Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 333

Ilipita wiki nzima pasipo ya Edna na Roma kuongeleshana, Edna alijua mambo yake na Roma hivyo hivyo alijua mambo yake.

Roma aliendelea na kazi yake katika kampuni , uwepo wa Amina ndani ya kampuni ulisaidia sana kutokana na uzoefu wa Amina , kazi hio alionekana kuipenda kweli na kilichomfurahisha Zaidi ni Projekti ya Kizazi Nyota.

Umaarufu aliokuwa nao Amina tokea akifanya kazi na kituo cha Habari cha kimataifa BBC, ulimfanya kufatiliwa sana mara baada ya Habari kufikia watu kwamba mrembo huyo anafanya kazi ndani ya kampuni mpya ya habari ya Vexto.

Hata kwa upande wa Daudi na Wendy ambao walikuwa wafanyakazi wa kampuni ya Vexto Media walishindwa kuelewa nini kilitokea mpaka mrembo kama huyu kuja kufanya kwenye kampuni ambayo inaanza , ambayo umaarufu wake bado upo chini, lakini licha ya kujiuliza maswali walikosa majibu ya moja kwa moja na jambo moja ambalo walifanyia hitimisho kwenye vichwa vyao ni kwamba Roman ni mtu mzito na mwenye koneksheni na ndio maana ameweza kumfanya mrembo kama huyu kufanya kazi kwenye kampuni yao mpya.

Naam ni siku ya jumapili sasa siku nne tokea Vexto TV(V-television) kuwa hewani kwenye ving’amuzi vyote, siku hio watu wengi ambao walikuwa ni mashabiki wa muziki walikuwa na hamu ya kushuhudia tukio la kihistoria , tukio la mahojiano ya msanii maarufu duniani yaani Christen.

“Director zimebaki dakika 10 tayari na Miss Christen hajawasili”Aliongea Daudi mara baada ya kuingia kwenye ofisi ya Roma, muda huo ilikuwa ni usiku saa mbili , muda ambao ndio’Interview’ ya Christine ilikuwa ikitarajiwa kufanyika mubashara.

Sasa zilikuwa zimebaki dakika kumi kabla ya muda wa ‘interview’ hio kuanza na Christine mlengwa mkuu wa tukio hilo bado hakuwa amewasili.

Upande wa nje ya jengo hili waandishi wa Habari walikuwa wamefurika kiasi kwamba walinzi walikuwa wakifanya kazi ya ziada kuwazuia watu hao kutokuingia ndani ya uzio.

Maswali mbalimbali yalikuwa yakiulizwa juu ya muda ambao Christine alitarajiwa kuwasili , watu wengi walikuwa na hamu ya kumuona Chrisitjne, sio kwenye runinga bali ana kwa ana na ndio maana wakajaa nje ya jengo wakitarajia ujio wa Chrisitne.

Roma alifikiria kidogo na kisha akageuza kiti chake na kuangalia mazingira ya nje na kuona watu kibao wakiwa wamejaa na kwa hali hio aliamini hata Christne akifika ndani ya eneo hilo itakuwa ngumu kupita , kwani watu walikuwa wameziba njia kila sehemu.

“Daudi huna haja ya kuwa na wasiwasi , Christene atafika hapa muda si mrefu kabla ya muda wa mahojiano kuanza”Aliongea Roma na Daudi licha ya kuwa na wasiwasi , aliitikia kwa kichwa na kisha alitoka kwenye ofisi ya Roma na ile anafunga tu mlango , Roma alijikuta akitabasamu.

“Aphrodite unaweza kujitokeza sasa , wafanyakazi wangu wana wasiwasi utachelewa”Aliongea Roma na kufumba na kufumbua mwanamke mrembo sana alionekana mbele ya Roma.Alikuwa ni Christine ambaye alionekana kupendeza kweli usiku huo.

“Hades nisifie nimependeza”Aliongea Chrisitne kwa kingereza na Roma alitabasamu nakuinuka kwenye kiti chake na kumsogelea Chrisitne karibu.

“Hakuna siku ambayo uliwahi kuniangusha kwenye swala la uvaaji , umependeza Christen”Aliongea Roma kwa tabasamu na Christine alitabasamu.

Hakukuwa na meongzi mengi kwani muda ulikuwa umewadia , Roma aliongozana na Christine kutoka kwenye ofisi yake na ile wanafika nje watu walishangazwa na ujio wa ghafla wa Christine b , jambo hilo lilimfanya hata Daudi kushangaa na kujiuliza mara moja imewezekana vipi mrembo huyo kufika ndani ya muda , tena kwa namna ya Ghalfa , lakini licha ya kuwa na maswali mengi juu ya namna Chrisitne alivyofika , hakutaka kuuliza Zaidi kwani muda huo kitu kilichokuwa kikitegemewa kufanyika ni mahojiano na muda ulikuwa ndio unakaribia na watanzania pamoja na Afrika mashariki kwa ujumla walikuwa wakisubiria kumuona Christine akihojiwa kutokea Tanzania , Vexto Television.

Upande wa Osterbay wanafamilia wote walikuwa sebuleni wakisubiria mahojiano hayo , Blandina , Bi Wema , Yezi , Sophia Lanlan, Qian Xi na Edna wote walikuwa wameketi sebuleni wakiangalia runinga.

“Ni mtangazaji gani anakwenda kuapata nafasi ya kumfanyia Christine mahojiano?”Aliuliza Sophia kwa shauku.

“Hatuwezi kujua kwasababu bado wafanyakazi wa V Tv hatuwahafamu , ila naweza kuotea watakuwa ni wafanyakazi hawa hawa waliozeoeleaka hapa Tanzani” .Aliongea Yezi akimjibu Sophia.

Saa mbili na nusu hatimae mahojiano yalianza rasmi na mtangazaji amaybe alipata nafasi ya kuongoza mahojiano hayo alikuwa ni Amina Kanani , mtangazaji maarufu kutoka shirika la Habari duniani la BBC.

Kila mmoja alishangazwa baada ya Amina kuonekana ndio mtangazaji anaemfanyia Christine mahojiano.

“Mbona mnamshangaa?”Aliuliza Blandina kwa shauku, na Sophia alimwangalia Edna kwa macho flani hivi ya kutaka kuzungumza jambo , kitendo ambacho kilimfanya na Blandina kumwangalia Edna.

“Lanlan twende ukalale , unasinzia”Aliongea Edna akimwamsha Lanlana ambaye alikuwa akisinzia , sasa haikueeweka Edna alikuwa akikimbia mahojiano hayo mara baada ya kugundua mtanganzaji alikuwa ni Amina au Lah.

Wanafamilia hao walishangazwa na Edna kutaka kuondoka hapo kabla hata ya mahojiano hayajaanza rasmi na wote kwa pamoja waligeuza macho na kumwangalia , ukweli hakuna ambae alikuwa akijua kinachoendelea kwani Edna ule uchangamfu aliokuwa nao ulikuwa umepotea kabisa na kati ya watu wote ambao waliokuwa na ufahamu na kile ambacho kimetokea alikuwa ni Sophia peke yake.

Sophia aliapata nafasi ya kuongea na Amina na alijitambulsiha kwa Sophia bila aibu kwamba yeye ni mpenzi wa Roma , jambo ambalo lilimshangaza Sophia.

“Sophia dada yako anasumbuliwa na nini , kuna chochote unafahamu?”Aliuliza Blandina na Sophia aliinua mkono wake na kunyoosha kuelekea kwenye runinga.

“Bro Roma yule ni mwanamke wake mwingine na Sister Edna anafahamu”Aliongea Sophia na kumfanya Blandina kuangalia mwanamke mwenye kupendeza aliekuwa akionekana kwenye Runinga.

“Unamaanisha Amina ana mahusiano na Roma?”Aliuliza Blandina kwa mshangao, ukweli Mama yake Roma alikuwa akimfahamu sana mrembo Amina kwani alishawahi kumuona mara kibao akitangaza taarifa ya Habari na kituo cha BBC , hivyo alikuwa akimtambua , lakini sasa swala la kwamba mwanamke huyo alikuwa akijihusisha kimapenzi na Roma , lilimshangaza kwani lilikuwa jipya kwake.

“Ndio maana Sister Edna hayupo sawa , Miss Amina anafanya kazi kama Sekretary wa Bro”Aliongea Sophia na kufanya wanafamilia hao wote kushangaa kwani lilikuwa jambo jipya kwao.

Blandina alianza kumwangalia mwanamke mrembo aliekuwa kwenye runinga na alijikuta akijiambia kimoyo moyo licha ya kwamba mambo ambayo Roma anafanya yamezidi , lakini mwanamke huyo alikuwa mrembo sana na alijikuta akishindwa kumuelewa mwanae ana kitu gani cha ziada cha kuwafanya wanawake warembo kama hao kumpenda.

Sasa ndio wanaelewa kwanini Edna alikuwa amenuna wiki nzima na hakutaka sana stori kabisa na Roma , kumbe yote yalikuwa ni makosa ya Roma kumuajili mchepuko wake kwenye kampuni , tena kampuni ya mke wake.

“Ila Bro Roma kazidi hata mimi ningekuwa kwenye nafasi ya Sister Edna ningekasirika mno, Siste Edna ni mvumilivu mno, ndio maana hata hawalalai chumba kimoja yote Bro anayasababisha”Alipigilia msumari Yezi kwa hasira na maneno yake yalionekana kuungwa mkono na kila mmoja jambo ambalo kwa upande wa Blandina lilimuumiza ndani kwa ndani kwani aliona ni kama yeye ndio mwenye makosa.

Blandina hata ile hamu ya kuendelea kuangalia rungina ilimwishia na alichokifanya ni kutoka hapo na kupandisha mpaka chumbani kwa Edna , licha ya kwamba hakua akijua namna ya kumfariji Edna kurudi kwenye hali yake ya kawaida , lakini alijiambia anaweza kufanya kitu na Edna akarudi kwenye hali yake ya kawaida.

Edna ukweli alikuwa na hasira sana na mwenyewe alikuwa akijishangaa ni kwanini alikuwa na hasira namna hio , kwani sio kwamba ilikuwa mara ya kwanza kwa Roma kuwa na mwanamke, alishindwa hata kutafsiri hasira zake zilikuwa zikisababishwa na wivu au ni kitu gani, mrembo huyu kwa mara ya kwanza alianza kuwachukia Dorisi, Rose , Neema , Amina na Nasra na wiki hio kazini Edna alikuwa ni mwendo wa amri tu na hakuwa na utani hata kidogo jambo ambalo liliwafanya warembo hao wawili kushangaa, mabadiliko ya bosi wao.

“Mama utanisamehe ila nadhani yatanishinda”Aliongea Edna mara baada ya Blandina kuingia kwenye chumba hiko cha mke mwana.

“Edna unamaanisha nini yatakushinda?”Aliuliza Blandina kwa mshangao huku akiomba kile ambacho anakiwazia kisiwe kweli.

“Kama Roma akiendelea hivi nitaachana nae kwa talaka, siwezi kuendelea nae hivi”Aliongea Edna na kuketi kwenye sofa huku macho yake yakionekana kujawa na machozi , kitendo ambacho kilimfanya Blandina amsogelea haraka haraka na kumkumbatia na Edna alianza kulia kwa kwikwi.

“Edna mwanangu usiwe hivi , nitaongea na Roma naomba uvumilie niachie swala hili mimi…”Blandina moyo wake ulikuwa ukiuma , aliona hata kama ni yeye angekuwa kwenye nafasi ya Edna basi huenda angekuwa ashakata tamaa , kwani anachokifanya Roma kilikuwa hakikubaliki kabisa kwa tamaduni za kitanzania..

Edna mwenyewe hakuwa akijielewa ni nini kinamtokea ukweli wiki kadhaa zilizipita alijiona kwamba anaweza kumvumilia Roma kuwa na wanawake wengine , lakini alivyorudi Japani alijihisi ni kama kuna mabadiliko makubwa kwenye mwili wake kiasi cha kumpelekea kutotaka kabisa kumuona Roma na mwanamke mwingine na aliweza kuhisi hali hio alivyoweza kuwafumania Amina na Roma..

