Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mkuu ,Asante kwa kutupigania aisee , ukinunua simulizi kwa muhisika inatia hamasa na mwandishi anajituma zaidi
Mimi no zenu wandishi wengi ninazo hata status zenu na view daily hahaaaaaa au nikwambie leo umepost nn[emoji3][emoji3][emoji3]
 
SEHEMU YA 176

Roma alijikuta akitabasamu na kupenda kwa wakati mmoja kwa namna ambavyo Goodman alikuwa vizuri katika kazi yake , kwani kwa jinsi alivyomuona aliona kabisa ni sehemu ya kazi yake anapokutana na watu wakubwa kujenga konekesheni.

“The Cromwell Family…Goodman, are you saying that they’re the descendants of the Lord Protector?”

”Ukoo wa Cromwell…Goomna unamaanisha kwamba hawa ni mwendelezo wa uzao wa The Lord Protector?”

“Yes Exactlly! This gentleman here Mr Stern is the heir apparent of the Lord Protector title in the Cromwell clan while Miss Alice is his younger sister given birth by the same mother.”

“Ndio! Hakika , huyu Stern unaweza kusema ndio mrithi mkuu wa Familia ya Cromwell na huyu Alice ni mdogo wake kutoka kwa mama mmoja”Aliongea huku akiwa na mchecheto wa hali ya juu na hata uwoga ulikuwa umepungua.

Lord Protector ni jina la kikatiba alilokuwa akipewa mkuu wa nchi katika kipindi cha ‘Common Wealth of England’ kwa kuzingatia nguvu ya kikanisa enzi hizo , sasa basi katika historia ya Uingereza , Oliver Cromwell ndio mtu wa kwanza kupewa cheo hiko cha Lord Protector baada ya kushinda vita (War of Three Kingdoms),Vita vilivyokuwa vikipiganwa na mataifa matatu yaani Scotland , Ireland na England na Cromwell alitawala kama Lord Protector mpaka pale alipokuja kushindwa katika vita vingine na Charles Mfalme wa pili na kuchukua utawala na kuanzia hapo jina la Lord Protector halikutumika sana na ndio maana ni ngumu sana kulisikia huko duniani, kwani lilibakia katika historia , lakini hio sio kweli kulingana na vitabu vya kihistoria vya Uingereza , ukweli ni kwamba licha ya kwamba Cromwell aliuliwa kipindi hiko lakini ukoo wake haukuangamizwa , Ukoo wa Cromwell ulibakia na kuendesha Maisha yao pasipo kuwa na uongozi wa juu ndani ya serikali lakini kutokana na kwamba hapo mwanzo Oliver alikuwa mkuu wa nchi basi utajiri wake haukupotea na ulienda moja kwa moja kwa familia yake, na kwanzia kipindi hiko Cromwell Familly wakaanza kujitengenezea koneksheni ndani ya taifa la Uingereza na hata kuendesha taasisi za siri sana na unachotakiwa kuelewa pia ni kwamba hii familia ndio wenye nguvu katika kanisa la Pretsbyrean Church, hapa kumbuka Archimonde wakati akiwa ameshikilia Holy Grail alivyokuwa akiongea na Moses na kusema wanapaswa kufikisha kikombe kwenye kanisa la Pretsbyrean Church.

Kuhusu hili kanisa nitaelezea mwishoni kama kujazia , lakini unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba kupitia Pretsbyirean Church ndio kulitokea makanisa ya waprotestant waliosambaa huko Marekani na kuna kitu kinaitwa ‘Five Solas’, kuna mambo mengi hapa ya kuelezea ndugu msomaji ambayo yanawaunganisha Cromwell na Dark Parliament.

Hivyo Edna kusomea Oxford Uingereza ni lazima angeweza kusikia kuhusu historia ya ukoo wa Cromwell, kwahio haikumshangaza Roma kwa Edna kuifahamu familia hio.

“Kwahio kumbe wewe ndio mrembo Edna kutoka kampuni ya Vexto kutokaTanzania?, Umrembo kama nilivyoweza kusikia Habari zako”aliongea Alice na kumfanya Edna kushangaa inawezekanaje watu kutoka ukoo wa Cromwell kumfahamu.

