Mkuu
singanojr tuwekee sehemu ya 584 ili tupate muunganiko mzuri
SEHEMU YA 583.
Baada ya chakula cha usiku Aloni ndio aliemfuata Roma na kuondoka nae kuelekea Club ya Pink Lady.
“Bro mmiliki wa Pink Lady ni mwanamke ambae ametokea kuwa rafiki yangu sana, lazima atatuletea warembo wa kutosha leo hii ili kusindikizia bia zetu”Aliongea Aloni huku akiendesha gari.
“Umenialika mimi tu na Omari?”
“Hapana , Bro Denisi hajakuambia nimemualika pia?”Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kukaa kimya.
Dakika chache mbele waliweza kufika nje ya hoteli hio na eneo lilionekana kuchangamka kutokana na uwingi wa magari na watu waliokuwa wakiingia , zilikuwa ni taa tu za rangi maalumu zilizokuwa zikimuliika na kufanya eneo lote kupendeza na ilimfanya Roma kushangaa kwani hakutegemea uwepo wa eneo kama hili kwa mkoa huo wa Iringa.
Omari alikuwa tayari amekwisha kufika na alikuwa akimsubiria Roma huku kidogo akionyesha hali ya wasiwasi kwenye macho yake.
“Bro ni mara chache sana nakujaga kwenye maeneo kama haya , kidogo sijiamini”
“Kama ni hivyo kwanini upo hapa?”
“Mimi ni mwanaume pia , siwezi kukaa nyumbani muda wote na kwasababu upo hapa kidogo hali yangu ya wasiwasi imeondoka”Aliongea Omari na kumfanya amwangalie na kutabasamu na kuona licha ya kujiamini kwa Omari lakini bado alikuwa akiogopa vitu vidogo kama hivyo.
Ilionekana Denisi bado hakuwa amefika kwani mara baada ya wote watatu kuingia kwenye Club hio iliochangamshwa na mziki pamoja na warembo hawakumuona.
Aloni alionekana kujizolea umaarufu kwani alisalimiwa na wateja wengi ndani ya hilo eneo.
“Bro tutaenda moja kwa moja upande wa VIP na nitaita warembo kadhaa kuja kutufanyia masaji”Aliongea Aloni kwa kujigamba.
Dakika hio hio wakati Aloni akiwa anajaribu kupamba eneo hilo kwa maneno mazuri kuhusu huduma zinazopatikana , ghafla tu mhudumu aliekuwa ameshikilia tray la glass za bia alikumbana nae na kumwagikiwa na baadhi ya bia na glasi kupasuka na kumfanya kuloana.
“Ah!…Samahani , samahani sana kaka sio maku ..”Yule muhudumu alijikuta akiwa katika mshituko huku akimwangalia Aloni na uso uliojaa woga.
“What the f**…. Una shida gani wewe?”Alijikuta akipandwa na jaziba huku akiangalia nguo zake zilizochafuka kwa kumwagikiwa na mapombe.
“Unafikiri kuomba msamaha kunatosha eh? Unajua hii suti bei yake ni shilingi ngapi wewe?, au unafikiri kwa kujiuza kwako unaweza kuinunnua”Aliongea huku akimshika yule mwanamke ukola wa tisheti yake ya kihudumu.
Alikuwa ni msichana mdogo mno aliekuwa amepaka kwa mbali vipodozi , hakuwa mrembo sana wala mjanja lakini alikuwa na muonekano flani hivi tofauti na makahaba waliokuwa hapo ndani.
Makelele ya Aloni yaliweza kumfikia mwanamke ambae alikuwa meneja wa Club hio na kusogea haraka kujua nini kinaendelea na baada ya kuona suti ya Aloni na glassi zilizodoka chini na kupasuka hakuwa na haja ya kuuliza maswali.
“Mr Aloni tafadhari punguza jazba , huyu msichana ndio ameanza kazi, ni mwanachuo tu ambaye anafanya kazi ya muda na huenda akawa amechoka mchana yote kwa kufanya kazi”Aliongea kumtetea lakini Aloni ni kama hakuwa akisikia alichokuwa akiongea na kuendelea kumwangalia yule msichana kwa macho makali .
“Samahani kaka yangu ninaweza kukufidia ,, naomba nikaisafishe..”Aliongea yule mshichana kwa kutetemeka.
Roma muda wote yeye alikuwa kimya tu lakini upande wa Omari alianza kungiwa na huruma mara baada ya kusikia mwanamke huyo ni mwanachuo , alikuwa akijua maisha ya chuo kwa hapa Tanzania muda mwingine yanavyokuwa magumu na huenda ndio ilisababisha mrembo huyo kuja kufanya kazi katika mazingira kama hayo.
