Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 269.

“Dady Stop..”Aliingialia Ashley akimtuliza Raisi Senga .

“Blandina nikuweke wazi tu , haitokuja siku nikamtambua Roma kama mwanangu na sitokuja kutambua kama nishawahi kuzaa na mwanamke kahaba kama wewe”Yalikuwa ni maneno mazito mno Kwenda kwa Blandina , lakini hata hivyo Blandina alionekana kuwa katika hali ya utulivu.

“Ni kweli Senga , unaweza kunitukana uwezavyo lakini chonde chonde usimtukane mtoto wako kwani unajitafutia laana, nitukane mimi ambaye nilifanya makosa na Roma hahusiki”Aliongea Blandina kwa sauti ya kinyonge.

“Senga naomba uache tafadhari , unajikosesha heshima mbele za watu”Aliongea Damasi na kisha alimpa ishara Kabwe kusogea.

“Kabwe mheshimiwa atarudi Ikulu sasa hivi”Aliongea Damasi.

“Senga nisikilize mimi unarudi ikulu sasa hivi na nitashughulikia swala la Denisi mwenyewe”Aliongea Damasi kwa msisitizo na Senga aliekuwa akitweta kwa hasira alimwangalia Damasi kwa dakika kadhaa na kisha bila yakuongea neno aligeuka na kuondoka na Damasi alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.

“Blandina maneno ya mume wangu naomba usiyachukue moyoni , najua kuna mengi ya kuongea lakini swala hapa ni kuangalia afya ya mtoto wangu Denisi ambayo imeharibiwa na Roma”Aliongea Damasi kwa msisitizo na Blandina hakujibu Zaidi ya kukaa kwenye benchi na kugeukia pembeni.

“Ashley niambie ni njia ipi inaweza kumsaidia Denisi?”Aliongea Damasi.

“Mtu anaeweza kumtoa katika kifungo cha kupalalaizi ni Roma peke yake”Aliongea Ashley na kumfanya Damasi kushangaa.

Kwa wengine hawakuweza kushangaa , kwani Roma alisema kule nyumbani kwamba anampa Denisi adhabu ya kupalaizi mwili kwa Maisha yake yote.

“Unamaanisha Mr Roma anaweza kumsiadia mwanangu kupona , Ashley una uhakika?”Aliuliza Damasi kwa shauku kubwa huku tumaini jipya likiibuka kwenye macho yake.

“Naamini hivyo mama”Aliongea Ashley na kumfanya Damasi kutabasam.

“Kama ni hivyo basi nitaenda kumuomba Roma amsaidie Denisi , najua mwanangu amemkosea na nitamuombea msamaha”Aliongea na kisha aligeuza macho na kumwangalia Edna na baada ya kuona Edna na yeye aamwangalia alimsogelea na kisha akamshika mikono.

“Edna naomba unisaidie kuonana na mume wako, niko chini ya miguu yako naomba unisaidie mwanangu apate kupona”Aliongea Damasi kwa kujishusha mno kiasi kwamba Mage na Magdalena kumuonea huruma na kujua uchungu wa mama kwa mtoto wake.

Na kabla ya Edna hajamaliza kuongea mlango wa chumba cha matibabu ulifunguliwa na madaktari watano walitoka wakionekana kuchoka mno na wote kwa Pamoja waliwasogelea..

“Dokta vipi hali ya mtoto wangu?”Aliuliza Damasi na Dokta Manyani Sepengo alimwangalia Damasi kwa heshima.

“Madam kwasasa Denisi yupo kwenye hali ya kawaida, licha ya kwmaba yupo mahututi lakini tushaondoa hatari zote ambazo zinaweza kumsababishia kifo”

“Ninaweza kumuona sasa hivi?”

“Ndio madam unaruhusiwa kumuona lakini sio wote”Aliongea dokta kwa heshima na Damasi alishukuru na kuanza kutembea akiongozwa na daktari mpaka chumba alichokuwa akipatia matibabu Denisi , chumba cha ICU .

Damasi baada ya kumuona mtoto wake amefungwa mapita mdomoni na puani ya kumsaidia kuhema alijikuta moyo wake ukiuma , hakuwahi kumjuona Denisi akiwa kwenye hali kama hio.