Saa tano kamili za usiku ndio muda ambao Roma aliweza kurudi kutoka kazini na hio ni mara baada ya mahojiano kumalizika , Roma baada ya kushuka kwenye gari , alishangaa kuona mpaka muda huo taa za sebuleni bado zilikuwa zinawaka , alitembea mpaka sebuleni na hapo ndipo aliposhangazwa kumkuta mama yake ambaye alionekana ikuwa amesinzia kwenye sofa.

“Mama mbona hujaenda kulala mpaka muda huu ?”Aliuliza Roma akimwangalia mama yake.

“Nilikuwa nakusubiria urudi , vipi huko ushakula , ngoja nikakupashie chakula moto”Aliongea huku akinyanyuka ila Roma alimzuia.

“Nitaenda kuchukua mwenyewe mama wewe nenda ukalale sawa”Aliongea Roma huku akielekea upande wa jikoni kwa ajili yakutafuta chakula , alikuwa na njaa ndio maana kwani tokea apate chakula cha mchana akuweza kula chakula kingine.

Roma hakuwa na haja ya kupasha chakula yeye alijipakulia kama vilivyo na kutoka nacho, lakini mama yake aliemwambia kwamba aende kulala bado alikuwa hajaenda na alionekana alikuwa akimsubiri.

“Mama mbona unaonekana kuwa na wasiwasi?”Aliuliza Roma.

“Nina wasiwasi na mkeo Edna..”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Mke wangu anashida gani?”Aliuliza Roma huku akikaa kwenye kiti.

“Nilikuwa sijui kinachoendelea mpaka usiku wa leo Sophia alivyoeleza kinachoendelea..”Roma alijikuta akimwangalia Mama yake , alikuta akishangaa ni kipi kinachoendelea , ukweli swala la kufumaniwa alikuwa ashalipotezea, licha ya kwamba Edna hakuwa kiongea nae alijiambia hasira zikishuka atarudi kuwa sawa tu , kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Edna mkeo anafikiria talaka “Aliongea Blandina kwa sauti ya upole na kumfanya Roma kuweka kijiko chini , alikuwa ni kama hajasikia vizuri.

“Mama aliesema hivyo ni Edna?”

“Roma nishakuelezea fanya mambo yako lakini usimfanye Edna akakosa uvumilivu, nimekusubiria hapa ili nipate kujua unachowaza, kama upo tayari kuachana na Edna na kuoa moja ya wanawake wako mimi sina pingamizi , ila sitaki kuona haya Maisha mnayoishi wewe na Edna yanaendelea ni bora muachane tu , wanandoa gani hamlali chumba kimoja”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kufikiria.

“Mama nitaongea kesho na Edna, kuhusu mimi kumuacha Edna na kumuoa mwanamke mwingine hicho kitu hakiwezi kutokea”Aliongea Roma na Blandina alivuta pumzi na kuzitoa kwa wakati mmoja.

“Sawa kesho hakikisha unayamaliza na amani irudi”Roma ilbidi kuitkia kwa kichwa huku akiendelea kula.

Asubuhi Roma aliamka mapema na Kwenda mpaka kwenye chumba cha mazoezi huku akili yake ikiwaza namna ya kuyamaliza na Edna , ukweli hakuelewa ni kwa namna gani anaweza kumrudisha Edna kwenye hali yake.

Roma baada ya kumaliza kuchukua mazoezi alirudi chumbani kwake na kuoga kwa ajili ya kuelekea kazini asubuhi , hio kwani ilikuwa ni jumatatu.

“Sophia Edna yuko wapi?”Aliuliza Roma mara baada ya kukuta kiti cha Edna kikiwa tupu jambo ambalo Roma hakuwa amelizoea kwani muda wa asubuhi kama huo Edna angekuwa pembeni ya Lanlan.

“Mama yake Lanlan kaenda kazini na amesema akirudi ataniletea mdoli unaofanana na Tembo”Aliongea Lanlan na kumfanya Roma kidogo kuwaza na kisha kuketi kwenye kiti, alijikuta akimwangalia Lanlan na kuishia kutabasamu , siku zote Lanlan akiwa anakula hakuwa akitaka utani kabisa yaani hakutaka hata kuongea, lakini swala ambalo linamuhusu mama yake likiongelewa atasikiliza kwa umakini.

Mashindano yalikuwa yakitarajiwa kuanza rasmi siku ya kesho , kwahio Roma alikuwa ni lazima aende kwanza kazini , lakini bado akili yake haikuwa sawa kwani bado hakuwa ameonana na Edna na wakaongea kuyamaliza , hivyo Roma aliona jambo la kwanza asubuhi hio kwanza ni Kwenda Posta kumuona Edna kwanza.

Roma baada ya kumaliza kunywa chai alimchukua Sophia na kumpeleka mpaka kwenye jengo la kampuni.

“Bro mbona haushuki?”Aliuliza Sophia baada ya kumuona Roma hashuki.

“Sophia wewe nenda kachukue mazoezi , kesho ni siku yako kuonyesha kipaji , ngoja kwanza niende kuonana na Mke wangu”.

“Eti ‘ Mke wangu’, ujitahidi sasa , maana Sister Edna anaonekana kukasirika kweli , najikuta muda mwingine namuonea huruma kama mwanamke mwenzake , anyway Goodluck”Aliongea Sophia na kisha aliondoka kuelekea ndani ya jengo huku Roma yeye akigeuza gari.

Dakika chache tu Roma aliweza kufika kwenye jengo la kampuni na baada ya kuegesha gari moja kwa moja aliingia ndani ya jengo hilo , alikuwa na wiki kadhaa hakuwa amefika kwenye hilo jengo na ilifanya wanawake wengi kumwangalia kwa macho ya husuda na Roma alitambua kwanini walikuwa wakimwangalia , ujio wa Christine ulifanya wafanyakazi wengi kujiuliza Roma aliwezaje kumualika mtu mzito kama huyo, ndio maana walionekana kujiuliza maswali , lakini kumuheshimu kwa wakati mmoja.

“Miss Airport za siku nyingi?”Alisalimia Roma mara baada ya kumfikia Sekretary wa Edna na baada ya Monica kumuona Roma alijjifanyisha yuko bize na kazi zake , yaani alikuwa nikama hakumuona, ila Roma hakujali alinyoosha moja kwa moja kuusogelea mlango wa kuingia kwenye ofisi ya Edna.

“Boss hayupo”Aliongea Monica kwa sauti kavu na kumfanya Roma kugeuka na kumwangalia.

“Kaenda wapi nina shida nae”

“Wewe jua tu hayupo acha maswali mengi”Alijibu kwa kejeli na kumfanya Roma kumsogelea.

“Kama hutaki kuniambia basi nitamsubiri ndani ya ofisi yake “Aliongea Roma huku akiurudia mlango.

“Kaenda uwanja wa ndege kuna mgeni wake muhimu amesema anakwenda kumpokea”Aliongea Monica huku akimwangalia Roma kwa macho makavu.

“Airport , yeye mwenyewe?”Aliuliza Roma , ukweli alishangaa ni mgeni gani ambaye Edna kaenda kumpokea yeye mwenyewe na sio dereva wa kampuni.

“Mbona una maswali mengi hivyo , nishakupa jibu unaweza kuondoka”Aliongea.

“Kandoka saa ngapi?”Aliuliza Roma na kumfanya Monica kumwangalia kwa mara nyingine.

“Hata dakika kumi hazijaisha tokea aondoke”Aliongea na Roma hakuendelea kusimama hapo , alipiga hatua kuondoka na kuingia kwenye lift , huku akili yake ikipata moto ni mgeni gani ambaye amemtoa Edna ofisini na Kwenda kumpokea.

Roma akili yake ilimwambia aende huko huko Airport, alijiambia kwasabau Edna alitoka ndani ya dakika Zaidi ya kumi na tano zilizopita basi ni rahisi kumkumkuta njiani.

Na ni kweli dani ya dakika therathini tu hivi baada ya kuendesha gari kwa spidi hatimae aliweza kuona Mercedenz Benz ya Edna ikisonga taratibu taratibu , Roma alitabasamu na kupunguza mwendo.

Baada ya dakika kama ishirini hatimae Roma aliweza kufika uwanja wa ndege na hio ni baada ya kama dakika tano ya Edna kufika , Sasa ile Roma anashuka kwenye gari , alimuona Edna mita kadhaa mbele yake akimkimbilia mwanaume mmoja wa kizungu na wakakumbatiana kwa furaha kubwa.

Roma ni kama hakuamini macho yake , kwani hakutegemea hata siku moja kumuona Edna kumkimbilia mwanaume na kumkumbatia kwa furaha kiasi kile.
 
SEHEMU YA 334.

“Edna I missed you so much , very happy to see you again”

“Edna nilikumisi sana , nimefurahi Zaidi kukuona kwa mara nyingine”

“Mimi pia Rich, karibu Tanzania”Aliongea Edna ,mwanaume mzungu mkononi akiwa ameshikilia mbwa mdogo mweupe pamoja na mkoba.

Edna alionekana kuwa na furaha isiokuwa ya kifani , kwa jinsia mbavyo alikuwa akionekana ni kama vile mtu aliekuwa mbele yake walipotezana kwa miaka mingi na sasa wameonana tena na juu ya yote alikuwa amemisi , yaani ilikuwakama mtu ambavyo amemuona mtu wake wa karibu sana baada ya miaka mingi.

Kitendo cha Edna kukumbatiana na mwanaume ambaye hakuwa akimfahamu , lakini pia kuwa na furaha mno , kilimfanya Roma kuhisi wivu usiokuwa wa kawaida , ghafla maneno ya mama yake usiku wa jana yalianza kuibuka kwenye akili yake.

“Edna anafikiria talaka”

Kwa nafasi aliokuwa nayo Roma ilikuwa sahihihi kabisa kuwa na mawazo ya aina hio , kwani mwanaume aliekuwa mbele yake akiwa na mke wake alikuwa ni kijana mtanashati alievaa akapendeza , alikuwa mzungu lakini ambaye alionekana kijana Zaidi mwenye kujipenda.

Roma hakujielewa ni muda gani alitoka kwenye gari , lakini ghafla tu alikuwa amewafikia Edna na yule mwanaume aliefahamika kwa jina la Rich.

“Wewe ni nani ambaye unakumbatia wake za watu bila kuwa na wasiwasi?”Aliongea Roma kwa sauti kavu na hio ni mara baada tu ya kuwafikia , aliongea kwa kingereza hivyo mwanaume yule alielewa haraka sana.

“Are you crazy?”Aliongea yule mwanaume akimwambia Roma je ni chizi , ukweli yule mwanaume alimuona Roma wa kawaida sana na hivyo hakumtambua ndio maana akamwita chizi.

“Romaa..!!!” Edna alijikuta akipatwa na mshangao baada ya Roma kumsukuma ngumi mgeni wake na kudondoka chini kama furushi , kitendo kile kilimfanya Edna kushangaa mno huku hasira zikianza kumpanda kiasi kwamba alishindwa hata kupumua.

“Unajifanyisha hutaki kuniongelesha wiki nzima , kumbe unamipango yako kichwani eh.. unafanya hivi kunikomoa sio?”Aliongea Roma kwa namna ya kumfokea Edna.

Upande wa yule mwanaume hakuamini kama amesukumwa chini ghafla sana aijikuta akitema damu kwani alijigonga vibaya.

Edna alimwangalia Roma kwa hasira sana , huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake , licha ya macho yake kujawa na machozi lakini alimwangalia Roma kwa chuki sana na hakujibu chochote Zaidi ya kumpiga kikumbo Roma na kumpita.

“Rich I am so so sorry”Aliongea Edna kwa huzuni huku akimsaidia Rich mzungu kusimama .

“Edna huyu mtu chizi ni nani?”Aliuliza Rich kwa hasira huku akimwangalia Roma ambaye alionekana kutweta kwa hasira , kitendo cha Edna kumpita na kumsaidia mwanaume yule kilimfanya kupandwa na hasira maradufu.