“Ni koti tu lilichofauka sana , unaonaje ukaachana nae isitoshe ushaambiwa ni mgeni hapa hebu punguza hasira zako”
“Sawa Bro Omari..”Alitikia kinyonge.
Yule meneja mara baada ya kusikia jina la Omari aliweza sasa kujua watu hao ndio watu muhimu ambao alikuwa wakitarajiwa kufika na kwa haraka sana alitoa tabasamu lake la ukarmu na kushukuru na yule msichana ambae waliweza kumjua kwa jina la Fetty aliwashukuru kwa kutoyafanya mambo kuwa makubwa.
Baada ya kuonyeshwa eneo maalumu lililojitenga kwa ajili yao kama VIP muda huo huo warembo walifika huku wahudumu na wenyewe hawakucheza mbali kwani waliweza kuwahudumia vinwaji walivyotaka.
Roma alijikuta akicheka mara baada ya kahaba mmoja kumshika mabega yake na kuanza kumfanyia masaji kwa namna ya kumtekenya na kumfanya Omari kuruka kama kijana ambaye hajaifikia balehe.
Muda huo huo na Denisi na yeye aliweza kufika na kumkuta kila mtu akiwa amezungukwa na warembo , alikuwa ameshikilia sigara mkononi na alitoa tabasamu mara baada ya kumuona Omari anavyofumba fumba macho kutokana na kushikwa shikwa na mikono ya mwanamke mrembo.,
“Bro Omari naona mwenyewe huduma imekukolea , warembo wa hapa ni wa viwango”
“Unaonekana haya ni maeneo yako “Aliuliza Roma.
“Ni kwasababu Aloni anafahamiana na mmiliki ndio maana nakuja mara kwa mara”
“Bro Denisi kaa kwa kutulia muda si mrefu Sister Tasi analeta ndafu tushushie na bia zetu”Aliongea akimaanisha mbuzi wa kuchoma
Ni muda huo huo mwanamke ambaye alikuwa amevalia suruali na blauzi ya rangi ya pink mikono mirefu aliweza kuingia huku akiwa amevalia miwani kwenye macho yake , hakuwa peke yake bali alikuwa ameongozana na watoto wa kike na kwa haraka haraka walionekana kuwa ni wanachuo ambao wamezoea kuja hapo kujipatia ‘madanga’, wote walikuwa wamevalia nusu utupu na kumfanya Omari mwili wake kumsisimka.
“Aloni nimechelewa kidogo kutokana na kuwa bize kuwaandalia warembo wa kuusindikiza usiku wenu vizuri , wote hawa ni warembo wa chuo na wako ‘fresh’ na watamu balaa lakini kidogo wana aibu , unaonaje?”
Roma aliangalia wanawake hao walioletwa na kwa upande wake hawakuwa warembo sana lakini maumbo yao yalikuwa yakivutia mno na kupagawisha.
“Bro hii ndio mara ya kwanza nakuja katika haya maeneo , hapa vipi napaswa kuchagua au inafanyika vipi?”Aliuliza Omari.
“Ndio maana yake na unaweza hata kumchagua mmiliki kama hao wengine hawakuridhishi”Alijibu Roma huku akimnyosshea mwanamke mwenye nywele zilizopakwa rangi ya pinki.
Upande wa Roma aliweza kuona sura ya mwanamke huyo anaefahamika kama mmiliki kama ameiona mahali lakini hakuweza kujua ni wapi lakini kwasababu kila kitu kilionekana kuwa kawaida ilimfanya kujawa zaidi na shauku.
“Au sijaumbiwa kuja haya maeneo , nahisi kama vile nawaonea hao wanawake kwa kuchagua”Aliongea Omari.
“Hao wasichana hawajali huruma zako bro na wapo hapa kwa ajili ya hela zako tu kama utaamua kucheza nao wala sio kulala nao basi watakuwa tayari pia”
“Hamna leo hii nipo hapa kwa ajili ya kuonyesha watu , ili kupunguza maneno ya watu wanaosema nimewekewa Limbwata na mke wangu”
“Sister Tasi kwa muonekeno wa Mabraza hapa inaonyesha hawa warembo sio wazuri kwao , tunaomba awamu nyingine tafadhari”Aliongea Aloni alionekana mzoefu sana kwenye hayo maeneo lakini hata hivyo shughuli ililiuwa ya kwake ndio maana alikuwa akijitahidi kumfanya kila aliemualika kuwa katika hali ya kufurahi.
