Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 51

Upande wa Chini kabisa ndani ya Mashua, kwa nje kabisa alikuwa amesimama mzee mmoja hivi aliekuwa ameshikilia panga lake Refu akiwa anaangalia Chopa iliokuwa hewani , mzee huyu alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , alikuwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya kichina huku akiwa na kipara chake, alikuwa na macho flani hivi ya kutisha kama ana makengeza na mboni za macho hazikuonekana ni rahisi kusema anajicho lisilokuwana kiini cheusi..

Ndani ya mashua hio walionekana vijana wanne hivi wote wakorea waliokuwa wameketi kwenye visturi huku wakinywa kilevi ambacho kilikuwa kikifanana na ulanzi , huku pembeni yake kukiwa na Sanamu Varicana ambalo walikuwa wamelifunika na nguo.

Upande wa kushoto ndani ya mashua hii kulikuwa na maboksi flani ya mbao , kama yale ya kuhifadhia Nyanya wakati wa kuzisafirisha kutoka shambani , chakushangaza ni kwamba maboksi hayo yalikuwa yakitingishika na nikama kulikuwa na mnyama ndani ya maboksi hayo na watu hawa hawakuwa wakijali sana kutingishika kwa maboksi waliendelea kunywa kwa furaha huku wakiongea , lakini muda huohuo ndio walipoanza kusikia mngurumo wa Chopa na wote kwa pamoja walikurupuka na kubeba Bunduki zao na kutoka nje haraka na walimkuta kama kawaida Tzeng akiwa anaingalia ile chopa huku akionekana ni mwenye kukata tamaa , ni kama mtu ambaye alikuwa akisubiria kitu kikubwa Zaidi na hakijatokea.

“Master Tzeng”Aliita kijana mmoja wa kikorea huku akimwangalia Monk kwa wasiwasi.

“Mtu ninaemsubiria hayupo kwenye hio chopa , naona wale makafir wamenidanganya,imenikatisha moyo , walitaka kunitumia tu kukamilisha mambo yao ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng.

“Master lakini haujatuambia unaemsubiria kila siku umekuwa wakutuambia kuna mtu unaemsubiria”.

“Unafikiri kwa miaka yangu yote niliohudumu kusalia Budha ninaweza kuisaliti huduma yangu kuja kuiba sanamu,Nimewakubalia Dhoruba Nyekundu kuiba hilo sanamu kwasababu wamenihakikishia nitapata nafasi ya kupambana na Hades ,Inasikitisha sana”

“Master Hades ni nani?”

“Huna haja ya kumjua , kwangu ni mtu ambaye natamani kuupima uwezo wangu wa kimapigano kwa kupambana nae , lakini nimekatishwa tamaa na kutoonekana kwake, nahisi sitoweza kuufamu uwezo wangu wa kimapigano mpaka nakufa inasiikitisha sana”.

Upande wa Chopa kule juu wakati wakiendelea kushangaa chini baharini kama watamuona Roma , Mara walijikuta wakianza kushambuliwa kwa mbele.

“Sh**t Ni ni kikosi cha watu wa Dhoruba Nyekundu washafika, Kapteni kuwa makini wasiharibu chombo”.

“Pumbavu tulishindwaje kuwagundua wamekaribia? , Boti yao ile”

“Sio Boti wewe mpuuzi , ile ni SubMarine(Manuari)”Aliongea Kobota akimrekebisha Mbwa Mwitu , lakini wakati huohuo lilirushwa kombola na ilibakia kidogo tu ligonge Chopa yao na Rubani alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani aliipindisha Ndege na kugeuza kushoto, mashambulizi yalikuwa makali sana na watu wa Dhoruba Nyekundu walionekana kudhamiria kuidondosha kabisa hio chopa.

“Bang .. Bang !!”Ni milio ya risasi iliokuwa ikigonga chopa huku na waliokuwa kwenye ndege wakirusha Risasi.

“Hawa wajamaa wanateknolojia kubwa ndio maana ndege yetu imeshindwa kuwanasa kwenye Radar, tusipokuwa makini hii misheni itafeli”Aliongea Rubani msaidizi kwa kijapani.

“Sema Pluto naamini ashakufa mpaka sasa , niliwaambia hana lolote yule, na nimeshangaaa kumuhusisha kwenye hii misheni”Aliongea Kibonge huku akimdharau Hades na hio ni kutokana zimepita Zaidi ya dakika tano bila ya kumshuhudia Roma.

“Mother***ker!”

Rubani alijikuta akitoa tusi mara baada ya kurushiwa Kombora kiasi kwamba Chopa ilianza kutoa mlio wa Alarm lakini ile anataka kulikwepa kwenda kulia , wa kwanza kuruka alikuwa ni kibonge , alionekana kuwa shapu na akafatia Kobota na Mbwa mwitu na hapohapo ulisikika mlio wa ‘BOOM’ Chopa ilikuwa imelipuka ikiwa na Sunami na Rubani msaidizi Jani ,na wengine , ulikuwa ni mlipuko mkubwa uliosababisha mwanga kutawala kwa sekunde kadhaa mpaka kufifia huku mabaki ya ndege yakidondokea baharini.

“Haya yote hayana maana ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng baada ya kuona mlipuko wa ndege , lakini ile anageuka tu Roma alietoka kwenye maji kama samaki jamii ya Dolphin ,kama mshale huku akijilenga kwa Tzeng , lakini Tzeng alikuwa mwepesi mno kwani aliinama chini kama mti ambao umepindishwa na kichwa kugusa chini huku miguu haijasogea hata kidogo , yaani ni kama mti ulikuwa umechomekwa kwenye shimo na ukapindishwa na Roma akapita na kumvaa kijana aliekuwa akiuliza maswali na akaenda kudondokea baharini .

