Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 339

Edna alionekana kama hakuwa akiamini kile ambacho alikuwa amekisoma alibeba tena ile bahasha na kuangalia ndani kama kuna kitu kingine zaidi ya ile karatasi na ni kweli ndani yake kulikuwa na picha mbili.

Edna alizitoa na kuanza kuangalia moja moja na alijikuta akishika moyo wake , watu wawili waliokuwa kwenye picha ya pamoja alikuwa akiwajua, mmoja akiwa ni mama yake Raheli na mwingine akiwa ni Raisi Jeremy wa Rwanda, na katika pozi ambalo walikuwa wakionekana ni dhahiri kabisa walikuwa ni wapenzi.

Edna akili yake ilipata moto na sasa ni kama anakumbuka kwa mara nyingine kitabu cha mashairi ambacho mama yake alikuwa akikisoma mara kwa mara siku zote , kitabu ambacho ndani yake kulikuwa na picha ya mwanaume ambaye hakuitambua mara moja mara baada ya kuiona , lakini sasa kwa kupitia picha zilizokuwa kwenye mikono yake anatambua kuwa ile picha pia ilikuwa ni ya Raisi Jeremy na ni yeye ambaye alishindwa tu kuitambua.

Karatasi ambayo Edna alikuwa akiisoma , ilikuwa ikionyesha majibu ya DNA kati yake yeye na Jeremy Paul ambaye ni raisi wa Rwanda na majibu hayo ndio yaliomfanya Edna kutetemeka kwani ni swala ambalo hakuwaji kulitegemea kabisa.

“Kwahio baba yangu mzazi ni Raisi Jeremy wa Rwanda?”Alijiuliza Edna huku machozi yakianza kumtoka taratibu taratibu, picha mbalimbali zilikuwa zikipita kwenye akili yake na alishindwa hata kujielewa kwa wakati huo , Edna alikumbuka namna Maisha yake na baba yake Adebayo yalivyokuwa magumu na alijikuta moyo ukiuma.

Kila kitu sasa kilikuwa kipo wazi , Edna anatambua baba yake ni Raisi Jeremy wa Rwanda , lakini jambo moja ambalo anashindwa kufahamu ukweli wake ni juu ya kuzaliwa na pacha wake aliopewa jina la Lorraine.

Edna alikaa ndani ya chumba chake kwa takribani lisaa ndipo akili yake iliporudi na kufanya kazi na hapo hapo alimkumbuka Bi Wema , aliamini Bi Wema lazima atakuwa anaufahamu ukweli juu ya baba yake mzazi kwakuwa alimlea tokea akiwa amezaliwa.

Edna alitoka haraka haraka na kushuka chini kumtafuta Bi Wema ili kumuuliza maswali juu ya Jeremy Paul wa Rwanda kuwa mzazi wake huku mkononi akiwa ameshikilia picha zile mbili ambazo zilikuja ndani ya ile bahasha.

Bi Wema ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Edna akiwa kwenye hali ambayo sio ya kawaida.

“Edna kuna shida gani , mbona unatokwa na machozi?”Aliuliza Bi Wema huku akimsogelea Edna ,kwa upande wa Blandina aliekuwa bize na kuandaa chakula moyo wake ulidunda aliamini tayari mwanae Rpma kashayakoroga tena.

Edna alimpatia Bi Wema zile picha na baada ya bibi huyo kuzipokea na kuangalia alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa wakati mmoja na mpaka hapo Edna alimuona Bi Wema alikuwa akijua swala hilo.

“Bi Wema huyu ndio baba yangu?”Aliuliza Edna kwa huzuni na swali lile lilimfanya na Blandina kumsogelea Bi Wema na kuchukua picha iliokuwa kwenye mikono yake.

Blandina mara baada ya kuona picha moja kati ya mbili , alijikuta na yeye akivuta pumzi , picha aliokuwa ameishikilia ilikuwa imepigwa eneo la ufukweni.

Edna baada ya kuona hata Mama Mkwe wake hashituki licha ya kuona picha hio , alijikuta akishangaa na kujiuliza maswali, hata Bi Wema alijikuta akiwa ni mwenye kushangaa kuona Blandina hakuwa ni mwenye kushangaa juu ya swala hilo.

“Mama hata wewe unafahamu hili?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi.

“Edna hio picha nilipiga mimi , hapo ni Sydney Australia Bondi Beach ni miaka mingi iliopita”Aliongea na kumfanya hata Bi wema kushangaa ni kama hakuwa amesikia vizuri.

*********

Ni muda wa saa kumi na nusu mchana , Roma alishaweza kufika ndani ya nyumba ambayo wanaishi wanajeshi wake wa The Eagles na muda huo Diego na Adeline walikuwa wameketi kwenye masofa wakiwa wanamuelezea Roma kuhusu ripoti juu ya uchunguzi walioufanya kuhusiana na kifo cha Raheli.

Kwa maelezo ya Diego ni kwamba waliweza kufanya uchunguzi kwa kudukua Barua pepe binafsi ya Raheli na katika kufatilia kwa ukaribu mawasiliano ya Email yake alionekana wiki kadhaa kabla ya kifo chake aliweza kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dr Robert kutoka Marekani na mazungumzo yao yalionyesha yalikuwa ni ya mgonjwa na Daktari, yaani Robert akiwa ni daktari huku Raheli akiwa ni mgonjwa, Roma alishangazwa na maneno ya Diego.

“Diego kwahio kwa maneno yako unamaanisha kwamba Raheli alikuwa na daktari binafsi?”Aliuliza Roma.

“Ndio Mfalme Pluto ,ijapokuwa Raheli alikuwa akipatiwa matibabu na Dokta Hubery, dokta wa familia , lakini wakati huo huo alikuwa na dokta binafsi ambaye ni huyu Dokta Robert ,tumeweza kufatilia ‘Profile’ ya Dokta Robert na tumegundua ni daktari ndani ya hospitali ya kimafunzo ya Mayo Clinic Marekani”Aliongea Diego na Roma alitingisha kichwa kumpa ishara ya kuendelea.

