Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mzigo tayari search mabaduni wa Serikali utauona huo uzi
 
Kesho jumatatu saa 15:00 pm
Sehemu ya 2 inashuka.
Kaa macho nitakutag ikiwa bado ya moto kabisa.
 
Ni Bora nisubiri huku jf a WhatsApp kule telegram hutufanyii haki..

Unatutia hasira kukulipa.
 
SEHEMU YA 561.
Hata kwa Faridi mwenyewe alishangazwa na kuhusishwa katika swala hilo na mshangao wake ulimfanya Roma aamini kwamba Faridi hakuwa akijua chochote na hakuwa akiongea ukweli.
“Nadhani mtu ambaye amefanikisha hilo sio mdogo kwako kwa namna ambavyo amefanikisha kukuchezea akili na wewe kushindwa kumfahamu”.Aliongea Farid.
Roma aliona hakika mtu huyo hakuwa wa kawaida kabisa , kama kweli ameweza kutengeneza sura ya udanganyifu na kumuigiza Farid basi kweli mtu huyo ni wa levo nyingine na hapo hapo akili yake ilijiambia huenda aliemfanyia hivyo ni Raphael.
Hermes pekee ndio aliekuwa na uwezo wa kutengeneza Illusion na mtu yoyote asione utofauti, kama ingekuwa ni mtu wa kawaida ambaye alicheza na akili yake basi asingeweza kumdanganya kijinga.
Roma alikumbuka kipindi wakati alipotaka kumuua Denis ni Hermes ambaye aliingilia kwa kumtengenezea udanganyifu kwa kumuona Denisi akimuua mama yake mpaka kughairisha.
Alijiambia kama ni Hermes basi inaleta maana kutokana na uwezo wake kulingana na wa kwake , kwa kutumia siraha yake tu maarufu ya kichawi iliofahamika kwa jina la Caduceus anaweza kuwafanya hata ndugu zake kuwa katika hali ya usingizi wa ndoto.
“Nadhani nishajua nani kafanya hivyo lakini nashindwa kuelewa nia yake halisi”Aliongea Roma na Farid alitingisha kichwa kuelewa .
Balozi Ramadhani aliondoka kuelekea Dodoma na kazi iliokuwa inabaki ni Roma na Edna kutafuta njia ya kusafisha jina la Sophia na kutuliza hali ya hewa.
Mchana wote Edna alikuwa bize kushughulika na swala hilo , Roma ndio ambaye alipaswa kushughulika na swala hilo kama mkuu wa kampuni ya Vexto Media lakini kwasababu yeye amehusishwa na pia lilimuhusu Sophia aliona aingilie majukumu ya Roma kumsaidia.
Ingekuwa rahisi kudili na swala hilo kama watu waliokuwa wakisambaza ni waajiriwa wa kampuni flani , lakini kwasababu ni watu binafsi waliokuwa wakisambaza na kuongezea chumvi ilimfanya Edna kushindwa kuzuia swala hilo mara moja na kukosa kabisa namna ya kudili nalo moja kwa moja.
Kilichomchukiza zaidi watu walitumia uzushi huo kupata ‘attention’ kutoka kwa watu ili kufanya peji zao mtandaoni zifatiliwe kwa wingi.
Roma alijikuta akichukia mno kwa jinsi ambavyo Edna alikuwa akihangaika kudili na swala hilo.
Baada ya muda wa kazi kuisha Roma alimlazimisha Edna kuondoka nae kurejea nyumbani.
Edna alikuwa akipanga kufanya kazi mpaka jioni ili kushugulikia hilo swala lakini alishindwa kumshawishi Roma kumuacha ofisini na mwishowe akaamua kumkabidhi majukumu yote Benadetha kushughulika nayo.
Muda wa kutoka kazini ni kama waandishi wa habari walikuwa wakimsubiria kwani walijaa katika eneo la kuingia ndani ya kampuni hio wakiwa na kamera zao pamoja na vifaa vya kurekodi sauti , walionekana walitaka kusikia chochote kutoka kwa Edna.
Roma alimwagiza Recho kuachana nao na asitokee mfanyakazi yoyote kuongea chochote , hata hivyo hawakuwa na cha kuongea kwani kinachoendelea hakikuwa na ukweli wowote na hata kama wakanushe hakuna ambaye angeamini na wangeendelea kuuliza maswali yasio na msingi , lakini kubwa zaidi Edna hakuwa mtu wa kupenda kuongea ana kwa ana na vyombo vya habari kwani hakupenda sana umaarufu.
Ilibidi wapitie moja kwa moja kwenye Basement katika eneo la maegesiho na baada ya kuingia kwenye gari , Roma aliliondoa na kulipeleka moja kwa moja mpaka nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani Lanlan alikuwa tayari ashatoka shuleni na alikuwa akiangalia katuni , baada ya kuwaona wazazi wake wamefika nyumbani aliwakimbilia na kumsalimia mmoja mmoja kwa kuwakumbatia na kisha akakimbia na kurudi kwenye sofa.
Alionekana kukolea kile ambacho alikuwa akiangalia na Edna na Roma waliangaliana na kuishia kutabasamu.
Edna kidogo alijisikia vizuri mara baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku pamoja na familia yake .
Waliangalia Tv Pamoja mpaka wakati ambao Lanlan alipotelea usingizini na Qiang alimbeba na kumpeleka juu kulala wakati huo Edna alimwambia Roma amfuate hadi kwenye Yadi kuna kitu waongee.
Roma na yeye alikuwa akitarajia Edna kumwambia kile ambacho anafikiria , kwani alimuona wakati wote akiwa ni mwenye mawazo.
Baada ya kukaa kwenye viti maalumu vilivyoweka kwa nje katika Yadi , Edna alivuta pumzi nyingi na kisha kumgeukia Roma.
“Hubby si ulishaniambia utanitimizia chochote na kunisikiliza ili mradi tu sikulazimishi kuachana na wanawake wako?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake na kujiuliza inatokea wapi.
“Nilisema hivyo lakini sikumaanisha katika kila ombi”
“Kwahio unavunja ahadi yako?”
“Kama utaomba kuniacha ulifikiri nitaweza kukubaliana na ombi lako , sijali kama utachokoza mtu mwingine kwani nitakusapoti muda wote”
“Nilijua tu utasema hivyo”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma kwa jicho la pembeni.
“Kama ni hivyo basi naomba nikuulize , je ni kweli kwamba hutonipinga kwa maamuzi yoyote nitakayoyafanya yanayohusiana na kampuni ya Vexto?”
“Bila shaka , kampuni imeasisiwa na wazazi wako na wewe ni urithi wako , sina mpango kabisa wa kuingilia taaluma yako pamoja na uendeshaji wa kampuni”Aliongea Roma bila ya kufikiria na kumfanya Edna kuvuta pumzi nyingi na kuzishsuha.
“Vipi kama nitasema napanga kujiuzuru na kumchagua mtu mwingine kuwa CEO wa kampuni na mimi kumsaidia kwa pembeni? , Je utasapoti maamuzi yangu?”Aliuliza na kumfanya Roma kushangazwa na swali lake hilo.
“Niliweza kuhisia haya ndio maamuzi unayotaka kuchukua , lakini je ndio kitu unachopenda kufanya?”
“Nimechoka , sina nguvu tena za kudili na maswala haya zaidi na isitoshe na mimi ni binadamu, naweza kuonekana mkatili kwa watu wa nje lakini sijui namna ya kudili na marafiki zangu pamoja na familia”
“Unafanya haya yote kutokana na kilichomtokea Sophia, si ndio?”
“Hilo ni moja , iwe ni Dorisi au Nasra wote wanashikilia nafasi muhimu katika kampuni na siwezi kufanya kazi bila wao , lakini kila ninapofikiria uhusiano wako na wao , moyo wangu unakosa utulivu , kwasababu ni wafanyakazi wenzangu najitahidi kujizuia na kujiambia hakuna kitu kibaya kitakachotokea , lakini je unafikiri ni rahisi kwangu?”
Roma alijikuta akikosa neno , alijua Edna ashapotezea mambo hayo muda mrefu kumbe alikuwa akijizuia muda wote huo.
“Pia kama ningekuwa sina uhusiano wowote na Sophia huenda ningeweza kufanya maamuzi ya kumzuia kutoonekana hadharani kwa muda kidogo, lakini siwezi kufanya hivyo kwani mimi ni Bosi wa kampuni na itaonekana namnyanyasa nikifanya hivyo , ukweli sijui namna ya kudili na hili swala nahisi kuchoka…”
Kilichokuwa kikimpa hofu zaidi Edna ni juu ya uhusiano wa Roma na Nasra pamoja na Dorisi , alifikiria je kama itafahamika katika jamii kwamba na wao wana mahusiano ya kimapenzi na mume wake si itamchafua zaidi na zaidi , alichukulia tu kwa mfano tukio la Sophia lilivyokuwa likimuumiza kichwa ndio maana alifikia maamuzi ya kutaka kuachia ngazi.
“Naelewa unachojisikia lakini hata kama utajiuzuru na kutoa nafasi yako kwa mtu mwingine hawawezi kufanya chochote na watu watasema ulikimbia”
“Najua, ndio maana mpango wangu baada ya kijiuzuru ni kuita waandishi wa habari na kisha nitawalezea uhusiano wangu na Sophia na kuwaambia hahusiki katika uzushi unaosambazwa . ni sababu nzuri kujiuzuru kwa kuwajibika ili kulinda taswira ya kampuni”
“Kwannini unataka kuwajibika , watu walioanzisha huo uzushi ndio ambao wanapaswa kuwajibika”
“Lakini angalau kuwepo na mtu wa kubeba lawama zote , sina mpango wa kuendelea kufanya kazi na kujiuzuru ndio kitu pekee ambacho naweza kufanya kwa ajili ya Sophia”
Roma alona kabisa maamuzi ambayo anataka kuchukua Edna ni ya kijinga na akifanya hivyo kwasababu ya Sophia aliamini kabisa ingemfanya na Sophia mwenyewe kukosa ujasiri wa kujitokeza hadharani tena.
Muda huo wakati wakiongea Bi Wema aliwafuata huku akionekana kuwaita.
“Miss kuna taarifa huku , njooni muone , kuna habari mbaya”Aliongea Bi Wema kwa kupaniki.
********
Muda huo huo ncha ya kaskazini mwa dunia , ndani ya maabara kubwa iliotengenezwa na Yan Buwen, hali ya hewa haikuonekana kuwa nzuri.
Vifaa vyote vya maabara vilionekana kufanya kazi , huku Skrini zikionyesha baadhi ya data ngumu kuelekeweka kupanda na kushuka.
Katika meza kubwa ya kisasa kama zile za hospitalini kulionekana mirija mingi ikiwa imeunganishwa katika mwili wa binadamu.
Upande wa kulia na kushoto wa meza hio kulikuwepo baadhi ya vifaa vilivyokuwa na maumbo ya ajabu ambayo ndani yake kulikuwa na vitu kama maji maji.
Juu kabisa ya mwili wa binadamu uliolazwa kwenye meza hio kulikuwa pia na kifaa cha muundo wa kipekee ambacho ndani yake kulikuwa na mwanga mkali wa kung’aa uliokuwa ukionekana huku ukizunguka zunguka , ilikuwa ni nishati ambayo ilionekana kuunganishwa moja kwa moja na mwili wa binadamu huyo.
Mtu wa ngozi nyeusi alielazwa katika meza alikuwa uchi wa mnyama huku miguu yake ikiwa imebananishwa na kufungwa kwa kamba ngumu maalumu ili kumzuia asisogee.
Alikuwa ni Denisi , ijapokuwa alionekana kuwa na fahamu lakini ilionyesha muda wowote angezimia, yote hayo ni kutokana na kwamba nishati iliokuwa imewekwa juu yake , ilionyesha kujiandaa kuuvamia mwili wake .
“Punguza wasiwasi , utakuwa sawa muda si mrefu , isitoshe hili linafanyika kwa faida yako”
Mwanaume aliekuwa pembeni ya meza hio ya kufanyia operesheni alionekana kutabasamu kifedhuli , alikuwa amevalia koti la maabara ambalo tayari lilikuwa na madoa mengi na alionekana ana muda mrefu hakuwa amenyoa ndevu zake kwani zilionyesha kuota kwa wingi.
Josesph Bikindi muonekano wake ulirudi na kuwa kama ule wa miezi kadhaa nyuma wakati alipokuwa akifahamika kwa jina maarufu la Lekcha.
Nguo pekee ambayo ilikuwa imeusitili mwili wake ni koti la maabara na alikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo , kwani alionyesha kukonda tofauti na alivyokuwa siku kadhaa nyuma kabla ya kuingia katika mabara hio ya marehemu Yan Buwen.
Katika eneo la kifua chake karibu na moyo kulikuwa na kitenesi cha nishati ya Anti- matter ambayo imeshikiliana na mwili wake na huenda Roma angekuwepo moja kwa moja angejua kitenesi hicho cha nishati ni jiwe la kimungu.
Kama ilivyokuwa kwa Yan Buwen , Lckcha alitumia teknolojjia ile ile ilioachwa na kuunganisha jiwe la kimungu na mwili wake , lakini utofauti tu ni kwamba teknolojia hio yeye alikuwa ameindeleza kwa viwango vya juu na kumfanya kuwa na uwezo ambao ni mkubwa zaidi kuliko aliokuwa nao Yan Buwen.
“Unataka kufanya nini?”Alipaniki Denisi mara baada ya Lekcha kuanza kuchezesha lile boksi ambalo lilikuwa limejaa nishati.
“Hehe.. hutaki kuwa na nguvu , hii ni gunduzi yangu mpya nilioweza kuifaikisha kupitia muendelezo wa teknolojjia ya Yan Buwen…”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kejeli kama kawaida yake.
“Hiki ni kifaa nilichokipa jina la ATD(Ant -matter transfomation device) ninachopaswa kufanya ni kukiwasha kwa kutumia jiwe la kimungu na kitaibadilisha nishati yote isio ya maada kwa kuwa na nguvu kwa zaidi ya mara mia moja, kinaweza pia kutumika kufuta Genome za mwili wako na kama kitaonyesha mafanikio kwako basi na kwangu kitafanya kazi na yatakuwa mafanikio ya teknolojia kubwa ya kuwasha link ya vinasaba vya mwili wangu na kuungana na muundo wa viambata vya nishati ya Ant-matter na kwanzia hapo nitakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya ninachotaka”
“Unamaanisha nini?”Aliuliza Denisi kwa hofu.
“How would I know ..,, according to Yan Buwen idea the transformation on the test subject is still unknown . Well no matter how it turned out to be , I’ m sure I will benefit from it ,you won’t understand even if I explain it to you”Aliongea akimaanisha kwamba hawezi kujua kwasababu mchakato wa mabadiliko kwa mtu anaejaribiwa haujulikani , lakini anaendelea kusema licha ya matokeo ya aina yoyote ana uhakika kwamba atafaidika nyao hivyo hata kama amwelezee kila kitu hatoweza kumuelewa.
“Kwahio unataka kunitumia kama chombo cha majaribo , kwanini unataka kunifanyia hivyo , sisi si marafiki?”Aliuliza Denisi kwa wasiwasi mkubwa lakini Lekcha aliishia kucheka sana.
“Umesema marafiki, Wewe?.. wewe ni mbwa tu wangu , unafikiri unafaida kubwa kuliko yule malaya ?”
Baada ya kuongea palepale aliwasha jiwe la kimungu kwa kutmia akili yake tu na palepale mwanga ulizidi kufunika maabara hio baada ya mlipuko wa mng’ao wa mwanga wa ajabu uliotoka katika jiwe la kimungu.
Kila mlipuko wa mwanga ule wa Ant matter unavvyotokea uliakisiwa na kifaa ilichofungwa kwa kuning’inizwa juu ya mwili wa Denisi na kisha palepale kifaa kile cha ATD kilikuza nguvu ya mwanga ule na kisha kumulika katika mwili wa Denisi.
Lekcha alirudia kwa mara ya pili na awamu hio kulitokea mlipuko mkubwa zaidi wa mwanga na kisha ukasharabiwa wote na kile kifaa na kisha ukaelekezewa katika mwili wa Denisi na kumfanya asionekane kabisa kwani kifaa kile kilimulika mwili mzima mpaka kwenye kucha za miguu.
Lekcha alizidi kuinua mikono yake na kuruhusu nguvu ya jiwe la kimungu kumezwa na vifaa na kisha kuelekezewa katika mwili wa Denisi , alirudia mara nyingi mpaka ikafikia wakati sasa mwili wa Denisi ulianza kuonekana kama vile unatoa shoti za umeme wa rangi ya bluu.
Aliendelea vilevile bila kuacha , ilionekana matokeo anayoyataka bado, aliendelea kutoa nishati isio maada kumuingia Denisi huku makelele ya milipuko ya umeme kama vile nguzo inapiga shoti ilisambaa chumba kizima , lakini bado Lekcha hakuacha kufanya anachokifanya alizidi kuruhusu nishati ya ant-matter kuuvaa mwili wa Denisi kwa muda mrefu na ilifikia mwili wa Denisi hakuonekana kabisa.
Ni ndani ya nusu saa tu kulitokea mlipuko mkubwa mno kiasi kwamba kwa macho ya kawaida yasingeweza kuhimiri mn’gao wake kwani ulimkuwa mkali sana wenye wavelength za kuumiza macho.
Lekcha alirudi nyuma na kuacha kile kitendo alichokuwa akiendelea nacho na kisha macho yake yote aliangalia katikati ya maabara hio kama vile mtu anaetegemea mtu kutokea katikati ya mlupuko huo wa mng’ao.
Ni ndani ya dakika kama kumi na tano tu , ule mng’ao ulianza kujikusanya taratibu taratibu na kuanza kupungua na mpaka wote unaisha Denisi hakuweza kuonekana wala ile meza haikuonekana, ni kama vile imeyeyuka na kitu pekee kilichobakia ni mpira wenye kung’aa uliobakia sakafuni, ulikuwa ni mpira wa nishati , huenda ni nishati ya nguvu ya Ant-Matter.
Lekcha alijikuta akijawa na mshangao huku uso wake ukiwa katika hali ya tabasamu pana na alisogea kwa haraka.
Na kwa kutetemeka mikono aliunyanyua ule mpira wa nishati wenye mwanga uliokuwa ukicheza.
Baada ya kuusihikilia mkononi aliuachia hewani na palepale hakudondoka chini bali ulielea na kisha ukamsogelea katika eneo la kifua chake upande wa jiwe la kimungu.
Ilikuwa ni kama lile jiwe la kimungu lilikuwa likiuvuta kwani baada ya mpira ule wa nishati kufika katika kile kifua ulimezwa wote na kupotelea ndani ya mwili wa Lekcha.
“Haha.. I did it … I did it”Aliongea kwa furaha huku mwili wake ukianza kutetemeka , alikuwa akihisi kabisa seli za mwili wake zilikuwa zikicheza na ngozi yake alihisi ikiwa na muwasho usio kuwa wa kawaida , ni kama vile mwili wake umegeuka kuwa kidonda na sasa ulikuwa ukipita katika hatua ya kupona.
Palepale alitupa koti lake chini na kubakia uchi , lakini baada tu ya kutoa lile koti alidondoka chini na kuanza kutetemeka kwa kurusha miguu kama vile alikuwa mgonjwa wa kifafa na ghafla tu jiwe lililokuwa katika kifua chake lilitoa mwanga mkali kwa sekunde tu na kisha ukapotea na palepale mwili wa Lekcha ulianza kupitia mabadiliko kwa kasi kubwa mno kama vile ni kiumbe cha ajabu kwani hata nywele zilianza kubadilika..
Baada ya dakika tano Lekcha mwili wake ulibadilika na alifanana kwa kila kitu na Denisi , alikuwa ni Denisi mtupu.
Baada ya kutulia kabisa na kuhisi mwili wake haupo kwenye maumivu na ule muwasho wa mwili umeisha palepale alisimama na kisha akakisogelea kioo.
“Denis”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli huku akiwa uchi , na alianza kujikagua mwili mzima akiwa kama mtu asieamini kama ameweza kubadilika na kuuvaa mwili wa Denisi.
Lekcha muda uleule hakusubiri tena hata sekunde kwani alipotea ndani ya maabara ile kama jini na alipokuja kutokezea ni nje kabisa juu ya barafu na ile anatua tu , vivuli vya watu wawili vilivyoakisiwa na mwezi vilionekana,Alikuwa ni Kizwe pamoja na Desmond.
“Denisi..!”Aliita kizwe kwa mshango na kisha alimpita Lekcha kwa mbele na kumkagua.
“Little Cripple dear , you finally succeded should I call You Denis Senga now?”
“Mpenzi wangu kilema naona umefanikiwa , vipi nikuite Denisi Senga sasa?”Aliongea Kizwe kwa kingereza.
Lekcha palepale alimsogelea kwa spidi na kabla hata Kizwe hajaelewa alijishutikia akiwa kwenye mikono ya Lekcha mwenye muonekano wa Denisi.
Kizwe alikuwa ashazoea namna ambavyo Lekcha alikuwa akimfanyia kila anapotaka huduma kutoka kwake na palepale hakuleta ubishi na alimsogezea mdomo mwanaume huyo na wakaanza kubusiana.
Desmond alisimama bila hata ya kujali kile kinachoendelea , hata hivyo licha ya kwamba mama yake alifufuliwa lakini hakuwa mama yake anaemjua , alionekana ni mtu mwingine kabisa na hakuwahi kumkubali.
“Mmefanikuwa kupata chochote?”Aliuliza Joseph Bikindi au ukipenda mwite Lekcha.
“Ni kama nilivyotarajia Jeremy ameita ndugu zake kutoka ujinini , kuna mwanaume mmoja anaeitwa Nix pamoja na Gesha , wote wana uwezo wa mafunzo ya mbingu na ardhi”Aliongea Kizwe.
“Vizuri .. tutachukulia swala hilo kwa manufaa kwetu”Alijibu Lekcha.
“Lekcha kwanini usiuvae mwili wa Jeremy na ukawa raisi wewe?”Aliuliza Kizwe.
“Acha ujinga wewe mwanamke , unafikiri hao majini ni rahisi kushindana nao , ninaweza kuwamaliza ndio lakini vipi kuhusu huko wanakotokea , unafikiri nitaweza kuwashinda wakija duniani kupambana?, kwasasa mimi ni Denisi na lazima nichukulie mwonekano wangu kama fursa”
“Unamaanisha …”Kizwe alitaka kuongea lakini palepale alijikuta akitoa tabasamu pana kama vile taa imeweshwa kwenye akili yake na kugundua anachopanga Lekcha .
“Kilema , hakika wewe ni mwenye akili sana”Aliongea Kizwe huku akitoa kicheko cha kebehi na Lekcha alimwangalia kwa kejeli mwanamke huyo na kisha akanusa nusa shingo yake lakini hakuonyesha tamaaa ya kumuhitaji Kizwe tena
“Clelia Allisanto” Jina hilo lililipuka kwenye akili yake na palepale alimtua chini Kizwe na kuonyesha tabasamu.
“Tumetumia muda mwingi sana kukaa huku Ncha ya Kaskazini…. Kituo chetu cha kwanza ni nchini Tanzania, Tuondokeni kazi ya kulipa kisasi imeanza rasmi”Aliongea Lekcha na palepale wote kwa pamoja walipotea.
Ilionekana hata Desmond alikuwa na mabadiliko makubwa kwani hakuwa wa kawaida tena.
Muda wote ambao Lekcha alikuwa akijibadilisha kuwa Denisi alikuwa akiangaliwa na mtu alievalia Mask na mavazi meusi , alikuwa ni bwana yule ambaye alipigana na Roma nchini Korea na Australia.
Lekcha hakuweza kumuona bwana huyo kutokana na kwamba alikuwa akitumia nguvu za kijini kujificha na hata baada ya Lekcha kuondoka ndani ya maabara alimfuata kwa nyuma.
Muda uleule wakati Lekcha na wenzake walivyoondoka , akitaka kugeuka na yeye kuondoka hilo eneo , kivuli cha mtu mwingine kilionekana nyuma yake .
“Your Highness Athena , you’re here”Aliongea kwa heshima huku akiinamisha kichwa chake na Athena alitingisha kichwa tu na kisha akaongea.
“He did it..”Aliongea kwa sauti yake ya kike akimaanisha , Amefanikiwa?
“Yes as you said , he activated the genetic link technology and ate Denis .He Transfomed into Denis and his power had improved greatly”Aliongea akimaanisha kwamba ameweza kufanikiwa kuwasha teknolojia ya Genetic Link na kummeza Denis, Amebadilika na kuwa Denis na nguvu zake pia zimeimarika sana.
“He is still slower , looks like he’s not as good as Yan Buwen”Aliongea akimaanisha kwamba bado yupo taratibu , na inaonekana hayupo vizuri zaidi kama Yan Buwen.
Kwa kauli yake hio ilionyesha kifo cha Yan Buwen kilikuwa hasara kubwa kwake.
“Kwa maoni yangu , Yan Buwen anaweza kuwa na kipaji na uwezo mkubwa wa akili lakini Joseph ana tamaa kubwa halafu ni mkatili , nina uhakika anaweza kuwa tishio kwetu muda si mrefu , sijui kwanini unamuacha afanye atakavyo , si tayari amefanikisha misheni ya kuendeleza utafiti wa namna ya kuwasha teknolojia ya Genetic link?”Aliuliza Bwana mwenye Mask.
“I need the results from his research but he still has values , stop asking about it”
“Nilihitaji matokeo kutoka kwa tafiti yake lakini bado ana thamani , acha kuuliza kuhusu hilo”Aliongea Athena.
“Yes Your Highness”Aliongea bwana mwenye Mask.
“Hamisha vifaa vyote ndani ya maabara katika sehemu salama na haribu kila kitu , baada ya hapo nenda nchini Tanzania na endelea kumfatilia , hakikisha Roma hakuoni asije kukumeza maana sitoweza kukukoa tena”Aliongea na kumfanya Bwana mwenye Mask kukakamaa mwili, baada ya kukumbuka tanuru la Maafa(Chaos Cauldron).
Baada ya kutingisha kichwa kuitikia palepale aliondoka hapo na kuelekea katika maabara kufanyia kazi maelekezo aliopatiwa , kwa uwezo wake ilikuwa rahisi sana kuhamisha baadhi ya vitu muhimu vyote katika sehemu salama ndani ya muda mfupi tu.
Lakini hata hivyo alizidi kumuogopa Athena , hio yote ni kutokana na kwamba mipango yake ilikuwa ipo kimahesabu zaidi .
Licha ya kuwa na uzoefu wa karne lakini alishindwa kabisa kufahami ni kipi anafikiria na mpango wake unaofuata ni upi.

SEHEMU YA 562.

Hakika ilikuwa habari mbaya sana kwa Edna na Roma kulingana na juhudi kubwa ya kumfanya Sophia kuwa maarufu.

Taarifa ambayo ilikuwa ikiwasilishwa katika runinga ilionekana ni ambayo Sophia alikuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kitendo cha Sophia kufanya ‘Press conference’ bila ya kushirikisha kampuni inayomsimamia kilimshangaza Edna na Roma kwa wakati mmoja , mbaya zaidi haikuwa kikao na waandishi wa habari kukanusha tu uvumi bali alienda mbali zaidi kutangaza jambo kubwa zaidi.

Katika kikao hicho kwanza kabisa alikiri kwamba Edna ni dada yake na hata kuanzishwa kwa lebo ya kusimamia wasanii chini ya Vexto media ilianzishwa kwa ajili yake.

Baada ya kuongea hivyo waandishi hawakuonyesha hali ya kuridhika na kutaka kujua ukweli wote kuhusu yeye na Roma kama wana uhusiano wowote na hapo ndipo Sophia aliharibu kabisa kwani alikiri kwamba alikuwa na hisia za kimapenzi na Shemeji yake , lakini hakuwahi kuweka hisia zake wazi wala kujihusisha nae kwani ni mume wa dada yake.

Kauli ya Sophia ilimshutua mno Edna na hakutaka kabisa hata kuendelea kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea kwani palepale aliondoka na kusema anaenda kulala.

Roma alishindwa kuongea chochote kutokana yeye ndio chanzo ya kila kinachoendelea hivyo alimwangalia mke wake kwa huzuni akipandisha ngazi kwenda juu kwa ajili ya kulala.

Sophia mara baada ya kutoa kauli yake hio alitoa tangazo Rasmi kwamba anaachana na maswala ya Mziki na Usanii.

Ilikuwa kauli ambayo ilishangaza kila mmoja ambaye alikuwa ni shabiki yake na hata waandishi wa habari waliokuwa wakiuliza maswali walitaka kujua kwanini Sophia kaamua kufanya maamuzi makubwa ya namna hio ilihali alishatolea swala la uhusioano wake na Shemeji yake, waliuliza je kuna sababu nyingine ya kufanya maamuzi ya kuachana na mziki, lakini licha ya maswali hayo Sophia hakutaka kujibu na alifunga mkutano huo.

Roma aliekuwa sebuleni akiangalia na Bi Wema alijikuta akiwa kwenye mshangao na kushindwa kujua kitu cha kufanya kwa wakati mmoja, alitamani kupotea hapo hapo na kwenda mpaka Dodoma.

Lakini aliona hata kama akianzisha safari hio na kufika Dodoma hakuna ambacho angeweza kufanya kama tu Sophia kaamua mwenyewe kufanya kikao bila kumshirikisha , kuna hisia zilimwambai kabisa Balozi atakuwa amehusika katika hilo.

Mjuda uleule Roma akiwa ni mwenye kuwaza cha kufanya simu yake ilianza kunguruma ikishiria ilikuwa ikiita na alipoangalia namba ambayo inampigia ni mpya na alipokea palepale na alipoweka sikioni na kusikia sauti ya mwanaume aliejitambulisha hapo hapo alijua ni nani ambaye alikuwa akiongea, alikuwa ni Balozi baba yake Sophia.

“Hades nadhani mpaka sasa umeona taarifa?”Sauti ya Balozi ilisikika.

“Nimeona taarifa ndio , lakini kwanini mmefanya maamuzi bila ya kutushirikisha mnajua ni kwa nguvu kiasi gani ambayo Edna mke wangu aliwekeza ili kumfanya Sophia kuwa maarufu”

“Hayo yalikuwa maamuzi yake , nadhani mpaka sasa unaelewa ni upi msimamo wa Sophia”

“Naelewa vipi msimamo wake ilihali sijaongea nae tokea tukio litokee”Aliongea Roma huku sauti yake ikianza kukosa uvumilivu.

“Sophia mpaka sasa hataki kuendelea na maswala ya mziki tena na ninarudi nae Japan, ukitaka kumjumuisha sehemu ya wanawake wako mfuate Japan, nilimleta Sophia kwako sio kwasababu nilitaka umfanye kuwa maarufu bali nilitaka umfanye mke wako wa pili”

“Lakini mziki ni kitu ambacho Sophia alikuwa akipenda , hatukukurupuka kumuingiza katika ulimwengu wa kistaa”

“Una uhakika ndio kitu anachokipenda au unausemea moyo wake?”

“Unataka kumaanisha nini?”

“Hades wewe ni mwanaume kwanini unazunguka zunguka ilihali unaujua ukweli , kama unahitaji kuonana na Sophia kwa mara nyingine umfuate Japan”Aliongea Balozi kitemi na palepale alikata simu yake na kumfanya Roma akijikune kichwa chake na kukosa kabisa cha kufanya.

Siku iliofuata wakati wakipata kifungua kinywa , Roma alionekana kabisa kukosa raha zote , ukweli ni kwamba usiku mzima hakulala kutokana na maamuzi alioyafanya Sophia.

“Sophia karudi Japani?”Aliuliza Edna.

“Umejuaje?”

“Kanitumia meseji jana ya usiku ya kuniomba msamaha kwa kila kitu na kuniambia kaachana na mziki”Alijibu Edna na kumfanya Roma kushangaa .

“Kwanini mimi hajaniambia chochote hata kunitumia tu ujumbe?”Aliongea Roma huku akicheka kicheko cha kukata tamaa.

“Unapanga kwenda kumfuata?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kuwa katika hali ya mshangao kidogo na kushindwa kujibu swali lake.

“Kama unataka kwenda sitokuzuia”

“Najua huwezi kunizuia kwasababu ni Sophia lakini hio ndio sababu pekee ambayo inanifanya nisiende”Aliongea na kumfanya Edna kutoa tabasamu hafifu.

“Hapa hata sijui napaswa kukasirika au kuwa na furaha”

“Usifikirie sana , hakuna ambaye amefanya kosa, baadhi ya vitu katika maisha haviendi kama tunavyopanga lakini haimaanishi kwamba haiwezekani kwa sisi kutosahau , Sophia bado ni mdogo anaweza kusahau kila kitu wakati akiendelea kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi”

Ndio hata Sophia alikuwa akifanya mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi ili asizeeke kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine.

Hivyo Roma aliaminig nishati ya akili ambayo ageweza kuipata Sophia moja kwamoja ingemfanya kusahau yaliopita na kuanza maisha mengine.

Roma alivyokuwa akifikiria ni tofuati na Sophia alichokuwa akifikiria , Sophia alifanya mziki kwasababu tu ni sehemu ya kitu anachopenda kwasababu hakuwa na kitu kingine ambacho angeweza kufanya , malengo makuu ya Sophia ni kuwa katika mahusiano na Roma na kadri siku zilivyokuwa zikisonga alikuwa kabisa akikosa uvumilivu wa kuzishinda hisia zake , huenda hata maamuzi ya kuondoka bila kumuaga Roma ilikuwa ni sababu maalumu ya kumfanya Roma kuweza kumkumbuka.

Edna kuna kitu alichokuwa akikiona kutoka kwa Roma na alijua fika hiko ndio kilichomfanya kuwa na mwonekano wa kukosa furaha asubuhi hio.

Baada ya kula kidongo tu aliweka uma na kijiko chini na kisha akamshika Lanlan nywele na kumpa maagizo Qiang Xi kumuwahisha shule na kisha alichukua mkoba wake na kuaga anaenda kazini.

