Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Tushasikia unachomaanisha. Tulipe!!! Kwa hivyo kama huna jingine fyata mkia. Kama huna contenti nyingine, enda Whatsapp utilize kalio huko. Shenzi!!!
Sasa msimsumbue mwandishi kila mda kuuliza anaweka saa ngapi kama unaona una haraka nenda wasap ununue ila kama huna hela kaa utulie siyo kila mda kumwita Singano siku akijisikia ataweka
 
Sasa msimsumbue mwandishi kila mda kuuliza anaweka saa ngapi kama unaona una haraka nenda wasap ununue ila kama huna hela kaa utulie siyo kila mda kumwita Singano siku akijisikia ataweka
Punguza kihelehele na sura lako kama avatar yako.
 
Usimwitee kila mda kaa utulie siku akijisikia atatums
Ni mkeo??? Kama ana shida ya kuitwa na mafans wake ni yeye ambaye anafaa kusema hilo. Wacha kiherehere mwenzangu. Ama unadhani atakukatia tonge la Whatsapp baada ya kulialia watu walipe???
 
Sasa msimsumbue mwandishi kila mda kuuliza anaweka saa ngapi kama unaona una haraka nenda wasap ununue ila kama huna hela kaa utulie siyo kila mda kumwita Singano siku akijisikia ataweka
sema unajua nini wewe kama ni mtoto wa kiume punguza kiherehere utapakatwa ila kama wewe ni kibinti unaweza endelea na nyege zako siku ukipata wa kukuna fresh utulie sasa
 
SEHEMU YA 358

Ilionekana pia Blandina aliwasiliana na Edna pia kumuelezea kile kinachoendelea ndio maana alirudi nyumbani haraka haraka, akiwa kama haamini kama kweli ndugu zake na Yezi wamejitokeza baada ya miaka mingi.

Edna hakujali wanaume hao walivyokuwa wakimwangalia kwa mshangao , bali alisogea na Kwenda kuketi kando ya Roma kwenye sofa na kuweka mkoba wake pembeni.

“Kama wewe ni Park JongHyun basi naamini babu yake na Yezi atakuwa ni Park Juan mwanzilishi wa kampuni ya Starmoon Group?”Aliongea Edna

“Yeah My Grandfather is Park Juan , you must be Boss Edna From Vexto international Group . your reputation precedes you , its my honor to meet you”

“Ndio babu yangu ni Park Juan , lazima utakuwa ni Boss Edna kutoka kampuni ya Vexto Sifa zako zinakutangulia, ni heshima sana kwangu kukutana na wewe”Aliongea huku akishindwa kuzuia mshangao wake juu ya urembo wa Edna , alijikuta akimeza mate kwa wakati mmoja huku akipena mkono na Edna.

“Mke wangu unaonekana kuifahamu vizuri hii kampuni ya StarMoon, unaonaje ukinielezea kidogo maana sijawahi kuisikia”Aliongea Roma na kumfanya Edna kidogo kumshangaa.

“Starmoon Group is one of the largest chaebols in Korea. President Park is a legendary businessman from Korea. Starmoon has significant market shares in both the automotive and electronics industries. At the same time, they do real estate, tourism, and various retail chains. Mr Park Juan has been shortlisted as one of the top ten wealthiest people in Asia for over a decade. It’s estimated that Starmoon Group is worth more than 100 billion US Dollars. It’s seriously an impressive family business.”

“Starmoon ni jumuia ya makampuni yaliopo chini ya kampuni moja kutoka Korea ikiwa kama sehemu ya Chaebol kubwa zaidi , CEO Park ni shujaa na mfanyabiashara maarufu Zaidi kutoka Korea anaemiliki hii kampuni ya Starmoon ambayo inamiliki hisa nyingi sana katika soko la magari na vifaa vya kielekroniki, lakini sio hivyo tu kampuni yake inajihusha na maswala ya ‘Real Estate’(Biashara ya mali zisizohamishika), utalii pamoja na minyororo ya biashara mbalimbali , Park Juan ameorodheshwa kama mmoja wa watu kumi matajiri Zaidi barani Asia kwa Zaidi ya miongo kadhaa , inakadiriwa makampuni ya Starmoon yenyewe tu yana thamani ya ‘Asset’ Zaidi ya Dollar bilionni 100, ni biashara ya kuvutia ya kifamilia”Aliongea Edna kwa mchecheto mkali sana na Roma aliweza kuelewa sasa kweli babu yake Yezi alikuwa na pesa nyingi , maana kampuni kuwa na thamani ya Dollar bilioni mia moja ni pesa nyingi ambazo hata kwa kampuni ya Vexto ilikuwa nyuma sana , lakini hata hivyo kwake haikumshtua sana kwani sio mtu wa kujali sana pesa.

“Miss Edna sikujua kama utakuwa na maelezo ya kutosha kuhusu kampuni yetu, ulichoongea ni sahihi kabisa , ijapokuwa Maisha ya babu yangu yamekuwa ya kujificha ficha , lakini naweza kusema kwamba najivunia kwa mafanikio yake, lakini pia niseme kwamba hata kwako wewe Boss Edna hakika ni mfanya biashara mkubwa kwani kuwa na kampuni kubwa Zaidi tena kutokea Tanzania ni swala ambalo watu wengi hawawezi kulifanikisha kwenye Maisha yao”Aliongea na Edna alijikuta aakitabasamu.

“Hata wewe Mr Park ni mfanyabiashara mkubwa , umeweza kuwa mkurugezi wa makampuni ya Starmoon ukiwa kwenye umri wa miaka therathini tu , ni hakika unaweza kuwa mrithi siku za usoni”Aliongea Edna.

“Hapana mimi sitokuwa mrithi , nina msaidia babu kwa muda tu , swala lakuja mpaka Tanzania kwa ajili ya Yezi ni kwajili ya kumrudisha Korea kwa ajili ya kumrithi babu”Aliongea na kuwafanya wote kushangaa akiwemo Roma

“Lakini Yezi bado ni mdogo sana hata miaka ishirini bado hajafikisha , siamini kama kweli mnataka kumuachia aongoze kampuni yenye thamani ya mabilioni?”

“Miss Edna hakika naelewa wasiwasi wako , lakini Yezi hatokuwa peke yake , kuna watu wengi kwenye ukoo ambao watampa msaada, Yezi kuwa mrithi imekuwa ndoto ya kubwa ya babu ambayo anataka kuiona kabla ya kifo chake”Walijikuta wote wakiwa kwenye mshangoa ,sio kwamba jambo hilo halikuwa likiwezekana , lakini ilikuwa ngumu kwa wao kuamini kama Yezi ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa kibiashra kuweza kuongoza kampuni kubwa kama hio.

Muda huo huo wakati wakiendeleza maongezi , alionekana Yezi akishuka kutoka juu gorofani , akiwa na macho mekundu yaliovimba kutokana na kulia, bwana Park baada ya kuja hapo alimuelezea Yezi kwa ufupi kilichotokea mpaka akajikuta akiwa analelewa kama yatima na alijikuta akiwa ni mwenye kukasirika kweli.

“Cousin I am real your relative , please come back to Korea with us”Aliongea bwana Park akiwa amesimama.

“Siwezi kwenda Korea , nyie watu ni mashetani kisa mna hela , huenda yote haya Maisha niliokuwa nayo ni kutokana na kumfanya kitu kibaya mama yangu, naomba urudi tu na uwaeleze ndugu zenu kwamba mimi sio mkorea bali ni Mtanzania”Aliongea kwa hasira pasipo ya kujali kama ameelewa au hajaelewa kwani alitumia Kiswahili.

Pia katika utafiti ambao familia ya Park waliweza kugundua mama yake na Yezi ni marehemu na inasemekana alifia ndani ya hospitali ya wilaya ya Bagamoyo baada tu ya kujifungua kwa kupoteza damu nyingi, ilioambatana na kupanda kwa presha na yote hayo aliweza kuambiwa Yezi ndio maana alikuwa kwenye kilio kikubwa sana kujua mama yake na baba yake wote wamefariki.

Park Jonhyun alitaka kuongea tena , lakini alizuiwa na Edna ambaye alisimama na Kwenda kumkumbatia Yezi na kumbembeleza.

“Nyie watu nadhani hamjafahamu ni Maisha gani ambayo Yezi aliweza kuishi alivyokuwa kituo cha kulelea Yatima, kama Yezi hataki kurudi Korea haina haja ya kumlazimisha kuondoka nae , ninamjali kama mdogo wangu na nitahakikisha anaishi vizuri na kufikia ndoto zake kimasomo”Aliongea Edna.

“Lakini Boss Edna…”Alitaka kuongea lakini Edna alimgeukia Roma ambaye muda wote alikuwa kimya.

“Roma ongea chochote kwanini upo kama gogo?”Aliongea Edna na kumfanya Roma kukuna kichwa chake.

“Bwana Park kama alivyosema mke wangu , haina haja ya kumfosi Yezi kuondoka na wewe na kurudi Korea nadhani hata nyie mnaona namna ambavyo mke wangu anamjali Yezi kuliko hata mimi mwenyewe mume wake , hivyo nadhani mnapaswa kuondoka, hamuwezi kurahisisha mambo kwasababu tu mnataka arudi”Aliongea Roma. Na kumfanya Park Jonhyun kushindwa kuongea chochote cha ziada Zaidi ya kusimama na kuaga.

“Mr Roma napaswa kutoa jibu kwa babu yangu Korea juu ya Yezi kurudi nyumbani , lakini nitamuelezaje kwamba Yezi hataki ukilinganisha na hali yake ya kiafya?”

“Wewe kaelezee kama vilivyo , huna haja ya kubadili maneno , babu yako hawezi kukulaumu kwa kushindwa kumrudisha Yezi nyumbani kwani asingetemgemea wewe kumfunga Kamba na kisha kumrudisha kwa ulazima”Aliongea Roma baada ya Roma kuwafikisha nje kwenye magari yao.

