SEHEMU YA 276.
Zilipita takribani siku sita na sasa ilikuwa ni siku ya ijumaa tena, katika siku zote hizo hakuna kilichotokea kwa Edna wala kwa Roma Zaidi ya Maisha ya kawaida waliokuwa nayo wanandoa hao kila siku.
Jambo moja kubwa tu ni kwmaba Edna alikuwa kwenye mawazo na hio yote ni baada ya jumapili iliopita Kwenda kituo cha yatima kwa minajili ya kumuona Lanlan , lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakuweza kumpata kabisa na hata alipoenda sehemu ambayo wanaishi , nyumba ilikuwa imefungwa na hilo lilimuongezea huzuni mrembo huyo kwani alikuwa amemkumbuka sana mtoto huyo.
Siku hii ya Ijumaa ilimbidi Roma Kwenda kwenye kampuni mpya ambayo imefunguliwa na mke wake Edna na hii yote ni mara baada ya kupigiwa simu na Daudi kwamba mwekezaji Rose Situ anataka kuonana na boss mwenyewe kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara, hivyo Roma hakuona shida ya Kwenda kuonana na Rose ambaye ndio mwekezaji , alijua Rose alikuwa akitumia nafasi hio kutaka kumuona hivyo aliona ni sawa tu Kwenda kwani hata yeye amemiss.
Kwasababu alikuwa akiishi Osterbay , alitumia dakika ishirini mpaka theratini kuendesha gari mpaka kwenye jengo la kampuni.
Roma aliingiza gari baada ya kufika na kuliegesha na kisha alitembea na kuingia kwenye Lift ndani ya jengo hili la Ghorofa na kubonyeza kitufe namba kumi na tisa na ndani ya dakika chache tu alikuwa juu kabisa ya Floor ambayo ndio kampuni ya Vexto Media ilikuwa na makao yake hapo.
Mrembo Rose alievaa akapendeza alionekana kuketi eneo la mapokezi akiongea na Wendy , alikuwa mrembo haswa na mavazi aliochagua kuja nayo siku hio yalimpendezesha mno na hakuna mtu yoyote anaweza kugundua kuwa mwanamke huyo ni muuzaji madawa ya kulevya kwani haiba yake iliwakilisha upole, Roma alitabasamu kumuona Rose na kabla hajamfikia sauti ya Daudi ilimwita kwa nyuma yake.
“Director, you are here, Miss Rose waited for a long time."”Aliongea Daudi kwa furaha na Roma alitabasamu na kutingisha kichwa huku akimkonyeza Rose ambaye aliishia kutabasamu.
Roma aliwapa ishara kwa ajili ya kuongozana wote mpaka kwenye ofisi yake ikiwemo Rose na ndani ya sekunde kadhaa waliingia ndani ya ofisi hii na Roma alienda kuketi kwenye kiti chake cha kibosi na kumfanya Rose kuridhika na mwonekano wa mpenzi wake.
“Boss tulikuwa tukijaribu kumuelezea Miss Rose kuhusu mipango tuliokuwa nayo juu ya kampuni yetu , lakini pia shindano la kuibua vipaji ambalo tunakwenda kuanza nalo na ameridhishwa sana na wazo letu”
“Tumezungumza na kuamua shindano hili tulipe jina la Kizazi Nyota ,linaonekana halijakaa vizuri ila tumeamua kufanya haraka ili kuanza matangazo juu ya shindano hili”Aliongea Daudi na Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Sina maoni yoyote nakubaliana na kila mlichopanga , kama kuna lingine la ziada inabidi mniambie , Mpango wenu kwa sasa ni upi?”Aliuliza Roma
“Kwasaabu taratibu za shindano hili hazina utofauti sana na za Bongo Star Search, tumeona turahisishe kwa kutumia namna wanavyoendesha mashindano yao, kilichobaki kwasasa ni namna ya kuchagua majaji ambao watasimamia shindano zima”Aliongea Wendy na Roma alifikiria kidogo.
“Okey ni vigezo gani ambavyo mnaona vinafaa kwa ajili ya majaji?”
