Jaya_lchemist
Senior Member
- Oct 12, 2022
- 123
- 207
Singanojr hupitia wakati mgumu. USUMBUFU!!!!!Mkuuuu tukumbukeee
Kaketu ana moyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Singanojr hupitia wakati mgumu. USUMBUFU!!!!!Mkuuuu tukumbukeee
Mwandishi wa hii stori nakupa pongezi unajua Kaka Sina kinyongo nitakuwa nasoma story zako Mara kwa Mara Ila nakuomba jikite Sana kwenye hizi stori za kijasusi na mapenzi kozi soko lake lipo juu kaka
Bila shaka kakuelewa vizuri kozi umenena pointi
tunasubiria mkuuBadae nitashusha mzigo heavy
OhoooooSEHEMU YA 302
Naam ni siku nyingine ndani ya Japan-Hokkaido, pembezoni mwa bandari ya Ishikari wanaonekana wanafamilia wa familia ya Tajiri Khalifa kutoka Dubai wakiwa wamesimama kwenye mlango wa kuingia kwenye meli ya kifahari ambayo ilikuwa na chata la Emaar , yaani ikimaanisha kwamba meli hio ilikuwa ikimilikiwa na kampuni ya Emaar ambayo ilikuwa chini ya Familia ya Khalifa kutoka Dubai.
Meli hii ilikuwa ni ya kifahari haswa na kufanya hata baadhi ya wajapani waliokuwa pembezoni mwa bandari hii kutamani kujumuika na wageni waliokuwa wakiingia kimakundi makundi.
Familia ya Amina Kanani ikiwakilishwa na baba yake na baadhi ya ndugu wengine pia ilikuwa nje ya mlango wa kuiingilia , huku pembezoni mwa mlango huo kukiwa kumependezeshwa haswa kwa maua ya aina tofauti tofauti , huku chini sakafuni kukiwa kumetandazwa zulia jekundu.
Kila mgeni aliekuwa akiingia hapo ndani alikuwa akikaribishwa kwa bashasha sana kutoka kwa wahudumu waliovalia sare, kama vile ni wahudumu wa ndege kwa jinsi walivyopendeza , lakini pia familia zote mbili zilikuwa zikiwakaribisha wageni hao , ambao walikuwa wanavyeo vikubwa vikubwa , wengine wakiwa ni wanasiasa , huku upande mwingine wakiwa ni matajiri wakubwa sana.
Ukumbuke sherehe hii ilikuwa ikifanyika kwa siri , hivyo sehemu ya eneo hili hakukuwa hata na mwandishi wa Habari Zaidi ya wapiga picha ambao walikuwa wamepewa kazi hio maalumu ya kuchukua kila kinachoendelea ndani ya eneo hilo kama kumbukumbu.
Khatibu Omari mpwa wa Fayezi ndio aliekuwa ni kama mshehereshaji , kwani kwa jinsi ambayo alikuwa akipokea wageni ni kama vile alikuwa akitaka kuweke ‘Impression’ nzuri.
Huyu Khatibu Omari alikuwa ni moja ya vijana ambao walimkejeli Roma Ramoni kipindi alivyohudhuria na Edna kwenye tukio la mnada ulioandaliwa na raisi Kigombola Mlimani City , Mnada ambao uliharibika kutokana na uwepo wa ‘Holy Grail’. Sasa Khatibu Omary alimkejeli Roma mpaka siku hio Neema Luwazo akaingilia.
Lisaa limoja baadae , yaani ikiwa imetimia saa tatu za asubuhi hatimae maharusi , yaani Amina Bin Kanani na Dodi Bin Fayez bin Khalifa walifika ndani ya eneo hilo wakiwa ndani ya Chopa.
Ujio wao ulifanya macho ya watu wote kuangalia juu kabisa ya sehemu maalumu ya kutua kutua kwa ndege(Helpad) juu ya meli hio.
Amina aliekuwa kwenye mavazi ya kupendeza sana ya kitamaduni za kiislamu , alishuka kwenye ndege hio huku akifuatiwa na Fayezi alievalia kanzu na kiremba kwenye kichwa chake , kwa jinsi wanawali hao walivyokuwa wakionekana walipendeza sana na kuendana na kufanya hata mzee Kanani aliekuwa akipokea wageni kuona kabisa alikuwa amefanya maamuzi sahihi ya kumuyozesha mwanae kwenye familia ya kitajiri ya Khalifa kutoka Dubai, kwa jinsi Mzee kanani alivyokuwa akijisikia kwenye mwili wake , alijiambia hata asile chochote kilichoandaliwa ndani ya meli hio kwa ajili ya sherehe , kwani tendo la ndoa tu kwake lilikuwa linamtosha sana , alikuwa akipokea wageni mbalimbali huku mawazo yake yote yakiwa kwenye biashara zake , kila mgeni aliekuwa akimpokea na kutambulishwa kwake alijiambia ndio , huo ndio muda mwafaka wa kujenga koneksheni na hatimae kupanua biashara zake Zaidi na Zaidi , alijiambia ndani ya miaka michache tu ndani ya taifa la Tanzania kampuni yake ya Kanani Group itakuwa kubwa Zaidi hata kuzidi ya Vexto International ambayo ndio namba moja kwa kuwa na ‘Asset’ nyingi, sasa mpango wake ulikuwa ni kuifanya kampuni yake kuizidi ndani ya miaka michache kwa kutengeneza koneksheni na wakwe zake kutoka Dubai , Mzee Kanani hakuwa akihofia sana kuhusu furaha ya mwaname wa pekee Amina , alijiambia mwanae akishaonja utajiri uliopo ndani ya familia ya Khalifa basi furaha itajitengeneza yenyewe automatically , alikuwa akiamini pesa ndio chanzo cha furaha timilifu.
Upande wa Amina licha ya kuwa ndani ya eneo hilo kwa ajili ya sherehe yake , lakini kuna jambo moja ambalo lilikuwa likimshangaza sana , jambo hilo lilikuwa ni juu ya Fayezi, kwani alikuwa amebadilika sana , hakuwa Fayezi ambaye alikuwa akiongea sana , huyu Fayezi ambaye amekutana nae asubuhi alikuwa mpole sana na mkimya muda wote mpaka kumfanya kujiuliza ni kipi ambacho kimempata , ni kweli kwamba Fayezi alikuwa mpole , lakini kwa huyo ambaye yupo nae ndani ya meli hio alikuwa tofauti sana , lakini hata hivyo hakutaka kabisa kusumbua kichwa chake , aliamini kwanza ndoa hio ni ya maigizo na muda si mrefu ataondoka na babe wake Roma Ramoni na Kwenda Tanzania kuendeleza mapenzi yao, licha ya kwamba hakufahamu Roma alikuwa na mpango gani , lakini aliamini kila alichopanga kitaenda sawa.
