SEHEMU YA KUMI NA TISA.
Tembo ni kikundi ambacho kilikuwa kikijihusisha na mambo mengi ndani ya ulimwengu usioonekana,moja ya kazi kubwa ilikuwa ni Smuggling(kuingiza bidhaa mbalimbali kimagendo),Kuuza ngada,na kusafirisha meno ya tembo lakini pia kundi hili kama yalivyokuwa makundi mengine , lilikuwa likitumiwa na viongozi wa juu wa kisiasa na wafanya biashara katika kazi haramu , kama kuua , kuteka na mengineo yanayofanana na hayo.
Katika ulimwengu usioonekana mambo ambayo mengi si ya kihalali kwa kipimio cha haki na sheria katika ulimwengu unaonekana mambo hayo yote ni halali.
Katika ulimwengu usionekana kanuni kubwa ni ‘survive for fittest’yaani ndani ya ulimwengu huo unaishi kutokana na uwezo na nguvu zako za kumtawala mwingine , sasa basi baina ya hizi pande zote mbili , mara nyingi zinaenda sambamba , unaweza usielewe ila viongozi wakubwa duniani pamoja na wafanya biashara wanaelewa sana umuhimu wa huu ulimwengu usionekana.
Hivyo wafanyabiashara na wanasiasa siku zote wanahakikisha kuna uwiano sahihi kati ya hizi pande zote mbili, sasa kwa hapa bongo pia kuna sehemu ya ulimwengu huu usioonekana na raia wake tunaishi nao.
Ushawahi kukutana na mtu hana kazi maalumu mjini , ila yeye anavaa anakula na kutanua maisha kuliko wewe ambaye unahangaika kila siku , basi jua huyo mtu huenda anacheo kikubwa katika ulimwengu huo usionekana , unaweza kuupa majina utakayo , unaweza kuita ulimwengu wa kiza , ila wazungu wanapenda kuita ‘Underworld’ yaani the world of criminals(ulimwengu wa wahalifu) sasa usishangae sana ukaona mwanasiasa anatoka hadharani na anakemea matendo mabaya yanayofanyika ndani ya ulimwengu wa kiza lakini yeye akawa ni moja ya wahusika wa wahalifu hao, hii ndio sababu inayofanya ulimwengu huu kuja kudumu milele na inaweza ikafikia siku ule uwiano ukavunjika na ulimwengu huu ukawa na nguvu na hapa ndipo utaona mambo mengi ya kihalifu yakifanyika katika dunia,wewe ishi ila kuna mambo mengi yanafanyika eneo unaloishi na ni ya kutisha na usifahamu, na hautofahamu kwakuwa wewe upo kwenye unaishi kwa kutazama uhalisia unaonekana lakini yapo mengi yanayofanyika nyuma ya huo uhalisia. Unaouona.
Sasa kundi la Tembo , Black Mamba ndio makundi makubwa yaliokuwa yakifanya kazi ndani ya jiji hili la Dar Es Salaam , yapo makundi mengi ila hayo ndio yenye nguvu huku mmiliki wa kundi la Tembo akiwa ni Rose na mmiliki wa Black Mamba akiwa ni Marehemu Karimu.
“Huyu The Don ni nani haswa Rose?”Aliuliza Roma
“Hata mimi si mtambui , ila ndio mwenye nguvu kubwa sana hapa nchini , hafamiki kwa jina ila inasemakana ni mwanasiasa mkubwa na mfanyabiashara na mimi kabla ya kuweka makazi yangu hapa Dar nilipitia hatua za kuomba ruhusa kwa The Don”Aliongea Rose.
“Hebu niambie kwanza uliwezaje kuweka kundi lako hapa Dar?”
“Ni stori ndefu Roma ila ukweli ni kwamba ,damu nyingi zilimwagika mpaka kupata koloni hili na baadae kuingia mkataba na Black Mamba”aliongea Rose na Roma alielewa anachomaanisha na hakutaka maelezo mengi kwani muda umeenda , Rose alienda kuandaa chai na Roma alijiandaa vizuri na kunywa chai , na baada ya k ushiba , alitoka na kuingia kwenye gari yake.
“Hapa niende moja kwa moja kazini”Aliwaza Roma wakati akipita maeneo ya Rangi tatu sokoni.
*****
Juma alishangaa sana kumuona Najma baada ya kumfungulia Geti , bwana huyu alionekana kuwa na wasiwasi sana wakati wote ambao Najma alikuwa ameshikiliwa.
“Najma uko salama?”Aliuliza Juma , lakini Najma hakuongea kitu Zaidi ya kupita na kuingia chumbani kwake na kujirusha kitandanni huku akianza kulia kwa kwikwi , akiwa amejikunyata.
Jjuma yeye hakuweza kuingia kwenye chumba cha dada yake hivyo aliona jambo pekee ni kutulia , lakini kwa hali aliomuona nayo Najma aliamini kabisa kuna jambo ambalo limemkuta Roma.
“kwa hali aliokuwa nayo Najma lazima Roma hatupo nae tena Duniani na mpango wangu utakuwa umeenda kama nilivyokuwa nimepanga”Aliwaza Juma huku akionekana kutabasamu na kujiona mshindi.
“Ila yale maneno ya Mganga yatakuwa ya uongo yale”Alifikiia Juma maneno alioambiwa siku kadhaa zilizopita na mganga huko Chanika.
Ilikuwa hivi baada ya siku ile Roma kuondoka , swala lile lilimuuma sana Juma , yaani sio kidogo na kilichomuuma yeye lilikuwa ni swala la mafanikio ya Roma , katika maisha yake ashajiwekea kuwa Roma siku zote atakuwa masikini na yeye atakuwa tajiri , lakini mabadiliko yaliotokea ghafla yalimsononesha mno na alikuwa hana Amani hata kidogo katika moyo wake na ndio maana baada ya siku mili zilivyopita alienda kwa mganga chanika.
Mganga Maluweluwe alikuwa akisifika sana upande huu wa Chanika kwa tiba zake zake za kuaminika , watu wengi walienda kwake kwa ajili ya kutatua matatizo yao , sio viongozi wa kisiasa sio wafanya biashara walikuwa wakienda kwa Maluweluwe kwa ajili ya kutatua shida zao.
Sasa na Juma aliaminni swala lake linaweza kutatuliwa na mganga huyu na ndio maana alifunga safari kutoka Rangi tatu na kwenda kwa Maluweluwe .
Ilikuwa asubuhi Juma alifika mtaa huu wa Maluweluwe na kwenda moja kwa moja kwa mganga , Mganga huyu alikuwa yuko vyema sana kiuchumi, kwani katika eneo hilo nyumba yake ndio ilikuwa kubwa tena ya Ghorofa mbili kwenda juu huku ikiwa imezungushiwa ukuta mkubwa, na mafanikio ya Maluweluwe ni kutokana na tiba yake hio ya kienyeji ambayo alikuwa akiwafanyia watu.
Juma alikaribishwa pale na wasaidizi wa Maluweluwe , huku akishangaa baadhi ya magari yaliokuwa hapo ndani ya watu waliokuja kufata Tiba , hali hio ilimfanya Juma moyo wake unyong`onyee na kujiona ni mwanaume mwenye laana , kwani ukilinganisha na watu waliokuwa wapo hapo ndani na yeye , alijiona yeye pekee ndie ambae alikuwa masikini, sasa cha kushangaza Zaidi ni kwamba alikuwa hapo ndani kwa ajili ya kumroga mwenzake ili afanane nae.
Baada ya foleni hii kuisha hatimae Juma ilikuwa zamu yake , Maluweluwe alikuwa Profesheno kwenye kazi yake , kwani alikuwa na mhasibu kabisa na ukishalipia kwa mhasibu unaingia kwenye chumba ambacho juu kabisa kuna kibao kimeandikwa ‘Chumba cha Daktari’.
