma mara kwa mara.
“One of her favourite book”Aliwaza kwenye kichwa chake akisema kwamba moja ya kitabu pendwa cha mama yake huku akigeuza geuza, baada ya dakika kadhaa ya kukigeuza aliamua kukifungua.
“Kumbe mama alikuwa ni mpenzi wa Mashairi?”Aliwaza Edna baada ya kugundua kuwa kitabu ambacho amekishikilia kina mkusanyiko wa mashairi ambayo yamewahi kuwandikwa duniani, ukweli mwanzoni hakuwa akijua kitabu hiko kilikuwa kikihusiana na nini kutokana na kutokuwa na kava ambalo lilikuwa likielezea nini kimeandikwa ndani yake , hivyo baada ya kufungua ndio aligundua kumbe ni kitabu ambacho kilikuwa kikihusu mashairi.
Edna wakati anafungua ukurasa wa pili kuna kitu kilidondka chini na kumfanya akiangalie na alikuja kugundua ilikuwa ni picha , aliweka kitabu chini na kuiinua na kuishikilia na kukuta sura ambayo inakuja na kupotea kwenye kichwa chake ni kama mtu aliekuwa kwenye picha alikuwa akimfahamu lakini hakuwa akikumbuka amemuona wapi, aligeuza nyuma ya picha hio na kuona kuna maandishi yalioandikwa.
“Sonnet 116 by Shakespeare , I dedicate it to you Rahel My Love”Ndio mwanzo wa maneno yaliosomeka juu ya picha alioshikilia Edna , maandishi ambayo yalikuwa yakimaanisha kwamba “Najitolea kukupa shairi hili mpenzi wangu Rahel, shairi la Sonnet 116 kutoka kwa mtunzi Williams Shakespeare.
Edna alijikuta akshangaa na hisia zake tayari zilimwambia mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni mpenzi wa mama yake na moyo wake ulipiga kite , kwani maandishi yaliofuatiwa yanayohusiana na shairi hilo yalidhihirisha upendo wa dhati sana kutoka kwa mwanaume aliekuwa kwenye picha kwenda kwa Rahel mama yake.
“This guy could be my father”Aliongea Edna akimaanisha kwamba mtu aliekuwa kwenye picha anaweza kuwa ndio baba yake.