“Rich samahani nitakuelezea kwenye gari , tuondoke kwanza hapa”Aliongea Edna kwa kubembeleza sana , mtu aliekuwa mbele yake alionekana kuwa mtu muhimu kweli kiasi ambacho kilizidisha wivu kwa Roma.

“Edna unapaswa kuwa na maelezo ya kutosha siwezi kuacha hili lipite , kudhalilishwa siku yangu ya kwanza tu kuja Tanzania”Aliongea yule mwanaume huku akichukua begi lake na alimwangalia Roma kwa kumkagua na kisha alianza kupiga hatua.

Edna hakutaka kubakia pale hata sekunde kwani watu walikuwa wakiwaangalia na ndio maana alitaka kuondoka mara moja , kwani kitendo alichofanya Roma kilikuwa cha udhalilishaji kwa mgeni wake.

“Edna nipe majibu kabla ya kuondoka”Aliongea Roma kwa amri na Edna alisimama na kumwangalia Roma.

“Sijui nini kimekufanya ukanifatilia mpaka huku na kuja kunidhalilisha asubuhi yote hii ,Sina cha kukujibu”Aliongea Edna na kisha akaanza kupiga hatua kumsogelea Rich Mzungu.

Roma ni kama hakuwa akiamini aliekuwa mbele yae ni Edna , alimuona kama tu mwingine kabisa, alisimama kwa dakika kama tano hivi, alikuwa ni kama hajielewi na ile akili yake inakaa sawa , gari ya Edna haikuonekana mbele yake.

“Nimefanya nini tena?”Alijiuliza Roma mara baada ya akili yake sasa kurudi kuwa kawaida alianza kujilaumu ka kitendo ambacho alifanya na ukweli hakuelewa hata kilichomfanya kuchukua uwamuzi ule ni nini na alianza kujilaumu na kujiona kafanya jambo la kijinga pasipo ya kujua undani wa jambo lenyewe.

Roma aligeuka kuangalia mazngira na kuona watu walikuwa wakimshangaa na kumuonea huruma , huku wengine wakionekana kama walikuwa wakimcheka, walikuwa ni kama walikuwa wakimnanga kwa kukataliwa na mwanamke asubuhi asubuhi, sura zao zilikuwa zikionyesha kabisa kila kilichopo mioyoni mwao’ Bro tafuta wa saizi yako’ hivyo ndio namna sura zao zilivyoonekana.

Roma alitembea mpaka kwenye gari yake na kuingia ndani na kulitoa nduki, huku akiwa ni mwenye majuto kwenye kitendo alichokifanya , kwenye Maisha yake hakuwahi kupatwa na hisia ambazo alikuwa nazo mara baada ya kumuona Edna kuwa na mwanaume mwingine , alijihisi ni kama visu vilikuwa vikimkata mkata kata kwa ndani, lakini licha ya hivyo aliona kitendo alichofanya kilikuwa cha kipumbavu kwani angeuliza kwanza.

Sh**t , nimefanya ujinga kweli”Aliwaza Roma huku aking’ata meno kwa hasira , alionekana kujikasirikia kwa kitendo chake.

*******

“What!!!.. Edna..!! , you are married?”Aliongea yule mzungu kwa mshangao mkubwa mara baada ya Edna kumweleza Rich Mzungu kwamba yule mtu aliemsukuma ni mume wake wa ndoa kisheria , jambo ambalo lilimfanya Rich Mzungu kushangaa mno.

“Edna kwanini hukuniambia mapema kama umeolewa?”

“Rich sikufanya makusudi kutokuwaambia , mambo yalitokea haraka haraka sana na hata harusi hatukufanya”Aliongea Edna huku akiweka umakini kwenye usukani.

“Edna huna haja ya kuwa na wasiwasi tena , nilimdhania ni kichaa , baada ya kuingilia mazungumzo yetu ghafla kumbe ni mume wako , Nisamehe kwa kumuita mume wako Chizi”Aliongea Rich huku akionekana kujutia,, ukweli hakujua kama Edna alikuwa ameolewa na ndio maana hata walivyoonana alikuwa huru kwake.

“It1s fine Rich ,I am so embarrassed right now”

“Usijali Rich , ninaona aibu sana”

“Huna haja ya kuwa na aibu alichokifanya mume wako ni ubinadamu, unajua hata mimi nishawahi kumpiga ngumi mwanaume mwenzangu , baada ya kumuona akiwa na ukaribu na mke wangu Sasha”

“Really!!”

“Ndio .. hahaha,,, Edna huwezi kuamini kila nikikumbuka lile tukio mpaka leo najionea aibu, muda mwingine ukimpenda mtu sana pia inakuwa tatizo kwa afya yako kwani kila mwanaume anaekuwa karibu na mkeo anakuwa adui yako , kwa jinsi nilivyoona mumeo anakupenda mno ndio maana alichukua maamuzi kama yale , udhoefu wangu katika mahusiano inaonekana mpo kwenye migogoro”Aliongea Rich Mzungu na Edna aitingisha kichwa kuashiria ni kweli wapo kwenye migogoro.

“Edna usijali ilimradi nimekuja Tanzannia kwa ajili ya kazi ambayo umenipatia nakuahidi Sasha akija hapa atakufundisha mbinu za kuishi vizuri na mume wako, Edna naongea hivi kwasababu najua udhaifu wako haha..”Aliongea na Rich na kumfanya Edna kuona aibu , lakini licha ya maneno ya Rich hasira zake juu ya Roma hazikuwa zimeisha kabisa na alikuwa akipanga kuchukua hatua kubwa Zaidi , alijiambia kitendo kile kilikuwa ni udhalilishaji, pili aliumia bada ya kugundua Roma alikuwa akimfatilia na mpaka hapo aliona Roma hakuwa akimwamini.

“Ananiona mimi ni Malaya kama yeye”

Richard Odswelo ni mwanamitindo Mzaliwa wa Ufaransa ,ni rafiki wa siku nyingi sana na Edna , walikutana kwa mara ya kwanza walivyokuwa masomoni Oxford na wakawa marafiki , kilichomfanya Edna kumfahamu Rich ni kupitia kwa mwanadada aliefahamika kwa jina la Sasha Raymond ambaye ndio mke wake Rich,

Sasha Raymond na Edna walikuwa wakichukua kozi moja , hivyo ukaribu wa kimasomo ndio uliowafanya wawili hao kufahamiana , baada ya Sasha siku moja kumtambulisha Rich kwa Edna ndio ukaribu wao ulipoanzia, hivyo Edna marafiki zake wakubwa mpaka anamaliza masomo yake Uingereza walikuwa ni Sasha na Shemeji Rich.

Rich alikuwa mtu mchangamfu sana , hivyo aliweza kuzoeleka haraka haraka na Edna na kukumbatiana ilikuwa ni moja ya salamu ambayo walikuwa nayo tokea walipokuwa masomoni , hivyo Edna alichukulia swala la kawaida sana na sio kwamba kuna mapenzi kati yao , bali ni ule uzungu wa Rich aliomzoesha Edna.

Edna ameanzisha project mpya ya mavazi ndani ya kampuni yake, lakini kutokana na kwamba kampuni hio ilikuwa ikiyumba sana kimapato ndio akamshawishi Rich kuja Tanzania kwa ajili ya kumsaidia katika kudizaini mavazi kwa kutumia ‘material’ mapya ambayo yanatarajiwa kusambawa mwezi mmoja mbele na kampuni yake , malighafi zinazozalishwa na Yamakuza.

Sasa Edna baada ya kupigiwa simu na Rich kwamba amefika Tanzania , aliona haitakuwa vyema kumwagiza mtu Kwenda kumchukua na akaona jambo hilo alibebe yeye mwenyewe, sasa kutokana na kwamba ni Zaidi ya miaka minne hawajawahi kuonana Zaidi ya kuwasiliana kwa simu , ndio maana Edna akawa ‘Excited’ sana baada tu ya kumuona rafiki yake wa kitambo.

Upande wa Rich hakuwa na taarifa ya Edna kuolewa na hata alivyomuona Roma hakuweza kumdhania kabisa kama anaweza kuwa mume wa Edna wala mchumba kutokana na muonekano wa Roma.

‘Umdhaniaye kumbe sie’ ndio kilichotokea.

*******

Roma hakurudi kabisa nyumbani siku hio na usiku ulimkutia Upepo Beach akiwa na lishangazi lake Neema Luwazo ,yeye ndio alekuwa wa kwanza kufika kwenye hayo maeneo na Neema ndio alimkuta.

Mzee Chino alikuwa amepona kabisa na hakuwa yule ambaye wiki zilizopita kuchomwa kisu , alikuwa mzima kabisa na alikuwa ameketi na Roma , mzee huyu alikuwa akitafuta nafasi ya kumshukuru Roma kwa kile alichokifanya , lakini hakupata nafasi hio , hviyo mara baada ya kumuona Roma kaja hayo maeneo aliona hio ndio nafasi nzuri ya kumshukuru.

“Mzee Chino huna haja ya kunishukuru namna hio , nilichofanya ni kwa ajili ya Neema , sikutaka kumuona akiwa mwenye huzuni kwasababu yako ulikuwa wajibu wangu kwake kumsaidia ”Aliongea Roma lakini Mzee Chino hakukubali kabisa aliona bado alikuwa na deni kwa Roma, lakini wakati huo akitaka kujua angalau ni muujiza gani ambao Roma kaingiza kwenye mwili wake , kwani hakuwa kama yule mzee wa mara ya mwanzo , Mzee Chino alihisi mwili wake ni kama umerudi kwenye ujana wake na siku ya jana aliweza kulala na mwanamke na alipiga shoo kwa muda mrefu kiasi kwmaba alijishangaa yeye mwenyewe, kwani tokea afikishe miaka sabini na tano alikuwa kila akikutana na mwanamke dakika tano zilikuwa nyingi sana kwake na utakuta tayari kashamaliza lakini siku ya jana alienda Zaidi ya dakika arobaini.

Reborn of Chino The Master”Aliwaza kwenye kichwa chake huku akimwangalia mrembo alikuwa akijigalagala kwenye kitanda cha sita kwa sita kwa uchomvu, Chino The Master ndio jina alilokuwa akiitwa wakati wa ujana wake, sasa baada ya kumpelekea moto mrembo kwa dakika arobaini na tano alijiona amezaliwa upya na alijihisi mwepesi kweli.

“Mr Roma nadhani sasa najua kwanini Neema anakupenda sana?”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Roma kumwangalia , hakujua alikuwa akitaka kumaanisha nini.

“Unamaanisha nini Mzee?”

“Tokea uufanyie mwili wangu muujiza , nimejikuta nimerudi katika hali ya ujana , nguvu zangu zilizopotea zimerudi upya hahaha..”Aliongea na Roma alitabasamu.

“Mzee Chino nilichokufanyia naomba Kibaki kuwa siri yako na hakikisha damu yako haigusani na ya mtu mwingine , kwani inaweza kuleta maafa”Aliongea Roma huku akinywa bia yake mfululizo na maneno yake ni kama yalimchanganya mzee Chino na alishindwa kuuliza Zaidi baada ya ujio wa Neema.

Neema alikuja ufukweni hapo pasipo ya kutegemea kama atamwona Roma na alijikuta akifurahi mno na Roma alirabasamu mara baada ya kumuona mwanamama huyu na alijiambia hakuna kurudi nyumbani , kwanza hakuwa na sababu ya kurudi , kwani sio kwamba angepokelewa kwa shangwe , Edna ndio huyo kwanza alikuwa amemchunia na ni Zaidi ya wiki sasa hawajaongea na siku hio akayakoroga Zaidi , hakutaka hata kujua tena yule mwanaume ni nani na muda huo alitaka kupumzisha kichwa chake tu.

Na ndio kilichotokea kwani walichukuana na Neema na Kwenda kwenye hoteli yake na walifanyana kila aina ya staili na Roma kupitiwa na usingizi.

