Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Jamaa mbabaishaji sana..
Tuwe na subira.mana kwa mzigo anaotumaga.akisema aweke kwa epsd moja kila ck.mzigo mmoja unawezaenda mwez mzima.atatuma tu maadam alishaleta utangulizi.na aliahd ni mwanzo mwenga yani ni mpaka tamat
 
Ni kweli kabisa
Tuwe na subira.mana kwa mzigo anaotumaga.akisema aweke kwa epsd moja kila ck.mzigo mmoja unawezaenda mwez mzima.atatuma tu maadam alishaleta utangulizi.na aliahd ni mwanzo mwenga yani ni mpaka tamat
 
Salamu Mkuu singanojr samahani kama nitakuwa nakusumbua nilikuwa naomba mtiririko kamili (ascending order) wa hawa miungu. Nimepitia hapo nikaona hades ni wa 12 samahan lakn kama nitakuwa nakuchosha katika kuwapangilia.
 
Nasikia kwenye group la WhatsApp hii Riwaya ipo mbele Zaidi.Sasa kwa kuwa Mwamba ametingwa AU yupo ICU/mahututi mngeendelea kutupia humu ili kumsaidia kuleta muendelezo🤔
 
Nasikia kwenye group la WhatsApp hii Riwaya ipo mbele Zaidi.Sasa kwa kuwa Mwamba ametingwa AU yupo ICU/mahututi mngeendelea kutupia humu ili kumsaidia kuleta muendelezo[emoji848]
Nitaweka mwendelezo saa nne usiku inshallah...mimi ndio nawajibika kutoa mwendelezo hapa maana ndio nimeanzisha uzi... mtu mwingine kuweka mwendelezo hapa ni kuharibu uzi na hasara zake ni kwamba simulizi hii haitofika mwisho hapa.
Kwasababu nikileta mwendelezo ni vipande vingi basi mnivumilie nisipokuwa hewani maana natingwa muda mwingine
 
Nitaweka mwendelezo saa nne usiku inshallah...mimi ndio nawajibika kutoa mwendelezo hapa maana ndio nimeanzisha uzi... mtu mwingine kuweka mwendelezo hapa ni kuharibu uzi na hasara zake ni kwamba simulizi hii haitofika mwisho hapa.
Kwasababu nikileta mwendelezo ni vipande vingi basi mnivumilie nisipokuwa hewani maana natingwa muda mwingine
Nitasubiri mkuu hiyo Saa 4 usiku
singanojr
 
P1 sana kk tuwekee mzigo wa kutosha apo badae ili utufidishie na hz cku ambz tumekukosa kaz njm kwako...
 
Nitaweka mwendelezo saa nne usiku inshallah...mimi ndio nawajibika kutoa mwendelezo hapa maana ndio nimeanzisha uzi... mtu mwingine kuweka mwendelezo hapa ni kuharibu uzi na hasara zake ni kwamba simulizi hii haitofika mwisho hapa.
Kwasababu nikileta mwendelezo ni vipande vingi basi mnivumilie nisipokuwa hewani maana natingwa muda mwingine
Sina shaka na wewe mwamba
 
SEHEMU YA 576.

Wote walijikuta wakiinua macho yao kumwangalia mwanamke mwenye nywele nyeusi ndefu aliefika hapo, alikuwa hajavaa kitu miguuni na sura yake haikuonekana vizuri kwa kutambulika lakini ngozi yake ilikuwa ileile alioiona Roma nchini Korea kusini.

Ni kama vile jua limekosa nguvu muda ambao aliingia katika eneo hilo , huyu mwanamke alikuwa katika hali ya ukauzu na hali ya kujivunia kama siku zote na alikuwa ni kama vile sio yeye alietumia ngao yake kuwaokoa wale majitu na Magdalena.

Kila mmoja alimwangalia kwa namna isioelezeka , haikujalisha kuna ambao walikuwa wakimchukia katika eneo hilo lakini hakukuwa na hata mmoja ambaye aliekuwa hatambui uwezo wake.

Pengine alikuwa na haki zote za kujivunia , macho yake yalikuwa ya kejeli ni kama vile alikuwa akiangalia watu wa hadhi ya chini sana na hata baada ya kuona majitu hayo yeye hakuwa na mshangao wa aina yoyote kama waliokuwa nao ndugu zake mara baada ya kuwaona kwa mara ya kwanza.

Kwa kunyoosha mkono wake tu , ile ngao yake ilimrudia kwenye mikono yake kwa namna flani hivi ya kipekee..

Ilikuwa ni ngao kubwa huenda ambayo ilikuwa ikilingana na urefu wake huku ikiwa na michoro isioweza kutambulika kwa haraka , ilikuwa ya kizamani sana.

Athena aliangalia kile chungu cha maafa kwa macho ya masikitiko , na kwa upande wa ile roho iliokuwa ndani yake ni kama vile ilijua nani wa kushindana nae na nani sio wa kushindana nae kwani palepale kilipungua ukubwa wake na kisha kikapotea..

Roma palepale mara baada ya chungu chake kupotea na yeye alipoteza fahamu na kudondoka chini na kusaidiwa na Magdalena pamoja na Rose.

“Hubby Amka , Unajisikiaje?”Rose alijitahidi kumtingisha Roma kuamka lakini hakukuwa na majibu kabisa.

Walijaribu hata kuchunguza mwili wake kwa kutumia nguvu zao za kijini lakini hakukuwa na majibu .

Nguvu zake za ndani zilikuwa kubwa mno kuliko mwanzo lakini kwa sababu zisizofahamika hakuweza kushituka hata alivyoamshwa na hata uwezo wake wa kiuungu haukuwa ukifanya kazi.

Warembo hao walikuwa katika hali ya kutojua cha kufanya , lakini licha ya hivyo hawakuwa na hofu kubwa kutokana na uwezo wao , baada ya kuona Roma alikuwa anapumua vizuri waliamua kutulia na kugeuza macho yao kwa Majitu yaliokuwa chini.

Majitu yale yalikuwa yakijitahidi kusimama lakini kwasababu ya mashambulizi ya chungu cha maafa walikuwa dhaifu mno na hata wale ambao waliweza kusimama walikuwa wakihema kama mbwa aliekimbia maili nyingi , baadhi yao hawakuwa na miguu na mikono kutokana na kunyofolewa na Cauldron.

“Hades anaendeleaje?”Aliuliza Christen .

“Sijui haamki lakini pia hajaumia popote”Aliongea Rose.

Athena alimwangalia Roma kwa sekunde na kisha akageuza macho yake kwa yale majitu kwa mwonekano wa kikauzu.

“Pumbavu zako Athena , nilijua tu ulikuwa unafanya haya makusudi, inaonekana ulijua haya yatatokea lakini kwanini ndio umekuja sasa hivi au ndio umekuja kutukejeli ?”Aliongea Hermes mara baada ya kumtupia Prince kwa Christen.

“Bado tu mpo hai?”Aliuliza kwa kejeli..

“Unamaanisha nini? Au ndio ulitaka kutuona wakituua , usisahahu kwamba huwezi kufufua moyo wa Gaia bila sisi”Aliongea Hermes kwa hasira.

“Acha kuvuka mipaka, nilishakusamehe kwa kupanga njama na yule mpuuzi , siku zote nimekuwa mtu mzuri kwako na hivi sasa huwezi kunificha kwani najua alishaamka muda mrefu tu”Aliongea

Alikuwa akimaanisha yule mwanamke aliekutana na Hermes nchini Tanzania katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Mingu mingine walijikuta wakishangazwa na kauli yake , walikuwa wakijua nini anamaanisha lakini walikosa kuamini.

“Nilijua unabii wako ni wa ukweli lakini kwanini umeshindwa kumtafuta?”Aliuliza Hermes.

“Sina haja ya kumtafuta kwani atajitokeza mwenyewe”

“Hehe , nafikiri ni kwasababu nguvu yako ya kiroho bado ipo chini mno ndio maana unashindwa kumtafuta kwasababu amekuzidi nguvu na uwezo, hii inanipa uhakika kwamba huwezi kushindana nae”Aliongea Hermes kwa majigambo.

“Sina matamanio ya kumtafuta mtu asiejiamini mimi , kama kweli sifa unazompatia zinamstahili kwanini anafanya mambo yake kwa siri na kunipangia njama?”

“Nyie watu mnaongea nini , mbona sisi hatuwaelewi?”Aliuliza Apollo.

“Hakuna kitu , hata hivyo hampaswi kuelewa”Aliongea huku akiwaangaia na muda uleule alichezesha mkono wake na ile ngao yake ikapotea .

“Niambie nini maana halisi ya Cauldron na nguvu ya roho ya mnyama iliomo ndani yake, kwanini hatujawahi kukiona?”

“Sidhani kama inahaja ya kufahamu kinatokea wapi kwani ni ngumu sana kushindana nacho mpaka Athena alipotumia ngao yake”Aliongea Ares lakini Athena hakujibu swali la Poseidon na alipaa mpaka kwenda kusimama juu zaidi usawa wa yale majitu.

“Athena wewe mwanamke ni kichaa , unapata wapi ujasiri huo ,kwanini unatokea wakati tushakuwa dhaifu , kama kweli unajiamini shindana na sisi tukiwa tushapona”Aliongea Briareus.

“Tayari nyie ni nusu wafu , mtaweza kupona vipi?”

“Acha upuuzi , hatujapoteza pambano bado , njoo kama unajiamini”Aliongea Brontes kwa hasira kali huku akijaribu kunyanyua nyundo yake lakini kutokana na kupoteza kiwango kikubwa cha damu kwenye mwili wake alishindwa kabisa kulibeba kutokana na kuwa zito kwake.

Walianza kupatwa na kiwewe mara baada ya wote kuona wanashindwa kutumia siraha zao katika hali waliokuwa nayo , hawakuamini kama wameweza kushindwa na Pluto mpya ambaye kwao alikuwa binadamu tu.

Athena aliwaangalia kwa tabasamu la kejeli na palepale alinyooosha mkono wake na mwanga wa mng’ao rangi ya Zambarau uliweza kuonekana katika kiganja chake.

“Moyo wa Gaia!!!”

Kila mmoja alijikuta akibwabwaja kwa mshangao , wale majitu na yenyewe yalijikuta yakianza kurudi nyuma kwa wasiwasi na walionyesha kilichokuwa katika mkono wa Athena walikuwa wakikifahamu na kiliwaogopesha.

“Hapana.. hapana ., haiwezekani , kwanini una moyo wa Gaia?”Aliongea Brontes huku akirudi nyuma kwa woga.

Miungu wengine walikuwa katika hali isioelezeka wakimwangalia Athena kwa shauku kwa kile anachotaka kukifanya.

Athena palepale aliachia ule moyo wa Gaia uliokuwa kwenye mikono yake na kuusukumia upande wa yale Majitu na ilikuwa kama vile ulikuwa ukijua wapi pakwenda kwani uliongeza spidi na moja kwa moja ulianza kumvamia Gyeges aliekuwa amebakia kiwiliwili na alijikuta akitoa ukulele wa maumivu.

“Noooo..!!”

Alijikuta akitoa ukulele lakini kutokana na kuwa dhaifu alishindwa kufanya chochote na alikiona kifo, wakati huo kiwingu cha mwanga wa zambarau kilimfunika mwili wake mzima kiasi cha kutoonekana na ndani ya sekunde kumi tu kulitokea mlipuko kama ule wa mafataki na kile kiwingu kikapotea na lile Jitu halikuonekana tena, ilionekana lilikuwa tayari limekwisha kumezwa.

Moyo wa Gaia ni kama vile ulikuwa na ufahamu , huenda ulikuwa ukivutiwa na damu ya Titan kwani ulianza kushambulia yale majitu mengine kwa staili ileile iliomtokea Jitu mwenzao.

Walijitahidi kutoroka lakini walishindwa kutokana na udhaifu wao, ilikuwa ni milipuko midogo kama vile mafataki iliotokea kwa zaidi ya mara sita na palepale yale majitu hayakuonekana tena na hata yale manyundo yao na yenyewe yalipotea.

Christen na Alice alijikuta wakijawa na sura za huzuni mno ni kama vile walikuwa wakiomboleza kwa kile kilichotokea , lakini wengine walikuwa katika hali ya woga kwa kile wanachokishuhudia.

“Athena nadhanni umesubiria hii siku kwa hamu sana kwa wao kujidhihirisha ili uweze kutumia damu yao ya Titan kufufua moyo wa Gaia”Aliongea Poseidon.

Muda uleule ule moyo wa Gaia ambao sasa ulikuwa umebadilika umbo lake na kuonekana kuwa hai zaidi ulirudi katika mikono ya Athena huku ukitoa toa cheche kama shoti.

“Why can’t I do this unless you want me to use one of you to activate Gaia’s heart”Aliongea akimaanisha kwamba labda kama wanataka atumie mmoja wao kuufufua moyo wa Gaia.

“Sijamaanisha hivyo , lakini kama kweli ulikuwa ukijua haya yangetokea kwanini umekuja kwa kuchelewa?”

“Sina haja ya kuelezea matendo yangu kwa mtu yoyote”

“Haha..Unakiburi cha kuchukiza sana wewe na..”Aliongea Alice akitaka kutanguliza tusi lakini alijizuia huku wengine wote walimwangalia kwa kukunja sura .

“This is over and the revival of Gaia’s heart has just begun , I’ll leave first of you have nothing else to say”

‘Hili limekwisha na ufufuo wa moyo wa Gaia umeanza , nitaondoka wa kwanza kama hamna lingine la kuongea”Aliongea Athena akipotezea maneno yao ya kejeli na hakuonyesha alikuwa na mpango wa kubakia hapo na kuendeleza maongezi.

“Simama hapo hapo?”Aliongea Rose ambaye tayari alipaa na kwenda kusimama mbele yake.

“Unataka nini?”Aliuliza kikauzu huku akikunja sura.

“Kwahio unajiona una nguvu kubwa saana hivyo kuhitaji shukrani zetu kwa kutuokoa?”Aliuliza Rose huku akimwangalia Athena kwa sura ya kejeli..

“Unajaribu kuongea nini?”Aliuliza Athena akikunja sura kwa hasira.

“Ninachomaanisha ni kwamba unaonekana ulikuwa ukijua kila kitu kitatokea leo hii , ulikuwa ukijua maelfu ya watu watakufa hapa”

“Sina muda ya kuwazia huo upumbavu”

“Upumbavu !, uko sahihi kwasababu tayari wamekwisha kufa ni upumbavu , nilishasikia habari zako kutoka kwa mpenzi wangu kwamba unafanya juu chini kuweza kulifufua kabila lako kwa miaka na miaka , ijapokuwa sikuwahi kuwaza tunaweza kukutana , lakini nilishawahi kukuwazia kwa kukuona mwanamke jasiri , mwenye nguvu , mvumilivu na mwenye imani kubwa lakini leo hii nimekuja kugundua kwamba yale niliokuwa nikiyawazia ni tofauti kabisa , Mwanamke ninaemwona hapa ni yule anaetumia ujanja ili tu kutimiza malengo yake , mwanamke mbinafsi na mnafiki ambaye anadharau maisha ya wengine kwa ajili tu ya kutimiza malengo yake”Aliongea Rose kwa hasira na kufanya kila mmoja aliekuwa hapo ndani kuwa katika hali ya mshangao na wasiwasi , hakuna ambaye alkuwa akiamini kama Rose angechukua hatua ya kumuongelesha Athena hivyo.

Athena maneno ya Rose yalionekana pia kumgusa na palepala aliachia mkandamizo wa hewa , ilikuwa ni kama vile bomu lilikuwa likitaka kulipuka.

“Labda kwako unadhani binadamu ni tofauti hivyo maisha yetu kutokuwa na thamani lakini ushawahi kufikiria unaishi katika mwili wa nani , unaishi ndani ya mwili wa binadamu pia , nani kakupa haki ya kutudharau kama tu hata wewe unategemea mwili wa biandamu kuendelea kuishi? , Roma ameishi kwa zaidi ya miaka ishirini tu , hajui ni mangapi nyie watu mmefanya katika maisha yenu hapa duniani lakini licha ya hivyo anawachukulia kama ndugu kutokana na uungu wake , alikuwa na uwezo wa kuondoka hapa ndani na kukimbia kwani kufungwa kwa anga hakukuwa kukimwathiri lakini alijitahidi kuhakikisha anafanya liwezekanalo kulinda ndugu zako , lakini vipi kuhusu wewe , ulijua kabisa ndugu zako wapo katika hatari lakini ukaamua kuja mwishoni kabisa , huku ukianza kjifanyisha ndio mwokozi wao , wewe ni nani mpaka ujione unaweza kufanya utakalo?”Rose aliongea kwa hasira huku akitokwa machozi aliamua kumtolea uvivu The Don.

Tokea mara ya kwanza kuja kufahamu kwamba The Don alikuwa ni mwanamke aliekuwa akiitwa Athena alijikuta akimkubali na kuoan huenda ni mwanamke jasiri na mvumilivu mpaka kuwa na ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa kawaida na ule wa Underwold, lakini kitendo chake cha kuja wakati ambapo maelfu ya watu wamekufa kilimkasirisha mno.

Athena alifumba macho yake kwa dakika kadhaa na kisha palepale aliachia ule mkandamizo wake wa hewa na amani ikarudi.

“Yaliopangwa kuja kutokea yatatokea na hakuna wa kubadilisha kinachokuja, waliopangiwa kufa watakufa na waliopangiwa kuishi wataishi, sihitaji kujielzea matendo yangu kwa mtu yoyote yule , sitokuua kwa sababu ya Hades lakini siku nyingine usije ukathubutu kuvuka mpaka”Baada ya kuongea hivyo alimwanagalia kama kituko na kumpita..

“Hivi unajiona unaweza kuwa Mungu kwasababu huonekani na unaogopwa? , haijalishi kama huonekani lakini bado utabakia kuwa binadamu tu milele, mchawi mkubwa wewe”Aliongea Rose lakini Athena hakujali maneno yake na palepale alipotelewa kwenye mawingu kama malaika.

Rose aliishia kutoa tu machozi huku akihema kwa hasira, mabega yake yalikuwa yakimtetemeka kwa kulia kwa kwiki huku akimsogelea Magdalena aliemshikilia Roma.

Miungu ilimwangalia kwa macho ya mshangao hawakuamini alikuwa na ujasiri wa namna hio , lakini kwa wakati mmoja kile walichoongea ni kama aliwasaidia.

Maneno ya Rose yaliwafanya kuelewa ni kwa kiasi ganni matendo ya Athena yalikuwa ya kishetani.

“Usilie tena , Hades atakuwa sawa, Athena siku zote yupo hivyo hivyo ni tabia yake na hakuna wa kumfanya lolote”Aliongea Christen akimkumbatia bega lake.

Ukweli huenda baadhi yao hawakuona kuna haja ya kufufua ndugu zao na kabila lao kwa ujumla, huenda ni kwasabbau ya hofu waliokuwa nayo kwa kile ambacho kitaitokea dunia , lakini licha ya hivyo Athena siku zote alikuwa mkubwa kwao ndio maana hawakuwa na cha kumfanya.

Hata wao pia walikuwa na hofu kubwa kwani kama Athena angeweza kufanikisha kufufua moyo wa Gaia ilimaanisha kwamba angewatawala mpaka kimawazo na angezidi kuwa na nguvu kubwa duniani na kufanya kila anachotaka.

“Tuondoke hapa tukaangalie kama kuna waliosalia karibu na hapa na ndio tufikirie namna ya kumuasha mpenzi wetu”Aliongea Magdalena na Rose alikubali na wengine wote waliondoka katika hilo eneo.

Tukio lilikuwa limekwisha kuisha , ijapokuwa sio mwisho ambao ulitarajiwa.

Baada ya kutafuta kwa madaika kadhaa , Rose na Magdalena walijikuta wakiwa na ahueni mara baada ya kugundua Sauron na wengine wote hawakuweza kuathirika kutokana na kutokuwa karibu na uwanja .

Lakini ilikuwa bahati mbaya wale wanajeshi wote walioshiriki katika mashindano wakiwakilisha kundi la The Eagles kufariki wote na hakukuwa na miili yao kutokana na kumezwa na chungu.

Baadhi ya wanasiasa wakubwa waliweza kupona na ilikuwa ni kama walikuwa wakitegemea hilo lingetokea kwani waliweza kuondoka mapema na ilikuwa ni afadhari kwani ingeleta migaongano ya kisiasa kimataifa.

Upande wa Prnce kijana kutoka Scotland wa kundi la wachawi la Siraha kwenye Jiwe aliweza kuhojiwa na alisema alishindwa kukataa kutokana na kwamba wapendwa wake walikuwa hatarini hivyo mwisho wa siku akachukua maamuzi ambayo yalipelekea vifo vya watu wengi.

Kilichofanyika mwishoni haikuwa kumua badala yake waliamua kumkabidhi kwa uongozi unaondaa mashindano hayo kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria kuchukua mkondo wake.

Roma hakuweza kurejewa na ufahamu wake kwa muda mrefu sana na ilibidi Ron awashauri wamchukue na kumpeleka Uingereza kwa Profesa Clark.

















SEHEMU YA 577.

Profesa Clark aliweza kumpokea Roma akiwa Wales na kumfanyia vipimo vya awali ili kujua hali ya afya yake lakini katika hali ambayo hakuitegemea alishangaa kuona uvimbe uliokuwa katika ubongo wake ulikuwa umeongezeka ukubwa wake kwa kiwango kikubwa sana ambacho kilikuwa ni tofauti na mwanzo kabisa.

Hali ya Roma ilimfanya kuwa na wasiwasi mkubwa kiasi kwamba alijikuta hata yeye akikosa cha kufanya na ilibidi awape maelekezo Rose na Magdalena juu ya hali ya Roma na kuwaambia kwamba wanapaswa kuelekea London kwani ndio kwenye hospitali maalumu alioijenga mahsusi kwa ajili ya kumtibia Roma.

Magdalena na Rose waliweza kuona wasiwasi aliokuwa nao Clark lakini hawakubisha na kumsikiliza na kuondoka Wales na kwenda London.

Ukweli ni kwamba katika kipindi chote ambacho Clark alimsaidia Roma kimatibabu hakuwahi kumuona akiwa na hali kama hio ya kumchanganya , mwili wake ulikuwa ukifanya kazi kawaida licha ya kwamba uvimbe katika ubongo wake ulikuwa umeongezeka ukubwa, tatizo lake lilimfanya kukosa kujua namna ya moja kwa moja kumponyesha Roma kwa kumpa madawa.

Wakati Clark akiwa katika mawazo upande wa Roma alikuwa ni kama vile yupo kwenye ndoto.

Ilikuwa ni ndoto ambayo ni kame vile alikuwa mawinguni akielea huku mbele yake akiona mtu wa kufanana nae kwa kila kitu na yeye mwenyewe.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma aliekuwa ndotoni akiangalia sura ya mtu mwingine inayofanana na ya kwake.

“Mimi ni wewe?”Ile sura ya mtu mwingine ilijibu huku ikitoa tabasamu la kifedhuli.

“Wewe sio mimi lakini unatoa msisimko ambao nishawahi kuhisia hapo kabla”

“Haha.. hata mimi nishawah kuhisia msisimko unaotoa”

“Kwanini unafanana kwa kila kitu na mimi na kwanini nipo hapa?”Aliuliza Roma , ilikuwa ni kama vile nafsi mbili zilikuwa zikiongeleshana nafsi ya Roma halisi na nafsi nyingine.

Upande wa nafsi ya Roma ilikuwa na wasiwasi na kutaka kujua kinachotendelea katika ulimwengu wa kawaida juu ya hali walizokuwa nazo wapenzi wake, yaani Magdalena na Rose ,alikuwa na wasiwasi wa kutoweza kufahamu watakuwa katika hali gani wakati huo.

“Unaonekana kuwa na wasiwasi , usiwe hivyo kwasababu kila kitu nimekusaidia”

“Wewe ndio ulionisaidia kupambana na wale majitu?”

“Hapana nimejisaidia mwenyewe kwasaabu wewe ni mimi”

“Hapana wewe sio mimi , umesema umenisaidia je wewe ndio Roho ya mnyama wa maafa iliofungiwa ndani ya Cauldron?”

“Nadhani sasa unaelewa , vipi mtoto unaonaje utamu wa nguvu yangu niliokupatia?”

“Kwanini umenileta hapa?Una ufahamu wako mwenyewe?”

“Nimekuleta hapa ili kukuambia kwamba kile chungu hakiwezi kunishikilia kwa muda mrefu , walionifungia h ni wanafiki tu , wanadhani kuharibu mwili wangu ndio nini , nilizaliwa na nguvu ya maafa hivyo mimi ni wa milele na milele , imenichukua muda mwingi mpaka kuamka katika usingizi wangu lakini shukrani muda si mrefu nakwenda kuwa huru’

“Haha..”

“Unacheka nini?”Iliuliza nafsi ya mnyama wa maafa.

“Nakucheka wewe ,unasema umeishi miaka mngi lakini bado tu unapenda kujifariji”

“Mpumbavu wewe , sijafanya hivyo bali nilikuwa nikikuelezea ukweli”

“Kama kweli ulikuwa na nguvu kipindi hicho kwanini ukaishia kufungiwa kwenye Cauldron kwa miaka yote hio , labda nikuambie kitendo cha wewe kufungiwa inamaanisha huna nguvu kubwa”

“Hivi unajua kama sio mimi ungeuliwa na wale majitu wewe mpuuzi”

“Na wewe usisahau ni roho tu ambaye upo kwenye dhana yangu , mimi ndio Master wako na unafanya kazi kwangu”

“Wewe mtukutu.. unathubutu vipi?”Nafsi ya Mnyama ndani ya Caulrdon ilionekana kuwa katika hasira.

“Kwanza kwanini ukaamua kutumia sura yangu kuongea na mimi , una uharibu uso wangu wa kihandsome”Nafsi ya Roma iliendelea kujibizana na nafsi nyingine iliokuwa ndani ya mwili wake.

“Ipaokuwa sijui hapa ni wapi lakini najua kimwili sina ufahamu , naamini kuna kitu unataka kuniambia ndio maana hutaki nikirudi katika mwili wangu , hivyo niambie na usije ukaona ukinitishia unawea kuniweza kwani siogopi vitisho tokea nilivyokuwa mdogo”

“Upo sahihi lakini sio ombi wala kukutishia bali ninakwenda kukupa nafasi”

“Nafasi!!?”

“Ndio nafasi ya wewe kuwa mmiliki wa dunia yote , nafasi ya kupita vizuizi vyote vya dunia na siri zake nitakufanya usionekane lakini kwa wakati mmoja ukiogopesha , nakwenda kukupa nafasi ya kuwa zaidi ya Mungu”

“Unanisaidiaje wakati wewe mwenyewe huonekani na umezungumzia kuhusu Mungu , je unaamini Mungu yupo?”

“Kila kitu kina mwanzo na kabla ya mwanzo wetu kuna alietuanzisha ,nakuambia unakwneda kutokuonekana kama Mungu kwasababu mbinu yako ya mafunzo ya kijini unayojifunza ni ya kipekee sana na sijui nani ambaye ameitengeneza , ni mbinu ambayo sijawahi kuona hata wale majini wa zamani kuitumia na kama sio kwa mbinu yako hii nisingekusaidia lakini hata hivyo nguvu ya kiroho ya ulimwengu huu imeshuka kwa kiasi kikubwa na kuwa nyembemba tofauti na zama zile, hivyo itakuwa ngumu kwako kufikia levo ya kutawala Radi , kama utakubali kunipatia mwili wako nitakusaidia kunyonya kila aina ya nishati katika vyanzo vyote juu ya dunia kwa kupitia nafsi yangu isiokufa na nikishamaliza kufanya hivyo utakuwa na uwezo mkubwa sana na utaweza kupita levo ya kutawala Radi na kuwa mkuu zaidi, hutovuna tena nishati ya mbingu na ardhi bali wewe ndio unakwenda kuwa nishati yenyewe na ulimwengu utakuwa chini yako , utabudiwa na kile kiumbe chenye pumzi”

“Kwahio katika kuonyonya kwako hizo nishati na binadamu anahusika ,si ndio?”

“Kiumbe dhaifu ni chakula cha wenye nguvu , hivi ndivyo dunia inavyofanya kazi”

“Wewe ni shetani , siwezi kutumia binadamu wenzangu kwa ajili ya kupata nishati na kupanda levo , ndio maana ulifungiwa kwa uovu wako, ulistahili kabisa”

“Unathubutu vipi kuniongelesha hivyo?”

“Utanifanya nini sasa kama nimeongea hivyo , ni kheri niishi bila ufahamu maisha yangu yote kuliko kukupatia mwili wangu , wewe ni mtumwa tu kwangu , inashangaza kukuona unaota ndoto za mchana kutaka kumiliki mwili wangu”

“Hehe .. unakiburi sana lakini ngoja nikuambie utafikia hatua hutokuwa na chaguo kwani muda si mrefu utakuwa mgonjwa na hutoweza kutawala fikra zako na isitoshe bado huna nguvu kubwa , itafikia mahali utahitaji msaada wangu na ukiniita nikusaidie ndio wakati ambao nitauchukua mwili wako na kuua nafsi yako na kuishi milele haha..”

“Bado tu unathubutu kunitishia , labda nikuambie utabakia kuwa chini yangu na nitakutumia kufika levo za juu na baada ya hapo nitakutupa na kukufungia milele”Aliongea Roma na kufanya ile sura ya nafsi ya Chaos Cauldron imwangalie kwa dharau na kisha ikapotea kwenye macho yake.

******

Ilikuwa ni usiku wa manane ndani ya jiji la London na Roma alikuwa hajarejewa na fahamu kwa siku tatu mfululizo.

Tokea Clark amwingize Roma hapo ndani na kuanza kumfanyia matibabu alionekana kabisa kukata tamaa kwani tatizo la Roma lilikuwa la aina yake , ijapokuwa ubongo wake ulikuwa na uvimbe lakini katika vipimo vyake vya kitabibu ilionyesha ubongo wa Roma ulikuwa ukifanya kazi kwa spidi kubwa.

Clark alikuwa amechoka mno kutokana na kukosa usingizi kwa muda mrefu na pia hakuwa na mafunzo ya kijini kama Magdalena na Rose, ukweli alijitahidi kuficha hisia zake na kuvaa taaluma yake lakini licha ya kuona hakukuwa na majibu alijihisi kunyongea sana na uvumilivu ulikuwa ukielekea kumshinda.

“Clark pumzika sasa, ilimradi mwili wake upo sawa kwa sasa nadhani ataamka tu”Aliongea Rose.

“Siwezi kulala , Uvimbe wake umeongezeka ukubwa kwa kiasi kikubwa sana , sijawahi kuona akiwa katika hali kama hii nina wasiwasi na sijui kama nitaweza kupata usingizi”Aliongea na kumfanya Rose mwenyewe kuwa katika hali ya wasiwasi , haikuwa mara yake ya kwanza kumuona Roma kuwa katika hali mbaya na ndio maana alikuwa na wasiwasi.

“Ni kwa muda gani amekuwa na hii hali?”

“Sijui ni kwa muda gani lakini naweza kusema ni tokea alivyokuwa mdogo na hali yake ilikuwa mbaya zaidi kutokana na athari alizopata kutokana na majaibio ya kisayansi aliofanyiwa na Zeros, nilisomea udaktai kwa ajili ya kumsaidia lakini tofauti na kupunguza dalili nimeshindwa kumponyesha moja kwa moja”

“Kama ni hivyo je unaamini ataamka , je atapatwa na tatizo zaidi huko mbeleni?”

“Sina uhakika lakini sayansi haiwezi kuelezea hali aliokuwa nayo na kama asingejifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi angekuwa katika hatari zaidi, kadri anavyopitia hili tatizo ndio anazidi kuwa katika hatari kubwa zaidi na itafikia muda atashindwa kujitawala kabisa na maumivu yake yatakuwa ni afadhali ya kifo”Aliongea na kuwafanya washindwe kabisa kuvuta pumzi kwa wasiwasi.

“Nadhani hatupaswi kuwa katika hali ya wasiwasi kwasasa na tunachopaswa kufanya ni kuamini uwezo wake”Aliongea Magdalena na Clark na Rose walitingisha vichwa vyao kukubaliana nae na kukaa kwenye sofa.

“Ah.. ulikuwa ni usingizi mzuri kweli”Waliweza kusikia sauti nyuma yao ambayo iliwafanya wageuke.

Alionekana Roma akiamka mwenyewe na kukaa kitako katika kitanda cha matibabu.

Furaha ndio kitu pekee ambacho kilionekana katika sura za warembo hao na hata Roma mwenyewe alifuurahishwa kuona hakuna hata mmoja ambaye alikuwa amepatwa na shida.