Amina mpaka muda huo alikuwa ashakubali kabisa Roma hakuwa mtu wa kawaida , kwani kitendo cha kuja Japani kwa ajili yake kilikiwa ni kitendo ambacho mtu wa kawaida hawezi kukifanya hata kama atakuwa na mapenzi ya aina gani , kwani alikuwa akijua kabisa walinzi ambao walikuwa wakimlinda wote hawakuwa wa kawaida , walikuwa ni wanajeshi kutoka kitengo cha Special Forces na ndio maana hata ule usemi wa kwamba hakuna kinachoshindikina mbele ya penzi la dhati , kuona kauli ile ilikuwa ikionyesha udhaifu kwenye hali aliokuwa nayo.
Fayezi alitangulia mbele , huku yeye Amina akiwa nyuma , watu waliaamgalia kwa macho ya wivu sana, wazazi wenye Watoto wao wa kike walikuwa wakiugua ndani kwa ndani kwa wivu, kwani walitamani mabinti zao ndio wawe kwenye nafasi ya Amina kuolewa na mtoto wa Tajiri Khalifa.
Taratibu ya harusi hio ilikuwa hivi , kwanza kabisa wageni wote watashuhudia uvishwaji pete kama ishara ya ndoa chini ya uongozi wa Mashekh , baada ya hapo taratibu zingine za kusherehekea zingeendelea kama kawaida kwa muda wa siku mbili mfululizo ndani ya meli hio ya kifahari.
Meli hio Emaar Cruise Ship iling’oa nanga na kuanza kuambaa ambaa kuyaelekea maji ya katikati ya bahari ikitoka eneo la Ishikari Bay , ilikuwa na safari ya siku mbili kamili kukaa juu ya maji mpaka pale sherehe ya harusi itakapomalizika.
Ndani ya meli , licha ya kwamba sherehe kamili ya ndoa kutokuanza , lakini wageni waalikwa walikuwa washaanza kusherehekea kwa kula vinono vilivyoandaliwa , Raisi Kigombola akiwa ni moja ya wageni waliokuwa wakifurahia, roho yake ilikuwa nyeupe sana , kwanza kabisa alikuwa akijisikia ufahari wa hali ya juu sana kuwa moja ya watu wa karibu na familia ya Khalifa , ijapokuwa ukaribu wake na familia hio uligharimu kipande cha Ardhi ndani ya taifa la Tanzania na Wanyama mbalimbali kutoka mbuga za taifa , lakini yote hayo aliona yalikuwa ni mawazo sahihi kuyafanya wakati ule akiwa kiongozi wa taifa.
Runinga za kutumia teknolojia ya OLED zilikuwa zimefungwa kila kona ili kumfanya kila mgeni kuwa shahidi wa kushuhudia ndoa hio kati ya Amina na Fayezi , kwa jinsi mpangilio wa kiufahari ulivyokuwa hapo ndani ni lazima ungemuona Amina kama mwanamke mwehu kuwahi kutokea katika ulimwengu wa sasa , yaani mtu anakuwa analazimishwa kuolewa na familia Tajiri kama hio eti kisa tu hana mapenzi na mwanaume anaetaka kumuona , walimwengu wangemshangaa sana , kwani ni wanawake wangapi ndani ya dunia hii wameacha wapenzi wao wanaowapenda sana na Kwenda kuolewa na wanaume wenye pesa? ,nani kamwambia watu wanaona kwasababu ya mapenzi? , sasa kuna utofauti gani kati ya Amina na wanawake wengine , hakika wanawake ulimwenguni wangemshangaa kwa maswali ya namna hio.
Kanani na Mzee Khalifa walikuwa wakiongea kwa furaha sana, wote kwa Pamoja wakiwa waemvalia kanzu huku upande wa juu wakisindikiza na koti la suti na kuwafanya kupendeza sana kwa mahadhi yao ya uvaaji wa kitamaduni.
Baada ya lisaa kupita hatimae mashekhe waliokuwa wakitakiwa kufungisha ndoa hio walikuwa wamekaa katika eneo maalumu, huku upande wa kulia kukiwa na wajomba kutoka familia ya Khalifa na upande wa kushoto pia kukiwa na wajomba na ndugu kutoka upande wa familia ya Tajiri Kanani.
“Unamaanisha nani kapotea?”Ilisikika sauti ya Khatibu ikiongea kwa kwa mshangao na kwa juu kabisa kwa lugha ya kiarabu , huku akimwangalia msaidizi wa karibu wa Fayezi.
Kwa maelezo ya mhudumu huyo ni kwamba Fayezi haonekani na ndio maana Khatibu alishangaa na kuuliza kwa nguvu , sasa maneno yake yaliwafanya Masekhe Pamoja na wajomba kuuliza ni nini kinaendelea.
“Khatibu ni nini kinaendelea?”
“Anasema eti Fayezi haonekani , wakati mtu aliingia hapa ndani ya meli wote tukamshuhudia , huyu mtu atakuwa ameghafirika ala”Aliongea.
“Mpumbavu , kama unatudanganya basi tambua nitakurusha kwenye maji ya bahari”Aliongea Khatibu kwa hasira , alishindwa kuamini kama mpwa wake Fayezi anaweza kupotea wakati kila mtu alimuona akiingia ndani ya meli hio.
“Siwezi kudanganya , ni kweli kapotea nilikuwa kwenye chumba kimoja nikimwandaa kwa ajili ya kutokeza kwa tukio , lakni nilivyomgeukia kwa mara ya pili kwenye chumba chake baada ya kumpa kisogo hakuwemo”Aliongea yule msaidizi kwa namna ya wasiwasi kabisa na maneno yake yaliwafanya kila mtu kuwa na wasiwasi na walijikuta wenyewe wakinyanyuka.
Upande wa pili Amina alikuwa akisubiia Fayezi atokeze na yeye ajongee mpaka sehemu maalumu kwa ajili ya ndoa yao kufungwa , sasa wapambe wake walimnong’oneza na kumueleza kuwa Fayezi haonekani na Amina alishangaa kidogo huku akijiuliza je kupotea kwake ni mpango wa Roma, lakini hakutaka kuonyesha utofauti.
“Is this something you did? Where is Fayez?”Sauti ya Kanani ilimshitua amina aliekuwa kwenye mawazo.
Sasa unachotakiwa kuelewa ni kwamba siri ya Amina kutotaka kuolewa na Fayezi ilikuwa ikijulikana kwa watu wachache sana , yaani Fayezi mwenyewe na mzee Kanani Pamoja na Amina , na hata kufungiwa kwa Amina hapo Otaru mpango huo familia ya Fayezi hawakuutambua kabisa.