“Edna leo umeongea na Roma?”Aliuliza Blandina baada ya kumaliza kula chakula cha usiku na Edna alitingisha kichwa kwamba hajaongea nae.

“Kuna jambo lingine limetokea leo Edna?”Aliuliza Blandina kwa wasiwasi , ukweli tokea Edna alivyorudi nyumbani alimuona hayupo kawaida kabisa na kwa uzoefu wake alihisi kuna kitu kimetokea ila alishindwa kujua ni kitu gani , kwani Edna alikuwa akimwangalia Lanlan kwa huzuni.

“Hakuna kilichotokea mama , usiwe na wasiwasi”Aliongea Edna huku akimchukua Lanlan na kupandisha nae juu, ilikuwa ni short short tu Edna alivyokuwa akijibu.

Edna baada ya kumuogesha Lanlan na kumvisha nguo za kulalia na kumlaza , alifungua droo anayohifadhia vitu vyake muhimu na kisha akatoa bahasha ambayo ndani yake ilikuwa na karatasi za mkataba wa ndoa kati yake na Roma.

Baada ya kuzitoa alikaa kwenye sofa na kuanza kuzisoma na alijikuta ni kama mwenye kushangaa kwani aligundua mkataba wao na Roma ulikuwa umebakia siku kumi na tano tu mpaka kuisha.

Edna aliangalia mkatabaa huo kwa dakika kadhaa mpaka alipouweka kwenye meza na kutafuta simu.

“Suzzane inawezekana kupata kibali cha kumlea mtoto bila ya kuwa na ndoa?”Aliongea Edna mara baada ya simu kupokelewa na alionekana alikuwa akiongea na Suzzane.

“Unamaanisha nini boss, usiniambie unapanga..”

“Just incase….Suzzane”Alijibu Edna na kikatokea kimya cha muda kidogo.

“Boss inawezekana kabisa ni makubaliano tu na upande wa kituo cha kulelea Watoto kama watakubali kusaini karatasi na kukuruhusu kulea kihalali”Alijibu Suzzane na Edna alitabasamu.

“Okey Suzzane asante”Alijibu Edna na kukata simu na kisha alimwangalia Lanlan na kutabasamu na kuanza kupitisha mkono wake kwenye kichwa chake.

(Masikini sijui siku akijua Lanlan ni mtoto wa Roma itakuwaje)
 
SEHEMU YA 335.

CANADA-TORONTO.

Ni nje ya jengo kubwa la taasisi ya utafiti ya MAYA anaonekana Yan Buwen akitoka kwenye gari kampuni ya Bentley huku akipokelewa na mzungu mmoja wa makamo kati ya umri wa miaka hamsini hivi , mwanaume ambaye amevalia suti , huku akiwe na nywele za rangi nyeupe (Blonde hair)

“Mr Yan Buwen karibu sana kwenye taasisi yetu , naitwa Profesa Elon John Mkurugenzi”Aliongea yule mzungu kwa Kingereza na Yan Buwen alitabasamu.

“Nakufahamu Profesa Elon nimefurahi kukutana na wewe ana kwa ana”Aliongea na kumfanya Profesa Elon kutabasamu huku akimpa ishara ya kumfuata.

Taasisi ya Maya ni moja ya kampuni kubwa sana za kitafiti ambazo zipo kwenye mji huu wa Toronto, jengo la taasisi hili lenyewe limejengwa kwa usanifu wa hali ya juu , likiwa limeenda hewani kwa jumla ya Floor ishirini na lote lilitumiwa na wanasayansi ambao wapo chini ya kampuni ya MAYA.

Profesa Elon ni mwanasayansi maarufu ndani ya taifa la Canada ndio ambaye alikuwa akiongoza taasisi hii , Profesa Eloni alijizoelea umaarufu baada ya kuongoza utafiti wa chanjo ya Ebola chini ya taasisi hio , wakati huo akiwa bado hajafahamika kwa watu wengi na baada ya kuweza kuongoza timu yake na kugundua chanjo ya Ebola ndipo alipopandishwa cheo na kuwa mkuu wa taasisi hii inayomilikuwa na Maya Group kwa asilimia sitini na serikali ya Canada kumiliki asilimia arobaini zinazobaki.

Profesa huyu pia aikuwa akimfahamu Yan Buwen , kifupi tokea siku ambayo Yan Buwen alikataa tuzo ya Noble Prize aliweza kuwa maarufu sana kwa wanasyansi wengi, katika historia hakuna mtu ambaye ashawahi kukataa tuzo ya Noble Prize hata siku moja lakini miaka miwili iliopita Yan Buwen mara baada ya kushinda Tuzo hio aliikataa , huku akitoa sababu kwamba kazi yake ya utafiti haiwezi kupimwa kwa kupitia Tuzo ya Noble Prize.

Ujio wa Yan Buwen ndani ya taasisi ya Maya ulikuwa ukifahamika na ndio maana Profsa mwenyewe alitoka kumpokea Yan Buwen.

“Mr Yan Buwen nataka nikutembeze kwenye idara mbalimbali katika taasisi yetu kama hutojali”Aliongea Profesa Elon.

“Profesa muda wangu hapa Canada unahesabika , nipo hapa kwa ajili ya kuona teknolojia ‘Growth Acceleration’ peke yakee , labda siku nyingine nikipata nafasi nitaweza kuona idara zenu”Aliongea Yan Buwen kwa namna ya upole , kwa namna ambavyo alikuwa akiongea utadhania kwamba alikuwa mtu mmoja mpole sana , lakini ukweli Yan Buwen anakidhi vigezo vya kuitwa Mad Scientist.

Profesa Elon alitabasamu na kumwambia Yan Buwen kumfata na wote kwa pamoja waliingia kwenye Lift na palepale Lift iliwachukuwa Kwenda chini ya jengo hilo na ndani ya sekunde kama arobaini hivi hatimae Lift ile ilifunguka na wakatokea kwenye korido ndefu ambayo ina msururu wa vyumba kulia na kushoto , ni sehemu ambayo haikuwa na mwanga mkali Zaidi ya mwanga wa LED na kufanya eneo hili kuonekana kupendeza sana , ikichangizwa na namna ambavyo limejengwa kwa usanifu wa hali ya juu.

Profesa Elon alihesabu vyumba mpaka kufikia kwenye chumba ambacho kilikuwa na kibao juu ambacho kimeandikwa kwa namba za kirumi XVIIXVII.

“Ulinzi hapa ndani ni wa kawaida sana Profesa, sijaona ‘Security Layer’ yoyote”Aliongea Yan Buwen.

“Sio kweli Mr Yan Buwen , nadhani umegundua sijabonyeza kitufe chochote tulivyoingia kwenye lift , lakini tumekuja mpaka hapa?”

“Ndio ni kweli”

“Our institution is Computalized with AI system that is how security works here, there is threshold criteria for a person to pass through security layers, this building is full automated”

“Taasisi yetu imeunganishwa na mfumo wa akili ya kutengeneza , ndio ulinzi unavyofanya kazi hapa, kuna vigezo vya vizingiti kwa mtu kupita kwenye matabaka ya usalama , hili jengo linajiendesha lenyewe”Aliongea na palepale mlango ulitoa sauti ya ‘chwii .. chwii; na ulifunguka na wote kwa pamoja wakaingia ndani.

Ni kweli kabisa alichoongea , yaani hapa hakuna maswala sijui ya ‘Finger Print’ wala ‘password’ kila kitu kilikuwa ni cha kiotomatiki.

Yan Buwen alijikuta akisifia muundo wa eneo lote la taasisi kwani kila sehemu aliopita ilikuwa imejengwa kwa usanifu ambao ni ngumu sana kuonekana sehemu nyingine yoyote , ilikuwa ni kama yupo mbele ya muda(From the future).

Mbele yake ndani ya chumba hiko kulikuwa na makabati ya vioo yaliopangiliwa kwenye meza , kabati moja lilikuwa ni kama sanduku na ndani yake kulionekana mtu akiwa amelala kwenye majimaji huku akiwa amepitishiwa vifaa vingi ambavyo kazi yake haikueleweka mara moja. Kubati lingine lilikuwa na mifupa kama mifupa iliokuwa ikiogelea kwenye majimaji mazito pia.

“This is what you requested , acceleration growth technology”Aliongea profesa Elon na kisha alisogelea kijimeza kilichokuwa upande wa kulia. Na kunyanyua kijirimoti kidogo na pale vioo vilivyokuwa vimetenganisha makabati yale na wao , vilibadilika na kuwa kama runinga na ikaanza kuonyesha namna ambavyo mtu anaanza kujitengeneza tokea yai la mwanamke linaporutubishwa na mbegu za kiume , yaani hatua zote za namna kiumbe kinavyokuwa kwenye tumbo la mwanamke ndio kilichokuwa kikionekana kwenye skrini hizo.

“Hatua zote hizi zinachukua mwezi mmoja tu mpaka kukamilika na kuwa mtu kamili na sio miezi tisa “Aliongea Profesa Elon.

“Mwezi mmoja!!?”

“Yes!, one month give or take “Aliongea akimaanishwa kwamba kwa kutumia teknolojia yao , wanaweza kufanya mtoto kukua kwenye mashine hizo mara baada la yai la mwanamke kurutubishwa na mbegu za kiume na mtoto kuzaliwa baada ya mwezi mmoja tofauti na miezi tisa ya kawaida ya binadamu kuzaliwa , hio ndio maana ya teknoljia hio ya kuongeza kasi ya ukuaji wa kiumbe.

“Baada ya kiumbe kuzaliwa anachukua muda gani mpaka kuwa mtu mzima?”Aliuliza.

“Miezi minne pekee , angalia huu mfupa”Aliongea huku akibonyeza na rimoti na skrini ilianza kuonyesha kijimfupa kidogo sana kwenye skrini , lakini mara baada ya kuwekewa majimaji palepale mfupa ule ulianza kuongezeka ukubwa kwa kasi kubwa sana, yaani ikimaanisha kwamba ulikuwa ukikomaa huku ukiongezeka urefu.Yan Buwen alijikuta akitabasamu bila kupenda.

“Kwahio kupitia hii teknolojia naweza kujitegengenezea Clone ndani ya miezi tisa kamili”


“Ndio kupitia hii teknolojia unaweza kukuza kichanga na kuwa mtu wa miaka ishirini ndan ya miezi tisa kamili Mr Yan Buwen ,ni mafanikio makubwa sana ambayo taasisi yetu mpaka sasa imefikia”Aliongea na Yan buwen alitabasamu.

“Kupitia teknolojia hii nitaweza kutengeneza kopi ya Hades ndani ya miezi tisa kamili”Aliwaza Yan Buwen kwenye kichwa chake.

“Teknolojia ya kupunguza ukuaji wa hata yenyewe si ipo , maana kwa spidi hio mtu si atazeeka kwa haraka?”Aliuliza.

“Kila kitu tunacho Mr Yan Buwen,tumegundua homoni kinzani(Antagonist Super Growth Hormone) ya ukuaji , ukisharidhika na kiwango cha ukuaji kilipofikia unachofanya ni kuingiza milimita 200 za ujazo na mtu wako atapitia mchakato wa ukuaji asili(Natural Growth) hivyo ataanza kukua kama mtu wa kawaida”Aliongea na Yan Buwen alifurahi sana kusikia.

“Hahaha… a miracle in the making , it is very good to worship science , light has illuminated us”

“We are illuminat , everything is light and science is light”

“Sisi ni tuliomulikwa na Nuru , kila kitu ni Nuru na sayansi ni Nuru”Alijibu Profesa Elon huku akiweka ishara ya ‘Triangle’ kwa kutumia vidole vya mikono yote miwili na vilevile kwa Yan Buwen.

ITAENDELEA SIKU YA JUMATATU

NICHEKI WATSAPP 0687151346 ULIZIA MWENDELEZO
 
edina muda sio mrefu itabidi akubali kwa hiari kukojozwa, maana ashaanza wivu wa waziwazi........
 