“Tulifanya mawasiliano na wenzetu waliopo Marekani kwa ajili ya kutusaidia kumhoji Dokta Robert na jambo lilikuwa Rahisi kwani dokta Robert alitupa ushirikiano wa kutosha na aliweza kutupatia faili linalohusu matibabu ya Raheli na tumeweza kugundua Raheli alikuwa amewekewa sumu kwenye mwili wake”

“Sumu!!”Roma alishangaa.

“Ndio Mfalme pluto”

“Sumu ya aina gani na kwanini awekewe sumu?”Aliuliza Roma na kumfanya Deigo kumpa ishara Adeline aliekuwa pembeni yake.

“Kabla ya kufanya uchunguzi tulikuwa tukitumia ‘reference’ kutoka kwa taarifa aliotupatia Miss Christine inayohusiana na ‘Resurrection Fluid’(Kimiminika) na tuliweza kupata taarifa ya utafiti iliofanyika juu ya hiko kimiminika”Alinyamaza kisha akaendelea.

“Mfalme Pluto kupitia taarifa iliotoka taasisi ya Innova inaonyesha kwamba ‘Ressurection Fluid’ ikitumiwa kwa mtu ambaye yupo hai inageuka na kuwa sumu mwilini, hivyo kumpelekea mhusika kuanza kupata matatizo ya ogani za mwili kufeli taratibu taratibu , ukijaribu kufanananisha na ripoti ya Dokta Robert inaonyesha Bi Raheli mwili wake ulikuwa na sumu ambayo haikuwa ikifahamika bado na ilikosa ‘Antidote’ na hiko ndio kilipelekea kifo chake”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuvuta pumzi mpaka hapo alikuwa na uhakika kwamba sasa maneno ya Christine kwa Raheli kuhusishwa na majaribioa ya kisayansi ni ya kweli.

Antidote ni dawa inayotumika kuyeyusha sumu mwilini , sasa baada ya Resurrection Fluid kuwekwa kwenye mwili wa binadamu anaeishi inashindwa kufanya kazi na kugeuka kuwa sumu ambayo haina hio ‘Antidote’ hivyo kupelekea mtu kufa kwa matatizo mbalimbali , aidha moyo kufeli kufanya kazi au figo.

“Kwahio sasa kwanini Raheli akawa sehemu ya majaribio hayo?”

“Mfalme Pluto katika kufuatilia jumbe za ‘Email’ binafsi ya Raheli tumegundua pia Raheli alikuwa na adui ambaye alikuwa akimtumia jumbe za vitisho , ijapokuwa Email hio ililikuwa ikituma jumbe pasipo ya mtumaji kufahamika , lakini tuligundua ni maswala ya kimapenzi ndio yaliokuwa yakiendelea na Miss Raheli alikuwa akishutumiwa kwa kutoka kimapenzi na mume wa mtu inaonyesha mtu ambaye alikuwa akimtumia jumbe za vitisho alikuwa ni rafiki yake wa karibu na hii ilitufanya kufatilia Maisha ya nyuma ya Raheli na tuliweza kupata hizi picha kutoka chuo cha Durban South Afrika”Aliongea Diego na kumpatia picha Roma , katika picha hizo moja tu ndio Roma aliweza kuitambua na picha hio ilikuwa ni ya Raheli ,Roma ashawahikuona picha ya Raheli mara nyingi ndio maana ilikuwa rahisi kwake kuifahamu.

Kwa maelezo ya Diego picha hio ilikuwa ni ya wadada watatu ambao walipiga pamoja siku yao ya kuhitimu , wanadada hao walikuwa ni Raheli , Nahita na Kizwe mke wa Raisi Jeremy kutoka Rwanda.

“Mfalme Pluto angalia na hii picha”Aliongea Diego na kumpatia Roma picha ya mwanaume na mwanamke wakiwa kwenye pozi la kimahaba ,ilikuwa ni picha ya First Lady wa Rwanda na Raisi Kigombola na haikuhitajika elimu kubwa kugundua kilichokuwa kikiendelea ,wawili hao walionekana kuwa wapenzi.

“Mmeipataje hii?”

“Kuna mtu ametupatia Mfalme Pluto?”Aliongea Diego na kumfanya Roma kushangaa.

“Nani kawapatia?”

“Mfalme picha hizi tumeweza kuletewa na mtoto mmoja ambaye aliagizwa wiki iliopita siku ya ijumaa, hazikuja picha tu bali ilikuja bahasha yenye karatasi zingine na ndio ambazo ziliturahishia kuweza kujua kile ambacho kilikuwa kikiendelea, inaonekana mtu ambaye ametukabidhi hakutaka kufahamika , lakini kwa namna moja ama nyingine ni kama alikuwa akifahamu tunafanya uchunguzi unaohusiana na kifo cha Miss Raheli”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuomba ambiwe hizo karatasi zingine zinahusiana na nini.

Kwa maelezo ya Diego ni kwamba karatasi hizo zilikuwa zikielezea Siri inayohusiana na Maabara ya siri iliokuwa chini ya jengo la Bima ya Taifa, katika Ripoti hio ilionyesha kwamba majaribio ya ‘Resurection Fluid’ yalifanyikia ndani ya maabara hio kwa usimamizi wa kampuni ya Innova pamoja na Maya.

Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba majaribio yaliokuwa yakihusiana na Kimiminika yalifanyikia hapa Tanzania , hivyo taarifa ambayo waliweza kuletewa na mtu asiejulikana ilikuwa ni ya siri sana , mtu alieidhinisha utafiti huo ni Raisi Kigombola kwani sahihi yake ilionekana kwenye hio karatasi.

