singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #321
SEHEMU YA 51
Upande wa Chini kabisa ndani ya Mashua, kwa nje kabisa alikuwa amesimama mzee mmoja hivi aliekuwa ameshikilia panga lake Refu akiwa anaangalia Chopa iliokuwa hewani , mzee huyu alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , alikuwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya kichina huku akiwa na kipara chake, alikuwa na macho flani hivi ya kutisha kama ana makengeza na mboni za macho hazikuonekana ni rahisi kusema anajicho lisilokuwana kiini cheusi..
Ndani ya mashua hio walionekana vijana wanne hivi wote wakorea waliokuwa wameketi kwenye visturi huku wakinywa kilevi ambacho kilikuwa kikifanana na ulanzi , huku pembeni yake kukiwa na Sanamu Varicana ambalo walikuwa wamelifunika na nguo.
Upande wa kushoto ndani ya mashua hii kulikuwa na maboksi flani ya mbao , kama yale ya kuhifadhia Nyanya wakati wa kuzisafirisha kutoka shambani , chakushangaza ni kwamba maboksi hayo yalikuwa yakitingishika na nikama kulikuwa na mnyama ndani ya maboksi hayo na watu hawa hawakuwa wakijali sana kutingishika kwa maboksi waliendelea kunywa kwa furaha huku wakiongea , lakini muda huohuo ndio walipoanza kusikia mngurumo wa Chopa na wote kwa pamoja walikurupuka na kubeba Bunduki zao na kutoka nje haraka na walimkuta kama kawaida Tzeng akiwa anaingalia ile chopa huku akionekana ni mwenye kukata tamaa , ni kama mtu ambaye alikuwa akisubiria kitu kikubwa Zaidi na hakijatokea.
“Master Tzeng”Aliita kijana mmoja wa kikorea huku akimwangalia Monk kwa wasiwasi.
“Mtu ninaemsubiria hayupo kwenye hio chopa , naona wale makafir wamenidanganya,imenikatisha moyo , walitaka kunitumia tu kukamilisha mambo yao ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng.
“Master lakini haujatuambia unaemsubiria kila siku umekuwa wakutuambia kuna mtu unaemsubiria”.
“Unafikiri kwa miaka yangu yote niliohudumu kusalia Budha ninaweza kuisaliti huduma yangu kuja kuiba sanamu,Nimewakubalia Dhoruba Nyekundu kuiba hilo sanamu kwasababu wamenihakikishia nitapata nafasi ya kupambana na Hades ,Inasikitisha sana”
“Master Hades ni nani?”
“Huna haja ya kumjua , kwangu ni mtu ambaye natamani kuupima uwezo wangu wa kimapigano kwa kupambana nae , lakini nimekatishwa tamaa na kutoonekana kwake, nahisi sitoweza kuufamu uwezo wangu wa kimapigano mpaka nakufa inasiikitisha sana”.
Upande wa Chopa kule juu wakati wakiendelea kushangaa chini baharini kama watamuona Roma , Mara walijikuta wakianza kushambuliwa kwa mbele.
“Sh**t Ni ni kikosi cha watu wa Dhoruba Nyekundu washafika, Kapteni kuwa makini wasiharibu chombo”.
“Pumbavu tulishindwaje kuwagundua wamekaribia? , Boti yao ile”
“Sio Boti wewe mpuuzi , ile ni SubMarine(Manuari)”Aliongea Kobota akimrekebisha Mbwa Mwitu , lakini wakati huohuo lilirushwa kombola na ilibakia kidogo tu ligonge Chopa yao na Rubani alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani aliipindisha Ndege na kugeuza kushoto, mashambulizi yalikuwa makali sana na watu wa Dhoruba Nyekundu walionekana kudhamiria kuidondosha kabisa hio chopa.
“Bang .. Bang !!”Ni milio ya risasi iliokuwa ikigonga chopa huku na waliokuwa kwenye ndege wakirusha Risasi.
“Hawa wajamaa wanateknolojia kubwa ndio maana ndege yetu imeshindwa kuwanasa kwenye Radar, tusipokuwa makini hii misheni itafeli”Aliongea Rubani msaidizi kwa kijapani.
“Sema Pluto naamini ashakufa mpaka sasa , niliwaambia hana lolote yule, na nimeshangaaa kumuhusisha kwenye hii misheni”Aliongea Kibonge huku akimdharau Hades na hio ni kutokana zimepita Zaidi ya dakika tano bila ya kumshuhudia Roma.
“Mother***ker!”
