Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Unawaza nini mkuu? Au kuna tusichokijua kuhusu afya yako kwa siku ya leo?
 
SEHEMU YA 409

Saa mbili kamili za usiku ndio Roma alirudi kutoka anapishi Nasra mara baada ya kuhakikisha yupo salama kiafya mara baada ya kumfanyia uchawi wake kwani kilichomfanya Nasra kupoteza fahamu ni kukaa muda mrefu nje kwenye mvua pamoja na kutopata usingizi kwa siku chache , Roma njia nzima alikuwa akiwaza namna ya kumaliza hasira za mke wake Edna , lakini kwa muda huo hakuwa na namna aliona itafaa.

Baada ya kuingiza gari yake ndani ya nyumba yao alijikuta akivuta pumzi ya ahueni mara baada ya kugundua gari zote zimerudi ,yaani gari aliotoka nayo Sophia na ile ambayo alitoka nayo Edna , na mpaka hapo alijua Edna atakuwa ndani pamoja na Sophia.

Roma aliegesha gari yake na kutembea kivivu mpaka ndani na ile anafika sebuleni aliweza kumuona Yezi pamoja na Sophia waliokuwa wakipiga soga.

“Roma umerudi , karibia kabisa mezani ni muda wa chakula”Aliongea Blandina kwa ukarimu akimkaribisha mwanae kwenye meza , ijapokuwa hakupendezwa na kitendo kilichotokea mchana , lakini hakuwa kwenye nafasi ya kumlaumu mwanae kwa jambo lile , alichoshukuru tu ni kwamba mke mwana alirudi baada ya kuondoka kwa hasira.

“Sophia naYezi mtaongea baadae ni muda wa chakula huu”Aliongea na Roma aliwaangalia wasichana hao kwa tabasamu na kisha akatangulia Kwenda kukaa na wakafuatia, Sophia na Yezi walionekana walikuwa kawaida tu kama vile walipotezea kile kilichotokea.

Muda huo Roma alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona Edna akitokea jikoni akiwa amebeba mabakuli ya chakula , hakutarajia kwa namna alvyokasirika angerudi na kujishughulisha na kazi za nyumbani.

Edna aliweka mezani pasipo ya kumwangalia Roma usoni na kisha akaaa chini akifuatia Bi Wema na Blandina na ulaji wa chakula uliendelea pasipo kugusiwa kwa swala lililotokea na ni baadhi ya stori tu za hapa na pale ambazo alikuwa akiongea Sophia katika ziara yake nje ya nchi..

Baada ya chakula Roma hakuenda juu kwenye chumba chake alisubiria hapo hapo sebuleni kwa ajili ya kupata nafasi ya kuongea na Edna ambaye alikuwa akisafisha vyombo jikoni akisaidiana na Bi Wema.

Baada ya madakika kadhaa Edna alimaliza na Roma alivyomuona anapandisha Kwenda juu alimfuata huko huko.

“Edna ..!”Aliita Roma na Edna alisimama pasipo kugeuka huku akiwa ameshikilia kitasa cha mlango.

“Edna naomba unisamehe kwa kile kilichotokea mchana , najua sikupaswa kufanya vile ila sikuwa na namna nyingine bora Zaidi , sitaki kuongea Zaidi kukasirisha ila kuna kitu nilipanga kukupatia kama zawadi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kugeuka na kumwangalia kwa macho makavu.

“Nini unataka kunipatia?”Aliuliza Edna akisubiria kwa matarajio makubwa ni kitu gani cha thamani Zaidi ya pete ya almasi anataka kupatiwa.

Roma aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yake na kisha alitoka na saa ile ya mfukoni alioichukua kwa marehemu Robert Mueller na kisha akampatia Edna mkononi.

Edna aliangalia saa ile kwa kuichunguza, alikuwa akijua kuhusu ‘Pocket Watch’ nyingi kutokana na ‘Exposure’ aliokuwa nayo , lakini saa aliopewa ya Roma aliiona ya kawaida sana na Zaidi ya kuwa ya chuma kilichopambwa na madini ya dhahabu hakuna kingine cha kuridhisha , kwanza kabisa ilionekana kupita kwenye mikono ya watu wengi.

Edna alijiambia yaani Mchepuko unapewa pete ya Almasi lakini yeye anapewa saa ya mfukoni isiokuwa na thamani..

“Nilikuja na zawadi za aina mbili kutoka Marekani mpango wangu ulikuwa ni nikukupatia ile pete ya almasi lakini nilipatwa na wasiwasi na Nasra ndio maana nikampatia , lakini nimebakiwa na hii saa naomba uichukue kama zawadi ni nzuri sana”Aliongea Roma.

“Asante sana mume wangu kwa zawadi hii yenye thamani kubwa sana , Hongera kwa kunijali”Aliongea Edna huku akiangalia lisaa lile la chuma kinafiki.

“Edna hio saa ni nzuri nimeichukua kutoka kwa Kamishina mkuu wa FBI”Aliongea.

“Kamishina wa FBI? Je utaniambia ni nini kimetokea mpaka ukaichukua kutoka kwake , najua una uwezo mkubwa na ndio maana uliweza hata kutoa pete ya Almasi ya pink kwa mwanamke mwingine, hata hivyo mimi ni mke wako nadhani sipaswi kulalamika kwa kile unachonipatia kama zawadi, Asante sana Mungu kwa kumfanya mume wangu kumkumbusha kuniletea zawadi na sio presha”Aliongea Edna kinafiki pamoja na hasira zilizokuwa juu juu na alionekana kuwa mvivu sana hata kuikagua saa ile na alifungua mlango wa chumba chake na kuingia ndani huku akifunga mlango kwa nguvu..

Baada ya kufunga mlango alijikuta machozi yakianza kumtoka mfululizo huku akiangalia juu , wakati anamuona Roma anamkabidhi mwanamke mwingine pete ya Almasi alitamani kupoteza Maisha ili maumivu alioyasiikia yampotee mara moja,

Ni kweli kwamba alimuonea huruma Nasra kwa hali aliokuwa nayo na katika maisha yake alishaomba mara kibao aje kupata mwanaume atakaye mpenda na kuanzisha familia , lakini nani angejua mwanaume anaekuja kumpenda ni mume wake.

Aliona ni kama mbingu zilikuwa zikimuonea kwa kumpitisha kwenye wakati huo na alijimbia kama sio kufanya maamuzi ya kujitoa kwa mwanaume huyo na kuwa mume wake huenda Maisha yake yasingemfikisha kwenye wakati huo mgumu wa kuumiza kihisia.

Edna akili yake alihisi ilikuwa imemvurugika alishindwa kuelewa alikuwa na hasira , wivu au makasiriko kwa kile kilichotokea , alitamani ampige Roma mpaka ahakikishe ametoka damu huenda akapunguza hasira zake.

Alifikiria juu ya talaka lakini aliona halitakuwa suluhisho na itakuwa ni kama amekubali kushindwa na michepuko kitu ambacho hakipo kwenye falsafa yake kabisa , Edna alijiambia hajawahi kukubali kushindwa hivyo kuachana na Roma atakuwa ametoa ushindi.

Hakutaka wanawake wale siku moja wakae chini na kumnyooshea vidole wakimsimanga kwa kumwambia alishindwa kumtunza mume ndio maana akaachwa..

Alijiambia hata kama ataishi kwa kumlaani Roma Maisha yake yote lakinni hawezi kumuacha akawa na amani na wanawake wake wengine , alijiambia ataishi kwa kumkoroga yeye na wanawake wake.

Ndio maana akaamua kurudi nyumbani ,aliumia mume wake kumpa zawandi mwanamke mwigine mbele ya mama yake na wadogo zake , lakini licha ya hivyo aliona sio sababu ya kutosha kuachana na Roma , alifikiria alikuwa tayari na mtoto Lanlan aliekubali kumlea kwa kushirikiana na mume wake , hivyo kama angeachana na Roma pia angemkosesha Lanlan malezi ya baba, hakutaka Maisha aliopitia yeye ya kutopata mapenzi ya baba yajirudie kwenye Maisha ya Lanlan.

Ni kweli kwamba alikuwa na uwezo wa kupata mwanaume mwingine kutokana na uzuri wake , lakini ni nani angempenda kwa mapenzi ya dhati tofauti na utajiri wake.

Lakini licha ya hivyo pia kuna mengi ambayo yalikuwa yakiendelea swala la mama yake kupoteza Maisha kwa kuuliwa na mtu lilikuwa likimfikirisha sana na alikuwa akifikiria hatua ya pili ya kufatilia juu ya hilo , lakini kutokana na namna mama yake alivyokufa alikuwa akihitaji ulinzi , hivyo ni kama kuishi na Roma licha ya kwamba alikuwa na wanawake wengine ni jambo ambayo anaweza kuendelea kulivumilia huku akiendelea kutimiza mambo yake.

Hata alipokutana na Sophia njiani aliemfuata nyuma alimpa ushauri ule ule wa kile alichokifikiria na ndipo alipopata nguvu ya kurudi nyumbani huku akijifariji ile ni pete tu ya kawaida ya bei rahisi na anao uwezo wa kununua hata mia moja ya aina zile.

Alikaa chni kitandani huku akiwa ameshikilia zawadi yake na kuanza kuigeuza kwa namna ya kuichunguza , licha ya kuwa saa inayofanya kazi yenye vimishale vingi visivyoeleweka pamoja na baadhi ya maandishi yaliosomeka kwa ndani lakini aliiona kama chuma Kizito tu chenye ubaridi kwenye mikono yake.

Alijiambia saa hio ilikuwa kama moyo wake , ulikuwa ukifanya kazi lakini ulikuwa wa baridi, alijikuta akiikumbatia saa ile na mikono yake kwenye moyo wake huku akitoa machozi.

……….

Kwa jinsi alivyomuona mke wake ni kama alimuongezea maumivu mara baada ya kumpatia ile saa na hakuna cha maana alichokifanya , lakini hata hivyo aliamini ingemrudisha katika hali yake ya kawaida , lakini matokeo yake yalikuwa tofauti.

Baada ya kumaliza kuoga na kujiweka sawa , simu yake ilitoa mlio kuashiria inaita na baada ya kuangalia jina la mpigaji lilikuwa ni babu yake Afande kweka , alipokea na kuweka sikioni.

“Brat nasikia ulikuwa Marekani?”Ilisikika sauti ya upande wa pili mara baada ya kupokea simu.

“Umeweka watu wa kunifuatilia?”

“Ni vibaya kumfuatilia mjukuu wangu kwa kile alichokifanya hata nisikuwekee watu wa kukufuatilia kwa utukutu wako nitajua tu”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Usharudi kutoka Iringa nitakuja kumchukua Lanlan”Aliongea Roma , aliamini Lanlan kidogo anaweza kurudisha mudi ya mama yake kama atawepo.

“Ndio nilichokupigia , kiukuu changu mwenye akili nyingi kuliko wewe anataka kurudi nyumbani kwasababu amemkumbuka mama yake , kesho unaweza kuja kumchukua na Zenzhei anataka kuzungumza na wewe”Aliongea na kumfanya Roma kuguna kidogo, tokea aachane na Zenzhei mara ya mwisho hakuongea nae tena na ni mengi ambayo yametokea.

“Sawa nitakuja mchana kumchukua Lanlan, ulale salama mzee”Aliongea Roma na hakusubiri jibu upande wa pili na alikata kwanza hakupenda mzee huyo kumwita ‘Brat’ akimaanisha yeye ni mtukutu.

Siku iliofuata Roma ilibidi kwanza kuelekea kazini hata hivyo alikuwa amemkumbuka mrembo wake Amina hivyo aliona sio mbaya Kwenda kumuona asubuhi hio kabla hajaanza safari ya kuelekea bagamoyo kumchukua Lanlan.

Roma baada ya kufika kazini aliweza kupokelewa na Amina ambaye siku hio alifika na walisamiana kwa mahaba kama kawaida , Roma hakuwa na wasiwasi kabisa anapokuwa na wanawake wengine , ijapokuwa alikuwa na ugomvi na mke wake lakini hakutaka ugomvi wake kuathiri mahusiano yake na watu wengine kabisa.

Usiku mzima wakati Roma alivyokuwa akiwaza alikumbuka tokea aanzishe mahusiano na wanawake wote , hakuna hata mmoja ambaye alikuwa ashapata ujauzito na hilo lilimshangaza kidogo , ijapokuwa ashawahi kuhisi labda ni kwasababu ya Godstone lakini kuna hisia nyingine zilimwambia huenda kinachomfanya kutoweza kutungisha ujauzito kwa mwanamke ni kutokana na mbinu ya kijini ya Kimaandiko ya Urejesho , wazo hilo lilimjia mara baada ya Mzee kweka kumwambia kesho anatakiwa kuonana na Zenzhei kutokana na kwamba kuna kitu alichokuwa akitaka kumwambia , Roma alijiambia akifika huko atamuuliza ili kujua kama kuna uhusiano wowote na mafunzo yake ya kijini na kutoweza kupata mtoto, maana kwa Seventeen iliweza kufanikiwa licha ya kwmaba aliamini mtoto wake hakuzaliwa kutokana na kifo cha Seventeen.

Roma kazi zote ni kama zilimalizwa na Amina , hivyo hakukuwa na kazi nyingine kubwa Zaidi ya kupiga stori na Amina kiasi cha kumfanya kucheka sana kwani Amina alikuwa akifanya vituko vingi mbele yake na Roma alijiambia katika warembo wake wote Amina alikuwa ni wa aina yake , kwani licha ya kuwa mzuri lakini alikuwa mjamja mno na muongeaji mwenye stori nyingi za kuchekesha , Roma aliona huenda ndio maana akawa mwandishi wa habari.

Roma ilivyofika saa sita mchana aliaga na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Afande Kweka , alipanga akale chakula cha bure huko huko ndio maana alichagua muda huo , dakika chache tu aliweza kufika na mtu wa kwanza kumuona ni Lanlan aliekuwa akicheza na mbwa mdogo wa saizi ya kati jambo ambalo lilimshangaza na kujiuliza mbwa huyo amemtoa wapi.

