SEHEMU YA 305.
Ilionekana Dhahiri kwamba watu wote waliokuwa juu ya meli hio ya kifahari walikuwa wakionekana kwA ukaribu kabisa kutoka kwenye meli ya kivita iliokuwa ikiongozwa na Makedoni, kwani baada ya Khalifa kuonyesha Tatoo iliokuwa kwenye mgongo wake kulitokea kimya cha takribani dakika kama mbili hivi mpaka sauti ya Kapteni Makedoni kusikika tena.
Watu waliokuwa ni wageni ndani ya hili eneo hawakuwa na uelewa wa aina yoyote ile juu ya alama aliokuwa akiongelea Tajiri Khalifa, lakini pia hawakuwa wakielewa alikuwa akimaanisha nini kuhusu jina la Hades , hata kwa upande wa Amina mwenyewe hakuwa akimfahamu Roma kwamba ndio Hades, alietambua hilo jina alikuwa ni Mheshimiwa Kigombola na Tajiri Khalifa peke yao , wageni wote hawakuwa na ufahamu na jina la Hades na hata kwa Khatibu ambaye alikuwa mshukiwa wa kwanza kumkasirisha Roma alikuwa hafahamu chochote kuhusu Hades , yeye alichokuwa akijua kuhusu Roma Ramoni ni kwamba bwana huyo alikuwa ni mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi tatu na aliacha kazi yake hio baada ya kupata shavu la kuona na mwanamke mrembo Tajiri ,Edna Adebayo, ni Dhahiri kabisa kwamba hata Fayezi mwenyewe licha ya kumtambua Roma kama Hades hakuwa na faili lote la utambulisho linalohusiana na Hades na laiti kama angekuwa nalo basi asingefanya vitu vya kumchokoza, ama kuingizwa kwenye mtego na Jasoni Pamoja na kundi la Takamagahara.
Watu wote sasa tumaini lao ilikuwa ni kwa Tajiri Khalifa pekeee , waliomba tatoo iliokuwa kwenye bega lake iwe na msaada kwao na Imani zao zilikuwa juu kidogo kutokana na ukweli kwamba Khalifa alikuwa ni muislamu haswa wa swala tano na alikuwa akifuatisha taratibu zote za uislamu, na sheria kubwa ya uislamu haikuwa ikiruhusu michoro ya tatoo kwenye miili, sasa kitendo cha Tajiri Khalifa kuwa na tatoo hio licha ya miiko ya dini waliamini kabisa kuna maana kubwa kwenye mchoro huo.
“Rafiki yangu ameona alama unayozungumzia na ameitambua . lakini licha ya hivyo anasema kuwepo kwa alama hio kwenye mwili wako hakubadilishi jambo lolote”Ilisikika sauti ya Makedoni na kufanya Tajiri Khalifa akiwa myonge na kukaa kwenye kiti.
“Haiwezekani , nafurahi kwamba ameitambua na hili linanitibitihsia kwamba ndio mtu niliekuwa nikimsubiri kwa muda mrefu , lakini kwanini anakataa kutoa msamaha kwangu na watu waliopo kwenye meli hii”Aliwaza Tajiri Khalifa.
“Upande wa meli ya kivita Roma alikuwa kwenye chumba maalumu, kikubwa ambacho kilionekana kama ofisi , kutokana na uwepo wa mpangilio wa viti na masofa , pembeni yake walikuwa wamesimama wanajeshi kama kumi hivi wakiwa wamemzunguka , Roma alieonekana kutokuwa mtu mwenye wasiwasi kabisa , kwanza kabisa alikuwa ameweka miguu juu ya meza huku akigida Wine ya Cheval Blanc iliohifadhiwa tokea mwaka 1948 ikioezeshwa tu , ilikuwa ni wine ya bei mbaya mno na kwa mahesabu ya haraka haraka chupa yake inagharimu Zaidi ya Dollar za kimarekani laki tatu sawa na milioni mia saba za kitanzania.
Yaani kwa jinsi alivyoonekana ni tofauti na maneno ya Makedoni , kwani alisema kwamba rafiki yake huyo alikuwa kwenye makasiriko ya hali ya juu sana , lakini haikuwa kweli kwani Roma alikuwa akiburudika na Wine huku akiwa amezungukwa na wanajeshi walio kwenye sare tofauti tofauti, alionekana kama mfalme kamili na jambo la kushangza Zaidi ni kwamba wanajeshi waliomzunguka walionekana kuwa wenye umri mkubwa kuliko yeye ambaye umri wake ulikuwa miaka ishirini na nane tu.
Roma alikuwa akiona kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwenye meli ya kifahari kwa kupitia runinga iliokuwa imefungwa ndani ya meli hio ya kivita ya Hatakaze.