“Amitabha.. Hades”Aliongea Mzee huku akikunja mikono miwili , alionekana kushukuru ujio wa Hades.

“Inashangaza kuona Monk kuwa mwizi”Aliongea Roma.

“Kuna Muda inapaswa kuwa hivyo , kama unania ya kutimiza dhumuni kuu kwenye maisha yangu”Aliongea huku wale Wakorea wakiwa wamemzingira na Bunduki zao ila Roma hakuwa ni mwenye kuwajali.

Wakati huo huo ile Submarine(Manuari) ilikuwa ishafika usawa wa mashua na walikuwa wakimshuhudia Tzeng na Roma waliokuwa wakiangaliana.

“Jason ni Hades , inapaswa kuchukua Sanamu tuondoke wakati akiendelea kupambana na Tzeng”

“Jessy tulia kwanza tuone mtanange , tukiona dalili za kushindwa kwa Tzeng tunakimbia ”Aliongea Jason wakati huu chombo chao kikiwa

Upande wa Kibonge alionekana kusalimika hukuu akiogelea upande wa ilipokuwa mashua ,aliangalia nyuma na kuwaona wenzake pia wanatapatapa kwenye maji.

“Okey!Tzeng nataka nikamuokoe mpenzi wangu,kwasababu umeshindwa kutumikia Budha na kugeukia njia Ovu nikikuua nitakuwa nimefanya jambo la kiimani kwa Mungu wa Budha”Aliongea Roma.

“Bothisativa Sabejatha” Alitamka Tzeng huku akimnsogelea Roma akiwa amenyoosha upanga wake , akilenga tumbo na Roma hakuondoka alipokuwa amesimama na ile Tzeng anafika Roma alisogea kidogo na Upanga ukapita kwenye kwapa , lakini Tzeng alionekana kutumia nguvu isiokuwa ya kawaida , kwani alimsukuma Roma na wote walitumbukia kwenye maji huku wakiwa katika staili kama ya kukumbatina ,Tzeng baada ya kutua kwenye maji mita kadhaa chini kabisa , alimsukuma Roma na kujitoa kwake na kisha akaleta tena pigo huko akizungusha upanga wake kwa spidi kiasi kwamba ulikuwa ukionekana kama sinndano na ile anamfikia Roma kwa nia ya kumchoma Roma aliuzuia na viganja vya mikono kwa kuubana , kitendo ambacho kilimfanya Tzeng kuuvuta ila Alishindwa na kujikuta akishangaa ni uwezo gani wa nguvu za mikono za Roma, lakini ile anashangaa Roma aliruka sarakasi na miguu ikawa juu na mikono ikiwa chini imeshikilia lile panga na kisha akazunguka kama Pia kitendo kilichomfaya Tzeng kukosa mhimili wa kushikilia lile Panga,Baada ya Tzeng kuona Roma anazunguka na yeye alizunguka vilevile kwa spidi kiasi kwamba Jason ,Jessie ,Kibonge na wenzake kushangazwa na Wimbi lililojitengeneza juu sehemu ambayo wametumbukia.

****

ATLANTIC OCEAN-ISLAND X

PROJECT LADO MONITORING CENRE(PLMC)​

Ni ndani ya kisiwa ambacho kilipewa jina la Kisiwa X,kisiwa hiki kilipewa jina hilo kutokana na kwamba kimetolewa kwenye Ramani , yaani ni kisiwa , lakini kwenye Ramani ya dunia hakionekani na ndio maana kikapewa jina la Kisiwa X.ni kisiwa ambacho kipo kwenye bahari ya Antlantic.

Ni sehemu ambayo ina ulinzi mkubwa sana kiasi kwamba kama upo habarini kilomita 60 kutoka ndani ya kisiwa hiki utaona mkanda mkubwa wenye maandishi ya DON’T GET CLOSER ,IT`S DANGEROUS yalioandikwa kwa Rangi nyekundu kuzunguka eneo lote la kisiwa ,ni sehemu ambayo inabaridi kali sana na mkondo mkubwa wa maji na ni mara nyingi kuona meli zinapita karibu na eneo hilo na kama itatokea mtu akifika kwenye eneo hilo ni ngumu sana kutoka hai.

Ndani ya eneo hili la kisiwa kuna jengo ambalo kwa juu linaonekana kama kibakuli kilichofunikwa, na jengo hilo lina rangi nyeupe huku pembezoni mwa jengo hili kukiwa na Bendera zinazopepea za mataifa ishirini yenye nguvu, ambazo zimepangiliwa kwa umbali sawia kiasi kwamba zilifanya jengo hilo kupendeza.

Basi ndani kabisa ya jengo hili ndani ya hiki kisiwa , walionekana watu wanaume na wanawake walio na utofauti wa umri ,yaani kuna wale ambao walionekana kuwa na miaka hamsini na kuna wale ambao walikuwa na miaka Therathini kimakadirio , hapo ndani hapakuonekana mtu ambae yuko chini ya miaka ishirini.

Watu hawa wote walikuwa wamevalia tisheti za rangi ya Bluu huku kila mmoja ikiwa na chata la ‘O’ na jicho katikati ambalo limenakishiwa kwa rangi nyekundu, halafu chini ya tisheti hio kuna maneno yanayosomeka Zero`s Organisation.