Ukweli Roma aliamka muda kidogo na alikuwa amesikia maelezo yote ya Clark juu ya shida yake hivyo hakuwa na haja ya kuuliza sana kwani kwa kauli ya Clark tu alijua fika ugonjwa wake utakuwa umeibuka upya na kuwa hatari zaidi.

Uvimbe katika ungongo wake ulikuwa ni kama kidonda cha mgonjwa mwenye ugonjwa wa kisukari ambacho kinaanza kupona na kurudia katika ukubwa wake , mpaka hapo Roma alijua kila kitu kimesababishwa na Cauldron na mawazo ya kutafuta dhana mbadala yalimwingia akilini mwake palepale , alijiambia kama ataendela kukitumia basi ni kweli itafikitia siku hatokuwa katika akili zake yeye mwenyewe na anaweza kubadilika kabisa na kuwa mtu mwingine.

Roma aliwauliza kile kilichotokea na Magalena na Rose walimwambia kila kitu kilichotokea na namna ambavyo Athena alitokea na kuwaua wale majitu wote kwa kutumia moyo wa Gaia na kuongea kauli ya ufufuo wa Moyo wa Gaia kuanza,

Roma mara baada ya kusikia kuhusu Moyo wa Gaia moyo wake ulifurukuta na hakuwa akijua ni kitu gani kinakwenda kutokea , hakujua kama Athena kweli anaweza kufanikisha kufufua ndugu zao waliolala , lakini kwa wakati mmoja alihofia athari zake kwa dunia zitakuwaje , lakini kwa wakati huo alijiambia kabisa hilo sio la kwake la kuwazia na atasubiria kuona matokeo yake ni nini, maana hata kama aseme anataka kumzuia Athena ukweli ni kwamba asingeweza kwani uwezo wake ulikuwa mdogo sana.

Baada ya maongezi ya muda mfupi Roma hakutaka kuendelea kukaa hapo , alikumbuka tokea atoke Tanzania ni zaidi ya siku sita sasa na anapaswa kurudi mapema kama alivyomwahidi mke wake kurudi mapema ndani ya wiki moja.

Hivyo baada ya Magdalena na Rose kurudi visiwa vya wafu yeye moja kwa moja aliunganisha kurudi Tanzania.

Muda ambao aliweza kufika ilikuwa tayari ni mchana wa saa sita siku ya jumapili na mara baada ya kuingia nyumbani hakuweza kuona mtu yoyote eneo la sebuleni na hali ya hewa ilionekana kuwa tulivu mno.

Alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Edna na ile anakaribia mlangoni aliweza kusikia sauti ya Mke wake na Lanlan na ilionekaa kuna mchezo ambao walikuwa wanacheza huku Lanlan akisikika kumtuhumu mama yake kwa kuwa mdanganyifu kwani yeye ameshinda.

Tokea Edna aachane na maswala ya kampuni muda mwingi alitumia kushida na Lanlan anaporudi shuleni na pale anapokuwa shuleni alishinda na Rufi na kumfundisha baadhi ya mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kumuona baba yake na kumkimbilia kumkumbatia kwa furaha.

“Wife njoo na wewe”Aliongea Roma kwa tabasamu akimpa ishara Edna kumsogelea ili kumkumbatia na Edna alifikiria kidogo na kiabu aibu alisimama na kumsogelea Roma na kumkumbatia.

Yale mazoea ya kumuona Roma kila wakati yalimfanya siku zote saba kumkumbuka sana na kumsubiria kwa hamu kurudi kwake na mara baada ya kumuona karudi alijisikia furaha ya kutamani kuwa kama Lanlan lakini alijitahidi kujizuia.

Baada ya wote kutoka chumbani na kushuka sebuleni Roma hakuongea sana kuhusu kile kilichotokea Sicilly bali alimuuliza kilichotokea hapo wakati alipokuwa hayupo na ukweli ni kwamba hakukuwa na kubwa ambacho kilitokea zaidi ya Edna kupewa zawadi na Amina kutokana na kumsaidia kuweza kushinda zabuni kutoka serikalini na Roma alifurahi kuona Amina na Edna wana ukaribu mzuri.

***********

Ni siku mbili tokea Roma aweze kurudi, katika siku hizo aliweza kukaa karibu na Lanlan kuanza kumpima akili yake, alitumia njia mbalimbali kujaribu kumpima uwezo wake na njia moja wapo ambayo ilimridhisha sana ni njia ya kucheza nae mchezo wa Chess.

Roma alitumia masaa sita kumwelekeza Lanlan namna ya kucheza mchezo wa Chess na ajabu ni kwamba mara baada ya Lanlan kuweza kujua namna mchezo huo unavyochezwa alimletea Roma upinzani mkubwa sana.

Ilikuwa ajabu hata kwa Edna ambaye alikuwa akiangalia namna ambavyo Lanlan aliweza kuelewa kwa haraka mchezo huo na kuanza kucheza kisawa sawa mpaka kumshinda Roma.

Roma mwenyewe alijikuta akishangazwa zaidi na zaidi na uwezo wa Lanlan kwani kwa upande wake mchezo wa Chess alikuwa na uzoefu nao kwa miaka mingi sana na alikuwa akicheza sana , lakini tofauti yeye na Lanlan ni kwamba ilimchukua muda mrefu mpaka kuweza kuujua namna ya kuucheza na hata kushinda.

“Wife hakika tunabinti ana akili sana”Aliongea Roma mara baada ya Lanlan kuweza kumshinda Roma michezo mwili mfulululizo.

“Dady Lanlan kashinda , hivyo unipeleke kuona wanyama”Aliongea Lanlan kwa shangwe maana aliambiwa akishinda michezo miwili mfufluizo atapelekwa kuona wanyama.

“Lanlan baba atakupeleka kuona wanyama”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kufurahi.

“Daddy is best”Aliongea na kumfanya Roma kuchekeshwa na kibonge huyo na kumwangalia Edna ambaye alikuwa amepambwa na tabasamu.

“Tokea urudi umekuwa karibu sana na Lanlan na kama nipo sahihi ,ni kama unaupima uwezo wake wa akili , si ndio?”

“Upo sahihi na leo hii nimekamilisha uchunguzi wangu , Lanlan ana uwezo mkubwa wa akili”

“Unataka kumfundisha na yeye namna ya kuvuna nishati ya mbingu na ardhi?”Aliuliza Edna.

“Umenipata vizuri , nadhaini ni muda sahihi kumrithisha Andiko la Urejesho lisilo na kikomo”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Lakini si uliesema bado ni mdogo na hupaswi kumfundisha kutokana na hatari?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kuwaza.

Ukweli ni kwamba mwanzoni hakupanga kumfundisha Lanlan namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi lakini kutokana na hali yake ya kiafya kuanza kuwa tishio aliona ni muda sahihi wa kumfudisha Lanlan ili hata kama kuna jambo lolote ambalo lingemtokea mbinu hio asipotee nayo.

“Mwanzoni nilipanga iwe hivyo lakini nimegundua Lanlan ana kipaji cha juu sana na itakuwa vizuri kama nitamfudisha akiwa na umri mdogo na isitoshe kama atakuja kuelewa kanuni ya Kimaandiko ya urejeshi isio na kikomo hatochukua muda mwingi kufikia levo ya Nafsi baada ya kukamilisha hatua zote, njia hii ndefu na itategemea zaidi uelewa wake pamoja na kipaji na akifanikisha nadhani hatutakuwa na wasiwasi wa usalama wake”Edna alijikuta akitingisha kichwa kumwelewa Roma.

“Lanlan kwanzia leo baba atakufundisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , si siku zote unataka kujua namna ambavyo baba anajua kupaa , unaweza kuwa kama mimi kama utafanya kile kitu nitakachokuambia”

“Really? Daddy quick teach me”Aliongea Lanlan huku akiwa ametoa macho kwa furaha.

“Kabla ya kukufundisha unatakiwa kuniahidi mimi baba yako , kwamba hutomwambia mtu yoyote mbinu yako ya mafunzo hususani kwa mtu usiemjua , umenielewa?”

“Je mama siruhusiwi kumwambia?”Aliuliza.

“Ndio hata mimi usiniambie kwasababu mama hatokuuliza hivyo usiniambie pia , usimwabie mtu yoyote”Aliongea Edna na kumfanya Roma kumwangalia mke wake kwa tabasamu akionyesha kumwelewa na Lanlan alitingisha kichwa.

Baada ya kukubaliana Edna aliaga kwenda Supermakerk kununua mahitaji ya nyumbani huku Roma yeye akimchukua Lanlan kwa ajili ya kumfudisha.

Roma alianza kumfundisha kwa kumkaririsha maneno ambayo yalikuwa kwa lugha isioeleweka na Lanlan alirudia maneno yale kwa kuyakariri na baada ya hapo Roma alimwelekeza namna ya kufanya Tahajudi huku akiongea maneno hayo kwa kuyarudia kwenda mbele na nyuma na Roma aliridhishwa na namna ambavyo Lanlan alifanikisha kukariri kwa haraka maneno yake ya kimaandiko.

Kwake alijisikia vizuri sana kumfundisha Lanlan na ilikuwa ni kama vile ilikuwa imepangwa kukutana na Lanlan na kumfundisha namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi kwa njia ndefu.

“Lanlan kumbuka nilichokuambia , usiharakishe mambo , mbinu ya Maandikio ya urejesho usio na kikomo inategemea zaidi uelewa wako kuliko mazoezi ya kila siku, haijalishi ni kwa namna gani umeelewa andiko lenyewe ila usijilazimishe kwa kufikiria kipi ni sahihi na kipi sio sahihi , usifikirie kuhusu kufeli na kufanikiwa, chukulia uelewa wa kila unachokiona mbele yako ni sawa bali sio sahihi ama kutokuwa sahihi?”

“Je kama Lanlan haelewi kitu , ninapaswa kukuuliza?”

“Swali zuri Lanlan , usiniulize kwasababu siwezi kukujibu ni wewe mwenyewe unaepaswa kutafuta majibu kwasababu kila mtu ana mawazo tofauti, lakini kumbuka hakuna kukata tamaa kwasababu unadhania ni ngumu kuelewa, siku zote amini kwamba maadamu bado ungali hai ni wewe pekee unayeweza kuishinda nafsi yako mwenyewe”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kutingisha kichwa na palepale katoto hako kalikunja miguu yake kwenye kitanda cha mama yake na kufumba macho kana kwamba yupo kwenye hali ya kutafakari na Roma alimwangalia kwa dakika kadhaa na kisha akatoka nje ya chumba hiko kumuacha.





















SEHEMU YA 578.

Roma mara baada ya kurudi Sebuleni aliweza kukutana na Edna ambaye alikuwa akitokea jikoni na aliegamia kwenye sofa huku akimwnagalia Roma.

“Yameendaje?”Aliuliza.

Swali lake ni kama vile amemtuma mtoto wake kufanya mtihani na sasa anataka kujua mtihani uliendaje , kwa Edna kulingana na aina ya familia yake alijua kabisa maisha yao sio kama binadamu wengine hivyo Lanlan kuwa na uwezo wa kujilinda yeye mwenyewe ilikuwa muhimu.

“Dear wife , natakuwa kukujibu vipi swali lako , kwanini umeuliza kwa staili hio?”

“Nauliza kama ameelewa au imekuwa ngumu kwake kuelewa?”

“Kwasasa sijui kama ameelewa lakini amefanikisha kukariri kila kitu nilichomwambia , sikuwa na uwezo mkubwa wa akili kama yeye lakini niliweza kufika levo ya sita ndani ya miaka kumi tu, kwa kutumia vidonge ambavyo tunakwenda kumpatia haitokuwa ngumu kufikia levo ya saba maadamu kipaji chake kitakuwa kikubwa, kuhusu levo ya nane na tisa itategemea zaidi na yeye mwenyewe”

“Kwanini usimwambie kila kitu namna ambavyo ulifanikiwa na uzoefu wako kwa ujumla , si umwambie kila kitu ili iwe rahisi kwake na asiumize kichwa”Aliongea Edna.

“Uzoefu wangu …. ?,Moja wapo ya Uzoefu wangu ni kifo cha mpendwa wangu na uzoefu mwingine ni mimi kupitia hali ya kifo na uhai ,unadhani ninaweza kumfundisha uzoefu wa namna hio?”

“Unamzungumzia Seventeen?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma aone ameropoka.

“Usifikirie sana , kipindi hicho sikuwa nikikufahamu na isitoshe kila mtu ana historia ya maisha yaliopita”

“Lakini sijasema chochote , kwanini unajielezea”

“Hehe ni kweli , nilichomwambia Lanlan ni kwamba njia hii ndefu ina hatua tisa ambazo ni: Kujifikiria mwenyewe , Kufikiria wengine , Hatima , Mwisho wa safari , Kukosa swali , Giza , Nuru , Uhai na kifo na Kuzaliwa upya, kila anapopitia hatua moja ndio ugumu unavyoongezeka ,Hatima ni fumbo kubwa kwa binadamu na Giza ndio kitu kigumu kupitia, nitampa motisha kwa kila hatua atakayofikia kwa kumpatia kile nilichomwahidi, sitegemei atafikia hatua ya Nuru ndani ya miaka michache ijayo lakini natumani atakuwa mvumilivu”

“Majina ya hizo hatua ni magumu sana na unakisumbua kichwa cha Lanlan”Aliongea Edna.

“Ni sahihi, lakini hii ni mbinu ambayo ni majaribio ya kipaji cha mu kuliko kitu chochote kile , nadhani sijafanya makosa kumchagua Lanlan kama mrithi wangu na sitojihisi huzuni kumwangusha Master kwa kufanya maamuzi ya kunirithisha na mimi , angalau andioo hili halitoshia kwangu tu”

“Mbona unaongea kama vile unakufa , naamini lazima itatokea siku ukafundisha tena”Aliongea na kumfanya Roma aone kidogo tu afichue siri yake , ukweli kuhusu ugonjwa wake alipanga kutokumwambia Edna na hata Rose na Magdalena aliwaambia iwe siri kwa wakati huo kwanza.

“Nimesahau kukuambia Queen kajifungua , Omari alijnipigia simu”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Mbona kama muda ni mapema sana”

“Ndio anasema mtoto kazaliwa kabla ya muda lakini anaendelea vizuri”

Roma alijikuta akimfikiria Omari , ukweli ni kwamba alijitofautisha na Omari kwa uwezo wake mkubwa wa kuweza kumkubali mwanamke ambaye tayari ana ujauzito wa mtu mwingine.

Licha ya kwamba Omari alikubali kwamba angemlea mtoto huyo kama baba lakini mwisho wa siku angebakia tu kuwa mtoto wa Yan Buwen na kitu kikubwa ni kwamba swala hilo lisingefichika kwani rangi ya mtoto huyo ingekuwa tofuati kabisa na ukoo wao na ingefika mahali mtoto angehitaji kujua kwanini yupo tofauti na wazazi wake.

Roma alijaribu kujiweka katika viatu vya Omari na alijiambia asingeweza kufanya hivyo hata kama mwanamke amempenda vipi,

Muda wa chakula cha usiku, ikiwa ni zaidi ya masaa mawili kupita hatimae Lanlan alishuka kutoka juu huku akionekana kuwa na macho yenye viashiria vya usingizi.

“Sio mbaya angalau umetumia muda mwingi , Mtoto mzuri sana wewe”Aliongea Roma akimsifia Lanlan kwa kumshika shika kichwa.

“Lanlan amefikiria kwa muda mchache lakini akakwama na alijikuta amepotelea usingizini na nimeamka sasa hivi nina njaa”Akiongea Roma na kauli yake ilimfanya kumeza maneno yake , alidhani Lanlan alikuwa akifikiria kumbe alikuwa amelala na kaamshwa na njaa lakini hata hivyo hakulaumu kwani akili ya Lanlan haijakomaa vizuri.

*****

Siku mbili zilizofuata Roma Edna na Lanlan waliondoka kwenda Iringa kama ratiba ilivyowataka kufanya hivyo.

Haikuwa safari ndefu kutokana na kutumia gari binafsi na mara baada ya kufika Iringa mjini walikuja kupokelewa na Ashley.

Roma alifurahi kumuona mrembo huyo kuwepo Iringa na ilikuwa ni kipindi kirefu kidogo hawajaonana , ukweli ni kwamba alikuwa amesahau kama Ashley alikuwa mdogo wake wa damu kabisa na wazo hilo lilimjia mara baada ya kuonana nae.

Upande wa Edna katika wiki hio ambayo Roma alikuwa nje ya nchi alikuwa ashakutana na Ashley zaidi ya mara mbili kabla ya kuanza safari ya kuja Iringa..

“Bro ninafuraha sana kwa mara ya kwanza tunakusanyika kama familia”Aliongea Ashley na kumfanya Roma kutabasamu na alifikia hatua ya kujiuliza weupe wa Ashley karithi kwa nani kwani baba yake na mama yake wote walikuwa ni weusi.

“Vipi kila kitu kipo sawa huko nyumbani?”

“Kila kitu kipo sawa lakini mama na baba wamekuwa kwenye malumbano ya hapa na pale kuhusu Denisi”Aliongea na kumfanya Roma kukunja sura kidogo.

“Denisi!!, kafanya nini mpaka kupelekea malumbano?”Aliuliza Roma huku akipotezea swali la uwepo wa baba yake nyumbani.

Ndio Raisi Senga alikuwa Iringa katika ikulu ndogo kwa ajili ya mapumziko na ilikuwa ni fursa kwake pia kuwa karibu na familia yake yote kwa mara ya kwanza , alijua hakuwa na namna zaidi ya kumkubali Roma lakini kubwa zaidi alikuwa na changamtoto binafsi ambazo aliamini kumuweka Roma karibu zingemfanya kuzitatua na hata yeye mwenyewe alikuwa akijiuliza kama anafanya yote hayo kumkubali Roma kutokana na matatizo yake au ni mapenzi yake mwenywe.

“Denisi tokea amerudi alikuwa akifanya kazi jeshini lakini licha ya hivyo kaanza tabia nyingine mpya ya kuambatana na watoto wa matajiri na kufanya starehe na anasa, ijapokuwa tabia yake haiingilianni na kazi yake lakini inamkwaza sana baba kutokana na kuhofia taswira yake kuchafuka kama raisi wa nchi lakini Mama yeye yupo upande wa Denisi akimtaka baba asimfokee na kumuacha afanye kinachompa furaha na ndio chanzo cha ugomvi wao, ijapokuwa baba yupo sahihi lakini najua wasiwasi wa mama ni nini, anaogopa Denisi kuondoka nyumbani kwa mara nyingine”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia Roma.

“Nadhani ni tabia ya kurithi hata kaka yake hapa hana tofauti”Roma mara baada ya kusikia kauli ya Edna hakupenda lakini hakuwa na haja ya kupinga kwani ilikuwa karibu na ukweli, wakati huo alikuwa bingwa wa anasa huenda zaidi hata ya Denisi anaezungumziwa,

Nusu saa mbele waliweza kufika katika makazi hayo , ilikuwa ni mara yao ya kwanza lakini kwa pande wa Lanlan ilikuwa ni mara yake ya pili na alionekana kuwa na mchecheto mno.

Roma alifurahishwa na mazingira ya uoto wa asili wa misitu , ukiachana na Songea eneo hilo lilikaa kizungu zaidi na hali yake ya hewa ya ubaridi iliridhisha na kumfanya kuona kama vile yupo Ulaya.

Baada ya kufika Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kutoka na kukimbilia ndani ya jumba hilo huku akiita jina la babu yake.

Kulikuwepo na baadhi ya watu waliokuwa wakiwasubiria nje ya nyumba hio na Afande Kweka mara baada ya kusikia jina lake linaitwa aliweka kikombe chake cha chai chini na kusimama na kumbeba Lanlan juu juu.

“Lanlan , did you mis your Great grandfather?”

“Yes but Lanlan wants to eat roast pork”Aliongea kwa furaha akimaanisha anataka kula nyama ya kitimoto na kumfanya Afande Kweka kucheka huku akishikilia vimashavu vyake kwa furaha.

Damasi mke wa raisi Senga alikuwepo na alimsogelea Lanlan na kumshika mkono.

“Lanlan unafikiria kula nyama tu umesahau kunisalimia bibi yako , nisalimie na nitahakikisha unakula kila unachotaka”Aliongea na kumfanya Lanlan palepale amsalimie.

Baada ya kuingia ndani ya jumba hilo kila mmoja aliekuwepo hapo ndani alimsalimia Roma na Edna , kulikuwa na ulinzi mkali mno kiasi cha kumfanya Roma kuamini uwepo wa baba yake hapo ndani.

“Nyie watu mmekuja mapema kesho kuna mahali mnapaswa kwenda kuniwakilisha”Aliongea Afande Kweka mara baada ya kusalimiana na Roma.

“Unamaanisha sisi wawili tu? Mbona tutakuwa wachache sana?”Aliongea Roma.

“Haijalishi ni wangapi wanaenda ila ukubwa wa mtu ndio kinachoangaliwa zaidi hata kama ukoo mzima ukienda haitalingana na nyie wawili mkienda”

“Nimependa, ni mara chache sana kunisifia wewe”Aliongea huku Edna akiwa kimya muda wote.

“Edna nimesikia umejiuzuru nafasi yako kama raisi wa kampuni?”Aliuliza Damasi.

“Ndio mama”

“Umefanya vizuri muda mwingine sisi wanawake tunapaswa kujikita kwenye maswala ya kifamilia zaidi , watoto wanakuwa kwa haraka sana na haileti maana kuwa nao mbali kimalezi, lakini pia nikwambie tu sio rahisi kuwa mama wa nyumbani”Aliongea Damasi huku kidogo akiwa na huzuni katika uso wake ni kama vile kuna kitu kinachomsumbua na hata Edna aliweza kuona hilo , huenda sababu ilikuwa ni juu ya Denisi.

“Wifi yangu sio mama wa nyumbani moja kwa moja bado ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Ernest ni kama anamsaidia tu kwani bado ana maamuzu makubwa ndani ya kampuni”Aliongea Ashley huku akiwa amemshika Edna mkono , ukichana na Edna kubadilika kuwa wifi yake lakini walikuwa ni marafiki tokea utotoni kutokana na kusoma shule moja.

“Ni vizuri pia , kampuni ni mali yake na lazima iwe hivyo, isitoshe muasisi ni bibi yake hivyo hawezi kuiuza”Aliongea.

“Upo sahihi mama lakini kwasasa sina wasiwasi kwasababu kampuni kwasasa ina mfumo wa kujiendesha ambao haunitegemei kwenye mambo mengi ndio maana nilijiamini kutoa nafasi yangu kwa Ernest”Aliongea Edna.

Ukweli kitendo cha Edna kuachia ngazi kilimfurahisha sana Blandina mama yake Roma na aliweza hata kumpigia simu na kumpa hongera kwa kufanya maamuzi sahihi lakini Edna alivyoona na Mama Ashley anampongeza kwa kitendo hicho aliona huenda kweli alikuwa bize sana na kampuni kipindi cha nyuma na maamuzi alioyafanya yalikuwa sahihi zaidi.

“Damasi chakula cha mchana bado tu sitaki mjukuu wangu kuendelea kukaa na njaa”Aliongea Afande Kweka.

“Chakula kipo tayari baba lakini Denisi mpaka muda huu hajafika tu na alisema atakuwepo muda wa chakula cha mchana”

“Kama hisia zangu ni sahihi naamini sasa hivi atakuwa amelewa huko na kahaba akiwa pembeni yake”Sauti kutoka upande wao wa kushoto iliweza kusikika na palepale alionekana Raisi Senga alievalia koti kubwa akiiingia huku akiwa ameshikilia mkasi mkononi wa kukatia miti alikuwa ameongoza na msaidizi wake ambaye alikuwa ameshikilia mfuko wa maparachichi.

“Grandpaa..!!”Lanlan aliongea na kutoka kwenye mikono ya babu yake mkubwa na kumkimbilia Raisi Senga na kumkumbatia kwa furaha na kumfanya Roma na Edna kushangaa pasipo ya kuelewa ni lini Lanlan aliweza kufahamiana na Raisi Senga maana katika kumbukumbbu zao hakuna siku ambayo Lanlan aliweza kukutana na baba yake Roma.

Raisi Senga alimbeba Lanlan juu juu kwa furaha na kisha akamgeukia Edna na Roma na kuweka uso wa tabasamu.

Muda huo huo iliingia gari aina ya Range ya rangi nyeusi na akashuka Denisi aliekuwa katika kombati za kijeshi zenye nyota moja begani na alianza kuachama kama mtu mwenye njaa kali huku akishika tumbo lake akisogelea mlango wa kuingilia na kumfanya Roma kunasa Aura yake na kukunja sura.
 
SEHEMU YA 579.

Tokea Edna afahamu Roma ni mtoto wake hawakuwahi kuonana nae na siku hio ilikuwa ni kama wanakutana sasa na kwa wakati huo hakujua amwite mheshimiwa au baba mkwe.

“Edna karibuni nyumbani”Aliongea mheshimiwa Senga kwa tabasamu mara baada ya kumuweka Lanlan chini.

“Asante sana mheshimiwa”Alijibu Edna kwa aibu.

“Umekosea mimi ni baba mkwe wako hivyo ni sawa kuniita baba”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Roma amwangalie Edna na kisha macho yake akayahamishia kwa raisi Senga , ukweli kauli yake ilitafsirika alikuwa sasa akimtambua Roma kama mtoto wake hivyo kumchukulia Edna kama mke wa mwanae na kila mmoja alifurahishwa na kauli yake ikiwemo Afande Kweka na Damasi lakini kwa Roma ilikuwa tofauti.

“Asante sana baba”Aliongea kwa mara nyingine kwa aibu kidogo na kumfanya Raisi Senga kutabasamu na muda huo huo na Denisi aliingia hapo ndani na kumfanya kila mmoja kumuangalia, lakini yeye mwenyewe macho yake yote yalikuwa kwa Roma na alimsogelea moja kwa moja huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu.

“Kaka , Shemeji karibuni sana nyumbani”Aliongea Denisi kwa bashasha huku akinyoosha mkono kuwasalimia akiwa katika tabasamu pana.

Upande wa Roma na Edma hawakuweza kuzoea namna ambavyo alikuwa mkarimu kwani alionekana kama vile hawakuwahi kuwa na mgogoro.

Roma alichokifanya ni kutingisha tu kichwa tu akiwa kabisa hana mudi ya kuanzisha maongezi nae na upande wa Denisi hakuonyesha tofauti na alimsogelea Lanlan aliekuwa kwenye miguu ya baba yake.

“Huyu lazima atakuwa ni Lanlan si ndio , hebu njoo umsalimie Uncle wako hapa”Aliongea Denisi huku akichanua mikono yake kumpa ishara ya Lanlan kumsogelea amkumbatie lakini Lanlan baada ya kuona Denisi anamsogelea palepale alijificha nyuma ya babu yake Raisi Senga huku akiikumbatia miguu yake kwa wasiwasi.

“Lanlan una tatizo gani?”Aliuliza Afande Kweka.

“Lanlan hataki kubebwa …”

“Lanlan kuwa mtoto mzuri , huyo ni baba yako mdogo(Uncle)”Aliongea Damasi lakini Lanlan alitingisha kichwa kukataa kabisa kusogelewa.

Baada ya kuona Lanlan kamkataa waziwazi mbele ya watu Denisi palepale alirudisha mikono yake chini na kutoa kicheko hafifu.

“Labda ni kwasababu natoa harufu ya pombe ,hua watoto hawaipendi”

“Huenda ni kweli haipendi harufu yako, tuelekee mezani sasa kwa ajilki ya chakula wageni wetu wana njaa”Aliongea Afande Kweka huku akitangulia yeye na kila mmoja alitingisha kichwa na kutangulia.

Baada ya kukaa Raisi Senga alimwangalia Denisi kwa macho makali .

“Wewe mtukutu ni wapi umeenda kufanya ujinga awamu hii?”Aliuliza kwa kufoka kidogo.

“Baba sijaoenda kufanya ujinga nilikuwa tu nikibadilishana mawazo na baadhi ya watu , kama kweli nilikuwa nikifanya ujinga kama unavyosema nisingeweza kuja nyumbani mapema kumpokea Kaka na Shemeji”Aliongea kwa sauti ya upole.

Afande Kweka alimwangalia Raisi Senga akimpa ishara ya kupotezea wakati huo wa chakula na kumfanya amwangalie Denisi kwa dakikika na kuonyesha ishara ya kusikitika na kisha akaendelea zake.

Wakati wa chakula kila mtu alijaribu kuongea na Afande Kweka lakini mzee huyo alikuwa bize muda wote na Lanlan akionyesha hali ya kuridhika kabis ana kitukuu wake huyo.

Lanlan hakuwa na wasiwasi tena, baada ya kukaa mezani na kuona nyama ya kukaanga woga wote wa kumuogopa Denisi uliisha na kuweka umakini kwenye kula na kumfanya Afande Kweka kufurahishwa na hamu kubwa ya kula ya kitukuu chake.

Upande wa Edna aliekuwa karibu na Roma alimgusa kwa mguu chini ya meza akimpa ishara Roma amwangalie Lanlan , ilikuwa ni kama vile anamwambia Roma ilikuwa sahihi kwa wao kumchukua Lanlan kama binti yao na kumuasili kutokana na namna ambavyo alikuwa kivutio kwa macho ya kila mmoja, lakini zaidi kumfanya Afande Kweka kuwa mwenye furaha sana.

Upande wa Raisi Senga hata yeye alionekana kufurahishwa na mwonekano wa Lanlan.

Mara ya kwanza kukutana na Lanlan ilikuwa ni siku ambayo Roma na Edna walikuwa kwenye mgogoro uliopelekea Edna kuondoka nyumbani , siku alioenda kuonana na baba yake ndio alimkuta Lanlan nyumbani na kumfahamu kwa mara ya kwanza na kilichomfanya kumpenda Lanlan ni kutokana na kuwa na tabia kama ya Ashley alivyokuwa mdogo.

“Nikimuangalia Lanlan ni kama namuona Ashley alivyokuwa mdogo”Aliongea Damasi.

“Mke wangu na wewe umeliona hilo?”Aliuliza Raisi Senga na Damasi alitingisha kichwa huku akitabasamu.

‘Mama wewe si ulisema nilisumbua sana nikiwa mtoto na sikupenda kula?”

“Ulisumbua ndio lakini mara nyingi ulivyokuwa na hamu ya kula hukupenda kulishwa na ulivyokuwa ukishika kijiko ni kama Lanlan kabisa”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia Ashley na kutabasamu

“Bro gonga Cheers , nakubali sikuwa na tabia nzuri zamani na nimejutia makosa yangu, Sasa nimeamua kulitumikia taifa langu kwa kujiunga na jeshi na natumaini utanisaidia wakati nitakapohitaji msaada”Aliongea Denisi huku akiinua glass ya mvinyo juu akimpa ishara Roma kunyanyua ya kwake na wagongesheane

“Haina haja ya kuongea kwa heshima hivyo kwani sina taaluma yoyote na ninachojua ni kuongea matani tu”Aliongea.

“Usiongee hivyo najua unaona sio sahihi kunfanya kitu kama hiki cha kawaida lakini kwangu ina maana kubwa , kipindi kile baada ya Yan Buwen kufariki niligundua kwamba nilikuwa mtukutu sana na mwenye fujo lakini licha ya yote ukaendelea kunivumilia nina shukuru sana”Aliongea Denisi na kumfanya Damasi kumwangalia mtoto wake kwa huzunni

“Roma kaka yako hatimae kakomaa akili , nyie wawili ni ndugu natamani kuona mnakuwa na urafiki wa karibu na kumfundisha baadhi ya vitu ambavyo haelewi”Aliongea Damasi na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu kila kitu kilikuwa kama kweli vile lakini kutokana na uzoefu wake aliona anachokifanya Denisi hapo ndani yalikuwa maigizo tu.

“Mama hata usijali kaka sio mtu wa kukaa na vinyongo , Bro jana nimekutana na Aloni na amesema anapanga kuja kututembelea baada ya kusikia unakuja Iringa , hakubahatika kukutana na wewe na ameniambia nikufikishie ujumbe”Aliongea Denisi.

“Aloni ndio nani?”Aliuliza Roma.

“Ni ndugu wa shangazi yako Mama Theresia upande wa mume wake ana umri sawa na Denisi na anafanya kazi katika ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali , ni mchapa kazi mno”Aliongea Damasi.

Roma alikuwa akimfhamu MamaTheresia ni shangazi yake kwani ni mdogo wake Raisi Senga lakini ukweli ni kwamba watoto wa Shangazi yake huyo hakuwa akiwajua sembuse huyo ndugu wa upande wa mume wake.