“Dadii..”Lanlan mara baada ya kumuona Roma akishuka kutoka kwenye gari alimkimbilia na kumvaa kifuani na Roma alimdaka vizuri na kumbeba juu.

“Lanlan umepata wapi mbwa?”

“Lanlan amempata rafiki yake huko msituni tulikoenda na Grandpa”Aliongea Lanlana kwa kingereza na kumfanya Roma kucheka

“Kwaho rafiki yako amekuwa mbwa?”

“Ndio ni rafiki wa Lanlan na ananipenda sana ,nataka mama kumuona”Aliongea Roma na kufurahishwa na maelezo ya kitoto ya Lanlan huku akizunguka upande wa nyuma baada ya kukutana na Qiand Xi ambaye alimsalimia kwa kuinamisha kichwa chini kwa heshima.

“Mzee kwahio zawadi kubwa uliohisi inamfaa Lanlan ni mbwa?”Aliuliza Roma mara baada ya kumkuta Afande Kweka akinyweseha maua na bomba la maji kwa mkono mmoja huku akiwa ameshika mkasi wa kunyooshea maua kwa kuyakata.

“Haha… huyu mtoto anafurahisha , sijamtafutia mbwa mimi ila alimtafuta mwenyewe , Lanlan mwelezo baba yako jinsi ulivyompata mbwa wako”Aliongea Afande Kweka huku akionyesha kuwa katika mudi nzuri kweli

”Lanlan ataongea baada ya Mama kuwepo”Aliongea Lanlan kwa sauti ndogo na kumfanya Afande Kweka kucheka tena.

“Okey ! Okey! Lanlan unapaswa kufanya hivyo ukirudi nyumbani kwa Mama”Aliongea na Lanlan alitingisha kichwa kukubali na Roma alimtua chini Lanlan ili amshikilie mbwa wake ambaye habanduki nyuma yao.

“Hebu shika nyweshea nyweshea mpaka kule mwisho”Aliongea Afande Kweka akimpatia Roma bomba la maji.

“Mzee unaonekana hujawahi kuwa mkulima wenzako wananyweshea asubuhi wewe mchana?”

“Mimea ina utofauti gani na binadamu , wote tunashauriwa kula angalau mara tatu kwa siku hivyo hivyo hata kwa mimea hakuna ubaya wowote ukiyanyweshea mara tatu kwa siku ukizingatia ukali wa jua ”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Roma kutoongezea nano na kuendelea na kazi ya umwagiliaji.

“Roma unafikiria lini kurudi rasmi kwenye familia yako na kutambulika kama mjukuu wangu?”

“Kuna utofauti gani na sasa , au unapanga niishi hapa kwako?”

“Sijamaanisha hivyo , familia hii sio ndogo kama unavofikiria naweza kukutambua kama mjukuu wangu lakini kuna ndugu zako wengi ambao wanapaswa kukutambua pia wamesikia juu juu Habari za kurudi kwako lakini hakuna hata mmoja amethibitisha kuwa za kweli na wanahitaji kukuona, kurudi kwako hapa Tanzania ilikuwa ni kwa ajili ya kukutana na familia na sasa umeipata unapaswa kuwajua wote”Aliongea Afande huku akitumia mkasi kuchimba chimba karibu na shina la maua.

“Andaa siku yoyote unayotaka , sina tatizo na hilo”Aliuongea Roma na kumfanya Afande kweka kutabasamu.

“Nadhani itakuwa vyema ikiwa ni siku ya tarehe ishirini na tano , utakuwa muda mzuri kwani watu wapo mapumziko ya sikukuu ya christimasi”Aliongea Afande Kweka na Roma hakuona haja ya kukataa , kwanza alikuwa free muda wote lakini pia hakuona kuna ubaya kufahamiana na watu wanaosemekana kuwa ndugu zake.

Baada ya kuongea ongea na Afande Kweka muda wa chakula uliwadia na hata Zenzhei alikuwepo na alikuwa akimwangalia Roma kwa mshangao mno na Roma aligundua hilo , alijua ni lazima Zenzhei atakuwa anajiuliza kwanini Roma hakuwa akionekana kuwa na nguvu zozote kwenye mwili wake kama ilivyokuwa kwa Christen na Poseidon walivyoshindwa kuona uwezo wake..

Roma alijiambia alifanya maamuzi sahihi ya kuja muda huo kwani ilionekana Afande Kweka alichinja mbuzi na nyama yake ilionekana kuwa tamu kweli na yeye na Lanlan waliifagilia vilivyo.

Baada ya chakula Roma hakutaka sana kukawia kuondoka na ndio maana aliomba kuongea na Zenzhei.

“Mr Roma umebadilika sana tokea mara ya mwisho tulivyokutana”Aliongea Zenzhei mara baada ya kuketi kwenye bustani.

“Ninaonekana vipi?”Aliuliza Roma kwa tabasamu huku akiuliza swali ambalo ni kama alimpima.

“Siwezi kusema unaonekana vipi , lakini ninaweza kujibu kwa kutaka kujua ni kwa namna gani umefanikisha kuficha uwezo wako nisiweze kabisa kuuona?”

“Unaamini ninao uwezo wangu?”.

“Naamini kuna uwezekano wa kuficha uwezo wa kijini na kutoruhusu watu kujua upo kwenye levo ipi , lakini ni mara chache sana kukutana na watu wa aina hio kwenye jamii ya kijini”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu na kuona angalau alikuwa akiongea na mtu sahihi.

“Unaweza kuniambia mbinu ambayo inatumika ujinini kuficha watu kuona levo uliopo?”

“Mr Roma mara ya mwisho mara baada ya kunielezea kuhusu stori ya Zeus na Athena kudhibitiwa na majini ilinifikirisha na kunifanya kuchukua hatua ya kufahamu kile ambacho sikuweza kukijua na niliweza kukutana na mjumbe kutoka jamii ya kijini na akanipa baadhi ya taarifa zilizotokea”

“Enhe inafanana kabisa na nilivyokuambia?”Aliuliza Roma alitaka kufananisha na stori alioambiwa na Christen pamoja na ile ya Master Chi.

“Inavyoonekana ulikuwa ni sahihi licha ya ulichoniambia kutokukamilika , Mjumbe amenielezea ni kweli Zeus na Athena waliweza kushambuliwa na moja ya mababu zetu waliopo kwenye historia mpaka sasa kwa kuweza kufikia levo za juu za kijini….”

Maelezo ya Zenzhei yalikuwa yakifanana kwa kiasi kikubwa sana na ya Christen japo kulikuwa na kilichoongezeka.

Zenzhei anasema ni kweli kwamba Zeusi na Athena walikuwa ni tishio kubwa kwa majini mara baada ya kufika duniani kutokana na uwezo wao wa juu wa kutumia kanuni za anga , lakini pia siraha walizokuwa wakimiliki , hivyo kupelekea majini kutofanikiwa kuwashindwa katika uso wa dunia ya kawaida na ndipo moja ya Grand Master kutoka miliki ya kijini ya milima ya PANAS alivyoingilia kati mpaka kuwaingiza Athena kwenye mtego.

Zenzhei anasema Zeus na Athena mara baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na GrandMaster kutoka miliki ya kijini katika ulimwengu wa kawaida walishangazwa na namna ambavyo mwili wake ulikuwa wa kawaida sana na kutokua na msisimko wa aina yoyote wa nguvu za kijini , jambo ambalo liliwafanya kujawa na shauku kwanini yeye alikuwa tofauti na wengine kuwa na uwezo wa aina hio na wakati mmoja kuwa na uwezo mkubwa wa kimapigano na kutengeneza maajabu ndipo Grandmaster alipowaambia yupo tayari kutoa siri yake kama tu watakubali Kwenda kushindana nae kwenye eneo ambalo amelichagua yeye.

Kutokana na majigambo ya Zeus alikubali mara moja licha ya Athena kumsihi kwamba unaweza kuwa mtego , lakini Zeus alijiambia hakuna jini lolote ambalo linaweza kumzidi akili lakini pia alikuwa na shauku kuona miliki ya kijini ilivyofanana ili kuangalia pia namna ya kuiangamiza hivyo akawa tayari kufuatishana na GrandMaster.

“Kwahio unamaanisha GrandMaster alitokea katika miliki ya PANAS na alikuwa na levo ya juu ya nguvu za kimajini pasipo ya kudhihirisha uwezo wake?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Ndio Mr Roma na niliuliza mbinu hio jina lake na mjumbe alinielezea mpaka leo ipo kwenye maktaba za kijini katika mfumo wa lugha isioeleweka, na ni majini mengi wamejitahidi kujifunza lakini walishindwa kuielewa naamini ni mbinu ambayo wewe umejifunza , mara ya mwisho kabla ya Kwenda Marekani nilikuona ulishapanda kwa haraka levo na kufikia mwanzo wa levo ya Nafsi na ilinishangaza sana na mpaka sasa naamini umefika levo ya juu Zaidi ndio maana umefanikiwa kuweza kuuficha uwezo wako?”Aliongea Zenzhei kwa shauku na Roma hakutaka kumficha Zenzhei kile kilichotokea aliamua kumwelezea mwanzo mwisho namna alivyopigwa na radi na mbinu yake ya kimaandiko ya urejesho usio na kikomo ilivyomsaidia na mpaka anamaliza Zenzhei alijikuta akifuta jasho akiwa kama haamini vizuri.

“Mr Roma unamaanisha umeweza kufikisha levo ya kuipita Dhiki ndani ya mwezi mmoja tu?”Aliuliza huku akihema kwa tabu , kwenye ulimwengu wa kijini iliwachukua majini Zaidi ya miaka mia moja kufikia levo ya Nafsi sembuse hio ya kuipita Dhiki , ilikuwa hakika jambo jipya na la kushangaza kwake.

“Naweza kusema nimefika kwenye levo hio , licha ya mimi mwenyewe kutoelewa ukubwa wake na namna mwili wangu ulivyobadilika tofauti na mwanzo , sasa hivi najihisi kuwa kama binadamu wa kawaida sana napatwa na hisia ambazo ni kama naelewa kinachoendelea chini ya nyayo zangu na juu ya utosi wa kichwa changu”

“Mr Roma kwanza nikupe hongera kwa kuweza kufikia levo kubwa namna ya haraka nimeweza kufurahi mno mno”Aliongea Zenzhei huku akijiambia kama kweli Roma ameweza kufikia levo ya kuipita Nafsi kwa kupitia radi ya mipangilio tisa basi anaweza kuwa kama Grand Master ambaye anaogopwa na majini yote na anaweza kumsaidia sana katika kisasi chake , lakini hata hivyo hakuwa tayari kumwambia juu ya mpango wake kitendo cha kutaka afike ni nyumbani hapo ni kuangalia levo ya Roma aliyofikia , ijapokuwa mwenyewe aliamini Roma anaweza kupanda levo kwa haraka lakini sio kwa uharaka huo.

“Bi Zenzhei naomba kuuliza swali moja ambalo linanitekenya sana?”

“Unaweza kuuliza Mr Roma?”

“Kuna athari zozote za uzazi kwa binadamu anaejifunza mbinu za kijini?”

“Nadhani nimelewa swali lako Mr Roma, unamaanisha kutokana na kwamba mpaka sasa umeshindwa kupata mtoto unaamini kuna uwezekano wa kutoweza kutungisha mimba kutokana na nguvu za kijini , si ndio hivyo?”

“Ndio swali langu”

“Ni kweli kabisa Mr Roma , kuna athari na sio kwa binadamu tu mpaka ujinini ikitokea umeenda levo ya juu sana na mkeo akawa levo ya chini au kukosa kabisa nguvu zozote za kijini hatoweza kupata ujauzito , ijapokuwa jambo hili sio tatizo sana kwa majini kutokana na uwepo wa Dhana mbalimbali lakini jini au binadamu ambaye ana kiwango kidogo cha nishati ya Ardhi na mbingu kwa pande zote za mwanamke na mwanaume kunaweza kusitokee mafanikio yoyote yakatayoleta mtoto duniani”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma kushangaa.

“Unaweza ukanyoosha vizuri maneno”

“Labda nikuelezee kidogo namna inavyofanyika huko ujinini, kwa mfano kama mwanaume tuseme akawa kwenye levo ya Nafsi na mwanamke kukosa nguvu yoyote ya mbingu na ardhi basi mume atashauriwa kumfundisha mwanamke wake angalau kufikia levo ya mzunguko kamili na baada ya hapo atamvalisha Dhana maalumu kwa ajili ya kubusti mwili wake ili kutengeneza mazingira ya mimba kutunga katika mfuko wake wa uzazi”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi na kuzishuaha.

“Kwahio inamaanisha kama hana kabisa nishati hakuna uwezekano wa kupata ujauzito?”

“Ndio Mr Roma na kwa mfano wako ili uweze kupata mtoto ni lazima mwanamke wako angalau afikie mwishoni mwa levo ya Nafsi na kisha avalishwe Dhana ndipo ataweza kuhimili mbegu zako na hatimae kuleta jawabu la mimba”Aliongea na kumfanya Roma kunyong’onyea alijiambia kama ni hivyo basi hakuna mwanamke wake ambaye ataweza kubeba ujauzito wake.
 
SEHEMU YA 410

Edna siku hio alivyofika kazini aliweza kuonana na Suzzane , haikueleweka ni kipi alichoongea ila alionyesha mwishoni maagizo Edna anayompatia kuyatoa kwa msisitizo mkubwa na kisha Suzzane akaondoka.

Licha ya yale yaliotokea jana alionekana kutokuwa na aina yoyote ile ya kuonyesha kama alikuwa na mawazo kwasababu alionekana kuwa wakawaida tu , lakini kidogo akiwa siriasis kuliko siku zote.

Baada ya Suzzane kuondoka Edna alichukua rimoti ya Tv iliokuwepo ndani ya ofisi yake na kisha akaiwasha na taarifa ya kwanza alioweza kuisona ni ile inayohusu kifo cha mke wa raisi Jeremy na ilionekana siku hio ilikuwa ni ya mwisho ya kuagwa kitaifa.

