SEHEMU YA 219
Ni siku ya asubuhi , siku nyingine baada ya Roma kumuahidi Edna kwamba ataelekea Kenya kwa ajili ya kumchukua mama yake , Asubuhi hii Roma alikuwa ashamaliza kujiandaa na ilikuwa ni saa mbili kamili akishuka kutoka juu kuelekea Sebuleni kwa ajili ya kuaga ili aondoke.
Jumla ya wanafamilia wote walikuwepo , Edna Sophia Bi Wema na Yezi walikuwepo wote mezani wakijiandaa kupata ‘Breakfast’ , Roma ilibidi aungane nao kabla ya kuanza safari yake.
“Anko ndio ushajiandaa kwa safari?”Aliuliza Yezi na kumfanya Roma amwangalie na kutabasamu na kisha alitingisha kichwa kuashiria ndio.
“Mr Roma nimefurahi sana hatimae umeweza kuifahamu familia yako, nadhani unapaswa kuwapa taarifa walezi wako”Aliongea Bi wema na kumfanya Roma akumbuke kuwa alishatoa uongo wa kulelewa Marekani na aijikuta akiangaliana na Sophia na kisha akamgeukia na Edna , lakini Edna alionekana kuwa bize na anachofanya.
“Bi wema nitawajulisha naamini watafurahi pia”Aliongea Roma huku akitabasamu.
“Kunywa chai tuwahi , nishakata tiketi”Aliongea Edna.
“ Sister na wewe unaenda?”Aliuliza Sophia.
“Ndio nitamsindikiza Roma….”
“Miss umefanya maamuzi ya busara”Aliongea Bi wema huku akitabasamu , lakini kwa upande wa Roma alishangaa , kwani mke wake hakuwa amempa taarifa kama alikuwa akimsindikiza kuelekea Kenya.
“Wife unaonekana una hamu ya kumuona mama mkwe wako kuliko hata mimi”.
“Sisi wote ni wanafamilia , tukikuacha ukienda mwenyewe ni kama tunakutenga”Aliongea Edna.
Ukweli Edna hakutaka kumuacha Roma aende mwenyewe , alijua tabia ya Roma , hivyo aliona akienda mwenyewe anaweza akajiingiza kwenye matatizo ndio maana akaona ni heri Kwenda nae ili akamchunge.
………….
Kutoka Tanzania mpaka Kenya ni lisaa moja kamili , ukijumlisha na muda wa kupaa na kutua ni takribani kama lisaa limoja na nusu, Saa nne kamili Roma na Edna walikuwa ndani ya jiji la Nairobi wakitoka nje kabisa ya uwanja wa Jomo Kenyata, Edna alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi na suruali pamoja na viatu vya High Heels rangi ya Zambarau, licha ya kuonekana kiofisi Zaidi lakini hakuacha kuonekana mrembo kutokana na mavazi yake na yalimfanya kuonekana mwanamke mwenye kujiamini sana.
Kwa upande wa Roma alikuwa amevaa koti la suti tisheti rangi nyeupe na suruali ya jeans rangi nyeusi na viatu vya Ngozi , licha ya kuoenekana kavaa Simple lakini mwili wake uliojengeka kimazoezi hakuacha kujionyesha kutokana na kutofunga koti la suti.
“Tunaelekea wapi?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma ajikune kichwa, Roma alikuwa amekuja Kenya ila hakuwa na mpango wowote , yeye alikuwa akifikiria Kwenda kumtoa mama yake ndani ya ikulu ya Kenya pekee , kama alivyoambiwa na Mzee Kweka na alikuwa ashajiambia kama atapata ukinzani wowote basi hatosita kubomboa ikulu yote.
“Mr Roma ..!!!”Ilisikika sauti ya mwanaume alievalia kombati za jeshi akiwa mbele yao , ndani ya eneo hili la uwanja wa ndege kabla hawajazifikia Taksi, na mwanaume huyu hakuwa amekuja peke yake , alikuwa na Escort ya magari mawili ya jeshi na gari moja aina ya V8.