“Something I did? You dragged me to Japan, forcefully I might add, and I have been kept monitored ever since. This place is within the domain of the Khalifa Clan, what do you think I can do here? He’s a living man, what can I do to him?”
“Nimfanye nini mimi? , umenileta kwa nguvu Japani na nilikuwa nikifuatiliwa kwa kila kitu tokea hapo, juu yayote hili eneo lote lipo chini ya ukoo wa familia ya Khalifa , unafikiri ninaweza kufanya nini hapa , yeye ni mtu na pumzi zake naweza kumfanya nini mimi?”Aliongea Amina kwa hasira akimjibu baba yake mara baada ya kumuuliza ni yeye ndio kafanya mpango wa Fayezi kupotea.
Licha ya kumjibu hivyo Amina kwenye moyo wake alikuwa akichekelea , mwanzoni alikuwa na wasiwasi , kwani aliamini kama ndoa itafungwa kabla ya mpango wa Roma , basi kwa taratibu za kidini atakuwa ni mke halali wa Fayezi , lakini sasa kupotea kwa ghafla kwa Fayezi kulimridhisha sana na kuona yes, mpango wa babe wake Roma unafanya kazi.
Vikosi vya ulinzi vilipewa jukumu la kutafuta kila kona ndani ya meli hio kumpata Fayezi , lakini kwa takribani dakika kumi zote hawakuweza kumpata , Fayezi hakuonekana na kufanya familia kuwa katika sintofahamu na wasiwasi juu.
“Boss Angalia ..!!!”Aliongea kijana mmoja mlinzi akimwamrisha Khatibu kuangalia Skrini za runinga zilizofungwa kila kona ndani ya meli hio na baada ya Khatibu kuangalia alijikuta akikosa pumzi na sio kwake tu hata kwa Tajiri mwenye mtoto , Khalifa alijikuta akiwa kwenye mshituko mkubwa.
Kwenye runinga hizo kilichokuwa kikionekana ni sura halisi ya mtu waliekuwa wakimtafuta , Fayezi alionekana akiwa kwenye chumba cha kiza ambacho kilikuwa na mwanga hafifu , huku akiwa amefungwa Kamba mwili mzima akiwa hana nguo hata moja akiwa amekaa kwenye kiti , jambo la kuogofya Zaidi ni kwamba Fayezi hakuwa peke yake , kulikuwa na mwanamke bonge la jitu , ambaye alikuwa na tatoo mwili mzima kwanzia mgongoni mpaka kwenye makalio , mwanamke huyo alikuwa amekalia msumali wa Fayezi huku akiangusha kwa spidi zote, upande wa bwana Fayezi alikuwa akigugumia , sasa haikueleweka migugumio yake ilikuwa ni utamu au ni maumivu , lakini usingeweza kutofautisha kwani kilichosikika ndio kilichozoeleka kusikika pale wanaume wanapokuwa wakipata utamu wa kiwango cha ‘SGR’ wakiwa kunako sita kwa sita,
Fayez alionekana kuchoka mno , midomo yake ilikuwa imepauka mno , haikueleweka kafanyiwa nini , lakini kwa hali ilivyokuwa ilionekana ni kwamba muda wowote anaweza kupoteza fahamu , kilichokuwa kikishangaza pia ni kwamba licha ya kuwa kwenye hali kama hio , lakini kiungo chakc cha uzazi kilikuwa kimesimama wima.
“Lahaulaa…lala..!!!!, Astghafilulla…!!!!” hayo ndio maneno yaliokuwa kwenye midomo ya kila mtu aliekuwa akishuhudia tukio hilo.
Upande wa Tajiiri Khalifa presha ilikuwa ishapanda kiasi kwmaba muda wowote anaweza patwa na kiharusi na kupoteza fahamu , watu wa karibu wakimwemo wake zake walimsogelea karibu na kumshikilia.
“Zimaa… zima zima zimaa….. huu upuuzi ni feki , sio uhalisia”Aliongea Khatibu Omary huku akisahau kwamba watu waliokuwa hapo ndani ni wachache sana waliokuwa wakielewa Kiswahili.
Lakini hata hivyo walinzi walielewa alichokuwa akimaanisha na paleple waliinua juu simu zao za upepo kuwasiliana na watu waliokuwa wakiongoza runinga hizo , lakini waliambulia patupu.
“Boss tunashindwa kuwasiliana na watu wa ‘Control Room’” Aliongea mlinzi na kumfanya Khatibu kuanza kutembea huku na huko.
“Mnasimama mnafanya nini hapa nendeni kwenye chumba hiko mkazime , wapumbavu nyie”Aliendelea kufoka kwa Kiswahili na ni Mheshimiwa Kigombola na baadhi ywa Watanzania waliemuoelewa vyema , lakini walinzi hao walikuwa wapo shapu kwenye kusoma mtu hata kama kaongea lugha totaufi, palepale walikimbilia kutoka eneo hilo.
“Hahahaha…!!!!”upande mwingine Amina alishindwa kujizuia na kujikuta akitoa cheko na kumfanya baba yake kumwangalia kwa hasira , mpaka hapo alijua huo wote ni mpango wa Amina , lakini alijiuliza imekuwaje mpaka akafanikiwa , kwani kile kinachoendelea ni kama miujiza , kwani haikuwezekana kabisa Fayezi aliekuwa hapo ndani muda mchache uliopita , sasa yupo upande mwingine akifanya mchezo ulikuwa ukionekana mubashara kwenye meli hio , ukishuhudiwa na watu waliokuwa wamekuja kwa ajili ya sherehe yake.
Wakati akifiria mara walinzi walikupushana kuingia ndani ya eneo hili la ukumbi wa sherehe , na kila mmoja alimsogelea boss wake.
“Kuna nini?”Aliuliza khatibu Mshereheshaji
“This is bad! This is bad! Boss! A missile-equipped destroyer is behind us. They sent us a signal warning us that they want to launch a missile at us!”
“Hili ni tatizo boss , kuna mtambo wa mabomu kutoka kwenye meli ya kivita , umeelekezwa kwenye meli yetu na tumepokea Signal na waliopo kwenye meli hio wanatuambia wanataka kulipua meli yetu…”Aliongea Mlinzi mmoja kwa kuhema na maneno yake yaliwafanya kila mtu kupagawa.
SEHEMU YA 303.
