SEHEMU YA 358
Ilionekana pia Blandina aliwasiliana na Edna pia kumuelezea kile kinachoendelea ndio maana alirudi nyumbani haraka haraka, akiwa kama haamini kama kweli ndugu zake na Yezi wamejitokeza baada ya miaka mingi.
Edna hakujali wanaume hao walivyokuwa wakimwangalia kwa mshangao , bali alisogea na Kwenda kuketi kando ya Roma kwenye sofa na kuweka mkoba wake pembeni.
“Kama wewe ni Park JongHyun basi naamini babu yake na Yezi atakuwa ni Park Juan mwanzilishi wa kampuni ya Starmoon Group?”Aliongea Edna
“Yeah My Grandfather is Park Juan , you must be Boss Edna From Vexto international Group . your reputation precedes you , its my honor to meet you”
“Ndio babu yangu ni Park Juan , lazima utakuwa ni Boss Edna kutoka kampuni ya Vexto Sifa zako zinakutangulia, ni heshima sana kwangu kukutana na wewe”Aliongea huku akishindwa kuzuia mshangao wake juu ya urembo wa Edna , alijikuta akimeza mate kwa wakati mmoja huku akipena mkono na Edna.
“Mke wangu unaonekana kuifahamu vizuri hii kampuni ya StarMoon, unaonaje ukinielezea kidogo maana sijawahi kuisikia”Aliongea Roma na kumfanya Edna kidogo kumshangaa.
“Starmoon Group is one of the largest chaebols in Korea. President Park is a legendary businessman from Korea. Starmoon has significant market shares in both the automotive and electronics industries. At the same time, they do real estate, tourism, and various retail chains. Mr Park Juan has been shortlisted as one of the top ten wealthiest people in Asia for over a decade. It’s estimated that Starmoon Group is worth more than 100 billion US Dollars. It’s seriously an impressive family business.”
“Starmoon ni jumuia ya makampuni yaliopo chini ya kampuni moja kutoka Korea ikiwa kama sehemu ya Chaebol kubwa zaidi , CEO Park ni shujaa na mfanyabiashara maarufu Zaidi kutoka Korea anaemiliki hii kampuni ya Starmoon ambayo inamiliki hisa nyingi sana katika soko la magari na vifaa vya kielekroniki, lakini sio hivyo tu kampuni yake inajihusha na maswala ya ‘Real Estate’(Biashara ya mali zisizohamishika), utalii pamoja na minyororo ya biashara mbalimbali , Park Juan ameorodheshwa kama mmoja wa watu kumi matajiri Zaidi barani Asia kwa Zaidi ya miongo kadhaa , inakadiriwa makampuni ya Starmoon yenyewe tu yana thamani ya ‘Asset’ Zaidi ya Dollar bilionni 100, ni biashara ya kuvutia ya kifamilia”Aliongea Edna kwa mchecheto mkali sana na Roma aliweza kuelewa sasa kweli babu yake Yezi alikuwa na pesa nyingi , maana kampuni kuwa na thamani ya Dollar bilioni mia moja ni pesa nyingi ambazo hata kwa kampuni ya Vexto ilikuwa nyuma sana , lakini hata hivyo kwake haikumshtua sana kwani sio mtu wa kujali sana pesa.
“Miss Edna sikujua kama utakuwa na maelezo ya kutosha kuhusu kampuni yetu, ulichoongea ni sahihi kabisa , ijapokuwa Maisha ya babu yangu yamekuwa ya kujificha ficha , lakini naweza kusema kwamba najivunia kwa mafanikio yake, lakini pia niseme kwamba hata kwako wewe Boss Edna hakika ni mfanya biashara mkubwa kwani kuwa na kampuni kubwa Zaidi tena kutokea Tanzania ni swala ambalo watu wengi hawawezi kulifanikisha kwenye Maisha yao”Aliongea na Edna alijikuta aakitabasamu.
“Hata wewe Mr Park ni mfanyabiashara mkubwa , umeweza kuwa mkurugezi wa makampuni ya Starmoon ukiwa kwenye umri wa miaka therathini tu , ni hakika unaweza kuwa mrithi siku za usoni”Aliongea Edna.
“Hapana mimi sitokuwa mrithi , nina msaidia babu kwa muda tu , swala lakuja mpaka Tanzania kwa ajili ya Yezi ni kwajili ya kumrudisha Korea kwa ajili ya kumrithi babu”Aliongea na kuwafanya wote kushangaa akiwemo Roma
“Lakini Yezi bado ni mdogo sana hata miaka ishirini bado hajafikisha , siamini kama kweli mnataka kumuachia aongoze kampuni yenye thamani ya mabilioni?”
