Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kesho tunaendelea
mkuu kesho tena?
Acha tusubiri tuKesho tunaendelea
Nmekuchek WhatsApp mkuuKesho tunaendelea
Response n ndogo sana mkuu ukitafutwaSEHEMU YA 160.
“Wife kile kikombe kinaonekana kuwa kizuri sana, kama utakinunua na kutumia kuwekea Wine , kitakufanya upate usingizi mapema na hata urembo wako kuongezeka”Aliongea Roma kupotezea,Na Edna alibetua mdomo.
“Nunua wewe kama unakitaka, kwanza kinaonekana sio ghali”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu kwa uchungu m aliona mke wake hakuwa akielewa maana ya kikombe kile kilichokuwa mbele yake ndio maana.
“Ladies and gentlemen, this treasure is provided by a seller who requested to remain anonymous. It’s a wine cup used before Christ. The long and mysterious history was the biggest feature of this item. No one was able to tell its name. Today, it starts at the price of two million Dollar, but the real value is very difficult to be determined. I hope everyone seize this opportunity..”
Kwa maelezo ya Mhereheshaji alikuwa akisema kwamba kikombe hiko kilikiuwa kimetolewa na muuzaji ambaye hakutaka jina lake lifahamike , ni kikombe ambacho kilitumika kipindi cha karne zilizopita na kilitumiwa na Yesu na mpaka kufikia wakati huo , hakuna mtu ambaye ameweza kukipa jina sahihi, na akaongezea kwamba Thamani ya pesa ya kikombe hiko itaanzia Dola Za kimarekani milioni mbili , ni pesa nyingi sana ambazo ukizileta kwa kitanzania ni Takribani bilioni mbili na ushee.
Edna mwenyewe alishangaa , kwani kikombe hiko alikiona cha kawaida sana , lakini alivyosikia bei ya kuanzia alijikuta akimwangalia Roma na Roma hakujibu chochote Zaidi ya kutingisha mabega kumuonesha kwamba hana anachokijua.
Sasa Wakati Edna akishangaa , wale wazungu ambao waliingia hapo ndani , kuna mmoja mwanake hivi mtu mzima kati ya miaka Arobaini hivi , alitamka kwa nguvu.
“Dollar Milioni kumi”
Watu walishangaa sana kwani ni pesa ndefu mno yaani takribani bilioni ishirini na mbili za kitanzania na hata Roma mwenyewe akashangaa.
“M16 naona kwa namna yoyote wako hapa kwa ajili ya kukipata hiki kikombe , inanifikirisha ni nani aliekifikisha Tanzania”Aliwaza Roma.
M16 ni shirika la Kijasusi la Uingereza mwanzoni lilikuwa likifahamika kwa jina la SIS(Secret Intelligence Services) ni shirika linalofanana kwa asilimia mia na mashirika ya kijasusi kama vile MOSSAD ya Israel ,FSB la Urusi ambalo mwanzoni lilikuwa likifahamika kwa jina la KGB ,CIA shirika la Marekani na pia kama vile TISS shirika la kijasusi la Tanzania.
Kwanza kwa namna wazungu hawa walivyoingia hapa ndani hawakuwa wamealikwa , kwnai watu wote ambao walikuwa wamealikwa , walikuwa wamepewa vibao maalumu vya kunyayua kama watataka kutaja bei , lakini huyu mzungu yeye hakutmia kibao Zaidi ya kusema kwa mdomo na hata watu walishangazwa na uwepo wao.
Mheshimiwa Kigombola aliekuwa amekaa mbele kabisa upande wa kushoto alimgeukia msaidizi wake aliekuwa akijulikana kwa jina la Frank.
“Una taarifa za hao wazungu?”
“Mheshimiwa licha ya kwamba hawajaalikuwa , lakini kwa taarifa ambazo ninazo hapa, yule mama yupo hapa nchini kama muwakilishi wa Wizara ya Kibiashara kutoka uingereza anafahamika kwa jina la Lilith, lakini pia ni moja ya mwanafamilia ndani ya jumba la kifalme(Royal Families)”Aliongea Frank na Mheshimiwa Kigombola alitingisha kichwa chake kuelewa.
“Kwasababu wamekuja , nadhani muwapatie vibao vya namba”Aliongea Mheshimiwa Kigombola na Frank akanyanyuka kutimiza maagizo na ndani ya dakika tano tu zoezi lilikamilika.
“Okey Mgeni wetu namba 139 ametuanzia na bei ya Dollar Milioni kumi , kuna anaetaka kuongeza..”Aliongea Actionieer.
“Dollara Milioni 12…”Aliinua kibao Magdalena aliekuwa amekaa karibu na pacha wake Mage na kumfanya hata Roma ashangae ,haikuwa kwake tu hata Edna pia alishangaa kwani ni kiasi cha pesa kikubwa sana ambacho ameinua na kwa alivyokuwa akiijua familia ya Mama P haikuwa na uwezo wa kuwa na kiasi hiko cha pesa kwa ajili ya kununua kitu kama kile alichokuwa akikona mbele.
