SEHEMU YA 535.
Edna hakujua ni wapi Roma alitoka na tokea aondoke usingizi ulimpotea na akaamua kukaa macho kumsubiria na wakati Roma anafika hapo ndani akiwa ametangulizana na Babu yake Yezi ndio alijifanyisha kulala.
Sasa mara baada ya Roma kurudi na kuanza kukaa katika mkao wa kufanya tahajudi moyo ulimfurukuta kwani alitaka kujua kila kilichotokea..
“Wewe kiumbe , kwahio ndio hutaki kunipa maelezo ni wapi umetokea?”Aliuliza Edna.
“Umelala , hivyo sikutaka kukuamsha”
“Mh!, Bora hata hujajua kama nilikuwa nikikusubiria”Aliongea kivivu alionyesha kabisa anataka maelezo , alijua kabisa kuna jambo ambalo limetokea ndio maana.
Roma alitabasamu na kisha akamwelezea Edna kila ambacho kimetokea mpaka kushindwa kumsaidia Park Juan kurudisha hadhina yao ya kifamilia.
Kwa ufupi alidanganya kwamba ameshindwa kumdhibiti mtu alievalia mask na ndio maana akashindwa kuirudisha hadhina hio ya familia ya Park, Roma alifanya hivyo ili kuepuka kumuelezea Athena pamoja na kukutana na Alice na Sterrn ambao Edna alikuwa akiwahafamu, hakutaja kuhusu moyo wa Gaia pia hata hivyo hakuwa akijua nguvu yake.
“Tokea ulivyokuja kwenye maisha yangu kila kitu ninachosikia kutoka kwako kimekaa kimajabu ajabu tu”Aliongea lakini licha ya hivyo hakushangaa kabisa kwani alikuwa ashaanza kuzoea na mambo ya kimaajabu ambayo amekutana nayo mara baada ya kuanza kuishi na Roma.
“Kama ni hivyo kwanini unafanya Meditation , si utakuwa umechoshwa na kilichotokea?”
“Kuna kitu kimenichanganya wakati napigana na mtu mwenye Mask, hivyo najaribu kufikiria ni kwa namna gani aliweza kunidhibiti na akakimbia”Aliongea Roma kwa kudanganya , alichokuwa akimaanisha ni kinyume chake , alikuwa akitaka kufanya meditation kujua ni kwa namna gani Athena amemfanyia shambulizi lile , alitaka kujua ni namna gani kama siku nyingine atakutana nae atakavyomdhibiti.
Edna hakutaka kupinga , hata kama hajaelewa alijifanyisha kuelewa ili kutotengeneza maswali mengi.
Roma alikesha usiku mzima akiwa amekaa chini amefumba macho , kwa haraka haraka ni kama ametumia masaa matano kufanya meditation na hata Edna alivyoamka na kumkuta kakaa staili moja alishangaa.
Roma mara baada ya kufumbua macho yake aliweza kumuona Edna ambaye alikuwa mbele yake akiwa anamwangalia.
Waliangaliana kwa dakika kama tatu hivi na kumfanya Edna kushangaa na Roma kumwangalia muda mrefu.
“Vipi umegundua kitu?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma atingishe kichwa.
“Nadhani nilikuwa nakosa kuangalia vitu viwili muhimu kwa umakini?”
“Umegunda Vitu viwili , Vitu gani?”
“Hivyo viwili chini ya kifua chako”Aliongea Roma huku akitabasamu na kuinua kichwa chake kuchungulia vizuri.
Edna hakujua anamaanisha nini lakini alivyoinamisha kichwa kuangalia kifuani aliijikuta akiwa mwekundu kama yai la kisasa.
Nguo yake ya kulalia ilikuwa imeachia vifungo viwili na kufanya manyonyo yake kuwa wazi sasa kitendo cha kuinama kilimfanya yaonekane vizuri ndio maana Roma akamtania .
“Wewe Roma muhini sana , leo nakuua”Aliongea kwa aibu na palepale alichukua mto uliokuwa karibu yake na kumpiga nao Roma kichwani kwa hasira na kitendo hiko kilimfanya Roma kutoa cheko na kusimama baada ya kuzidiwa na kisha akambeba juu juu na kumrushia katikati ya kitanda na yeye kumfuata huko huko na kumpiga mabusu kumtuliza.
“Ndio maana hukupata majibu , kumbe ulichokuwa ukiwaza ni kunichokoza tu”
“Kumchokoza mke wangu hakuingiliani na maswala yangu ya mafunzo , nahitaji kuwa na nguvu zaidi ili kuwalinda , nikajua ushaelewa hilo wewe mtoto”
“Acha kuongea ujinga na kajiandae tukapate kifungua kinywa na tutatumia muda huo huo kumuaga Park Juan na kutafuta tiketi za ndege kuturudisha nyumbani.
“Kwanini kuharakisha kurudi , kwanini tusikae angalau kwa wiki moja?”
“Nimemkumbuka mwanangu Lanlan , sijapiga simu siku mbili hizi na nina wasiwasi na kile kinachoendelea nyumbani ..”.
“Akishaanza kukolea shule , nadhani atakusahau kama mama yake?”
“Kama kuna mtu wakunisahau ni wewe mwanaharamu , ndio maana hata Lanlan hakujali kama baba yake”Aliongea Edna huku akitangulia mlangoni na Roma hakutaka kuongeza neno , isitoshe tokea Lanlan aje kwenye maisha yake siku zote atakuwa ni wa pili kwenya moyo wa Edna hivyo aliona ni kheri kuridhika na nafasi yake.
Baada ya kushuka chini Yezi na babu yake walikuwa tayari washafika mezani kwa ajili ya kifungua kinywa na Park juan aliwakaribisha wajiunge pia, lakini wakati huo huo akiwa na shauku ya kutaka kumjua Roma zaidi kutokana na kile kilichotokea siku ya jana.
Wakati wakiwa kwenye kifungua kinywa Edna alichukua nafasi hio kuelezea nia yao ya kutaka kurudi nchini Tanzania kwani ziara yao nchini hapo ilikuwa imekamilika kwani kama ni kushuhudia Yezi kitanganzwa kama mrithi wa mali za Park juan waliweza kushuhudia hivyo hakukuwa na jambo la ziada ambalo lingewabakiza hapo zaidi.
Yezi mara baada ya kusikia kuhusu wenza hao wakiaga , alijikuta moyo wake ukipatwa na huzuni kwani alitamani wabakie angalau kwa muda mrefu kidogo kumpa kampani.
“Kama ni hivyo nitawaandalia mimi tiketi, mnapanga kuondoka lini?”Aliuliza Park Juan lakini kabla hata hajajibu simu yake ilianza kuita na alipoitoa aligundua inatokea Tanzania na anaepiga ni mama mkwe wake.
“Hello.. mama.. kila kitu kinaendaje , Lanlan!!?.. , nini kimtokea? Ah imetokeaje?”Alionekana Edna akiongea kwa wasiwasi na kufanya kila mmoja kujua simu hio ilionekana imebeba ujumbe ambao haukuwa mzuri.
“Mama amesemaje?” Aliuliza Edna mara baada ya kumaliza kuongea na simu.