“Diego kwahio ripoti yenu mmeikamilishaje, nini kilipelekea na Raheli kuhusika kwenye majaribio haya?”

“Mfalme Pluto baada ya kuletewa hio Nyaraka tuliona hakuna sababu ya kufanya uchunguzi zaidi kwani majibu yote yapo kwa mtu alietufikishia hizi karatasi, hivyo akili yetu tuliiwekeza kumfahamu, na bahati nzuri tuliweza kupata kupita ‘Fingerprint’(Alama za vidol) kwenye hii karatasi , ijapokuwa ilikuwa ngumu kutokana na karatasi hizi kushikwa na watu tofauti tofauti lakini ‘Fingerprint’ ya mara ya mwisho kushika hii nyaraka tuliweza kuitafuta kwenye mfumo wa ‘DataBase’ ya taifa na imeweza kutuletea jina la Suzzane Masanyika.

“Suzzane!!”

“Ndio Mfalme Pluto , Suzzane ni msaidizi wa karibu na alikuwa mwanasheria binafsi wa Marehemu Raheli na mpaka sasa anafanya kazi kama msaidizi binafsi wa Madam Persephone”Aliongea Diego na kumfanya Roma kukuna kichwa huku akionekana kuelewa.

“Mshawasiliana na huyu Suzzane?”

“Mfalme bado hatujawasiliana nae ila tunaamini anajua kila kitu , tulitaka kwanza mchango wako katika hili kabla ya kuendelea zaidi”

“Okey! Diego kama mnaamini majibu yote atakuwa nayo Suzzane basi mimi mwenyewe nitaongea nae, naamini alikuwa ananilenga mimi baada ya kuleta nyaraka hizi”Aliongea Roma na Diego alikubali..

Kwahio ripoti waliokuwa nayo wanajeshi hao haikuwa imekamilika bali iliishia kwa upande wa Roma Kwenda kuongea na Suzzane , Diego na Wenzake waliona sio vyema kwenda moja kwa moja kumhoji mfanyakazi wa karibu wa Edna pasipo kumhusisha Mfalme Pluto mwenyewe.

Roma akiwa kwenye gari akielekea nyumbani alikuwa na mawazo ya hapa na pale lakini mawazo ambayo yaliteka zaidi akili yake ni swala la Suzzane kuwa na nyaraka ya siri kama hio na kuamua kuileta kwake , kwa haraka haraka aliona huenda Suzzane alikuwa akijua mambo mengi zaidi ya yale ambayo yapo kwenye zile karatasi lakini hakuwa na namna ya kuzifanyia kazi.

Dakika kama hamsini hatimae Roma aliweza kuingiza gari yake ndani ya nyumba yao na muda ambao alikuwa akiingia ilikuwa ni saa moja moja hivi Kwenda na nusu.

Muda ambao Roma alifika ndio wakati ambao Edna alikuwa akitoka na Blandina mpaka eneo la Sebuleni kwa ajili ya kuongea kile alichokuwa akikifahamu kuhusu Raheli , mpaka akawa mpiga picha wa Raheli pamoja na Raisi Jeremy.

“Kuna nini kinaendelea, Edna mke wangu mbona macho yako mekundu?”Roma baada ya kuuliza vile Bi Wema alimpatia zile picha na Roma mara baada ya kuziangalia alifahamu sasa ni kipi kilikuwa kikiendelea.

SEHEMU YA 340.

Kwa maelezoo ya Blandina ni kwamba miaka Zaidi ya ishirini nyuma kabla ya kuzaliwa kwa Denisi ambaye ni Roma ndio kipindi ambacho Blandina aliweza kukutana na Raisi Jeremy pamoja na Raheli.

Blandina kipindi ambacho alikutana na Jeremy ni wakati alipomaliza masomo kwa ngazi ya Degree(Shahada) kwenye chuo cha Sydney, akichukua kozi ya Economics(Uchumi) na wakati huo huo kwa upande wa Raisi Senga akiwa mwaka wa mwisho wa masomo yake ya Shahada ya kwanza upande wa ‘Political’ (Siasa).

********

Raisi Kamau Kamau alisoma kwanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne katika shule ya kimataifa ya Braeburn ,katika kipindi chote hicho cha masomo rafiki yake mkubwa alikuwa ni Blandina mwanafunzi mrembo kutoka Tanzania , ukaribu wao ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba wanafunzi wengi waliamini walikuwa na mahusiano ya kimapenzi , lakini hilo halikuwa kweli kwani walikuwa ni marafikii tu wa karibu pasipo ya kuwa wapenzi kabisa mpaka wanamaliza kidato cha nne ndipo kwa mara ya kwanza Kamau Kamau akalala na Blandina siku ya mahafali yao.

Haikuwa ridhaa ya Blandina kulala na Kamau kutokana na kwamba kitendo hicho kilitokea baada ya Blandina kuwekewa dawa za usingizi na Kamau Kamau.

Kamau Kamau alikuwa akimpenda sana Blandina kimapenzi na sio kiurafiki , lakini kila alipokuwa akiweka hisia zake wazi kwa Blandina , mrembo huyo alikuwa akimchomolea huku akimwambia kwamba wabakie kuwa marafiki pekee , jambo ambalo Kamau Kamau hakuliafiki kabisa kwani licha ya kuendelea kuwa na urafiki na Blandina , kwenye akili yake alikuwa akipanga mengine, mipango yake ikaja kukamilika baada ya kumaliza kidato cha nne siku ya mahafali.

Tukio la kuwekewa dawa ya usingizi na kufanya mapenzi nje ya ridhaa yake na kupelekea kupoteza usichana wake lilimuuzi na kumuumiza sana Blandina na aliapia kwa majina yote hatokuja kumsamehe tena Kamau, lakini likawa swala la muda tu kwani baada ya wote Kwenda masomoni ngazi ya Shahada nchini Australia, Kamau Kamau ndio akatumia nafasi hio kuomba msamaha kwa Blandina na alifanya yote hayo kwakuwa alikuwa akimpenda Blandina sana.