Ni jengo ambalo kwa ndani lilikuwa limejengwa kitaalamu sana , jengo hili lilikuwa limetenganishwa mara mbili upande wa kulia kuna vyumba ambavyo vimejengewa kwa mfumo wa nusu duara , lakini pia kwa upande mwingine kuna vyumba ambavyo vimejengwa kwa mfumo wa nusu duara huku katikati pakiachwa wazi huku juu yake kukiwa na paa ambalo lilikuwa likipitisha mwanga na matundu ambavyo yametengenezwa kwa muundo wa nyota.

Ukiachana na hili jingo kwa pembeni yaani nje kabisa kulikuwa kumejengewa pia nyumba ambazo zilikuwa kwenye muundo tofauti tofauti ,zilizofanya eneo hili kupendeza sana ukijumlisha na bustani zilizokuwa zimetenezwa kwa muundo wa kuvutia.

Sasa ndani ya hili jengo kuna Idara inayofahamika kwa jina la PLMC(PROJECT LADO MONITORING CENTER), ndani ya hii idara walionekana jumla ya watu kumi na mbili , watano wanawake na saba wanaume wenye umri tofautt tofatui , ndani ya hii idara mbele kabisa kuna ukuta mkubwa ulionjengwa huku ukiwa na skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionesha eneo la baharini , lakini ajabu ni kwamba mazingira yanayoonekana ndani ya hili eneo ni yale yale ambayo Roma na Tzeng wakipigana.

“Unafikiri Agent 13 atashinda Carlos?”Aliuliza mwanamke mmoja wa kizungu makadirio ya miaka hamsini hivi kupanda ambaye alikuwa akila Popcon zake zilizokuwa kwenye kopo bila habari huku akiangalia mpambano kati ya Roma na Tzeng , mwanamama huyu alikuwa amekaa huku pembeni yake kulikuwa na bwana mmoja mweusi kijana, akiwa amekaa pamoja na mwanamama anaekula Popcorn huku nyuma yao wakionekana wenzao ambao wamesimama wakiwa wanangalia mtanange huo , kwa jisi walivyo makini ni kama walikuwa kwenye ukumbi wa sinema wanaangalia muvi.

“Sina mashaka na Agent 13 Dyana, Tzeng ni mtu ambaye ana mafunzo ya juu na ndio maana tukamchagua kupambana na Agent 13 lakini haimaanishi kama anaweza kushinda ni uwekezaji mkubwa na maarifa yaliofanyika kumtengeneza Agent 13 na hatakiwi kushindwa na Tzeng”Aliongea bwana huyu aliefahamika kwa jina la Carlos huku akirudisha umakini wake kwenye pambano.

“Sema Agent 13 tokea Agent 17 kufariki , ukatili wake umepungua kwa asilimia mia moja ,nadhani mpango wa kumuua Agent 17 ulikuwa bora sana”Aliongea mwanamama huyu lakini bwana Carlos hakujibu.
 
SEHEMU YA 52​

Ilikuwa ni kama kimbunga Jobo kilichokuwa kimejitengeneza ndani ya hili eneo kiasi kwamba ile mashua na Manuari pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Dragoni walisukumwa mbali.

“Ni nguvu gani hii?”Aliongea Kibonge huku akiendelea kushangaa , kilichowashangaza Zaidi ni kwamba zilipita dakika kumi pasipo ya Roma na Tzeng kuonekana juu ya maji , ikimaanisha kwamba walikuwa wakipigana chini ya maji.

“Mbwa Mwitu kimbia..!”Aliongea Kobota baada ya kuona tukio la kutisha na hio ni mara baada ya eneo wanalopigana Tzeng maji yake kutengeneza barafu kwa spidi kiasi kwamba sehemu waliokuwa wamesima Kobota kuhisi ubaridi wa hali ya juu sana na maji yalikuwa yakigana kuelekea upande wao na kuwafanya waogelee kwenda kusimama mbali.

“What is happening?”Aliuliza Jessie kwa mshangao baada ya duara la Barafu kujitengeneza .

“That is Hades Jessie , I told you we have to stay here to enjoy this live show”A;iongea Jason akiwa amekalia ukingo wa Manuari yao ambao ilikuwa imefungua ufuniko kwa juu , licha ya kwamba walikuwa wakisikia barindi kali lakini hawakutaka kuondoka , walitaka waone mpaka mwisho wake.

Wakati wakiendelea kuongea Ghafla katikati ya lile barafu paliachia mpasuko wa nguvu kiasi kwamba kurusha vipande vya mabarafu juu na Tzeng Alionekana akichomoka kama mshale lakini wakati huo huo Hades na yeye alitokea , lakini sasa muonekano wa Roma uliwafanya kila mtu kushangaa…

“It`s yellow Glows not what I wanted to experience Jessie ,Tzeng is Disapointing”Aliongea Jason na kumfanya Jesie ashangae.

“What do you mean?”

“When his eyes emit Yellow glows mean he is using half of his power , I need to see red glows Come on Tzeng” Jesie alizidi kushangaa,huku Jason akionesha kutofurahishwa na uwezo wa Tzeng kwani alitegemea kuona macho ya Roma yakitoa mwanga mwekundu.

Roma Macho yake sasa hayakuwa ya kijani tena kama alivyokuwa amezeleka hapa macho yake yalikuwa ya njano huku yakitoa miale flani hivi kama mwanga wa jua lakini usio kuwa mwingi, kiasi kwamba haukuwa ukisambaa , na kutokana na eneo hili kuwa na giza alionekana vyema.