“Ni Lanlan..!”Aliongea Edna huku akionyesha kukosa utulivu
“Mama anasema jana Lanlan shuleni kwao walikuwa na Event ya kimasomo na imetokea Lanlan kupigana na wenzake”
“Kavunja mbavu za wenzake nini ?”Aliongea Roma kwa kutania
“Unaongea nini wewe, Lanlan hawezi kugombana na wengine bila sababu”
“Ni vizuri kama hakuna aliepata majeraha makubwa , lakini haina haja ya kunifokea hata kama nimekuwa sio wa muhimu kwako kama Lanlan siku hizi”Aliongea Roma akionyesha hali ya kukubali kushindwa ,
“Unaonaje tukiondoka baadae ya leo?”Alipendekeza Roma.
“Nadhani itakuwa vyema kama tukiondoka sasa hivi , tunatakiwa kwenda shuleni kwao kwani tumeitwa kama wazazi wake”Aliongea Edna na Roma hakutaka kupinga , kama Lanlan alikuwa kwenye matatizo inamaanisha kwamba hata yeye pia ni swala linalomuhusu.
Kutokana na kuwa na bahati pamoja na hela waliweza kupanda ndege ya shirika la Qatar airways mpaka Doha Qatar na kisha wakapanda ndege ya shirika hilo hilo mpaka Dar es salaam , walitumia takribanni masaa ishirini na nne mpaka kufanikiwa kufika nchini Tanzania.
Walifika asubuhi ya saa mbili kwenda tatu na siku hio Lanlan alipaswa kutangulia kwenda shuleni kwao , lakini aliwagomea nyumba nzima na kuwaambia haendi.
“I’m not going! Lanlan doesn’t wanna go!”Aliongea Lanlan asubuhi hio baada ya kuvalishwa Track Suti na Qiang Xi lakini aligoma kwenda na sasa alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa amepandisha miguu yote ameikunja akileta kiburi kwamba hataki kwenda.
Katika shule yao ya kimataifa ya Braeburn tawi la Dar es salaam sehemu ambayo alikuwa akosomea walikuwa na vipindi maalumu vya matukio wakati wa likizo,hayakuwa matukio ya kusoma bali ya michezo ili kuwaweka wanafunzi sawa na juzi yake baada ya kushiriki kwenda shule ndio likatokea hilo tukio.
“Lanlan kama hutaki kwenda shule niambie mimi bibi yako tukio zima lilivyotokea”Aliongea Blandina ambaye amesimama na Qiang Xi wakimwangalia Lanlan kwa wasiwasi huku wakionyesha sura za kujikatia tamaa kumbembeleza.
Muda huo huo mlango ulifunguliwa na wote kujikuta wakigeuza macho na baada ya kumuona Roma na Edna ambao wameshikilia masanduku walijikuta wakijawa na ahueni.
“Mommy!”
Lanlan mara baada ya kumuona mama yake alitoka nduki na kumrukia na kama mtu asingekuwa na mazoezi basi angedondoka nae , Lanlan alikunja mikono yote kwenye shingo ya mama yake akionekana alikuwa amemkubuka.
Lakini muda huo huo Edna alijikuta akishangaa mara baada ya Lanlan kuanza kutoa kilio
“Aww.. Lanlan unalia nini , niambie mama nini kimetokea?”Aliongea Edna huku akimuonea huruma na kumfuta machozi kwa mkono wake wa kulia.
“Asante Mungu Edna umerudi, maana kichwa kinataka kunipasuka , Lanlan tokea asubuhi analeta ugumu wa kukataa kwenda shule na mwalimu wake amekuwa akipiga tumpeleke kwani wazazi wa mtoto aliepigwa wamechachamaa na wapo shuleni”
“Huyo mtoto amekufa?”Aliuliza Roma.
“Wewe mtoto unaongeaje hivyo, kama amekufa ungetukuta hapa?”Aliuliza Blandina huku akimpiga Roma kwenye mkono.
“Lanlan mwambie mama kilichotokea shuleni ni nini , siamini kama unaweza kupiga wanafunzi wengine bila sababu?”Aliuliza Edna kwa kingereza na kumfahya Lanlan kufuta kamasi na kuanza kuelezea.
“Lanlan alimuona yule Hamadi akimpiga Nurya , hiyo .. hivyo Lanlan alitaka kumsaidia Nurya asipigwe lakini Hamadi akaleta wenzake wakitaka kunipiga hivyo Lanlan nikawapiga wote na nikanyofoa nywele zake”Aliongea Lanlan kwa kutia huruma na kisha akainamisha uso wake chini.
Lakini wengine wote walijikuta wakishangazwa na jambo hilo , kwani licha ya kusikia Lanlan amepiga mtu shuleni hawakuwa wakijua nini kimetokea zaidi ya kupigiwa waende shuleni na Lanlan.
“Nurya ni rafiki yake na Lanlan na kuhusu Hamadi ni moja ya watoto wakorofi ndani ya darasa analosoma Lanlan”Aliongea Qiang Xi ambaye alikuwa anayaelewa mazingira halisi ya Lanlan shuleni kwao kwani alikuwa akienda mara kwa mara.
“Kilichotokea kishatokea , kama wazazi wa huyo Hamadi wanataka kutushitaki kwa mtoto wao kuumizwa hakuna jinsi na sisi tutapambana kwa upande wetu”Aliongea Edna.
“Kama ni hivyo una mpango gani kichwani au tutumie njia za mkato kutatua hili?”Aliuliza Blandina.
“Lanlan ni mtoto wetu , kama kuna mambo yametokea sisi kama wazazi tunapaswa kuwajibika, mwalimu wao si amesema twende nae shuleni kwao basi tutaanzia huko”Aliongea Edna.
Hakukuwa na sababu ya kubakia tena nyumbani, hivyo hata kukaa chini hawakukaa zaidi ya kumchukua Lanlan na kwenda nae hadi shuleni kwao.
Ijapokuwa Lanlan hakutaka kwenda shule kutokana na woga uliomwingia lakini alikubali kwenda na mama yake baada ya kuambiwa hivyo.
Upande wa Roma aliona ni tatizo dogo sana , kama mtoto hajafa haina haja ya kusumbuana, isitoshe Lanlan ameseima amenyofoa nywele kidogo tu kwenye kichwa cha mwenzake.
Lakini hayo yalikuwa mawazo yake , kwani upande wa Edna alikuwa na wasiwasi na alichukulia ni tatizo kubwa.
Upande wa Roma huenda hio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwajibika kama baba kwani tokea Lanlan afike hapo hakuwahi kupatwa na changamoto yoyote ambayo ilimhitaji yeye kama baba kuwajibika.
Lanlan muda wote alikuwa ameng’ang’ania mkono wa mama yake akionyesha wasiwasi , wakati wakiingia katika ofisi ya mwalimu.
Baada ya kuingia ofisini , licha ya uwepo wa walimu baadhi wakike, walikuwepo wazazi wa mtoto aliefahamika kwa jina la Hamadi ambaye wazazi wake wote upande wa mwanaume alikuwa na asili ya kihindu na upande wa mwanamke alikuwa na asili ya kiarabu , wazazi wa mtoto Nurya pia walikuwepo na mtoto wao wakiwa wamejitenga pembeni , walionekana kuwa wapole mno.
Hamadi ambaye alikuwa amefungwa bandeji kichwani alionekana karithi mwili wa baba yake , kwani wote wawili walikuwa na mwili wa kibonge , na kwa muonekano wao ilionyesha ni watu waliokaa kishari shari kwani sura zao zilikuwa zimekunjamana mara baada ya kumuona Edna na Roma wakiingia hapo ndani.