Wakati wakiwa wanaongea kijakazi alikuja mpaka eneo hilo na kuwapa taafira kwamba Aloni amefika.

“Sir Mr Aloni amefika”Aliongea

“Ameweza kuja mapema mno , viajana wa siku hizi sio wavumilivu , hebu mwambie aingie”Aliongea Afande Kweka.

Dakika chache mbele mwanaume wa maji ya kunde mwenye sura ya kihandsome alievalia suti ya rangi nyuepe aliweza kuingia ndani ya eneo hilo huku mkonini akiwa ameshikilia boksi ambalo kwa haraka haraka lilionekana kuwa la Zawadi , alikuwa na tabasamu pana kwenye uso wake.

“Mniwie radhi janani kwa kuja mapema sana , Babu Jemedari tafadhari naomba usikasirike”Aliomngea , alionekana alikuwa kiijua sehemu yake katika ukoo huo.

“Ni sawa tu , lakini nilishakuambia uache kuniita Babu Jemadari linasikika vibaya kwangu”Aliongea Afande kweka.

“Lakini babu wewe ni mwanajeshi Jemadari mstaafu , wazazi wangu siku zote ni wenye kuniambia nijifunze kutoka kwako”Aliongea lakini hata hivyo Afande kweka hakukataa sifa hizo.

“Babu jemadari nimekuletea zawadi ndogo tu , nilikuja kwa haraka hivyo sikuweza kununua Zawadi nzuri ya kukufaa lakini natumaini utaipenda”Aliongea huku akimkabidhi mhudumu boksi ambalo ameshikilia na Mzee Kweka alilipokea na kufungua ndani na kukuta ni koti kubwa la baridi pamoja na gloves nzito na Afande Kweka alishukuru kwa zawadi hio.

Baada ya kumalizana na mzee huyo alisalimiana na mheshimiwa raisi kwa heshima zote na kisha aliwageukia Edna na Roma na baada ya kukutanisha macho yake na Edna alionekana kumwangalia bila kuojndoa macho yake huku akiwa katika hali ya mshangao.

“Wewe ndio utakuwa binamu yangu Roma na Shemeji yangu kama sikesi , mara nyingi nilisikia sifa zako tu kupitia sehemu mbalimbalo lakini sijawahi kukuona ana kwa ana , ni heshima kwangu kukutana na wewe kwa mara ya kwanza ,, haha Binamu aisee una bahati sana”Aliongea huku bado akimwangalia Edna kwa macho flani hivi ya kuchanganikiwa na uzuri wa Edna.

“Haina haja ya kumwangalia sana wakati unajua ni mke wangu”Aliongea Roma bila kuonyesha urafiki mara baada ya Aloni kugeuza geuza macho yake kumwangalia Edna.

Lakini sasa eneo lote lilikuwa kimya kutokana na kauli ya Roma , hawakutegemea anaweza kuongea hivyo kwa siku ya kwanza ya kukutana na Aloni

Edna aliekuwa karibu na Roma aliishia kumfinya Roma kwenye suruali yake kutokana na mgogoro wa nafsi aliotengeneza hapo ndani , ni kama vile alikuwa akiwapa onyo na kila mmoja aliekuwepo hapo kutomwangalia Edna kwasababu ni mke wake , ni kama waliogopa kushushuliwa na Roma.

Baada ya masaa kadhaa kupita Aloni aliweza kuaga kinyonge sana na hio ni mara baada ya zawadi aliomletea Edna kukataliwa kistaarabu.

Raisi Senga na yeye aliaga kuondoka kuelekea ikulu ndogo kwani alikuwa na mgeni ambaye anamtarajia kufika hapo Iringa jioni hio na hakuna ambaye alimzuia.

Roma , Edna na mtoto wao walitumia fursa hio kutembezwa katika eneo lote kuzunguka jumba hil, lilikuwa eneo kubwa mno ambalo nusu kilomita kutoka mahali walipokuwa wakiishi kulikuwa na mifugo ya wanyamwa mbalimbali ikiwepo Farasi na ng’ombe.

“Mzee ulisema kuna mahali tunapaswa kwenda kukuwakilisha ila hujaniambia ni wapi?”Aliuliza Roma.

“Nilisikia una urafiki mkubwa na mtoto wa Afande Tozo lakini kwa muonekano wako wa kutofahamu kitu nadhani ni mbali na nilivyofikiria”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Roma kumwangalia Edna ili kuona kuna habari ambayo hajamwambia na Edna alimnong’oneza na kumfanya Roma sasa kuelewa.

“Mzee nilijua Omari asili yao ipo Mwanza?”

“Mwanza ni makazi yao ya kudumu , Dar es salaam ni makazi yao baada ya baba yake kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi lakini asili yao ni Makambako hapa Iringa”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa.

“Inaonekana kweli wamemua kumkubali mtoto wa Yan Buwen kuwa wa ukoo wapo mpaka kumfanyia sherehe”Aliongea Roma akiwa kwenye mshangao.

“Unaonekana kutojua mambo mengi yanayoendelea hapa nchini, ijapokuwa ni kweli wamemkubali kama mtoto lakini sherehe hio ni kama Geresha tu anaefanyiwa sherehe ni mtoto wao wa kike ambaye amejifungua hivi karibuni”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa nusu , lakini hakuhoji zaidi.

“Kwasababu unakwenda kuwa mrithi wangu ujiandae na mambo ya aina hii yanaweza kuonekana ya kawaida kwenye macho yako lakini mara nyingi huambatana na vikao vya siri”Aliendelea kuongea.

“Vikao vya siri!!”

“Ndio , mara nyingi sherehe za aina hii ni kwa ajili ya kutengeneza Kava kwa nje ili kuficha vikao hivyo, ukishanirithi majukumu yangu moja kwa moja unakuwa kiongozi wa ‘Deep state’ ya taifa hili ndio maana watatokea wengi wa kukupinga”Aliongea na kumfanya sasa kuelewa kwanini hata siku ya kwanza kulikuwa na wengi ambao wanampinga kupewa naafasi ya ukoo wa familia kumbe ilikuwa ni zaidi ya kurithi ukoo.

Kwa maneno marahisi ni kwamba Roma akisharithi nafasi ya Afande Kweka moja kwa moja anakuwa na nguvu ndani ya taifa ya kuamua raisi awe nani.

Mara nyingi vikao hivi vinavyohusisha watu wazito wa taifa vinapofanyika ni ngumu sana kugundua kwani vinakuwa ni vya siri na hutengenezewa tukio kama sherehe ili kukusanya washirika.

Tokea Roma afanikishe kumuua Mzee Longoli na Raisi Kigombola kufariki ni kama nguvu ilizidi kurudi katika mikono ya ukoo wao na kuzidi kuwa na nguvu, isitoshe familia nyingine ambayo ilikuwa na nguvu nchini ilikuwa ni ya Mzee Atanasi lakini mzee huyo alivyofariki majukumu yake yarithiwa rasmi na mmoja wapo ya wanafamilia ambae pia alipaswa kushiriki katika vikao hivyo vya siri ambavyo vilitarajiwa kufanyikia hapo Iringa katika kipindi hicho.

*********

Ni baada ya saa moja kupita , Afande Kweka na Lanlan mara baada ya kuchoka kuangalia mifugo waliamua kurudi ndani kwa ajili ya kupumzika, Lanlan alikuwa amechoka mno na alikuwa akisinzia sinzia na kumfanya Mzee Kweka kushangaa kwani siku zote Lanlan sio mwenye kusinzia sinzia.

“Lanlan kwanini unasinzia leo mapema, jana haujalala vizuri?”

“Hapana , baba anamfundisha Lanlan namna ya kuvuna nishati na amesema sitakiwi kuzembea, Lanlan hawezi kuvuna nishati akiwa hajakula hivyo nilikuwa nikifikiria baada ya kula na sasa nahisi usingizi baada ya kuwaza kwa muda mrefu”Aliongea

“Oh.!!”Afande Kweka alionekana kuwa kwenye mshangao kidogo alikuwa akijua nini anamaanisha na alioona ni sahihi kwa umri wake, hata kama alikuwa na mwili wenye nguvu kuelewa baadhi ya vitu vigumu kama hivyo huusumbua sana ubongo wake , haikumshangaza kumuona akiwa amenyongea hivyo.

Afande Kweka hakuuliza sana maswali alimbeba juu juu na kwenda kumlaza kwenye kitanda na yeye akapanda kwa ajili ya kupumzika huku akimpiga piga mgongoni kumbembeleza alale.

“Lanlan kwanini hukutaka uncle wako kukubeba muda ule?”

“Lanlan alikuwa akiogopa , uncle anaonekana sio mtu mzuri”Aliongea kinyonge na kumfanya Afande Kweka kufumba macho kwa dakika kama mtu anaefikiria jambo na akaishia kutabasamu.

“Hahaha ,, naona kweli sio mtu mzuri ,, una akili sana”Aliongea akiwa anajiongelesha mwenyewe kwani Lanlan alishapotelea usingizini na dakika chache mbele ni sauti za kupumua za babu na mjukuu zilizosikika.

*********

Upande mwingine nchini Rwanda ilikuwa tofauti kidogo na Tanzania , baada ya muda wa miezi kadhaa ya kupotea kwa Desmond hatimae aliweza kurudi na hata habari za kurudi kwake zilienea kwa watu wengi wlaiokuwa karibu na raisi Jeremy.

Muda wa saa sita mchana wa siku hio alionekana Desmond akiingia ndani ya ikulu ya baba yake akiwa amevalia suti , baada ya kushuka kwenye gari wtu walikuwa wakimwangalia kwa kumshangaa , ilikuwa ni kama vile walikuwa wakimuongelea dakika hizo na sasa kile walichokuwa wakiongelea kinathibitika katika macho yao.

Upande wa Desmond hakujali namna macho ya watu yanavyomwangalia , isitoshe ni yeye mwenyewe aliesambaza uvumi wa kurudi maana baba yake alimfungia na kutotaka watu kufahamu karudi ili mradi tu asimpe cheo serikalini.

Hivyo Desmond mbinu yake ya kwanza aliorudi nayo ni kuvumisha kurudi kwake ili tu baba yake ampatie kazi serikalini ya kufanya kwa kushurutishwa na wasaidizi wake.

“Baba nina jambo la kuzungumza na wewe”Aliongea mara baada ya kufungua mlango wa ofisi hio”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kukunja sura huku akimwangalia na kisha akampa ishara ya kuingia.

Tokea kurudi kwa Desmond raisi Jeremy alimuona mtoto wake huyo kuwa ni mwenye kujiamini zaidi ya alivyoondoka na jambo hilo kidogo lilimfanya muda wote kuwa na wasiwasi juu yake.

“Unataka kuongea nini , nipo bize”

“Baba nipo hapa kwa ajili ya kupata ruhusa yako , nataka kuelekea nchini Tanzania kuna baadhi ya marafiki zangu nahitaji kuonana nao”Aliongea na palepale Raisi Jeremy alimwangalia Desmond kwa macho makali.

“Kwanini unataka nirudie mara mbili mbili, nishasema huruhusiwi kutoka”

“Baba kuna tatizo gani mimi kutotoka , nahitaji kuonana na marafiki zangu isitoshe mimi ni mtu mzima ambaye nina mambo yangu”

“Marafiki umesema , je hao wakikuuliza ni wapi ulikuwepo kwa muda wote utawaambia uongo ulioniambia mimi? , kwamba ulipoteza kumbukumbu zako,Kwanini Umeshindwa kuniambia ukweli wapi ulikuwepo na nini kimetokea na ni kwa namna gani umeweza kupona?, Hivu unaniona mimi ni mjinga sana kiasi cha kuukubali uongo wako?”

“Baba sikudanganya kubali au ukatae ni kweli nilipoteza kumbukumbu zangu na nashangaa kwanini mimi kama mtoto wako ambaye nimeweza kupona kimiujiza hufurahishwi?”

“Acha kubadili mada , kama kweli unanichukulia kama baba yako basi niambie ukweli wote ni kwasababu ipi imekurudisha m ni nani unaefanya nae ujinga, jana nimewapa kazi mabodigadi kukulinda lakini iliwezekanaje ukawatoroka , umefanya watu wengi ndani ya Kigali kufahamu kurudi kwako ili mradi tu nikurudishe kwenye nafasi yako si ndio , je unafikiri ninaweza kufanya kama unavyotaka , sasa nakuambia hivi unapaswa kukaa nyumbani mpaka nitakapopata mwanga wa kila kitu, kwanzia sasa nitakipatia walinzi wa wale wajomba wawili , Gesha pamoja na Nix na ndio watakuwa walinzi wako”

“Kwasababu baba hutaki kuniambini mimi sina cha kusema , lakini kwa ruhusa nilioomba….”

“Nishasema huwezi kutoka nje ya hii nchi , toka ofisini kwangu”Aliongea na kumfanya Desmond kukunja ngumi yake na kuiachia hapo hapo na kisha akageuka na kuondoka.

Muda huo huo wakati akitoka walionekana Nix na Gesha wakiingia na palepale aliupamba uso wake na tabasamu na kuwapa ishara ya salamu ya heshima na kisha akawapita”

“Wazee nadhani mmeweza kusikia kila kitu hivyo mnaonaje mkinisaidia kumwangalia huyu shetani mtu, nadhanni kuna mambo sio mazuri wanapanga na yule msukule”Aliongea Raisi Jeremy.

“Usiwe na wasiwasi tutahakikisha tunakuwa nae makini , Unafanya kazi nzuri Jeremy,Desmond mpaka sasa hatumwelewi na hawezi kukurithi na kama tutamuacha afanye atakavyo itaharibu mipango yetu”Aliongea na Raisi Jeremy alitingisha kichwa kukubaliana nao.

“Nimepokea taarifa kutoka Tanzania , Roma na Edna wapo Mkoani Iringa nyumbani kwa Afande Kweka kwa ajili ya kukusanyika kifamilia , nimeongea na rafiki yangu Senga na amenialika niwatembelee nadhani itakuwa vizuri nikienda kujitambulisha vizuri kama baba mkwe mnaonaje mkinisindikiza kwenda huko leo maana yule Roma haeleweki mudi yake”

“Bila shaka na ndio sababu iliotuleta hapa , Edna kwasasa nido ‘target’ yetu na unapaswa kubadilisha jina lake haraka iwezekanayvo na aitwe Edna Jeremy”

“Kuwa na amani nitahakikisha Roma anakuwa mkwe wangu na kufanya mipango yetu kwenda sawa”Aliongea na kufanya wote kucheka kwa sauti.

Vicheko hivyo vilisikika kwa Desmond ambaye hakuwa ametoka kwenye mlango na kumfanya chuki kuzidi kumvaa kutokana na kusikia kile kitu.

“Jeremy umeipoteza nafasi yako ya kuwa hai , kwasababu umeyataka mwenyewe usije kunilaumu kwa kitakacho kutokea”Aliwaza kwenye akili yake huku sura ikijikunja na kupiga hatua kuondoka katika eneo hilo bila ya kujali walinzi wanaomwangalia.











SEHEMU YA 580.

Ni wakati wa usiku katika maeneo ya Iringa mjini, eneo hili lilionekana kuchangamka sana kuliko isivyokuwa kawaida licha ya baridi kali.

Katika maeneo mengi ya starehe yalikuwa yamejaa kwa kiasi kikubwa watu mbalimbali wakubwa kwa wadogo wakipoteza muda kwa kupata vinywaji vyenye vilevi ndani yake.

Ilikuwa ni hivi karibuni tu tokea hoteli na Club moja maarufu ndani ya jiji hilo kununuliwa na kubadilishwa jina na kufahamika kwa jina la Pink Lady hotel & Club.

Hoteli hii ilikuwa maarufu sana kutokana na Club yake kuwa na mabadiliko makubwa , inasemekana ndani ya hoteli hii kulikuwa na anasa za kutisha zinazofanyika hivyo kuvutia watu wengi wapenda anasa kufika katika eneo hilo kujionea wenyewe , huku shauku kubwa ya watu wengi ndani ya eneo hilo kuona, ni juu ya uwepo wa mwanamke mrembo ambae ndio mmiliki anaefahamika kwa jina hilo hilo linalofanana na hoteli hio yaani Pink Lady.

Sasa usiku huu ndani ya Club hii alionekana Aloni akiwa amekaa eneo laVIP pamoja na mwanamke aliefahamika kwa jina la Shishi, tokea Aloni afike Iringa mwanamke huyo ndio aliekuwa akistarehe nae , alikuwa mzuri wa umbo lakini sura alikuwa wa kawaida lakini licha ya hivyo alionekana kuvutia kwa macho kutokana na mavazi yake na ngozi yake ilivyokuwa nyororo.

“Mpenzi una nini leo mbona ni kama haupo sawa leo”Alilalamika yule kahaba aliefahamika kwa jina la Shishi.

“Nilikoenda kusalimia leo kumenitibua na sina hamu ya kufanya chochote”Aliongea na kumfanya yule mwanamke ambaye alikuwa amevalia nusu utupu kutabasamu.

“Au ni kwasababu umekutana na Edna mwanamke rajiri na mrembo , ijapokuwa sijabahatika kumuona ana kwa ana lakini nimesikia uvumi kwamba ni mwanamke mrembo kuliko mwanamke yoyote ndani ya taifa hili, je maneno hayo ni kama yanavyosemwa?”Aliuliza Shishi.

“Upo sahihi ni mwanamke mrembo kweli na hiki ndio kilichonifanya kuwa katika hali unayoniona sasa hivi , kutokana na urembo wa yule mwanamke nilijikuta nikishindwa kuacha kumwangalia na mwisho wa siku nikaishia kumkasirisha Binamu yangu Roma na mipango yangu yote imeharibika”Aliongea kwa hasira huku akichukua glass ya pombe na kuipeleka mdomoni yote.

“Lakini si ulienda na zawadi m je hawakuipokea?”Aliuliza yule Shishi na kumfanya Aloni kuegamia kwenye sofa kivivu na uso wa kinyonge zaidi.

Ukweli ni kwamba Aloni hakuenda kusalimia akiwa na zawadi ya Afande Kweka pekee , bali alikuwa pia amempelekea Shemeji yake Edna zawadi.

Ilikuwa ni zawadi ya gari aina ya Lamborgin , gari ambayo imemgharimu kiasi kikubwa cha pesa kuinunua, japo sio pesa nyingi sana kutokana na kukwepa kodi bandarini.

Ukweli ni kwamba licha ya familia ya Aloni kujiweza kiuchumi lakini walitegemea biashara za familia yao kwenda vizuri kwa kutumia koneksheni ya familia ya Afande Kweka na ndio maana aliamini kujenga ukaribu na Roma ambaye muda si mrefu anakwenda kukabidhiwa kuongoza ukoo ni kipaumbele kikubwa ili kuendelea kula keki ya taifa.

Sasa kilichompa huzuni ni kwamba kwanza kabisa alikosana na Roma kwa kitendo chake cha kumkodolewa macho mke wake na pia baada ya kutoa zawadi ya gari licha ya Edna kuipokea lakini aliamua kumbadilishia na gari nyingine aina ya Aston Martin ambayo ilikuwa na thamani zaidi kuliko hata aliowapatia na kitendo hicho kwake alikitafsiri kama dharau.

“Nimewaonyesha zawadi ya gari nilioenda nayo lakini tofauti na kuipokea walinibadilishia na gari nyingine ya thamani kubwa zaidi

“Nini kwanini wafanye hivyo na ni Astorn Martin ipi hio ya kuizidi ile Lamborgin?”Aliuliza Shishi kwa shauku.

“Najua wamepokea zawadi yangu nisijisikie vibaya lakini kunibadilishia ni kama wanatengeneza mpaka kati ya familia yangu na wao , najua familia yetu licha ya kuwa na biashara lakini haina nguvu ndani ya taifa hili lakini hawapaswi kutudharau ,kama sio baba kuniambia nije na zawadi hio nisingejaribu”Aliongea huku akuonyesha kukasirika.

“Lakini mpenzi hujaniambia ni gari gani wamekubadilisha?”

“Kaa kimya wewe mpumbavu , haya ni One- 77 umeridhika?”Aliongea na kumfanya yule mrembo kuachama kwa mshangao

“One 77 Aston martin gharama ya hio ghari si inakaribia bilioni moja za Kitanzania?”Aliuliza yule mwanamke , ilionekana alikuwa na uelewa mkubwa wa magari.

“Unashangaa nini sasa , kama mtu ana utajiri za zaidi ya bilioni ishirini za kimarekani unadhani kwake ni ngumu kutoa gari kama hio , anayo mengi zaidi ya ghari kuliko hata hilo alilonibadilishia”Aliongea huku akionyesha kutoridhika , ni kweli gari aliopewa ni ya bei ghali lakini bado haikumfanya kuwa na furaha hata kidogo.

Wakati wakiendelea kuongea na mrembo huyo aliongezeka mtu mwingine katika eneo hilo na kufanya baadhi ya watu waliokuwepo hapo ndani kusimama wote akiwemo Aloni mwenyewe na kwa wakati mmoja wakifukuza wale makahaba.

Aliefika alikuwa ni Denisi ambaye hakuwa peke yake , alikuwa ametangulizana na mwanamke mrembo mwenye nywele zilizopakwa rangi ya Pink.

“Bro Denisi , Sister Tasi”Aliongea kwa heshima akionyesha ishara ya kuwakaribisha.

“Relax bro , tupo hapa kwa ajili ya kula bata haina haja ya kukamaa hivyo”Aliongea Denisi huku akisogea mpaka kwenye sofa na kuketi

“Vipi vijana hapa mnainjoi , nielezeni dada yenu hapa kama kuna shida yoyote”Aliongea yule mwanamke huku akiwaangalia vijana waliopo ndani ya hilo eneo, walikuwa wote ni marafiki wa Aloni na ni watoto wa matajiri ndani ya Iringa na wengine wametokea Dar es salaam.

“Hehe .. hawa warembo wako vizuri lakini wana tofauti sana na wewe kwenye yale mambo yetu”Aliongea Aloni bila ya kuonyesha heshima kwa yule mwanamke mwenye nywele za pink na kumfanya yule mwanamke mrembo kusogelea Aloni kimadaha na kuchukua glasi yake yenye kilevi na kisha akapiga pafu pasipo kumeza kisha akaweka chini na akaikumbatia shingo yake na kukaa chini na kumpa ishara ya kusogeza mdomo wake na wakagusanisha lips zao kisha akatoa kile kilevi kwenye mdomo wake na kukihamishia kwenye mdomo wa Aloni., kitendo kile kilimfanya yule bwana kushika usawa wa zipu yake ilioanza kutuna kwa msisimko alioupata.

Kilikuwa kitendo cha kikahaba kutoka kwa mwanamke aliekubuhu kweli kweli na kuwafanya kila mwanaume aliekuwa hapo ndani kutamani nafasi ile iwe yao.

“Aloni unajua sana kuniridhisha na maneno yako , hio ni zawadi kwako”Aliongea Kimadaha huku akimwachia na kulamba midomo yake.

Ijapokuwa Aloni alijona kama vile yupo anganni kwa matendo hayo aliofanyiwa lakini hakumsahau Denisi aliekuwa mbele yake.

Ukweli ni kwamba mwanamke huyo mwenye muonekano wa utu uzima ndio ambaye alikuwa mmiliki wa hio Club na hoteli na ndio ambaye alifanya vijana na wazee wapenda starehe kujazana ndani ya hio club kwa ajili ya huduma yake tu.

Denisi alimwashiria yule mwanamke kwa kidole na kumpa ishara ya kumsogelea na yule mwanamke aliefahamika kwa jina la Tasi alisogea kimadaha na baada ya kumfikia Denisi alipiga busu kwenye shavu na kisha akachukua mkono wa Denisi wa kushoto na kuuchomeka ndani ya suruali yake kwa mbele karibu na zipu na kumfanya bwana huyo kutabasamu kifedhuli huku akianza kupekenyua.

“Aloni hauna wasiwasi? , hautokuwa na uwezo wa kuishi kwa amani mara baada ya kaka yangu kuwa mrithi wa ukoo na isitoshe leo mara yenu ya kwanza kukutana haijaenda vizuri”Aliuliza Denisi.

“Bro kwasababu ndio umeyaanzisha haya maongezi , je unaweza kuni.., “

“Usiwe na wasiwasi kwangu wewe ni rafiki yangu ukiachana na kwamba ni binamu upande wa shangazi yangu, hivyo sitoruhusu ukiwa na maisha magumu wakati nipo hai”Aliongea Denisi na baada ya kufukunyua upande wa chini alihamishia mkono wake kwenye midomo ya yule mwanamke akimpa ishara aulambe na baada ya hapo akahamishia kwenye tisheti yake na kushika maembo dodo na kuendelea kuyaminya minya bila wasiwasi.

Aloni alimwangalia Denisi kwa tamaa ya kutaka kufanya kile anachofanya lakini hakuwa na nafasi ya kuingilia kutokana na kumhofia Denisi na familia yake.

“Bro Denisi niseme kwamba wewe ndio mzizi wa familia na imekuwa hivyo kwa miaka mingi , ijapokuwa Roma ndio mkubwa lakini hana uelewa na mambo yanavyoenda ndani ya taifa hili na isitoshe hajaingia jeshini , ninaona kabisa Afande Kweka hajafikiria vizuri kutokukurithisha”

“Anaweza akawa amefanya maamuzi yake , lakini familia siku zote haiundwi na mtu mmoja, baba na mama wapo upande wangu na wengine pia ninatarajia wataniunga mkono , kazi yako kubwa kwasasa ni kumshawishi Shangazi Theresia kuniunga mkono pia”Aliongea.

“Nimekuelewa bro nitafanyia hilo kazi , usijali kabisa itahakikisha Shangazi Theresia anakuunga mkono kwa namna zote isitoshe ananisikiliza kwa kila ninachomwambia”Aliongea

“Vizuri na kwanzia sasa usiwe na wasiwasi mbele yangu , nichukulie kama rafiki yako na kama kuna shida popote wewe niambie na nitakusiadia”Aliongea Denisi na kumfanya Aloni kufurahi.

“Sema Bro umeimarika sana siku hizi , tokea urudi unaonekana kuwa mtabe sana lakini kubwa zaidi umefanikiwa kumpata mwanamke mrembo kama Tasi”Aliongea na kumfanya Denisi kutoa tabasamu la kejeli na kisha palepale alimwangalia mwanamke aliekuwa akiitwa Tusi na kutoa mkono wake na kisha akamsukumia kwa Aloni.

“Kwasababu umesema huyu mwanamke ni mzuri , unaonaje ukimtumia usiku wa leo kama zawadi na mimi niangalie unavyoiweza kazi?”

“Huna haja ya kunisukuma kwa ajili tu ya kucheza nao hao vijana kwani nipo tayari”Aliongea yule mwanamkeTasi.

Dakika chache mbele yule mwanaume aliefahamika kwa jina la Tasi kila tundu katika mwili wake lilikuwa limevamiwa na vijana waliokuwa tayari wapo chakali kwa ulevi wa pombe na wala hakuonyesha hali ya maumivu na alikuwa akionekana kufurahia.

Kwa mtu wa nje angeona ni kitendo cha kifirauni sana na uchafu kuwahi kufanyika hapo ndani lakini kwa watu hao wapenda starehe wao waliona ni kitu kizuri sana na starehe na walijihisi ni kama vile wanasafiri mawinguni. .

Denisi ambaye alikuwa akiangalia hakuona kabisa kinyaa wala kuonyesha muonekano wowote wa wivu licha ya kufahamika mwanamke huyo kuwa wa kwake.

Dakika chache mbele sio Aloni na wenzake wote kila mmoja alipotelea usingizi mara baada ya kumaliza.

“Hivi viumbe ni dhafu sana , kidogo tu wanaonekana hivyo hawafanani kabisa na wewe”Aliongea yule mwanamke huku akijifuta na kumfanya Denisi kumwangalia kwa Dhihaja.

“Inaonekana unaifanya kazi vizuri kwa kipindi chote ulichokuwa hapa , mpaka kuweza kumudu watu watatu kwa wakati mmoja”

“Nani kakuambia usije kunitembelea mara kwa mara , hawa watoto wanaonekana kuhitaji kila saa lakini hawajiwezi , jana tu niliweza kumudu watu saba lakini wote wamesinzia kabla hata ya kuniridhisha, nisipofanya hivi biashara yangu haitofanya vizuri na mipango yetu kufeli.”

“Wewe malaya kadri siku zinavyoenda unazidi kukosa aibu , una miaka hamsini tayari , usijifanye unazidi kuwa mrembo kadri unavyofanya mambo yako ya kipuuzi itakufanya ugundulike kwa urahisi kwa ijinga wako, nakukumbusha tu usisahau kuhusu kitu nilichokuambia uandae”

“Usijali kila kitu kinaenda sawa , pia nimewasliana na Desmond na kasema Jeremy amegoma kabisa kumpatia nafasi serikalini na mpango wake ni kutaka kumrudisha yule malaya Edna kwenye ukoo wake”

“Kweli … kama ni hivyo basi hana thamani tena kwetu”

“Unaonaje tukimuua kabisa na kuchukua nafasi yake, ijapokuwa yupo na wale walinzi wake wawili wenye nguvu za nishari za mbingu na ardhi lakini kwa uwezo wako hawawezi kukushinda”

“Bado ni mapema na isitoshe nina mpango wangu naendeleza , endelea kufanya kama ninavyokuambia na hakikisha mpango wetu unaenda kama tulivyopanga”

“Jeez nimekuwa mtiifu kwako kwanini unakuwa msiri kiasi hicho kwanini usiniambie ni kipi unapanga?”Aliongea Kizwe kwa kuonyesha hali ya kutoridhika lakini Denisi palepale alimbeba juu juu kwenye mikono yake na kwenda kumbwaga bafuni.

“Jisafishe kwanza ni zamu yangu inayofuatia”Aliongea

********

Siku hio hio ikiwa ni usiku gari tatu aina ya Audi ziliingia ndani ya jumba la Afande Kweka , zilikuwa zote ni nyeusi na mara baada tu ya kusimama walitoka wanaume waliovalia suti na miwani za jua huku wakiwa na vifaa vya mawasiliano masikioni , baada ya kuangalia usalama kwa dakika mbili palepale mmoja wao aligeuka na kufungua mlango wa abiria wa gari ya katikati na kisha akatoka mwanaume alievalia suti mwenye mvi na kukanyaga ardhi ya eneo hilo , alikuwa ni Raisi Jeremy na mara baada ya yeye kutoka nje ya gari na wale watu wake kutoka jamii ya kijini ya Panas walionekana.

Muda huo huo kiongozi wa ulinzi wa zamu alisogelea watu hao waliofika na alishangaa mara baada ya kugundua ni raisi wa Rwanda.

“Mheshimiwa … Afande yupo kalala”Aliongea kwa kukakamaa mwili na kumfanya Raisi Jeremy kutabasamu.

“Sipo hapa kwa ajili ya kuonana na Marshal, naomba unitolee taarifa kwa binti yangu Edna umw
 
SEHEMU YA 581.

Wakati raisi Jeremy anafika upande wa Edna na Roma walikuwa kwenye chumba chao , Edna alionekana akiwa ameshikilia kishikwambi akiangalia baadhi ya majina ya watu wa kiserikali ambao alikuwa akitarajjia kwenda kukutana nao katika sherehe ya Arobaini ambayo alipaswa yeye na Roma kwenda kuhudhuria kumuwakilisha Afande Kweka.

Upande wa Roma yeye ndio kwanza alikuwa amemaliza kuwasiliana na mama yake ambaye alimpa taarifa ya kurudi nchini hivi karibuni akitokea Afrika ya Kusini.

“Babe Edna unamaliza saa ngapi?”Aliuliza Roma aliekaa kitandani akimwangalia Edna aliempa mgongo.

“Bado sijamaliza unaweza kuendelea kulala”Aliongea Edna kwa kauli moja tu ya kutotaka kuendeleza mazungumzo..

“Hehe… wife na haka kabaridi unaniambiaje nilale hivi hivi , tunapaswa kupasha kitanda joto”.

“Nilijua tu huo ndio mpango wako .. na usije kunisumbua mpaka nimalize kazi yangu”Aliongea Edna kwa sauti ya kutoridhika na kumfanya Roma amwangalie kwa kutoridhishwa na kauli ya mke wake , kwa baridi hilo la hapo Iringa aliona kulala mwenyewe kusingemletea usingizi.

“Jeremy amefika”Aliongea Roma mara baada ya kimya kifupi.

“Mh..!”

“Nakwambia ni kweli amefika”Aliongea Roma na kumfanya Edna mapigo ya moyo kudunda kwa kasi mno na kusihdwa kujielewa.

“Kaja kufanya nini muda huu?”