Roma alimwangalia mwaname aliekuwa mbele yake , licha ya kuwa katika mavazi ya jeshi , lakini hakuwahi kumuona.
“General Wambai Rai’ ndio jina lililosomeka kwenye kombati yake ya jeshi ambayo imechafuka kwa kuwa na vyeo vingi.
“Naitwa Jenerali Wambai Rai ,Mkuu wa Majeshi”Alijitambulisha mwanaume huyu na kumfanya Edna ashangae , hakuelewa kwanini mkuu wa Majeshi alikuwa akimfahamu Roma.
“Habari General Wambai , limekuwa jambo zuri sana kwa kukutana na wewe”Aliongea Roma na Generali alitabasamu huku akionekana kumkagua Roma juu hadi chini , ni kama hakuwa akiamini mtu aliekuwa mbele yake ni Hades.
“Miss Edna karibu sana Kenya”
“Asante General”
“Nadhani wote mnamaswali mengi juu ya ujio wangu hapa uwanja wa ndege , mnaonaje tukienda kuongelea kwenye gari , maana ujio wangu hapa ni kwa ajili ya kuwapokea”Roma alitabasamu baada ya kugundua kuwa mkuu wa majeshi amekuja hadi hapo kwa ajili ya kumpokea , aliona ni jambo jema kwani dakika chache nyuma alikuwa akiumiza kichwa namna ya kuonana na mama yake.
“Edna alimwangalia Roma , ni kama alikuwa akisubiri aanze kutembea ndio afuatie na Roma alimwangalia na kutabasamu na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea upande wa pili magari yalipokuwa yamesimama.
Wanajeshi waliokuwa wamemleta Generali Wambai walionekana kumwangalia Roma kwa mshangao, ni kama walikuwa na maswali mengi , ila Roma na Edna hawakujali macho ya wanajeshi hao.
“Mr Roma nimepata taarifa za ujio wako hapa Kenya kutoka kwa Afande Kweka , kanipa maagizo nikusaidie na kuhakikisha hakuna mikwaruzano kati ya taifa letu na wewe”Aliongea
“Unaonekana kuwa na uhusiano mzuri na yule mzee?”
“Haha.. Afande kweka ni mwalimu wangu , wakati nilipokuwa jeshini na mambo mengi nimejifunza kutoka kwake , hivyo nampa heshima yake”Aliongea
“Okey Afande nadhani mpaka sasa unajua nipo hapa Kenya kwa ajili ya kuonana na mama yangu , hivyo nadhani ili tusipoteze muda , unaonaje tukielekea Ikulu moja kwa moja maana na uwepo wako itakuwa rahisi na sisi kuingia”Aliongea Roma na Afande Wambai alitabasamu.
“Mr Roma kama nilivyosema nipo hapa kwa ajili ya kuhakikisha ujiio wako ndani ya Kenya hauleti mtafaruku baina ya Tanzania na Kenya na safari hii ni ya moja kwa moja kuelekea sehemu ambayo mama yako yupo”
“Unamaanisha sio Ikulu tena?”
“Ndio M r Roma Blandina hayupo Ikulu ila yupo kambi ya Jeshi la Anga Moi”aliongea huku gari ikizidi kusonga mbele ndani ya barabara ya OutRing .
Upande mwingine wakati Roma na Edna wakielekea Moi upande wa mheshimiwa Kamau na yeye alikuwa kwenye msafara akielekea upande wa Moi Airbase na hii yote ni baada ya kupata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wake kuhusu ujio wa Roma nchini Kenya , alikuwa ametoa amri ya vikosi vya jeshi kuchukua hatua kali kama Roma atafosi kumchukua Blandina , lakini oda hio ilionekana kutopokelewa na wanajeshi kutokana na kupewa oda nyingine kutoka kwa mkuu wa jeshi Mwambai Rai.
Sasa mheshimiwa Kamau baada ya kuona wanajeshi hawa wanashindwa kutii amri yake , aliona afanye safari ya kuelekea Moi Aibase kwa ajili ya kumchukua Blandina na kumrudisha Ikulu.
