Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Ningekuwa kama Yan Buwen huyo Roma ningemaliza mapema sana maana bado akili zake za ki yoso umefunga harusi bado unawazia kuishi na wanawake wengine tena na mkeo. Hata vichwa vingi vilivyowahi pita dunia hii havikuwa na sifa hiyo. Yan Buwen ndiyo anajua nini maana na Bwana Tozo Omary.
 
SEHEMU YA 461.

Profesa Clark wakati Roma anafika aliteleza na kugonga kwenye kabati lakuhifadhia vitabu pamoja na vifaa vya kufanyia majaribio.

Roma baada ya kuingia ndani alishangaa kumkuta chini na vitabu vikiwa vimesambaa , ilionyesha alikuwa akisoma baadhi ya tafiti ambazo ziliachwa na Profesa Shelukindo.

Profesa Clark alikuwa amevalia miwani ndogo ya kusomea pamoja na gauni la kulalia , mwonekano wake na namna nywele zilivochanguka na kumfunika uso Roma alijikuta akiishia kucheka tu.

“Acha kucheka bwana nisaidie kuokota vitabu”Aliongea kwa kulalamika huku akijinyanyua kivivu

“Imekuwaje mpaka ukadondoka sehemu kama hii?”

“Nilikuona wakati ukiingia na nilitaka kukimbilia kukusalimia lakini nilijikuta nikiteleza nilishikilia hilo kabati kama sapoti lakini lilionekana liliegeshwa tu na nimedondoka nalo”Aliongea na kumfanya Roma akohoe kwa namna ya kuigiza na kisha aliinamanna kulibeba na akaanza kupangilia vitabu vilivyokuwepo chini.

Baada ya kumaliza aliokota Headphone iliokuwa na mwonekano wa kipekee .

“Hizi ni Headphone za aina gani?”

“Ni Headphone ambazo zinatumia teknolojia mpya nilioigundua , jaribu kuvaa uone”Aliongea na Roma akafanya hivyo..

“Nini kinafuata baada ya hapa?”Aliuliza Roma maana hazikuwa zikitoamziki wowote.

Profesa Clark alifikiria kidogo na kisha alibadili lugha na kuanza kuongea kwa Lugha ya kiebrania.

“Hizo ni Headphone ambazo zinatumia teknolojia ya kipekee kutafsiri sauti”Aliongea na Roma aliweza kushangazwa na kubadili lugha lakini palepale alielewa alichokuwa akijaribbu kufanya kwani sauti ilitoka kwenye zile Headphone kwa lugha ya kiswahili.

“Is it real time translation divices?”Aliuliza Romakwamba je ni kifaa cha kutafsiri sauti

“Upo sahihi ni Headphone ambayo inatumia Artificial intelligence kutafsiri lugha ya maongezi ya wakati husika, ina uwezo wa kutafsiri lugha zaidi ya mia moja hivyo kurahisisha baadhi ya mazungumzo, ni mbadala wa wakalimani katika lugha, Vipi unaonaje?”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa kukubali , hata hivyo alijua kulikuwepo na vifaa vya kutafsiri lugha , lakini kwa alivyokuwa akimwamini Profesa Clark aliamini ni kifaa ambacho kingekuwa na uwezo mkubwa sana.

Alijikuta akimkumbuka Lanlan , Bi Wema alikuwa akipata shida ya kuongea na Lanlan kutokana na kutokuelewa lugha ya kingereza na kuna hata muda Edna alifikiria kumfundisha Lanlan kuongea lugha ya kiswahili.

“Hiki kifaa kinaweza kutoa changamoto za watu kuwasiliana kwa lugha tofatu , kwanini hujavitengeneza kwa uwingi?”Aliuliza

“Niligundua teknolojia yake miaka miwili iliopita lakini nilishindwa kuiweka wazi”

“Kwanini?”

“Gharama ya kuitengeneza hii Headphone moja ni sawa na gharama zilizotumika kutengeneza I phone 14 , hivyo inamaanisha kama nitaizindua ni nusu ya watu duniani kote ambao watamudu gharama , lakini licha ya hivyo kuna mamilioni ya watu wanaingiza kipato kwa kutafsiri lugha , kama hii bidhaa itaingia sokoni wataathirika moja kwa moja , lakini kubwa zaidi ukijifunza lugha ya jamii husika ni rahisi pia unajifunza tamaduni ya jamii hio , hivyo nikaona ni bora niache dunia iendelee kama ilivyo”Aliongea na kumfanya Roma aone ana mantiki kwenye maneno yake.

Clark alizichukua na kuzihifadhi kwenye kabati na kuanza kumuonyesha Roma teknolojia nyingine ambazo amegundua.

Kila kitu alichoonyeshwa kilimfanya Roma kushangaa kwani ni gunduzi za juu sana ambazo zimeweza kufanywa na mwanamke ambaye hajatimiza hata miaka ishirini na tano.