Makedoni yeye hakuwa hapo kwenye hiko chumba , ilionyesha alikuwa upande wa chumba cha kuendeshea meli hio kwani yeye mwenyewe alikuwa ndio Kapteni wa meli, lakini kila alichokuwa akiongea Makedoni Roma alikuwa akikisikia na mbele yake kwenye meza kulikuwa na simu ambayo alikuwa akiwasiliana moja kwa moja na Makedoni akimpa maelekezo, hata baada ya kusikia maneno ya Tajiri Khalifa Pamoja na kuona alama iliokuwa kwenye bega lake alishangaa kidogo na kukunja uso kwa sekunde , ilikuwa ni mara yake ya pili kuona mtu ambaye hakuwa akiishi ndani ya visiwa vya wafu kuwa na alama hio , mtu wa kwanza alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa akimuona kama mpumbavu tu kutokana na ndoto zake za kuiangusha Marekani , mwanamke aliekuwa akiitwa Mellisa, ukweli Roma licha ya kwamba Tajiri Khalifa alisema alama hio kaipata kutoka kwa Hades wa zamani , yeye hakuwa ni mwenye kujua sababu gani ya Hades wa zamani kuwachora alama hio ambayo ilikuwa ni kama kitambulisho cha uraia, kwa wananchi wake kutoka Visiwa cha wafu.
Roma licha ya kuona alama hio haikuwa na sababu ya kutaka kuacha kile kilichopo kwenye kichwa chake , ni kweli kabisa alikuwa akijihisi moyo wake kubadilika na kujihisi kama Mlokole, lakini alivyomshudia Khatibu mpwa wa Fayezi na kukumbuka Kejeli zake kipindi akiwa kwenye tukio la mnada , aliamini hio roho ambayo ilikuwa ikimwambia asiue , alijiambia hawezi kuitii sana kwani inavunja moja ya sheria zake na aliamini namna nzuri ya kuikomesha sauti hio yenye upole ndani yake ni kuhakikisha anaenda nayo kinyume kwa namna yoyote , na mpango wa kwanza ni kushuhudia kifo cha Khatibu.
Roma alichukua kifaa cha mawasiliano na kuwasiliana na Makedoni na kumpa maelekezo juu ya msimamo wake.
Dakika kadhaa tu , yaani kama dakika tatu hivi baada ya tajili Khalifa kukosa tumaini licha ya kujigamba kwamba alikuwa rafiki na Hades wa zamani na pia kuwa na uthibitisho wa Tatoo , alijikuta akirejewa na tumaini tena , yeye Pamoja na wageni wake wote na hio ni mara baada ya Makedoni kutoa msimamo wa rafiki yake.
“Kama nilivyosema kwamba rafiki yangu kaitambua hio alama , lakini licha ya hivyo hawezi kutoa msamaha kwa alama ambayo kwake haina maana hata kidogo na haiwezi kupunguza kile anachojisikia moyoni , hivyo basi anasema kwamba anajisikia angalau kutoa msamaha kwa familia nya Khalifa Pamoja na wageni wote , ila kwa sharti moja tu,Khatibu Omary atupiwe baharini , pili hataki ugomvi wowote na familia ya Khalifa licha ya kwamba anapanga kumuua mtoto wenu Fayezi kutokana na makosa yake, hivyo kama mnakubaliana na uamuzi wake Tajiri Khalifa utaongoza adhabu ya kifo kwa Katibu Omary.”
Maneno ya Makedoni licha ya kuwa na tumaini kwa wageni , lakini kwa upande wa mama mzazi wa Fayezi ilikuwa ni kilio kikubwa mno, hakuwa tayari kwa mtoto wake Fayezi kufa, alijua alikosa na alitaka mtoto asamehewe na kabla hata ya Tajiri Khalifa kutaka kutoa tamko kwa kile alichoamua , mzazi huyo alimkwapua kipaza sauti na kuongea.
“Tafadhari naomba mwanangu asamehewe , naomba Fayezi asife jamani nipo tayari kufanya lolote hata kufa kwa niaba yak… hiii… jamani naomba..”
“Tajiri Khalifa tunachotaka kuona ni agizo kutekelezwa sio kusikia kilio kutoka kwa mke wako , maamuzi ni ya kwako , ‘ofcourse’ kuna mbadala , kama utakubali tulipue meli yenu na kufuta kila uhai wa mtu alieopo kwenye hio meli basi utachagua na mtoto wenu Fayezi ataachwa hai”Yalisikika maneno ya Makedoni aliongea kwa niaba ya Roma Ramoni a.k.a Hades.