Edna alijikuta akiangalia Habari hio na moja ya watu ambao walionekana katika runinga hio alikuwemo mheshimiwa Jeremy ambaye alikuwa ameketi kwenye jukwaa akionekana kuwa katika huzuni pamoja na Desmond.

Mrembo Edna alijikuta akiegamia kiti chake cha kiofisi huku hata kile alichopanga kufanya akikisahau kwa muda , ijapokuwa kuna hali iliokuwa ikimwambia kifo cha Kizwe amehusika kwa namna moja ama nyingine lakini mtu aliemuonea huruma Zaidi ni Raisi Jeremy , alijua raisi huyo ni baba yake na huenda ndio kilichomfanya kuwa na uso ulionekana kuwa na huzuni.

Baada ya kufumba macho kwa dakika kadhaa alijikuta akiangalia tarakishi yake na Kwenda upande wa barua pepe na kutafuta baadhi ya jumbe za barua pepe ambazo zilishawahi kutumwa na mtu aliejiita The Protector.

Ukweli ni kwamba tokea siku ambayo aliweza kuokoa kampuni yake kutoka kwenye kufilisika na kuzidi kupaa kiumaarufu alitarajia kuona ujumbe kutoka kwa The protector hata wa kumsifia , lakini ajabu licha ya kusubiria hakuweza kupata ujumbe huo , zamani Edna hakuwa na ile tabia ya kufatilia sana kama The Protector atatuma ujumbe au lah , lakini mara baada ya kujua baba yake ni Raisi Jeremy alionekana kuwa na ukaribu sana na Email hio lakini licha ya hivyo alijihisi ni kama The Protector amempotezea.

Edna mara baada ya kufika kwenye barua pepe hio , alisukuma mouse mpaka kwenye sehemu ya ‘Replay’ na kisha akaanza kuandika ujumbe mfupi wa maandishi na kisha akautuma kwa kusista sita , ulikuwa ni jumbe mfupi uliokuwa wa salamu za pole, ijapokuwa hakuwa na uhakika kwamba The Protector anaweza kuwa baba yake , lakini aliona afanye hivyo kuthibitisha kitu.

Ukweli moyo wake ulitamani sana raisi Jeremy kumtafuta na kumtambua kama mtoto wake , haikueleweka kwanini Edna alikuwa akihisi hivyo lakini huenda ni kwasababu Maisha yake ya makuzi alikosa mapenzi ya upande mmoja , yaani upande wa baba ndio maana alitamani angalau kuongea na baba yake.

Baada ya kumaliza kutuma ujumbe huo alijikuta akihema kama vile amefanya kazi kubwa na kisha akatulia kwenye kiti chake kwa madakika kadhaa , akionekana kuwaza hili na lile.

Alitumia angalau lisaa limoja kufikiria mpaka pale mlango wake ulipofunguliwa na Dorisi ambaye alimtaka waende wote kupata chakula cha mchana , lakini Edna alimkatalia na kumwambia hajisikii kula siku hio na Dorisi hakutaka kuuliza sana na kisha akafunga mlango kuondoka kwa kuungana na Nasra.

Saa tisa kamili alijikusanya kwa kila kitu chake na kisha alitoka kwenye ofisi yake kwa ajili ya kurejea nyumbani , alikuwa amemkumbuka Lanlan mno na ndio maana alipanga kuwahi kwani alikuwa na taarifa ya kurudi kwake siku hio.

“Edna..!” alijikuta akigeuka mara baada ya kusikia sauti ikimwita kutoka nyuma na kumfanya kutabasamu na kugeuka , aliemwita alikuwa ni Rich mzungu rafiki yake.

“Leo unaonekana kuwahi mno Kwenda nyumbani sio kawaida yako”Aliongea Richie huku akiangalia saa yake ya mkono.

“I missed my daughter very much”Alijibu Edna na kumfanya Richie kutoa macho ya mshangao.

“Edna kwanini , kwanini, kwanini… , kwanini unapenda kunielezea vitu nusu nusu Come on , Una mtoto , tena wa kike?”Aliongea Richie kwa namna ya utani na kuhuzunika na kumfanya Edna kucheka kidogo.

“Ndio Richie mimi na mume wangu tulifanya maamuzi ya kulea”Aliongea Edna na kumfanya Richie kuachama kwa mshangao.

“That is great But why adopting!?”Aliuliza akimaanisha kwanini alee.

“Najua unachokifiria lakini ni maamuzi tu Richie , hata hivyo ungemuona mtoto wangu hakuna namna ya kunitofautisha nae, She is so cute”Aliongea Edna na moyo wake ulizidi kumkumbuka Lanlan, muda kama huo ambao alionekana kuwa na mawazo alijiambia kuwa karibu na Lanlan huenda kungemfanya mudi yake kuwa sawa.

“Hata hivyo Edna mimi na mke wangu tunataka siku kuona mtoto utakaemzaa mwenyewe atakuaje, Je kama ni wakike atakuwa mrembo kama wewe na kama ni wa kiume atakuwa Handsome”Aliongea Richie muda huo wakitokezea nje kabisa ya lift kwenye Parking ya magari.

“Really !Hata mimi pia natamani kuwaona marafiki zangu nyie mtaleta kiumbe wa aina gani”Aliongea Edna na wote walijikuwa wakicheka.

“Edna usisahau ahadi tuliowekeana sku kadhaa zilizopita”Aliongea Richie na kumfanya Edna kufikiria kidogo.

“You mean…,”

“Kusanyiko letu , si unakumbuka marafiki zetu wa chuo watakuja hapa Tanzania ndani ya hii wiki kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu na watakamilisha siku zao kwa sisi kukutana kwa mara nyingine , usisahau tunataka kumuona mumeo”Aliongea Richie na kumfanya Edna kukumbuka Richie ashawahi kuzungumzia hilo swala.

“Okey Richie kama nilivyoweka ahadi tutafika”Aliongea Edna.

“Tarehe ni 26 mwezi huu baada ya sikukuu ya Christmass” Aliongea na Edna alitingisha kichwa kwa tabasamu na Richie alifurahi kusikia hivyo na waliagana kila mmoja akaingia kwenye gari yake.

Edna mara baada ya kuingia alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa wakati mmoja na akaanza kuhesabu siku zilizobaki mpaka siku ya tukio lenyewe na aligundua siku hio ni tarehe kumi na mbili na zilibaki kama siku kimi na nne tu.

*********

Roma alishangazwa sana na maelezo ya Zenzhei na alijiambia hakuna kitu ambacho hakina hasara , mbinu za kijini alizipenda kutokana na faida kubwa kwenye mwili wake , lakini hakuwahi kufikiria upande wa athari zake kimwili

“Bi Zenzhei kwahio hizi Dhana ni za aina gani?”Aliuliza Roma na kumfanya Zenzhei kutabasamu kidogo.

“Mr Roma inaonekana kweli master wako hakukuelezea mambo mengi kuhusu mbinu zetu za kijini , ijapokuwa kwenye ulimwengu wetu tunavuna nishati ya Ardhi na mbingu haimaanishi kwamba hakuna dhana ambazo zinaweza kuboost uwezo wetu , kwa maneno ya kingereza ili uwelewe Dhana hizi ni kama unavyosikia kuhusu Artifact”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Unamaanisha ‘Artifact’ zinatumika kama siraha katika ulimwengu wa majini?”

“Ndio Mr Roma kuna matumizi mengi sana likija swala la Dhana na zipo kwenye makundi mbalimbali , kuna Dhana za mababu ambazo zilitumiwa enzi za kale na kuna Dhana ambazo zinaendelea kugunduliwa ndani ya jamii ya majini , hivyo licha ya kwamba unaweza kuwa na uwezo mkubwa wakijini unaweza ukashindwa kuhimili Dhana hizo , sasa utofauti wao ndio unakuja kuna baadhi yao hutumika kama njia ya kusaidia katika Uzazi kwa majini ambayo yana nguvu kidogo”Aliuongea na Roma kuelewa na alijikuta akikumbuka Edna alishawahi kupewa bangili na Afande Kweka.

“Kuna Bangili Afande Kweka aliweza kumpatia mke wangu , je ina uhusiano wowote na Dhana hizo unazozungumzia?”

“Ndio bangili hio naifahamu pia , ina uhusiano mkubwa kabisa na dhana hizo , lakini ile sio kwa ajili ya kumsaidia kwenye maswala ya Uzazi ile ni kama ulinzi kwake na maroho mabaya yanayoweza kumfanyia mashambulizi lakini pia inamuongezea bahati”Aliongea na kumfanya Roma sasa kuelewa.

Hamu ya kuendelea kujua Zaidi ilimwishia ,ukweli mpaka hapo kidogo alionekana kuwa na mawazo , kama ni hivyo ilimaanisha hakuna mwanamke yoyote ambaye anaweza kumpa mimba na njia moja labda awafundishe mbinu za kijini na apande levo na kisha atafute hizo Dhana na kuwavalisha.

“Kwahio nikitaka hizi Dhana ni lazima niende ujinini?”

“Mr Roma unafikiria kufanya nini?”Aliuliza Zenzhei.

“Nafikiria mengi ya kuwezekana , itakuwa huzuni kama nitaishi kwa kokosa mtoto”Aliongea Roma na kumfanya Zenzhei kuvuta pumzi , ijapokuwa alishindwa kumsoma Roma mawazo lakini aliona amsaidie kwa yale machache aliokuwa akiyafahamu.

“Kuhusu hizo Dhana ni kweli lazima uende ujinini kuweza kuzipata na mathalani ni katika miliki za Hongmeng kwani ndio jamii ambazo wana uelewa na wanajifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi , jamii nyingi licha ya kuwa na mbinu zao lakini sio wenye kujifunza sana”Aliongea na Roma alivuta pumzi.

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale Roma aliaga na kupakiza zawadi za Lanlan kwenye gari yake , Afande Kweka ilionekana mara baada ya kujua mjukuu wake alikuwa akipenda nyama alichinja mbuzi na nyama kuzihifadhi kweye masanduku ya baridi ili Roma kuondoka nazo.

“Bye Grandpaaa..!!!”Aliongea Lanlan akitokezea uso wake Dirishani na kupungiana mkono na babu yake aliekuwa anamwangalia na Roma alitabasamu huku akimwangalia Lanlan alivyokuwa na furaha.

“Lanlan tukifika nyumbani nisaidie kumfurahisha mama yako”

“Mama yake na Lanlan anafuraha muda wote na atafutahi kukutana na rafiki yangu”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu lakini Qiang Xi aliishia kucheka.

“Ooh! Niahidi utanisimulia ulivyokutana na rafiki yako nikiwa na mama yako”

“Lanlan anaahidi atasimulia tukiwa wote na Mama”

“Okey Lanlan hakikisha unatimiza ahadi yako , hakuna kumhadithia mama yako nikiwa sipo”Aliongea Roma na Lanlan alitingisha kichwa kukubali .

********

“Zenzhei vipi umemuonaje?”

“Ni kama nilivyotegemea Camilius , hakika Mr Roma amekuwani wakushangaza”

“Unamaanisha?”

“Sasa hivi yupo kwenye levo ambayo hata mimi mwenyewe sipaswi kumchokoza”Aliongea na kumfanya Camilius macho yake kuongezeka ukubwa kidogo.

“Kwahio unamaanisha alichokuambia mjumbe ni sahihi?”

“Ndio Camillius naamini mpaka sasa haina haja ya Mr Roma kuwa na koneksheni ya moja kwa moja na Zeros na hili litakuwa faida katika mipango inayoendelea”

“Hahaha.. Zenzhei unanifurahisha , kama unayosema ni kweli basi naamini mjukuu wangu ameweza kujikomboa”Aliongea na Zenzhei alitabasamu.

“Ulimwambia kuhusu mpango wako?”

“Sijamwambia Camillius , lakini naamini itakuwa rahisi kuliko nilivyotegemea”

“Unamaanisha nini?”

“Ameulizia swala la athari za kijini katika uzazi na nimemuelezea kila kitu , nitasubiria kuona ni maamuzi gani atayachukua na hatua ya pili ya mpango wangu utafuatia”Aliongea na kumfanya kidogo Afande Kweka kuwa na huzuni.

“Nilitegemea kupata kitukuu wa damu kabisa kutoka kwa Roma na Edna , nadhani hili linapaswa kusubiri”

“Camillius huna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya hilo , Mr Roma atatafuta namna ya kumsaidia Miss Edna kupata ujauzito mapema”Aliongea na kumfanya Afande kweka kuvuta pumzi ya ahueni.

“Zenzhei Roma anayokazi kubwa sana , kwa jinsi anavyoonekana kutokuwa siriasi huwezi kuamini kuna mengi yanayoandaliwa kwa ajili yake ili kuyakamilisha”

“Camillius unazungumzia kuhusu mpango wa Ant- Illuminat?”Aliuliza na Afande Kweka alitingisha kichwa kuitikia.

“Mr Roma anao uwezo mkubwa wa akili naamini ataelewa kila kitu na kukamilisha kila kilichopo mbele yake”

“Naelewa hilo Zenzhei lakini natamani mipango hio ikianza awe tayari ashapata wajukuu, kuna muda natamani kumuelezea aelewe kilichopo mbele yake lakini nashindwa kutokana na maaagizo ya wenzetu”

“Naelewa unachoongea Cammilius , lakini nadhani ni swala la kusubiria , mnao msemo wenu katika Kiswahili wa mvumilivu hula mbivu”

“Hahaha.. upo sahihi”

*********

Dakika chache mbeleni waliweza kufika na kupokewa na Blandina na Bi Wema pamoja na Sophia ambao wote walifurahishwa na kurudi kwa Lanlan kwani alikuwa ni kama pambo kwenye nyumba.

“Bi Wema unaenda wapi?”Aliuliza Roma mara baada ya kuona Bi Wema akiwa amevalia kimtoko mtoko kwa ajili ya kutoka.

“Roma unaonaje ukimsindikiza Bi Wema Bagamoyo?”Aliuliza Blandina.

“Mr Roma usiwe na wasiwasi nitapanda tu daladala ndio kwanza unarudi utakuwa umechoka”Aliongea Bi Wema kwa namna ya kujitetea.