Pembeni yake alikuwa yupo Ashley, na yeye alijikuta akiumia baada ya kumuona mdogo wake yupo kwenye hali kama hio , Denisi alikuwa mwanafamilia kwake hivyo hakuwa tayari kumuona baya lolote likimkuta.

Baada ya dakika kama tano za kutoa machozi , Damasi alitoka kwenye chumba hiko na Kwenda mpaka alipokaa Edna na kumuomba amsaidie kuonana na Roma na Edna hakuwa tayari kukataa , kwanza alishaongea na mama mkwe wake kwamba wafanye chochote ili hali ya Denisi iweze kurudi katika hali ya kawaida , ili kuepusha migongano ya kifamilia.

“Mama nitakusaidia kuonana nae , ngoja nimpigie simu aje hapa”Aliongea Edna.

“Hapana Edna nitaenda popote pale alipo kumuomba msamaha kwa ajili ya mwanangu na kisha amsaidie kupona , hali ya kupalalaizi kwa mwanangu itaniumiza sana kwani yote haya yanatokea kwa kutokuwa mama bora”Aliongea na kumfanya Edna aone huruma na hakuwa na sababu za kukataa alichofanya ni kumwambia Mama Ashley kwamba wataongozana Kwenda nyumbani.

“Ashley utabaki hapa hospitalini kwa ajili ya kumwangalia mdogo wako”

“No mama tutaenda Pamoja”Aliongea Ashley. Na Damasi aliona asikatae kwni aliamini Ashley atakuwa na sababu ya kutaka Kwenda nae Pamoja, kwani juzi tu waliweza kusikia namna Ashley alivyoweza kukutana na Roma huko Uingereza stori ambayo ilimhuzunisha sana Damasi lakini kwa Senga hakuhuzukina kutokana na chuki zake.

Wanafamilia wote walirudi kwa Pamoja na ndani ya dakika kadhaa tu walikuwa wakiingia ndani ya nyumba ya Edna, wa kwanza kutoka alikuwa Edna na kisha wakafuatia wengine.

Edna alivuta pumzi ya ahueni baada ya kuona gari ya Roma ipo hapo nyumbani kwani alikuwa na wasiwasi wa kutomkuta.

“Mama nitaenda kumuita ashuke chini?”Aliongea Edna na Damasi alishukuru huku Bi Wema , Yezi na Sophia wakishindwa kuelewa kinachoendelea kwani wao hawakwenda hospitalini.

Roma alikuwa ashalala kitambo , yaani ni kama hakuna alichokifanya masaa kadhaa nyuma , alikuwa akikoroma kabisa akifurahia usingizi wake, Edna aliingia ndani ya chumba cha Roma bila kugonga na baada ya kumkuta Roma kalala bila wasiwasi alijikuta maswali mengi yakijaa kwenye kichwa chake.

Yaani alijiambia Roma kaua mtu jana yake na leo asubuhi kamfanya mtu kupalalaizi , lakini haoni shida wala hatia yoyote ile , alishindwa kumuelewa Roma kwa wakati mmmoja , ni kweli Roma alikuwa na historia ya kipekee ambayo hakuwa akiifahamu, lakini swlaa la kuua na kutokuwa na hatia juu ya hilo bado ni kitu ambacho kinamfikirisha Edna na kujiuliza inakuwaje Roma akawa hivyo.

“Romaa..!!”Aliita Edna akimshika Roma mgongoni na sauti yake nyororo ilionekana kumwingia Roma vizuri lakini hata hivyo hakutaka kuamka mapema alitaka Edna asumbuke kumuamsha kwanza , alijiambia hakuna kitu kizuri kama kuamshwa na mwanamke unaempenda halafu ukajifanyisha kama humsikii.

“Paah!..Amka wewe”Aliongea Edna lakini Roma hakuamka na Edna alijikuta uvumilivu ukimshinda na kujiandaa kumsindilia kibao na ile anakishusha kuukaribia mgongo wa Roma alijikuta akivutwa kwa spidi kali na kutua kitandani na Roma akampandia kwa juu.