Tajiri Khalifa alijikuta akifumba macho kwa muda mrefu kidogo na kufanya kila mtu kumwangalia , hata kwa Raisi Kigombola hakuweza kumsoma Tajiri huyo atachukua maamuzi gani , ni kweli mpaka muda huo licha ya Makedoni kuongea , lakini hawakuweza kusikia sauti ya Hades mwenyewe , hivyo hata Kigombola kuwa katika hali ambayo ina mashaka ndani yake , jana yake alionyeshwa pucha za Hades akiwa mfu , leo hii wanavamiwa na meli ya kivita na mtu anaejitambulisha kwa jina la Makedoni , huku akiongea kwa niaba ya Hades , aliona huenda Hades mwenyewe alikuwa maiti na Makedoni anataka kulipiza kisasi , lakini hata hivyo pia alikuwa akikumbuka na maneno ya Yan Buwen juu ya kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kumuua Hades Zaidi yake mwenyewe , hivyo pande zote mbili zilikuwa zikipigana vita katika akili yake , ubongo wa kulia ulikuwa ukimwambia Hades yupo hai na anapaswa kuamini maneno ya Yan Buwen kwamba hakuna mtu anaeweza kumuua Zaidi yake na upande wa kushoto alikuwa akikumbuka picha alizoonyeshwa na Fayezi , lakini pia upande huo ukiwa na sababu nyigine ya kusapoti kutokana na kwamba sauti ya Hades yenyewe haijasikika Zaidi ya mtu aliejitambulisha kwao kama rafiki yake.
“Kigombola unahisi ni maamuzi gani napaswa kuchukua? , nimwache Mwanagu Feyezi kufa kama adhabu ya makosa yake , au niruhusu kundi hili la wageni wote kufa Pamoja na mimi na kuacha Fayezi awe hai?”Aliuliza Khalifa na mheshimiwa Kigombola aliona swali hilo ni kama la mtego..
Upande wa meli Roma akiwa anaendelea kuburudika na mvinyo wake mara macho yake yalitua kwa Mheshimiwa Kigombola, kwanza kabisa hakushangazwa na uwepo wake hapo, kwani alikua akijua machache kwamba mheshimiwa huyo mstaafu alikuwa na ukaribu na familia ya Khalifa , hivyo kualikwa halikuwa jambo la kushangaza , kilichomfanya Roma kumwangalia kwa namna ya udadisi ni kutokana na taarifa ambayo aliipata muda huo kutoka kwa kundi la Yamata Sect kupitia kiongozi wao , Tanya.
“Boss Mheshimiwa Kigombola ndio mtu wa mwisho kuongea na Fayezi ndani ya hoteli ya El-Fadhi na kwa maelezo ya shushu wetu kaeleza kwamba kilichokuwa kikizungumziwa ni juu ya kifo chako , baada ya mazungumzo hayo mheshimiwa alioongea na simu ambayo tumefatilia na kujua imepigwa Kwenda Tanzania na ameongea na mtu alieopo ndani ya hoteli ya Serena na bado hatujaweza kufahamu ni mtu gani aliekuwa akiwasiliana nae , kwani namba yake Special”Aliongea Tanya na kumfanya Roma kufikiria kwa dakika kadhaa.
Sasa kabla hata hajamjibu Tanya simu nyingine iliingia kutoka Tanzania kwa njia ya satilaiti yake , licha namba hio kutokuwa na jina lakini kodi zake zilimfanya kujua kabisa alikuwa akipigiwa simu na The Eagles na alipokea haraka haraka na kuweka sikioni na hapo ndipo alipojikukuta akivuta pumzi nyingi , mtu aliekuwa akiwasiliana nae ni Diego kutoka Tanzania na alimpasha Habari ya uvamizi uliotokea nyumbani kwake.
“Diego nimeumia kusikia kifo cha Chiara na pia kuumia kwa John , wasiliana na Sauroni ili kupata utaratibu wote wa kusafirishwa kwa Chiara mpaka visiwa vya wafu kwa ajili ya maziko, taratibu zote za fidia kwa familia zitapangwa na Sauroni kutokana na sheria za wanajeshi wetu”Aliongea Roma huku akionekana hata mudi yake ya kunywa bia ikimtoka, na hata mawazo aliokuwa nayo juu ya mheshimiwa Kigombola aliyaacha kwa muda.
Roma alimshukuru Aphrodite kumsaidia kuiokoa familia yake , kwani kama sio yeye huenda ingekuwa huzuni zana kwa upande wake na angepoteza watu anaowapenda kwa mara nyingine, lakini hata hivyo aliamini lazima kuna malipo , kwani alikuwa akimuelewa sana Christine anapopata msaada wake , lakini hilo hakutaka kulipa kipaumbele sana, aliamini chochote atakachoongea Christine ni lazima atakitimiza kwani jambo alilofanya kwake ni kubwa sana, lakini pia wakati huo huo alikuwa akijiuliza ilikuwaje Christine akafika nyumbani kwake ndani ya muda na kuokoa familia yake.