“Okey Mr Roma , kwasasa nadhani sina cha kufanya tena hapa Tanzania na nitarudi Korea na kuelezea kilichotokea , lakini hata hivyo licha ya kwamba sijafanikiwa awamu hii haimaanishi kwamba ndio mwisho wa Yezi kutotambua familia yake , nitarudi baada ya muda kwa ajili ya kumrudisha Korea, kwani ndio nyumbani kwake na ndio asili yake ilipo , hivyo Mr Roma naomba uendelee kumshawishi”

“Okey hakuna shida , nitajitahidi japo sitaki kukuahidi chochote kwani mwamuzi wa mwisho ni Yezi”Aliongea Roma na kisha wakaagana , lakini kabla hajaingia ndani gari nyingine aina ya Maserati ya rangi ya bluu ilifika eneo hilo na mlio wa breki ndio uliomfanya Roma kugeuka na aliweza kumuona mwanamke akitoka kwenye gari akiwa amevalia miwani ya jua , Roma aliweza kumtambua mara moja , kwani alikuwa ni Yoon He, kwa muonekano wa Yoon He ni Dhahiri kabisa alikuja hapo kwa haraka kwani hakuwa hata amejiremba kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Jonghyun siamini kama ni wewe?”Aliongea YoonHe kwa kikorea akishindwa kujali uwepo wa Roma mita kadhaa.

Park Johyun alimwangalia Yoon He na kisha akapumua kama mtu ambaye hakupenda kuonana na mwanamke huyo.

“YoonHe unafanya nini hapa? , si nilisha kuonya usinifatilie fatilie”Aliongea kwa Kikorea akiwa siriasi.

Kutokana na jibu alilotoa Jonghyun , lakini pia muonekano wake, Roma aliamini wawili hao kuna kitu ambacho sio cha kawaida kinaendelea baina yao na ilimfanya kutoingia ndani kwanza ili kuendelea kujua ni nini kinaendelea. Na haraka haraka alihisi huenda ni maswala ya kimapenzi , kwani ni jambo la kawaida sana kwa mtu tajiri kama Park Jonghyun kutembea na mwanamke Star kama Yoon He.

“Yoon He naomba usiendelee kunifuatilia , nishakuambia mara kibao kwamba sina hisia na wewe”Aliongea na kisha aliingia kwenye gari pasipo ya kumjali lakini kabla hajafunga vioo Yoonhe aliinama kumwangalia kwa kioo cha gari.

“Unadanganya , unadangaya najua unanipenda ila unaogopa kwasababu tukiwa wapenzi watu wataanza kutuzungumzia , najua unanipenda sana Jonghyun”

“Unafikiri naogop watu kunizungumzia , kama nilikuwa nikiogopa nisingeanzisha mahusiano na wewe tokea mwanzo, ni kweli wewe ni mwanamke mrembo , lakini sikupendi kutokana na maringo yako na roho yako isiokuwa na utu, uvumulivu wangu una kikomo hivvyo nakuonya mara ya mwisho usinifuatilie vuatilie”

“Acha kujishaua Jonghyun najua umekuja Tanzania kwa ajili yangu pekee,, kwanini usiwe muwazi”Aliongea lakini mara baada ya kumaliza sentensi yake alijikuta ni kama kuna kitu kimemjia akilini na alinyanyua uso wake na kumwangalia Roma aliekuwa mita kadhaa na Roma mara baada ya mwanamke huyo kumwangalia alimpungia mkono na kutabasamu.

“Kwahio hiki ndio kilichokuleta hapa … Hahaha masikini Jonghyun kumbe…”Alijikuta akishindwa kuendelea kuongea kutokana na kuzidiwa na kicheko alikuwa kama chizi .

“Jonghyun naamini pua yako inaweza kunusa mbali sana , lakini nikushauri usiwe ni mwenye furaha kwa sasa mimi sio mjinga na wengine pia kwenye familia yetu sio wajinga, Park Jonghyun itafika muda ambao utataka unipigie magoti .. na hio siku ikifika nitahakikisha unalamba miguu yangu “Aliongea kwa Lugha ya Kikorea ambayo ilisikika vyema masikioni mwa Roma.

“Wewe ni mwanamke mjinga sana sijawahi kuona”Aliongea na kisha alimwangalia Roma aliekuwa amesimama mita kadhaa kutoka kwao.

“Mr Roma please disregard this crazy woman , I sincerely hope to gain your assistance , which I’ll surely reward greatly”

“You are welcome”Aliongea Roma huku akimpungia mkono na Park Jonghyun alipandisha kioo na palepale magari yaliondoshwa akiachwa Yoon He akiwa amesimama.

Yoonhe baada ya kuachwa alimgeukia Roma na kumwangalia kwa macho yaliojaa dharau na kisha aliingia kwenye gari yake na kuondoka eneo hilo.

Roma alivyogeuka aliweza kumshuhudia Edna akiwa amesimama mlangoni na alijikuta akitabasamu na kumsogelea.

“Babe wife umekoswa na tamthiliya ya kibabe , nyie si mnapenda kuangalia filamu za kikorea , basi kilichokuwa kikiendelea hapo nje ni uhalisia kabisa na mnachozoea kuangalia”

“Wamesemaje?”

“Mambo ya mapenzi ya watu walioachana kati ya Yoon He na Park Jonghyun , inaonekana mapenzi yao yamegeuka na kuwa chuki”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuwa na wasiwasi

‘Mh! , Naamini pia kwa huyu Park Jonghyun nia yake ya kumtaka Yezi kurudi Korea ni zaidi ya tunavyofahamu , YoonHe najua pia upande wa familia yake ina uwezo mkubwa kiuchumi na bado sijajua kwa undani, naamini uhusiano wao una mambo mengi makubwa Zaidi , kwasasa siwezi kuongea chochote , Yezi hisia zake sasa hivi hazipo sawa na siwezi kumwambia chochote”

“Ni kweli unachoongea mke wangu , hata mimi siwezi kuchukulia swala hili kirahisi hivyo”

“Hata wewe umehisi kuna kitu hakipo sawa?”Aliongea Edna akionekana kuwa mtu ambaye anahitaji uthibitisho wa maneno yake.

“Ndio sikutaka kuongea chochote maana nilihitaji tu waondoke hapa , lakini kwasababu babe wangu unataka niongee basi nitakuambia ninachohisi..”

“Kwanza nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kama kampuni kubwa kama ya StarMoon inayojiendesha kwa mabilioni ya hela kurithishwa kwa mtoto aliepotea kwa miaka mingi ambaye Maisha yake yote ni ya hapa Tanzania , ambaye hata tamaduni za Kikotea hazifahamu, ijapokuwa Park Jonhyun maneno yake yamejaa urembo wa kutaka kumrudisha Yezi Korea , lakini alichoongea ni upumbavu kabisa ambao hauaminiki, lakini hata hivyo licha ya kwamba Yezi hataki kurudi Korea haimaanishi kwamba baadae hatorudi , siku zote damu ni nzito kuliko maji na Yezi lazima atarudi kwenye familia yake , lakini kuhusu kurithi kampuni , hilo siamini kama litakuja kutokea, naamini kuna mpango unaandaliwa Zidi ya Yezi baada ya babu yake kuweka wazi nia yake thabiti ya kutaka kumrithisha na hili ndio linalomuweka kwenye hatar”

“Sasa ni kipi ambacho wanataka kumfanya Yei , Maisha yake ya makuzi yenyewe yalikuwa na shida lakini bado matatizo yanaonekana kutaka kumuibukia mbele”Aliongea Edna kwa kutia huruma.

“Hata mimi kwa sasa siwezi kujua mpango wao , lakini inaonekana Yezi ni muhimu Zaidi kwa Park Jonghyun , umesema kwamba yeye ni Mkurugenzi wa Starmoon basi naamini anajua kila kitu kinachoendelea ndani ya familia na kwenye kampuni , lakini pia anaonekana kuwa muigizaji mzuri , lakini hata hivyo jambo moja ambalo ninashauku nalo ni kutaka kujua uhusiano uliokuwepo kati ya Yoon He na yeye , kwa muonekano wake siamini kama angeweza kujihusiha kimapenzi na mwanamke kama Yoon He tokea mwanzo kuna Zaidi ya mahusiano ya kimapenzi”Aliongea Roma

“Muda ule niliona ni vyema kama Yezi angerudi kwa familia yake , lakini sikutaka aondoke na Park Jonghyun , nilitaka wewe ndio umpeleke , lakini kwa namna ulivyozungumzia hili swala naona ni vyema Yezi akabakia tu Tanzania na wasimsumbue tena , lakini nimeshangazwa sana na Yezi kuwa na damu ya familia kubwa kama Ya Park”Aliongea Edna.

“Babe usifikirie sana kuhusu haya , unaonaje ukaenda kuandaa msosi mumeo nina njaa, babe siku hizi unajua kupika tofauti na nilivyokuoa”Aliongea Roma

“Hivi kwanini unapenda sana kula , si ufikiri namna ya kumsaidia Yezi muda huu , mtoto yupo juu analia mwenyewe lakini wewe unawaza kula tu”Aliongea Edna lakini Roma alimpita akijifanyisha hajamsikia na kumfanya Edna kukasirika na kumfuata kwa nyuma.

Sasa hapo unachotakiwa kuelewa kwanza kabisa YoonHe mtu ambaye alizungumza nae wiki kadhaa zilizopita kwa njia ya simu na kumuita baba sio mtu kutoka familia ya Park kwani kwanza kabisa jina lake halikuwa na uhusiano wowote na wa Park Family.

Upande wa Roma alishahisi tokea mwanzo kabisa Yezi familia yake sio ya kawaida kutokana na kidani alichokuwa nacho ambacho kilikuwa kikimtambulisha wazazi wake tokea siku ile anakabidhiwa hicho kidani na Yezi ndio maana siku ile alishangaa sana na kujiuliza ilikuwaje mtoto kama huyo kua na aina hio ya kidani halafu akawa na Maisha ya tabu namna ile.

Unafikiri ni mpango gani unaendelea , je Yezi atarudi Korea?”





SEHEMU YA 359

Zikiwa zimebaki siku kadhaa kufikia tarehe ya Vexto kuweza kuanza usambazaji wa malighafi mpya kupitia mkataba waliosaini na kampuni ya Yamakuza wakishirikiana na kampuni ya Maple Group.