“Miss Edna hakika naelewa wasiwasi wako , lakini Yezi hatokuwa peke yake , kuna watu wengi kwenye ukoo ambao watampa msaada, Yezi kuwa mrithi imekuwa ndoto ya kubwa ya babu ambayo anataka kuiona kabla ya kifo chake”Walijikuta wote wakiwa kwenye mshangoa ,sio kwamba jambo hilo halikuwa likiwezekana , lakini ilikuwa ngumu kwa wao kuamini kama Yezi ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa kibiashra kuweza kuongoza kampuni kubwa kama hio.
Muda huo huo wakati wakiendeleza maongezi , alionekana Yezi akishuka kutoka juu gorofani , akiwa na macho mekundu yaliovimba kutokana na kulia, bwana Park baada ya kuja hapo alimuelezea Yezi kwa ufupi kilichotokea mpaka akajikuta akiwa analelewa kama yatima na alijikuta akiwa ni mwenye kukasirika kweli.
“Cousin I am real your relative , please come back to Korea with us”Aliongea bwana Park akiwa amesimama.
“Siwezi kwenda Korea , nyie watu ni mashetani kisa mna hela , huenda yote haya Maisha niliokuwa nayo ni kutokana na kumfanya kitu kibaya mama yangu, naomba urudi tu na uwaeleze ndugu zenu kwamba mimi sio mkorea bali ni Mtanzania”Aliongea kwa hasira pasipo ya kujali kama ameelewa au hajaelewa kwani alitumia Kiswahili.
Pia katika utafiti ambao familia ya Park waliweza kugundua mama yake na Yezi ni marehemu na inasemekana alifia ndani ya hospitali ya wilaya ya Bagamoyo baada tu ya kujifungua kwa kupoteza damu nyingi, ilioambatana na kupanda kwa presha na yote hayo aliweza kuambiwa Yezi ndio maana alikuwa kwenye kilio kikubwa sana kujua mama yake na baba yake wote wamefariki.
Park Jonhyun alitaka kuongea tena , lakini alizuiwa na Edna ambaye alisimama na Kwenda kumkumbatia Yezi na kumbembeleza.
“Nyie watu nadhani hamjafahamu ni Maisha gani ambayo Yezi aliweza kuishi alivyokuwa kituo cha kulelea Yatima, kama Yezi hataki kurudi Korea haina haja ya kumlazimisha kuondoka nae , ninamjali kama mdogo wangu na nitahakikisha anaishi vizuri na kufikia ndoto zake kimasomo”Aliongea Edna.
“Lakini Boss Edna…”Alitaka kuongea lakini Edna alimgeukia Roma ambaye muda wote alikuwa kimya.
“Roma ongea chochote kwanini upo kama gogo?”Aliongea Edna na kumfanya Roma kukuna kichwa chake.
“Bwana Park kama alivyosema mke wangu , haina haja ya kumfosi Yezi kuondoka na wewe na kurudi Korea nadhani hata nyie mnaona namna ambavyo mke wangu anamjali Yezi kuliko hata mimi mwenyewe mume wake , hivyo nadhani mnapaswa kuondoka, hamuwezi kurahisisha mambo kwasababu tu mnataka arudi”Aliongea Roma. Na kumfanya Park Jonhyun kushindwa kuongea chochote cha ziada Zaidi ya kusimama na kuaga.
“Mr Roma napaswa kutoa jibu kwa babu yangu Korea juu ya Yezi kurudi nyumbani , lakini nitamuelezaje kwamba Yezi hataki ukilinganisha na hali yake ya kiafya?”
“Wewe kaelezee kama vilivyo , huna haja ya kubadili maneno , babu yako hawezi kukulaumu kwa kushindwa kumrudisha Yezi nyumbani kwani asingetemgemea wewe kumfunga Kamba na kisha kumrudisha kwa ulazima”Aliongea Roma baada ya Roma kuwafikisha nje kwenye magari yao.