SEHEMU YA 306.
Kabla hata ya mheshimiwa Kigombola kujibu wanaume wawili ambao walikuwa ni wageni wa kualikwa walimkamata Khatibu ambaye alionekana kutafuta namna ya kutoroka , na wanaume hao walionekana kuungwa mkono na kila mgeni , walikuwa tayari kumtoa Khatibu kama sharti walilolopewa na hawakuata kuyaweka Maisha yao mikononi mwa Khalifa na Kigombola ndio maana walaiona kufanya maamuzi wenyewe ndio busara iliokuwepo kwa muda huo.
Kitendo cha Khatibu kukamatwa kilimfanya kuloa mwili mzima , huku akianza kujikojolea, sasa ukumbuke walikuwa juu kabisa ya meli hii , hivyo Wanaume wale wawili walimsogeza Katibu mpaka kwenye ukingo wa meli ile kwa ajili ya kumtupia majini, huku wakisaidiwa na baadhi ya walinzi.
“Mtupee…!!”Zilikuwa ni kelele za watu wote na Khatibu kuna sauti alijikuta akisikia kwa upande wa kulia kwake na hakutaka kuamini kama sauti hio ni ya mtu anaeyemfahamu na kumjali sana, alijikuta akigeuza kichwa chake na hapo nipo alipoamini kwamba sauti ile ilikuwa ikitoka kwa mtu ambaye anamfahamu , mpenzi wake Hadija ni mojaya watu waliokuwa wakikemea kwa juu kuhusu kutupwa kwake majini , Khatibu moyo wake uliuma Zaidi ya kile kitendo ambacho kitatokea dakika kadhaa mbele , kwake aliamini ni afadhari kutupiwa majini kuliko kusalitiwa na mwanamke ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wote, hakuamini mwanamke Hadija aliekuwa amejtolea kumpenda Zaidi na Zaidi ndio huyoo ambaye anaungana na wageni wengine kuruhusu kifo chake, Khatibu aliangalia upande mwingine na kuangalia ndugu zake wengine na kila mmoja alionekana kutojali kifo chake , mtu pekee ambaye alikuwa na huzuni alikuwa ni mama yake Fayezi na huzuni yake sio kwa ajili ya kifo ambacho kinataka kumkumba bali ni juu ya mtoto wake Fayezi na mama huyo alikuwa akimwangalia Khatibu na katika moyo wake ni kama alikuwa akisema anatamani kifo cha Khatibu kiponye kifo cha mwanae , yaani kwa maneno marahisi mama huyo alikuwa akitamani kwamba kufa kwa Khatibu kuwe mbadilisihano wa uhai wa Fayezi.
Sasa baada ya Khatibu kuona kila mtu alikuwa akitamani kifo chake , hakutaka hata kusikia na mjomba wake Khalifa atasema nini , alijua kabisa mjomba wake huyo lazima ataruhusu kifo chake na kwanza kabisa alishaonyesha nia ya kutoumizwa na kifo chake.
“Chubwii..!!!!” Khatibu hakutaka kufa kwa kusukumwa , baada ya kuona hakuna mtu ambaye alikuwa akihuzunishwa na kifo chake , hata kwa wale aliokuwa anawapenda , aliona ni bora kufa kishujaa kuliko fedheha ambayo inataka kumkumba , maumivu aliokuwa akisikia kwenye moyo wake alijiambia ni bora kujirusha majini.
Katika maji ya katikati ya bahari hio , hatimae Khatibu kifo chake kinadhihirika kwa wengi , hakuna mtu ambaye anaweza kuamini kama Khatibu anaweza kupona kwenye maji hayo mengi , hivyo moja kwa moja alihesabika kama mfu na jambo hilo liliwafanya watu wote kuvuta pumzi ya ahueni.
Dakika nne baada ya kupita hatime chopa ilitua kwenye meli hio , chopa ambayo haikuwa na nembo yoyote , ilikuwa ikiendeshwa na wazungu wawili wote wakiwa wakike waliovalia mavazi ya uniform. Za kijeshi.
“Miss Amina na Baba yako mnapaswa kupanda kwenye hio Hawk , hayo ni maelekezo kutoka kwa rafiki yangu “Aliongea Makedoni na kuwafanya watu wote kumwangalia Amina na baba yake Kanan ambao walikuwa hapo ndani .