Alijikuta akimwangalia Clark ambaye sura yake ilionekana kuwa na furaha kuliko siku zote , tokea swala la ndoa yake kughairishwa alionyesha kama amepewa uhai mwingine.

“Kwanini unaniangalia hivyo? Au maelezo yangu yamekuywa mengi ,hivi vitu nimetengeneza nikiwa sina mudi ya kufanya chochote”

“Nikiri kwamba ijapokuwa nilikuwa nikikuchukulia kama mwanasayansi mkubwa lakini kuna vitu vingi sijavifahamu kutoka kwako , una heshima yangu”.

“Nikajua ungeniita mwanamke kichaa”

“Kwaninni nikuite kichaa wakati kazi yako ni kubwa , hata hivyo nimejikuta hata nipata ahueni ya kupunguza mawazo kwa kusikiliza maelezo yako”Aliongea Rom.

“Una mawazo gani wakati umezungukwa na watu wanaokupenda?”Aliuliza huku akionyesha hali yakutaka kujua nini kimemsibu Roma mpaka kuwa kwenye mawazo.

Roma ilibidi amuelezee Clark kuhusu Rufi namna ambavyo alifanya makusudi kudukua mawasiliano ya frequency za Tv Chanel yao lakini pia namna alivyogongwa na Edna mpaka kufanikiwa kuweka ukaribu lakini pia namna alivyomharibia siku yake nzuri..

Mpaka Roma anamaliza Clark alishangazwa na maelezo hayo , hakuamini siku ile mdukuzi alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na mahusiano na Roma.

“Clark nipo najidharau hapa kwa kushindwa kujizuia na nahisi ubongo wangu umejaa Protini na sio akili”

“Sio kama umeshindwa kujizuia Roma, kama ni hivyo basi ungekuwa ushanigusa na mimi au huyo Rufi ni mrembo kuliko mimi?”

“Nishakuambia wewe ni wa tofauti kwangu”

“Jibu lako ndio linaelezea hali uliopo nayo kwa sasa , ukweli ni kwamba hukutaka kujizuia mara baada ya kumuona Rufi”

“Unamaanisha nini kusema hivyo?”

“Sijui sana kuhusu wanaume wengine lakini wewe nakufahamu ,kipindi cha nyuma licha ya kwamba ulikuwa ukishindwa kujizuia kwa sababu ya ukali wa Devine light kwenye mwili wako lakini hata hivyo ulikuwa ukichagua wanawake wa kulala nao , hivyo maelezo ya kwamba kwanini ulilala nae na sio mimi ni kwasababu Rufi ulimchukulia kama mwanamke ambaye hana umuhimu kwako , ulimchukulia kama Malaya wa kupumzisha akili na asubuhi kumpotezea ni kama kipindi kile ulivyokuwa Ninja wanawake hawakuwa na umuhimu kwako na hukujiuliza hata mara mbilimbili kuyachukua maisha yao wanapovuka mpaka”

“Wanawake niliowaua hawakuwa wanawake kwangu bali maadui , unapaswa kuwatofautisha”

“Sawa na ndio maana nakuambia ulivyomuona Rufi hukumzingatia kama mwanamke muhimu kwako hivyo ukaruhusu hisia zako kukuongoza na matokeo yake ni kwamba alikuwa ni mwanamke mwenye akili tofauti na ulivyomdhania, hivyo ulichomfanyia Edna ni usaliti wa kimwili na sio usaliti wa kihisia”

“Wewe pekee ndio unaweza kuelewa hivyo lakini sio Edna, matendo yangu yamemuumiza kihisia kwani moja kwa moja anamchukulia Riufi kama mwanamke ninaempenda”

“Ndio!, hawezi kukuelewa labda angefahamu hata nusu ya maisha yako ya nyuma huenda angekuelewa na hata mimi pia nisingekuelewa”

“Kwanini?”

“Kuna sababu moja tu, ulishaacha tabia ya kulala na kila mwanamke unaekutamanisha , hivyo naweza kuamini moja kwa moja hisia zako kwa Rufi hazielezeki na haumchukulii kama malaya tena na kama ingekuwa hivyo huenda muda huu angekuwa ni marehemu kwa kukuchokoza”

“Kwahio kimsingi ni kwamba mimi ni mbwa”

“Sio kila mmoja atakuona kama mbwa , Mimi mwenyewe natamani uendelee kutokuwa mwaminifu huenda nikapata nafasi kuwa mpenzi wako, ndoa ni ustaarabu wa kibinadamu zaidi na unachotakiwa kuelewa mwanamke yoyote anavutiwa na mwanaume mwenye nguvu na kujiamini , kwa mfano tu marafiki zako Sauroni na Makedoni wana wapenzi wengi kuliko hata wewe , mimi kwa uwezo wako naona bado ni muaminifu”

“Kwahio ndio unavyoniona?”

“Unafikiri ni mimi tu , naamini hata wapenzi wako wengine , Rose , Nasra , Amina na Dorisi wamekupenda kutokana na kutokuwa mtu wa kawaida , unafikiri ungeweza kuwa nao kama ungekuwa mtu wa kawaida ambaye unafanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto?”