Ukweli licha ya Juma kumsikia sana sifa za Maluweluwe hakuwahi kumuona , lakini leo hii ndio amemuona na katika akili yake alikuwa akidhania kuwa anaenda kukutana na mzee mwenye mvi , ila Maluweluwe alikuwa kijana ambae kwa haraka haraka ungemkadiria umri wake kuwa miaka therethini kwenda juu.
“Karibu kijana”Aliongea mganga huyu ambae hakuwa na utofauti sana kimuonekano wa kimavazi na mitindo kama wale waganga unaowaona kwenye Bongo muvi , au kama wewe ushawahi kwenda kwa mganga basi utakuwa unajua muonekano wa Maluweluwe.
Basi kama kawaida ya waganga alianza mbwembwe za hapa na pale , na kupandisha mashetai ya kimchongo na kisha alimruhusu Juma kueleza shida yake kwa kina.
“Kuna rafiki yangu juzi juzi hapa kapata mke tajiri , jambo ambalo halijanifurahisha , kwani maisha yake yamebadilika sana, hivyo nimekuja umfanyizie aachwe na azidi kuwa masikini”.Mganga huyu alimwangalia Juma na ujasiri wake na kisha alianza kupandisha mashetani.
“Leta jinaaaa… Leta jinaaaa”Aliongea mganga huyu kwa sauti nzito na kumfanya Juma moyo wake utabasamu kuona yes hapa kafika mahali penyewe maana sio kwa mashetani hayo.
“Anaitwa Roma,, yes Roma Ramoni anaitwa”.Mganga baada ya kufanya mbwembwe zake pale aliita jini lake la utambuzi ili kumpa taarifa zinazomuhsu Roma na ndani ya dakika chache mganga huyu alionekana kutoa jasho.
“Kijana mtu unaetaka kumroga hashikiki ,,,, nasema haogekii , harogekii”
“Unamaanisha nini Maluweluwe?”
“Majini yamekataa kujihusisha na mtu huyo unaweza kuondoka”
“Maluweluwe nishalipia hela yangu , nataka tiba”Juma alijifanya haelewe na kumkazia mganga.
“Tiba sahihi kijana ni kukaa mbali na Roma , ni Zaidi ya mchawi na simuwezi na majini yamekataa kutoa tiba”
HIvyo ndivyo ilivyokuwa huko kwa mganga na maneno hayo yalikuwa yakimfikirisha Juma kwa siku nzima mpaka pale alipokuja kupata jambo jipya.
Juma siku ya pili yake akiwa kazini baada ya kutoka kwa mganga , alifuatwa na bwana mmoja hivi mwenye kijitambi cha pesa, na ni baada ya bwana huyu kuulizia ulizia ndani ya soko hili la Mbagala na ndipo alipokuja kumpata Juma aliekuwa bize kuhamisha magunia ya yeboyebo kwenda kuyahifadhi na muda huo ulikuwa jioni saa moja.
“Sikia nitakulipa mara mbili ya hela unayopata kwa kusukuma hayo magunia”Aliongea bwana huyu ili aweze kupata nafasi ya kuongea na Juma , na kutokana na ofa hio Juma hakukataa na kukubali na kuingia kwenye Gari ya Verosa nyeusi na bwana huyu mwenye kitambi na gari hii ilikuja kusimamishwa mtaa wa Zakiem kwenye mgahawa mmoja hivi pembeni ya barabara inayoenda Kijichi.
“Naitwa Ahmedi ni Meneja mauzo kampuni ya Tigo mkoa huu na nimekuomba kuongea na wewe juu ya mdogo wako Najma”Juma alishangaa ila alitaka bwana huyo aendelee kuongea.
“Sikia Juma nimetokea kumpenda sana Najma na nipo tayari hata kumuoa , lakini dada yako nimejaribu kila mbinu kumpata ila amekuwa mgumu na hio ndio sababu inayonifanya tuwe na haya maongezi , nataka unisaidie kumpata Najma maana kaniambia ana mtu anampenda , lakini anaonekana kunidanganya”.Juma kwanza alishangaaa , lakini alitabasamu moyoni kwa wakati mmoja, kwa bwana kama huyu mwenye pesa zake kumpenda dada yake , Juma mtu aliekuwa mbele yake sio mtu pekee anaempenda dada yake ila aliona fursa Adhimu sana.
“Bro nimekuelewa sana , pia nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kumuoa Najma”Jamaa alitabasamu.
“Sasa unanisaidiaje kumpata Najma au ni kweli ana mtu kama alivyosema?”
“Ndio kuna jamaa mmoja hivi anampenda , ila mimi naamini sio upendo ila ni ujinga wa dada yangu tu kwani hajawahi kuingia kwenye mapenzi”Jamaa alitoa tabasamu la ushindi.
“Huyo mtu ni nani na anafanya kazi gani?”
“Huyo jamaa, alikuwa ni mbeba mizigo kama mimi anaitwa Roma , lakini kwa sasa ameoa na haishi maeneo haya..Broo tusiongee mengi mimi nimekukubali bro na Najma ni wako”Aliongea Abuu , lakini wakati wanaendelea kupiga Stori mara aliingia jamaa flani ambae alikuwa na nywele za kisomali hakuwa mweusi na pia hakuwa mweupe sana.
“Karim umejuaje niko hapa?”Aliongea bwana huyu Ahmed akimchangamkia Karim na walionekana walikuwa wakifahamiana.
“Kuna mtu nia miadi nae maeneo haya , ila naona tumekutana”Aliongea huku Juma akimwangalia Karim maana alikuwa akimjua vyema na hakuna ambae hakuwa akimjua Karim ndani ya meneo hayo ya mbagala maana alikuwa akimiliki biashara nyingi.
“Huyu ni kaka yake Najma”Aliongea Ahmedi na Karimu alimwangalia Juma na kisha akatingisha kichwa na wakati huo huo alifika bwana mmoja hivi alievalia kibishoo na kusogea meza waliokuwa wamekaa Juma .
“Vipi Zonga ni taarifa gani unayo , ambayo umesema ni muhimu”Aliongea Karim mara baada ya Zonga kufika .
“Bro huyo jamaa ndio anatoka na Rose”Aliongea Zonga huku akimkabidhi Karim picha , ambayo Juma baada ya kuiona tu aliitambua maana alikuwa amekaa karibu na Karim.
“Huyu Fala anaitwa nani na anakazi gani hapa mjini?”.
“Hana mishe yoyote ya kueleweka ila kwasasa anamke”Aliongea Zonga.
Ahmedi na Juma waliendelea na mazungumzo yao huku wakiacha kumfatilia Karim, lakini wakati wakiendelea kuongea simu ya Ahmedi iliita na baada ya kuona jina la mpigaji alijikuta akikunja sura yake na kunyanyuka na kutoa waleti yake na kumpa Juma nyekundu tatu huku akimpa simu ndogo aandike namba zake za simu.
“Sasa sikia Juma tutawasiliana , Karim ninadharula ngoja kuna mishe niwahi nitakutafuta mida basi”
“Okey poa”Alijibu Karim huku akiendelea kumsikiliza Zonga na Juma alinyanyuka na kutoka nje ya Mgahawa huo na zilipita dakika chache tu Zonga alitoka na kuondoka na baadae kidogo akatoka Karim na kuiendea gari yake.
“Broo”Karim aligeuka na kuangalia mtu anaemwita na alimwona ni kaka yake Najma.
“Vipi?”Aliuliza karim maana hakutaka stori sana maana alimuona Juma wakawaida sana kuongea nae , na bwana huyu alikuwa akijisikia mno na alikuwa akichagua wakuongea nae.