Ikiwa ni siku ya ijumaa , Roma akiwa nyumbani kwa Nasra akimbembeleza mama yake na Nasra kumkubalia ili kuendelea na mtoto wake, Nasra aliekaa pembeni aliweza kupokea simu kutoka kwa mafanyakazi aliekuwa akikamu nafasi yake ya uhasibu ndani ya kampuni ya Vexto.

“Zaina kuna nini?”Aliongea Nasra kwa wasiwasi kwani hakuwa akitegemea simu ya Zaina msaidizi wake kumpigia wakati kama huo wa jioni.

“Boss angalia hisa za kampuni yetu zinavyoporomoka kwa kasi kutokana na taarifa inayosambaa mtandaoni”Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Nasra kukata simu haraka haraka na kuingia upande wa mtandaoni na kuangalia nini kinachoendelea na kumfanya hata Roma aliekuwa akiongea na mama yake kushangazwa kidogo na mabadiliko ya ghafla ya Nasra.

“Nasra kuna nini..?”Aliuliza Roma na Nasra hakujibu Zaidi ya kuangalia simu yake , lakini muda huo huo na simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mpigaji ni Daudi msaidizi wake.

“Director umeweza kuona kinachoendelea mtandaoni?”Aliuliza Daudi.

“Sijaweza kuona , ni nini kinaendelea?”

“Kuna siri za kampuni ambazo zimevuja na zinasambaa mtandaoni , mikataba yote ya kampuni iliosainiwa na ile ambayo inapangwa kusainiwa na kampuni imewekwa mtandaoni na mtu asiefahamika na kufanya hisa za kampuni kushuka thamani kwa kiwango kikubwa ndani ya lisaa limoja”Aliongea Daudi na kumfanya Roma mpaka hapo kuelewa ni kwanini Nasra alibadlika ghafla , mpaka hapo aliamini mke wake alikuwa kwenye matatizo.

“Daudi asante kwa taarifa ngoja nifautalie hili”Aliongea Roma na kisha alikata simu na palepale alitafuta namba ya simu ya mke wake Edna huku akinyanyuka kwenye sofa , lakini simu ilionekana kuita tu bila kupokelewa , ilibidi kumtafuta mama yake nyumbani na kuulizia kama Edna kasharudi , lakini aliambiwa bado alikuwa kazini.

Roma na Nasra wote wlaijikuta wakiwa kwenye wasiwasi na ilibidi watoke kwa pamoja na kuelekea posta makao makuu ya kampuni ya Vexto .

Dakika chache tu Roma na Nasra waliweza kufika na kutokana muda huo ilikuwa ni wa saa kumi na wafanyakazi wengi washatoka kazini , kampuni ilionekana kutulia , lakini Roma aliweza kuona gari ya mke wake ikiwa imeegeshwa na alijiambia bado atakuwa kazini.

Roma baada ya kuingia ofisini kwa mke wake , Edna alionekana akiwa ameketi kwenye kiti chake cha mzunguko, na kwa kumuangalia tu aliamini Edna hakuwa sawa kimawazo , kwani macho yalikuwa mekundu.

“Edna nini kimetokea , imekuwaje siri za kampuni zikasambaa mtandaoni?”Aliuliza Nasra kwa wasiwasi huku akihema na Edna ilibidi awaangalie watu waliokuwa mbele yake na alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja.

“Nashindwa kuelewa nini kimetokea, lakini kwa namna moja ama nyingine naamini kuna mtu yupo nyuma juu ya hili swala na amechagua siku hii ya ijumaa wafanyakazi wakiwa wanatoka kazini ili kuweza kufanikiwa katika malengo yake”Aliongea Edna na kumfanya Roma kumuonea huruma Edna kwani sauti yake ilionekana kuwa ya kinyonge mno.

“Nasra jaribu kuangalia kama kuna wafanyakazi wa upande wa fedha waliobakia kazini ambao wataweza kutusaidia angalau kudili na hii hali”Aliongea Edna na Nasra alitingisha kichwa na akatoka nje haraka lakini muda huo mlango wa ofisi ya Edna uliweza kufunguliwa, na alionekana mwanadada Benadetha akiingia hapo ndani mkuku mkuku na alionekana kuwa na wasiwasi kweli na ile anaingia ndani tu aliangaliwa na Edna kwa macho yasio kawaida na kujikuta akizidi kutetemeka.

Taarifa iliokuwa ikisambaa mtandaoni ilikuwa ikihusina na mafaili ya siri sana ambayo alikabidhiwa Benadetha siku kadhaa zilizopita na Edna akayatunze kwenye ofisi yake , kwahio ni Dhahiri moja kwa moja mtu ambaye angeshukiwa kwa kuvuja kwa taarifa hizo ni Benadetha pekee.

“Boss sio mim niliovujisha, naapa kwa mungu wangu ninaemsalia sihusiki katika hili”Aliongea Benadetha na alivvyokuwa na wasiwasi , ilimfanya hata Roma kuona huruma kwani hakuwahi kumuona Benadetha kuwa kwenye hali kama hio.

“Nini kinaendelea , mbona sielewei , Edna niambie ni nini kinaendelea , kwanini Benadedhta anasema sio yeye?”Aliongea Roma akitaka maelezo na Edna alielezea kwa ufupi kwamba taarifa inayosambaa mtandaoni ilikuwa kwenye faili la siri la kampuni ambalo lilikuwa likimilikiwa na mkuu wa idara ya Masoko pamoja na uhusiano wa jamii ambaye ni Banadetha , Roma baada ya kusikia taarifa hio alijikuta akishangazwa sana.

“Wife naamini sio Benadetha, ijapokuwa simafahamu vizuri Benadetha lakini kwa machache ninayomfahamu nayo hawezi kuvujisha siri za kampuni mitandaoni”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumkata jicho la hasira.

“Boss ni kweli taarifa zinazosambaa zilikuwa chini yangu , lakini sihusiki kabisa , siwezi kufanya jambo kama hili”

“Benadetha usilie , kaa kwanza kwenye sofa , mimi pia nakuamini huwezi kuvujisha siri za kampuni kwenye mitandao”Aliongea Roma huku akimsogelea Benadetha na kisha akamkarisha chini kkwenye sofa na kisha akamgeukia Edna.

“Edna naamini katika hili swala hata wewe unajua ni dhaihiri kabisa mtu ambaye anahusika ni washindani wako wa kibiashara , siamini kama Benadetha anaweza kuhusika na swala hili”Aliongea Roma.

“Roma huu sio muda wa wa kumtetea Benadetha , kwani mafaili yote yalikuwa chini yake na nilimkabidhi mimi mwenyewe na nilimpa maagizo ya kuyatunza vizuri, awe amehusika au hajahusika ni mtuhumiwa namba moja na haupo kwenye nafasi ya kumtetea”Aliongea Edna akiwa katika ubora wake wa ukauzu na maneno yake yalivyokuwa makali ilimfanya Benadetha kuanza kulia Zaidi, kwa mara ya kwanza hakuamini jambo hilo linaweza kutokea ndani ya kampuni na mshukiwa wa kwanza akawa yeye.

Muda huo huo mlango wa ofisi ya Edna ulifunguliwa na Monica na alimtaarifu kwamba watu kutoka polisi wamefika na Edna aliwaambia waingie na muda huo huo waliingia wwanaume wawili na mwanamke mmoja waliovalia sare za kipolisi.

Kitendo cha kuingia kwa polisi hao kilimshutua sana Roma , kwani alijua mtu anaekuja kukamatwa ni Benadetha na ilikuwa kweli kwani baada tu ya kuingia ni kama walikuwa na taarifa zote.

“Miss Benadetha upo chini ya ulinzi kwa kosa la kuvujisha siri za kampuni , una haki ya kuomba mwanasheria, lakini kwa sasa unapaswa kuongozana na sisi mpaka kituo cha polisi kwa mahojiano”Aliongea yule polisi wa kike na alimsogelea Benadetha aliekuwa akitetemeaka na kisha akamfunga pingu mikononi.

“Edna hii sio sawa kabisa , huwezi ukamuacha Benadetha kupelekwa polisi , najua ni mshukiwa lakini swala hili linaweza kuisha hapa hapa sio lazima apelekwe kituoni”

“Mr Roma sina ujuzi wowote wa kuhoji watuhumiwa na Benadetha ataenda Polisi kwa ajili ya mahojiano na kama hajahusika basi ataachiwa, Afande mnaweza kuondoka nae tu”Aliongea Edna na kisha aligeuza kiti na kuangalia upande wa nje.

“Boss sihusiki katika hili , naomba usiwaruhusu wakinipeleka kituoni tafadhari”

“Benadetha sina cha kukusaidai kwa sasa ,, unajua ni hasara kiasi gani nimepoteza ndani ya lisaa limoja tu, naomba unisamehe ila siwezi kuzuia wasiondoke na wewe”Aliongea Edna na kwa jinsi sauti yake ialivyokua kavu ilimfanya Roma sasa kuona upande mwingine wa Edna ambao hakuwahi kuuona na alijikuta akishindwa kujua cha kufanya.

Dakika chache tu Benadetha aliekuwa akilia alitolewa na kuchukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha magogoni kwa ajili ya mahojiano.

Roma alijitahidi kumsihi Edna asiruhusu Benadetha kulala kituoni , lakini Edna alikuwa ni kama gogo, hakusikia la kuambiwa kabisa na kadri ambavyo Roma alikuwa akimbembeleza ndio ambavyo alikuwa akipandwa na hasira Zaidi, kilichofanya kukasirika Zaidi ni kwamba badala ya Roma kukaa upande wake yeye kama mume , alikuwa upande wa mhalifu Benadetha na hicho kilimuuzi sana , ukichanganya na wivu alimkaushia kabisa Roma.

“Kama kilichokuleta hapa ni kumsaidia Benadetha basi nikuambie sina cha kufanya na naomba uondoke nahitaji kuwa mwenyewe , kama unamjali sana na unaamini hajahusika tafuta muhusika ukamtoe kituoni”Aliongea Edna kwa sauti kavu na Roma alijikuta akipandwa na hasira lakini hakutaka kuzionyesha wazi zaidi ya kutoka ndani ya ofisi hio na ile anafika nje ya mlango aliweza kukutana na CEO msaidizi Ernest Komwe ambaye na yeye alioenekana kufika kwenye kampuni mara baada ya kusikia taarifa iliokuwa ikiendelea na Roma hakutaka kumjali kwani alimpita bila hara ya salamu.