“Lazima kaja kwa ajili yako , vipi si unaenda kuonana nae?”Aliuliza Roma ukweli aliweza kufahamu ujio wake kutokana na kuhisi nguvu mbili za watu wa mafunzo ya kijini kukaribiana na yeye.

“Siwezi kuonana nae…”Baada ya kuongea kauli hio mlango wa chumba chao uligongwa na kumfanya Edna aende kufungua.

“Madam mheshimiwa Jeremy, Raisi kutoka Rwanda kafika na anasema anahitaji kuongea na wewe”Aliongea Kijakazi wa nyumba hio na kumfanya Edna ageuke na kumwangalia Roma.

“Unaweza kwenda haina haja ya kuniangalia hivyo”

“Kama hutaki sitoenda kuonana nae”

“Unaongea nini, naweza kuwa mume wako lakini yeye ni baba yako mzazi na kama ulivyowahi kusema mwenyewe ni ngumu sana kubadiilisha mahusiano ya mzazi na mtoto hata kama kuna makosa kiasi gani , hivyo usijali kuhusu mimi unapaswa kuonana nae”Aliongea Roma na kumfanya Edna atingishe kichwa na kutaka kufungua mlango kutoka lakini alizuiwa na Roma.

“Wife badilisha kwanza nguo ndio uende”Aliongea na kumfanya Edna ajiangalie na kuona aibu kwa mavazi aliovaa na alirudi na kubadilisha haraka haraka na kisha akamwangalia Roma.

“Twende wote”Aliongea na Roma alitingisa kichwa na kutoka kwenye kitanda na kutangulizana nae.

Uponde wa nje licha ya kwamba familia hio imezoea kupokea wageni wazito wazito lakini ujio wa raisi Jeremy wa ghafla uliwafanya wafanyakazi kuwa katika hali ya wasiwasi , lakini kubwa zaidi ni ile hali ya kujiuliza ni kipi ambacho kimemfikisha Raisi Jeremy katika nyumba hio kama hahitaji kuonana na Afande Kwek.

Baada ya Edna kutoka waliweza kumkuta Raisi Jeremy na walinzi wake wakiwa eneo la sebuleni na Rima haraka haraka alipitisha macho yake kwa wale wazee wawili wa jamii ya Panasi na kisha akayarudisha kwa raisi Jeremy.

“Haha.. Edna Binti yangu asante kwa kukubali kuniona, Mr Roma asante kwa kutokumzuia binti yangu kusalimiana na mimi”Aliongea.

“Kwanini nimzuie , labda kama una mipango yako ovu nyuma ya pazia”

“Hapana .. hakuna kitu kama hicho nilichotaka ni kuonana nae usiku huu huu mara baada ya kufika hapa Tanzania , Edna nisamehe baba yako kwa kutokuja kukusalimia mapema , nilikuwa bize na majukumu ndio maana”Aliongea na kumfanya Edna kutingisha kichwa.

Wale wasaidizi wa nyumba hio walijikuta wakiwa katika hali ya mshangao mara baada ya Raisi Jeremy kumuita Edna binti yake , ilikuwa ni habari mpya kwao na waliishia kuangaliana.

“imefurahi kusikia umestaafu katika nafasi yako ya CEO wa kampuni , Edna maamuzi ulioyafanya ninayaunga mkono kwa asilimia mia moja, ijapokuwa umekuwa mama wa familia lakini unahitaji mapumziko , Mr Roma asante kwa kusimama na binti yangu na kufanya maamuzi kwa faida yake”Aliongea na Edna kusikia anaungwa mkono na baba yake kwa kustaafu kama CEO wa kampuni ilimgusa lakini licha ya hivyo alikosa neno la kuongea na Roma na yeye hakuongea chochote na kumfanya Raisi Jeremy kuzungusha macho yake kama anatafuta mtu

“Mjukuu wangu Lanlan nadhani kashalala?”

“Ndio kalala na babu yake mkubwa”Alijibu Edna.

“Oh .. sio mbaya kama kalala na Marshal mwenyewe, sipaswi kumsumbua na nitaonana nae siku nyingine , ila nimemletea zawadi ya nguo za kujikinga na baridi na wewe Edna binti yangu sijakusahau , nimekuletea zawadi pia”Aliongea na palepale wasaidizi wake waliingia eneo hilo na maboksi mawili moja la njano na lingine la kijani.

“Edna hizi ni keki nimeziandaa nikiwa nchini Rwanda , najua kwenye utoto wako wote ndio kitu pekee ambacho ulifurahia kula na mpaka sasa hivi bado unazipenda hivyo nimeona ni zawadi nzuri kukupatia kama baba yako”Aliongea huku akifungua lile boksi na kumuonyesha Edna.

Roma mara baada ya kusikia kauli ile alikunja sura na kujiambia mzee huyo kweli ni mwanasiasa zawadi hio ilikuwa sahihi kabisa.

Edna mara baada ya kuona vile vijikeki vya aina yake kwenye boksi alijikuta akishindwa kujiuzuia na kutoa machozi na kumfanya Raisi Jeremy kuona kitu kile na kumwangalia Nix aliekuwa pembeni yake na kupeana ishara za ushindi.

Upande wa Roma aliishia kumwangalia mke wake kwa huruma , alijua siku zote udhaifu wa Edna upo kwenye ndugu zake tu na huenda anapaswa kujiandaa kuukumbatia udhaifu wake ili kuweza kujua ni ndugu yupo mwenye nia mbaya kwake..

Baada ya kutoa zawadi zile aliahidi atakuwepo nchini kwa siku ya kesho na ataonana na Lanlan na Afande na kisha aliaga na kuondoka.

********

WIKI MBILI ZILIZOPITA.-SOUTH POLE (Ncha ya Kusini)

Ni katika ncha ya kusini mwa dunia katika bara la barafu yaani Antarcticta , ilikuwa ni siku ambayo katika Visiwa vya Sicilly kulitokea maafa ya zaidi ya wapiganaji elfu moja wa kulipwa wa makundi mbalimbali ya Kimasenari kumezwa na Cauldron , lakini pia Athena kuua majitu kwa kutumia moyo wa Gaia ili kuamsha na damu ya Titan.

Sasa mara baada ya Athena kutoka nchini Italy moja kwa moja alienda kutua kwenye maabara ya kitafifi ambayo alikuwa amempatia Naira kufanyia majaribio.

Athena mara baada ya kuingia ndani ya maabara hii ilionekana kuwa kimya sana lakini hisia zake za kiuungu zilimfanya kujua ni upande upi Naira alikuwepo lakini licha ya hivyo hakujisumbua kwenda upande wake zaidi ya kunyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha baridi .

Jambo moja la tofauti kuhusu Atnena ni namna ambavyo alibadilika muonekano kutoka mwanamke mweye ngozi ya kiafrika kuwa mwanamke mwenye mwonekano wa Clelia Allisanto, haikueleweka ni kwa teknolojia ipi aliweza kujibadilisha wala ni kwa madhumuni yapi kuwa katika mwonekano aina mbili tofauti.

Athena mara baada ya kuingia katika chumba cha teknolojia ya baridi , maarufu kama ‘Cryosleep Room’ moja kwa moja alienda kusimama katika sanduku ambalo lina mwili wa Hades wa zamani usio kuwa na uhai na mara baada ya kusimama kwa dakika kadhaa tu alitoa ule moyo wa Gaia na kuushikilia kiganjani kwake.

Moyo huo wa Gaia ulikuwa umaebadilika umbo na ulikuwa ukicheza cheza na kutoa cheche kama za shoti ya umeme au radi ndogo ndogo lakini kwa wakaiti mmoja ukibadilika badilika rangi kwenda njano zambarau na nyekundu , kwa kuutazama tu ungeweza kugudua ni kitu ambahco kina uhai ndani yake kutokana na vinyuzi nyuzi ambavyo vilionekana kupitisha mawasiliano.

“Hades unaonaje? Hatua ya kwanza ya kuufufua moyo wa Gaia imeanza , mpaka sasa unadhani ni kipi kinachoweza kuzuia mpango wangu usifanikiwe?”Aliongea kwa sauti ya Kingereza huku akionyesha tabasamu na macho yake yote yakikodolewa ule Moyo.

“Najua uliweza kusafiri mbele ya muda ndio maana unajiamini kila kitu kitaenda kulingana na mipango yako, lakini maadamu tabasamu la huyu mwanamke halibadiliki mipango yangu pia haiwezi kubadilika”Aliongea huku picha ya mwanamke mrembo wa ngozi ya kiafrika anaefanana kwa kila kitu na Edna na Seventeen ilionekana kwa mfumo wa Hologram, ilikuwa ni picha ileile aliomuonyesha Naira siku kadhaa zilizopita.

“Kitu kimoja tu ambacho hukuweza kuona na ambacho kinakwenda kutimiza mipango yangu, ‘ni yeye kuwa mimi na mimi kuwa yeye’ huo ndio unabiii ulivyo… ninakwenda kurudisha roho zote za ndugu zetu zilizopotea na kupitia wao ninakwenda kutengeneza ulimwengu mpya , ulimwengu tuliopoteza nina kwenda kuufufua”Aliongea kwa hisia kubwa kwa dakika kadhaa na kisha akageuza na kutoka nje ya chumba chicho lakini ile anatoka tu aliweza kukutana na Naira aliekuwa katika mavazi ya kitafiti.

“Umefanikisha?”Aliuliza Athena bila ya kumpa salamu Naira au huenda alimsalimia kabla ya kuondoka .

“Yes kila kitu kipo tayari”Aliongea na kumfanya Athena kutabasamu.

“Una swali la mwisho?”Aliuliza.

“Unamaanisha nini?”Aliuliza.

“Utafiti wako umeisha na umeweza kuikamilisha kazi kwa asilimia mia moja na najivunia kwa hilo na kwa ajili ya kukupongeza nakupa nafasi ya kuuliza swali kabla haujaanza safari ya kurudi Zeros organisation HQ”Aliongea na kumfanya Naira kuonyesha mshangao huku akikunja mikono yake ambayo ilikuwa ikitoa jasho licha ya eneo hilo kuwa na ubaridi.

“Napaswa kuuliza maswali mangapi?”

“Mawili tu, hivyo fikiria kwa umakini”Aliongea Athena na kumfanya Naira kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Mara ya mwisho ulisema Agent 13 ameukamilisha unabii kwa kukuwezesha kupata Moyo wa Gaia , je ndio mwisho wa mpango LADO uliofanikisha kumtengeneza?”

“Itakuwa sahihi sasa ukimwita Hades na sio Ajenti 13, kujibu swali lako uwepo wa Hades sio kwasababu ya kutimiza unabi tu wa mimi kupata moyo wa Gaia bali vilevile ni kunisaidia kuziwezesha fikra zangu kuwa katika uhalisia , mpango LADO ulishafika kikomo siku na saa ambayo Ajent 13 aliporithi uungu wa Hades wa zamani”Alijibu na kumfanya Naira kuonekana kuridhika.

“Ili kutimiza malengo yako ya kutengeneza dunia kamaUtopia, je kuna hasara yoyote itakayotokea katika dunia hii ya sasa ambayo haipo kamilifu?”Aliuliza Naria na kumfanya Athena kutabasamu.

“Kumbka hili ni swali lako la mwisho na nitakujibu hivi….”Aliongea na kisha alianza kuangalia mazingira ya maabara hio kwa dakika kadhaa na kisha akamgeukia Naira.

“Wherever there is success , there is sacrifices and imbalance”Aliongea akimaanisha kwamba mahali popote penye mafanikio kuna kafara na ukosefu wa uwiano, ni jibu ambao lilimuacha Naira katika tafakari lakini kwa wakati mmoja alikuwa amejibiwa swali lake hivyo hakuwa na nafasi ya kuuliza tena na alijikuta na yeye kugeuka na kuangalia maabara hiyo kama vile mtu ambaye hakuwa tayari kuondoka.

Ni mara baada ya mazungumzo kati ya Naira na Athena kuisha palepale Athena kwa spidi ambayo Naira hakuweza kuona alijikuta akilegea na kupoteza ufahamu kwa kuguswa shingoni na Athena alimshikilia.

Ilikuwa ni kama ambavyo Naira aliingizwa hapo ndanni ndio namna ambavyo anatolewa na kurudishwa makao makuu ya siri ya Zeros organisation kwani mara baada ya Naira kubebwa mikononi palepale Athena alipotea nae katika eneo hilo.

Ilionekana kazi ambayo alikuwa amepewa kuifanyia kazi ilikwisha kukamilika.

















SEHEMU YA 582.

Ni asubuhi ya siku nyingine ndani ya mji wa Iringa , katika familia ya Afande Kweka ulikuwa ni wakati wa kupata kifungua kinywa.

Afande Kweka ambaye jana alilala mapema na mjukuu wake aliweza kupata taarifa asubuhi hio juu ya ujio wa Raisi Jeremy, haikumshangaza sana baada ya kupata taarifa hio lakini alitaka kusikia mwenyewe kutoka kwa Edna kama alikuwa na mpango wa kutaka kurudi katiia ukoo wa baba yake.

“Edna una mpango wa kurudi kwenye ukoo wa baba yako?”Aliuliza Afande Kweka.

“Sijajua bado na nimezoea ukoo wa Adebayo”

“Haha.. kwangu mimi ukirudi ni sawa tu kwani haijalishi unaitwa nani lakini Jeremy atabakia kuwa baba yako , lakini kumbuka kwasasa wewe ni mke pamoja na mama wa mtoto hivyo una zaidi ya familia moja”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia Lanlan na kisha akatingisha kichwa.

“Ndio babu”

Ukweli Afande Kweka alikuwa akimuonea huruma Raisi Jeremy , huenda ni kutokana na hatia aliokuwa nayo ya kuhusika katika mpango LADO , mpango ambao ulimhusisha na mtoto wake wa kike , ndio maana hakuona tatizo kama Edna atamkubali baba yake kwani alimuona raisi huyo akiwa ni mwenye kuteseka sana katika maswala ya familia , alikuwa na mafanikio ya kisiasa lakini kwenye familia alikuwa na matatizo makubwa.

Baada ya kifungua kinywa Roma na Edna walipaswa kwenda nyumbani kwa Omari ili kuhudhuria sherehe ya Arobaini ilioandaliwa , Edna alikuwa tayari amekwisha kuandaa zawadi hivyo upande wa Roma hakupanga kutoa chochote, hawakupanga kwenda wao tu bali na Lanlan waliongozana nae.

“Daddy are we going to the zoo to see elephants today ?”Aliuliza Lanlan aliekuwa siti ya nyuma ya abiria akimuuliza Roma kama ndio wanaenda Zoo kwa ajili ya kuangalia Tembo.

Roma alijikuta akijilaumu kwa kusahau ahadi yake kwa Lanlan maana ndio alimuahidi mwenyewe kwenda kuona wanyama mara baada ya kushinda mchezo wa Chess.

“Lanlan tunaenda kumsalimia ‘Uncle’ Omari , tutaenda kuona wanyama siku nyingine sawa mtoto mzuri”Aliongea Edna lakini Lanlan alionekana kutoridhika.

“Lakini si mlisema mtanipeleka baada ya kuja huku , baba na mama mnanidanganya tena”Alilalamika.

“Tunakudanganya kivipi Lanlan , ni kweli tutakupeleka lakini sio leo , hivyo kuwa msikivu”Aliongea Edna akiwa mkali kidogo na kumfanya Lanlan kuangalia pembeni na kuanza kulia.

Roma ambaye alikuwa akiendelsha aliinua uso wake kwenye kioo cha nyuma na kumwangalia Lanlan akilia na alijikuta akivuta pumzi na kuzishsuha.

“Lanlan usilie , leo nitakupeleka kuona wanyama baada ya chakula cha mchana , Baba hatakudanganya tena”

“Kweli?”Mudi yake ilirudi na kumwangalia Roma kwa shauku.

“Hapana , hatuwezi kwenda leo hatutopata muda , Omari amekuwa kama rafiki wa familia yetu kwanini tuondoke mara tu baada ya chakula cha mchana?”Aliongea Edna akikataa.

“Omari ni muelewa na tukimweleza ataelewa wewe ukifika toa tu zawadi kuonyesha nia yetu ya dhati basi”

“Lakini tunaweza kwenda huko kwenye Zoo siku yoyote kuna ulazima sana kwenda leo , hatuwezi kumdekeza mtoto hivi”

“Lakini sisi wenyewe ndio tulimwahidi mara baada ya kushinda mchezo , kwasababu tulimwahidi tutampeleka tukifika huku basi hatupaswi kwenda kinyume na ahadi zetu , Wazazi hatupaswi kudanganya watoto angalau kwa binti yangu napaswa kutimiza hadi zote ,Lanlan sio mjinga anajua kila kitu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushindwa kuongea neno lingine , hakutegemea Roma kuongea hivyo lakini kwa upande mwingine alimuunga mkono.

Aligeuza macho yake na kumwangalia binti yake anaetia hruuma pembeni yake na kushika kichwa kwa kumbeleza.

“Wewe na mtoto wako mmenishinda tabia , mkitaka kitu lazima mtimiziwe kwa lazima , kwa staili hii mtanifanya nizeeke mapema”

“Unazeekaje mapema , nitajitahidi kuipaka ngozi yako mafuta kila ifikapo usiku kama unahitaji”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuona aibu za kike.

“Shuuu!!..huna aibu wewe, unaongea nini mbele ya mtoto”Aliongea lakini hata hivyo Lanlan hakuwa akielewa sana lugha ya kiswahili hivyo asingeelewa nini maana ya kupakwa mafuta usiku.

Dakika chache mbele waliweza kufika mahali husika , haikuwa ngumu kupajua kutokana na kupewa maelekezo ya kutosha ambayo yalikuwa rahisi kuyafuata na kufika nyumbani kwa Afande Tozo.

Baada ya kuingia ndani ya eneo hilo na kushuka waliweza kupokelewa na Omari mwenyewe ambaye alikuwa kwenye sura ya bashasha , tokea mara ya mwisho kuonana kwenye harusi yao hawakuweza kukutana tena kwa muda mrefu na Omari alikuwa vilevile na hata uwezo wake wa kuvuna nishari za mbingu na ardhi haukuwa umeongezeka sana.

Ijapokuwa walikuwa wamewahi lakini eneo hilo lilikuwa na watu wengi ambao tayari walishafika .

Roma mara baada ya kuona jumba la rangi nyeupe la familia ya Omari alijisemea hawa watu ndio wanakula mema ya nchi, kwani ni eneo ambalo lilikuwa limekaa kifahari mno.

Baada ya kusalimiana na baadhi ya ndugu ambao Roma hakuwa akiwafahamu na kutambulishwa moja kwa moja alizungushwa mpaka nyuma kwenye ukumbi na kukutana na Afande Tozo mwenyewe alievalia kanzu na kusalimiana nae, baadhi ya wanaume vijana waliokuwa hapo walimwangalia Edna aliemshikilia mkono Lanlan kwa macho ya tamaa na wivu kwa wakati mmoja.

“Bro mtoto wako ni mrembo mno unaonaje tukianza taratibu za ndoa na mtoto wangu mapema”Aliongea Omari na kumfanyaEdna ambaye alikuwa ameshikilia Lanlan kukaza mkono wake bila ya kujielewa , alionesha hali ya kupaniki katika macho yake licha ya kwamba Omari aliongea kama utanni.

“Nenda zako , binti yangu hawezi kuolewa na mtu yoyote”

“Hehe tutaona , watoto wakike wanaishi kwa muda tu na wazazi wao , itafikia muda hutoweza kuwazuia kufanya wanachotaka”

Ijapokuwa Omari mtoto sio wa kwake lakini alionekana kujivunia mno kwa kuzaa mtoto wa kiume na kumfanya Roma atamani na yeye mtoto wake wa atakaezaliwa awe ni wa kiume.

Zilipita dakika chache tu Roma aliweza kumuona Neema Luwazo akitokea ndani akija eneo la nje huku amebeba mtoto , Roma alishangaa kutokana na kwamba hakumtegemea kumuona eneo hilo lakini hakuwa peke yake baada ya yeye kutoka alifuatia mwanamke mrembo wa maji ya kunde ambaye pia alikuwa amebeba mtoto , Roma aliweza kumfahamu mara moja , alikuwa ni Matilda dada yake Queen na yeye pia alikuwa amebeba mtoto mchanga aliefunikwa na nguo nzito kukingwa na baridi.

“Lanlan umenimisi shangazi yako?”Aliongea Neema mara baada ya kumsogelea Edna wa kwanza na Lanlan alitoa tabasamu na kutingisha kichwa kuitikia.

“Sikukutegemea kukuona hapa”Aliongea Roma.

“Lazima niwepo , mtoto wa msechu na Ratifa ametimiza siku arobaini pia hivyo sherehe yao kuunganishwa ”Aliongea na kumfanya Edna na Roma kuangaliana

“Msechu unamaanisha mtoto wa Mzee Chino?”Aliuliza Roma na Neema aliitikia kwa kichwa na kuanza kuelezea uhusiano uliopo.

Ilionekana Msechu kaoa katika familia ya Afande Tozo, Roma alishagaa kwani alijua bwana huyo hakuwa na mke kutokana na alivyokuwa akionekana kutokomaa kiakili siku ambayo alienda kumsaidia kurudisha gari ya Neema ambayo aliibetia lakini mawazo yake yalikuwa tofauti.

Matilda ambaye alikuwa akisalimiana na baaadhi ya wageni alimwangalia Roma kwa wasiwasi kidogo na kumfanya Edna kumuona na kumsogelea kumtoa hofu.

“Edna..!!”Aliita Matilda.

“Huyu ndio mtoto wa..”

“Huyu ni wa Ratifa na Msechu”Aliongea na kumfanya Edna kumwangalia yule mtoto na kuishia kutabasamu , alikuwa ni mtoto mwenye afya nzuri.

Upande wa Roma alitumia nafasi ya kumwangalia mtoto wa Omari ambaye alikuwa amebebwa na Neema , ijapokuwa alikuwa ameshatimiza siku arobaini tokea kuzaliwa kabla ya kutimiza miezi kamili, lakini afya yake ilionekana kuwa nzuri.

Kile Roma alichotarajia kukiona ndio kilikuwa hicho hicho , mtoto wa Omari kwa asilimia zaidi ya sabini alionekana kufanana na Yan Buwen , waswahili wanasema baba yake ana damu kali basi ndio ambacho kilionekana alikuwa mweupe kabisa kitu pekee ambacho amerithi kutoka kwa mama yake pengine ni macho tu.

Hata Edna mara baada ya kumuona mtoto huyo aliishia kuguna tu , lakini kwa wakati mmoja akimuona Omari kama mwanaume jasiri , licha ya mtoto kutofanana nae lakini bado tu hakuonyesha kujali na alionekana ni mwenye furaha.

Lilipita kama lisaa limoja wakati Roma akiendeleda kuongea kwa furaha na baadhi ya watu aliokuwa akiwajua , hatimae waliweza kufika wageni wengine ambao walifanya hali ya hewa kubadilika..

Alikuwa ni Raisi Jeremy aliembatana na Raisi Senga na wingi wa mabodigadi uliwafanya baadhi ya wageni kutokuamini watu wakubwa kiasi hicho kuja kwa ajli ya sherehe hio.

Lakini ukweli ni kwamba licha ya eneo hilo kijaa watu wakubwa wakubwa , lakini kuhudhuria kwao kulikuwa na ajenda nyingine.

Baada ya Raisi Jeremy kusalimiana kwa ufupi na Afande Tozo na baadhi ya viongozi wa juu wa jeshi na wa kisiasa moja kwa moja aligeuza shingo yake kuangalia upande ambao Edna amesimama na kisha akamsogelea huku akiwa amepambwa na tabasamu.

“Huyu ni Lanlan si ndio ..?”Aliuliza mara baada ya kumfikia Edna aliemshikilia Lanlan mkono na Edna alitingisha kichwa kukubali.

“Edna unaonaje ukimruhusu baba kumbeba mjukuu wake”Aliongea kwa sauti kana kwamba alikuwa akitaka kila mtu aliehudhuria kusikia kauli yake na ni kweli iliweza kusikika vyema na kufanya baadhi ya watu wasiokuwa wakiujua ukweli kuwa katika hali ya mshangao.

Hakuna ambaye aliamini kama Mrembo Edna na mfanyabiashara mkuwa nchini Tanzania baba yake ni Raisi wa Rwanda , mpaka hapo wengi waliokuwa wakifatilia habari zinazomuhusu Edna walikumbuka miezi kadhaa nyuma skendo ya Edna kutokuwa mtoto wa Adebayo iliosambazwa na sasa kwa kuunganisha Doti ilionyesha kuleta mantiki.

Upande wa Raisi Senga mwenyewe hakutarajia raisi mwenzake kuweka hadharani mahusiano yake na Edna.

Lanlan alimwangalia mwanaume huyo mzee aliekuwa mbele yake na kisha akageuza macho kwa mama yake na akapewa ishara ya kukubali kubebwa.

“Lanlan ni mzito kwa kiasi chake lakini mtiifu na haogopi watu”Aliongea huku akimrusha rusha juu.

“Babu wewe ni nani?”Aliuliza Lanlan na kumfanya Raisi Jeremy kucheka.

“Mimi ni baba wa mama yako , hivyo wewe unaniita babu , Sawa Lanlan”Aliongea kwa sauti huku picha mbalimbali na baadhi ya matukio yakirekodiwa.

“Senior hongera kwa kukutana na binti yako pamoja na mjukuu wako , lakini leo ni siku ya kusherehekea arobaini ya wajukuu wa mzee mwrnzetu hivyo usihamishe ‘attention’ kwa kiasi kikubwa haha..”Aliongea raisi Senga aliekuwa amesimama na Raisi Jeremy kwa utani na kufanya watu wote kucheka.

Baada ya maongezi ya muda mfupi hatimae kila mtu alichukua siti yake kwenye meza maalumu zilizoandaliwa na kukaa , upande wa Roma , Edna , Omari na Queen walikaa meza moja karibu na waheshimiwa.

Sasa zilipita kama dakika arobaini hivi tu ulisikika mtafaruku baina ya watu wawili upande wa kuingilia katika eneo hilo , ulikuwa mtafaruku mkubwa ambao ulifanya swatu waliokuwa upande wa nyuma kwenye ukumbi kuweza kusikia.

“Ngoja nikaangalie”Aliongea mzee mmoja upande wa familia ya Afande Tozo.

Upande wa Roma kadri sauti za mitafaruku hio baina ya watu wawili zilivyokuwa zikiwasogelea upande wao ni kama sauti ya mmoja wapo alikuwa akiifahamu, na ni kweli kwani muda mchache tu waliweza kutokezea watu wawili mmoja alikuwa ni Aloni na mwingine Roma hakumfahamu lakini kwa kumwangalia tu alikuwa ni mchanganyiko wa Muarabu na muafrika.

Meza aliokuwa amekaa Roma na Edna ndio ilikuwa karibu kabisa na wao na mara baada ya Aloni kumuona Roma na Edna aliwasogelea karibu zaidi huku akiwa amemshika yule bwana Kola ya shati lake.

“Binamu upo hapa , huyu mtu alikuwa akiwaongelea vibaya wewe na shemeji”Aliongea pasipo ya kujali watu wa heshima waliokuwa hapo ndani ,ilikuwa ni kama vile amelewa wote wamelewa.

“Aloni mtoto wa Sauli , mwachie mwenzako kwanza”Aliongea yule mwanaume ambaye alisema anaenda kuangalia.

Watu wengi walishangazwa na kitendo cha Aloni kutokana na kwamba walikuwa wakimfahamu aliekuwa ameshikiliwa tai.

“Umesikia wewe mjinga , hebu niachie mimi”Aliongea yule bwana.

Muda huo walinzi walikuwa washachukua tahadhari tayari ya kiusalama kwa waheshimiwa na walishindwa kuwazuia hao mabwana kutokana na kuwafahamu wote.

“Wewe ni Huruna mtoto wa Raisi Hassani!!?, imekuwaje ukawa kwenye ugomvi na Aloni?”Aliuliza.

“Nimeongea kauli ya kumtania tu , lakini mwenyewe akatafsiri vibaya na kukasirika na kuanzisha ugomvi”Aliongea

“Haruna ni familia ipi anatokea?” Roma alimuuliza Edna.

“Sina uhakika kama namjua vizuri..”

“Ni mtoto wa Raisi wa Zanzibar lakini pia mjukuu kwa marehemu mzee Longoli , ndio familia yenye nguvu zaidi Zanzibar na angalau naweza kusema ndio familia ambayo wanashikiria muungano mpaka sasa kutokana na mizizi yao”Alijibu Omari

“Mr Haruna na Aloni kwa heshima ya familia zenu mnaombwa kuacha ugomvi mara moja mbele ya wageni wetu”Alioingea mjomba wa Omari kwa kutahadharisha ila yule bwana Haruna alimwangalia Roma kwanza kwa dakika kama vile anamjua na kisha akageuza macho kukagua kila mmoja na kuishia kutoa tabasamu la kejeli.

“Hakuna mtu wa kunituliza hapa kati yenu , ni muda muafaka leo hii mimi kutoa ya moyoni, ninakwenda kutoa dukuduku langu lote mahali hapa na kila mtu asikie na ole wake mtu aniguse muone , kila mtu hapa anajua baba yangu ni nani”Aliongea Haruna huku akimwangalia Roma kwa macho makali.

Upande wa walinzi walitaka kuchukua hatua , lakini walipewa ishara ya kutulia , walipaswa kuwa makini kutokana na cheo cha baba yake Haruna, isitoshe hivi karibuni baada ya kifo cha kutatanisha cha Mzee Longoli kulikuwa na fukuto linaloendelea chini kwa chini kati ya Visiwani na Bara.

“Haruna kama unashida kwanini usisubiri mpaka baadae kuliko kuharibu sherehe ya mwanangu”Aliongea Omari na kumfanya Haruna kucheka sana

“Eti mwanangu , una mtoto gani , mtoto unaejisumbua kumfanyia sherehe na kukusanya watu wote hawa kumbe ni mtoto wa Yan Buwen mchina , mwanaume mzima umejikaza unajitia na wewe una mtoto, kila mtu anajua Queen alichezewa na Yan Buwen na akaachwa lakini mmekusanya watu wa heshima wote hawa kwa ajili tu ya kusherekehea kiumbe ambacho baba yake alikuwa tishio kwa taifa, kama sio baba yangu kunituma kuja kuwakilisha nisingefika hapa, Ujinga mtupu”

Maneno yake yalikuwa na ukweli mtupu na yalikuwa kama kisu cha moto katika moyo wa Queen , tokea aolewe na Omari familia yake haikuwahi kumtenga lakini alijua tu siku atakayojifungua mtoto hatokuwa na mwonekano na mtu yoyote ndani ya familia ya Omari na huenda mbeleni yeye na mtoto yake kukosa furaha kutokana na wanafamilia kushindwa kuvumilia zaidi.

Kauli ya mwanaume afahamikae kwa jina la Haruna ilimuumiza kiasi kwamba palepale alijikuta akitoa kilio cha kwikwi.

“Queen..!!”Omari aiekuwa pembeni ya mke wake alijikuta akipandwa na hasira mno.

“Wewe mjinga , unathubutu vipi kumfanya mke wangu kulia , umetumwa kuja hapa kuharib hii sherehe si ndio?, Bro Roma hapa anaweza asisite kukuua lakini haimaanishi mimi ni mpole pia”Aliongea huku akisimama.

“Niguse uone nishawatahadharisha nini matokeo yake, nasema hivi nina nguvu iliopo nyuma yangu na asitokee mtu wa kunigusa”Aliongea kwa sauti lakini upande wa Roma kauli ile aliitafsiri kama kutishiwa amani na aliishia kukunja sura kwa dakika na akili yake ilimwambia mtu huyu alikuwa tayari amekwisha kufa na haina haja ya kumuacha hai.

Ni kufumba na kufumbua tu Roma alikuwa mbele ya Haruna na kufanya watu wote kuangalia kwa mshangao akiwemo Lanlan.

“Wewe msukule umefika hapa kwa nia ya kukitafuta kifo na mimi ninakupatia hitajio lako”Aliongea Roma na kabla ya Haruni hajatamka neno lingine palepale alipigwa ngumi kwenye kichwa chake na kikafumuka chote na kufanya vitu vyeupe vyeupe kusambaa ndani ya eneo hilo.

Hata wale mabodigadi wlaiokuwa wakilinda viongozi ndani ya hilo eneo walikosa ujasiri wa kuandelea kuangalia, ilikuwa afadhali watu waliokuwa nyuma sana hawakuona kilichotokea kutokana na mabodigadi kuzingira.

Roma mara baada ya kukamilisha kazi ake aligeuza macho na kuangalia sura ambazo zilikuwa zikimwangalia kwa wasiwasi na kisha akageuza macho yake kwa Lanlan na kugundua binti yake hakuwa na hofu ya aina yoyote na aliangalia kitendo kile kama mtu ambaye ashazoea kuona.