Kanani baada a kusikia maneno hayo alijiambia hawezi kupanda , kwani alikuwa akikiendea kifo chake , Mzee huyu licha ya kusikia baadhi ya maelezo , lakini hakuwa akimfahamu huyo rafiki ambaye Khalifa alimtaja kama Hades , aliamini kupanda chopa hio ni kukiendea kifo chake.
Wakati akiwa anafikiria cha kufanya, Amina ndio aliekuwa wa kwanza kupanda upande wa juu kabisa wa meli hio kwa ajili ya kupanda chopa hio.
“No ..Amina mwanngu usipande , watu wale ni wabaya kwetu na huenda tunajiingiza Zaidi kwenye matatizo ni heri kufa tukiwa wengi”Aliongea Mzee Kanani kwa wasiwasi na Amina alimgeukia baba yake.
“Baba yangu mpendwa , unaamini kubakia hapa ndio utakuwa salama , lakini unajuaje huko tuendako tunakwenda kufa , huenda mtu alietuita anataka kuongea na sisi tu na kisha atatuachia”Aliongea Amina na kisha kupewa mkono na mzungu mwanajeshi kwa ajili yakupanda juu ya chopa.
Sasa kwakuwa lile ni agizo kutoka kwa Makeodni basi wageni wote walimwangalia Kanani kwa macho ya kumtaka kutii maagizo na mzee huyo baada ya kukumbuka kilichomtokea khatibu hakuwa na ajizi kwani alipanda kinyonge kwenye ndege hio na ajabu mara baada ya kuipanda wanajeshi hao hawakuwaangalia kwa macho ya chuki zaidi ya kuwapa heshima na kisha chopa kuondoshwa.
Na kutoka na wa wanajeshi hao walivokuwa wakimpa heshima alianza kujiuliza maswali ni mtu gani ambaye anaitwa Hades ambaye anataka kuonana nae , yeye Pamoja na mwanae , mwanaume huyu mpenda pesa , hakuwa na uelewa kwamba mtu ambaye anakwenda kukutana nae ndio yule ambaye alimtoa bikra mtoto wake Amina , mwanaume ambaye alimsahau siku ileile na kuendelea na mipango ya ndoa kwa Binti yake na Fayezi.
Baada ya Chopa kuondoka hatimae meli iliwashwa na kufanya wageni wote kushangaa kwani dakika kadhaa zilizopita walikuwa na taarifa kwamba meli hio ilikuwa haina kapteni.
“I’m very satisfied with each of your cooperation. Everyone is safe now, while the countdown on our missile launcher has stopped. The cruise will arrive at the port in an hour’s time, I hope everyone to have a happy journey…”
“Nimeridhishwa sana na ushirikiano kutoka kwa kila mtu , kwasasa kila mmoja yupo salama , bomu letu tumelizima na meli yenu itafika bandarini ndani ya lisaa limoja baadae , natumaini kila mmoja atakuwa na safari iliojaa furaha”Aliongea Makedoni na watu wote walishangilia mara baada ya kusikia kwamba wamepona, wengi walishasahau kabisa jambo ambalo ilikuwa limewaleta hapo ndani wengi wao hawakumkumbuka Khatibu na Fayezi , wala hali za machungu waliokuwa nayo wanafamilia wao , akiwemo mama yake mzazi wa Fayezi, Tajiri Khalifa na yeye pia licha ya kuwa kwenye majonzi , ila hakuwa na jinsi kabisa na hakutaka kabisa ugomvi na Hades , kwani kuna baadhi ya meneno kutoka kwa rafiki yake Hades wa zamani aliokuwa akiyakumbuka na aliamini kifo cha Fayezi ni kwa ajili ya kusudio kubwa Zaidi na hakijatokea bure , hakuwa na maneno ya faraja ambayo alitakiwa kumpatia mke wake kwa wakati huo Zaidi ya kuwapa maagizo wasaidizi kumchukua na Kwenda kumpumzisha , upande pia wa Wake zake wengine wlaikuwa wakichekelea kwani siku zote hawakuwa wakimpenda Fayezi kutokana na kupendelewa na baba yake na mpaka muda huo ni kwamba Khalifa hana mrithi wa kiume tena kwani Watoto wake wengine waliobakia ni wanawake.
Upande wa kwenye meli ye kivita ya Hatakaze , hatimae chopa ile ilitua na wa kwanza kushuka alikuwa ni Amina ambaye alishangazwa na uwepo wa wanajeshi waliokuwa wapo kwenye meli hio wakiwa katika mavazi ya kijeshi ambayo yana rangi tofauti tofauti.
