SHEMU YA 174
Goodman alijikuta uso ukimshuka , alijua Roma alikuwa kweli ana njia kumbe alikuwa hana , alijikuta akijiegemeza kwenye kiti kama mtu aliekosa tumaini na ndani ya dakika chache mbele gari ilizidi kuyoyoma na ilikuwa kwenye spidi kali kweli .
âRoma Go to HellâAliongea Edna huku akimfinya Roma kwenye paja la Mguu baada ya kuona Roma anafanya utani kwenye hali ya kifo kama hio , ila Roma hakutikisika Zaidi ya kuchukua chupa nyingine ya wine na kunywa kidogo huku akiendelea kuvuta sigara.
Gari ilisonga mbele na dereva hakuonekana kabisa kusimamisha na Waliokuwa ndani ya gari walioweza tu kushuhudia baadi ya mabango yaliokuwa yamewekwa barabrani ,lisaa la kwanza likapita la pili mpaka yakatimia manne gari ilikuwa kwenye mwendo na mbaya Zaidi hawakuona tena mbango na gari ilikuwaikihama hama kwenye barababara na hali ilizidi kuwa mbaya kwa Goodman kwani alipoteza fahamu na kujilaza na kumfanya Roma atoe tabasamu la kifedhuli.
âNilijiua yuko imara kumbe ni dhaifu kiasi hikiâAliongea Roma huku akimwangalia Edna na mpaka muda huo Roma alikuwa ashamaliza chupa mbili za bia.
âRoma umefanya makusudi si ndio?â
âNini..?â
âNajua ulikuwa na uwezo wa kutoka kwenye hili gari , ila hujataka tu kufanya hivyoâAliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu.
âKweli wewe unasifa zote za kuwa mke wanguâAliongea Roma huku akimshika Edna mashavu , lakni Edna alimpiga na mkono.
âNataka kujua ni wapi wanatupeleka na nia yao ni nini ndio maanaâAliongea Roma ,
âKwa ninavyokujua , nilikuwa nishafahamu tu unafanya makusudi, ila usije ukafanya mambo ambayo yatafanya nichelewe kutimiza majukumu yangu yalionileta Parisâ
âUsijali mke wangu , kwanza kabisa bado hatujafanyana , toke tuoane , siwezi kuruhusu tufe kabla ya hiko kitendoâ
âRomaaâŚâAliongea Edna huku akimkodolea macho huku akimwangalia Goodman kuhakikisha kama amelala, maana maneno ya Roma aliyaona kama mazito , maana yalimfanya aone hata aibu.
Baada ya safari ya muda mrefu wasiokuwa wakijua uelekeo wake , hatimae Gari ile ilipunguza mwendo na kukata kulia ikiacha barabara kuu , ndani ya msitu na mtingishiko wa gari ulimfanya hata Goodman kushituka.
âTuko wapi?âAliuliza Goodman na kumfanya Edna amwangalie Goodman kwa kumkatia tamaa , alijiambia licha ya Goodman kuwa na damu ya kifalme , lakini hakuwa imara.
âHaieleweki mpaka sasa hivi ni wapi tulipo , kwani hii wametuzungusha kwenye barabara nyingi ili tukose uelekeo , hatujui ni wapi hapaâAliongea Edna.
âEdna hatuwezi kufa?âAliuliza Goodman kwa wasiwasi
âSidhani kama nia yao ilikuwa kutuaa nadhani tungekuwa tuashakufa mpaka sasa hiviâ
âMimi nina mawazo tofauti , nahisi wanataka kwanza kuhakikisha tunatoa pesa nyingi kutoka kwetu na baada ya hapo ndio watatuuaâAliongea Roma na kumfanya Goodman kuzidi kutoa macho na kutetemeka.
âRoma acha bwana kumuongoepesa , yaani haupo siriasis kila sehemuâAliongea Edna na Roma alitabasamu na kuona atulie na muda huo huo gari ilisimamishwa baada ya kutembea kilomita kadhaa na milango ikafunguliwa na walionekana wanaume wanne waliokuwa na siraha za bunduki wakiwa wameshikilia pia Tochi kubwa.