“Kwanini haraka hivyo , kuna jambo la muhimu huko kazini?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Nina miadi na lakini pia kuna vitu vya kuandaa kabla ya kikao”

“Wife ni kweli unapanga kustaafu”

“Ndio , nilishakuambia tayari jana na natarajia utasapoti maamuzi yangu”

“Lakini hauna haja ya kuharakisha kwasabu lazima kwanza uchague nani anakwenda kurithi nafasi yako , Vexto ni kampuni ya kimataifa, sio rahisi kupata mtu mwenye uwezo na ambaye ataweza kuongoza kwa ufanisi kama wewe”Aliongea Roma kushauri na kumfanya Edna kutabasamu.

“Unaweza ukaja makao makuu kama una shauku , nishachagua tayari mrithi wangu na mtu huyo atafika ndani ya kampuni baadae”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa , ijapokuwa alikuwa na hisia kwamba tayari Edna ashachagua mtu wa kumrithi lakini bado ilimfanya kama vile kawekwa gizani kwa mara nyingine.

Ukiachana na mchakato, taarifa ambayo anakwenda kutoa Edna huenda ingewashangaza wengi kwani ni ya ghafla sana , kubadilika kwa CEO wa kampunni kubwa kama hio ni jambo kubwa sana.

Edna alikuwa ashakusanya wafanyakazi wote wa juu wa kampuni siku ya jana kwa ajili ya kikao siku hio na baada ya kufika ofisini aliweza kupewa taarifa na Recho watu wote wamekusanyika katika ukumbi kwa ajili ya kikao.

Dorisi ,Nasra , Recho na Benadetha wote walikuwepo na baadhi ya wafanyakazi waliuliza sababu ya kikao hicho ni nini , lakini hawakuwa na majibu sahihi ya kuwapa kwani hawakuwa wakielewa pia kinachoendelea.

Saa nne kamili Edna aliweza kuingia katika ukumbi wa mikutano, kama kawaida yake akiwa na mwoneknao wa kujiamini na watu wote walisimamama kuonyesha ishara ya kumkaribisha .

Baada ya miaka mingi ya kufanya nae kazi pamoja na licha ya kuwa mdogo ki umri lakini alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa wafanyakazi wake.

Roma hata yeye alikuwepo , hakuhudhuria kikao kama mfanyakazi wa kampuni lakini yeye alisimama nje ya mlango wa kuingilia akitaka kujua nani anakwenda kuwa mrithi wa Edna.

Recho ambaye muda wote alikuwa akimsaidia Edna katika majukumu yake akili yake ilikuwa kwenye wasiwasi , yeye ndio aliekuwa akijua kinachoendelea kwani siku ya jana yote ndie aliekuwa na jukumu la kupigia simu viongozi wa juu wote wa kampuni Tanzu kufika makao makuu kwa ajili ya kikao.

Sasa alijiambia kama Edna anakwenda kustaafu vipi kuhusu yeye kazi yake , inamaana na yeye anapaswa kuacha kazi kwasababu hatokuwa msaidizi tena wa Edna.

“Have a seat”Aliongea Edna kwa kingereza akiwaambia wafanyakazi hao wote kukaa chini.

Chumba chote kilibakia kuwa chini ya ukimya wa hali ya juu sana na macho yao yote walikuwa wameyaelekezea kwa Edna.

Edna upande wake alitulia kwa dakika kadhaa na kisha akaonyesha tabasamu ili kuondoa hali ya hewa ya wasiwasi kwa wafanyakazi hao.

“Najua mna wasiwasi mkubwa na kama mmechanganyikiwa na kujaribu kufanya makisio na kupelekea kuwa katika hali ya wasiwasi lakini yote hayo hayatozuia mimi kutoa tangazo langu , Ninaachia ngazi katika nafasi yangu kama raisi wa makampuni yote ya Vexto”Aliongea Edna na kufanya watu wote kuwa katika hali ya mshangao na kauli yake.

“Raisi Edna nini kinaendelea , kampuni yetu inafanya vizuri tutawezaje kuendelea bila ya wewe?”Aliuliza mmoja ya wafanyakazi alieshindwa kuzuia mshangao wake.

“Ndio CEO, tuambie matatizo yako, tumepitia magumu mengi kuifikisha kampuni katika hatua hii tukiwa pamoja , hakuna lingine la kutuogopesha”Alichangia mwingine na mwingine akadiakia hivyo hivyo na mwishowe likaibuka Zogo la wafanyakazi wote kutaka Edna atengue kauli yake na Edna alisimamia katika msimamo wake.

“Ninajiuzuri kama CEO lakini haimaanishi kwamba naitelekeza Vexto , Bibi yangu na mama yangu waliyatoa maisha yao kwa ajili ya maendeleo ya kampuni hii na ishakuwa kama sehemu ya familia yangu , siwezi kuitekeleza familia yangu , ninachosema ni kwamba najiuzuru katika nafasi yangu lakini bado nitakuwa na asilimia hamsini za hisa zote za kampuni na nitaendelea kubakia kama mwenyekiti wa bodi .. sababu ya mimi kujiuzuru ni kwasababu ya maswala binafsi , siwezi kfuanya kazi kila siku kama nilivyokuwa nafanya kipindi cha nyuma”Aliongea na wafanyakazi hao walijikuta wakipata ahueni kidogo kwa maneno yake lakini bado walikuwa katika hali ya mshangao na kutoridhika.

“Raisi Edna unataka kubakia kama mwenyekiti wa bodi kwasababu umechoshwa na kazi?”Aliuliza mwanamke mmoja.

“Kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea kufanya maamuzi haya , naamini wote mnajua kwamba nimeolewa na pia nina mtoto tayari , ninataka kutumia muda mwingi kuwa na binti yangu ili kumwangalia kwa ukaribu akiendelea kukua na isitoshe mume wangu hapendi nikifanya kazi kwa muda mrefu, nadhani ni wakati wa mimi kuwa karibu na familia yangu , nimechoka sana na nadhani napaswa kujipa muda wa mapumziko , ninaweza kabisa kustaafu hata uwenyekiti na kumpa mtu mwingine kushika nafasi yangu”Aliongea na kufanya chumba chote kuwa kimya na watu kuangaliana .

“Madam , kama unajiuzuru nani anakwenda kushika wadhifa wako , mrithi lazima awe na uelewa wa namna kampuni ya Vexto inavyoendeshewa pamoja na sera zake ili kuwa na ufanisi , lazima awe pia na uwezo wa kutushawishi na sisi tumkubali kama kiongozi wetu”Aliongea mwingine na kumfanya Edna kuangalia saa ya ukutani.

“Mrithi wangu atakuwa hapa muda si mrefu , tafadhari subirini kwa muda kidogo”Aliongea.

Muda huo Roma aliekuwa nje ya mlango akitaka kujua nani anakwenda kuwa mrithi wa Edna , alijikuta akipatwa na mshangao mara baada ya kuona sura za watu wawili zikitokea kwenye Lift .

Alikuwa ni mwanaume ambaye amevalia suri safi ya bei ghali na tai nyekndu na kumpelekea kuonekana ni mtaaluma maridadi na kwa upande wa mwanamke alionekana kuwa na sura ya kawaida lakini alikuwa ni mwenye tumbo kubwa akiashiria ni mjamzito , lakini licha ya hivyo alitembea kwa muondoko wa kuonyesha kujiamini huku akitoa Aura kama ya mfanyabiashara mkubwa.

“Ernest Komwe na Monica !!?”Roma alijikuta akiongea katika nafsi yake kwani hakutegemea watu hao ndio ambao Edna alikuwa akizungumzia kwenda kumrithi.

“It’s been a while Mister Roma , I hope you are not irked by our appearance”

“Imekuwa kipindi kirefu Mr Roma , natumaini hujakerwa na kuonekana kwetu?”Aliongea Ernest Komwe akiweka tabasamu huku akionyesha heshima mbele ya Roma , alikuwa makini sana na ni kama mtu ambaye aliogopa kumkosea Roma.

Upande huo wafanyakazi wote waliweza kumuona Ernest akisalimiana na Roma walijikuta wakishangaaa mno.

Hawakushangaa kumuona Ernest Komwe tu , bali pia walishangaa kumuona Monica kwani taarifa walizokuwa nazo ni kwamba watu hao walihamia Marekani.

Nasra, Dorisi na Benadetha mara baada yakumuona Ernest walijikuta sura zao zikikunjamana.

Roma aliishia kuangalia mkono wa Ernest Komwe na kumfanya Edna kumwangalia Roma kwa mwonekano wa kuomba asifanye chochote kibaya.

Roma hakupokea hata mkono wa Ernest zaidi ya kutoa tabasamu la machungu na kisha aligeuza na kuondoka kuzifuata Lift na kupotelea ndani.

Kutokana na yaliotokea hakuwa kabisa na hamu ya kuongea na Ernest wala kuendelea kusikiliza kikao hicho ndio maana akaondoka.

Alijiambia ndio maana Edna alikuwa akimuomba kumsapoti kwa maamuzi yoyote kumbe mtu ambaye aliona anafaa kumrithi ni binamu yake Ernest.

Licha ya hivyo Roma alikubali maamuzi ya Edna , kwanza kabisa Ernest ashafanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto kwa muda mrefu na ana uelewa na maswala yote ya kampuni lakini pia alikuwa ni mwenye uwezo mkubwa , pili ingekuwa ngumu kwa Ernest kumsaliti Edna kutokana na kwamba alishuhudia uwezo halisi na ukatiri wa Roma , mwisho kabisa uwepo wa Monica pembeni yake ungeongeza ufanisi mkubwa kwani Monica alihudumu katika kampuni ya Vexto kwa vipindi vya mabosi wote wawili yaani Rahel pamoja na Edna mwenyewe hivyo uzoefu wake ulikuwa mkubwa.

Lakini jambo la umuhimu sana Ernest alikuwa ni binadamu yake , huenda aliona ngumu kuchagua mtu wa nje ya familia kuongoza kampuni.

Roma aliona pia mpaka Edna kufikia maamuzi hayo huenda alikuwa na mawasiliano ya karibu na Ernest , kwani isingekuwa kitendo cha kufanya maamuzi jana na baada ya hapo kumrihisha kampuni.

Baada ya Roma kuondoka Edna alionyesha hali ya wasiwasi , lakini aliweza kujizuia na kisha akawakaribisha Monica na Ernest kungia ndani ya chumba hicho cha mikutano.

Monica na Ernest walijisikia vibaya kutokana na Roma kuondoka bila kuonyesha furaha ya kuwaona , lakini na wao walijitahidi kutoonyesha hali ya kuathirika na kusalimia kila mmoja aliekuwa ndani ya ukumbi huo.

Baada ya muda wa kusalimiana kwa wale waliokuwa wakimjua Ernest na Monica hatimae Edna aliamua kuwatuliza ili kuendelea na kikao.

“Jamani mpo sahihi huyu ni Ernest , alikuwa ni CEO Msaidizi , jina lake la mwanzo la ukoo alikuwa akiitwa Komwe lakini sasa hivi anafahamika kwa jina la Ernest Kayage, nadhani kila mmoja anafahamu uwezo wake katika kazi hivyo kurudi kwake akiwa ameambatana na Bi Monica ni jambo la bahati sana , Baaada ya kustaafu kwangu nafasi yangu itachukuliwa na Ernest Kayage na Monica atakuwa msaidizi wake , Recho msaidizi wangu atachukua nafasi ya Benadetha kama mkuu wa kitendo cha idara ya uhusiano na masoko na Benadetha atapandishwa cheo na kuwa CEO msaidizi namba mbili akisaidiana na Nasra”Aliongea Edna na kufanya kila mmoja kushangazwa na taarifa hio ya ubadilikaji wa vyeo.

Nasra, Dorisi , Benadetha na Recho walipatwa na mshangao , aliekuwa kwenye mshangao zaidi wa kutokuamini ni Recho baada ya kusikia kwamba anapandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara, kila kitu kwake kilikuwa kama ndoto.

Edna muda wote aliaminika katika maamuzi yake na hata baada ya kutamka mabadiliko hayo madogo hakuna ambaye alipinga kwani walimuamini.

Baada ya mkutano kuisha Dorisi na Nasra walimsogelea Edna haraka haraka wakionekana kuwa na maswali.

“Edna ulimwambia Roma kabla ya kufanya haya maamuzi?”Aliuliza Nasra.

“Aliniambia atanisapoti kwa kila maamuzi nitakayochukua lakini nadhani sasa hivi amekasirika”

“Ndio lazima akasirike , unajua kabisa kilichotokea kati yake na Ernest na sasa hivi..”Aliongea lakini muda huo huo na Ernest aliwasogelea na alioekana kusikia maongezi yao.

“Samahani sana Makamu Nasra , najua tunaonekana kama tumekosa aibu kwa kitendo cha sisi kurudi licha ya mabaya tulioyafanya”

“Vizuri kama unaelewa , Edna anakuchukulia kama binamu ndio maana Roma alikuacha hai , la sivyo tusingekumbuka jina lako muda huu”Aliongea Dorisi akionyesha hajafurahishwa, Monica na Ernest waliangaliana wakikosa neno la kuongezea kupinga kauli yake.

“Hayo yote ni mambo yaliopita na tuachane nayo , hakikisha unafanya vizuri kusimamia Vexto wakati ambao sitokuwepo , sikutaka tu kuona ndugu wa mama yangu wakiishi uhamishoni kwa muda mrefu bila msaada”Aliongea na kumfanya Nasra na Dorisi kuangaliana kwa ishara.

“Edna kama wewe unaondoka na mimi sina sababu ya kubakia hapa kuendelea na kazi , nitatafuta mtu wa kumpendekeza kurithi nafasi yangu”Aliongea Nasra.

“Nilijua tu utaongea hivyo , vipi na wewe Dorisi una mpango wa kuacha pia?”Aliuliza Edna na Dorisi alitingisha kichwa.

“Nitaondoka baada ya kukamilisha majukumu yangu , sitaku kuachwa hapa peke yangu na kuwa nyuma ya mazoezi”Aliongea akimaanisha kwamba hawezi kuendelea na kazi na kushindwa kuendeleza mazoezi ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Monica na Ernest walishindwa kuelewa Dorisi amemaanisha nini kwani kauli yake ilionekana kuwa na zaidi ya maana.

“Juu ya yote Monica Hongera , naona unatarajia mtoto”Aliongea Dorisi.

“Asante sana Dorisi”Alijibu Monnica huku akiweka tabasamu na Nasra na yeye pia alimpa hongera.







SEHEMU YA 563.

Ni muda wa mchana baada ya kikao , Roma hakuwa ameondoka bado ndani ya jengo la kampuni na hata wakati wa Dorisi , Nasra na Edna wanashuka katika Kantini ya kampuni kwa ajili ya chakula waliweza kumkuta.

“Hubby unaonaje ukiungana na sisi kwa ajili ya chakula cha mchana , unaweza kuchagua chochote utakachopenda na sisi tutakula hicho hicho”Aliongea Edna mara baada ya kukutana na Roma njiani lakini Roma hakutaka kuongea nae na kuanza kupiga hatua za kutaka kuondoka akionyesha hali ya kukasirika.

Edna alionyesha kuwa na hofu kwenye macho yake na jambo lile liliwashangaza wafanyakazi waliokuwa wakiona kinachoendelea na hawakutegemea kuona mwanamke mrembo kama Edna kumuogopa mume wake, Edna hakutaka kumpa nafasi Roma ya kuondoka na alimzuia kwa kumshika mkono.

“Unafanya nini , si ulisema wewe mwenyewe siku zote utakuwa ni mwenye kunisapoti? Sikukuomba kuachana na wanawake wako kama tulivyokubaliana lakini kwanini … na isitoshe hili haliwezi kutuletea matatizo , unadhania naweza kumuacha binamu yangu kuzurula huko ugenini bila msaada wowote licha ya yaliowatokea?”Aliuliza Edna na upande wa Roma alijifanyisha kutoridhika.

“Kama nilijua utawarudish kwanini nilitumia juhudi kubwa kuwafukuza kwenda nje ya nchi , naona kabisa binamu wako ni muhimu zaidi kuliko mimi mume wako”Aliongea Roma na kumfanya Edna kukamatika maana alikuwa akimjaribu kuishi ndani ya ahadi yake lakini ilishindikana

“Basi sawa , nakubali nimefanya kosa na sijakutendea vizuri , ni kipi naweza kufanya ili unisamehe?”Aliongea Edna na kumfanya Roma moyo wake kutabasamu ndani kwa ndani , ukweli ni kwamba hakuwa na hasira ila alikuwa akitaka kutumia nafasi hio kuweka mpango wake wazi.

“Okey kwasababbu unaonyesha kubembeleza basi kitu unachopaswa kunifanyia ni kuniruhusu kwenda Cicilly kuwasindikiza Rose na Magdalena wiki ijayo … hivyo sitopata muda wa kukaa na wewe pamoja na Lanlan…”Aliongea Roma lakini palepale sura ya Edna ilijikunja na aliishia njiani kutokumalizia sentensi yake.

“Lakini kama hukubaliani na pendekezo langu , bado tunaweza kujadiliana.. si wewe umesema ni kipi unataka ufanye ili nikusamehe”Aliongea Roma huku akibadili sauti yake.

“Okey hakuna shida unaweza kwenda , hatuwezi kufa au kupotea kwasababu haupo na isitoshe ninaweza tu kumwambia Lanlan baba yake amechagua kusindikiza shangazi zake bada ya yeye”

“Kwanini unataka kumwambia mtoto hivyo ? Nina uhakika Chubby wangu lazima atatafsiri vibaya”

“Hakuna cha kutafsiri vibaya , unaenda kusindikiza wanawake wengine”Aliongea huku akimwangalia kwa macho makali na kumfanya Roma ayakwepeshe ya kwake.

“Sio kama unavyofikiria , marafiki zangu wengi waliopo Cicilly wanataka niende nikaangalie , siwezi kuwapotezea , nipe angalau wiki moja tu na nitawahi kurudi haraka iwezekanavyo baada ya kumaliza kazi yangu”

“Kama ni hivyo kwanini ni Rose na Magdalena ambao wanaweza kwenda huko na sio mimi na Lanlan?”

“Edna haiwezekani , unajua mwenyewe kinachokwenda kutokea huko ni kama vita kati ya wanajeshi na wanajeshi na nadhani mwenyewe unajua tabia ya Lanlan”Aliongea Roma na kumfanya Edna angalau kuelewa maana yake na kujituliza lakini bado hakuridhika.

Wakati Roma akiendelea na maongezi yake na Edna mara palepale simu yake ilianza kuita na alivyoangalia mtu anaepiga ni mama yake mzazi.

Roma palepale alipokea kutaka kujua tatizo ni nini maana mama yake hakuwa na tabia ya kupiga muda kama huo na isitoshe jana usiku tu aliwasiliana nae.

Baada ya kusalimiana ndio muda ambao Blandina alimweleza Roma kuhusu Najma kupata kazi katika wizara kama Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam.

Roma alifurahishwa na taarifa hio , lakini ilimshangaza kwa wakati mmoja mara baada ya kusikia mtu aliewezesha Najma kupata nafasi hio ni raisi Senga na kwa namna ambavyo mama yake alikuwa akisikika ni kama alikuwa na maelewano mazuri na baba yake mzazi, ijapokuwa alikuwa na hisia za aina hio , lakini bado alishangaa kuona mama yake amepiga hatua , lakini hata hivyo alifurahi kwa ajili yake

“Roma baba yako anajitahidi kuanza kujenga ukaribu na wewe , nadhani itakuwa jambo zuri kama utampigia simu na kumshukuru kwa kumsaidia Sophia , isitoshe ni mwanamke wako pia”Roma alifikiria kidogo maelezo yake na kutaka kumuuliza mama yake ni lini akawa na mahusiano ya karibu na Senga lakini alijizuia.

“Mama ni jambo dogo kama hilo amefanya na halihusiani kabisa na mimi kumsogelea , yeye ndie aliekuwa wa kwanza kunikataa kwanini nimfuate na kujipendekeza kwake”Aliongea Roma.

“Najua ndio , lakini ni hasira tu , Senga baba yako amepitia magumu mengi kukuomboleza, huwezi jua lakini alikuwa akikupenda sana wakati ulivyokuwa mdogo na alifanya kila kitu kukuona una furaha, isitoshe ni jambo zuri kama atakutambua , naamini pia uhusiano wako na Denisi utaimarika, ni muda sasa alikuwa na mawazo juu ya Denisi na amekwisha kurudi nyumbani, Roma nakushauri kuepuka ugomvi na Denisi”

“Mama umesema Denisi amerudi?”

“Ndio amerudi baada ya kutokuonekaan kwa mwezi mmoja”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kuhisi kitu cha hatari lakini alipotezea.

Baada ya maongezi ya muda mrefu kidogo Roma alikata simu na Edna alionekana akitaka kujua nini walikuwa wakiongea mara baada ya kusikia jina la Denisi.

“Nimesikia kuhusu Denisi , vipi amerudi?”Aliuliza Edna , alikuwa akijua kutoweka kwa Denisi kupitia Ashley ambaye alikuwa akiongoza projekti yake ya dawa aliongia nayo mkataba na Profesa Clark.

Ashley alikuwa na mwezi mmoja tokea arudi nchini Tanzania na aliteuliwa rasmi kama mkemia mkuu wa serikali na baba yake na kutokana na mafanikio yake hakuna mtu aliepinga nafasi yake, lakini licha ya hivyo Roma hakuwahi kukutana na Ashley tokea arudi nchini , huenda ni kwasababu ya ubize wake ndio maana.

“Mama amesema kwamba Denisi amerudi na kwa maelezo yake anasema hatoondoka tena na mpango wake ni kubadilika na kuwa mtoto mwema na ameweza hata kwenda nyumbani kwa Afande Kweka na kumuomba amuunganishe na jeshi kwani anataka kulitumikia taifa”Aliongea Roma.

“Kama ni hivyo kwanini uso wako upo hivyo , je una kwenda kumuua?”Aliuliza Roma na alishindwa kujibu swali lake , ukweli ni kwamba Roma hakuwa kabisa na mpango wa kumua tena Denisi tena , na hakujali pia makuzi yake yalikuwaje na isitoshe kwa muda huo hakutaka mitafaruku zaidi kwani alipenda amani ndani ya familia yake.

Lakini licha ya hivyo alihisi kuna kitu kinaendelea kuhusu kuonekana kwa Ghafla kwa Denisi na kuanza kutaka kujiunga na jeshi, ijapokuwa hakuwa na sababu ya msingi ya kujisikia hivyo lakini hisia zake zilimwambia kabisa kuna kitu hakipo sawa kuhusu Denisi.

“Tutaona pia namna itakavyokuwa , si unakumbuka mzee Kweka alituhitaji tukusanyike Iringa siku zijazo kama familia , nadhani nitapata fursa ya kujua mchezo anaopanga kucheza., siwezi kuogopa kumuua kama kuna kitu kibaya anachopanga lakini siwezi kufanya hivyo mbele ya Lanlan na kuja kufahamu kwamba nilimuua mdogo wangu”Aliongea Roma.

Roma siku ambayo alienda kumchukua Lanlan mara baada ya kurudi Dubai aliweza kuambiwa na Afande Kweka kufika Iringa mwanzo wa mwezi unaokuja.

Afande Kweka alikuwa akihamia rasmi Iringa na kufanya makazi ya kudumu, alitaka angalau kukaa karibu na mifugo yake na kuufurahia uzee wake, Roma hakuuliza sana juu ya safari hio ya kwenda Iringa.

Ukweli ni kwamba siku hio ilipangwa maalumu na Afande Kweka kuwakutanisha rasmi Raisi Senga na Roma ili kumaliza tofauti zao na hio ni mara baada ya Raisi Senga kufika nyumbani na kuweka nia yake wazi na kuomba baba yake mzazi kumsaidia katika kuirudisha familia yake katika mstari.

Edna aliridhishwa na kauli ya Roma kwamba hawezi kumruhusu Lanlan kushuhudia yeye mwenyewe akimuua mdogo wake.

“Naona mume wangu umezidi kuwa na busara”Aliongea Edna huku akitoa pumzi ya ahueni lakini kauli yake ilimfanya Roma kuona aibu kidogo za kiume , tokea aoe na hatimae kuwa na mtoto alianza kuzingatia mambo mengi .

“Turudi kwenye topiki yetu mke wangu , naomba uniruhusu niondoke angalau kwa siku saba , ninakuahidi nitarudi mapema na wote kwa pamoja tutaenda Iringa, nyie wawili mtachceza mtakavyo mara baada ya kufik, sawa babe?”Aliongea kwa kubembeleza.

“Ole wako uchelewe kurudi na kutumia siku nyingi na kututelekeza mimi na mtoto , nakuambia hutoweza kuvumilia matokeo yake”Aliongea Edna , hata hivyo alijua asingeweza kumzuia , alifurahi kwamba alikuwa akiombwa ruhusa hivyo hakutaka kuleta mambo mengi.

******

Katika siku zilizofuata Edna tayari alianza taratibu za kuhamisha uongozi wake kwenda kwa Ernest na kumkabidhi kila kitu.

Upande wa Roma na yeye baada ya kuona Edna kaacha kazi na yeye hivyo hivyo aliacha na nafasi yake akampatia Daudi.

Edna rasmi akawa sio CEO tena wa kampuni ya Vexto na maswali mengi katika vyombo vya habari yaliibuka lakini kampuni iliishia kutoa maelezo kwa ufupi kwamba Edna alijiuzuru kwa sababu za kifamilia.

Ilikuwa ikishangaza kwani Edna alikuwa amejijengea jina kubwa sana katika ulimwengu wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

Upande wa Edna alionekana kufurahia maamuzi yake na alitumia muda mwingi nyumbani kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi huku akipewa maelekezo na Rufi kutokana na uelewa wake ulioambatana na uzoefu.

Bi Wema alifurahi sana kuona namna ambavyo Edna alijenga ukaribu na Rufi mtoto wake, hata ile hali ya uzee aliokuwa nayo ilianza kutoweka na sasa alianza kuwa kijana zaidi , huenda mawazo ya kumkumbuka mwanae yalimtesa miaka na miaka na baada ya kurudi alijisikia vizuri zaidi.

Upande wa Amina baba yake alikuwa akiendelea vizuri na hio ni mara baada ya kupewa kidonge cha kijini na Roma, ijapokuwa ugonjwa wake haukuwa umepona lakini hali yake iliimarika kidogo lakini licha ya hivyo hakuweza kurudi kwenye kampuni tena.

Amina mara baada ya kusikia Edna kajiuzuru na yeye alitamani kufanya hivyo lakini hakuwa na mtu wa kumrithisha hivyo aliachana na mawazo hayo na kuendelea kufanya kazi huku akifanya mazoezi ya kuvua nishati za mbingu na Ardhi.

Upande wa Qiang Xi na yeye alikuwa na wasiwasi mara baada ya Edna kujizuru kwa kugopa kwamba kazi yake ya kumlea Lanlan moja kwam moja ingehamia kwa Edna , lakini Edna alijua wasiwasi wake na kumwambia hana haja ya kuwa na wasiwasi na Edna alimwambia kama atakuwa na mpango wa kutaka kurudi nchini China basi atahakikisha anamsaidia namna ya kwenda kuanza maisha , lakini mrembo huyo wa kichina aligoma na kusema anataka kubakia Tanzania kwa muda.

Kauli yake hio ni kama ilieleweka , walijua tu lazima Qiang Xi alikuwa akitegemea Master wake atarudi Tanzania kumuona Lanlan na yeye ndio maana hakutaka kuondoka , isitoshe pia aliogopa kwamba kuna baadhi ya majukumu hakuwa ametimiza kwa ajili ya Lanlan kama alivyoagizwa na Master wake.

Siku ya jumapili ndio siku ambayo Roma alianza safari yake ya kuelekea katika visiwa vya wafu.

Magdalena na Rose licha ya kwamba walisuburia kwa wiki tu , lakini kutokana na shauku yao ilimwafanya kuona kama wamesubiri muda mrefu na hawakuamini siku ya kesho ndio hio ambayo wanatarajia kuona mkutano huo wa kaisari au Baraza la kaisari ambalo hukutanisha vikosi vya wanajeshi wa kulipwa kutoka makundi mengi duniani.

Siku walizoishi katika visiwa vya wafu , ukiachana na kufanya mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini pia waliweza kuzoeana na raia wanaoishi katika visiwa hivyo.

Ijapokuwa walikuwa wakipata shida ya kuwasiliana kutokana na baadhi ya wengi wao kujua kitaliano , lakini kutokana na kwamba walikuwa katika levo ya Nafsi uwezo wao wa kujifunza lugha mpya ulikuwa mkubwa mno.

Lakini pia asilimia kubwa ya wakazi wa visiwa hivyo kuwa ni wanajeshi wastaafu basi ilikuwa rahisi kwao kupata watu ambao walikuwa wakizungumza lugha ya kingereza na kuelewana, walichofurahi zaidi hawakuonyeshewa ubaguzi kutokana na rangi zao.

Ron kwasababu ndio aliekuwa ana kwenda kuwa mwenyeji katika kipindi chote watakachokuwepo Cicily basi aliweza kufanya maandalizi yote ya safari.

Baada ya Roma kufika tu Ron tayari amekwisha kuandaa Ndege binafsi iliokuwa ikimsubiri yeye na wanawake wake kupanda na kuondoka visiwani hapo.

Kutoka Visiwa vya wafu mpaka Cicilly ulikuwa ni umbali wa nusu saa tu na kama wangependa kusafiiri kwa mbinu za kijini basi ingekuwa ni kufumba na kufumbua , lakini kutokana na kwamba ilikuwa kama safari ya kimatembezi basi waliona watumie ndege.

Cicilly kilikuw ani kisiwa cha watu wengi na kilikuwa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.

Kama ilivyoelezwa katika historia , Ugiriki ya kale , Warumi , Wabzantine(Byzantines), Vikings(Norman) na wengineo ndio ambao walitawala kisiwa hicho hapo kabla , baada ya mgawanyiko wa tawala ya kifalme ya Cicily wahispania na wao walikitawala na baada ya hapo ndipo utawala wa Italy ulikichukua na kuanzia hapo ndipo Cicily ilipoweza kujiendesha yenyewe.

Ni sehemu katika Italy ambayo ni maarufu sana kutokana na kwamba ndio mahali ambapo makundi ya Kimafia duniani yalitokea kwa wingi na kutawala eneo lote ,

Familia za kimafia walikuwa ni kama serikali kivuli ndani ya miji ya visiwa hivyo na walienda sambamba na serikali na hawakuweza kutokomezwa kutokana na makundi hayo kupandikiza watu wao serikalini.

Katika eneo hilo sheria ya kiserikali haikufanya sana kazi au kufuatwa na sheria ambazo zimetungwa na makundi hayo ya kimafia ndio ambazo zilikuwa na nguvu.

Familia ya Constantine ndio familia ambayo anatokea Ron na ndio moja wapo ya familia ambayo ilikuwa ikiogopeka kwa kumiliki kundi kubwa la Mafia Gang.

Lakini hata hivyo Ron alikuwa tayari ashaachia ngazi kama kiongozi wa familia hio na kuhamishia maisha yake katika visiwa vya wafu lakini licha ya hivyo ukubwa wake ndani ya familia bado ulikuwa ukichukuliwa siriasi na alikuwa akiheshimika.

Wakiwa katika ndege Magdalena na Rose waliweza kushangazwa na tamaduni nyingi ambazo Ron aliwaambia kuhusiana na watu wa Cicily lakini shauku yao yote ilikuwa kwenye umoja wa makundi ya kimafia ufahamikao kwa jina la Mafia Alliance.

“Mr Ron nimeweza kusikia kutoka kwa watu kule kisiwani kwamba ulikuwa raisi wa Mafia Allianace? Tuambie ni kwa namna gani uliweza kupata cheo hicho , inashangaza sana?”Aliongea Rose kwa shauku kubwa , kundi lake la Tembo lilikuwa kama chawa kwa makundi ya kimafia ya Itali, watu wa huko walikuwa ni Ma’gangstar wa kihistoria.

“Lady Rose hayo yote ni kwasababu ya Mfalme Pluto , ukweli ni kwamba kama asingetusaidia huenda makundi yote ya kimafia ndani ya Cicily yangetokomezwa”

“Roma ndio kafanya hivyo ?”Aliuliza Magdalena kwa shauku.

“Ukweli ni kwamba wale watu waliokuwa na nguvu ndani ya makundi yetu walikuwa wakipungua siku hadi siku hivyo kupunguza ukubwa wa shughuli zetu na zaidi ya yote watu wa dunia walianza kutuchoka na kipindi hicho serikali ilichukulia jambo hilo kama fursa na wakasambaza wanajeshi wa vitengo maalumu kupambana na sisi , ijapokuwa kipindi hicho tuliweza kupata taarifa mapema ya mpango wa serikali lakini ilikuwa ngumu kwetu kuweka ukinzani , unachotakiwa kuelewa ni kwamba kama serikali ikiamua lake hawachukui tahadhari za aina yoyote, kipindi ambacho tunakaribiwa kushindwa kwa kukosa siraha na watu wa kupambana ndio kipindi ambacho Ghafla tu mfalme Pluto alitokeza”Aliongea huku akionyesha hali ya kukumbuka kipindi kilichopita.

“Nakumbuka kabisa kipindi hicho Mfalme Pluto alitokeza mbele ya maadui zetu na kuharibu siraha zao na kuharibu magari yao ndani ya muda mfupi tu , wanajeshi waliotumwa kipindi hicho walikuwa ni kutoka kambi ya kijeshi ya Uingereza iliokuwa pembeni ya Rome na walisifika kwa uhodari wao lakini Mfalme Pluto aliweza kubadili hali ya hewa kwa kumuua Kamanda wao na mkono mmoja tu , baada ya tukio hilo kundi letu lote lilipata nguvu upya na tuliweza kupambana mpaka tukashinda na baada ya machafuko kuisha ndio nilivyoweza kupata cheo cha uraisi wa Mafia Alliance kama hsehima , lakini ukweli ni kwamba sikufanya chochote..”Aliongea huku akimwangalia Roma kwa namna ya kumkubali, Rose na Magdalena na wao walimwangalia kwa macho ya kiulizo

Muda huo Roma hakuwa ni mwenye kujali stori zao kwani alikuwa bize kula matunda ya zabibu yaliokuwa kwenye sahani na baada ya kugundua anaangaliwa aliwasogezea sahani.

Upande wa Magdalena na Rose waliweza kuona kuna utofaut mkubwa kati ya matarajio yao na uhalisia wanao uona na pengine wanaokwenda kuushuhudia.