“Tzeng huna uwezo wa kunishinda , ikibidi kimbia kabla sijakufanya ukose hewa ya oksijeni”

Aliongea Roma kwa sauti nzito kama Roboti kiasi kwamba watu waliisikia mara mbili kwenye masikio yao kwani ilikuwa na mwangwi, huku Tzeng akionesha wasiwasi wake , ukweli ni kwamba Tzeng aliponea chupuchupi chini ya maji, kwani wakati wakiendelea kupigana Macho ya Roma yalikuwa yakitoa miale ya kijani kiasi kwamba bwana huyu aliogopa kubakia chini ya maji na akataka akimbie , lakini ni kama Roma alijua mawazo yake , kwani alikimbia juu yake na kisha kujikakamua kama mtu ambaye anataka kulazimisha ushuzi na hapohapo na mwili wake ulibadilika Rangi nangi na kuwa kama sanamu ambalo limejengwa kwa barafu huku likimomonyoka kama unga kwa spidi kubwa kiasi kwamba eneo la juu ndio lilianza kutengeneza barafu na hapa ndipo alipoweza kujua kuwa mtu ambae alikuwa akipambana nae hakuwa wa kawaida , yeye katika kusikia kwake kuhusu stori za Hades ni kwamba alikuwa na uwezo wa hali ya juu wa ‘Martial Art’ pamoa na mbinu za kichawi za kichina Lakini hakuwahi kuwaza kama anaweza kugandisha maji.

“Shi*t he is using power to control Density , I can’t Move”Aliwaza Tzeng huku akiwa amejawa na kiwewe.

Sasa kile kitendo ch Hades kugandisha maji kwa juu kilimfaya ashindwe kutoka juu na pia Pumzi ilikuwa ikimuishia na aliona akizembea anakufa kizembe na hapo ndipo alipoamua kutumia uchawi wake ambao ulimuongezea nguvu kiasi kwamba alikuwa akisukumwa kutoka chini kwenda juu kwa spidi ya hali ya juu na kuweza kutoboa barafu na upanga wake na kutokezea nje.

“Hapa inabidi nikimbie , huyu sio mtu wa kawaida nitakufa ,Ngoa nikajipange upya nitaomba mpambano tena”.Aliwaza Tzeng wakati akiwa amesimama kwenye barafu iliotengenezwa na Hades huku ikielea juu juu.

“Hades tutakutana tena ngoja nikajipange upya”Aliongea Tzeng na palepale aliposimama pakajitengeneza vitu kama majivu na vikapelerushwa na upepo kuelekea magharibi.

Baada ya Tzeng kukimbia Roma mwili wake ulianza kurudi katika hali ya kawaida , lakini sasa nguo zake zote zilikuwa zimechania yaani zilijiachia kama unga na kubakiwa uchi.

Jasona baada ya kuona Tzeng kashindwa pambano waliona hapo sio mahala pake kukaa ,kwani wote waliingia kwenye manuari na ikaanza kuzama chini na kukimbia.

“Jason , hatujachukua sanamu”Aliongea Jesie.

“Sanamu la nini?”

“Kwani tumekuja kufanya nini?”

“Jesie acha kuwa na kichwa kigumu , unafikiri tumekuja kuiba sanamu ambalo halina thamani kwetu”

“Kwa hio tumekuja kufanya nini?”

“Kurusha pambano live , ndio ilikuwa misheni yetu Jesie”Aliongea Jason

Kibonge hakutaka kabisa hata kumsogelea Roma , kwa matukio ambayo alikuwa ameyashuhudia kwa macho yake ni kama alikuwa kwenye ndoto ,alimwangalia Roma ambaye alikuwa amesimama kwenye mashua hii akiwa uchi sehemu ambayo alikuwa amesimama Tzeng kabla ya pambano lao.

Wale wakorea ambao walikuwa wapo pamoja na Tzeng baada ya kumuona Master wao kakimbia na wao walijirusha majini bila kujiuliza mara mbilimbili , mziki walioushuhudia kutoka kwa Roma waliziambia nafsi zao ni heli kujaribu kufia kwenye maji kuliko kuliko kukutana na adhabu ya shetani aliekuwa mbele yao..

Roma licha ya kwamba eneo hili la baharini kuwa na baridi kali kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida ambaye hajazoea baridi anaweza kuzimia , lakini kwa Roma ni kama alikuwa amevaa nguo.

Mbwa mwitu alikuwa amesimama nyuma yake , kwenye boti , huku akimwangalia Roma kwa wasiwasi mwingi , kila akifikiria tukio ambalo limetokea dakika chache zilizopita , hakuwa akiamini kama mtu ambae amesimama mbele yake ndio alieweza kufanya yote hayo , zile dharau alizokuwa nazo zilikuwa zishaisha na sasa kilichokuwa kimebaki kwenye akili yake ni woga na hali ya kutokujiamini kila anapomuangalia Roma.

“Nilikuwa nikizisikia habari za Hades lakini sikuwa nikijua uwezo wake upo hivi”Aliongea Kobota mara baada ya kumsogelea Mbwa mwitu , muda huu wote wakiwa ndani ya boti hii.

“Nimeshaangazwa sana na kilichotokea dakika chache zilizopita Kobota huyu sio mtu”

“Kwani nani kasema ni mtu , wewe hujamsikia kampteni anamwita Mungu wa wafu?”

“Nilijua ni jina tu Kobota kama mimi ninavyoitwa Mbwa Mwitu”.

Kobota alitabasamu na bila kungea chochote alimgonga gonga begani Mbwa mwitu kama kitendo cha kumfariji na kisha akarudi ndani.

Baada ya Roma kusimama muda mrefu akiwa uchi aligeuka na kuanza kutembea na kuingia ndani ya chumba cha boti hii , huku akidhamiria kutafuta nguo kwa ajili ya kujisitiri.