“Naona hii ni kama mbinu yako ya kuzitakasa dhambi zangu?”

“Ninachofanya hapa ni kukuelewesha tu namna ninavyokuchukulia lakini maono yangu kwako ni tofauti na Edna atakavyokuona”

“Kwanini?”

“Kwasababu Edna tayari ni mkeo na wapenzi wako wengine wanamfanya kukosa haki zote kama mke , yeye ni mke aliekamilika kwako lakini wewe ni mume ambaye hujakamilika kwake kutokana na kuwa na wanawake wengi, hivyo anakuvumilia kwasababu anaogopa kukuacha ,nakupenda kama lakini ukweli unachomfanyia Edna ni ukatili”

“Daah! I feel so too that’s why I’m so disgusted with myself”Aliongea Roma huku akivuta pumzi.

“Ndio hivyo Mister Disgusting, unajua ni maneno gani matatu hupaswi kusema kwa mkeo pale unapomkosea?”

“Maneno gani?”

“I am sorry”Aliongea na kumfanya Roma kuona labda kukutana na Edna kwenye maisha yake ni jambo baya sana , kwani muda wote alikuwa akiongea hilo neno.

“Kwanini sasa hukuniambia mapema”

“Kwanini nikupe ushauri unaoimarisha ndoa yako, wakati na mimi ni mwanamke ninaekuwinda, ninaweza kuwa mwanasayansi lakini mimi ni binadamu mwenye hisia na hisia zangu zinaniambia ukiachana na Edna mfaidika mkuu aakuwa mimi”

“Nisaidie namna ya kutatua hili tatizo napanga kufunga nae ndoa mwezi ujao”

“Kwanini usimpe talaka tu”

“Acha ujinga ! Haitokuja ikatokea siku nikamuacha yule mwanamke labda yeye mwenyewe alazimishe kufanya hivyo , Kama ningekuwa simpendi nisingeishi nae mpaka sasa , unajua ni vita gani baridi nimepitia kukaa nae nyumba moja , yote ni kwasababu ameujaza moyo wangu kuliko mwanamke yoyote yule”Aliongea Roma akiweka usiriasi.

“Lakini hivyo sio Edna anavyofikiria , unachotakiwa kujua mapenzi ni kama Manati , unavyomuumiza kihisia ni kama vile unavyoivuta na kadri unavyoendelea kuivuta itaishia kukatika na haiwezi kurudi kwenye mwonekano wake wa mwanzo”

“Nitaiunganisha hata kwa kuifunga na mpira mwingine”Aliongea Roma na kumfanya Clark kukosa usemi kutokana na jibu lake.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kukuona ukiwa na wasiwasi namna hii inaonekana kweli unampenda sana”

“Nisamehe kama maneno yangu yamekuwa makali lakini nahitaji kutatua hii changamoto”

“Usijali hata sijakasirika”

“Kwahio unanisaidiaje sasa?”

“Unamuuliza mtu ambaye maisha yake yote hakuwahi kuwa kwenye mahusiano , nawezaje kutoa ushauri kwa mwanaume mwenye mke? Ila nina wazo lakini naona kama la kijinga”Aliongea na kisha akamnong’oneza“

*****

Molin ndio aliekuwa wa kwanza kumsogelea Edna , lakini kikumbo alichokutana nacho kilimfanya kutupwa upande wa pili wa mchanga.

Lanlan siraha yake kubwa ni mwili wake na ndio alichokifanya baada ya kuona Molin kutaka kumgusa mama yake.

“Why are you following Mama?, if you’re bad guys I’ll kill you”Aliongea Lanlan huku akianza kuminya minya pua zake kama vile anataka kutoa makamasi.

Wanajeshi wa The Eagles walikuwa wakifahamu Lanlan alikuwa na uwezo usio kawaida mara baada ya miezi kadhaa iliopita Edna waliposhambuliwa na misukule ya Yan Buwen iliofufuliwa kwa Ressurrection Fluid , sasa siku ile waliweza kuangalia ’footage’ za CCTV za tukio zima na ndipo walipogundua Lanlan hakuwa mtoto wa kawaida.

Lanlan aliwaangalia mmoja mmoja kwa namna ya kuwachunguza na alivyoweza kuona sura ya Adeline aligundua alishawahi kumuona nyumbani kwao.

The Eagles wakati wakiangaliana kwa tahadhari kwa kujiuliza cha kufanya walijikuta wakitoa macho mara baada ya kumuona Lanlan akimshika Edna masikio kwa kuyaingiza vidole pande zote na palepale Edna alishituka kama mtu ambaye alikuwa kwenye ndoto.

Afande Adeline na wenzake walijikuta wakiangaliana wakishindwa kuzuia mshangao wao, lakini hata hivyo walijikuta wakivuta pumzi za ahueni mara baada ya Edna kurudiwa na fahamu.