Moi Airbase , licha ya kuwa kambi lakini pia ni sehemu yenye uwanja mkubwa wa ndege ambao unatumika kwa ajili ya kuruka na kutua kwa ndege za kivita na zile za jeshi.
Ndani ya uwanja huu , ilionekana ndege kubwa ya Jeshi ikiwa imesimama huku ikiwa tayari kwa ajili yakupaa na hii yote ni kutokana na Rubani tayari alikuwa kwenye ndege na alikuwa akisubiria amri tu ya kuipaisha.
Nje ya ndege hii alionekana Blandina aliekuwa amesimama na wanajeshi waliokuwa wakimpa ulinzi , alikuwa kwenye mavazi yake ya jana aliotoka nayo Ikulu na alionekana kuwa na shauku kubwa mno kwani macho yake yote yalikua upande wa lango la kuingilia ndani ya uwanja huu wa Ndege.
Dakika kama nne tu hivi ving`ora vya msururu wa pikipiki za wanausalama na magari vilisikika vikikaribia ndani ya eneo hili la uwanja wa ndege, Blandina baada ya kusikia milio hiyo moyo wake ulikosa amani kabisa na hata ile shauku aliokuwa nayo ilimpotea Ghafla , alikuwa ashajua nini maana ya vongora hivyo.
Na ni kweli ndani ya dakika kadhaa tu gari za Mheshimiwa Raisi Kamau Kamau ziliingia ndani ya eneo hili uwanja wa ndege na baada tu ya kusimama Mheshimiwa Kamau alifunguliwa mlango na kutoka kwenye gari na kumsogelea Blandina ambaye alikuwa akimwangalia kwa wasiwasi huku machozi yakianza kujitegeneza kwenye mboni za macho yake.
Wanajeshi waliokuwepo hapa wote walipiga saluti baada ya mkuu wa nchi kufika huku nyuso zao zikijawa na wasiwasi pia.
“Maina mke wangu , nimekuja kwa ajili ya kukurejesha Ikulu , nisamehe sana mke wangu , najua unapitia kipindi kgumu ila tunaweza kuongea na haya yote yakaisha”Aliongea Kamau baada ya kumkaribia Blandina ambaye baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Senga machozi yalianza kufunika macho yake mfululizo.
Muda huohuo kabla ya Blandina hajaongea neno , gari nyingine aina ya Mercedenz Benz iliingia uwanjani hapo na kumfanya Kamau ageuke na kuangalia gari hio na dakika chache tu baada ya gari hio kusimama alitoka mzee mmoja mkongwe sana alieshikiliwa kwenye gari na walinzi waliovalia suti na Mheshimiwa Kamau baada tu ya kumuona mtu huyo macho alijikuta akishangaa na kukosa utulivu.
Wakati mzee yule akiendelea kusindikzwa kwa kushikiliwa kuwasogela Kamau na Blandina gari ya Afande Wambai na yenyewe iliingia ndani ya uwanja huo ikitanguliwa na gari ya wanajeshi na baada ya gari hio kusimama , wa kwanza kutoka alikuwa ni Edna na wa pili alikuwa ni Roma na akafuatia Afande Wambai.
Blandina macho yake yote yalikuwa kwenye gari hio na baada ya kumuona Edna Pamoja na Roma alijikuta akishangaa huku machozi yakianza kumbubujika kwa kasi.
SEHEMU YA 220
Roma kadri alivyokuwa akisogea karibu ndivyo akili yake ilivyoanza kukumbuka sura ya mwanamke aliekuwa mbele yake , licha ya kwmaba kumbukumbu zilikuwa zikija nusunusu.
Moja ya kumbukumbu ambazo zilikuwa zikipita kwenye kichwa chake ni kipindi akiwa mtoto kabisa wa miaka sita , akiwa amevalishwa gauni la Hospitalini huku akiwa amekalishwa kwenye chumba ambacho kilikuwa hakina madirisha Zaidi ya kamera na mwanga wa taa hafifu na mbele yake alionekana mwanaume wa Kizungu alievalia suti huku akimpatia picha.