“Ili mtu kuwa jaji lazima awe na umaarufu wa kutosha , mwonekano wake kwa jamii , lakini pia lazima atambulike kimataifa kwani shindano hili linakwenda kutoa watu wenye vipaji ambao watakwenda kufadhiliwa na kampuni yetu hivyo lazima tuwe makini kwenye kuchagua majaji , lakini hata hivyo Director umesema unajua namna ya kufanya shindano hili liwe maarufu hivyo tumeona tukuachie upande wa majaji”
“Okey sina sana ujuzi na maswala ya burudani , ila nina rafiki yangu ambaye ypo kwenye mambo ya burudani na ni msanii mzuri wa kimataifa , kama nilivyosema shindano hili nataka lipate umaarufu hivyo naamini kama tutamtumia watu wengi watalifatilia na kupata umaarufu”Aliongea Roma na kufanya Wendy , Daudi na Rose kushanga na Roma akatabasamu.
“Director tunaweza kumfahamu mtu unayemzungumzia?”Aliuliza Daudi na Roma alitingisha kichwa na kusema ndio na kuwapa ishara kuja nyuma ya meza yake na baada ya wote kuja aliingia kwenye mtandao wa Istagram na kisha alitype jina la Christine Stewart na akaunti yake ilitokea.
“Director usiniambie huyu ndio mtu ambaye unapanga kuwa jaji , itakuwa nni ngumu kumpata , lakini pia atahitaji malipo makubwa”Aliongea Wendy na Roma akatabasamu.
“Ni nani huyu kwanza hata simfahamu?”Aliongea Rose haikueleweka ni kweli hamfahamu au lah lakini macho yake yalidhihirisha kwamba hamfahamu huyo mwanamke mrembo aliekuwa akionekana kwa picha.
“Miss Rose naona hauangaliagi Muvi ,,Christine Stewart ni Hollywood Star mwenye mvuto mkubwa duniani kote , ameshinda tuzo mbalimbali kama vile ya Oscar , Grammy na tuzo ya mwimbaji bora wa karne , inasemekana ana umri wa miaka 26 na pia ana akili nyingi sana za kibiashara , duniani kote wanaume wengi wanahusudu urembo wake na kutamani siku moja kupata nafasi ya kulala nae hata mara moja”Aliopngea Daudi na kumfanya Wendy amfinye aliona anaongea sana , lakini kwa Roma ilionekana ni kawaida tu kwani Daudi alionekana ni moja ya shabiki wa Christine hivyo ni kawaida kwa mtu kumsifia mtu anayempenda kwa kupitiliza.
“Kwahio Daudi huyu anafaa kuwa Jaji au hafai, kuhusu Gharama hata msijali , kama nilivyokwisha kusema huyu ni rafiki yangu mkubwa na anaweza akawa jaji wetu bure kabisa”Aliongea Roma na kufanya Hata Wendy aone Roma anatania , alikuwa akimjua Christine hawezi kuja Tanzania kupoteza muda kisa ya kuwa jaji , lakini pia alikuwa ni mtu mkubwa sana katika ulimwengu wa burudani , hivyo Roma kuwa na urafiki na mwanamke mrembo kama huyo aliona anawapiga Kamba.
“Anafaa sana Director kama tungekuwa na uwezo wa kumpata , lakini huyu mrembo ni levo nyingine kwetu hivyo nashauri kama tutaangalia wasanii wa hapa hapa Tanzania kama Diamond au Alikiba”Aliongea Wendy na Roma hakujali sana , kwanza alienda upande wa direct Message(DM) kuangalia kama yupo online na alijikuta akitabasamu baada ya kuona mrembo huyo nyota wa dunia yupo online kwenye mtandano huo.
Roma kwakutmia akaunti yake ya jina lake la Roma , aliandika ujumbe wa meseji wa salamu Kwenda kwa Christine huku Rose, Daudi na Wendy wakimshangaa Roma , waliona Roma ni mtu mwenye vituko sana , lakini dharau zao ziliisha mara baada ya kuona Christine anapiga Vidio Call, na Roma alipokea na kumfanya Daudi na Wendy kutoa macho baada ya kuona sura ya mrembo Christine , ni kama hawakuwa wakiamini hivi kama ni yeye kweli.
“Christine nadhani sijakusumbua najua upande huo ni usiku?”Aliongea Roma kwa kingereza.