Lakini yule mwanaume kibonge mara baada ya kumuona Edna alijikuta akimwangalia kwa mshangao , ilionyesha dhahiri alikuwa mzee wa totozi na mke wake hakupendezwa na macho ya mume wake.
SEHEMU YA 536.
“Nyie sikilizeni , mtoto wangu hajainua mkono wake kumgusa mtoto wenu kabisa na yeye ndio kaanza kumsukuma mtoto wangu na kudondoka chini na baada ya hapo akamnyofoa nywele na kumfanya kutokwa na damu na hata sasa bado damu zinamtoka, hio ndio tabia ambayo mnamfuza mtoto wenu?”Aliongea Mama Hamadi kwa hasira na kiswahili chake ambacho hakikuwa na rafudhi nzuri na palepale alimfinya mume wake ambaye alikuwa muda wote akimwangalia Edna kwa mshangao aongee na yeye kumsapoti.
“Hakika ukorofi wa namna hii hatuwezi kusamehe , naapa kama hamtapiga magoti na kuomba msamaha hatuwezi kuruhusu hili lipite”
“Kwa maelezo tuliosikia ni mtoto wenu Hamadi alieanza kumchokoza Nurya na baada ya kuzuiwa na mtoto wangu ndio akaenda kuita wenzake kumshambulia , kama sio uwezo wake na kipaji chake huenda angeumia yeye, hivyo kama kuna anaepaswa kuwajibika hapa sio upande mmoja bali kwetu sisi wote”Aliongea Edna.
“Upo sahihi , hiko ndio kilichotokea “Aliongea mwalimu Aneth.
“Jamani hili swala limekwisha kutokea , hivyo Lanlan atamwomba msamaha Hamadi kwa kile kilichotokea na Hamadi vilevile atamuomba msamaha Nurya na Lanlan kutokana na kuwachokoza , na Hamadi kwanzia leo upunguze tabia yako ya ukorofi”Aliendelea kuongea mwalimu Aneth, akionyesha kwamba hakuwa akitaka mambo yawe makubwa na isitoshe yeye ndio aliekuwa msimamizi wao.
“Mtoto wangu hawezi kuomba msamaha , yeye ndio kakosewa mpaka kumpelekea kupatwa na majeraha ya kichwa, mwalimu nadhani unatuchukulia kiwepesi kwasababu hawa ni matajiri kutuzidi , mimi baba Hamadi siwezi kukubali mpaka nione mtoto wangu kaombwa msamaha kwa kile alichofanya na sio yeye tu lakini pia wazazi wake watuombe msamaha kwa niaba ya mtoto wao”Aliongea kibabe na kuwafanya walimu wengine kushindwa kujua namna ya kumaliza tatizo , kwani wazazi wa Hamadi walikuwa wana jazba sana.
“Tutalipia gharama za matibau kwa mtoto wetu na kisha wataombana msamaha na mambo kuisha kama alivyosema mwalimu”Aliongea Edna.
“Wewe mwanamke ni kiziwi au unajifanya husikii , haujamsikia miume wangu alichosema , hatutaki hela zako , tunachotaka ni nyie wawili kuomba msamaha kwa niaba ya mtoto wenu”
“Unapata wapi ujasiri wa kumfokea mke wangu?”Aliongea Roma aliekuwa kimya muda wote na kauli yake iliambatana na vitendo kwani alimpiga teke mguuni Mama Hamadi na kuwafanya kila mmoja kushangazwa na kitendo chake.
“Roma kwanini unafanya hivyo , mpaka sasa hatujui namna ya kumaliza tatizo na unaongeza tatizo”
“Kuzungumzia maswala ya watoto hapa ndio kilichotuleta , lakini kukufokea wewe ni jambo lingine , hivyo asipotuliza domo lake kama bakuli namuongezea, ni swala la kikanuni kwangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushindwa kuongea chochote, matendo yake ni kwamba alikuwa akionyesha kumjali lakini matokeo hakuridhika nayo.
“Wewe ni nani? Unapata wapi ujasiri wa kunipiga, unanijua mimi wewe?”Mama Hamadi aliamka huku akifoka na ule weupe wake ulibadilika na kuwa wekundu kiasi kwamba hata shungi aliofunga kichwani ilianza kumtoka na nywele zake ndefu kuonekana.
“Mimi ndio baba wa binti yangu na mume kwa mke wangu, na uache tabia ya kumfokea mke wangu kwa wivu wako”
“Wivu?Kwannini niwe na wivu juu yake?”Aliongea , lakini baadhi yao hawakuwa wakimjua Roma kama alikuwa mume kwa Edna, hata hivyo hakuwa maarufu sana.
“Roma mchukue Lanlan uende nae hadi kwenye gari , niachie mimi nitalimaliza hili swala”Aliongea Edna mara baada ya kuona Roma akiendelea kubakia hapo ndani swala linaweza kufikia pabaya zaidi na Roma hakuwa na haja ya kuendelea kukaa hapo ndani kwani ni kweli alijua uvumilivu ungemshinda na kuishia kumvunja mtu shingo.
“Kwahio ndio unakimbia sio?nani kakuruhusu uondoke?”
“Wewe mwanaharamu , unapaswa kupiga magoti na kuomba msamaha kwa kumpiga mke wangu na mtoto wako kumdhuru mtoto wangu’Alifoka Baba Hamadi.
“Naweza kukuadhibu hata wewe ukiendelea na maneno yako”Alitishia Roma
“Mzazi wa Hamadi tunaomba tuwe na maongezi kama watu waliostaarabika”
“Achana na mimi wewe”Aliongea na kisha aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali na kutoa simu.
“Nilidhani ninaenda kuwasamehe mara baada ya kuomba msamaha , lakini naona mnajifanya wajuaji , ngoja tuone nyie na sisi nani zaidi”Aliongea kwa jeuri bwana Mhindi ambaye ni baba yake na Hamadi , ilionekana ndio maana hata mtoto wao ni mtukutu , kumbe tabia karithi kwa baba yake na mma yake.
“Rasta ni mimi, kuna kitu nadili nacho muda huu katika shule ya Braeburn , kuna jitu limempiga shemeji yako licha ya mtoto wake kumuumiza mtoto wangu , leta vijana wakutosha haraka wamshikishe adabu, nitahakikisha vijana wako wanapata malipo mazuri katika hili”Aliongea na mara baada ya kukata simu alimwangalia Roma.
“Kama kweli wewe ni jasiri usikimbie , lakini nakuhakikishia hata utoke hapa lazima nitakukamata na kukushikisha adabu , hakuna mtu ambaye anaweza kunichokoza ndani ya jiji hili mimi”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa kejeli , hakuamini mara baada ya kuondoka muda mfupi ndani ya jiji la Dar kuna makundi ya ajabu ajabu yameamka.
Upande wa Edna hakuelewa wazazi hao walikuwa watu wa aina gani mpaka kushindwa kuelewa na kukubali mambo madogo kama hayo kuisha.
“Roma tunafanyaje?”Aliuliza
“Tutasubiri hapa hapa , ninashauku ya kuona ni watu gani ambao anakwenda kuwakusanya”Aliongea Roma kwa sauti.