“Namjua huyo Roma , jamaa aliekuonyesha picha na najua namna ya kumpata”Aliongea juma haraka haraka na hapa karim alimwangalia Juma na kuvutiwa na mongezi.
“Ingia kwenye gari”Juma aliingia.
“Unamjua vipi Roma?”
Juma alianza kueleza namna alivyokuja kumjua Roma sikuyakwanza na mpaka Roma alivyopata mke .
“Sasa ni namna gani ya kumpata Roma?”.
“Roma anampenda sana Najma Sana , hivyo kama tutamtumia dada yangu itakuwa rahisi”Karimu aliona wazo zuri kwani alikumbuka maneno ya Zonga kuwa Roma alikuwa akimnyandua Rose mwanamke anaempenda na kumhangaikia kila siku , ila huyo fala anaeitwa Roma anakula bila ya kufanya juhudi yoyote moyo wake uliuma na aliapia kwenye moyo wake kumpoteza Roma Duniani na kubaki na Rose wake lakini alikuwa hajui namna ya kumpata Roma, sasa baada ya Juma kujieleza aliona yes , mpango wake unakwenda kukamilika kirahisi.
“Sasa sikia tutamteka Najma baada ya kumteka tutampigia Roma aje kumuokoa Najma maana umesema anampenda na una uhakika atakuja na hapo tutamkamata Roma”.
“Yes huo ndio mpango wangu bro”Karim alimuona Juma ni asset kumtumia kwenye mpango wake na siku moja mbele mpango ulikamilishwa ,Majambazi yalikuja ndani ya nyumba ya Juma na kumbeba Najma , huku Juma akiahidiwa kuwa Najma atakuwa salama , mpango huo Ahmed hakujua , Juma alitaka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , yaani kwanza Najma ashuhudie Roma akifa mbele yake , pili baada ya Roma kufa itakuwa rahisi kumshawishi Najma kuolewa na Ahmedi na yeye atakuwa na shemeji mwenye pesa na ukali wa maisha utapungua na aliwaza kabisa angemuomba shemeji yake mtaji aanzishe biashara.
Sasa baada ya mpango wenyewe kutekelezwa na Najma kupelekwa Vikindu na Karimu kwa mara ya kwanza kukutana na Najma mwanamke ambaye alikuwa akisikia taarifa zake kwa Ahmed , Karim alishangazwa na uzuri wa Najma kiasi kwamba pepo la ngono lilimvaa hapo na alipanga lazima alalale na Najma baada ya kutekeleza nia yake ya kumuua Roma , hakutaka kujali ahadi yake na Juma kwani alimuona kama kapuku tu , lakini pia hakutaka kmfikiria Ahmedi kwanza alijua uyo mwanamke hampendi hivyo hakuwa na hasara kufanya yeye.
SEHEMU YA ISHIRINI
Ni saa mbili kamili za Asubuhi ndani ya hoteli moja maarufu ndani ya makao makuu ya nchi mjini Dodoma ,ndani ya chumba kikubwa cha hadhi ya juu ndani ya hoteli hii , anaonekana mzee mmoja mweupe mwenye nywele nyingi kichwani , lakini zilizokuwa na mvi ,Mzee huyu kwa makadirio ya umri hakuwa chini ya miaka Hamsini.
Mzee huyu alikuwa amesimama huku nyuma yake kwenye kitanda alionekana mrembo mmoja maarufu nchini akiwa amelala , akiwa hana habari na kinachoendelea kwa mgoni wake.
Mzee huyu alikuwa ameshikilia simu , lakini simu ilionekana nzito kwake , kwani alikuwa ni mwenye kutetemeka sana,Mzee huyu wakati akiendelea kuangalia simu yake , mara simu yake ilipata uhai na kuanza kuita na mzee huyu kinyonge sana aliipokea.
“Nini kimetokea Hassani , inakuwaje mwanangu akauwawa kikatili namna hii”
“Mzee hata sisi tumeshindwa kuelewa na swala hili tunaendelea kulichunguza kwanini limetokea ghafla hivi”
“Naomba hili lifanyike haraka Hassani , inaniuma sana kumpoteza Karim mrithi wangu”
“Sawa Mzee , swala hili lazima tutalichimba kujua undani wake nakuhakikishia lazima tulipize kwa aliemfanyia unyama huu Karim”Ilisikika sauti hio na mzee huyu alikata simu , huku akisogelea sofa lililokuwa pembeni kwa kujikokota huku akiwa amejishika kifua chake , mzee huyu alionekanna kuwa katika maumivu ya kumpoteza kijana wake.
Alichukua mvinyo uliokuwa kwenye chupa na kumimina kwenye glass na kunywa kwa pupa na kisha akarudisha glasi kwenye meza.
“Naapia kwa mbingu na Arfhi uliehusika na kifo cha mwanangu nitakusaka mahali popote na nitahakikisha na kukata kiungo kimoja kimoja mpaka kifo chako”.Aliongea mzee huyu huku akiegamia kwenye sofa na kufumba macho kwa sekunde lakini alikuja kushituliwa na simu ilioanza kuita mfululizo , baada ya kuangalia nani anampiga aliona ni mke wake na hapa ni kama mzee huyu alizinduka kwani haraka sana alikimbilia nguo zake na kuvaa.
“Sijui mke wangu ataipokeaje hii taarifa”Aliwaza mzee huyu huku akiangalia simu ambayo ilikuwa ikiita kwa mara ya pili , lakini hakupokea Zaidi ya kutoka ndani ya chumba hiko.
Naam huyu ni meya wa mji wa jiji hili la Dodoma afahamikae kwa jina la Bakari Juma lakini pia anafahika kama “The man behind the Power’ndani ya kundi la The Black Mamba.
****
Juma aliamka asubuhi na mapema sana kama kawaida yake , ili awahi kwenye kazi yake ya ubeba mizigo , siku hii bwana huyu alionekana kuwa na furaha sana , kwani kila akikumbuka tukio la jana moyo wake ulikuwa mweupe.
Baada ya kujiandaa alimuaga Najma na kuianza safari ya kuelekea kazini ndani ya mdakika kadhaa tu alikuwa ashafika na kupata dili la haraka na kulishughulikia.
Muda wa saa mbili ndani ya soko hili kulikuwa kumechangamka sana na kama ujuavyo Mbagala kwa kuwa na watu wengi ,Juma akiwa anapiga hadhithi na wenzake ndipo alipoanza kusikia habari ambazo hakuwa amezitarajia.
“Oy wadau inasemekana Karim amekufa jana kwa kuuliwa”Aliongea Yusuph na kumfanya Juma ashangae na kuona huenda Yusuph amechanganya majina kati ya Karim na Roma.
“Wee..! kweli acha utani ,ilikuwaje?”
“Mwamba nasikia kagusa pasipo gusika na hivyo kuingia kingi”
“Oy yusuph ni kweli Karim kafariki?”
“Habari ni za kweli kabisa , japo kwa sasa ni za chinichini ia , mwili wa Karim upo Muhimbili ninavyoongea hapa na hakufa peke yake”Kwa muonekano wa Yusuph wa uongeaji wake Juma aliamini bwana huyu hakuwa akidanganya kwani alikuwa akimwamini sana , lakini bado kwenye kichwa chake alikuwa na maswali ni kwa namna gani Karim amekufa na sio Roma , au watu wameona vibaya hayo ndio yaliokuwa mawazo yake.
Juma aliendelea kuchapa kazi mpaka muda wa saa tano na hapo ndipo aliposikia simu yake inaita na kuitoa mfukoni na namba ilikuwa mpya.
“Juma!!, Najma hali yake mbaya rudi umuone mdogo wako”Juma mara baada ya kusikia sauti hii aliitambua vyema kama moja ya wanawake waliokuwa ni wapangajii katika nyumba yao na Juma hakutaka kubaki ndani ya hili soko kkwani aliondoka haraka na kurudi nyumbani.