Blandina kwakuwa alikuwa ugenini na mtu pekee aliekuwa akimfahamu alikuwa ni Kamau basi wakasameheana na kwanzia siku hio ndio mwanzo mpya wa kufanya mapenzi , huku Blandina akimwambia Kamau kwamba siku akipata mwanaume anaempenda wataachana, yaani kwa manenno marahisi Blandina alimchukulia Kamau kama ‘Sexmate’(Mgoni) wake tu(We sex with no String attached or friend with benefit).

Blandina alifanya hivyo kupunguza munkali wa kuhisia aliozokuwa nazo wakati akiwa masomoni wala hayakuwa mapenzi, alijitahidi sana kumpenda Kamau , lakini moyo wake ukagoma kabisa lakini kwa upande wa Kamau akatokea kumpenda sana Blandina.

Mwaka mmoja mbele yaani wakiwa mwaka wa pili ndio mwaka ambao sasa kamau aliweza kukutana na Senga ambaye alifika pia Australia kwa ajili ya masomo ya ngazi ya juu yaani Shahada.

Kamau akawa mwenyeji kwa Senga Kweka kipindi hicho na kutokana na kwamba walitokea kwenye nchi ambazo zinaunganishwa na lugha moja na ujirani , basi urafiki wao ukawa mkubwa sana kiasi kwamba kupitia urafiki huo ndio Kamau akamtambulisha Senga kwa Blandina.

Sasa alichokosea Kamau ni kumtambulisha Senga kwa Blandina kama wao ni marafiki tu na hakukuwa na la ziada , utambulisho huo ndio ukazaa hamasa ya Senga kuanza kumwangalia Blandina kwa macho ya kimapenzi , kadri siku zilivyokuwa zikienda Senga akatokea kumpenda sana Blandina , lakini haikuwa kwake tu hata kwa Blandina hivyo hivyo alitokea kumpenda Sana Senga , lakini hawakuweza kuambiana kwa kipindi hiko, kila mtu alificha hisia zake , huku upande wa Kamau pia akishangazwa na mabadiliko ya Blandina kwani hakupewa tena ‘Kitumbua’ na mrembo huyo wakati huo huo Blandina akionyesha sana kumjali Senga kuliko Kamau.

Baada ya miaka mitatu kupita ndio Raisi Kamau na Blandina wakamaliza masomo yao, huku kipindi hicho Senga yeye akiwa mwaka wa pili akiingia wa mwisho , Raisi Senga hakutaka kuzembea tena , hakutaka Blandina kurudi nchini Tanzania kabla ya kumweleza kile ambacho alikuwa akijisikia moyoni.

Siku ya mahafali ndio siku ambayo Senga akaweka wazi kile ambacho anajisikia na kumuomba Blandina wawe mapenzi , kwa upande wa Senga kusema ukweli ilikuwa ni kama kupiga bomu mochwari kwani Blandina kipindi hicho alikuwa amekufa na kuoza kwa Senga, hivyo alikubwaliwa siku hio hio bila kipingamizi na hatimae ikawa wiki moja tokea penzi lao kuanza.

“Senga nimeamua kubakia hapa hapa Australia nimepata kazi kwenye kampuni nataka nifanye nijipatie uzoefu kabla ya kurejea nchini Tanzania , nimeongea na baba na amenikubalia”Aliongea Blandina siku chache tu mara baada ya mapenzi yake na Senga kuanza , siku hio wakiwa kwenye ‘mtoko’ katika eneo maarufu la Sydeney Park wakilamba Ice Cream.

“Unasema kweli mpenzi , Daah ! Blandina siamini kabisa ni maamuzi sahihi umefanya , nilikuwa na huzuni unaniacha nakurudi Tanzania”Aliongea Senga akiwa amevalia shati lake la draft la mtumba ambalo alilinunua kwenye soko maarufu sana hapo Sydney. Usishangae sana hata Asutralia mitumba ipo kipindi hicho.

Taarifa hio ilimfurahisha sana Senga kwani alikuwa na huzuni mno kumwachia Blandina akirudi Tanzania hivyo aliikubali kwa mikono miwili maamuzi yake , upande wa Kamau baada ya kumaliza Shahada yake akarudi Kenya akimwacha Blandina Australia pasipo ya kujua mahusiano kati ya Blandina na Senga huku kichwani akiwa na mpango wa Kwenda kumchumbia Blandina mara baada tu ya kurudi Tanzania.

Blandina aliendelea kufanya kazi kwenye kampuni moja hapo Australia kwa ruhusa kutoka kwa familia yake huku Tanzania , sababu kubwa ikiwa ni kigezo cha kuongeza uzoefu , lakini haikuwa kweli nia ya kubaki Australia ilikuwa ni kuendelea kula raha na mpenzi wake Senga.

Baada ya Senga kumaliza masomo aliunganisha na ‘Masters’ hapo hapo chuoni mara baada ya kupata ufaulu mzuri , huku Blandina akiendelea na kazi.

Siku moja wakiwa kwenye fukwe ya Bondi ndio wakakutana na Raheli pamoja na Jeremy , kipindi hiki Jeremy hakuwa raisi bado bali alikuwa tayari alishaoa , ila mwanamke aliefika nae huko Australia kula bata alikuwa ni mrembo Raheli.

Kwahio urafiki wa Raisi Jeremy na Senga ulianzia Australia kwenye fukwe maarufu ya kipindi hicho ya Bondi , wakati huo huo Kamau na Senga wakifahamiana huko huko Australia.

Baada ya miaka yote ya masomo ya Senga kumalizika ndipo alipoweza kurudi nchini Tanzania , huku swala la kwanza baada ya kurudi ikawa ni kutaka kuoa na kuanza Maisha, jambo ambalo lilipingwa vikali sana na Afande kweka ambaye alikuwa baba yake.