Kuna nini huko kwenye Kaisari Conference , je unadhani wanaenda tu kuangalia mapambano tu na Roma anawasindikiza tu warembo hao , jibu linakuja.
 
SEHEMU YA 564.

Ijapokuwa waliona kama alikuwa akitania , lakini walijiuliza anawezaje kula matunda wakati wao wanaongea stori zinazomuhusu, lakini licha ya hivo walipokea sahani ile ya matunda kubeba zabibu na kula.

“Tulikuwa tukiongea kuhusu wewe mwanaume , Hujatuambia chochote na mimi na Magdalena tunashauku ya kujua maisha yako yaliopita.”Aliongea Rose.

“Kuna nini cha kuongelea , sio mambo ya kufurahisha hata hivyo”Aliongea na kumfanya Magdalena kumgeukia Ron.

“Mr ulikutana vipi na Roma na kwanini akaamua kuwasaidia mpaka ukaja kuwa raisi wa Mafia alliance?”

“Miss Magdalena , kama nitakuwa mkweli hata mimi sijui chochote na ni swali ambalo namuulizaga sana Mfalme Pluto lakini mpaka leo hii hakuwahi kunipatia majibu, sikuwa kabisa nikimfahamu kipindi ambacho serikali inatuvamia wala hata kupishana nae mahali , katika muda huo kuonekana kwake kwa ghafla kulitushangaza sana lakini juu ya yote yeye ndio ambaye alituwezesha kupiga vikosi vya Muingereza, Italy na Ufaransa”Aliongea na kuwafanya kuangaliana , hawakutegemea Roma kuwa mtu mwema mpaka kusadia watu wanaotaka haki yao licha ya kwamba makundi hayo ya kimafia hayakujali sana kuhusu haki.

“Hubby kwanini ulimsaidia Ron kipindi hicho?”Aliuliza Rose na kumfanya Roma asugue pua yake.

“Kwanini mnataka kujua , huenda kipindi hicho nilikuwa nimelewa na nilikuwa nikijisikia kuua mtu”

“Acha kuzunguka , siku zote lazima usugue pua yako ukiwa unadanganya”Aliongea Rose huku akimfinya na kumfanya Roma afikirie na kisha akakaa vizuri.

“Ukweli ni kwamba nilimsaidia kwa bahati mbaya”

“Kwa bahati mbaya , unamaanisha nini?”

Rona hata yeye alionekana kusikiliza kwa umakini kwani alitaka kupata majibu kwanini Roma alimsiadia kipindi kile ghafla tu licha ya kwamba hakuwa na urafiki nae wala kuwa na udugu.

“Katika kipindi kile nilikuwa na makubaliano na Catherine ,, namaanisha mama yake Clark , yalikuwa ni makubaliano ya kumsaidia kuzuia vikosi Vya Uingereza kumkamata , lakini pia kumsaidia kupata nafasi yake kama mrithi wa kiti cha kimalkia, kwa bahati nzuri ni kwamba mtu ambaye alikuwa amepewa jukumu la kumtafuta Cathernine na mtoto wake popote walipo ili kuwaua alikuwa ni Kamanda wa kikosi maalumu ambaye pia alikuwa amepewa jukumu la kushambulia Sicily, hivyo siku ambayo alikuwa akiongoza kikosi kushambulia kundi la kimafia ndio niliweza kumtafuta mpaka kumpata , sikuwa na muda wa kusubiria amalize kupambana na kundi la Kimafia mpaka kuwamaliza kwani nilihitajika kurudi tena Uingereza kumaliza kazi , hivyo nikamuua hapo hapo na kuondoka”Aliongea na kumfanya Ron kuwa katika muonekano usioelezeka , akiwa sasa ameelewa kwanini Roma aliwasaidia kipindi kile , ni kweli kabisa sio kama alipanga kuwasaidia lakini kutokana na adui yake kuwa adui yao basi ndio ikatokea hivyo.

Akiwa na tabasamu la uchungu alishindwa kuongea chochote kwani licha ya hivyo bado alikuwa na deni kwa Roma , hivyo hakujisumbua sana.

Rose na Magdalena walishindwa kuzuia vicheko vyao namna ambavyo Roma alielezea kile alichokifanya , waliona ni Roma pekee dunia hii mwenye kufanya vitu bila kujali hali ya mazingira.

Ni muda mfupi tu wakati wakiendelea kuongeahatimae waliweza kufika Palermo mji mkuu wa Sicilly..

Palermo ni moja wapo ya jiji ambalo lilisifiwa sana na Dante katika mashairi yake kama taifa zuri la kiislamu duniani kipindi cha utawala wa Waarabu , ni jiji ambalo majengo yake yalikuwa na mchanganyiko wa usanifu wa kiarabu na kirumi pande zote, Warabu waliacha alama ya utawala wao kupitia majengo mpaka leo hii.

Baada ya kutoka katika ndege waliweza kupokelewa na bwana aliefahamika kwa jila la Fidero , alikuwa ndio mkubwa katika ukoo wa Constantine lakini pia alikuwa ni mtoto mkubwa wa kiume wa Ron , alikuja akiwa na magari kadhaa ya Bentley ambayo yalikuwa yakiwasubiria nje ya uwanja wa ndege.

Muonekano wa Fidero ulikuwa ukifanana sana na wa Ron , ni bwana mwenye masharubu huku akiwa amevalia miwani ya fremu za chuma zilizonakshiwa na madini ya dhahabu, kwa muonekano wake usingedhania kama ndio kiongozi wa kundi la kimafiaa la Constantine.

Baada ya Roma alievalia tisheti ya pundamilia ya rangi ya bluu na nyeupe kutokezea mbele ya Fidero na kundi lake , mabwana hao wote walionyesha hali ya kujiamini zaidi.

“Mfalme Pluto karibu ndani ya Sicily kwa mara nyingine”Waliongea kwa lugha ya kiitaliano pamoja na kisha wakainamisha wote vichwa chini kuonyesha heshima.

Baadhi ya watu waliokuwa wakipita hawakuona ni jambo la ajabu , ndani ya Sicilky hususani katika makundi ya Mafia ni jambo ambalo limezoeleka na haikuwa jambo la kushangaza pale anapoonekana mtu amepiga magoti kwenye barabara akimsujudu mwingine wa cheo cha juu yake.

“Fidero fanyeni hivyo kwa baba yenu , mimi kwangu sio lazima sana”

“Haha..Mfalme Pluto wanajaribu kuonyesha heshima yao kwako , wangekuwa wafu kama isingekuwa wewe kuwasaidia”Aliongea na kumfanya Roma kupandisha mabega , alijua watu hao hawawezi kubadilika licha ya miaka kusogea, hivyo hakujali sana.

Rose na Magdalena waliingia kwenye gari huku wakishangaa monekano wa jiji la Palemro kupitia vio vya gari , utajiri wa majengo ya ubunifu wa kigothiki , kirumi na mengineyo uliwafanya kuvutiwa mno maana ilidhihirisha historia ya mji huo.

Kwenye mitaa na masoko watalii pamoja na raia wa kawaida walitembea huku wakiongea kwa furaha , kulikuwa na makabila yote ya watu , weusi ,Wa’Asia na wazungu na kufanya jiji hilo kuwa kama tamaduni za dunia zimeuangana kwani kulikuwa na staili zote za kimavazi.

“Ni jiji la kawaida la kitalii sioni cha upekee sana m je hili ni jiji kweli linalosifika kuwa na makundi ya kimafia?”Aliuliza Rose.

“Babe Rose , unafikiri makundi ya Kimafia ni kama vile unayoona kwenye runinga , wanapaswa kuishi vizuri hata wao pia , sio watu wote wanapenda maisha ya vurugu na wao muda huu wamekaa na familia zao katika sehemu tulivu , Mafia ni kama watawala wengine ndani ya visiwa hivi na sio kama makundi ya kigaidi, ni kwamba tu wanapenda sana kutatua migogoro yao kwa njia za fujo”

“Ni kweli kabisa alichoongea Mfalme Pluto , ukweli ni kwamba vitu vingi unavyoviona vimejengwa na makundi yetu ya kimafia na kusimamiwa na muungano wetu , kwetu sisi hapa ndio nyumbani na sio eneo la fujo kama watu wanavyotuongelea”Aliongea Ron.

“Je ndio tunaelekea nyumbani kwa Ron sasa hivi?”Aliuliza Magdalena aliekuwa kimya muda wote.

“Hapana familia yangu ipo huko Caltanissetta , sisi tupo hapa Palermo kwasababu ufunguzi wa Caesar Conference, unafanyikia ndani ya Colosseum upande wa ufukweni karibu na bandari , sasa hivi tunaelekea katika hoteli ya Federico , tushafanya Booking tayari”

“Collosseum!! , si jengo hilo nasikia lipo Rome?”Aliuliza Magdalena

Colloseum ni eneo maalumu ambalo limetengenezwa kwa ajili ya maonyesho ya kimapigano , ni kama Arena(Ulingo) lakini katika wau wa enzi hizo waliita Colloseum.

“Hehe ..hio ndio Colloseum maarufu , ukweli ni kwamba kuna Colloseum nyingi duniani na ilioko hapa Palermo ni moja wapo lakini hata hivyo imejengwa kwa kujitegemea karibu na bandari , mara nyingi ilitumika kufundishia watu wetu wa makundi ya kimafia lakini kwanzia wiki inayoanza kesho litabadilika na kuwa sehemu ambapo Caesar Conference hufanyikia”

Kusikia maelezo yake iliwafanya Rose na Magdalena kujawa na shauku ya siku hio ya keshio itakapofika , maana walichukulia kama tukio kubwa lingine kubwa zaidi ndani ya dunia.

Baada ya zaidi ya dakika kumi mbele , Fidero aliekuwa ameketi mbele alionekana kuongea na simu yake kwa kutumia lugha ya kilatin na kisha akakata simu na sura yake ilionekana kubadilika.

“Fidero kuna tatizo lolote limetokea hotelini?”Ron aliuliza.

“Ndio baba , mmiliki wa hoteli ya Federico amasema kuna watu tayari washachukua vyumba vyetu vya VIP ambavyo tulikuwa tumevifanyia booking na wanatishia kuua mtu yoyote atakaewaambia watoke”

“Nani hao wenye ujasiri hivyo?”Aliuliza Ron.

“Sina uhakika , mmiliki amesema ni kundi la watu wahuni ambao wamevalia nguo aina ya Cloak rangi nyeupe na Mask za rangi ya njano , hawakutaka kujitambulisha na wameshindwa kutambulika hata kwa rafudhi zao , kuna baadhi ya wanajeshi ambao walitaka kupigana nao wakimsaidia mmiiliki lakini wote wamepigwa na kuumizwa , uwezo wao unaonekana kuwa mkubwa”Aliongea Fidero.

Cloak ni mavazi flani kama majoho ambayo yana kofia kubwa kama vile zile za sweta lakini ambazo huficha uso wote unaweza kugoogle kupata picha kamili.

“Cloak za rangi nyeupe na Barakoa za njano?”Ron alijikuta akikunja sura yake na kisha akamgeukia Roma.

“MfalmePluto sikumbiki kundi la kimasenari ambalo linatumia mtindo huo wa mavazi , je unafahamu chochote?”

“Sijui , huenda ni kundi jipya?”Aliongea Roma na kumfanya Ron kutingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kwanini wachukue vyumba vyetu , je ni maadui zetu?”Aliuliza Magdalena.

“Haiwezi kuwa hivyo , Hoteli ya Federico ni moja wapo ya hoteli za hadhi ya juu sana ndani ya Palermo , vyumba vyao vya VIP vinaendana na jina lenyewe , katika siku za hivi karibuni watu wa hadhi za juu , matajiri pamoja na makundi ya kijeshi kutoka pande zote za dunia ndio mahali wanapofikia , lakini kipindi ambacho Caesar Conference inafanyika wanaokaa katika vyumba hivyo ni wale wanajeshi wa hadhi ya juu sana kuliko wote , nadhani wamefanya hivyo ili kuonyesha kila mmoja kwamba ni wa hadhi ya juu na hawaogopi kitu”Alielezea Ron.

Baada ya kusikia maelezo ya Ron, Magdalena alionyesha kuwa katika hali ya wasiwasi , sio kwamba alikuwa akiogopa lakini wasiwasi wa mchecheto wa kwenda kuona kile kinachokwenda kutokea , isitoshe waliona kama ni jambo zuri kukaribishwa na mapigano.

Fidero yeye alikuwa na wasiwasi, baba yake alimwagiza kuandaa kila kitu ili kurahisisha matembezi ya Roma hapo jijini hayampi shida lakini kundi la wahuni ghafla tu wanatokea, alikuwa na wasiwasi kwa kuona Roma anaweza kumlaumu kwa kutokufanya kazi nzrri.

“Baba tulifanya booking ya vyumba vitatu ndani ya hoteli ya Federico , kimoja kilikuwa ni cha mfalme Pluto , kingine cha cha wanawake pamoja na vya wanajeshi wa The Eagles watakao shiriki , nina wasiwasi wanajeshi wetu watapitia changamoto wakishafika”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani sio kosa lako , nadhani tutafika mapema kabla ya The Eagles kwa spidi hii”

“Mr Ron je mnatuma The Eagles pekee awamu hii?”Aliuliza Rose.

“Madam Rose chaguzi ya washiriki ipo chini ya Sauron , ijapokuwa timu yetu inafahamika kwa jina la The ‘Eagles lakini wwanaohusika wanatokea katika sehemu mbalimbali katika idara zote zilizopo chini ya Mfalme Pluto , ukijumlisha na Maninja wa New Zero, ni kwamba hatuwezi kuhusisha The Eagles pekee kupamabana wenyewe hivo tunachokifanya ni kukusanya timu moja , katika kila Caesar Conference wanajeshi ambao wamepiga hatua ndio wanapangwa mbele ya wanajeshi wote waliochagauliwa “

“Wakati nilipokuwa Tanzania , nilikutana na Diego yeye nafasi yake ni ya ngapi katika kikosi chote?”Aliendelea kuuliza Rose.

“Kapteni Diego yeye anahusika na upande wa nchi za Ki’Nordic , ukweli ni kwamba yupo vizuri sana katika mapigano ya kwenye salutji na projekti nyingine, kivita nadhani naweza kusema ni moja wapo ya wanajeshi wa viwango vya juu ndani ya kosi lote la The Eagles, lakini licha ya hivyo hafikii hata kidogo wanajeshi ambao wanachaguliwa kushiriki katika Caesar Conference , kama nitamlinganisha na Maninja wa New Zero yuko chini sana”Aliongea na kumfanya Rose kushangaza , alikuwa akiujua uwezo wa Diego lakini ilimshangaza kwamba hakuwa akifikia watu ambao wanachaguliwa kwa ajili ya mashindano , alizidi kujawa na shauku ya kutaka kuona wawakilishi wa Roma katika mashindano hayo wanauwezo kiasi gani.

Roma aliwaangalia Rose na Magdalena namna ambavyo wana shauku ya kutaka kuona damu inavyomwagika , kama ingekuwa ni Edna angemzuia na kumwambia hataki ajihusishe na vitu ambavyo vingempelekea kuua , lakini kwa Rose aliamini asingemzuia kuua pale mtu anaestahili kuuliwa akiwa mbele yake.

Baada ya muda, gari walilopanda liliweza kufika katika hoteli kubwa na ya kifahari ya Federico .

Ilikuwa ipo kando ya bahari na ilivutia sana na staili yake ya ujenzi kama Serena kwa haba Dar es salaam lakini ilioenda hewani zaidi.

Ukilinganisha na muda huo jua lilikuwa likielekea kuzama lakini pia upepo wa baharini uliwafanya kujisikia vizuri mno mara baada ya kutoka kwenye gari.

Nje ya hoteli kulikuwa na magari ya kizamani yaliowekwa kama mapambo, yalikuwa ni matoleo ya juu ya magari ya vipindi maalumu katika miaka iliopita.

Baada ya Roma na wengine wote kutoka nje ya magari , baadhi ya gari za kubebea wagonjwa zilitoka katika eneo hilo la hoteli kuwahisha majeruhi hospitalini .

Mmiliki wa hoteli hio ya Federico alikuwa ni Mwarabu mwenye kitambi kikubwa na muda huo alikuwa akifanya swala kuomba hali ya hewa kuwa sawa na majeruhi kupona.

“Hassan hali ikoje hapa?”Aliuliza Fidero.

“Allahu Akbar!, Mr Fidero hatimae umefika , naomba unisamehe kwa uwezo wangu mdogo , hutoweza kupata vyumba vya VVIP kama ulivyoomba , watu waliovichukua ni wakatili mno , ninapaswa kufikiria na maisha ya wafanyakazi wangu pia”

“Hakuna kifo kilichotokea?”Aliongea na Mzee huyo mnene mwenye kibakarashia alipiga piga kifua chake kujituliza.

“Ndio hakuna kifo , ijapokuwa baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakipigana wameumizwa lakini hali zao sio mbaya sana , nadhani hawa watu walizingatia kwamab wakiua mtu hawatoruhusiwa kujiunga katika mashindano”

“Hapo afadhali”

“Wako wapi?”Aliingilia Ron na mara baada ya Hassan kumuona Ron aliinamisha kichwa chake haraka kuonyesha heshima.

“Oh! Raisi Ron kumbe na wewe umefika , tafadhari nisaidie wapo ndani ya vyumba vya VVIP”Aliongea na kumfanya Ron kutingisha kichwa na kisha akamgeukia Roma.

“Mfalme Pluto nitaenda na baadhi ya vijana ili kuongea nao , naamini hawatataka kwenda kinyume na muungano wote wa kimafia wa Sicily”Aliongea Ron kwa sauti.

Upande wa Roma hakuwa na tatizo lolote na kile kinachoendelea lakini kwa Ron alionyesha kabisa alikuwa akilinda taswira yake.

“Tuachie sisi hio kazi”Ilisikika sauti ya mwanaume akionge kwa Kingereza

Walikuwa ni wanaume na wanawake wenye miili ya saizi tofauti tofauti ambao walikuwa wakishuka katika gari yenye bodi nyuma.

Mwaname wa miraba minne mwenye meno yake ya njano ndio alietoa sauti hio huku akiwa na tabasamu.

Nyuma ya mwanaume huo alifuatia mwanamke mwenye kiuno chembamba mkakamavu mwenye asili ya Kiafrika akiwa na nywele zake ndefu nyeusi huku sura yake ikiwa ni ile ngumu ya kibabe., alikuwa ameambarana na mwanaume mwingine wa kichina ambaye macho yake yamekaa kiugomvi ugomvi , alikuwa ni kama vile muda wowote ataanzisha vurugu na wengine wote wawili walikuwa ni wazungu.

Jumla yao wote walikuwa ni watano na walivaa mavazi ya kawaida kama vile walikuwa ni watalii.

“Your Mojesty Pluto it is an honor to have you here watching ou Compitition this time”Aliongea yule bwana huku akiwa na tabasamu lililojaa wasiwasi akimwambia Romakwamba ni heshima kuwepo kwake hapo kuangalia mashindano yao.

“Nyie ndio wanajeshi mliochaguliwa na Sauron kushiriki katika mashindano?”Aliuliza Roma.

“Ndio mfalme Pluto, Sisi ndio wenyewe na kama huamini Afande Sauron atafika hapa muda si mrefu na atatuthibitsha kwako”Aliongea mwanamke aliekuwa ni mweusi akionyesha hali ya kutokumuogopa Roma.

Yule bwana wa miraba minne alimpa ishara yule msichana kuacha ukorofi na kisha akamgeukia Ron.

“Mr Ron naomba nijitambulishe kwako , mimi ndio kapteni wa timu yangu naitwa Nasri kutoka tawi la The Eagles upande wa Magharibi mwa Ulaya , tushapewa taarifa tayari na kwasababu vyumba vyetu vimechukuliwa kinguvu tunakwenda kuvirudisha muda huu”Aliongea kwa kujiamini.

Ron hakuwa amekutana na wanajeshi watano waliochagaliuwa katika mashindano na kwasababu aliamini walikuwa na uwezo , basi itakuwa sawa kwao kuweka mambo sawa katika hoteli hio, lakini pia walitaka kuangalia uwezo wao.

Nasri mara baada ya kupewa ruhusa alimsogelea Hassan mmiliki wa hoteli na kisha akaongea nae maneno machache na alionyeshwwa kwa kidole juu Ghorofani vyumba vyao ambavyo vimechukuliwa.

Katika kitendo cha kushangaza palepale Nasri alianza kuruka katika jengo hilo kupitia madirisha kama nyani na ndani ya dakika tu alikuwa juu kabisa ya jengo katika dirisha la vyumba vyao.







SEHEMU YA 565.

Lakini hata hivyo wanajeshi hawakuonyesha kushangaa kutokana na uwezo wake na wepesi wa kupanda kwa haraka licha ya urefu wajengo hilo, wanajeshi waliokuwa wakiangalia na wenyewe walikuwa na shaku ya kutaka kuona ni uwezo gani ambao Nasri anao kuweza kushindana na wahuni waliovamia vyumba vyao.

Nasri mara baada tu ya kufika kwenye Balkon alisukuma mlango wa kuingilia ndani lakini wakati anataka kuingia alijikuta akitoa ukulele wa maumivu

“Oh!!

Kivuli cha mtu mweupe kilionekana kikimshambulai Nasri moja kwa moja katika kifua chake na alionekana kutumia nguvu kidogo tu lakini Nasri alifyatuliwa na kurudi chini kama furushi.

Ron , Fidero na wengine walishangazwa na jambo hilo , uwezo huo ulikuwa mkubwa mno ambao kundi la Kimafia lisingeweza kuhimili , nguvu zao na spidi yao haikuwa ya kutabirika kabisa.

Nasri alionekana kama mtu aliebahatishwa lakini licha ya kudondoka chini aliweza kudhibiti mwili wake hivyo kumzuia kutopata majeraha makubwa lakini katika sehemu ambayo alipigwa eneo la kifuani kulionekana kuathirika kwani hata nguo zake zilichanika katika eneo hilo.

Roma yeye licha ya kwamba alitegemea kuona Nasri kuwa na uwezo mkubwa , lakini hakutarajia kumuona akiwa ni mtu anetumia nguvu za ziada mpaka kuweza kupanda ghorofa hilo kwa haraka , lakini pia kupigwa kurudi nchini na kuweza kudhibiti mwili wake na kudondoka vizuri na kukwepa madhara alionekana kumkubali kiana.

Muda huo huo yule bwana aliempiga Nasri kifauani , alijua kabisa hakuwa amempiga kisawa sawa hivyo aliruka kutoka juu kumfuata chini na sasa alifanya Roma na wengine kuweza kuona aina ya watu waliochukua vyumba vyao.

Ijapokuwa waliambiwa tu kwamba watu hao walikuwa wamevalia Cloak za rangi nyeupe na mask za rangi ya njano , lakini ukweli ni kwamba mavazi yao yalikuwa na michoro ambayo iliashiria kitu flani , walikuwa na machata kama vile ni aina ya maandishi yaliotumia Alama za kizamani maarufu kama Runes, lakini kilichomshangaza Zaidi Roma ni mara baada ya bwana yule alievalia maski na mavazi meupe kugeuka na kumpa mgongo Roma kwani palepale aliweza kusoma chata kubwa a maandishi lilokuwa kwenye mavazi yao.

‘DEICIDE ‘

Lilikuwa ni neno ambalo limeandikwa kwa maandishi ya rangi nyekundu maana yake kwa tafsiri ya kingereza ni godkiller au muuaji wa miungu kwa lugha ya kiswahili.

Roma alijikuta akianza kuchezesha midomo , aliamini kabisa jina hilo licha ya kuwa kama kiwakilishi lakini aliweza kujiambia sio neno ambalo limeandikwa kwa bahai mbaya kama watoto wa mtaani au vijana kutumia majina kwa ajili ya kujigamba.

Miaka kadhaa iliopita wakati Roma alivyoweza kurithi cheo kutoka kwa Hades wa zamani , haikuhesabiwa kama kumuua mungu kwasababu alikuwa na uungu ndani yake wa kumuwezesha kubeba jina la Plut

Ilisemekana ili uwe sehemu mungu kumi na mbili kwa kurithi unapaswa kumuua mmoja wapo wa miungu hio na Roma baada ya kurithi cheo cha Hades hakuwa akienea kwenye msemo wao wa kuua miungu na kuwa miungu kwasabau yeye alikuwa ni wa tofauti na Hades wa zamani alimchaga mwenyewe kwa hiari yake ili kuweza kumrithi.

Ukweli ni kwamba miungu yote kumi na mbili ilihesabika kama watu ambao hawafi kwasababu ya kuwa na uwezo wa kuhamisha nafsi zao kuvaa miili mingine , wanaweza kufa kama tu wataruhusu ule uwelewa wa uungu wao wa ndani kwenda kwa mtu mwingine kwa hiari hivyo kukosa hisia maalumu ambazo zinawasiadia katika kutambua mwili sahihi wa kuuvaa kuhamisha roho zao na hiko ndio kilichomtokea Hades wa zamani mpaka akapoteza maisha, yaani alihamisha ule uwezo wake wa kujihamisha kwenda kwenye mwili mwingine na kumrithisha Roma na kisha akaipoteza nafsi yake makusudi, sasa kuna tofauti ya kufa na kupoteza nafsi.

Kupoteza nafsi kwa watu hao wa sayari nyingine ni kuacha nafsi yako kuachana na mwili wako ukiwa huna uelewa ni mtu gai au kiumbe kinachokwenda kuivaa , kufa kwa upande wao tafsiri yake ni kwamba roho yao huangamizwa na miili yao , yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba wakishaipoteza nafsi yao hawana uwezo wa kuitawala kwa kuiendesha kutokana na kwamba uwezo wao huo ushawatoka tayari , binamu sisi pia baada ya kifo hatuwezi kutawala nafsi zetu hivyo mwenye kazi ya kuzitawala ni mtu mwingine kabisa, viumbe hao wanaamini kuzaliwa upya ni sayansi ya kiteknolojia na sio imani au dini.

Utofauti mkubwa kati ya hawa kumi na mbili na wale ndugu zao wengine walioweza kumezwa nafsi zao na binadamu ni kwamba ukiachana na kwamba katika sayari yao walitoea kwenye makabila yenye nguvu lakini pia walikuwa na uwezo wa juu wa kucheza na kanuni za anga na pia walimiliki kiasi kikubwa cha nguvu za kiroho.

Sasa Roma mara baada ya kuona kundi hilo la wavaa mavazi meupe kujiita DEICIDE kama utambulisho wao ilimfanya Roma kujawa na shaku ya kutaka kujua wametokea wapi.

Muda huo huo kwa Nasri ambaye ndio kwanza alikuwa akijipanga upya alitoa tabasamu la kejeli mara baada ya kumuona Adui yake amemfauta chini.

“Asante kwa kunifuata hapa chini maana tungeharibu vyumba “Aliongea Nasri na palepale alimsogelea yule bwana mwenye mavazi meupe kwa spidi kubwa kama vile alikuwa akivutwa na kamba na alisababisha hadi upepo kujitengeneza.

Bwana mwenye vazi jeupe palepale alitoa mkono wake aliouvalisha Glovusi nyeupe na kukunja ngumi kwa nguvu na mara baada ya Nasri kumsogelea kwa umbali kama wa mita moja palepale alionekana akipiga kwenye kitu hewani kama ukuta ambacho hakikuwa kikionekana na kurudishwa nyuma kwa nguvu na ile anakuja kutua chini aliburuzika kiasi kwamba hata viatu vyake vya ngozi alivyovaa viliharibika soli.

Wanajeshi wote waliokuwa wamezunguka wakiangalia pambano walijikuta wakipatwa na hamaki kwani yule mwanajeshi alievalia mavazi meupe hakufanya kitu kikubwa sana, lakini kilichomkuta Nasri ni pigo kubwa mno.

“Space barrier!!?”Aliongea Roma kwa hamaki akimaanisha kizuizi cha anga kwa namna ya mshangao mkubwa.

Ijapokuwa haikuwa ngumu sana kuweza kutengeneza Space Barrier lakini mtu ambaye anatengeneza lazima awe na uwezo wa kutumia kanuni za anga kufanya mashambulizi , hivyo ndio maana Roma alisahngaa.

Lakini licha ya hivyo hakuweza kuhisia msisimko wowote wa uungu ndani ya mtu huyo na alijikuta akijawa na maswali lukuki , kundi hilo limetokea wapi ambalo lina uwezo wa kutumia kaununi za anga.

Roma alijiambia kama binadamu wa kawaida anaweza kutumia kauni za anga , si miungu itapaswa kuachana na mkataba wa The gods treaty na kutumia kanuni za anga ili kujilinda.

Muda uleule baada ya tukio lile waliongezeka wengine wanne na kwenda kujipanga pembeni ya mwenzao , wote walikuwa wameficha mili yao mpaka ngozi zao hazikuonekana na haikujulikana ni wa kabila lipi.

Hawakuwa wakimwangalia tena Nasri kwani alionekana kutokuwa tishio kwao , lakini mtu waliekuwa wakimwangalia kupitia Mask zao ni Roma pekee ,

“Nasri vipi unahitaji msaada naona, unaonekana kupambana na maumivu , unajitia aibu tu mbele ya mfalme Pluto , utaweza kujielezea vipi kwa General Sauron”Aliongea mmoja wapo ya watu aliofika nao katika kundi la watu wa tano.

“Screw you Dimon , I haven’t put in full force yet”Aliongea akimwambia niache Dimon , sijatumia nguvu zangu zote bado.

Wakati Nasri anajiandaa kupeleka shambulio lingine palepale Roma alimsogelea na kumzuia.

“Mfalme Pluto nini tatizo , unataka upigane nao wewe mwenyewe?”Aliuliza kwa mshangao wa kutoridhika.

“Achana nao , ninachomaanisha ni kwamba kwasababu mashindano yanakwenda kuanza kesho na wao ni washiriki ni lazima utakutana nao hivyo kwasasa usiweke wazi mbinu zako zote za kivita”Aliongea Roma na kumfanya Nasri kuelelewa.

“Lakini mfalme Pluto vipi kuhusu vyumba vyetu?”

“Hassan ndani ya hoteli yako , vyumba vya VIP gharama yake ni shilingi ngapi kwasasa?”Aliuliza Roma

“Ni Euro mia nne kwa usiku mmoja”aliongea na Roma palepale alitingisha kichwa chake na kisha aliangalia Balkoni na alipaa na kwenda kuingia katika vyumba hivyo.

Kitendo cha Roma kupaa mpaka kwenye Balkoni kiliwafanya wale Wahuni wa mavazi meupe wanaojiita The Godkiller kumfuata Roma huko huko wakiachana na Nasri

Wakati kila mmoja akijiuliza ni kipi Roma anataka kufanya ghafla tu kulitokea mlipuko kutoka katika vyumba hivyo ,ulikuwa ni mlipuko kama wa bomu ambao uliambatana na moshi mzito.

Wale wahuni walipotaka kuingia ndani walijikuta wakisimama mara baada ya mlipuko huo ambao ulifanika .

Hassan mara baada ya kuona kitendo kile alijikuta akipiga magoti kwa mshangao , lakini licha ya hivyo hakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwani tayari lishatokea

Kila mmoja alipatwa na joto la uoga , hata Nasri kidogo alijihisi kutojosikia vizuri kwa kile kinachoendelea.

Baada ya wingu la moto na moshi kupotea , palepale wate mabwana wa mavazi meupe walionekana wakielea hewani wakiwa hawana majeraha yoyote

Roma mara baada ya kulipua vyumba vyote , aliweza kutoka na hakushangaa baada ya kuona watu hao hawakupata majeraha yoyote licha ya mlipuko.

‘Okey , sasa vyumba vyote vishaharibika kama bado mnataka kuendelea kukaa basi ni ruksa”Aliongea Roma kwa kingereza akiwaangalia wale mabwana

“Hades this is a perfomance of a coward , What is it, don’t you dare to compete with us head on”Aliongea yule bwana kwa rafudhi ambayo haikueleweka ni ya wapi alikuwa ni yule ambaye alipamabana na Nasri akimwambia Roma kwamb kitendo alichokifanya ni cha kiuwoga , kwani anaogopa kupambana nao ana kwa ana.

“Kama nitapigana na nyie mtaishia kufa na nikishawaua washirika wangu watakosa nafasi ya kushiriki mashindano hivyo nitawaacha kwa muda lakini niwahakikishe tu hamuwezi kuondoka hapa Sicilly”Aliongea Roma

“Such a bold statement you dont seem to understand what word on our back means?”Aliongea yule bwana akimwambia Roma na kauli zake za majigambo labda hajui maneno yaliokuwa mgongoni kwao yanamaanisha nini.

“Deicide inamaanisha Godkiller”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kishetani

“Nilijua nipo hapa kuwasindikiza wanawake wangu na kuchukulia safari hii kama ya matembezi lakini kuonekana kwenu hapa kuna nifanya niwe na shauku kubwa, nitaendelea kusubiri”Baada ya kumaliza kauli yake alirudi chini.

“Utampatia Hassan Euro elfu arobaini kwa ajili ya fidia, tuondokeni hapa”

“Mfalme ndio tunaondoka hivyo na kuwaacha?”Aliuliza Nasri.

“Acha kuwa mjinga , je unataka tukokose vigezo vya kuingia kwenye mashindano , tusiposhiriki Kamisheni zetu zitapungua , , je unataka wenzetu wote kutuchukia?”Aliongea bwana mmmoja aliefahamika kwa jina la Dimon.

Ron mara baada ya kumwandikia Hassan Cheki ya Euro elfu arobaini na kumkabidhi alimgeukia Roma.

“Mfalme Pluto kwasababu hatuwezi keundelea kukaa hapa nadhani tuelekea hoteli ya Casssano, hoteli yenye uwekezaji wa familia yetu, ijapokuwa inaweza kuwa mbali na Arena lakini hali ya kule ni nzuri zaidi tofauti na hapa”Aliongea.

“Lakiini baba mazingira ya pale si kidogo yatakuwa sio mazuri kwa…”Aliongea huku akiwaangalia Rose na Magdalena na palepale Ron aliweza kukumbuka kumbe walikuwa na wanawake wameambatana nao.