Makedoni , mwanaume mzungu mwenye ndevu nyingi alievalia kombati za jeshi pia alionekana kutoka kwenye chumba cha Kapteni na sasa alikuwa amesimama akiwa na wanajeshi wengine kwa ajili ya kumpokea mrembo Amina,yaani kwa jinsi Amina alivyokuwa akisubiriwa ni kama vile ni mtu mkubwa sana , kumbe ni mchepuko tu wa Roma Ramoni ndio maana alikuwa akipewa heshima kubwa ya namna hio.
Amina mara baada ya kumuona babe wake Roma Ramoni alisahau kila kitu na kumkimbilia na Kwenda kumkumbatia kwa fuaraha mno , hakuamini Roma alikuwa na uwezo wa aina hio , yaani kwa ajili tu ya kuzuia ndoa yake isifanikiewa kaleta meli ya kivita.
“Babe Amina angalia pembeni”Aliongea Roma na kumfanya Amina kuangalia pembeni na hapo ndipo alipogundua macho ya wanajeshi wote yalikuwa kwake na kumfanya kuona aibu.
Mzee Kanani sasa macho yake ni kama yalikuwa yakimdanganya , mtu aliekuwa akimchukulia kama kapuku kumbe ndio alikuja kufanya uchafuzi wa hali ya hewa wa namna hio , hakuwa akiamini kama mwanaume yule alieitoa bikra ya mtoto wake ndio huyo alievuruga ndoa na kuonyesha nguvu kubwa sana, alishindwa hata kuongea lolote Zaidi ya kumwangalia mtoto wake aliening’inia kwa mwanaume huyo.
“Kama ni hivi basi nilikosea kuchagua upande , kuna fursa hapa”Aliwaza Mzee Kanani huku akikagua wanajeshi wote hao , licha ya kwamba alikuwa kwenye misukosuko dakika kadhaa zlizopiita , lakini kuona mmeli huo wa kivita Pamoja na wanajeshi walivyokuwa wakimuheshimu Roma , aliona fursa , yaani kwake fursa ndio kila kitu mpaka kwa wakati huo.
“Babe sikufahamu unaweza kuja na meli kwa ajili tu ya kuzuia ndoa yangu , umenifurahisaha mno , lakini sikudhania kama una uwezo wa kua na meli kama hii ambayo mara nyingi naiona kwenye muvi”Aliongea amina kwa kingereza na kumfanya Roma kutabasamu.
“Hehe.. hii meli yenyewe sio yangu tumeiazima kutoka jeshi la Japani , si nilikuambia nilitakakufanya ndoa yako kuwa ya kipekee , huu ndio upekee wenyewee, mimi babe wako Roma Ramoni nakuja kukuokoa na meli ya kivita inakaaje hio , si Romantic?”Amina alishangaa , hakuamini maneno ya Roma.
“Unao uwezo wa kuazima meli ya kivita kutoka jeshi la Japani?”
“Ndio babe , Waziri mkuu wa Japani nilikuwa nikimdai hivyo nilipomwambia anilipe kwa kunikodisha meli ya kivita kwa masaa mawili hakusita kufanya hivyo.”
Roma aliamza kumtabulisha Amina kwa wanajeshi wake wote , akiwemo Makedoni na sasa Amina aliweza kupata kumjua aliekuwa akiongea kwa rafudhi ya kizungu.
Kazi ya kumuokoa Amina ikawa imekwisha kwa namna hio , kifo cha Fayezi kilitekelezwa na kundi la Yamata Sect kutoka kwa maagizo ya Roma.
“Mr Roma najua kuna mahali nilikukosea kwenye siku hizi za karibuni na siku ile nilikutolea maneno ya kejeli , hivyo naomba unisamehe mimi , na kwanzia leo hii nipo tayari mwanangu Amina umchukue kama mkeo?’Aliongea Tajiri Kanani huku akionekanna kumaanisha kile anchoongea na kumfanya hata Amina kushangaa baba yake kwa namna anavyobadlika badilika.
“Mzee msamaha nimekupatia kwasababu Amina ni mtoto wako , kuhusu kumchukua Amina kama mke wangu hilo sijalifikiria , kwani nina mke tayari na siwezi kuoa mwanamke mwingine Zaidi na niliekuwa naye”
“Hapana .. sijamaanisa umuache mkeo , ninachomaanisha umuoe kama mke wa pili , sisi katika Imani yetu tunaruhusiwa kuoa wanawake mpaka wa nne”Aliongea Kanani.
“Sasa kama nikifuata Imani yako ya kuoa wanawake mpaka wanne inaamana kwamba kuna baadhi ya wanawake wangu wengine watakosa nafasi”Aliongea Roma na alichoongea ni sahihi , kama kweli atafatisha sheria za Imani ya Mzee Kanani ni kwamba wanawake wake watakosa nafasi kwani mpaka muda huo walikuwa wamezidi wanne tayari.