“Bi Wema nitakupeleka wala usijali , sina kazi ya kufanya hapa nyumbani”

“Bi Wema ni kweli Bora ukaondoka na Bro kuliko kutumia madaladala”Aligongea msumari Sophia aliekuwa akicheza na Lanlan.

“Okey Mr Roma kama haitokuwa shida kwako nakubali”Aliongea Bi Wema na Roma alitabasamu.

Dakika chache mbele waliweza kutoka pamoja na kuanza safari kuelekea Bagamoyo.

“Bi Wema licha ya kwamba tumeishi muda mrefu ila sijawahi kusikia ukitaja ndugu zako?”Aliuliza Roma wakiwa njiani.

“Ni Stori ndefu Mr Roma na sina ndugu waliobaki duniani na ambaye nahisi amebakia duniani ndio sababu inayonifanya kuja Bagamoyo kila ikifika tarehe ya leo “Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Bi Wema unaweza kuniambia kwa ufupi nini kimekufanya mpaka ukawa huna ndugu , lakini kama ni ya kuhuzunisha tunaweza kuiacha”Aliongea Roma , ukweli tokea aanze kuishi na mwanamama huyu na kumjua kama mfanyakazi wa muda mrefu wa familia ya Edna hakuwahi kujua wapi alitokea na kwanini hakuwa na ndugu.

“Usijali Mr Roma nitakuelezea kila kitu, ni furaha kwangu kwamba unapenda kunifahamu”

“Ndio Bi Wema ushakuwa mwanafamilia wangu sio mbaya kukufahamu vizuri”Aliongea Roma na Bi Wema alitabasamu.

Upande mwingine mara baada ya Edna kurudi alipokewa kwa shangawe na Lanlan aliekuwa akicheza na mbwa nje na kushangaa kama vilevile alivyoshangaa Roma na kila mmoja aliemuona Lanlan kurudi kutoka Iringa akiwa na mbwa.

“Mama Lanlan alikumisi sana”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kutabasamu huku akimbusu shavuni mara kibao.

“Mama pia amekumisi Lanlan, Mbwa umemtoa wapi?”

“Ni rafiki yake Lanlan na nimekutana nae huko tulikoenda na Grandpa”

“Unaonaje sasa ukinielezea namna ulivyoonana na Rafiki yako”Aliongea Edna na kumfanya Edna kufikiria kidogo.

“Mama nitasimulia baba akiwepo , Lanlan hataki kuvunja ahadi”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa na kutabasamu kwa wakati mmoja.

“Mama Bi Wema kaenda wapi, simuoni?”Aliuliza.

“Amesema anaenda Bagamoyo , Roma kamsindikiza”Alijibu na kumfanya Edna kushangaa kidogo na kuvuta pumzi kwa ahueni.

“Nimesahau tena hii tarehe ni kheri Roma ameweza kumsindikiza”Aliongea Edna.

“Sister Edna kwanini umesema hii tarehe ya leo?”

“Leo ndio siku ambayo Bi Wema aliweza kumpata mtoto wake wa kike aliepotea miaka mingi iliopita baada ya kuzaliwa”Aliongea Edna na kumfanya Sophia kushangaa kumbe Bi Wema anahistoria ya kupoteza mto
 
SEHEMU YA 411.

Stori ya Bi Wema aliyomwambia Roma ni kwamba alishawahi kuwa na mwanaume wake wa kwanza ambaye alitokea kumpenda sana , mwanaume kutoka bara la Asia , yaani China , mwanaume ambaye alikuwa akifanya kazi ya umachinga , mahusiano yake na mwanaume huyo yalikuja kuwa makubwa mpaka kumpelekea Bi Wema kubeba ujauzito.

Kipindi Bi Wema anabeba ujuauzito bado alikuwa anaishi nyumbani kwa Edna na anasema mara baada ya kujifungua , wakati wanarudi nyumbani wakitokea hospitalini ndipo mtoto wake alipokuja kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha huku ujumbe ukiachwa nyuma, ujumbe ambao ulimfanya Bi Wema kugundua aliemchukua mtoto wake kimazingara alikuwa ni huyo mchina ambaye ni mpenzi wake.

Jambo hilo lilikuja kumuumiza sana Bi Wema kihisia , ilikuwa ni kilio kwake kwani mtoto wake alimuona kwa muda mfupi sana tokea ajifungue , alitafsiri alichokifanya mwanaume huyo wa kichina ulikuwa ni ukatili wa aina yake na sio kwa Bi wema tu alieweza kutafsiri hivyo bali kila mmoja aliona alichokifanya mwanaume huyo wa kichina ulikuwa ni ukatili mno , kwani alimtesa sana Bi Wema na ilionekana kabisa hata mapenzi ya mwanaume huyo tokea mwanzo yalikuwa ni ya kuigiza na alimtumia Bi Weka kama chombo cha kumzalia mtoto na hakukuwa na mapenzi..

Sasa kuanzia siku hio mwanaume huyo hakuwahi kurudi wala kujitokeza kwenye Maisha ya Bi Wema tena na mtoto hakuwahi kumuona tena kwa Zaidi ya miaka ishirini.

Kwanzia siku hio Bi Wema Maisha yake yaliendelea kuwa ya huzuni sana na kukumbuka siku ambayo alimpoteza mtoto wake huyo wa kwanza na wa mwisho wa kike katika Maisha yake na kila inapofikia ndani ya tarehe kumi na mbili ya mwezi wa kumi na mbili tarehe ambayo ni ya mfanano na aliojifungua , atafika Bagamoyo Kerege kwenye nyumba ambayo alijenga kwenye kiwanja ambacho alisaidiana kununua na mchina wake wakati wakiwa wapenzi kwa kuwekeana ahadi watakuja kujenga

Kuhusu ndugu wengine wa Bi Wema anasema alizaliwa na kulelewa na mama pekee katika familia ya kawaida , mama yake alitelekezwa huko nyumbani kwao Kagera akiwa mjamzito na mama yake alifariki alipofikisha umri wa miaka kumi na tano na ndipo wakati ambao alikuja kufanya kazi jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na Marium bibi yake Edna , hivyo ni rahisi kwamba Bi Wema hakuwahi kutambua ndugu wa familia ya mama yake , lakini vilevile hakuwahi kumjua baba yake.

Hivyo watu pekee ambao aliwafahamu kama ndugu ni familia ya Adabayo na kuanzia hapo Maisha yake yalikuwa ni ndani ya familia hio na ndio aliemlea Edna kutoka ututoni mpaka akawa mkubwa na ni hapo hapo nyumbani ndipo alipoweza kukutana na mchina huyo aliekuwa akifanya biashara ya kuuza vyombo kama Machinga.

Hivyo Bi Wema kila inapofikia kipindi cha tarehe hio hununua viatu kwenye moja ya duka maarufu la viatu vya Ngozi vya kike na kiume na hukadiria saizi ya mtoto wake kwa kila baada ya ‘Birthday’ yake, hayo ndio yaliokuwa Maisha ya mlezi wake Edna.

Roma alishangazwa na Stori hio , kwani hakuwahi kuijua hapo kabla na ilikuwa ni ya kuhuzunisha mno na alimchukulia Mchina aliemchukua mtoto pasipo hata ya kumpa nafasi Bi Wema kumnyonyesha ilikuwa ni ukatili wa aina yake.

“Bi Wema naamini siku moja utakuja kukutana na mtoto wako wa kike”Aliongea Roma.

“Mr Roma unaamini nitakua kweli kukutana na mtoto wangu?”

“Ndio naamini hivyo Bi Wema kuwa na Imani tu”Aliongea na Bi Wema alitabasamu kwa maneno hayo machache ya Faraja.

“Hata mimi naamini siku moja nitamuona mtoto wangu kabla maisha yangu hapa duniani hayajafikia kikomo”Aliongea na Roma alitabasamu na kutingisha kichwa kwa wakati mmoj.

Roma alimsindikiza mpaka kwenye duka ambalo hununua viatu eneo la Tegeta na akanunua saizi husika kutokana na kukisia umri wa mtoto wake huyo wa kike aliepotea na kisha walielekea eneo la Kerege kwenye nyumba ya Bi Wema.

Roma mara baada ya kufika alijikua akishangaa, kwani licha ya kwamba ilikuwa nyumba ya wastani ya chini lakini ilikuwa ya kisasa mno iliokuwa ndani ya uzio na eneo lake lilikuwa kubwa mno ambalo unaweza kujenga nyumba nyingine ndani yake , ilikuwa ni sehemu nzuri yenye kupambwa vizuri na bustani.

“Bi Wema hii nyumba ni nzuri sana na ni safi mno , nani anafanya usafi”Aliongea Roma huku akishindwa kujizuia kusifia mandhari ya eneo hilo.

“Hapa kuna mama mmoja ananisaidia mara moja moja kufanya usafi , japo hata mimi mwenyewe nakuja mara chache kufanya usafi”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma kuelewa.

Ilionekana Bi Wema alitenga chumba kimoja ndani ya nyumba hio kwa ajili ya mtoto wake huyo wa kike ,kwani kilionekana kuwa na vitu vingi sana kwanzia vya utotoni mpaka ukubwani , huku viatu vikiwa vingi.

Roma alijikuta akishangazwa na mbinu ambayo Bi Wema aliemua kuifanya kama ya kumkumbuka mtoto wake , alijikuta akifikiria stori ya Bi Wema na kukumbuka sehemu ambayo Bi Wema anasema mtoto wake alipotea kwa mazingira yasiokuwa ya kawaida , lakini licha ya hivyo hakutaka sana kufikiria jambo hilo kwani halikuwa likimuhusu sana na hata hivyo lilitokea miaka mingi iliopita.

Baada ya madakika kadhaa ya kumsubiri Bi Wema kufanya taratibu zake hatimae waliweza kuondoka mara baada ya kukutana na mwanamama ambaye Roma alitambulishwa kama ndie aliekuwa akihusika kutunza nyumba hio.

Ijapokuwa Roma alimpa ushauri Bi Wema kama mtoto wake atakuja kurudi , lakini ilionekana Bi Wema alikuwa akiamini mtoto wake atarudi na kuja kuishi kwenye hio nyumba na ndio maana akachagua kuitunza na sio kuipangisha aliajiambia Bi Wema ni mwenye Imani kali kuliko hata alivyotegemea.

******

Zilipita kama siku nne yaani siku ya jumamosi wakati Roma akiwa kazini aliweza kupigiwa simu kutoka Korea Kusini na Bwana Park Jonghyun juu ya hali mbaya aliokuwa nayo Park Juan babu yake Yezi..

Bwana Park alikuwa akiwasilisha ombi kwa Roma kumsaidia kumshawishi Yezi kukubali Kwenda Korea kwa ajili ya kumuona babu yake aliekuwa kwenye hatua za mwisho.

Simu hio Roma alipigiwa akiwa ofisini , hivyo hakumpa jibu la moja kwa moja bwana Park hivyo aliahidi tu kwamba atajaribu kuongea na Yezi na Park alimsisitizia kufanya hivyo kwani ni muhimu.

Mara baada ya simu kukatwa Roma alifikiria kidogo na kuona kuna haja Yezi kwenda kuiona familia yake hususani babu yake ambaye alikuwa kwenye hatua za mwisho za ugonjwa wake, ila alijiambia atashauriana na mke wake kwanza na ndipo aweze kuongea na Yezi.

Roma mara baada ya kurudi nyumbani aliweza kukaa na Edna na kumweleza juu ya simu ya bwana Park kutoka Korea na jambo hilo lilipomfikia Edna hata yeye aliona ni kheri kama Yezi angepata nafasi ya kumuona babu yake hata kwa mara ya mwisho.

Hawakutaka sana kumfosi juu ya Kwenda Korea Lakini walishauriana wangeweza kumpa ushauri ambao ungempa nafasi ya kufikiria na kufanya maamuzi yeye mwenyewe na Edna alinwambia Roma akae chini aongee na Yezi na Roma alikubali juu ya jambo hilo.

Roma usiku aliweza kukaa na Yezi na kuongea nae juu ya umuhimu wa kuonana na familia yake , mathalani babu yake aliekuwa kwenye hatua za mwisho za uhai wake kutokana na ugonjwa wake wa saratani, Roma aliongea kwa urefu kwa kutumia kiasi cha busara alichokuwa amejaariwa na Yezi alionekana kumuelewa na Roma alimwacha ili apate kufikiria na kufanya maamuzi yeye mwenyewe kwani alishakuwa mtu mzima.

Ijapokuwa Roma alijua huenda kuna mpango uliokuwa ukaindaliwa nchini Korea juu ya Yezi lakini aliamini hata kama iwe hivyo hakuna kitu kibaya kitakachomkuta Yezi , kwani aliamini babu yake sio mwenye kukosa akili mpaka amtafute mjukuu wake na kisha kumuingiza kwenye hatari.

Siku iliofuata Yezi alionekana alishafikiria na kufanya maamuzi na aliwaambia wanafamilia kwamba alikuwa yupo tayari Kwenda Korea kwa ajili ya kuonana na babu yake , jambo ambalo lilipokelewa kwa pongezi na wanafamilia wote akiwemo Blandina.

Roma baada ya kupata maamuzi ya Yezi aliweza kuwasiliana na Park Jonghyun na kumuelezea kuwa Yezi alikuwa tayari kufika Korea kuungana na familia yake na jambo hilo lilipokewa kwa shangwe mno , Park Jonghyun aliweza kuomba taratibu za vidhibiri kuandaliwa kwa ajili ya Yezi.

Siku chache mbele hatimae Yezi alifuatwa na Park Jonghyun na kuaga familia ya Roma na Edna kwa ajili ya kuelekea nchini Korea , Yezi alionekana kuwa na huzuni wakati wakuondoka ,ilikuwa ni kama hatorudi , lakini Edna na Roma walimtoa hofu kwamba watakuja huko kumtembelea muda si mrefu na asiwe na wasiwasi na kama angetaka kurudi Tanzania kuendelea na chuo basi anakaribishwa.