Tasi mara baada ya kuambiwa hivyo hakuchelewa kwani dakika chache tu mara baada ya wale kuondoka waliweza kuingia wanawake wengine ambao awamu hio walikuwa wameziba maeneo machache tu kwenye miili yao huku wakiacha sehemu zingine zote kuwa wazi kwa ajili ya matangazo.
“Gentlemen!!, hawa ni warembo ambao wamemaliza chuo kabisa na ni wastaarabu, unaweza kuwaita ‘high classic chicks’ sidanganyi na kama mnataka kuwaonja hawatowaangusha lakini bei yao imechangamka kidogo lakini naamini kwauzito majina yenu hamna wasiwasi na bei”
Omari macho yake yalichangamka , ijapokuwa hakuwa muhuni lakini alipenda kuona wanawake warembo .
Upande wa Denisi hakutaka kupoteza muda , palepale alinyoosha mkono wake na kuwapa ishara wanawake wawiri warembo wamsogelee na wale warembo walichangamka kwa kutabasamu na kumkimbilia kwa mbwembwe zote za kimadaha.
“Bro Omari kama hawakupendezi bado Sister Tasi anao wengine ni wewe tu kutaja aina ya mwanamke unaemtaka”Aliongea Aloni na kumfanya Omari kukohoa kidogo , moyo wake ulikuwa ukisukuma damu kwa haraka sana na ili asionekane mshamba alinyooshea wanawake wawili ambao walikuwa na shepu kubwa na wakamsoogelea.
Upande wa Roma alishangaa kidogo kwani wanawake Omari aliochagua walikuwa na maumbo sawa kama la Queen
“Mr Roma wewe utahitaji yupi hapa?”Aliuliza Tasi na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli.
“Hakuna alienivutia hapo tofauti na wewe mwenyewe”Alongea Roma na kumfanya Tasi tabasamu lake kidogo kubadilika kwani hakutegemea kauli yake lakini palepale alipotezea na kutoa kicheko.
“Hehe Mr Roma unatania bwana, mimi nishazeeka tayari na isitoshe nipo bize na biashara”
“Mimi sijali chochote kama una biashara au mambo gani , kama hutonihudumia basi nitaharibu hili eneo usiku huu”Aliongea Roma kibabe na palepale yule mwanamke alijikuta akikosa kujiamini na kumwangalia Denisi aliekuwa pembeni na kisha akamgeukia Roma kinyonge.
“Kama ni hivyo basi sina usemi, lakini kwanini unataka kuadhibu mwanamke mzee kama mimi jamanii..”Aliongea kimadaha na kisha aligeukia wale wanawake waliobaki na kisha akawapa ishara ya kuondoka na akamsogelea Roma huku akijiegamiza kwake na kufanya manyonyo yake kugusana na kifua cha Roma,
Mwili wa mwanamke huyo ulikuwa mlaini mno na harufu ya manukato yake yalikuwa ni yale ambayo hayasahualiki kwa haraka.
“Binamu hakika una macho makali , Sister Tasi ndio habari ya mjini hapa”Aliongea Aloni akimsifia Roma
“Mr Aloni usiongee kuhusu mimi kwanza lakini kwanini hukuchagua mtu wa kuusindikiza usiku wako leo”Aliuliza Kizwe na ni kweli Aloni hakuwa na mtu ambaye ameambatana nae kama ilivyokuwa kwa kile mtu hapo ndani.
“Kuna yule mrembo uliesema ni mgeni , anaitwa Fetty ndio namuhitaji , nataka umlete chumba cha pili nimalizane nae usiku huu”Aliongea na kumfanya Tasi sura yake kubadilika kidogo.
“Aloni unajua kwamba sitaki kukuangusha lakini hao wasichana wapo hapa kwa ajili ya kazi tu na sio kujiuza”
“Huo ni ujinga , kwahio unaniambia kwamba kuna wanawake hapa waliokuja kuafanya kazi na hawapo tayari kujiuza hata kama nikitoa hela za kutosha?”
“Bro hebu achana nae , ushaambiwa kaja hapa kwa ajili ya kazi tu , si halali kufanya hivyo”Aliongea Omari na mwonekano wa Aloni ulikuwa ni ule wa kukosa uvumilivu.
“Bro inaonekana huna uzoefu sana wa kuja maeneo ya starehe , nimeingia kwenye Casino na Bar nyingi na wanawake wa namna hii nimekutana nao sana tu na mara nyingi wanajifanyisha kufanya kazi kwa kutotaka kujiuza lakini ukweli wapo tayari kufanya chochote ukiwapa hela , wanachokifanya ni sitaki nataka ili kupandisha hadhi yao tu wapate hela nyingi na isitoshe sisi wanaume hatutoshelezwi na mwanamke mmoja na mwanaume dhaifu pekee ndio atabakia kuwa na mwanamke mmoja, halafu muda mwingine kama utachagua mwanamke ambaye muda wowote yupo tayari kukubali inapunguza radha bro , ukipata kanakojifanyisha fanyisha kanakuwa katamu balaa”
Upande wa Oamri sura yake ilijikunja mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwaAloni kwani ni kama anadhihakiwa na alijikuta akimwangalia Roma kwa dakika lakini upande wa Roma hakutia neno.