“Wife tofauti na kumpiga mumeo , ni kipi kingine unaweza kufanya , huenda ungenibusu shavuni ningewahi kuamka kuliko kunipiga”Aliongea Roma akimwangalia Edna aliekuwa chini yake.

Upande wa Edna aliangalia kifua cha Roma chenye minywele na alijikuta akipata msisimko wa ajabu kiasi cha kutuma mawasiliano kwenye viungo vyake vya uzazi.

“Unasubir….”Kabla hajamaliza sentesi yake Roma ashaunganisha mdomo wake na wa Edna.

“Mhmh..!!!”Edna aliishia kuguna na alitamani kujitoa lakini kwa jinsi Roma alivyomshikilia mikono ilikuwa ngumu kwake.

“Okey Wife hio ndio adhabu yako ya kunipiga mumeo na vibao badala ya kuniamsha kwa upendo”Aliongea Roma akitabasamu kifedhuli na kumwachia Edna.

Edna alijikuta akiona aibu za kike , lakini hata hivyo akili yake bado ilikuwa kwa wageni upande wa chini.

“Mama yake Denisi anakusubiria chini , vaa haraka”Aliongea Edna na kutembea mpaka kwenye kabati la nguo za Roma na kisha kumrushia tisheti na Track Suit huku akikwepesha macho yake na mwili waRoma , kwani sehemu ya mbeleya bukta aliovaa Roma ilikuwa imetuna kiasi cha kumfanya ubaridi kumpitia.

Roma alifurahishwa na viaibu vya Edna na kisha alichukua suruali aliorushiwa kitandani na kuvaa.

“Anataka nini huyo mama yake Denisi , au kaja kunifokea”Aliongea Roma lakini Edna hakutaka kumjibu Zaidi ya kumpa ishara ya kutoka.

“Wife nitaenda kama utanipiga busu shavuni”Aliongea Roma kiutani lakini jicho alilopigwa na Edna alijikuta akighairi na kuanza kutembea kutoka huku Edna akiwa nyuma yake.

Roma alishangazwa na watu waliopo sebuleni kwani lilikuwa ni kundi na kwa haraka haraka jumla yao walikuwa sita.

Roma alishuka bila wasiwasi mpaka chini sebuleni huku macho yote yakimwangalia na kisha akamsogelea Mama Ashley.

“Roma naomba umsamehe mwanangu Denisi , nipo hapa kuomba msamaha kwa ajili yake”

“Mamaa…!!!”Aliita Ashley hakuamini mama yake angepiga magoti lakini alikuwa ashachelewa kwani Damasi alikuwa amepiga magoti tayari na kufanya kila mtu kushangazwa na kitendo hiko.

“Mama Denisi , hupaswi kunipiga magoti kwani sina sababu ya kumsamehe mtoto wako”Aliongea Roma bila ya kubadili muonekano wake , yaanni alishindwa kutafsrika kama yupo na hasira au yupo kawaida.

********

Upande mwingine , ndani ya hoteli ya Serena anaonekana Yan Buwen akiwa kwenye chumba chake alichochukua hotelini hapo akiwa amejifunga taulo huku akiwa ameketi , kwenye meza ya kioo ilionekana Laptop kampuni ya Apple ikiwa imewashwa huku akionekana akisoma maswala ya Ant-matter, huku akijiburudisha na mvinyo uliojaa kwenye Glass.

Bwana huyu alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa na umakini wake wote alikuwa ameuelekezea kwenye tarakishi mpaka pale simu yake ilipoanza kuita na kumfanya aache kila anachokisoma na kuichukua.

“Nipe Update`s”

“Denisi yuko hospitalini”Ilisikika sauti upande wa pili ya kiume.

“Nini kinaendelea”

“Mheshimiwa Senga alikuwa hapa hospitalini kwa muda mrefu kwa ajili ya kumuona lakini ashaondoka na baaada ya kumuacha mke wake kwa madakika kadhaa na yeye anaonekana kutoka akiongozana na familia ya Roma”Ilisikika sauti na kumfanya Yan Buwen kutabasamu.