“Roma ijapokuwa sijapenda simu yako ya muda huu , lakini niamini mimi haijawahi hata siku moja ukatoa taarifa ya eneo ulipo” Baada ya Daudi kusikia maneno hayo alijikuta akishangaa Zaidi baada ya kusikia Christine akitaja jina halisi la Roma.
“Nadhani napaswa kueleza shida yangu haraka haraka nikuache upumzike , sasa hivi nimekuwa Director wa kampuni kwenye maswala ya burudani na wewe ni gwiji kwenye idara hii, nimepanga kuanzisha mashindano ya kusaka vipaji na bado sina jaji ambaye anaweza kufanya shindano la kampuni yangu kuwa maarufu , hivyo naona wewe unafaa kabisa”Aliongea Roma kwa kingereza cha kimarekani kabisa.
“Hahaha.. Roma sijui nini kimekukuta huko Tanzania ila nimefurahi kusikia kama umekuwa Director wa kampuni”Aliongea Christine mrembo kwa mapozi na kumfanya hata Rose kuanza kushikwa na wivu kwani alihisi huenda Roma na Christine ni wapenzi na akiangalia Christine amemzidi sana urembo.
“Kwahio nichukulie haya maneno yako kama jibu ni ndio?”Aliuliza Roma huku akitabasamu kawaida , licha ya kwamba mtu aliekuwa akiongea nae alikuwa mtu mzito lakini alionekana kawaida kabisa na ni kama walikuwa wakifahamiana sana.
“I can participate. I originally planned to give myself a good holiday this year, but I can't do every contest, so other judges will do the most work”Aliongea Christine akimaanisha kwamba atashiriki kama jaji lakini sio kwa mashindano yote , kwani alikuwa akipanga kufanya mwaka huo kuwa wa mapumziko , hivyo kazi nyingine zitafanywa na majaji wengine.
“Miss Christine usiwe na wasiwasi kabisa , sisi tunakuhitaji siku moja tu ya fainali na hatutakusumbua tena , karibu sana Tanzania na asante kwa kukubali ombi letu”Aliongea Daudi kwa shauku kubwa baada ya kusikia Christine yupo tayari kuja Tanzania kwa ajili ya kuwa jajii.
“Huyu ni msaidizi wangu , anafahamika kwa jina la Daudi , atazungumza na wewe juu ya kazi yote utakapofika hapa Tanzania , mimi nimetumia sura yangu tu ili ukubali ombi la kuja Tanzania”Aliongea Roma na kumfanya Christine kutabasamu kivivu na kuachama akiashria kwamba anataka kulala
“I understand, my contact information, you know, I am sleepy now, good night, Roma”
“Goodniht”Aliongea Roma na palepale video Call ilikatwa na Daudi na Wendy walijikuta wakianza kupiga makofi kwa furaha , waliamini kwa kupitia Christine umaarufu wake basi hata wao watakuwa maarufu sana na pia kampuni yao kujulikana ndani ya muda mfupi.
Roma aliwaandikia Email ya Christine Daudi na Wendy kwa ajili ya kuwasiliana na management yake na kisha wakatoka ndani ya ofisi hio wakimuacha Roma na Rose.
“Nini tatizo Rose?”Aliongea Roma baada ya kuona Rose anamwangalia Roma kwa macho yasio ya kawaida.
“Huyu mwanamke mremo uliekuwa unaongea nae , niambie ukweli na yeye ni mpenzi wako?”
“Babe Rose huyu ni rafiki yang tu , ni kweli ni mrembo lakini sina mahusiano nae kabisa huo ndio ukweli ni rafiki yangu wa karibu sana”Aliongea Roma.
“Ulishindwa vipi kulala na mrembo kama huyo ulipokuwa nje ya nchi kama ni rafiki yako , ilihali wanaume wengi wanatamani hio nafasi?”
“Haha.. ni kweli lakini mimi sina njaa ya kila mwanamke, au naonekana kuwa na njaa ya wanawake?”Aliongea Roma na Rose alibetua mdomo na kushindwa kujibu swali na Roma alimsogelea na kisha kumbusu.