Roma aliishia kutabasamu na alipata Ari mpya ya kuendelea kuona kile kitakachotokea, na kwa akili yake haraka haraka aliamini Magdalena yupo hapo kwa maagizo maalumu na yupo kwenye misheni, kwasababu alijua kabisa kikombe hiko hakina uhusiano kabisa na familia ya Afande Tobwe.
Lilith baada ya bei hio kutajwa alimwangalia Magdalena na kutabasamu na kisha akanyanyua kibao kingine.
“Dollara Milioni 15”Alitaja
“Dollara Milioni 18”Alitaja tena Magdalena au Ajenti Flamingo na kufanya watu wazidi kushangaa , huku wakimwangalia Mage kwa macho ya kiulizo , unajua kwa mwanamke mwenye umri mdogo na mrembo kama Magdalena ilikuwa jambo la kushangaza sana kwa yeye kutaja bei hio.
Roma alijikura akishangaa Zaidi , hata kama Magdalena alikuwa ametumwa aliona kuna jambo haliko sawa kabisa, ilikuwa ni sahihi kwa Lilith kutaja hio bei ukilinganisha na Kikombe hiko kuhusiana moja kwa moja na dini ya Kikristo na kilikuwa ni kikombe chenye maana kubwa kwao na kilikuwa kama utambulisho, yaani Holy Grail au Sangreal.
“Naamini Lilith anachonunua sio kikombe bali ni maana iliokuwa nyuma ya kikombe , lakini Magdalena inanishangaza kama anao uelewa huo , ila ngoja nione mwisho wake”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake akimaanisha kwamba kuna maana nyingine ambayo ilikuwa ikisimama juu ya neno lenyewe la Holy Grail na sio kikombe kama kikombe.
Mchuano ulikuwa mkali mno , na ulikuwa ni wa watu wawili pekee yaani Magdalena pamoja na Lilith , na bei ilikuwa imefikia mpaka Dollara milioni Ishirini na saba na hapa Lilith alionekana kukosa utulivu kabisa na kumwangalia Magdalena kwa hasira.
Lakini ajabu ni kwamba baada ya Magdalena kuongeza Milioni Therathini Lilithi alinyanyuka alipokuwa ameketi na kisha akapiga hatua kutoka kabisa nje ya ukumbi huo kama walivyokuwa wameingia akifuatishwa na wenzake na kufanya watu watabasamu na kuona hao wazungu wameshindwa na Magdaelana na hata kwa Mheshimiwa Kigombola mwenyewe alishangazwa na swala hilo.
Mhereheshajj alijikuta akijifuta jasho kwani hakuwa ametegemea kikombe kama hiko kufikia thamani ya pesa ambayo imefikia.
“Kwa mara ya kwanza , kwa Mara ya pili , Kwa mara ya…”
“BOOM!!,BOOM , BOOM”
Ni mtingishiko mkubwa uliosikika, ulikuwa ni mtikisiko kama wa bomu uliosikika na kumfanya Edna ajifiche kwenye mwili wa Roma kwa woga na muda huo huo na umeme ulikatika na eneo lote kuwa giza na kufanya watu waanze kuhaha huku wanawake wakitoa vilio vya woga.
Mabodigadi waliokuwa ndani hapa walianza kutoa mabosi wao kutoka nje kwa usalama Zaidi na ndani ya kama dakika kumi kupita hatimae umeme ulirudi tena na kufanya mheshimiwa Kigombola atoe macho , kwani ile sehemu ya mbele ambayo yule mshereheshaji alikuwa akitangaza , ilikuwa imebomoka na mhereheshaji alikuwa ametupwa pembeni na kwa hali aliokuwa nayo , hakuonesha kabisa kuwa na uhai.
Walinzi wa hili eneo waliingia haraka haraka na kukimbilia ile sehemu ya mbele na kuangalia ni nini kimetokea na ile wanafikia hata zile kabati zilziokuwa zimehifadhia baadhi ya vitu zikiwa zimepasuka na hakuna alielewa mara moja ni nini kimetokea.
“Piga simu polisi”Aliongea Mheshimiwa Kigombola huku akianza kupiga hatua kutoka nje ya ukumbi huu.
Upande wa Roma wakati watu wakiendelea kupaniki akiwemo mheshimiwa Azizi na mke wake walivyokimbia kama wehu, yeye alikuwa amemshikilia Edna aliekuwa amejikunyata kwenye mwili wake na Roma alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa, ni kama mtu ambaye alionekana kutegemea tukio hilo, na aliangalia upande ambao Magdalena alikuwa amekaa na hakuwa akionekana Zaidi ya kuwepo kwa Mage peke yake ambaye alionekana pia kutetemeka.