Roma wakati akiwa kwenye gari alijikuta akiwa ni mwenye mawazo sana yaliochangayika na hasira , alimuona Edna kama mwanamke mkatili sana hasa ukizingatia namna ambavyo Benadetha alikuwa akijituma likija swala la kazi , aliona kitendo cha Benadetha kuchukuliwa na polisi kama mhalifu na kupelekwa kituoni haikuwa cha kiuungwana kabisa.

*********

Upande mwingine ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu julias Kambarage Nyerere , alionekana mrembo Queen alievaa akapendeza akiwa amesimama katika eneo la kupokelea wageni akiwa ameambatana na dada yake Matilda ambao wote walikuwa wamevalia miwani za jua, walikuwa wamependeza sana ukijumlisha na uzuri wao ulifanya baadhi ya vidume waliokuwa maeneo hayo kumeza mate kwa uchu.

Queen na Matilda walionekana wapo mahali hapo kwa ajili ya kumpokea mtu ambaye anawasili kutoka nje ya nchi , kwani walikuwa ndani ya jengo la Terminal 3 ambalo linahudumia wasafari wanaofika kutoka mataifa ya nje.

Matilda muda wotea likuwa akiangalia simu yake huku akiwa anatabasamu , ukumbuke muda huu ilikuwa ni muda wa saa kumi muda sawa na kile kinachoendelea ndani ya kampuni ya Vexto na Matilda alikuwa akiangalia namna hisa za kampuni ya Vexto zinavyoshuka kwa kasi na alijikuta akiwa ni mwenye furaha mno kutokana na matokeo hayo.

“Edna awamu hii ukitoka kwenye huu mtego utakua na heshima yangu”Aliwaza Matilda huku akiweka tabasamu la kifedhuli kwenye uso wake akiendelea kuangalia abiria wanaoingia na kutoka ndani ya jengo hilo.

“Dada nina hamu kweli ya kumuona baba?”

“Kweli eh! Mwenzio nikajua humpendi na unakuwa na amani akiiishi nje ya nchi kuliko akirudi”Aliongea Matilda na kumfanya Queen amwangalie dada yake kwa macho yasiokuwa yakawaida.

“Nani kasema simpendi , unapenda sana kunisukumizia kile unachojisikia kwenye moyo wako mimi Matilda , nampenda baba na nafurahi akiwa nyumbani”Aliongea huku akijinunisha na kumfanya Matilda kutabasamu.

“Nilikuwa nakutania tu , kinachokufanya kujaa povu ni nini ,niliona utakosa uhuru wa kula bata na mchina wako”Aliongea Matilda na kumfanya Queen kumwangali dada yake kwa mshangao.

“Umejuaje natoka kimapenzi na mchina?, nakumbuka sijawahi kukuelezea chochote kuhusu mtu ninaetoka nae”Aliongea Queen na kumfanya Matilda kucheka kidogo kicheko cha kebehi.

“Nilikiuona hoteli ya Serena , wiki kadhaa zilizopita ukiwa na mchina wako mnakula ‘Goodtime’, sikutaka kukushitua tu kwasababu nilikuwa na mambo yangu na mimi”Aliongea na kumfanya Queen kupooza kidogo lakini tabasamu likaibuka upya.

“Kama ushajua sitaki umuite Mchina , jina lake ni Profesa Yan Buwen , labda hata haujawahi kumsikia kwasababu haupo kwenye fani ya Sayansi , ukigoogle tu utaona jina lake , ni mwanasayansi maarufu”Aliongea Queen kwa kujigamba na kumfanya Matilda kuvuta mdomo akionekana kutokubaliana na mdogo wake.

“Huamini , ngoja nikuonyeshe “Aliongea na kisha alianza kutafuta kwenye mtandao jina la Yan Buwen na ndani ya dakika moja tu alipata na kumuonyesha Matilda na kumfanya ashangae.

“Wewe muongo Queen, mwanasayansi mkubwa kama huyu afanye nini hapa Tanzania halafu awe na mpenzi kama wewe”

“Usichoamini nini sasa , subiri siku nitakayo mtambulisha kwako ndio utajua ni ukweli au uongo”Aliongea Queen huku akimpokonya Matilda simu yake.

“Queen awe Yan Buwen au asiwe Yan Buwe hainihusu , lakini kwa jinsi nilivyowaona pamoja na yule mchina hakupendi na anakuchezea tu, najua umempenda kwasababu amekutoa bikra na hilo ni kosa litakalo kugharimu mdogo wangu”Aliongea Matilda na Queen alijikuta akimkata dada yake jicho lisilokua la kawaida.

“Ananipenda au hanipendi , hayakuhusu Matilda , huyo mwanaume anaekupenda wewe kwanza yuko wapi au kazi kujaji mahusiano yangu, unaona wivu nikidate na mwanasayansi mkubwa”

“Haha.. Masikini Queen , ndio alivyokudanganya kwa kujifananisha na mwanasayansi mkubwa.. haya bwana sitii neno”Aliongea Matilda na muda ule ule abiria mbalimbali walianza kutoka wakiwa wanaburuza mabegi yao na ndani ya dakika kama mbili tu hivi Queen ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Mzee Alex akitoka akiwa ametangulizana na kijana mmoja mtanashati sana alievalia miwani ya jua , mwenye mwili uliojengeka kimazoezi.

Mwanaume yule mara baada ya kumuona Queen alijikuta akisimama akiwa kama anashangaa.

“Hahaha..Queen mpenzi wako wa utotoni huyo”Aliongea Matild huku akisogea upande ambao anakuja baba yake ,Mzee Alex kwa ajili ya kumpokea , huku upande wa Queen akionekana furaha yake yote kuyeyuka ghafla.
 
SEHEMU YA 360.

Mzee Alex awamu hii afya yake ilionekana kuboresheka kwa kiasi kikubwa , kwani hata tembea yake ilikuwa imebadilika sana na hakuwa akitumia tena mkongojo wa kutembelea kama alivyoondoka hapa Tanzania kwa mara ya mwisho baada ya kukorofishana na Roma.

Mzee huyo alitabasamu sana kuwaona Watoto wake wakiwa wamependeza wakiwa na afya bora.

“Dadi tulikumisi sana , jamani umezidi kupendeza”Aliongea Matilda huku akipenda kumbatio na baba yake.

“Nyie pia mmezidi kupendeza”Aliongea huku akikumbatiana na Queen pia

“Queen umenenepa sana mwanangu , ni tofauti na nilivyoondoka na unaonekana kuwa mwenye fuarah pia”Aliongea Mzee Alex na kumfanya Quuen kutabasamu , huku macho yake akiyageuzia kwa mwanaume aliekuwa ameambatana na baba yake.

“Omari nadhani umeona namna mchumba wako alivyopendeza , Queen msalimie Omary , mbona unajifanyisha kama hujamuona”Aliongea Mzee Alex na kumfanya Matilda aliekuwa amesimama kumwangalia Queen.

“Queen umezidi kuwa mrembo , ni tofauti na mara ya mwisho tulivyo onana”Aliongea Omari huku akitoa miwani yake.

“Mh! hata wewe umezidi kuwa mbaba sasa na bitozi, watakomaje”Aliongea Queen kinafiki huku akikwepesha macho yake kumwangalia Omari huku wote kwa pamoja wakianza kutembea kutoka eneo hilo.

“Hawawezi kukoma au hujamsikia baba yako , nimerudi rasmi Tanzania nikiwa na wazo moja tu , ambalo ni wewe”Aliongea Omari pasipo ya kuwa na wasiwasi kwamba Queen alikuwa mbele ya baba yake , alionekana kijana ambaye alikuwa akijiamni mno na maneno yake yalimfurahisha sana Mzee Alex.

“Omari huna haja ya kuwa nawasiwasi kabisa kuhusu Queen , huyo ni wako tu na kwasababu usharudi Tanzania , kila kitu kitaenda sawa , twendeni kwanza nyumbani , Matilda ninataka unielezee Zaidi kinachoendelea kwenye kampuni”Aliongea Mzee Alex huku wote wakitoka.

“Dady kuna mambo mengi ya kuelezea na hima umerudi , basi ni mengi ya kufurahisha yanaendelea kwa sasa”Aliongea Matilda na kumfanya mzee Alex kumwangailia binti yake na kisha akatabasamu.

“Abubakari simuoni hapa , inaamna hafahamu kurudi kwangu Tanzania?”

“Anajua sana , huenda hakuona umuhimu wa kuja kukupokea”Aliongea Queen , lakini baada tu ya kutoka nje ya jengo la wanaowasili hatimaee waliweza kumuona Abubakari akiwa amesimama nje kabisa ya eneo hilo na alivyowaona aliwasogelea huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu.

“Dady Welcome Back”

“Thank you Son”Aliongea Mzee Alex huku akimshika Abubakari hamadi begani na kisha akamuoneysha gari.

“Nitapanda gari moja na Matilda nina mengi ya kuongea nae, utamchukua Omari na kumsindikiza nyumbani kwao”Aliongea Mzee Alex na Abubakari aling’ata meno na kikubali kwa kichwa.

Dakika chache tu Omari na Abubakari walikuwa kwenye gari wakiondoka eneo hilo la uwanja wa ndege.

“Unashine sana Mzee siku hizi na mwili umejengeka sana kimazoezi huo”Aliongea Abubakari na kumfanya Omari kutabasamu kidogo.

“Sio kweli haya ni mavazi ninayo yaona ya kawaida tu kwangu , labda kutokana na mabadiliko ya mwili wangu ndio maana”.

“Hahaha, ni kweli kabisa umebadilika kabisa , ujeda umekaa mahali pake”Aliongea na Omari alittabasamu.

“Vipi kuhusu mdogo wako Queen?”

“Queen ana nini?”