Ni kweli mara baada ya kuingia ndani ya chumba cha Najma alimuona dada yake alivyokuwa akitoa jasho jingi , huku hali yake ikiwa mbaya , ule weupe aliokuwa nao Najma ulikuwa umebadilika na kuwa mwekundu , huku mwanadada huyu akitetemeka.
Juma hali ile ilimuogopesha na maamuzi alioyafanya haraka haraka ni kumchukua Najma na kuita bajaji kwa ajili ya kuelekea hosputalini akishirikiana na mpangaji aliempigia simu.
Ndani ya madakika kadhaa tu walikuwa washafika ndani ya hospitali ya Zakhiem na kupokelewa , huku Najma akiingizwa kwenye chumba cha daktari pamoja na Juma.
Juma alitoa maelekezo ya haraka haraka huku akiingiza maeneno mengi yasio na ukweli na kisha dokta huyo aliandika vipimo na Najma akatolewa na kuingizwa wodini .
Zilikuwa ni dakika kadhaa tu za Juma baada ya kutoa maelezo kwa dokta na kumuacha mpangaji aendelee kumwangalia Najma kutokana na yeye kutoruhusiwa kuingia wodi za wanawake , alitoka nje kabisa ya geti na wakati anatoka tu ni kama alikuwa akisubiriwa kwani , vijana wawili waliovalia mavazi ya kawaida walimsogelea.
“Oy Broo wewe ndio Juma?”
“Yes ni mimi”.
“Kuna inshu Fulani tunataka kukuuliza , ila hapa si salama tuna gari yetu upande wa pili itakuwa vyema kama tutaenda wote”Juma alifikiria kwa muda huku akiwangaalia vijana hawa na kuona hawakuwa na hatari yoyote kwake na aliona ni vyema kuongozana nao.
Gari walikuwa wameipaki upande wa kushoto mbele kabisa na ukumbi maarufu jijini Dar es salaam unaofahamika kama Dar Live , vijana wale waliisogelea gari nyeupe aina ya Toyota Corola na kisha mmoja aliingia wa kwanza na kisha akafatia juma na yule mwingine akaingia mbele.
Kitendo cha juma kuingia tu kwenye gari alishituka akiwekewa kitambaa kwenye pua zake na mtu ambaye ilionesha ni Dhahiri kabisa alikuwa ndani ya gari hili kabla ya Juma kuingia.
Baada ya ukio lile lililofanyika bila ya mtu yoyote kuona kinachoendelea hatimae gari ile ilitolewa kwa spidi kueekea upande wa kariakoo na ikawa Juma katekwa kiulaini.
****
Roma kama kawaida alifika kazini huku kwenye akili yake akiwa na mawazo ya kwenda kupoteza poteza muda kwa kucheza magemu ili arudi zake nyumbani kula na kwenda kiwanja cha bata.
“Hiii kazi nafanya kumridhisha tu Edna , ila kutokana na ugonjwa wangu sipaswi kufanya kazi ambayo inanifikirisha , lazima nijichunge”Alijiongelesha Roma wakati akiingia ndani ya ofisi yake ya kazi.
Na siku hii haikueleweka , ila Wafanya kazi walionekana kuwa bize kweli na kazi na hata Roma alishangaa kwani hata Recho ambaye alikuwa akipenda kuongea sana , alionekana kuwa bize na Zaidi ya salamu hakukuwa na Zaidi ya maongezi, ila Roma hakujali sana yeye aliendelea zake na kucheza gemu.
Muda wa chakula ulivyowadia ndio alikuwa mtu wa kwanza kuinuka kwa ajili ya kuelekea kula kitendo kilichowafanya wawafanya kazi wenzake wamwangalie , ila hakujali , kwani Roma sifa yake kubwa ni kwamba jamaa huyu mshipa wa Aibu ni kama umekatwa.
Roma baada ya kujiona ameshiba , alimkumbuka Doris sana na alitamani amuombe mchezo baadae , ila alikumbuka kuwa alikuwa amenuniwa tokea tukio la yeye kulala na waziri Neema Luwazo , hivyo hakutaka kujihangaisha kwake , aliona kama Neema atarudi kwake basi wataendelea na kama hatorudi hana haja ya kwenda kuomba msamaha na kubembeleza.
Roma baada ya kushiba alichuku maji yake ya Kilimanjaro makubwa na kisha alitoka sehemu hii ya kantini lakini ile anakata kulia ili kuingia upande ambao zipo Lift alikuja kukutana na Edna njiani akiwa na Doris , walionekana walikuwa ndio wanaelekea kula ,Doris hakuongea na Roma na hivyohivyo hata kwa Edna , alimpita Roma kama hamjui , ila kwa Roma hakujali licha ya kujisikia vibaya moyoni.
Ilikuwa ni muda wa saa kumi za jioni Roma akiwa ndani ya sehemu ya kuegeeshea magari , akilisogelea gari lake V8 , mara gari aina ya BMW M4 ya pink ilikuja kupaki pembeni yake kiasi kwamba ilitaka kumgonga.
Roma wakati akishangaa , kioo cha gari hio kilishushwa na kumuona mwanamke mrembo na huyu hakuwa mwingine bali aalikuwa ni Nasra.
“Roma naomba unisindikize mahali?”Ilisikika sauti ya mrembo huyu na Roma alimwangalia huyu mwanadada na kisha aliitikia kwa kichwa na kuingia kwenye gari ya huyu mrembo na kisha ikatolewa ndani ya jengo hili kwa spidi.
Gari hii haikwenda mbali sana , kwani ilikuja kusimama nyuma ya hospitali ya Aghakhani ,Baada ya gari hii kusimama mwanadada Nasra alishuka kwa maringo na Roma nae alishuka na mwanadada huyu alielekea upande wa Beach, chini kidogo sehemu ambao ilikuwa na miti.
“Nasra yuko wapi?”Ilikuwa ni sauti ya Roma akimwangalia mwanadada aliekuwa mbele yake , swali hilo ni kama lilikuwa la kijinga kwani mtu aliekuwa mbele ya Roma alikuwa ni Nasra , lakini sio kweli kwani baada ya Roma kuuliza swali hilo mara mwanadada yule alibadilika sura na kuwa mtu mwingine kabisa ,Alibadilika kama Jini.
Alikuwa ni mwadada wa kijapani mrefu saizi ya kati. Mwenye mwili mwembamba na ungejiuliza ni kwa namna gani mwanadada huyu aliweza kuchukua muonekano wa Nasra mfanyakazi wa kampuni ila huo wote ni uchawi wa kijapani.
“Yamata sect ! Naona wajapani mmezidi kuimarika kwenye mbinu yenu ya kichawi ya kuiba uhusika wa mtu”Aliongea Roma kwa lugha ya kijapani.
“Tunazo mbinu nyingi za kichawi Hades , ambazo ni mpya na hauzitambui”.Roma alitabasamu na kumwangalia mwanamke huyu wa kijapani akimwita Hades.
“Jina lako ni nani kabla sijakuua”Aliongea Roma.
“Jina langu ni Tanya na nipo hapa Tanzania kwa aili ya kuchukua jiwe la Kimungu(Godstone)”Roma alitabasamu na hapo hapo akakumbuka kiboksi alichokuwa amekificha kule nyumbani kwenye chumba cha mazoezi , alikumbuka pia siku ambayo alisachiwa kule nyumbani kwa Juma alikokuwa amepanga , aliweza pia kukumbuka siku ambayo anaenda ikulu na Edna kuna gari iliokuwa ikiwafatilia nyuma.
“Inaonekana mpo hapa nchini kwa muda mrefu kidogo kuliko nilivyowadhania”.