“Endelea kunipatia taarifa kwa kila kinachoendelea”

“Sawa boss”

“Haha.. Hades umekwepa mtego wangu wa kwanza kwa kushindwa kumuua kaka yako , kweli damu nzito kuliko maji , lakini hii haimaanishi mpango wangu umefeli , mimi ndio jiniasi Yan Buwen nilieaminiwa na mremboo Athena kutimiza kazi yake ili anipe tunda , mtego wangu wa pili siamini kama utaepuka, nahitaji damu yako kwa namna yoyote ile ili niweze kutumia Godstone kwenye mwili wangu”Aliwaza Yan Buwen huku akichukua Glass yake na kunyanyuka na kusogelea dirisha huku akitabasamu kifedhuli.

Kwa hapa inaonekana Yan Buwen alikuwa akitumia ‘trick’ ili kupata damu ya Roma , alijua hawezi kupata damu yake kwa urahisi pasipo kutumia mpango kabambe,

Ni damu ya Roma pekee ambayo ilikuwa na uwezo wakuhimili ‘Devine light inayodharishwa na Godstone na pasipo kuipata basi sayansi na kanun izote za profesa Shelukindo haziwezi kukamilika.

“Hahahaha.. hahaha …. Hades ukumkubalia mke wa Raisi Senga kumponya mwanae basi hilo ndio kabuli lako , najua huna namna ya kumponya Denisi katika hali yake ya kupalalaizi mpaka utumie damu yako, hiko ndio ninachohitaji .. hahahaha… hahahah.. I am Genius Yan Buwen hahaha”Aliongea kwa furaha bwana huyu alijiona kuwa mshindi.







SEHEMU YA 270.

Damasi hakuamini kama Roma anaweza kumuwekea ngumu , licha ya kwamba alijitoa kimasomaso kupiga magoti ili mradi tu mwanae kuponyeshwa ugonjwa wa kupalalaizi , mwanamama huyu moyo wake uliuma mara baaada ya kusikia jibu la Roma kwamba hawezi kumsaidia.

“Roma tafadhari naomba umsaidie Denisi , najua amefanya makosa na ndio maana mimi mama yake nimepiga magoti kuomba msamaha , naomba uniadhibu mimi na sio mwanangu Denisi , mimi ndio sijamlea vizuri”Aliongea Damasi lakini Roma bado hakutaka kuonyesha ishara ya kutoa msamaha alichokifanya ni kuinama na kumnnyanyua Damasi..

“Naelewa machungu uliokuwa nayo juu ya mtoto wako hivyo usinipigie magoti tena , swala ambalo unaniomba ni gumu kutekelezeka”Aliongea Roma.

Ukweeli Roma kwa jinsi alivyomuona Denisi alijua kabisa kama atamponya yeye huenda kuna hatari kubwa inaweza kutokea na ndio maana hakuwa tayari kufanya chochote kwa ajili ya kumponyesha Denisi , hata kama mama yake amepiga magoti.

“Edna nisaidie kumuomba mumeo amsamehe mtoto wangu , Blandina tafadhari najua Denisi amekosa lakini kupalalaizi Maisha yake yote ni adhabu kubwa sana kwake”Aliongea Mama Ashley kwa uchungu mkubwa sana na Edna alijikuta hata yeye akishindwa kujua cha kufanya , aliamini maamuzi yanatakiwa kufanywa na Roma mwenyewe na sio yeye kuingilia licha ya kwamba kila kitu kimeanza kwasababu yake.

“Hakuna mtu wa kunishawishi na nikamsamehe Denisi , ni kweli ninao uwezo wa kumrudishia afya yake , lakini taratibu ambazo nitazifanya kumrudishia uwezo wake ni za hatari na zinaweza kuniletea matatizo mimi mwenyewe”Aliongea Roma kwa msisitizo na maneno yake wengi walionekana kuelewa lakini sio kwa Ashley wala kwa Damasi , hawakuwa tayari kumuona Denisi akiishi Maisha yake yote akiwa amepalalaizi.

“Roma nilishawahi kuyatoa Maisha yangu kwako kama kaka yangu wa damu naomba umsaidie na mdogo wangu”Aliongea Ashley baada ya kusogea mbele.