Walianza kuwakagua mmoja mmoja na muda huu wote waikuwa hawaonekani sura kwanni walikuwa wamevalia ma helmet makubwa , baada ya kuwakagua kwa dakika , walimmulika Goodman na kutulia kwa dakika na mmoja wao muda ule ule akakodi siraha yake
âKacha Kachaâ
*******
Upande wa Tanzania ndani ya nyumba ya mrembo Nadia , baada ya safari ya Roma na Edna kuelekea Ufaransa kuanza , mrembo huyu alionekana nje ya Balconi , kwenye chumba chake cha kulalia huku akiwa amevalia Bukta ndogo yenye maua maua , akiwa na sweta la mikono mirefu rangi nyeupe , huku , mkononi akiwa na simu upande wa kulia na upande wa kushoto akiwa na Glass yenye mvinyo ,Alionekana kuongea na mtu mrembo huyu kwenye simu.
âNadia umefikia wapi?â
âBoss bado naandaa mpango wa kuhakikisha wanaachana naomba uwe mvumilivuâAliongea Nadia, lakini alihisi kusikia pumzi ndefu upande wa pili.
âHauko siriasi Nadia , narudia Hauko Siriasi muda unaenda na hakuna majibu ya kuridhisha, ni mpango gani huo unaandaa?â
âBossâŚâ
âSikia Nadia mpaka sasa umeshindwa kazi , na leo nasikia Hades na Edna watafika UfaransaâIlisikika sauti hio nzito na kumfanya Nadia Glass ile imponyoke na kutua chini.
âBoss umewezaje kujua juu ya swala hili , naomba usimdhuru Roma tafadhali , nipe wiki mbili ,,, Hapana wiki moja kila kitu kitakuwa tayariâ.
âNadia sijakupigia hapa kusikiliza ngonjera zako,, na mpaka sasa misheni yako imefeli kwa asilimia mia moja na ukae mbali na mimi la sivyo na wewe kifo kitakuhusu , nina watu wangu kila kona ya duniaâIlisikika sauti hio na muda huo mtu aliekuwa akiongea nae alikuwa akiongea kwa lugha ya Kingereza na simu pale pale ikakatwa na kumfanya Nadia wasiwasi uonekane kwenye macho yake na kugeuka kwa ajili ya kupiga hatua kurudi ndani
âArrgh..!âAlijikuta akitoa mlio wa kuumia na ni baada ya kukatwa na kipande cha Glasi iliokuwa imedondoka chini na kupasuka.
******
Upande mwingine nchini Kenya , hali kwa mheshimiwa haikuwa nzuri hata kidogo na hii yote ni baada ya kusikia taarifa kutoka kwa mtu wao aliekuwa ndani ya ikulu Tanzanis , taarifa iliokuwa ikihusiana juu ya Blandina.
âMheshimiwa anapanga kuonana na baba Yake Mzee Kweka kwa ajili ya kumwambia juu ya uwepo wa BlandinaâHio ndio taarifa iliokuwa imemfikia Mheshimiwa Kamau Kamau na kujikuta akichanganyikiwa.
Ukweli bwana huyu hakuwa tayari kuona ukweli unatoka mapema kiasi hicho na ndio maana alikuwa akifanya kila linalowezekana kuzuia jambo hilo na ni jana yake tu pia aliweza kusaini nyaraka zinazohusiana na mpango TASAC mpango ambao ulikuwa ukihusiana na taifa la Urusi na hiyo yote ni katika kuzuia siri yake aliokuwa nayo kwa muda mwingi isifahamike.
âNoo..!Hapana hili swala lazima lisifanikiwe kwa namna yoyoteâAliongea Mheshimiwa Kamau na kisha alivuta simu yake aina ya Google Pixel , Siku zote ukimuona Mheshimiwa Kamau akishika hio simu , jua tu kuna jambo ambalo ni baya sana linakwenda kutokea.
âAndaa mazingira , Someone has to be TerminatedâAliongea Mheshimiwa akisema kwamba mazingira yaandaliwe kuna mtu anapaswa kufa.
âName pleaseâ
âSenga KwekaâAliongea Mheshimiwa Kamau.
âCopy thatâIlisikika sauti upande wa pili na simu ikakatwa.