Kwenye watu ambao walikuwa wamekasirika kwa kiwango kikubwa sana kwa mvurugiko huo wa ndoa alikuwa ni Khatibu, jamaa huyu alikuwa ni moja ya watu ambao walikuwa wakitaka kwa nguvu zote ndoa ya Amina na Fayezi ifanikiwe , moja ya sababu kubwa ni kwamba alikuwa ameahidiwa na mpwa wake kwamba , ndoa hio ikifanikiwa watamuua Tajiri Kanani kwa sumu na baada ya hapo Khatibu ataendesha makampni ya Kanani Group nchini Tanzania kwa niaba ya Fayezi, hii yote ni kwamba Amina angekuwa ni mke wa Fayezi na katika tamaduni za kiarabu mwanamke mali zake zote zinaendeshwa na mume wake , kwani yeye ndio kichwa, hivyo Amina licha ya kwamba mali za baba yake zingekuwa urithi wake lakini moja kwa moja ungekuwa ni urithi wa Fayezi.
Sasa khatibu mvurugikano huo ulikuwa ukifanya ndoto zake kufifia kabisa, aliamini hatokuwa tena na uhalalai wa umiliki wa mali za Tajiri Kanani.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba licha ya kwamba Kanani kampuni yake haikuwa kubwa kuzidi kampuni inayoendeshwa na Edna , lakini Kanani Group ilikuwa ni kampuni kumi kubwa ndani ya Afrika Mashariki yote, huku Kanani akiwa ni mmiliki wa sheli nyingi za mafuta zilizokuwa Tanzania Pamoja na mabasi maarufu sana yaliosambaa Tanzania nzima, hivyo utajiri huo ulikuwa kwenye ndoto za Khatibu kwa muda mrefu , mpango wao ulikuwa jikoni , alikuwa akitaka ndoa ikamilike na hatua ya pili iwe ni kutekeleza kifo cha Kanani na moja kwa moja mali kuwa kwenye mikono yake kutokana na ahadi ya mpwa wake Fayezi.
Wageni sasa walikuwa washapata taarifa juu ya meli ya kivita inayotaka kulipua meli yao , watu walianza kuhaha yale mawazo ya kutumbua raha ndani ya meli hio yalipotea na kila mmoja alitafuta upenyo wa kujiokoa , licha ya walinzi kuwazuia kutotoka sehemu hio , lakini walishindwa kwani walichomoka na kupanda juu kabisa ya meli hio ili kusalimisha roho zao.
Mheshimiwa Kigombola pia alikuwani moja ya watu ambao walikuwa wakihaha, lakini licha ya hivyo hakuwa mbali sana na familia ya Tajiri Khalifa , alitaka kuonekana ni mwenye msaada kwa namna yoyote ile, hata kama msaada wake hautotiliwa maanani.
Khatibu alikimbilia juu kabisa ya meli mara baada ya kuona wageni wote wametoka , huku akiwa na kipaza sauti chake.
Upepo ulikuwa mwingi , ulioambatana na jua la saa tano asubuhi , meli ilikuwa imepunguzwa mwendo kwa kiasi kikubwa sana na nikama ilikuwa imesimama , upande wa kushoto kwao waliweza kuhuhuduia meli ndogo ya kivita ya rangi ya Silver ikiwa imetaguliza mkonga wake wa kurushia mabomu kuelekea upande wa meli yao , huku bendera ya zama za kale ikiwa juu , bendera ambayo kama ni mfatiliaji wa tamthilia za kijapani ungejua kuwa ilikuwa ikiashiria ‘Pirates’(Majambazi ya baharini).
Sasa mpaka muda huo watu walielewa ni adui gani anataka kuwaangamiza , kila mtu aligeuza macho kulia kushoto na mbele kuona kama kunaweza kuwa na msaada lakini waliona wapo katikati ya bahari na eneo hilo halikuwa hata na dalili ya meli Zaidi ya ukungu unaonekana kwa mbali , ukiashria kwamba macho yao yamefikia ukomo wa kuona Zaidi, magoti ya miguu yao yalilegea mara baada ya kuanza kuhisi kifo , huku wenye presha wakiitafuta hewa kwa taabu.
“Jamani naomba tusikilizane , hakuna haja ya kuogopa , ijapokuwa meli ya kivita iliokuwa mbele yetu ni ya majambazi wa baharini , lakini sio swala la kutufanya kugopa nishapigia simu jeshi la Japani na muda wowote watafika na manuari zao kutuokoa , msiwe na wasiwasi”Aliongea Khatibu kwa niaba ya familia ya Khalifa , alijikuta yeye ndio jasiri kuliko watu wote waliokuwa hapo ndani wakiogopa, lakini waarabu hao na baadhi ya wazungu , walimuona kama kichaa tu , hawakuamini maneno yake kabisa, lakini hata hivyo kwa wale wanaoweza kufikiria vizuri , waliamni manano yao yake yana mantiki ,waliamini kwamba walikuwa kwenye bahari ya Japani na hawakuwa wameingia kwenye ‘international water’ , hivyo Japani haiwezi kuruhusu majambazi kufanya uhalifu kwenye eneo la maji yao.
Lakini dakika hiohio alionekana mlinzi ambaye dakika kadhaa Khatibu alimpa maagizo ya Kuwasiliana na makao makuu ya jeshi la Japani.
“Boss tumepatiwa majibu “Aliongea kwa sauti.
“Jamani tumepata majibu haraka”Aliongea Khatibu kwa kiarabu kabla hata hajajua nini ambacho mlinzi anataka kumwambia.
“Boss! Boss! Not good! Our cruise somehow sailed out of Ishikari Bay and entered international waters! After scanning us on their radar, they said this place didn’t belong to them!”
“Boss Boss, hali sio nzuti , Meli yetu imetoka kwakiasi fuani kutoka eneo lote la Ishikari na imeingia akwenye maji ya kimataifa , baada ya kupigia jeshi ssimu walijaribu kutuskani kwa kutumia rada zao na wametuambia kwamba eneo ambalo tupo sio eneo la Japani , hivyo hawataki kuhusika”Aliongea yule mlinzi kwa kingereza na kufanya zogo kuibuka upya.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kwa sheria za kimataifa , eneo katikati ya maji ambalo lipo umbali wa kilomita ishirini na mbili kutoka kwenye fukwe , linatambulika kama eneo ambalo halina mmiliki kwa taifa lolote lile , sasa chukulia kwa mfano nchi ya Japani ambayo ni visiwa , inachukua muda mchache sana kwa meli kusafiri kwa umbali wa kilomita ishirini na mbili , sasa hiki ndio watu wasichokuwa wamekifahamu , waliamini wamesafiri kwa muda mfupi sana na ndio maana walihisi bado wapo kwenye eneo la maji ya nchi ya Japani kumbe walishaingia kwenye Internnational water.
“Jibu lao ni la kipuuzi , kwanini hawajali haki za kibinaadamu , sisi tumevamiwa na majambazi na kama wanatii sheria za binadamu wanatakiwa kutusaidia , kwanini wanatoa jibu kama hilo”Aliongea mmoja ya maboss waliokuwa hapo ndani.