Baada ya taratibu za Rose kusaini mkataba wa uwekezaji wa pesa zake ndani ya kampuni ya Roma , aliaga kwa ajili ya kuondoka , lakini Roma hakutaka kabisa kumwacha mrembo huyo kuondoka peke yake na aliamua kumsindikiza.
“Rose mpenzi sijawahi kukununulia zawadi yoyote , leo nataka nikakufanyie Shopping”Aliongea Roma na Rose tabasamu lilimtoka ni kweli Roma hakuwahi kumpa zawaidi na pia hakuwahi kujali juu ya hilo , lakini kwasababu Roma alikumbuka mwenyewe juu ya hilo alijikuta akifurahi kweli na kuona Roma anampenda.
Roma aliendesha gari mpaka mlimani City sehemu ambayo aliona inafaa kwa ajili ya kumfanyia shopping mchepuko wake Rose , hakuwa na wasiwasi kabisa baada ya kuegesha gari na alikuwa amependezana na Rose kiasi cha kupelekea hata waliokuwa ndani ya eneo hilo kuwaonea wivu , kwa jinsi walivyokuwa wakionekana hakuna mtu ambaye anaweza kusema Roma ana mke na yupo kazini akipambana , Roma alionekana kujiachia mbele ya Rose na kumfanya mrembo huyo kutabasamu.
Roma aliingia kwenye duka la nguo za kike ndani ya duka kubwa lililopo hapa mlimani duka la Singa fashion Wear, walianza kuchagua mavazi mbalimbali na kila Rose aichopenda Roma alitoa maelekezo kwa muhudumu ndani ya duka hilo kukichukua na kuhifadhi kwa ajili ya Kwenda kujaribisha , na iliwachukua takribani lisaa mpaka kumaliza na hapo ndipo Roma a Rose walipohamia upande wa duka la viatu vya kike na kuanza kumchagulia Rose.
“Nimekipenda hiki babe ni kiatu kinachotamba sana mjini kwa sasa”Aliongea Rose na kukichukua na kujongea mpaka kwenye sofa kwa ajili ya kujaribu , hakutaka kujaribu hapo hapo kwani nguo aliokuwa amevaa ni fupi na kama angeinama basi wanaume waliokuwa nyuma yake wangeona vyote vya siri.
“Leta nikusaidie kukuvalisha”Aliongea Roma na kuchukua viatu vile kwenye mikono ya Rose na kisha alichuchumaa kwa ajili ya kumvalisha tukio ambalo lilifanya wanawake waliokuwa hapo ndani kuona wivu jinsi Rose anavyojaliwa na mpenzi wake.
Wakati Roma akiwa bize kumvalisha Roma , mara macho ya watu yaligeuka upade mwingine baada ya mwanamke mrembo kuingia ndani ya eneo hilo la Mlimani City kwenye duka hilo hilo la viatu.
“Miss karibu sana”Aliongea muhudumu wa duka hilo na kumfanya hata Roma kugeuka na hio yote ni mara baada ya kuhisi pafumu ya bei mbaya anayoifahamu , moyo wake ulipiga kite na kugeuka nyuma na hapo ndipo macho yake yalipogongana na mke wake Edna na hakuelewa Edna alikuwa akifanya nini muda huo ndani ya maduka hayo kwani aliamini muda huo angekuwa kazini.
Kwa upande wa Edna hivyojivyo hakuamini kama mwanaume aliekuwa mbele yake anaemvalisha mwanamke mrembo kiatu ni yule mume wake ambaye alikuwa akiamini muda huo alikuwa kazini akiendelea na majukumu yake.
SEHEMU YA 277
Haikueleweka Edna alikuwa ndani ya eneo hilo la Mlimani City kwa ajili ya kufanya nini, alimwangalia Roma aliekuwa anamvalisha Rose kiatu kwa sekunde kadhaa na kisha alisonga mbele pasipo ya kuongea neno , ni kama alimpuuza Roma.
Upande wa Rose mwenyewe hakuwahi kuonana kabisa na Edna na kwa na siku hio ndio kwa mara ya kwanza anaonana nae na alihusudu urembo aliokuwa nao mwanamke wa Roma na alijiambia hakuwa akiingia kwa chochote kwa mke mkubwa , lakini licha ya mke mkubwa kuwa mrembo lakini aliogopeshwa mno na macho yake.