“Mzee licha ya kwamba sitomua mtoto wako kwa ndoa, lakini naweza kukuhakikishia kwamba Amina ni mwanamke wangu kuanzia sasa na nilioyafanya haya yote na ninayotarajia kuyafanya juu yake ni kumhakikishia kwamba ana nafasi sawa na cheo cha mke, hivyo usiwe na wasiwasi na uhakikishe siku zinazokuja haufanyi jambo ambalo litanisabibishia kukasirika”Aliongea Roma kwa usuriasi na Mzee Kanani alitingisha kichwa kwa heshima kubwa , alikuwa yupo tayari kuwa upande mzuri na Roma kwa namna yoyote ile ili atumie fursa ya kupanua biashara zake.
“Babe kumbe una wanawake wengine tofauti na mke wako?”Aliuliza Amina kwa kulalama.
“Hehe… ndio ukimuacha mke wangu wewe ni mwanamke wangu wa nne”Aliongea Roma kwa kujiamini na kumfanya Amina kumwangalia Roma usoni kama asieamini na aliishia kucheka na kumfanya Roma atabasamu na kupendezwa na urembo wa Amina kwa jinsi alivyokuwa akicheka.
“Nikifika Tanzania lazima nijitambulishe kwao wote ili wanitambue kama moja ya mwanamke wako”
“Babe unauhakika na unayoongea?”
“Niko siriasi , kubwa Zaidi nitajitahidi kumfurahisha mkeo ili asije akanichukia, siko tayari kukukosa Darling”Aliongea Amina na kumfanya Roma kutabasamu na kisha kumfinya Amina mashavu yako.
Ni baada ya masaa kama manne kupita Roma alikuwa kwenye ndege binafsi ya Yamata Sect akirejea Tanzania akiwa na Amina , ndani ya ndege hio kilichokuwa kikifanyika hakikuwa kikielezeka , kwani kila staili ya mapenzi ilifanyika , hata zile ambazo hazina majina zilifanywa na mtaalamu Roma, kiasi kwamba Amina kuwa mwekundu mno kutokana na rangi yake.
Jambo ambalo lilimfurahisha Roma ni kwamba katika wanawake wake wote , Amina pekee ndio mwanamke ambaye alikuwa yupo Romantic kuliko wanawake wote na alikuwa mvumilivu mno, kwani aliweza kuhimili Kwenda mizunguko miwili kwa wakati mmoja jambo ambalo lilikuwa tofauti kwa wanawake wake wengine kama Rose , Roma akienda mzunguko mmoja tu Rose atakuwa amechoka na hana hamu tena ya kuendelea , lakini kwa Amina alikuwa na joto kiasi kwamba mpaka mizunguko miwili alikuwa akienda na angalau kumfanya Roma kupunguza moto uliokuwa ndani ya mwili wake,sasa Roma mwenyewe kutokanana mwili wake, ili hamu ya kufanya mapenzi iishe ni lazima Kwenda mizunguko tisa kitu mabcho ni ngumu sana kutekelezeka kwa wanawake wake wote , yaani kama ataamua Kwenda nao mizunguko yote nay eye kuridhika basi watakufa.
Saa moja kamili za usiku ndio muda ambao Roma aliweza kufika Tanzania na kuachana na Amina ambaye alienda kulala nyumbani kwao , Amina hakuwa amesafiri na baba yake , kwani mzee huyo alibakia Japani na kuwaruhusu kitu na mpenzi wake kusafiri Pamoja.
Mzee Kanani alifanya hivyo kwa kuona kwamba ni wakati wa kumuacha Roma na Amina kuwa na ukaribu mzuri ili Roma azidi kudata kwa binti yake , huku yeye akitafuta namna ya kutumia ‘Ukwe’ kujiendeleza kibiashara Zaidi, aliamini Roma alikuwa mtu mzito sana , kwani aliweza hata kusikia Roma akisema meli ile ya Hatakaze alipewa na jeshi la Japani kwa kuiomba tu kwa masaa , sasa hakuwa mjjinga wa kutoelewa kwamba hakuna nchi ambayo ilikuwa na uwezo wa kumuazimisha meli ya kivita mtu bila kuleta shida , aliamini Roma ni mtu mzito sana na mpango wake kwanzia muda huo ni kuchimba taarifa za Roma na kumfahanu ni nani , na akishaelewa ndio aanze kuangalia atanufaika vipi.
“Allah ananiepusha na hili na ananileta kwenye jambo kubwa Zaidi , nadhani ananikusudia mtoto wake nitengeneneze pesa nyingi sana”Aliwaza Mzee Kanani mara baada ya kumpigia mtu wake ambaye humtumia mara nyingi anapokuwa anataka taarifa za mtu Fulani , hivyo mtu huyo alimpa kazi ya kumfuatilia Roma ni nani haswa, muda huo alikuwa hotelini jijini Tokyo akiwa amepumzika.