Rubani alijikuta akitoa tusi mara baada ya kurushiwa Kombora kiasi kwamba Chopa ilianza kutoa mlio wa Alarm lakini ile anataka kulikwepa kwenda kulia , wa kwanza kuruka alikuwa ni kibonge , alionekana kuwa shapu na akafatia Kobota na Mbwa mwitu na hapohapo ulisikika mlio wa ‘BOOM’ Chopa ilikuwa imelipuka ikiwa na Sunami na Rubani msaidizi Jani ,na wengine , ulikuwa ni mlipuko mkubwa uliosababisha mwanga kutawala kwa sekunde kadhaa mpaka kufifia huku mabaki ya ndege yakidondokea baharini.
“Haya yote hayana maana ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng baada ya kuona mlipuko wa ndege , lakini ile anageuka tu Roma alietoka kwenye maji kama samaki jamii ya Dolphin ,kama mshale huku akijilenga kwa Tzeng , lakini Tzeng alikuwa mwepesi mno kwani aliinama chini kama mti ambao umepindishwa na kichwa kugusa chini huku miguu haijasogea hata kidogo , yaani ni kama mti ulikuwa umechomekwa kwenye shimo na ukapindishwa na Roma akapita na kumvaa kijana aliekuwa akiuliza maswali na akaenda kudondokea baharini .
“Amitabha.. Hades”Aliongea Mzee huku akikunja mikono miwili , alionekana kushukuru ujio wa Hades.
“Inashangaza kuona Monk kuwa mwizi”Aliongea Roma.
“Kuna Muda inapaswa kuwa hivyo , kama unania ya kutimiza dhumuni kuu kwenye maisha yangu”Aliongea huku wale Wakorea wakiwa wamemzingira na Bunduki zao ila Roma hakuwa ni mwenye kuwajali.
Wakati huo huo ile Submarine(Manuari) ilikuwa ishafika usawa wa mashua na walikuwa wakimshuhudia Tzeng na Roma waliokuwa wakiangaliana.
“Jason ni Hades , inapaswa kuchukua Sanamu tuondoke wakati akiendelea kupambana na Tzeng”
“Jessy tulia kwanza tuone mtanange , tukiona dalili za kushindwa kwa Tzeng tunakimbia ”Aliongea Jason wakati huu chombo chao kikiwa
Upande wa Kibonge alionekana kusalimika hukuu akiogelea upande wa ilipokuwa mashua ,aliangalia nyuma na kuwaona wenzake pia wanatapatapa kwenye maji.
“Okey!Tzeng nataka nikamuokoe mpenzi wangu,kwasababu umeshindwa kutumikia Budha na kugeukia njia Ovu nikikuua nitakuwa nimefanya jambo la kiimani kwa Mungu wa Budha”Aliongea Roma.
“Bothisativa Sabejatha” Alitamka Tzeng huku akimnsogelea Roma akiwa amenyoosha upanga wake , akilenga tumbo na Roma hakuondoka alipokuwa amesimama na ile Tzeng anafika Roma alisogea kidogo na Upanga ukapita kwenye kwapa , lakini Tzeng alionekana kutumia nguvu isiokuwa ya kawaida , kwani alimsukuma Roma na wote walitumbukia kwenye maji huku wakiwa katika staili kama ya kukumbatina ,Tzeng baada ya kutua kwenye maji mita kadhaa chini kabisa , alimsukuma Roma na kujitoa kwake na kisha akaleta tena pigo huko akizungusha upanga wake kwa spidi kiasi kwamba ulikuwa ukionekana kama sinndano na ile anamfikia Roma kwa nia ya kumchoma Roma aliuzuia na viganja vya mikono kwa kuubana , kitendo ambacho kilimfanya Tzeng kuuvuta ila Alishindwa na kujikuta akishangaa ni uwezo gani wa nguvu za mikono za Roma, lakini ile anashangaa Roma aliruka sarakasi na miguu ikawa juu na mikono ikiwa chini imeshikilia lile panga na kisha akazunguka kama Pia kitendo kilichomfaya Tzeng kukosa mhimili wa kushikilia lile Panga,Baada ya Tzeng kuona Roma anazunguka na yeye alizunguka vilevile kwa spidi kiasi kwamba Jason ,Jessie ,Kibonge na wenzake kushangazwa na Wimbi lililojitengeneza juu sehemu ambayo wametumbukia.
****
Ni ndani ya kisiwa ambacho kilipewa jina la Kisiwa X,kisiwa hiki kilipewa jina hilo kutokana na kwamba kimetolewa kwenye Ramani , yaani ni kisiwa , lakini kwenye Ramani ya dunia hakionekani na ndio maana kikapewa jina la Kisiwa X.ni kisiwa ambacho kipo kwenye bahari ya Antlantic.