Siku ya maagano hayo hata Mama Issa alilala nyumbani kwa Roma kwa ajili ya kumuaga mtoto wake huyo aliemlea kwa mapenzi ya dhati na hata kuweza kukutana na bwana Park Jonghyun.

Upande wa Roma mara baada ya kumalizana na swala la Yezi mawazo yake yalihamia kwenye swala ambalo aliambiwa na Zenzhei , swala ambao lilikuwa likihusisha tatizo la yeye kutoweza kupata mtoto kama tu mmoja ya wanawake wake hawatokuwa na uwezo wa mafunzo ya kijini angalau kwa levo ya Nafsi.

Roma mara baada ya kufikira kwa kina aliona jambo pekee ambalo anaweza kutatua changamoto hio ni kumfundisha Rose namna ya kutumia nguvu za kijini, aliamua kuanza na Rose kutokana na kwamba alimuona alikuwa na mwili uliokuwa vizuri kujifunza kuliko wanawake wake wote , hivyo akaamini kama Rose ataanza kujifunza ni rahisi kwa yeye kupanda levo.

Baada ya kufikiria swala lake alifanya safari ya Kwenda Kimara kwa ajili ya kumshawishi Rose juu ya jambo hilo ili aone kama anaweza kukubaliana nae na kujifunza mbinu hizo.

Rose na Dorisi walikuwa washaanza kuishi pamoja na Rose Club B alikuwa akienda mara moja moja , kwani biashara zake alikuwa akizifanyia Ubungo na zile za madawa alimwachia Zonga kuendeleza

Muda Roma alioweza kufika nyumbani kwa Rose ulikuwa ni wa jioni hivyo hata Dorisi alikuwepo, Roma mara baada ya kucheza na wanawake wake hao kwa kuwajumlisha pamoja na kufanya nao mapenzi ndipo alipoweka swala lake mezani bila ya kumbagua Dorisi.

Roma alielezea kwa ufupi kuhusu nguvu za kijini ambazo alikuwa akijifunza na mpaka anakuja kumaliza sio kwa Rose tu lakini kwa Dorisi pia alikuwa na mchecheto wa hali ya juu, kilichowafanya kufurahia Zaidi ni mara baada ya Roma kugusia kwamba kama watafanikiwa kupanda levo basi kuna uwezekano kuishi muda mrefu pasipo ya kuzeeka na Dorisi mara baada ya kusikia mbinu za kijini zilikuwa zikimfanya mtu kuwa na uwezo wa kuishi miaka mingi pasipo ya kuzeeka hakutaka kuwa nyuma kujifunza.

Ni tabia ya mwanamke kuogopa sura yake kujikunja kutokana na umri na kama utamwelezea kuna dawa ya ya kuufanya mwonekano wake wa kirembo kuwa wa muda mrefu , basi atafanya kila namna kuhakikisha anatimiza masharti yote ili kupata dawa hio, alichoeleza Roma kilimwamsha Dorisi na kutaka na yeye kujifunza.

“Babe hata mimi nipo tayari kujifunza”Aliongea Dorisi mara baada ya Roma kutoa pendekezo kama Rose angetaka kujifunza.

Kutokana na Rose kuwa na ndoto ya kumzalia Roma toka muda mrefu na aliyoweza kusikia juu ya swala hilo alikubali mara moja , lakini sio Rose tu ambaye alikuwa akitaka kumzalia Roma hata Dorisi pia alikuwa akitaka kumzalia Roma hivyo na yeye alitaka ajumuishwe kwenye kufundishwa mbinu za kijini ukiachilia mbali kubeba ujauzito alikuwa akiamini angekwenda kuwa mrembo pasipo kuzeeka kwa muda mrefu kama tu angefikia levo za juu za kijini.

Na Roma mara baada ya kuona hata Dorisi anataka kujaribu hakuona haja ya kumkatalia na Zaidi sana aliweza kufurahi , jambo hilo la Dorisi lilimrfanya Roma kufikiria tena , alijiambia kama wanawake wake wengine wanaweza kukubali kufundishwa basi anaweza kuwafundisha pia, ijapokuwa aliamini ingeweza kuchukua muda mrefu , lakini kama watakuwa makini na maelekezo yake basi wangeweza kupanda levo kwa haraka.

Mahusiano yake na Edna hayakuwa mazuri sana , Edna alionekana kutokuwa mchangamfu sana na Roma lakini licha ya hivyo haikumfahya Edna kutotii majukumu yake , siku zote angerudi mapema kutoka kazini licha ya mambo mengi yaliokuwa yakiendelea na angefanya baadhi ya kazi za nyumbani kwa kusaidiana na wanafamilia wenzake.

Tokea Edna amtumie ujumbe The Protector hakukuwa na majibu ya kurudishwa kwa ujumbe , jambo ambalo pia lilimfanya kuona kama Raisi Jeremy alikuwa akimpotezea , ijapokuwa hakuwa na uhakika kwamba barua pepe hio ilikuwa ya Raisi Jeremy , lakini kuna hisia zilimwambia lazima atakuwa tu yeye , sasa mwenyewe alishindwa kuelewa ni kipi ambacho alitegemea kutoka kwa The Protector , lakini ndio hivyo hakukuwa na majibu lakini wahenga wanasema damu ni nzito kuliko maji , huenda anachokifanya ni kile kinachoendana na msemo huo ukizingatia pia Edna hakuwa na ndugu mwingine wa kufanana kwa damu.

Naam zikawa zimetimia siku kumi na tatu kamili siku ya tarehe ishirini na tano ya mwezi wa kumi na mbili ikiwa ni siku kama nne tu tokea Yezi kuelekea Korea Kusini ,Roma alitambulishwa rasmi kwa ukoo nzima na ndugu wote wa Afande Kweka.

Familia ya Afande Kweka ilikuwa ni familia kubwa mno tofauti na Roma alivyotegemea, ukiachana na Watoto wawili wa Afande Kweka yaani Senga na dada yake lakini kulikuwa na Watoto wengine upande wa marehemu mke wa Afande Kweka , lakini pia kulikuwa na ndugu wa Afande Kweka ambao wote walikuwa na muunganiko wa moja kwa moja na ukoo huo.

Kulikuwepo na vitukuu na wajukuu wakubwa tu ambao kuna waliokuwa ni wanajeshi wenye vyeo jeshini na kuna wale ambao pia walikuwa ni viongozi ndani ya serikali wakiwa kama wanasiasa ukiachana na Raisi Senga, lakini ukiachana na hiyo kuna ambao pia walikuwa nje ya nchi.

Jambo hili lilimfanya Roma kuelewa kwanini Afande Kweka alikuwa akiogopwa nchini kumbe ilionekana alikuwa na mizizi ndani ya taifa la Tanzania.

Raisi Senga , Damasi , Ashley, Denisi wote walikuwepo siku hio , Raisi Senga licha ya kufika hakukaa sana muda mrefu kwa visingizio kwamba alikuwa na majukumu mengi ya kiserikali na Afande Kweka hakumzuia kuondoka , alijitahidi kumfanya kumkubali Roma kama mwanae kutokana na kurudi kwenye familia , lakini Raisi Senga alionekana kuwa na msimamo wake uleule na pia hakupendezwa na mpango wa baba yake kutaka kumpa Roma uongozi wa ukoo wa kusimamia mali na ‘Legacy’ ya familia , hivyo waliishia kutokuelewana na akaondoka.

Roma mwenyewe licha ya uwepo wa baba yake hakujihangfaisha kabisa hata kuongea nae , alikuwa akimjua hakuwa akimpenda hivyo hakutaka pia kulazimisha kupendwa, kwanza alifikia umri huo pasipo ya kuwa na baba , hivyo sio kama alikuwa akimuhitaji sana.

Edna ambaye hakuwahi kuijua vizuri familia ya Afande Kweka licha ya kuisikia juu juu , aligundua ilikuwa ni familia kubwa sana yenye ndugu wengi , jambo ambalo hata yeye mwenyewe alitamani kuona angekuwa na familia yenye ndugu wengi namna hio , ambao angalau kwa mwaka wanakusanyika pamoja na kufahamiana.

Ndugu hao walimpa Edna heshima yake kutokana na umaarufu wake katika maswala ya kibiashara na kuwa Tajiri mkubwa na wengi wao walijiuliza ilikuwaje mwanamke mrembo na Tajiri akaja kuolewa na mwanaume kama Roma.

Ijapokuwa wanandugu wengi walimfahamu Roma , lakini kuna wale ambao hawakumpenda kabisa hasa baada ya kuona kwamba Mzee Kweka anataka kumrithisha mwana huyo mpotevu mali za familia na kuziongoza, jambo hilo walionekana kutoliafiki kwani wao ndio waliokuwa wakipambana kufanya jina la Kweka kuwa juu ndani ya taifa la Tanzania , hivyo hawakutaka mtu ambaye hakuwa na mchango wowote kwenye familia hio kupewa uongozi wa juu na urithi wa familia.

Wengi wao walimchukulia Roma kama masikini ambaye alikuwa akitegemea hata chakula kutoka kwa mke wake lakini Roma licha ya kuangaliwa na dharau na kejeli kama kawaida yake alionekana kutojali kabisa na hakuwa na haja ya kuwaonyesha ni kipi anamiliki wala ni heshima gani amejitengenezea huko duniani.

Lanlan pia alikuwepo akiwa amesindikizwa na mbwa wake ambaye aliamua kumpatia jina lake na alikuwa kama kivutio kwenye kusanyiko hilo la kifamilia siku hio , kutokana na uchangamfu wake , lakini kuwa na akili ya kiutu uzima lakini pia wanafamilia hao kushangazwa na uwezo wake wa kula.

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , asubuhi siku hio Edna alikuwa ashajiandaa Kwenda kazini na alikuwa amejumuika na wanafamilia wengine wakiwa mezani kwa ajili ya kifungua kinywa na kwa upande wa Roma licha ya kwamba alikuwa hajajiandaa lakini pia alikuwa na mpango wa Kwenda kazini , lakini kubwa Zaidi kuna mtu pia alipanga kuonana nae siku hio.

“Roma uko free usiku wa leo?”Aliuliza Edna baada ya kumaliza kunywa chai akiwa wa kwanza kwa ajili ya kuondoka kuelekea kazini, kutokana na vita baridi aliokuwa akiiendeleza Edna , alishangazwa na kuylizwa na mke wake swali hilo.

“Niko free mke wangu , unataka Kwenda matembezi na mimi , niko tayari hata Kwenda visiwa vya Maldives ilimradi tu niwe na wewe”Aliropoka Roma pasipo ya kujali kama kuna watu waliokuwa kwenye meza na hata yeye mwenyewe alivyoona aliongea kwa kurupuka alijikuta akijizuia kuendelea maana alivyomwangalia mama yake alimuona akiwa ametabasamu ni vile tu Qiang Xi hakuwa akielewa Kiswahili , huenda ndio ambaye hakumshangaa Roma.

“Leo usiku Richie na mke wake wamenialika kwenye kusanyiko linalojumuisha baadhi ya marafiki zetu ambao tumesoma nao Chuoni , wengi wao ni wageni na wamefika Tanzania muda kidogo kwa ajili ya mapumziko hivyo walipenda kukamilisha matembezi yao kukusanyika pamoja”Aliongea Edna.

“Wow! Nilijua haya mambo yapo mataifa ya nje kumbe hata hapa kuna aina hio ya utaratibu , Mke wangu huna haja ya kuwa na wasiwasi nitavaa nipendeze leo”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu lake.

“Ni kweli huo utamaduni huku hakuna , lakini usisahau Edna kasomea nje ya nchi na marafiki zake ni wa nje vilevile ”Aliongea Blandina na Roma aliona ni kweli.

“Sister Edna nitamsaidia Bro kuhakikisha anapendeza”.

“Asante Sophia kwa kujali , lakini najua mwenywe nivae vipi ili mke wangu kuniona nimependeza ”Aliongea Roma huku akimkonyeza Edna na kumfanya Sophia kuvuta mdomo na kumfanya Blandina kucheka, hakuamini waroro hao kukosa aibu na kuongea kwa uhuru mbele yake na Bi Wema.

“Edna kwanini usirudi na mkaondoka wote na kuhakikisha mumeo kavaa vile unavyotaka aonekane mbele ya marafiki zako?”.

“Kuna kazi nitafanya nahisi inaweza kunichelewesha kurudi mapema”Aliongea Edna.

Ni kweli tokea malighafi mpya kuingia sokoni rasmi kazi ni kama zilikuwa zimemuongezekea ofisini , ijapokua siku hio ilikuwa ni ya pili ya Christmasi lakini aliihitaji Kwenda kazini kuweka mambo sawa.

Baada ya madakika kadhaa ya kuondoka kwa Edna ,Roma aliweza kupokea simu kutoka kwa Omari Tozo ili wapate kuonana na Roma alimwambia afike ofisni kwake na Omari alionekama kukbali ojapokuwa hakujau ni kwa namna gani Omari akaweza kupata namba yake ya sim u lakini hakujihangaisha sana kuuliza.
 
SEHEMU YA 412.

Omari mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ya Roma alishangazwa na uwepo wa mwanamke mrembo kama Amina, Omari kutokana na kutofatilia sana mambo mengi hakuwa akimjua Amina, kwa namna mrembo huyo alivyokuwa akimwangalia Roma alijua lazima kungekuwepo na mahusiano , hata hivyo alikuwa akisikia Habari za Roma kuwa na wanawake wengi , jambo ambalo lilimshangaza na kujiuliza yeye kafanikiwa vipi , kwani yeye mpaka muda huo alikuwa akihangaishana na Queen ambaye ni mjamzito na hakuwa akimtaka licha ya kwamba alikuwa akitaka kumuoa na mimba yake.

Roma wala hakujali Zaidi ya kutabasamu na Omari alichukulia hilo kama jibu.

“Hades ni mbinu gani unatumia kuwapata hawa warembo mbona mimi wananikataa”

“Umeanza lini kujilinganisha na mimi?”Aliuliza Roma na kumfanya Omari kucheka.