“Umepatia tupo hapa nchini kwa Zaidi ya mwezi sasa na , tumekuwa tukikufatilia kwa kila unachokifanya kila siku , lakini Master anahitaji jiwe la kimungu mapema na hataki tena tukiongeza hata siku moja hapa nchini , hivyo leo utaniambia ni wapi jiwe hilo lilipo”
“Sijui mnacho kiongelea kwani sina jiwe hilo na hata kama ningekuwa nalo nisingewapatia”
“Unajidanganya Hades, Nasra yupo mikononi mwetu na kama unataka aishi huna budi kutupatia kile tunachotaka”
Aliongea Tanya mwanadada huyu wa kijapani akimwita Roma Hades , yaani Mungu wa wafu au Mungu wa wahalifu na jina hili linatoka katika historia ya Ugiriki ya kale.
Roma alimwangalia Tanya na kuona huyu mwanadada hakuwa akitania hata kidogo , lakini licha ya hivyo hakuwa tayari kutoa Jiwe alililokuwa nalo kwani alihofia nguvu ya jiwe hilo endapo likitua kwenye mikono ya watu ambaoo sio sahihi dunia inaweza ikawa sio salama na hata mtu aliemkabidhi jiwe hilo alikuwa na maana kubwa kani aliamini kwamba Roma ndio mtu pekee ambaye ana uwezo wa kulilinda lisiwafikie wahalifu..
Roma hasira zilianza kuonekana kwenye macho yake , na kiini cha macho yake kikaanza kubadilika rangi na kuwa cha kijani , tena kijanni kilichokolea kiasi kwamba kilianza kumuogepesa mwanadada huyu wa kijapani.
“Hades ukifanya ujinga Nasra atakufa , yupo kwenye mikono yetu na sipo hapa kwa ajili ya kupigana”
“Mpaka kunileta mahali hapa ni Dhahiri upo kwa ajili ya kupigana na hata haupo hapa kwa ajili ya kupigana umevunja sharia kuu mbili nilizoweka , sipendi kutishiwa na pili sipendi mtu anaetumia watu wengine kunipata”Baada ya kusema hapo Roma kama upepo alitoweka sehemu aliokuwa amesimama na kumsogelea Tanya ,lakini ile anafika ile sehemu Tanya alipotea ghafla na hapa Roma alitabasamu.
“Kajinga sana haka kademu , kanaona kwa vijimtego vyake vya kichawi kanaweza kunizidi hakuna mchawi aliewahi kunizidi”Aliwaza Roma na kisha alifumba macho huku masikio yakiwa juu juu kama popo na hapa alionekana alikuwa akipambana kwa hisia kwani , sekunde chache tu alikuwa ashahama aliposimama na kwa spidi ya ajabu alirusha ngumi na kilichosikika ni:
“Aiii...”.Na hapa mwanamke yule alijitokeza kwa mara nyingine.
“Leo nakuua hapahapa”Aliongea Roma huku akianza kupeleka mashambulio kwa kasi , yaani kwa namna wawili hawa walivyokuwa wanapigana kama ungekuwepo eneo la tukio ungehisi upepo tu ambao sio kawaida.
Tanya aliruka hewani huku akija upande aliosimama Roma kwa spidi ya hali ya juu , na ile anamkaribia karibu alirusha kisu ambacho alimlenga nacho kwenye koo la shingo , lakini tendo hilo Roma aliliona na alichofanya ni kuruka juu na kisha akazuia kile kisu kwa mkono kiasi kwamba kikaenda kutua kwenye mchanga wa baharini , baada ya kutua Roma kwa spidi ya hali ya juu alikichukua na kumrushia Tanya , lakini mwanadada huyu alionekana mwepesi balaa kwani alijibiringisha hewani mara mbili na kupotea , lakini kwa upande wa Roma ni kama vile alitegemea kitendo hicho kwani ile Tanya anapotea alisogea upade wa kushoto na kurusha ngumi nzito na mguno wa kike wa maumivu ulisikika na Tanya alikuwa chini , ngumi ile ilionekana kumtaiti vyema , Roma hakuishia hapo tu alimsogelea na kumshika koo.
“Niambie Nasra yuko wapi kabla sijakuvunja shingo”Aliongea Roma kwa sauti kama ya Roboti , sauti ambayo ilimuogopesha Tanya lakini kabla Tanya hajavunjwa shingo mara gari nyingine ilifika na wakashuka watu wawili kwa haraka sana na kusogelea uande aliokuwepo Roma.,wote walikuwa wanaume pia wakiwa wajapani.
“Naona wenzako wamefika na hii inanirahisishia kazi , nitawaua wote hapa hapa”Aliongea Roma huku akijiandaa kumvunja shingo Tanya .
“Hades Acha usimuue tupo tayari kukupatia Nasra”Aliongea mwanaume yule wa kijapani kwa lugha ile ile ya kijapani na Roma alimwangalia na kisha kuwajibu kwa kijapani.
“Siwezi kuwaamini”.
“Nasra yupo kwenye gari , unaweza kumchukua Tanya mpaka kwenye Gari na ukithibitisha kwa kumuona Nasra tunaomba umuachie”
“Nikora niko tayari kufa , ila hakikisheni tunapata jiwe na mumpelekee Master”
“Hapana Tanya Master alitupa maagizo ya kukulinda kwa namna yoyote ile”Aliongea huyu jamaa ambaye Tanya alimwita kwa jina la Nikora.
Roma aliona afanye kama walivyokuwa wanataka na alimchukua Tanya kama mateka na kwenda nae kwenye gari , na akafungua mlango na kumuona Nasra akiwa hajitambui huku akiwa hana nguo hata moja.
Baada ya kujiridhisha , Roma alimpiga Tanya ngumi na mwanadada huyu alitoa ukulele na baada ya kuridhika Roma alimsukuma kwa nguvu na kwenda kutua kwenye mchanga wa Beach na kitendo hiki kuna baadhi ya watu waliokiona ,ila walikuwa bize na mambo yao.
Roma alitoa gari ya Nasra na kwenda kuisimamisha kwenye duka moja la nguo ,alinunua nguo za kike na kurudi nazo kwenye gari na kulitoa kurudi kwenye kampuni , baada ya kuingiza gari sehemu ya maegesho alimshika kwa kumuwekea Nasra kiganja cha mkono kwenye kifua na akashituka.
Nasra alijishangaa akiwa uchi pembeni ya Roma , alimwangalia Roma huku akionekana ni mwenyekuchanganyikiwa na kitu cha kwanza kuziba ni sehemu zake za siri , lakini Roma wala hakujali alikuwa ametabasamu tu akimwangalia mwanadada huyu anavyoona aibu.
ITAENDELEA
SEHEMU YA 21
Nasra alikuwa na aibu mno kama mwanamke , hakuwahi kuwaza atakuja kuwa uchi mbele ya Roma , alijishangaa ilikuwaje maana hakuwa ni mwenye kukumbuka kabisa , kumbukumbu zake za mwisho zilimwambia alikuwa ndani ya eneo hili la kuegeshea magari akijiandaa kwenda nyumbanni , lakini baada ya hapo hakujua nini kilitokea.
“Roma nini , kimetokea kwanini umenivua nguo?”
“Nasra mrembo ,hebu vaa kwanza hizo nguo maana unaniweka kwenye wakati mgumu”Nasra alichukua nguo zile na kisha alivaa harakaharaka , hakujali tena macho ya Roma ambayo yalikuwa yanamwangalia , alijiambia hana cha kuficha kwani mwanaume huyo alikuwa ashaona kila kitu.
“Nataka kujua nini kimetokea Roma kwanini niko hivi na nguo zangu ziko wapi?”.
“Hata mimi sijui nini kimekutokea , nimekukuta kwenye gari ukiwa hauna nguo ndio nikaenda kukununulia hizo unazoona”Alimdanganya , lakini bado Nasra hakuelewa ila alikumbuka alipopatwa na usingizi ghafla.