SEHEMU YA 275
Saa moja na nusu ndio muda ambao Roma alirejea nyumbani , alionekana mudi yake imerudi na hio yote ni kutokana na kwamba yeye na Nasra mapenzi yao yamerudi kama zamani na ashatuliza hasira zote za mrembo huyo na mipango yao ya kwenda kijijini ilikuwa ikiendelea na zilikuwa zimebaki takribani wiki mbili mpaka kufikia siku yenyewe.
Mama yake Roma siku hio alionekana hakuwa nyumbani, lakini hakujali sana , Edna alionekana kuwa sebuleni akiwa ameketi pamoja na Yezi , Sophia na Bi Wema na walionekana walikuwa wakipiga soga na Roma alitabasamu kuona wanaendana vizuri na mke wake yupo kwenye hali ya kuchangamka.
Ukweli ni kwamba Edna hakumjua mwanaume aliekuwa kwenye picha , ni kweli sura yake ilikuwa ikija na kupotea lakini hakuweza kuitambua na kukumbuka aliiona wapi , hivyo hakutaka kusumbua kichwa chake , kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia kuwa mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni baba yake , lakini aliamua kupotezea , kwanza hakuwa na mpango kabisa wa kumfahamu baba yake na alijiambia labda baba mwenyewe ndio amtafute yeye , mrembo huyu hakujua kuwa mume wake Roma Ramoni alikuwa na maongezi mchana huo na baba yake mzazi , baba ambaye amemkataa mbele ya mume wake.
Sasa Edna aliona asiendelee kukaa zake chumba cha kujisomea na aungane na wanafamilia sebuleni.
“Roma jumatatu Yezi anatarajjia kuanza kufanya usaili Kwenda chuo , unapaswa kumsindikiza”Aliongea Edna na Roma alishangaa kidogo , ukweli mara nyingi ni kama Yezi alikuwa akimwepuka hivyo hakupata wasaa mwingi wa kuongea nae tokea warudi Ufarnsa na kumkuta nyumbani.
“Yezi umepata chuo gani?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Yezi , lakini Yezi alikuwa ni kama anamshangaa Roma.
Ukweli ni kwamba Yezi alikuwa akiangalia kicheni ambacho kipo kwenye shingo ya Roma na hii ni baada ya Roma kuinama wakati wa kukaa na ndipo kiliponekena , kidani ambacho yeye alimpatia kama zawadi, jambo lile kwake limemgusa sana kwani hakuamini kama Roma anaweza kuthamini zawadi yake na kuivaa shingoni.
“Mbona hunijibu unaniangalia tu”
“Kapata UDSM , yaani wewe Yezi ni mwanafamilia lakini umeshndwa hata kufuatilia maendeleao yake”Aliongea Edna na kumfanya Bi Wema kutabasamu namna Edna anavyomkosoa Roma na Roma lilimwingia kweli , kwani ni kweli hakuwa akifatilia sana maendeleo ya Yezi na ndio maana hata hakufahamu ni chuo gani ambacho Yezi amepata lakini ni wakati gani amabo Yezi kaanza kufanya maombi.
“Ni sawa tu Sister Edna , Anko ana mambo mengi”aliongea Yezi kwa namna ya kumtetea Roma na Edna alitaka kuongea neno ila alijiambia ngoja anyamaze.
“Okey wife Yezi mimi nitampeleka chuo siku ya jumatatu na kuhakikisha kafanya usaili”Aliongea Roma na Yezi alitabasamu.
“Simuoni mama, kaenda wapi?”Aliuliza Roma.
“Kaenda kumsalimia MzeeAtanasi, baba yake”Alijibu Edna na Roma alitingisha kichwa kuashiria kwamba ameelewa.
********
Kila mmoja alitamani kusikia jibu litakalotoka kwa Sheikh Assad , swali ambalo ameulizwa na Zoe Kovac kwanini Hades wa Zamani aliamua kujidhihirsha kwake ilihali hakufanya hivyo kwa wengine kama vile Pastor Cohen ambaye alionekana kuwa ni mtu muhimu katika mipango yake.
“Sababu ya Hades wa zamani kujionyesha kwangu , huenda ikawa ni kutokana na kazi kubwa ambayo alinipatia kuliko watu wote mliopo hapa ndani na wale ambao hampo hapa ndani , najua kila mtu amefanya kazi ambayo ina mchango mkubwa katika mipango ya Hades wa zamani kwa kila mtu na nafasi yake , lakini kwa upande wangu kazi yangu ilikuwa kubwa mno na nilikataa kuifanya mpaka ajionyeshe kwangu”
“Unamaanisha kwamba Hades , alikupa kazi kubwa kiasi kwamba ulikataa kuifanya na ukataka kwanza ajionyeshe kwako?”Aliuliza Pastor Cohen , ukweli ni kwamba hakujua kama kuna mtu ambaye anaweza kumzidi yeye kwa kufanya kazi ngumu , misheni zote ambazo zinaendelea mpaka kwa wakati huo Pastor Cohen aliamini zilianzia upande wake.
“Ndio kazi alionipa ilikuwa ngumu katika utekelezaji wake , kwani ilikuwa ni ya hatari , ya kujishusha, kudharaulika nahata kuonekana kichaa muda mwingine , hivyo ilihitaji uvumilivu mwingi”Aliongea.
“Ni kazi gani ambayo alikupatia ?”Aliuliza Afande Kweka aliekuwa kimya muda wote akigusa gusa ndevu zake zenye mvi.
“Najua wengi wenu hapa mnaamini kwamba nyie wote ni wanachama lakini hamjawahi kufahamu mpo kwenye chama gani mpaka mkaitwa kuwa wanachama na hii ndio ajenda kubwa ambayo imenileta hapa Afrika na kupitia Ajenda hio mtaweza kuelewa ni ipi kazi yangu ambayo nilikuwa nikifanya tokea nifike ndani ya mataifa ya Uarabuni”Aliongea na kisha akavuta pumzi ili kuendelea.
“We Are Ant-Illiminat Society”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa kwani ni kama hawakumuelewa kasoro upande wa Cohen.
“Nadhani sio mara yenu ya kwanza kusikia neno ‘Illuminat’ lakini ni mara yenu ya kwanza kusikia neno Ant-Illuminat?”Aliuliza Sheikh Assad na kunfanya wote hapo ndani kuangaliana , ni kweli walikuwa wakisikia juu ya neno Illuminat , lakini hawakuwahi kusikia neno la Ant-Illuminat.