Upande wa Omari na Edna na wenyewe licha ya kuwa katika hali ya mshangao kwa maamuzi alioyafanya Roma lakini walikuwa katika muonekano ambao haukuwa na lawama ndani yake.

Raisi Senga kwa tukio lile alijiambia hata ule mpango aliokuwa nao wa kumkubali kama mtoto wake uliingia dosari.

“Kuua ni kuua tu na anaekufa amekufa na sijali athari zitakazotokea baada ya hapa”Aliongea Roma huku akiangalia kama kuna damu zilizomrukia , licha ya kufanya tukio hilo la kutisha mbele ya watu hakuwa na hatia yoyote.

“Mjomba natumaini utasafisha”Aliongea Roma akimwangalia Mjomba wake Omari na kisha alimsogelea Lanlan na kumshusha kwenye kiti.

“Lanlan ni muda wa kuongozana na baba kwenda kuona wanyama”

“Yess daddy!!”Aliongea Lanlan kwa furaha na kisha Roma akamgeukia na Edna aliekuwa kwenye mshangao lakini alipokutanisha macho na Roma aliishia kusimama na kumwambia wampeleke mtoto kuona wanyama.

Raisi Jeremy aliishia kumwangalia binti yake aliekuwa akitokomea kwenye upeo wa macho yake na kujiambia , binti yake hakika kaoana na mtu zaidi ya shetani .

******

Ni dakika chache tu mara baada ya mwili wa Haruna kuingiziwa Mochwari katika hospitali ya halmashauri zilionekana nyuzi nyuzi flani hivi za aina yake ambazo zilikuwa na rangi nyeusi isiokolea sana zikitoka katika mwili wa Haruni , ilikuwa ni kama vile mwili wake unaoza kwa kasi ya ajabu na kutoa nyuzi kama vile minyoo.

Nyuzi nyuzi hizo zilionekana zikitoka katika mishipa ya damu ya mwili wa Haruni , zilitoka kwa kasi mno na ndani ya dakika chache tu nyuzi zile zilionekana kwenye sakafu zikiwa nyingi mno kama furushi huku zikiendelea kutembea , ilikuwa ni kama minyoo mirefu ilioungana ugana na kutengeneza furushi na ziliendelea kutambaa, mara baada ya kufikia katika upenyo wa mlango zilianza kupotelea nje kwa kujipanga mpaka zikaisha zote kwa pamoja.

Mwili wa Haruni na wenyewe ulibadilika na kubakia kama mtu ambaye amekufa siku nyingi na kuoza kiasi cha kutoa harufu na ilikuwa ni dhahiri watu watakaokuja kuchukua mwili wake kwa ajili ya kwenda kuuzika watakumbwa na mshangao wa aina yake.

Dakika kadhaa mbele katikati ya msitu pembezoni mwa hospitali hio ya halmashauri zile nyuzi nyuzi zilionekana zikijikusanya pamoja na kuanza kuongezeka kwa namna ya kutengeneza umbo ikiwa ni kama v ile ujiuji wa mpira wa plastik ambao haujapoa , kilikuwa ni kitendo ambacho kilikuwa kikifanyika haraka sana , umbo lilianza kama mpira na likaongezeka ukubwa na kuwa kama mtu na ndani ya dakika nyingine mbele muoneno wa nyuzi zile ulibadilika kabisa na kuwa mtu kamili.

Dakika hio hio sehemu ile iliokuwa ikifanyika maajabu ya nyuzi nyuzi aliweza kuonekana Denisi ambaye alikuwa kwenye mavazi ya gwanda za kijeshi huku akiwa na sura ambayo ilikuwa ikionyesha uovu ndani yake.

Denisi alizunguza kichwa chake kwa staili ya kipekee na kufanya misuli ya shingo kama mifupa kusikika ikipishana pishana na baada ya kujiweka sawa alipiga hatua kutoka katika msitu huo na kutokelezea barabarani.

“Hehe… vipi ilikuwa furaha kwako kuweza kuutumia mwili wake, unaonaje baada ya kurudi katika hali yako ya kawaida?”Alilikuwa ni Kizwe ambaye alikuwa kwenye tabasamu na muonekano wake ni kama vile alikuwa akijua Denisi angetokea katika eneo hilo.

“Sikutaka kuharibu mwili wote , nimewaachia familia yake angalau uozo kwa ajili ya kwenda kuzika”Aliongea

“Umeharibika sana , Hasara kubwa sana , Haruna nilikuwa nikimpendea sana kiungo chake cha mwili kilikuwa na nguvu isiokuwa na kawaida”

“Ndio maana nimemuua , kupunguza watu wanaokuchezea”

“Wanaume wa aina yake ni wengi , utaweza kuwamaliza wote?”

“Sijali kama unatafuta wengine lakini hakikisha huzembei kwenye kazi yako “

“Kuwa na amani kila kitu kipo sawa , ni wakati sasa wakusubiri samaki wetu kunasa kwenye ndoano hahaha…”











SEHEMU YA 583.

Upande wa Zoo ya Mkwawa ambayo ipo upande wa kusini mwa mji wa Iringa Roma na Edna walikuwa washatoka kwenye gari na kuanza kutembea kufuata njia ambayo inawapeleka moja kwa moja kuingia kwenye Zoo hio huku wakiwa wamemuweka Lanlan katikati wakiwa wote wamemshika mikono upande upande.

Edna alikuwa amevalia miwani ya jua na kofia ya Hat ili kufanya watu wasimfahamu kwa haraka .

“Daddy Lanlan anataka kuona Tembo tu”Aliongea Lanlan kibonge huku akitembea akiangalia chini kama vile anahesabu hatua za miguu yake.

“Najua unataka kuona Tembo na ndio tunaelekea huko”Aliongea Roma na muda huo aliweza kuona kundi la wazungu wakija upande wao na kumfanya Roma ambebe Lanlan na kumuweka kwenye shingo huku wakiendelea kutembea ili wasichukue nafasi kubwa njiani.

Lanlan kwa namna ambavyo alikuwa ameshikilia shingo ya baba yake ni kama vile alikuwa akiendesha Farasi.

“Itakuwa ngumu sana kumfundisha huko baadae kama utaendelea kumdekeza kiasi hicho”Aliongea Edna.

“Unaambiwa malezi ya mtoto wa kike yanatakiwa kuwa ya upendo , sioni kama kuna ubaya kumfanya akalie shingo yangu wakati tupo njiani kama hivi”Aliongea Roma huku akishika mguu wa Lanlan na kuung’ata kwa namna ya kuutekenya na kumfanya akenue.

Dakika chache mbele waliweza kufika nje ya Zoo hio na kulipia kiingilio kisha wakaruhusiwa kuingia , lakini mara baada ya kuingia hawakuweza kuona Tembo katika Zoo hio na kwasababu eneo lilikuwa kubwa Roma moja kwa moja aliamua kutumia uwezo wake wa kijini kujaribu kuangalia kama kuna Tembo anaepatikana lakini aligundua hio Zoo ilikuwa ni ya wanyama wa kawaida tu.

“Daddy Tembo wako wapi , kwanini siwaonni?”

“Lanlan hakuna Tembo ndani ya hii Zoo , lakini kuna wanyama wengine wa kuvutia unaonaje tukiangalia hao?”Aliongea Roma lakini Lanlan bado alionyesha hali ya kutoridhika , ilionekana kiu yake kubwa ni kuona Tembo na Roma aligundua hilo.

“Lanlan niambie kwanini unapenda kuona Tembo na sio wanyama wengine?”

“Tembo wanampenda Lanlan , kulikuwa na mbwa mkubwaa alitaka kumng’ata Lanlan lakini yule Tembo akamfukuza na pia Tembo alinipa nafasi ya kupanda kwenye mgongo wake na kuendesha”Aliongea Lanlan na kumfanya Roma kushangaa.

“Wewe kibonge nyanya acha kumdanganya baba , ilikuwa ni lini hio na uliwezaje kuendesha Tembo na ilikuwa ni wapi?”Aliuliza Roma lakini Lanlan aliishia kutingisha kichwa chake kukataa.

“Lanlan hajui ni sehemu gani , kuna nyasi ndeefu , jua kali na Farasi wengi pamoja na Mbuzi(Swala) , Babu ndio anapajua lakini aliniambia amesahau panaitwaje , ndio yeye ambaye aliniona nikiwa peke yangu, Lanlan hawezi kudanganya yule mbwa mkali alinisogelea na nikamrushia jiwe lakini bado akawa ananikimbilia ndio maana Tembo akanisadia”

Edna na Roma walijikuta wakisikiliza kwa umakini namna ambavyo Lanlan anahadithia, walijua kabisa hizo ni kumbukumbbu zake za huko alikotoka .

Lakini Roma kwa uelewa wake alijua ni sehemu chache duniani ambazo kuna Tembo wengi ni hapa hapa Afrika na baadhi ya maeneo ndani ya Bara la Asia.

“Lanlan je ulikuwa peke yako au kuna mtu alikuwa pembeni yako?”Aliuliza Edna kwa shauku kubwa.

“Mama umeshasahau , ulisema kabisa unaenda mbali kwa muda mrefu na utakuja kunichukua lakini Lanlan alikuwa na njaa sana hivyo niliondoka na kwenda kutafuta chakula … mama tafadhari naomba usikasirike Lanlan hawezi kukimbia tena”Aliongea huku akimshika mkono Edna kwa kumbembeleza asikasirike.

“Mimi?”Aliongea Edna huku akijinyoshea kidole chake lakini palepale alipotezea baada ya kugundua siku zote Lanlan anamuona yeye kama mama yake mzazi.

Ijapokuwa maelezo yake yalikuwa machache sana , lakini yalionekana kusikitisha.

“Nashindwa kuelewa ni mama gani huyo kuweza kumuacha mtoto sehemu kama hio peke yake”Aliongea

“Tutaujua ukweli wote siku moja tu ,. Lanlan tukaangalie Twigga na Manyani kwanza”Aliongea Roma huku akipotezea ile mada na kumshika mkono Lanlan na kuungana na watu waliokuwa upande wa pili wakiangalia Twiga.

“Daddy yule Nyani anafikiria nini kwanini amenuna sana na anaangalia upande ule muda wote?”

“Lanlan mimi najuaje anafikiria nini na kwanini kanuna , ila ngoja tuone maana baba ni bingwa wa kuchekesha Manyani”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumshangaa.

“Kweli , unajua kuchekesha Manyani?, Daddy , Dady nifundishe na mimi kuchekesha Manyani”

“Hehe ni rahisi Lanlan , na baba yako nitakufundisha namna ya kuyachekesha , unachotakiwa kufanya ni kuniigilizia ninachokifanya”

“Okey Daddy”

Baada ya kuongea Roma alianza kuchekea lile nyani kwa sauti bila aibu na Lanlan na yeye aliigilizia , kitendo chao kilifanya watu kuwaangalia na kuwa kama kivutio na wengine wakiwacheka na walifurahi zaidi mara baada ya yule nyani kutoa meno yake ya njano nje na kucheka.

Upande wa Edna aliona Roma anachomfundisha Lanlan ni cha aibu na aache lakini Roma alimwambia atafanya chochote ili mradi kiwe kinamfurahisha binti yake hivyo asiingiliwe.

“Sijui hata nimekupendea nini mimi”Alilalamika Edna huku akiangalia wanaomwangalia kwa aibu.

“Hehe .. kutokujua kwako ndio maana halisi ya uwezo wangu”Alijibu Roma

******

Ilikuwa ni usiku sana wakati baadhi ya wanafamilia ndani ya jumba la Afande Kweka wakiwa wamelala , Denisi alionekana ndio kwanza anarudi kutoka kwenye starehe zake huku akiwa amelewa kiasi cha kumfanya kuanza kuimba nyimbo ambazo hazikuwa zikieleweka.

Upande wa wafanyakazi na walinzi wala hawakusahngazwa na kuchelewa kwake pamoa na hali yake ya ulevi kwani sio kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza.

Baada ya kuingia eneo la sebuleni kupita kwenda kwenye chumba chake alikuta bado taa zilikuwa zimewashwa na baada ya kuchunguza vizuri alishangaa kumuona Damasi akiwa amesinzia kwenye Sofa na kujikuta akisogea taratibu lakini muda huo huo na Damasi alishituka kutoka kwenye usingizi.

“Umerudi mwanangu , mama yako nilikuwa nikikusubiri na nilijua tu utarudi muda huu kama kawaida yako … lakini mh na hio harufu ya pombe jamani hata kama unaonekana kuwa na mwili wa mazoezi hupaswi kunywa pombe sana , utamfanya baba yako aendelee kutoridshindwa na matendo yako”Aliongea Damasi na palepale alisimama na kuelekea kwenye meza ya chakula na kufungua chakula ambacho amewekewa Denisi na kuona kimepoa na alihamia na upande wa bakuri na kulifungua na kukuta Supu alioandaa na yenyewe imepoa.

“Usiendelee kusimama hapo , njoo ukae hapa nikupashie hii supu ya kuku , itakufanya usijisie vizuri baada ya kuinywa”Aliongea huku akichukua lile bakuri na kuelekea jikoni na kupasha kwa dakika chache na kisha akarudi na kumkuta Denisi bado akiwa amesimama katika eneo moja bila ya kusogea.

“Mama kuna kitu ulihitaji kuongea na mimi?”

“Unamaanisha nini , nilikaa macho kukusubiria ili kuhakikisha angalau umekula na upo salama , hebu njoo ukae acha kuwa mtoto mjinga”Aliongea na Denisi kwa wasiwasi alienda kukaa na kuwekewa karibu ile supu ambao ilikuwa ikitoa harufu nzuri ya kutamanisha.

“Kwahio mama umekaa macho kwa ajili tu ya kunisubiria mimi kunywa supu?”

“Unadhani naweza kuwa kama baba yako ambaye anakufokea kila siku tokea urudi, niliona ni muda mrefu sijawahi kuonyesha kukujali tokea urudi ndio maana , hebu kunywa huko usifikirie sana”

Denisi alijikuta akiangalia bakuli lile la supi ambayo imechanganywa na viungo na kusababisha kubadilika rangi , baada ya kuchota mchuzi kidogo na kunywa aligeuza macho yake kumwangalia mama yake .

“Unaionaje ni nzuri au ina mafuta mengi?”

“Hapana ni nzuri tu”Aliongea na kumfanya Damasi kuvua pumzi na kuzishusha.

“Denisi najua ni mambo mengi yametokea, kutokea kwa kaka yako ghafla najua kumekufanya uwe mnyonge, lakini pia namna baba yako kushindwa kukujali kwa kujiweka bize sana na mambo yake ya siasa , Denisi kama kuna kitu chochote kinakusumbua naomba uniambia na nitakusaidia , nisamehe pia mimi mama yako kwa kutokuwa karibu yako muda wote”Aliongea Damasi na kumfanya Denisi kuendelea kunywa supu yake na kutingisha kichwa.

“Vijana siku zote mnakuwa kama hivi kabla ya kuoa , mimi mama yako najua kabisa wewe ni mkarimu na sio mtu mbaya kama wengi wanavyokuona , hivyo Denisi kuwa makini usimkasirishe mara kwa mara babu yako na baba yako na wao pia hawatoweza kukukasirisha”

Kauli za Damasi zilimwingia kisawa sawa na alijihisi moyo wake kuuma , alijjihisi kitu ambacho kilikuwa kimemshikilia koonni kiasi cha kumfanya ashindwe kuendelea kumeza supu ile.

Mwanamke aliekuwa mbele yake asingeweza kudhania mtu anaeongea nae sio mtoto wake bali yeye ni Joseph Bikindi au Lekcha ambaye anatumia mwili wa Denisi.

Ni sawa na kusema yeye alikuwa ni muuaji wa mtoto wake lakini kutokana na kutofahamu yote hayo mama huyu alitoa mapenzi yake waziwazi kwa mtoto wake

“Mbona unashangaa , kunywa haraka ukalale muda umeenda kama utapenda zaidi nitaenda kukuongeza imebaki nyingi jikoni”Aliongea na kumfanya Denisi kusita.

“Mama , je kaka na shemeji tayari wamekwisha kurudi?”Aluliza na kumfanya Damasi kuwaza kidogo.

‘Tokea waondoke asubuhi kwenda kuhudhiria Sherehe ya Arobaini ya watoto wa familia ya Mzee Tozo hawajarudi mpaka sasa hivi”

“Kuna chochote kilichotokea , kwanini mpaka sasa hawajarudi?”

“Tumeweza kupewa taarifa ya Roma kumuua mtoto wa raisi wa Zanzibar na mpaka sasa hali haijatulia kabisa kwani simu nyingi zimepigwa siku ya leo kuja kwa babu yako lakini hajajibu hata moja na baba yako yupo ndio anahangaika namna ya kutatua mgogoro unaoendelea”Aliongea na kumfanya Denisi kutokuongezea na hakuna ambaye alikuwa na wasiwasi na kutorudi mapema nyumbani kwa Roma na familia yake.

“Denisi mwanangu niambie kama kuna mwanamke unaempenda , kuna siku ulionyesha kumpenda yule msanii Sophia nasikia amerudi Japani kama upo tayari nitaongea na baba yake kuona kama kuna uwezekano kumuoa”Aliongea Damasi akimwangalia Denisi kwa shauku.

“Mama yale yamepita na sasa sina mwanamke ninaempenda ila nikipata nitakuambia , usijali mama yangu”Aliongea na kumfanya Damasi kutabasamu huku akitingisha kichwa kumuelewa mtoto wake.

Baada ya Denisi kufika kwenye chumba chake alijikuta moja kwa moja akienda kusimama katika dirisha huku akilifungua na kuangalia upande wa nje msituni na ghafla tu palepla macho yake yalianza kubadilika rangi huku misuli ya macho ikisimama na kutengeneza michirizi ya mistari ya rangi nyeusi mwili mzima.

“Wewe sio mama mama yangu ,,,, eti mama hahaha ,, mama yangu alishafariki”Aliongea hukua akianza kucheka na kung’ata meno kwa hasira kama vile mtu ambaye yupo kwenye maumivu makali , ilionekana ni kama alikuwa akipatwa na hatia kwa kumuua Denisi na kutumia mwili wake na kumchanganya mama yake, alijua siku ambayo ataachana na mwili wa Denisi itakuwa ni kama kilichomtokea Haruna.

*********

Siku iliofuata muda wa mchana wakati Raisi Senga na Afande Kweka wakijadiliana namna ya kumaliza swala lililojitokeza hatimae Roma na Edna pamoja na mtoto wao waliweza kurudi.

Kila mtu alimshangaa Roma mara baada ya kufika hapo ndani lakini upande wa Roma hakujali macho ya watu , alishajua alichokifanya jana lazima kingeleta athari kwa familia hio lakini alijiambia si baba yake ni raisi na babu yake ni mkuu wa majeshi mstaafu basi wanapaswa kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo.

Lanlan ambaye hakujali kinachoendelea alimkimbilia babu yake mkubwa na kwenda kumkumbatia mara baada ya kuingia eneo la sebuleni na kumuhadithia namna ambavyo ameweza kuona Tembo.

Afande Kweka alishangaa na kumuuliza Lanlan ni wapi kaweza kuona Tembo na maelezo yake yalimfanya sasa kuelewa ni wapi Roma na familia yake walilala na kutokurudi jana usiku , ilionekana Roma baada ya kutopata Tembo ndani ya eneo la Iringa alimchukua Lanlan na kwenda kuwatafuta katika mbuga za wanyama.

Ukweli ni kwamba asubuhi yote hio Afande kweka na Raisi Senga walikuwa wakijaribu kutuliza moto kutokana na familia ya raisi wa Zanzibar kuhitaji Roma kufikishwa mbele ya sheria kwa kutekeleza kifo cha mtoto wao.

“Roma kwanini jana ukaamua kumuua Haruni mtoto wa Raisi wa Zanzibar, mpaka muda huu bado familia yao inatushuku kwa kuhusika kwa kifo cha Mzee Longoli kwanini umeongeza mafuta ya petroli kwenye moto unao waka?”Aliuliza Afande Kweka.

“Mzee nilichokifanya ni kama kumsaidia tu yule bwana kwani hakuwa kwenye akili yake timamu”Alingea Roma na kufanya washangae na hata Edna mwenyewe ambaye hakuhoji kile kilichotokea alitaka kusikia nnini Roma anamaanisha.

“Yule Haruni akili yake ilikuwa ikiendeshwa na hakuwa katika utimamu wake sawa sawa , sijui tabia ya maisha yake ya nyuma lakini jambo moja ambalo ninaweza kusema ni kwamba alichokifanya jana kama mtoto wa Raisi mwenye akili timamu asingeweza kufanya vile”Aliongea Roma na kumfanya Raisi Senga mwenye kuwaza.

“Ni kweli hata mimi nilishangaa , Haruni ni kijana ninaemjua na ni mwenye utulivu wa aina yake na alikuwa akisimamia asilimia kubwa ya biashara za familia yake”

“Roma unamaannisha nini kusema hayupo kwenye utimamu wake?”Aliuliza Edna ambaye alionekana kutoridika na maneno ya Roma.

“Namaanisha alikuwa kama Roboti , kulikuwa na nguvu ya ziada ambayo ilikuwa ikimwendesha , kwasasa sitoongea sana lakini naamini muda si mrefu kila kitu kitakuwa wazi tuweni wavumilivu”Aliongea Roma na kufanya Raisi Senga kuvuta pumzi mwanzoni alikuwa na mpango wa kumuweka Roma karibu yake lakini matatizo ambayo amekuja nayo Iringa ni kama yalimfanya kuanza kusita sita.

“Senga najua Roma ni mtukutu sana na mwenye hasira na asiejali athari zinazotokea lakini hili swala la Haruni tunapaswa kumuamini , kikubwa ni kuanza ufanya ucuhuguzi wa kupata ushahidi wa maneno yake”Aliongea Afande Kweka.

“Lakini baba nani anaweza kuamini kitu kama hichi?”

“Haina haja ya kuwaaminisha kwasasa , tunapaswa kuwapa sababu ya kuamini lakini sasa hivi ni mapema hivyo tafuta mbinu ya kuvuta muda huku uchunguzi ukiendelea”Aliongea na kisha akamchukua Lanlan na kuondoka nae na kumfanya Raisi Senga kumwangalia Roma kwa dakika kadhaa na kisha alisimama na kuaga na kuondoka.

Dakika chache tu mara baada ya raisi Senga kutoka , simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Omari na alipokea palepale.

“Roma ulikuwa umeenda wapi , kwanini umetoweka ghafla na simu yako haikuwa ikipatikana?”Aliuliza Omari bila hata ya kusalimia kama mtu mwenye wasiwasi.

“Kuna kilichotokea mpaka kuwa na wasiwasi namna hio ya kunitafuta mara nyingi?”

“Hakuna kilichotokea , hata hivyo ni bora umepatikana ndani ya muda muafaka, unaonaje leo tukitoka usiku”

“Kwenda wapi?”

“Kuna Club maarufu imefunguliwa hapa Iringa mjini inaita Pink Lady , binamu yako Aloni katualika leo hii kuhudhuria”

“Sina mpango wa kuhudhuria Club nishaachana na hayo maisha , kwanini usiende wewe peke yako?”

“Bro unajua mwenyewe natafuta kisingizio cha kutoka usiku , tokea nimeoa mara nyingi saa kumi na mbili nipo nyumbani , lakini kama utakubali itakuwa rahisi ya kuaga na kuondoka bila kuleta wasiwasi kwa mke wangu”Aliongea Omari na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli alijiambia haikuwa mimba ya Yan Buwen tu lakini Omari na mke wake alikuwa akimuogopa.

“Basi hakuna tatizo , nitahudhuria”Aliongea Roma na Omari alicheka kwa furaha na kisha akakata simu.

Upande mwingine dakika kadhaa tu wakati Raisi Senga akiwa safarini kuelekea jijini Kabwe alimwangalia mheshimiwa mara baada ya kuona kitu katika simu yake.

“Nini unataka kuongea”

“Kuna picha imetumwa na mtu wetu kutoka ikulu ya Zanzibar”Aliongea Kabwe na palepale alimsogezea karibu mheshimiwa na kumuonyesha.

“Hiki ni kitu gani?”

“Ni mwili wa Denisi ulivyokutwa Mochwari dakika kadhaa tu baada ya kuhifadhiwa”Aliongea Kabwe na kumfanya Raisi Senga kuzoom vizuri ile picha na kuonyesha mwonekano wa kutokuamini.
 
SEHEMU YA 585.

Roma mara baada ya taarifa hio kugonga masikio yake alianza kujiuliza maswali , alijiuliza imekuwaje alama zake zikawepo na ni nani ambaye amefanya mauaji hayo kwa staili inayofanana kama ya kwake, alijua kabisa tukio hilo limetengenezwa kumchafua lakini alishindwa kujua muhusika mkuu ni nani.

Alijiambia kama ni kupindi cha nyuma basi moja kwa moja angejua aliefanya hivyo ni Yan Buwen lakini tayari amekwisha kumuua hivyo hakuweza kukisia ni nani kwa wakati mmoja zaidi ya kuwa na hisia tu za kushuku baadhi ya watu.

Damasi na Edna waliweza kusikia taarifa hio pia na alijikuta akiwa na wasiwasi mkubwa huku akiwa na wasiwasi juu ya Roma, ijapokuwa alijua Roma alikuwa ni mwepesi kuua mtu lakini moyo wake ulimwambia kabisa sio yeye , lakini kwa maelezo aliopatiwa alikosa ushihidi wa kumkingia kifua..

Upande wa Jopo lote lilimwangalia Roma kwa macho ya hasira , ni Afande Tozo na Afande Kweka pekee ambao walionyesha kuwaza.

“Afande Maeda kulingana na Ripoti inavyosema ni Mr Roma ambaye amehusika si ndio?”Aliuliza Afande Tozo akivunja ukimya.

“Ndio Afande?”

“Je uchunguzi uliofanyika umeweza kujua ni sababu gani ambayo Roma alimuua Aloni , kwasababu huwezi kuua tu bila sababu na wote hapa tunajua kabisa familia ya Aloni na familia ya Afande Kweka ni ndugu upande wa wakwe, ushahidi ambao upo kwasasa ni wa alama za vidole na namna kifo kilivyotekelezwa lakini hakuna dhamira yoyote ambayo inamfunga Mr Roma kutaka kumuua Aloni””

“Afande baada ya tukio hilo polisi waliweza kfanya uchunguzi zaidi na waliweza hadi kufanya mahojiano na mmiliki wa Hoteli na Club ya Pinky Lady na kwa maelezo yake amesema siku ya jana kulitokea mgogoro kati ya Roma na Aloni”Aliongea Afande Maeda na kufanya watu wote kushangaa kidogo.

“Mgogoro umesema , ni mgogoro gani?”Aliuliza Raisi Senga kwa shauku.

Muda huo Damasi na Edna waliweza kuruhusiwa kuingia kujua kinachoendelea na Edna alikuwa ameambatana na Lanlan na walikuwa wakisikia kile kinachoendelea hapo ndani na hakuna ambaye aliwazuia.

“Maelezo ya mmiliki anasema Mr Roma na Aloni walitokea kugombania mwanamke aliefahamika kwa jina la Fetty Abdully , baada ya kitolewa kwa maelezo hayo polisi walijaribu kuhoji baadhi ya walinzi wa hoteli hio na wenyewe walikiri kutokea kwa mgogoro huo kwani walishuhudia Mr Roma akimfukuza Aloni kwenye chumba ambacho alikuwa na Fetty na kubakia nae yeye”

“Lazima polisi na wao watakuwa wamemkamata na Fatty kumhoji , maelezo yake yako vipi?”Aliuliza Raisi Senga na kumfanya Roma aliekuwa kimya kuzidi kupatwa na shauku , hakushangaa sana kwani jana alijua kwanzia kualikwa kwenda kwenye ile Club kuna mtego aliokuwa akiandaliwa lakini alikuwa akimwamini Fetty ndio maana alisikiliza kwa umakini.

“Polisi walipofanya mahojiano nae ya mwanzo alikiri kwamba alikuwa alikuwa na miadi na Mr Aloni lakini wakati wakiwa chumbani ndipo alipofika Mr Roma na kumfukuza Aloni na ndio sababu ya kutokea ugomvi baina yao”

“Afande kwa hio unasema maeneno hayo katamka Fetty mwenyewe? Na kama ni kweli je naweza kumhoji mimi mwenyewe?”Aliuliza Roma kimtego mara baada ya kumwangalia Edna ambaye alikuwa na mwonekano usioelezeka lakini kauli yake ilimpa uso wa huzuni afande Maeda.

“Fetty mara baada ya mahojiano ya muda mfupi aliachiwa huru kwa kupewa maagizo ataitwa muda wowote kwa mahojiano zaidi lakini asubuhi ya leo amekutwa amejinyonga kwenye chumba alichopanga”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu.

“Afande kwa taarifa hio unatoa hitimisho gani?”

“Kwa taarifa iliopo nadhani haijitoshelezi kusema Mr Roma ni muhusika , kuna mengi hapa ya mashaka ambayo tunapaswa kwanza kuyafanyia uchungzi”Aliongea.

“Kuna haja gani ya kufanya uchunguzi zaidi ilihali kila kitu kinajieleza , mimi maoni yangu ni haya wakati haya yakiendelea ili kutuliza hali kwanini Mr Roma asikamatwe kwanza na kupelekwa kituoni ili kuituliza hali?”Alishauri mwanajeshi mzee kidogo ambaye Roma alimfahamu kuwa ndugu yao upande wa bibi yake ,yaani mke wa Afande Kweka , alikuwa akiitwa Afande Kigoda..

“Mzee kigoda unapendekeza nikamatwe kwa kosa lipi labda?”

“Wewe hujui makosa yako , kila kitu kinachoendelea wewe ndio chanzo , hatuwezi kuruhusu uendelee kuwa huru ilihali umeleta machafuko ndani ya taifa linalosifika kwa amani , maoni yangu nadhani kila mmoja hapa anaunga mkono”

“Nimekuuliza swali acha kuzunguka , napaswa kukamatwa kwenda kituonni kwa kosa gani?”

“Kwa kosa la kumuua Aloni na mtoto wa Raisi wa Zanzibar haina haja ya kuelezea zaidi ilihali kila kitu kipo wazi”

“Namuunga mkono Mzee Kigoda hapa , nadhani kukamatwa kwa Mr Roma kutasaidia kupunguza hasira za wananchi , kwani nia yao ipo wazi wanachotaka ni Mr Roma kuwajibishwa kisheria kwa makosa yake”

“Ujinga, unadhani ninaweza kukubali hilo kutokea , muda na saa ambayo Roma akikamatwa na polisi mimi ndio ninaekwenda kuchafuliwa kisiasa”Aliongea Raisi Senga.

“Mheshimiwa nisamehe kwa kusema haya , lakini ndio suluhu ya kwanza kabla ya kufikiria mbinu nyingine”

“Kama sitokubali kwenda polisi unakipi cha kufanya?”Aliongea Roma.

“Nipo radhi kufa mbele ya kila mmoja ila sio kuona taifa hili likichafuka kwa ajili yako, hivyo lazima ukamatwe na upelekwe mbele ya sheria”Aliongea Mzee Kigoda.

“Kama upo tayari kufa basi ngoja nitekeleze kifo chako hapa hapa”Aliongea Roma na sekunde tu alikuwa mbele ya Mzee Kigoda na kumtoa kwenye kiti chake kwa kumshikilia shingo.

Kitendo kile kiliwafanya watu kuwa katika hali ya wasiwasi na kuanza kumsihi Roma apuguze jazba lakini alionekana amedhamiria kufanya kile anachotaka kufanya.

“Roma unafanya nini hebu acha ukichaa wako?”Aliongea Raisi Senga kwa kuamrisha lakini Roma hakuonyesha kumsikiliza.

“Roma msikilize baba yako anachokuambia , ukimuua utaongeza tatizo lingine , hebu muachie”Aliongea Afande Kweka.

“Mzee tangu lini nikagopa, kama ni matatizo tayari ninayo kwanini nisiyapunguze kwa kumuua na huyu anaekitaka kifo”Aliongea Roma na kuzidi kukaza mkono na kumfanya Mzee Kigoda kutapa tapa .

“Roma mume wangu naomba uache , Lanlan anakuangalia”Sauti ya Edna kutoka mlangoni ilisihi kwa urulivu na kumfanya Roma kugeuza macho na kumwangalia Lanlan aliekuwa akimwangalia kwa shauku na alijikuta akivuta pumzi , alishaua mbele ya Lanlan kwa mara ya kwanza hakutaka kufanya hivyo kwa mara pili mbele yake kwani aliona kabisa ni mfano na kumfanya Lanlan asijali maisha ya wengine.