Licha ya kutafuta kwakuchangua maboksi yaliokuwa kwenye hii boti hakuambulia chochote Zaidi ya kuona vitu ambavyo wale wakorea wameviiba,ni vitu ambavyo vilikuwa na thamani kwani kulikuwa na baadhi ya vifaa vya udongo ambavyo alipovichunguza kuna vilivyokuwa ni vya miaka mingi,ikiwemo uwepo wa ‘Porcelain’ ya ‘Song Dynastry’ na makolo kolo mengine

Roma baada ya kuona amekosa alirudi na kuungana na Kobota na Mbwa Mwitu waliokuwa wamekaa sehemu ile ile ambayo wale wakorea waikuwa wakinywa na kuongea , lakini kabla hajakaa chini kuna kitu kilimvutia, yalikuwa ni maboksi ya mbao mawili.

Aliyasogelea na kuanza kuyasukuma kwa mguu lakini yalikuwa mazito, Kobota na wenzake walikuwa wakimwangalia Roma kwani hata wao waliona hayo maboksi lakini hawakua na habari nayo , ni kama watu ambao walikuwa wamekosa na hamu ya kila kitu kutokana na kuponea chupuchupu kwenye kudunguliwa na ile Chopa na sasa walikuwa wakifikiria kurudi nchi kavu tu.

Roma baada ya kuona maboksi haya kuwa mazito , alibeba moja na kuligeuza kwa juu na kisha akafyatua kimlango ambacho kilikuwa kimegongelewa na chuma na hapo ndipo alipojikuta akishangaa , kwani ile anafungua tu boksi ,ulitokea mkono uliokuwa kwenye hali ya ulegevu na hapo ndipo alipojua kuwa ndani ya hayo maboksi kuna watu amba wamefungiwa.

Hata Kobota na wenzake walishangazwa na jambo hilo na walisimama na kumsogelea Roma.

Walikuwa ni wasichana wawili mmoja Mjapani na mwingine alikuwa ni muafrika kutokana na ngozi yake ,wasichana hawa walionekana kuzimia kutokana na baridi kali na kuelekea mpaka midomo yao kupasuka pasuka na kutengeneza nyufa.

“Wamepoteza fahamu , wanaonekana kuwa hai”Aliongea Roma kwa kijapani na kufanya Kobota na mbwa mwitu waangaliane na kisha kumgeukia Roma kwa mshangao.

“Hades tunapaswa kufanya nini kuwaokoa?”Aliuliza Kobota na Roma hakujibu chochote na kuinama huku akimwnaglaia yule mwanadada mwenye rangi ya chocolate ya kiafrika, baada ya kumwangalia kwa dakika aliweka mkono wake kwenye kifua cha yule mwanadada na kisha akafumba macho.

Kobota na kibonge walikuwa wakijiuliza Hades anafanya nini , lakini walitulia kuona mwisho wake , lakini ndani ya dakika kadhaa , walihisi joto kiasi na kumkazia macho Hades.

Roma alimuwekea mwanamke yule mweusi kiganja kwenye moyo na kisha akahamia kwenye uso kwa dakika kama tano hivi, na kilichotokea kiliwaacha kobota midomo wazi , kwani ngozi ya yule mwanamke iliokuwa imepauka ilirudi kama kawaida , licha ya kwamba alikuwa bado hajarejewa na fahamu lakini alionekana kuwa na afadhari kuliko alivyokuwa mwanzo.

“Hii ni ‘Endless Resolve restoration Energy’ nimejaribu kumuingizia na haitamchukua muda mrefu kurejewa na fahamu”Aliongea Roma.

Kobota na Mbwa mwitu waliangaliana kwa mshangao huku wakionekana kutoelewa kile ambacho Roma ameongea na Roma hakuwajali , alijua hawajaelewa ,alimsogelea na yule mwanadada wa kijapani na kisha akamuwekea kiganja cha mkono kwenye moyo na kisha akahamia kwenye uso na tumboni na ndani ya dakaika tano na yeye mwili wake ulionekana kurejea katika hali ya kawaida.

“Niko wapi?”Ilikuwa ni sauti ya msichana aliewekewa mikono na Roma wa kwanza, sasa kilichomshangaza Roma ni kwamba mwanadada huyu alitumia lugha ya Kiswahili kuuliza

Lugha ambayo Kobota na Mbwa mwitu hawakuweza kuielewa

UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 72 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
embu hao kina mbwa mwitu wampe nguo sugari ya warembo(roma)
 
daaaaah kma ya leo imekuwa fupi kdgo boss
 
SEHEMU YA 34.

Ni jumatatu asubuhi iliokuwa imekucha na makucha yake , wengi huwa hawaipendi hii siku kutokana na mambo mengi ambayo huwa yanatokea wikiend , sio wanafunzi , sio waajiriwa kila mtu anasababu yake ya kutokuipenda hii siku , lakini kwa mwanadada Edna alikuwa na motisha , kwake jumatatu aliichukulia kama safari ya wiki ya kimafanikio.

Mwanadada huyu alikuwa na jambo kubwa sana mbeleni ambalo alikuwa akilipanga kulifanikisha , dili ambalo kama likienda kama alivyokuwa amepanga , lingezidi kumfanya kuwa mwanamke Tajiri Zaidi , lakIni pia kampuni yake ingezidi kuchanja mbuga na kufahamika duniani kote na ndio maana hakutana ‘glitches’ za aina yoyote katika mkataba anaokwenda kusaini na kampuni ya Yamakuza , kampuni kubwa ndani ya taifa la Japani.