“Kwenye macho yangu wewe ndio mwanamke mrembo kuliko wote ndan ya dunia hii”Aliongea Stern na walianza kubusiana , kitu na dada yake na hilo wala halikumshangaza Roma ila kwa Edna lilimshangaza.

“Umesema hawa ni ndugu kwanini ni wapenzi?”Aliuliza Edna akimwangalia Goodman.

“Ni wapenzi ndio na inafahaika ndani ya uingereza yote na hata familia yao haipingi hili swala na wanabaraka zote,hivyo sio siri,nadhani ushawahi kusikia msemo wa ‘Maintaining the Pure Blood’?”Aliongea Goodman na kumfanya Edna kutingisha kichwa kwa kuelewa

“Bebi Edna usishangae sana , hili sio jambo jipya , ukweli nishaona mambo kama haya yakitokea , hata hivyo sioni ubaya kwa kaka kumtamani dada yake kisa ni mrembo”Aliongea Roma huku akitoa cheko la kinafiki.

“Unaonekana kujua mengi?”Aliongea Edna huku akimfinya Roma mkononi kiasi cha koti kutaka kumdondoka na Roma alimvalisha vizuri na kisha akachuchumaa na kuwamulika tena usoni.

“Mnaonaje sasa mkiacha kuvyonzana , na mkatueleza mmefikaje hapa , na hali yote kwa ujumla?”Aliongea Roma.

Baada ya Roma kuuliza , Stern alimuachia dada yake na kisha kumwangalia Roma.

“Hata sisi hatujui hali inayoendelea hapa , ukweli ninachojua tulitekwa mchana kweupe wakati tukiwa tunatoka hotelini na tulifunikwa na vitambaa na ninachojua tu ni kwamba hapa hata simu mawasiliano hakuna kabisa ,Halafu nimekumbuka pia inaonekana kuna vyumba vingine , kwani niliweza kusikia sauti ya mwanamke ikitoa kilio ikiomba msaada naamini kuna wenzeru pia”Aliongea .

“Unamaanisha zile tetesi za watu matajiri kutekwa ndani ya jiji la Parisi ni za kweli?”Aliuliza Goodman.

“Nani anaweza kujua,Sisi tumekuja hapa Paris kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Fasheni na hatujui kitatokea nini baada ya hapa , lakini mimi sijali sana , ilimradi nipo na mpenzi wangu Alice”Aliongea Stern na kumwangalia Alice na wakaanza kudendeka tena.

Roma aliwapuuza na kuwaza kutumia uwezo wake kujua mazingira yote ya hili eneo na aliweza kushuhudia watu wengi waliokuwa kwenye vyumba vingine kama walichokuwepo na kushangaa lakini pia kujiuliza kwa Pamoja , kwanini watu hawa wameletwa hapa na waliowaleta hawafanyi chochote.

“Stern Mpenzi nanuka jasho nataka nikaoge , ongea na hao walinzi basi”Aliongea Alice baada ya kujitoa kwenye mwili wa Stern huku akijidekeza,

“Miss Alice huu sio muda wakufikiria kuoga , tunapaswa kufikiria njia za kujikoa”Aliongea Goodman

“Kwanini siruhusiwi kuoga kisa nimetekwa?” Alice alimjibu huku akisimaa na kusogelea upande wa mlangoni.

“Kitendo unachotaka kufanya ni Harari Alice”Aliongea Goodman

“Usijali hakuna cha kunipata kwa urembo wangu huu niliokuwa nao”Aliongea akitabasamu kwa namna ya kushawishi na kumfanya Goodman ameze mate, maana ni kama kahaba aliekuwa kazini.

“Bam,Bam Bam”

“Jamani hebu mkuje hapa , ninataka Kwenda kuoga mimi”Aliongea Alice huku akigonga chuma kwa nguvu na sauti kusambaa.

“Wanaonekana kama hawana akili vizuri wewe huwaoni , inakuaje mtu tupo kwenye hali kama hii halafu akafikiria kuoga?”Aliuliza Edna kwa Kiswahili.