Ant-Illuminat ni neno ambalo linamaana ya kinyume na neno lenyewe la Illuminat , yaani wapingaji wa jamii ya siri ya Illuminat ndio chama ambacho sheikh Assad alikuwa akizungumzia.
“Lazima tuelewe historia ya Illuminat kabla ya kuwa mwanachama halisi wa Ant-Illuminat , lakini sio hivyo tu ili uweze kuwa mmoja wapo wa jamii hii ya siri itakubidi kwanza ujue kila kitu kuhusu Illuminat na hii ndio kazi yangu ambayo nilipewa na Hades, kazi ya kujiunga na Illuminat.
“Your are Illuminat?”Aliuliza Mellisa kwa mshangoa.
“Yes , I am”Pastor Cohen alishangaa.
“But I am also Ant-Illuminat”Aliongea.
Mpaka hapo ni kama sasa wanaanza kupata picha ya kwanini Sheikh Assad alisema kazi yake ni ngumu sana kuliko wengine wote.
“Sheikh tupo kwenye kiza mpaka sasa , na nadhani litakuwa jambo jema kama utatuweka wazi , ili kila mmoja wetu apate kuelewa.”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Sheikh Assad kukubali na kuanza kuelezea.
Kwa maelezo yake ni kwamba baada ya kuokolewa na Hades wa Zamani na kupelekewa nchini Saudi Arabia kitu cha kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha Sheikh Assad kutoka kwenye hatia ya kutafutwa na CIA Pamoja na FBI na hilo kutokana na kwamba Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa upande wa mataifa ya kiarabu , hivyo kuongea na serikali ya Marekani kwa ajili ya kumfutia kesi Profesa Assad lilikuwa jambo jepesi sana ,h na serikali ya Saudi iliweza kufanya hivyo kutokana na uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya mfalme wa Saudi na Hades wa zamani.
Anasema baada ya kuisha kwa kesi hio ndio mwanzo wa kazi mpya ambayo alipewa kuikamilihsha naHades ama moja ya misheni yake na kazi yenyewe ilikuwa ni juu ya kujiunga na jamii ya siri ya Freemason.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Illuminati ipo ndani ya ufreemason , hivyo kujiunga kwake ndani ya jamii hii ilikuwa ni kwa ajili ya kazi moja tu , kutambua wanachama wote waliokuwa na asili ya Illuminat na hio ilikuwa kazi ngumu sana kwake kutokana na usiri wa jamii hizi.
Sheikh Assad baada ya kufanikiwa kujiunga na jamii hio alipewa kazi nyingine ya kushawishi mataifa ya kiarabu kuanza uwekezaji nje ya mipaka yake, hii haikuhusisha serikali tu bali mpaka kwa sekta binafsi, kwahio kazi hioi ilikuwa ikimaanisha kwamba ashawishi matajiri ambao wapo kwenye serikali za kiarabu kuanza kuwekeza kwenye mataifa makubwa , hususani yale yenye uchumi mkubwa , ikumbukwe mataifa ya kiarabu kwa asilimia kubwa wamejaaliwa utajiri wa mafuta hivyo kuwa na matajiri wengi ambao hawakufahamika kabisa duniani, hivyo kazi ya Assad ilikuwa ni kushawishi sasa hao matajiri.
Anasema kwamba licha ya kwamba ilichukua muda mwingi kufanikiwa kwa asilimia kubwa , lakini jambo hilo liliwezekana, kwani mpaka muda huo ni makampuni mengi ya kiarabu yameweza kushikilia taasisi nyingi duniani kwa kuzimiliki, ikiwemo vilabu vingi vya mpira kama vile Man City Club na PSG , kampuni za kimitandao kama vile Twitter na maeneo mengi muhimu ambayo yangeweza kuongeza ushawishi wa mataifa ya Kiarabu ulimwenguni.
“Kwanini Hades alichagua Zaidi mataifa ya kiarabu na akaacha mataifa mengine?”Swali zuri sana Zoe.
“Hades wa zamani anaamini kwamba roho nyingi ambazo zilivamia miili ya binadamu hazijatawala sana bara la Asia, hivyo kama Athena ataweza kufanikiwa katika mipango yake ni rahisi kwa sisi kutekeleza mpango wa dharula”Aliongea na kuwafanya wasielewe tena.
“Najua hamuwezi kuelewa maana ya maneno yangu , ila mtaelewa kadri siku zitakavyoendelea kusogea , kwasasasa hatua tunayokwenda kuanza nayo ni kuhakikisha tunatambua miungu yote kumi na mbili”
“Unamaanisha miungu yote kumi na mbili ya kigiriki?”Aliuliza Zoe kwa shauku.
“Ndio najua kwasasa tunamfahamu Artemis , Appolo na Hades na hatumfahamu Athena ni nani na kavaa mwili upi , hatumfahamu Poeseido nani na kavaa mwili upi , hivyo hivyo kwa Aphrodite ,Hermes , Ares na wengine”Aliongea.
“Sheikh Assad ,kuna umuhimu gani wa kufahamu hii miungu na kwanini Hades asingeweza kutuonyesha moja kwa moja kwani ni ndugu zake?”Aliuliza Nadia Alfonso na mrembo huyu aliekuwa kimya muda wote sasa alionekana kuelewa somo.
“Hades wa zamani katupatia kama ‘Assignment’ nah io inamaana kubwa sana kwetu katika kushindana na Athena na miungu mingine lakini hata hivyo Hades hatuwezi kutuambia”Aliongea.
“Roma anaifahamu miungu mingine?”Aliuliza Nadia kwamara nyingine.
“He is God , So he is aware of them and most of all there is god`s treaty?”Aliongea.
“God`s treaty?”
“Ndio kuna mkataba ambao wamesaini miungu yote kumi na mbili”Aliongea.
“Unahusiana na nini?”Aliuliza Pastor Cohen.
“Mambo mengi ambayo siyajui lakini jambo moja ninalojua kwa uhakika ni kwamba mkataba huo pia ulikuwa ukiwazuia miungu kutotajana wala kutoa siri juu ya miili waliovaa labda kwa matukio maalumu pekee”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa.

ALUTA CONTINUARA

CONTACT :0687151346 WATSAPP
 
Daaaah
 
Back
Top Bottom