Tatizo Roma ni bwege hawezi kujua kijacho huko mbele...yaani huo uungu uliomo ndani yake hajui kuutumia
Anazingua sana...plan anayo mzee wa kichaga yy anaishi tu na kupambana na watu wanaochokoza mademu zake tu.
 
Lete mavitu tuenjoy
 
Singanojr chukua karne nzima lakini ukituma usitume sentensi kadhaa. Tuma mzigo mzito unaolingana na karne unazochukua kuposti!!!!!
 
SEHEMU YA 336.

Ilikuwa ni siku ya Jumanne , Roma alirudi nyumbani kwenye muda wa saa moja asubuhi maana usiku mzima hakuwa amelela nyumbani, muda ambao alirudi Edna alikuwa tayari ashaondoka na alijua hilo baada ya kutokuoona gari yake.

Roma aliingia ndani ya nyumba yao na kupokelewa na Bi Wema na Qiang XI ambao walikuwa wakiendelea na majukumu ya kuweka sawa usafi wa nyunba ,Roma alisalimiana nao na kisha moja kwa moja alielekea kwenye chumba chake na kubadilisha mavazi na baada tu ya kumaliza alipandisha juu kwenye chumba cha Edna na kisha alifungua mlango wa chumba cha mke wake ,bahati nzuri mlango ulikuwa wazi hivyo haikuwa kazi kwake kuingia.

Lanlan alikuwa amelela muda huo na ilionekana wakati Edna akiondoka hakuwa amemka bado , Roma alimwangalia Lanlan alivyolala na kutabasamu , aligeuzia macho yake juu ya meza na aliangalia Bahasha iliokuwa juu ya meza , aliichukua na kutoa karatasi ambazo zipo ndani yake na baada ya kuzisoma aligundua ni za mkataba wa ndoa yake, yeye na Edna.

Alizirudisha ndani na kisha aliangalia kulia na kushoto kama mtu anaekagua chumba hiko na kisha alionekana kuridhika , alimsogelea Lanlan alielala na kupitisha mkono wake kwenye kichwa chake kwa sekunde kwa namna ya kupeti peti na kisha alisimama na kutoka kwenye chumba hicho huku akiwa ameshikilia zile kartasi , haikueleweka alikuwa akifikiria nini , lakini ndani ya dakika chache alionekana akitoka akiwa ameshikilia ile bahasha na ile anafika sebuleni aliweza kukutana na mama yake ambaye ndio alionekana anaamka.

Roma alimsalimia mama yake ambaye alionekana kuwa na usngizi bado kutokana na kuchelewa kulala jana yake akimsubiri mtoto wake arudi , Romajana alisahau kumtaarifu kwamba harudi.

“Roma subiri kwanza unywe chai?”Aliongea Blandina mara baada ya Roma kumwambia mama yake anaenda kazini.

“Mama nitakunywa mbele ya safari , nitawahi kurudi leo”Aliongea Roma huku akitoka nje kabisa na kumuacha Blandina kuangalia mlango kwa wasiwasi. Alijiuliza Edna hakuwa amekunwa chai na Roma hivyo hakuwa amekunywa chai , hakuelewa ni kipi kinaendelea , ila aliona atulize kichwa na kuacha mambo ya wanandoa hao yawe ya kwao kutafuta suluhisho pasipo yeye kuingilia.

“Bi Wema nina wasiwasi kweli na hawa Watoto”Aliongea Blandina mara baada ya kuingia jikoni akinuia kumsaidia Bi Wema.

“Blandina huna haja ya kuwa na wasiwasi , mimi nishawazoea, haya unayo yaona hapa yataisha na amani itatawala , ninachowaza hapa ni kuhakikisha tunawafanya wawe pamoja Zaidi”Aliongea Bi Wema.

“Unamaanisha nini Bi Wema?”

“Tumlazimishe Edna kulala na mume wake Roma , hio ndio namna pekee ya kuepusha migogoro Zaidi , Lanlan atarudi kulala na Qiang Xi”Aliongea Bi Wema na kumfanya Blandina kutabasamu , aliona wazo la Bi Wema ni zuri Zaidi.

“Edna atakubali , nina wasiwasi , yule mtoto licha ya kuwa mke wa Roma lakini nashindwa kuelewa anachofikiria”Aliongea na Bi Wema kutabasamu.

“Wewe ni mama kwao ,tumia nafasi yako kuwalazimisha kulala chumba kimoja , ila waache kwanza wapatane wenyewe ndio uchukue hatua ya kuongea na Edna”Aliongea Bi Wema na Blandina aliitikia kwa kichwa , aliona mawazo ya Bi Wema sio mabaya , kama Edna anakataa kulala na Roma inabidi wamlazimishe afanye hivyo kwani aliona ni ujinga wa Edna ndio maana Roma anachepuka.

Ukweli Bi Wema asingeweza kumlazimisha Edna kulala na Roma kwani hakuwa kwenye hio nafasi , kwani yeye alikuwa ni kama mfanyakazi tu ndani ya familia hiyo na alikuwa akilipwa mshahara wake licha ya kwamba Edna alikuwa akimchukulia kama mzazi , hivyo aliona mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya kazi hio alikuwa ni Blandina.

Upande wa Roma hakuwa akienda kazini kwake , bali alichukua barabara ya Kwenda Posta na ndani ya dakika kama therathini tu hivi alikuwa ashafika nje ya jengo la kampuni ya Vexto , baada ya kusimamisha gari moja kwa moja alielekea kwenye lift na kubonyeza kitufe cha floor ya mwisho kabisa , ambayo ndio ofisi ya Edna ilikuwa ikipatikana , muda wote akiwa ameshikilia karatasi ya mkataba na haikueleweka alikuwa akifiria nini au alikuwa akipanga nini kufanya na hio karatasi.

Roma baada ya kutoka kwenye lift , alimfikia Monica na hakusimama Zaidi ya kumpungia tu mkono na kupita moja kwa moja kuingia kwenye ofisi ya Edna.

Edna alikuwa bize na kazi na baada ya kuona alieingia ndani ya ofisi yake ni Roma aliendelea kujiweka bize na kazi yake, Roma hakujali sana Zaidi ya kujongea na kuzunga nyuma ya meza ya Edna na kisha alizungusha kiti na kumwangalia usoni huku akiwa siriasi.

“Mr Roma unafanya nini , nipo bize na kazi”Aliongea Edna huku akitaka kugeuza kiti , lakini Roma hakumpa nafasi alimshika mkono na kumnyanyua.

“Nifuate kuna sehemu twende , haijalishi unakazi gani ila tii maagizo”Aliongea Roma kwa sauti ya kibabe na hakumpa nafasi Edna ya kujitetea.

“Roma niachie , nimesema nina kazi na siwezi kuondoka ofisini” Aliongea Edna kwa ukali huku akitoa mikono yake kwa Roma.

“Kwahio hutaki Kwenda?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Edna.

“Nishasema nina kazi Roma siwezi kuondoka na huwezi kunilazimisha”Aliongea Edna na Roma alitabasamu kifedhuli na Edna hakujua hata ilitokea vipi kwani alijikuta tayari yupo juu akielea kwenye mikono ya Roma akiwa amepakatwa.

“Nilitaka unifuate kwa hiari yako , ila naona unaniletea za kuleta”Aliongea Roma huku akimtoa Edna ndani ya ofisi akiwa amempakata , Edna licha ya kujaribu kujitoa kwenye mwili wa Roma , lakini ilishindikana na aliishia kurusha rusha miguu.

Monica aliekuwa akiongea na Dorisi eneo la mapokezi alijikuta akiduwaa mara baada ya kumshuhudia Bosi wake akiwa amepakatwa na Roma , alitaka kutoka kwenye kiti chake Kwenda kumzuia Roma , lakini Dorisi alimzuia.

“Usiingilie”Aliongea Dorisi na kumfanya Monica kumwangalia kwa mshangao.

“Nini kinaendelea , kwanini unaniambia nisiingilie wakati Roma anamteka Bosi”Aliongea Monica na Dorisi alitabasamu.

“Unaonekana kutomfahamu vyema bosi wako , unashindwaje kufahamu mahusiano ya Roma na Edna, hata kuunganisha doti umeshindwa Monica na uzoefu wako”

“Miss Dorisi unamaanisha Roma na Edna ni…”

“Ndio ni mume na mke”Aliongea Dorisi na kuchukua faili kwenye mikono ya Monica na kisha aliondoka na kumuacha Monica alieduwaa akikaa chini kwenye kiti bila kupenda kama mzigo.

“Kumbe ndio maana… kwanini sikujua hapo kabla”Aliongea mwenyewe

“Monica unawaza nini , nahitaji kuonana na CEO”Aliongea Ernest Komwe mara baada ya kufika kwenye meza ya Monica aliekuwa kwenye mawazo.

“Monica..!!!”

“Abee…!”

“Unawaza nini bwana… usiniambie unawaza tulichofanya usiku wa jana”

“Ernest kimyaa…”Aliongea Monica Kibabe mara baada ya Ernest kuingizia jambo ambalo Monica hakupenda lifahamike.

“Nimeacha kipenzi .. niambie CEO yupo nahitaji kuonana nae”

“Ametoka”Aliongea Monica kwa sauti ya upole huku akimwangalia Ernest Komwe kwa macho ya kumsanifu ilikuwa ni kama mwanamke anavyomchunguza mpenzi wake ndio ambavyo Monica alikuwa akimwangalia Ernest Komwe.

“Niachie Roma nitakufuata mwenyewe tafadhari”Aliongea Edna kwa kubembeleza mara baada ya kuona hakuna dalili ya Roma kumuweka chini mara baada ya kuingia nae kwenye Lift , hakutaka kuumbuka Zaidi , kwani kitendo cha kubebwa na Monica kuona tukio lile ilikuwa ni aibu tosha kwake na hakutaka wafanyakazi wengine wamuone mara baada ya lift kufunguka.

Roma baada ya kuona Edna anaomba sana , ilibidi amtue chini, Edna alipumua huku bado hasira zake zikiwa juu , alijiambia yaani mtukalala kwa wanawake zake pasipo ya kujali jana yake kamdhalilisha na anakuja ofisini kwake akiwa na kazi na anamkwapua tu bila ridhaa yake , alisema hawezi kuliacha hilo lipite.

“Ukifanya ujinga wa kutaka kurudi ndani nitafanya jambo kubwa Zaidi ya nililolifanya, nafikiri unajua kwamba sinaga aibu”Aliongea Roma huku akiwa hana utani kabisa.

Licha ya Roma kushikilia bahasha , lakini Edna hakugundua bahasha ile ni ile yenye mkataba wao wa ndoa na alijiuliza ni jambo gani ambal Roma alikuwa akijaribu kufanya, ila hakuelewa na ilimbidi kutii amri kwani alijiambia akifanya jambo la kurudi basi Roma hashindwi kufanya kitu kikubwa cha aibu mbele ya watu.

Dakika chache mbele waliweza kuingia kwenye gari ya Roma.

“Tunaenda wapi?”

“Utajua mbele ya safari , usiulize maswali mengi”Aliongea Roma na kisha alitoa gari kwa spidi isiokuwa ya kawaida na kumfanya Edna kufumba macho.

Roma aliendesha gari kama hana akili nzuri vile mara baada tu ya kuliingiza kwenye barabara kuu , ndani ya dakika chache tu alikuwa Mororogo Road akisonga mbele na muda huo alikuwa akipita Magomeni mapipa, dakika nyingine mbele alikuwa akipita Kijazi Interchange na alikuja kukata kulia akichukua barabra iliokuwa ikielekea hoteli ya Grand Palace.

Edna baada ya kuona Roma anaingiza gari kwenye uzio wa hoteli hio alijikuta akishangaa na kujiuliza Roma alikuwa akifanya nini , kwani sehemu hio alikuwa akiikumbuka vyema , ndio sehemu ambayo alimuomba Roma kumuoa.

Baada ya Roma kumfungulia Edna mlango alimshika mkono na kuingia nae ndani ya hoteli hio.