Ni sehemu ambayo ina ulinzi mkubwa sana kiasi kwamba kama upo habarini kilomita 60 kutoka ndani ya kisiwa hiki utaona mkanda mkubwa wenye maandishi ya DON’T GET CLOSER ,IT`S DANGEROUS yalioandikwa kwa Rangi nyekundu kuzunguka eneo lote la kisiwa ,ni sehemu ambayo inabaridi kali sana na mkondo mkubwa wa maji na ni mara nyingi kuona meli zinapita karibu na eneo hilo na kama itatokea mtu akifika kwenye eneo hilo ni ngumu sana kutoka hai.
Ndani ya eneo hili la kisiwa kuna jengo ambalo kwa juu linaonekana kama kibakuli kilichofunikwa, na jengo hilo lina rangi nyeupe huku pembezoni mwa jengo hili kukiwa na Bendera zinazopepea za mataifa ishirini yenye nguvu, ambazo zimepangiliwa kwa umbali sawia kiasi kwamba zilifanya jengo hilo kupendeza.
Basi ndani kabisa ya jengo hili ndani ya hiki kisiwa , walionekana watu wanaume na wanawake walio na utofauti wa umri ,yaani kuna wale ambao walionekana kuwa na miaka hamsini na kuna wale ambao walikuwa na miaka Therathini kimakadirio , hapo ndani hapakuonekana mtu ambae yuko chini ya miaka ishirini.
Watu hawa wote walikuwa wamevalia tisheti za rangi ya Bluu huku kila mmoja ikiwa na chata la ‘O’ na jicho katikati ambalo limenakishiwa kwa rangi nyekundu, halafu chini ya tisheti hio kuna maneno yanayosomeka Zero`s Organisation.
Ni jengo ambalo kwa ndani lilikuwa limejengwa kitaalamu sana , jengo hili lilikuwa limetenganishwa mara mbili upande wa kulia kuna vyumba ambavyo vimejengewa kwa mfumo wa nusu duara , lakini pia kwa upande mwingine kuna vyumba ambavyo vimejengwa kwa mfumo wa nusu duara huku katikati pakiachwa wazi huku juu yake kukiwa na paa ambalo lilikuwa likipitisha mwanga na matundu ambavyo yametengenezwa kwa muundo wa nyota.
Ukiachana na hili jingo kwa pembeni yaani nje kabisa kulikuwa kumejengewa pia nyumba ambazo zilikuwa kwenye muundo tofauti tofauti ,zilizofanya eneo hili kupendeza sana ukijumlisha na bustani zilizokuwa zimetenezwa kwa muundo wa kuvutia.
Sasa ndani ya hili jengo kuna Idara inayofahamika kwa jina la PLMC(PROJECT LADO MONITORING CENTER), ndani ya hii idara walionekana jumla ya watu kumi na mbili , watano wanawake na saba wanaume wenye umri tofautt tofatui , ndani ya hii idara mbele kabisa kuna ukuta mkubwa ulionjengwa huku ukiwa na skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionesha eneo la baharini , lakini ajabu ni kwamba mazingira yanayoonekana ndani ya hili eneo ni yale yale ambayo Roma na Tzeng wakipigana.
“Unafikiri Agent 13 atashinda Carlos?”Aliuliza mwanamke mmoja wa kizungu makadirio ya miaka hamsini hivi kupanda ambaye alikuwa akila Popcon zake zilizokuwa kwenye kopo bila habari huku akiangalia mpambano kati ya Roma na Tzeng , mwanamama huyu alikuwa amekaa huku pembeni yake kulikuwa na bwana mmoja mweusi kijana, akiwa amekaa pamoja na mwanamama anaekula Popcorn huku nyuma yao wakionekana wenzao ambao wamesimama wakiwa wanangalia mtanange huo , kwa jisi walivyo makini ni kama walikuwa kwenye ukumbi wa sinema wanaangalia muvi.
“Sina mashaka na Agent 13 Dyana, Tzeng ni mtu ambaye ana mafunzo ya juu na ndio maana tukamchagua kupambana na Agent 13 lakini haimaanishi kama anaweza kushinda ni uwekezaji mkubwa na maarifa yaliofanyika kumtengeneza Agent 13 na hatakiwi kushindwa na Tzeng”Aliongea bwana huyu aliefahamika kwa jina la Carlos huku akirudisha umakini wake kwenye pambano.
“Sema Agent 13 tokea Agent 17 kufariki , ukatili wake umepungua kwa asilimia mia moja ,nadhani mpango wa kumuua Agent 17 ulikuwa bora sana”Aliongea mwanamama huyu lakini bwana Carlos hakujibu.

ATLANTIC OCEAN-ISLAND X
PROJECT LADO MONITORING CENRE(PLMC)