“Okey Mr Roma , kwasasa nadhani sina cha kufanya tena hapa Tanzania na nitarudi Korea na kuelezea kilichotokea , lakini hata hivyo licha ya kwamba sijafanikiwa awamu hii haimaanishi kwamba ndio mwisho wa Yezi kutotambua familia yake , nitarudi baada ya muda kwa ajili ya kumrudisha Korea, kwani ndio nyumbani kwake na ndio asili yake ilipo , hivyo Mr Roma naomba uendelee kumshawishi”
“Okey hakuna shida , nitajitahidi japo sitaki kukuahidi chochote kwani mwamuzi wa mwisho ni Yezi”Aliongea Roma na kisha wakaagana , lakini kabla hajaingia ndani gari nyingine aina ya Maserati ya rangi ya bluu ilifika eneo hilo na mlio wa breki ndio uliomfanya Roma kugeuka na aliweza kumuona mwanamke akitoka kwenye gari akiwa amevalia miwani ya jua , Roma aliweza kumtambua mara moja , kwani alikuwa ni Yoon He, kwa muonekano wa Yoon He ni Dhahiri kabisa alikuja hapo kwa haraka kwani hakuwa hata amejiremba kama ilivyokuwa kawaida yake.
“Jonghyun siamini kama ni wewe?”Aliongea YoonHe kwa kikorea akishindwa kujali uwepo wa Roma mita kadhaa.
Park Johyun alimwangalia Yoon He na kisha akapumua kama mtu ambaye hakupenda kuonana na mwanamke huyo.
“YoonHe unafanya nini hapa? , si nilisha kuonya usinifatilie fatilie”Aliongea kwa Kikorea akiwa siriasi.
Kutokana na jibu alilotoa Jonghyun , lakini pia muonekano wake, Roma aliamini wawili hao kuna kitu ambacho sio cha kawaida kinaendelea baina yao na ilimfanya kutoingia ndani kwanza ili kuendelea kujua ni nini kinaendelea. Na haraka haraka alihisi huenda ni maswala ya kimapenzi , kwani ni jambo la kawaida sana kwa mtu tajiri kama Park Jonghyun kutembea na mwanamke Star kama Yoon He.
“Yoon He naomba usiendelee kunifuatilia , nishakuambia mara kibao kwamba sina hisia na wewe”Aliongea na kisha aliingia kwenye gari pasipo ya kumjali lakini kabla hajafunga vioo Yoonhe aliinama kumwangalia kwa kioo cha gari.
“Unadanganya , unadangaya najua unanipenda ila unaogopa kwasababu tukiwa wapenzi watu wataanza kutuzungumzia , najua unanipenda sana Jonghyun”
“Unafikiri naogop watu kunizungumzia , kama nilikuwa nikiogopa nisingeanzisha mahusiano na wewe tokea mwanzo, ni kweli wewe ni mwanamke mrembo , lakini sikupendi kutokana na maringo yako na roho yako isiokuwa na utu, uvumulivu wangu una kikomo hivvyo nakuonya mara ya mwisho usinifuatilie vuatilie”
“Acha kujishaua Jonghyun najua umekuja Tanzania kwa ajili yangu pekee,, kwanini usiwe muwazi”Aliongea lakini mara baada ya kumaliza sentensi yake alijikuta ni kama kuna kitu kimemjia akilini na alinyanyua uso wake na kumwangalia Roma aliekuwa mita kadhaa na Roma mara baada ya mwanamke huyo kumwangalia alimpungia mkono na kutabasamu.
“Kwahio hiki ndio kilichokuleta hapa … Hahaha masikini Jonghyun kumbe…”Alijikuta akishindwa kuendelea kuongea kutokana na kuzidiwa na kicheko alikuwa kama chizi .
“Jonghyun naamini pua yako inaweza kunusa mbali sana , lakini nikushauri usiwe ni mwenye furaha kwa sasa mimi sio mjinga na wengine pia kwenye familia yetu sio wajinga, Park Jonghyun itafika muda ambao utataka unipigie magoti .. na hio siku ikifika nitahakikisha unalamba miguu yangu “Aliongea kwa Lugha ya Kikorea ambayo ilisikika vyema masikioni mwa Roma.
“Wewe ni mwanamke mjinga sana sijawahi kuona”Aliongea na kisha alimwangalia Roma aliekuwa amesimama mita kadhaa kutoka kwao.
“Mr Roma please disregard this crazy woman , I sincerely hope to gain your assistance , which I’ll surely reward greatly”
“You are welcome”Aliongea Roma huku akimpungia mkono na Park Jonghyun alipandisha kioo na palepale magari yaliondoshwa akiachwa Yoon He akiwa amesimama.