“Ajent 13 unaitambua hio picha?”Aliuliza mwanaume huyo wa kizungu aliekuwa mbele yake kwa lugha ya Kingereza na Ajenti 13 aliangalia picha hio ya mwanamke wa kiafrika aliekuwa kwenye pozi a kutabasamu na kadri alivyokuwa akivuta kumbukumbu kumfahamu mtu aliekuwa kwenye picha hakuwa akimfahamu hata kidogo na aliishia kutingisha kichwa kuwa hamfahamu na mwanaume yule alichukua picha zile na kuziweka kwenye faili alilokuwa nalo.
“Vizuri sana Ajent 13 kwa leo tutaishia hapa”Aliongea mwanaume yule na kisha akanyanyuka na kuchuua vitu vyake na kuondoka.
Ssa hizi ni kumbukumbu ambazo Roma alikuwa akizipata baada ya kumwangalia mwanamke aliekuwa amesimama mbele yake na alihisi maumivu makali ya kichwa , mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa akifanana kwa kila kitu na picha alizoonyeshwa akiwa kwenye utoto wake , lakini si hivyo tu picha ya aina hio aliiona tena alivyokuwa ndani ya kituo cha kulelea Watoto cha Son And Daughter Orphanage.
“Deniss…!!!!”Aliita Blandina huku akimsogelea Roma kwa wasiwasi kwa nanmna ya kujikokota ni kama haamini mtu aliekuwa mbele yake alikuwa Denisi, wiki kadhaa nyuma alishaonana na mwanaume aliekuwa mbele yake lakini hakuweza kumtambua kama mtoto wake , licha ya kwamba kuna hisia ambazo hazikuwa za kawaida alizipata kwa mara ya kwanza baada ya kukutana na Roma kwenye kituo cha kuelela Yatima lakini hakuweza kumtambua kama mtoto wake.
Siku ambayo anapata kupewa picha za utoto wa Denisi na Linda hisia zake juu ya Roma kuwa mtoto wake wa damu ziliongezeka maradufu, kuna Roho mbili zilikuwa zikimwambia Roma alikuwa mtoto wake na kuna Roho nyingine ilikuwa ikimwambia Roma sio Denisi lakini ambayo ilikuwa na nguvu ilikuwa ni ya Roma kutokuwa Denisi ilikuwa na nguvu kubwa.
Blandina alijiambia siku kadhaa nyuma kwamba kama Roma angekuwa ni Denisi basi angeweza kumtambua siku ileile kama ni mtoto wake hivyo hata wazo la Roma kufanana na Denisi alilipotezea , lakini muda huu sasa mawazo yake anagundua hayakuwa sawa hata kidogo na Roma ambaye hakumdhania kuwa Denisi ndio yeye mtoto wake.
“Denisi…!!!!”Aliita kwa mara ya pili Blandina huku akimsogelea Roma.
Lakini kwa upande wa Roma alishindwa kutembea Zaidi ya kusimama huku akimwangalia Blandina , lakini kama ilivyokuwa kwa watu waliokuwa hapo ndani wakiwaangalia ,kwa upande wa Roma ni kama macho yake hayakua hapo bali yalikuwa sehemu nyingine kabisa , ni kama alikuwa akikumbuka sauti hio ikimwita lakini hakuweza kufahamu ni muda gani na mwaka gani sauti hio ilikuwa ikimwita.
Mawazo yake hayakuwa uwanjani hapo kwa muda huo , lakini yalikuwa kwenye tafakari nyingine kabisa na hata Blandina alivyomfikia hakuelewa kabisa , Edna aliona mabadiliko ya Roma lakini alishindwa kuongea neno , aliishia kutokwa na machozi na kushindwa hata kujielewa kwanini na yeye alikuwa akilia ilihali swala lililokuwa mbele yake halikuwa likimuhusu.
“Denisi..mwanguuu….hiii..hii….nisamehe…”Blandina alishindwa kujiuzuia na alianza kulia kwa kwikwi na kumkumbatia Roma ambae alikuwa amesimama kama gogo.