“Madam uko sawa, tunaomba tukupeleke hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo” Aliongea Adeline mara baada ya kutoka kwenye mshituko.

“Nipo sawa na sihitaji ulinzi wenu, mnaweza kurudi na muambieni aliewaagiza sitaki kumuona tena”Aliongea Edna kwa kiburi.

“Madam hupaswi kuongea hivyo , Mfalme Pluto hatopenda tukukuache bila ya ulinzi”Aliongea Adeline

“Ndio Madam ,jambo lolote baya lilikupata hatoweza kutusamehe”Aliongezea Fanny.

“If mama tells you to go you must go and if you don’t I will kill you both”Aliongea Lanlan kuingilia yale mazungumzo huku akimshika Edna mkono

Maneno ya Lanlan yalimfanya Edna amwangalie Lanlan kwa mshangao kwani kauli zake zilikuwa za kibabe sana , kuna muda alifikiria huenda Roma na Lanlan ni kitu na baba yake , kwani walikuwa wakifanana kwenye mambo mengi.

Lanlan alikuwa anapenda chakula sana na hivyo hivyo Roma alikuwa akipenda kula sana ,wote walionekana sana kupenda kuua sana na kutoa kauli za ugomvi.

Ijapokuwa walikuwa wakiongea na Edna lakini macho yao yote yalikuwa kwa Lanlan , walimwangalia kwa wasiwasi.

Molini bado alikuwa akiugulia maumivu kwani mwili wake ni kama uligongwa na jiwe .

“Tunapaswa kuondoka , Madam hatopatwa na tatizo kutokana na uwepo wa Lanlan hapa , Huyo mtoto anaonekana kuwa na nguvu kuliko sisi wote hapa”Aliongea Molin kinyonge akiwashauri wenzake.

“But..”

“We ‘ll head back and report to Captain Diego , From there we will await for further orders”Aliendelea kuongea akimaanisha kwamba wanapaswa kurudi wakatoe ripoti kwa Kapteni Diego na kusubiria oda nyingine.

****

Roma akiwa ameketi eneo la sebuleni ndipo alipopigiwa simu na Diego na kupewa taarifa ya kile kilichotokea , alishangazwa sana na kuwa na wasiwasi kwa kile kilichotokea mara baada ya kuambiwa Edna alidondoka na kupoteza fahamu na kisha Lanlan akamshika masikio na akazinduka.

Alijua Lanlan alikuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida lakini kitendo cha kumzindua mama yake baada ya kupoteza fahamu kilimshanganya ,lakini kubwa zaidi ni kwanini Edna adondoke na kupoteza fahamu au ni kwasababu alimuumiza kihisia ,alijikuta moyo wake ukiuma mara baada ya kuhisi huenda yeye ndio chanzo.

“Ndio unaondoka?”

“Ndio shukrani kwako umenisaidia kupoteza mawazo”

“Mpango wako ni upi sasa?”

“Umeniambia nisubiri mpaka atakapokuwa sawa mwenyewe , hivyo sitofanya chochote na zaidi yoyote nawajibika pia kwa wapenzi wangu wengine”

“Ngoja nikupe kuna chupa za pombe zipo kwenye friji , maana siruhusiwi kunyw apombe”

“Mbona kuna ile chupa ambayo ipo wazi?”

“Nilipunguza upweke ile siku nilivyotoka kwako nikiwa na hasira baada ya Edna kuniambia niolewee na Maksim , ila situmii pombe kabisa”

“Clark nisingekuwa nimemuoa Edna ningekuoa wewe”

“Nah Being Clark suits me more than being Edna”

“Umeeleweka”Aliongea Roma na kisha alipunga mkono na kutoka ndani ya nyumba hio.

“Pumbavu kama ningekuwa mpenzi wako nisingependa kuwa Clark tu”Aliongea Clark baada ya kujibwaga kwenye Sofa.

*****

Edna aliondoka eneo la ufukweni kutokana na kukosa amani kwani watu wengi walikuwa wakimwangalia kwa mshangao kutokana na tukio la kudondoka lakini pia Lanlan kumpiga Molin kikumbo mpaka kudondoka.

Safari yao ya kwanza ilikuwa ni Mlimani na alimnunulia Lanlan baadhi ya zawadi ikiwemo mdoli na kisha akaianza safari ya kurudi nyumbani.

Uwepo wa Lanlan ilikuwa ni nafuu kwake kwani mawazo yalikuwa yamepungua kwa kiasi kikubwa lakini hasira na Roma hazikuwa zimeisha na alitamani asimuone kwa zaidi ya wiki nzima.

Aliendesha gari huku akifikiria tukio lilomtokea , haikuwa mara yake ya kwanza kupoteza fahamu , mara ya kwanza ilikuwa ni Hongkong na hisia zilikuwa zinafanana, lakini awamu hii ilikuwa tofauti kidogo.