Afande Kweka alitaka Senga ajiunge na jeshi mara moja ilikuendeleza ‘Legacy’ ya familia na kuacha na mambo yake ya kutaka kuoa mapema , lakini Senga akasimamia msimamo wake wa kutaka kuoa , huku akienda mbali kabisa hawezi kujiunga na jeshi, jambo hilo lilimkasirisha sana baba yake , kwani haya kuwa makubaliano yake na Senga.

Afande kweka alimtaka Senga akasome na akirudi ndio ajiunge na Jeshi lakini kutoka na Senga kukolewa na penzi la Blandina aligoma Kwenda Jeshini na akataka kuoa na hapo ndio wakatofautiana na baba yake na kufukuzwa nyumbani.

Senga hakuwa na tatizo alimchukua Blandina na wakahamia Rasmi Songea na wakaanza Maisha , huku Blandina akitumia utajiri wa nyumbani kwao kumnufaisha Senga kwani waliweza kufungua kampuni ya usafirishaji kwa kutumia mtaji ambao ulitolewa na Blandina.

Upande wa Raisi Kamau aliumia sana mara baada ya kusikia wawili hao wamefunga ndoa lakini kwakua alikuwa nchini Kenya kipindi hiko na Senga na Blandina walikuwa watanzania alishindwa kufanya chochote lakini kubwa Zaidi hakuwahi kuwa na mahusiano na Blandina licha ya kwamba walikuwa wakifanya ngono.

Raisi Kamau na yeye alioa mwanamke wa Kikuyu na kuanza Maisha na alipojaliwa Watoto wawili ndipo mke wake akafariki kwa ajali, kwahio Blandina alikuwa mke wa pili wa Raisi Kamau bala baada ya tukio la kupotea kwa ndege ya M-Airline.

Raisi Kamau hakuonyesha wazi chuki zake kwa Senga ila ukweli alikuwa akiungua sana na kumchukia kwa wakati mmoja na chuki ilizidi mara baada ya Blandina kumtamkia waziwazi kwamba alikuwa akimpenda Senga kufa kuzikana.

Baada ya miaka kadhaa kupita baada ya kupotea kwa ndege, Raisi Jeremy wa Rwanda akatumia maumivu ya Senga kumshawishi kujiunga na siasa ilikuwa na nguvu itakayomwezesha kulipiza kisasi juu ya njama iliofanyia kupoteza ndege ya M Airline.

Kipindi hicho kwakua Senga alikuwa kwenye maumivu makali ya kumpoteza mtoto wake Denisi pamoja na mke wake kipenzi Blandina , lakini pia mara baada ya Raisi Jeremy kumdokezea juu ya ajali ile ya ndege kuwa yakupangwa , basi iliamsha moto wa Raisi Senga kujiimarisha kwenye mambo ya siasa , huku akilini mwake akiwa na ile nia ya kutaka kulipiza kisasi kwa ajili ya Blandina na mtoto wake Denisi.

Upande wa Afande Kweka mara baada ya kuona Senga karudi kwake alimpa sapoti ya kutosha , huku akijiona mwamba kwani kila kilichokuwa kikiendelea kilikuwa ndani ya mipango wake alikuwa jasusi haswa mwenye Roho ngumu kwani licha ya mtoto wake kupitia kipindi kigumu yeye alikuwa akinywa kahawa kwa kutulia kabisa.

Kwanza kabisa ndie aliemtoa Denisi pamoja na Lorraine kafara kwa kuingiza kwenye mpango LADO, lakini wakati huo huo akihakikisha Blandina anaendelea kubakia nchini Kenya kwenye himaya ya Kamau, Afande Kweka hakumpenda Blandina kutokana na kwamba aliamini Senga alikuwa akipoteza mwelekeo kwa sababu yake, na ni kweli Senga kipindi hicho aliloea sana kwenye penzi la Blandina kiasi kwamba alikuwa akimuona Blandina kama ndio mzazi wake, alikuwa ni kama amewekewa Limbwata.
 
SEHEMU YA 341.

Edna sasa alielewa kwanini Blandina alisema kwamba picha hio alikuwa amepiga yeye, kumbe alishawahi kukutana na Raisi Jeremy huko Australia akiwa na mama yake wakila bata.

Roma mwenyewe alishangaa kumbe mama yake ni msomi mkubwa tu, lakini hata hivyo ilikuwa ni halali kabisa, kwani mambo ambayo Blandina aliweza kuyafanya kwa jamii kupitia sura ya Maina yalikuwa makubwa sana, kwani kama utaweza kupiga hesabu ya thamani ya vituo vyote ambavyo alivianzisha kwa nguvu zake ni Zaidi ya Dollar milioni mia moja.

Upande wa Roma yeye hakushangaa sana kwani alikua akijua mzazi wa Edna , ila mbele ya Edana alijifanyisha na yeye kushangaa , kwani alijua kama atasema alikuwa akifahamu na akakaa kimya , Edna angekasirika.

Maelezo ya Bi Wema hayakuwa na utofauti sana, kwani alishaelezwa na Raheli mwenyewe juu ya baba mzazi wa Edna, lakini sasa jumla yao wote wakajiuliza swali moja ni nani ambaye ameleta taarifa hio, na ni kwa madhumuni yapi, upande wa Roma aliamini sio Raisi Jeremy alieleta hio karatasi aliamini kuna mtu mwingine ambaye ameleta barua hio ila hakujua sababu ni nini na aliajiambia ni swala la muda tu atafahamu.

Edna sasa anajikuta akianza kuhisi huenda hata mtu aliekuwa akijiita The Protector alikuwa ni Raisi Jeremy , kwani mambo mengi ambayo aliokuwa akimsiadia yalikuwa yakihataji intelijensia ya hali ya juu.