Kwake uwekezaji huo ndio mkubwa Zaidi kuwahi kuutekeleza tokea aichukue kampuni hio kutoka kwenye mikono ya mama yake na kama dili hilo pia litafanikiwa ndio dili ambalo litaifanya kampuni yake kuwa na mafanikio makubwa ndani ya mwaka huo.

Asubuhi ya leo alikuwa ameketi kwenye kiti akipata ;Breakfast’ , huku Roma akiwa mbele yake , upande wa kushoto kwake kulikuwa na Bi Wema ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Roma kwa tabasamu akiwa ni mwenye kufurahishwa na uwezo wa kula wa Roma.

“Siku zote nyumba ikiwa na mwanaume inaonekana kuwa hai”Aliwaza mwanamama huyu Mzungu wa Roho.

Upande wa Edna , macho yake yalikuwa kwa Roma , aliwaza Roma ni mwanaume wa aina gani , kwanza amerudi asubuhi hio akitoka kwa wanawake wake , lakini alionesha kutokuwa na hatia hata kidogo , ndio ndoa yao ni ya mkataba lakini angalau aonyeshe ile heshima ambayo ambayo ipo ndani ya neno ‘Ndoa’ lakini kwa Roma hakuwa ni mwenye kujali.

Edna aliendelea kutafakari , kwanini Roma yupo kama alivyo Roma , kwanini hakuwa siriasi na Maisha , haoneshi kuwa na mipango ya kimaisha ya baadae , yeye anafikiria kufanya mageuzi katika biashara lakini mume wake wa mkataba yeye anafurahia chakula na wanawake pasipo mpango wowote alikuwa akishangaa na kujiuliza maswali lakini alikosa majibu.

“Mke wangu , itoshe kusema najivunia sana kuwa mumeo ,maana hii ‘breakfast’ ni nzito , wakati nabeba mizigo kwenye soko la Mbagala kuna siku nilikuwa nashindia mihogo”Aliongea Roma na kisha alibeba bakuli iliokuwa na mchuzi na kupeleka mchuzi wote tumboni.

“Roma unaonaje kwanzia sasa ukiwa siriasi na kazi?”Aliongea Edna aliekuwa akimwangalia ,Roma kabla ya kujibu alichukua yai la kuchemsha na kuligonga mezani na kisha akaanza kulibandua na kisha akalipeleka mdomoni lote , akavuta kikombe cha chai na kushushia..

“Aargh … mke wangu umeng`ang`ania na mimi kuwa siriasi na Maisha , lakini mimi najiona niko siriasi”.

“Uko siriasi kivipi Roma , kila siku naletewa ripoti ya wewe kucheza magemu tu kazini na kwenda kula , huo usiriasi unaozungumzia ni upi, haya ukirudi nyumbani badala ya kukaa kutulia na kuwaza siku ya kesho ,ila wewe unawaza wanawake na unaenda huko unalala na unarudi asubuhi kweli Roma”Edna leo hii asubuhi alionekana kuwa na nongwa sana , kiasi ambacho kilimfanya Roma kushangaa nini kimempata mke wake mpaka kuanza kulalamika.

“Mke wangu wewe piga kazi , mimi nitaishi kama mtoto wa Tajiri , nitafute mapesa mengi ya nini wakati hizi hatutazimaliza …Bebi Edna labda tukipata mtoto na nikiitwa baba naweza kuishi kama baba”.

Edna hakutaka kuongea maana aliona kuongea na Roma hakuna heri yoyote , alichukua mkoba wake na kumuaga Bi Wema na kisha akatoka.

“Sijui ninamfanya nini angalau awe siriasi na Maisha?”Aliwaza Edna wakati akiwasha gari yake .

Roma alifika kazini kama kawaida , na kuingia kwenye jengo hili ambalo kwake kila siku sehemu hii ilizidi kumvutia kutokana na harufu nzuri za pafumu za warembo.

“Romaa..”Ilikuwa ni sauti iliomwita Roma akiwa anaingia kwenye Lift na mwanadada aliekuwa akimwita alikuwa ni Benadetha.

Benadetha kwenye macho ya Roma alikuwa mrembo sana ambaye alitamani pia angalau apate wasaa mzuri wa kumjua nje na ndani , hayo ndio yalikuwa mawazo yake , lakini mwanadada huyu alionekana kuwa bize sana na kazi , muda mwingi hakuwa akipenda sana kupiga Stori kama ilivyokuwa marafiki zake.

“Niambie mrembo, za wikiend?”

“Nzuri vipi wewe?”

“Njema kabisa”Alijibu Roma wakati wakiwa wamesimama wakisubiria Lift ifunguke waingie , lakini mara nyuma yao wakasimama wanaume wawili na wanaume hawa hawakuwa wengine bali alikuwa ni Abu na Elvice .

Elvice baada ya kumuona Roma alijikuta akikumbuka tukio ambalo alifanyiwa na Roma na alijikuta hofu ikianza kumjaa,Benadetha alisalimiana na Abu pamoja na Elvice , ila Roma alionyesha hali ya kutofurahia uwepo wa mabwana hawa.

“Mmekuja kufanya nini hapa?”Aliuliza Roma pasipo kusalimia , huku Benadetha yeye akitangulia akiwaacha Abu na Elvice wanamwangalia.

“Mr Roma nadhani uwepo wetu hapa haukuhusu , kwanza nasikia una nafasi ndogo sana kwenye hii kampuni kwanini tuongee na wewe juu ya swala lililotuleta hapa?”Aliongea Abu kwa kejeli na Roma kwanza alitabasamu.

“Ni kweli sipaswi kujua nini kimekuleta hapa , lakini naamini unakumbuka onyo nililokupa mara ya mwisho , hivyo kuwa makini”Aliongea Roma na muda huo huo Lift ilifunguka na Roma aliingia huku Abu na Elvice wakiwa wamesimama wakiangalia Lift hio inajifunga taratibu na Roma akamwangalia Elvice na kumkonyeza.