“Sitaki kujilinganisha na wewe , hata hivyo wewe ni mfalme Pluto ni haki kwako kupendwa na warembo sifa yako inakutangulia pasipo ya kutambulishwa”Aliongea Omari huku akiendelea kumwangalia Roma , ukweli alikuwa akimuona kuwa na mabadiliko makubwa tokea mara ya mwisho walivyoachana.

“Hades kabla hatujaendelea nataka uniambie imekuwaje sioni uwezo wako wa kijini tena , mara ya mwisho nilikuacha ukiwa katika levo ya mzunguko kamili , na kama nitasahihisha kauli yangu naweza kusema nilikusaidia kufikia levo ya mzunguko kamili?”

“Nishavuka hio levo na sasa nipo ya juu Zaidi, Levo ya kuipita Dhiki”Aliongea Roma na kumfanya Omari kushangaa na kusimama , akiwa kama haamini.

“Unadanganya, haiwezekani?”

“Hahaha,.. hata mimi najua haiwezekani , lakini ndio hivyo nipo levo ya kuipita Dhiki na huwezi kuniletea upinzani tena”Aliongea

“Kama ni kweli upo Levo ya kuipita Dhiki kwanini siwezi kuona uwezo wako wa kijini ndani yako na kugundua levo uliopo?”

“Hio ndio sababu kati yangu na nyie , mimi nilianza kujifunza mbinu za kijini za njia ndefu”

“Unamaanish ya Maandiko ya Urejesho?”Aliuliza kwa mshangao na Roma alitingisha kichwa na kumfanya Omari kuduwaa mno , alijiambia kama ni hivyo si atakuwa sawa na wale Grand Master waliopo kwenye vitabu vya historia huko ujinini, alijiambia kama ni kweli basi Roma hakuwa mtu wa kawaida kabisa na sio kwake tu lakini mpaka kwa viumbe wasioonokena.

“Nilikuja nyumbani kwako wiki kadhaa zilizopita , nadhani mkeo hajakuambia kama nilifika?”Aliongea Omari na Roma alimwambia hajui.

“Ndio niliweza kupata namba yako ya simu kupitia mkeo mrembo Edna”

“Edna ndio kakupa namba yangu? Hajaniambia kuhusu swala hilo”

“Ndio , kilichonileta nyumbani kwako ni kutaka kuhakiki kile kilichotokea kwa Meli ya kivita ya Marekani kulipuliwa , kwani jeshi letu lilipokea malalamiko kutoka taifa la Marekani walionyesha hofu yao juu ya ushirikiano wetu wa karibu na taifa la China”Aliongea na kumfanya Roma kumeza mare kidogo.

“Wewe unahisi ndio niliehusika na kushambuliwa kwa meli ya kimarekani ya kivita?”

“Jeshi letu limethibitisha hauhusiki na hata kilichonileta nyumbani ilikuwa ni kuthibitisha Alibi yako na tumeweza kutoa ushirikiano wa kutosha na Serikali ya kimarekani na swala limemalizwa juu juu , lakini hata hivyo halijafika mwisho”

“Unazungumzia kuhusu mtu aliegizia sura yangu?”Aliuliza Roma na Omari alitingisha kichwa.

“Nafasi yako katika ulinzi wa taifa ni ipi, ijapokuwa nakufahamu kama una mafunzo ya kijini , lakini sijakufahamu vizuri”

“Hahaha.. Hades inaonekana haupo siriasi , inamaana umeshindwa hata kutafuta kuhusu taarifa zangu?”

“Niliona hazina umuhimu , kwanza kwanini nizitafute kama wewe mwenyewe unaweza kuniambia , au yale maneno yako siku ile yalikuwa hewa , ukitaka tuwe marafiki lazima uniweke wazi nafasi yako hapa nchini , nione kama una faida au hauna faida”

“Na kama sina faida?”

“Ni bora niendeleze urafiki na warembo wangu”

“Hahaha… , naweza kukuelezea lakini vipi kuhusu wewe , unaweza kuniambia kila kitu”

“Kuna utofauti mkubwa kati yetu”Aliongea Roma na kumfanya Omari kuona kuna ukweli , hata hivyo hakuna siku ambayo aliamini angekuja kuongea na Hades ana kwa ana namna hio , ilikuwa bahati kwake mara baada ya kusikia Hades yupo Tanzania.

Ilibidi ili maongezi yaendelee Omari ajitambuliesha vizuri kwa Roma juu ya nafasi yake ndani ya serikali ya ulinzi ya Tanzania na mpaka anamaliza Roma aliweza kufahamu Omari alikuwa ni mtoto wa CDF wa majeshi ya Tanzania bwana Gambino Tozo na akiwa kama mtoto wa kwanza na wa mwisho wa kiume ndani ya familia hio lakini pia kilichomfurahisha ni kwamba Omari alikuwa akifanya kazi chini ya kitengo cha usalama wa taifa.

“Sio mbaya kuwa na urafiki wa mtoto wa mkuu wa majeshi , tokea nifike hapa nchini sijapata rafiki lakini bado nakuona hunifai maana umezidi ubahiri , inakuwaje mtoto wa CDF unaendesha kirikuu?”Aliuliza Roma kwa kebehi huku akijisahaulisha hata yeye alivyokuja Tanzani alikuwa akibeba mizigo.

“Mzee hanipi hela yoyote ya matumzi na ndio kwanza nimerudi Tanzania , kutembelea kirikuu ni kubana matumizi maana muda si mrefu nataka nioe”.

“Nielezee sasa kwanini ukataka kuonana na mimi?”Aliongea Roma akipotezea sababu za Omari zisizokuwa na mashiko.

“Kilichonileta ni kutaka kupata jibu kutoka kwako , nipo nafanya uchunguzi binafsi”

“Uchunguzi gani?”.

“Kuhusu Profesa Yan Buwen”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa kidogo

“Naona unaonekana kumfahammu ?, ndio ninaemfanyia uchunguzi binafsi kwa sasa na ndio kazi za aina mbili zilizonirudisha hapa Tanzania”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo alikuwa akikumbuka kuhusu Yan Buwen kuhusika na kifo cha Profesa Shelukindo , lakini kitendo cha wanajeshi wake kutowaruhusu kuendelea kufanya uchunguzi Zaidi alikuwa na maana yake.

“Hades labda haufahamu hili , unadhani kwasababu gani nimeweza kujifunza mbinu za kijini na kufikia levo ya Nafsi na kuja uraiani?, Katika kanuni za Hongmeng binadamu yoyote aliebahatika kujifunza mbinu za kijini na kufikisha levo ya Nafsi haruhusiwi kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida”.

“Kwahio kutoka kwako Hongmeng ni kutokana na maagizo ya kumfuarilia Yan Buwen?”Aliongea Roma na kumfanya Omari kutabasamu.

“Una uwezo mkubwa sana Hades wa kuelewa mambo, labda kwa kitu ambacho haukifahamu ndani ya taifa la China , kuna mgogoro kati ya Serikali pamoja na Hongmeng”

“Unataka kumaanisha nini?”

“Hongmeng hawaungwi mkono kwa asilimia mia moja na familia zote kubwa ndani ya China na wanatafuta mbinu kuondoa Koneksheni iliopo na Serikali kujitegemea kwa asilimia mia moja”Aliongea Omari na kumfanya Roma kuguna.

“Hilo nililitegemea , licha ya kwamba sina sana uelewa na jamii hizi za Hongmeng , lakini hili linahusiana vipi na Yan Buwen?”

“Kwasasa siwezi kujibu hili swali mpaka uchunguzi ukamilike lakini Afande Yang kutoka China ambaye ni mkuu wa majeshi ya Ardhini ni moja ya familia ambayo haikubaliani na jamii za siri kuingilia maswala ya kiserikali na wasiwasi wa Hongmeng ni Afande Yang kushirikiana na Athena”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa, ijapokuwa mwenyewe alikuwa akiijua nguvu ya Athena ndani ya dunia kwa kufahamika kama The Doni lakini hakuwahi kuwaza sana ushwishi wa Athena ndani ya serikali ya China.

“Unamaanisha kuna uwezekano wa Afande Yang kushirikiana na Athena? , hili ni jipya kwangu na sijawahi kulifikiria hapo kabla, lakini hata hivyo kwanini liwe na muingiliano na Yan Buwen?”

“Yan Buwen ni mwanasayansi na mbinu pekee ambazo Familia yote ya ukoo wa Yang unachoamini ni katika sayansi , wanaamini sayansi inaweza kuwaweka kwenye nafasi ambayo Hongmeng haiwezi kuingilia maswala ya serikali , mathalani katika jeshi ndio maana inawapa wasiwasi Hongmeng na kuona Athena anaweza katumia udhaifu wa mgogoro uliopo kupindua ushawishi wao katika ulimwengu wa kawaida , mathalani ndani ya serikali ya China , nguvu ambayo waliweza kuidumisha kwa miaka mingi”Aliongea na kumfanya Roma kuona huenda hilo likawezekana.

“Wewe uko upande upi?”

“Nimeweza kupata nafasi ya kuishi katika ulimwengu wa kawaida licha ya kuwa na levo ya Nafsi ya mafunzo ya kijini kutokana na kuahidi nitafanya uchunguzi ya kile kinachoendelea na kazi niliopewa ni kumfuatilia Yan Buwen , kuhusu Hongmeng kuendelea na utawala wao wa siri ndani ya Serikali ya China , hili ni jambo ambalo halina athari yoyote kwangu hata hivyo mimi ni mtanzania”Aliongea.

“Mtanzania ambaye ni shushu wa Hongmeng naweza kusema hivyo”

“Unaweza kuniita hivyo, mwanzoni nilivyoanza kujifunza mbinu za kijini niliwaza jambo moja tu , kuponyesha jicho langu na mwanamke ninaempenda kuniona wa kawaida na kunipenda , lakini mara baada ya kupanda levo na kufikia ya Nafsi na kutimiza haja zangu uhitaji wa kuwa na mwanamke wa ndoto yangu ulirudi upya lakini sheria zinanibana, hivyo naamini mimi na wewe hatuna utofauti sana , naamini upo tayari kufanya lolote kwa jina la Mapenzi”

“Unachoongea ni sahihi ninaweza kufanya chochote kama mtu wangu yoyote wa karibu kama ataguswa , hata kama ni kupindua miliki zote za kijini”Aliongea Roma na kumfanya Omari kucheka sana.

“Inaonekana sisi tunafanana sana Roma?”

“Hapo kwenye kufanana usiniingize kuna mambo unayafanya mimi siwezi kuyafanya , kwanza mimi sio mbahiri , ninavyokuona huna aibu mimi mwenzio nina aibu , nina wanawake wengi na wewe unaonekana unahaingaika kwa mwanamke mmoja…”Aliongea Roma na kumchekesha sana Omari.

“Haina haja ya kuendelea sijamaanisha tunafanana kwa asilimia mia , ila kuna vitu vinatufanya tufanane”Aliongea

“Niambie kwanza kwanini ukaamua kunielezea maswala ya Hongmeng ?”

“Kwasababu wewe ndio unajua Zaidi kuhusu kanuni za Anga lakini pia Afande Yang alionekana kutembelea Tanzania hivi karibuni , kwa taarifa nilizonazo jambo hili nimeamua kulifanya kimya na hata kuacha kuhusisha familia yangu, swali langu kwako ni je kuna namna unavyohisia mtu alieigiza kuwa wewe?”

“Nina maadui wengi na jambo la kufurahisha maadui zangu hawajawahi kukaa chini na kutulia ni wenye kusubiria nafasi ili kunichokoza , mtu ambaye ameigiza kuwa mimi sina haja ya kumtafuta ,mpango wake ulikuwa ni kunichokoza na naamini bado hajatimiza malengo yake na atarudi tena , kuhusu yeye kufanana na mimi hilo halinipi shida sana”Aliongea na kumfanya Omari kukuna kichwa.

Omari na Roma waliongea kwa muda mrefu mpaka ilipofikia muda wa chakula cha mchana Omari aliondoka.

********

Muda wa jioni Roma aliweza kuendesha gari aina ya Rolly Royce mpaka kwenye kampuni ya Vexto kwa ajili ya kumchukua Edna kuelekea kwenye kusanyiko la marafiki wa chuo,, kwasababu alikuwa washawasiliana ni ndani ya dakika mbili tu Edna alievaa akapendeza alitokea eneo la maegesho ya gari na kumfanya hata Roma mwenyewe kushangaa kidogo , ijapokuwa aliamini Edna asingevaa mavazi aliotoka nayo nyumbani lakini hakutarajia angeweza kupendeza kwa kiasi hicho.

Roma alimfungulia mke wake mlango huku akiwa amepambwa na tabasamu na kwa upande wa Edna alionekana kuridhika na namna ambavyo Roma amevaa na kuweka sawa nywele zake , ilionekana Roma siku hio kabla ya kurudi nyumbani alienda saluni.

Ni ndani ya dakika chache tu Roma aliweza kuingiza gari kwenye lango la hoteli ya Hyatt Kilimanjaro iliokuwa pembezoni mwa bahari , mwanga wa hoteli hio usiku ulifanya eneo lote kupendeza.

Baada ya wote kushuka kwenye gari Roma hakuwa na haja ya kulipeleka maegeshoni bali alimpatia mtu wa kazi hio ufunguo na kisha alimsogelea mke wake mrembo Edna na kisha kumpa ishara ya kushikilia mkono wake.

Edna hakusita sana kwani haikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo,

This is far as you go , Don’t test your luck”Aliongea Edna akimpa onyo Roma kwamba asijaribu kupeleka mkono wake sehemu zingine za mwili, Edna alionekana kuwa siriasi mara baada ya Roma kumvuruga,

“I am your to command”Alijibu Roma huku akitabasamu lakini kabla hawajaanza kupiga hatua kuelekea ndani iliingia gari nyingine eneo hilo na Kwenda kusimama mbele yao.

Ilikuwa gari zuri kweli ya kifahari kampuni ya BMW Sport Car ambayo ni machache sana kuyaona Tanzania.