Upande wa Rose na Magdalena walikuwa na shauku kubwa kuhusu hao Ma’freaks na hawakuweza kusikia mazungumzo ya Ron na mtoto wake.

Roma mara baada ya kuona wasiwasi wao ni nini aliwasogelea na kisha akamshika Fidero mabegani na kumpiga piga.

“Usiwaze wanawake wangu sio wakawaida na hakuna kitu kibaya kinachoweza kuwatokea”Aliongea Roma na Ron na mtoto wake walikubali huku kidogo wakionyesha hali ya aibu na muda huo huo waliamrishana na kurudi ndani ya magari na safari ya kwenda hoteli ya Cassano ilianza mara moja.

Baada ya watu waliokuwa nje ya hoteli ya Federiko wakianza kutawanyika wale watu wenye mevazi meupe walipaa hadi kwenda kutua juu kabisa ya jengo hilo la hoteli na kisha kugeuka upande ambao msururu wa magari ya Roma unakoelekea

“Ares je tunamuacha aondoke hivi hivi , anaonekana hana tishio lolote kwetu”Aliongea mmoja wapo wakitumia lugha ya Kirusi.

“Kitendo cha kuweza kuwa sehemu ya miungu bila kupambana hakimfanyi kuwa na uwezo mkubwa , msijali Show ndio kwanza imeanza , wakati wakiwa wote hapa, itakuwa vizuri zaidi kuwamaliza wote kwa pamoja”Aliongea kwa kujiamini, ilionekana walikuwana mpango wao kichwani , lakini kubwa zaidi mmoja wapo aifahamika kwa jina la Ares yaani moja wapo ya miungu kumi na mbili.

Wakiwa safarini kuelekea hoteli ya Cassano , Roma alionekana kuwa kimya akionyesha kuna jambo analifikiria na hata Ron na Fidero walimwangalia huku wakijiuliza ni jambo gani Master wao anafikiria.

“Tafuta taarifa zote zinazowahusu , majina yao walioandikisha kama washiriki , jina la timu yao na maisha yao ya nyuma , taarifa ya kujitosheleza itakuwa vizuri zaidi , ripoti kwangu kabla ya ufunguzi wa mashindano”Aliongea Roma

“Yes , your Majesty Pluto”Alijibu Fidero kwa heshima, ukweli ni kwamba tayari alikuwa ashatuma mtu kwenda kuuliza watu hao wanatokea wapi na ni wakina nani kwa undani.

Muda huo huo mara baada ya kumaliza kauli yake alitoa simu yake na kuitafuta namba ya Christen.

“Hades uko wapi kwa sasa , kwanini namba yako inaonyesha eneo nje ya Tanzania?”Aliuliza Christen mara baada ya kupotkea simu.

“Nipo Sicilly”

“Oh! , Bado tu unamatamanio ya kuangalia Caesar conference? Au upo hapo ili kuwatia nguvu wanajeshi wako? Nadhani watakua na presha kubwa wakijua unawaangalia”Aliongea kwa kutania.

“Sipo kwenye mudi ya kujali kuhusu mkutano huo kwa sasa, Otea nilichokutana nacho dakika kadhaa zilizopita?”Aliongea Roma.

“Umeona nini , umeona mrembo nini kuzidi Edna nini?”

“Nipo siriasi bwana, sitanii hapa”

“Okey , vizuri vizuri ongea sasa nataka kupata kifungua kinywa muda huu”

“Nimekutana na wanaume watano waliovalia mavazi aina ya Cloak na Mask za rangi ya dhahabu, wamesema watashiriki katika Caesar conference lakini wanajua kutumia kanuni za anga licha ya kwamba hawana uungu ndani yao”Aliongea Roma na kumfanya Christen kuwa kimya kwa muda.

“Una uhakika wametumia kanuni za anga na bado hawana uungu?”

“Ndio , labda naweza kusema nguvu zao zipo za levo ya juu sana kitu ambacho nimeshindwa kuelewa , ndio maana nafikiri huenda itakuwa vizuri wewe na wengine mkifika huku kuangalia”

“Okey nitawasiliana na Poseidon na wengine”Alijibu Christen na kumfanya Roma kukunja sura.

“Unaonekana kujua jambo kupitia sauti yako?”Aliongea Roma na Christen upande wa pili alicheka kidogo.

“Sina uhakika bado hivyo haina maana kama nitakueleza sasa hivi , nitakuambia nikiona kwa macho yangu”Baada ya kuongea tu palepale alimkatia simu bila ya kumpa Roma nafasi ya kuuliza swali lingine .

Roma alipatwa na stress maana ni kama mara ya pili sasa Christen anamkatia simu kila akitaka kumuuliza maswala yanayohusiana na wao , hisia zake zilimwambia kabisa kuna kitu ambacho anafichwa lakini hakuweza kumlazimisha Christen kumwambia ukweli wote lakini kwa wakati mmoja alijimbia itakuwa vyema kama hakutatokea tatizo lolote wakati watakapokuwa hapo Sicilly.

Kitendo cha Roma kuonyesha hali ya huzuni kilionekana kwa Rose aliekuwa ameketi pembeni yake na alimshika mkono kumtuliza.

“Usiwe na huzuni sana , wote tupo hapa kama kuna chochote ambacho kitakutokea mimi na Magdalen tutahakikisha tunakulinda”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Roma kucheka sana na kugeuka siti ya nyuma kumwangalia Magdalena ambaye alikuwa akitabasamu

Haikuchukua muda mrefu waliweza kufika ndani ya hoteli ya Cassano , hali ya hewa ya Sicilly ilitofautiana sana wakati wa mchana na usiku na upepo wa baharini uliokuwa ukiwapuliza kwenye nyuso zao uliwafanya kupata hali ya unyevu nyevu.

Ilikuwa ni giza tayari na mwanga hafifu uliotoka katika hoteli hio ulipendezesha sana macho , karibia eneo lote la maegesho ya magari lilikuwa limejaa magari ya aina tofauti tofauti , ni hoteli ambayo ilikuwa kabisa katika fukwe na maeneo yalikuwa yamejengewa mahema, licha ya kuwa usiku warembo kibao waliovalia nguo kusitiri tupu zao tu walikuwa wakizunguka huku na huko wakifanya starehe na kufurahisha wanaume waliokuwa nao.

Hali ya hewa ya hapo ilikuwa ya makelele zaidi , pengine zaidi ya hoteli ya Federico ambayo eneo lake lilikua tulivu , hio ni hoteli kwa ajili ya dhambi huenda ndio maana ikapewa jina la Cassano.

Wakati hawajaanza kupiga hatua kuelekea ndani , wanawake waane wenye makalio saizi tofauti tofauti walipita mbele yao wakiyatingisha kwa makusudi, ilikuwa ni dhahiri wanatafuta soko, mikononi mwao walikuwa wameshikilia chupa za kama za manukato lakini zenye kutoa moshi wa rangi wakizipuliza hewani kwa maringo ya kikahaba.

Wageni wote walioingia hapo macho yao yote yalikuwa kwa wanawake hao ambao walikuwa wakitingisha , Rose na Magdalena waliweza kuhisi kabisa hio sio hoteli ya kawaida kabisa na mambo yanayoendelea sio ya kawaida , lakini kwa upande wa Rose hakujisikia vibaya kutokana na kwamba alishawahi kuongoza Club B , ijapokuwa Club B haikuwa na mambo ya kihuni kama hayo , lakini hakukuwa na utofauti mkubwa , aliekuwa na hali isiokuwa ya kawaida ni Magdalena ambaye maisha yake yote yalikuwa ni katika mazingira ya mbali na maeneo ya starehe.

“Msiwe na wasiwasi hili ni eneo maarufu la wazi ndani ya hiki kisiwa ni kama Red light street na hoteli hii ya Cassano ndio kubwa ambayo watu hukusanyika kwa ajili ya starehe”Aliongea Roma

“Unaonekana kulijua sana hili eneo si ndio?”Aliuliza Rose

“Ni kwasabau Ron ashawahi kulitaja sana katika stori zake , kwasaabu nimethubutu kuwaleta hapa kwanini niwafanye msiwe na furaha?”

“Ni kweli kabisa , Mfalme Pluto hawezi kuja kucheza na vitu vya hadhi ya chini kama hapa , haina haja ya kuwa na wasiwasi na yeye”Ron alitetea.

Baada ya kuona wanawake hao hawakuuliza maswali zaidi , Roma alimpa ishara Ron na Ron alimrudishia , walionyesha kuwasiliana kwa namna yao.

Waliweza kuzama kabisa ndani huku wakishangazwa na idara mbalimbali za starehe ndani ya hoteli hio , kulikuwepo na Swimming Pool , Makasino , Gympnasiums na mambo mengine mengi , kwa haraka haraka ilionyesha ni uwekezaji mkubwa sana umefanyika.

Baada ya kuingilia kwenye chmba cha kifahari chenye ubunifu wa tamaduni za kigiriki waliweza kupokewa na picha kubwa iliotundikwa ukutani iliokuwa ikionyesha Mashujaa mbalimbali wa enzi hizo, umaliziaji wa kimtindo ndani ya chumba hicho ulikuwa ni rahisi lakini wa kuvutia.

Kulikuwa na kitenda kikubwa katikati cha duara kilichotandikwa na shuka la rangi nyeupe na madirisha makubwa pembeni ambayo yalirihusu upepo kuingia ndani.

Kutokana na uchache wa vyumba ilibidi wapewe chumba kimoja na kitendo hicho kiloimfanya Magdalena kukosa utulivu , hakuelewa wangelala vipi na Roma katika kitanda kimoja.

Wakati Roma akiendelea kutaniana nao ili kuwatoa wasiwasi mlango wa chumba chao uligongwa na Roma aliruhusu anaegonga kuingia, alikuwa ni Ron na uso wake ulikuwa umebadilika tofauti na mwanzo.

“Mfalme Pluto , Sauron amekwisha kufika akiwa na Makedon pamoja na Edward wote wanakusubiri , wanahiraji kuongea na wewe muda huu wamesema ni dharula”

“Muda huu , kuna siri gani inaendelea , unaweza kuniambia maana kwa mwonekano wako nadhani ni jambo la siriasi”Aliongea Roma huku akikunja sura.

“I sincerely hope that Your Majesty Pluto to spare General Sauron’s life on behalf of the many years of brotherhood”Aliongea Ron akimaanisha kwama kwa dhati kabisa anaomba Roma ayasamehe maisha ya Sauroni kwa niaba ya muda wote waliofahamiana na kufanya mambo pamoja kama ndugu.

Ilionekana kuna kitu kibaya ambacho kimetokea, maana sio kawaida kwa Ron kumuombea Sauron msamaha kabla ya kosa lake halijajulikana lakini vilevile uwepo wa Edward binamu yake Clark uliwasha taa ya hatari.

Unafikiri Sauron kafanya nini mpaka kuombewa msamaha na Ron , vipi kuhusu watu wa mavazi meupe.
 
SEHEMU YA 564.

Roma mara baada ya kuona namna ambavyo Sauroni anaongea aliona aongozane nae akaangalie nini kinaendelea.

“Inaonekana kuna jambo baya limetokea , kwasababu umekataa kuniambia hapa tuondoke nikajionee mwenyewe”Aliongea Roma na kisha akawageukia Rose na Magdalena.

“Nyie wawili mbaki hapa , haina haja ya kukutana nao kwa sasa’Aliongea Roma na hawakujali sana hata hivyo isitoshe ndani ya hoteli hio kulikuwepo na sehemu nyingi za kutembelea.

Baada ya kumfuata Ron nyuma nyuma , hatimae waliweza kuingia eneo la mapokezi katika floor ya vyumba vya VIP.

Karibia watu wote waliochini yake walikuwa washajikusanya ndani ya eneo hilo wakiwa wamesimama kwa kupanga mstari wakiwa katika mavazi ya kawaida ya suti kasoro tu Sauron alikuwa amevalia gwanda.

Jopo lote liliinamisha vichwa chini kwa ishara ya kutoa heshima lakini Roma hakujali sana.

Kwa muonekano wa Roma kwa nje na jopo hilo la watu wenye miili iliojengeka kimazoezi , hakika ilikuwa ikishangaza kwa namna yake , ni kama sasa amefika katika utawala wake rasmi.

Roma alizungusha kichwa chake na alipoangalia kwa umakini mbele yake alisimama kwa kuonyesha ishara ya mshangao.

“Clark!”Aliita.

Alikuwa ni mwanamke mrembo aliepiga magoti huku akiwa amefungwa na pingu kwenye mikono yake , akiwa amevalia koti la kitabibu kama daktari.

Lakini Clark huyo alikuwa akimwangalia Roma kwa macho yasio ya kawaida , akionyesha kabisa ishara ya dharau.

Roma palepale akili yake ilicheza na kuona kuna kitu ambacho sio cha kawaida na alimwangalia mwanamke yule kwa umakini mkubwa sana na akatingisha kichwa kupinga kauli yake.

“Hapana wewe sio Clark , licha ya kwamba unafanana nae, macho yako , muonekano wako vinakutofautisha kwa kiasi kikubwa na yeye”Aliongea Roma.

Wengine wote mara baada ya kusikia maneno ya Roma walijikuta wakivuta pumzi na kuzishusha lakini kumkubali mara moja Master wao kwa kumua Clark huyo ni feki kwa kuangalia tu.

“What is going on, Who is this?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikianza kubadilika , mpaka hapo alianza kuhisi maana ya kauli ya Ron dakika chache zilizopita.

Roma alijikuta akianza kuwaangalia kwa macho makali kila mtu aliekuwa ndani ya eneo hilo na watu wote walijikuta katika hali ya kunywea na kuwa wadogo kabisa.

Sauron aliekuwa upande wake wa kulia akiwa na gwanda zake za kijeshi alisogea mbele na kisha akapiga magoti mbele ya Roma.

“Your Majesty Pluto it’s my dereliction of duty, Princess Clark was kidnapped”

“Mfalme Pluto ni kutoweza kutimiza wajibu wangu , Princess Clark alitekwa nyara”Aliongea Sauron na palepale kauli yake ilipiga kama shoti katika mwili wa Roma na dakika hio hio alikuwa tayari ashamsogelea Sauron na kumshika na mkono mmoja kwenye Collar na kumuasha huku akimkaba kwa hasira.

“Will you come again?”Aliuongea akimaanisha arudie tena.

Makedon na wengine walikuwa na wasiwasi na walitaka kumshawishi apunguze hasira lakini Ron aliwapa ishara wasiongee chochote.

“Yes… Princess Clark , she was kidnapped”Aliongea Sauron.

“Ujinga Clark kama alikuwa Uingereza imewezakanaje akatekwa , unafanya nini nimekupatia mamlaka makubwa ya kamandi , hao wanajeshi wako siku hizi wamegeuka kuwa mapambo?”Aliongea kwa sauti nzito kabisa na kufanya chumba chote kuwa na ubaridi wa aina yake wa woga na wasiwasi wa kile ambacho kinakwenda kutokea.

Hakuna ambaye alikuwa akishangaa kwa Roma kuwa na hasira za namna hio kwasababu walikuwa wakimfahamu Clark na mama yake ni watu wa kipekee katika maisha ya Roma.

Roma wakati akiwa na miaka kumi na nne tayari ashamfahamu Clark , na katika miaka yote hio tokea wafahamiane alikuwa karibu sana na msichana huyo katika makuzi yake yote , mpaka kuja kuwa mtu mkubwa, ukiachana na yote Clark alikuwa kwa ndoto moja tu ya kuwa daktari ili kumsaidia Roma na ugonjwa wake.

Clark alikuwa ni mwanamke ambaye maisha yake yote aliishi kwa kujitengeneza kuwa na thamani ya kuhitajika na Roma na ndio maana pale tu Roma aliposema anashida mwanamke huyo angetimiza bila ya kujitaji malipo ya aina yoyote.

Kama Clark alikuwa akifanya kulipa fadhila basi angekuwa ashakamilisha fadhila hizo miaka mingi iliopita kwani amefanya mengi, ni yeye pekee ambaye alimsaidia Roma kuweza kudhibiti hali yake ya ukichaa.

Sasa watu wote waliokuwa hapo , akiwemo Edward, Ron na wengine walikuwa wakifahamu nini maana ya Clark katika maisha ya Roma.

Usalama wa Catherine mpaka leo hii upo chini ya Roma na hata baada ya yeye kuamua kurudi nchini Tanzania madaraka aliotoa kwa Sauron wajibu wake pia ni kuhakikisha usalama wa Malkia Catherine na Clark unaimarishwa.

“Ni kushindwa kutimiza wajibu wangu , watu waliomteka Princess Clark walitumia akili ya kumuweka mwingine feki ili isigundulike kama ametekwa , wakati nikiwa nataka kumleta kwenye Caesar Conference niliweza kugundua utofauti wa Clark na hapo hapo nikajua aliekuwepo ni feki, kwasababu Clark licha ya kuwa bize lakini hajawahi kusahau miadi yake na wengine”

Roma alimtupa Sauroni chini , kwa hali kama hio hata kama alikuwa ni komredi mwenzake katika jeshi asingeweza kumtendea vizuri kwa kosa ambalo amefanya.

“Kwahio huyu mwanamke ni feki umesema?”

“Ndio “Aliitikia huku akinyanyuka na kusimama kikakamavu mbele ya Roma na kisha akaendelea kuongea.

“Mfalme Pluto nimekuja kwa kuchelewa kwasababu nilikuwa sijui namna ya kulifikisha hili kwako na lingine ni kutoa maagizo kwa watu wangu kufanya utafiti wa kujua mwanamke huyu ni nani haraka iwezekanavyo, na tuliweza kugundua aliwahi kuwa shushu kutoka Urusi chini ya kundi la kigaidi lifahamikalo kwa jina la Black Widow l akini aliasi , sura yake imeweza kubadilishwa kwa kutumia mjumuisho wa Nanotechnology na 3D printing technology, teknolojia ambayo bado haijawa hadharani , ni teknolojia ya viwango vya juu sana”Aliongea Sauroni akimaanisha mtu huyo alikuwa akifanana na Clark kutokana na sura yake kutengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Nano na ya uchapishaji ya 3D(Three dimension).

“Kwahio unamaanisha bado hamjapata Clark?”Aliuliza na Sauron alitingisha kichwa kukubali .

“Mfalme Pluto , nimetuma majasusi wote wa Mossad waliochini yangu kutafuta kila kona ya dunia , kama kutakuwa na taarifa yoyote itaripotiwa kwetu kwa haraka sana”Aliongea Makedon na Roma alimpotezea na kumgeukia Edward.

“Catherine anajua kuhusu hili?”

“Shangazi yangu hajui chochote mpaka sasa , yupo bize na maandalizi ya Summer Bank holiday kwa zaidi ya wiki tatu sasa nchini Scotland na hajakutana kabisa na binamu yangu na hatujapanga kumwambia bado”Aliongea.

Katika maelezo yao ilionyesha kwamba ni zaidi ya wiki mbili tokea Clark kutekwa na haikuwezekana kugundulika kutokana na kwamba kulikuwepo na feki yake.

“Kama ni hivyo agiza vijana kuongezea ulinzi wake kwa siri ili isije ikawa analengwa na yeye pia kama ilivyomtokea kwa binti yake”Aliongea Roma na baada ya hapo alimgeukia yule mwanamke na kisha alinyoosha mkono wake bila ya kumshika na nguvu kubwa ya kijini ilitoka kwenye mikono yake na kumwinua yule mwanamke huku akiwa kama vile amekabwa shingonii bila ya kushikwa.

Huyo Clark Feki alikuwa na sura ya dharau licha ya kwamba alikuwa akiona kifo chake na hakutaka kuongea neno lolote ni kama alikuwa ashajiandaa kufa kwa muda mrefu.

“Najua kwamba wewe ni Ajenti ambaye una mafunzo ya hali ya juu na najua sana mbinu zenu za kujiua lakini pia hutoongea chochote licha ya kukutesa lakini hata hivyo sina mudi ya kupoteza muda kukutesa hivyo kama hutaki kutoa ushirikiano kwa hiari yako nitakupasua kichwa chako”Aliongea Roma na yule mwanamke alitoa tabasamu la kejeli.

“Hades wewe ni shetani , Umechokoza watu na kuamsha ghadhabu ya Mungu na muda wowote yatakufikia mabaya , kwasababu nilikuja kushiriki katika hii opereshini sijawahi kuwaza kurudi nikiwa hai , niue na nitakuwa kuzimu nikisubiria kila mmoja anaekuzunguka kuungana na mimi”Aliongea kwa kejeli kwa lugha ya kingereza.

“Naona umekiomba kifo chako mwenyewe na sina budi kukupatia”Aliongea Roma na palepale hakusita tena kwani alisukuma nguvu yote ya kijini kutoka katika mkono wake na ni sauti ya mivunjiko ya mifupa tu ilioweza kusikika na palepale kichwa chake kilipasuka kama tikiti na ubongo wote ukamwagika huku damu nyingi zikimwagika na kuchafua kapeti.

Kwa jinsi mwanamke huyo alivyopelekwa kuzimu ilikuwa ni kikatili mno kiasi kwamba watu wote hapo ndani walikunja sura na kujiambia ukatili huo ni kama vile Roma amerudi katika enzi zake akiwa kama shetani mwenye kiu ya damu.

Kipindi hicho ambacho hakujali kufanya ukatili huo mbele ya Seventeen na Clark.

Kila mmoja alikuwa na wasiwasi mno na hakuna ambaye alithubutu kuongea neno lolote la kutoa michango yao namna ya kumpata Clark.

Wakati kila mmoja akisubiria kwa hofu nini kinakwenda kutokea , palepale Roma aliirusha ile maiti ya mwanamke katika miguu ya Makedon.

“Nenda na chukua Fingerprint zake na DNA uthibitishe ni wakati gani ambao aliingia ndani ya maabara ya Clark , inaonyesha Clark alitekwa kwa muda mrefu na hamkuweza kujua kwasababu ya uwepo wa sura yake feki , pengine wanajaribu kuvuta muda wakitaka kupata tafiti zote za Clark alizogundua , nina uhakika mpaka sasa yupo hai , kwa hao watu naamini wanachokita kutoka kwa Clark ni kwa ajili ya kutengeneza siraha za maangamizi , hivyo basi kwa umakini mkubwa anzeni kutafuta katika maeneo yote ambayo yana viwanda vya kudhalisha siraha za kipekee”

Baada ya kusikia maelezo ya Roma wote waliunga mkono , ilikuwa ni kweli kama walimteka kwa ajili ya kutaka kitu chochote kutoka kwao wasingeweka mtu feki kama mbadala , lakini licha ya hivyo ilionekana walichagua muda mbaya kwani kipindi hicho ni cha Caesar Conference na Clark alikuwa ni moja wapo ya watu waliokuwa wakihudhuria kila tukio hilo linapofanyika”

Ron na wenzake waliogopa kwamba kama taarifa hio ingemfikia Roma basi asingeweza kudhibiti ukichaa wake uliokuwa ukimwendesha miaka na miaka na kuishia kuwaua , lakini ilionekana mfalme wao ameimarika tokea ajipe likizo ya kwenda Tanzania..

Makedoni aliahidi na kisha akawapa maelekezo vijana wake kusafisha na baada ya hapo aliondoka katika eneo hilo akiwa na watu wake kwa ajili ya kuanza kazi ya kumtafuta Clark , alijua kabisa kama chochote kikimtokea Clark basi halitakuwa jambo jepesi .

“We the Rothchild family are involved in the international undergound trading of all rare metals and elements , I will chek it ou and hope it helps”Aliongea Edward akitoa pendekezo kwamba familia yao ya Rothchild inahusika na biashara zote zinazohusu madini adimu na kuahidi kwamba atajaribu kuulizia huko ili kuona kama inaweza kusaidia.

“Ni bora uanzie kwa wanafunzi wa Clark wote wakubwa na kuona Projekti zao za hivi karibuni”

“Understood”

Roma mara baada ya hapo alimwangalia Sauron kwa muda huku akionekana kuwaza, Sauron uso wake ulikuwa mwekundu mno kwa wasiwasi akiwa amesimama katika eneo moja pasipo ya kusogea hata hatua moja.

“Sauron unapaswa kujiandaa , kama Clark asipoweza kurudi akiwa salama hakikisha haitokei wewe ndio wa kulaumiwa , siwezi kukuua lakini huu uwezo wako mdogo utakuandama kwa maisha yako yote mpaka unaingia kaburini”

“Mfalme Pluto wewe ndio ulifanya familia yangu mpaka sasa ipo hai , ni mwenye soni juu ya ahadi yangu kwa kufeli kumlinda Princess Clark , nipo tayari kwa hiari yangu kuwajibika , tafadhari nipe nafasi nyingine ya kurekebisha makosa yangu , nitamtafuta Profesa Clark alipo ndani ya muda mfupi sana”

“You better not Disappoint me again”Aliongea Roma akimaanisha kwamba ni kheri kama hatamwangusha tena na Sauron alipiga saluti ya kikakamavu akiahidi atafanya kila namna ya Clark kupatikana.

Baada ya pale wanajeshi wote wa kikosi cha The Eagles na viongozi wa juu wa New Zero walipiga saluti na kisha wakaondoka wakiongozwa na Sauron.

Baaada ya watu kuondoka aliekuwa amebakia ni Ron na alimsogelea Roma akionekana na maoni yake binafsi.

“Mfalme Pluto kama adui aliefanya hivyo akawa na uwezo mkubwa wa kimapigano Sauron anaweza asiweze kufanikiwa kumshinda”

‘Unafikiri sijaliona hilo?”Aliongea Roma katika hali ya urafiki.

“Hapana ,, najua mfalme Pluto hukutaka kumlaumu kila kitu Sauron ndio maana ukaamua kumuacha bila kumuadhibu”

“Najaribu tu kuwaaamsha watimize majukumu yao ipasavyo , yule mwanamke alichoongea ni sahihi nimeua watu wengi sana hivyo nimejitengenezea maadui dunia nzima wanaotaka kuinywa damu yangu ikiwa ya moto , ndugu zao , marafiki zao na hata wapenzi wao niliwaua , na sasa wanatafuta nafasi ya kutaka kulipiza kiasasi, hata kama nilishastaafu na kuacha mambo hayo kwa zaidi ya miaka mitatu , lakini hawa watu wana madoa makubwa ya damu na chuki katika mioyo yao, kuna msemo maarufu kutoka Asia usemao ‘Iwe ni kwa kuwahi au kwa kuchelewa hakuna muda sahihi wa mwanaume kulipiza kisasi’, hivyo hata kama hawatakamilisha ndani ya mwaka mmoja au miwili kwao hata ichukue miaka kumi haitakuwa tatizo mpaka siku wapate nafasi”

“Nafikiri awamu hii huyu adui anajaribu kutumia muda kwa faida kutokana na nguvu ya chuki za watu ambazo zinaelekezewa kwako ili kujificha , hatujawahi kutegemea kama ataenda moja kwa moja mpaka London na kuteka mtu nyara”

“Kuna uwezekano wa mambo ambayo hatujawahi kutegemea yakatokea hapo mbeleni.Halafu wale watu wa mavazi meupe kuna taarifa zozote mlipopata zinazowahusu?”

“Oh, Fidero tayari ashapata baadhi ya taarifa na nilikuwa nikihatiaji kukuambia”Aliongea na kisha alimpa karatasi iliokunjwa .

Roma alisoma karatasi ile kwa haraka haraka na palepale uso wake ulijikunja huku akitabasamu kifedhuli.

“Mbinu yao kujificha..”Aliongea.

Sababu ya kuongea hivyo ni kwamba , ukiachana na neno Deicide au godkiller washiriki wote wa kundi hilo hawakuandikwa kwa majina yao halisi bali ni namba tu zilizotumika kuwatambulisha kama washiriki.

Hata hivyo ulikuwa ni utaratibu wa wasimamizi wote wa Caesar conference washiriki wote kutoka makundi tofauti hawakutambulika kwa majina yao halisi.

“Wamekuja wakiwa wamejiandaa sana”Aliongea Roma huku akitoa kicheko hafifu.

“Mfalme Pluto je kuna ulazima wa kutuma mtu kuwafatilia ili kujua kila wanachokifanya? Nina wasiwasi kwamba inawezekana ndio waliohusika na kumteka Princess Clark”

“Achana na hilo , ukituma watu watakachoambulia ni majeraha tu , mimi mwenyewe nimeshindwa kugundua wanatokea wapi inamaanisha wamejiandaa kwa kila kitu , ngoja nisubiri Christen na wenzake wakiwa hapa nione ni kipi wanafahamu na maamuzi watakayo chukua”

Roma hakuona haja ya kumtafuta Clark yeye mwenyewe , na isitoshe Clark hakuwa na mafunzo yoyote ya nguvu za mbingu na ardhi huenda ingekuwa rahisi kumtafuta kwa kutumia Aura yake hivyo aliona njjia pekee ni kutulia na kusubiria taarifa kutoka kwa Makedo na Sauron.

Lakini pia hakutaka taarifa hio kumfanya kukosa raha na kuwaathiri Magdalena na Rose ambao ameambatana nao kuja hapo kufurahi.

Roma mara baada ya kurudi katika chumba alichowaacha Rose na Magdalena aliambiwa kwamba wanawake hao wametoka na kwenda Casino , taarifa hio ilimshangaza kwa kutotarajia Rose kuweza kupata sehemu ya kupoteza muda .

Kasino iliokuwepo ndani ya hoteli ya Casaano licha ya kwamba asilimia kubwa ya watu wanaocheza kamari wlaikuwa ni mabandidu wa makundi ya kimafia , lakini walitii sheria zote za kamari na hakukuwa na utapeli.

Cassino yao ilikuwa na kila aina ya michezo ya Kamari kutoka katika kila tamaduni dunia nzima na sio hivyo tu hali ya hewa ilikuwa nzuri zaidi kutokana na kwamba kulikuwa na wanawake warembo waliokuwa wakitoa huduma na kufanya wacheza kamari wasiathirike kimawazo , ni eneo ambalo lilikuwa likifanya kazi usiku na mchana bila mapumziko, wengine kucheza kamari wanachukulia kama kazi yao ya kujiingizia kipato.

Roma akiwa ameambatana na Ron waliweza kumpata Rose na Magdalena katika meza ya gemu ya karata maarufu kama Blackjack na walionekana kuweka umakini wao katika gemu..

Ni Magdalena pekee ambaye hakuwa akicheza zaidi ya kumwangalia Rose kwa wasiwasi kwani tokea aanze kucheza alikuwa amepoteza Chips(hela katika mfumo wa vipande) za kutosha mpaka zote zimeisha na bado tu hakuwa ni mwenye kukata tamaa.

Roma alijaribu kumshawihi Rose aache maana hatoshinda kwa wazungu hao wataalamu , lakini aliweka ngumu na kusema mpaka arudishe hela zake zote alizopoteza na Roma hakutaka kumlazimisha ilimradi alikuwa akichezea hela zake.

Ilibidi amchukue Magdalena aliekuwa na wasiwasi akimwambiwa wakatembee tembee nje maana Kasino haikuwa mahali pake.

Magdalena alipata ahueni mara baada ya kuambiwa waondoke hapo ndani maana alijihisi kukosa uvumilivu.

******

UNKOWN SECRET BASE.

Ni katika mojawapo ya kambi ya siri sna ambayo haijulikani ipo eneo gani katika dunia.

Ndani ya chumba kikubwa kulikuwa kumefungwa taa za mwanga mweupe ambazo ziliangaza chumba kizima na kufanya kila kitu kilichopo ndani yake kuonekana, ni chumba ambacho kilionekana kabisa kimejengwa kwa chuma kigumu , mathalani kama mahali pakufungia mateka.

Muda huo huo mlango wa chumba hicho ulifunguliwa kwa kuteleza kwenda kulia na alionekana mwanaume wa kizungu mwenye nywele za kahawia zilizojikunja kunja ambaye amevalia koti la maabara.

Ni mwanaume ambaye alikuwa na mwonekano mwembaba lakini macho yake yalikuwa ni yale yasiokuwa na utani huku akiwa ameyafinika kwa miwani ya macho.

Katika chumba hicho kulikuwa na meza pamoja na kiti pekee na katika kiti alionekana mwanamke ambaye alikuwa amevaaa koti pia la kimaabara akiwa amekalishwa huku akiwa ameinamisha kichwa chake na kufanya nywele zake ndefu zilizochanguka kumfunika na asionekane sura.

“Professor , I came to see you again”Aliongea yule mwanaume na kumfanya yule mwanamke kuamsha kichwa chake taratibu na kufanya angalau sura yake ionekane.

Alikuwa ni Profesa Clark ambaye sura yake ilionekana kupauka sana , huenda ni kutokana na hofu pamoja na kukosa kula na kiua ya maji.

“Jerry tafadhari naomba uache”Aliongea Clark huku akimwangalia yule mwanaume kwa macho ya kukata tamaa. Lakini kauli yake licha ya kwamba haikuwa ikichekesha lakini mwanaume alieitwa kwa kjina la jerry alianza kucheka mfululizo.

“Profesa ni kipi ambacho unaota mpaka sasa , yaani niache , tangu nilipokutembelea mara ya mwisho nilikuwa nikiisubiria sana hii siku halafu unaniambia vipi niache , hivi unajua kwamba sina mpango wowote wa kuacha eti”

“Jerry wewe ndio mwnafuzni wangu pekee ambaye ulionyesha uwezo mkubwa licha ya kwamba nilikuwa na hofu na uelekeo wa tafiti zako lakini bado nikakuamini na kuendelea kukufundisha mambo mengi lakini sikuwahi kuwaza unaweza kunifanyia hivi , umenihuzunisha sana”Aliongea na kumfanya kidogo Jerrey kupatwa na hatia lakini alipotezea.

“Teacher I will ask you again , what is the last sythethic element of FURY?”Aliuliza Jerry akimuuliza Clark ni element ipi ya mwisho ya utengenezai wa FURY, alionekana alikuwa na kanuni ambayo haijakamilika na ni Clark pekee ambaye alikuwa akiifahamu ndio maana alikuwa akimuuliza.















SEHEMU YA 567

Clark mara baada ya kuulizwa hilo swali alivuta pumzi nyingi na kuzishusha , mtu huyu anaefahamika kama mwanafunzi wake alikuwa ameuliza mara kibao swali la aina moja lakini hakuwa amempatia majibu anayoyataka.