“Bado unajifanya kuwa jasiri ,usije tu kujikojolea wakija kufika hapa”Aliongea kwa kujigamba.
Walimu wa shule hio walijikuta wakianza kujawa na wasiwasi, wazazi wa Nurya pia walionekana kuwa na wasiwasi kwani hawakuzoea mitafaruku na walitaka jambo hilo liishe kiamanni.
Dakika kaka kumi na tano iliingia Noah ya rangi nyeusi ndani ya eneo hilo na kwa jinsi walivyoingia ilionyesha walifanya vurugu getini na kupita, walikuwa watu kama kumi hivi wote walioshikilia virungu, walionekana kama mabodigadi , wakiwa na sare zao za rangi nyeusi na baada ya kutoka kwenye gari walisogea mbele na kupanga mstari huku wakimwangalia Roma.
Bwana ambaye alikuwa na mwili uliotuna mwenye rasta kichwani akiwa amesikilia sigari akivuta alimsogelea Baba Hamadi, alionekana yeye ndio alikuwa kiongozi wa kundi.
Baada ya kusogeleana walionekana kuongea jambo ndani ya dakika chache na kisha akamnyooshea Roma kidole.
Muda huo Edna na wale walimu ndio walikuwa na waswasi lakini Lanlan na Roma wote walikuwa kwenye mchecheto wa furaha.
“Wewe ndio unapata ujasiri wa kumchokoza Mr Wambi?”Aliongea yule bwana na mara baada ya kugeuka na kumwangalia mwanaume aliekuwa amempa mgongo alijikuta akishituka.
“Master Roma..!!”Aliongea kwa kutetemeka Roma alikuwa akimjua mmoja wapo wapo wa hao vijana.
“Ah! , kumbe ni wewe Rasta , nilikuwa nikijiuliza ni Rasta gani huyo anapigiwa simu , kumbe ni wewe mbwa kichaa usie na meno , lakini sijashangazwa na uwepo wako hapa”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa mara baada ya kuona anamfahamu mwanaume huyo aliekuja na kundi lake la watu waliokaa kijambazi.
“Hubby Rasta ndio nani?”
“Unakumbuka namna tulivyokutana , mtu ambaye alihusika kukuwekea dawa ya usingizi kwenye kinywaji ni huyu mwanaume”Aliongea Roma huku akimgonga gonga vibao vya mashavuni bwana aliefahamika kwa jina la Marasta
Na Edna alikumbuka tukio ambalo lilimtokea katika hoteli ya JR , tukio ambalo lilimfanya kukutana na Roma.
“Rasta yupo katika kundi la Black Mamba , baada ya Rose kuteka jiji lote hili upande wa underwold na kuwa na nguvu aliunganisha makundi yote kuwa chini yake na ndio bwana huyu Marasta alivyoweza kupanda cheo mara baada ya kuacha kufanya kazi chini ya bosi wake Abubakari Hamadi”Aliendelea kuongea Roma na kumfanya Edna kuelewa , lakini hapo hapo alijikuta akijawa na hasisra juu ya mtu huyo ambaye yuko mbele yake mara baada ya kugundua alihusika katika kumuwekea dawa ya usingizi katika kinywaji.
Marasta alionyesha kuuwa na wasiwasi mno mara baada ya kumuona Roma eneo hilo , kwani hakumtegemea kabisa na isitoshe hakuna mtu ambaye ypo ndani ya kundi la Black Mamba na la Tembo ambaye hamfahamu Roma , kila mmoja aliweza kusikia namna ambavyo Baba yake Rose , bwana Situ alivyolishwa kwa Papa na Roma.
“Master Roma , Mrs Edna sikutarajia kama nitakutana na ninyi eneo hili, kama ningejua mapema ni wewe nisingeleta vijana ndani ya hili eneo”Baba yake Hamadi ambaye aliitwa na Rasta kwa jina la Wambi alishangazwa na mabadiliko hayo na kuzidi kuwa na wasiwasi pamoja na hasira juu.
“Rasta unamjuaa huyu mshenzi ?”Aliliuliza yule bwana mhindi na kumfanya Marasta kutamani kumpiga ngumi palepale , lakini alijitahidi kutuliza hasira zake na kumvuta pembeni ili kumuwelesha.
“Mr Wambi nafikiri unapaswa kupotezea hili swala ,yule mwanaume sio mtu ambaye unaweza kuchokoza”
“Kwanini nisimfanye chochote , yeye ni nani?”
“Elewa tu Master Roma ni mtu ambaye sisi kundi la Tembo hatuwezi kukiuka maagizo yake”
“Nyie ni waoga , inamaana unashindwa kuelewa nguvu iliokuwa nyuma yangu mpaka unashindwa kumwadabisha huyu mshenzi?”
“Kama unataka kufanya hivyo fanya wewe mwenyewe , ila siwezi kuhatarisha maisha ya vijana wangu”aliongea Rasta na kisha akawapa ishara vijana wake waingie kwenye gari kuondoka kwenye hiloe haraka lakini Roma aliwazuia.
‘Hamuwezi kuondoka , bado hali haijatulia”Aliongea Rona na kumfanya Rasta kuingiwa na ubaridi.
“Master Roma naomba utusamehe najua tumekosea lakini hatukuwa tukijuwa kinachoendelea”
“Ni kwasababu nimekaa nje ya jiji la Dar es salaam kwa kuda wa mwezi ndio maana nyie watu mnafanya mnavyotaka , inamaana kundi la Tembo siku hizi limegeuka kuwa la wahalifu wa kukodi?”
“Kundi kwasasa halipo sawa kama kipindi likiwa chini ya Boss Rose, lakini hata hivyo kiongozi mpya wasasa sio mbaya pia”
“Kwahio huyu mtu hapa akiwaita popote mnaenda na kuanza kumnyenyekea?”
“Master Roma huyu bwana ana koneksheni kubwa ambayo ipo nyuma yake na hawa ni sehemu ya watu ambao tunajitahidi kwenda nao sawa ili wasije wakafanya maisha yetu kuwa magumu na kuishia kushikiliwa na polisi”Aliongea na kumfanya Baba Hamadi aliekuwa kwenye hali ya uwoga kuingiwa na hali ya kujiamini mara baada ya Rasta kuanza kusifia watu waliokuwa nyuma yao.
“Rasta siku hizi hutaki kufanya kazi yako vizuri si ndio , kumbuka nikipiga simu moja tu wote nyie mtakuwa kituo cha polisi na hakuna ambaye anaweza kutoka”
“Mr Wambi hakuna mahali ambapo tumekukosea , hivyo tunaondoka”
“Yaani niwaite halafu muondoke , kama msipotafuta namna ya kumuadhibu huyu mshenzi nitahakikisha wahusika wa kundi lenu mnaenda gerezani , msisahau wengi wenu mafaili yenu yapo kituoni, ni mwendo wa kufufua kesi zenu tu”Aliongea na kumfanya Rasta kuonyesha hali ya wasiwasi.
“Achana nae , hakuna chochote kitakachowapata , kwasasa nataka unisikilze mimi ninachoongea”Aliongea Roma.
“Ndio mr Roma, ni maagizo ganni unataka tuyafanyie kazi?”
“Nataka mumshikishe adabu, wewe na vijana wako”Aliongea Roma na kumfanya Rasta kushangaa.