“Usiwajali sana , waone tu kama watu wa kawaida”Alijibu Roma kwa Kiswahili.

Mshindo wa viatu uliwasogea na ndani ya sekunde alionekana mwanajeshi aliekuwa ameshikilia bundui lake na akamwangalia Alice.

“Hatuna huduma ya kukuogesha humu , tunaweza kukupa maji tu na chakula”

“Mhmh jamani kaka jambazii… mbona unakuwa na roho mbaya hivyo, nataka Kwenda kukojoa na kujisafisha mwili , usiniambie unataka mwanamke mrembo kama mimi nikojoe hapa ndani”Aliongea Alice kwa kujidekeza kwa kaka jambazi.

“Hahaha… Stern dada yako bwana.. hahaha ila ni mcute hatari”Aliongea Roma huku akicheka.

“Roma umeona eh , ndio maana nampenda , huwa namuona Alice kuvutia sana kwa vitendo vya kitoto”Aliongea Stern na Edna aliwaangalia Roma na Stern na kisha akabinua midomo, aliona hao wanaume wanaongea upuuzi.

“Rudi ukae ukatulie usinipigie kelele tena , la sivyo nitakufumua na hii bunduki”

“Usinifanyie hivyo jamani.. kaka Jambazi”

“Usinijaribu Rudi ndani”

“Bebi hawataki ,napaswa kufanya nini mimi nataka kuoga ..”

“Hata mimi mpenzi siwezi kujua ni nini tunapaswa kufanya, Labda Roma na Edna wana njia ya kukusaidia mpenzi”Aliongea Stern.

“Okey!Mimi nitawasaidia”Aliongea Roma akijitolea na yule mwanajeshi hakuwa hata na muda nao na hakujali wanachoongea.

“Hey! Unaonaje mkamsaidia huyu mrembo akatoka kujisaidia?”Aliongea Roma.

“Acha upuuzi tuliza mbupu zako , unakitafuta kifo eh”Aliongea mwanajeshi kwa hasira na kumuwekea mdomo wa bunduki kwenye paji la uso na kumfanya Edna awe na wasiwasi na kutaka Kwenda kumzuia Roma , alikuwa ashasahu kabisa kuwa Roma alikuwa na uwezo wa kimaajabu , na alijawa na wasiwasi.

“Usisogee Edna”Aliongea Goodman akimzuia kwa mkono lakini Edna alimkwepa Goodman , lakini kabla hajafikia mlango mara giza lilitawala kwani simu ya Roma tochi aliizima na kiza kiliendana na milio ya Bunduki ikikohoa risasi kama tatu hivi

‘Bang ..Bang ..Bang’

“Romaa.. Romaa”Aliita Edna kwa wasiwasi kweli baada ya kusikia mlio wa riasisi baada ya kufumba masikio Pamoja na macho kwa sekunde kadhaa na ile anafumbua macho yalikuwa na machozi tayari huku akitetemeka.

Stern alitoa simu yake kubwa na kuwasha tochi na hapo hapo ndipo Edna aliweza kushuhudia mlango ushafunguliwa muda na Roma hakuonekana kabisa ni kufuri pekee lililokuwa limedondoka chini.

Stern baada ya kuona mlango upo wazi alitabasamu na kisha akamshika mkono mchumba wake.

“Stern msisogelee geti mtapigwa risasi na nyie , Roma ashadhurika , hatutakiwi kufanya kosa tena”Aliongea Goodman akiwa anatetemeka akitaka kuwazuia.

“Hey Goodman naona unaniwangia sasa , nani kadhurika?”Ilisikika sauti ikitokea upande wa kona kwenye njia ndefu ya handaki , huku Roma akiwa na Bunduki begani huku mkononi akiwa na ile sigara kubwa aliokuwa nayo kwenye gari na alikuwa akivuta na kutoa moshi kwa wakati mmoja.





SEHEMU YA 177

Sasa Goodman hakuangalia vizuri , ila alipoangalia chini ndipo aliweza kushuhudia Roma akiwa ameegemeza mguuu wake kwenye kichwa cha yule Jambazi Mwanajeshi na Damu zilikuwa zimetapaa chini.