“Roma nadhani hatukupaswa kuja hapa , nimekuwa na bahati mbaya sana na mke wako kwa siku ya kwanza”Aliongea Rose lakini Roma aliishia tabasamu na kumalizia kumvisha Rose kiatu mpaka akamaliza.
“Babe Rose naona umependeza sana”Aliongea Roma huku akimwangalia Rose kwa tabasamu , lakini Rose alishindwa kumuelewa kabisa Roma , kwani yeye anazungumza swala la mke wake lakini yeye analipotezea.
“Rose najua una wasiwasi na mke wangu , ila hilo lisikuumize kichwa unapaswa kuwa na amani , mimi ndio nimekuleta hapa na huna makosa yoyote , mimi nitatafuta namna ya kuyamaliza na Edna”Aliongea Roma na Rose alitabasamu , kwanza mpaka hapo alishukuru kwa kitendo cha Roma kutokumuacha na kumkiimbilia mke wake , kwake swala hilo aliona ni kama heshima ambayo Roma amempa hivyo aliishia kutabasamu.
Upande wa Edna haikueleweka alikuwa amekuja kuchukua nini , lakini ndani ya dakika kadhaa alikuwa akitoka na bahati nzuri hakuweza kuwaona Rose na Roma tena kwani washasogea upande mwingine na tofauti ya sehemu aliowaona , hivyo aliona akaushe na kurudi, alionekana kuwa kauzu kweli , licha ya kwamba jambo ambalo amelishuhudia lilimuumiza lakini alijiambia kwamba anapaswa kuvumilia kwani hakujua namna ya kumdhibiti Roma , hivyo aliona ajue mambo yake.
Edna baada ya kurudi ofisini kwake alikaa kwenye kiti chake na kisha kuvuta pumzi nyingi na kisha alichukua mkoba wake alioingia nao na alitoa kasha la plastiki ambalo linatumika kuhifadhia nyaraka na kisha alitoa bahasha iliokuwa ndani ya kasha hilo na alifungua ndani yake na kutoa baadhi ya karatasi na kuanza kuzisoma moja baada ya nyingine kwa umakini mkubwa, takribani dakika kama ishirini hivi alitumia kusoma karatasi hizo na alijikuta akifikiria kitu na hapo hapo alitoa simu yake na kutafuta jina la Athena.
“Amiri kuna kazi mpya nataka kuwapa muifatilie kwanzia sasa”Aliongea Edna kwa sauti yake kavu.
“Ndio boss nakusikiliza”
“Nataka mfuatilie kwanini Serikali ilivunja mkataba wa ujenzi wa jengo la Bima ya Taifa na Vexto Construction mwaka 2014 ilihali jengo hili lilikuwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi”
“Sawa boss , kuna taarifa nyingine ya ziada ambayo inaweza kutupa mwanga?”Aliuliza Amiri aliekuwa akiongea kwa simu na Edna aliinua karatasi zilizokuwa kwenye meza na kisha kuziangalia.
“Mnaweza kuanza kuchunguza kampuni ya INNOVA na MAYA juu ya uhusikaji wao katika hili, nahitaji pia maelezo kwanini jengo lilichukua miaka mingi kumalizika ilihali lilikuwa kwenye hatua za mwisho wakati Vexto wanavunja mkataba”
“Sawa boss nitalifanyia kazi kwanzia sasa”
“Swala hili lifanyike kwa siri sana na kwa weledi mkubwa”
“Sawa boss” Na simu palepale ilikatwa. Na mlango ulifunguliwa na akaingia Monica katibu wake.
“Boss kuna mgeni mapokezi anahitaji kuonana na wewe kwa shida binafsi”Aliongea Monica kwa heshima na kumfanya Edna ashangae kwani hajazoea kuonana na watu wenye shida binafsi muda wa kazi.
“Amejitambulisha kwa jina gani?”
“Desmond Jeremy”Aliongea Monica na Edna alijikuta akishangaa , alikuwa akimjua Desmond , lakini hakujua kwanini amekuja mpaka kwenye kampuni yake.
“Mwambie sipokei wageni wenye shida binafsi muda wa kazi”
“Sawa boss”Aliitikia Monica na kutoka.