Alivyopoteza fahamu ni kama alikuwa akiota ndoto akiwa aneo la msituni katikati ya mbuga huku akimuona mwanamke mwenye mwonekano wa kufanana kabisa na yeye lakini mwanamke aliekuwa mbele yake hakuwa peke yake , alikuwa akimwangalia Lanlan ambaye amepanda juu ya mnyama mkubwa mwenye kufanana na Tembo lakini muda uleule ghafla yule mwanamke aligeuka nyuma na kumuona yeye na kuanza kuonyesha mshituko uliojaa hofu na palepale alimkimbilia Lanlan huku akiita jina lake.

“Lanla…!!!”Edna kabla hajamaliza ndoto alijikuta akirudiwa na fahamu na ni muda ambao Lanlan alimuwekea vidole masikioni.

Alijikuta akimgeukia Lanlan aliekuwa pembeni akicheza na mdoli wa kike , alijiambia mwonekano wa Lanlan pembani yake si kiasi cha pesa chochoe ambacho kinaweza kukamilisha hilo, alijikuta akiwa ni mwenye faraja , uwepo wa Lanlan kwenye maisha yake ni kama sababu nyingine ambayo inamfanya kuyapenda sana maisha yake.

Dakika chache mbele aliweza kufika Ununio na kuingiza gari ndani na ni muda huo huo na Roma na yeye aliweza kuingia hapo ndani baada ya kushushwa na Taksi nje ya geti.

Edna alivyoshuka kwenye gari na kumuona Roma anaingia alijikuta sura akiikunja na hasira zikianza kujikusanya upya.

“Kwanini upo hapa?”Aliuliza Edna akiwa na sura iliojaa usiriasi.

“Edna mke wangu sidhani kama ndio unanifukuza ndani ya hii nyumba?”

“Unaweza kwenda popote unapojisikia , kwanza una wanawake wengi hivyo hukosi pakulala, Hapa ilikuwa ni nyumbani kwako na si sasa na kama hutaki kuondoka hapa nitaondoka mimi na Lanlan”Aliongea kwa kufoka.

“Edna hatuwezi kukaa chini na kuongea?”

“Sitaki maongezi na wewe”

“Edna najua una hasira na mimi , lakini kilichotokea mimi na Rufi ni kitendo cha mara moja tu na hakiwezi kujirudia tena na hata sijui ni sababu gani ametaka kutuvurugia , hata hivyo sio mwanamke wa kawaida na wasiwasi wangu angekuwa hatari zaidi kwako na huenda angekuumiza”

“Wewe ndio umeziumiza hisia zangu sio Rufi”

“Okey basi nitaondoka na nitarudi ukiwa umetulia”Aliongea Roma na kisha alichukua ufunguo wa gari yake kwenye mikono ya Edna na kisha akaliwasha na kuondoka , muda huo ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu kwenda saa moja na kigiza kishaanza kuingia.

Edna alisimama palepale pasipo kuamini Roma anaondoka kweli , alimwambia aondoke kwasababu alikuwa na hasira lakini hakuwa akimaanisha kwenye moyo wake, alitaka kuona Roma akiomba msamaha na kujielezea , lakini akaondoka nje ya mategemeo yake.

“Mama don’t cry”Lanlan alimwangalia mama yake kwa huzuni na Edna alijikuta akiyafuta machozi haraka haraka na kisha alimwangalia kwa tabasamu na kumwambia halii.











SEHEMU YA 462

Upande wa juu ghorofa ya pili Qiang Xi alikuwa akishuhudia wana ndoa wakigombana na alijikuta hata yeye moyo ukimuuma , hasa alipomwangalia Lanlan alieshikwa mkono na Edna.

Waliingia ndani na nyumba ilikuwa imetulia kuliko isivyokuwa kawaida ,maana wanafamilia walikuwa wamepungua kwa kiasi kikubwa , Yezi alikuwa ashaondoka kwa zaidi ya miezi kadhaa , Sophia kahama, Blandina alikuwa anaishi Masaki nyumbani kwao , hivyo waliobaki ni Bi Wema na Qiang Xi.

“Sister Edna kama ukija kuwa na mtoto mwingine wa kike unadhani atakuwa ni kama Lanlan?”Aliuliza Qiang Xi na haikueleweka kwanini ameuliza hilo swali.

“Mama , Don’t get me a sister I want a brother”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kushangazwa na jibu lake na Bi Wema ndio ambaye hakuelewa pekee na ilibidi Edna atafsiri.

Edna hakuwahi kuwaza kupata mtoto mwingine bado na hakuelewa namna alivyojisikia mara baada ya kumsikia Lanlan kusema anataka mdogo wake wa kiume na sio wa kike.

*****

Roma mara baada ya kutoka nyumbani safari yake ya kwanza ilikuwa ni mjini na alipitia njia ya Kawe na kwenda kusimamisha gari nje ya jengo la Apartment za PalmVillage Mikocheni kwa Warioba.