Yoonhe baada ya kuachwa alimgeukia Roma na kumwangalia kwa macho yaliojaa dharau na kisha aliingia kwenye gari yake na kuondoka eneo hilo.
Roma alivyogeuka aliweza kumshuhudia Edna akiwa amesimama mlangoni na alijikuta akitabasamu na kumsogelea.
“Babe wife umekoswa na tamthiliya ya kibabe , nyie si mnapenda kuangalia filamu za kikorea , basi kilichokuwa kikiendelea hapo nje ni uhalisia kabisa na mnachozoea kuangalia”
“Wamesemaje?”
“Mambo ya mapenzi ya watu walioachana kati ya Yoon He na Park Jonghyun , inaonekana mapenzi yao yamegeuka na kuwa chuki”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuwa na wasiwasi
‘Mh! , Naamini pia kwa huyu Park Jonghyun nia yake ya kumtaka Yezi kurudi Korea ni zaidi ya tunavyofahamu , YoonHe najua pia upande wa familia yake ina uwezo mkubwa kiuchumi na bado sijajua kwa undani, naamini uhusiano wao una mambo mengi makubwa Zaidi , kwasasa siwezi kuongea chochote , Yezi hisia zake sasa hivi hazipo sawa na siwezi kumwambia chochote”
“Ni kweli unachoongea mke wangu , hata mimi siwezi kuchukulia swala hili kirahisi hivyo”
“Hata wewe umehisi kuna kitu hakipo sawa?”Aliongea Edna akionekana kuwa mtu ambaye anahitaji uthibitisho wa maneno yake.
“Ndio sikutaka kuongea chochote maana nilihitaji tu waondoke hapa , lakini kwasababu babe wangu unataka niongee basi nitakuambia ninachohisi..”
“Kwanza nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kama kampuni kubwa kama ya StarMoon inayojiendesha kwa mabilioni ya hela kurithishwa kwa mtoto aliepotea kwa miaka mingi ambaye Maisha yake yote ni ya hapa Tanzania , ambaye hata tamaduni za Kikotea hazifahamu, ijapokuwa Park Jonhyun maneno yake yamejaa urembo wa kutaka kumrudisha Yezi Korea , lakini alichoongea ni upumbavu kabisa ambao hauaminiki, lakini hata hivyo licha ya kwamba Yezi hataki kurudi Korea haimaanishi kwamba baadae hatorudi , siku zote damu ni nzito kuliko maji na Yezi lazima atarudi kwenye familia yake , lakini kuhusu kurithi kampuni , hilo siamini kama litakuja kutokea, naamini kuna mpango unaandaliwa Zidi ya Yezi baada ya babu yake kuweka wazi nia yake thabiti ya kutaka kumrithisha na hili ndio linalomuweka kwenye hatar”
“Sasa ni kipi ambacho wanataka kumfanya Yei , Maisha yake ya makuzi yenyewe yalikuwa na shida lakini bado matatizo yanaonekana kutaka kumuibukia mbele”Aliongea Edna kwa kutia huruma.
“Hata mimi kwa sasa siwezi kujua mpango wao , lakini inaonekana Yezi ni muhimu Zaidi kwa Park Jonghyun , umesema kwamba yeye ni Mkurugenzi wa Starmoon basi naamini anajua kila kitu kinachoendelea ndani ya familia na kwenye kampuni , lakini pia anaonekana kuwa muigizaji mzuri , lakini hata hivyo jambo moja ambalo ninashauku nalo ni kutaka kujua uhusiano uliokuwepo kati ya Yoon He na yeye , kwa muonekano wake siamini kama angeweza kujihusiha kimapenzi na mwanamke kama Yoon He tokea mwanzo kuna Zaidi ya mahusiano ya kimapenzi”Aliongea Roma
“Muda ule niliona ni vyema kama Yezi angerudi kwa familia yake , lakini sikutaka aondoke na Park Jonghyun , nilitaka wewe ndio umpeleke , lakini kwa namna ulivyozungumzia hili swala naona ni vyema Yezi akabakia tu Tanzania na wasimsumbue tena , lakini nimeshangazwa sana na Yezi kuwa na damu ya familia kubwa kama Ya Park”Aliongea Edna.
“Babe usifikirie sana kuhusu haya , unaonaje ukaenda kuandaa msosi mumeo nina njaa, babe siku hizi unajua kupika tofauti na nilivyokuoa”Aliongea Roma
“Hivi kwanini unapenda sana kula , si ufikiri namna ya kumsaidia Yezi muda huu , mtoto yupo juu analia mwenyewe lakini wewe unawaza kula tu”Aliongea Edna lakini Roma alimpita akijifanyisha hajamsikia na kumfanya Edna kukasirika na kumfuata kwa nyuma.