“Come on , unajua ninachozungumzia Abuu”

“Haha,, nilikuwa nakutega , lakini sikudhania kama utamkumbuka Queen baada ya miaka mingi ulivyoondoka hapa nchini Kwenda Urusi”

“Huwezi amini , tokea nilipokuwa mafunzoni kipindi chote mwanamke aliekuwa kwenye akili yangu ni Queen pekee, na nimerudi Tanzania kwa wazo moja tu la kumuoa mdogo wako na hakuna cha kunizuia kutotimiza ndoto yangu”Aliongea Omari na kumfanyaAbubakari kucheka kwa namna ambavyo Omari alikuwa serios na maneno yake , aliamini kweli bwana huyo ni mwanajeshi , kwani alikuwa akiongea moja kwa moja , hata kwenye swala la hisia zake.

“Usicheke Abuu , usiniambie Queen tayari anamwanaume?”

“Hilo sidhani , licha ya kwamba simfatiliagi sana , ila naamini hakosi , si unajua Queen ni mwanamke mrembo , ambaye muda wote anajiachia , ni ngumu sana wanaume kumuacha hivi hivi , ila kwasababu umerudi mzee nadhani kila kitu kitaenda sawa , cheza nafasi yako kama mwanaume , tumia ujeda wako kumrudisha mtoto kwako na kumpokonya boya yoyote anaemmiliki, isitoshe kwenu mkwanja upo pia”

“Hahaha.. Asante kwa maneno yako ya kutia moyo”

“Haha usijali , muda wote nipo hapa kama unahitaji msaada, vipi lakini kuhusu jicho lako , sasa hivi linaona?”Aliuliza Abubakari huku akiweka umakini kwenye barababara.

“Wewe unaonaje , macho yangu yote yanaona kabisa na hayana matatizo yoyote”Aliongea na Abubakari hakutia neno.

“Kuna jamaa mmoja anaitwa Roma Ramoni , una ukaribu nae au mawasiliano yake?”Aliongea na kumfanya Abubakari kupunguza mwendo wa gari na kukunja sura.

“Unamfahamu vipi huyo choko?”

“Kwanini unamuita Choko, nijibu swali langu kama una mawasiliano nae?”Aliongea Omari huku akishindwa kufahamu kwanini mwenzake kabadilika mara tu ya kuuliza habari za Roma.

“Sina mawasiliano yoyote lakini kama unataka kumpata ni rahisi sana , kwani kamuoa mrembo Edna Adebayo”.

“Kuhusu hilo najua , lakini siwezi kumfuata Edna na kumuona namba ya Roma , niliona utakuwa njia ya rahisi Zaidi kama ungekuwa na mawasiliano naye , ila isiwe kesi bro”Aliongea na kisha kapiga kimya.

Upande mwingine mara baada ya Mzee Alex kufika nyumbani kwake alijikuta akianzisha mazungumzo na Matilda ili kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu maswala ya kikampuni na mengineyo na taarifa aliopewa mzee Alecx ilimfurahisha lakini pia kumtia wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Kwahio Matilda unamaanisha kwamba una ushiriikiano na mke wa aisi wa Rwanda?”

“Ndio baba , nilikutana na Madam Kizwe kipindi cha nyuma kidogo baada ya kutoka masomoni na kuanzia hapo alikuwa mtu wangu wa karibu na hata mpango wa kuingia kwenye kampuni ya JR na kua CEO ni mpango wake na ndio alienishawishi”Aliongea Matilda na kumfanya Mzee Alex kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Kwahio hiki kinachoendelea ndani ya kampuni ya Edna , pia anahusika na wewe pia unahusika?”Aliuliza na Matilda alitingisha kichwa.

“Matilda naomba unisikilize ,ijapokuwa sikupendezwa na namna Edna anavyofanya maamuzi kwa niaba ya kampuni yetu , haswa swala la benki lakini naomba usijihusishe sana na maswala ya mke wa raisi wa Rwanda , sitaki baya lolote likukute”

“Unamaanisha nini baba, Kizwe ana nia ya kumuondoa Edna kwenye kampuni , hilo lina ubaya gani kwetu?”

“Ushawahi kujiuliza kwanini anataka kumtoa kwenye kampuni , kwanini anafanya hayo yote kwa ajili ya mfanyabiashara kama Edna?”Aliuliza Mzee Alex na kumfanya Matilda kukosa jibu.

“Ndio maana nakuambia sitaki sana uhusika katika visasi vyake, kwa taarifa yako tu Edna ni mtoto wa Raisi Jeremy , na Kizwe anamchukia mama yake na Edna kwa kutembea na mume wake mpaka kumzaa Edna”

“Baba unasema kweli!!!”Aliuliza Matilda kwa mshangao.

“Ndio maana nakuambia usijihusishe moja kwa moja na Kizwe kwani haitokuwa na faida kwako kabisa Zaidi ya kutumika , nimekuwa nje ya nchi kwa muda mchache sana , lakini nimejifunza mengi sana ambayo sikuwa nikiyafahamu na nakiri ndio mambo ambayo yamenifanya kutofanya vizuri kwa muda wote mpaka kampuni ikaingia mikononi mwa Edna , nimerudi sasa hivi kufanya mambo kwa usahihi na wewe utanisaidia katika hilo”Aliongea Mzee Alex na kumfanya Matilda kumuelewa baba yake nusu nusu.

“Lakini baba kwa hili linaloendelea kwasasa ninahusika na siwezi kujitoa mapema hivi na nina uhakika hakuna namna Edna ambayo anaweza kushinda mtego mkubwa uliowekwa kwa ajjili yake awamu hii”

“Unachoongea kinaweza kuwa sahihi ama kisiwe sahihi , lakini jambo moja ambalo nimeamini , siku zote ndio maana tulikuwa tukishindwa kuiangisha Vexto katika biashara ni kutaka kumtoa Edna katika ulingo wa biashara Zaidi ya kuangalia ni namna gani tunaweza kumshinda akiwa bado ulingoni , wivu umetufanya mara zote kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maslahi ya kampuni yetu na ndio maana tumerudi nyumana Edna ametumia wivu wetu kama siraha ya kutuzidi akili”

“Baba kweli umebadilika sana , inaonekana ulipokuwa nje ya nchi uliishindia kufanya tahajudi , sio mabadiliko ya mwili tu uliokuwa nayo bali pia busara na utulivu vimeongezeka”Aliongea Matilda na kumfanya Mzee Alex kucheka kidogo.

“Nimekutana na watu bora Zaidi yangu na nikaishi miongoni mwao na nilichojifunza ni kikubwa Zaidi na kama ningefanikiwa kujua mapema JR ingekuwa kampuni kubwa sana kuliko ilivyo sasa”Aliongea,

“Baba tutaongea Zaidi siku zijazo , kuna sehemu napaswa kuwepo”

“Hakuna shida mwanangu , ila nakusihi sana kuwa makini, nina wasiwasi na mlichokianzisha kufeli”

“Baba unamaanisha nini kuhusu hilo , hili sio swala la kumtoa Edna kwenye kampun bali ni swala la Edna kukosa uhalali kwa kuingoza kampuni ya Vexto na ikitokea akatolewa wa kulaumiwa sio sisi bali ni familia yake hususani bibi yake ambaye siku zote alikuwa akiwadanganya yeye na mama yake na kushindwa kuwaweka wazi juu ya kilichotokea mwanzoni”Aliongea Matilda na Mzee Alex alifikiria kidogo.

“Matilda sitaki sana kuzungumzia maswala ya biashara kwasasa , ni muda wangu wa kupumzika chochote kitakachotokea ilimradi kina kufanya kuwa salama na hakiathiri familia basi endelea nacho”

“Usiwe na wasiwasi baba yangu , pumzika na pole kwa safari”Aliongea Matilda na kisha akatoka.

Saa moja kamili Roma alikuwa nyumbani kwake akiwa mezani akijipatia chakula cha usiku bila ya kuwa na wasiwasi , katika meza walikuwepo wanafamilia wote kasoro Edna ambaye alitoa taarifa kwamba atalala huko huko na pia Sophia ambaye tokea mashindano yaishe hakuweza kurudi nyumbani kutokana na kampuni kuwasafirisha Kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya utalii kama sehemu ya ahadi iliotolewa na kampuni.

Wanafamilai wote walioenekana kuwa na wasiwasi kweli na kile ambacho kinaendela kwenye kampuni , huku Bi Wema na Blandina wakionekana kuwa wenye wasiwasi Zaidi.

“Roma utamuachaje mkeo alale huko huko ofisini , kuna usalama kweli?”

“Mama , Edna ndio kaamua kulala ofisini na kwa tabia yake nadhani unaelewa hata nikimfosi kuja nyumbani hatokuja , ni bora kuacha afanye anachotaka kwa sasa”

“Lakini huu ndio wakati wa kuwa nae karibu , unajua anapitia wakati mgumu , kampuni ipo kwenye matatizo”

“Mama hata kama nikienda hakuna cha maana ambacho nitasaidia na isitoshe sidhani kama yupo peke yake , yupo Dorisi na Nasra ambao siku zote wanamsaidia kwenye mambo ya kampuni, michango wangu ni mdogo sana na Edna hata kama nitatoa ushauri hawezi kunisikiliza, cha kufanya ni mimi kula nishibe na kisha nikapige usingizi”Aliongea Roma.

“Lakini anko Roma kwanini wewe usichukue nafasi ya sister Edna na kuwa CEO , isitoshe nyie ni wanandoa na kusaidiana ni muhimu” Aliongea Yezi na kumfanya Roma kutaka kucheka.

“Siwezi kuwa CEO , ni kazi ambayo siiwezi nafikiri mnajua kabisa hata nikienda kazini nashindia kucheza gemu tu”

Ukweli Roma alikuwa akiongea kujifurahisha tu , lakini ndani ya moyo wake alikuwa na wasiwasi na Edna, lakinni pia wakati huo huo alikuwa na makasiriko baada ya Edna kutomsikiliza na kumfanya Benadetha kupelekwa polisi.

Lakini hata hivyo Roma hakuacha kucheza nafasi yake licha ya kwamba Edna alionyesha kutomsikiliza mbele yake na kuleta kiburi , wakati akiwa njiani kurudi nyumbani aliwapa kazi The Eagles kufanya uchunguzi kujua ni nani kahusika na kuvujishwa kwa siri za kampuni mitandaoni.