Baada ya gari hio kusimama alishuka mwanaume mmoja wa kizungu kijana alievalia suti nyeusi kampuni ya ‘Armani ‘ huku akiwa na miwani nzuri ya macho ilionakshiwa na madini ya dhahabu , alikuwa amependeza haswa kwa mwonekano wake na ilimfanya kuonekana wa kuvutia mno, kitendo cha mwanaume yule kushuka kilimfanya Edna kumsogelea Roma karibu zaidi kuliko isivyokuwa kawaida.

Upande mwingine wa mlango ulifunguliwa na akatokea mwanamke mwingine wa kizungu pia alievalia Earings kubwa na gauni lake la maua mua ambalo linavikamba vilivyoshikilia mabegani ambalo lilifanya umbo lake kuonekana vyema , ijapokuwa hakuwa na mwili mkubwa lakini alionekana kupendeza sana.

“Edna Long time no see”Aliongea yule mwanaume kwa kingereza akimaanisha kwamba hawajaonana muda mrefu na Edna alimwangalia mwanaume huyo aliekuwa mbele yake na kisha macho yake yakageukia upande wa mwanaumke mrembo alieambatana nae.

“Not Long enough”Alijibu Edna akisema sio kitambo sana.

“Glad to see you’re still the same old stone -Cold Edna”

“Nimefurahi kukuona ukiwa Edna yule yule kauzu”Aliongea yule mwanamke huku akishika shika nywele zake kwa mapozi , lakini Edna hakujali kuendelea kuongea nao Zaidi ya kumpa ishara ya Roma kuendelea na safari yao kuingia ndani ya hoteli hio

Jambo hilo lilimfanya Roma kushangaa kwani Edna alionekana kutokuwa na muda wa kuwatambulisha watu hao kwake, wanaume wale walifuatishana na Edna na Roma kiupande upande.

“Edna kwanini usinitambulishe mume wako , nimesikia kutoka kwa Richie umeolewa , sikushawishika mwanzoni lakini nadhani ni kweli”Aliongea na kumfanya Edna kusimama na kisha kumwangalia yule mwanaume.

“You think you are only ones who can get married?”

“Mnafikiri nyie ndio mnaweza kufunga ndoa tu?”

“Edna nafikiri sio alichokimaanisha , wote hakuna alietarajia mwanamke kauzu wa chuo kama wewe unaweza kupata mwanaume hivi karibuni na kufunga ndoa, kama marafiki zao tunazo kila sababu za kujua maendeleo yako”Aliongea yule bidada wa kizungu na kisha akamgeukia Roma.

“Naamini huyu ndio mume wako Edna, Mr Roma kwa jina naitwa Hanson nilikuwa chuo kimoja na mkeo , huyu hapa ni mke wangu anafahamika kwa jina la Cindy hata yeye alikuwa darasa moja na kozi moja na Edna”Aliongea bwana Hanson lakini Edna alionekana hakutaka Roma aongee nao licha ya kutojua imekuwaje Hansoni kuweza kufahamu jina mume wake.

“Kwasababu mnafahamina wote , mnaonaje tukiingia sasa ndani?”Aliuliza Edna na akampa ishara Roma ya kufuatishana nae Kwenda ndani pasipo kuwajali.

Baada ya kuwaona wameingia ndani Cindy alimwangalia Hansoni usoni na kisha akatoa tabasamu la kejeli.

“Babe you miss that woman , don’t you?”

“Babe unammisi yule mwanamke si ndio?”

“She is even prettier than she was back in college , A beuty that has only grown , how can I not miss that?”

“Amekuwa mrembo kuliko alivyokuwa chuo , kwa uzuri ule uliongezeka kwanini nisimkumbuke?”

“Hanson huoni kwamba unavyomsifia mbele yangu nitapata wivu?”

“Hahaha,, kipindi kile aliponikataa kule chuoni , sikuweza kumzingatia tena , Mwanamke yoyote ambaye anauwezo wa kunikataa mimi no matter her beuty is nothing but a pitfull insect”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli la kuonyesha kutojali.

“Edna nini kinaendelea mbona unaonekana kuwakwepa?”Aliuliza Roma wakati wakiingia kwenyeLift.

“Hanson alikuwa ni rafiki yake Richie na mwanadarasa mwenzake kipindi ambacho nilikuwa nikisomea Masters , Cindy yeye tulikuwa darasa moja”

“Sio mbaya , Hanson sasa hivi anajihusiaha na nini?”

“Hanson ni moja ya familia kubwa sana ndani ya Norway na wanamiliki makampuni yanayojihusisha na maswala ya mabenki sio maarufu sana kwani mabenki yao yapo ndani ya bara la ulaya pekee , baada ya kumaliza masomo niliweza kufahamu familia yao pia wanamiliki baadhi ya viwanda vikubwa vya utengenezaji wa magari makubwa lakini pia ni moja ya wamiliki wa hisa kwenye kampuni ya Fyatt ya kiitaliano, kuhusu Cindy yeye ni Mwafrika kutoka South Afrika lakini familia yao yote Maisha yao yapo Uingereza, Mama yake anafanya kazi kwenye shirika la kimataifa la IMF”Aliongea Edna kwa kirefu

“Mh ndio maana wamekuja kwenye gari kali , inaonekana ni wazito huko duniani”Aliongea Roma.

“Upo sahihi labda tu ni kwasababu sijakutambulisha vizuri kwa Richie lakini hata yeye usimchukulie wa kawaida kwasababu ameamua kuja kufanya kzi kwenye kampuni yangu, Richie hakuwa akisomea kama mwanamitindo Oxford , yeye alikuwa akichukua maswala ya Banking and Finance na maswala ya mitindo ni kama fani tu anayopenda nje ya taaluma yake , wakati napendekeza aje kunisaidia Tanzania alikuwa amepata ofa ya Kwenda kufanya kazi ndani ya kampuni ya Kimarekani ya JP Morgan lakini Richie hakupenda kazi za kukalishwa chini , hata hivyo ukiachana kuwa marafiki zangu lakini pia alikuwa akipenda mazingira ya Tanzania ndio maana alikubali nilipopendekeza aje kunisaidia , ni rafiki mkubwa sana wa Hanson”.

“Hehe .. Babe kwa maelezo yako nadhani sisi tunaweza kuwa masikini kati ya wageni wote wa Richie?”Aliongea Roma kwa utani, lakini Edna alionekana kutopenda lakini alipotezea.

“Unachoongea ni sahihi , ijapokuwa nimeweza kuipaisha Vexto kimataifa lakini watu kama Hanson siwezi kujilinganisha nao , utajiri wa familia zao hakuanza juzi ni watu waliojikita kibiashara tokea zamani”

“Wakati ndio naanza masomo yangu nchini Uingereza bibi alinilazimisha kujihushisha na maswala yote yaliokuwa yakijumuisha familia za kitajiri zilizokuwa ndani ya chuo , hio yote ilikuwa ni kunifanya kupata ‘Exposre’ lakini pia kutegneneza koneksheni” Wakati Edna anamaliza kuongea lift ilifunguka juu kabisa na kuingia kwenye korido ambayo walichukua moja kwa moja mpaka eneo husika , mara baada tu ya kuingia kulikuwepo na watu wengi kidogo kuliko Roma alivyotarajia akiwemo Richie ambaye alikuwa na mke wake.

Ingekuwa Roma anafuatilia mambo mtandaoni angegundua uwepo wa meli ya kifahari iliokuwa ikitangazwa kutia nanga kwa kuleta matajiri kutarii ndani ya maeneo ya Dar es salaam na Zanzibar , wengi wao waliluwa ni hao waliokuwepo hapo ndani.

“Oh! !My beloved Edna you’re finally here So this is your husband Mr Roma I suppose ?”

“Oh Mpendwa wangu Edna , hatimae umefika , nadhani huyu ndio mume wako Mr Roma nadhani?”Walilakiwa na mwadada mwingine wa kizungu aliekuwa na macho ya bluu na lipsi zilizokuwa nyekundu mno kwa kupakwa marangi.
 
SEHEMU YA 413.

Edna mara nyingi hakuzoea sana kulakiwa namnahio , lakini alijitahidi kutoonyesha utofauti .

“Sasha welcome in Tanzania” Aliongea Edna kwa tabasamu huku akikumbatiana na mwanada huyo , alikuwa ndio mke wa Rich.

“Rich alivyoniambia ulimwalika wewe mwenyewe kuja kwenye kampuni yako ya Vexto niliamini ni Idea nzuri sana , alikuwa ni mwenye Maisha mabaya sana nyumbani , hivyo niliamini kuja Tanzania kungemchangamsha”Aliongea na kumfanya Edna kukumbuka mara ya mwisho wakati anapiga Stori na Rich. alisema alidhulumiwa na kampuni moja ya kimarekani.

“Nimefurahi sana pia baada ya Rich kunikubalia”Aliongea Edna na sasa Sasha alimgeukia Roma na kuanza kumkagua juu mpaka chini kama vile ujuavyo tabia za wanawake.

“Mr Roma what a man you must be , What magic do you posses to get Edna to marry you ? She is well known for her reclusiveness and discreet way of living?”

“Mr Roma wewe ni mwanaume wa namna gani?, Unamiliki uchawi gani mpaka kumfanya Edna kukubali kuolewa ?, Alikuwa akifahamika kwa kujitenga na kuwa Maisha ya kujificha ficha?”

“I gues its something that has happened between the two of us , I would tell you but I don’t think Edna is keen to that”

“Nadhani ni vitu vilivyotokea baina yetu , ningekuambia lakini sidhani kama Edna anaweza kukubali?”Aliongea Roma kwa kingereza safi.

“Oh! Hahaha… Mr Roma unaonekana kuwa mtu mzuri sana , hata hivyo sijawahi kumuona Edna akiwa na aibu namna hii”Aliongea na ni kweli Edna aliona aibu kwa maneno ya Roma kwani ni kama amekumbushia kile kilichowatokea mara ya kwanza walivyokutana kule Mbagara , Edna aliishia kujibana kwa Roma na kisha akapitisha ukucha na kumfinya.

Muda huo huo alionekana wenza wawili wakiwasogelea huku wakiwa na tabasamu kwenye nyuso zao , mwanamke alikuwa ni mwafrika aliekuwa na ukibonge kidogo ulioendana na sura yake ya duara , alikuwa amevalia mavazi ya kifasheni lakini yaliomkaa vyema , upande wa mwanaume alivalia kawaida lakini kwa namna ya kipekee huku akiwa na uso mpole sana , hata yeye alikuwa ni wa rangi nyeusi.

“Edna bado unanikumbuka?”Aliuliza yule mwanadada baada ya kuwafikia

“Miss Lele Nawezaje kukusahau?”Aliongea Edna kwa sauti ya ukarimu na Lele alimsogelea Edna na wakakumbatiana kwa furaha.

“Babe umeona sasa nilivyokuambia , niliamini Edna hawezi kutusahau”Aliongea Lele akimwangalia mwanaume wake aliemwita Babe. Na mwanaume yule mwuesi tii mwenye sura ya upole alitingisha kichwa kwa tabasamu.

“Nilikuwa natania kama utaweza kumkumbuka lakini inaonekana umemkumbuka Lele kweli”Aliongea huku akipena mkono na Edna.

“Wewe ni Abaiku si ndio? , nyie wawili mlifunga ndoa?”Aliuliza Edna

“Ndio sikudhania ungeuliza swali hilo , haikuwa rahisi kwetu kufikia kufunga ndoa”Alijjibu Abaiku, alikuwa ni raia kutoka Ghana na hata Lele vile vile na wote walisoma pamoja na Edna, Lele hakuwa na ukaribu sana na Edna wakati walivyokuwa chuo ,ijapokuwa Edna alikuwa kwenye muunganisho wa Watoto matajiri enzi alivyokuwa chuo lakini kutokana na umaarufu wake hakuweza kuwafahamu watu wote ndio maana Lele aliuliza kama anamkumbuka.

Watu walikuwa wengi na wengine hata Edna hakuwa akiwafahamu walionekana kuwa marafiki wa Richie na ilionekana ni kama kuna sherehe siku hio ndani ya ukumbi huo ambayo alieandaa ni Rich.

Kwa maelezo ya Edna Kwenda kwa Roma ni kwamba wote waliokuwepo humo ndani walikuwa na fani tofauti tofauti , ukiachana na wale Watoto wa matajiri lakini pia kulikuwa na wafanyakazi waliokuwa na heshima kubwa na walikuwa wakifahamiana , mtu ambaye alionekana kuwa mgeni ni Roma , kwani kwanza licha ya kuwa mume wa Edna lakini mabwana hao waliona Roma atakuwa anamtegemea Edna kwenye mambo mengi na hata hawakumzingatia sana.

Jambo hilo hata Edna hakulipenda na pia asingewaambia watu kuhusu ukubwa wake kwenye jamii , hakupenda walivyokuwa wakimuangalia kwa dharau , lakini hakuwa na hiari ya kuweka wazi kwani aliamini hakuna hata mmoja hapo ndani ambaye angemzidi Roma kwa pesa na koneksheni.

Upande wa Roma wala hakujali sana , kitu kikubwa mbacho alikuwa akitegemea kwa hamu zote ni aina ya misosi ambayo ingeandaliwa

“Kwanini simuoni Hanson na Cindy hapa , nakumbuka niliwaalika?”Aliongea Rich lakini muda huo huo mlango ulifunguliwa na wenza hao ambao walikutana na Roma na Edna njiani waliingia wakiwa na tabasamu kama lote , huku wakisalimina kila mtu aliekuwa karibu yao , walionekana kuwa maarufu na zaidi ya yote walionekana kushobokewa Zaidi.

“Samahani kwa kuchelewa kufika , kuna mfanyabiashara mmoja tulikuwa na mazungumzo nae ya muda mfupi”Aliongea Hanson

“Nadhani sio mbaya kwako ,hii Sherehe bwana Hanson ni kama ya kwako kutokana na umaarufu wako, Jamani wote hapa tunaelewa Hanson sio moja ya watu wa kawaida kati yetu”Aliongea jamaa mmoja kibonge ambaye alionekana kuwa Chawa wa waziwazi.