Sasa hapo unachotakiwa kuelewa kwanza kabisa YoonHe mtu ambaye alizungumza nae wiki kadhaa zilizopita kwa njia ya simu na kumuita baba sio mtu kutoka familia ya Park kwani kwanza kabisa jina lake halikuwa na uhusiano wowote na wa Park Family.
Upande wa Roma alishahisi tokea mwanzo kabisa Yezi familia yake sio ya kawaida kutokana na kidani alichokuwa nacho ambacho kilikuwa kikimtambulisha wazazi wake tokea siku ile anakabidhiwa hicho kidani na Yezi ndio maana siku ile alishangaa sana na kujiuliza ilikuwaje mtoto kama huyo kua na aina hio ya kidani halafu akawa na Maisha ya tabu namna ile.
Unafikiri ni mpango gani unaendelea , je Yezi atarudi Korea?”
SEHEMU YA 359
Zikiwa zimebaki siku kadhaa kufikia tarehe ya Vexto kuweza kuanza usambazaji wa malighafi mpya kupitia mkataba waliosaini na kampuni ya Yamakuza wakishirikiana na kampuni ya Maple Group.
Ikiwa ni siku ya ijumaa , Roma akiwa nyumbani kwa Nasra akimbembeleza mama yake na Nasra kumkubalia ili kuendelea na mtoto wake, Nasra aliekaa pembeni aliweza kupokea simu kutoka kwa mafanyakazi aliekuwa akikamu nafasi yake ya uhasibu ndani ya kampuni ya Vexto.
“Zaina kuna nini?”Aliongea Nasra kwa wasiwasi kwani hakuwa akitegemea simu ya Zaina msaidizi wake kumpigia wakati kama huo wa jioni.
“Boss angalia hisa za kampuni yetu zinavyoporomoka kwa kasi kutokana na taarifa inayosambaa mtandaoni”Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Nasra kukata simu haraka haraka na kuingia upande wa mtandaoni na kuangalia nini kinachoendelea na kumfanya hata Roma aliekuwa akiongea na mama yake kushangazwa kidogo na mabadiliko ya ghafla ya Nasra.
“Nasra kuna nini..?”Aliuliza Roma na Nasra hakujibu Zaidi ya kuangalia simu yake , lakini muda huo huo na simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mpigaji ni Daudi msaidizi wake.
“Director umeweza kuona kinachoendelea mtandaoni?”Aliuliza Daudi.
“Sijaweza kuona , ni nini kinaendelea?”
“Kuna siri za kampuni ambazo zimevuja na zinasambaa mtandaoni , mikataba yote ya kampuni iliosainiwa na ile ambayo inapangwa kusainiwa na kampuni imewekwa mtandaoni na mtu asiefahamika na kufanya hisa za kampuni kushuka thamani kwa kiwango kikubwa ndani ya lisaa limoja”Aliongea Daudi na kumfanya Roma mpaka hapo kuelewa ni kwanini Nasra alibadlika ghafla , mpaka hapo aliamini mke wake alikuwa kwenye matatizo.
“Daudi asante kwa taarifa ngoja nifautalie hili”Aliongea Roma na kisha alikata simu na palepale alitafuta namba ya simu ya mke wake Edna huku akinyanyuka kwenye sofa , lakini simu ilionekana kuita tu bila kupokelewa , ilibidi kumtafuta mama yake nyumbani na kuulizia kama Edna kasharudi , lakini aliambiwa bado alikuwa kazini.
Roma na Nasra wote wlaijikuta wakiwa kwenye wasiwasi na ilibidi watoke kwa pamoja na kuelekea posta makao makuu ya kampuni ya Vexto .
Dakika chache tu Roma na Nasra waliweza kufika na kutokana muda huo ilikuwa ni wa saa kumi na wafanyakazi wengi washatoka kazini , kampuni ilionekana kutulia , lakini Roma aliweza kuona gari ya mke wake ikiwa imeegeshwa na alijiambia bado atakuwa kazini.
Roma baada ya kuingia ofisini kwa mke wake , Edna alionekana akiwa ameketi kwenye kiti chake cha mzunguko, na kwa kumuangalia tu aliamini Edna hakuwa sawa kimawazo , kwani macho yalikuwa mekundu.