Sasa asichokijua Roma ni kwamba Edna alikuwa kwenye Zaidi ya mtego, na kuvujishwa kwa siri za kampuni mtandaaoni haukuwa mpango wenyewe bali kulikuwa na bomu kubwa Zaidi ambalo linaandaliwa , bomu ambalo linahusiana na siri ambayo Marium bibi yake hakuwaeleza Edna pamoja na Raheli inayohusiana na kampuni ya Vexto.

Roma wakati anajiandaa kulala aliweza kupokea simu ya namba mpya ya kitanzania.

“Mr Roma naitwa Samweli Nguluma ni baba wa Benadetha , nimesikia mtoto wangu kashikiliwa kituo cha polisi na nimeshindwa kufanya lolote kwa ajili yake ili apate dhaman , Mr Roma nadhani unashangazwa kwanini nimekupigia, Benadetha alishatueleza kuwa wewe ni mwanaume anaekupenda na anatamani kuolewa na wewe hivyo naamini swala la mkeo kumuacha alale kituo cha polisi linahusiana moja kwa moja mahusiano yenu”

“Mzee una..”

“Sijakuruhusu uongee Shwain…, ninachokuambia ni mtoto wangu kutoka kituo cha polisi kabla sijatia mguu ndani ya jiji la Dar , hatutoelewana kabisa , Narudia kamtoe mtoto wangu kituo cha polisi ,nafikiriTanzania hainifahamu vizuri mimi nani haswa na mshaanza kunishika sharubu”Simu palepale ilikatwa na Roma alijikuta akiwa kwenye mshangao , kwenye Maisha yake hajawahi kupigwa mkwala wa aina hio , lakini kubwa Zaidi hakuwa akijihusisha kimapenzi na Benadetha , ilikuwaje Benadetha akwaiambia familia yake kwamba yeye ni mtu wake.

******



Upande mwingine muda wa saa mbili kamili , katika chumba pendwa cha Yan Buwen katika hoteli ya Serena hoteli , alionekana mrembo Queen akiingia ndani ya chumba hicho akiwa amevaa kivazi matata sana ambacho huko alikopita kiliacha lawama kwa wanaume wengi waliomuona.

Queen kwa staili ambayo alivaa ni hakika kwamba alikuwa akienda kumpagawisha mwanaume wake ambaye ni Yan Buwen.

Yan Buwen mara baada ya kumfungulia mlango Queen alijkuta akitabasamu sana na kupandwa na midadi ya kufanya mapenzi kutokana na mavazi aliovaa mrembo wake Queen.

“Babe umependeza , unaonekana kama malaika”Aliongea Yan Buwen kwa kingereza na kumfanya Queen kutabasamu na kumsogelea karibu na wakakumbatiana huku wakipeana busu nyevu.

“Babe nina surprise kwa ajili yako nataka kabla hatujaanza kufanya chochote nikuonyeshe”Aliongea Queen kwa hamasa kubwa na kumfanya Yan Buwen aliekuwa kifua wazi kumwangalia Queen kwa shauku.

“Unanifanya najawa na shauku , unaonaje ukionyesha sasa hivi?”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Queen kutabasamu.

“Fumba macho kwanza”Aliongea na Yan Buwen alitabasamu na kisha akafumba macho na Queen baada ya kuona Yan Buwen kafumba macho alifungua mkoba wake na kutoa kijidude na kisha akamwambia Yan Buwen kufumbua macho.

“Babe I am Pregnant…”Aliongea Queen akimwambia Yan Buwen kwamba ni mjamzito na kilichokuwa mbele yake ni kipimo cha mimba cha kutumia mkojo(UPT).

Yan Buwen alijikuta akimwangalia usoni Queen na kisha akachukua kile kipimo na kukiangalia na kweli aliweza kuona kilikuwa kikionyesha mwanamke huyo ni mjamzito.

“Babe say something please..”

“Ongea chochote mpenzi”Aliongea Queen baada ya kuona Yan Buwen amekuwa kimya.



MWISHO WA SEASON 12

Haya sasa Queen ndio huyo analiwakilisha taifa kwa kubeba mimba ya limwana sayansi wa kimataifa Yan Buwen unafikiri ataikubali au atakuwa kama wanaume wa kiafrika wanaotelekeza wanawake wapatapo ujauzito

Edna nae mikononi mwa Kizwe , unafikiri ni siri gani ambayo Marium bibi yake Edna hakumueleza mama yake Edna , vipi kuhusu Yezi

Aluta continuara …..
 
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: DR SINGANOJR

SEASON 13.

UTANGULIZI

Summary ya tulipotoka mpaka tulipofikia

Katika simulizi hii kwanza kabisa tunaona maisha ya Edna na Roma yalivyoanza mpaka wakafikia hatua ya kufunga ndoa ya mkataba , Maisha ya Roma na Edna mara baada ya kufunga ndoa ya mkataba kwa miezi yote tisa , ni mengi sana ambayo yamejifunua katika miezi, Tumeweza kumfahamu Roma kwa majina ya Hades au Mfalme Pluto , cheo cha kiuungu ambacho ameweza kukipata kutoka kwa Hades wa Zamani , tumeweza kuona mpango LADO uliokuwa ukiratibiwa na Zeros Organisation ulivyomfanya Roma kuweza kuishi na saratani ya ubongo , Tumeweza kuona pia baadhi ya madhumuni ya kufika kwa Raisi Barack Mabo hapa Tanzania.

Lakini kubwa Zaidi tumefahamu uwepo wa miungu watu inayoishi hapa Duniani kwa sura za binadamu wa kawaida akiwemo Poseidoni ambaye anaishi kwa kufahamika kwa jina la Mr Kelphin , tumeweza kumuona Apollo ambaye anaishi kwa jina la Stern Cromwell , Tumeweza pia kumuona Artemis ambaye anaishi pia kwa jina la Alice Ceomwell , tukapata pia kumuona Ares ambaye anaishi kwa jina la Mendelev , tukamtambua pia The Doni kuwa ni Mmoja wa miungu ambaye anajulikana kwa jina la Athena.

Lakini kubwa Zaidi ni Maisha ya Roma na Edna… historia ya familia ya Edna inaonyesha kuwa na muunganiko mkubwa sana na kwa kile ambacho kinaendelea , kila kitu kilianzia miaka mingi nyuma kabla ya Roma kukutana na Edna , kwanzia kipindi cha utekelezaji wa mpango LADO ambao uliratibiwa na Zeros huku wafanikishaji wakuu akiwa ni Hades wa Zamani pamoja na Athena , Kukutana kwa Roma na Edna nchini Tanzania pia kunaonekana sio kwa bahati mbaya kwani ni mwendelezo wa yale yalitokea nyuma na yale yanayokuja kutokea mbele.

Roma ana washirika wake , lakini vilevile Athena na yeye anao washirika wake duniani kote na inaonekana Roma ana kazi kubwa Zaidi ya kufanya kwenye Maisha yajayo , moja ya kanuni ya Roma ni kuhakikisha watu wake wa karibu wanaishi wakiwa salama , hivyo lazima dunia iwe salama kwa ajili ya wapendwa wake kuwa salama , hivyo ni hakika kwa chochote ambacho atafanya Athena kikiwa na madhara kwa watu wake wa karibu aidha kwa njia ya moja ka moja au isio ya moja kwa moja ni dhahiri Roma atachukua hatua ya kudili na Athena , lakini swali linabakia je ataweza , kwani tunaona Athena ana uwezo mkubwa sana wa kutumia kanuni za Anga , lakini Roma tofauti na miungu wenzake yeye akachagua kutumia mbinu za kupambana kwa kumeng`enya nishati inayozalishwa kati ya mbingu na Ardhi, mbiuu ambayo inatumiwa Zaidi na viumbe visivyoonekana ambavyo binadamu huviita majina watakayo kutokana na tamaduni zao , kwa mfano baadhi ya vitabu wanatambua viumbe hivi visivyoonekana kama majini , lakini upande baadhi ya nchi za Asia kama vile China wanaita viumbe hivi kama walinzi wakuu yaani Hongmeng.

Moja ya kauli kuu ya kusisimua Zaidi ni kutoka kwa Christen msanii maarufu ambaye roho ya Aphrodite huishi ndani yake , kauli yenyewe ni pale Christen anapomtahadharisha Roma kuhakikisha kwamba asije karuhusu jiwe lingine la Kimungu linamfikia Athena , kauli ambayo kwa Roma anshindwa kuielewa kwani jiwe la kimungu ambalo alikuwa akilimiliki tayari lilikuwa kwenye mikono ya Athena.

Lakini sisi kama wasomaji pia tunaona kwamba kuna majiwe ya kimungu kumi na mbili kwa ujumla wao kupitia historia iliotolewa na Athena na katika majiwe hayo kumi na mbili ni kumi na moja pekee ambayo yamepatikana ambayo yote yapo kwenye mikono ya Athena na ni jiwe moja tu ambalo bado halijapatikana jiwe ambalo Athena anaamini limebeba roho ya Gaia, Roho ambayo kama Athena atafanikiwa kuifufua ataweza kuongoza miungu yote kumi na mbili pamoja na kuirudishia nguvu zao zilizowapotea kutokana na kufanya Transmigration , lakini pia Athena ataweza kufufua Roho za ndugu zake ambazo zimemezwa na binadamu na yote hayo anayafanya akiwa na lengo moja kichwani mwake , Lengo la kumtengenezea binadamu Mungu anaeonekana ambaye anauwezo wa kufanya miujiza yote , Mungu ambaye anaamini anaweza kukizi kila hitajio la binadamu na kufanya ulimwengu kuwa kama Utopia , huku akiwafanya biandamu kumsahau Mungu mkuu ambaye haonekani , Mungu ambaye kwa maelezo yake mwenyewe Athena anjiweka kwenye nafasi kama Adui yake namba moja.

Maswali ni haya , je Athena ndio Shetani , je mipango yake itafanikiwa, Athena anaonekana kujua kila kitu kinachoendelea katika Maisha ya Hades , lakini Roma hafahamu kila kinachoendelea kwenye Maisha ya Athena , Je Hades ataweza kumzuia Athena kama maelezo ya Hades wa Zamani yalivyo. Vipi kuhusu unabii aliokuwa akizungumzia Christen?