“Ninauhakika na hawa wazungu ndio wanahusika kwa asilimia mia moja na Magdalena anaweza akawa kwenye matatizo kama atahitaji kupambana nao”Aliwaza Roma na kisha akamshika Edna na kumwangalia usoni na kisha kutabasamu , unajua licha ya kwamba Edna alionekana kuwa na wasiwasi mno , lakini hakuwa kama wanawake wengine ambao walitoa vilio na kulia kwa nguvu.
“Wife nitaenda kuangalia hali ilivyo huko nje , Mage yule pale kaa nae ukiona nachelewa rudi nyumbani”Aliongea Roma na kunyanyuka na Edna ile anataka kuongea Roma alikuwa amepotea kama jini na kumfanya Edna atoe macho.
Baada ya Roma kufika nje kimiujiza , alijikuta akianza kuvuta hisia kwa uwezo wake wa kimaajabu na alitumia sekunde tano tu alipotea , sehemu aliokuwa amesimama na ile anaibuka alikuwa ndani ya msitu mkubwa ambao hata yeye mwenyewe hakujua ni msitu wa upande upi ndani ya Tanzania , lakini kwa hisia zake aliamini alimesafiri kilomita nyingi na kilichomfanya asijue uelekeo ni kutokana alikuwa akifuata hisia zake katika kusafiri kutokana na ukinzani wa nguvu zake na zile za wale wazungu.
Baada ya kuibuka alijikuta akitabasamu baada ya kuhisi msisimko ukiongezeka Zaidi na kuhisi kabisa watu anaowatafuta wapo ndani ya hayo maeneo.
SEHEMU YA 161
“Inabidi kuharakisha kufika Pangani ndani ya muda, tukishaingia kwenye Submarine tunaweza kuwa na amani.”Aliongea mwanaume ambaye amevalia mavazi ya kitamaduni meusi , kama majoho , lakini alikuwa ni mzungu huku kichwani wote wakiwa na kofia mfano wa ‘Cloak’ yalikuwa kama mavazi ya kitamaduni ya dini za kale.
“Archimonde, the execution of the plan is much easier than we previously imagined. I have a bad feeling about it”.(Archimone namna tulivyofanikisha huu mpango imekuwa rahisi mno kuliko tulivyotegemea nina hisia mbaya juu ya hili)Aliongea bwana mwingine ambaye alikuwa na mavazi kama ya mwenzake kwa sauti nzito akimwambia Archimonde.
“No matter what, now that we obtained the Holy Grail, we should deliver it to the Presbyterian Church”(Haijalishi ,kwasasa tushapata ‘Holy Grail’ na lazima tukifikishe kanila la Presbyterian kama tulivyoagizwa)Aliongea Archimonde
Sasa hapo unatakiwa kuelewa kwamba Lilith hakuwepo kama vile Roma alivyokuwa akitarajia , ila hawa walikuwa ni watu tofauti kabisa na walikuwa wamesimama wakiongea na jumla yao walikuwa wanne , na licha ya kwamba kulikuwa na giza , lakini walikuwa wakionana vyema kabisa na walionekana kuwa na guvu ambazo sio za kawaida , ungesema ni wachawi vile.
“Moses, you’re overthinking again. Don’t you think it’s more exciting if some people were to appear to stop us? I heard that Lilith came this time. I really miss the chick whose sweet blood can be smelled from a mile away.”
“Moses unafikiria sana , Wewe huoni kama itakuwa vizuri kama kutatokea watu kujaribu kutuzuia ?Nasikia Lilith na yeye amekuja , Nimemisi sana yule kahaba mwenye damu ambayo unaweza kuinusa hata kama yupo maili kadhaa”
“Charlie, don’t take her too lightly if you don’t want your other hand to be slain by Lilith as well”
“Charlie acha kumchukulia kirahisi namna hio kama hutaki mkono wako mwingine kufyekwa na Lilith”
Sasa mpaka wakati huu tunaamini kwamba waliokuwa wamepiga bomu ndani ya ule ukumbi ni hawa ambao jumla yao walikuwa ni tisa waliokuwa kwenye mavazi yanayofanna kabisa , na kwa kuaangalia tu utagundua kuwa ni wajeshi wanaohudumu katika Imani flani , mavazi yao yalikuwani ni ya kitamaduni kabisa kama ya Roma ya kale
Baada ya kuongea hayo maneno walianza kuondoka kwa spidi tena na walionekana walikuwa wakijijaza nguvu , Lakini sasa kabla hata hawajafika mbali mara Archimonde alimpigia kelele mwenzake aliekuwa upande wa kulia.
“Kuwa makini”Aliongea na yule mwenzake aliinama ghafla kwa spidi kali na hapo hapo kikapita kitu kama chuma kilichokuwa kina meno manne kikizunguka kama pia , vilikuwa ni kama vile wanavyotumia maninja na ile anainama tu , vilipita vingine viwili kwa spidi kali na alierusha alionekana kuwa mtaalamu kweli , lakini licha ya hivyo pia hata hawa wazungu walionekana kuwa makini sana kwani walivikwepa vyote kwa wakati mmoja na hivi Vidude vilionekana Dhahiri kutokana na kwamba vilikuwa vikitoa mwanga mweupe kama wa Mwezi na kufanya hawa wazungu waliovalia mavazi meusi ya kitamaduni waonekane vyema na hawakuweza kujificha.