“Ni kweli uongeayo , lakini unatakiwa kujua kwamba kuna mvutano sana wa kuingiza wanajeshi wa taifa husika kwenye maji ya kimataifa pasipo kupata ruhusa kutoka Marekani , hususani kwa Japani, hivyo taratibu za kutuokoa lazima zianzie Marekani, lakini hata hivyo mnachopaswa kuelewa ni kwamba meli hii ina raia wachache sana wa kijapani sisi wote ni warabu kwa asilimia themanini , hivyo wametuambia tuwasiliane na mamlaka za kiarabu kujikomboa”Aliongea yule mlizi na kufanya watu kuzidi kuwa katika hali ya woga Zaidi na Zaidi.
“Pumbavu kabisa…”Aliongea Khatibu kwa hasira.
“Boss nimesahau pia kukueleza kwamba Kapteni wa meli na mabaharia wote wamepotea pia , hivyo hii ni meli bila Kapteni” Aliongea yule mlinzi na kugongelea Zaidi msumari wa woga.
Upande wa Mheshimiwa Kigombola alianza kuhisi jambo ambalo lilimfanya tumbo lake kugnuruma na kuanza kujilaumu kwanini ameingia mkenge na kuingia kwenye meli hio , alikumbuka vyema maneno ya jana ya Fayezi Pamoja na Yan Buwen , juu ya kifo cha Roma , mpaka apo alihisi kabisa kinachendelea hapo ndani huenda kinahusiana na Fayezi kumchokoza Roma , alikumbuka faili la Roma na kuona kama kweli yale yalioandikwa yalikuwa ya kweli basi ni jambo la kawaida la Hades kuleta meli ya kivita na kutaka kuwashambulia , lakini pia kumfanya Fayezi kufanya ngono huku wazazi wake wakishuhudia.
“Nafikiri najua chanzo cha haya yote”Aliongea Kigombola baada ya kumsogelea Tajiri Khalifa aliekaa pembeni akipumua kwa shida na hio ni mara baada ya madaktari kufanya jitihada za kumuamsha.
“Kigombola unataka kusema nini?”Aliuliza Tajiri Khalifa kwa tabu sana. Na ilibidi sasa Kigombola aanze kuelezea alichofahamu jana kwa kuambiwa na Fayezi, lakini sasa alaivyofiikia kwenye neno Hades , Tajiri Khalifa alijikuta akisimama kwa haraka sana kwa mshangao mkubwa na kufanya hata wake zake na wajomba kushangaa kwanini kashituka namna hio.
Upande wa Tajiri Kanani na yeye alikuwa hapohapo na sasa alipata kusikia alichokifanya Fayezi , ukweli hakuwa na uelewa wowote juu ya jambo hilo na alikuwa akishangaa , lakini alishangaa Zaidi mara baada ya kusikia jina la Hades , kwani hakuwa akimfahamu mtu huyo anaeitwa Hades ni nani mpaka kumfanya tajjiri Khalifa kusimama wima kama mwanajeshi, wakati dakika chache nyuma alikuwa akikaribia kufa.
Amina yeye alikuwa hana wasiwasi , kwanza mavazi aliokuwa amevaa ya sherehe alishayatupilia mbali na kubadilisha mengine na sasa alikuwa amevalia koti lake kwa juu na alitoka na yeye kusimama mbele kabisa ya meli hio huku akiangalia meli ya kivita , huku mawazo mgando mgando yakipita hapa na pele , kuna muda alikuwa na woga na kudhania kwamba meli hio ilikuwa ya majambazi kweli kwani hakuwa akiamini kama babe wake Roma Ramoni anauwezo wa kukodi meli ya kivita , lakini licha ya kufikitia hivyo alikuwa akijiuliza kama huyo sio Roma , Roma mwenyewe na mipango yake yuko wapi , masikini mrembo huyu hakujua kama alikuwa akitoka kimapenzi na mfalme Pluto Aka Hades, aliekuwa akigopwa dunia nzima kwa wale waliokuwa wakiifahamu shoo yake na huenda upande wa pili asiokuwa akiufahamu kuhusu Roma ndio umemfanya kumpenda kupindukia mwanaume huyo lakini pia wanawake wengine upande mwingine wa Roma ndio uliwafanya kumpenda kupindukia pasina kujali anaye mke tayari.a.
Warembo waliokuwa ndani ya meli hio walianza kulia kwa namna kwikwi , walikuwa wakilalamika kwamba bado ni wadogo na wanahitaji kuishi , hawa kustahili kufa wadogo hivyo na urembo wao..
Sasa baada ya kama dakika tano za watu wote kusubiria kujua nini kinakwenda kujili juu ya Maisha yao , hatimae mawasilianno kutoka kwenye meli ya kivita yalianzishwa.
“Good morning ladies and gentlemen. Don’t be surprised by this. I’m the commander of this missile destroyer Hatakaze. My name is Barbour Hussein Makedon, you guys may call me Captain Makedon”
“Habari za asubuhi mabibi na mabwana , msishangazwe sana na hili , mimi ndio kamanda wa hii meli ya kivita ya Hatakaze , jina langu nafahamika kama Barbour Hussein Makedon , mnaweza kuniita Kapteni Makedoni”
“Sasa nitatangaza kwanini meli hii ya kivita imewalenga na kutaka kuwashambulia , familia ya Khalifa ikiongozwa na mtoto wao Fayezi wamemchokoza rafiki yangu mpendwa na kumsababishia makasiriko ya hali ya juu sana, hivyo basi kwakua wengi wenu humo hamna makosa basi ili kutuliza hasira ya rafiki yangu mpendwa nitatoa chaguzi mbili ambazo mnapaswa kuchagua ndani ya dakika tano , kwanza kabisa tuwapate familia yote ya Khalifa waliohusika katika mchakato wote wa kumkasirisha rafiki yangu kwa hiari yao wenyewe pili mbebe dhambi za wote na tuizamishe hio meli , kuwasaidia kwa haraka haraka Bwana Khatibu Omary ni moja ya watu ambao rafiki yangu hapa ameniambia walishawahi kumkasirisha”Aliongea Makedoni na kufanya Khatibu kuanza kuhisi tundu la haja ndogo na haja kubwa likitanuka , hakujua ni rafiki gani huyo ambaye ashawahi kumkasirisha.
“Jamani tulieni wanachojaribu kufanya ni kutupanikisha , hakuna ukweli wowote kwani sijawahi kumchokoza mtu mimi , Maisha yangu yalikuwa ni yenye rehema mbele za mwenyezi”Aliongea Khatibu kiwoga woga lakini Amina alikurupuka na kumjibu kwa nguvu.