Karibuni kwenye ngwe nyingine ya msimu wa kumi na mbili wa simulizi hii inayoletwa kwenu na mwandishi SinganoJr.
Nawakumbusha tu kama unajali kazi hii hakikisha unanisapoti kadiri uwezavyo , kwa namna ya kunivumilia kwa siku ambazo sileti mwendelezo , kwani sio makusudio yangu kutoleta mwendelezo , lakini pia kuniunga mkono kwa kiasi cha pesa kisichopungua 2500 kama ada ya grupu kwa mwezi , kwa wale amba mpo eligible.







SEHEMU YA 361.

Haikueleweka mara moja ni namna gani Queen akakutana na Yan Buwen , bali mahusiano yao yalikuwa ya takribani miezi kadhaa tokea yaanze, Queen ni mtoto wa pili wa Mzee Alex mfanyabiashara mahili maarufu ndani ya Tanzania, licha ya Queen katika Maisha yake kuonekana kama mwanadada ambaye alikuwa ni wa kujiachia , lakini tunaweza kumuona Queen kwa namna nyingine kama mwanadada ambaye aliweza kushinda vishawishi vingi katika Maisha yake ya ukuaji kama msichana , Kwanza mrembo huyu licha ya kuwa katika mahusiano na wanaume kadhaa lakini jambo moja ni kwamba hakuwahi kulala na mwanaume yoyote yule mpaka anakuja kumfahamu Yan Buwen.

Licha ya dada yake Matilda kuwa na akili Zaidi kumzidi mdogo wake Queen lakini Queen ni msichana wa tofauti sana na Matilda , Queen ni msichana ambaye hana ndoto kubwa sana kwenye Maisha yake , msichana ambaye sio mtu wa kujali sana vitu ambavyo vinamzunguka, kama vile mali za familia na mengineyo yeye alichokuwa akijali ni kupendwa na kuishi vizuri tu basi.

Yan Buwen ukweli licha ya kwamba Queen alikuwa mpenzi wake , lakini hakuwahi kumchukulia Queen siriasi kabisa , alimuona kama mwanamke wa kujiburudisha tu kadiri atakavyokuwa anakaa hapa Tanzania kwa ajili ya kutimiza misheni zake , ukumbuke Yan Buwen alikuwa akitoka kimapenzi na mtoto wa raisi kutoka China lakini hakuwahi kuonyesha kabisa kuzingatia hisia zake, sasa kama Yan Buwen alishindwa kumkubali mtoto wa raisi anashindwaje kumkataa Queen licha ya kuwa na mimba yake.

Katika kichwa cha Yan Buwen mwanamke ambaye alitokea kumpenda na alijiapiza kuja kufanya kitu chochote kwa ajili yake ni The Doni au Athena , yote ambayo yamemfanya kuja hapo Tanzania ni kwa ajili ya mwanamke Athena pekee.

Yan Buwen mara baada ya kusoma majibu yale ya kipimo cha mimba na kuona ni kweli Queen alikuwa na ujauzito wake , alijikuta akikaa chini akiwa kama mtu ambaye hakufurahishwa na Habari hio na jambo hilo hata kwa Queen aliweza kuliona.

“Babe mbona haufurahii , ongea chochote mpenzi”Aliongea Queen akijaribu kuchuchumaa mbele ya Yan Buwen.

“Queen unaongea ujinga, nyie wanawake wa kitanzania mna matatizo gani?, nani alikwambia nahitaji mtoto?”Aliongea Yan Buwen huku akianza kubadilika taratibu taratibu na kumfanya Queen kuogopa kwani tokea amfahamu Yan Buwen alikuwa akimuona mtu mpole sana.

“Queen hio mimba ukaitoe , sihitaji kuwa na mtoto ambaye atakuwa na mchanganyiko na Ngozi nyeusi , labda nikueleze tu ukweli , wewe haukuwahi kuwa mwanamke ninaekutaka , nilikuwa nikikutumia kama kahaba na kwanzia leo thamani yako kwangu ishaisha , hio mimba siitaki na ukaitoe na usinitafute tena”Aliongea kwa Kingereza na kumfanya Queen akiwa kama mtu ambaye haamini kile anachosikia , hakuamini kama Yan Buwen anaweza kumbadilikia namna hio kisa mimba , alijikuta akishindwa kuzuia machozi yake, kwa mara ya kwanza alijihisi moyo wake ukiuma sana.

“Yan Buwen unaniumiza moyo wangu … kwanini unaongea maneno ya kikatili namna hii , kisa kukueleza mimi ni mjamzito?”

“Hupaswi kuendelea kuongea Queen na sitaki kukuona hapa ndani ya sekunde sitini zijazo , la sivyo nitakuua, nikihesabu mpaka tano uwe umeondoka”Aliongea Yan Buwen akiwa ameshikilia mvinyo na alisogea mpaka kwenye kijimeza cha kitanda na kuvuta droo na kisha akaibuka na bastora.

“Nikihesabu mpaka tano bado upo hapa ndani nakupaasua kichwa”Aliongea Yan Buwen na kisha kuitoa Bastora kwenye mfumo wa Safety na kumyooshea Queen.

Queen macho yalimtoka , hakuamini kama Yan Buwen anaweza Kwenda Zaidi mpaka kufikia hatua ya kumnyooshea bastora.

“Yan Buwen mpenzi wangu , najua umekasirika , nitaitoa hii mimba na tutaendelea na mapenzi yetu , naomba usikasirike, weka siraha chini tafadhali , nakupenda Yan Buwen”Aliogea Queen huku kamasi la kilio likimtoka , lakini kwa Yan Buwen alimuona Queen kama kituko.

“Queen nimekuambia ondoka moja … mbili…, tatuu ……, nikifikisha tano hujaondoka nitakupasua ubongo na hakuna mtu wa kunifunga hapa Tanzania”Aliongea .

“Nnee..”Ile anaongea tu Queen alijikuta akinyanyuka pasip ya kupenda.

“Nitaondoka Yan Buwen, kwasasa una hasira , ila nitarudi kwasababu nakupenda na mtoto aliekuwa tumboni kwangu naapia sitokuja kumtoa na utakuwa baba yake”Aliongea Queen kwa hasira na kisha alichukua mkoba wake na kutoka akimwacha Yan Buwen akitoa tabasamu la dharau.

“Hahaha.. wanawake wa Tanzania bwana , kidogo tu washamuamini mwanaume na wanataka kuzaa , Stupid … mimi Yan Buwen hakuna mwanamke ambaye anahadhi ya kuzaa na mimi tofauti na mrembo The Doni, nitahakikisha nakuwa na nguvu kumzidi Hades, hata kumzidi The Doni mwenyewe ilimradi tu aweze kunikubali kama mume wake na anizalie Watoto, nitahakikisha ndoto yangu inatimia”Aliongea huku macho yake yakianza kubadilika rangi na kuwa mekundu, alionekana kuwa na uchungu moyoni mwake.

Quuen chozi lilimtoka wakati akiwa kwenye Lift akielekea chini, hakuamini ndio hivyo mchina wake hakuwa akimtaka tena, lakini licha ya kwamba amekataliwa na Yan Buwen aliamini lazima mwanaume huyo atamkubali tu kwani tayari ana kiumbe chake kwenye tumbo lake.

“Nitamzalia mtoto , akishamuona mtoto alivyokuwa mzuri lazima atanikubali tu, huenda nimeharakisha kubeba ujauzito wake”Aliwaza Queen akijipa maneno ya Faraja , na maneno aliojiambia yalionekana kuwa na nguvu Zaidi , kwani tumaini jpya lilichipuka, tumaini la kuendelea kushikilia penzi lake juu ya Yan Buwen kwa kutumia kigezo cha mtoto aliekuwa tumboni kwake.

Sasa ile anatoka kabisa nje ya hoteli hii , akiwa eneo la maegesho ya magari alijikuta akishikwa bega na ile anageuka alikutanisha macho na mwanaume alievaa akapendeza.

“Omari unafanya nini hapa?”.

“Kuna mtu amenialika kwa ajili ya chakula cha ofa”Aliongea Omari huku akiweka tabasamu na kumfanya Queen kushangaa kidogo kuhusu chakula cha ofa.

“Mbona macho yako hivyo Queen , unaonekana ulikuwa ukilia , nini kimekupata , niambie nani kakuuzi nitaenda kumpasua sasa hivi?”Aliongea Omari na kumfanya Queen kupatwa na huzuni, lakini hakutaka kumjibu kwani alifungua gari yake na kuingia ndani na pasipo ya kumuaga Omari aliliwasha na kuondoka.

“Pumbavu , yoyote ambaye amemfanya mke wangu mtarajiwa kutoa machozi nitahakikisha namuua”Aliongea Omari huku akikunja ngumi.

********

Nyaraka za siri zilizovuja zilikuwa zikihusiana na mawala ya manuzi ambayo yanatarajiwa kufanyika ndani ya miezi sita ijayo , mipango ya tenda zote za kampuni , mipango ya mazungumzo ya kibiashara , wateja wakubwa wa kampuni , baadhi pia ya michoro mipya ya kampuni , lakini baadhi pia ya uzinduzi mpya wa malighafi za kampuni , vyote hivyo ndio vilikuwa vikisambaa mtandaoni.

Sasa unachotakiwa kuelewa katika biashara kuna baadhi ya taarifa zinazotakiwa kuwekwa hadharani na baadhi ya taarifa ambazo hazitakiwi kuwekwa hadharani , kama itatokea taarifa zozote ambazo ni siri ya kampuni zikawekwa hadharani moja kwa moja italeta athari kubwa kwa kampuni , kwasababu biashara ni mashindano na katika vita ili uweze kumshinda mwenzako kibiashra lazima uwe na siraha ambazo unaweka wazi na zile ambazo huweki wazi ili kufanya mashambulizi yasiotarajiwa , sasa ukiachia vitu vyote hadharani matokeo yake ni kwamba wapinzani wako watakuwa wanajua sasa namna ya kukuzidi na hili linakuwa pigo kubwa kwako kabisa.