“Sister Tasi namhitaji yule Fetty kwa ajili ya usiku wangu wa leo , ukweli najua taarifa zake zote na nimeambiwa anatokea katika vijiji vya huko Bukoba na familia yake ni ya kimasikini sana na mkopo anaopata haumtoshelezi kulipia ada na mahitaji yake , kama atakubali kuwa na mimi usiku huu nitahakikisha namtafutia kazi nyingine na akimaliza chuo nitamtafutia kazi Dar, nasikia hao warembo wanatembea na Dawasa zao nataka nijionee mwenyewe haha..”
Baada ya kuona Omari kaomba sana alimpa ishara meneja na upande wa Aloni alitabasamu na kisha akasimama na kutoka kuingia chumba cha pembeni huku akimkonyesha Denisi
Upande wa Roma alikuwa kimya muda wote na mara baada ya Aloni kutoka hapo alimgeukia mrembo wake aliekuwa pembeni yake.
“Hey mrembo umekuwa hapa kwa muda gani”Aliuliza Roma na Tasi alitabasamu.
“Kaka kwanini unauliza maswali hayo , maswala ya biashara yanaondoa mudi kwanini usiendelee kunywa kinwaji chako na tuhamie kwenye mchezo?”
“Je kama bado nataka kujua ?”
“Nimeanza kufanya biashara katika hili eneo kwa zaidi ya miaka mitano licha ya mwanzo nilikuwa nimejikita upande wa hoteli tu”Aliongea
“Kweli?, ndio umejenga hii hoteli?”
“Ndio nilijenga mimi”Alijibu na kumfanya Roma kutabasamu.
“Kwa taarifa nilizokuwa nazo hii hoteli imejengwa miaka kumi iliopita na imeweza kuwa na wamiliki wawili tofauti kabla yako na ilianza kama ukumbi wa uliotambulika kwa jina la Golden Hall na baadae ikaja kuwa hoteli ikitambulika kwa jina la Golden Hotel”Aliongea Roma.
“Sina uhakika kama taarifa uliokuwa nayo ni sahihi , lakini wewe si mgeni hapa Iringa? umejuaje yote hayo au kuna kitu unataka kujua kutoka kwangu?”
“Nilikutana na rafiki yangu nje ya nchi miaka kadhaa iliopita na wakati narudi Tanzania aliniambia alishawahi kukutana na mwanamke nchini Tanzania na ni mmiliki wa hoteli ya The Golden kwa zaidi ya miaka kumi na kuniomba kama nitafika nijaribu kumtafuta nimfikishie salamu”Aliongea Roma.
“Samahani kama ni hivyo kwani siwezi kukusaidia”Aliongea Tasi huku akijaribu kutingisha mabega na aliishia kumwangalia Denisi ambaye alikuwa kimya muda wote lakini alikuwa kama vile hakuwa akisikia chochote na aliendelea kutaniana na warembo aliokuwa nao akiwashika shika katika maeneo nyeti..
“Mr Roma kama utakuwa unakuja mara kwa mara huenda ninaweza kukutafuuta huyo mtu , isitoshe hili eneo kuna watu wazee sana ambao wameanza kufanya kazi muda lakini pia kuna wageni wengi wanafika”
“Kama ni hivyo nitashukuru sana”Aliongea Roma.
Ukweli ni kwamba alitunga kuhusu mwanamke na rafki yake lakini kuhusu hoteli hio kuitwa The Golden hakuwa amekosea kwani kabla ya ujenzi wake kulianza kujengwa ukumbi ambao ulikuwa ukifanyia matamasha mengi ndani ya eneo hilo la Iringa ,ukumbi uliofahamika kwa jina la Golden Hall, Roma maelezo hayo alikuwa nayo kutokana na kwamba kabla ya kuja alishafanya utafiti wake tayari.
Muda huo huo mlango wa kuingilia ulifunguliwa kwa nguvu na msichana alidondoka chini akionekana kama vile alikuwa akikimbia.
“Sister Tasi tafadhari nisaidie”
Alikuwa ni yule msichana aliefahamika kwa jina la Fetty na baada ya kusimama alienda moja kwa moja kupiga magoti mbele ya Tasi.