Licha ya kwamba alihuzunishwa na jambo hilo , aliona mama yake hakuwa mtu wa kulaumiwa , kwani kulikuwa na mkataba wa yeye kutambulika kama mtoto wa Adebayo, lakini pia aliweza kufurahi na kuchukia kwa wakati mmoja kwa kumfahamu baba yake , kilichomfanya kufurahi ni kwamaba alikuwa ashatoka kwenye sintofahamu aliokuwa nayo kwa muda mrefu lakini kilichomfanya kuchukia ni kitendo cha kuwa mtoto wa nje ya ndoa lakini pia Raisi Jeremy kutoonyesha dalili yoyote ya kumtambua mbele yake.

“Bi Wema Raisi Jeremy anafahamu kama mimi ni mtoto wake wa Damu?”Aliuliza Edna.

“Juu ya hilo sifahamu , kwani mama yako alipofahamika ni mjamzito tayari alikuwa anafahamika kama mke wa Adebayo”Aliongea Bi Wema na Edna alitingisha kichwa na kisha kwa huzuni alirudi chumbani kwake.

Roma alijikuta akimuonea huruma mke wake , kwani aliweza kukumbuka maneno ya Raisi Jeremy juu ya kutokuwa na mpango wa kutomfanya Edna kuwa mtoto wake licha ya kwamba anamtambua, Alimuona mke wake hakuwa na utofauti na Yatima licha ya kwamba alikuwa na pesa nyingi, hisia ambazo zilimrudisha miaka kadhaa nyuma akiwa peke yake na Lorraine kwenye kisiwa , wakiwa hawana Baba wala Mama.

*******

Zilipita siku kumi , upande wa kwenye kampuni mashindano yalikuwa yakiendelea kama kawaida na Sophia alikuwa akifanya vyema sana kiasi cha kumpelekea kujipatia mashabiki wengi sana , kwani kwenye mitandao ya kijamii alikuwa akizungumziwa sana , huku Clip zake akiwa anaimba zikisambaa sana, watu wengi wakimtazamia kuwa mshindi wa mashindano hayo.

Mashindano yalikuwa na mvuto mkubwa sana kwani yalikuwa ya kipekee na mpangilio wake kupendwa na wengi lakini pia ndio mashindano ambayo yalikuwa yakifuatiliwa kwenye nchi nyingi sana na hio ni kutokana na kuhusika kwa Christen kwenye mashindano hayo kama jaji ambaye anatazamiwa kushiriki siku ya mwisho ya fainali, lakini pia Christen kitendo chake cha kuyapigia mashindano hayo ‘Promo’ wakati akiwa kwenye mahojiano na Vexto Tv , iliyapaisha sana duniani mashindano ya Kizazi nyota na kufanya taifa la Tanzania kutambulika Zaidi kimataifa.

Zilikuwa zimebakia hatimae wiki tatu mpaka mashindano hayo kuhitimishwa , kwani kila wiki mashindano yalikuwa yakifanyika mara mbili na washiriki watano walikuwa wakitoka kwenye kila siku michuano.

Ikiwa ni siku ya jumamosi , kabla ya mashindano kuanza mshereheshaji Amina kanani aliweza kutoa tangazo juu ya ujio wa msanii mkubwa atakaetumbuiza siku ya fainali , msanii wa kike mrembo kutoka Korea Kusini afahamikae kwa jina la Yoon- He

Yoona- He ni moja ya wasanii maarufu ambaye anauza sana kazi zake za kisanaa ndani ya Korea na nje ya Korea , alikuwa na mashabiki wengi sana na kitu ambacho kilimfanya pia kutambulika kimataifa ni pamoja na uwezo wake katika mambo ya uigizaji , akiwa ameshiriki kwenye muvi na Tv Shows mbalimbali mbali ambazo zilifanya vizuri sokoni kimnataifa.

Licha ya kuwa msanii lakini pia inasemekeana mafanikio ya Yoon-He yalichangiwa na ukwasi wa pesa wa familia yake, kwani babu yake Yoon-He ni moja ya wafanyabiashara wakubwa walijikita katika udhalishajii wa vifaa vya kidigitali vya mambo ya nyumbani , akitajwa kama Tajiri namba kumi ndani ya Korea.

Hivyo baada ya Tangazo hilo liliibua munkari sana kwa mashabiki na wafatiliaji wengi pamoja na wale ambao walikuwa shabiki wa Yoon -He,menejimenti ya Yoon He ndio iliofanya mawasiliano na kampuni ya Vexto na kuomba ushiriki katika kuimba siku ya fainali jambo ambalo lilikubaliwa na Daudi pamoja na Amina mara moja , huku upande wa Roma kwakua hakuwa sana mpenzi wa nyimbo wala shabiki wa mtu yoyote alikubali tu ilimradi Yoon He angeongeza mapato.

Yalikuwa ni mafanikio makubwa sana ambayo yamepatikana tokea mwanzo wa shindano hilo ndani ya siku chache tu , kwani faida ilikuwa ikionekana lakini pia wafatiliaji walikuwa wengi hivyo kufanya matanganzo ya kampuni ya Vexto International kufikia watu wengi sana na kufanya hata hisa za kampuni kupanda ndani ya muda mfupi , jambo ambalo lilimfurahisha sana Edna na kuona kwamba yalikuwa mawazo sahihi ya kufungua kampuni ya Habari na burudani, lakini pia lilikuwa wazo sahihi kumwachia Roma kuongoza kampuni hio.

Edna akiwa ofisini kwake alikuwa kwenye mawazo ya hapa na pela huku akiangalia Skrini ya tarakishi yake iliokuwa ikionyesha namna ambavyo mauzo ya hisa yamepanda kwa siku hio mara baada ya kutangazwa kwa ujio wa msanii Yoon-He.