Siku hio Desmond ni kama alifanya makusudi kabisa , kwanza kabisa alfika ndani ya eneo hilo la kampuni na gari aina ya Roll Royce ya mwaka 2022 , gari ambayo inaaaminikuka kuwa na thamani ya shilingi bilioni mbili za kitanzania , kitu cha pili ni kama alivunja kabati kwani alikuwa amependeza kweli kuliko isivyokuwa kawaida na cha ajabu Zaidi alikuwa amebeba ua zuri siku hio na alitoka nalo kwenye gari na kufanya kila mtu kuona ua hilo zuri alilobeba.
Kampuni ya Edna ilikuwa inaongoza kuwa na wafanyakazi wa kike , hivyo kitendo kile kilivutia sana wanawake hao na kujiuliza HB huyo alikuwa hapo ndani kwa ajili ya nani, kila mmoja mwanamke mrembo alitamani awe kwenye nafasi ya kupewa ua ambalo limeshikiliwa na Desmond.
“Samahani kaka nikusaidie nini?”Aliuliza mtu wa mapokezi chini kabisa ya jengo hili na kumfanya Desmond kutabasamu.
“Nipo hapa kwa ajili ya kumuona Edna Adebayo”Aliongea Desmind kwa kujiamini na kumfanya hata mhudumu kushangaa na mpaka hapo aliamini huenda Desmond ndio mpenzi wa boss wake Edna , mwanamke mrembo sana ambaye siku zote kila mmoja ya mfanyakazi alitamani kujua mwanaume anaetoka nae kimapenzi na kwa muonekano wa Desmond aliamini wanaendana kabisa , kwanza mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa na pesa , pili alikuwa na mvuto mkubwa sana kiasi ambacho hata yeye angejitoa kwa usiku mmoja kwa mwanaume huyo kama angemtaka, mwanadada wa mapokezi licha ya kwmaba mwanaume aliekuwa mbele yake hakuwa akimfahhamu vizuri , lakini pia licha ya kuvutia kwake hakutaka kabisa kuvunja taratibu za kampuni kwa ajili yake na alitanguliza taaluma yake.
“Kaka samahani , unamiadi nae?”
“Sina miadi nae , lakini kama utamwambia Desmond mume wake mtarajiwa yupo hapa ataniruhusu kumuona”Aliongea Desmond na kuzidi kumpagawsiha mno mwanadada wa mapokezi na baada ya kuona mwanaume huyo ni mwenye kujiamini na haonyeshi ishara yoyote ya kuwa mgonjwa wa akili , ilibidi afanye hima kuwasiliana na katibu Muhtasi wa Edna ili kujaribu kuuliza
“Hello Monica , kuna mgeni wa boss anafahamika kwa jina la Desmond hapa mapokezi”Aliongea mwanadada huyo kwa Kiswahili safi.
“Anashida gani na boss?, Binafsi au kikazi?”Aliuliza Monica na Mwanadada yule alimwangalia Desmond na kuona kabisa huyo mwanaume yupo kwa shida binafsi.
“Binafsi”
“Okey! Subiri niwasiliane nitakupatia jibu”Aliongea Monica na ndani ya dakika chache simu ya mapokezi iliita na akapokea.
“Mwambie boss hapokei watu binafsi muda wa kazi”Aliongea Monica na kisha kukata simu na mwanadada wa mapokezi alimwangalia Desmond kwa namna ya huruma.
“Boss amesema hapokei watu kwa shida binafsi”Aliongea mwanadada wa mapokezi na kumfanya Desmond kutoa tabasamu la uchungu.
“Usijali mrembo , mke wangu namfahamu ni mchapa kazi na asubuhi niligombana nae , nitamsubiri hapa mpaka atakapotoka”Aliongea Desmond.
“By the way kuna huyu mfanyakazi anafamika kwa jina la Roma Ramoni , yupo hapa kazini?”Aliulizia Desmond na mwandada yule alifikiria.
“Mr Roma ni Director wa Vexto Media na hafanyi kazi hapa makao makuu”Aliongea na Desmond alitabasamu na kisha alijongea mpaka eneo la Kantini kwa ajili ya kumsubiria Edna , alijiambia pasipo ya kumuona Edna haondoki siku hio.