“Ashley kwanza sijui umefika lini nchini , lakini sijui unachomaanisha”

“Ni kweli hujui ninachomaanisha kwasababu mimi na Profesa Clark tulifanya iwe siri yetu, lakini haifuti ukweli kama nilihatarisha maisha yangu kukuokoa katika hali ya kifo”Alionga Ashley.

“Ashley sijui nini unataka kumaanisha lakini jambo ambalo mnaniomba siwezi kulifanya”Aliongea Roma.

“Roma kama hukumbuki kilichotokea miaka minne iliopita nitakueleza sasa hivi”Aliongea Ashley huku akijiambia mbwai na iwe mbwai lakini ataeleza kile alichomficha Roma ili mradi kumuokoa kaka yake hio ndio tabia kubwa ya Ashley hakuwa tayari kuona kiumbe kingine kinateseka ili hali njia ipo

*********

2018-WALES SCIENTIFIC RESEARCH CENTER(WSRC)

Ni ndani ya kituo cha utafiti wa maswala ya syansi kilichomo ndani ya nchi ya Wales , kituo ambacho kipo chini ya mamlaka ya familia ya kifalme ya Wales , sasa ndani ya kituo hiki mwaka 2016 mpaka 2018 wanasayansi wote waliokuwa wakifanya kazi ndani ya hiki kituo waliondolewa(Evacuated) , haikueleweka sababu maalumu ya kuondolewa kwa wanasayansi ndani ya kituo hiko ni nini , lakini licha ya kwamba wanasayansi hao kuondolewa wote, mwaka 2017 mpaka 2018 kituo hiki kilikuwa chini ya mwanadada mwanasyansi nguli Profesa Clark Stephanie pamoja na mwanafunzi msaidizi wake Ashley Senga Kweka.

Haikueleweka nini kilikuwa kikiendelea ndani ya hiko kituo lakini hakuna mtu aliekuwa akiruhusiwa kuingia ndani ya taasisi hio ya utafiti kwa mwaswala ya kisayansi pasipo ruhusa kutoka kwa jumba la kifalme.

Ilikuwa ni siku ya ijumaa ya tarehe kumi na moja mwezi wa sita ndani ya mwaka 2018 anaonekana Ashley mwanafuzni wa Masters akiwa bize na kazi za utafiti ndani ya taasisi hio kama sehemu yake ya masomo.

Ashley alikuwa ni moja ya wanafunzi pendwa sana wa Profesa Clark kutoka chuo cha Cambridge na hio yote ni kutokana na uwezo wa akili yake lakini pia udadisi aliokuwa nao, na hio ndio ilimpelekea Profesa Clark kumchukua Ashley kama mwanafunzi wake wa karibu sana,yote ni kutaka kupata mrithi wake katika maswala ya sayansi , Profesa Stephanie ni moja ya maporefesa ambao hawakujali sana rangi ya mtu ,wala ukabila bali alichojali sana ni akili ya mwannfuzi na hio ndio ilikuwa fursa kubwa kwa Ashley kwani aliweza kupata ‘attention’ kutoka kwa Profesa Stephanie na baadae kuingizwa mpaka kwenye maabara binafsi ya profesa ilioko Wales(WSRC)

Sasa ilikuwa ni miezi minne tokea Ashley kuanza kufanya kazi kwa ukaribu na Profesa Clark ndani ya maabara ya Wales.

Sasa siku hio ya tarehe kumi na moja ndio jambo la kushitusha lilitokea kwa mara ya kwanza tokea kwa Ashley kufanyakazi ndani ya taaisi hio ambayo haikuwa na watu kabisa.

Ulikuwa ni mtikisiko mkubwa sana uliotokea akiwa chini ya vyumba vya Ardhi katika maabara ya maswala ya kibailojia na kumfanya mwanadada huyu kujawa na kiwewe kwani alikuwa peke yake na Profesa alikuwa ametoka.

Ashley baada ya kuhisi mtetemeko huo wa Ardi alidhania huenda ni tetemeko lakawaida tu kwani alipotezea na kuendelea na kazi yake ya kuchanganya kemikali huku akiwa amevalia PPE.

“Thudd..!!, Bang!!!”