Lakini sasa muda huo huo wakijishangaa , ili kujua cha kufanya mara Archimonde alishuhudia mwanga flani uliokuwa na mchoro, yaani ilikuwa ni kama vile mwanga wa Bunduki mwekundu , uliokuwa umejishora kama Msalaba kwenye kichwa cha mwenzake pembeni.
“Pumbavu ni yule mbwa wa Vatican anaejiita kama Msalama wa Shaba”
Aliongea Achhimonde kwa hasira akiwaaangalia wenzake kwa tahadhari na baada ya kusema hivyo hawa mabwana walionekana kujawa na wasiwasi , kwani wote walikuwa wakionekana kumfahamu vyema mtu aliekuwa akifahamika kwa jin la utani kama vile Mbwa wa Vatican(Vatican Dog).
“Chukueni tahadhai , kufikisha Holy Grail sehemu husika kwa sasa iwe kipaumbele chetu”Aliongea Arichimonde na wenzake wote wakatingisha kichwa na alionekana yeye ndio aliekuwa ni kiongozi wa hiko kikosi.
Lakini sasa muda huo huo wakiangalia namna ya kuondoka hapo kwenye hilo eneo , mara walijikuta wakizungukwa na watu jumla yao kumi na hawa pia wlaikuwa wamevalia mavazi kama yao ya kitamaduni , lakini utofauti wake ni kwamba hawa ya kwao yalikuwa na rangi nyekundu na nyeupe na yalionekana vyema huku mbele ya kifua chao yakiwa na alama kubwa ya Msalama ulionakshiwa kwa rangi nyekundu.
“Archimonde inaonekana yule mzee kutoka Vatican kaamua kutumia jeshi lake kubwa Zaidi kuja kupambana na sisi , kama niko sawa hawa ni jeshi la Msalaba Mwekundu, na nahisi uwepo wa Gabriel hapa”Aliongea Charlie yule ambaye alikuwa anatumia mkono bandia na alionekana kujiamini kabisa na alionekana kutotishwa na kikosi alichokiita Msalaba Mwekudu(Red Cross Army).
Muda ule ule alionekana mtu ambaye alikuwa amevalia dude juu kama Helmeti , kwa kingereza wanaita ‘Cloak’ bwana huyu alikuw ana midevu mingi mno , na baada ya kutokea mita kadhaa kutoka walipokuwa wamesimama hawa wazungu walipvalia nyeusi , jamaa yule mwenye mwili mkubwa alivuta upanga wake ambao sehemu ya kushika ulionekana kunakshiwa na madini ya Shaba, ulikuwa ni upanga unaowaka kiasi kwamba licha ya kuwa kuna giza ulionekana vyema na huyo mzungu alikuwa siriasi mno kutokana na uso wake ulivyokuwa ukiogopesha.
“Archimonde tupatie Holy Grail na Mkuu wetu atawasamehe”Aliongea kwa sauti nzito kabisa iliosikika.
“Gabriel, you’re indeed arrogant as ever. Do you really think that we’d give up something in our hands easily?”Aliongea Archimonde akimjibu Gabriel.
“Wewe Binadamu mwenye Dhambi , unafikiri unaweza kupata ulinzi kutoka kwa Mungu kwa kuiba Holy Grail?”Aliongea Mzungu mwingine aliefanana na wenzake wengi , alikuwa mwembamba na yeye akiwa na siraha kama mkuki , ambayo mbele yake ilikuwa na chuma kilichokuwa na muundo wa meno matatu.
“Dogo tulia, huu sio muda wako wa kuongea”Aliongea Archimonde.
“Hahaha..Wewe Bata hebu kaa kimya mimi ndio Arthur Vince mwanajeshi(Templer) mwenye umri mdogo ninaeheshimika ndani ya Vatican ,Mtu yoyote akisikia jina langu lazima atetemeke , nahisi hata wewe hapo unahisi haja kubwa”Aliongea yule bwana mwembamba kwa dharau.
“Hahaha…Grablieli inaonekana Damu halisi ndani ya Vatican sasa hivi inapotea na imebakia mchanganyiko tu wa vijana wenye dhambi ,Yaani hata huyo anajiita mlinzi wa Kanisa takatifu hahaha…”Arthur alijikuta akipandwa na hasira ambayo ilidhihirika kwenye macho yake na palepale akataka kufyatuka ili akamfyeke Archimonde, lakini pale pale kuna mwanajeshi mwingine alievalia tofauti na wenzake alitokeza alimkinga na mkono huyu alikuwa amevaa mavazi ya kitamaduni ya kitemplar meupe kabisa ila mbele yalikuwa na msalaba wa rangi nyekundu , alikuwa na mwili mnene kweli.
“Arthur usiwe na haraka , Archimonde anatutukana ili kutufanya tupandwe na jazba”Aliongea kwa kingereza.