Alikuwa na mpango wa kuonana na Rufi kwa mara nyingine , haikujulikanaa ni sababu ipi ya kuonana nae tena , lakini sasa kwasababu hakuwa akijua ni Apartment namba ngapi aliokuwa akiishi alishindwa kushuka na kuingia ndani.

Baada ya kuwaza kwa muda mfupi alikumbuka Mika alikuwa na ukaribu na Rufi lakini hata hivyo hakuwa na mawasiliano yake hivyo moja kwa moja alimkumbuka Benadetha na palepale alitoa simu yake na kumpigia.

“Roma siamini kama umenikumbuka leo?”Sauti laini ya kike ilisikika upande wa pili huku ikionyesha kufurahishwa na simu hio.

“Kwanini useme hivyo wakati sina sababu ya kukupigia simu” Aliongea Roma.

“Oh! Kwahio ni sababu gani umepata leo mpaka ukanikumbuka?”

“Nahitaji namba ya simu ya mdogo wako Mika , nitumie kwa meseji”Aliongea Roma.

“Mh! Haya”Aliongea Benadetha na kisha simu ilikatwa na dakika hio hio namba ya Mika ilitumwa kwa meseji na Roma alipiga simu palepale

“Dogo niambie ni Apartment namba ngapi Rufi amechukua ndani ya hili jengo”

“Shemeji Roma..Aaa Bro!”Sauti upande wa pili ilisikika na Roma aliweza kufahamu Mika yupo Bar kama sio Claub kutokana na sauti za watu na mziki lakini alishangazwa kuitwa shemeji.

“Ndio ni mimi Roma na sio Shemeji yako”

“Okey Bro , Anaishi number 101 floor 14 , Password ni siku, mwezi na mwaka mliokutana”Aliongea Mika kwa sauti.

“Wewe dogo ndio kakuambia uniambie na Pasword”

“Bro nimesema hivyo kwasababu sifahamu hata mmekutana lini hivyo hata mimi hio Pasword siiijui”Aliongea na Roma alikata simu na kisha alitoka kwenye gari na kuzama ndani kupitia upande wa Supermarket.

Dakika chache mbele alikuwa kwenye Korido ya Floor 14, hili jengo halikumpa shida kwasababu Nasra alikuwa akiishi hapo pia hivyo watu wa usalama walikuwa wakimfahamu.

Roma mara baada ya kufika mbele ya mlango uliokuwa na kibao cha namba anuani 101 pembeni yake , alifikiria kwa muda kuminya kengele au kuingiza Password ,lakini akili yake ilimwambia aingize Pasword kwa kukumbuka tarehe aliokuana na Rufi L.A kwa kutumia mfumo wa tarehe na kweli palepale mlango ulifunguka.

Alijikuta akitabasamu na kisha akaingia ndani taratibu na kuita jina la Rufi lakini hakujibiwa , kulikuwa kimya kama hakukuwa na mtu lakini kutokana na uwezo wake usio kuwa wa kawaida alihisi uwepo wa mtu akiwa bafuni hivyo alisogelea dirisha lililokuwa likiangaliana na jiji kwa muda na kisha akarudisha pazia na kujibwaga kwenye sofa.

Rufi hakujua kuna uwepo wa mtu hivyo mara baada ya kumaliza kuoga moja kwa moja alitoka mpaka sebuleni akiwa uchi huku taulo mkononi akijifura maji.

“Ahh..!”Sauti ya kike ilisikika upande wa kulia kwake na alipomuona Rufi akiwa uchi ameziba sehemu zake za siri kuzificha na kukimbilia chumbani alikotoka.

Roma alijikuta mawazo yake yakisafiri kurudi nyuma mpaka siku ambayo alikutana na mrembo huyo ndani ya jiji la Loss Angeles na hatimae kumvua nguo na kufanya nae mapenzi

“Umeingiaje nyumbani kwangu?”Rufi aliongea mara baada ya kuvaa tisheti na kijikaptura kilichoishia kwenye magoti.

“Unafikiri wewe ndio mwenye akili nyingi ndani ya dunia hii?”Aliuliza Roma maana hakuwa tayari kumtaja Mika.

“Nadhani ni swali la kijinga , kama umeweza kuniponyesha sumu iliokuwa mwilini mwangu kwa muda mrefu naweza kukufananisha na wazee wa jamii za kijini”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia kwa mshangao kidogo.

“Lakini siamini kama unatokea jamii za kijini kama ingekuwa kweli usingeoa binadamu kwani usingeweza hata kumpa ujauzito”Aliongea na kuzidi kumshangaza Roma na kujiuliza kama Rufi alikuwa ametokea kwenye jamii hizo za kijini lakini alikaa vilevile kwenye Sofa bila ya kumjibu swali hata moja , haikueleweka alikuwa akiwaza nini.

“Roma naomba nikuulize swali?”Aliongea

“Umeuliza maswali mengi na umejijibu mwenyewe “Roma aliongea huku akitoa kicheko hafifu bila kuelewa hata yeye mwenyewe anacheka nini.