Awamu hio mlio huo ulimfanya kufahamu sasa kwamba kinachoendelea sio cha kawaida na kwa haraka haraka alifuata itifaki za haraka haraka za kutoka ndani ya maabara mpaka maeneo ya nje kuangalia nini kinatokea na ile anatoka na kufika kwenye korido ndefu , ambayo mwisho wake upande wa kushoto kulikuwa na mlango uliofungwa , mlango ambao hakuwahi kuusogelea wala kujua ukifunguka unaelekea wapi , mara mlango ule ulifunguka na likatokea jitu.

“Mamaaaa……!!!!! Clarki alijikuta akitoa ukulele mkubwa mno baada ya kushuhudia kiumbe cha ajabu kikiingia ndani ya maabara, kwajinsi alivyo ona kiumbe hiko alishindwa hata kukielezea kwani zombie sio zoimbe.

“Its hulk.. Yes maybe”Aliongea Ashley huku akitetemeka , ndio kiumbe kilichokuwa mbele yake kilikuwa ni kama Hulk ambaye alimuona kwenye filamu mia kadhaa nyuma na ndio maana akakiita kiumbe hiko kwa jina hilo .

“Where is Clark”Iliongea sauti kama vile ya ngurumo za radi na kumfanya Clark kuogopa mno , muda huu mrembo huyo alikuwa ameshindwa kukimbia kwani aikuwa amedondoka chini kabisa akiwa na koti lake la maabara , akiangalia kiumbe kilichokuwa mbele yake kwa wasiwasi.

“Hiki kiumbe kinamfahamu Profesa?”Aliwaza Clark.

“Hades..!!!”Sauti ilisikika nyuma ya Ashley na kumfanya kugeuka na alivyoona alieingia hapo ndani ni Profesa Clark alipata nguvu na kunyanyuka na kumkimbilia na Kwenda kumkumbatia huku akihema na kuanza kulia .

“It`s Okey Clark , he is not going to hurt you , we need to help him”Aliongea Profesa akimtuliza na kumfanya Ashley kushangaa mno.

“Profesa ni nani ,You know this hulk thing?”

“Nitakueleza , kaandae Injection ZT, plus Stabilizer X now , hurry”Aliongea Profesa kwa sauti na Ashley alimwangalia Profesa Clark usoni na kugundua kwenye macho ya mwalimu wake hakukuwa na woga bali wasiwasi na macho yaliojawa na huruma na hakutaka kuongea Zaidi ya kutoka nduki na Kwenda chumba cha kuhifadhiwa vitu alivyoagizwa.

“Profesa Clark alitoa ishara kwa kiumbe alichokiita jina la Hades na palepale kile kiumbe kilipotea kwenye macho yake na kisha alitembea kwa haraka kwenye korido ndefu kushoto kwenye vyumba hivyo hivyo vya Ardhi, na kufungua mlango uliokuwa unamandihi makubwa juu ‘ROOM X LAB’.

Baada ya nusu saa kupita hatimae Ashley alionekana kutuliza presha na sasa alikuwa kwenye maabara akiwa Pamoja na Profesa Clark na kilichomfanya kutulia ni kutokana na maelezo ya haraka haraka aliopewa na Profesa.

“Profesa kwahio unaamaanisha sio kiumbe bali ni binadamu na mwili wake umevimba kutokana na kirusi kilichopo kwenye mwili wake?”Aliuliza Ashley kwa mshangao.

“Ndio Ashley huyu ni binadamu wa kawaida , anafahamika kwa jina la Hades na tunatakiwa kumsaidia ili kurudisha hali yake ya ubinadamu”Aliongea Profesah uku akisoma ‘Data’ ambazo zinaonekana kwenye Skrini huku kiumbe kinachofahamika kwa jina la Hades kikiwa ndani ya mashine upande wa pili na ilionekana Profesa Clark sindano alizomuagiza Ashley ndio zilitumika kumchoma Hades kiumbe cha ajabu na kumfanya kusinzia.

“There is no way I can help him this time , I am so stupid I don’t have sulution till now”aliongea kwa kujilaumu na kumfanya Ashley kumwangalia Profesa na kutaka kujua kwanini anaongea hivyo.