“Acha kushangaa , nimesema mpigeni mpaka aombe msamaha”Aliongea na kumfanya Rasta kuanza kutetemeka kwa woga , akishidnwa kujua ni maamjuzi gani ayachukue
“Rasta acha kuwa mjinga , kama unataka kwenda jela msikilize na kama unataka kuishi hakikisheni mnampiga”Aliongea Mr Wambi lakini hakukuwa na namna ya Rasta kwenda kinyume na maagizo ya Roma kwani aliamini muda wowote angeweza kufa , hivyo moja kwa moja aliona njia pekee ya kujiokoa katika hio adha ni kumpiga Mr Wambi mpaka aombe msahama.
Dakika chache tu Mhindi aliweka chini na kuanza kupigwa mateke na virungu , aliishia kupoiga kelele za malalamishi lakini hakuna ambaye alimsikiliza zaidi ya kupigwa.
Roma mara baada ya kuona wale walimu walivyokuwa wakiogopeshwa na hali hio alitabasamu.
“Mimi ni mtu mwenye kinyongo sana , yeye si ndio kaita watu kunipiga sasa lazima arudishiwe”Aliongea Roma.
Upande wa Lanlan mara baada ya kuona tukio lile alijikuta akifurahi mno na kukunja ngumi akitaka kujiunga kumpiga yule mwanaume.
“Angalia unavyomharibu mtoto , anaiga kila kitu unachokifanya”Aliongea Edna
“Kuna haja gani ya kuogopa , kwanini usiongee na Lanalna namna ambavyo ameweza kumsaidia rafiki yake kwa kuwaadhibu maadui zake , sio tatizo kupiga mtu pale anapotaka kukupiga”Aliongea Roma na kisha aliwapa ishara vijana waache kupiga.
“Nadhani umeweza kupata adhabu yako , sasa kifuatacho ni kupiga magoti na kutuomba msamaha na kisha ukubali mbele ya walimu mtoto wako ndio mwenye makosa , kubali ulikuwa ukituletea dharau na kisha omba msamaha na tutaachana kwa amani”
“Mimi ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama tawala , huwezi kunifanyia hivi mimi”
“Niachie ujinga”Aliongea Roma na kumpiga teke na kumfanya kudondoka tena chini akiugulia maumivu.
“Kwahio ukiwa mjumbe wa halmasharuni ya chama inanihusu nini , kwanza nani kakupigia kula mpaka ukafika huko ?”Aliongea Roma.
“Master anachoongea ni kweli , ni mjumbe na mwanachama hai wa chama cha Mageuzi(CCM), lakini kafikia huko kutokana na sapoti kutoka familia ya Mzee Longoli kutoka Zanzibar, Mzee Longoli mtoto wake ni raisi wa Zanzibar na kamuoa dada yake”Aliongea.
Alichokuwa akimaanisha Rasta ni kwamba dada yake Mr Wambi kaolewa na raisi wa Zanzibar, raisi wa Zanzibar baba yake ni mzee Longoli.
Roma mara baada ya kusikia jina la Mzee Longoli alijikuta moyo wakuua ukimvaa , palepale alikumbuka watu ambao waliiba damu yake ukiachana na Marehemu raisi Kigombola mmoja wapo alikuwa ni huyu Mzee longoli na kipindi kile alipotaka kumuua babu yake alimzuia na sio hivyo tu hata Afande Maeda alimzuia.
“Kwahio kurahisisha maneno yako , unamaanisha huyu bwana ana udungu na familia za viongozi wakubwa sio?”Aliongea Roma huku ghafla tu na mudi yake kurudi upya.
“Upo sahihi familia ya Mzee Lomgoli ndio watu ambao wanashikilia muungano wa Tanganyika na Zanzibar , ndio kama msingi ndani ya nchi ya Zanzibar hivyo wanashirikiana moja kwa moja na raisi wa Tanzania Bara”
“Asante kwa kunielewesha , nadhani sasa hili jambo nilichukulie siriasi kama huyu mtu nikimuacha aende hivi hivi naamini atarudi na kuanza habari za kunishitaki, hivyo kabla ya hayo hayajatokea , wewe bwana mhindi sijui mwarabu koko piga magoti na uombe msamaha kwa niaba ya mtoto wako na mkeo mambo yasiende mbali”
“Mr Roma haina haja ya kuendelea na hili, kama vipi liishe na kila mtu aondoke hapa kwa amani”Alianza kujirudi akitaka sasa kuyamaliza.
‘Utapiga magoti au hutopiga?”Aliongea Roma huku awamu hii Roma akibadilika na kumsambazia nguvu ya kijini ya kumwingiza woga.
“Nitapiga , nitapiga”Aliongea
“Okey fanya hivyo na usisahau kuongea kwa sauti kwamba ulinikosea mimi na mke wangu pamoja na mtoto wako akamkosea binti yangu mrembo pale”Aliongea Roma na kisha alitoa simu yake na kuanza kumrekodi akipiga magoti na Mr Wambi mhindi alifanya kama alivyoambiwa, alipiga magoti na kusema amekosea yeye na mtoto wake ndio alikuwa mkorofi.
“Mr Roma tunaweza kuondoka sasa?”Aliuliza na kumfanya Roma kumgeukia Edna ili kujua kama na yeye ana adhabu ya kutoa , lakini Edna hakuongea zaidi ya kuingiza mkono wake kwenye mkoba na kisha akatoa karatasi ya cheki na kucharaza maandishi na kisha akampatia.
“Hii ni pesa ambayo inatosha kama fidia kwa yaliomkuta mtoto wako , naomba msamaha kwa niaba ya matendo ya binti yangu , hibyo naamini baada ya hapa utaacha swala hili lipite”Aliongea Edna na kumpatia karatasi ile mke wake Mr Wambi ambaye muda wote alikuwa kimya akimwangalia mume wake akitaabika.
Baada ya wale wazazi watukutu kuondoka , sasa hali ilionekana kurudi kwenye utulivu na ambao hawakuwa wameondoka ni kundi la watu wa Tembo.
“Mr Roma naamini lazima atarudi kulipiza kisasi , lakini sisi tunakuamini wewe, nadhani tukipelekwa kituoni kuhojiwa utatusaidia kutoka”
“Haina haja yakuwa na wasiwasi , kama atataka kulipiza kisasi mtu atakeanza nae ni mimi”
“Inawezekana Master Roma , lakini ndio hivyo hofu yetu ni kutokaa na familia yake kuwa na nguvu sana ndani ya upande wa Visiwani”
“Nishesema acheni wasiwasi , ondokeni sitaki kuwaona tena hapa”Aliongea Roma na kuwafanya wote waingie kwenye gari na kisha kupotea eneo hilo na kufanya eneo hatimae kuwa kimya.
Edna ilibidi kwanza aombe msamaha kwa kile kilichotokea kwani ilikuwa ni uchafuzi wa mazingira wa aina yake , lakini licha ya hivyo hakuna mwalimu ambaye alikuwa na ujasiri wa kuonyesha kutoridhishwa ,isitoshe sio kwmaba hawakuwa wakimjua Edna na Roma walikuwa wakielewa licha ya kuwa matajiri lakini familia zao zina koneksheni kubwa na wanasiasa.