“Kwanini unatamaa sana na kanuni hio, nilifikiri kama utakuja kujua nini maana ya FURY utaacha kuuliza kabisa”

“Kwanini niache , nilikufuata kwa miaka miwili yote na hatimae nimepata ninachokitaka kwanini niache”

“Jerry acha kuruhusu chuki zako kukufanya kipofu , unajua kabisa kama FURY itatengenezwa nini kitatokea , baada ya kutengeneza muundo kamili wa kimfumo miaka mitatu iliopita sikuwa na mpango wa kuendeleza zaidi , itakuwa ni dhambi kwa kizazi chote cha binadamu, ni kitu ambacho sisi wanasayansi hatupaswi kutengeneza na kama kuna mtu yoyote atajaribu kutengeneza basi ni matusi kwa binadamu wote”

“Lakini bado huu muundo kamili uliojaribu kutengeneza si bado unao , Profesa wewe ni Idol wangu , hapo zamani za kale wakati nilipokuwa chini yako nilijitahidi kusoma na kuelewa kila unachofundisha na nilichimba nikachimba haswa na kila ulichonielekeza na nikajua maana yake niliendelea kukuheshimu , kitu pekee ambacho kilikufanya kunipenda kama mwanafunzi ni kwasababu tuna tabia zinazofanana , wote sisi ni wagumu sana kupotezea gunduzi zetu licha ya uhatari wake , ijapokuwa unasema hutaki kuunda FURY lakini bado taafiti yake hujaiharibu na kuificha , hakuna uchizi kama huo sisi wote tunafanana”

“Inaonekana kila nitakachoongea hakitakufanya uache, kama ni hivyo unaweza kuondoka kwani hata kama nikifa hapa siwezi kukuambia kanuni yake”

“Profesa unadhani nitashindwa kuijua hio karuni hata kama hutoniambia , kuna mamilioni ya Elementi katika dunia hii ambazo zinaweza kukamilisha kanuni ya uwiano wa kikemikali, ninao uwezo wa kujaribu moja moja mpaka nifanikiwe, hivyo acha ubishi jaribu kutoa ushirikiano kwetu , nina uhakika kwa talanta yako wakuu wangu hawatokuacha bure, kwanini unajisumbua kufanya kazi kwa ajili ya yule shetani si kheri sisi”Aliongea na kumfanya Clark kucheka sana.

“Unacheka nini?”

“Shetani uliemtaja ni kweli kwamba ameua watu wengi na naelewa wapo watu wengi ambao wanataka kulipiza kisasi lakini nini unafanya sasa hivi , hebu fikiria je kama utafanikiwa kutengeneza FURY unadhani utaweza kumuua , hivi unajua uwezo wake ukoje kwanza?”

“Hilo sio juu yako , hata kama sitoweza kumuua nitawaua watu wake wa karibu wanaomzunguka ili nimwonyeshe nini maana ya sherehe ya kifo na uhai”

“Kwa kufanya hivyo utakuwa mkatili zaidi kuliko shetani mwenyewe, Roma yeye kaua watu wengi lakini mpango wako wewe ni kuua binadamu wote”Aliongea na kumfanya Jerry kutabasamu kwa kebehi.

“Profesa huna haja ya kuwazia usalama wa dunia , kama nitaingudua hii elementi ya mwisho kubalansi matokeo ya kikemia . utakuwa ndio mwanzo wa sisi kutengeneza New word order”

“Wewe ni mpumbavu Jerry , hivi unadhani mpaka mimi kuwa mwalimu wako naweza kulingana na wewe? , kama FURY elementi yake inaweza kupatikana kirahisi basi mimi sio Clark”Aliongea na kumfanya Jerry kushituka na kukunja sura.

“Kama usemavyo ni sahihi je hii elementi ni ya kutengeneza?”

“Upo sahihi katika dunia nzima hakuna ambaye anafahamu elementi hio zaidi yangu na haitokuja siku ukaweza kufahamu”Aliongea na kumfanya Jerry kuwa katika hali ya kujidharau , amefanya kazi kwa muda mrefu kuweza kgundua elementi hio lakini kazi yake inaonekana haikuleta mafanikio.

“Profesa kweli kuna gepu kubwa kati yako na mimi sikuwaza kwamba utakuwa na uwezo wa kufiria nje ya binadamu wa kawaida lakini haijalishi kama hutatotoa ushirikiano na kutuambia basi elewa lile kundi la watoto katika kanisa la Santa Maria hawatoliona jua la kesho”Aliongea na kumfanya Clark kumwangalia kwa macho makali.

“Wewe ni kichaa? Wale ni watoto tu wanakosa gani kwanini unataka..”

“Ninaweza kuwafanya chochote ndio , kwanza kama huwezi kuwatibia Saratani kwanini nisiwakutanishe na Mungu mapema, nakupa nafasi ya mwisho toa ushirikiano wako”Aliongea na kumfanya Ckark kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akainua kichwa chake.

“Okey , nitaongozana na wewe ili kukuonyesha inavyofanyika ..”Aliongea na kumfanya Jerry kutoa kicheko cha juu sana kwa furaha zote .

‘”Hahaha.. profesa ijapokuwa una akili kuliko mimi lakini bado wewe ni mtoto , angalia sasa umekubali, FURY , oh FURY wangu wewe. Haha”

Kicheko cha mwanaume wa kizungu kilisikika akicheka kama vile ni chizi.

******

Wakati Roma akiwa na Magdalena katika mgahawa pamheni ya hoteli wakimalizia kula chakula cha baharini , palepale alijiambia ni zaidi ya lisaa limepita tokea aachane na Sauroni na wengine lakini mpaka muda huo hakuna majibu , hivyo aliona atoe simu yake kujaribbu kumpigia Ron ili kujua nini kinaendelea.

Kabla hata hajaanza kupiga aliweza kuona kundi la watu likiwasogelea na aliekuwa akiongoza ni Sauron na walionekana na sura zilizokuwa na mwonekano wa wasiwasi pamoja na kuwa na msisimko.

“Mfalme Pluto , tumeweza kugundua kitu”Aliongea Sauron mara baada ya kungia ndani ya magahawa huo.

Ijapokuwa walikuwa wengi na ndani ya eneo hilo kulikuwa na watu , lakii kama ilivyokuwa kwa jiji hilo watu hawakushangaa sana wala kuhofia kwani Sauron alikuwa kwenye mavazi ya kijeshi.

“Umempata Clark?”

“Hakuna uelekeo maalumu wa sehemu aliopo lakini majasusi wa Mossad hivi karibuni wameweza kukusanya baadhi ya taarifa ambazo zina viashiria , Korea Kaskazini hivi majuzi wamefanya kazi na moja wapo la kundi la kigaidi kwa siri ndani ya Ulaya ya Mashariki kupitia mkondo wa kimawasiliano wa Kusini mashariki mwa Asia , ulikuwa ni ushirikiano wa majaribio ya utafiti wa siraha ya kinyuklia ambao ulianza mwaka mmoja uliopita , kama sio uhusikaji wa ghafla wa Korea kaskazini isingekuwa rahisi kuweza kupata viashiria kwa haraka”

“Korea Kaskazini , Majaribio ya nyuklia , Ulaya ya Mashariki … unajairbu kuamini kwamba ndio waliomkamata Clark ili kumalizia utafiti huo?”

“Inawezekana kabisa , tumeweza pia kugundua North Buyeo umoja wa siri uliopo nchini Korea Kusini ndio waanzilishi(instigators) wa mpango mzima , taarifa zinaonyesha wamenunua kiasi kikubwa cha madini adimu kutoka kwa Wamarekani wanaofanya biashara kimagendo pamoja na Maabara za siri na kuyaingiza Ulaya kitu kilichopelekea ushirikiano wa ghafla , na madini hayo adimu kwa maelezo ya Ashley Senga mwanafunzi wa karibu wa Profesa Clark anasema kwamba madini hayo licha ya kugundulika uuwepo wake lakini ni wanasayansi wachache sana duniani wanaojua kazi zake na namna ya kuyatumia na Profesa Clark ni mmoja wapo ,Pointi ya msingi ni kwamba tumeweza kukadiria muda kupitia Vinasaba vya damu vya yule mwanamke shushu wakati alipongia ndani ya maabara na imeonyesha ni zaidi ya wiki tatu sasa . kati ya wanafunzi ambao wapo chini ya Clark kuna anaefahamika kwa jina la Jerry , aliomba likizo wiki tatu zilizopita na hakuonekana mpaka sasa na hajulikani alipo , hivyo tunaamini huenda mipango yao imefanikiwa kwa kupitia mtu wa ndani wa karibu na Clark ambaye ni huyu Jerry”

“Hawa Buyeo wa Kaskazini …”Roma alitaka kuongea lakini alijikuta akianza kwaza kidogo , hakutaajia kwamba watu ambao waliomsumbua ndani ya Korea kusini walikuwa na mipango mikubwa zaidi , ijapokuwa hakujua ni sababu ipi ya kuwekeza katika tafiti za maswala ya nyuklia na wapi wanalenga lakini aliamini ni mpango ambao sio mdogo kabisa.

“You have said so much , then how narrow is the scope?”Anauliza kwa kusema ameongea sana lakini je ni namna ipi ameweza kufupisha utafutaji.

“Mfalme Pluto baada ya madini hayo adimu kuingia Ulaya yalitolewa katika mfumo wa kawaida wa kiusafirishaji na kuingizwa katika mfumo wa Black Market na tumeshindwa kujua uelekeo upi ni sahihi na upi sio sahihi na naogopa kama tukiendelea kutafuta kwa staili hii hatuwezi kumuokoa Princess Clark ndani ya muda”

“Kama ni hivyo kwanini upo hapa?”Aliuliza Roma akionyesha sio mwenye furaha.

“Ijapokuwa hatuwezi kutafuta uelekeo sahihi lakini tunaweza kujaribu kutafuta katika njia zote lakini hata hivyo kulingana na uelewa wako wa ramani ya ulaya pamoja na spidi yako inaweza kurahisisha kazi”Aliongea na sasa akamfanya Roma kuelewa kile ambacho Sauron anataka kumaanisha.

Ni kweli kama ataenda yeye mwenye kufuatilia basi ingekuwa rahisi zaidi kuliko watu wake na kitu kingine yeye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa mambo yasiokuwa ya kawaida kwa haraka kuliko wao.

Baada ya kufikiria Clark amefungiwa kwa muda mrefu na huenda yupo katika hali ya kukata tamaa , moyo wake ulifurukuta na palepale alisimama.

“Kama ni hivyo niambie uelekeo upi nianzie kupitia simu yangu na nitafuta kila eneo moja baada ya lingine”

“Utuwie Radhi mfalme tunaona hata aibu ya kukuomba kulifanyia kazi hili mwenyewe..”

“Haina shida , umefanya sahihi kuja kwangu”Aliongea Roma na kisha alimwangalia Magdalena.

“Magdalena nisamehe nadhani sitoweza kukutembeza katika eneo nililokuwambia , tufanye siku nyingine”

“Hakuna shida , muhimu ni kuweza kumtafuta Clark kwanza , je unataka nikusaidie chochote?”Magdalena alikuwa akijua maana aliambiwa na Roma.

“Haina haja , huwezi kuelewa kwa ukubwa wake Ramani ya Ulaya ya Mashariki , unaweza kurudi hotelini kwa sasa ,Ron ataandaa utaratibu wote namna ya kushiriki katika mashindano ya Caesar Conference”

“Okey kuwa makini lakini”Aliongea Magdalena na kumfanya Roma amwangalie kwa dakika na kisha akatabasamu na kuondoka.

Sehemu ya kwanza ambayo alipaswa kwenda kutafuta ni katika kisiwa cha Gotland kwenye bahari ya Baltic.

****

Muda huo huo wakati akiondoka katika maabara sehemu ambayo amekamatwa Clark .

Alionekana Clark ambaye alikuwa amevalia Gloves mkononi na miwani maalumu ya kulinda macho huku nywele zake ambazo zilikuwa zimechanguka dakika chache zilizopita alikuwa amezifunga kwa nyuma, akiendelea kufanya majaribio ya kisayansi.

Maabara aliokuwemo ilikuwa ni kubwa , huenda zaidi ya maabatra kubwa za kitaifa ambayo inamilikiwa na shirika binafsi ambalo halijajulikana bado , ilikuwa na kila aina ya vifaa ambavyo vina teknolijia ya halli ya juu, ulikuwa ni uwekezaji mkubwa sana uliofanyika kutokana na ubora wa maabara hio.

Clark alikuwa amesimama kwenye tarakishi kubwa ya kioo iliokuwa imewekwa kwenye meza ya kupangusa kwa mikono na alikuwa akiandika kwa spidi kubwa akijaribu kutengeneza muunganiko wa kikanuni wa kemia ambao ulikuwa mgumu kueleweka hata kwa mtu ambaye ana msingi wa kawaida sana wa somo la Kemia.

Sasa katika sehemu aliosimama upande wa mbele kulikuwa na mkono wa roboti ambao ulikuwa ukifanya kila kitu unachoelekezwa kwa kutumia kanuni zinazo andikwa katika tarakishi.

Nyuma yake kulikuwa na wanaume wenye miili iliojengeka waliokuwa wamesimama , wakiwa wamevalia makoti ya maabara wakimwangalia Clark kile anachokifanya kwa shauku kubwa na kadri alivyokuwa akichapa kwa haraka katika keybord ndio walivyozidi kutoa macho yao , kwa muda huo walionekana kama walinzi lakini kwa wakati mmoja walionekana kama wanafunzi.

Kati ya wote ambao walikuwa na macho kodo ni bwana aliefahamika kwa jina la Jerry , alikuwa akiangalia na kukariri kila aina ya taarifa iliokuwa ikionekana kwenye Skrini hio kubwa , ijapokuwa taarifa hizo zilionekana kuwa nyingi na ngumu kukariri lakini alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuweza kupata msingi wake huku akipotezea baadhi ambazo hazikuwa na msingi, macho yake yalikuwa yamejaa tamaa kubwa.

“Its wonderfull.. I never thought that there would be such a way to perfom fusion reactuon .. the power fo FURY was originally constructed like this”

“Hakika inashangaza , sikuwahi kufikiria kutakuwepo na njia ya kuunganisha matokeo ya kikemia ya namna hio .. nguvu ya FURY ilitengenezwa mwanzoni kama hivi”Aliongea.

Mwonekano wa mrembo aliekuwa akiandika mlolongo wa taarifa, katika maisha yake aliwafanya wanawake wengine kumuonea wivu , hakujaliwa uzuri tu lakini pia amejaaliwa uwezo wa kuchanganua maarifa na kudhalisha maarifa mengine , ilifanya hata watu kuona wasiwasi kumsogelea na kumtongoza kwa kuona kwamba hawana hadhi ya kuwa nae.

“Profesa usingekuwa upande wa yule shetani hakika lingekuwa jambo zuri sana..”Aliongea lakini Clark alikuwa kama mtu ambaye hajamsikia kwani aliendelea na kazi yake pasipo kumzingatia na aliendelea kuchapa kwenye skrini kwa dakika kadhaa na kisha akaacha na baada ya hapo alisogea upande wa kulia mwa meza iliokuwa na baadhi ya kemikali na kuanza kuziandaa.

“Profesa unafanya nini , kwanini umeacha?”

“Itachgukua zaidi ya masaa nane mpaka kukamilisha muunganiko , kwasasa nahitaji kuthibitisha usafi wa baadhi ya elementi ambazo zinakwneda kuathiri moja kwa moja matokeo ya Elementi unayotaka”Aliongea.

Jerry alimwangalia Clark kwa macho ya shaka , ijapokuwa hata yeye amebobea katika fani ya kemia lakini alikuwa mbali sana na maarifa aliokuwa nayo Profesa wake ndio maana alikuwa katikati kwenye kuamini maneno yake au asiyaamini.

“Profesa nakushauri usije ukafanya hila ya aina yoyote , nadhani unajua nini matokeo yake”

“Haina haja ya kunikumbusha”Aliongea pasio ya kuamsha kichwa chake , wakati akiendelea na kile anachokifanya kumbukumbu za utoto wake zilimjjia akilini , alikumbuka siku ambayo alikuwa ndani ya hosteli ya kanisa katika jiji la Milan akiwa na mama yake , wakiwa kama watu wakimbizi na ghafla tu akatokea kijana mdogo alievalia nguo za kininja na kuwaokoa katika mikono ya maadui zao , mwanaume aliewaokoa siku hio ni mwanaume huyo huyo ambaye amkuwa upande wake mpaka kufikia umri huo, lakini katika hali aliokuwa nayo alikosa tumaini na kujiuliza je mwanaume huyu atakuja kumuokoa kwa wakati kama huo ambao anamhitaji sana, ili kuepusha kutoa kanuni ambayo ingekuwa na athari kubwa kwa watu wa dunia.

*******

Baada ya Roma kuondoka Ron aliweza kuja katika mgahawa na kulipia gharama za chakula Roma alichokula na Magdalena.

“Miss Magdalena , je utahitaji kuudi hotelini sasa hivi au unataka kuendelea kuzunguka zunguka , ninaweza kumuita binti yangu ili kuwa mwenyeji wako na kukutembeza tembeza”Aliongea Rona kwa lugha ya unyeyekevu.

“Asante sana Mr Ron kwa ukarimu wako , kwasasa nadhani nitarudi hotelini kuungana na mwenzangu”Aliongea Magdalena alionekana kukosa ile furaha aliokuwa nayo.

“Naelewa unajisikia vibaya mara baada ya mfalme Pluto kuondoka ghafla , ninatamani sana wewe na Miss Rose kuwa na furaha kwa Trip yenu”Aliongea.

Ni kweli Magdalena mara baada ya Roma kuondoka alihisi hisia mchanganyiko huku ile ya kukasirika ikiwa imemtawala zaidi ,katika maisha yake tokea ayafahamu mapenzi mtu wa kwanza kumpenda ni Roma, lakini mwanaume huyo licha ya kwamba anaishi nae karibu lakini kwake ni kama alikuwa umbari mrefu sana ambao anakosa kabisa namna ya kumfikia.

Siku hio alijisikia vizuri sana kutembea pembeni ya mwanaume huyo anaempenda na alijikuta akipenda kuweka hisia zake wakati wakiendelea kula chakula, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembea na Roma ki upande upande , safari yao ya China ilikuwa ni kwa misheni maalumu lakini hapo ilikuwa ni kwa ajili ya matembezi na ndio maana kulikuwa na utofauti mkubwa , lakini sasa wakati akiwa ndio kwanza anaionja raha ya kukaa meza moja na mwanaume anaempenda wakifurahia chakula ghafla tu kunatokea dharula tena dharula yenyewe ni kwenda kutafutwa mwanamke mwingine kama mwanamke alijisikia uchungu.

“Ni sawa tu Mr Ron , siwezi kufa kwa kukosa mwanaume na isitoshe nimezoea maisha ya kuwa peke yangu”Aliongea na kumfanya Ron kushangaa.

“Hakika una hulka sawa kabisa na Malkia Persephone”Aliongea.

“Persephone !!.. unamanisha Edna?”

“Ndio japo imekuwa huzuni hayupo hapa”Aliongea

Magdalena aliona maneno ya Ron yamekaa kinyume, yamkini hawana uelewa kwamba mwanaume wanaemwita Pluto alikuwa akimuogopa sana mke wake na kumnyenyekea na asingekuwa hata na ubavu wa kumleta eneo kama hilo, hayo yalikuwa mawazo ya Magdalena.

Wakati wakiwa wanakaribia kuingia hotelini ghafla tu walisogelewa na mwanaume mzungu mwenye nywele nyeusi zilizojikunja , pamoja na macho ya bluu huku akiwa na tatoo kubwa eneo la shingoni , alikuwa akitembea kwa kuonyesha namna ambavyo anajiamini, hakuwa mbaya wa sura alikuwa na mwonekano mzuri.

Magdalena baada ya kumwangalia vizuri tu aliweza kumjua kwani sura yake alishawahi kuiona.

“Hades yuko wapi?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza mara baada ya kumsogelea Magdalena.

“Ares”Aliita Magdalena , alikuwa akimfahamu Ares kwani aliweza kumshuhudia kipindi alipokuwa akipambana na Roma katika mlima wa Oldonyo ole lengai , waliweza kumfahamu mara baada ya kufanya uchuguzi wa kuijua sura yake chini ya jeshi na yeye kama mkuu wa kitengo cha wachawi aliweza kuwa na taarifa ya sura yake licha ya kwamba uchugnuzi wao ulifanywa kuwa taarifa za siri za jeshi.

Magdalena hakushangazwa na uwepo wa Ares katika maeneo hayo kwani Roma aliongea nao na kuwaambia kwamba angeita miungu mingine kuja mpaka hapo, upande wa Ron ndio kwanza anamfahamu Ares kwani alikuwa akimsikia tu na palepale aliinama kuonyesha heshima baada ya kumfahamu.

“Mfalme Ares , Mfalme Pluto ameelekea bahari ya Baltic na ataendelea kusafiri kuzunguka baadhi ya maeno ya Ulaya kumtafuta mtu kwa zaidi ya siku mbili”

“Nini!!, kwahio unamaanisha kwamba hayupo hapa visiwani , ndio maana imenishangaza namtafuta simuoni”Aliongea huku akionyesha hali ya kutokuwa na furaha.

“Nilikuwa nikipanga angalau twend raundi moja ya mapambano, nadhani siwezi kufanya lolote”Aliongea.

Upande wa Magdalena huenda kabla ya kuingia levo ya Nafsi angemhofia Ares, lakini tokea aifikie levo hio alijihisi kabisa kuwa mkubwa juu ya binadamu wengine, moja ya athari kubwa ya nguvu za kijini ni hali ya kuwa na aina flani hivi ya ukiburi na hali hio ilimvaa Magdalena kwa wakati huo.

“Inahaja gani , ulipoteza pambano kipindi kile kule Tanzania, alikuwa na nguvu kidogo lakini kwasasa amezidi kuimarika , unafikiri unaweza kuwa mshindani wake?”

“Wewe mwanamke unajua nini , sikuwa nikipambana kwa uwezo wangu wote kipindi kile na pia nilimdharau adui yangu , kama ningejua alikuwa na mbinu zilizojificha kipindi kile ningejipanga , unaniambia ameimarika kwasasa , ngoja nikuelezee sisi tushapigana na wale viumbe wasionekana na tukawashinda licha ya levo zao kuwa za juu, unafikiri naweza kumuogopa Hades”Aliongea lakini licha ya hivyo haikumuogopesha Magdalena kwani alikuwa na taarifa zote juu ya kwamba Ares ndio aliekuwa dhaifu kuliko wote.

“Haha.. inapendeza , ni muda mrefu sana tokea mara ya mwisho tulipokutana lakini bado tabia yako ya kujikweza haijaisha tu”Sauti ya kume ilisikika nyuma yao na kuwafanya wote kugeuka

Alikuwa ni mwanaume mrefu , mzungu na ‘Handsome’ alievalia shati la mikono mirefu lenye michoto , hakuwa peke yake ameongozana na mwanamke mrembo mwenye nywele zake nyeupe., alikuwa ni Stern aliembatana na Alice ambao walifahamika kwa jina la Apollo na Artemis.

Alice mara baada ya kumwangalia Magdalena alitoa tabasamu pana na kumnyooshea mkono kumsalitimia.

“Hello beutifull wewe ni mmoja wa wanawake wa Hade pia ? Hehe naona unatoa msisimko wa nguvu za mbingu na ardhi . sio mbaya..”Aliongea

“Kuna haja gani ya kuuliza , kama sio mwanamke wa Hades ningekuwa nishamuua sasa hivi , hujui kuna sheria ya kuua binadamu na majini yote yaliofikia levo ya Nafsi yanayotuingilia katika ulimwengu wa kawaida?”Aliongea Ares.

“Acha kujigamba , swali muhimu la kujiuliza je unaweza kuniua?”Aliongea Magdalena kwa kiburi

“Unasemaje wewe?”Aliuliza Ares huku akianza kupandisha hasira zake.
 
SEHEMU YA TAT U.

Siku tatu zilikuwa zimepita pasipo ya Roma kuonana na Najma , jambo ambalo halikumshangaza kwani alikuwa akikumbuka vyema kuwa Najma alimuona mwanamke kahaba alielala nae siku mbili zilizopita , hivyo alijua fika kuwa mrembo huyo atakuwa na hasira kali sana juu yake , kwani alikuwa akijua sana kwamba alikuwa akimpenda , hivyo hata yeye hakutaka kujishugulisha sana juu ya Najma , kwanza aliona ni jambo zuri kwani angejiweka mbali na Najma.

Upande wa Juma pia jambo hilo lilimfurahisha sana , kwani aliamini kwa jambo ambalo Roma amefanya litamfanya dada yake kutomfikiria kabisa Roma na kuendelea na maisha yake huku akimtafutia mpango wa kueoelwa na mwanamke mwenye pesa zake na ili kuhakikisha Najma hafikiriii kabisa kuendelea kumpenda Roma alifanya kila njia kuhakikisha taarifa za Roma kulala na kahaba mpaka asubuhi zinasambaa ndani ya wapangaji pamoja na majirani.

“Mh! Roma kabisa … siku zote nilikuwa namuona kama anamatatizo flani hivi kumbe anaonekana na yeye anapenda wanawake . lakini alishindwa nini kumchuku Najma mwanamke mrembo mpaka kwenda kuchukua mwanamke kahaba mtaani”

“Heheee… huenda Najma kuna kitu anakosa katika mwili wake ambacho hakimvutii Roma” Hao walikuwa ni wapangaji waliokuwa wakiongea kishambenga wakiwa wanasukana , na yote hio ilikuwa ni kumuumiza Najma ambae alikuwa akiingia kutoka kazini , na Najma aliwasikia vizuri tu na kuzidi kumchukia Roma kwa kitendo cha kuleta kahaba kwenye nyumba yao.

Najma alionekana ni mwenye mawazo , mengi mno , lakini licha ya hayo yote ambayo yalikuwa yakiendlea kwa wapangaji , moyo wake ni kama umegawanyika vipande viwili , kwani kuna upande ulikuwa bado ukimpenda sana Roma na hakuwa tayari kumuacha , lakini pia kuna upande ambao ulikuwa ukimchukia sana Roma, Pande zote mbili zilionekana kushindana vikali sana , huku upande unaompenda Roma ukichukua ushindi kila baada ya pambano., baada ya upande huo kushinda kila mara , hamu ya kutaka kumuona Roma ilizidi kujaa katika moyo wake , alikuwa amemkumbuka sana na alipanga usiku wa leo kumuona kwa namna yoyote ile.

Muda nao haukukawia sana kwani ulienda kwa haraka haraka , kwani ile Najma anakuja kushituka kutoka usingizini ilikuwa ni saa kumi na mbili , alinyanyuka haraka haraka na kisha alielekea gengeni kununua mboga za usiku , na siku hio alipanga kupika wali na Choroko , hivyo alinunua choroki na kuzichemsha na kuanza kuandaa chakula cha usiku.

“Noja leo nipike kingi , nitamuwekea Roma wangu katika chumba Chake akirudi ale”Alijiongelesha mwenyewe wakati huo akichambua mchele.

“Vipi mwenzetu mbona leo unaonekana ni mwenye furaha hivyo”Aliuliza mama Debora moja ya wapangaji , huku akimwangalia Najma usoni, Mama Debora ndio mpangaji pekee ambaye hakuwa na umbea mwingi na alikuwa ni Mlokole katika kanisa flani lililokuwa mita chache kutoka nyumbani kwa Najma na pia ndio mpangaji pekee aliekaa kwa muda mrefu mno , kwani yeye pamoja na mume wake walianza kupanga hapo kwao tokea wakianza kuona na mpaka sasa ambapo walikuwa na mtoto mkubwa tuambaye alikuwa chekechea anaefahamika kwa jina la Debora ,Mama Debora hakuwa mtu wa Nyumbani sana kwani alikuwa akifundisha shule ya msingi Ikwiriri , sehemu ambayo ilikuwa mbali na kumfanya kudamka sana asubhi na kurudi jioni , hivyo hakuwa akijua maswala yoyote yaliokuwa yakimuhusu Roma kuingiza kahaba.

“Hakuna jipya mama Debo , ni ile tu leo nimejikuta kuwa ni mwenye furaha”Aliongea Najma na kumfanya Mama Debo atabasamu.

“Hehehe .. acha kunificha Roma kakutamkia anakupenda nini?” Najma aliona aibu kwa sentensi hio na kuzidisha tabasamu .

“Nilijua tu , unaonekana kumpenda sana Roma Najma”

“Hhaha .. ndio”

“Muone sasa anavyoona aibu … nimekuja kuweka umeme mimi”Aliongea Mama Debo huku akimpita Najma na kuingia ndani kwa ajili ya kuweka umeme kwani Luku ilikuwa kwa ndani.

Najma alidumu sebuleni kwao kwa muda mrefu sana huku akiwasubiria kaka yake na Roma kurudi kazini licha ya kwamba alikuwa na usingizi mzito uliokuwa ukimnyemelea , lakini hamu yake ya kutaka kumuna Roma iliushinda usingizi na kuendelea kusubiri , siku hii ya leo si kama siku zingine kwani walichelewa kurudi mno , kwani mpaka inafika saa tano na nusu kaka yake hakuwa amerudi , baada ya kusubiri kwa takribani dakika ishirini hatimae mlango uligongwa na Najma haraka haraka alikwenda kufungua mlango.

“Najma hujalala tu , leo mbona umekua kunifungulia wewe”Aliongea Juma huku akiwa ni mwenye kumshangaa dada yake ,kwani siku mbili za nyuma alionekana sio mwenye kujali kuwafungulia yeye na Roma.Kwa Najma licha ya swali hilo , hakujali kabisa kwani alichokuwa akitaka kuona ni Roma Tu , lakini kilichomshangaza ni kwamba siku hio alimuona kaka yake pekee jambo ambalo lilimshangaza.

“Roma yuko wapi kaka , mbona haingii”

“Nilijua tu unataka kumuona Roma”Aliongea Juma huku akiweka uso wa hasira na kumpita baada ya kufunga mlango , lakini Najma hakuridhika alifungua mlango na kuangalia nje lakini Roma hakuonekana , jambo ambalo lilimfanya kuwa katika hali ya maswali , alifunga mlango na kukimbilia ndani.

“Kaka Roma yuko wapi , mbona hujaja nae”.

“Bwana eeh usiniulize maswali yako mimi , kwani umeona natembea nae mfukoni”Aliongea Juma na alikerwa sana na maswali ya mdogo wake , na aliona kabisa si kama alivyofikiria kuwa Najma alikuwa ashaachana na Roma baada ya kumuingiza kahaba geto kwake, alikula chakula alichowekewa na mdogo wake huku akitabasamu kwa kuona kuwa mdogo wake anajua kupika na baada ya kushiba aliignia kwenye chumba chake na kujilaza.

“Najma akiolewa na mimi naoa , nyumba yote inakuwa yangu na ili hili litimie sitaki Najma aolewe na Roma maana nina uhakika kwa maisha ya Roma atataka aishi na Najma hapa hapa”Alijiongelesha huku akiwa amejilaza na kukodolea macho taa mpaka pale alipopitiwa na usingizi pasipo ya kuzima taa.

Upande wa Najma yeye hakuweza kupata usingizi kabisa , muda wote masikio yake yalikuwa kwenye geti tu , ili asikie geti likigongwa ili akamfungulie Roma , lakini muda ulizidi kwenda , lakini alichokuwa akitegemea hakikuweza kutokea kabisa, baada ya kuona atasinzia alienda kusbiria Sebleni mpaka pale alipokuja kupotelea usingizini , na alikuja kushituka kukiwa kumekucha kabisa na hii ni baada ya kaka yake kumkuta Najma akiwa Sebleni, alijikuta hasira zikimpanda baada ya kuona dada yake kalala hapo sebleni na kung`atwa na mbu huku akimsubiria fukara Roma arudi.

“Huyu mpuuzi akirudi leo na mfukuza akapange kwingine , kwa hali hii Najma hawezi kuoelewa”Aliongea Juma na kisha alitoka mpaka vyumba vya nje vya wapangaji na kwenda kwenye chumba cha Roma na kukifungua na kuingia , ndani na kitu cha kwanza alichoona ni mabakuri mawili makubwa ambayo alikuwa akiyafahamu yakiwa kwenye kijimeza , aliyasogelea na kisha kufungua bakuli la kwanza na hapo nipo alipotoa macho huku sura yake ikianza kujikunja.

“Yaani huyu mpuuzi anamuwekea Roma mapaja ya kuku halafu mimi kaka yake ananiwekea wali na Choroko, hii haiwezi kuendelea hivi”Aliongea Juma kwa hasira huku akinyanyua yale mabakuli na kutoka nayo nje huku akipishana na Najma ambaye alimkata jicho , baada ya dakika chache Juma alitoka akiwa na kufuri lingine na kisha alifunga mlango wa Roma na kisha kurudi ndani na kupasha kiporo kile na kula.

Wakati yote hayo yakiendelea Najma ambaye alikuwa kwenye hali ya wasiwasi , alikuwa akimwangalia kaka yake tu , huku akiogopa hata ya kumuuliza chochote kuhusu Roma alipo , baada ya kusimama nje kwa dakika kadhaa , Juma alitoka nje huku akionekana safari ya kwenda kazini kwake ikiw aimewaidia.

“Kaka najua umekasirika lakini naomba uniambie Roma yuko wapi”.

“Usiniulize maswali ya kupuuzi na , kwa upendo wako wa kijinga jinga Roma kwanzia leo akirudi anaenda kutafuta chumba kwingine na nisikie fyoko fyoko uone”Aliongea Juma huku akiweka kibakrashia chake vizuri na kutoka huku mlango wa geti ukiipigiza kwa nguvu.

“Halafu huyu Mpuuzi kaenda wapi , tokea jana mchana sijamuona tena alipofuatwa na yule mtu mwenye suti”

****

JANA YAKE SAA SABA MCHANA

Roma mpaka kufikia muda wa Saa saba mchana alikuwa amepiga kazi kubwa sana ya kuteremsha mizigo ya Cement , kwenye Duka kubwa la vifaa vya ujenzi la Bozi , yeye pamoja na wenzake walikuwa wamechafuka mno kiasi kwamba hawakuwa wakitamanika , lakini wala hawakujali sana , kwani kwao pesa ilikuwa ndio kila kitu.