“Nataka kujua kama unanichukia na upo hapa kuniadhibu?”Aliuliza kwa wasiwasi.

“Kwanini nikuchukie ?”

“Kwasababu nimekugombanisha na mkeo?”

“Kwani tulishawahi kufanya mapenzi?”

“Acha kunidhalilisha , Ndio tumefanya tena mara nyingi , mchana wote”Aliongea kwa hasira.

“Kama ndio hivyo basi hatuna ugomvi , ulichomwambia mke wangu haujatunga na uliongea ukweli, ijapokuwa sijafurahishwa lakini sina sababu ya kukuchukia”Aliongea .

“Roma you are so nice to me”Aliongea huku akianza kutoa machozi.

“Wewe ni mtu mzuri ambaye nishawahi kukutana nae kwenye maisha yangu yote nimekugombanisha na mkeo lakini bado hunichukii , nilikaa nikawaza labda ndio mwisho wa kukuona tena kwa nilichokufanyia”

“Acha maigizo kwa mwonekano wako usingekosa mwanaume wa kukupenda na akawa mzuri kwako”

“Wewe hufahamu nilipotoroka nyumbani na kufika Marekani nilikutana na wanaume ambao asilimia kubwa walinisogelea kwa kunihitaji kingono pekee , hata wale ambao walijifanyisha kuwa marafiki zangu hawakuweka wazi lakini nia zao zilionekana wazi”

“Ulimwengu huu sio wa giza kama unavyofikiria watu wazuri na wabaya wapo”

“Kuwa na bahati ya kuzungukwa na watu wazuri haimaanishi kila mtu anaweza kuzungukwa na watu wazuri , mimi ni mwenye bahati mbaya”Aliongea na Roma alishindwa kujua cha kuongea na kuamua kuanzisha maongezi ya kile kilichomfikisha hapo.

“Umeuliza maswali mengi , hivyo ni zamu yangu na mimi kukuuliza . Niambie unataka nini kutoka kwangu na wewe ni nani haswa , maana matendo yako yanaonyesha unatafuta ‘attention’ yangu hivyo niweke wazi?”

“Kama nitakuelezea ukweli wote , je unaweza kuniahidi kitu kimoja?”

“Kitu gani?”

“Kunisaidia kulipiza kisasi?”

“Nini?”

“Nimesema kunisaidia kulipiza kisasi , ukiniahidi katika hilo nitahakikisha nafanya kila utakachotaka kutoka kwangu, nilichokuambia kuhusu mama yangu mzazi kutokea Afrika Mashariki ni kweli lakini sababu yangu ya kukufuata Tanzania ni kwa ajili ya kutaka msaada wa kulipiza kisasi”Aliongea .

“Unamaanisha nini?”

“Unatakiwa kukubali kwanza kuahidi ndipo nitakapokuelezea nimetokea wapi?”Aliongea kibishi.

“Wewe mwanamke ijue mipaka yako , huna haki ya kunilazimisha kufanya chochote kwa ajili yako , nikiamua kukuua hutokuwa na uwezo wowote wa kujitetea na kama unajihisi wewe ni mrembo na unaweza kunitega nadhani tayari ushamuona mke wangu”Aliongea Roma huku awamu hii akiwa siriasi mno.

“Nilijua tu hutotaka kunisaidia?”

“Nilishakuelezea mara ya mwisho usinikaribie tena kwasababu sikutaka ugomvi, hunidai wala sikudai lakini ukaamua kunivuruga ..”

“Ni kwasababu naogopa watanikamata tena?”

“Unamaanisha kuna watu wanataka kukuua?”

“Bora ingekuwa ni kifo ingekuwa afadhali lakini wakinikamata wataishia kunipa mateso makali ya muda mrefu pasipo ya kuniua”Aliongea na kuanza kutokwa na machozi

“Okey huna haja ya kutoa machozi mbele yangu na sitokuuliza maswali mengine hata hivyo uvumilivu wangu unakikomo , nataka uondoke Tanzania kwanzia siku ya kesho , umenunua hii Apartment nitakurudishia hela zako”

“Mbona unakuwa mkatili namna hio?”

“Unahisi ni wapi nimekuwa mkatili?”

“Umeniponyesha maumivu niliokuwa nayo kwa zaidi ya miaka ishirini na juu ya yote umesema hunichukii , inaonyesha kabisa unanipenda na hutaki kukubali ukweli”

“Unaongea ujinga ,kwangu wewe ni kama mwanamke wa kutumia na kuacha tu na sio wa kurudia mara ya pili , acha kujipa umuhimu kwangu”

“Wewe…!!”Aliongea huku akionyesha hasira waziazi.

“Sina haja ya kuongea na wewe mimi , ninachotaka ni wewe kuondoka hapa Tanzania , ikitokea umekuja kunivuruga tena itakuwa ndio mwisho wa uhai wako”Aliongea Roma na kisha alipiga hatua kuelekea mlangoni ili kutoka nje, hakuwa tayari kukubaliana na mwanamke huyo juu ya kitu ambacho hakuwa akikifahamu , hata hivyo alikuwa sio wa kawaida alijiambie je kama ni jambo litakalomwingiza kwenye matatizo.