“Nurya yule Hamadi hawezi tena kukuchokoza kwanzia sasa , tunaweza kuedelea na..”Aliekuwa akiongea ni Lanlan na kabla hajamaliza sentensi yake Nurya alijificha nyuma ya mama yake , alionekana kumuoogpa Lanlan.
Lanlan aliweza kujenga ukaribu na msichana huyo kutokana na kwamba alikuwa akielewa lugha ya kingereza vizuri tofauti na wanafunzi wengine.
Lanlan mara baada ya kuona rafiki yake anamuogopa , alijikuta akipoteza furaha palepale na kumgeukia mama yake na kumwangalia kwa huzuni na kujikuta akianza kuangaa kilio.
SEHEMU YA 537.
Kila mmoja alishangazwa na tukio lile na hata mama yake na Nurya alijisikia vibaya na kumwangalia mtoto wake.
“Nurya kwanini unajificha , wakati rafiki yako anajaribu kukuongelesha?”Aliongea mama yake lakini bado Nurya alionyesha hofu mbele ya Lanlan , huenda ni vile ambavyo aliweza kumshuhudia Lanlan akishindana na kundi la watu wengi kwa wakati mmoja.
“Nurya..you ,… don’t ignore Lanlan?”Aliongea Lanlan huku akiendelea kulia na kumfanya Roma aliekuwa akifikiria kujikuta kama kuna kitu kimemgusa kwenye eneo la moyo wake mara baada ya kuona Lanlan anavyolia na kuomba rafiki yake asimkatae na palepale alijikuta mawazo yakimrudisha nyuma sana.
Edna mara baada ya kuona mtoto wake analia mara baada ya Nurya rafiki yake kuonyesha ishara ya kumkataa , alijikuta moyo wake ukiuma na kumkumbatia kumpoza.
“Lanlan usilie , usilie kipenzi changu ,unaonekana mrembo hata ukilia oo..”Alijaribu kumbembeleza lakini Lanlan bado aliendelea kulia
Wazazi wa Nurya hawakuwa wakijua kipi cha kufanya zaidi ya kukaa kimya kwani hawakuwa na uwezo wa kumsemea mtoto wao mdogo kile anachokifikiria ukilinganisha bado alikuwa mdogo.
“Miss Edna labda kuna jambo hujapata kulijua , Jana mara baada ya tukio kutokea watoto wote walijitenga na Lanlan na hawakutaka kucheza nae tena , walionyesha kumnyanyapaa…”
Aliongea na kuanza kuwalezea na Edna aliona inaleta maana kwa Nurya kumuogopa Lanlan , ijapokuwa ni kweli Lanlan alipigana kwa ajili ya kumsaidia rafiki yake , lakini kitendo cha kuwpiga wavulana karibia sita wote na hata kumtoa damu Hamadi ni jambo ambalo mtoto mdogo wa kawaida hawezi kulifanya na baada ya watoto wenzake kuona Lanlan anatisha ndio walianza kujitenga nae.
Edna kutokaa na kumjali Lalan alizidi kuumia akimwangalia mtoto wake kuwa katika huzuni kwa kutokana na rafiki yake aliekuwa akimjali kumuogopa.
Alikumbuka hata yeye kutokan ana ukauzu wake aliokuwa nao kpindi akiwa anasoma hakuweza kupata marafiki, hivyo ni kama alikuwa akijua kile Lanlan anachopitia.
“Mume wangu tunafanyaje Lanlan ana huzuni sana?”Aliuliza Edna na kumshtua Roma ambaye alikuwa kwenye mawazo na sasa kumwagalia Lanlan aliekuwa akilia na kisha akageuza macho yake kwa Nurya ambaye alikuwa akiogopa kuongea.
“Mwache alie kwa muda mtoto anaetoa machozi mara kwa mara ni mzuri zaidi kuliko asielia”
“Unaongea nini , unashindwaje kumfariji mtoto wako mwenyewe?”Aliongea Edna na kumpotezea Roma na kisha alimwangalia Lanlan.
“Baby mama atakupeleka sehemu nzuri kwa ajili ya kula , nitakununulia chochote unachotaka”Dakika hio hio Lanlan mara baada ya kusikia kuhusu chakula kidogo hali yake ilirudi.
“Nataka nyama”
“Nyama gani nataka?”
“Beef”Aliongea na baada ya Edna kuona amenyamaza na kurudiwa na mudi yake kidogo alipatwa na ahueni.
Baada ya kuwaaga walimu na wazazi wa Nurya waliondoka katika shule hio na kutafuta mgahawa mzuri wa kisasa ambao waliamini ungeweza kuwahudumia chakula , hata wao wenyewe walikuwa na njaa maana hawakupata kula chochote tokea wafike nchini.
Walichagua sehemu ambayo haikuwa na mwingilianao mkubwa na watu na bahati nzuri mgahawa huo ulikuwa na vyumba maalumu ambayo vlikuwa na meza tatu kwa ajili ya wateja na Edna aliamua kununua meza zote ili asiingie mtu mwingine, maana alijua Lanlan na udogo wake akianza kula macho ya wengi humuangalia kwa mshangao.
Nusu saa mbele wote walikula wakashiba na Lanan alikula kile alichopenda kwa furaha zote.
“Lanlan umeshiba?”
“Ndio , lakini mama kwanini wengine wananiogopa mimi Lanlan, Je hawampendi Lanlan?”
“Hawakuchukii Lanlan , wewe ni mtoto mzuri sana umeweza hata kumlinda rafiki yako”
“Lakini kwanini Nurya hataki kucheza na mimi tena na ananiogopa?”Aliongea Lanlan , ilionekana alitaka kwanza kula ashibe ndio aanze kulalamika kwani hali yake ya huzuni imerudi yote na kumfaya Edna kuingiwa na huzuni.
Roma alimwangalia mke wake ambaye tayari machozi yapo karibu kwa kumuonea huruma Lanlan na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha.
“Unaonaje ukilipia, utatukuta nje”Aliongea Roma na kisha alimbeba Lalan juu na kutoka nae nje.
Baada ya kutembea kidogo umbali mfupi kutoka mgahawani hatimae waliweza kuona sehemu yenye bustani iliojengewa kwa ajili ya mapumziko na Roma aliona hio ni sehemu sahihi kwa wao kukaa kupumzika.
Edna muda wote alikuwa nyuma nyuma na ilikuwa afadhali mtaa huo haukuwa na watu wengi kutokana na majumba mengi kuwa ya mageti.
“Lanlan nikusimulie stori?”Aliuliza Roma na Lanlan alitingisha kichwa .
“Lanlan anapenda kusikiliza stori”Alijibu na kisha Roma alianza kumsimulia na hata Edna aliekuwa pembeni alikuwa akipenda stori na alitega sikio vizuri kusikiliza.
“Hapo mwanzo kulikuwa na kijana mdogo , ijapokuwa alikuwa mdogo lakini alikuwa na nguvu kushinda hata watu wakubwa , anaweza kukimbia kwa haraka na kuweza hata kupasua jiwe na ngumi yake moja tu , kijana mdogo aliishi sehemu ambayo kuna Vijana wengine ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa akili pamoja na nguvu , wakijifunza kwa pamoja kila siku namna ya kutumia bundiki , visu , ngumi na sumu , kwenye maisha ya Kijana mdogo ilikuwa ni kuua au kuuliwa…...”Roma aliendelea kusimulia na Lanlan alijikuta akiongeza umakini na kumfanya Edna kupata ahueni mara baada ya kumuona Lanlan , lakini pia alihisi anachosimulia Roma ni kama stori yake ya maisha.