“Hawa mafala wote wamekuja kufanya nini hapa?”Alijiuliza Roma wakati akiingia ndani ya ofisi aliokuwa akifanyia kazi na aliiendeea meza yake , huku akisalimiana na baadhi ya wafanya kazi wenzake ambao walikuwa bize , isipokuwa tu Recho pekee ambaye hakuonekana kwenye meza yake na alijiuliza ni kwannini mwanadada huyo hakuwa amefika kazini , lakini alipotezea.

“Hapa nicheze EuroTrack simulator nipoteze poteze muda , hii kazi siipendi , sema ndio hivyo kuna warembo wanaonipa motisha lakini pia nataka kumridhisha mke wangu”Aliwaza Roma na kuwasha gemu na kuanza kucheza , lakini bado akili yae ilionekana kutofarahia gemu hilo , ni kama moyo wake haukuwa na amani , baada ya kuona hafurahii aliinuka kwenye meza yake na kutoka nje ya ofisi, huku wafanyakazi wenzake wakimshangaa , aliingia moja kwa moja kwenye Lift na kwenda juu.

“ Miss Airport nahitaji kuonana na CEO”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Monica mwanamke ambaye alikuwa sekretari wa Edna , kwa Roma mwanadada huyu alimuona kama mbaya kuliko wanawake wote wa hii kampuni , kwanza kabisa alimuona kuwa na kifua ambacho hakikuwa na manyonyo na kilikuwa Flati kama vile barabara za Airport.

Kwa huyu Monica na yeye hakuwa akipendezwa kabisa na Roma , alionekana kutompenda kwenye hii kampuni na alitamanni awe na uwezo amfukuze , lakini licha ya kutokumpenda hakuwa akijua kuwa Roma ni mume wa Boss wake.

“Yupo ila ana wageni huwezi kuingia”Aliongea Miss Airport .

“Miss Airport haujui kujibu maswali , darasani ulikuwa unapata ngapi mimi nimeuliza swali moja ila wewe umajibu mawili”Aliongea Roma na kuuendea mlango wa CEO na kuufungua na kuzama ndani na Monica alipandwa na Jazba na kumfuata Roma.

Roma baada ya kuingia alikutana na Sura tano , ya kwanza ilikuwa nni ya Mke wake ambaye yuko ‘Composed’ kama ilivyokuwa kawaida yake ya kujiamini akiwa amekunja nne na suti yake ya rangi nyeupe , wa pili alikuwa ni Nadia mwanasheria Mpya wa kampuni na Roma hakumtaraia ndani hapo na watatu alikuwa ni Doris ambaye alikuwa amependeza kama kawaida , lakini alikuwa na uso wa usiriasi, wawili wa mwisho ni wanaume ambao Roma hakuwa akiwapenda hasa wakiwa karibu na mke wake yaani Abubakari Hamadi na Elvice Temba.

Kwanza wote watano walijikuta wakimwangalia Roma ambaye aliingia bila hodi na muda huo huo na Monica aliingia.

“Boss nisamehe nimejaribu kumzuia lakini hakunielewa”Aliongea Monica kwa wasiwasi mno , aliogopa kumkasirisha bosi wake.

“Unaweza kwenda kuendelea na kazi Monica”Aliongea Edna ambaye alionekana kuwa kawaida , lakini alikasirishwa na kitendo cha Roma kuingia hapo ndani moyoni kwani alikuwa na kikao muhimu sana na wageni wake, baada ya Monicca kutoka Roma alijongea mpaka upande wa kiti anachokaa mke wake na kisha akaketi huku akizunguka zunguka , hakuwa na wasiwasi hata kidogo, Abuu alikuwa na hasira alitamani afanye shambulizi palepale kwa Roma , kwani alikuwa akimchukia sana bwana huyo , lakini hakuwa na ujasiri wa kupambana na Roma ana kwa ana , alijua sio saizi yake , kwa upande wa Elvice na yeye alikuwa hampendi kabisa Roma , hasa akikumbuka bwana huyo ni mume wa Edna alijikuta akitaka kuonyesha uwezo wake wa kimapigano aliokuwa ameupata akiwa jeshini , lakini alivyokumbuka namna ambavyo Roma macho yake yalibadilika na kutaka kunyongwa na mkono mmoja aliogopa na kuona atulize mshono

Upande wa Doris na Nadia haikuelewaka walikuwa na mawazo gani ila walimwangalia Roma kwa macho ambayo yalikuwa na maswali mengi , upande wa Edna alikuwa akimwangalia kila mmoja aliekuwa hapa muonekano wake , na kisha akamgeukia Roma.

“Mke wangu kipenzi , Endelea na kikao chako sijaja kukuvuruga”Aliongea Roma na kisha aligeuza kiti chake na kuangalia upande wa nje kwa kutumia Dirisha akiangalia upande wa bandari hii ya Dar es salaam ilivyokuwa bize.

Edna hakuwa na chakumfanya Roma , kwanza angeonekana sio mke bora kama angemfukuza , lakini pia lilikuwa ni jukumu lake kumlindia heshima Roma kama mume wake , walikuwa wameoana kwa mkataba lakini alikuwa akiheshimu sheria za ndoa , hivyo aliwasihi wenzake waendelee na kikao.