“Wewe..we.. umewezajee!!?”Aliongea Goodma huku akijivuta kwa wasiwasi na kuangalia maiti iliokuwa chini kwenye sakafu.

“Mr Roma nimekukubali sana… nadhani ni muda wa sisi kuondoka , ili nirudi hotelini nikaoge,Ila hao Majambazi wengine unadili nao vipi”Aliongea Alice huku furaha ikiwa kwenye macho yake , hakuona woga maiti iliokuwa chini yake kama ilivyokuwa kwa Edna ambaye alikuwa akiangalia kiatu cha Roma kilivyokanyyaga kichwa cha Maiti.

“Hehe.. hata usijali mpaka sasa hivi nimeua watatu,Toka uwaangalie nilichokifanya nikuvuta Triger tu na nikashangaa wanadondoka wenyewe”Aliongea Roma huku akitabasamu na Alice Pamoja na Goodman walitoka na hapo ndipo waliposhuhudia majambazi matatu yakiwa chini , na wote walionekana kupigwa risasi za Koromeo .Goodman alimwangalia Roma kwa mshangao na kujiuliza huyu Roma ni nani haswa , wakuweza kufanya yote hayo kwa sekunde tu.

“Hapana haiwezekani?”Aliongea kwa sauti Goodman.

“Kwanini isiwezekane Mdogo wangu Goodman , ngoja nikuonyeshe tena ninavyoweza”

Bang! Bang Bang!

Roma alisambaza Riasi upande wa kulia kwake kwenye kiza kwa spidi .

“Haha ..Mdogo wangu Goodman iko hivyo , ni rahisi sana”kusema ukweli hapa Goodman alimuona Roma yeye ndio kama Jambazi , kwa jinsi alivyokuwa akitoa moshi wa sigara na pua zake , aliona kinachomtofautisha Roma na Jambazi ni nguo safi pekee alizovaa.

“Halafu mimi sio mdogo wako”Aliongea Goodman.

Wakati huu Edna na yeye alisogea taratibu mpaka aliposimama Roma huku akiwa na uso wa ukauzu hatari , lakini licha ya hivyo machozi hayakujificha kwenye macho yake , alimkata jicho Roma.

“Edna kwani…”

“Unaona ni sifa sio , kisa umeua majambazi Eeh, unajiona mwamba sana hapa ndani na unatufanya tuogope…Unapenda kufanya wenzako tuwe na wasiwasi kwa ajili yako..?,Nakuuliza?”

“Aa…!”Roma alishindwa hata kujitetea , maana Edna licha ya kuwa na machozi , lakini Jazba yake ilikuwa waziwazi., na Edna hakutaka hata jibu alitoa simu yake kwenye mfuko wa suruali ya Jeansi na kisha akawasha tochi na kuanza kupiga hatua kusonga mbele.

“Edna kuwa makini , utawashitua walinzi”Aliongea Goodman huku akimsogelea kwa spidi , akiwa na wasiwasi.

“Nitakuwa sawa”Aliongea Edna akizidi kusonga

“Acha kelele hakuna wa kumdhuru”Aliongea Roma akimuongelesha Goodman.

“Kwanini unasema hivyo?”

“Kwasababu wote washakufa”Aliongea Roma na kumfanya Goodman asimame , ni kama hajaelewa vizuri ila Roma hakumjali alimpita kumuwahi Edna na Alice na Stern pia wakampita na kumfanya Goodman na yeye atoe simu yake na kuanza kuwakimbilia kutoka kwenye pango.

Roma alikuwa ashamfikia Edna tayari na walikuwa wakitembea kiupande upande na Roma alitupa siraha upande wa ushoto na kisha akamshika Edna mkono.

“Unafanya nini..?”