Rufi alijikuta machozi yakimtoka mfululizo huku akimwangalia Roma akifungua mlango na kutoka nje.

“You Coward man the more you try to get rid of me the harder it will be”

“Wewe mwanaume muoga , kadri unavyojitahidi kuniondoa ndivyo itakuwa ngumu zaidi”Aliongea kwa hasira bara baada ya kufungua mpango akimwangalia Roma aliekuwa kwenye Lift ilioanza kujifunga..

Roma hakujali maneno yake , baada ya kurudi kwenye gari aliwaza ni wapi akamalize usiku maana amefukuzwa , hakuwa na mpango wa kutembelea mwanamke yoyote ambaye yupo karibu na nyumbani kwani alijua lazima Edna angefahamu hivyo kumuongezea hasira zaidi.

Wakati akiwa anawaza ni safari ya wapi aanzishe, simu yake ilianza kuita na baada ya kuangalia namba ilikuwa ni ngeni , lakini ilikuwa ni ya Kitanzania.

“Roma za siku nyingi”Sauti laini ya kike ilisikika kwenye masikio ya Roma , ni sauti ambayo haikuwa ngeni lakini ni kama ameisahau”

“Naongea na nani?”

“Ni Mimi Nadia Alfonso , tunaweza kuonana?”Aliongea Nadia na kumfanya Roma kushangaa na kujiuliza mwanamke huyu alijuaje yupo nje ya nyumba muda huo sa saa mbili za usiku.

“Nadia nadhani unajua nimeoa na muda kama huu nipo na familia”

“Najua haupo nyumbani kwako ndio maana nikakupigia simu”Aliongea na kumfanya Roma kuanza kuchungulia mazingira ya nje na kuangalia mbele zaidi mita kadhaa aliweza kuona mwanamke mrembo alievalia suruali ya jeans rangi ya bluu , viatu vyeupe high heels na kijiblazier cha mikono mirefu rangi ya pink isiokoleza.

Alikuwa ni Nadia ndio akiwa ameangalia gari yake huku akiwa ameshikilia simu na mkono mmoja na mkoba wa Brand ya Hermes mkono mwingine.

“Nilipanga nikutafute kesho asubuhi , lakini imekuwa bahati upo maeneo haya”Aliongea huku akipunga mkono kw akuinua mkoba wake juu.
[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Ningekuwa kama Yan Buwen huyo Roma ningemaliza mapema sana maana bado akili zake za ki yoso umefunga harusi bado unawazia kuishi na wanawake wengine tena na mkeo. Hata vichwa vingi vilivyowahi pita dunia hii havikuwa na sifa hiyo. Yan Buwen ndiyo anajua nini maana na Bwana Tozo Omary.
Hao mademu watamsaidia sana Edna wakati Roma akiond9ka watakuwa na mafunzo ya kimapigano ya hatar
 
Edna mke wangu , sikujua kama una mbinu zako za siri, umefanya kwa kudhamiria nini , unaonekana kama mzoefu umewezaje kuifinyia kwa ndani”Aliongea Roma lakini Edna alishindwa kujibu chochote zaidi ya uangalia pembeni kwa kuona aibu kumwangalia usoni hata hivyo alishindwa kumuelewa anamaanisha nini kusema kufinyia kwa ndani.
 
Edna mke wangu , sikujua kama una mbinu zako za siri, umefanya kwa kudhamiria nini , unaonekana kama mzoefu umewezaje kuifinyia kwa ndani”Aliongea Roma lakini Edna alishindwa kujibu chochote zaidi ya uangalia pembeni kwa kuona aibu kumwangalia usoni hata hivyo alishindwa kumuelewa anamaanisha nini kusema kufinyia kwa ndani.
 
Mwamba singanojr uko vizuri sana..sema fanya kuangusha moja moja kama twanga pepeta.
 
Kupitia hi story unaweza kuwaelewa kidogo watu wa jami intelligence na madude yao yale....
 
Kupitia hi story unaweza kuwaelewa kidogo watu wa jami intelligence na madude yao yale....
Kwa hiyo hata yule fala Buwen naye ni mtu wa kueleweka na madude yake?

Kizwe katafuna biringanya la Buwen kimasihara huku Lekcha akimchinja kama kuku mchina wa watu hatimaye kusitisha ndoto ya Buwen kumnyandua mrembo msagaji the don😂
 
Kwa hiyo hata yule fala Buwen naye ni mtu wa kueleweka na madude yake?

Kizwe katafuna biringanya la Buwen kimasihara huku Lekcha akimchinja kama kuku mchina wa watu hatimaye kusitisha ndoto ya Buwen kumnyandua mrembo msagaji the don
 
Back
Top Bottom