Ukweli ni kwamba alikuwa akijiamini mno kwasababu moja , kwanza alikuwa akijua wafanyakazi wa Vexto karibia wote hawakufahamu Roma na Edna ni mume na mke na jambo hili lilimfurahisha sana yaani, na alijikuta akiamini maneno ya rafiki yake Elvice juu ya Roma kutopendwa na Edna na wameoana kwa sababu maalumu ambayo hawakuwa wakiijua , hivyo maneno hayo kwake yalikuwa yakitosaha kabisa na kumpa motisha ya kuendeleza mapambano ya kumpata Edna.
Edna siku hio hakutoka kabisa hata kula chakula cha mchana , alionekana kuwa bize sana na hata Monica alimpomkumbusha kuhusu chakula alimwagiza amletee Karanga na juisi ya matunda aina ya Apple.
“Desmond!”Aliita CEO msaidizi wa Edna bwana Ernest Komwe baada ya kumuona Desmond.
“Hahaha… Komwe ni wewe , siamini amini”Aliongea Desmond kwa bashasha na wakakumbatiana.
Muda huu ErnestKomwe alionekana ndio anashuka kwa ajili ya chakula cha mchana na ndio alibahatika kuonana na Desmond ambaye alijipa kazi ya kumsubiria Edna.
Walisalimiana na walionekana walikuwa wakifahamiana kitambo sana kwani walikumbushiana baadhi ya mambo ya chuo.
Desmond alijikuta akishangaa na kufurahi kwa wakati mmoja baada ya kugudnua Komwe ni Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya Vexto.
“Unafanya nini hapa Desmond?”Aliulizia Komwe huku akiangalia ua lililokuwa kwenye meza.
“Nipo kwenye harakati”Aliongea na kumfanya Komwe kucheka sana.
“Kama zilezile za siku zote?”
“Unakumbukumbu wewe .. hahaha”
“Haha.. ni pisi gani imekutoa Rwanda mpaka hapa Tanzania?”
“Boss Wenu”aliongea Desmond na kumfanya Komwe kushangaa mno.
“Mh! Kazi unayo kijana wangu”
“Kwanini?”
“Yule mwanamke ni kauzu hatari , nikwambie tu licha ya mimi kuwa msaidizi wake lakini nimeongea nae maongezi binafsi mara chache sana , muda wote yuko bize na kazi , siamini kama unaweza kumpata na jambo kubwa nasikia ana mume”Aliongea Komwe kwa sauti ya chini kwani wafanyakazi washaanza kujaa kwa ajili ya kupata chakula.
“Haha… kama ana mume basi mimi ndio nitakuwa mume wake”
“Haha.. si kweli rafiki yangu , Roma Ramoni ndio mume wake, taarifa zote ninazo”Aliongea Komwe na kumfanya Demsond kutabasamu.
“Unaonekana kuwa jasusi wa kujitegemea?”
“Haha.. kawaida sana, Desmond huwezi kumpata Edna , licha ya kwamba nazielewa swaga zako lakini pale jiachie tu, frequency za yule mrembo ili uendane nae itabidi ufe ufufuke au upate maono hahaha..”Aliongea Komwe kama mtu anaemkatisha tamaa , lakini Desmond hakujali kwanza aliamini Komwe hakuwa akimjua vyema Edna, kwake mrembo Edna ashawahi kumpenda na akalijua hilo , hivyo alijiambia ni rahisi sana kumpata kuliko wengine wanavyofikiria.
“Nadhani hupaswi kusubiria hapa rafiki yangu , kama kweli unataka kumzawaida hilo Ua basi kasubiri kwenye eneo la maegesho kwani anashuka na Lift yake binafsi mpaka maegeshoni kwake”Aliongea Komwe na kumfanya Desmond kushukuru.
Saa kumi kamili Edna akiingia eneo la maegeso ya magari kwa ajili ya Kwenda nyumbani alijikuta akishangaa baada ya kumuona mwanaume kaegamia gari yake , baada ya kumwangalia vizuri aligundua ni Desmond na alishangazwa imekuwaje walinzi wakamruhusu kuingia eneo la kwenye maegesho yake binafsi.