“Edna nini kimetokea , imekuwaje siri za kampuni zikasambaa mtandaoni?”Aliuliza Nasra kwa wasiwasi huku akihema na Edna ilibidi awaangalie watu waliokuwa mbele yake na alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja.
“Nashindwa kuelewa nini kimetokea, lakini kwa namna moja ama nyingine naamini kuna mtu yupo nyuma juu ya hili swala na amechagua siku hii ya ijumaa wafanyakazi wakiwa wanatoka kazini ili kuweza kufanikiwa katika malengo yake”Aliongea Edna na kumfanya Roma kumuonea huruma Edna kwani sauti yake ilionekana kuwa ya kinyonge mno.
“Nasra jaribu kuangalia kama kuna wafanyakazi wa upande wa fedha waliobakia kazini ambao wataweza kutusaidia angalau kudili na hii hali”Aliongea Edna na Nasra alitingisha kichwa na akatoka nje haraka lakini muda huo mlango wa ofisi ya Edna uliweza kufunguliwa, na alionekana mwanadada Benadetha akiingia hapo ndani mkuku mkuku na alionekana kuwa na wasiwasi kweli na ile anaingia ndani tu aliangaliwa na Edna kwa macho yasio kawaida na kujikuta akizidi kutetemeka.
Taarifa iliokuwa ikisambaa mtandaoni ilikuwa ikihusina na mafaili ya siri sana ambayo alikabidhiwa Benadetha siku kadhaa zilizopita na Edna akayatunze kwenye ofisi yake , kwahio ni Dhahiri moja kwa moja mtu ambaye angeshukiwa kwa kuvuja kwa taarifa hizo ni Benadetha pekee.
“Boss sio mim niliovujisha, naapa kwa mungu wangu ninaemsalia sihusiki katika hili”Aliongea Benadetha na alivvyokuwa na wasiwasi , ilimfanya hata Roma kuona huruma kwani hakuwahi kumuona Benadetha kuwa kwenye hali kama hio.
“Nini kinaendelea , mbona sielewei , Edna niambie ni nini kinaendelea , kwanini Benadedhta anasema sio yeye?”Aliongea Roma akitaka maelezo na Edna alielezea kwa ufupi kwamba taarifa inayosambaa mtandaoni ilikuwa kwenye faili la siri la kampuni ambalo lilikuwa likimilikiwa na mkuu wa idara ya Masoko pamoja na uhusiano wa jamii ambaye ni Banadetha , Roma baada ya kusikia taarifa hio alijikuta akishangazwa sana.
“Wife naamini sio Benadetha, ijapokuwa simafahamu vizuri Benadetha lakini kwa machache ninayomfahamu nayo hawezi kuvujisha siri za kampuni mitandaoni”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumkata jicho la hasira.
“Boss ni kweli taarifa zinazosambaa zilikuwa chini yangu , lakini sihusiki kabisa , siwezi kufanya jambo kama hili”
“Benadetha usilie , kaa kwanza kwenye sofa , mimi pia nakuamini huwezi kuvujisha siri za kampuni kwenye mitandao”Aliongea Roma huku akimsogelea Benadetha na kisha akamkarisha chini kkwenye sofa na kisha akamgeukia Edna.
“Edna naamini katika hili swala hata wewe unajua ni dhaihiri kabisa mtu ambaye anahusika ni washindani wako wa kibiashara , siamini kama Benadetha anaweza kuhusika na swala hili”Aliongea Roma.
“Roma huu sio muda wa wa kumtetea Benadetha , kwani mafaili yote yalikuwa chini yake na nilimkabidhi mimi mwenyewe na nilimpa maagizo ya kuyatunza vizuri, awe amehusika au hajahusika ni mtuhumiwa namba moja na haupo kwenye nafasi ya kumtetea”Aliongea Edna akiwa katika ubora wake wa ukauzu na maneno yake yalivyokuwa makali ilimfanya Benadetha kuanza kulia Zaidi, kwa mara ya kwanza hakuamini jambo hilo linaweza kutokea ndani ya kampuni na mshukiwa wa kwanza akawa yeye.
Muda huo huo mlango wa ofisi ya Edna ulifunguliwa na Monica na alimtaarifu kwamba watu kutoka polisi wamefika na Edna aliwaambia waingie na muda huo huo waliingia wwanaume wawili na mwanamke mmoja waliovalia sare za kipolisi.