“Una bahati sana binti yangu yupo mbele yangu la sivyo ingekuwa mwisho wako, narudia tena siogopi kumpatia mtu hitajio lake hata kama ni la kifo”Aliongea kibabe na kupelekea eneo lote kuwa katika hali ya ukimya hata Raisi Senga mwenyewe alikuwa akimuogopa mtoto wake.

“Afande Maeda tumefanya kazi kwa kipindi kirefu na nadhani hata wewe mwenyewe kuna kitu unafikiria kama mimi , hivyo nitakuachia hili swala uendelee nalo”Aliongea Roma na kisha alimshika Lanlan mkono na kuondoka nae eneo hilo akifuatiwa na Edna.

Huku nyuma kila mtu alijikuta akivuta pumzi ya ahueni mara baada ya kuona hakuna baya ambalo limetokea.

“Afande anamaanisha nini kusema unajua kinachoendelea?”Aliuliza Afande Tozo.

“Afande kwasasa nina maneno pekee ambayo hayaa ushahidi , ninaweza kuongea ninachofikiria lakini naweza kuonekana nimechagua upande”

“Tunataka kusikia hayo maneno hata kama hayana ushadhidi”Aliongea lakini palepale raisi Senga alinyoosha mkono kuzuia watu wasiongee.

“Afande Maeda kama huna ushihidi haipaswi kuongea, kwanzia sasa nakupakazi ya kusimamia swala hili kikamilifu na kuchunguza ni ni kinaendelea , naamini kuna maswaa ya chini chini yanaendelea na mimi siyajui , hivyo nataka ripoti mapema sana kabla ya kesho”Aliongea baada ya hapo maelezo mafupi ya kila mtu kuimia wazijibu wake yalitolewa na kikao kikaisha.

Upande wa Roma asubuhi yote aliitumia kumfundisha Lanlan namna ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi na roma alifurahi kuona maendeleo yake yalikuwa makubwa sana kwani aliweza kuvuka levo ya kwanza ya kujifikiria yeye mwenyewe na sasa aliingia katika levo ya kufikiria wengine na kujisahau yeye mwenyewe.

Mpaka muda wa chakula cha mchana Lanlan alikuwa akielekezwa na mara baada ya kula chakula cha mchana tu alikimbilia kitandani mwenyewe na kulala na kumfanya Edna kumuonea huruma binti yake na kuona alikuwa akisumbbua saa kichwa mpaka kumpeleka kupatwa usingizi wa haraka namna hio lakini hakutaka kutia neno kwani alijua yote hayo yanafanyika kwa ajili yake.

Mnda wa jioni Roma mara baada ya kuongea kidogo na Afande Kweka alirudi chumbani kumtafuta Edna lakini hakuwa amemuona na alijikuta akimuuliza mfanyakazi ameelekea wapi na ndipo alipoambiwa kwamba yupo nyuma ya bustani amekaa.

Roma mara baada ya kufika upande wa nyuma alishangaa kumuona Edna akiwa amekaa bila ya kufanya chochote huku akiwa amekodolea mti macho kama vile ulikuwa na kitu cha ajabu , lakini haikuwa hivyo Roma aliweza kugundua Edna alikuwa ni mwenye mawazo.

“Boss Edna tokea ustaafu kazi umekuwa ukiota ukiwa macho kwa saili hio utageuka kwua mjinga kabisa”Aliongea Roma mara baada ya kukaa pemeni yake na kumfanya Edna kumfinya kwenye paja.

“Wewe ndio unaanza kuwa mjinga , hivi huoni matatizo haya yote yanaoyendelea kuwa magumu sana kiasi cha kushindwa kujua nini chanzo chake?”

“Unamaanisha kwanini alama za vidole vyangu zikapatikana katika mwili wa Aloni si ndio?”Aliuliza Roma mara baada ya kutoa kicheko hafifu.

“Hicho ndio kinachoniumiza kichwa na kunifanya nishhuku kila kitu kinachoendelea na isitoshe alama za vidole haziwezi kuwa feki na familiaya Aloni lazima wataongea mambo ya ajabu , unakwenda kuelezea vipi hili?”Aliongea Edna.

“Unakumbuka kile kipindi kuhusu Clones alizotengeneza Yan Buwen ? Namaanisha watu waliotengenezwa maabara kwa kutumia seli za mwili wangu?”Aliuliza Roma na kumfanya Edna kuonyesha hali ya kuchanganyikiwa kidogo.

“Unamaanisha kwamba Yan Buwen hakufariki?”

“Sijasema kwamba anaweza kuwa yeye , ninachotaka kusema ni kwamba kifo chake haikumaanisha kwamba matokeo ya majaribio yake ya sayansi na yenyewe yamefikia mwisho , Isitoshe licha ya kufa kwake hatukuwahi kujua maabara yake ipo wapi?”

“Mimi najuaje hayo yote , siku zote unafanya mambo kwa kunificha , lakini kama kuna uwezekano huo nadhani linaleta matinki , lakini hii inamaanisha kwamba adui anafanya mambo yake gizani wakati sisi tukiwa tunaonekana , naamini utakuwa na shauku kubwa kwanini hao maadui wanajaribu kutulenga sisi?”

“Ukichana na hayo nimejikuta nikijawa na shaku kuhusu huyu msichana anaefahamika kwa jina la Fetty nia yake halisi ilikuwa ni ipi , mtego ambao wameniwekea umenifanya nijishangawe kuweza kuchezewa akili na muhudumu wa bar”

“Mhh … inaonekana jana ulikuwa ukila raha kwenda mbele kiasi cha kugeuka kipofu”Aliongea huku akitabasamu kwa uchungu.

“Sikuwa hivyo , kwanza nnitawezaje kura bata ilihali mwanamke ambaye ni shushu alikuwa karibu yangu ?”

“Mwanamke shushu unamaanisha nini?”Aliuliza Edna kwa shauku na Roma hakutaka kuficha kilichotokea jana usiku na alimwambia kila kitu na kumfanya edna kusangaa.

“Sasa kama ulijua huyo mwanamke hakuwa na jema kwanini ukamuacha , kwanini hujamkamata kwa ajili ya mahojiano?”

“Nimkamate? Hakuwa na lolote zaidi ya kutumika tu na kubwa zaidi sikuwa na ushihidi wa kusema kwamba ananipangia njama , na kama nigefanya hivyo unajuaje kama angejiua na yeye na kunifanya nionekane muuaji?”Aliongea na kumfanya Edna kumuelewa nia yake.

“Kama ni hivyo mpango wako ni nini , nimesikia kwamba ukiachana na raia wanao adamana lakini na kesho pia jeshi abalo lipo visiwani mpango wao ni kufanya Parade ya shinikizo, nina uhakika kila kitu kimeandaliwa kwa ajili ya kukupa lawama”

“Hakuna kitu kama hicho , unadhani atakuwa hai kufanya maandamano hayo?”

“Honey unamaanisha unapanga kwenda ku..”Aliongea Roma huku akishindwa kuzuia tabasamu lake la kikatili na akaingiza mokno kwenye mfuko wake wa Jeans na kutoa simu.

“Unadhani maandamano yao yanaweza kuwa na nguvu kwasababbu tu Kamanda mmoja wa jeshi kaamua kukiuka sheria za nchi, nadhani haitakuwa mbaya nikiingilia hili swala , nni bora kafara za watu wa chache kwa ajili ya amani ya nchi na naamini kila mtu ataelewa nini maana yangu”Aliongea Roma huku akitoa Lock simu yake ambayo hakuwa ameigusa tokea asubuhi na alikuwa akipanga kumpigia Makedon ajaribu kumsaidia kupitia koneksheni zao kujua eneo ambalo yupo Afande Razaq.

Lakini sasa simu yake ilionyesha ilikuwa na ujumbe wa meseji ambao ulikuwa umeingia muda mrefu na aliufungua na kuusoma maana namba ilikuwa mpya na alijikuta akibadilika na kumfanya Roma kumwangalia.

“Unasoma nini , mbona uko hivyo?”Aliuliza Edna na Roma alimpatia simu yake kujionea mwenyewe.

“Asante kwa kujitoa kwako kumsaidia msichana masikini kama mimi kutoka kijiji , naomba unisamehe kwani nilifanya yote kwa kuhofia usalama wa wazazi wangu pamoja na wadogo wangu , walinichoma na sindano ya mgonjwa alieambukizwa na Ukimwi na wakaniambia maaamu kama nitafuta wanachoniambia hawatoniua na familia yangu itaweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa , najua nyie ni watu wazuri lakini kila mtu anashida zake anazopambana nazo , samahani sana..”

Ijapokuwahakukuwa na jina lakini ilikuwa ni dhahiri kabisa mtumaji alikuwa nani .

Kulingana na muda iliotumwa ilikuwa ni saa kumi na moja kamili za aflajiri.

Edna alijikuta akitokwa na machzoi mara baada ya kusoma meseji hio iliotumwa mara tatu kupunguza urefu na alijikuta akimrudishia Roma simu yake.

“Nadhani nimejua kwanini ulishindwa kugundua, ni kwasabababu alikuwa katika hali ya woga sana na alifanya yote kutii kutokana na kutishiwa lakini hakuwa na namna ya kujua cha kufanya”

“Hii inanitekenya zaidi na ziadi kujua nani yupo nyuma ya haya yote , huyu mtu inaonyesha anatumia hila zaidi hata ya Yan Buwen”Aiongea Roma

*******

Upand mwingine nchini Rwanda raisi jeremy alikuwa na kila taarifa ya kinachoendelea nchini Tanzania na hio yote ni kutokana na kupandikiza msururu wa majasusi katika kila idara.

Mudahuo wa jioni alikuwa nyumbani kwake na kama kawiada wale watu wawili kutoka miliki za kijini hawakucheza nae mbali kutokana na kuhofia usalama wake.

“Jeremy kwanini hhuongei chochote , je kuna uwezekano kuwa na makosa kwa ripoti iliotumwa?”

“Ripoti hii ni ya kuaminika sana kwani mtu alienitumia ni mtu wangu ndani ya Tanzania ambaye anajua mambo mengi yanayoendelea kwenye mzunguko wao”

‘Kwahio kama ni hivyo inamaanisha kwamba familia ya Kweka ipo kwenye anguko la kupoteza nguvu yao na kama utabiri wangu upo sahiihi itahusisha mgongano wa ndani kwa ndani , Roma ana muunganiko wa moja kwa moja na familia yake na sina uhakika kama anaweza kutatua kinachhoendelea, vipi hakuna namna nzuri ya kutoa msaada ili kujenga nao ukaribu?”Aliuliza na kumfanya Raisi Jeremy kufikiria kidogo.

“Upo sahihi lakini mpaka sasa kuna kitu kinaniumiza kichwa sisi tumeweza kupata taarifa hii lakini mkuu wa majeshi bado hajui kinachoendelea na hata kwa taarifa nizliokuwa nazo Senga hajui kinachoendelea hii inamaanisha hata baba yake hajui licha ya kwamba wana mlolongo wa intellijensia karibia kila kona ya nchi , hata hivyo hili ni swala ambalo nilitabiri litatokea tangu kifo cha Mzee Longoli na Kigombol”

“Kama una uhakika hii taarifa hawaifahamu kwanini tusiwavujishie na kujilinda na mpango unaoendelea?, itakuwa ni msaada mkuwa tumewapatia na mipango yetu ya baadae itakuwa imara zaidi kama tutakuwa tunaungwa mkono na familia yanye nguvu Tanzania na Kenya?”

“Unajua kwanini nimekuwa imara katika idara ya intelijensia kwa miaka mingi?”Aliuliza Raisi Jeremy na Nix alitngisha kichwa kwamba haelewi.

“Serikali ya Tanzannia inajua mara nyingi nina mashushu ndani ya taifa lao kutokana na kujua taarifa nyingi , lakini mpaka leo mfumo wangu wa ki intellijensia hawajui namna unavyojiendesha , hii yote ni kutokana na ninacyochakata kila taarifa inayonifikia , kama nikivujisha moja kwa moja hii itaarifa na mpango huu ulivyokuwa umesukwa kwa siri basi nitatoa mwanya wa wao kuelewa intellijensia yangu inavyofanya kazi “

“Kma nni hivyo unapanga kutulia na kuangalia tu?”Aliuliza na kumfana kufikiria kwa muda na ksiha akatoa tabasamu.

“Kinachotokea kwa sasa ni Power Balance , baada ya kifo cha kigombola kutokea mzani iliokuwa katika uwiano uliyumba , kama ujuavyo Kigombola alikuwa na nguvu nyingi sana kwenye upande wa siasa na ndio maana alifanya anavyotaka licha ya kustaafu kwake, mfumo wake ulikuwa mzuri lakini alichokosea ni kujijumlisha katika msingi wa mfumo wake na baada ya kifo msingi umeyumba sana ,natamani sana kuona namna swala hili linavvyoisha , ila kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho Senga anajua kila kitu kinachoendelea”

“Unamaanisha nini?”

“Senga na baba yake ni watu wawili wenye miazamo tofauti , ukitaka uijua maana yangu lazima ujue historia ya Senga katika harakati zake za kuwania uraisi, icha ya Senga kuwa kiongozi wa taifa lakini hakuwa na nguvu kisiasa kama Kigombola , hili linakupa picha gani?”Aliuliza Raisi Jeremy na kumfanya Nic kutingisha kichwa , ilikuwa ni haki kwake kutokelewa kwani hakuwa mwanasiasa.

“Picha ya moja kwa moja inatuonyesha kabisa kuna mstari uliotenganisha famiia ya Kweka na maswala ya kisiasa na ndio maana nikasea Senga na baba yake ni watu wawili wenye mitazamo miwili tofauti na ndio maaha hakuwahi kuwaza kumrithisha nafasi yake mtoto wake bali akamchagua Roma”

“Kwahio unamaanisha yule mzee hataki nguvu yake ya kijeshi ikiingiliwa na siasa na anataka iwe hivyo milele?”

“Nadhani mshaanza kunipata?”

“Kama hayo ni kweli kwanini unasema Senga anahusika katika hili?”

“Senga anahitaji kijijengea nguvu ya kisiasa nchini , anataka nguvu yote ambayo alikuwa nayo Kigombola ihamie kwake lakini kwa wakati mmoja watu ambao walikuwa chini ya Kigombola wanataka kuendelea kuimarisha nguvu ya kisiasa ilioachwa lakini kikwazo chao kikubwa ni Roma , hivyo haya yote yanayoendelea ni kutaka kupunguza nguvu ya Roma na asiwe na uhalali wa kuwa na nguvu ya kumrithi babu yake , licha ya hivyo naamini kuna nguvu nyingine ambayo imefanya haya yote kutekelezwa , namaanisha watu wa kigombola wamepata nguvu ambayo wanaamini inaweza kumshinda Roma , upande mwingine Senga kama Raisi naamini anajua vikao vyote vya siri ambavyo vinafanywa na hawa wanasiasa walipo chini ya Kigombola wakiongozwa na mke wake lakini kaamua kunyamaza na kutochukua hatua”

“Bado umeniacha hapo?”

“Ninachotaka kumaanisha ni kwamba Senga kaamua kucheza mchezo wa kubahatisha , kaamua kutulia ili aone ni maamuzi gani ambayo mtoto wake Roma atayachukua kutatua hili tatizo na bila kuzingatia njia yoyote matokeo yoyote chanya yatakayotokea yatampa nguvu kubwa kisiasa”

“Kwamba anaamini swala hili Roma ataweza kulimaliza na kama atalimaliza inamaanisha ni kwamba atakuwa amepunguza nguvu ya owte walipo nyuma ya huu mpango na automatically nguvu ya kisiasa itarudi kwake?”

“Ndio”Aliongea huku akitabasamu na kumfanya Nix na mwenzake kuangalia.

“Hizi ndio mnaita siasa?”

“Hahaha.. wazee wangu mkisikia siasa mchezo mchafu ndio hiki kinachotokea ndio maana nakaa kimya nione kinachoendelea , ila nitatumia nafasi hii kuwasiliana na Edna kumuonyesha namna gani namjali na kumwambia awe makini”Aliongea.

“Ukishawasiliana nae moja kwa moja atajua kabisa unajali si ndio?”

“Hahaha… ndio maana yake, Edna ni binti yanguna udhaifu wake mkubwa ni familia”Waliongea na kucheka.

*****

Upande mwingine ndani ya ikulu ndogo nchini Iringa raisi Senga alikuwa bize mno na kazi na mbele yake kulikuwa na mafaili ambayo taarifa zake ni za siri.

Moja ya mbinu kubwa inayotumiwa na maraisi pale wanapofanyia kazi jambo lenye unyeti wa hali ya juu ni kujipa likizo ya kikazi na kutoka ikulu na kwenda kufanyia kazi katika ikulu ndogo au kusafiri nje ya nchi kikazi , hizi ni mbinu moja wapo zinazotumika sana na ndio alichokuwa akikifanya Raisi Senga , lica ya kwamba ilijulikana yupo Iringa kwa likizo ya kikazi lakini kwa namna ambavyo anafanya kazi usingekubali.

Sababu ya kufanya hivyo ni kupunguza uvujaji wa kile kinachoendelea , mara nyingi ikulu ni taasisi na taasisi huhusisha watu wengi na katika watu wengi huwezi kuamini wote kwani hata mpishi wako tu anaweza kuwa shushu , lakini kama ukitoka nje ya nchi au kwenda kukaa kwenye ikulu ndogo basi unapunguza nafasi ya aarifa kuvuja.

“Nipe ripoti Kabwe”Aliongea Raisi Jeremy mara aada ya kumruhusu mtu aliekuwa akigonga mlango.

“Mipango inaendelea kama walivyopanga lakini tumeshindwa bado kujua muhusika mkuu mpaka muda huu?”

“Vipi kuhusu Denisi?”

“Hajaonyesha ishara yoyote kama anahusika”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kukuna kichwa.

“Hisia zangu zinaniambia kuna kitu kimemtokea Denisi lakini nashindwa kulitbitisha hili , hofu yangu ipo kwa mke wangu”

“Mheshimiwa tokea Dennisi alvyorudi nimeweza kuona wasiwasi wako , lakini bado kwa upande wangu sijaona utofauti wowote”

“Kabwe ukisikia damu nzito kuliko maji hii kauli usiichukulie kirahisi , kuna tofauti kubwa kati ya baba na mama katika muunganiko wa kihisia,Denisi(Roma) ni mtoto ambaye nilimpenda sana wakati alipozaliwa na siku zote ambazo niliishi nikijua amefariki nilitamani kurudisha siku nyuma na niliishi kwa kuhesabu kila umri wake na kujiambia mwaka huu Denisi angekuwa na muonekano huu na ikifika mwaka mweingine nitasema ana muonekano huu , lakini ajabu hata baada ya Denisi kurudi akiwa hai ule muunganisko wa kihisia kati yangu na mtoto wangu umeondoka, hisia zangu zinanniambia kuna kitu hakipo sawa kuhusu Roma licha ya kwamba kila kitu kinaniambia ni mtoto wangu niliemzaa , lakini ukija kwenye swala la Denisi ninapatwa na hisia ambazo nashindwa kuzitafsiri ni nusu ya zile nilizopata nipojua Roma yupo hai na nusu yake nimeshindwa kuifahamu ndio maana nazungumza kuna kitu kimemtokea Denisi au kuna kitu kinakwenda kumtokea”Aliongea kwa kirefu Mheshimia Senga na kumfanya Kabwe kutingisha kichwa kumuelewa.

“Kabwe hivi unajua ni ipo hofu ya raisi aliekuwa madarakani?”Aliuliza Raisi Senga na kumfanya Kabwe kutingisha kichwa kwamba haelewi.

“Kila raisi ambaye yupo ikulu hofu yake yote ni maisha mara baada kustaafu na kuachia madaraka”Aliongea na kumfanya Kabwe kutoa macho kidogo ya mshangao lakini aliwaza na kujikuta akielewa.

“Mheshimiwa kama mpango wako ukienda sawa naamini hutokuwa na hofu ya kustaafu?”Aliongea na kumfanya Raisi Senga kucheka.

“Upo sahihi na ndio maana nakutaka uwe makini , nikifanikiwa mimi hata wewe utafanikiwa”Aliongea huku akisimama na kumgusa gusa begani na Kabwe alitingisha kichwa kwa heshima.

“Kwasasa naenda kupumzika , hakikisha unanipa taarifa ya kila kinachoendelea”Aliongea na muda uleule simu yake ubwa ilitoa mlio ikionyesha kuna mtu anampigia na baada ya kuangalia jina ni Blandina alitoa tabasamu na kukaza mwendo zaidi.

























SEHEMU YA 586.

Upande mwingine kabisa katika visiwa vya Zanzibar katika kambi kubwa ya kijeshi ya Jangu.

Vikosi vya kijeshi vilikuwa vipo katika hali ya tahadhari ya kupokea maagizo muda wowote na kuchukua hatua , hayo yote ni kutokana na kile kinachoendelea.

Wanajeshi wa vikosi maalumu wote kwa pamoja walikuwa kwenye magwanda ya kijeshi huku wakiwa wamevalia Buller Proof , ilikuwa ni kama vile wako vitani na wanasubiria adui ajjitokeze wachukuea hatua.

Mbele yao kulikuwa na vifaa vya kila aina vya kijeshi , kuanzia magari na vifaru na vyote vilikuwa vipo tayari kwa matumzii kutokana na kuwa tyaari vina wataalamuw a kuviendesha.

Ukichana na matawi yaiokuw yakipepelerushwa na upepo wa baharini hakusikikika sauri nyingine kwani eneo lote lilikuwa kimya kiasi kwamba kama mtu unapiga hatua basi kuna uwezekano ukashitukiwa.

Sasa basi ikiwa muda huo ni kama saa saba za usiku kwenda na Robo , nje kabisa ya geti ya kambi hio kulikuwa na walinzi ambao walikuwa macho amabo wametulia kimya , lakini ndani ya dakika chache tu utulivu wao ulitibuliwa na sauti za hatua za mtu anaesogelea upande wa eneo la getini.

Baada ya kujipanga sawa kwa kukosi siraha zao walikaza macho kila pande ili kusubiria mtu anawasogelea kufika karibu wawee kumuona na hisia zao kwa wakati mmoja ziliwaambia mtu huyo hakuwa akija kwa kugopa kwani ilikuw ani kama vile anatembea ili tu sauri za mituu yake ziweze kusikika na hili liliwatia hofu kidogo.

“Weweni nani?”Kiongozi wa ulinzi aliongea kwa nguvu lakini hakukuwa na jibu zaidi ya sauri za viatu kuzidi kuwasogelea na ndani ya dakika chche tu waliweza kumuona kijana wa makamo alievalia jaketi la kawaida Leather akiwasogelea , kwa muonekano wa mtu huyo hakuwa na chochote cha kuoneysha kwamba alikuwa sio wa kawaida , lakini licha ya hivyo walinzi wale hawakutaka kumchukulia wa kawaida licha ya kwamba alionekana wa kawaida.

“Mwambieni Kamada Razaq , mimi Roma Ramini nimekuja kuonana nae”Aliongea yule mtu mara baada ya kusimama huku akionyesha tabasa,u la urafiki.

“Roma Ramini”Aliongea mmmoja apo na kisha wote walianaliana ilikuwa ni kama vile wanamjua mtu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni.

“Umefikaje hapa na unaweza vipi kututhibitisha wewe ni Roma Ramoni?”Aliuliza kiongozi na kumfanya mtu alijitambulisha kama Roma Ramoni kutabasamu huku akihema kwa namna ya kuonyesha kukosa uvumulivu na kufumba na kufumbua Roma Ramoni alipotkea aliposimama na ile anakuja kutokea alikuwa nyuma yao na palepale alimpokonya siraha mmoja wapo ya wale wanajeshi na wale wengine kabla hata hawajachukua hatua wakiw katika mshangao waliambulia Risasi za shingo ambazo ziliwapeleka cchini na kukata roho.

Mlio wa bunduki wa mara tatu uliweza kusikiika katika eneo lote na wanajeshi ambao walibakia palepale walipaza sauti zao wakiliita jina la Roma Ramoni kama ishara ya kutoa tahadhari.

Kitendo chao cha kutoa sauti pamoja na kutaja jina la Roma Ramoni kiliwakurupiusha wanajeshi waliokuwa ndani na palepale walijipanga katika Formation ya kimapigano na wengine wakisogelea geti kwa kukimbia huku sirha ao zilikuwa zipo tayari kuachia siraha.

Upande wa nje bwana Roma Ramoni hakujali tena wale wanajeshi waliokuwa wakipiga kelele na kulitukuza jina lake zaidi ya kwamba alipotea palepale na ile anakuja kuibukia alikuwa ndani kabisa ya kambi hio na ilikuwa ni kama vile alikuwa na taarifa kwani alikuja kuibukkia ndani kabisa ya nyumba na ofisi ya Afande Razaq.

“Roma Ramoni”

Aliongea kwa nguvu Kamada Raz ambaye alikuwa kwenye gwanda za kijeshi , hakuwa amelele na ilionekana alikuwa na kikao na wakuu wa jeshi kwani hapo ndani alikuwa na baadhi ya makamanda wa jeshi na ilionekana kabisa walikuwa wakuongelea mipango yao ya kesho.

“Wanajeshi wenu wote wa kipumbavu washaondoka na nyie ndio mmebaki , je mna maneno ya mwisho ya kuongea?”Aliuliza Roma Ramoni .

“Wewe , kwanini upo hapa?”Aliuliza Afande Razaq huku sura ikiwa imeshuka , alikuwa na taarifa zote kuhusu Roma Ramonni ndio maana alikuwa akimhofua lakini kubwa zaidi ni namna ambavyo ameweza kungia kirahisi kwenye kambi ambayo ilikuwa na amamia ya wanajeshi wanaolinda.

“Sitaki maswali ya kijina , nishasema kama mna maneno ya mwisho ongeeni na kama hamna nitaanza kazi yangu”Aliongea lakini hakuna ambaye aliongea na kila mtu alimwangalia kwa tahadhari na ilimchukua dakika chache tu wale wanajeshi wote walikuwa washapoteza maisha huku damu zikitapakaa kila kona kuanzia kwenye mapazia masofa na sakafuni.

Afande Razaq ndio aliekuwa amebakia na aliangalia kia kitu kilichotokea , namna wanajeshi wake walivyouliwa kinyama , ijapokwua alikuwa nani mwanajeshi jasiri lakini kwa hali hio alikuwa kama piritoni kwa hofu.,

“Wewe ni nani ki uhalisia?”Aliuliza kwa sura ya kuogpa.

“Mimi tena!!.. hahaha ,,, mimi ni Roma Ramoni” Aliongea kwa kucheka huku akimwangalia na palepale alipiga hatua na kumsogelea Afande Razaq aliekuwa amesimama bila ya kusogea , alikuwa kama vile nni mtu ambaye ashakubali chochote kitakachomtokea hapo angekubaliana nacho.

Roma mara baada ya kumfikia Afande Raza alimkumbatia kwa mbele na kupitisha mikono kwenye kiuno chake na palepale Roma alianza kubadilika muonekano na kuwa na mwonekanno unaocheza cheza, alikuwa na mwonekano kama ule wa karatasi la foil , makaratasi flani hivi yalipondo ndani ya pakiti za sigara na hakubadilika yeye tu hata Afande Razaq na yeye alianza kubadilika na ndani ya sekunde kadhaa Afande Razaq hakuonekana ni kama vile amegeuka kuwa hewa lakini sekunde n nyingine alitokea tena lakini wakati huo Roma akiwa haonekani tena, kilikuwa kitendo cha maajabu mno kwasni Afande Razaq hakuonekana na jeraha la aina yoyote.

Baada ya pale Afande Razaq alianza kujinyoosha mwili kama vile mtu anaetoka usingizini na kisha akageukia miili ya wanajeshi ambao walikuwa wamepasuliwa vichwa kwa ukauzu mkubwa bila ya hatia wala huzuni kwenye macho yake.

Muda huo huo kundi la wanajeshi waliweza kuingia kwa kukimbizana katika nyumba hio na ofisi kumwangalia kamanda wao kama alikuwa salama.

“Kamanda upo salama ..?”Aliuliza mmoja wapo huku akitoa macho mara baada ya kuangalia mairi zilizokuwa zimelala chini.

‘Haya yote yamefanywa na Roma Ramon?”

“Huuyu Roma hakika ni shetani , lakini hata hivyo nadhani ameniona sio wa kuchukulia poa kwani ameshindwa kunuia , nadhani ameogopa vita inaweza kutokea , lakini bado sijui nia yake ya kuua wenzangu na kuniacha hai”

“Kamanda familia ya Kweka ina ukiburi wa madaraka sana lakini hata hivyo hatuwezi kukata tamaa”

“Upo sahihi hatuwezi kukata tamaa , lakini mnaona kwamba sio wakawaida kwani kaingia na kuondoka bila mtu yoyte kumuona”Aliongea na pale pale baadhi ya wanajeshi waliingia na kuanza kusaidia kutoa wale wanajeshi na akabakia tu kiongozi wao.

“Afande famlia ya Kweka ina msingi mzuri sana wa kimadaraka ndani ya Tanzania bara hysusani upande wa kijeshi , kama tunataka kushinda hatuwezi kutumia vikosi vyetu kwani ni ngumu kuingia Tanzania , kwanini tusimpe maagizo ya Kamanda Makwera kuizingira familia ypte ili watupatie Roma Ramoni?”

“Ijapokuwa kamanda Makwera kakubaliana kwenye mpango wetu lakini wasiwasi wangu ni kwamba bado ana mheshimu afande Kweka kama mwalimu wake , hivyo inaweza ikawa ngumu kwake kumchukulia hatua”

“Afande lakini kila kitu kinaenda kama kilichopangwa , hakuna mwanajeshi wa Tanzania ambaye anaweza kukubali kuendelea kuona nchi inaingia kwenye machafuko kwasababu ya mtu mmoja na isitoshe ushahidi wote tunao na tunasapoti ya raia “Aliongea mwanajeshi yule wa cheo cha Meja akitoa ushauroi.

“Upo sahihi nitawasiliana nae muda huu huu na mpango kutekelezwa kama ilivyopangwa , tuombe kila kitu kiende sawa la sivyo nitajuitia kushawishiwa na wanasiasa na kukiuka sheria za muungano”Aliongea na yule bwana alitoa tabasamu.

Ukweli ni kwamba kuna mengi ambayo yalikuwa yakiendelea , lakini waliokuwa wakisuka mpango mzima walikuwa wakimhofia sana AfandeRazaq asije akabadilisha mawazo na ndio maana walikuwa wakihakikisha anaendelea kupata sababu ambayo itahakikisha anaendelea kufanya kazi chini ya mpango.

*******

Ni siku nyingine nchini Tanzania ikiwa ni asubuhi ambayo jua tayari lishachomoza , Roma mara baada ya kutoka kwenye chumba chao na kutoka kibarazani aliweza kumuona Edna ambaye macho yake yote yalikuwa upande wa mlimani akiangalia namna wingu linavyotawanyika kila dakika ambayo jua lilikuwa likizidi kuangaza.

“Bado unafikiria kuhusu mtu wa jana aliekutumia ujumbe?”Aliuliza Roma huku akimkumbatia Edna kwa nyuma na kumbusu shingoni na kisha kwenda kusimama pembeni yake.

“Nafikiria alivyoniambia kwamba napaswa kuwa makini , bado sijamuelewa?”Aliongea.

“Mbona inaeleweka kwasasa familia yetu inachukiwa sana huenda ndani ya Tanzania yote , naona sio mbaya kama utaamua kwenda nchini Rwanda, kuendelea kunifuata mimi ni hatari zaidi”Aliongea Roma na kumfanya Edna ampige teke.

“Bado tu una mudi ya kufanya matani muda huu , mimi nilikuwa na wasiwasi usiku mzima ila wewe mwenzangu umelala kiasi cha kunguruma kabisa ,Kamanda Razaq leo atafanya Paradi , wewe mpango wako ni upi?”

“Usiwe na wasiwasi , kinachomfanya afanye maamuzi hayo ni kutokana na ruhusa ya raisi wa Zanzibar na kama nitafanikiwa kumkontrol na akashindwa kujitokeza moja kwa moja maandamano yao yatakosa nguvu”

“Nilijua jana ulikuwa ukipanga kwenda kumua , lakini mbona kama naona nimewaza rofauti?”

“Sikuwa na mpango wa kumuua licha ya kwamba nilitaka kufanya hivo , kama ningemuua ingezidi kufanya mambo kuwa mabaya zaidi..”Aliongea lakini aliishia katikati mara baada ya jina lake kuitwa na msaidizi wa afande Kweka na Roma alipewa taarifa kwamba anasubiriwa upande wa nje kwenye jiko la kuota moto.