“Najua lakini simuogopi hata kidogo”Aliongea Arthur huku akijiuzuia na Archimonde alijikuta akitabasamu ni kama hakuwa amemuona huyo mzee aliemzuia Arthur.
“Ooh !your Majesty Thomas, long time no see. Is this young fellow your disciple? When did your Knights of the Holy Palace get its Standards this low?”
“Ooh ! Mfalme Tomasi muda mrefu hatujaonana , vipi huyu bwana na yeye ni mwanafuzi wako ,Imekuwaje wanajeshi wenu wa jumba takatifu la kifalme mkawa na vigezo vidogo namna hio?”Aliongea Archimode.
“Archimonde Marquis tupatie Holy Grail, Leo huna uwezo wowote wa kutushinda , lichaya kwamba vijana wako wanaonekana vizuri kimapigano , lakini hawawezi kumshinda Gabriel , Arthur , mimi na hawa wanajeshi ambao wanahusika na ulinzi wa Papa”Aliongea Mfalme Thomas bila ya kukasirika , yaani alikuwa akiongea kawaida sana.
“Thomasi huna haja ya kututishia na wanajeshi wako wenye mafunzo ya kizaman….”Lakini kabla hata hajamaliza walitokea wanajeshi waliovalia gwanda za jeshi la Tanzania na kumfanya Archimonde ashangae na muda huo huo akatokea Magdalena na muda huo alikuwa katika mavazi ya kijeshi na aliungana na kikosi cha Gabriel. Na kumfanya Archimode kushangaa.
Upande mwingine wakati haya yanaendelea mtaalamu Roma alikuwa juu ya mti amekaa ametulia kabisa kama nyani na alikuwa akisikia kila kitu , huku akionekana kuwa na hamu ya kujua kile kilichokuwa kinataka kutokea muda huo.
“Jeshi la Tanzania mnajisumbua sana , hivi mnashindwa kuelewa kwamba ‘ Dark Parliament’ ni mamlaka kubwa ambayo hakuna taifa ambalo linaweza kuingilia”Aliongea Charlie yule mwanamke na Magdalena alijitokeza mbele.
“Hatuna utambuzi ndani ya dunia ya kitu kinachoitwa Dark Parliament , sisi tunatambua Vatican pekee kama taasisi ya kidini yenye nguvu kijeshi na tupo hapa kuwapa msaada juu ya nyie Shetani mnaotegemea damu za binadamu kama chakula chenu muweze kuishi , inashangaza sana kwa Bara a Ulaya kuwalinda watu kama nyie miaka na miaka , sisi kwetu nyie ni adui kwa dunia”AliongeaMagdalena.
Muda ule ule Gabriel alikosa utulivu na kujiweka sawa kimapambano.
“Archimonde hatuna muda wa kupoteza na shetani kama wewe , utaondoka hapa kama utaweza kutushinda”Aliongea Gabriel.
“Gabriel umeenda mbali sana mpaka kushirikisha jeshi la Tanzania juu ya hili swala , huo unaonesha kama wewe na jeshi lako ni dhaifu”Aliongea Archimonde kwa hasira
“Acha woga Archimonde mimi hayo hayanihusu , mimi ni mwanajeshi na kamanda kwa kikosi cha Msalaba Mwekundu na nikipewa maagizo kutoka kwa Papa kwa ajili ya kupambana napambana ni wajibu wangu”
“Kwasabau umesema hivyo nadhani sina jinsi Zaidi ya sisi kupambana na ninyi, na sidhani kama Gabriel utaniweza tena , tumekuwa tikipambana miaka na miaka na haukuwahi kunishinda”Aliongea Archomonde na pale pale ghafla tu mikono ya Archimonde ilionekana kushikilia Ngao na kumsogelea Gabriel kwa spidi huku wenzake wakifuatia na pambano kali likaanza rasmi.
NB:Kuhusu Dark Parliament(Bunge la kiza) sitoelezea sana juu ya hawa watu kwenye hii simulizi mpaka kwenye simulizi yangu nyingine kabisa ila kwa haraka haraka Bunge la Kiza ni taasisi kama taasisi ya siri ambayo ipo duniani , ambayo ni kama jamii ya Freemason, hawa watu wapo kama jamii ya Mazombie kutokana na kwamba wanaishi kwa kunywa damu za watu, nadhani ushawahi kusidikia juu ya Taasisi ambazo unapata utajiri kwa kujiunga na kutoa kafara , sasa hizo kafara ambazo zinatolewa kwenye hizo jamii za siri damu yake wanakunywa hawa watu, kundi hili makao makuu yake yalianzia ndani ya bara la ulaya na wamesambaa sana na wanafahamika sana kwa jina la ‘Blood Race’ yaani kabila la damu .Eniwei hii ni Stori tu msiwe siriasi sana mkaanza kuota vitu vya ajabu usiku.