âGumilaaaaâŚ!!!âAliongea mheshimiwa kwa sauti kubwa kidogo akiwa ndani ya hii ofisi yake ya ikulu yenye ulinzi mkubwa sana na baada ya kuongea tu hilo neno Gumilaa ,,, mara muda huo huo kama mwanga wa Radi , ulipiga kwenye Ofisi yake na akashuka mtu kutoka juu pasipo kueleweka ametokea wapi , lakini mtu huyu akiwa mjapani kabisa , tena Ninja aliekuwa kwenye mavazi meusi , huku akiwa ameshikilia panga lake refu , alikuwa na sura ngumu hatari na macho yake ni kama yalikuwa yakitoa damu , lakini ajabu ni kwamba Raisi huyu hakumuongopa hata kidogo huyo mtu.
â Noriko Gumila nataka kujua spidi ya kuua ndani ya kundi la Yamaguchi , inachukua dakika ngapi?âAliuliza kwa lugha ya Kingereza.
âInategemea na aina ya kifoâIlisikika suati nzito.
âKisichokuwa cha kumwanga damu , Mshituko wa moyo, but very Discretlyâ
âThat is ten secondâ
âNoriko najua kabisa sheria moja ya The Doni inakuhitaji kunilinda masaa ishirini na nne , kwasababu umekuwa ukinilinda kila siku tokea nikiwa kiongozi wa ikulu hii , nataka unifanyie jambo mojaâAliongea Mheshimiwa na Gumila alikuwa haeleweki sura yake ilikuwa ikiashiria nini , ilikuwa ni ngumu kumsoma kabisa , na ikumbukwe kwamba moja ya maneno ya Yan Buwen wakati akiongea na Scorpion ni kwamba kila nchi ina angalau Ninja Mia moja ambao wapo karibu na watu wenye nguvu kwa kila taifa , ambao muda wowote wakiambiwa kuua wanaua , sasa halikuwa jambo la kushangaza kwa uwepo wa Noriko Gumila ndani ya ikulu hii ya Kenya , akitoa ulinzi kwa Tageti yake , akiwa chini ya maelekezo ya The Doni.
âSheria zinaniruhusu kutii ombi lako moja tu mheshimiwa kwenye Maisha yangu yote, lakini nikutahadharishe mheshimiwa ningekuacha hai kama tu ningeagizwa kufanya hivyo na ukafanya ombi hilo , lakini kwasababu unataka ombi hili kwa ajili ya kumuua mtu nipo tayari , lakini uelewe kwamba hauna ombi lingine unaweza kufanya kwanguâAliongea Gumila na kumfanya Mheshimiwa kamau afikirie.
âGumila nipo tayari , nifanyie ombi langu hilo moja na baada ya hapo nitaishi Maisha yangu yote kumtii The Doni na kuhakikisha hatokuwa na sababu ya kukupa maagizo ya kuniua Zaidi ya kuhakikisha ulinzi wanguâAliongea Mheshimiwa na Gumila palepale alinyanyua mikono yake juu kama vile anasali na kisha akapiga magoti chini na kugusisha kichwa chake chini kama vile mtu anesujudu kwa dakika kadhaa na kisha akanyanyuka , bwana huyu ukimangalia utadhani ni wale waigizaji wa filamu za kale za kijapani , hakuw hana utofauti wa aina yoyote
âNipo tayari kupokea ombi lako la kwanza na la mwishoâAliongea kwa sauti yenye kitetemeshi.
âAnaitwa Raisi Senga Kweka ni raisi wa Tanzania , nahitaji afe ndani ya masaa mawili kwanzia sasaâAliongea Mheshimiwa kwa sauti ndogo sana na Gumila aliinamisha kichwa chake chini kama ishara ya kukubali na hapo hapo kama Radi alipotea kwenye macho yake.
âNisamehe Senga , wewe ni rafiki yangu , ila ili nchi zetu ziendelee kuwa na urafiki lazima mmoja wetu atoweke kwenye huu uso wa duniaâAliwaza mheshimiwa na kuanza kupiga Simu kwa mtu aliempigia dakika chache zilizopita na ilionyesha alikuwa akimwabia muda halisi wa âTarget kuwa terminatedâ