Njaa nayo haikuwaacha salama , na baada ya kupewa ujira wao , Juma aliwaongoza wenzake kuelekea upande wa pili wa barabara ili kwenda kujipatia chakula cha mchana kwa Mama Joshua. Kama ilivyokuwa desturi yao.

Baada ya dakika kadhaa tu Roma alikuwa ndio alikuwa mtu wa mwisho kunawa mikono , alianza kunawa uso ili kutoa vumbi la Cement na kisha alimalizia mikono , lakini ile anamaliza tu mita kadhaa kwenye barabara kuu , ilisimama gari aina ya V8 nyeupe , gari ambayo iliwafanya baadhi ya watu kuikodolea macho .

Baada ya gari hii kusimama , alitoka mwanadada mmoja aliekuwa amevalia suti ya rangi ya bluu na viatu vya rangi ya Pink , mwanadada huyu alitoa picha kwenye mkoba wake na kisha aliangaza kulia na kushoto huku akitoa simu yake iliokuwa ikiita na kisha kuiweka sikio mara baada ya kuipokea na baada ya maongezi machache alikodolea upande wa kimgahawa cha Mama Joshua huku akikagua mtu mmoja mmoja na baada ya kuona kile alichokuwa akitafuta alisogea kuelekea upande huo wa mgahawa ,. Huku baadhi ya watu wakishangazwa na urembo na shepu ya mwanamke huyo , lakini hakuna aliekuwa ni mwenye kujali.

“Habari yako kaka”Aliongea mwanamke huyu kwa sauti ya kujiamini kabisa na kuwafanya wakina Juma na wenzake kushangazwa na kitendo hicho , kwani mtu aliekuwa akisalimiwa alikuwa ni Roma.

“Salama”Aliitikia Roma pasipo kujali uzuri wa mwanamke aliekuwa mbele yake na kusogelea meza ya plastiki ya rangi ya bluu na kuketi kwenye kiti huku mrembo huyu kuonesha kuchukizwa na kitendo cha Roma kutokumuangalia usoni , licha ya kumsemesha , kwake alitafsiri kama dharau kubwa ambayo ameonyeshwa kwa mwaka huo , yaani katika maisha yake na urembo wake , hakuwahi kudharauiwa na mwanaume wa aina yoyote ile , lakini kwa Roma ilikuwa tofauti na hio aliingiza katika Top Ten ya dharau alizowahi kuonyeshwa katika maisha yake, lakini licha ya hivyo , mwanadada huyu bado alionekana kuwa ni mwenye shida ya kuongea na Roma kwani alisogea mpaka kwenye meza aliokuwa amekaa Roma na kumwangalia kwa kumshusha kwa mavazi yake ya kimasikini na uchafu uliomjaa.

“Mama Joshua nipe ugali mkubwa na Samaki “Aliongea Roma na kuwafanya marafiki zake wazidi kumshangaa Roma kwa kitendo hicho cha kutokujali , licha ya kuongeleshwa na mwanamke mrembo kama huyo ambaye kwao , ilikuwa ni kama ndoto kupata bahati ya kuongeleshwa na mrembo kama huyo.

“kaka nimekusalimia”

“Ooh !,, sorry sister , nilikuwa bize kidogo , kumbe ulikuwa ukiniongelesha mimi”.

“Ulifikiri na muongelesha nani , au dharau tu kaka yangu , sio vizuri”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake ya kuvutia huku akionekana amekereka kweli kwa kitendo cha Roma kujifanya hakumsikia wakati wote huo aliokuwa anamsalimia , na kilichomkera Zaidi mwanadada huyu ni kutokana na watu waliokuwa wakimwangalia , alichokuwa ametegemea mwanamke huyu ni Roma kumnyenyekea , lakini swala hilo likawa nje ya mategemeo yake na kumfanya yeye ndio aonekane mwanamke mwenye shobo na katika baadhi ya watu waliamini huenda huyo mwanadada alikuwa ni demu wake.

“Ulikuwa unasemaje sista”.

“Wewe si ndio Roma”

“Ndio ni mimi”

“Basi naomba utangulizane na mimi kuna mtu muhimu sana anataka kuonana na wewe”Aliongea mwanadada huyu na kuwafanya watu wote waliokuwa hapo mgahawani kushangazwa na maneno hayo , ila kwa Roma hakuonekana ni mwenye kushangaa sana , kwani alipokea chakula chake na kuanza kula.

“Sister naomba ukae , kwanza unisubirie nimalize nipige msosi ndio tuongee maswala ya mtu Muhimu .. maana hii ni moja ya starehe yangu na mara nyingi ni kila sipendaki kusumbuliwa”Aliongea Roma kwa kujiamini huku akianza kumega bonge la tonge na kulichovya kwenye mchuzi na kisha kulimeza lote , kitendo ambacho kilimshangaza sana huyu mrembo , na kumkera kwa wakati mmoja.

“Nitasubiri kwenye gari , ukimaliza naomba tufutatishane kama nilivyokuambia”Aliongea ule mwanadada pasipo kusubiri jibu , na kisha kuondoka .

“Halafu we Ms**nge unapenda kuifanyisha matawi ya juu , mtoto mkali kama yule anakuongelesha unajifanya unaongea kama hutaki kama vile Mondi , vile au unatuoshea tu washikaji zako hapa”Aliongea Yusuph huku akiungwa mkono na wenzake.

“Ila jamaa nimemkubali sana , ile pia ni heshima”:Aliongea jamaa mmoja ambaye yeye hakuwa muongeaji sana , ila siku hio alionekana kuchangia.

“Hahaha .. Mhando hata wewe leo umechangia mada , inaonekana pia umeguswa sana na jambo hili”Aliongea Juma na kuwafanya wengine wacheke maana ni kwa mara ya kwanza kwa Mhando kuchangia mada , yeye alikuwa ni mkimya wa hali ya juu

Baada ya Zaidi ya nusu saa ya Roma kumaliza msosi wake , alipiga maji kwenye kikombe , na kisha alijishika tumbo lake na kujiona kushiba vyema na kutoka mgahawani na moja kwa moja alielekea kweye gari , na kugonga mlango wa kioo ulioshushwa.

“Ingia kwenye gari”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti iliojaa machukizo na kwa Roma wala hakujali , baada ya kuingia kwenye gari , ilitolewa nduki kuelekea upande wa Kongonwe na kuja kugeuzwa na kurudi upande wa kuelekea kariakoo.

“Unanipeleka wapi Mrembo”Aliongea Roma lakini hakujibiwa , Zaidi ya kusonywa na Roma aliamua kutulia kwenye kiti chake , huku akifurahia kiyoyozi kilichokuwa kwenye gari hilo, na kutokana na uchomvu aliokuwa nao , alipitiwa na usingizi na hata pale alipokuja kushituka alijishangaa akiwa mbele ya jengo refu mno maeneo ya Mawasiliano Sehemu ambayo alijua haraka kwani alikuwa ni mwenyeji wa maeneo hayo , baada gari hii kusimama kwenye jengo hili Geti lilifunguliwa na gari ile iliingizwa mpaka ndani na kuegeshwa na kisha mwanamke yule mrembo alishuka .

“Karibuni Grand palace hoteli wateja wetu”Ilisikika sauti ya muhudumu iliowakaribisha kwa tabasamu na ucheshi wa hali ya juu ,Roma alimwagalia mwanamke huyo aliekuwa amevalia sare ya hoteli hio na kisha alimkonyeza kitendo ambacho yule mwanadada aliekuja na Roma kukiona na kubetua midomo , lakini kwa muhudumu alirudisha kwa tabasamu la kuita.

“Watu wenye pesa wanakula maisha sio poa”Aliongea Roma baada ya kuingia kwenye lift huku akiwa si mwenye kuacha kumkonyeza mrembo huyu ambaye amenuna kama muuza sumu.

Baada ya lift kufunguka katika Floor namba kumi na nane , Roma alifuata nyuma nyuma mpaka walipofika kwenye mlango wa chumba namba 708 na kisha huyu mrembo aligonga mlango na ndani ya dakika kadhaa mlango ulifunguliwa na mwanaume alievalia suti.

“Karibu Suzzane”Aliongea mwanaume huyu alievalia suti huku akiwa ni mwenye tabasamu lakini pia macho yake hayakuwa mbali na uso wa mwanaume aliekuwa nyuma ya Suzzane , mwanaume ambaye kwa macho ya haraka haraka alionekana kama Fukara.

“Bossi nisharudi na nimemleta”Aliongea mrembo Suzzane kikakamavu huku akimwangalia mwanamke aliegeukia dirishani , akionekana kuangalia nje akiwa amewapa watu wote katika chumba hiko mgongo.

Mwanamke huyu alikuwa amependeza mno kwa vazi lake la suti alilokuwa amevaa ,suti ya rangi nyeupe

“Asante Suzzane , mnaweza kuondoka mpaka pale nitakapowaita”

“Boss!!”Aliongea Suzzane kwa hali ya wasiwasi .

“Fanya kama nilivyosema Suzzane”Aliongea mwanadada huyo kwa sauti ya Amri na kumfanya Suzzane amkate jicho Roma ambaye alikuwa akikagua uzuri na ufahari wa chumba hiko.

Licha ya Roma kushangazwa na ufahari wa chumba hicho , lakini pia sauti ya mwanadada aliekuwa mita kadhaa mbele yake aliempa mgongo ilikuwa ikimsisimua mno , ilionekana kama inamkumbusha mbali sana.

Baada ya Suzzane na mwanaume yule kutoka nje , mwanadada yule aligeuka na kumwangalia Roma , kitendo ambacho kilimfanya Roma atoe mshangao na kutamka:

“Kahabaaa…!!!”

ITAENDELEA SIKU YA KESHO JIONI..
Naye alidhani kuwa ulikuwa muaminifu kumbe kahaba
 
SEHEMU YA 568.

Stern mara baada ya kuona kitu kibaya kinakwenda kutokea , palepale alisogea na kumshika Ares ili asije kuleta malumbano na Magdalena.

“Kwasababu ni mwanamke wa karibu na Hades basi ni mmoja wetu , Ares hasira zako za haraka haziwezi kubadilika hata kama utapewa miaka elfu therathini ya kuishi , kwasasa wote turudini hotelini muda ambao Poseidon na Hermes watafika hapa tutasalimiana na marafiki zetu”Aliongea Stern

“Nitaacha hili lipite kwa leo”Aliongea Stern huku akimwangalia Magdalena kwa hasira kubwa na kisha akaondoka katika hilo eneo.

*********

Anga la Norway katika bahari licha ya kwamba kulikuwa na jua lakini bado kulikuwa na ubaridi wa aina yake.

Mbele yake ni bahari isionekana mwisho wake , na alichoweza kuona ni mawingu ambayo yanatawanyika kila pande.

Usiku ulikuwa ushapita tayari , Roma alikuwa ametafuta katika kila sehemu ambazo hazikuwa na watu wengi sana na kutofikika kwa urahisi hususani milimani na katika pembezoni mwa bahari katika maeneo yote ya Kaskazini mwa Ulaya

Alianzia Gotland katika bahari ya Baltic akaeda Stockholm halafu Oslo na Bergen , katika maeneo yote hayo kulikwa na vituo nane ambavyo vyote vilikuwa ni vya kimitengo ambavyo vimetengenezwa na wahalifu ili kuchanganya watu wanaowatafuta.

Roma aliweza kupata moja wapo ya kambi ya siri katika kijiji kimoja lakini licha ya hivyo hakuweza kuona dalili yoyote ya majaribio ya sayansi ya nyuklia .

Mpaka hapo aliona kabisa ilikuwa sahihi kuja yeye kutafuta , kwani kama ni watu wake wasingefanikisha chochote, yeye licha ya spidi yake kubwa lakini bado tu hakuwa amefanikisha kumpata Clark.

Roma alitoa simu maalumu aliokabidhiwa na Sauron ili kuwasiliana nae moja kwa kwa moja kupitia satilaiti.

“Sauron wapi kumebakia?”Aliuliza.

“Mfalme Pluto kutoka bahari ya Norway kwenda Kaskazin kuna kituo katika eneo la Wilwick na ukielekea magharibi zaidi kuna meli inayoelekea Iceland na nyingine inaelekea Nuuk Greanland , Kusini kutoka sehemu ulipo pia kuna kituo cha Rotterdam nchini Uholanzi , Leipzig nchini Ujerumani , Marseille nchini Ufaransa na Lodz nchini Poland na kuendelea”Aliongea Sauron kupitia simu na kumfanya Roma kung’ata meno yake kwa hasira.

“Pumbavu kabisa yaani wamefanya makusudi kutengeneza vituo hewa vingi ili wasikamatike kirahisi”.

Ukumbuke hapa kwamba Roma anachofatilia ni uelekeo wa madini adimu yalikosafirishwa hivyo vituo anavyozungumzia Sauron ni vile ambavyo wanaamini meli iliosafirisha mzigo ilisimama.

Kama kutakuwa na sehemu meli imesimama na kushusha mzigo moja kwa moja ingemaanisha kwamba katika ukanda huo wote kutakuwa na maabara ya siri na hicho ndio ambacho Roma alikuwa akitafuta.

“Mfalme Pluto nafikiria kwamba tachane na baadhi ya vituo , kwa mfano maeneo ya Ufaransa yapo karibu sana na bahari ya Mediterranian na yana idadi kubwa ya watu hivyo kukosa sifa kujificha na uwezekano wa wao kufanyia majaribio ya sayansi ya nyuklia katika maeneo hayo , lakini pia hawawezi kuyachagua kwani wangehofia kukamatwa haraka na jeshi , hivyo nashauri uelekee upande wa magharibi na mimi nitaamrisha vikosi kutafuta upande wa miji ya Kaskazini”

“Mimi nashauri tufanye kinyume chake , tutaanza kuafuta kutoka katika latitiudo za chini kwenda latitudo za juu , miji na maeneo ambayo yapo zaidi karibu na bahari ya Mediterranian tutaanza kutafuta huko kwanza”

“Mfalme Pluto unadhania kwamba wamefikiria kinyume makusudi kuchagua maeneo ambayo sisi hatwezi kufikiria kama wameyachagua si ndio?”

“Haiwezi kuwa rahisi Sauron , nakumbuka umesema haiwezekani kwa maabara kuwepo katika watu wengi waliozagaa , njia zuri kwa kundi la watu wengi kama hao kujificha basi kwa angalau miaka ni katika maeneo ambayo yana idadi kubwa ya watu, kwahio nafikiri maeneo sahihi ya kutengeneza maabara ni katika maeneo hayo , hata hivyo kwasasa ni makisio yangu tu lakini tunaweza pia kuotea baadhi ya maeneo tofauti na kutafuta bila uelekeo”

“Uko sahihi nitawaagiza vijana kuanza kutafua upande wa kusini sasa hivi?”Aliongea Sauron na palepale walikatisha maongezi yao

Baada ya Roma kukata simu palepale aliichukua safari ya kuelekea Marseille nchini Ufaransa , ijapokuwa anakwenda kuonekana katika maeneo hayo kukiwa mchana kweupe lakini hakujali kama anaweza kuibua taharuki , alijiambia akifika katika hayo maeneo atatumia spidi kubwa kuzunguka ili hata kama kuna mtu atakae weza muona asiweze kuamini kama ni mtu bali maluweluwe.

Alikuwa akifikiria kinachoendelea Sicilly kwa muda huo katika mashindano ya Caesar Conference na kwa haraka haraka alijua mpaka muda huo mashindano hayo yatakuwa yamefunguliwa rasmi , lakini hata hivyo alijituliza kwa kujiambia hakuna baya ambalo linaweza kutokea kama tu Christen atakuwa ametaarifu miungu wenzake kufika katika.

*******

Wakati Roma akielekea Ufaransa upande mwingine katika jiji la Palermo karibu na bandari kulikuwepo na Colloseum kubwa ya kizamani iliokuwa imejazwa na makelele.

Ukumbuke Colloseum ni uwanja au Ulingo unaotumika kwa michezo ambayo huhusisha damu na hicho ndio ambacho kilikuwa kikienda kuanza ndani ya uwanja huo.

Ulikuwa ni uwanja mkubwa sana uliokaa kama duara na kwa upande wa nje ulionekana kama vile ni jengo la Ghorofa la froo nne liliojengwa kama duara.

Licha ya kwamba ni jengo ambalo lipo kama makumbusho lakini lilikuwa limefanyiwa maboresho makubwa na umoja wa makundi ya kimafia ya Sicilly kwa kazi maalumu ya kufundishia watu wao , kwa nje ni jengo lililoonekana kuwa na muundo wa kizamani lakini ndani yake lilikuwa na mwonekano wa kisasa zaidi kama vile kiwanja cha mpira.

Ni Ulingo uliokuwa ukiruhusu zaidi ya watu elfu therathini kwa mpigo na cha kushangaza sana asilimia kubwa katika siti zote hujazwa na wanajeshi wa makundi mbalimbali duniani ambao hushiriki.

Ukichana na watu hao kuwa wanajeshi lakini kwa jinsi walivyoketi katika viti vyao ni kama vile ni mashabiki wa mpira , kwani waliongea lugha mbalimbali na kufanya zogo kubwa kusikikika katika rafudhi mbalimbali.

Katika eneo la VIP , Magddalena na Rose walikuwa tayari washachukua siti zao mapema sana , katika eneo hilo alikuwepo Stern na dada yake Alice , vilevile alikuwepo mrembo Christen na kwa upande wa Ron na mtoto wake Fidero walikuwa wapo pembeni yao wakihakikisha kuwahudumia kwa kila kitu watakachotaka.

“Wanaanza kupigana saa ngapi ni zadii ya lisaa tokea sherehe za ufunguzi kumalizika?”Aliongea Rose aliekuwa na shauku ya kuona mapambano haraka iwezekanavyo.

“Unaonaje tukicheza raundi moja ya kadi ili kupoteza muda?”Aliogea Magdalena kwa kutania huku akicheka na kumfanya Rose kubetua midmo.

“Cheka uridhike mama, nimepoteza hela nyingi kwenye kamari lakini kwangu sio tatizo , wale watu hata hivyo walikuwa na maprofesheno kwenye kucheza kamari ingeshangaza mimi kushinda”Aliongea , ilionyesha siku ya jana alikuwa amepoteza hela nyingi sana.

“Oh! Miss Christen nimekumbuka , je napaswa kukuita Venus si ndio?”Aliuliza Rose.

Wakati huo Christen na Alice alikuwa wameshikiria jarida na fasheni na mitindo wakiangalia baadhi ya picha za nguo ambazo zimewekwa.

“Vyovyote utakavyoniita sawa tu lakini usije kuniita Venus kwenye kundi la watu”Aliongea.

Kitendo cha Rose kuwa karibu na Roma kwenye maisha yake kimemfanya kujua uwepo wa hao viumbe kutoka sayari nyingine ambao serikali nyingi duniani kubwa hujaribu kuficha uwepo wao.

“Nataka nikuulize swali , je unafahamu wale watu wa mavazi meupe?”

Baada ya kuulizwa swali hio alionyesha upande wa kulia kwake katika eneo la VIP , kulikuwepo na wanaume watatu waliokuwa wamekaa , alikuwepo Poseidon ambaye amevalia kombati za jeshi la Marekani lakini pia Ares na Hermes ambao walikuwa wamevalia suti na viatu vya ngozi wakiwa kawaida.

Majamaa hao hawakuwa wakipendelea sana kukaa karibu na wanawake kutokana na kwamba hawakupenda sana kuongea ongea lakini kitu kingine ukiachana na Hermes , Ares na Poseidon walikuwa wakifanana kitabia walikuwa wakipenda sana fujo.

“Angalia na wale wanasubiri kama sisi tu , tutaweza kuthibitisha wakati watakapotokea na isitoshe Hades hayupo hapa na Athena pia hayupo , haitakuwa rahisi kama tutaweza kukutana na maadui wetu wa zama zile”Aliongea.

Maneno yake ni kama yalizidi kumuongezea Rose shauku ya kutaka kujua watu hao ni wakina nani na alitamani muda huo hata Roma aweze kurudi mapema baada ya kumpata Clark , lakini akili yake haikuwa mbali na kufikiria kama kuna uwezekano wa kitu kibaya kimetokea.

Wakati wa watu kuanza kuchoka hatimae msherehesaji katika jukwaa maarufu alitangaza kwamba raundi ya kwanza ya mapigano ingeanza .

Kutokana na timu nyingi ambazo zilikuwa zikishiriki siku ya kwanza kulikuwa na raudi ya mtoano , kulikuwa na timu sita ambazo zilikuwa zinacheza kila raundi na kila mshindi atakae toka katika kila pambano basi atakuwa ameingia katika nafasi ya kucheza siku inayofuata.

Mkutano wa Kaisari mara nyingi huzuia mauaji ndani ya ulingo lakini kama itatokea kifo cha bahati mbaya au kumpelekea mshiriki kupata ukilema basi hawezi kukosa vigezo kuendelea na hayo ni makubaliano ambayo yanasainiwa na kila timu kabla ya kuanza.

Ukweli ni kwamba licha ya kwamba kuna makundi ya wanajeshi wapiganaji ambao walikuwa na asilimia ndogo za kushinda lakini walikuwa na uwezo wa kibunifu wa kuweza kutoroka pale wanapozidiwa na hilo limesaidia sana kupunguza mauaji yanayotokea katika ulingo kwa zaidi ya miaka nane mfululizo.

Uwanja ulikuwa umegawiwa katika maeneo matatu na muda huo mwanajeshi mmoja baada ya mwingine aliweza kutoka na kwenda kusimama katika eneo ambalo ameelekezwa.

Kulikuwa na ulingo tatu ambazo zote zilipaswa kila timu kupigana na mshindani wake katika mgawanyo wa timu mbilimbili.

Kilichomkatisha tamaa Rose ni kuona The Eagles sio timu ya kwanza ambayo imeanza katika randi hio , lakini palepale alionekana mtu mmoja aliekuwa kwenye mavazi meupe ambae aliingia katika ulingo akiwa peke yake na kuonyesha kutaka kushindana na timu ya watu watano.

Yaani mtu mmoja wa mavazi meupe alikuwa akitaka kudili na timu ya watu watano na ilifanya hali ya hewa kuwa katika ukimya wa hali ya juu kuangalia kinachokwenda kutokea.

Baada ya watu hao kujitokeza Christne na wenzake wote walijikuta wakisimama na kumwaangalia mtu yule kwa mshangao.

“It is real hem .. how did they come back”Aliongea Hermes akisema ndio wenyewe , wamewezaje kurudi.

“Kuna haja gani ya kuwa na wasiwasi , hili ni jambo zuri pia, kipindi kile tuliwaacha hai nadhani muda huu itakuwa nafasi nzuri kuwamaliza kabisa”Aliongea Ares.

Upande wa Poseidon yeye alionekana mwenye kujiamini wala kutokuwa na mshangao mkubwa na alikunja sura baada ya kumuangalia namna ambavyo Ares anaongea kwa kujigamba.

“Unasema kuwamaliza , hivi unafikiri wewe ni Zeus au Athena?Unafikrii unaweza kuwamaliza wewe kama wao walishindwa? , kwasababu wameweza kurudi lazima watakuwa na njia yao maalumu ya kuingia na kutoka , kama sio hivyo wasingekuwa ni wenye kujiamini kujitokeza mbele yetu”Aliongea Poseidon mpishi huyo na mwanajeshi kwa wakati mmoja.

“Poseidon nafikiri unaishi nyuma ya muda na unazidi kupoteza kujiamini , hawa ni kundi tu la wezi na wauaji wa miungu , hata baada ya miaka elfu ishirini hawawezi kubadili kilichopo ndani yao”

“Acheni kulumbana mara moja, muda huu lazima tufikirie namna ya kumtaarufu Athena ,Wakati huu Zeus hayupo na hatujui kama Hera na Dionysus wameamka , kama hatokuja hapa sijui namna ya kudhibiti hali’Aliongea Hermes.

“Umeanza lini kumkubali Athena wewe , si siku zote ulikuwa ni mwenye kumchukia na kutaka kuonyesha una uwezo mkubwa kuliko yeye?”Aliongea Ares kwa kejeli huku akicheka.

“Hata kama namchukia lakini kwasasa tupo upande mmoja kushindana na adui mmoja”

“Acha unafiki”

“Hehehe ..vyovyote unavyofikiria”

Kila aina ya kelele na vifijo vilisikika katika uwanja mzima , watu wengine walikuwa kwenye mchecheto mara baada ya kuona labda ni majivuno na kujiamini kwingi kwa timu ya kundi la DEICIDE kutuma mtu mmoja kushindana na timu ya watu watano.

Ni wakati huo huo kundi la wapiganaji ambalo lilijiatambulisha kama wawakilishi wa Afrika kumvamia yule mtu wa mavazi meupe kwa fujo zote.

Hawa Masenari wa kiafrika walikuwa na miili mikubwa mno na ni wenye nguvu ,ijapokuwa namna wanavyopigana sio kwa utaratibu maalumu na kwa wepesi lakini walikuwa na spidi na walichagua maeneo muhimu ya kumpiga adui

Mtu wa mavazi meupe aliekuwa na sura iliofunikwa na Mask ya madini ya Dhahabu alisimama katika eneo moja bila ya kusogea na hata maadui zake walivyomsogela hakufanya chochote na aliwaacha wafanye wanachotaka, walijaribu kurusha ngumi kumpiga katika maeneo ya kifuani , usoni na kwenye kiuno kwa kuunganisha nguvu lakini hawakuweza kumsogeza hata inchi., ni kama vile mtu anapojaribu kupunguza maji chumvi ya maji ya bahari kwa kumwaga maji safi.

Tukio hilo liliwafanya wale watu kushindwa kujua ni kipi cha kufanya zaidi , maana wamepiga kwa kutumia mbinu zao zote , lakini hakukuwa na matokeo ya adui yake kuonysha kuumia ni kama wanajaribu kulima jiwe kwa kutumia majembe.

Muda uleule kulisikika sauti isiokuwa ya kawaida,ilioashiria dharau kutoka kwa yule mtu wa mavazi meupe na palepale wale waafrika wenzetu ni kama vile walikuwa wakivutwa kwani wote walirushwa pembeni na nguvu isiokuwa ya kwaida na kwenda kudondokea mbali nje ya ulingo.

Ijapokuwa hawakuwa wameumia , lakini mshindani wao aliwashangaza na kumuona sio wakawaida kabisa kwa namna ambavyo anapambana na walikosa ujasiri wa kueondelea na palepale kengere ya refarii kupitia vifaa vya Eletronik ilisikika na kutangaza timu ya DEICIDE imeshinda kuingia raundi nyingine.

Licha ya hivyo mtu wa mavazi meupe alionekana kama vile hakuwa hata na haja ya kuingia raundi nyingine bali alikuwa amesimama akiwa ameangalia upande mmoja ambao ni wa VIP.

Miungu sita iliokuwa katika eneo la VIP ndio walengwa wake wakuu na macho yake kama yalivyoonekana katika Mask yalikuwa ni yale aliokuwa na dharau lakini pia ya kiuchokozi.

“Haiwezi kuwa makosa , muonekano wao na nguvu bila ya kuwa na msisimko wowote wa nguvu ya kiroho , ni wao bila shaka”Aliongea Sten huku akikunja sura.

“Lakini kama kweli ni wao na wametoka walipokuwa , kwanini wameshiriki katika mashindano ya binadamu , si maadui zake ni sisi?”Aliuliza Alice.

“Sina uhakika kwasasa , lakini kwasababu tayari washatangaza vita basi haitakuwa rahisi kama miaka elfu ishirini iliopita na inaweza kusababisha dunia kuingia katika taharuki , tunapaswa kuona mambo yatakavyokwenda”Alijibu .

“Hao ni wakina nani , kwasababu unaonekana unajua kwanini na sisi usitutoe gizani?”Aliuliza Rose , yeye na Magdalena hawakuwa wakijua chochote na Christen alivuta pumzi na kuzishusha na kisha akaongea.

“Have you heard about .. A race named GIANT?”Aliuliza akisema je ashawahi kusikia kabila la watu waliofahamika kwa majina ya GIANT.

“Giant!!?”Aliongea Magdalena huku akionyesha mshangao na kuonekana akifikiri.













SEHEMU YA 568.

Magdalena mara baada ya kufikiria kwa muda alikumbuka maneno ya Roma na Ron walivyokuwa wakizungumzia kuhusu kundi la Kimasenari ambalo linajiia Ps linalohusiana na Cyclops.

“Nimesikia mshindi wa mashindano yaliopita ni kutoka kwa familia iliopewa jina la Cyclop ?”

“Upo sahihi , Cyclops ni sehemu ya Giants(Majitu) wana uhusiano wa karibu pia na Centimani , kulingana na historia Centimani iliwakirisha majitu mia moja katika vita , Hadithi za miungu kuna nyingine ni za uongo na nyingine ni za ukweli ambazo zilikuwepo enzi hizo zilizoandikwa na binadamu, kabila la Cyclop ni uzao mchanganyiko kati ya Giants na binadamu wa kawaida , hivyo unaweza kusema Cyclop wamerithi tu damu yao na sio muonekano. licha ya hivyo uwezo wao ulikuwa mkubwa kushinda makundi yote ya kimasenari katika mapigano.

Sasa basi hawa Cyclops halisi pamoja na Centmani wanatokea katika uzao mmoja ambao ni sawa na wa kwetu lakini hayo ni mambo ya zamani sana ambayo yametukia katika sayari yetu , nguvu zao za kimwili ni kubwa mno kuliko za kwetu lakini nguvu zao za kiroho hazikuwa kubwa kutupita hivyo wakawa na uwezo mdogo sana wa kutumia kanuni za anga na sio washindani wetu kabisa kipindi hicho na katika sayari yetu walikuwa ni kabila lenye hadhi ya chini kabisa ambalo lilikuwa chini yetu lakini mara baada ya sayari yetu kukosa uwezo wa kusapoti maisha sisi tlikuja duniani lakini wakati huo sio kama tulikuja duniani tukiwa peke yetu, baadhi ya Cyclops na Centiman walikuja duniani kwa kupewa msaada na Hepheastus ambaye alikuwa ni mwanasayansi aliebobea katika utengenezaji wa dhana , utofauti wa hawa Majitu na sisi wao walivyofika duniani waliweza kuhimili mazingira lakini kwetu sisi tulishindwa hivyo uwezo wetu wa kuendeleza kizazi chetu ukawa mdogo sana na ni kipindi ambacho waliweza kugundua tulikuwa tumeivaa miili ya binadamu ili kuweza kuishi walituchukulia kama dhaifu sana na baada ya kuona hilo hawakutaka tena kuwa chini yetu bali juu yetu na walianza kutuwinda ili watuue lakini matokeo yake Zeus akagundua mipango yao na akatumia kauuni za anga kupitia siraha yake ya Thunder na kuwafungia katika ‘Dimension’ mbalimbali na kwanzia hapo ndipo walipoweza kupotea katika uso wa dunia , lakini hakuna ambae alitarajia leo hii wataonekana tena kwa zaidi ya miaka elfu ishirini katika miili ya kibinadamu”Aliongea

“Kama ulivyosema ni sahihi , mbona hawaonekani kuwa na uwezo mkubwa, kwanini Zeus hakuwaua kabisa”Aliuliza Rose

“Ilikuwa ni ngumu sana kuwaua kwasababu ya miili yao ndio maana Zeus akaamua kuwafungia kwenye Dimension nyingine kwa kutumia kanuni za anga, ijapokuwa hatuwaogopi lakini ni ngumu sana kupambana nao na zaidi ya yote kama wametoka wakiwa hivi inamaana wanao uwezo mubwa na kama sio hivyo wasingetokea”

“Kama Zeus ndio aliekuwa na nguvu kuliko wote na alishindwa vipi kuhusu sasa hivi?”

“Kama tungekuwa na miili yetu kama kwenye sayari yetu na nguvu zetu kuwa asilimia mia moja wasingekuwa na ubavu hata wa kutusogelea”

“Unamaanisha nini?”

“Haha..Usiulize maswali mengi , Inabidi mjaribu kuwasiliana na Hades arudi haraka iwezakanavyo”Aliongea Christen huku akicheka

*****

Ni katika nchi ya Ujerumanni katika ukanda wa eneo la Bavaria , Roma ndio kwanza alikuwa amefika katika eneo hilo akitokea Marseille Ufaransa akijiandaa kuelekea Leipzig.

Sasa wakati akiwa anapita katika jiji la Munich alisimama ghafla , wakati huo alikuwa akiongea na Sauron ili kumpa maelekezo lakini mfumo wa mawasiliano ulionekana kuingiliwa na kumfanya Roma kusimama.

“Mfalme Pluto kuna kitu umepata?”Aliuliza Sauron mara baada ya kuona Roma yupo kimya.

“Sauron hii njia ya mawasiliano tunayotumia si mtandao wake unajitegema na tunatumia satilaiti binafsi?”

“Ndio Mfalme , njia hii inazuia baadhi ya taasisi nyingine kuingilia mawasiliano yetu na kutudukua, tumeweza pia kuweka nywira ili isiwe rahisi”

“Kwahio inamaanisha kwamba kama itatokea mawasiliano yakayumba inamaana kuna mtu alieingilia kutoka ndani si ndio anaejua mfumo wetu?”

“Ndio Mfalme na kama ni hivyo basi nakubaliana na wewe kwani mawasiliano yetu yalikuwa mazuri tokea tuanze msako”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria huku akianza kuchunguza kila upande na aliweza kusikia tena mawimbi ya frikwensi yakiingiliana na mawasiliano yao

“Hebu jaribu kuangalia kama kuna sehemu gani ndani ya eneo la ukanda wa Bavaria ambalo kuna uwezekano wa uwepo wa kambi”Aliongea Roma na Sauron alichukua agizo hilo na kulifanyia kazi.

“Mfalme Pluto hilo eneo ni mahususi kwa ajili ya Viwanda na hakuna kingine ukiachana na sehemu mbili zilizotelekezwa ambazo kuna migodi mwili ya makaa ya mawe iliotelekezwa kwa miaka mingi”

“Migodi ya makaa ya mawe , unamaanisha ambayo ilichimbwa miaka mingi iliopita?”