Kitendo cha kuingia kwa polisi hao kilimshutua sana Roma , kwani alijua mtu anaekuja kukamatwa ni Benadetha na ilikuwa kweli kwani baada tu ya kuingia ni kama walikuwa na taarifa zote.
“Miss Benadetha upo chini ya ulinzi kwa kosa la kuvujisha siri za kampuni , una haki ya kuomba mwanasheria, lakini kwa sasa unapaswa kuongozana na sisi mpaka kituo cha polisi kwa mahojiano”Aliongea yule polisi wa kike na alimsogelea Benadetha aliekuwa akitetemeaka na kisha akamfunga pingu mikononi.
“Edna hii sio sawa kabisa , huwezi ukamuacha Benadetha kupelekwa polisi , najua ni mshukiwa lakini swala hili linaweza kuisha hapa hapa sio lazima apelekwe kituoni”
“Mr Roma sina ujuzi wowote wa kuhoji watuhumiwa na Benadetha ataenda Polisi kwa ajili ya mahojiano na kama hajahusika basi ataachiwa, Afande mnaweza kuondoka nae tu”Aliongea Edna na kisha aligeuza kiti na kuangalia upande wa nje.
“Boss sihusiki katika hili , naomba usiwaruhusu wakinipeleka kituoni tafadhari”
“Benadetha sina cha kukusaidai kwa sasa ,, unajua ni hasara kiasi gani nimepoteza ndani ya lisaa limoja tu, naomba unisamehe ila siwezi kuzuia wasiondoke na wewe”Aliongea Edna na kwa jinsi sauti yake ialivyokua kavu ilimfanya Roma sasa kuona upande mwingine wa Edna ambao hakuwahi kuuona na alijikuta akishindwa kujua cha kufanya.
Dakika chache tu Benadetha aliekuwa akilia alitolewa na kuchukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha magogoni kwa ajili ya mahojiano.
Roma alijitahidi kumsihi Edna asiruhusu Benadetha kulala kituoni , lakini Edna alikuwa ni kama gogo, hakusikia la kuambiwa kabisa na kadri ambavyo Roma alikuwa akimbembeleza ndio ambavyo alikuwa akipandwa na hasira Zaidi, kilichofanya kukasirika Zaidi ni kwamba badala ya Roma kukaa upande wake yeye kama mume , alikuwa upande wa mhalifu Benadetha na hicho kilimuuzi sana , ukichanganya na wivu alimkaushia kabisa Roma.
“Kama kilichokuleta hapa ni kumsaidia Benadetha basi nikuambie sina cha kufanya na naomba uondoke nahitaji kuwa mwenyewe , kama unamjali sana na unaamini hajahusika tafuta muhusika ukamtoe kituoni”Aliongea Edna kwa sauti kavu na Roma alijikuta akipandwa na hasira lakini hakutaka kuzionyesha wazi zaidi ya kutoka ndani ya ofisi hio na ile anafika nje ya mlango aliweza kukutana na CEO msaidizi Ernest Komwe ambaye na yeye alioenekana kufika kwenye kampuni mara baada ya kusikia taarifa iliokuwa ikiendelea na Roma hakutaka kumjali kwani alimpita bila hara ya salamu.
Roma wakati akiwa kwenye gari alijikuta akiwa ni mwenye mawazo sana yaliochangayika na hasira , alimuona Edna kama mwanamke mkatili sana hasa ukizingatia namna ambavyo Benadetha alikuwa akijituma likija swala la kazi , aliona kitendo cha Benadetha kuchukuliwa na polisi kama mhalifu na kupelekwa kituoni haikuwa cha kiuungwana kabisa.
*********
Upande mwingine ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu julias Kambarage Nyerere , alionekana mrembo Queen alievaa akapendeza akiwa amesimama katika eneo la kupokelea wageni akiwa ameambatana na dada yake Matilda ambao wote walikuwa wamevalia miwani za jua, walikuwa wamependeza sana ukijumlisha na uzuri wao ulifanya baadhi ya vidume waliokuwa maeneo hayo kumeza mate kwa uchu.
Queen na Matilda walionekana wapo mahali hapo kwa ajili ya kumpokea mtu ambaye anawasili kutoka nje ya nchi , kwani walikuwa ndani ya jengo la Terminal 3 ambalo linahudumia wasafari wanaofika kutoka mataifa ya nje.