“Nahitaji chumba namba 708, nishafanya booking , jina Roma Ramoni”Aliongea Roma na baada ya maneno hayo kutua kwenye masikio ya Edna , moyo wake ulipiga kite , chumba ambacho Roma alitaja ni chumba kile kile alichokutana nae kwa mara ya pili.

Mhudumu wa hoteli alitoa kadi haraka haraka , alionekana kumfahamu Edna na ndio maana alifanya kwa haraka haraka huku akiwa ni kama mwenye kutetemeka.

Dakika mbili mbele Edna akishindwa kujua Roma anachokiwaza, aliingizwa kwenye chumba hiko na kukalishwa kwenye sofa.

“Nakumbuka ulikaa kwenye hili sofa, utakaa hapa hapa kama siku ile”Aliongea Roma na yeye kukaa kwenye sofa alilokalia siku ile ile miezi sita iliopita.

Roma hakujali mshangao wa Edna alichokifanya ni kutoa karatasi ya ule mkataba na kisha alimpatia Edna.

Sasa kitendo cha Edna kugundua katatasi ile ilikuwa ni ya mkataba wao wa ndoa , moyo wake ulipiga kite kwa nguvu na hakuelewa hata machozi yalitoka wapi kwani yalianza kuloanisha mboni za macho yake.

Kwahio kumbe kanileta hapa ili tuachane”Aliwaza Edna kwenye kichwa chake huku akiwa ameshikilia ule mkataba wa ndoa na alijikuta bila kupenda akiurudisha kwenye meza , ila Roma hakujali , alionekana kujipanga , alitoa karamu kwenye mfuko wa shati na kumpatia Edna.

“Edna kwenye maisha yangu nina kanuni moja tu ,nikishafanya maamuzi hakuna kitu ambacho kinaweza kunifanya nikayabatilisha, lakini leo hii kwa ajili yako nipo tayari kuvunja kanuni yangu, ulivyonilazimisha miezi sita iliopita tuoane nilianza kukataa kwasababu kwenye Maisha yangu nilipanga mwanamke ambaye nitafunga nae ndoa ndio atakuwa huyo huyo kwenye Maisha yangu yote… kama niliamua kufunga ndoa nje ya ridhaa yangu na wewe, nipo tayari pia kuibatilisha ndoa yetu na kila mtu ajue Maisha yake”Aliongea Roma kwa hasira na kumfanya Edna kuzidi kulia, mtu aliekuwa mbele yake hakuamini ni yule Roma ambaye alikuwa akimjua siku zote , mwanaume ambaye hata kama hakuwa akimpa mwili wake kama mke , lakini bado alionekana kumjali , Edna hakuamini kama akisaini karatasi hio ndio utakuwa mwisho wake yeye na Roma, moyo wake uliuma, aliamini akishaachana na Roma basi huenda kati ya Dorisi au Nasra ndio watachukua nafasi yake na kuitwa mke wa Roma , moyo ulimuuma mno , moyo wake haukuwa tayari kabisa kusaini karatasi iliokuwa mbele yake kubatilisha mkataba wa ndoa..

“Edna unanipotezea muda, Saini karatasi hizo na mimi nitie sahihi yangu kila mmoja ajue mambo yake , si ndio unachotaka , nitakuacha uwe na amani”

“Roma tafadha….”

“Edna Saini, sitaki maelezo mengi”Aliongea Roma kibabe na Edna aliinua macho yake yaliojaa machozi na kumwangalia Roma na kuona kabisa hakukuwa na chembe ya utani kwenye macho yake, aliona hakuwa na jinsi Zaidi ya kusaini karatasi hizo licha ya kwmaba moyo wake ulikuwa mzito kufanya hivyo.

Kwa mara ya kwanza kwenye Maisha yake , alikosa kujiamini , Edna alishika karamu kwa kutetemeka sana, alivuta karatasi na kisha kabla ya kutia Saini alimwangalia Roma kwa mara nyingine ,alikuwa ni kama akitaka kumsikia Roma akimwambia nilikuwa nakutania , lakini Roma alionekana kuwa siriasi vilevile.

“Daah!!!... ndio naachika hivyo”Aliwaza Edna huku akichukua karatasi karibu na kutia Saini, ili kuachana na Mfalme Pluto A.k. a Hades.









SEHEMU YA 337.

Kabla ya Edna kutia Saini kwenye karatasi ile , Roma alimshika mkono na kumzuia kitendo ambacho kilimfanya Edna kumwangalia Roma.

“Edna mke wangu nilikuwa nakutania”Aliongea Roma huku akirudi kwenye hali yake ya kawaida iliozoeleka kwenye macho ya Edna kitendo ambacho kilimfanya Edna kupumua kwa nguvu ,alikuwa ni kama ametua mzigo mzito kwenye moyo wake na alijikuta akimwangalia Roma huku machozi yakimtoka zaidi.

Edna alijikuta akinyanyuka na kumkumbatia Roma kwa nguvu na kuanza kulia kwa kwikwi kama mtoto, hakuamini Roma alikuwa akifanya utani na yeye , dakika zilizopita alijikta akiwa kwenye mtihani ambao kwake hakuwahi kukutana nao, Edna alijiambia hata yale mawazo yake ya kutaka kuachana na Roma aliokuwa nayo wiki nzima yalikuwa yakitoka kwenye akili yake na sio kwenye moyo wake , hisia zake zilikuwa nyingi sana ambazo zilikuwa zikimtaka Roma abaki kwenye Maisha yake.

“Edna mke wangu nakupenda sana kuliko kitu chochote kwenye dunia hii , ijapokuwa ndoa yetu imeanzia kwenye makaratasi, lakini mimi na wewe ilipangwa tuwe mke na mume, hivyo mimi Roma Ramoni, pamoja na majina yangu yote siwezi kukuacha wewe malkia wa moyo wangu, wewe ndio mke wangu na hakuna mtu mwingine anaweza kukutoa kwenye nafasi yako kwenye moyo wangu”Aliongea Roma huku akimwangalia Edna usoni.

“Nakupenda pia Roma..”Aliongea Edna kwa aibu sana ,lakini sauti yake ilisikika kwenye masikio ya Roma.

“Mke wangu sijakusikia , rudia tena”Aliongea Roma huku akitabasamu, kwa mara ya kwanza Edna alisema kila ambacho anajisikia moyoni mwake.

“Unanifanya naona aibu sasa , kama hujasikia basi”Aliongea Edna na alionekana kama mtoto.

“Hahaha,,, mke wangu unaonekana kama mtoto mdogo inakufanya uzidi kuwa mrembo”Aliongea Roma huku akimkumbatia kwa mara nyingine na kumbusu kwenye paji la uso.

Naam na hivyo ndivyo ilivyokuwa , hasira zote za mrembo Edna zikawa zimeyeyuka na kwa mara ya kwanza aliweka wazi kile anachojisikia moyoni , kwa mara ya kwanza alitamka bila kulazimishwa kwamba anampenda Hades.

Roma alimrudisha mke wake kazini mara baada ya wao wote kunywa chai ndani ya hoteli hio, alijisikia raha kweli maana alikuwa amerudisha amani na mke wake na kubwa Zaidi Edna amemtamkia mwenyewe anampenda ,jambo hilo lilikuwa likitosha sana kwake na hakuhitaji kitu kikubwa Zaidi.

“Miss Airport nimerudisha mke wangu”Aliongea Roma mara baada ya kufika kwenye meza ya secretary wa Monica, ukweli Roma hakuona haja ya kumficha tena Monica juu ya uhusiano wake na boss wake na Edna pia hakuwa na haja ya kuficha tena , kwani kitendo cha kubebwa juu juu na Roma Monica alikiona.

Monica kwa mara ya kwanza alimwangalia Roma kwa heshima na ile jeuli yake ikawa imemshuka huku akijuitia baadhi ya majibu yake mabaya aliokuwa amempatia Roma kila alipokuwa akionana nae.

Monica alikuwa mfanyakazi wa muda mrefu sana ndani ya kampuni hio ya Vexto , alikuwa amefanya kazi kama secretary wa mama yake na Edna kabla ya kifo chake na baada ya Edna kuchukua majukumu ya kikampuni ndio moja kwa moja akawa secretary wa Edna na ndio aliemuongoza Edna katika kila kitu kilichokuwa kikihusiana na kampuni , hivyo kwa lugha rahisi unaweza kusema kwamba Monica ni mfanyakazi wa kuaminika wa kampuni ya Vexto.

“Boss kwanini haukuniambia mapema jamani , najiona mjinga kwa kutogundua muda wote tokea Roma afike kufanya kazi hapa kwenye kampuni”Aliongea kwa kulalama.

“Nisamehe Sana Monica , nilipaswa kukuambia lakini niliamua kufanya siri, Roma ndio mume wangu”Aliongea Edna na Monica hakuwa kwenye nafasi ya kulalamika sana , aliamua kumuelewa Edna.

Ukweli kilichomfanya monica kutogundua mahusiano ya Edna na Roma ni kutokana na namna ambavyo Roma alikuwa akijiweka kwanza alionekana kuwa mtu ambaye hayupo siriasis na Maisha , hivyo alijiambia Edna kwa tabia yake ya uchapakazi ni ngumu sana kuwa na mwanaume suruali kama Roma anaeshindia kucheza magemu kila akifika kazini, lakini kumbe ndio hivyo tena , Roma ndio alikuwa anammiliki Edna boss.

Muda wote wa kazi Monica aliwaza sababu ambayo imempelekea Edna kumpenda Roma , lakini kila alipofikiria , aliona Roma hakuwa na hata sehemu moja ambayo ilikuwa inamvutia yeye na aliishia kujiambia ni sahihi kabisa kwa wanaume kutowaelewa wanawake.

Roma hakurejea kwenye kampuni yake bali alienda idara ya PR kucheza gemu kupoteza muda kwani nafasi yake bado ilikuwa wazi kama alivyowekeana ahadi na mke wake kwamba ataendelea kuwa mfanyakazi wa Vexto licha ya kwamba anakwenda kuongoza kampuni mpya , walipanga muda wa mchana kutoka pamoja na Kwenda Kunduchi kwa ajili ya kumsapoti Sophia.

Mashindano yaliendelea , shukrani uwepo wa Amina kila kitu kilienda vyema s , Amina aliweza kusimamia vizuri shughuli ya shoo na uzuri ni kwmaba alikuwa ndio mshereheshaji wa tukio zima , jambo ambalo liliongeza Zaidi mvuto.

Sophia kabla ya nafasi yake ya kuingia kuonana na majaji haijafika , alionekana kuwa na wasiwasi kweli , alionekana kila saa alikuwa akigeuza macho yake kukagua watu wanaongia ndani ya hoteli hio ya Maple iliokuwa maeneo ya Kunduchi Beach.

Ukweli Sophia alitaka kumuona Roma kabla ya nafasi yake kufikiwa , wakati akiwa anashangaa ghafla alitoka mbio mara baada ya kumuona mwanamke alieingia eneo hilo , alievalia mavazi ya mahadhi ya kiislamu , alikuwa ni mwanamke wa kiarabu , alikuwa ni mama yake mzazi.

“Mama siamini kama umekuja”Aliongea Sophia kwa furaha.

“Kwanini nisije kukuona mwanangu , nimetua na ndege ya asubuhi ya leo”Aliongea mama yake Sophia na walijikuta wote wakicheka mara baada ya kuangaliana walionekana kuongea kwa ishara.

Wakati wakiendelea kuongea , muda huo ikiwa ni saa saba mchana hatimae Sophia alijikuta akigeuza macho mara baada ya kumuona Edna na Roma wakiingia ndani ya eneo hilo, alishangaa, ni kama vile hakuwa akitarajia wawili hao kuja pamoja, kwani kwa vita baridi ilivyokuwa baina yao , aliamini kupatana kwao kutachukua muda , lakini kwa jinsi Edna alivyoonekana ni dhahiri kabisa ule ugomvi umeisha.

“Ednaaa…!!!”Mama yake Sophia alimsogelea Edna na kumkumbatia kwa furaha.

“Mama huyu ni Bro Roma”Aliongea Sophia akimtambulisha Roma kwa mama yake.