“Nakuongoza njia ya kutokea”

“Niachie hata huna haja ya kunijali”Aliongea kwa hasira

“Mke wangu mtiifu usiwe na hasira bhana , nisamehe kwa kukufanya uwe na wasiwasi , sitorudia tena na kila nitakachofanya nitahakikisha na kushirikisha , nikiua tutaenda wote kuua , ..Enhee hata pia nikienda kutafuta warembo”Aliongea Roma na kumfanya Edna Asimame na kummulika Roma usoni huku akimwangalia na Roma aliweka tabasamu la Kifisi na kumkonyeza na kumfanya Edna ashinwe kujizuia kutabasamu.

“Fanya mambo yako mwenyewe , Acha kujimwambafai”Aliongea

“Hehe .. nitafanya chochote ili mradi usikasirike”Aliongea Roma huku moyo wake ukiwa na amani maana alijiambia kumfanya mwanamke kauzu kama Edna kutabasamu ni shughuli kweli kweli., Wengine hawakueweza kuwaelewa kwa lugha waliokuwa wakiongea , lakini Alice na Stern waligundua kitu kutokana na matendo ya Edna na Roma na waliangaliana na kukonyezana na kisha wakatabasamu.

“Jamani eh , hatutakiwi Kwenda moja kwa moja mpaka nje kule , tunapaswa kwanza kutafuta magari yetu kwanza hapahapa ndani kwenye maeneo ya karibu , watakuwa wameyahifadhi huku”Aliongea Roma na Edna aliona Roma kaongea Pointi.

“Aiiii..Jamani nisaidieni”Goodman aliekuwepo nyuma alipika ukulele na kuwafanya wote wageuke na kumwangalia na walipomulika waliona Goodman akiwa ameshikiliwa na Jambazi na mkono kwenye mguu wake na pale pale lile jambazi likamwamchia na kulala tena , lilionekana lilikuwa likikata Roho na hata Edna hakuelewa ni namna gani Roma aliweza kuua watu wote kwa wakati mmoja , ila hakutaka hata kuuliza , ilimradi walikuwa salama.

“Goodan ashakufa huyo”Aliongea Edna na Goodman alinyanyua macho yake na kuangalia na kweli yule Jambazi alikuwa ameshakufa,lakini Roma baada ya kuangaza macho upande wa kushoto alijikuta akitabasamu baada ya kuona gari lao walilokuja nalo , na kufanya kila mtu kutabasamu akiwemo Alice alieshangilia kabisa na kuonekana kama mtoto alieharibiwa kwa kudekezwa.

“Edna usikae huko , njoo tukae mbele na mimi, Goodman atakupigia makelele ya ajabu ajbu”Aliongea Roma na kumkonyeza Edna na kisha akafungua mlango na kumvuta Edna na kuingia na yeye akizunguka na kuingia ,na ndani ya dakika nne wote walikuwa kwenye gari na Roma aliwasha taa za gari baada ya kufanya mautundu yake na eneo lote la msituni kuwa na mwanga.

Lakini ajabu ni kwamba eneo lote lilikuwa na miili ya wanajeshi waliokufa na kumfanya Goodman kushaangaa,

“Nani alikuja kuwaaua?”Aliuliza Goodman akimwangalia Stern na Alice.

“Goodman unasahau haraka , Si Mr Roma alisema ndio kawaua wote, Bebi tuachane nae bwana anasumbua hadi anakera”Aliongea Stern akimvuta Alice kifuani,..

Edna na yeye aliekuwa amekaa upande wa Dereva na Roma alishuhudia miili hio na kumwangalia Roma.

“Wakati unaua watu wote hawa na giza totoro ulikuwa ukiwaona mmoja baada ya mwingine?”

“Mke wangu haijalishi na namna gani nilivyowaua , ila washakufa tayari na hawana thamani tena”Aliongea Roma na Edna alinyamaza.

“Tunaelekea uelekeo wa wapi sasa kutoka hapa?”

“Tutaelekea Parisi mke wangu”

“Unajua hapa tuko wapi na njia ya kuturudisha unaijua maana naona msitu tu mbele”

“Hapa tupo kaskazini mwa Paris msitu wa Romilly-sur-Seine,kutoka hapa mpaka mjini ni kama masaa mawili , ngoja tuwahi tukapige msosi wa maana mke wangu”Aliongea Roma na kukanyaga pendeli ya spidi kwa nguvu na gari ikanguruma kama Simba na kufyatuka Kwenda mbele.