“Profesa unamaanisha nini huwezi kumtibu , tunapaswa kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida kama ulivyosema ni binadamu”

“Ni kweli lakini kwa sasa hakuna njia , dawa ambayo nilikuwa nikiitegemea haiwezi kufanya kazi kwa hali aliokuwa nayo, maybe kuwe na damu”Aliongea na kumfanya Ashley kushangaa.

“Profesa mbona tatizo lishatatulika hilo kama ni swala la damu pekee?”Aliongea lakini Prfesa alionekana kuwa na huzuni.

“Sio rahihi kama unavyosema Ashley , damu inahitajika ndio kwa ajili yakupunguza makali ya kirusi ndipo dawa yangu iweze kufanya kazi , lakini damu hio sio ya kawaida”Aliongea.

“Unataka kumaanisha nini profesa , damu isio ya kawaida ni ipi hio?”

“Namaanisha damu yenye vinasaba vinavyofanana na damu yake , sio grupu za damu wala Rhesus factor , it`s about DNA compatibility”Aliongea kwa sauti ndogo yenye msisitizo uliojaa wasiwasi., Ashley alijikuta akishangaa mno.

“Tunaweza kuita ndugu zake” Aliongea Ashley na kumfanya Profesa Clark kutabasamu kwa uchungu .

“Hana ndugu”Aliongea kwa sauti ndogo .

“He is in much pain, and if we can’t do anything the situation will become permanent Irreversible”

“Yupo kwenye maumivu makali na kama hatutafanya jambo , hali yake itakuwa hairudishiki milele”

“Profesa you mean he will be like that forever”

“Not Forever, until he Dies”

“Profesa do you have choice to make?”

“Profesa una chaguzi ya kufanya?

”I do have choice to make and before this ,we discussed , if his situation become worse to the point it’s irreversible I have to kill him with leathal dosage”

“Ndio nina chaguzi na niliongea nae kabla ya kutokea hili , kama hali yake itakuwa mbaya kufikia hatua hawezi kurudishika , ninatakiwa kumuua na dozi ya sumu”Aliongea Profesa na machozi palepale yalianza kumdondoka , alionekana chaguzi aliokuwa nayo asipomsaidia Hades basi atahitaji kumuua yeye mwenyewe jambo ambalo hayupo tayari kufanya

Hapana lazima nimsaidie Profesa katika hili , ameniamini sana kwamba nina akili nyingi na ndio maana kanileta kwenye maabara yake kufanya nae kazi Pamoja, lazima nimsaidie , lakini sijui namna ya kumsaidia , Ashley napaswa kufanya nini mimi”Aliwaza Ashley huku akiwa na wasiwasi mwingi mno na kumwangalia Profesa Clark ambaye alionekan kukata tamaa , mtu aliekuwa akionekana kupitia kioo akiwa kwenye kitanda cha chuma fofofo akiwa amefungwa na Kamba nzito alionekana kuwa muhimu mno kwa Profesa Clark na ndio maana alihitaji kumsaidia.

“Profesa Try mine”Aliongea Ashley na kumfanya Profesa Clark kumwangalia ni kama hakuwa amemsikia vizuri.

“Try what?”

“Damu yangu , jaribu kutumia damu yangu”

“Ashley you should know the main difference between blood group and Genotype , why are you saying to try yours?”

“Ashley unatakiwa kujua tofauti kati ya grupu la damu na vinasaba vya damu kwanini unataka tujaribu yako?”

“But we have no choice , should we let him die without trying or let him die while we try?”

“Lakini hatuna chaguzi , vipi tumuache afe tukiwa hatujajaribu au tumuache afe tukiwa tunajaribu?”

“Both Question are incorrect Ashley , what you are saying I already did it , the situation is very complicated in science terminologies”

Profesa alikuwa na haki ya kutokumuelewa Ashley , alichokuwa akitaka yeye ni damu ambayo inavinasaba vya kufanana ndio aweze kumuwekea Hades kupunguza makali ya virusi ili dawa yake aliotengeneza iweze kufanya kazi , lakini Hades hakuwa na ndugu lakini pia hakujua kuwa Ashley ni ndugu wa damu wa Hades.