SEHEMU YA 162
Mwonekano wote wa jeshi la upande wa Archimonde lilibadilika kwa asilimia mia , yaani kwanza kucha za mikono yao zilibadilika na kuwa ndefu na macho yao pia , walikuwa na mwonekano wa Zombie kabisa na walikuwa wakitisha na mbaya Zaidi licha ya kwamba kulikuwa na giza sana , macho yao yalionekana yakitoa mwanga flani wa ajabu, huku kuanzia sehemu ya macho yao na kwenda mashavuni kukibadilika na kuwa na michinirzi mieusi kabisa ,, yaani miili yao haikuwa kama ilivyokuwa , bali sasa walionekana kama mashetani kamili.
Upande wa jeshi la Gabriel hawakutishwa na mabadiliko ya jeshi la Archemonde na kwa upande wa jeshi la Tanzania na wao hawakuwa na woga kabisa , yaani walionekana kama watu ambao walikuwa na mafunzo juu ya watu waliokuwa mbele yao.
“Fyuu…..Shwaaa ….Kaaaa….Fyuu”ilikuwa ni mivumo ya hewa ambayo imechanganyika na hewa nzito ndani ya hili eneo harufu ambayo haikuwa ikieleweka kabisa,
“Nuru ya Msalaba wa Bwanaa Iangazee…!!!!”Ilikuwa ni sauti ya Gabrieli iliosikika na hapo hapo upanga wake ulionekana uking`aa mno mithiri ya mwezi , huku kule alikoshikilia kukiongezeka urefu na upanga ukaonekana kama Msalaba.
“Kafaraaaaa ya damuu……..!!!!!”Ilisikika sauti ya Archimonde na hapo hapo upanga wake aliokuwa ameshikilia ulijaa damu ambayo iliokuwa ikifyatuka kwa spidi kuelekea upande aliosimama Garbriel na mwanga wa lile Panga la Gabriel ulizima ghafla na kukawa na Giza sehemu yote na palepale Archimonde alirudi nyuma kwa spidi na kumsogelea Moses na kuingiza mkono wake kwenye mfuko na kutoa kile kikombe na kumpatia.
“Hakikisha unatoweka hapa na unafika Ufukwe wa Pangani mapema na ukiona hatutokei unaweza kuondoka”Aliongea Archimonde kwa sauti ndogo na Moses aliichuku akile kikombe na kukificha kwenye nguo zake na Archimonde akamgeukia Charlie na kumpa ishara ya kuondoka na Moses
Kwa hali ilivyokuwa ilionekana , hawa majeshi ya Dark Parliament yalionekana kuzidiwa na walionekana kuanza kujihami mapema na ndio maana Archimonde alitaka awategenezee njia Charlie na Mobses kwa ajili ya kutoweka hapo kwenye huo msitu kuelekea pwani , sehemu ambayo walikuwa wakiamini kuna Submarine ambayo ilikuwa ikiwasubiria.
Charlie alimwangalia Archimonde kwa kumhurumia na kisha akageuka na kupotea , lakini ni kama walikuwa wakitegemewa maana mara ‘Fyuuu’ Arthur yuko mbele yao huku upanga wake ukitoa Nuru kali inayoumiza kiasi cha kuwafanya Charlie na Mobses kufumba macho kwani walionekana kuathirika na huo mwanga.
“Msifikirie mnaweza kututoroka , hatujaja hapa kupiga vigelegele”Aliongea Arthur huku akipeleka upanga wake unaotoa mwanga upande aliosimama Moses , huku ukitoa miale miale , na Moses aliukinga na upanga wake huku akibadilika na kuwa mtu mwusi Tii , kama sanamu.
“Dogo usipende kuwa na dharau juu ya mshindani wako..”Aliongea Moses kwa sauti ya hasira, huku akipiga sarakasi ya hewani na kurudi mita kadhaa nyuma.
Pambano lilikuwa la aina yake , wanajeshi wa Tanzania wa kitegno cha uchawi waliokuwa wakiongozwa na Ajenti flamingo walikuwa wakipigana na mtu mmoja mmoja kwa wakati mmoja na kosi la’ Dark Parliament’ walionekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa kimapigano , kwani licha ya kuwa wachache waliweza kukinga mapigo yaliokuywa yakija kwao kwa kila namna.
Archimonde na Gabriel na wao walikuwa wakipigana upande wa juu angani , na kilichosikika na kunekana ni miale ya mwanga na harufu ya damu pamoja na upepo mkali, ambao kwa chini yake ulitengeneza kimbunga.
“Fuhiiii…chwaaaa,, tuu”
Lilikuwa ni pigo la aina yake lililotoka kwa Moses kwenda kwa Arthur na kumfanya Arthur kudondoka chini na kumfanya Moses kutabasamu kifedhuli.
“Arthur wewe ni mtoto wa juzi sana , huwezi kushindana na Kabila letu la wanywa damu , ambao tumeishi miaka na miaka pasipo kuzeeka”Aliongea Moses kwa dharau na kumpa ishara Charil wapotee.