“Sister Tasi walinzi wanataka kunikamata tafadhari waambie mimi ni mhudmu tu sio kahaba”Aliongea akijitetea mbele ya Tasi na kufanya wale makahaba wengine kumwangalia na kisha wakamsonya.
Ilionekana mara baada ya ya mwnamke aliefahamika kwa jina la Tasi kutoa maelekezo kwa meneja alimuelekeza kwenda kwenye chumba cha Aloni lakini akakataa na kupelekea kukamatwa na wale walinzi ili kulazimishwa.
Alikuwa akilia wakati ambao alikuwa akiomba na kwa muonekano wake alikuwa akitia huruma sana na muda uleule wale walinzi waliingia katika Cabin yao wakiwa wameongozana na Aloni.
“Wewe Malaya unathubutu vipi kuonyesha ujeuri wako?”Aliongea Aloni huku akijaribu kumshika yule msichana ili kumvutia kuelekea kwenye chumba lakini Fetty alitaka kukimbia tena lakini wale mabodigadi walimzidi nguvu na kumbeba juu juu.
Upande wa Tasi hakuonyesha uso wa huruma hata kidogo lakini upande wa Omari ambaye alikuwua akimiminiwa mvinyo na mrembo alikosa uvumilivu wa kushuhudia kitendo kile.
“Hey Aloni hebu muache huyo msichana kama hataki”Aliongea kwa sauti.
“Bro tusiharibiane starehe zetu kwasababu kila mmoja hapa yupo kwa ajili ya kuburudika”
“Kwahio kubaka ndio unakuita Sterehe , kama msichana hafanyi kazi hio haina haja ya kumlazimisha kwani unakuwa ni kama ubakaji”Aliongea na kumfanya Aloni kumgeukia yule mrembo alieshikiliwa na mabodigadi na kisha akamshika mkono na kuongea nae kwa sauti ya chini.
“Fetty wewe mwambie braza yangu pale , je upo tayari kuwa na mimi kwa hiari yako au lah?”Aliuliza lakini Fetty alikuwa akitoa machozi , alionekana ni wale wasichana aina flani hivi wachanga wenye ujinga wa kutoelewa mambo mengi ya kimjini.
Lakini kitu cha kushangaza mara baada ya kuulizwa lile swali alitingisha kichwa kwamba anakubali.
“Acha kuwa muoga kama haupo tayari wewe niambie au kuna kitu kakutishia nacho?”Aliendelea kuuliza Omari lakini Fetty aliishia kung’ata meno yake kwa hasira na kisha akatingisha kichwa kwa namna ya kukataa kwamba hakuna kitu ambacho ametishiwa nacho.
“Nishakuambia braza hawa wanawake wa siku hizi ni waelewa sana maadamu utakuwa na faida kwao , wewe furahia maisha na warembo na mimi ngoja nikainjoi nae niyatiririshe haha..”Aliongea kwa furaha na huku akaondoka lakini Omari bado alikuwa kwenye hali ya kutoridhika.
“Bro Ommy kuwa mpole , yeye ndio kaamua na atapata malipo, haina haja ya kuwa na wasiwasi”Aliongea Denisi.
“Hapana siwezi kutulia , Roma, Aloni ni binamu yako na lazima atakusikiliza hebu chukua hatua, nina uhakika kuna kitu amemtishia yule mwanamke ndio maana amekubali kishingo upande”Aliongea na kumfanya kwanza Roma kucheka.
“Umenialika kuja hapa nikusindikize kwa ajili ya burudani lakini ninavyokuona unanitafutia tu matatizo”Aliongea Roma lakini kwa namna ambavyo Omari alikuwa na uso wa usiriasi Roma aliamua tu kusimama na kuelekea upande wa pili wa chumba alichoingia Aloni na yule msichana.
Baada ya Roma kufundua tu mlango kidogo aliweza kusikia sauti za kilio kutoka kwa Fetty huku akitoa makelele ya kumwambia Aloni aache na mabodigani waliokuwa mbele walitaka kumzuia Roma kuingia lakini yule mwanamke Tasi aliwapa ishara ya kuondoka.
“Bro Roma kwanini upo hapa tena”Aliuliza Aloni kwa mshangao mara baada ya kumuona Roma kaingia..
Aloni muda huo alikuwa kwenye kitanda tayari akiwa amemkalia yule msichana kwa juu na ilionekana alikuwa akimlazimisha kuvua nguo ya ndani na Roma hakujali sana zaidi ya kusogea mpaka kwenye kile kitanda na kisha akamtoa kwa nguvu..
“Ondoka hapa na katafute wanawake wanaopenda hayo mambo ndio ucheze nao”
“Kwasababu Bro wewe ndio umeongea basi nitaondoka, sisi ni binamu hata hivyo”Aliongea na kisha akatoka na kufuatiwa nyuma nyuma na Tasi.