“Tunaweza kuendelea , Roma ni mume wangu hivyo hakuna kinachoharibika akiwepo hapa , labda kama kuna mwenye shida na uwepo wake”Aliongea Edna na kuwaangalia wenzake na Nadia ndio aliekuwa wa kwanza kutingisha kichwa chake kuonyesha anakubaliana na Edna , na wengine wote wakaonyesha sura za kwamba hakuna tatizo , ila ukweli kila mmoja hapo ndani hakufurahishwa na kauli ya Edna , kila mtu aliona kauli hio kama Risasi iliozama moja kwa moja moyoni na kutibua chemba za moyo.

Kikao kiliendelea na Roma aligeuka na kuanza kutumia Computer ya mke wake , kama kawaida alikutana na gemu la nyoka na kuanza kucheza huku akila Karanga zilizokuwa kwenye kibakuli.

“Kutokana na ukubwa wa uwekezaji huu naamini viongozi wote wa juu tunapaswa kwenda Japan kusaini huu mkataba na hayo pia ni mapendekezo ya Viongozi wa Yamakuza”Aliongea Abubakari.

“Kuna ulazima wa CEO wote kusafiri mpaka Japan ?”Aliuliza Edna.

“Ndio Edna” Maagizo niliopewa na Yamakuza ni kwamba CEO Abubakari na wewe lazima muwepo , hili ni dili kubwa sana ambalo kampuni ya Yamakuza inafanya kwa mara ya kwanza na kampuni za Afrika ,tusilichukulie kwa wepesi”Aliongea Elvice na alionekana yupo hapo ofisini kuwakilisha kampuni ya Yamakuza.

“Kuna ulazima gani wa mke wangu kwenda?”Aliuliza Roma kwa sauti na alionekana kukerwa sana na Elvice kwani aliona hakukuwa na sababu ya Edna kwenda kama tu anataka kuwakilishwa na mtu mwingine.

“Mr Roma hili ni swala ambalo linahusu uongozi wa juu wa kampuni , hivyo unatakiwa ukae kimpya mabosi wako tukiongea”Aliongea Abubakari na Roma kwanza alitabasamu.

“Kwanza nikurekebishe , unaonekana hauko profesheno na kazi yako , mimi sio boss wako , pili sioni haja ya Edna kwenda kama anataka kuwakilishwa na mtu kutoka kwenye kampuni , sioni utofauti mtu mwingine akienda , kwani mazungumzo ya kibiashara yashafanyika kupitia mkataba na kule ni kitendo cha kutia sahihi , kuna tatizo gani hapo , au shida tu uende na mke wangu”

Abu na Elvice walionekana kukasirishwa sana na Roma , ni kweli hakukuwa na shida ya Edna kwenda ila Elvice alitaka atumie nafasi ya kwenda Japan na Edna ili akajiweke karibu na angalie namna ya kumpata mrembo huyo, na mpango wa Elvice na wa Abuu hakukuwa na utofauti na kila mtu aliona hio ndio nafasi ya kuongeza ukaribu na Edna , lakini waliona mipango yao Roma anaingilia , kwanini wafurahi.

“Alichongea Roma ni sahihi , hakuna haja ya CEO kwenda kama anataka kutuma mwakilishi naweza kwenda mimi au Doris na hata Nasra ambaye ni mhasibu mkuu wa kampuni”Aliongea Nadia na Roma alikumbuka kwanini Nasra hakuwa kwenye kikao hicho kwani na yeye pia swala hili la mkataba lilikuwa likimhusu.

“Swala hili sio nani kwenda , swala ni kwamba kampuni ya Yamakuza wamotoia ombi hilo kama Sharti”Aliongea Elvice na alimfanya Roma akasirike Zaidi , jambo ambalo kwa Nadia na Doris hawakulipenda , kwani Roma alikuwa akionyesha wivu waziwazi.

“Mimi Roma Ramoni .. Edna ni mke wangu licha ya kwamba ni kiongozi mkubwa wa kampuni hii lakini pia lazima apate baraka zote kutoka kwangu hilo ni la kwanza , la pili naomba nimuulize mke wangu ..” huku akimwangalia Edna

“Mke wangu kwenye huo mkataba kuna kipengele chochote ambacho kinakulazimisha wewe kwenda Japan??”Edna alitingisha kichwa kama hakuna na Roma alitabasamu.

“Sasa nasema hivi nisikie mtu anaongea tena kuhusu Mke wangu kwenda kusaini huo mkataba uone ..”

Aliongea Roma na kurudi kwenye kiti na kuendelea kucheza gemu baada ya kutoa biti ambalo lilimkasirisha kila mmoja Abu na Elvice walikasirishwa na kitendo cha Roma kuharibu mipango yao na Doris na Nadia walionekana kuwa na wivu wa Roma kumlinda Edna , walitamani nafasi hio iwe ya kwao.

Elvice na Abuu japo ya kukasirika walipiga kimya , hakutaka tena kuongea swala hilo, kwani waliogopa.

“Okey kwa upande wangu ataniwakilisha Doris pamoja na Mume wangu”Aliongea Edna na kufanya hali ya hewa ibadilike.
Tehtehetehteh, mambo yanazidi kuwa mambo
 
Hii story nimeanza leo na nimeimeliza leo kumbe kuna watu wanaenjoy tyuu huku JF halafu hatushtuani mbn mmekuwa wasiri hvyooo[emoji39][emoji39][emoji39]

Sema ningekuwa Roma vitumbua vyote vua JF ningevitia mchanga tena sio na kijiko[emoji5][emoji5][emoji5]

Oy Wakuuu mnitag mzigo ukishukaaaa[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
Aisee tamu sana story alafu watu wamekaa kimya, huko mbele huyu traffic Mage sidhani kama Roma atamuacha salama...atatafunwa tu.
 
Back
Top Bottom