Nasra aliona hana haja ya kuendelea kuuliza maswali , kwani alimuona Roma kama mtu ambae hakuwa na maelezo ya ziada kwake kumfanya aelewe , lakini pia alijiona hajatumika na hilo likawa ni ahueni.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi Nasra kwa sasa nenda nyumbani”Aliongea Roma kwa kujiamini na akijiandaa kutoka , lakini alishangaa kuvutwa na Nasra na midomo yao ikagusana na Roma alijikuta akishangaa maana ilikuwa ghafla sana.
“Asante Roma”Aliongea huku akiona aibu za kike akijitoa kwa Roma , lakini Roma alitabasamu na kumvuta tena na wakaanzza kunyonyana kwa spidi.
“Twende ninapoishi Roma”Aliongea Nasra
“Poa”
Roma ndio aliekuwa ameshikilia Usukani na ndani ya madakika machache tu walikuwa ndani ya mikocheni kwa Warioba , wakiingia ndani ya Apartment.
Roma alisifia mahali anapoishi Nasra maana palionekana ni pakishua ,baada ya wawili hawa kuingia ndani walizama bafuni na kilichosikika huko ni miguno ya kimahaba.
“Roma miguu haina nguvu twende kitandani”Aliongea mwanadada huyu na Roma hakumsemesha Zaidi ya kumbeba kwa mtindo wa Nasra kumkumBatia Roma huku miguu akiwa ameipitisha kiunoni na Mtwangio wa Roma ukiwa ndani ya kinu.
“Roma nioe”Aliongea Nasra mara baada ya Roma kufikia kileleni.
“Nina mke Nasra na sina mpango wa kuoa tena”Aliongea Roma na kumfanya Nasra ahuzunike.
“Ila usijali ninaweza kuwa Zaidi ya mume kwako kama utanihitai mrembo eh”Huku akimimnya minya kalio kama Embe na kumfanya Nasra Atabasamu.
Roma alikuwa ashasahau kabisa kurudi nyumbani na wala hakuwa na mpango , walipika wakala na kupakuana na kupumzika na kupakuana tena , huku Nasra akiwa ni mwenye kupiga magoli mengi mno yasio kuwa na idadi na aliishia kujisemea moyoni kuwa katika siku zote alizofanywa siku hio kafanywa kweli na hata alivyokuwa anakaa alishindwa kubana miguu.
Roma baada ya kuamka asubuhi , alimwamsha Nasra na kisha walipiga cha Asubuhi na Roma akaoga na kisha akaondoka , alipanga arudi nyumbani kwake maana hakurudi Zaidi ya siku mbili.
Saa moja na nusu alikuwa akiingia ndani nyumbani na kupokelewa kwa ukarimu na Bi Wema lakini pia akipokelewa na jicho kali kutoka kwa Edna.
“Bebi nimerudi”Aliongea Roma huku akikaa kwenye meza kwani Edna na Bi wema walikuwa wakinywa chai asubuhi ila kwa Edna aliitikia kwa kutingisha kichwa na kuinuka.
“Bi Wema naelekea kazini sijisikii kuendelea kunywa chai leo”Aliongea Edna na kisha akaanza kupiga mwendo huku Roma akimwangalia mke wake anavyotokomea nje.
“Kwenye wanawake niliowahi kukutana nao Edna ni kiboko ya makauzu hafananii na urembo wake”Aliwaza Roma
Bi Wema licha ya kukasirishwa na kitendo cha Roma kutokurudi nyumbani mfululizo , ila hakuwa na la kusema ,aliwaacha wanandoa na ndoano zao.
Edna alionekana hakuwa sawa hata kidogo , alionekana ni mambo mengi sana aliokuwa akiyawaza katika kichwa chake, moja ya vitu ambavyo vilikuwa vikimpa wakati mgumu mwanadada huyu ni jambo ambalo amepata kulijua baada ya kuangalia kilichokuwa kwenye Flash aliokabidhiwa na mheshimiwa Senga.
Alijikuta akiingia kwenye ofisi yake baada ya kusalimianana Sekretari wake na kujibwaga kwenye kiti chake huku akionekana ni mwenye mawazo.
“Kwanini Mama hakuniambia haya ,Juhudi zake zote za kuiendesha hii kampuni kumbe yote hayo hayakuwa na maana kwake Zaidi ya kisasi alichokuwa nacho moyoni ,kwanini kanichagua kumsaidia katika kulipiza kisasi chake kupitia hii kampuni?”Aliwaza mengi mwanadada huyu na ilionekana kuna siri kubwa ambayo alikuwa ameipata kwenye ile Flashi aliokuwa amepewa na mheshimiwa Senga , Siri ambayo inamfanya kugundua kuwa mama yake ana kisasi juu ya jambo Fulani , lakini pia ilionekana kisasi hiko alishindwa kukitimiza mpaka wakati kifo kinamkuta na mtu pekee ambae alikuwa akipaswa kutimiza kisasi hiko ni yeye.
Mara nyingi sana ni ngumu kuona mzazi kumtaka mwanae kumsaidia kulipa kisasi , lakini jambo hilo lilionekana kufanywa na mama yake Edna.
“Nitajua tu nini kilitokea miaka ishirini na tano iliopita,kwa maisha alioishi mama yangu ya kufanya kazi kama hakukuwa na kesho nadhani litakuwa ni jambo kubwa sana lililotokea”Aliwaza mwanadada huyu na alionekana pia kutokujua Zaidi ni nini kilitokea miaka ishirini na tano iliopita , kitu ambacho kinamfanya mama yake kuishi nacho moyoni kiasi cha kutaka kulipa kisasi na hata aliposhindwa kumtaka mwanae kumsaidia kulipa kisasi hiko.
Wakati mwanadada huyu akiendelea kufikiria , aliingia Monicca sekretari wake na kumtaarifu kuwa kuna mgeni wake na Edna alimwambia amruhusu na alionekana Abubakari Hamadi CEO akiingia ndani ya ofisi ya huyu mwanadada.
“Karibu Mr Abubakari”Aliongea Edna akiweka sura ya kikarimu na kutoka kwenye kiti chake na kwenda kuketi kwenye masofa.
“Asante Edna”.Aliongea Abuu huku akimwangalia Edna kwanzia miguuni hadi kwenye kichwa.
“Anazidi kuwa mzuri ,roho inaniuma fala kama Roma ndio anaeufaidi huu uzuri”
“Nadhani hujaja kunikodolea macho Mr Abubakari”Aliongea Edna mara baada ya kumuona jinsi Abu anamvyokodolea macho ya kifisi.
“Hakika unazidi kuwa mrembo kila siku ninayokuona Edna, inaniuma kila siku kuona hutaki kuzielewa hisia zangu”.
“Abu nadhani unapaswa kuwa Profesheno , huu ni muda wa kazi na tunapaswa kuongelea maswala ya kazi , na isitoshe sipendi uvuke mpaka , mimi ni mume wa mtu na unavyoniambia hayo maneno ni kama kunivunjia heshima na kuniona mimi Malaya”Aliongea Edna huku akionekna ni mwenye kuwa na usiriasi wa hali ya juu na kumfanya Abu azidi kumchukia Roma moyoni.
“Nini umekipenda haswa kutoka kwa yule masikini Edna?”.
“Abu kama huna jambo la maana ambalo limekuleta hapa naomba uondoke nipo kazini”.
“Sorry Edna”Aliongea ila Edna hakujali na Abuu baada ya kumwangalia mrembo huyu alivyokasirika aliingiza mkono wake kwenye koti na kutoa bahasha na kisha alimkabidhi Edna.
Edna alichukua kile kijibahasha na kisha akakifungua na kusoma kilichoandikwa .