Fetty ambaye tayari alikuwa nusu uchi aliishia kukumbatia vigoti vya miguu yake huku akitoa machozi na kutetemeka.
“Asante sana kaka”Aliongea kushukuru.
“Nilijua unaigiza mwanzoni lakini baada ya kuona hisia zako sio feki nikaona nije nikusaidie”
“Naigiza…! Kivipi kaka?”alitaka kuongea huku akifuta machozi yake kumwangalia Roma kwa mshangao lakini Roma alimzuia.
“Hakuna kitu”Aliongea Roma huku akimwangalia yule msichana kwa dakika kadhaa na kisha akatabasamu mara baada hana kitu cha pekee kwenye mwili wake zaidi ya nguvu ya kawaida ya kiulinzi ya kichawi aliowekewa kimila.
Alijiambia huenda anafikiria mbali , kwanini msichana mpole kama huyo kumuigizia na kumuingiza kwenye mtego hivyo aliamua kupotezea.
“Bro je unaweza kuniambia namba yako ya simu, ninataka kukushukuru siku moja , baba yangu ameniambia kama hutoweza kulipa fadhila basi nitapigwa na radi”Aliongea huku sauti yake ikitoka katika hali ya huzuni na kuwa ile ya kike ya kushawishi mwanaume.
SEHEMU YA 584.
Roma bakutaka kuvutana nae hivyo aliamua tu kumpa namba yake ya simu na kisha kumuacha.
Baada ya kurudi kwenye Cabin yao aliwakuta Denisi na Omari akiwa tayari washachangamka na walikuwa wakila ‘goodtime’, ijapokuwa Aloni alionekna hakuwa amependezwa na kumkosa yule msichana lakini tayari alikuwa ashajitafutia mwanamke mwingine.
Sister Tasi aliita wanawake(Chicks) wawili kwa ajili ya kukaa na Roma mpaka muda wa usiku, upande wa Roma na Omari kutokana na mafunzo yao ya kijini ilikuwa ngumu sana kuelewa na mara baada ya kuona muda umeenda alimpa ishara kwamba waondoke.
Omari alichukua njia yake kwa kuendesha Range yake na Roma aliendesha gari ya Aloni mpaka nyumbani.
Roma kabla hata hajaingia ndani simu ya Omari iliingia na akaipokea palepale na kumwambia ashafika nyumbani.
“Bro nadhani nimezima maneno ya watu kwa leo hii , nilikuwa nikijisikia vibaya sana pale kuwa mbali na mke wangu”
“Nilijua ulikuwa ukiburudika na wale warembo kumbe ulikuwa ukimuwazia mkeo?”
“Unanichukuliaje wewe , ninaweza kuwa na hela kama wewe lakini mimi nina sheria zangu na isitoshe sasa hivi ni baba wa mtoto hivyo lazima niishi kama baba , tukiachana na hayo vipi kuna kitu chochote ambacho sio cha kawaida uliona pale?”
“Nimeona lakini sio sana , angalau nimeweza kujua yule Tasi sio mmiliki halali wa ile hoteli licha ya kwamba anaonekana kabisa kama mmiliki wa mwanzo, lakini bado sio yeye”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Unakumbuka nilisema hoteli ile ilikuwa ikiitwa Golden na ilianzia kama ukumbi?, kabla ya kuja pale nilikuwa nishafanya tafiti zangu tayari na ni kweli wakati ilipobadilishwa jina ilinunuliwa na mwanamke ambaye kwenye picha nilionyeshwa kabisa ni yule yule wa leo , lakini ajabu ni kwamba nilivyomuuliza kuhusu jina la hoteli hio miaka kumi iliopita hakuwa akifahamu , kwa maelezo niliopewa yule Tasi mmiliki wa ile hoteli ni Mkinga ambaye alirithi mali kutoka kwa mume wake ndio akainunua na ni mkazi wa hapa hapa wa muda mrefu, kitu kingine muda wote yule mwanamke alikuwa akimwangalia Denisi , ijapokuwa alikuwa na uwezo mkubwa wakuigiza lakini bado hakuwa mkamilifu, lakini siwezi kusema wana uhusiano wowote mpaka sasa kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja”
“Kwanini tusimkamate yule Tasi , kuna uwezekano kabisa akatuamnbia kila kitu na kugundua uhusiano uliopo kati yake na Denisi pamoja na yule Haruni”
“Iwe ni familia ya Mzee Longoli au yule mwanamke hata kama pia ni Denisi , sidhani kama ndio watu pekee ambao wapo nyuma ya kila kitu , mchezo wao haujafikia patamu bado nikiwa na haraka unafikiri ninawezaje kumkamata muhusika mkuu?”Aliongea Roma.