“Punguza mwendo Romaa..”

“Hahaha…Funga mkanda nina njaa nataka niwahi”Aliongea Roma na kumfanya Edna azidi kuwa na wasiwasi na sekunde tu kama mshale waliingia kwenye barabara ya Rami , na Roma aliona hii ndio raha ya kuwa kwenye mataifa makubwa kwani Rami ni mpaka misituni.

“He is Crazy ….”Aliongea Goodman kwa sauti , huku akiogopa mwendo wa Gari maana alishuhudia vimiti vikipishana kwa kasi, lakini kwa Stern na Alice waliinua Glasi za Wine juu.

“Cheers!!”Waligongesheana kwa kujipongeza na kisha kupeleka kinywani na kunywa kwa furaha, yaani hawakujali kabisa kinaochendelea kwao kila jambo ni fursa na walionekana kutimiza Fantansy zao , Kwanza walishatimiza Fantansy ya kufanya mapenzi wakiwa wametekwa jambo ambalo walikuwa wakiliota kwa muda mrefu , lakini sasa hivi Roma anawakamilishia Fantansy yao nyingine ya kunywa Wine kwenye gari iliokuwa kwenye mwendo kama wa mashindano.,watake nini , Pesa kwao haikuwa tatizo , Mapenzi wanayo ya moto moto na isitoshe ni kaka na dada , wasingeweza kuachana.

Dakika chache mbele Edna aliweza kushuhudia mto maarufu ufahamikao kwa jina la Seine , na kwa mbaali akiliona jiji la Parisi likionyesha mataa , na wakati akiendelea kushangaa , mara gari ilisimama na Roma alifunuga mlango na kutoka.

“Unafanya nini tena Roma?”

“Mke wangu nimesahau kuripoti kwako , nadhani unakumbuka kuwa mle ndani hatukua peke yetu , nataka niwe msamalia mwema leo kwa kuwasiaida”Aliongea Roma na kutoa simu yake mfukoni na kubonyeza bonyeza na kisha akaweka sikioni

“Anafanya nini tena?”

“What is he doing?!”

“Mr Goodman, it looks like you have night blindness. Isn’t Mr Roma making a call?”Aliongea Alice huku akimpuuza kwa kumwambia atakuwa na upofu wa kuona kwenye giza.

“Look at the situation! Why is he making a call now?!”

“The signal was jammed inside the Cave. I guess it’s an urgent one.”Aliongea Akimaanisha kuwa ndani ya lile pango kulikuwa hakuna mtandao ndio maana.

Lakini sasa muda huo huo wakati wakiwa ndani ya eneo hili la msitu , mara mivumo ya gari kutoka upande wa kulia ziliwashataa huku zikija kwa kasi.

“Damn it , Their Backups are here”Aliongea Goodman kwa hasira ,ila kwa upande wa Roma baada ya kuona taa za gari hizo zilizokuwa mita kama mia tatu , alifungua tena mlango na kutoa bunduki aliokuwa ameiweka juu ya Dashboard na kutoka nayo huku akiendelea kupiga simu.

Na dakika cheche mbele Roma aliweza kushuhudia wanajeshi waliokuwa kwenye gari aina ya Pickups kampuni ya Jeep zote zikiwa na mabaka baka ya kijeshi huku nyuma yake walikuwepo wanajeshi , na wawili walionekana kubeba Kombola aina ya RPG huku wakilengesha upande wao.

Roma aliangalia gari ya nyuma na ya mbele na kisha lile bunduki akaliweka Begani na kusogea kwa kupiga hatua kadhaa mbele , na kisha akatoa tabasamu la Kifedhuli.

“Nimemisi sana haya mambo, kwa muda mrefu”Aliongea Roma pasipo kuwa na wasiwasi na Gari iliokuwa mbele yake ilizidi kumsogelea kwa spidi kubwa na ni kama ilikuwa ikitaka kumgonga , lakini Roma aliendelea kuiangalia huku akiweka kisimu chake mfukoni.
 
Back
Top Bottom