“Siku moja kijana alipewa misheni ya kuishi katika kituo cha kulelea yatima kwa ajili ya kutafuta namna ya kumuua mfadhili mkuu wa kituo hiko , alipewa kazi ya kufanya hivyo kutokana na kwamba mkuu huyo licha ya kufadhili kituo hiko , lakini pia alikuwa akiwachukua watoto hao na kwenda kuwauza kwa kuwasafirisha nje ya nchi.
Kijana mdogo alifanikiwa kukamilisha misheni yake kwa ufanisi mkubwa , lakini kutokana na kuishi kwa muda kidogo na kundi lile la watoto Yatima alitokea kupenda mazingira na kuona utofauti uliokuwepo kati yake na wale watoto , Watoto wale aliokuwa akilingana nao umri walikuwa wakicheza na kufurahi na kuendelea na maisha yao pasipo kufanya vitendo vya kihalifu kama yeye.
Kijana mdogo alijawa na shauku na kuwauliza wale wenzake ni kwanini wao walikuwa wakitabasamu muda wote na kuwa na furaha , ilihali yeye aliikuwa akinuna muda wote na walimjibu michezo wanayocheza ndio inawafanya kuwa na furaha , baada ya kijana kuambiwa hivyo aliomba na yeye kufundishwa michezo hio na watoto wenzake hawakukataa, kwani walianza kumfudisha michezo mingi, katika siku alizokaa kijana mdogo katika kituo hiko aliweza kugundua kulikuwa na maisha zaidi ya kuua au kuuliwa ,hivyo maisha yake yakawa usiku anapewa misheni ya kuua na mchana anacheza na watoto Yatima, maisha ya kijana mdogo yaliendelea mpaka siku ambayo walikuja watu wengine kwa ajili ya kununua watoto kuwasafirisha na jambo lile lilimkasirisha kijana mdogo mara baada ya kuwaona wenzake wameswekwa kwenye gari hivyo kumpelekea kuchukua maamuzi ya kumuua mkuu wa kituo na wale watu , lakini mara baada ya polisi kuja na kuuliza nani kafanya mauaji watoto wote aliokuwa akicheza nao walimtaja kama ni yeye ndio kawaua hivyo polisi wakata kumchukua na kumpeleka kituoni”
“Kwanini waliamua kumtaja Kijana mdogo , licha ya kuwasaidia?”Aliuliza Lanlan.
“Kwasababu walikuwa wakimuogopa kijana mdogo kwa kile alichokifanya , walihofia kijana mdogo anaweza kuwaua pia , ijapokuwa watu wabaya walitaka kuwanunua na kwenda kuwauza mbali lakini angalau wasingewaua , hivyo kwao kijana mdogo aligeuka muuaji ambaye anaweza kuwaua muda wowote na mpaka hapo wakaona kijana mdogo ni mtu ambaye sio sawa na wao hivyo walimnyanyapaa, haikujalisha kijana mdogo alivyojitahidi kujenga nao ukaribu lakini watoto wale walijitenga nao na kujilinda na kijana mdogo na hawakutaka kumjua kabisa yeye ni nani?”
“Kama ni hivyo nini kimemtokea Kijana mdogo?”Aliuliza Lanlan kwa shauku.
“Wakati huo kijana alikuwa kwenye mshangao na mabadiliko ya watoto aliokuwa akicheza nao , amewaokoa kwa kuwasaidia lakini wakaamua kumuza kwa polisi hivyo wakati polisi anataka kumpeleka kijana mdogo kituoni , ghafla alitokea msichana mdogo na kuwashambulia wale polisi na kisha akamsogelea kijana mdogo na kumwambia , hukustahili kuwa hapa sehemu yako unaijua”Alisimulia Roma kihisia na kumfanya Edna kumwangalia Roma kwa huzuni pamoja na wasiwasi , alijua lazima simulizi hio inamuhusu yeye mwenyewe pamoja na Seventeen.
“Na baada ya hapo..?”Aliuliza Lanlan.
“Baada ya hapo kijana aliondoka na hakuweza kurudi tena na hkujaribu tena kuwa na urafiki na mtu wa aina yoyote , alikuja kuelewa rafiki yake pekee ni yule msichana mdogo ambaye anaweza kuua kama yeye na haogopi damu”
“Kama ni hivyo maisha si yalikuwa ya huzui na upweke sana?”Aliuliza Edna bila kujielewa.
“Hapana ,Msichana mdogo alimweleza kijana mdogo kwamba hapaswi kuwa na huzuni kwani yeye ana nguvu kuliko wao , wao ndio wanapaswa kuwa na huzuni, ukiwa na nguvu watu watakuonea wivu na watataka kuwa kama wewe hivyo sio jambo la kuhuzunika bali ni la kujivunia”
“Lanlan nimeelewa sasa , kwasababu Lanlan ananguvu kuliko wengine ndio maana wanamuogopa , Mimi Lanlan ni mzuri zaidi kuliko wao”Aliongea Lanlan mara baada ya kusimuliwa stori na kupewa nafasi ya kuuliza maswali na Roma
“Una akili sana , Lanlan unatakiwa kukumbuka hata mama yako ni mzuri zaidi kuliko wengine , hivyo mama mzuri lazima awe na Lanlan mwenye nguvu, wewe unaonaje?”
“Ndio”Alijibu huku akitabasamu.
“Unaongelea nini , usimfundishe mtoto huo ujinga”Aliongea Edna lakini Lanlan alimkumbatia Roma kwenye shingo kwa furaha.
“Also Lanlan Daddy is better than other children”
“Hehe..ofcourse”
******
Saa kumi kamili za jioni ndio waliweza kuanza safari ya kurudi nyumbani,Lanlan alikuwa asharejewa na hali yake ya kawaida kabisa na alifurahi kushinda na wazazi wake ambao hawakuwa nae kwa wiki kadhaaa.
Wakati Roma akirudi nyumbani aliweza kupigiwa simu na Mage akimwelezea juu ya mashtaka yaliofunguliwa na Mr Wamb.
Ilionekana Mr Wambi alikuwa na ushawishi mkubwa kwani mpaka Mage kufikia hatua ya kuona waasiwasi basi Roma aliona ni kama alivoambiwa , lakini hata hivyo hakujali kabisa kuhusu ushawishi wake.
Kwanza alikuwa na kisasi kwa mtu aliefahakima kwa jina la Longoli kutokaa na kula njama na maadui zake mpaka kuchukua damu yake , ijapokuwa wahusika waku ambao ni raisi Kigombpla na Yan Buwen kufariki lakini hakutaka kuona bwana Longoli akiendelea kuvuta hewa.
Siku baada ya Edna kwenda kazini na yeye pia ialienda kazini, kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea, baada ya wafanyakazi kumuona walionekana kukosa amani baada ya kumuona bosi wao.
Roma hakujali sana na aliishia kusalimiana na baadhi na kupanda kwenye lift ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka ofisini kwake na baada ya kufika eneo la mapokezi aliweza kumkuta Tanya aliekuwa tayari ashafka akiwa bize.
Aliishia kutabasamu na kisha mara baada ya kumwambia amefika aliingia moja kwa moja ofisini na kumwambia waonanae ili ampe taarifa za kila kilichoendelea kwa kipindi chote ambacho hakuwepo nchini.