“Nilikuwa na shauku huenda ukakosa uvumilivu lakini naona , hebu tutaongea kesho nasikia sauti za jembe langu likilia huko ndani , ngoja nikambembeleze.”Aliongea na kisha akakata simu bila ya kuaga na kumfanya Roma kutabasmau kwa uchungu aliona licha ya bwana huyo kutoka katika mafunzo ya kijinni lakini amegeuka kuwa ‘Super daddy’.
Roma alikuwa akiongea huku akitembea na muda huohuo alikuwa tayari nje ya mlango wa chumba chao na alishangaa kukuta bado taa zinawaka , lakini hakufikiria sana zaidi ya kufungua mlango na kuingia.
*****
Kule kwenye ile Club ya Pink Lady katika chumba kikubwa cha kifahari , Denisi alionekana akiwa amelela uchi chali huku mdomoni akiwa na sigara inayotoa moshi , chini ya kiuno chake alikuwepo Kizwe aliekuwa kama ‘Ndama’ yenye njaa ya maziwa kwa namna alivyokuwa akinyonya.
Denisi mara baada ya kuvuta sigara kwa dakika kadhaa na kuitupia pembeni aliinua uso wake na kumwangalia mwanamke anaejaribu kumfurahisha na alikumbuka jambo na palepale aliinua mguu na kumpiga teke.
“Uwii…!!”
Alitoa ukulele yule mwanamke wa maumivu huku akimwangalia Denisi kwa macho ya kupaniki na mshangao.
“Kilema wangu , ni kosa gani ambalo nimefanya mpaka kunipiga?”
“Tofauti na kuwa Malaya nadhani ubongo wako ni kama wa ng’ombe , ni mara ngapi nilikuambia ujiandae? , hivi unajua jina la Golden hoteli na Golden Hall aliotaja Roma yana uhusiano gani na hii hoteli?, kwanini hujafanya kazi yako kikamilifu , si nilikuambia kuchukua uhusika wote wa Tasi bila kusahau chochote?”
“Nini.. ! nilimfatilia kwa kila kitu mpaka ndugu zake lakini sikuweza kufikiria mbali kufanya uchunguzi wa hoteli hii miaka kumi iliopita , isitishe ni kipindi kirefu nadhani ameweza kugundua?”
“Unafikiria Roma ni mjinga kama wewe mpaka kuuuliza vile , ni kwasababu tu hajajua ni nani ambaye yupo nyuma ya kila kitu ndio maana akakaa kimya , lakini bado naona anakiburi cha kudhania anaweza kuifanya dunia yote ikawa chini yake”
“You seem to know him well”(Unaonekana kumjua vizuri?”)
“Because I am not the second Yan Buwen”(Kwasaabu mimi sio Yan Buwen mwingine”.
Aliongea huku akicheka akimaanisha kwamba yeye ni tofauti na sio kama Yan Buwen .
“Kwahio tunafanya nini ?”
“Tutafanya kinachopaswa kufanyika , ni kama ilivyopangwa , kete yangu ni kumfanya aamini kabisa huu ni mpango uliotengenezwa lakini mwisho wa siku ashindwe kufanya chochote na kuishia kukubali tu”
Baada ya kuona tabasamu la Denisi ilimuaminisha kwamba kila kitu kinaenda sawa na hakuacha na yeye kutoa tabasamu lililojaa kisasi ndani yake.
*******
Siku nyingine asubuhi wakati Roma na Edna wanafika eneo la Dining kwa ajili ya kupata kifungua kinywa , Lanlan tayari alikuwa amekaa na alikuwa ashaandaliwa uji wa maziwa na bibi yake Damasi kwenye bakuli kubwa na alikuwa akihangaika nalo.
Aliongekana kutopenda aina ya kifungua kinywa kilichopo kutokana na kukosekana kwa nyama , lakini alijitahidi kula kwa namna zote kukamilisha kile alichoandaliwa .
Kilichomshangaza Roma ni kwamba kwenye meza alikuwepo Damasi tu mama yake wa kambo na Babu yake hakuwepo na Ashley pia hakuwepo pamoja na Denisi.
“Mama Ashley huyu mzee kaelekea wapi?”
“Asubuhi aliweza kuondoka kwenda kwenye kikao pamoja na baba yako ,Raia wa Zanzibar wameanzisha maandamano kutaka mabadiliko ya kisheria kati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama tu hutofikishwa mbele ya sheria kwa kile ulichokifanya , hivyo wanajeshi wa vyeo vya juu wamekutana kwa ajili ya kikao cha dharula”
“Kwanini sijaambiwa chochote wakati mimi ndio chanzo?”