Roma mara baada ya kufika aliweza kumkuta baba yake , Raisi Senga aliekuwa kwenye mavazi ya suti na ilionekana ndio kwanza amefika na juu ya meza kulikuwa na picha mbalimbali na Roma mara baad aya kuzipiga macho aliweza kuona sura yake huku pembeni ikionekana miili ya watu waliouliwa kwa kupasuliwa pasuliwa kwa staili ileile kama aliotumia kumuua Haruni.

Afande Kweka alimuacha Roma kuangalia picha zile kwa dakika kadhaa na kisha akaongea.

“Afande Razaq ameuliwa akiwa usingizini masaa manne yaliopita”Alongea Afande Kweka.
 
SEHEMU YA 549.

Edna alijikuta akimeza maneno yake aliotaka kuongea kutokana na namna Roma alivyomwangalia.

Maneno yale aliongea Roma ni kama yaligeuka na kuwa jiwe ambalo limetua moja kwa moja kugonga katika moyo wake uliokuwa kama barafu.

Alimwangalia machoni kwa muda mrefu kabla ya kuvuta pumzi na kuzitoa na kisha akalamba lipsi za midmo yake na kuongea.

“Wewe ni mbinafsi sana”

“Nakubali mimi ni mninafsi , ndio maana sitokubali sisi kutalakiana . siwezi kukuruhusu ukaondoka kwenye maisha yangu ,siwezi kupiga magoti pia na kukuomba tena wala sitoomba msamaha , unayo kila haki yakubakia hapa lakini wewe ni wangu na hilo haliwezi kubadilika”

“Unaongea mambo ambayo hayana sababu ya msingi”Aliongea huku akishikilia kwa nguvu nguo yake ya kulalia.

“Nataka uone uhalisia ulivyo , wewe unadhani mama amekukera sana kwa kualika wale wanawake nyumbani , unafikiria sisi wote tulikuwa tukikuchokoza kwa kukushuku , mbona unakuwa mwenye kutukandamiza , unaweza kuwa na kisirani chako kwangu utakavyo na naweza kuvumilia lakini hasira zako za haraka zilifanya kila mtu kukosa furaha , je unadhani wewe ndio unaepaswa kufanya tu hivyo , kwanini unataka kushindana na mimi? , mimi ni mume wako na uyle ni mama mkwe wako na sisi ni wanafamilia , kwanini unataka kutuletea tabu”

“Wewe… nilijua tu hujawahi kunionea huruma”

“Naongea ukweli”

“Inaniuma kwasababu kila kitu ulichoongea ni ukweli”Baada ya kumaliza kauli hio aliingia ndani na kufunga mlango wa balkoni na Roma aliishia kumwangalia lakini hakuwa na sababu ya kumsogelea tena kuingia ndani , aliamua zake kupotea na kurudi nje.

Alijikuta akisimama nje kwa muda akivuta upepo mkali unaotoka baharini na baada ya dakika tano aliingia kwenye gari , lakini ile anataka tkuliwasha simu yake ilianza kuita na aliekuwa akimpigia ni Neema Luwazo.

“Kipenzi changu , uko wapi?”Sauti ya kichokozi ya kumnyanyua nyoka pangoni ilisikika kwenye ngoma zake za masikio.

“Sauti yako inaonyesha kama unajua kinachoendelea”

“Wewe hujui wafanyabiashara mtaji wetu ni taarifa na isitoshe ni swala linalokuhusu , nasikia umekosana na mkeo na amehama kabisa nyumbani?”

“Umesikia wapi , Nasra ndio kakuambia?”

“Ah..,! Nasra sio mtu wa kuongea ongea umbea nadhani hata wengine hajawaambia , nilienda nyumbani kwenu nikakuta hakuna mtu ndio nilipofanya maamzui ya kumpigia Bi Wema na akaniambia kinachondelea , kwanini unajaribu kutuficha , haujui mtu kama mimi ambaye siku zote nina ajenda za siri nilikuwa nikisubiria hii siku itimie kwa hamu zote , namchukulia Edna kama mshindani wangu hata hivyo”Aliongea huku akicheka na kumfanya na Roma pia kucheka kutokana na utani wake.

“Inakupasa usubiri muda mrefu, kwani kisheria haturuhusiwi kupeana talaka angalau tuwe tumeishi pamoja miaka miwili”

“Haha.. Naamini atarudi tu ndani ya siku chache zijazo , nadhani sina haja ya kuendela na mpango wangu , unaonaje ukinisindikiza twende Shopping, hutujaonana muda mrefu”

“Si kwasababu muda wote unasema upo bize wewe , uko wapi nije sasa hivi kukuchukua”

“Nipo nyumbani kwangu , Donyi kaondoka leo asubuhi kulekea Los Angels na mchumba wake Kasimu nipo mpweke mno”

Baada ya kuambiwa hivyo moja kwa moja aliendesha gari kurudi uelekeo wa nyumbani kwa ajili ya kumfuata Neema.

Ndani ya madakika kadhaa Roma aliweza kufika na kusimamisha gari nje ya geti na Neema Luwazo alikuwa ashatoka nje na kumpokea kwa kumbatio , alionekana ashajiandaa tyaari kwa ajili ya kuondoka, aikuwa amevalia blauzi na suruali ya jeans ambayo ilimpendeza na kuchora umbo lake namba nane.

“Unaangalia nini , ingia kwenye gari tuondoke”Aliongea kwani Roma alikua akiangalia mtetemno kwa nyuma huku akiwa ameweka tabasamu a kifedhuli , aliishia kucheka na kungia ndani ya gari.

“Mh! Jamani mbona hili gari linanuka sigara”Aliuliza lakini Roma hakujibu zaidi ya kuguna na kumfanya Neema kumwangalia.

“Kwahio mawazo yamekuwa mengi , sijawahi kukuona ukivuta sigara , nilidhani mwanaume wangu ni wa kipekee lakini inaonekana kumbe hauko imara kudhibiti mawazo yako”Aliongea huku akivuta mdomo na kumfanya Roma kucheka.

“Okey kwanzia leo nitaacha, Wapi unataka kwenda?”

“Mimani City , tunaweza pia kula huko huko chakula cha mchana , unaonaje?”Aliuliza na Roma hakubisha kwanza hata hivyo asingerudi nyumbani na kukaa peke yake wikiend yote hio , hivyo aliona huenda ingekuwa afadhali.

Baada ya kufika Mlimani walianza kupita kwenye kila duka kwasababu Neema hakuwa na kitu kichwani anachotaka kununua hivyo alijaribisha kila kitu kilichomfurahisha , lakini mwisho wake hakuridhika na wakaishia kwenda kwenye Brand maarufu za Balenciarga , Dr Martens, Luis Vuiton na lancome.

Roma aliishia kumsindikiza maana wafanyakazi walikuwa wakimsaidia kushika kila ambacho anachagua , lakini Roma kwenye upande wa nguo hakuona kwanini Neema anachagua aina hizo za nguo kwani hazikuwa zikimvutia.

“Hey , kama unataka kununua nguo nadhani ulizopita kule nyuma ndio zinakufaa zaidi , hizi nguo nadhani ni kwa ajili ya maonyesho ya fasheni, hakuna maana kuziangalia”Aliongea Roma.

“Wewe mwanaume huelewi kama nisipovaa nguo ambazo ni za brand kubwa nikienda kwenye vikao wataniona kituko , sisi wanawake siku hizi tunajali sana kile ambacho tunavaa kuendana na wakati”

“Kuna haja gani ya kujali watu wanasemanini , kwani hakuna anaeweza kuipima thamani yako kupitia mavazi”.

“Hehe ndio dunia inavyoenda , kama sio hivyo unadhani makampuni kama haya yangekuwa maarufu , kampuni ya mkeo ukiachana na upande wa kampuni zake ndogo ndogo za ujenzi na mambo ya mafuta lakini pia upande wa fasheni umemuinua sana kiuchumi”

“Inaonekaa hufatilii sana kile ambacho kinaendelea kwenye kampuni , hivi majuzi tu aliweza kuingia ubia wa kibiashara na kampuni zenye majina makubwa makubwa kuomba haki ya kusambaza bidhaa zinazotokana na malighafi mpya , kampuni alizoingia nazo mkataba ni kama Prada , Hermes na Burberry , faida alizopata kwenye ubia na kampini hizo ni mara mbili yake anayopata kwenye kampuni zake za ujenzi ukiachana na mafuta pamoja na viwanda vya utengenezaji wa bidhaa za ndani”

“Ana kipaji cha kufanya biashara , lakini nadhani anapaswa kujifunza namna ya kuwa mke bora”Aliongea lakini Neema alicheka.

“Mbona unacheka?”

“Ni hivyo uliposema ana kipaji cha biashara lakini kwa mtazamo wangu naamini ni kinyume chake , ameweza kufanikisha yote hayo kutokana na ukweli kwamba baba yake ni mtu mzito na ana ushawishi mkubwa kwa Raisi Senga na nchi zote za Afrika ya mashariki na kati

“Unamaanisha nini?”

“Wafanyabiashara kama sisi siku zote tunapaswa kufanya vitu kwa wakati sahihi , sehemu sahihi na watu sahihi , kuwa na watu sahihi sio kitu kigumu kwasababu unachotakiwa ni kuwa na ushawishi tu na maipo mazuri , kuhusu sehemu sahihi inategemeana na bahati yako katika biashara , kama sio kampuni ya Vexto kuchagua maeneo sahihi katika kufanya biashara basi siamini ingeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa nchi kama hii ya kwetu ambayo ndio kwanza inaendelea , kitu kigumu katika biashara ni kufanya vitu kwa wakati sahihi kwasababu kikawaida inategemnea sana na sera za nchi , kadri utakavyofanya vitu ndani ya sera za serikali basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu fursa za kibiashara , kama sera haiendani na biashara yako hata uwe na mtaji mkubwa kiasi gani huwezi kufanikiwa na ndio maana wawekezaji wanapoenda kuwekeza kufanya biashara katika mataifa ya nje wanachoangalia ni Sera”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Raisi Jeremy alikuwa akimsaidia Edna katika maswala ya sera ndio maana kampuni yake inafanya vizuri?”

“Ndio maana nakushauri kuwa makini na Raisi Jeremy , ijapokuwa hakuwahi kumtambua Edna waziwazi kama mtoto wake, lakini amesaidia sana kampuni ya Vexto kufikia pale ilipo, huenda kama atakuja kumwambia Edna mambo ambayo amefanya Edna moja kwa moja ataguswa”Aliongea Neema na kumfanya Roma kukumbuka kuna siku Edna ashawahi kumwambia kuhusu mtu anaefahamika kwa jina la the Protector ni kama maneno ya Neema yamemkumbusha kuhusu hilo jina kwani alikuwa amesahau kwa muda mrefu.

“Kwanini unaniambia haya ghafla tu, unadhani kwanini Jeremy anaushawishi mkubwa ndani ya Afrika mashariki na kati?”

“Kuna kitu sikukuambia kwasababu nilikuwa bize na kazi , lakini katika moja ya vitu ambavyo niliweza kugundua katika baadhi ya nyaraka alizoacha mstaafu Kigombola ni juu ya raisi Jeremy na siri zake”

“Siri zake!”

“Ukweli kama ningeona taarifa hizo miaka ya nyuma kabla ya kukutana na wewe nisingezielewa wala kuamini , lakini kwa kipindi ambacho tumekutana na nikajua mengi ambayo hayaonekani katika huu ulimwengu ndio maana nimefanikiwa kuelewa kile alichoandika”

“Umegundua nini?”

“Kwa maelezo ya Kigombola ni kwmaba Raisi Jeremy ana nguvu kubwa nyuma yake ambayo inamlinda na inahusiana na viumbe wasioonekana(majini) , katika nyaraka nilizoweza kupata kusoma jamii hio inafahamjka kwa jina la Panas kama sikosei”Roma alishangaa maneno ya Neema.

“Amejuaje kuhusu hii jamii kuwa nyuma ya Jeremy , mwenyewe nilianza kufikiria hili swala mara baada ya kuona watu wawili kutoka Panas ambao tayari wapo katika levo ya Nafsi wakimsindikiza kama mabodigadi”

“Nini!!, kwahio nilichosoma ni kweli jamii hio ipo, kama ndio hivyo inamaanisha kwamba wametoka katika maficho yao sasa wanataka kuingilia amswala ya kawaida ya dunia?”Aliongea Neema Luwazo kwa mshangao.

“Siwezi kujua, lakini uwepo wao hapa nchini ulinipa maswali mengi ambayo sijayapatia majibu bado na kama uliosema ni kweli basi naanza kupata picha lakini pia shauku yangu kuzidi kuongezeka , je hakuna kitu kingine ambacho uliweza kupata katika maelezo uliosoma?”

“Maelezo niliosoma ni hayo pekee na ndio nguvu kubwa ya Raisi Jeremy nchini Rwanda , ilionekana Kigombola bado hakuwa na majibu ya kutosha na hata alichokiandika hakikuwa na ushahidi , lakini baada ya wewe kusema wameonekana hapa Tanzania sasa naamini maneno yake”Roma alifikiria kidogo na kuona huenda kuna sababu ambayo watu wa Panas wakaamua kuja upande wa duniani , lakini kama ni hivyo kwanini Aphrodite na wenzake hawakumweleza kuhusu hii jamii maana kama na wao walikuwa wakitumia nguvu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi basi wangewalaetea mtafaruku wakati walipokuja duniani.

“Kama ni hivyo je unadhani swala hili linaweza kumuhusu Edna?”

“Lazima liwe linamuhusu , nadhani mpaka sasa huna taarifa, ukweli ni kwamba mpaka sasa mtoto wa pekee wa Raisi Jeremy hafahamiki alipo , ijapokuwa taarifa hio ni ya siri lakini hawezi kuificha kwa watu kama sisi ambao tunahusiano wa moja kwa moja na serikali, kama hisia zangu zitakuwa sahihi basi naamini anataka kumfanya Edna kuwa mrithi wake”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa kitu.

“Nadhani ndio maana alionekana kuwa na haraka ya kumtaka Edna kumtambua kama baba”

“Unamaanisha alishaanza kuongea na Edna?”

“Siku ambayo niliwaona hao watu kutoka Panas ndio wakati ambao alifika nyumbani kwetu kwa ajili ya kuongea nae , lakini inaonyesha Edna hakuwa tayari kukubali”

“Wasiwasi wangu ni kwamba ataishia kukubali na kama hilo litatokea mkeo anaweza akakuingiza kwenye mtego , mpaka sasa naamini Hongmeng ni maadui zako na hata jamii hio ya Panas sidhani kama wanakuchukulia kama rafiki au adui, Jeremy ndio mtu pekee ambaye atafanya kila kitu kwa faida yake na mawazo yake yote ni kuona Rwanda inakuwa kimaendeleo kwa kunyonya rasimali za nchi zinazomzunguka kupitia njia za kijasusi”Roma alijikuta akianza kuwa na wasiwasi, alijua msimamo wa Edna ulivyo likija swala la familia.

“Lakini sidhani Edna anaweza kuwa mwepesi namna hio”Aliongea Roma.

“Hata mimi natumaini asiwe mwepesi wa kukubali kila kitu”

“Okey, nimekuja kurelex sio kuongea mazungumzo haya , hebu tuendelee na kilichotuleta”Aliongea Roma na kisha waliendelea kufanya shoping.

Ni muda wa saa saba wakati wakiwa kwenye mgahawa wakipata chakula cha mchana Roma aliweza kupata msisimko wa kuongezeka kwa mtu mwenye nguvu za kijini na kujikuta kugeuza shingo yake kuangalia upande wa kulia na palepale aliweza kumuona Omari Tozo akiingia eneo hilo.

Omari alikuwa amevalia mavazi ya suti na kwa mwonekano wake ni kama vile amekuja hapo ndani kwa ajili ya kuonana na mtu , baana ya kukagua baadhi ya watu palepale aligeukia upande wa aliposimama Roma na kisha akatabasamu na kupiga hatua kumsogelea.

Tokea siku ambayo waliweza kuhudhuria harusi yake hawakuwahi kuonana tena.

“Madam Neema nadhani hutonilaumu kwa kuingilia muda huu mzuri kwenu wa chakula cha mchana nikimchukua kwa dakika huyu kiumbe , si ndio?”Aliongea Omari huku akiweka tabasamu.

Kwa muonekano wa Omari alivyo alijua tu kuna kitu anahitaji kuongea nae.

“Nadhani ndoa tamu , naona una mabadiliko makubwa ya kiafya”Aliongea Neema kwa utani na kumfanya Omari kutoa cheko kama kawaida yake.

“Nadekezwa mwenzenu , nashindwaje kunenepa sasa”Aliongea na kisha wakasogea meza ya pembeni kwa ajili ya kuongea,.

“Kwa muonekano wako nadhani hatujakutana hapa kwa bahati mbaya si ndio?”

“Upo sahihi , nipo hapa kwa niaba ya serikali chini ya TSS kukuuliza maswali kadhaa ya kiusalama”

“Maswala ya kiusalama , tangu lini serikali ikaniuliza maswala ya kiusalama wakati mimi ni rais mwema?”Aliuliza Roma kwa mshangao.











SEHEMU YA 550.

Roma alijua sio rahisi kwa Omari kumtafuta na kutaka kuongea nae maswala ya kiusalama , lazima kutakuwa na kitu ambacho kinaendelea ambacho yeye hakifahamu , imepita wiki kama tatu tokea The Eagles kuondoka Tanzania na kurudi visiwa vya Mediterranian hivyo hakuwa na chanzo sahihi cha taarifa.

Aliwaondoa kwasababu ya kwamba tishio la kiusalama lilishaisha kutokana na kumuua Yan Buwen na washirika wake akiwemo Mzee Longoli.

“Kwa muonekano wako naamini huna taarifa ya makundi ya watu waliongia Tanzania hivi majuzi?”

“Ndio sina taarifa nadhani mnafahamu The Eagles project yao hapa Tanzania imesitishwa na kurudi, kwasasa nipo mwenyewe tu hapa Dar es salaam”

“Ndio maana hujaweza kupata taarifa”

“Kuna nini kinachoendelea?”

“Intellijensia ya usalama wa taifa imeweza kubaini kikosi cha giza cha Siraha Kwenye Jiwe(SIS) kutoka Scotland ,Bunge la Kiza likijumuisha wanachama wao wa kundi la Camarilla na Sabbat wapo hapa nchini , kuna pia baadhi ya makundi madogo ya watu wanaotumia nguvu za giza pia wamefika”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa.

“Wamekuja hapa Tanzania , kwasabau gani , kama ni jiwe la Kimungu nadhani wanajua halipo chini ya umiliki wangu?”

“Nadhani hawajaja kwa ajili yako na isitoshe sidhani kama wana uwezo wakupigana na wewe”

“Kama sio hivyo kwanini wamefika?”

“Intellijensia tulioweza kuvujishiwa kutoka nje ya nchi ni kwamba wapo hapa kwa ajili ya siraha ya kichawi ifahamikayo kwa jina la Magical Girdle”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa kwani neno la Magical Girdle ashawahi kusikia.

“Unamaanisha siraha iliopo kwenye hadithi za miungu ya kigiriki ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Aphrodite?”

Katika hadithi za miungu ya kigiriki na kiroma , mungu wa urembo aliefahamika kwa jina la Venus kwa kirumi au Aphrodite kwa kigiriki alikuwa na siraha ya mvuto ya mshipi wa kichawi wa dhahabu ambao uliwafanya miungu mingine kuvutiwa nae sana kimapenzi.

Inasemekana alitumia siraha hio kuwapumbaza miungu na kutawala akili zao kihisia , alifikia hatua ya kushindana na Athena pamoja na Hera katika kujiongezea mvuto kwa kutumia siraha hio na alifanya miungu yote kumchagua yeye kama mrembo zaidi.

Lakini hata hivyo ni hadithi tu , kitu ambacho kilitungwa na binadamu wakiwa wamedhibiitwa kiakili ili kufanya binadamu wengine kuwaabudu viumbe hao waliovamia dunia na kuona Binadamu ni kiumbe dhaifu.

Sasa Roma hakuwahi kusikia kutoka kwa Christen kama kweli alishawahi kuwa na siraha hio ya kichawi ifahamikayo kwa jina a magical Girdle lakini kama ilivyokuwa kwa Hades wa zamani kutokumuambia kuhusu siraha yake ya Helmeti of Invisibility(Helmet la kutokuonekana) wakati alivyomuachia urithi basi aliona huenda ni sawa kwa Christen pia.

Siraha za aina hio hata hivyo hazikuwa na maana sana kwa viumbe hawa wa sayari nyingine ambao wameishi hapa duniani kwa muda mrefu , kutokana na kwamba wanakosa miili yao halisi.

Na Roma aliona kama Christen kweli alikuwa na huo mshipi kwa alivyokuwa akimtamani huenda angeshaidhibiti akili yake na kumfanya alale nae au kufanya zaidi ya hivyo na hana uhakika kama angeweza pia kutawala akili ya Zeus na wengine.

“Kama ni hivyo unamaanisha wanatafuta huo mshipi hapa Dar es salaam ,unamaanisha mshipi huo umeonaka hapa Tanzania?”

“Hata sisi hatuna uhakika pia , na tumeshindwa kuweza kujua taarifa kamili”

“Kama ni hivyo wamejuaje kama Mshipi huu wa kichawi upo hapa Tanzania?”

“Kuna mtu ambaye ametumia Mshipi huo wa kichawi kuwadhibiti wanajeshi wa kitengo maalumu na aliweza kuonekana kwenye Rekodi ya Vidio , hio Vidio ndio ambayo imesambazwa kwa Kundi la SIS , Bunge la Kiza na baadhi ya makundi madogo madogo, Eneo ambalo limeonekana kwenye Vidio hio ni katika kambi yetu ya kijeshi ya Ruvu”

“Kama unayo hio vidio unaweza kunionyesha?”Aliuliza Roma huku akianza kuwa siriasi na Omari alionekana alishajiandaa kabla ya kufika hapo na alitoa simu yake na kuchezesha kicha akamkabidhi Roma.

“Kwenye Vidio hio ilionyesha kivuli cha mtu mwenye ngozi nyeusi yaani muafrika akijaribu kutawala akili za wanajeshi waliokuwa katika Demo ya mazoezi ya siraha na kwa kutumia Mshipi wa Dhahabu palepale wale wanajeshi waligeukana wao wenyewe na kupigana risasi.

“Ni Vidio fupi sana , tukio hili mpaka sasa ni siri ya serikali na limetokea wiki iliopita , baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na kivuli cha mtu kinachoonekana kwenye hio Vidio kutotambulika Serikali ilipanga kikao kuzima swala hili ili kubakia siri , lakini ajabu ni kwamba hio Vidio ilisambaa nje ya nchi kwa makundi hayo ya watumiaji wa nguvu za giza”

“Inasemekena pia mtu ambaye anatumia hio Dhana ametangaza kwamba ameipata kwabahati mbaya na anashindwa kufahamu namna ya kuitumia hivyo anapanga kuiachia kwa watu wengine wenye uwezo na ameificha ndani ya jiji la Dar es salaam na mtu ambaye atabahatika kuipata ndio atakuwa mmiliki”Roma alijikuta akiwaza kidogo kusharabu maneno hayo.

“Nadhani sio sawa ,kama kweli hio dhana ni yenyewe sidhani Aphrodite angeshindwa kuinasa kihisia, lakini mpaka sasa hakuna hatua aliochukua na isitoshe siraha hio haiwezi kutumiwa na mtu yoyote kwani inahitajika kuwa na nguvu ya kiuungu ndani yake, Kwahio hamjatambua kabisa hiko kivuli cha mtu ni nani na nia yake ya kufanya hivyo?”

“Bado hatujaweza kufahamu , ni swala ambalo ucunguzi wake unaendelea kwani mpaka sasa linaumiza vichwa vya wakuu wa majeshi , maana tukio la kupigana risasi wanajeshi kwa wanajeshi ni la kuogofya sana kwa usalama wa nchi”Aliongea na kumfanya Roma aanze kufikiri.

Kuna kipindi wakati alipokuwa Ufaransa watu walikusanyika kwa ajili tu ya kutaka kuipata siraha ya Thanatos , lakini sio hivyo tu hapa Dar es salaam ni kama tukio hilo linajirudia , kwani mara ya kwanza Dhana ya Holly Grail ilionekana Tanzania na makunndi ya nguvu za giza na za Nuru walifika na kuanza kupigana kuipata.

Roma mara baada ya kuwaza aliishia kucheka , alijua hata kama inaweza kuwa halisi , hakuna uwezekano kwamba wanaweza kuitumia kupumbaza watu kwani ni siraha inayomjua mmiliki.

“Lakini kwanini hili swala naona kama ni mtego , nadhani nyie watu msijisumbue , ngoja wafanye wanachoweza kufanya na sisi tuone”Aishauri Roma,

“Bro unapaswa kutusaidia katika hili , hawa watu kama itatokea wakahatarisha usalama wa nchi vikosi vyetu vya idara ya uchawi sidhani kama wanaweza kufanikisha kuwadhibiti na isitoshe wewe pi ni mtoto wa raisi na familia yenu imeweka mizizi katika usaama wa taifa”

“Ohoo!, siwezi hata kumdhibiti mke wangu mwenyewe, halafu nijihusishe katika haya mambo . kwanini niingilie?”Aliongea Roma akijaribu kukataa.

“Kama huwezi kuingilia tunalo ombi moja kwa sasa , wewe unafahamiana na miungu wenzako mathalani Aphrodite mungu wa urembo, kama kutakuwa na uwezekano wa kujitokeza na kutusaidia , maana kama watu hao wataanzisha vurugu mambo yanaweza kuwa nje ya uwezo wetu”Roma alifikiria kidogo.

“Okey nitampigia simu baadae”

“Mpigie sasa hivi Bro wakuu wanasubiri majibu muda huu”Aliongea kwa msisitizo na kumfanya Roma kukosa neno la kuongea na palepale aliamua kutoa simu yake na kutafuta namba ya Christen na kupiga na iliita kwa muda mrefu kidogo lakini Roma hakukata tamaa kwani alijua muda huo Los Angeles itakuwa ni usiku kukikaribia kupambazuka.

“Hades , are you calling to ask me about Magical Girdle too?”Aliuliza akimaanisha kwamba je anampigia kwa ajili ya kuulizia mshipi wa kichawi pia.

“Ndio”Alijibu Roma.

“Mshipi wangu wa thamani kubwa haujaibiwa , ninao siku zote hivyo naomba usiulizie tafadhari , Mshipi ambao umeonekana kwenye vidio unafanana sana na wa kwangu lakini ni feki , kuna wachawi wengi wa kiroho dunia hii, kwa mfano kundi la kichawi la Siraha kwenye Jiwe wanaweza kutengeneza udanganyifu , hivyo kwanini iwe dhana yangu ya Mshipi wa dhahabu”Aliongea kwa namna ya kujitetea na kukereka kwa wakati mmoja na kumfanyaRoma kukunja sura.

“Kwanini sasa unaonekana kuwa na hasira , miimi nimepiga simu kwa niaba ya jeshi la Tanzania kitengo cha wachawi kwani hawana uwezo wa kukuuliza moja kwa moja na isitoshe nilijua usingeshindwa kunasa kihisia pale mtu anapotumia dhana yako”

“Tatizo mnanisumbua , muda si mrefu Poseidon ,Hermes na Artemis wamenipigia na kuniamsha kwenye usingizi , naomba usijihusishe , waache watafute kama wanavyoamani lakini kama utagundua muhusika wa kuzusha uongo huo ni nani niambie nitahakikisha namchuna ngozi akiwa hai”

“Sawa lakini kwa nilivyosikia kundi la Sabbat pia lipo hapa nchini , nadhani chuki zako uzielekezee kwa Raphael kwani ndio kiongozi wa kundi hilo ambae ameagiza watu wake kuja hapa nchini na wakafatia kundi la Camarilla”

Raphaeli ndio kiongozi wa kunti la Tzimisce ambaye anatumia mwili wa Vampire , ni kiumbe kutoka sayari nyingine ambaye alifanya watu duniani wamuabudu kwa kumuita Hermes mchunga kondoo.

“Hermes ni mtu wa ajabu na sipendi kuongea nae, nadhani amefanya hivyo kutokana na kuficha uhusika wake, mpaka sasa hakuna Vampire anaemfahamu kwa jina la Hermes, Hades nitakuw amkweli kwako kila dhana ambayo tulikuja nayo imeunganishwa na roho zetu kuna zile zilizopotea na tulizobakiwa nazo , ndio maana hata Artemis aliweza kuhisia uwepo wa Selene nchini Korea kusini licha ya kwamba alikuwa umbali wa takribani nusu ya dunia, mpaka sasa dhana pekee ambayo imepotea na na imeshindikana kufahamika imepotelea wapi ni Helmeti la kutokuonekana ambalo ni siraha yako , kama hujui, Helmet hilo ni kama taji na nitofauti sana na dhana tulizokuja nazo kwani teknolojia yake ilikuwa ni ya hali ya juu sana na Hades wa dhamani kwasababu alikuwa ni mwanasayansi ndio anajua siri yake”

“Ndio maana Hades wa zamanni sikuwahi kumuona nalo , kumbe ni dhana ambayo haionekani”

“Nadhani umeelewa sasa narudi zangu kulala , kama utakuwa na muda naomba uniangalizie nani kaanzisha huo uvumi , niambie na nitakuja kumuua mwenyewe , anadhani kujificha Tanzania siwezi kumpata na kumuua”

“Kuhusu hilo usijali nitakusaidia ,lakini na mimi utanisaidia kujibu maswali yangu yote ya kile kilichotokea Korea kusini bila kunificha kitu”Aliongea Roma na kauli yake ilimfanya Christen kuwa kimya.

“Nilishakujibu tokea muda mrefu hukuzingatia ndio maana , mimi nalala”Aliongea na kisha akakata simu na kumfanya Roma kukuna kichwa chake na kujiambia atajua tu ukweli wote kuliko mambo nusu nusu wanayomwambia.

Roma ilibidi amwelezee Omari juu ya alichoweza kupata na wote walijikuta wakiwa na ahueni na aliwathibitisha hakuna mgogoro unaoweza kutokea baina ya wageni hao kama tu Mshipi huo hautakuwa halisi.

“Asante sana Bro , nadhani napaswa kuondoka sasa nikuache na shemeji, tutakutaarifu tukimpata muhusika”

“Haina haja ya kunifahamisha , hilo ni swala ambalo halinihusu”Aliongea na Omari aliaga na kuondoka.

Neema hakumuuuliza sana maswali Roma juu ya kile ambacho alikuwa akiongea na Denisi , kwani mara baada ya kurudi kwenye meza walikula chakula kama wapenzi huku wakishushia na mvinyo.

Wikiend nzima Roma alimalizia kwa Neema Luwazo na walipika na kupakua na alimsaidia pia kwenye kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Siku ya jumatatu mara baada ya kuamka mawazo ya Edna yalianza kukisumbua kichwa chake na wakati alipokuwa akipata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Neema alimkumbuka na alijiambia kutokana na anavyo mjua Edna muda huo atakuwa hajapata chochote , hivyo alimwambia Neema amwandalie vitu vya kuondoka navyo kwani anampelekea mke wake, aliongea bila ya kupindisha kauli.

Neema baada ya kuambiwa hivyo alimuonea wivu Edna lakini aliishia kuandaa kwani alijua yeye ni mchepuko tu na ili aendeee kufurahia penzi na kijana huyo mdogo basi ni kuhakikisha anamfurahisha na kumsapoti kwa kila kitu na isitoshe anapata faida kubwa ya kuvuna nishati kitu kitakachompeekea kuwa mrembo muda mrefu.

Roma asubuhi hio mara baada ya kufika nje ya ofisi ya Edna aliweza kukutana na Recho ambaye alikuwa akitoka katika ofisi ya Edna na kwa haraka haraka alijua huenda alikuwa akisafisha na kuweka mazingira sawa lakini aligundua sio hivyo mara baada ya kuona amebeba mabakuli na juisi kwenye mfuko wa plastiki.

Hakuwa amemuona Recho kwa muda mrefu kidogo ni kama zaidi ya miezi mwili , lakini alionekan hakuwa amebadilika sana zaidi ya kwamba kipindi hiko alionekana ni mwanamke mwenye kujiamini sana kuliko alivyokuwa mwanzo na ni kama urembo wake umeongezeka zaidi.

“Ni wewe .,… nikajua Boss ndio amefika”Aliongea huku kidogo akionyesha hofu.

Tokea kitendo kilichotokea miezi kadhaa iliopita ilifanya wao kujihisi vibaya kila pale wanapokutana .