“Nadhani hujasahau kuwa wewe ni mmoja wa mwanachama wa Umoja wa wawafanya biashara nchini, hivyo kama ilivyokuwa tamaduni kwa kila mwaka wafanya biashara nchini hukusanyika kwa pamoja mara moja kwa mwaka, kadi hio ni ya mwaliko”
“Ndio ni ya mwaliko , lakini kuna haja gani ya Hafla hio kuwa siku ya kunipongeza kwa kupata mume , naona swala hili ni binafsi”.
“Najua unachomaanisha Edna , lakini tamaduni ni tamaduni,wanachama wanataka umtambulishe mume wako kwao , sidhani swala hili lina tatizo Edna na isitoshe wewe sio wa kwanza kufanya hivyo , hizi ni taratibu ambazo zinafanyika kila mwaka kwa wanandoa wapya katika ulingo wa biashara kufanya hivyo”Aliongea Abu.
Edna alivuta pumzi nyingi na kisha akazitoa na kuangalia tena tarehe ya kadi hio na kisha akamwangalia Abu,
“Hakuna shida , itakuwa jambo jema pia kwa wafanya biashara kumjua mume wangu”Aliongea Edna na kumfanya Abuu achukie moyoni ila alionyesha tabasamu usoni.
Hilo ndio jambo lililonileta hapa japo ni dogo , lakini nimepata nafasi ya kukuona Edna na angalau moyo wangu unaokuwazia kila siku umepata ahuieni”.
“Kama ndio hivyo basi unapaswa kwenda Abu nina kazi nyingi za kufanya”Abu hakutaka kumkera Edna , alitoka ndani ya ofisi.
“Hivi jamani mnamuonaje CEO Abu?”Aliongea Recho kwa sauti kiasi cha kumfanya Roma aliekuwa akicheza gemu atege sikio kwa umakini na kujiuliza kwanini Stori za Abu zimeingia katika maongezi ya warembo hawa.
“Namuona kama mwanaume mwenye mvuto na handsome , alie na mafanikio ya juu na msomi sidhani kama kuna mwanamke ambaye anaweza kumkataa hapa mjini”Aliongea Benadetha
“Wewe nae unajiongelesha kama umesahau kuwa Abu anateseka juu ya Edna miaka na miaka lakini ameshindwa hata kuambulia kisi”.Aliongezea mwanadada mmoja anaefahakika kwa jina la Tina huku akiendelea kujipaka poda na kuendelea kujiangalia kwenye kioo.
“Bosi wetu na ukauzu wake kuna siku tu ataingia kingi”.
“Haiwezekani labda mimi sio Roma”Aliropoka Roma na kufanya warembo hawa waliokuwa wamemsahau kama yupo wamwangalie na kisha wote wakaanza kucheka.
“Eti Roma mpenzi , kwenye maisha yako wewe ni jambo gani kubwa ulilokamilisha?”Aliuliza Recho na kuwafanya wadada hawa wote wamwangalie.
“Hii ndio hasara ya kufanya kazi na wanawake tu , angalia wote wanavyoniangalia , inabidi niwatembezee bakora za kimkakati waache kuniangalia kwa dharau”
“Kusema ukweli sina nilichokamilisha katika maisha yangu , mimi kila kitu natumia cha mke wangu gari kanipa mke wangu , nguo mke wangu”
Waliangaliana na kisha wote wakacheka ,lakini walikuja kunyamazishwa mara baada ya mrembo Nasra kuingia ndani ya ofisi hii, alikuwa ameshika mkononi juisi na alienda nayo mpaka kwenye meza ya Roma na kuiweka.
“Roma nimekuja kuna jambo Nataka unisaidie , sina mwingine wa kunisaidia na wewe pekee ndio mwanaume hapa ndani”
“Niambie ni jambo gani hilo Mrembo,Mimi ni nani hata nisikusadie mwanamke mzuri kama wewe”Aliongea huku akimkonyeza na Nasra kuona aibu za kike huku akikUmbuka namna ambavyo amekunjwa jana yake na mpaka wakati huo mbususu bado haijapoa na kuona aibu zaidi.
“Utaona tukifika , ila ni nje ya hapa”Aliongea mwanadada huyu na Roma akaona itakuwa vyema akinyoosha nyoosha mwili , maana hakuwa na kazi Zaidi ya kucheza magemu.
Roma alimkonyeza Recho aliekuwa akiwashangaa wawili hao namna wanavyoongea tofauti na siku zote na kuhisi kuna kitu kinachoendelea.
“Nina wasiwasi na Roma hajamtia kweli Doris na Nasra huyu?”
Aliwaza Recho huku akikumbuka ile skendo ya waziri Neema Luwazo , licha ya kuona picha ile iliokuwa ikifanana na Roma akili yake ilikataa katakata kama mtu yule ni Roma ,na sio yeye tu hata wafanya kazi wenzake walivyokaa kikao na kujadilina swala hilo walifikia maamuzi kwamba yule bwana hakuwa Roma , maana walikuwa wakimjua vyema Neema alikuwa Mzuri na wa hadhi ya juu.
Laiti wangejua kuwa Roma alimfanya huyo mwanamke mpaka akayaita maji ‘mma’ wasiongekuwa na mawazo ya kejeli ya namna hio.
*****
Upande mwingine ndani ya jengo refu la PSSF flour namba kumi na moja , walionekana wafanyakazi wa juu wa MapleGroup(Top executive officers) wakiwa wamezunguka meza kubwa wadada na wanaume wakiwa na tarakishi zao za kimapakato za bei ya juu , wakiwa wamekaa kulia na kushoto , huku mwisho wa meza alionekana mwanadada mrembo akiwa ameketi huku wafanya kazi hawa waliovalia suti kumwangalia kwa kutamani kuketi kwenye kiti alichokalia , ndani hapa kulionekana kukiwa na kikao kilichokuwa kikiendelea.
“Kama nilivyokwisha kutangulia kusema kwamba kwa sasa Hoteli za kampuni yetu zimezidi kuwa maaufu sana hapa nchini na nje ya nchi kutokana na ubora wa huduma zake , lakini licha ya umaarufu huo mapato yanaonekana bado hayajaongezeka kwa kiasi kikubwa nje ya malengo ya mwaka hun ya kampuni , hivyo kwa utafiti niliofanya nimekuja na hitimisho ambalo litaipelekea kamapuni kuongeza mapato katika upande wa hoteli na hitimisho hilo ni kufungua hoteli za nyota tatu nyingi Zaidi nchini , katika maeneo ambayo yanatembelewa sana na watalii kama Lushoto ,Iringa ,Kahama na kwingineko”Aliongea bwana mmoja hivi mweupe aliekuwa amevalia miwani huku akiwa na suti yake ya Kaunda ya bei mbaya , bwana huyu alionekana alikuwa akielezea namna ya kuinua mapato ya kampuni hii ya Maple Group.
Baada ya kijana huyu kukoma kuongea , alimgeukia mwanamke ambaye alikuwa kiongozi wa kampuni hii , lakini mwanamke huyo mrembo alionekana kuwa mbali kimawazo na hata wafanya kazi hawa walimshangaa bosi wao, kwani hawakuwa wamemzoea kuwa katika hali kama hio , walimjua kama moja ya wanawake wachapakazi.
“Mheshimiwa?”Aliita kijana huyu na kumshitua mwanamke huyu mrembo na kumwangalia kijana aliekuwa mbele yake.
“Alhaji naamini katika mipango yako , hivyo endelea na huo mpango ila naomba uniwekee mpango huo katika maandishi na umpe Grace auingize katika kashabrasha langu”
“Sawa Bosi”Aliongea Alhaji na kisha mwanamke huyu aliondoka , huku akiwaacha wafanya kazi wakimpigia Alhaji makofi kwani waliliridhishwa na wazo lake.