“Upo sahihi lakini hata kama ni ya zamani ilikuwa ni mikubwa mno na inaenda sana chini na imetawaliwa na joto la kiwango cha juu , hivyo eneo hilo haliwezekani kuwa sahihi kwa ujenzi wa maabara”

“Umekosea Sauron , huu ndio ufunguo kwasababu jotoridi kuwa juu inafanya eneo hili kuwa sahihi kujenga maabara”Aliongea Roma na kumfanya Sauron upande wa pili kushangaa.

“Could it be.. Geotharmal energy”Aliongea Sauron akimaanisha je wanatumia nguvu ya umeme wa mvuke.

Maabara ya siri ya utafiti wa siraha kubwa za nyuklia ingeweza kugundulika kwa haraka kama tu ingetumia umeme kutoka katika gridi ya taifa kwani wangekuwa na matumzi makubwa sana ya umeme hivyo wagetiliwa mashaka , lakini kama ni umeme unatokana na mvuke ingekuwa rahisi sana kwani ni wa kujitegemea.

Sauron alishngaa kuona Roma aliweza kufikira jambo la namna hio lakini upande wa Roma hakutaka kufikiria mara mbilimbili kwani aliweza kushuka moja kwa moja mpaka chini.

Eneo lote la Bavarian lilikuwa na utajiri wa kutisha ndio kitomvu cha utajiri wa taifa la Ujerumani , lakini licha ya kuwepo kwa viwanda vingi vinavyofanya kazi na maendeleo makubwa ya jiji lakini kulikuwepo na maeneo ambayo yalikuwa wazi , hususani yale ya migodi kama hio ya makaa ya mawe.

Roma mara tu baada ya kukanyaga chini na kukagua eneo hilo aliweza kutumia uwezo wake kukagua mazingira kutoka juu kwenda chini na hatimae aliweza kuona utofati wa eneo moja kuwa na muundo ambao ulikuwa ukitofautiana na baadhi ya migodi mingine na alijiambia huenda ikawa eneo ambalo alikuwa akitafuta.

****

Dakika kumi zilizopita lwenye maabara , alionekana Clark ambaye alikuwa amesimama kwenye kioo chenye uwezo mkubwa wa kuzuia mionzi akiangalia kwa umakini upande wa pili namna mkono wa Roboti ulivyokuwa ukifanya kazi kutoa majibu ya kikanuni ambayo umepewa maelekezo yake.

Mkono huo uliokuwa ukifanya kazi kiotomatiki ulikuwa ushafanikisha kudhalisha vitu viwili vyenye maumbo makubwa muundo wa risasi.

Jerry akiwa na macho ya furaha aliangalia matokeo hayo kwa tamaa huku muda wote akicheka cheka kama chizi.

“FURY hatimae upo mbele yangu , Profesa naamini unafuraha pia hii ni Masterpice ambayo itabadilisha kabisa ustaarabu wa dunia mzima wa kibinaadamu , hata miungu hawatoweza kuwa na nguvu ya kuhimili si ndio?”

“Sijawai kufikiria ingefika siku ningetengeeza kitu kama hichi , kama bado unanichukulia kama mwalimu wako fuata ushauri wangu , usije ukaitumia..”

“Haha..”Alicheka na muda uleule alibonyeza kitufe na kuruhusu zile Fury zilizokamilika kutoka katika eneo la matengenezo na kuingia upande mwingine kwa ajili ya matumizi.

“Usijali Profesa kama yule shetani atashuruti , bila shaka sitakuwa na haja ya kuitumia lakini kabla ya hapo lazima tutengeneze mtaji mkubwa ambao hata siku tukisema tuiharibu dunia inawezekana , kwasasa wafadhili wa hii projekti wanasubiri “

“Ijapokuwa sijui nani yupo nyuma yako na ni taasisi ipi lakini nguvu ya FURY haiwezi kuogozwa na binadamu , nakwambia utajutia hili”Aliongea kwa kujaribu kumbembeleza.

“Profesa au hapana kwanzia sasa nitakuita Clark , mimi nido napaswa kukushauri kuanzia sasa hivyo acha maigizo , wewe na mimi ni sawa tu , sisi wote ni watu ambao tunatumia juhudi kubwa kaika kufanya tafiti bila kujali athari zake na mwisho wa safari yetu ni pale ambapo tutapita vizingiti vyote alivyowekewa binadamu na kujua nini maana ya msingi wa ulimwengu , kama hukuwa na mpango wa kutengeneza FURY na kuvuka mipaka ya kibinadamu katika siraha za nyuklia basi usingethubutu hata kufikiria hii tafiti , wewe si ulisoma maswala ya tiba kwanini ukajiunga na maswala ya tafiti za siraha , Hawa binadamu wote ni wapuuzi kwako na unawachukulia kama vifaa vya majaribio , hawana utofauti na panya wa maabara waliofngiwa kusubiria wakati muafaka kufanyiwa majaribio kwani hakuna utofauti , kama hukutegneneza Fury kwa ajili ya kuharibu dunia nina uhakika ulikuwa ukisubiria madhara yake, Au nakosea Clark?”



“Sijatarajia utanifikiria mimi hivyo , nilisoma maswala ya tiba kwa ajili ya mwanaume ninampenda kuondokana na maumivu na nilitengeneza Fury nikiwa na matarajio kwamba itasaidia binadamu kuweza kutumia nishati kwa kiwango kikubwa zaidi ya ilivyosasa kupitia teknolojia iliopo lakini licha ya hivyo niliishia njiani kwasababu niliogopa kama itatumiwa na taifa kutengenezea siraha , upo sahihi maisha yangu yote yatakuwa ni kufanya tafiti lakini sio hapo tu , kuna vitu vingi katika dunia hii ambavyo vinahitaji hasira zetu lakini hatupaswi kuwa watumwa wa hasira na chuki”

“Acha kuongea upumbavu wako , usijifanye wewe ndio mtakatifu, unaweza kuwa mwalimu wangu lakini sasa wewe ni mateka wangu na mimi ndio master wako”Aliongea na palepale alimsogelea Clark na kisha akakikumbatia kiuno chake na Clark kwasababu alikuwa amengalia upande wa mbele yake hakuweza kutegemea kitendo kile kutoka kwa Jerry aliekuwa nyuma yake.

“Jerry unataka kufanya nini?”Aliongea huku akijitoa kwake.

“Unaiuliza tena , huu ni muda sasa wa kurelax baada ya kumaliza kazi yangu nzito , kwanini nisifurahie uzuri wako, itakuwa hasara kumuacha mtu mwingine”

“Wewe, mimi ni mwalimu wako uthithubutu”

“Acha ujinga , sijali wewe ni nani , kwanza kabisa wewe ni mdogo kwangu kwa miaka miatu , unafikiri nitakuabudu kwasababu tu ulikuwa mwalimu wangu na uwezo wako ni mkubwa , sahau katika kichwa chako na kwanzia sasa hivi hakuna kitu kinachoitwa mwalimu na mwanafunzi, hapa ni mwanaume na msichana ambaye anajiandaa kuwa mwanamke”Aliongea huku akimsogelea tena.

Clark alikuwa na uwezo wa kumdhibiti Jerry kwa wakati huo kwani alikua yupo peke yake katka hilo eneo kwasababu ya kuwa na mafunzo ya kujilinda lakini alisita kufanya hivyo..

Upande wa Jerry mara baada ya kuona Clark anakwenda kuleta ugumu palepale alichomoa bastora na kumnyooshea Clark.

“Samahani najua kabisa wewe ni mgumu hivyo niliandaa kabisa bunduki , kukwambia tu ukweli nje ya hii maabara kuna walinzi kibao wanalinda na hauwezi kutoroka”Aliongea na kumfanya Clark kukunja ngumi yake na kung’ata lipsi kwa wakati mmoja .

“Unaota nini , vua nguo haraka , nina sehemu ya kwenda pia kuonyesha mafanikio kwa wakubwa zangu, nimeisubiri hii siku kwa zaidi ya miaka mitatu kufanya mapenzi na wewe na hatimae leo ninapata nilichokuwa nikipania sana , hivyo naomba unirhuhsu nifurahi kistaarabu kabisa..”

“Nipige risasi kama una ujasiri huo”Aliongea Clark akiwa katika ukauzu.

“Kama unakitaka kifo utakipata lakini kama hutotoa ushirikiano basi wale watoto ndani ya kanisa la Santa Maria nitawaua kwa bomu tena nikuambie nitaenda mbali kuharibu shule ambayo umewekeza”

“Ushetani””

“Ndio ujue sasa mimi ni shetani , hivyo vua haraka”Aliongea na kumfanya Clark amwangalie kwa huzuni kubwa na palepale aliingiza mkono wake katika mfuko wa koti na kutoa kijichupa kidogo na kupeleka mdomoni na kuonekana alikuwa akinywa kimiminika.

“Unafanya nini?”Aliongea Jerry kwa mshangao na kumfanya Clark kucheka kwa dharau.

“Wewe huoni , ni kheri nife kuliko kuruhusu shetani kama wewe kuunajisi mwili wangu , kama hutojali mwili wenye sumu na wa baridi unaweza kunitumia utakavyo..”Aliongea na muda uleule sura ya Clark ilianza kubadilika na kupauka na alianza kuhema kwa shida na palepale alikosa mhimili na kudondoka chini huku povu likianza kumtoka mdomoni na palepale macho yake yaliongezeka ukubwa.

“Wewe umewezaje kupata sumu..”Aliongea kwa kutetemeka akiwa haamini.

Muda huo huo ndio aliweza kukumbuka kauli yake masaa kadhaa yaliopita kwamba anajaribu kuangalia usafi wa elementi.

Wakati ule hakuwa akielewa ni mchanganyo gani wa kemikali aliokuwa akitengeneza , lakini sasa anajua kumbe ilikuwa ni simu aliokuwa akitengeneza.

Baada ya kuona kwamba mwanamke huyu alimdaganya jana na kujitengenezea sumu alijikuta hasira zikimvaa na alimsogelea kwa kasi na kumpiga teke tumboni na kumfanya Clark kudhidi kutapatapa akielekea kupoteza maisha.

“Mh hata hivyo sina tamaa kihiivyo ya mwili wako , lakini siwezi kukuacha ukafia hapa ndani , tutakutoa na kufanya wanyama wakali wa msituni kukufanya chakula , itashangaza baade ikija kugundulika mwanamke mwenye busara kama wewe umejiua na sumu”Aliongea na baada ya kumaliza hakujali tena na alirudisha siraha yake kibindoni na kugeuka ili kuondoka hilo eneo.

BOOM!

Wakati akiwa anajiandaa kutoka alijikuta akisimama na kufunga masikio yake baada ya mlango wa kuingilia kudondoka chini kwa kuonyesha kwamba umepigwa na nguvu isiokuwa ya kawaida.

Na mpaka akili yake inamkaa sawa na kuamsha kichwa kuangalia knachoendelea , alijikuta akiachama mara baada ya kuona sura ya mtu ambaye hakuitarajia kuiona hapo ndani , alikuwa ni Roma.

ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 570.

Jerry alidhani alikuwa akiota , mlango huo ulikuwa ni wa chuma kigumu sana , imewezekanaje ukabobolewa kirahisi namna hio.

Muda huo ni shoti pekee za umeme ambazo zilikuwa zikisikika ndani ya eneo hilo na Roma wala hakujali kabisa aliingia kama vile ni mnyama.

Nyuma yake kulikuwepo na damu nyingi ambazo zilikuwa zimetengeneza mfereji mkubwa wa damu kuingia ndani mara baada ya mlango kuvunjika.

Zilikwa ni damu za walinzi ambao walikuwa walilinda katika hilo eneo na ilionekana dhahiri kabisa Roma aliwapasua pasua viungo vyao pasipo huruma.

Roma mara baada ya kugundua eneo ni lenyewe , alitolea hasira zake zote za kutafuta usiku kucha kwa walinzi hao na aliwaua vifo vibaya sana, huenda ni aina ya vifo ambavyo havijawahi kutekelezwa hapa duniani , vilikuwa ni vya ukatili wa hali ya juu sana.

“Clark!!”Aliita mara baada ya kumuona Clark aliekuwa yupo chini sakafutni akitetema kama mgonjwa mwenye kifafa na palepale alimkimbilia na kumkalisha.

“Nini kimetokea ?Umepewa sumu?”Aliuliza Roma kwa wasiwasi mkubwa na hakuacha kujaribu kumchunguza kwa kumuingizia nguvu za kimaandiko.

“I… I knew it ..you.. would save me ..just like ten years ago..”Aliongea kwa tabu sana akisema kwamba alijua tu atakuja kumuokoa kama miaka kumi iliopita.

Roma macho yake yalianza kuwa mekundu hakuwa na uwezo wa kujua ni aina gani ya sumu ambayo ipo kwenye mwili wa Clark , alikuwa na uwezo wa kuhisia sumu iliokuwa kwenye mwili wake ilikuwa ikinyong’onyesha saa utendaji kazi wa mwili.

Lakini alishindwa kumponyesha kwani sumu iliokuwa kwenye mwili wake iliionekana tayari ishaingia kwenye mfumo wa damu moja kwa moja na wakati akiwa amemshikilia palepale alitema damu nyingi nje mara baada ya Roma kujaribu kumponyesha.

“Ni sumu ya aina gani hii , niambie namna ya kukuponyesha”Aliongea Roma akijaribu kumtingisha lakini Clark aliishia kutingisha kichwa chake akimuonyesha ishara kwamba hakuna namna ya kumponyesha.

“Ni sumu ambayo niliiandaa dakika ya mwisho kabisa na ili kuhakikisha hawawezi kuniponyesha nilitumia mbinu ya kipekee ambayo inafanya viungo vya mwili kutofanya kazi sawasawa .. kwasasa haiwezekani kitu”Aliongea kwa tabu na kumfanya Roma palepale kumgeukia Jerry ambaye alikuwa amemsahau kwa muda.

“Wewe mnyama , yote haya ni kwasababu yako , kama utafanikisha kumponyesha mwalimu wako nitakuua lakini mwili wako sitouharibu”Aliongea Roma kimkwara huku akisambaza msisimko wa hali ya juu wa nguvu za kijini ili kumuogopesha Jerry.

Muda huo Jerry alikuwa ameshikwa na ubaridi wa aina yake hasa baada ya kuona damu nyingi zikiingia ndani kutokea nje , lakini licha ya hivyo chuki yake zidi ya Roma ziliifunika hofu yake na kaunza kucheka kama kichaa.

“Wewe shetani ijapokuwa sijui namna ulivyoipata hii sehemu lakini nakuambia hivi hakuna namna ya kumuokoa , sumu ambayo Clark ametengeneza anaweza kutengenza dawa yeye mwenyewe , inatia huruma kwamba anakufa kwenye mikono yako ukiwa huwezi kumsaidia “

“Unakiomba kifo wewe..”Aliongea Roma huku akitaka kumshambulia lakini Jerry alimzuia kwa kumpigia makelele.

“Usinisogelee, ukinigusa tu hii maabara yote italipuka na zile FURY mbili zitalipuka, madhara hayatakuwa kwako tu lakini kwa ukanda wote wa eneo la Bavaria, Ujerumani yote itageuka na kuwa toharani ya dunia, Je upo tayari kutoa kafara mamilioni ya watu kwa ajili ya kuniua mimi?”Aliongea na kumfanya Roma kunasa neno FURY.

“FURY siraha aliotaja je ndio sababu ambayo imewafanya wakuteke?”Alimuuliza Clark.

“Ndio .. niliipatia jila hilo ikimaanisha neno kisasi”Aliongea .

“Inahusiana na nini?”

“Ni aina ya siraha ya nyuklia ambayo teknolojia yake imeboreshwa zaidi … risasi yake moja ni sawa na risasi mia tano za bomu la Hydrojeni”

“Nini..!!”

Roma alishangaa kwa uhatari wa siraha hio , kama kweli risasi moja ni sawa na risasi mia tano za bomu la Hyrdrojeni si ni hatari hio , maana kama siraha hio ikatumika basi mionzi yake isingeathiri tu Ujerumani huenda na nchi za karibu.

Alijiuliza inakuwaje watu wa North Buyeo na kundi la kigaidi kutafuta teknolojia ya namna hio, ni kipi ambacho wanalenga?.

“Hehe.. sasa nadhani tayari ushajua ukuu wake, ninataka kuona kama utathubutu kuniua …Wewe shetani utapata maumivu makubwa sana baada ya mwanamke unaempenda akifa mbele yako …Hahaa, nimesubiria hii sku kwa muda mrefu sana , na unastahili kwa kila kitu , unapaswa kwenda jehanamu”Aliongea kwa hasira .

Roma alikuwa katika kiwango cha juu cha hasira na alitamani kumfanya kitu kibaya , lakini hakuweza kuthubutu kufanya maamuzi ya haraka kwani maisha ya watu zaidi ya mamilioni yalikuwa hatarini.

“Nini tatizo , Umekosa ujasiri tena?, Umejileta mwenyewe hata hivyo , ninakwenda kulipiza kisasi cha vifo vya familia yangu , baba yangu , mama yangu na dada yangu ambaye alikuwa na miaka mitatu tu”

“Kisasi? Ni kipi nimekufanyia mpaka kutaka kulipiza kisasi?”

“Bila shaka hukumbuki , umeua watu wengi sana unawezaje kuwakumbuka wote , umesahau ulichokifanya miaka mitano iliopita pale Simbokrog nchini Belarus kwenye kijiji cha Wozic si ndio?”

“Kijiji cha Wozic ?”Aliongea Roma huku akikunja sura , hakuwa akikumbuka kabisa kama kuna sehem kama hio na isitoshe kulikuwa na maeneo mengi madogo madogo aliopita ambayo hakuyakumbuka na kote hhuko huenda aliua.

“Unaonekana hukumbuki , Kijiji chetu kilikuwa na watu 186, kati yao therathini walikuwa ni watoto na wakati huo ni mimi pekee ambaye sikuwepo nyumbani kutokana na kwamba nilienda shuleni kwenye mji mwingine wa pembeni , lakini wewe ukaja na kufyeka kila mtu uliemkuta kijijini bila kujali wana hatia au hawana kwasababu tu adui yako alikuja kwenye kijiji chetu , kwanini usingeacha hata maisha ya watoto wadogo ambao walikuwa hawana hatia , kwanini ulivyomaliza ukawachoma na moto…”Aliongea Jerry kwa hasira kubwa na kauli yake ilimfanya Roma sasa kukumbuka lakini hakuwa akikimbuka vizuri sana , kipindi anafanya hivyo alikuwa katika hali ya ukichaa na ugonjwa wake ulikuwa ndio unaitawala akili yake.

Alikumbuka kabisa kitendo cha kuua watu wa kijiji kile ndio kilichosababisha Seventeen kumkimbia na mwisho wa siku akaingia kwenye mikono ya maadui na kumuua akiwa na ujauzito tumboni mbele ya macho yake.

Roma alishindwa kujizuia kusikia uchungu kutokana na maelezo ya Jerry , haikujalisha alikuwa akitamani kuwa na maisha ya amani , lakini mambo ambayo ameyafanya miaka iliopita yalimfanya kutengeneza maadui wengi ambao muda wowote watataka kulipza kisasi na aliona hata kwa Jerry ni mwanzo tu.

Lakini licha ya hayo yote , kipindi hicho akili yake ni kama ilikuwa ikiendeshwa kwa rimoti , ugonjwa wake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba alikuwa ni kama shetani na bila kumwaga damu kwa siku hakuweza kutulia.

“Naona sasa unakumbuka ..?”Aliongea Jeryy huku akifuta machozi .

“Unapaswa kuadhibiwa pia , mwanzoni wakubwa waliniahidi watanisaidai katika kulipiza kisasi , na nikaamua kuishi na chuki na kuvumilia mpaka leo hii , lakini kwa leo kwasababu umepajua hapa sina mpango wa kuondoka hapa nikiwa hai”

“Unapanga kufanya nini , je unafikiri kulipua hilo bomu la FURY na kuniua kutakufanya ulipize kisasi cha ndugu zako , sahau kabisa hizo ni ndoto za kufikirika utaua watu wengi kuliko mimi”

“Inanihusu nini , ni matendo yako ya kishetani ndiio ambayo yamenifanya kuwa katika hali hii , usijaribu kunidanganya, hata kaam nitaondoka leo utanitafuta na kuniua , ni kheri niende na mamia ya watu katika kaburi langu , maisha ya hawa watu yatakuwa yametolewa kafara kwa sababu yako hahahaa..”

Baaada ya kuongea huku akicheka kwa kejeli palepale alisogea upande wa kulia wa kile kioo cha kuzuia mionzi na kukipiga ngumi kwa nguvu kubwa.

“Twiii , Twi, Twiit”

Ilionekana ndio namna maabara ilivyotengenezwa ili kuilipua njia ya mkato ya kuwasha bomu ni kupiga ngumi kioo na hicho ndio ambacho kilikuwa kikienda kutokea , hata hivyo maabara nyingi za kufanya majaribio ya siraha hutegeshewa bomu la kuiharibu kabisa pale panapotokea tatizo.

Muda uleule alivyoopiga ngumi kile kioo sauti kutoka kwenye tarakishi humo ndani ilisikika ikiwatahadharisha.

“Destruction Mode has been turned on , the labaratory will be exploding after the countdown , thirty .. twenty nine…”

“Ni mwisho haha , hatimae imekuwa mwisho”Aliongea Jeryy.

Roma alishangaa , hakutaka kumuua Jerry kwasababbu aliogopa siraha hio ya FURY ingelipuka , lakini sasa hivi maabara yote inakwenda kulipika , ilikuwa haiwezekani kwa yeye kuzuia kutokulipuka kwa bomu hilo la nyuklia.

Roma aligeuza macho yake na kumwangalia Clark aiekuwa kwenye mikono yake ambaye afya yake inaelekea ukingoni alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira

Baada ya kuona hana uwezo wa kuzuia mlipuko wa maabara hio pamoja na mlipuko wa FURY kitu pekee ambacho aliona angeweza kufanya ni kujiuoko yeye na Clark kuondoka katika hilo eneo.

Kufumba na kufumbua alikuwa ashatoka nae na kwenda kutua mbali kabisa na eneo hilo katika mlima na msitu usiokaliwa na watu, Kusini mwa nchi ya Austria.

Alikadiria kwa umbali huo hata kama bomu hilo la nyuklia litalipuka upande wa Ujerumani halitowaathiri kwa muda kupitia mionzi yake.

Baada ya kutafuta sehemu yenye majani makavu aliamua kumuweka Clark chini na kuanza kumfanyia uchunguzi wa mwili wake.

Haikuleta maana kwake kuomba msaada kwa muda huo , kwani aliona asingepata msaada huo ndani ya muda , hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujaribu kufamnya ni kumpontysha yeye.

Mapigo ya moyo ya Clark yalikua ya chini mno na yalikuwa yakiendelea kuwa ya chini na muda wowote yangeacha kabisa kudunda na kupelekea kifo chake.

Roma alijikuta akijikatia tamaa mara baada ya kumungizia nishati ya mbingu na Ardhi kwa kuunganisha na ya Urejesho lakini bado alishindwa kumponyesha.

Mwili wake ulikuwa ni kama vile seli zake zinaoza ndani kwa ndani na hiko ndio kilichomuogopesha zaidi , kwani aliona dakika yoyote Clark angeweza kufa kwenye mikono yake maana tayari alishaanza kuwa wa baridi.

“Damn it … Clark , jarobu hata kuongea kidogo , ninaweza vipi kukuokoa?”Roma ujasiri wake wote ulimwishia na aliishia kuukumbatia mwili wa Clark huku akishindwa kuzuia machozi yaliochanganyika na hofu.

Ni mwanamke huyo ambaye hakulala usiku na mchana kwa ajili tu ya kumtengenezea dawa, na katika kipindi chote ambacho alihisi kuwa mpweke ni yeye pekee ambaye alifanya kila liwezekanalo kumsaidai , lakini sasa mwanamke huyo anafia kwenye mikono yake bila ya kuwa na msaada kwake.

Aliogopa kwamba bado hakuwa amelipa fadhila zake zote kwa yale aliomfanyia , alijilaumu na kuona yatakuwa makosa yake kuruhusu akifariki kwenye mikono yake kwani itamaanisha kwamba alishindwa kumlinda na maadui ambao aliwatengeneza yeye mwenyewe.

Clark alijitahidi kuamsha kinyonge sana mkono wake akimfuta machozi roma ,Roma hakujua hata alikuwa akilia alihisi maji yanaririka katika mashavu yake , lakini hakujua kama ni machozi yake .

“Ni sawa … wewe .. usilie tena .. nina furaha , mtu wa mwisho ninaemuona .. ni wewe”Aliongea Clark kwa kukata kata maneno.

Alishindwa kujizuia zaidi na zaidi mara baada ya mwanamke huyo kuongea kauli hio na alizidi kutoa machozi na kulia kwa kwikwi.

“Huwezi kuondoka hivi … utakuwa umenikatili sana ,,,, siwezi kujisamehe tena , umeniokoa mara nyingi sana na umefanya mambo mengi kwa ajili yangu ,, lakini mimi nashindwa kukukoa ,, sina thamani kabisa kwako , mimi ni mjinga”Aliongea huku akiinua mkono wake na kujipiga kibao kwa nguvu na kutokana kutumia nguvu za kijini ilisababisha mpaka majani ya miti kuanza kudondoka lakini bado aliendelea kujipiga vibao mara nyingi zaidi na kumfanya Clark azidi kutoa machozi ya kumuonea huruma na huzuni kwa wakati mmoja.

“Usi.. usi , fanye hivyo”Alijitahidi kuongea.

“Clark naomba usife , naomba usife tafadhari , siwezi kufikiria nitakuwa na maisha ya namna gani ukishaniach…”Alianza kulia kama mtoto huku akimwangalia mwanamke huyo kwa kuomba.

“Na.. naomba,, nikuulize swali na unijibu kabla sijafa?”

“Niulize chochote na nitakujibu”Aliongea haraka haraka.

“Roma … nataka tu .. kujua kama .., je .. unanipenda?”

“Ndio , Nakupenda , siku zote nilikuwa nikikupenda sana ,… wewe ni moja wapo ya wanawake ninaowapenda sana..”Roma aliongea bila kujiuma uma , hayo ni maneno ambayo hakupanga kumwambia mwanamke huyo katika maisha yake.

Zamani hakutaka kabisa kumsogelea mwanamke huyo kutokana na madhambi ya umwagaji damu alioyafanya, lakini baada ya kurudi Tanzania na kujipatia mke ndio kabisa hakutaka kumfanya mwanamke huyo mchepuko kwa kuamini alistahili kitu kikubwa zaidi.

Roma hakuwa na mashaka kabisa juu ya mapenzi yake kwa Clark, ni mapenzi ambayo hayakuanza jana wala leo , ni tokea alivyokuwa mdogo na kadri mrembo huyo alivyokuwa anakuwa alizidi kumpenda.

Mapenzi yake kwa mwanamke huyo yalikuwa sio ya kawaida ambayo yanaweza kueleweka kirahisi kwa binadamu.

Pengine katika dunia kuna wanawake wengi ambao aliwapenda na wao pia kumpenda na kumpa kila kitu na yeye kufanya kila kitu kushinda magumu yote kwa ajili yao lakini mapenzi yake ya kweli katika kumbukumbu zake yapo kwa Seventeen na katika uhalisia yapo kwa Edna na mpenzi anaemuona kama ndoto ni Clark.

“Kweli!?”Aliuliza Clark akiwa kama haamini na alijitahidi kufumbua macho yake ..

“Ni kweli , nilichokwisha kukisema ni ukweli , na unapaswa kuniamini , sijawahi kukuweka wazi kwasababu tu niliona hustahili kuwa na mtu kama mimi , … samahani sikukuambia hili mapema”Macho ya Clark yalionyesha kabisa kufurahishwa na kauli yake na tabasamu la furaha lilifunika uso wake .

“Honey … I knew it , you loved me..”Aliongea.

Roma alikuwa akilia hivyo hakuwa akiongea zaidi ya kutingisha kichwa tu kumwaminisha ni namna gani anamkubali huyo mwanamke.

Clark alipanua mdomo wake huku akiinamisha kichwa chini na alionekana kama anataka kung’ata kitu flani..”

Roma aliweza kuona lakini hakujua Clark anataka kufanya nini na alimwangalia kwa kuchanganikiwa.

“Collar …”Aliongea Clark kwa sauti dhaifu akimaanisha Kola ya koti lake.

Roma palepale alielewa sasa anataka kung’ata nini na alifanya haraka na kumsaidia kumpelekea karibu Kola ya koti ili kuweza kugusanisha na lipsi zake.

“Clark unafanya nini, kwanini unamg’ata Kola ya koti, ni kwa ajili ya nini?”Aliuliza lakini Clark hakuongea neno na muda huo alikuwa kama mtoto anaetafuna nguo kwani alifyonza kwa nguvu ule ukola wa koti mpaka ukaanza kujaa mate.

Ni muda huo huo aliweza kuona Ukola ule wa shati ukibadilika rangi na kuwa wa bluu ambayo haijakolea sana na kama sio kwa kuloana basi isingetokea

Wakati akishangaa palepale aliweza kushangaa mara baada ya Clark kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha baada ya kuonekana kumaliza alichokuwa akifanya na kadri dakika zilivyokuwa zikisogea ndio ambavyo alizidi kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Unashangaa nini mpenzi? , sijafufuka ni kwamba tu sijafa”Aliongea huku akitabasamu.

“Wewe , umewezaje kufanya hivyo.. nini..?”

“Unataka kuuliza nimewezaje kurudi katika hali ya kawaida si ndio , basi ni kwasababu nimejiponyesha mwenyewe”Aliongea huku akijaribu kukusanya nguvu na kukaa mwenyewe chini.

Roma aliangalia ile Kola ya koti kwa mara nyingine jinsi ilivyokuwa na doa la rangi ya bluu na kisha akamgeukia Clark aliekuwa na uso wa furaha .

“Ulinidanganya?”

“Nani kakuambia udanganyike kizembe , mimi ni nani , mimi ni Profesa Clark, mwalimu wa mwanafunzi mjinga kama Jerry , hivi unadhani naweza kuzidiwa akili na mwanafunzi niliemfundisha mimi?”

Roma alikosa cha kusema, alimwangalia mwanamke huyo namna ambavyo aliweza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa haraka sana na alijikuta akichoka kabisa na kujikalia chini.

“Huu ulikuwa ni mpango wako?”Aliuliza Roma.

“Ndio , hivi unafikiri ungeweza kunipata kwa kubahatisha , wakati nilipokuwa nikitumia tarakishi zao nilituma Link kwa siri katika satilaiti yenu , kama mwalimu nilimjua Jerry hakuwa vizuri kwenye maswala ya Compyuta hivyo hakuweza kujua ninachokifanya kabisa , nilijua tu kama mtafika maeneo ya karibu na nilipo basi mngehisi mawasiliano ni kama yameingiliwa kutoka ndani”Aliongea na kumfanya Roma asipinge kwani ndio alivyoweza kumpata.

“Kama ni hivyo vipi kuhusu Sumu ni nini kile?”

“Ile ni sumu kweli , niliweza kuchanganya aina mpya ya sumu nilioitengeneza pale, ni sumu ambayo inavilegeza viungo vya mwili na kukufanya uonekakane kama umekufa na kama hutachukua dawa yake basi utakuwa wa baridi kwa masaa ishirini na nne na ikiisha makali yake mwili utarudiwa na joto lake na utaweza kuamka , nilipanga kama wataniona nimekufa watatafuta sehemu ya kunizika au kunipatia matibabu na ndio nitajua namna ya kutoroka ,lakini hio ilikuwa ni mpango wangu wa mwisho kabisa kwani sikuwa na uhakika kama hawatachoma mwili wangu lakini nilipanga kama hakuna ambae atakuja kuniokoa basi moja kwa moja nitadanganya nimekufa ili kuepuka wasinidhuru, lakini bahati nzuri umeweza kuja ndani ya muda hivyo nikatumia mpango B”Aliongea na kisha akashika Kola ya koti lake.

“Nililoanisha hii Kola na dawa maalumu ya sumu ,ilihitajika tu mimi kunyonya na ndani ya lisaa limoja ninarudi kuwa sawa tena”

“Kama ni hivyo kwanini ulinichezea hila hata mimi , hivi ulijua ni kwa kiasi gani moyo wangu uliuma?”Aliongea Roma huku akisimama na palepale mrembo huyo alisimama na kupitisha mikono yake yote mwili katika shingo ya Roma na kumbusu kwenye paji la uso..

“Kama nisingetumia fursa hii , usingeweza kuniambia nilichotoka kusikia kutoka kwako kwa muda mrefu”Aliongea na wakati Roma anataka kuongea neno alizuiwa na lipsi laini za mwanamke huyo.

Baada ya busu jepesi , Clark alionyesha uso wa kuomba huku macho yake yakionyesha hali ya kutia huruma.

“Honey usinikasirikie , nilitaka tu kuwa na wewe kama mpenzi wako , nilijua kama hutoniambia nitakuwa na huzuni milele”

Roma alijiambia ile siku ambayo alikuwa akiiepuka kwa miaka mingi hatimae imewadia na hakujua anakwenda vipi kumwelezea mke wake kwa maneno marahisi na kumuelewa.

“Umeandaa mpango wako , ili kunifanya niingie katika mtego na ukanifanya nilie kama mtoto , aisee inatia aibu Daah”Aliongea Roma huku akitabasamu kwa uchungu na kumfanya Clark amwangalie kwa macho ya utani huku akimtolea ulimi nje kama anamcheka.

“Nilikuwa nikienda na hali inavyoruhusu , Jerry alinitishia kwenda kuwaua wale watoto wsio na hatia , sikuwa na chaguo lingine..”Baada ya kusikia hivyo alijikuta akikumbuka kitu alichosahau.

“Oh nimesahau kuhusu FURY Ujerumani ndio kwaheri”Aliongea.

“Haha.. nilikuambia kila kitu nilipanga mimi , unadhani ninaweza kutengeneza kitu hatari namna hio”

“Kwahio ulichotengeneza ni nini , ni feki pia?”

“Hebu fikiria , unadhani ninaweza kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu kwasababu ya watoto , hata kama niwe kwenye hali gani siwezi kwenda mbali kiasi hivyo , teknolojia ya FURY kwasasa ipo katika nadharia tu , inawezekana vipi kuitengeneza ndani ya siku mbili au moja? , kutengeneza tu elementi ya mwisho inayokamilisha kanuni inahitajika mchanganyo wa kikemia ambao unaweza kuchukua mwaka mzima kutoa matokeo”

“Kwahio unasema sasa hivi Jerry atakuwa na hasira sana mara baada ya kuona umemdanganya?”