“Edna yuko wapi , bado hajafika kazini?”Aliuliza Roma na kumfanya Recho kushangaa kidogo.

“Kuna chochote kilichotokea kati yako na Boss? Kwanini amehamia Msasani?”

“Nadhani haina haja ya kuongelea hilo kwasasa”Aliongea Roma maana hakutaka kutanganza matatizo ya ndoa yake hadharani.

“Ulichobeba ni kifungua kinywa kwa ajili ya Edna?”Aliulizia Roma kupotezea mada.

“Ndio , amenipigia simu nimwandalie ..”Aliongea Sekretari Recho huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza chini , alikuwa na aibu za kike kwani alishindwa kumwangalia Roma usoni.

Ukweli ni kwamba Recho licha ya kwamba alikuwa na maisha mazuri na kule kukataliwa na wanaume kuisha , lakini akili yake haikufuta tukio la kufanya mapenzi na Roma , ni tukio ambalo muda mwingine hujirudia hata wakati anapofanya mapenzi na mpenzi wake mpya na kadri siku zinavyozidi kuendelea ndio ambavyo tukio lilizidi kutawala akili yake lakini hakupata ujasiri wa kumsogelea Roma tena kwani ni mke wa bosi wake na aliogopa ikija kugundulika , kwani maisha yake wakati huo na familia yake yalikuwa mazurri kutokana na mshahara mnono pamoja na posho anazopata kutoka kwa Edna.

Muda huo ambao hawakuwa wakijua ni topiki gani waendelee nayo kuongea wakimsubiria Bosi hatimae Edna alitokea kwenye lift na kuingia eneo hilo na alijikuta akipatwa na ubaridi mara baada ya kumuona Roma mbele yake.

Jicho moja tu kwa Recho ni kama aliona lazima kuna kitu kilichotokea kati ya Roma na sekretari wake na hapo hapo alizidi kuongeza ukauzu wake.

“Boss karibu kazini , nimekuandalia ulichoniagiza”Aliongea Recho kwa mtindo wa heshima kwa bosi huku akiwa na afadhali.

Edna alimpita Roma kama hamjui na kisha alimsogelea Recho na kuchukua mfuko alioshikilia mkononi na kisha akatingisha kichwa kama ishara ya kushukuru na kupiga hatua kuingia ofisini kuingia kwake , lakini kabla hajafikia mlango Roma alianzisha maongezi.

“Edna na mimi nimekuletea kifungua kinywa mke wangu, niliju tu muda huu utakuwa hujapata chochote”Aliongea huku akimwonyeshea mfuko alioshikilia na Edna alijikuta akitoa kicheko hafifu cha kukera.

“Una uhakika umeleta kwa ajili yangu?”











SEHEMU YS 551.

Upande mwingine nyumbani kwa Afande Kweka mara baada ya Lanlan kufika nyumbani hapo akiwa ametangulizana na Qiang , aliweza kupokelewa kwa furaha na wazee wawili ngozi tofauti ,mmoja akiwa ni Mzee Kweka mwenyewe na mwingine alikuwa ni Pastor Cohen.

Pastor Cohen mara baada ya kumuona Lanan alimwangalia Afande Kweka kwa tabasamu kubwa na kutingisha kichwa kuonyesha ishara ya kukubali jambo.

Ukiachana na maswala mengi ambayo Afande Kweka na Pastor Cohen waliweza kuzungumza lakini kubwa zaidi ni swala la Lanlan kuwa mtoto wa Seventeen pacha wa Edna ambaye aichanganywa na Roma kwenye mpango LADO.

Pastor Cohen na Afande Kweka ndio watu ambao walioratibu mchakato wa kumuingiza Roma na Seventeen katika mpango LADO na moja wapo ya matokeo hayo ni uwepo wa Lanlan duniani.

“Komredi nikiri hapa hakuna ubishi , lakini nashindwa kuelewa inakuaje Roma kushindwa kumfahamu binti yake mwenyewe”

“Komredi hilo ni swali gumu kwangu , najua nilihusika kuwaingiza kwenye mpango LADO lakini uendelevu wake sikuhusika”

“Sio wewe tu ambaye hukuhusika , wote hatukuhusika, mpango LADO kumbuka ulikuwa chini ya Zeros organisation na sisi tulichokifanya ni kufuata maagizo ya kuchomeka watu ambao hawakuwa katika mpango ili kutengeneza mafanikio”Aliongea na Afande Kweka alionekan kutopinga.

“Nadhani imekuwa ngumu kutokumfahamu mtoto wake kutokana na kilichomtokea Seventeen”

“Nakuunga mkono , lakini bado kuna kitu nashindwa bado kuelewa , kama wewe umeweza kumfahamu mjukuu wako kwanini yeye baba ameshindwa hilo”

“Ukiniuliza hilo nitasema ni uzoefu lakini nikikujibu kwa niaba yake nitasema licha ya mengi ambayo yametokea lakini bado mtoto wake ameweza kurudi nyumbani kumfuata , damu ni nzito kuliko maji”

“Ningetamani kujua kila kilichotokea , nadhani mzee mwenzangu una shauku ya kujua pia nini kilitokea baada ya kupotea kwa ile ndege , kwani mpaka sasa ni mpango wa siri ambao ni watu wachache sana duniani wanaoufahamu”

“Ninatamani sana , lakini kwa uzee huu nadhani naweza kuangulie mbele za haki bila kujua kile kilichotokea”Aliongea na kumfanya Pastor Cohen kutingisha kichwa.

“Wewe ni mimi Komredi hatuna haja ya kuwa na huzuni ilimradi tulichokifanya kinakwenda kuisaidia dunia , kwasasa nadhani shauku yangu imetimia sasa , nimemwona kitukuu chako, nadhani ni muda wa mimi kuondoka , lakini kabla ya yote nataka kukueezea kile kinachoendelea ndani ya umoja”

“Nakusikiliza Komredi”

“Kwasasa ndani ya kundi , kuna ‘interval’ kubwa ya tarehe katika kalenda kwa kile ambacho wanachana wanapaswa kufanya”

“Unamaanisha nini Komredi?”

“Ukiachana na taratibu za kawaida ambazo zinaendelezwa kufanywa na wanachama kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya kwanza ya mvua ya theluji kwa bara la Afrika”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushangaa.

“Mvua ya kwanza ya Theluji katika bara la Afrika , unamaanisha Tanzania Mvua ya Theluji itawezekana kunyesha?”

“Hakika , ndio ishara kubwa inayosubiriwa “

“Ishara hii inamaanisha nini?”

“Katika umoja wetu ishara hii inamaanisha ule wakati uliosubiriwa umetimia ni kama unabii umetimia , kwa upande wa Illuminat na Allien kwao ni ishara ya utawala wao duniani kuanza”

“Nini kitatokea baada ya hapo?”

“Kwasasa hakuna majibu sahihi ,mpaka itakapojulikana ni kipi kingine kinapaswa kufanyika kulingana na Kalenda , lakini mpaka sasa tunaweza kufanya makisio, nadhani unajua nini kinasababisha Theluji?”

“Najua ni Baridi?”

“Sahihi kabisa, makisio ni kwamba kuna uwezekano joto la dunia kushuka katika viwango vya chini sana kiasi cha kupelekea bara la Afrika kuweza kupitia vipindi vya majira ya mvua ya Theluji”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushika kidevu , ijapokuwa hakuonyesha mshangao wake waziwazi lakini ilikuwa dhahiri taarifa hio ilikuwa ya kumshangaza.

*****

Roma alijikuta akishangazwa na swali la mke wake kwani hakuwa amemulewa kabisa , alimbebea yeye kifungua kinywa lakini tena anatilia mashana nia yake ya kumletea.

“Edna unamaanisha nini?”

“Nadhani Recho hajapata kifungua kinywa bado , usipoteze hela zako kwa mtu kama mimi , nitajifanya sijaona chochote”Aliongea na Roma palepale aliweza kuelewa anachomaanisha na kushindwa kuzuia hasira zake .

“Edna hata kama unataka kuonyesha hasira zako hupaswi kwenda mbali hivyo , ndio nimefika sasa hivi na kukutana na Recho hapa , hata kama unadhani sina jema lakini huwezi kuongea hivyo kwa kumsingizia msaidizi wako”

“Nimeonyesha wapi hasira? , au umeelewa vipi kauli yangu , kwanini unajishtukia kama huna hatia?”Aliongea na kumfanya Roma kuwa katika mtego wa maneno.

Alikuwa na hasira na kauli ya Edna lakini alishindwa kukataa wala kukubali , kwani ni kweli kuna dhambi ambayo alishawahi kufanya na Recho.Aliona kama angekataa asingeweza kuituliza roho yake yenye dhamira ya kuhukumu.

“Madam , tafadhari naomba usituelewe vibava Mr Roma amenikuta hapa na amekuletea kifungua kinywa , hakuna chochote kinachoendelea baina yetu naomba usifikirie hivyo tafadhari”Aliongea kwa uwoga huku akiangalia chini.

Roma baada ya kumuona namna ambavyo Recho anajitetea ilimfanya amuonee huruma , kwani alikuwa kwenye hali ya taharuki mno , alikuwa kama mtu ambaye amekamatika katika jambo na sasa anahofia kibarua chake kuota nyasi.

“Recho wewe unaweza kutumia hiki kifungua , kama mtu hataki haina haja ya kumlazimisha ilihali wahitaji wapo”Aliongea Roma na kuweka kwenye miguu ya Recho ule mfuko na kisha aliondoka hilo eneo na kuzisogelea lift.

Recho mara baada ya kuona ameachiwa msala alitamani kupiga magoti , lakini palepale aliushika ule mfuko kwenye sakafu na kisha akamnyoshea Edna aupokee.

“Madam naomba usimfikirie vibaya , Mr Roma kakuletea hiki kifungua kinywa kwa ajili yangu naomba ukichukue..”

Edna aliangalia ule mfuko aliopewa na Recho ulivyotuna na kisha alimsogelea Recho na kuuweka chini.

“Unaweza kuchukua na hiki pia , sina hamu ya kula chochote leo”Baada ya kusema hivyo aliingia ofisini kwake.

Recho aliona siku hio imeanza vibaya sana kwake , alijikuta akiangalia ile mifuko yote miwili , alioleta Roma na alioleta yeye mwenyewe na kujikuta akikosa cha kufanya kwani aliishia kusimama katika sehemu moja bila ya kusogea.

**********

Upande mwingine katika ofisi ya Raisi Senga asubuhi hio , Raisi wa nchi ya Tanzania akiwa ofisini kwake akiendelea na majuku yake , aliweza kufika Kabwe nje ya ofisini huku ameshikilia faili mkononi na baada ya kuruhusiwa kuingia ndani moja kwa moja alimsalimia Mheshimiwa.

“Vipi kuna jipya , kuna chochote ambacho mmefanikiwa kupata?”Aliuliza Raisi Senga kwa shauku.

“Mheshimiwa mpaka sasa hatujapata mwanga wowote wa kumpata Denisi , lakini vijana wamejjitahidi kutafuta taarifa ambazo kwa kiasi flani zinatupa tafsiri ya kile kinachoendelea”Aliongea Kabwe.

“Nipe taarifa”

“Kuna baadhi ya watu hapa nchini tuliweza kuwahoji , mmoja wapo ni Abubakari Hamadi mtoto wa Mzee Alex mmiliki wa kampuni ya JR na mwingine ni Elvis Temba mtoto wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma”

“Na mlichogundua ni kitu gani?”

“Nadhani Denisi alikuwa na mpango anaoendeleza yeye na Yan Buween kwa siri hapa nchini kwani kwa maelezo tuliokusanya ni kwamba aliwaambia marafiki zake wote kwamba kuna kitu ambacho wanapanga kumfanyia Roma”

“Lakini Yan Buwen si ameshakufa?”

“Hili ni tukio ambalo limetokea miezi takribani mitano nyuma Mheshimiwa kabla hata ya mheshimiwa Kigombola na Yan Buwen kufariki”

“Kama usemayo ni sahihi basi hayapingani na taarifa tulioweza kupata ya Denisi kuwa na uwezo wa ajabu si ndio?”

“Ndio Mheshimiwa”

“Kama ni hivyo kapotelea wapi?, mwezi wa pii na nusu huu haonekani nyumbani na mbaya zaidi kakomba hela zangu zote zilizokuwa chini ya jina lake katika visiwa vya Shelishei , kapeleka wapi pesa zote hizo?”

“Mheshimiwa nadhani swala hili linahusiana na kinachoendelea nchini Rwanda kwani kati ya marafiki wa karibu wa Denisi ni Desmond mtoto wa Raisi Jeremy”

“Nimejaribbu kumuhoji Jeremy lakini anakuwa mgumu wa kufunguka , lakini chanzo kinaanzia katika kifo cha mke wake, sijui nini ananificha kwasasa inanipa wasiwasi kuhusu Denisi mahali alipo kama yupo salama”

“Mheshimiwa kwanini usifanye kama ambavyo Madam anapendekeza , nadhani Mr Roma atakuwa na majibu sahihi zaidi”Alipendekeza Kabwe na kumfanya Raisi Senga kusimama akitoka kwenye kiti chake.

Ukweli ni kwamba Raisi Jeremy familia yake haikuwa na amanni hata kidogo na yote hayo ni juu ya swala la kupotea kwa Denisi , lakini vile vile kuwa na uwezo wa ajabu ambao alikuwa na uhakika ni uwezo ambao amepewa na Yan Buwen.

Mama yake Denisi yaani Damasi alikuwa na mawazo sana na muda wote ni mwenye kumbebesha Lawama mume wake kwa kutokuwa makini na mtoto mpaka kufikia katika hatua ya kupotea.

Ilikuwa ni miezi miwlii imepita sasa , tokea Denisi alivyopotea ghafla mara baada ya kuweza kukwapua kiasi kikubwa cha pesa cha baba yake alichokificha katika visiwa vya Shelisheli.

Hofu ya Damasi ni kwamba alijua fika kuna uwezekano kuna jambo baya ambalo Denisi analiandaa na hilo linaweza kumuweka katika hatari ya kuuliwa na Roma kwani kwa muda mrefu alishaweza kufahamu kinyongo cha Denisi kwenda kwa kaka yake , hivyo hofu yake ilikuwa ni kubwa mno huku akimlazimisha mume wake kuchukua hatua za haraka kuweza kunusuru hali hio kabla kubwa zaidi halijatokea.

Kilichomshangaza zaidi Senga ni kwamba tukio ambalo linamtokea yeye mwenyewe ni kama linalomtokea rafiki yake Jeremy raisi wa Rwanda, kwani wote watoto wao wa kiume ambao wanaamini kuwa warithi wao hawaonekani walipo na kila dalili inaonyesha hawawezi kuwa sawa tena.

Ilikuwa ni afadhali kwa Raisi Senga kwani alikuwa na Ashley ambaye ni mkubwa na angemrithisha kila kitu chake , lakini bado sheria za ukoo wako zinampa nafasi kubwa mtoto wa kiume.

“Kabwe nadhani kwasasa sina jinsi , ni muda sahihi wa kumkubali Den.. namaanisha Roma kama mtoto wangu”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Kabwe kidogo kutoa macho ya mshangao.

“Mheshimiwa unataka nifanye nini?”

“Blandina aliniomba nimsaidie yule msichana Najma nafasi serikalini kama hatua ya kwanza ya kujenga uhusiano wangu na Roma nadhani kwanza nitekeleze hilo”

“Ndio mheshimiwa nitakuletea faili lake”

“Haina haja, fanya utaratibu wa kuangalia nafasi gani itaweza kumfaa katika Wizara ya elimu”

“Sawa mheshimiwa”

“Kingine nitaenda nyumbani kuonana na mzee jioni ya leo na nitapata chakula cha usiku huko huko”

“Sawa mheshimiwa nitaandaa itifaki?”Aliongea na kisha akampa ruhusa ya kuondoka na kumfanya Raisi Senga kuonekana kuwa katika mawazo.

“Huenda uamuzi wangu ukawa sahihi , nikirudisha ukaribu na Roma na kuzuia hatari yoyote kumtokea Denisi nitaweza kupata faida nyingine , naweza kuushinda udhaifu walionitengenezea Freemason na naweza kurudi kwenye mstali kama kiongozi wa taifa hili”Aliwaza mheshimiwa Senga lakini muda ule ule katibu Muhtasi aligonga mlango na kumshtua katika mawazo na aimruhusu kuingia.







SEHEMU YA 552.

Ilikuwa ni saa moja za jioni , haikueleweka Roma alishinda wapi lakini muda huo alionekana ndio kwanza anarudi kuelekea Ununio nyumbani, alikuwa na haraka kwani alikuwa na miadi na Rufi siku hio kwenda kula chakula cha usiku nyumbani kwa Bi Wema , kwani tokea Bi Wema anunue nyumba ambayo anaishi na Rufi mtoto wake wa kike hakuwahi kufika.

Sasa wakati akiwa Tegeta aliweza kupokea ujumbe wa meseji ambao ulimfanya atabasamu kifedhuli ulikuwa ni ujumbe unaotoka kwa namba ambayo hajaisajili kwenye simu yake lakini kutokana na kilichotokea dakika chache zilizopita alijua nani katuma ujumbe huo na alishangaa kwa kuona kwamba mtu huyo hakuwa amekata tamaa , kwani ilikuwa ni kama mwezi mmoja umepita huenda na zaidi tokea akutane nae.

Dakika chache nyuma wakati akiwa anatokea Mbagala akiwa anapita uwanja wa taifa aliweza kugundua kuna gari inamfuatilia nyuma na licha ya kugundua hilo hakutaka kwanza kumchezea mchezo mtu aliekuwa akimfuatilia , kwani aliendesha gari kusonga mbele bila wasiwasi lakini alipokuja kupita katika daraja la Kijazi interchange Ubungo ndio alipanga namna ya kumpotezea mtu ambaye alikuwa akimfatilia nyuma nyuma.

Mtu aliekuwa anemfuatilia alikuwa ashamtambua na ilionekana pia hata mtu huyo ashajua kama ashajulikana kutokana na kwamba alikuwa akisambaza nguvu za kijini na kwa kufahamu uwezo wa Roma alijuwa atakuwa amehisi uwepo wake, lakini haikumkatisha tamaa kutimiza dhamira yake.

Roma mara baada ya kuingia katika barabara ya Sam Nujoma sehemu pekee ambaye aliamini anaweza kumpoteza mtu anaemfatilia ni eneo la Mwenge Mataa na kweli aliweza kufanikisha hilo kwani alihakikisha alikuwa mbele kabisa anagalau mbele ya magari mawili kutoka kwa mtu anaemfatilia na hio alilifanikisha na wakati tu ambao anakaribia Mwenge taa za kijani zilimruhusu kupita lakini kitendo cha kupita tu taa za rangi nyekundu ziliwaka na kuzuia magari yaliokuwa nyuma yake kupita.

Ilikuwa ni tukio la kushangaza kwani ilionekana kwa wale wanaoendesha magari kama taa hizo zilikosea kimahesabu katika kupitisha magari kwani taa iliwaka kwa sekunde sita tu na kuzima na kisha ikawaka nyekundu.

Mtu aliekuwa akimfatilia Roma katika gari aina ya Toyota Camry alitoa tusi kwa lugha ya kichina huku akigonga usukani kwa hasira na kujiapiza.

Sasa Roma alipokuwa katika eneo la Mbuyuni akikaribia Tegeta aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa namba ambayo hakuwahi kuisevu lakini alikuwa akiikumbuka ilikuwa ikimtumia meseji za ajabu ajabu.

Roma licha ya kwamba aliweza kumpoteza mtu huyo lakini wasiwasi wake ni kwa Rufi kwani aliamini kama mtu huyo ataendeea kumfuatiia na kujua anapoishi na kuja mara kwa mara basi nafasi ya kumuona Rufi ingekuwa kubwa.

Ndio alikuwa ni msichana wa kichina afahamikae kwa jina la Xiao Xiao ambaye kwa maelezo ya Rufi alikuwa anatokea katika familia ya wakwe zake katika ulimwengu wa jamii za watu wasionekana za kichina.

Roma alipotezea kwanza swala hilo na kuwa na umakini katika kuendesha gari kwani muda umeenda, ndani ya dakika chache tu aliwea kufika nyumbani kwake na laishangaa kumkuta mtu akiwa amesimama nje ya geti na alipoangalia kwa umakini alikuwa ni Rufi na ilionyesha alishindwa kuingia ndani kwani alikuwa amefunga geti kabisa wakati wa kutoka.

“Rufi kwanini umenisubiri hapa, ungekaa nyumbani kwenu tu ningekukuta”Aliongea Roma mara baada ya kusimamisha gari.

“Ni sawa tu , nilikuwa nikipata hewa safi ya bahari”

“Msichana mjinga , huwezi kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mishipa yako ya damu ni myembaba kwasasbu ya kiwango kikubwa cha nishati ya Yin, unatakiwa ujali afya yako upepo kama huu unakuumiza”

“Kweli?”

“Ndio”

“Nilipatwa na wasiwasi maana sikukuona siku zaidi ya tatu zote , nilikuwa na shauku kubwa ulivyosema utakuja kuungana na sisi kwa ajili ya chakula cha usiku, niishindwa kuvumilia ndani ndio maana nikaja kukusubiri hapa”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na matedo yake na kumwambia aingie kwenye gari waelekee nyumbani kwao , kwani ilikuwa ni upande wa pili.

Baada ya kufika na kuingiza gari ndani Roma alishuka na kumfugulia Rufi mlango na kisha alimshika mkono na kumfanya mrembo huyo kutoa tabasamu na kuona aibu kwa wakati mmoja.

Bi Wema alikuwa amenunua nyumba nzuri , ijapokuwa haikuwa kubwa kama ya kwao , lakini ilitosha familia ya watu saba na mazingira yake yalikuwa mazuri pia kufanya watu wanaoishi hapo kuonekana wa kipato cha juu , lakini ajabu kwake ni kwamba hakuwahi kuingia ndani , licha ya kwamba alipafahamu.

Baada ya kuingia ndani aliweza kuona ubunifu wa mapambo ya ndani haukuwa na utofauti na nyumbani kwake , kitu kidogo kiichotofatiana ni kwamba nyumba hio haikuwa na mapambo mengi eneo la sebuleni , ubunifu wake ulikuwa ni ule wanaoitwa Simple enterior design.

Bi Wema alitoka akiwa ameshikilia mabakuli akionekana alikuwa jikoni akiandaa chakula.

“Sir ushafika , karibu sana ndio naandaa chakula na kuna vitu vichache naendelea navyo muda si mrefu chakula kitakuwa tayari , karibu uketi”Aliongea Bi Wema kwa ukarimu.

Ukwei Bi Wema hapo alikuwa akimchukulia Roma kama Mkwe wake sio kwa Edna bali kwa mtoto wake wa kike Rufi.

“Halafu nimesahau kwenye gari nimenunu samaki , ngoja nikawalete”Aliongea Roma akitaka kutoka lakini Bi Wema alimzuia na kumpa kazi hio Rufi aifanye na Roma alitingisha kichwa kukubali na kumwachia Rufi ufunguo.

Muda wa saa mbili wakati Roma aipojikaribisha Mezani kwa ajili ya kushambulia chakula mlango wa kuingiia ulifunguliwa na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia mgeni aliefika.

“Aisee, kunanukia vizuri jamani , naona nimechelewa , Bi Wema , Rufi nimekuja tena”Ilikuwa ni sauti ya Amina na kiswahili chake kisichonyooka na alijikuta akishangaa baada ya kumuona Roma pia yupo kwenye meza.

“Mpenzi kwanini uko hapa , na wewe umekuja kwa ajili ya chakula cha usiku?”Aliuliza kwa kingereza.

“Kwannini inaonekana kama vile unakuja mara kwa mara?”Aliuliza Roma huku akiwa ameupamba uso wake na tabasamu kwa furaha ya kumuona huyo mrembo na alishangazwa siku hio kumuona Amina akiwa amevalia Shungi kichwanni na kumfanya kupendeza zaidi.

“Anasema hajisikii kula peke yake , lakini pia anapenda mapishi ya Mama , amekuwa bize kwenye siku hizi chache hatujaonana kwa muda”Aliongea Rufi.

Amina kutokana na baba yake kusafiri kwenda nje ya nchi kimatibabu kwa mara nyingine alijikuta akiishi peke yake , kutokana na kwamba hakuwa na uzoefu na maswala ya biashara za baba yake ilimchukua muda mrefu kukaa kazini na kukamilisha majukumu yake.

“Mr unaweza ukawa hujui , ukweli ni kwamba Amina na Rufi ni marafikii wakubwa na kipidi ulipokuwa nnje ya nchi walikuwa wakitoka mara nyingi pamoja kufanya shopping na aimfundisha pia namna ya kujiremba”Aliongea Bi Wema.

“Yeah mimi sio kama nakula bure nafanya juhudi pia”Aliongea Amina na kisha aliweka chini mifuko aliokuja nayo na kusogea mezani.

Roma aligundua hakuwa makini na hawa wanawake, hakuwa na uelewa kwamba Rufi na Amina wamekuwa marafiki kama iivyokuwa kwa Dorisi na Rose kuwa marafiki, lakini ilileta maana , ukiachana na kwamba wote hawakuwa wakielewa vizuri kiswahili lakini pia walikuwa na tabia zinazoendana.

Muda wote wa chakula Amina alikuwa akipiga stori na Rufi ambazo hazikuwa na miguu wala kichwa na Roma hakutaka kuingilia zaidi ya kuweka umakini wake kwenye kula.

“Halafu sikukuona wiki nzima , ulikuwa umeenda wapi?”Aliuiza Rufi na kumfanya Amina kushika shingo yake kuizungusha kuonyesha ishara ya kuchoka.

“Nimekuja kugundua kuongoza kampuni sio mchezo , tokea nirithi nafasi ya baba yaani mambo ndani ya kampuni ni mengi , wakurugenzi wa bodi kazi yao ni kunilalamikia hili halipo sawa lile halipo sawa khaa”

“Nini kimetokea kwani?”

“Washindani wetu wa kibiashara wanahati hati ya kupata tenda ya kufunga mitambo ya gesi kwenye baadhi ya hoteli na majumbani hio ni mara baada ya kupata uwekezaji mkubwa kutoka nje ya nchi , nadhani unajua tunajihusisha zaidi katika uwekezaji wa nishati , sasa kama zabuni hio tukikosa hisa za kampuni zitaporomoka maana washindani wetu wanasapoti kubwa serikalini”Aliongea huku akitia huruma.

“Lakini kampuni yenu si ilifanya Merge na baadhi ya biashara zilizokuwa chini ya Tajiri Khalifa Tanzania , bado kuna kampuni inayoweza kuwaletea ushindani?”

“Hakika ipo , mambo kwasasa yanabadilika sana tena kwa haraka sana , ni rahisi kujenga kampuni yenye msingi mzuri wa kibiashara kadri utakavyokuwa na rasilimali watu wenye talanta kubwa ya ubunifu lakini pia wenye ushawishi wa juu , Washindani wetu inapokea sapoti kubwa kutoka serikaini hivyo kazi lazima ifanyike kwa umakini katika kudili nao , najihisi muda mwingine kuzimia nikiwa ofisini”

“Hubby tafadhari msaidie Amina anatia huruma , wewe si una hela nyingi kwanini usinunue hio kampuni?”Aliongea Rufi.

“Ujinga , kwanini nifanye hivyo wakati hawajafanya hila yoyote , wameonyesha ushindani wa haki na kama nitaingilia kwasababu tu mimi tajiri itanifanya nionekane muhun na sina maadilii, hata kama nikifanikiwa kununua vipi kuhusu makampuni mengine lazima na yenyewe niyanunue ili kumuondolea ushindani, haina haja ya kuwa na wasiwasi , Amina hata kama kampuni yako ikifilisika nitakuwa na pesa za kuwatunza wote”

“Okey nimeelewa , lakini sipendi kuona akipoteza kampuni ambayo ndio kwanza amepewa kuongoza”

“Nilishawahi kujiambia kuongoza kampuni sio jambo gumu sana lakini tokea nilivyopewa majukumu yote na baba , niligundua ni kazi ngumu mno , kuna baadhi ya vitu najikuta kwenye Dilemma hata kuvitolea maamuzi , nimejikuta nikimkubali Dada Edna , Ameweza kuwa CEO wa kampuni katika umri mdogo lakini anazidi kung’ara tu”Aliongea kwa kulalamika , lakini mara baada ya kmtaja Edna moyo wa Roma ulishituka tena na hata hamu ya chakula ikapungua palepale.

“Sir sijawahi kukuuliza , Je ulienda kumtafuta Edna nakuongea nae kwenye siku hizi mbli , amekubali kurudi nyumbani?”Aliuliza Bi Wema mara baada ya kusikia jina la Edna, kwa wakati huo Bi Wema alikuwa akijua kingeereza licha ya kwamba alikuwa na ugumu kwenye kuongea lakini aliweza kusikia baadhi ya maneno na alijifunza kwa ajili ya Rufi.

Amina na Rufi walimwangalia Roma wakitaka kusikia jibu kutoka kwake kuhusu Edna, lakini swali hilo lilimfanya Roma kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Bi Wema nafikiri Edna hatorudi nyumbani hivi karibuni?”

“Kwanini unaongea hivyo , nini kimetokea?”Aliliza Bi Wema kwa wasiwasi na Roma hakuona haja ya kuwaficha na aliwaeleza mambo alioyafanya katika siku zote alizoenda kuongea na Edna na kuchomolewa.

“Bi Wema nashindwa kujua ni namna gani naweza kumaliza tatizo , nilimpelekea kifungua kinywa kwasababu nilikuwa nikimuwazia lakini badala ya kunipoktea alinishuku na Recho ambaye nilimkuta ofisini akiwa yeye hajafika kazini, kwanini akaanza kupandisha jazba na kutaka ugomvi?”Aliongea kwa kulalamika na kumfanya Rufi na Amina kiumwangalia kwa huzuni na walishindwa kuongea chochote.

“Mr Najua umekasirika namna ambavyo Edna anakufanyia lakini naamini anajua unafanya hayo yote kumbembeleza , lakini muda mwingine wanawake wanapofikiria kitu hawazingatii kipi ni sahihi na kipi sio sahihi wala kujali nani anatakiwa kuwajibika “

“Kwahio anataka nini sasa?”

“Mtazamo wako”

“Mtazamo wangu?”

“Ndio wanawake wanajali sana mtazamo wa mwanaume kwao , inaweza ikaonekena labda napindisha lakini hata kama amefanya makosa kukufanyia hivyo , mtazamo wako ndio tatizo , kwa mfano ulienda anapoishi kuomba msamaha lakini hukumtaarifu kwamba unaenda na ulienda kama vile atakusikiliza na kukusamehe hapohapo, nadhani hicho kimemfanya ajisikie vibaya zaidi , Edna anatabia ngumu sana kuzoeleka lakini ni mtu mkarimu na mwenye moyo mzuri, angekusamehe kama ungeongea nae vizuri , kuhusu kifungua kinywa cha leo nadhani usingemjibu wala kuonyesha kukasirika , alikuwa anajaribu kutafuta sababu tu ya kukukasirikia , sidhani kama alifikiria kweli kuna kitu kinaendelea kati yako na Recho”Aliongea Bi Wema na Roma aliona ni sahihi , alikuwa akijiamini sana mambo yangekuwa marahisi kwake kusamehewa , ijapokuwa aliomba msamaha kwa dhati lakini hakuonyesha uhatari wa kuona kwamba hatosamehewa alionyesha mwonekano ambao ni kama vile ni haki yake Edna kumsamehe na hapo ndio alipoona amekosea..

“Bi Wema upo sahihi , lakini bado naweza kusema mpaka sasa hatua ambayo tumefikia sidhani mambo yatakuwa marahisi na sioni sababu yake ni hasira zake juu yangu kumshuku au kuna mengine , sina mpango wa kumtafuta kwa sasa”Aliongea Roma.

“Unaonaje mimi nikienda na kuongea nae?”Amina aliongea na kumfanya Roma kucheka.

“Amina humuogopi Edna ?”

“Namuogopa ndio lakini sidhani kama atakataa kuonana na mimi , kwasababu siku zote ananichukulia mimi ni mwepesi kwake .. ninaweza kwenda na kumuuliza baadhi ya mbinu za kibiashara pia”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria.

Ijapokuwa aliona sio wazo zuri kwani lingemkasirisha zaidi Edna , ila aliona ni kheri Amina na yeye kwenda kujaribu maana yeye amekwama.
ITAENDELEA - MAWASILIANO 0687151346
Watsapp tunaelekea mwishoni mwishoni mwa hii simulizi... tunaelekea sehemu ya 700 wiki hii nicheki kama unahitaji mwendelezo
Ohooooo
 
Back
Top Bottom