“Kwaho kama umeishi kwa rehema ndio sisi wote tufe , hakuna mtu ambaye ashawahi kujitokeza hadharani na kukiri yeye ni mtenda dhambi , hivyo maneno yako hayakubaliki na haatuwezi kufa kwa ajili yako”Aliongea na kufanya watu wote kuunga mkono hoja na kuanza kumwangalia Khatibu kwa macho ya chuki , macho ambayo yalimfanya yeye mwenyewe kuanza kuogopa.
“Yule fala nishamuua , hizi ndio picha za maiti yake Khatibu Bro nilikuambia siwezi kushindwa jambo mimi”Maneno hayo yalianza kuibuka katika kichwa cha Khatibu, alikumbuka jana yake asubuhi aliongea na Fayezi na kumueleza kuwa ameshamuua Roma Ramoni mpumbavu mmoja ambaye alilala na mchumba wake na taarifa hio kumfanya kufurahi sana mpaka kujipa ofa ya kulewa bia nyingi, sasa alianza kuhisi huenda Roma ndio huyo rafiki anaezungumziwa na Makedoni.
“Hapana , kinyamkela kama yule hawezi kuwa na rafiki anaemiliki Meli ya kivita”Aliwaza huku akikanusha kwamba Roma ni mtu mdogo sana na hana koneksheni za kuwa na rafiki kama Makedoni.
“Kabla ya kunihukumu nataka kumfahamu mtu ambaye ananisingizia kwamba nimechokoza , siwezi kufa huku sijui ni nani nimemkosea”Aliongea
“Usijifanye haumfahamu ni huyo huyo unaemfikiria”Aliongea Amina kwa kejeli , lakini sasa familia ya Khalifa haikuwa ikielewa kinachoendelea , kwanza walishangazwa na Amina kutokuwa na wasiwasi , kwani kwanza mpenzi wake amekuwa ametekwa na mpaka muda huo haijulikani kama yupo hai , kwani lile bonge lazma lingemmaliza.
Tajiri Khalifa aliamini kuna mambo ambayo hakuwa akiyafahamu na alimgeukia Tajiri Kanani kutaka maelezo na Tajiri Kanani alikwepesha macho hakuwa tayari kuongea na hapo ndipo ilibidi Mheshimiwa Kigombola kufupisha stori ili kuokoa muda na kuelezea matukio yote ya Dar es salaam, bila kuacha kitu.
Sasa Tajiri Khalifa alijikuta akivuta pumzi na kuelewa kinachoendelea na kuona uzee wake ulimfanya kutofiikiria vyema na kumuacha mwanae kufanya atakavyo , alijilaumu kwa wakati mmoja huku akiwa na uchungu mwingi.
“Naomba kifaa cha mawasiliano”Aliongea kwa tabu Tajiri Khalifa akitaka kipaza sauti kwa ajili ya kuwasiliana na meli upande wa pili na walinzi walifanya hima na palepale aliletewa.
“Ndugu Makedoni tumesikia ombi lako , lakini hata hivyo jambo moja bado rafiki yako hajapata kulifahamu , ni kweli mwanangu huenda amefanya mambo mengi ya kumkasirisha rafiki yako , lakini sisi kama familia hatukuwa na uelewa huo na ndio nimepata kujua kwamba Amina alikuwa akilazimishwa kuoelewa na mwanangu Fayezi nje ya ridhaa yake , jambo ambalo ni kinyume na taratibu za dini yetu lakini pia tamaduni za familia yetu , mwanamke kufungishwa ndoa ilihali sio mwanamwali, haya yote ni makosa yangu mimi kama baba kutokumuelekeza vizuri mwanangu , kama ikikupendeza naomba jambo hili kwa busara yako ulifikirie mara mbili , nipo tayari mimi kama baba kufa kwa ajili ya wageni hawa wote kutoka salama , lakini pia nipo tayari kwa Khatibu mlengwa kupata adhabu yake, lakini kabla ya hivyo nataka umwambie rafiki yako kwamba nafahamiana sana na Hades wa Zamani na alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na ili kuthibitisha uhusiano wangu na yeye nataka kuonyesha alama niliokuwa nayo kwenye mwili wangu”Aliongea na palepale alivua vazi lake la kanzu na kufunua bega lake na kugeuzia upande wa meli ya kivita mgongo wake na hapo ndipo ilipoonekana Tatoo ambayo inafanana kwa asilimia mia moja na ile ambayo alikuwa nayo Linda mlinzi wa raisi Jeremy , lakini pia aliokuwa nayo Mellisa , lakini pia aliokuwa nayo Phill Knight.
Kwa maelezo ya Shekhe Assadi ni kwamba alama hio ilikuwa ikimaanisha kwamba na Tajiri Khalifa na yeye ni mwanachama wa ‘Ant- Illuminat.
SEHEMU YA 304
Wakati hayo mengine yakiendelea huko Japani , upandewa taifa la Tanzania ikiwa ni usiku Edna na wanafamilia wake walikuwa wamekaa eneo la sebuleni huku macho yote yakiwa kwa Christine mrembo, msanii maarufu kutoka Marekani.
Wanafamilia hawa baadhi yao hawakuwa wakiamini kwamba wapo kwenye nyumba moja na Star mkubwa duniani ambaye alikuwa akihusudwa na wengi.
Yezi , Sophia na Qiang walikuwa ni wenye kusahau kabisa baadhi ya majina ya Christine , kama vile kujitambulisha kama Aphrodite , lakini pia kumuita Roma Hades , lakini pia kumuita Edna Persephone , wao walichokuwa wakitaka hapo ndani ni kuuthitishia ulimwengu kwa kavideo kwamba wapo na Christine nyumbani kwao.
Tukio la kuvamiwa lilikuwa limemezwa na furaha waliokuwa nayo kuwa mbele ya Star mkubwa duniani.
Kwa Edna hakuwa kwenye mshangao mkubwa kama wengine , yeye kwake licha ya kwamba alikuwa akimkubali Christine , lakini kuna jambo lilishaanza kuutekenya moyo wake , kwanza kabisa alianza kumkagua uzuri wote wa Christine na kujiona wamezidiana kidogo sana na huenda ni kwasababu yeye alikuwa mwafrika na Christine mzungu , sasa kwa jinsi Christine alivyowaokoa hapo ndani na alivyojitambulisha aliamini kuna asilimia kubwa kwa Roma kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Christine.
Na alijiambia kama hayo ni kweli basi huenda siku atakuja pia kusikia Roma anatoka kimapenzi na Malkia wa Uingereza , sasa mawazo hayo yalikuwa kinyume chake , kwani asichokijua yeye Roma alikuwa akimnyandua Malkia wa Uingereza tayari akiwakilisha vizuri Tanzania, tena alishuhudia yeye mwenyewe siku ya malkia huyo kutoka katika chumba cha Roma.