Kwa upande wa Ashley ni kama sauti ilikuwa ikimwambia kwamba apigilie msumari hapo hapo , damu yake itakuwa na msaada kwa Hades kwa namna yoyote ile , hakujua alikuwa akipata sauti hio kutoka wapi lakini aliamini anaweza kumsaidia Hades.

“Profesa nakuomba tafadhari , naomba tutumie damu yangu”

“Ashley I Don’t know why you are so persistent about trying yours but it will not going to work”Ashley baada ya kuona Profesa anakuwa mgumu alichokua kisu cha kufanyia upasuaji na kuchana mkono wake jambo ambalo lilimshangaza Sana Clark baada ya kuona damu ya Ashley.

“Ashley unataka kufanya nini?”

“Profesa narudia kwa mara nyingine nakuomba tutumie damu yangu tafadhari”Aliongea Ashley na kuanza kulia ni kama akili yake ilikuwa ikiendeshwa na mtu kwani alikuwa akisikia sauti zikimwambia damu yako itamtibu mgonjwa.

Mwisho wa siku baada ya Ashley kusisitiza sana ndipo Profesa Clark alipopima damu ya Ashley kutafuta ‘Compatibility’ na damu ya Hades na matokeo yake wazungu wanasema ‘she was Shocked’ , damu yake na ya Roma ilikuwa ikifanana asilimia mia moja na ya Ashley ikimaanisha kwamba kwa namna yoyote ile wao ni ndugu.

“Profesa nini mbona unashangaa?”

“Mhmh sijui nini kinatokea lakini nahisi Hades ni ndugu yako”Aliongea Profesa na kuanza kumchanganya Ashley lakini profesa tumaini lake lilirudi upya.

“That is Great news Profesa, now you can save him”Aliongea Ashley bila ya kufikira na kumshangaza Profesa kwa ujasili wa Ashley aliokuwa nao .

“Ashley licha ya kwamba ni kweli unadamu inayofanana nae kabisa , lakini haiwezi kukutosha wewe mwenyewe Pamoja na mgonjwa , kwani ni lita tatu na nusu ndio zinahitajika na wewe unaonekana kuwa na lita tano kamili”Aliongea.

“Profesa sidhani kama huna njia nyingine ya kumuokoa mgonjwa , anaonekana kuwa muhimu kwako kuliko ilivyokwangu , fikiria njia profesa tumuokoe”Aliongea Ashley kwa msisitizo lakini Profesa alikosa njia kila alipojaribu kufikiria hakupata jibu na baada yakama dakika kumi na tano alijikuta akipata tumaini lakini hata hivyo aliona njia anayokwenda kufanya inaweza kuhatarisha Maisha ya Ashley.

**********

Story ya Ashley iliwagusa wanafamilia wote hata kwa Roma mwenyewe , Blandina alikuwa amekaa mita kadhaa tokea alipoketi Ashley ,alinyanyuka na Kwenda kumkumbatia Ashley.

“Asante kwa kumuokoa Roma , nashukuru sana..”Aliongea na kuanza kulia ilikuwa ni stori ya kuumiza , kila mmoja alihusudu ujasiri wake na upendo.

“Ashley hujamalizia ilikuwaje?”Aliongea Sophia aliekuwa akifuta machozi alitaka kujua ilikuwaje.

“Kwasasa inatosha , kwani naamini mnaona sasa hivi Roma ni mzima kuhusu maswali mengine nitawajibu ila nataka kujua kama Roma yupo tayari kumsaidia kaka yangu au Lah?”Aliuliza Ashley na kisha Roma alimwangalia , Roma jambo ambalo anakwenda kufanya alimini ni la hatari kubwa , lakini kwa msaada aliotenda Ashley kwake aliamini alipaswa kulipa kwa namna yoyote kwa kumrudishia uzima Denis.

“Okey nipo tayari kumsaidia lakini haimaanishi kwamba nimemsahe ”Aliongea Roma

“Asante sana mwanangu , Asante sana baba.”Damasi alishukuru mno yaani.

MWISHO WA SEASON 9

ITAENDELEA
CONTACT: 0687151346 WATSAPP ONLY
ITAEND
 
Asante sana mkuu .usitubanie sana episode tunaomba za kutosha kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…