“Hahaha.. Asante sana lakini najulikana Zaidi ndani ya bara la Ulaya nadhani kwa hapa Tanzania mimi ni mgeni kama wengine, mfanyabiashara niliekuwa nikiongea nae ameomba kuja angalau kusalimia licha ya kwamba hajaalikwa”Aliongea akijifanyisha kuwa wa kawaida lakini ukweli alifurahishwa na kusifiwa kutoka kwa chawa wake.

“Hanson kwanini usituambie moja kwa moja Tajiri huyu ni nani kuliko kuzunguka?”Aliongea mmoja wapo lakini Hanson hakujali Zaidi ya kusogelea kiti chake na kisha kuketi pamoja na mke wake.

“Rich nadhani tutamjua mara baada ya kufika, mnaonaje tukianza”Aliongea na maneno yake yalichukuliwa vyema na Rich kwani alitoa maneno kidogo ya utani yaliowafanya wote kucheka na kisha chakula kiliandaliwa na wahudumu huku zogo likuwa la juu mno kutokana na wengi wao hapo ndani hawakuwa wamekutana muda mrefu , Wageni hao walionekana walikuwa wakimuongelesha sana Hanson kuliko wengine wote.

“Kwako Edna kwa kuwa mkarimu sana kiasi cha kuniachia Hanson na hatimae kuweza kufunga nae ndoa”Alisimama Cindy akiwa amenyoosha juu glass ya Wine akiwaaongelesha wengine wote, lakini kauli yake ilifanya kundi lote kumgeukia Edna.

Edna mwenyewe hakuwa kwenye mudi ya kuongea , alijikuta akisimama kivivu na kuinua Glass yake pia.

“I am sure this has nothing to do with me , Thank anyway”Aliongea Edna akimaanisha kwamba jambo hilo halina uhusiano wowote na yeye , lakini hata hivyo anashukuru na kisha pale pale alikunywa kidogo wine yake akiwa amesimama na kisha akaketi chini.

Upande wa Roma alionekana kama mtu ambaye hakupenda sana mazungumzo kwani yeye alikuwa bize na steki ya nyama aliokuwa akiikata mapande mapande na kupeleka mdomoni na kutafuna lakini ndani alimwonea huruma mke wake.

Hakupenda namna ambavyo Cindy alimwaibisha Edna hadharani maana aliyaona kama makusudi maana haikuwa na maana kusema hivyo akionyesha kama Edna alikuwa na mahusiano na Hanson

“Jamani hata mimi sikuwa na uhakika kama Edna angeweza kutoka kimapenzi na Hanson , nadhani baada ya Hanson kukataliwa ndio Cindy alipoweza kupata nafasi”Aliongea Lele.

“Sio mbaya nadhani yote yalipangwa , nadhani wote tunamwonea wivu Cindy kwa kuweza kumpata mwanaume kama Hanson”Aliongezea mwanamke mwingine ambaye alikuwa na asili ya kihindi.

“Jamani nashukuru kwa maoni yenu mazuri lakini nadhani yote hayo hayana maana , Edna na mimi hatukupangiwa kuwa wote na hata hivyo alikuwa akifuatwa na wanaume wengi wakati tupo chuoni , kunikataa kwake ndio kumenifanya kumpata Cindy, na kwasasa najitahidi kumpa mapenzi ya dhati kama mke”Aliongea Hanson.

“Wow! Hanson una maneno matamu sana kama mwanaume , mara ya mwisho nilivyompigia simu Cindy alinielezea uliweza kumzawadia jumba la kifahari kando kando ya bahari”

“Yeah ni kweli lakini wote tunajua pesa zipo kutumika , ni vyema kama mume anapofanya kazi na kuzipata kugawana na yule anaempenda”Alijibu Hanson na watu wote walionekana kuridhishwa na maneno yake na wa kuona wivu waliona.

“Well hakika naamini Edna na Mr Roma wanapendezana, ni mapenzi yalioje mume kufanya kazi katika kampuni ya mke wake , nina uhakika kafanya yote kutokana na mapenzi”Aliongea Cindy lakini maneno yake yalitafsirika kama ya uchokozi kwenda kwa Roma lakini hata hivyo baadhi yao walionekana kufarhi mno kwani walicheka .

“Babe ninapata matamanio ya kumvunja shingo yule mwanamke hata sijui kwanini”Aliongea Roma mara baada ya kumuinamia Edna aliekuwa ameweka mkono mmoja kwenye mkoba wake.

“Najua huogopi hata mmoja hapa lakini nadhani haina haja ya kupaniki na kuharibu hili tukio , ni utani mwingi tu hapa kutokana na mambo ya chuoni , naomba tuvumilie mpaka tufikie mwisho tuondoke”Aliongea Edna kwa kusihi.

“Nitafanya kama ulivyoongea , lakini akiongea ujinga tena sitamuacha salama”Aliongea na Edna aliitikia kwa kichwa.

“Abeiku nadhani tofauti na wote hapa wewe ndio mwenye uzoefu wa vitu vingi kutokana na fani yako ya kufanya minada kwenye matukio makubwa , mume wangu alishawahi kunizawadia zawadi nitataka utoa mawazo yako”Aliongea Cindy kwa sifa.

“Ni kweli lakini sio kwa kila kitu, asante sana kwa kutambua uwezo wangu lakini”Alijibu Abeiku mghana yule.

“Hakuna shida , kwa uwezo wako naamini huwezi kushindwa kufahamu ninachotaka kukuonyesha , Hanson amenipa zawadi lakini ni mwenye wasiwasi inaweza kuwa feki , nitataka uifanyie uthibitisho”Aliongea palepale na kisha akvuta mkoba wake na kisha kutoa kiboksi flani kidogo sana cha mraba rangi ya zambarau na kisha akamkabidhi Abeiku.

Baada ya Abeiku kupewa mkononi alikifungua kiboksi kile ndani na hapo hapo alijikuta akitoa macho , ilikuwa ni saa ya madini ya dhahabu yenye kung’aa mno ,ijapokuwa kuna waliokuwa mbali lakini waliweza kupenda sana uzuri wake.

“Wow! Saa nzuri sana , Abeiku upo kwenye fani yako ya kutambua saa”aliongea mpenzi wake Lele.

“My God could this be . a limited edition Vacheron Constantin ?”Aliongea huku akiwa na mshangao wa kutoamini..

“Najua saa za aina hizo zipo saba tu ndani ya dunia , Abeiku unaongea ukweli ni yenyewe?”Aliuliza mmoja wapo

“Hakika ndio yenyewe na kama sio yenyewe naamini Cindy asingenipatia kuithibitisha”Aliongea

“Ni kweli ni yenyewe , niliweza kuinunua kwa kushinda mnada Landon miezi mwili iliopita nililipia paundi milioni tatu , niliona ni zawadi nzuri sana kwa maazimisho ya miaka yetu mitatu tokea tufunge ndoa, nilisikia ni kweli zipo saba tu ambazo zimetengenezwa , Sio mbaya mtaalamu wetu tokea enzi za chuo kututhibitishia kwani hata mimi niliambiwa kuna feki nyingi”Aliongea Hanson

“Baada ya mume wangu kuinunua niliogopa hata kuivaa kwani niliona kama ni feki na ndio maana nilitembea nayo ikiwa kwenye kiboksi chake licha ya kwamba alilipa pesa nyingi”Aliongea Cindy lakini wote waliona ni aina ya wanawake ambao walikuwa wakitafuta kusifiwa hata hivyo haiwezekani mtu kulipia pesa zote hizo halafu mwisho wa siku saa iwe feki.

“Hakika ni ghali mno , unaweza kunnunua Boeng kwa gharama yake”Aliongea Lele huku akihema kwa tabu.

Upande wa Abaiku licha ya kwamba alikuwa mpole lakini tokea alivyokuwa chuo alikuwa akisifika kutolea maelezo ya vito vya thamani , alisomea kozi ya Gemmology and Jewellery ambayo ilikuwa ikimpa utaalamu wa kutambua vitu vingi sana duniani vya thamani vile vya miaka iliopita na vinavyotengenezwa kuanzia mpaka namna ya utengenezajia na kazi zake.

Hivyo aliitolea maelezo saa hio ya Vacheron kwa ufasaha kabisa , maelezo ambayo yaliridhisha mno na wanawake kutamani wangekuwa kwenye nafasi ya Cindy.

Hata hivyo mara nyingi nchi zilizoendelea wanafunzi waliosoma pamoja wakikutana ni kusifiana maendeleo yao , aidha kwa vitu wanavyomiliki au wanawake walio oa au kuolewa nao pamoja na nafasi zao katika jamii , ilikuwa ni kawaida sana kukuta watu kama Cindy wenye uhitaji wa kusifiwa.

Edna ambaye alitegemea hayo alijikuta akipatwa na wasiwasi , alijua kitendo cha Cindy kuweka saa hio hadharani alikuwa akimwandalia bomu ambalo ni lazima angemlenga mume wake kwa kutokuwa na uwezo wa kumpatia zawadi yenye thamani , Edna alijiambia ni bora ile siku Roma akampatia ile pete kuliko saa.

Roma aliekuwa pembeni ya mke wake aliona kabisa Edna alikuwa akimchukia kutokana na kinachoendelea ,

“Babe unaona wasomi wenzako walivyokuwa na msimsimko , je na wewe unatamani kushiriki?”Aliuliza Roma kwa kingereza na kwa sauati na kufanya watu wote kugeuza macho Kwenda kwa Roma, walijiambia mwajiriwa kama huyo ana kipi cha kushindana na saa ya bei mbaya kama Vacheron.

“Oh I suppose Mr Roma here has something to share too?”

“Oh naamini pia Mr Roma anakitu cha kuonyesha pia?”Aliongea Cindy huku akitoa kicheko cha kebehi , aliona hio ni nafasi ya kumdhalilisha Edna.

Sasa unaweza ukashangaa kwanini Cindy alikuwa akimchukia Edna ukweli ni kwamba wakati walivyokuwa chuoni . Cindy hakumpenda Edna kutokana na kwamba siku Edna alivyotua chuoni ni kama alikosa ule umaarufu aliokuwa nao kutokana na uzuri wa Edna na hata mwanaume anaempenda Hansoni alionekana kumtamani Edna huku akimpotezea yeye.

“Yeah , ijapokuwa sio jambo kubwa sana , lakini kuna saa ambayo nilimpatia mke wangu wiki kama moja iliopita , nadhani itakuwa vyema pia nikiwaonyesha”Aliongea Roma

Amejuaje nilikuwa nikitembea nayo kwenye mkoba wangu huyu na nimekuja nayo hapa?”Aliwaza Edna huku akisahau Roma alikuwa mchawi lakini hata hivyo siku zote aliichukulia saa hio kama lichuma tu na ilikuwa chakavu , hivyo alishangaa Roma kuongea hivyo , aliona haiwezi kushindana na Vacheton.

Ukweli Roma alipiga macho yake ya X-Ray katika mkoba wa Edna na kugundua alikuja nayo ndio maana aliongea kwa kujiamini.

Edna alijikuta akichukzwa na wazo la Roma na alijiambia kama saa yake itaonekana kituko mbele ya marafiki zake hao na kuharibu tawira yake atamkomesha.

Lakini Roma hakujali sana macho makali ya Edna alichokifanya ni kuchukua mkoba wake na kisha akaingiza mkono na kuitoa saa hio ya Analogi.

Sasa kwa namna alivyoitoa watu walikuwa wakitamani kucheka vile vile , maana ni mara chache sana kukuta saa ya thamani kutokuwa na boksi lake

“Mr Roma kwa kuangalia tu hio saa inaonekana imepitia changamoto nyingi tokea iulivyotolewa hahah..”

“Unaonaje kama tukiichunguza hatuwezi jua inaweza kuwa na thaman?i”Aliongea Roma.

Aliongea Roma na kufanya hata Rich na Sasha kucheka chini chini kwani aliona Roma anakwenda kutia aibu.

Wakati watu wote wakiona kitendo hiko kinakwenda kuwa kituko cha kufungia mwaka .Roma hakujali sana bali alitoa saa ile na kumpatia Abeiku ambaye alikuwa mtaalamu wa mambo hayo kwa ajili ya kuichunguza

Edna alijikuta akifumba macho yake akitegemea kile ambacho kinakwenda kutokea , ijapokuwa alikuwa anajiamini kwenye mambo mengi , lakini kwenye hali kama hio aliona anakwenda kuaibika pakubwa.

Wakati watu wote macho yakimwangalia Abeiku wakisubiria kucheka , mara walimuona akianza kutetemeka mikono huku akikakamaa kwa wakati mmoja

“Abaiku nini tatizo , kila mmmoja anakutegemea wewe kutoa maoni yako”Aliongea Lele

“Abaiku vipi , haifanyi kazi?”Aliuliza Hanson

“HENRYG ..!!!” Aliongea kwa sauti ndogo iliokuwa na mshituko ndani yake

“Nini?”

“Its.. Henry Graves”Watu wote walishindwa kumuelewa huku wakijiuliza huyu jamaa kapatwa na nini , kwanza Henry graves ndio kitu gani?

Hanson alijikuta akifikiria kwa muda , upande wa Edna mara baada ya kuona hali ya hewa imebadilika alimwangalia Roma kwa wasiwasi , lakini Roma hakuwa hata na Habari alikuwa akipiga msosi kama vile hana akili nzuri , huku akiacha watu wapambane kivyao.

“Abeiku hio saa jina lake ni Henry Graves?”Aliuliza Cindy lakini Abeiku macho yake yote aliyaelekeza Kwenda kwa Roma

“Forgive me for saying this but if I hadn’t seen a real Henry Graves today , I would ‘ve believed it to be myth”

“Samahani kwa kusema haya lakini kama sio leo kuona saa hii ya Henry Grave, Maisha yangu yote ningeamini uwepo wake ni hadithi tu”Aliongea na kufanya kundi lote kuduwaa.
Unaijua Henry Graves wewe>

ITAENDEEA JUMATATU NICHEKI WATSAPP KUPATA MWENDELEZONAMBA NI 0687151346
 
Back
Top Bottom