“Babe I am Back….”Roma aliongea mara baada ya kuingia ndani ya jumba ambalo ni mali ya mke wake , sasa ile anaingia mtu wa kwanza kukutana nae ni Edna aliekuwa akitoka jikoni na alionekana alikuwa akipika
“Mwaaa.,,, Welcome home Babe” Roma hakutarahia ukaribisho wa aina hio kabisa na macho yake yote yalikuwa kodo akiangalia mbele.
ITAENDELEA…..
Summary ya simulizi tulipotoka
Mpaka sasa nadhani tumeweza kuona chimbuko la Hades kwanzia mwanzo wa simulizi hii , tumeweza kumfahamu licha ya kwamba ni sehemu ya miungu kumi na mbili ya kipagani(Greek Olympian Gods) lakini yeye ni wa tofauti na wenzake.
Hades yeye kwa jinsi utlivyoona ni kwamba ni sehemu ya miungu ambaye sifa yake kubwa ni kwamba yeye ni ROHO HURU yaan hana muunganiko wowote na miungu mingine.
Tumeweza pia kuona misheni ya Athena ambaye anafahamika kwama The Don ndani ya ulimwengu wa wahalifu(Underwold) lakini pia kama Minerva ndani ya tamaduni za Kiroma.
Tumeshuhudia pia misheni kubwa ambayo Athena anayo ni kutaka kurudisha hai Roho za ndugu zake zilizomezwa na binadamu , roho ambazo zimetokea Pamoja na yeye katika sayari ya Utopia mara baada ya maangamizo na Mungu.
Sasa kama misheni yake itafanikiwa kutokana na maelezo ya Hades wa Zamani kupitia mawakala wake kama vile mtoto wa Profesa Banosi , mchungaji, lakini pia Shekh Assad ni kwamba dunia itabadilika kwa kiasi kikubwa sana na huenda hata ile amani ambayo ipo kwa sasa kutoweka na ikumbukwe kwamba chanzo cha maangamizo ya sayari ya Utopia ni kutokana na kumkaidi Mungu mara baada ya kuona wanao uwezo wa kufanya mambo makubwa Zaidi ya Mungu kupitia sayansi.
Athena pia anaelezea nia yake ya kutaka kuunda dini moja na kushawishi binadamu kuacha kumtumikia Mungu ambaye haonekani na kumtumikia Mugu ambaye atakuwa anaonekana , mungu ambaye atakuwa tayari kufanya miujiza yote huku akionekana , sasa kama tulivyo ona , ili mipango yake kuweza kufanikiwa mambo makuu mawili lazima yatimie kwanza lazima awapate wanachama wote wa Illuminat ambao anaamini wanachama hao wamebeba roho za ndugu zake , lakini baada ya hapo apate jiwe la Kimungu ambalo hajalipata bado , jiwe ambalo ndani yake kuna Roho ya Gaia(Mother of earth) , Roho ambayo itampa uwezo wa kutawala nafsi za miungu yote mingine na yeye pia na miungu hio kuweza kupata nguvu zao zote ambazo walipoteza mara walivyofika kwenye uso wa dunia, unafikiri atafanikiwa katika mipango yake.
Upande wa Edna pia anaonekana kutokufahamu kuwa alizaliwa na pacha ake , pacha ambaye anafahamika kwa jina la Seventeen , lakini pia anashindwa kufahamu kwmaba mama yake kifo chake sio cha kuitwa na Mungu bali kilisabishwa na First Lady mke wa baba yake mzazi ambaye bado hakuwa akimfahamu,
Edna anaendelea kutafuta siri iliopo juu ya kisasi ambacho mama yake alitaka kutimiza , kisasi ambacho mpaka muda huo hakufahamu kinahusiana na nini , mrembo Edna pia tunamuona hisia zake za mapenzi zikiibuka kwa mume wake wa mkataba Roma Ramoni licha ya udhaifu aliokuwa nayo mathalani kwa kupenda sana ngono na anaamua kuingia nae dili la kutokusumbua na michekupuko yake huku akitaka kuishi na Lanlan ambaye hafahamu kama ni mtoto wa Roma wa damu na pacha wake , yaani Seventeen.
Sasa unafikiri juu ya yote hayo nini kitaendelea , basi nikwambie tu simulizi ni ndefu sana na mimi SinganoJr nimejitolea kuhakikisha maswali yako yote nilioorodhesha na yale ambayo sijaorodhesha mwisho wa stori hii yanajibika kwa urahisi.