Wakati akiendelea kuwaza alijikuta akikumbuka maneno ya mama mkwe wake siku mbili zilizopita juu ya Roma kuhamia kwenye chumba chake huku Lanlan ahamie kwenye chumba cha Qiang Xi , Edna alionekana kutafakari kidogo , huku akikumbuka siku hizo kumi zote Maisha na Roma yalikuwa mazuri sana kiasi kwamba hawakugombana na kubwa Zaidi tokea amtamkie Roma anampenda ni kama vyumba vya hisia visivyoonekana kwa darubini za kiganga kwenye moyo wake vilifunguka wazi kiasi kwamba hisia za kimapenzi zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba hata akimuona tu alikuwa akinyegeka.

Zimebaki siku tano tu kufikia tarehe ishirini na Tisa, Babu yake Lanlan asipotokea ndio siku nitakayo mlea Lanlan kama mtoto wangu na Roma kama baba yake na ndio siku ambayo Lanlan ataenda kulala na Qiang Xi na mimi kulala na Roma kama mume wangu”Aliwaza Edna kwenye kichwa chake na kujikuta akitabasamu na alikuja kushituliwa na Monica ambaye aliingia hapo akiwa na faili tatu ambazo Edna anapaswa kuzisaini kabla hazijapelekwa kwenye kampuni Tanzu ili hatua Zaidi kuchukuliwa.

*******

Upande wa Raisi Senga alifanikiwa Kwenda Nigeria na kurudi salama salimini , lakini licha ya hivyo alionekana kutokuwa sawa kama alivyondoka , alionekana kuwa kwenye mawazo kiasi ambacho kilimfanya hata mke wake Damasi kujua mabadiliko ya mume wake.

“Senga ulivyoondoka sio kama ulivyorudi , unaonekana kuwa na mawazo mume wangu k ni jambo gani linaendelea?”

“Mama Ashley niko sawa ni maswala ya kikazi tu ndio yananifikirisha”Aliongea Senga kwa kujitutumua na muda huo alikuwa ndio anarudi kutoka ofisini.

Ukweli ni kwamba kilichomfanya Damasi kuwa na wasiwasi na mume wake ni kutokana na kwamba ,tokea arudi kutoka Nigeria alikoenda kikazi , hakumgusa kabisa na ndio maana Damasi alikuwa akipatwa na wasiwasi kwani haikuwa tabia ya Senga , lakini jambo lingine ni kwamba hakuwa sawa kimawazo , yaani Raisi Senga kuna muda alikuwa akiangalia sehemu basi macho yake yataganda sehemu hio mpaka ashituliwe na hiko ndio kikamfanya Damasi kuwa na mawazo.

“Senga nadhani unaelewa kauli yangu ya siku zote, licha ya kwamba wewe ni raisi wa Watanzania nikiwa mimi mmoja wapo ,lakini pia utambue mimi ni mkeo na unatakiwa kuwajibika kwangu na kwa familia”Aliongea Damasi kwa msisitizo na kisha akatoka kwenye chumba chao cha kulalaia na Kwenda upande wa Sebuleni kuendelea kuangalia Runinga.

Ikiwa ni siku nyingine baada ya Raisi Senga kuingia ofisini , asubuhi hio alionekana kuwa na ugeni ambao alionekana alikuwa akiusubuiria, ni kweli baada ya madakika kadhaa alionekana mwanaume mmoja wa kihindi mwenye umri kati ya miaka hamsini hivi akiingia ndani ya ofisi ya kukutania wageni akiwa ameongozana na Katibu Muhtasi.

“Mheshimiwa Mjumbe kutoka baraza la haki za binadamu kashafika”Aliongea Katibu na Mheshimiwa alimpa ishara ya kumruhusu , muda ule ule mjumbe yule wa kihindi aliingia ndani ya eneo hilo na walisalimiana kwa bashasha na baada ya Raisi Senga kumkaribisha mgeni wake , palepale alitoa maagizo juu ya kikao hicho kuwa cha siri kwa muda wa dakika kadhaa na baada ya hapo baadhi ya viongozi wa Ikulu wataruhusiwa kuingia kushiriki kwenye mazungumzo pamoja na kupiga picha na kuweka mitandaoni na kwenye gazeti la kiserikali.

“Mheshimiwa nadhani hakuja haja ya maongezi Zaidi kwani kila kitu kishaongelewa, kama nilivyojitambulisha mimi ni mwanachama wa baraza la haki binadamu kutoka UN nikihudumu upande wa Afrika (Umoja wa mataifa) na nipo hapa kwa ajili ya kupata sahihi yako juu upatikanaji wa haki za LGBTQ(Mapenzi ya jinsia moja) hapa Tanzania”Aliongea yule mwanaume ambaye alijitambulisha kwa Mheshimiwa Senga kwa jina la Vishnu Gupta.

Mheshimiwa alifikitia kidogo , mtu aliekuwa mbele yake alikuwa akitaka yeye asaini mkataba wa kulinda haki za mashoga hapa Tanzania , ijapokuwa makubaliano yake nchini Nigeria hayakuwa ni kwa ajili ya kutangaza hadharani kama anakubali mashoga lakini alitakuwa kutia sahihi kama mkuu wa nchi ili kuhakikisha kwamba serikali haingilii haki za mashoga nchini.

“Hakuna shida bwana Vishnu nitasaini mkataba kwani ni sehemu ya makubaliano yangu”Aliongea Raisi Senga na Vishnu alitoa karatasi na kumpatia raisi Senga na baada ya kuzisoma kwa muda mfupi hatimae aliweza kuzitia Saini , jambo ambalo lilimfanya Vishnu kutabasamu na alipeana mkono kama ishara ya makubaliano na baada ya hapo ndipo Kamera ziliruhusiwa na mazungumzo yakawa wazi , huku raisi Senga akitoa ahadi kwamba ataendelea kukomesha vitendo vyote ambavyo vnakiuka haki za kibinadamu.