Edna licha ya kwamba siku ile alimshuhudia mwanamke akitoka kwenye chumba cha Roma kule Ufaransa , lakini hakumfahamu kama ni Malkia wa Wales , kama angefahamu sijui angewaza nini. Usisahau kwamba malkia wa Wales ndio huyo huyo wa Uingereza
Sasa Edna kumuona Christine mwanamke mrembo na Tajiri kuzidi yeye , aliamini kama kuna mahusiano kati ya mume wake na Roma basi yeye ni wa kawaida sana na kuna karoho kalianza kumtekenya na kuona huenda ndio maana hata Roma hakuwa akilazimisha kuomba kitumbua chake kwa juhudi , kumbe amezungukwa na wanawake warembo Zaidi na wenye hadhi , akiwemo Chiristine , lakini pia alimkumbuka Profesa Clark.
“Miss Edna nilikuwa nikisikia Habari zako sana , niseme tu kwamba unafanana kwa asilimia tisini na saba na Seventeen , kati ya watu ambao wamebahatika kuonana na Seventeen , basi mimi ni mmoja wapo , hakika Hades hakukosea kukuchagua nadhani anajiliwaza kwako baada ya kushuhudia kifo cha Seventeen”Aliongea Christine huku akimwangalia Edna aliemshikilia Lanlan.
“Aunti nikiwa mkubwa nitajifunza kuua kama wewe , Mama yake Lanlan pia anajua kuua kwa kukata vichwa , lakini hataki Lanlan akiua”Aliongea Lanlan na kumfanya Christine kuhamisha macho yake kutoka kwa Edna Kwenda kwa mtoto Lanlan.
“Wow!Sikukuangalia vizuri , naamini wewe ni mtoto wa Hades na Edna , umechukua sura ya mama yako kuliko ya baba yako, Hades ana siri nyingi sana yaani kashindwa kuniambia miaka yote anamtoto huku Tanzania”Aliongea kwa namna ya kulalamika na kufanya hata Sophia kutabasamu.
“Lanlan sio mtoto wa Siste Edna na Bro Roma, wanatarajia kumlea kama babu yake asipotokea”Aliongea Sophia na kumfanya Christine kuashangaa kidogo na kumwangalia Lanlan na alijikuta akinoti kitu na kunyamaza.
Bi Wema na Blandina walienda kulala kabisa ,walikuwa kwenye mshituko hivyo hawakutaka kuendelea kubaki macho, Bi Wema na uzee wake alitamani hata Roma arudi mapema kwani uwepo wake hufanya familia kuwa katika hali ya usalama.
“Hades ni nani na kwanini unamwita Edna kama Persephone?”Aliuliza Yezi kwa shauku na Christine mpaka hapo alielewa kitu na kuona kwamba kumbe Roma hajajitambulisha vyema jina lake lingine.
“Umefahamiana kwa muda gani na mume wangu Roma?”Aliuliza Edna akipotezea swali la Yezi , alionekana kuwa na maana yake.
Kuna ile siku ambayo Ashley alisimulia namna ambavyo alikutana na Hades na kugundua ni kaka yake ,sasa katika maelezo ya Ashley hakumtaja Roma kama Hades bali alitumia jina lake halisi la Roma Ramoni.
“Nimefahamiana nae tokea akiwa mtoto, siwezi kujibu hivi wataniuliza nina umri gani?”Aliwaza Christine.
“Nimefahamiana nae kwa Zaidi ya miaka mitano iliopita , alinisaidia kwenye mambo mengi, kama ujuavyo kuna muda sisi wanawake tunahitaji msaada kutoka kwa wanaume , basi ndio nilivyohitaji msaada wa Roma , baada ya hapo ndio akawa rafiki yangu sana”Aliongea Christine kwa tabasamu na maneno yake ni kama aliyaweka hivyo makusudi ili kumsoma Edna.
“Shit nilijua tu na huyu ashalala nae , Roma Mshenzi sana , sijui ni wanawake wagapi hajalala nae , Eti nilihitaji msaada kutoka kwa mwanaume , si useme tu ulilala nae unaficha nini, Roma hawezi kukuacha mwanamke mrembo kama wewe, Labda kama sio yeye mfyuuu”Aliwaza Edna katika kichwa chake huku akitamani kumtukana Roma ,lakini kila akiwaza tusi zuri la kumtukana nalo hakulipata kwanza hakuwa na matusi makubwa makubwa Zaidi ya siku zote kumfananisha na Wanyama, kwa mfano Edna atamtukana Roma kimoyo moyo kwa kumuita Bata mzinga , au Mbwa , au Paka Shume au fisi , hayo ndio yalikuwa matusi yake mazito mazito , sio kama matusi ya wanawake wa uswahilini , unapewa tusi mpaka Shetani mwenyewe analihifadhi kwenye notebook yake kwa matumizi ya baadae.
“Anampenda sana Hades na anajaribu kuzuia hisia zake… hehe ngoja tuone nitakuchokonoa mwezi huu wote nitakaokuwa hapa Tanzania mpaka uyaonyehe mahaba yako waziwazi , ila Hades mtata kuja Tanzania kumbe kamfuata pacha wake na Seventeen .. looh! kwa staili hii sidhani kama atakuja kuninyandua maana atakuwa anamuona Edna kama Seventeen , hapa inabidi nibadilishe mbinu,Ijapokuwa Hades wa Zamani alikuwa ni mpenzi wangu , lakini kulala na Hades mchanga mchanga sio mbaya kama ameamua kumrithi kwa kila kitu kwanini ashindwe kunirithi pia, Hades utalala na mimi tu japo siku zote unanichomolea waziwazi na kuniona kikongwe”Aliwaza Christine kwenye kichwa chake.
Kwasababu muda ulikuwa umeenda , ilibidi Christine aonyeshwe chumba cha wageni kwa ajili ya kupumzika , ili siku inayofuata waweze kuongea.
“Edna usimtaarifu mumeo nipo hapa nyumbani , nataka akirudi kumukoa mchepuko wake anikute hapa kwake”
“Unamaanisha nini kumuokoa mchepuko?”Aliongea Edna kwa mshangao , kwani anajua Roma kaenda Japani kwenye maswala yake , sasa swala la mchepuko lilimfanya kutaka kujua.
“Hehe..inaonekana hujamjua mwanaume wako , yuko Japani anakiwasha kwa ajili ya mwanamke mwenzio hahaha…”Aliongea na kisha akapiga hatua kumfuata Sophia amuonyeshe chumba chake atakachopumzika.
Edna alijikuta akisimama pasipo ya kueleweka anawaza nini , yaani hakuamini wasiwasi wake wote aliokuwa nao siku mbili zilizopita kwa ajili ya Roma ,kumbe alikuwa akimuwazia mtu ambaye kaenda kumuokoa mchepuko wake , alijikuta hasira zikimpanda . lakini alijikuta akirudi kwenye hali ya kawiada mara baada ya Lanlan kumkumbatia kwa nyuma.