“Labdal , Ujerumani naamini watashughulika na tatizo hilo , kwasasa ninafuraha ya nilichoweza kutimiza baada ya muda mrefu , Roma naomba unibusu japo kidogo tu”

“Nini!”

“Umesema unanipenda hivyo unapaswa kunifidia kwa miaka yote nilioteseka kwa ajili yako”Baada ya kuongea alifumba macho na kunyanyua kichwa chake juu kuweka mdomo vizuri ubusiwe.

Roma aliangalia Lips zake zilizokuwa nyekundu kutokana na weupe wake wa kizungu na kisha palepale alitoa tabasamu la kifedhuli na kumshika kiuno kisha akamvutia kwake.

Clark mpaka hapo alijua kabisa alikuwa amefanya kosa kwa kujirahisisha mbele ya mwanaume ambaye alikuwa kama Simba mwenye njaa.

Dakika moja mbele wote walikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa ulioitwa Busu, inasemekana wazungu wapo vizuri sana kwenye Kubusu na hicho ndio kilichompagawisha Roma.

MWISHO WA SEASON YA 19



SEHEMU YA 571.

Katika jiji la Palermo giza tayari lilikuwa lishatawala na katika uwanja wa kivita uliokuwa ukifanyia mashindano , ulikuwa mtupu kwa wakati huo ikimaanisha kwamba mashindano kwa siku hio yamesha mpaka siku inayofuata.

Katika siku hio ya kwanza hakukua na maajabu makubwa kwani wale wanajeshi kutoka mashindano yaliopita wote kwa pamoja wameweza kuingia raundi inayofuata na kwa wale wahudhuriaji wenyewe wanasema mapigano yenyewe yanaanza siku inayofuata katika raundi ya pili.

Katika Moja ya Balkonni ya hoteli ya Cassano , mwanaume wa makamo mzungu alievalia mavazi ya upishi meupe alionekana akiwa bize kucharanga samaki aina ya Salmoni kwa haraka sana na kwa ufanisi mkubwa.

Kila kipande cha samaki kilikuwa kikilingana na kingine ni hivyo tu kwamba vilikuwa na ukubwa kidogo ambao unamuwezesha mlaji kutafuna kipande kimoja chote kwa wakati mmoja.

Mbali kidogo na alipokuwa anafanyia kazi mwanaume huyo kulikuwa na meza kubwa ambayo wahudumu wawili walionekana wakiwa bize kumsaidia kuhudumia kila anachokamilisha kupika na kuweka mezani.

Katika meza Christen alinyanyua Glasi yake ya Champagne na kumnyooshea Rose kugonga zao Cheers ambaye alikuwa karibu yake.

“Aphrodite, unaonekana kutokuwa kabisa na wasiwasi , vipi kuhusu hiko kinywaji?”Ares ambaye alikuwa ameegamia kwenye kiti kivivu aliongea kwa kuonyesha sura ya dhihaka.

“Wasiwasi wa nini , nipo hapa kwa ajili ya burudani sio kuteseka”Baada ya kusema hivyo alimgeukia Poseidon ambaye alikuwa akikomaa na upishi.

“Poseidon vipi hiko chakula bado tu? Nina njaa mimi”

“Hakuna mtu kugusa chakula kabla sijamaliza ,atakae fanya hivyo nitahakikisha hali chakula nilichopika mimi”

Upande wa Magdalena aliekuwa kimya alikuwa kwenye mshangao , bila shaka alikuwa akimjua Poseiodon ni mpishi maarufu duniani aliefahamika kwa jina la Mr Kelphin lakini hakuwahi kuwaza mtu huyo huyo kuwa mwanajeshi wa jeshi la Marekani upande wa majini.

“Christen kuna haja gani ya kusubiria amalize kila kitu , kwanini tusianze kula?”Aliuliza Magdalena ambaye alikuwa na njaa.

“Ndio sheria ya Poseidon hio kama atajitolea kupika chakula basi hataki mtu akiguse mpaka aridhike kimekamilika , anajali sana mlo kamilifu kuliko kitu kingine chochote”

“Kwa maneno marahisi Miss Magdalena ni kwamba bwana huyo ni mpishi Mbishi sana kwahi kutokea”Aliongezea Stern na Rose na Magdalena waliishia kushangaa tu.

Dakika chache mbele Poseidon aliweza kukamilisha sahani za Sashimi na kuwekwa kwenye meza hio kubwa , katika meza hio kilichoonekana ni aina mbalimbali ya vitoweo vya baharini ambavyo vimepikwa katika ubora wa hali ya juu.

Na kabla ya kuwaruhusu kula aliwaambia wasiguse kwanza chakula chake mpaka apige Selfie na palepale alitoa simu yake ya I Phone Toleo la juu na kupiga picha mbalimbali ya chakula chake na kisha kupost mtandaoni kwenye akaunti yakeiliokuwa ikifuatiliwa na watu zaidi ya milioni.

Baada ya kutaniwa na ndugu zake kutoka sayari nyingine , hatimae aliweza kukaa sasa na kuwaambia wale wahudumu waondoke.

Ukweli Magdalena na Rose walipata fursa ya kushiriki kwasababu ya heshima ya Roma pekee , lakini chakula hicho cha usiku ni kama vile kimeandaliwa kwa ajili ya ndugu hao ambao ni mara chache sana hukusanyika pamoja kama hivyo.

“Hermes tayari upo ndani ya hoteli , kwanini usivue hilo lisuti lako , huoni kwamba ni wewe tu hapa ulievaa suti na joto lote hili?”Aliongea Christen huku akimwangalia Raphaeli aliekuwa amekaa pembeni yake.

“Kuwa na amani sisi Vampire miili yetu ni ya baridi”

“Mwacheni nani anajali kama anahisi baridi au Joto , kwanza unaweza kunywa damu na ukaishi , kuna haja gani ya kula na sisi?”

“It’s recognition to Poseidon ‘s Culinary arts”Alijibu.

“Haina haja , chakula changu kipo Perfect”Aliongea Poseidon akijigamba.

Rose na Magdalena waliishia kuangaliana pasipo kuongea chochote , na walijiambia Poseidon na yeye ni kama Roma tu hana aibu kabisa kwa matendo yake.

Chakula kilichokuwa mbele ya Ares kilipotea kwa haraka sana na baada ya kumaliza kila kitu alisimama na kuelekea upande wa Balkoni.

“Ares unaenda wapi?”Aliuliza Stern.

“Hilo nalo ni swali gani?”

“Sio muda sahihi wa kuwatafuta, au unadhania unaweza kuwashinda?”

“Sina muda wa kupoteza kula na nyie mpaka usiku wa manane mimi wala sitamani kuangalia mapigano ya kibinadamu ya Caesar Conference nipo hapa kwa ajili ya kupigana nao”

“Hey Bro unataka kuzaliwa upya katika mwili mwingine labda?”

“So what , nevet try never know , I am not interested in their conspiracies , I dare to go if you don’t”(“Kwani vipi , usipo jaribu huwezi kujua , sina matamanio ya uzushi wao , ninathubutu kwenda kama wewe huwezi”Aliongea na kumfanya Stern na Alcie kukunja sura zao kutokana na ukichaa wa Ares.

Muda huo huo Rose na Magdalena waliweza kuhisi msisimko maalumu ambayo ni kama vile ni mawasiliano yao na Roma na walijikuta wote wakiangalia upande wa nje na waliweza kumuona Roma akiwasogelea kwa kasi na walijikuta wakiwa na furaha.

Kufumba na kufumbua Roma aliweza kutua katika Balkoni huku akiwa na tabasamu pana.

“The Annoying Hades , you finally came back , we thought you run away in fear”Aliongea Christen akimtania kama walidhania amekimbia kutokana na uoga.

Roma aliangalia kila mmoja aliekuwepo na alionekana kuridhika kupitia macho yake.

“Naona kila mmoja ameweza kufika , hakuna chochote kilichotokea wakati nilipokuwa sipo, nilienda Scotland ndio maana nimchelewa kuja”Aliongea.

Alikuwa amempeleka Clark Scotland kwani walikuwa na jukumu la kushiriki katika sherehe za Summer Bank Holliday , yeye na mama yake.

“Kwasasa bado lakini ni swala la muda tu”Aliiongea Stern huku akimwangalia Ares.

Baada ya hapo Roma aliongea na wanawake wake na kuwatoa hofu kwamba tayari alifanikiwa kumpata Clark na kumrudisha nyumbani.

Baada ya kuelezea kwa ufupi kwa upande wake na yeye alimuuliza Christen kile kilichotokea wakati ambao hakuwepo na alielezewa kila kitu kwa ufupi na namna ambavyo Ares anapanga kutoka hapo na kwenda kuwatafuta akiwa peke yake.

Upande wa Roma hakuwa na msingi mzuri wa historia nzuri juu ya hadithi ya miungu ya kigiriki hivyo hakuwa na uelewa mkubwa na licha ya kusikia stori zinazohusiana na majitu hakuwahi kuamini kama kweli walikuwepo.

“Nakushauri usiende kwanza mpaka ufahamu mbinu zao zote”Alishauri Roma.

“Acha kunidharau , Hades usijifanye wewe una nguvu kunishinda mimi kwasababu tu mara ya mwisho ulinishinda , kipindi kile sikuwa makini na nilikudharau na mbinu zako za kichawi”

“Kama unajiamini basi hakuna wa kukuzuia kufanya kile unachotaka, ni sawa kama unataka kufa lakini haitakuwa vizuri kwasisi kuja kuulizwa baadae”Aliongea Roma na kisha akajifanyisha kufikiria.

“Unaonaje ikawa hivi , kwasababu una uhitaji wa mtu wa kupigana nae , kwanini usipigane na Raphaeli”

“Damn it Hades , unanitania , nani anataka kupigana nae?”Alijitetea Hermes.

Ares baada ya kuambiwa pigane na Raphaeli alionyesha kuwa katika hali ya furaha mno , ukweli ni kwamba mikono yake ilikuwa ikimuwasha muda wote , hakujali kama angeweza kushinda au kushindwa alitaka kupigana tu.

“Hehe.. Hermes wewe ndio ulijifanyisha kuwa Farid kule Tanzania si ndio?”

“Farid !!, yupi huyo?”

“Haishagazi kwa mtu kama wewe kukosa makando kando na haina haja ya kujifanyisha hujui ninachomaanisha, ijapokuwa sijui kwanini ulileta mkanda wa kichawi feki Tanzania lakini haitokei tu ukaamua kunichokoza mimi peke yangu”

“Unamaanisha nini? , Hermes ule mkanda wangu feki ulionekana Tanzania wewe ndio uliehusika na kuzusha habari hizo?”Aliuliza Christen kwa mshangao.

“Aphrodite unaamini vipi anachoongea , kwanini nifanye kitu cha namna hio kwa faida ipi kwa mfano?”

“Acha kongea ujinga , Hades hawezi kuongea bila kuwa na ushahidi na zaidi ya yote Hermes tumejuana kwa muda mrefu tokea katika syari yetu, siku zote ukidanganya unakuwa na utulivu wa hali ya juu mno”

“Wewe..”Alitaka kuongea lakini aliishia kimwangalia Poseidon na wengine wanavyochukulia swala hilo.

“Mnaonaje na nyie , mnadhani ni mimi niliefanya kitendo hiko , mnamuamini Hades anachoongea tofauti na mimi , nitapata faida gani nikifanya hivyo kwanza?”Alijitetea. na Stern na Alice hawakuongea chochote na kuweka sura za maigizo.

“Hermes your skills in deception is not as good as your illusions”Aliongea Poseidon akimwambia uwezo wake wa kudanganya ni mdogo kuliko uwezo wake wa kutengeneza udanganyifu.

“Poa, nakubali kwamba wote nyie mnanijua vizuri , na nakubali nilifanya mimi , lakini sababu kubwa ni kwamba nilikuwa ninajisikia vibaya hivyo nikaona nikamchokoze Hades , kuna ttatizo juu ya hilo?”Aliongea kinafiki alikuwa akijua anadanganya.

“Hehe.. Hermes sijali sana kuhusua mambo yako ya kishenzi unayoyafanya , kama kweli umekasirika sasa hivi kwanini usitolee hasira zako kwangu kwa kujaribbu kunipiga”Aliongea Ares.

“Pumbavu , nina hasira kweli , lazima nikufundishe adabu wewe mshenzi”Aliongea kwa hasira huku akisimama na alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa na kisha alisogelea Balkoni na kupotea nje na mabawa yake kama vile ni Makerubi akimfukuzia Ares.

“Aphrodite , Hermes ndio aliezusha uzushi juu ya mkanda wako wa kichawi , huna mpango wa kwenda kuungana na Ares kumshikisha adabu Hermes?”Aliuliza Alice akitania.

“Hapana, uwezekano wa sisi kushinda au wa Hermes kutushinda ni asilimia hamsini kwa hamsini, nilikuwa nikijaribu kukaa upande wa Hades tu hapa , sijali kati yenu anaetumia jina langu kwa mambo yenu”

“Vyovote vile , lakini kumuacha Hermes kwenda kushindana na yule kichaa ili tu kutoa hasira zake ni sawa na kupigana na yale Majitu tu”Aliongezea Stern huku akicheka.

“Ni wazi kabisa wametuleta hapa kwa makusudi , vinginevyo wasingeenda ndani ya hoteli ambayo ulipanga kukaa Hades , inaonekana wanasubiria wote tuwe sehemu moja ndio watushambulia , hivyo kwa muda kama huu kama tutakuwa na haraka na kukosa mpango lazima tutaingia kwenye mtego wao , hivyo tunapaswa kusubiri kuona ni nini wanatuandalia , isitoshe Athena hayupo hapa na hatuwezi kujihakikishia ushindi wa moja kwa moja”Aliongea Poseidon.

“Mbona unamuamini sana Athena?”Aliuliza Roma.

“Tayari nasikia umekutana nae na kuona uwezo wake , je sipaswi kujiamini?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kuongea chochote , ukweli ni kwamba katika nyakati zoe ambazo aliweza kukutana na Athena hakuweza kufanya chochote mbele yake , tukio la Korea kusini halikuwa limefutika katika akili yake na kila siku alikuwa akifikiria ni kwa namna gani anaweza kuwa katika levo za juu kumpita Athena.

Lakini kwa wakati mmoja alishindwa kuelewa ni kwa namna gani hao watu wenye asili ya Ujitu wametoa wapi hali ya kujiamini mpaka kujitokeza na kuanza kuwachokoza makusudi.

****

Siku nyingine ya mashindano iliwadia katika jiji la Palermo , watu wengi walikuwa wakitarajia kwanzia siku hio mashindano yangekuwa ya moto sana kwani makundi makubwa makubwa ndio ambayo yalikuwa yakikutana.

Kila mmoja aliekuwa akimfahamu Roma alifurahi kwamba amerudi na alikuwa akishiriki , Kwa Sauron alonekana kama vile amezeeka tu ndani ya siku mbili zilizopita lakini mara baada ya kumfuata Roma hotelini asubuhi kidogo hali yake ya utulivu ilimrejea.

Roma hakuwazuia wasiendelee na uchunguzi, alihitaji kujua zaidi kuhusu tukio lile , alitaka kujua kuhusu kundi la kigaidi ambalo limemteka Clark na kutaka kuunda siraha ya kimaangamizi ya teknolojjia ya FURY.

Kwa wakati huo uchunguzi ulikuwa ni rahisi kutokana na kwamba Umoja wa Norh Buyeo kutoka Korea ulikuwa ukijihusisiha , hivyo Roma alimpa kazi Makedon na wengine kujaribu kutafuta nguvu ambayo ipo nyuma yao na pamoja na mipango yao yote.

Wakati mashindano yanaanza Roma alikuwa eneo la VIP huku kulia na kushoto akiwa na Mage na Magdalena.

Upande wa Magdalena alikuwa na aibu sana asubuhi hio kumwangalia Roma usoni , pengine huenda ni kwasababu ya kile kilichotokea usiku kucha.

Ukweli ni kwamba baada ya chakula cha usiku Rose yeye alichukuana na Christen na kusingizia wanaenda kufanya Shopping , ilikuwa ni usiku ndio kakini maduka katika jiji la Palermo yalifanya kazi masaa ishirini na nne na watu ambao walikua ni maarufu maarufu wanaofika katika jiji hilo walikuwa wakifanya Shopping usiku ili kuepuka macho ya wengi.

Sasa kilichotokea ni kama kuna mpango ambao Rose na Magdalena walikuwa wamepanga , kwani wakati Rose alivyotaka kwenda kufanya Shopping Magdalena yeye alisema amechoka na alitaka kulala, upande wa Roma na yeye alikuwa amechoka kwa kutolala siku mbili mfululizo hivyo alitaka kupumzika.

………….

Kutokana na wote kupewa chumba kimoja basi ilitokea , Roma na Magdalena wakalala kitanda kimoja.

“Magdalena vinauma?”Ni sauri ya mwanaume iliosikika usiku wa jana katika chumba cha hadhi ya juu alichokuwa akilala mfalme Pluto.

Licha ya mwanaume kuuliza swali la namna hio , hakukuwa na majibu kutoka kwa mwanamke mrembo aliekuwa amelaliwa kwa juu na mwanaume aliejengeka mwili kimazoezi, upande wa yule mwanamke alionekana kuwa katika raha ya ajabu kiasi kwamba alitumia miguu yake na kuipitisha katika kiuno cha mwanaume yule.

“Arggh..”Mwanamke alitoa mguno huku akiachama kama vile kabanwa na mlango , alionekana alikuwa akipitia hali ya maumivu na raha kwa wakati mmoja

“Samahani , lakini inaonekana kubanwa sana ndio maana unasikia maumivu”Aliongea mwanaume kwa sauti ya kunong’ona, ilionekana kwa upande wa mwanamke kinachoendelea kwake kilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanyiwa.

“Ni sawa tu , nitapona kwa haraka , isitoshe na mimi pia sio wa kawaida”Ilisikika sauti nyororo ya mwanamke.

“Kama ni hivyo basi nitaanza kuchezesha kiuno”

“Sawa , usije kunifanya niijutie hii siku”

“Usijali , nitahakikisha hii siku unaikumbuka katika maisha yako yote”Aliongea yule mwanaume kwa besi na kisha makalio yake yalionekana kubonyea chini.

“Argh…!!”

…………….

Naam hayo ndio maongezi yaliosikika nje ya mlango wa chumba cha mfalme Pluto usiku wa jana.

Sasa wakati wakisubiria pambano lianze , ndio Roma alimuuliza mrembo Rose namna usiku wake wa Shopping ulivyokuwa na mrembo huyo alimwelezea kwa ufupi.

“Hakuna kikubwa kilichotokea”Alijibu Rose.

“Pengine anaona aibu , jana kanunua nguo za ndani kibao ambazo zimekaa kiuchokozi uchokozi”Aliongea Christen bila aibu na kumfanya Rose amkazie macho na alijikuta akiona aibu, Bahati tu waliokuwepo karibu yao ni Stern na Alice , angejisikia aibu sana kama Ron na Sauron wangekuwepo hapo.

Christen hakujali namna Rose alivyokuwa akimwangalia na alitoa ulimi kumtania na kisha akageuza shingo yake mbele.

“Kama ni hivyo , hakikisha unanunua za kutosha”Aliongea Roma akiwa na uso uliokaa kifisi.

“Haikuwa hivyo..Usimsikilize Christen”

“Najua , mimi natoa maoni yangu tu , ila usisahau usiku wa leo nataka kuona namna utakavyopendez… sawa Babe?”

………………

Wakati wakiendelea kuongea hatimae ilifikia zamu ya The Eagles , washindani wao ilikuwa ni kundi la Kimasenari lifahamikalo kwa jina la Odin Mercenary Corp, walikuwa na makazi yao Kaskazini mwa ncha ya dunia.

Rose na Magdalena mara baada ya kuona ni watu wa Roma waliweza kuongeza umakini , lakini upande wa Roma alionekana kabisa kutopenda sana kuangalia maishindano ya aina hio kwani yalikuwa ya kawaida sana kwake.

Lakini licha ya hivyo alifurahi kuona wanajeshi wake walikuwa wameimarika sana , hususani Maninja upande wa New Zero kwani walionyesha uwezo mkubwa katika kupambana na wapiganaji wa kundi la Odin, mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa The Eagles waliibuka washndi na kuigia katika hatua inayofuatia.

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kuondoka na hakuwa na mpango kabisa wa kurudi tena, upande wa Rose mara baada ya kuona Roma kaondoka katika hilo eneo na yeye alifuata nyuma nyuma lakini kwa Magdalena yeye alisema ataangalia mashindano hayo mpaka mwisho

Ukweli ni kwamba alitaka kuendelea kuangalia , ila tu kumpa nafasi na Rose kuwa karibu na Roma kwani usiku wa jana kama sio Rose basi huenda asingeweza kuonja dunia ya mapenzi kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alikuwa na raha na akili yake yote ilikuwa ikiwaza usiku wa jana wote aliofanya mapenzi na Roma.

Hakuwaza rena kama Roma alikuwa mpenzi wa pacha mwenzake au mume wa rafiki yake wa utotoni Edna , bali muda huo alijiambia amefanya maamuzi sahihi kufata kile moyo wake unachotaka.

Wakati Roma na Rose wanakaribia hotelini waliweza kukutana na mwanaume wa Kijapani , Rose alionekana kumfahamu mwanaume huyo na upande wa Roma pia alikuwa akikumbuka sura ya mwanaume huyo, alikumbika kipindi alichosafiri kwenda Japani akiwa na Dorisi aliweza kukutana na huyo mwaname katika kambi ya jeshi wakati akienda kumpatia mateso Kapteni Kisu Mvunjiko na alishangaa kumuona akiwa hapo kwani alikuwa na cheo kikubwa mno serikalini.

Roma ilibidi kwanza amhoji Rose inakuwaje akawa anamfahamu huyo Mjapani na ndipo alipomuelezea kwamba alikutana nae usiku wa jana akiwa na Christen na huyo mwanaume ndio aliewasogelea na kuwachombeza kwa ajili ya kwenda kumpa huduma usiku kucha kwa malipo ya hela , lakini Christen akamjibu kwa kumwambia yeye atamlipa kwa kila pigo atakalompiga na ndio akaondoka na kuwaacha.

Roma mara baada ya kusikia hivyo aliguna , aliona sio jambo la kawaida kigogo wa serikali kutoka Japani ghafla tu kumsogelea Christen na Rose na kuwataka wampatie huduma.

Baada ya kuingiwa na wasiwasi ya uwepo wa mwanaume huyo hapo Sicilly haraka sana alimpigia simu Sauron na kumpa maelekezo ya kumfanyia uchunguzi , hisia zake zilimwambia huenda alikuwa akihusika na wale watu wa mavazi meupe au kundi la Cyclops.

*****

Ikiwa ni muda wa jioni kabisa wakati Roma akiwa ameuchapa usingizi mara baada ya kazi nzito alioifanya na Rose mlango wa chumba chao ulifunguliwa na Magdalena.

Mara baada ya kuona namna Rose na Roma walivyolala wakiwa hawana nguo mwilini alijikuta akiona aibu , lakini alijitahidi kujikaza na kwenda kumuamsha Roma.

Roma mara baada ya kuamka hakuona aibu licha ya kwamba alikuwa uchi yeye na Rose na alienda mbali kumtania Magdalena na kumwambia ajiunge na yeye lakini Magdalena aligoma na kumwambia kwamba amekuja hapo kumpa taarifa kwamba wenzake wanamuhitaji katika eneo lileile la siku ya jana kwa ajili ya maongezi.

Roma mara baada ya kupewa taarifa hio hakuwa na muda wa kupoteza , alikuwa na hamu kubwa ya kuwajua kiundani watu alioambiwa wana aasii ya Ujitu ndani yake hivyo ndani ya dakika chache tu alikuwa tayari amekwisha kujiandaa na kutoka.

Roma mara baada ya kufika aliweza kukuta kila mmoja alikuwa amekaa katika nafasi yake na yeye pia alisogelea kiti na kuketi , lakini wakati huo akiangalia barua iliokuwa juu ya meza.

“Nini kinaendelea hapa , hio ni nini?”Aliuliza Roma na kumfanya Christen aliekuwa akimwangalia Roma muda wote katika eneo la chini ya kiuno chake palivyotuna kuvuta mdomo na kisha kuchukua ile barua na kumpatia.

“Je ungependa kujifunza lugha yetu?”Aliuliza na kumfanya Roma kuangalia ile barua ilioandikwa kwa herufi zisizoeleweka na kumrudishia Christen.

“Haina haja , ninajua lugha nyingi sitaki kuongeza nyingine kwenye kichwa changu , niambie barua hii inahusu nini”

“Ni rahisi tu , ni kwamba kiongozi wa Cyclops anaefahaika kwa jina la Brontes ametutumia mwaliko , anatualika sisi wote kwenda kupata chakula cha mchana katika mgahawa siku ya kesho baada ya awamu ya kwanza ya mashindano ya asubuhi”Aliongea Poseidon.

“Kwanini wanataka kukutana na sisi? , hawajawahi kututafuta hapo kabla”Aliuliza Roma.

“Hata sisi imetushagnaza pia , wanaonekana kama hawatafuti kulipiza kisasi na wanajaribu kutualika namna hii , wanajaribu kufanya nini?”Aliongea Stern.

“Kwanini tujali wanachotaka , huenda wametualika kwa ajili ya kumaliza tofauti zetu , lakini kama wanataka kupigana na sisi tutapigana na kama wanataka amani tutawaacha waendelee kuishi”Aliongea Ares na kufanya wote wamwangalie kwa mshangao kidogo lakini haa hivyo washazoea Ares amekaa kifujo fujo.

“Hivi wasiwasi wenu ni kwamba tunaweza tusiweze kupambana nao?”Aliuliza Roma baada ya kimya cha muda mfupi.

“Kama tungekua kwenye sayari yetu , wasingethubutu hata kutusogelea na ningewapiga mimi mwenyewe, lakinii sasa hivi mambo ni tofuati bila ya Athena na Zeus tunaweza tusifanikiwe kuwashinda ijapokuwa tutakuwa na uwezo wa kujilinda”Aliongea Hermes.

“Mimi nipo , yupo pia Rose na Magdalena ambao wote wapo katika levo ya Nafsi , je bado tu haitoshi , kwanini tuwaogope?”Aliuliza Roma.

“Hades unawachukulia poa hawa majitu , ngoja nikuambie Cyclops na Hecatoncheires wanao uwezo mkubwa kuliko jamii zote za majini na hawaathiriki na nguvu za mbingu na ardhi kwasababu wana damu ya kizazi chetu , Damu ya Titan”Aliongea Artemis.

“Damu ya Titan!!?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Ndio …”Alice aliwaangalia wenzake kuona kama kuna ambaye anajaribu kumzuia na baada ya kuona wapo kimya aliendelea.

“Damu ya Titan ndio asili yetu kamili na sisi ni mwendelezo wa kizazi cha damu yake , ndio chanzo kikubwa cha nguvu zetu wakati tulipokuwa kwenye sayari yetu m sababu ambayo imetufanya uwezo wetu kushuka kufikia asilimia therathini ni kwasababu tulikosa miili yetu yenye asili ya damu ya Titan , hawa Majitu wenyewe ni sehemu ya uzao wetu hivyo wana asili ya damu ya Titan na kama tulivyosema mwanzo, wao walikuja duniani na wakaweza kuishi kwa miili yao lakini sisi ikashindikana, Mpaka sasa hivi damu yetu ipo Sealed”

“Hebu subiri kwanza , nilikuwa nataka siku zote kuuliza ilikuwaje miungu mkapoteza uwezo wenu kwa kiasi kikubwa , kama kweli hii damu ya Titan ndio chanzo cha nguvu zenu , kwanini ipo ‘Sealed’ mpaka sasa , je swala hili lina uhusiano na moyo wa Gaia?”Aliuliza Roma.

“Kuhusu hilo..”Alice alitaka kuongea lakini alisita lakini palepale Christen na yeye aliingilia.

“Usiulize maswali Hades , kwetu kumbukumbu hizo ni maumivu makali kila zinapojirudia .. nitaendelea kukuelezea kwa niaba ya Alice, hawa majitu wanao uwezo mkubwa kutokana na kuwa na damu ya Titan na ndio maana hawaogopi kabisa watu wanaovuna nishati za mbingu na ardhi , kwasababu ni nishati ya muunganiko wa dunia hii , Damu ya Titan unaweza kusema ina nguvu ya Kiroho kama mnavyopenda kuita hapa duniani , sasa unatakiwa kujua ni Zeus pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kutumia mwanga kuifubaza nguvu za damu hio na kuwafanya wawe dhaifu , hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kuwashinda hata Athena mwenyewe hakuwa na uwezo huo”

“Kwa maelezo yenu mnaamaanisha kwamba tunapaswa kufa kwenye mikono yao si ndio?”Aliuliza Roma huku akitabasamu kwa uchungu

“Hatuwezi kwenda mbali hivyo , kwasasa hatujui ni ipi mipango yao na isitoshe una nafasi kubwa , angalau unaweza kutumia kanuni za anga pamoja na nguvu za nishati ya mbingu na ardhi , lakini hata hivyo inatia huzuni kwasababu haupo kwenye levo ya juu zaidi ya kuweza kudhibiti Radi kama Majinni tuliokutana nayo kipindi tunafika la sivyo ungekuwa tishio kwao”Aliongea Poseidon.

Roma alijiambia hata kama hakuwa katika levo za juu kama watu waliowakuta miaka hio , lakini yeye alikuwa na chungu cha maafa hivyo alijiambia kwamba mwisho wa kila kitu bado haujulikani kama watapambana.

Hao watu kilichomuudhi sana ni kwamba ni wasiri sana kuhusu hio damu ya Titan na alijua kabisa ameelezwa nusu na ni kitu ambacho kinahusiana na moyo wa Gaia

Baada ya mazungumzo ya muda mfupi Poseion alimtaka Hermes kunagalia Ulingo kama haujawekwa mtego ili kuwa salama na haikuwa tatizo kwa Hermes kulingana na spidi yake

******

Siku ya tatu hatimae iliweza kuwadia na makundi therathini na mbili yalikuuwa ndo yamebakia , wawakilishi mbalimbali kutoka serikalini walikuwepo.

Kama kawaida Poseidon , Hermes na Ares walikuwa katika eneo lao la sku zote na Roma , Magdalena , Rose Alice , Stern na Christine wlaikuwa wamekaa katika eneo moja.

Kabla ya mashindano kuanza Roma aliweza kupokea ripoti kutoka kwa Makedoni juu ya baadhi ya chunguzi alizomwambia Sauron afanyie kazi.

Na kwa maelezo yake ni kwamba mwanaume wa Kijapani aliemuona katika hoteli ya Cassano alikuwa akifahamika kwa jina laKagawa Chusho na ni waziri wa ulinzi wa Japani na hana uhusiano wowote na kundi la watu wa mavazi meupe , lakini alimwambia kwamba wakati ambao alimuona hotelini ilionekana kulikuwa na kikao kilichokwisha kufanyika hivyo hawakuwa na uelelwa nini kilitokea au kilizungumzwa katika kikao hicho ndani ya hoteli ya Cassano.

Roma kuna hisia ambazo zilimwambia kabisa huenda serikali ya Japani ilikuwa ikihusika kabisa na uwepo wa hawa Majitu hapo Sicilly lakini hakuwa na namna ya kuthibtisha dukuduku lake kutokana na kwamba alijua fika kikao ambacho kilifanyika ndio kilikuwa na taarifa kamili lakini kwa bahati mbaya walichelewa kugundua mapema..

Wakati ambao Roma alikuwa katika mawazo alikuja kushituliwa na Sauron aliekuwa anakuja mbio mbio kwake .

“Your Majesty Pluto something is wrong”Aliongea Sauron akimwambia kuna tatizo.

“What are you saying?”(Unaongea nini?”);

‘Hapa , hebu angalia wahusika ambao wanakwenda kushiriki katika mecho inayofuatia”Aliongea Sauron na kushika Kishikwambi alichokuwa ameshikilia Sauron.

“Mechi inayofuata ni The Eagles na Deicide?”Aliongea Roma kwa mshangao akimaanisha kwamba mechi inayokwneda kuanza ni kati ya Majitu wanaojiita godkiller na wanajeshi wake wa The Eagles.

“Nini kimetokea , nilijua wanakwenda kukutana katika nusu fainali tu?”Aliuliza Roma huku akiwa na wasiwasi na kuanza kupitia orodha ya wanajeshi wake ambao wanakwenda kushindana katika mechi inayofuata.

“Kuna mtu ambaye amebadilisha na meneja anasema ni makosa tu yaliofanyika , nadhani ni makusudi kabisa wanataka tukutane kwanza na hao wauaji ili watudhalilishe kututoa katika mashindano mapema“Aliongea Sauron kwa hasira.

Lakini licha ya hivyo ni kama washachelewa , kwani tayari wanajeshi wa The Eagles walionekana wakiingia kwenye ulingo na walionekan kuwa na mchecheto mara baada ya kusikia wanakwenda kupambana na kundi la Deicide watu waliowaonyeshea kiburi katika hoteli ya Federico.

Wakati Nasri na wenzake wakiwa na shauku ya kulipiza kisasi kwa kuwashikisha adabu watu hao, upande wa Roma alikuwa na wasiwasi kwa kile kinachokwenda kutoktea kwa kuamini kwamba wanajeshi wake hao hawana uwezo wa kushinda na kwa mara ya kwanza jeshi lake linakwenda kudhalilishwa.

Makofi ya shangwe na vifijo yalisikika pande zote baada ya wanajeshi wa mavazi meupe kuingia kwa mbwembwe zote na baada ya kufika katikati waligeuka upande ambao wamekaa Poseidon , Roma na ndugu zake na kuwaangalia , ijapokuwa sura zao hazikuwa zikioneana kwa kuvaa Mask lakini likuwa ni kama vile walikuwa na sura za kejeli.

ITAENDELEA WIKIEND NJOO WATSAPP TUPIGE STORI NAMBA 0687151346
 
Back
Top Bottom