“Kamau unapaswa kumwachia sasa Blanidna kurejeaTanzania, kilichotokea hapa ni maagizo ya wazee , tumekaa na tukafikiria na kufanya maamuzi”Aliongea Mzee ambae aliingia hapo ndani ya uwanja, na aliongea kinyonge lakini kwa msisitizo.
“Lakini mze…”
“Nishamaliza kuongea Kamau unapaswa kumwachia Maina kuondoka Kenya taratibu zote za kiusalama juu ya swala hili zishachukuliwa… hatutaki makosa mengine wewe na Blandina mnaliweka taifa hili kwenye hatari ya kiusalama, kama sisi tumeamua kuppotezea hili swala na kuchukua hatua unapaswa kufanya hivyohivyo”AliongeaMzee Gichuru na baada ya kumaliza kuongea aliwapa ishara wasaidizi wake kumrudisha mpaka kwenye gari kwa ajili ya kuondoka.
Mheshimiwa Kamau licha ya kwamba anamheshimu Mzee Gichuru kutokana na mchango wake katika safari yake ya kisiasa , lakini moyo wake haukuwa tayari kwa ajili ya kumuachia Blandina.
“Mr Roma mnapaswa kuondoka”Aliongea Afande Mwambai baada ya kumsogelea Blandina Edna na Roma waliokuwa wamesimama wakifarijiana na kauli hio ni kama ilimshtua Roma aliekuwa kwenye mawazo.
“Roma Asante sana mwanngu kwa kuja kuniona mimi mama yako , hatimae naweza kufa hata sasa kwa amani, sikutegemea kukuona ukiwa hai tena”Aliongea Blandina kwa furaha huku akifuta machozi yake na kumfanyaRoma amwangalie mwanamke anaejulikana kama mama yake aliekuwa akitoa machozi , haikueleweka Roma anahisiaa gani kwa wakati huo.
“Hupaswi kuendelea kulia Zaidi , tumekuja kukuchukua mimi na mke wangu na tutarudi Tanzania ila kama unataka kuendelea kubaki nchini Kenya sitokuzuia maamuzi ni yako”Aliongea Roma pasipo kubadili muonekano wake.
“Edna..!... asante sana mwanangu, umekuwa baraka kila iitwapo leo.. asante sana kwa kuja na Denisi nitaondoka na nyie , siwezi kubaki hapa”Aliongea Blandina huku akifuta machozi na kumshika Edna mikono na kulazimisha tabasamu la uchungu.
“Mama hupaswi tena kutoa machozi , unapaswa kufurahi umeonana na mtoto wako kwa mara nyingine , sisi wote tunafuraha juu ya jambo hili kwako na kwa Roma”Aliongea Edna.
Ukweli Edna mpaka hatua hio hakuelewa hisia zake kabisa , alikuwa na mambo mengi ya kuyafahamu kuhusu Roma mpaka ikatokea wakatengana na wazazi wake , licha ya kusikia maelezo nusu kutoka kwa Afande Kweka lakini bado hakuna alichoelewa kabisa na alitamani kupata maelezo mengine.
“Mr Roma hii ndio ndege maalumu ilioandaliwakwa ajili ya kuwarudisha Tanzania”Aliongea Afande Wambai , alionekana kuwa na wasiwasi mno na alitaka waondoke ili yeye amalizane na mheshimiwa Raisi kwa kukiuka agizo lake.Roma na yeye hakuona haja ya kubakia hapo uwanja wa ndege.
“Afande Wambai asante sana kwa maandalizi haya”Aliongea Roma na kisha alimpa ishara Edna waondoke.
Muda wote ni kama mheshimiwa Kamau haamini kile alichokuwa akiangalia muda huo ,kwanza Roma ambaye alikuwa na faili lake lililokuwa linampamba kwa sifa kibao alimuona wa kawaida sana na alishangaa kwanini watu wanamuogopa.
“Blandina ukisogea hatua nyingine tu ninamfumua ubongo mtoto wako”aliongea Mheshimiwa Kamau na haikueleweka alitoa bastora muda gani , ila alionekana kumlenga Roma Ramoni.
“Mheshimiwa naomba upunguze jazba , hili lishapita”Aliongea Afande Wabai huku akimpa ishara Afande Kamau kuacha anachotoka kufanya.