“Mama Lanlan ana usingizi , mpeleke Lanlan akalale”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kukumbuka dili lake aliloingia na Roma baada ya kumwangalia Roma.
“Akirudi siongeni nae mbwa yule…. Yaani anatuacha tunakumbwa na mabalaa anaenda kufuata mke mwingine Japani , Shenzi zako kabisa Roma huko ulipo , Nguruwe mkubwa wewe , Naomba upigwe bomu ufe na usirudi kabisa , pumbavu kabisa, Jibwaa ”Aliwaza Edna kwenye kichwa chake.
******
Upande mwingine ndani ya hoteli ya Serena , makazi ya muda mfupi ya Yan Buwen , bwana huyo alijikuta akipasua pasua tableti alioshikilia kwenye mikonono yake dakika kadhaa nyuma kwa hasira nyingi sana , na hio yote ni mara baada ya vidoti vilivyokuwa vikionekana kwenye kishikwambi chake kupotea , ikimpa ishara kwamba watu wake aliowatuma wamekufa.
“Hades nadhani nakuchukulia wa kawaida ndio maana unanishinda kwa kila mpango ninaokutegea , shwaini kabisa , haiwezakani maiti nilizozifufua na kuzipa uwezo wa kimapigano kupitia Chip kufa wote kwa Pamoja… Yan Buwna , unaruhusu vipi mpuuzi kama Hades kukushinda… Shenzi”Aliongea na kisha akakaa kwenye sofa na kuchukua Whiskey na kuigida pasipo kuweka kwenye glass huku akifumba macho kwa uchungu wa Whiskey hio.
Na ndani ya dakika alionekana akili yake kutulia na alisimama na kuanza kutembea mpaka kwenye dirisha na kutoa pazia huku akiangalia mataa ya jiji la Dar es salaam. Huku akiwa amevalia taulo lake na visendo manyoya.
“Ngoja nitakapoweza kupata damu yako hutoamini kitakachotokea , nitatengeneza kopi yako halisi na kuipa nguvu kama zako kupitia Godstone na baada ya hapo nitakugombanisha na mataifa makubwa , nitaifanya kopi yako ishambulie kambi za jeshi la Marekani , Ufaransa na NATO , kama alichofanya mpuuzi Depney hahaha… baada ya hapo utaandamwa sana na kuonekana kiumbe hatari… mpango wa Neema Luwazo lazima ufanikiwe kwa asilimia mia moja, hahaha … Hades nitawafanya wanawake wako kuwa mwiba kwak…”Kabla hajamaliza kujiongelesha mlango uligongwa na alitabasamu kifedhuli na Kwenda kufungua na alijikuta akitabasamu baada ya kumuona mrembo aliekuwa mlangoni.
Alikuwani Queen mtoto wa Mzee Alex , sasa haikueleweka Yan Buwen aliweza vipi kukutana na mrembo huyo , lakini mavazi ya Queen yalidhihirisha kwamba siku hio kaja kufanya uzinzi.
“Karibu mrembo”Aliongea Yan Buwen huku akimwangalia Queen , licha mwanamke aliekuwa mbele yake kuwa mrembo haswa , lakini alijiambia kwamba hakuwa akiingia kwa chochote kwa Athena na hakuna mwanamke dunia nzima anaweza kufikia uzuri wa Athena ambaye anamjua kama The Doni , wanawake wote kwake aliona ni takataka tu , na ndoto yake kubwa ilikuwa ni siku ambayo atalala na mrembo Athena , katika mawazo yake anajiambia , siku hio atampa penzi mrembo Athena mpaka jeuri yake yote itakwisha na baada ya hapo atakuwa anamuongoza anavyotaka , hayo ndio mawazo ya Yan Buwen , alikuwa yupo radhi kufanya chochote tu ilimradi ndoto yake kutumia , ndoto ya kulala na The Doni , Aka, Athena , tishio la Dunia.Sasa usishangae sana Yan Buwen ndoto yake kubwa ni kula kitumbua cha Athena tu
Hahaaa… sijui kama atafanikiwa, ngoja tuone.
ITAENDELEA JUMANNE
KWA WALE WANAOTAKA KUJIUNGA NA GRUPU LANGU LA WATSAPPNICHEKI KWA NAMBA 0687151346, GRUPI NI SIMULIZI TU HAKUNA KUCHATI SIMULIZI HII IPO SEHEMU YA 371 NA INAENDELEA KILA SIKU VIPANDE VITATU MPAKA IFIKE MWISHO
Singano fupisha hii hadithi.umeivuta sana inakosa mvuto.nnachokiona utaishia njiani.utatuacha kwenye mataa.tukio moja la Roma kuwa Japan limechukua hadithi yote.Ohooooo
Kila tukio lina Correlation mbele , simulizi haiwezi kukosa mvuto kwasababu mbele ni kuzuri zaidi kuliko iliko toka , kwa taarifa tu simulizi ina vipande 600 jumla na inaendelea kwa kasi kwenye grupu na wale wa private inbox , kadri wadau wanavyoidhamini kwa michango ndio inawekwa hapa.Singano fupisha hii hadithi.umeivuta sana inakosa mvuto.nnachokiona utaishia njiani.utatuacha kwenye mataa.tukio moja la Roma kuwa Japan limechukua hadithi yote.
Singano fupisha hii hadithi.umeivuta sana inakosa mvuto.nnachokiona utaishia njiani.utatuacha kwenye mataa.tukio moja la Roma kuwa Japan limechukua hadithi yote.
Singano fupisha hii hadithi.umeivuta sana inakosa mvuto.nnachokiona utaishia njiani.utatuacha kwenye mataa.tukio moja la Roma kuwa Japan limechukua hadithi yote.
Mzee unajua mno alafu kinachonifurahisha ni unapita kwenye facts, mm huwa Nikimaliza kusoma episode kadhaa naenda google kuangalia baadhi ya fact zako nakuta ni kweli mfano issue za international water zone ni sahihi, ancient Greece gods ni kweli, technology unayozungumzia huku ni kweli na mambo ya invisible groups kama yamata sect ni kweli kabisa, big up mzeeKila tukio lina Correlation mbele , simulizi haiwezi kukosa mvuto kwasababu mbele ni kuzuri zaidi kuliko iliko toka , kwa taarifa tu simulizi ina vipande 600 jumla na inaendelea kwa kasi kwenye grupu na wale wa private inbox , kadri wadau wanavyoidhamini kwa michango ndio inawekwa hapa.
Hapo Japani kilicholengwa ni Baba yake Fayezi , Amina huyo na kundi lote la Yamata sect.