“Inamaa…!!!”Ni sauti ya Charlie ikimshitua Moses ainame , kwani kulikuwa na visu vya pembe nne vilivyorushwa kuelekea upande wao. Visu hivi vilikuwa vyeupe lakini muundo wa barafu kama barafu na vilifanya eneo zima kuwa la baridiii ghafla na Moses alijikuta akiinua macho yake na kuangalia mbele na hapa ndipo alipomshuhudia Magdalena ambaye macho yake na yeye yalikuwa yakionekana kama yamejaa maji ya njano yaliokuwa yakizunguka , alikuwa akitisha.
“Mh! Kumbe Magdalena na yeye ana uwezo kama huu , inaonekana amefuzu mafunzo ya juu China”Aliongea Roma kwa sauti ndogo , huku akivunja matawi kuweka sehemu aliokalia vizuri , kwani matako yalikua yakiuma.
“Hizi Sindano za Shaba umetoa wapi , wewe mpumbavu , nasikia hizi zipo kwenye jamii ya wachina pekee”Aliongea Charile kwa hasira akimwangalia Magdalena.
“Usishangae sana , jeshi letu lina wataalamu wengi wenye mbinu nyingi kimapigano , hizi sindano za Shaba mara nyingi kama ningetumia mashine yake zinatoka ishirini na saba kwa pamoja na zinaweza kuua Zaidi ya wanajeshi ishirini na saba kwa wakati moja”Aliongea Magdalena kwa lugha ya kingereza na muda ule ule Wanajeshi wa Kitanzania waliwazunguka Moses pamoja na Charlie wasiweze kutoroka.
“Magdalena kaa nyuma yangu , nitahakikisha nakulinda”Aliongea bwana mmoja hivi wa kijeshi mwenye sura nyeupe kabisa , mwenye Ngozi iliokosa Homoni ya Melanin.
“Unafikiri nahitaji ulinzi wako Jumbe”Aliongea Magdalena kwa dharau na kuendelea kusogea mbele.
“Heheh…. Najua una mafunzo ya juu , lakini wewe ni mwanamke na mimi ni mwanaume”Aliongea Jumbe kwa kejeli lakini Ajenti flamingo hakumjali kabisa. Aliona Jumbe anaongea upuuzi.
Mapignao kati ya Archimonde na Gabriel yalikuwa ni ya moto sana , lakini Archimonde alionekana kuchoka mno na Gabriel alikuwa bado anaonekana kuwa na nguvu ya kushinda pambano na sasa walikuwa wakiangaliana kama machui kwani walikuwa wameminyana huku mapanga yao yakiwa yamegusana ,na Gabriel alikuwa akiathiriwa mno na harufu ya damu ya Archimonde.
Ukweli kutokana na mwanga uliokuwa umekisiri ndnai ya hili eneo , uliwafanya hawa wanajeshi wa Kabila la wanywa damu kutoweza kutumia uwezo wao wote , kwani walikuwa wakiathirika mno na mwanga na kundi la Gabriel lilionekana kutumia upenyo huo kwa faida ya kuwazidi nguvu.
Charlie na Moses , pamoja na wajeshi wao waliungana pamoja kushambulia kwa wakati mmoja na Tomasi na Arthur baada ya kuona wameungana walisogea ili kuongeza nguvu , lakini wakati huo huo waliweza kusikia cheko la mwanamke likisikika kutoka magharibi ndani ya msitu huu.
“Hahahaa…. Hahahaaa,,,, hahaha,,,, hahahaa,,!”Aisee lilikuwa ni cheko kama la Shumileta wa Bongo muvi. Na sauti yake iliumiza masikio na lilikuwa na mwangwi.
Muda huo huo alionekana Lilith akitembea kuja upande wao huku nyuma yake akifuatiwa na wanaume takribani kumi na tatu waliokuwa wamevalia suti nyeusi na wote walikuwa ni wazungu na wote walionekana kuwa siriasi mno.
Ujio wao ulifanya mpaka mapambano yasimame kwa muda. na Charlie alitabasamu.
“Lilith umekuja muda muafaka kweli”Aliongea Charlie , Lilith ambaye alikuwa akionekana mrembo kweli licha ya giza , alimwagalia Lilith na kutabasamu.
“Binamu Charlie , jereha lako la mkono lishapona?”Aliuliza Lilith.
“Shukrani ziende kwa panga lako la maafa mkono wangu mpaka sasa hivi haujarudi kwenye hali yake ya kawaida , Binamu hakika upendo wako kwangu haupimiki”Aliongea Charlie kinafiki
“Binamu sikuwa na jinsi juu yako baada ya kuisaliti familia yetu na kujiunga na kundi la SAVATH , hata kama ni wewe ungekuwa kama mimi tu kukufanya nilichokufanyia”Aliongea Lilith na kwa jinsi hali ilivyoonekana , ni kwamba Lilith pamoja na Charlie ni ndugu , ila kila mmoja yupo kwenye kundi lake ,sasa hayo makundi hayakuwa yakieleweka , ila kuna moja ambalo lilikuwa likifahamika kwa jina la SAVATH na lingine lilikuwa likienda kwa jina la Camarilla ambalo ndio Lilith anapotokea.