“Ooh!, Mr Roma hatujawahi kuonana ana kwa ana kumbe ndio wewe, sikupata kabisa nafasi ya kukushuru kwa kumuokoa mwanangu kule japani , lakini pia kumpokea na kuishi nae , Asante sana baba , nimefurahi pia kuonana na wewe”Aliongea mama huyu na kumfanya Roma kutabasamu , hakudhania mama yake Sophia atakuwa mzuri namna hio na hapo kitendalwili chake ndio kiliteguka na kuamini Sophia kila kitu alichukua kwa mama yake na kwa balozi alichangia rangi kiasi na kumfanya Sophia kuwa kidogo mweusi.

Sophia alimwangalia Edna kwa furaha na kisha alimwonyeshea dole gumba , alionekana ni kama amefurahishwa na kurudisha amani na Roma.

“Sophia kwa kipaji chako ulichonacho naamini utafanya vizuri kuliko watu wote waliopo hapa, sisi wote tunakusapoti na ndio maana tupo hapa”Aliongea Roma na Sophia alitabasamu na kisha akawaaga na Kwenda kusimama kwenye eneo lake , kwani alikuwa ni mtu wa tatu kabla ya zamu yake kufika.

Roma alimchukua Edna na Kwenda nae mpaka ndani akiwa ametangulizana na mama yake Sophia na waliingia ndani ya ukumbi huo kwa ajili ya kusubiria zamu ya Sophia kuimba ianze.

Dakika kama ishirini hatimae Sophia aliweza kupata nafasi ya kuimba na kuonyesha kipaji chake na kabla hata ya kuanza kuimba alianza kuhojiwa na Amina ambaye alikuwa ndio mshereheshaji na baada ya hapo akawaruhusu majaji kumuuliza maswali kabla ya kuwanza kuimba.

Majaji jumla yao walikuwa ni watatu , Chief jaji akiwa ni msanii mkubwa tu Tanzania wa miondoko ya Hiphop ,AY , haikueleweka ni vigezo gani vilitumika AY kupewa nafasi ya kuwa Chief jaji , lakini alionekana kufanya vyema sana. Majaji wengine wawili walikuwa ni wanawake wasanii wakonwe maarufu Tanzania ambao walikuwa na tuzo za kimataifa mmoja wapo akiwa ni Lady Jaydee.

“Miss Sophia kwanza nikupongeze kwa kuwa mrembo sana , utaimba wimbo gani leo , kuonyesha kipaji chako ili kufuzu na kuingia hamsini bora?”Aliuliza AY.

“Nitafanya Cover version ya wimbo wa Alicia Keys unaokwenda kwa jina la No One”

“Wow!! Huo ni wimbo mzuri sana Sophia ninatamani kuona ni namna gani unaweza kuwa kopi halisi ya Alicia Keys, Tunaomba utushawishi kwa kutumia kipaji chako”Aliongea Jaji na kumpa nafasi Sophia kuimba.

“I just want you close,

Where you can stay forever,

You can be sure that it will only get better,

……………..

No one, no one no one,

Can get in the way of what I m feelin,

No oe , no one no one,“

Can get in the way of what I m feelin”


Sauti aliokuwa akitumia Sophia kusema ukweli ni kama wimbo wa Alicia Keys yeye ndio alieutunga , kwani ulisikika vizuri kuliko ulivyoimbwa na mtunzi mwenyewe.

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kusimama na kuanza kupiga makofi kwa shangwe , ukweli muda wote ambao Sophia alikuwa akiimba alikuwa ameangalia upande ambao Roma yupo , yaani ilikuwa ni kama alikuwa akimwimbia , hakika ilifurahisha kumsikiliza akiimba na kila mmoja alihusudu uimbaji wake.

Tukio lote hilo lilikuwa likionyeshwa mubashara kwa kupitia runinga , hivyo ni rahisi kusema kwa uwezo aliouonesha alikuwa amejibebea mashabiki sio ndani tu ya ukumbi lakini pia Tanzania kote kwa wale waliokuwa wakifuatilia matanganzo hayo moja kwa moja.

“Miss Sophia mimi sina cha kusema , umeonyesha kipaji kikibwa sana kukilo wenzako wote waliokutangulia , naomba nikuone tena raundi inayofuata kwenye hamsini bora , Welldone”

“Asante Chief Judge”Aliongea Sophia na zamu iliofuatiwa akapotea jaji mwingine ambaye tokea mwanzo alionekana kukandia watu kweli na kuwakatisha tamaa , alikuwa kopi halisi ya Salama Jabiri wa Bongo Star Search”

“See you Sophia on next round”Aliongea yule jaji na kumfanya Sophia kuinama kwa heshima sana kushukuru na Sophia akawa amepata asilimia zote na kupita raundi inayofuata ya hamsini bora , raundi ambayo inambidi kukaa kambi na wasanii wenzake mpaka pale mashindano yatakapoisha , au atakapoaga kama atafanya vibaya .

Edna alifurahi kumuona mdogo wake alifanya vizuri na alijiambia atamsapoti mpaka kuwa msanii mkubwa sana Afrika na duniani kwa ujumla , alijiambia Sophia ni dhahabu licha ya kwamba hakuwa akitaka pesa kutoka kwake ila alijiambia kama Sophia atapata umaarufu kupitia kampuni yake basi mauzo yataongezeka kwani itakuwa rahisi kufanya matangazo na kufikia watu wengi..

“Hongera Director kwa kuandaa vyema mashindano, ni nje ya matarajio yangu”Aliongea Edna akimsifia Roma.

“Hehe.. babe inabidi unipe zawadi hata ya kiss sasa mume wako”

“Zawadi kwani lazima iwe kiss , huwezi kuomba kingine mpaka uombe mambo ya kutia aibu”Aliongea Edna kwa aibu na Roma alijikuta akicheka.

Wakati wakiendelea kuongea Roma alisimaa na kumuacha Edna na alionekana alikuwa akienda kuongea na Daudi.

“Miss Edna… !”Sauti nyororo kutokea nyuma ilisikika kwenye ngoma za masikio ya Edna na alipogeuka , aligundua ni Amina.





SEHEMU YA 338

Amina alimuomba Edna msamaha kwa kile kilichotokea wiki iliopita na kueleza kwamba haikuwa nia yake ya kumgombanisha yeye na Roma , Edna alimsikiliza Amina kwa kila alichoongea na akahitimisha kwamba anaomba kuendelea kuwa Sekretary wa Roma kwani hana nia mbaya na kampuni na kumuahidi kwamba atawezekeza nguvu zake zote kuhakikisha kampuni ya Vexto inapata umaarufu ndani ya muda mfupi kwa kupitia uzoefu wake alioupata kwa kufanya kazi na vituo vikubwa vya Habari.

“Amina umeongea kila kitu lakini sijasikia ukiongea juu ya mahusiano yako na mume wangu”Aliongea Edna akimwangalia Amina.

“Edna kuhusu hilo…”Amina alijikuta akishindwa kujua ni namna gani ya kujibu kwani alishindwa kutamka moja kwa moja kwamba hana mpango wa kumuacha Roma,

“Edna naomba usinichukie tafadhali , please , please…. Nitakutii kwa kila utakachoniambia ila naomba japo siku moja moja niwe na mume wako , nakuomba tafadhari”Aliongea Amina huku akipasha viganja na kumfanya Edna kutamani kucheka , kwa namna moja Amina alionekana kama mtoto na hiko ndio kilichomfanya Edna kutamani kucheka, lakini pia kilichomfurahisha ni namna ambavyo Amina anajitahidi kuwa mkweli kwake.

Roma alikua ashamaliza kuongea na Daudi kwani mashindano yalikuwa yamesitishwa kwa masaa kadhaa ili watu Kwenda kupata chakula cha mchana , hivyo alivyogeuka aliweza kumuona mke wake akiongea na Amina na ilibidi kwanza asimame mbali , alijua ni jambo jema sana kama Edna atapatana na Amina , aliona utakuwa mwanzo mzuri sana wa wengine pia kupatana na Edna na Maisha kuendelea bila migogoro.

“Amina sipo kwenye nafasi ya kukuzuia wala kukuruhusu kuendelea na Roma kwani yeye ndio mwamuzi mkuu , ila ninachokushauri tu ni kwamba usije ukashikwa na tamaa , mimi ndio mke wa Roma na itabakia hivyo”Aliongea Edna akiwa siriasi , huku hata yeye mwenyewe akijishangaa kwanini amekuwa mrahisi kutamka maneno hayo.

“Edna siwezi kushikwa na tamaa nitashukuru kwa kile kidogo nitakachokipata kutoka kwa Roma na sitotamani kuwa mke wa Roma, nitakuheshimu kama mke .. na juu ya yote Edna nimetokea kukupenda pia ghafla, kuongoza biashara ya mabilioni ya pesa sio jambo rahisi kwa mwanamke kufanya , lakini wewe umeshinda vyote , Edna wewe ni Role model wangu, halafu umrembo sijawahi ona”Aliongea Amina na mwanamke huyo alikuwa ‘manipulative’ sio mchezo , alijua kucheza na akili za binadamu wenzake na kujua ni kipi aongee na kwa wakati gani na maneno ya Edna licha ya kwamba hakuonyesha waziwazi kuguswa , lakini alijisikia kitu sio cha kawaida , kwanza alijiambia Roma alikuwa akimpenda yeye kuliko wanawake zake wote , hivyo yeye ni kama ndio alieshikilia mpini , hivyo hakuwa na sababu ya kuogopa michepuko ya Roma.

Sophia ndio aliekuwa wa kwanza kufika nyumbani , kwani asubuhi aliletwa na Dereva wa Edna , bwana Innocent , hivyo hata muda wa kurudi nyumbani jioni alikuwa wa kwanza, Yezi na wanafamilia wengine siku hio walikuwepo nyumbani wakiwa wameketi kwenye runinga wakiendelea kuangalia tamthilia na hata kwa Blandina alikuwa ameketi kwenye masofa akiwa ameungana na wanafamilia.

Blandina alionekana kuwa na furaha na amani sana , na hio ni mara baada ya kupokea simu kutoka kwa moja ya mkuu wa kituo cha kulelea Yatima kilichokuwa Sudani.

Unajua katika vituo vyote ambavyo Blandina alifungua , kituo cha Sudani ndio kilikuwa kikubwa kuliko vituo vingine vyote , kilikuwa na uwezo wa kubeba Watoto elfu moja kwa wakati mmoja na wote kwa pamoja kupata huduma bora kabisa, ndio kituo ambacho alipata changamoto kubwa kwenye ujenzi wake , kwani ilimbidi kutembeza bakuli la michango pamoja kuomba ufadhili kwa matajiri wengi mpaka kikajengwa na kukamilika, wakuu wote wa vituo hivyo walikuwa ni wanawake na ni marafiki zake , haikueleweka aliwezaje kuwa na marafiki wengi kiasi hiko , lakini wanawake hao wote walikuwa wakimfahamu kwa sura yake halisi na hata kwenye hivyo vituo kuna picha yake.

Sasa siku hio mchana aliweza kupata taarifa kutoka kwa rafiki yake ambaye anaongoza kituo huko Sudani baada ya kituo hiko kupata ufadhili kutoka taasisi ya Bill and Mellinda Gate Foundation kutoka Marekani katika upande wa Elimu na Chakula , taarifa hio ilikuwa njema sana kwake kiasi kwamba alijiuliza jambo hilo limewezekanaje, kwani ni kwa miaka mingi sana kituo hiko kilikosa ufadhili wa kueleweka na mara nyingi kilitegemea watu wanaotembelea na kubeba zawadi , lakini pia pamoja na hela zake alizowekeza faida ilikuwa ikienda moja kwa moja katika kituo hicho.

Sasa moja kwa moja aliamini huenda Roma ndio alivyomsaidia na ndio maana akapata ufadhili huo.

“Wamepatana”AliongeaSophia mara baada tu ya kufika sebuleni akiwa na furaha.

“Sophia unamaanisha nini?”Aliuliza Yezi.