“Grace fanya maandalizi , kesho nataka kurejea Dodoma kwa ajili ya vikao vinavyoendelea Bungeni”Naama huyu ni mrembo Neema pisi ya Mheshimiwa Kigombola.
Neema mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake kubwa ndanni ya jengo hili , aliketi na kisha akazungusha kiti na kuangalia mandhari ya jiji huku akionekana ni mwenye kufikiria jambo.
“Yule mwanaume sijui nampataje tena , Kila ninapofumba macho kumbukumbu zangu zinanirudisha siku ile akiniingiza dudu lake,ni hisia ambazo sijawahi kuexperience kwenye maisha yangu,Natamani kumtafuta kwani nina uwezo huo , lakini ngoja niache, kama Mungu akitukutanisha tena naapa kwa majina yote ya mbingu na ardhi simuachii hata kama ni mume wa mtu nitakuwa mchepuko wake grade A”Aliwaza Neema Luwazo Naibu waziri huyu mrembo wa Sanaa.
Wakati akiendelea kufikiria mara simu yake kubwa ya Iphone ilianza kuita na kuangalia jina na lilisomeka ‘Mchomvu”.
“Huyu kizee nae msumbufu kweli, na kitumbua changu atakisikia kwenye bomba”Aliongea Waziri huyu huku akiangalia simu inayoita mpaka pale ilipokatika na ikaanza kuita tena ndipo alipo ipokea huku akikunja uso.
*****
Roma na Nasra walikua kusimamisha gari nje ya jengo la Zera Complex Mtongani kwa Azizi Ally.
“Tumekuja kufanya niini hapa Nasra?”
“Ndani ya hilo jengo kuna kampuni ya ulinzi inayofahamika kwa jina la PANZI ,miaka minne nyuma walikuja kukopa kwenye kampuni yetu kiasi cha shilingia bilioni mbili kwa makubaliano ya kurejesha baada ya miaka miwili , lakini mpaka sasa hawajarejesha na hawana mpango huo,hii ndio kazi yako ya kwanza ambayo unatakiwa kuifanya kwa kampuni , hivyo hakikisha pesa tunazowadai wanarudisha, yangu ni hayo tu mimi naelekea Mbagala kuna mteja namfatilia”Aliongea Nasra huku akitabasamu akimwangalia Roma.
“Sasa kama nyie mliowakopesha mmeshindwa mimi nitawezaje , na kwanini msitumie sheria kudai haki ya kampuni?”.
“Hilo limeshindikana Roma kuna kiongozi wa kisiasa anawakingia kifua sana na wanadai mkataba tuliowasainisha ni batili ,hivyo kwakuwa umekuwa ni wa kucheza gemu kila siku angalau fanya jambo kwa kampuni sio unakula mshahara tu kama kampuni ni ya mkeo”
Roma alishuka kwenye gari ya Nasra na kuliangalia jengo hili , na kuanza kutembea mdogo mdogo kuelekea mlangoni.
Nasra kwenye gari alionekana ni mwenye kuwaza hapa na pale , huku akikanyaga pedeli .
“Sijui Edna kawaza nini mpaka kuniambia nimpe kazi ile Roma , si watamuua yule mwanaume maana kwa ninavyojua ile kampuni kwanzia Bosi mpaka wafanya kazi wote ni wavuta bangi na wamepinda ni hatari na hata siui imekuwaje wakajiita kampuni ya Ulinzi , ingekuwa Japani au Korea wangeitwa ‘Gang’ au ‘Mafia’.”Aliwaza mrembo huyu.
Ukweli ni kwamba Edna alikuwa ni mwenye kuwaza hili na lile baada ya kuletewa mwaliko wa kuhudhuria mkusanyiko wa kibiashara unaowakutanisha wafanya biashara wakubwa ndani ya Taifa hili,kwa mkutano huo hili la kuhudhuria kwake lilikuwa la kawaida na halikumuogopesha wala kumtia mawazo kwani pia alipenda mkusanyiko huo kwani huleta fursa ya kujenga koneksheni na wafanya biashara wengine , tatizo kubwa lililokuwa likimfikirisha mrembo huyu , ni juu ya Roma , hakuwa tayari kumtambulisha Roma kwa wafanyabiashara wenzake kama mume.
Kwanza hakumpenda Roma kwasasabu hata ongea yake ilikuwa sio ya kiprofesheno na kuonesha kuwa ya kustaarabika , pili hakuwa na aibu hata kidogo na anafanya mambo bila kufikiria na kutojali chochote , kaliba ambayo mwanmke huyu membo hakuwa akiipenda kwani yeye alikuwa amestaarabika sana lakini kwa Roma hakuwa amestaarabika ,mambo yake alikuwa akifanya kimasikini masikini.lakini pia mwanadada huyu alikuwa akiujua kuwa kualikwa kwake kuhudhuria na Roma ni kama mtego , aliamini Abu kafanya hivyo kwa ajili ya kumkosoa Roma mbele ya wafanyabiashara hawa wakubwa na wenye heshima ili kumfanya Roma ajione kapuku lakini pia na yeye kuonekana kuchagua mtu ambae hakuwa wa hadhi yake .
Hii ni sawa kabisa katika ulimwengu wa kitajiri , matajiri hupenda kuoana na matajiri wenzao hivyo sio swala la kushanganza kwa mwanamke mrembo kama Edna kufikiria swala hilo.
Wakati Edna akiwa anawaza , aliinua mkonga wake w na kumuita Sekretari Monika na kumpa maagizo kuwa anamhitaji Mhasibu ofisini kwake na baada ya madakika kadhaa Nasra aliingia hapa ofisini.
“Ndio bosi”
“Nasra hivi PANZI walisemaje kuhusu hela tunayowadai?”
“Wanasema hawatorudisha na tukituma mtu kwenda kuwadai ,atarudi hana vidole”
“Mpe hio kazi Roma aifatilie”Nasra alishangaa
“Lakini bosi Roma hatoweza maana PANZI ni wajeuri sana ,na Roma anaweza kupata matatizo , maana ile siku walitupa onyo kama tukituma mtu kudai hela basi atarudi hana vidole”
“Fanya kama nilivyokuambia Nasra na akifanikisha hilo milioni mia ni yake”Aliongea Edna na kisha alichukua kitabu chake cha kingereza kilichosomeka uu ‘HOW TO LIVE WITH PERSON YOU DISLIKE’ yaani kwa tafsiri ya ‘JINSI YA KUISHI NA MTU USIEMPENDA’
“Ukijikuta katika nafasi ambayo huna chaguzi Zaidi ya kuishi na mtu usiempenda , hakikisha unafanya haya .kwanza kabisa kuwa na uhakika wa hisia zako za chuki zidi ya mtu huyo na andika chini kabisa sababu hizo ambazo zinakufanya umchukie sana huyo mtu , hii itakusaidia kujiwekea mipaka na mtu huyo ….”
Ni baadhi tu ya maelezo yaliokuwa yapo katika kitabu hiko Edna alichokuwa anasoma.
Upande wa Nasra hakujua kwanini bosi wake kaamua kumpa kazi hio ya hatari Roma .
“Na lile dudu lake lililivyokuwa kubwa , sijui kama akirudi litakuwa linafanya kazi”Aliwaza Nasra wakati akiingia hospitali ya Zakhem. Mbagala.
WEAKEND NJEMA WAKUU ,ITAENDELEA KUNAKO MAJALIWA
TOA SAPOTI YAKO KWA KULIPIA ANGALAU 2000 ILI NI KUUNGE GRUPU AU NIKUTUMIE INBOX NAMBA ZA MALIPO NI 0687151346 JINA ISSAI SINGANO AU TIGOPESA 0657195492 UKISHALIPA NICHEKI WATSAPP NA MESEJI YA MUAMALA NAMBA 0687151346