“Nyamaza wambai wewe ni mnafiki , nimetoa maagizo kama mkuu wa majeshi yote lakini ukaamua kunigeuka, nikitoka hapa ninaanza na wewe”
“Mr Roma narudia tena hatua nyingine mbele nawafumua”Aliongea Raisi Kamau .
“Kamau naomba uweke siraha chini tafadhari.. acha kuwa kama mnyama”
“Mnyama… Blandina unaniita mimi mumeo mnyama?”
“Unafikiri wewe ni nani , nimeishi miaka mingi kwa kuvumilia maumivu ya kuishi na sura ya mtu mwingine hii yote kwa ajili ya kukufurahisha nimejitoa kwa ajili yako kwa miaka yote , ni jambo gani ambalo umenifanyia Kamau mpaka kutaka kunizuia kutokuwa na mwanangu ambaye nilidhania kashakufa .. kwanini unatunyooshea Bastora , kama kweli unahisi utapata amani basi nipige risasi nife kwani sitokuwa na majuto tena kwani nishamuona mtoto wangu”Kamau alisikia vyema maneno ya Blandina na kwa hasira alizokuwa zilimpelekea mpaka kutetemeka mikono.
“Blandina hakuna kitu ambacho nilifanya kwa ajili yangu peke yangu , kila kitu ilikuwa ni kwa ajili yako na yangu , kwanini kwa Zaidi ya miaka yote ambayo tumeoana unaona haina umuhimu Zaidi ya mtoto ambaye kujamuona miaka na miaka, kwanini huthamini juhudi zangu na unataka kuniharibia wakati kama huu..”Aliongea Kamau kwa hasira , uzuri tu ni kwamba wanajeshi karibia wote walikuwa washapewa ishara ya kurudi nyuma mita kadhaa kwa ajili ya kutosikiliza kile kinachoendelea.
“Mheshimiwa kwenye Maisha yangu sitoruhusu mwanamke wangu au mama yangu kupigwa risasi kwa ajili yangu , kama umedhamiria basi inabidi ufanye haraka”Aliongea Roma huku akimrudisha Blandina nyuma.
“Roma…umeniita mama .. umenikubali kama mama yako?”Aliongea Blandina , mwanamke huyu alioenekana kuwa na hatia juu ya mtoto wake Roma.
Kila akikumbuka namna alivyokubali kumtanguliza Denisi kwenye ndege na yeye kubaki nyuma kwa ajili ya kufanya dhambi na Kamau alihisi Roma lazima amchukie juu ya swala hilo.
Roma wala hakumjali Blanidna aliekuwa akiongea , Zaidi ya kumuonea huruma kwani kwa muonekano wake alionekana hajakula chochote kwa muda mrefu na alijiambia huenda ilikuwa jambo zuri kwa kuja Kenya mapema kwani huenda angepatwa na shida kubwa Zaidi.
“Unaonekana hujala muda mrefu , inabidi tuondoke ili ukaoge , upate chakula na kisha upumzike , mke wangu ni Tajiri na nyumbani kuna msosi wa kutosha na isitoshe pia tunae Bi Wema mpishi mzuri , Edna mshikilie mtangulie mbele” Aliongea Roma.
“Okey Sawa , Kwanzia leo mimi mama yako nitakuwa ni mwenye kukusikiliza”Aliongea Blandina huku akijisikia vizuri kwa mara ya kwanza tokea siku alioamini Denisi mtoto wake kafariki.
“Nishasema hamruhusiwi kusogea , sitanii nimeshika bunduki na ninawezakuachia risasi muda wowote”
“Mheshimiwa mimi nimesimama hapa , wewe ndio umeshikilia siraha maamuzi ni yako ya kuachia risasi au lah”Aliongea Roma pasipo ya kuwa na wasiwasi na kwa upande wa Mheshimiwa Kamau hasira zilizidi kuongezeka maradufu.
“Paa.!!!”Ni mlio wa risasi uliotoka katika bunduki alioshikilia mheshimiwa Kamau.