“Umejitahidi sana”Roma na kumfanya Tanya kutabasamu mara baada ya juhudi zake kutambulika.
“Asante sana Master”
“Unazidi kubadilika kila siku na kuwa raia wa kawaida , kama utaendelea hivi ni hakika utajikuta unashindwa kuongoza kundi la Yamata na kunifanya nitafute mtu mwingine , sitaki kundi hilo kubadilika na kuwa kampuni ya kihalali”
“Master usiwe na wasiwasi, kwani hilo haliwezi kutokea , ijapokuwa kufanya kazi za kawaida ni kunafurahisha , lakini pia kuua ni hobi yangu”Aliongea na kumfanya Roma kuridhishwa na kauli yake na kabla hajawaza kingine cha kufanya simu yake ilianza kuita na alipoitoa ilikuwa ni ya babu yake Afande Kweka.
“Wewe mzee mbona umenipigia mapema sana, ni kwema huko?”
“Wewe mtukutu kwanini tabia yako haibadiliki , huwezi kuongea kwa heshima kwa wakubwa zako?”
“Unaweza usipende nikiongea kistaarabu na isitoshe nishazoea”Aliongea na kimya kifupi kilisikika.
“Mzee Longoli kanipigia leo hii anasema umempiga ndugu yake Mr Wambi , ameenda mbali na kusema Watanganyika hatuheshimu wazanzbar”Aliongea.
“Nikajua hili swala lishaisha”
“Nadhani unakumbuka nilichokuambia kuhusu familia ya Longoli na umuhimu wao kwenye taifa, anao ushawahi mkubwa sana ndani ya Tanzania visiwani na akiutumia vibaya anaweza kusababisha msuguano kati ya Zanzibar na Tanganyika”
“Kwahio anataka nifanyeje?”
“Mzee Longoli kapiga simu na alionekena kuwa mpole, alichohitaji ni wewe kwenda mpaka nyumbani kwake Zanzibar na mkae chini na kuyamaliza, lakini mimi sijaafiki”
“Kwahio mzee na wewe unanishauri niende? Au unampango gani?”
“Mimi ni mzee , sina mpango wowote , siwezi kuhangaishwa na nyie vijana mnayoyafaya , sasa hivi ni muda wangu wa kufurahia uzee wangu”
“Kama ni hivyo nitajua cha kufanya”
“Lakini napaswa kukumbusha kuwa makini ili usilete migogoro, Mzee Longoli licha ya kwamba anaheshimika Zanzibar lakini pia serikali yetu inampa ulinzi”Aliongea Afande Kweka na kumfaya Roma kucheka kidogo na kisha akakata simu na kumgeukia Tanya.
“Tanya nataka uende Zanzibar”
“Master Zanzibar natakiwa kufanya nini nikifika?”
“Kuna mtu nataka kusikia habari ya kifo chake, kifo chake lazima kionekane cha kawaida kabisa ambacho hakiibui mashaka”Aliongea Roma na kisha alimpa ishara ya kusogea karibu na kumnon’goneza jina la mtu ambaye anahitajika kumalizwa.
“Nimekuelewa Master”Aliongea Tanya
Roma hakutaka kuacha watu wasumbufu kama Mzee Longoli wanaendelea kuwa na nguvu ndani ya taifa , kwani wataendelea kumsumbua , hivyo njia pekee ya kumalizaa nae ni kumtanguliza , hata hivyo aliona sio hasara kwani ashaishi muda mrefu.Hakujali tena kama Mzee huyo mtoto wake alikuwa ni raisi wa Zanzibar.
Baada ya Tanya kutoka nje ya ofisi yake ,palepale aliweza kuingia Daudi na kusalimiana na kisha alimpatia habari za taarifa za Sophia juu ya maendeleo yake na kuigiza filamu chini ya ushirikiano wa kampuni yao na kampuni ya Penguin ya South Africa na Roma aliridhishw ana taarifa hio.
*****
Upande mwingine nchini Rwanda , muda huo huo wa asubihi alionekana Linda akiingia ndani ya Ikulu akifika kazini asubuhi.
Mara baada ya kusalimiana na baadhi ya wafanyakazi moja kwamoja alienda mpaka katika ofisi ya mheshimiwa Jeremy.
Linda mara baada ya kugonga mlango na kuruhusiwa kuingia alijongea mpaka katikati ya ofisi hio huku akiwa na sura ambayo ina muonekano usioelezeka.
“Linda habari ya safari?”
“Nzuri Mheshimiwa , nimefanikiwa kurudi”Aliongea a kumfanya raisi Jeremy kumwangaliaLinda kwa muda kama vile kuna kitu ambacho anafikiria.
“Una taarifa yoyote unataka kuniambia?”
“Ndio mheshimiwa , Wajumbe kutoka miliki ya PANAS wamefika na wanaomba mazungumzo na wewe”Aliongea Linda na kumfanya raisi Jeremhy kuwa katika hali ya mshangao kidogo lakini aliupotezea haraka.
“Wapo hapa nchini Rwanda?”
“Ndho mheshimiwa”Alijibu Linda na kumfanya raisi Jeremy kufikiria kidogo.
“Najua kitu kikubwa wataulizia kuhusu Desmond na mpaka sasa hajulikani alipo, hili swala linaniumiza kichwa”
“Lakinni mheshimiwa , kama Desmond asiporudi kwanini usianze kuandaa mpango mbadala”
“Upo sahihi Linda na hata mimi hili nilikuwa nikilifikiria kwa muda mrefu , najua siwezi kuwa na uhusiano sawa na Desmond tena kutokana na uwepo wa yule msukule anaeamini ni mama yake mzazi”
“Unapanga kufanya nini mheshimiwa?”
“Napanga kumrudisha Edna katika familia yagu , ndio mtoto wangu pekee ambaye anaweza kunirithi na kama nitaliweka hili wazi kwa wajumbe kutoka PANAS nadhani litawatuliza”Aliongea na kumfanya Linda kufikiria kidogo.
“Lakini kumrudisha Edna nchini Rwanda na kurithi nafasi yako ni ngumu kwani maisha yake yote amekulia nchini Tanzania mheshimiwa”
“Edna ndio kakulia nchini Tanzania , lakini ni mtoto wangu wa damu , nilo linatosha kabisa, jambo lingine sio lazima Edna kurithi nafasi yangu ya uongozi, bali ninacholenga ni kurithi ushawishi wangu ndani ya taifa ,na anaweza kumuendesha raisi ataekuwepo madarakani vile atakavyo hata kama sipo hapa duniani”Aliongea na kumfanya Linda kushangaa kidogo, kwani alikuwa akijua mheshimiwa anamaanisha nini kusema ushawaihi wake, lilikuwa ni swala ambalo linafungamana na jamii ya hio ya PANAS.
“Mheshimiwa kuna kitu naomba kukiweka wazi , ijapokuwa ni kinyume na kiapo changu kama mwanachama , lakini leo hii napaswa kukuelezea”
“Ni kuhusu hao Ant- illuminat?”
“Ndio mheshimiwa na ni swala ambalo linahusiana na mtoto wako Edna”Aliongea na kumfanya raisi Jeremy kumwangalia Linda kwa wasiwasi lakini na shauku kwa wakati mmoja .