Baada ya kikao kuisha mheshimiwa alijikuta akivuta pumzi kwa nguvu , licha ya kwamba alishasaini karatasi hizo ambazo zilikuwa ni ‘implicity’ kwenye utekelezaji wake , lakini bado alijiona kama mtu aliekosea watanzania , lakini pia aliejikosea yeye mwenyewe , lakini wakati huo huo Mheshimiwa Senga kuna tukio ambalo lilikuwa likijirudia rudia kwenye akili yake kiasi kwamba lilimfanya kabisa kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na mke wake mpaka kupelekea malalamiko.

Mheshimiwa Senga alijikuta akijiegamiza kwenye kiti chake huku akikusanya mikono yake pamoja , alionekana kuwaza sana , haikueleweka mara moja ni nini kilichotokea kwenye Ibada ya Mpasuko Wa Mwezi kutokana na usiri mkubwa uliokuwepo , lakini jambo moja ambalo ni dhahiri ni kwmaba mheshimiwa Senga alikuwa akifanya maamuzi ambayo yapo nje ya kile anachokisimamia kama Raisi licha ya kwamba alishasaini ‘Impilicity Law’ inayohusiana na Mashoga aliamini siku sio nyingi atalazimishwa kusaini ‘Explicity Law’ inayohusiana na mashoga.

(Implicity Law ni hitimisho la kisheria ambalo linampa mtu haki ya kitu pasipo kuingiliwa licha ya kwamba sheria hio haiwekwi wazi, kwa mfano kauli ya kiongozi mmoja wa dini akisema kwamba Mapenzi ya jinsia moja sio Kosa , sio uhalifu lakini ni Dhambi hio ndio sheria isio ya moja kwa moja lakini yenye kutekelezwa , yaani huwezi kusikia kiongozi akisema hadharani kama anakukataa ushoga ilihali sheria hio ishasainiwa.

Explicity Law ni aina ya sheria ambazo ni za moja kwa moja na zinapaswa kutekelezwa kwa namna yoyote ile na mara nyingi sheria hizi kwa hapa Tanzania hupitishwa na Bunge pamoja na mahakama halafu ndio raisi atasaini ili ianze utekelezwaji wake.

Wanasheria mtatusaidia Zaidi hapo.

**********

Naam ilikuwa ni siku ya jumamosi Roma alionekana Kibaha kwa Mathiasi akikunja kushoto akiwa anendesha gari yake kuelekea upande wa mji wa kisasa , mji ambao unamilikiwa na kampuni ya Vexto Group.

Roma aliendesha gari yake kwa utaratibu huku akifurahia mazingira safi yaliokuwa yapo kandokando ya barabara hii kuelekea kwenye mji huu, kusema ukweli licha ya kwamba ilikuwa mara yake ya pili kufika kwenye huo mji lakini muonekano wake siku hio ulikuwa kama ni mpya kwake na alijiambia ni uwekezaji mkubwa sana ambao umefanyika mpaka kujenga makazi hayo ya kisasa kabisa kwa nchi inayoendelea kama Tanzania.

Dakika kama tano aliweza kuingiza gari yake kwenye geti kubwa linarohusu magari kuingia kwenye ‘Apartment’ hizo na alikwenda moja kwa moja kuegesha kwenye Parking ya muda mfupi na akashuka na kuanza kutembea uelekeo wa jengo la Athena.

Alikuwa mahali hapo asubuhi hio kutokana na kwamba alikuwa na miadi na mrembo Suzzane , ambaye baada ya kuwasiliana nae alimwambia kwamba amfuate nyumbani kwake na Roma kwakuwa ndio alikuwa na shida ilimbidi kufanya hivyo ili kuonana na mrembo huyo.

Baada ya kufika chini kabisa ya hilo jengo alipiga simu Kwenda kwa Suzzane na alipewa maelekezo ya Kwenda mpaka Floor namba kumi na kusimama kwenye mlango wenye namba 200 ndio Apartment yake.

Tokea mrembo huyu aje kumchukua kwa mara ya kwanza kule Mbagala hakuweza tena kuongea nae moja kwa moja , kwanza Roma alimchukulai Suzzane kama mwanamke Siriasi asiependa utani , lakini pia Suzzane mara nyingi alikuwa ndani ya idara hii kwahio ilikuwa ngumu kwake sana kuonana nae mara kwa mara na kumzoea.

Dakika chache tu Roma alikuwa nje ya mlango namba 200 na alibonyeza kitufe cha kengele na kisha akasubiri mlango kufunguliwa na zilipita dakika kama mbili hivi hatimae mlango ulifunguliwa na mrembo Suzzane ambaye alikuwa amevalia gauni fupi la kumpendeza.

Suzznae alikuwa mzuri sana unaweza kumuitwa kwa jina la Black Beuty , kinachompoza ni ile hali yake ya kuwa siriasi na hata alivyosimama mbele ya Roma mara baada ya kufungua mlango alikuwa na sura yake yenye usiriasi vilevile na Roma alijiambia ilikuwa ni haki kabisa kwa mrembo huyu kuwa msaidizi wa Edna , kwani walikuwa wakiendana kwa asilimia mia moja tofauti yao tu ni kwamba Suzzane alikuwa na macho flani hivi akikuangalia ni kama anakudharau.

“Karibu”Alimkaribisha na Roma alitingisha kichwa na kisha kupita.

Roma licha ya kwamba alimpigia Suzzane , ila hakuweka swala lake wazi , alimwambia tu kuna mambo muhimu ambayo alikuwa akitaka kiuongea nae.

ITAENDELEA

WATSAPP 0687151346
 
Episode namba 336 Edna hatakaa aisahau maishani mwake[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
341 umeirudia mkuu
 
Nahisi hata Bwana Rais aliliwa kiboga
mwenyewe nimewaza hivyo hivyo,
ila haya mambo ya secret societies bana ni balaa sana, wengi wa watu wanaotajwa kuwa member huko wana character za ajabu ajabu.........(hili la upinde wengi huhusishwa nalo sana)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…