“Bro na Sister wamepatana”Aliongea Sophia na sasa kufanya kila mmoja kuelewa alichokuwa akimaanisha ni nini.

Blandina alimwangalia Bi Wema na kisha akatabasamu na aliona maneno yake ya asubuhi bibi huyo yalikuwa ya kweli , Bi Wema alimwambia asubihi Blandina kwamba awaache watapatana na imegeuka maneno yake kuwa ya kweli, Blandina alijiambia kilichobakia hapo ni kuhakikisha Edna na Roma wanalala pamoja na ili hilo lifanikiwe anatakiwa kuongea na Edna.

Upande wa Roma baada ya kumrudhisha mke wake Kazini yeye alirejea kwenye jengo la kampuni kwa ajili ya kuendelea kucheza gemu huku akivuta muda ili saa kumi arejee nyumbani.

Lakini wakati akiwa kwenye majukumu yake ndio alipopokea simu kutoka kwa Diego.

“Mfalme Pluto tumekamilisha uchunguzi wetu na ripoti ipo tayari”Aliongea Diego mara baada tu ya Roma kupokea simu na Roma alitabasamu.

“Diego mmefanya kazi kubwa nitapitia jioni ya leo kuona hio ripoti”Aliongea Roma

Ilivyofika saa kumi Roma aliingia kwenye gari yake na safari ya kuelekea Kigamboni ilianza mara moja , alikuwa na hamu ya kujua ni nini kilimtokea mama yake Edna mpaka akawa kwenye mpango wa majaribio , ulioratibiwa na kampuni ya Maya.

*********

Upande mwingine siku hio hio Raisi Senga alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kuanza safari yake ya Kwenda Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya mpasuko wa mwezi.

Sasa unachotakiwa kwanza kabisa kuelewa kuhusu ibada hii ya mpasuko wa mwezi maana yake ni kwamba ni ibada ambayo inafanyika katikati ya mwezi na ndio maana ikapewa jina la Mpasuko wa Mwezi(Rite of Moon Rift).

Hii ni sehemu ya ibada inayofanyika kila mwezi , ibada hii inakuwa na maana kubwa sana katika jamii ya siri ya Freemason, ilikuwa na maana Zaidi ya neno lenyewe la kupasuka kwa mwezi.

Moja ya matukio ambayo yanafanyika kwenye ibada hii ni kupokea wanachama wapya ambao wanataka kujiunga, ambayo wapo kwenye ngazi ya kwanza(First Degree) ambayo maana yake ni ‘Kukubaliwa’.

Sio kila mtu anaweza kujiunga na jamii hizi kutokana na kwamba kuna vigezo ambacyo vimewekwa mpaka mtu kukubaliwa na kuwa mwanachama kwa ngazi ya kwanza , kwanza kabisa kuna maombi ya kukubaliwa ambayo mtu anafanya ili aingie , maombi ambayo yanaambatana na ulipaji wa kiasi cha pesa kisichopungua milioni kumi na baada ya hapo kutaanza taratibu za aliefanya maombi kufuatiliwa ili kuangaliwa kama anakidhi vigezo, sasa moja ya kigezo kikubwa ambacho kinaangaliwa kwa mwombaji ni mchango wake kwenye jamii , lakini pia ushawishi wake kwa ujumla, kama huna ushawishi watasoma nyota yako kuangalia ni ‘Pontential’ gani ambayo mtu anayo kwenye miaka ya mbele(Nitaelezea kwa ufupi mbele)

Maswala hayo yote yanaongozwa na Lodge Grand Master kwa kutumia washirika ambao wapo kila nchi ndani ya Afrika.

Sasa sababu moja kubwa ambayo Illuminat wanakinzana na Freemason ni kwamba , Freemason yenyewe haimbagui mtu , wanachokiangalia ni uwezo wa mtu kukidhi tu vigezo , kwa mfano kama wewe ni mganga wa kutumia nguvu za giza wa kuaminika na ukakidhi vigezo unaingia huko , yaani hakuna kubaguliwa, upande wa Illuminat wenyewe hawa wanaabudu sayansi na wanaamini sayansi ndio kila kitu na ndio Mungu wa kweli na wanaamini ili mtu kukidhi vigezo na kuitwa Illuminat lazima awe na mchango chanya kwenye sayansi.

Anachotaka kukifanya Athena mpaka kumwagiza The Fisrt Black ili kufatilia wanachama wote wa Illuminat ni kwamba ,anataka kufufua upya nguvu ya kundi hili la Illuminat na kuwa wasaidizi wake wakati atakapoweza kuamsha roho za ndugu zake zilizomezwa na binadamu kwa kutumia Jiwe la Kimungu , yaani Godstone.

Sasa wiki iliopita , ikiwa ni baada ya siku nne baada ya kukutana na Blandina kule kwenye kituo cha kulelea Yatima , Raisi Senga aliweza kutembelewa na balozi wake tena kwa mara ya pili na kupewa taarifa ambayo kusema ukweli ilimfanya kuwa na amani sana.

Taarifa yenyewe ilikuwa ni inayomuhusu Blandina, taarifa hio ilikuwa ikimueleza kwamba juu ya kafara ya kiimani ambayo alipaswa kutoa imebatilishwa.

“Mheshimiwa licha ya kwamba kafara hio imebatilishwa haimaanishi kwamba hakuna namna nyingine ya kuipima Imani yako, Msingi wa Freemason sio kumwanga damu bali ni kuhakikisha wanachama wote wanakuwa na Imani thabiti , hivyo unapaswa kujiandaa kwa maelekezo mengine , kama huwezi kutoa kafara basi wewe mwenywe unatakiwa kujitoa kafara”Aliongea Balozi na kumtisha sana Raisi Senga.

“Samahani ndugu balozi unasema kwamba mimi ndio natakiwa kufa kwa niaba ya Blandina?”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Balozi alievalia suti nyeusi kutabasamu.

“Mheshimiwa kujitoa kafara haimaanishi kifo mara zote”Aliongea na kumfanya Raisi Senga kuvuta pumzi ya ahueni

“Kwahio nini kinakwenda kunitokea , ni kafara gani ambayo ninatakiwa kutoa kama sio uhai wangu , kama mambo yakiendelea kuwa magumu hivi nitaomba kubatilisha ombi langu”

“Mheshimiwa huna haja ya kuwa na wasiwasi , kinacho kuogepesha ni kwasababu Imani hii inakwenda kuwa mpya kwako , kuhusu pia kujitoa haiwezekani kwani ushaingia hatua ya kwanza ya KUKUBALIWA na pia kuna adhabu kama utataka kujitoa na inaweza kuwa kubwa Zaidi kuliko kujitoa wewe mwenyewe kafara”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa kuanza kujutia kwanini amejiingiza kwenye hayo mambo , kwani kila neno analotamka ndugu Balozi licha ya kwamba alikuwa akiongea kwa upole lakini maneno yake yaliambatana na ujazo wa hofu ndani yake.

“Mheshimiwa kuna aina mbili za kutoa kafara katika Imani za jamii yetu , ya kwanza ni kuthibitisha Imani yako kwa kutoa kitu unachopenda Zaidi kwenye Maisha yako na aina ya pili ya kafara ni kujitoa wewe mwenywe kwa kufanya kitu ambacho unakichukia sana kwenye Maisha yako , ambacho kinaenda kinyume na kanuni za Maisha yako, hivyo mheshimiwa kabla ya Ibada hakikisha unatambua ni jambo gani kwenye Maisha yako unalichukia sana na kamwe huwezi kulifanya”

Dunia imeumbwa katika msingi wa Uwili unaotofautiana(Kinyume nyume na kimbelembele) lakini unaovutana pamoja ,wazungu wanasema Black and White , wachina wanasema Ying And Yang ,maneno haya yanasimama kwa mfano wa kwamba, kama mtu kuna kitu anachokipenda kwenye Maisha yake sana na anaogopa kukipoteza(White) basi atakuwa na kitu anachokichukia sana kwenye Maisha yake na hata umfanye nini hawezi kukifanya(Black), kuna mifano mingi Zaidi kama vile uwepo jinsia ya kike na ya kiume.

Sasa katika jamii hizi kutoa kafara ni upande wa White yaani mtu anatoa kitu ambacho anakipenda sana na kama hawezi kutoa kitu hiko basi atachagua upande mwingine yaani Black(Kujitoa kafara) , huu ni upande ambao mtu anauchukia kufanya kwenye Maisha yake yote ,ijapokuwa kuna Zaidi ya maana kwa upande wa Black kwa mfano kama hupendi kufanya kitu unachokichukia unaweza pia kutota kafara kwa kupitia uhai wako.

Sasa mheshimiwa Senga alikuwa na mtihani wa kufahamu ni kitu gani anakichukia kwenye Maisha yake na hicho ndio atakifanya kwa namna ya kujitoa kafara yeye mwenyewe baada ya kushindwa kutoa kafara ili mradi atimize kigezo cha uthabiti wa Imani na baada ya mambo hayo yote kukamilika sasa ndio faida zitakapoonekana(Privelege’s of Brotherhood) ,lakini wakati huo akivuka sasa hatua ya kwanza ya kukubaliwa na kuingia hatua ya pili ya ‘Second Degree’.

Sasa inasemekana kwamba wanachama wengi huchagua upande mweusi(Black) upande wa kujitoa kafara na kinachofanya watu kuchagua huu upande ni kwasababu moja tu ya kwamba wanaume wote wanafanana sana kwenye kitu ambacho tunakichukia kwenye Maisha yetu kukifanya.

Wakati hayo yakiendelea upande wa huku Tanzania , upande wa Kenya ni hivyo hivyo Kamau Kamau baada ya kushindwa kumrudisha Blandina Kenya na kigezo cha kafara yake kubatilishwa alitakiwa kuchagua upande wa kujitoa kafara yeye mwenyewe kama ilivyo kwa raisi Senga.

Raisi Kamau kamau alikaa chini kwa masaa mengi sana akifikiria ni jambo gani ambalo analichukia kwenye Maisha yake , jambo ambalo hayupo tayari kulifanya na katika mahesabu yake yote kuna jambo moja kila alipokuwa akilifikiria , mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno.

“Naomba isiwe kweli , ninachokifiria”Aliwaza Raisi Kamau usiku mmoja kabla ya siku ya kesho kufika ili kuanza safari yake kuelekea Nchini Nigeria kuhudhuria Ibada ya mpasuko wa Mwezi.

******

Ni muda wa saa kumi na moja Edna alionekana akiingiza gari lake kwenye uzio wa jumba lake la kifahali analo ishi na familia yake.

Mrembo huyu mara baada ya kuegesha gari lake na kutoa mkoba wake , alifuatwa na Derick mlinzi wa geti na akamsalimia kwa heshima.

“Madam kuna huu mzigo wako umeachwa muda si mrefu”Aliongea Derick huku akinyoosha mkono kumpatia Edna bahasha ya khaki iliokuwa kwenye mikono yake.

“Ni nani ambaye kakupatia?”

“Hajajitambulisha kwa majina lakini alisema ni mzigo wako , nilijaribu kukataa kuchukua lakini alinilazimisha na kuniambia lazima nimfikishie muhusika, nisamehe Madam kama nimefanya kosa”

“Okey hakuna shida unaweza kuendelea na majukumu yako”Aliongea Edna huku akiingia ndani akiwa ameshikilia Bahasha yake, lakini kabla hajafika ndani Lanlan alitoka spidi spidi na kumrukia Edna kwa furaha akimlaki na Edna alimbeba juu juu na Kwenda nae ndani.

Yalipita masaa kadhaa , baada ya Eda kutulia , sasa alikuwa ndani ya ofisi yake ya kujisomea na mkononi akiwa anafungua bahasha aliopatwa na Derick , bahasha ambayo inatoka kwa mtu asiemfahamu.

Edna alitoa karatasi zilizokuwa ndani ya bahasha na kuanza kuzisoma na ndani ya sekunde ishirini tu , Edna macho yalimtoka na kudondosha chini zile karatasi huku akiwa ni mwenye kutetemeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…