Ndio maana hisa za kampuni ziliweza kushuka sana, kwa lisaa limoja tu ,Edna aliweza kushuka katika orodha ya matajiri duniani kwa nafasi tano nyuma , huku ikielezewa na mtandano wa Forbes pamoja na Wa Billioneaire index kwamba mpaka ifikapo saa sita usiku soko litakapofungwa Edna atapoteza Zaidi , lakini pia ikitarajiwa kampuni yake kushuka kimauzo kwa miezi minne mfululizo.

Kwahio kilichotokea ni pigo kubwa sana kwake na sio kwake tu kwa taifa zima kwa ujumla na hata kama aseme afanye mchakato wa kununua hisa za kampuni ambazo zinatupwa sokoni na wawekezaji , itakuwa haina maana kwani atakuwa anazidi kupata hasara na itapelekea kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara na kupelekea kuwafukuza kazi na hili litakuwa pigo kwa serikali , kwani kampuni ya Vexto ilikuwa imeajili Zaidi ya watanzania elfu tisini.

Kitengo cha Athena wenyewe licha ya kufanya kazi kwa bidii , walishindwa kujua ni kwa namna gani wanaweza kudili na hali inayoendelea katika kampuni..

Naam ilikuwa ni siku nyingine kabisa , siku ambayo Edna aliamkia kwenye kampuni na hakuweza kurudi kabisa nyumbani, asubuhi hio muda wa saa mbili ndani ya kampuni kulikuwa na kikao Kizito sana ambacho kilikuwa kikiendelea , kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na Edna kama kiongozi wa kampuni.

Wafanyakazi Zaidi ya ishirini walikuwa wamejipanga kwenye meza kulingana na vyeo vyao akiwemo Nasra , Dorisi na mwanasheria kutoka Nadia Law Firm ambaye alikuwa akimwakilisha Nadia kama mwanaeshria wa kampuni na wengineo akiwemo Ernest Komwe.

Kila mfanyakazi alikuwa akiongea lake , huku wakionyesha kukasirika Sana kwa kile ambacho kimetokea , wengi wao wakikasirika Zaidi kwani walionekana ratba zao za kula bata wikiendi zimeingia mdudu , hivyo kila aliekuwa na la kuongea aliongea na kufanya kikao hicho kuwa kama zogo , huku Edna akiangalia namna watu wanavyorushiana maneno, kuna wale ambao walikuwa upande wa Benadetha na kuna wale ambao hawakuwa upande wake na hiki ndio kilichofanya watu kugombana.

“Paah..!!” Edna alijikuta akipiga meza yake kwa nguvu kujaribu kuwatuliza wafanyakazi wake.

“Nimewaita hapa sio kuzomeana … I asked you all here not to explain the incident, what I want is to hear is a solution, A solution”Aliongea Edna kibabe akimaanisha kwamba amewaita kwenye kikao hiko sio kuelezea namna tukio lilivyotokea , bali ni kuangalia namna gani ya kudili na tatizo.

“Boss Edna , ndio ninachoona ni kipaumbele kwasasa ni kuhakikisha tunapata Ushahidi wa nani kaiba taarifa za kampuni na kuziweka mtandaoni ….if we can gather evidence within short period of time , then we can file criminal suit , with that we might be able to take control of the situation, ijapokuwa tutapata hasara lakini naamini tutaweza kulipwa fidia kupitia vipengele vya kisheria na naamini swala hili halihusiani na mtu mdogo bali ni mtu mkubwa ambaye anajaribu kuibomoa kampuni hii”Alitoa maoni moja ya mfanyakazi mmoja mwanamama mtu mzima ambaye muda wote alikuwa kimya.

“Ushahidi gani mnataka , tunajua wote hapa kwamba nyaraka zote zilikuwa kwenye safe box katika idara ya masoko na watu wawili tu ndio waliokuwa wakijua nyira za hizo box na ni Boss Edna pamoja na Benadetha, kwanini tunataka kuanza kutafuta Ushahidi mbali , wakujibu maswali yetu yote ni Benadetha pekee”Aliongea mwingine.

“Mimi nasema miaka ile ndio maana Benadetha alivyopandishwa cheo sikukubaliana kabisa na hili swala , siamini kama ameweza kufanya jambo kama hili”Aliongea mwanamke mwingine ambaye alionekana dhahiri hakuwa akimkubali kabisa Benadetha..

“Jamani nadhani tufikirie kwa mantiki , wote hapa tunajua Benadetha na boss Edna ndio ambao wanajua password za sehemu nyaraka zilipohifadhiwa , kama kweli mnadhani Benadetha ndio kafanya hivyo nadhani mnakosea , inawezekanaje mtu akafanya kitu ambacho kitamfanya yeye mwenyewe kuonekana mtuhumiwa , hakuna logic yoyote ya Benadetha kufanya jambo hili, na tunatakiwa kuanza kujua nani kahusika”Aliongea Nasra lakini alikatishwa na Ernest Komwe.

“Sikupingi Mhasibu mkuu wa kampuni , lakini muda mwingine hizi zinawezekana kuwa mbinu za mtuhumiwa tu , hebu tujaribu kufikiria huenda Benadetha alitaka wote sisi kuona ni ujinga kufanya jambo ambalo litamfunga yeye mwenyewe , lakini wakati huo huo akiwa amefanya yeye , jamani nawaambieni watu wana mbinu nyingi , hivyo nashauri Benadetha ahojiwe vizuri”Aliongea Ernest Komwe na kwa jinsi alivyokuwa akimkandia Benadetha na kwa jinsi ambacho walionekana kuwa marafiki siku kadhaa zilizopita ni dhahiri angeshangaa unafiki unaonyeshwa na Ernest

“Mr Ernest maneno yako yanamkandamiza moja kwa moja Benadetha ilihali hakuna Ushahidi”Aliongea Nasra.

“Miss Nasra nisamehe kwa namna yangu ya uongeaji wa moja kwa moja, huwa sipendi kusimama upande wowote kwenye jambo kama hili linalohusiana na maslahi ya kampuni, naongea kwa niaba ya wafanyakazi wote, Hivyo nakusihi uache kabisa upendeleo”Aliongea na kumfanya Nasra kumkata jicho Ernest.

“Wote naomba mnyamaze”Aliamrisha Edna na kisha akamgeukia Monica.

“Monica majibu ya makadirio yametoka?”

“Yes, Boss . I’ve done a rough estimation of the loss from those tender projects, purchasing projects, acquisition plans and design plans. We’re looking at a loss of at least five billion dollars. It’s mainly because our purchasing and acquisition plans this year are expanding at a global level. Our budget has been completely expanded. Our contingency plan did not account for accidents like this one.”

“Ndio Boss , nimefanya makadilio ya hasara kutoka kwenye miradi yote ya kizabuni , miradi ya ununuzi , mipango ya usanifu na hasara imefikia kiasi cha bilioni dola bilioni tano , hii yote ni kwasababuu mipango yetu ya ununuzi pamoja na ile ya upataji wa makampuni mengine kwa mwaka huu ilipanuka Zaidi kimataifa hivyo pia bajeti yetu kupanuka , mipango yote ya dharula ndani ya kampuni haikuweza kutabilia kutokea kwa swala kama hili”Aliongea Monica kwa lugha ya kingereza na kufanya watu wote hapo ndani kuwa kwenye mshangao , hawakuamini ndani ya masaa machache tu siku ya jana hasara imekuwa kubwa kiasi kama hicho.

“Naamini hio sio hasra pekee itakayo tokea, nawakumbusha tu leo na kesho soko limefungwa , soko la NASDAQ litakapofunguliwa jumatatu tutegemee hisa za kampuni kutupwa Zaidi sokoni kwasababu swala hili lishasambaa mtandaoni na hakuna muwekezaji ambaye atapata ujasiri wa kushikilia hisa zetu , hivyo itapelekea upungufu mkubwa wa ‘Asset’ za kampuni , hata kama tutaweza kupata mkopo benki kushindana na kinachoendelea , itakuwa ni swala la muda mfupi tu, hali ikiendelea kama hivi tutegemee hatuwezi kurudi tena kuwa imara kwa miaka kadhaa ijayo”Aliongea Richie Mzungu , mfanyakazi ambaye aliletwa na Edna siku kadhaa zilizopita.

“Daah , hakuna namna hata ya kurudisha mapigano , nikija kumpata muhusika wa hili nitamnyoa nywele na maji ya moto ”Aliongea bwana mmoja kibonge ambaye alionekana kushindwa kuzia hisia zake.

“Boss Edna nashauri Benadetha kutolewa polisi, najua swala hili ni kubwa lakini kuendelea kumuweka kituoni ni kama kumuonea kwani kwa ninavyomjua hahusiki”Aliongea Dorisi akijaribu kumtetea Benadetha.

“Dorisi naomba usiweke hisia zako kwenye maswala muhimu kama haya , hii ni biashara ilio rasmi na kuna wafanyakazi wengi ambao wanategemea kupata mishahara kupitia biashara hii na ni wajibu wangu kuilinda kwa namna yoyote ile, atakuwa chini ya uchunguzi mpaka nitakapohakikisha hahusiki na kumpata muhusika”

“Lakini Edna jaribu kuwa na huruma kidogo , akiendelea kuwa polisi unafikiri ni madhara gani ya kisaikolojia yatamtokea?”

“Miss Dorisi tafadhari kaa kimya , matendo yako yanatufanya tukuone unashirikiana na Benadetha katika hili”Aliongea Ernest Komwe.

“Naona unafurahia sana, lakini nikushauri ni mapema sana , mwisho wa siku lazima tutamfahamu muhusika”Aliongea Nasra.

“Hata mimi natumaini hilo litokee”Alijibu.

Muda uleule wakati wakiendelea kubishana, mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na akaingia mtaalamu Roma na kufanya kila mmoja kumgeukia.
Ni nini kitajiri hakikisha hukosi mwendelezo siku ya jummanne
wasiliana na mimi watsapp 0687151346
 
Mtaalamu Roma anaingia huku akiwa amepokea simu ya vitisho toka Jana yake
 
Back
Top Bottom