“Acha kuongea na huyo mnafiki Charlie”Aliongea Moses kwa hasira na Lilith alitabasmau kifedhuli.
“Mdogo wangu Moses najua sisi wote ni ndugu kutokana na kabila letu la wanywa damu , hivyo leo hii sitoweza kushindana na nyie bali tukusanye nguvu zetu kupambana na Wavatican na hili jeshi la Tanzania, ila niwahakikishe tu tukishawamaliza nitaondoka na Holy Grail”
Sasa mpaka kufikia kwenye hali hio kundi la Archimonde waliona waweke tofauti zao pembeni na wapambane kwanza na kundi la Vatican pamoja na jeshi lwa Tanzania kitengo cha wachawi na baadae wataangalia muafaka wan ani ataondoka na ‘Holy Grail’
Ujio w Lilith ndani ya eneo hilo uliongeza uhatari kwani Lilith alikuwa ni moto wa kuotea mbali , alitumia dakika chache tu kufyeka kikosi chote cha wanajeshi wa Vatican na wakabakia watu wanajeshi wa Vaticn tu watatu , yaani Gabriel ,Thomas na Arthur.
Huku upande wa jeshi la wanywa damu wakiwa na nguvu na ari mpya na pambani lilianza upya na ndani ya dakika chache zingine , wanajeshi wa Tanzania wote walifyekwa na panga la ajabu la Lilith lililokuwa limepewa jila la ‘Masacre Blade’ yaani panga la Maafa na kwa historia inasemekana , panga hilo linatumika kuchinja mazombie yaliohujumu jeshi, huko ulaya zamani.
Sasa pambanno likawa ni kati ya Charlie pamoja na Arthur , Gabriel pamoja na Archemonde , Lilith pamoja na Magdalena , huku Thomasi akiwa amejeruhiwa pakubwa na alishindwa kabisa kupambana na alikuwa chini ya ulinzi wa wanajeshi waliokuja na Lilith.
Lilikuwa ni pigo la kushitukiza , Magdalena alijikuta akiwa chini na nguvu zikiwa zimemuishiwa kwani alikuwa amepigwa sehemu ya moyo na Lilith na muda huu Lilith alionekana kama shetani , kwani baada ya kuona Magdalena kashaishiwa na mbinu zote za kichawi , aliona amalizane nae kabisa.
“Magdalena alikuwa amelala chini akikosa kabisa tumaini kabisa la kuishi na kusubiria saa yake ya mwisho , alianza kukumbuka familia yake mama yake , baba yake na pacha wake Mage na alijikuta machozi yakimtoka , alikumbuka mpaka wakati alipojiunga na jeshi baada ya kumaliza chuo na kisha akafumba macho, na Lilith alitabasamu kifedhuli na kuinua ‘Msacre Blade’ kwa ajili ya kumchinjia mbali Magdalena.
“Hata kama umeshindwa kupigana kabisa , hata mbinu ya kukimbia imekushinda”Ilikuwa ni sauti ambayo Magdalena aliisikia vyema kwenye masikio yake na hakuamini kabisa uwepo wa mtu mwenye sauti hio ndani ya hilo eneo.
“Fyuuu ….!”Ilikuwa ni kama upepo wa kimbunga uliopita na hapo hapo Lilith alitupwa mbali na mtaalamu Roma akatua chini kutoka juu ya mti.
“Hades!!!.. “Lilith alijikuta akitoa mshangao wa uwepo wa Roma ndani ya hilo eneo na sio Lilith tu alieshangaa ila hata Gabriel ,Archimonde na Arthur walijikuta wakishituka baada ya kusikia neno Hades likimtoka Lilith.
HAYA ITAENDELEA WIKI IJAYO SIKU YA JUMATANO.
NJOO CHAPU NA 2500 NIKUTUMIE MPAKA TULIPOFIKIA WATSAPP UACHE KUTESEKA NA AROSTO
0687151346 NDIO NAMBA ZA MALIPO. LAKINI PIA UNAWEZA KUNITAFUTA KWA NAMBA HIO WATSAPP
Hio juma5 naiona kama mwezi wa 5 mwakani,...huyu Hades aka Mfalme Pluto aka Mkatoliki ametushika pabaya😂Nimerudi online
Sasa Mkuu wakati tunasubiri kipande kijacho embu fanya bas ku flash back wahusika wa humu labda nani ni nani wa nani.Nimerudi online
Hivyo ni vipande vya mbele boss kuanzia 180 mpaka 200 hizo flash back zipoSasa Mkuu wakati tunasubiri kipande kijacho embu fanya bas ku flash back wahusika wa humu labda nani ni nani wa nani.
Pia ilikuaje Roma akawa na nguvu alizonazo sasa, za kawaida kwenye kupigana na za kichwani pia.
Maisha (historia yake) yake kwa ujumla.