Matilda muda wotea likuwa akiangalia simu yake huku akiwa anatabasamu , ukumbuke muda huu ilikuwa ni muda wa saa kumi muda sawa na kile kinachoendelea ndani ya kampuni ya Vexto na Matilda alikuwa akiangalia namna hisa za kampuni ya Vexto zinavyoshuka kwa kasi na alijikuta akiwa ni mwenye furaha mno kutokana na matokeo hayo.
“Edna awamu hii ukitoka kwenye huu mtego utakua na heshima yangu”Aliwaza Matilda huku akiweka tabasamu la kifedhuli kwenye uso wake akiendelea kuangalia abiria wanaoingia na kutoka ndani ya jengo hilo.
“Dada nina hamu kweli ya kumuona baba?”
“Kweli eh! Mwenzio nikajua humpendi na unakuwa na amani akiiishi nje ya nchi kuliko akirudi”Aliongea Matilda na kumfanya Queen amwangalie dada yake kwa macho yasiokuwa yakawaida.
“Nani kasema simpendi , unapenda sana kunisukumizia kile unachojisikia kwenye moyo wako mimi Matilda , nampenda baba na nafurahi akiwa nyumbani”Aliongea huku akijinunisha na kumfanya Matilda kutabasamu.
“Nilikuwa nakutania tu , kinachokufanya kujaa povu ni nini ,niliona utakosa uhuru wa kula bata na mchina wako”Aliongea Matilda na kumfanya Queen kumwangali dada yake kwa mshangao.
“Umejuaje natoka kimapenzi na mchina?, nakumbuka sijawahi kukuelezea chochote kuhusu mtu ninaetoka nae”Aliongea Queen na kumfanya Matilda kucheka kidogo kicheko cha kebehi.
“Nilikiuona hoteli ya Serena , wiki kadhaa zilizopita ukiwa na mchina wako mnakula ‘Goodtime’, sikutaka kukushitua tu kwasababu nilikuwa na mambo yangu na mimi”Aliongea na kumfanya Queen kupooza kidogo lakini tabasamu likaibuka upya.
“Kama ushajua sitaki umuite Mchina , jina lake ni Profesa Yan Buwen , labda hata haujawahi kumsikia kwasababu haupo kwenye fani ya Sayansi , ukigoogle tu utaona jina lake , ni mwanasayansi maarufu”Aliongea Queen kwa kujigamba na kumfanya Matilda kuvuta mdomo akionekana kutokubaliana na mdogo wake.
“Huamini , ngoja nikuonyeshe “Aliongea na kisha alianza kutafuta kwenye mtandao jina la Yan Buwen na ndani ya dakika moja tu alipata na kumuonyesha Matilda na kumfanya ashangae.
“Wewe muongo Queen, mwanasayansi mkubwa kama huyu afanye nini hapa Tanzania halafu awe na mpenzi kama wewe”
“Usichoamini nini sasa , subiri siku nitakayo mtambulisha kwako ndio utajua ni ukweli au uongo”Aliongea Queen huku akimpokonya Matilda simu yake.
“Queen awe Yan Buwen au asiwe Yan Buwe hainihusu , lakini kwa jinsi nilivyowaona pamoja na yule mchina hakupendi na anakuchezea tu, najua umempenda kwasababu amekutoa bikra na hilo ni kosa litakalo kugharimu mdogo wangu”Aliongea Matilda na Queen alijikuta akimkata dada yake jicho lisilokua la kawaida.
“Ananipenda au hanipendi , hayakuhusu Matilda , huyo mwanaume anaekupenda wewe kwanza yuko wapi au kazi kujaji mahusiano yangu, unaona wivu nikidate na mwanasayansi mkubwa”
“Haha.. Masikini Queen , ndio alivyokudanganya kwa kujifananisha na mwanasayansi mkubwa.. haya bwana sitii neno”Aliongea Matilda na muda ule ule abiria mbalimbali walianza kutoka wakiwa wanaburuza mabegi yao na ndani ya dakika kama mbili tu hivi Queen ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Mzee Alex akitoka akiwa ametangulizana na kijana mmoja mtanashati sana alievalia miwani ya jua , mwenye mwili uliojengeka kimazoezi.
Mwanaume yule mara baada ya kumuona Queen alijikuta akisimama akiwa kama anashangaa.
“Hahaha..Queen mpenzi wako wa utotoni huyo”Aliongea Matild huku akisogea upande ambao anakuja baba yake ,Mzee Alex kwa ajili ya kumpokea , huku upande wa Queen akionekana furaha yake yote kuyeyuka ghafla.