“Watu wa jeshi wanajua tabia yako ndio maana , hao watu wanakuona kama vile ni muuaji na unaweza kusababisha matatizo zaidi kama utahusishwa , kinachofanyika huko ni kujaribu kumpoza raisi wa Zanzibar kwani inaonekana ndio anaehusika kwa kila kitu”Aliongea Damasi na kumfanya Roma kushangaa kidogo , lakini aliamini huenda mtu ambaye amehusika na kila kitu ni Raisi Senga ili yeye asipatiwe taarifa.
Hata hivyo uzuri wa kikao hicho kilikuwa kikifayikia ndani ya eneo hilo hilo la Afande Kweka kwani lilikuwa limeandaliwa kwa baadhi ya vikavo vya siri sana vya Deep state ndani ya Tanzania.
Sasa upande wa eneo hilo maalumu la mikutano Raisi Senga ndio ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti cha mwanzo kama kiongozi , huku aifuatiwa na Afande Kweka na kisha mkuu wa majeshi Afande Tozo , huku wengine wote wakiwa ni wana usalama waandamizi pamoja na wanasiasa.
Upande wa Afande Kweka alionekana kusoma karatasi ambayo alikuwa amekabidhiwa na mpaka anamaliza kuisoma uso wake ulizidi kuwa mweusi na alipiga meza chini kwa nguvu.
“Jemadari vikosi vyote ambavyo vipo upande wa visiwani chini ya kamanda Razaq vinatii maagizo kutoka kwa raisi wa Zanzibar na kwenda kinyume na katiba ya muungano, tusipochukua hatua za mapema kesho wataanza kuungana na wananchi kufanya maandamano”
“Yeye ni raisi wa Zanzibar tu anapata wapi uthubutu wa kujjipatia madaraka ya kugeuza vikosi vya nchi kuwa upande wake , anachokifanya ni kujaribu tu kutupa presha”
“Ni zaidi ya presha , anajaribu kuchukua hii hali kama fursa ya kutaka kuonyesha ukubwa wa Visiwani, kama ataungwa mkono na baadhi ya nchi za kiarabu , kwa upande wetu hii itakuwa mbaya sana na itatengeneza mgawanyiko mkubwa sana ndani ya Tanzania maana tuna wanajeshi wa asili ya Zanzibar pia”
“Haya yote yanatokea kwasababu ya mtoto wangu ambaye amekosa maadili mazuri ya kimalezi na kiburi kilichozidi , naombeni radhi kwa niaba yake”Aliongea Raisi Senga na kufanya baadhi ya watu waliokuwa hapo ndani kujaribu kumfariji.
“Nadhani sijaomba mtu yoyote kuomba msamaha kwa ajili yangu na isitoshe sina mpango wowote wa kuyatambua makosa yangu”Sauti ya Roma iliweza kusikika akiingia hapo ndani huku walinzi wakimfuatia nyuma kwa tahadhari.
Watu wote hapo ndani walimwangalia kwa macho makali lakini yenye wasiwasi ndani yake , wale waliokuwa na gwanda za kijeshi na pia wale ambao walikuwa na mavazi ya kawaida ikimaanisha wanasiasa wote walikuwa wakimwangalia Roma kwa wasiwasi na yote hayo ni kwamba walikuwa wakimhofia.
“Nimepata taarifa kuna maandamano huko yanatokea kutokana na kifo cha Haruni , nimepewa taarifa pia Kamanda Razaq ni ndugu na mume wa Shangazi yangu Theresia, lakini taarifa nyingine nasikia ni mtu jasiri sana ndani ya jeshi ndio maana akapewa ukamanda upande wa Visiwani sijui taarifa hizi chache nilizopewa ni sahihi?”
“Upo sahihi ukiacha na sifa ulizotaja lakini pia Afande Razaq ni mtu ambaye anaheshimika sana kwa weledi wake sio upande wa bara tu mpaka visiwani kote wanajeshi wanamheshimu na ndio maana ana nguvu kubwa , tumemuweka upande wa Visiwani kwasababu tuliamini ni mtu ambaye yupo ‘neutral’ na hapendi siasa kuingiliana na jeshi”Aliongea Afande Tozo.
“Kama ni hivyo kwanini akachagua upande na kuungana na raia kwenye kuandamana?”
“Hio ndio sababu ambayo mpaka sasa hivi haijatufikia na ndio maana tupo hapa kujadili namna ya kumaliza hili tatizo , niseme chanzo cha migongano hii kilianzia kwa kufariki kwa Mzee Longoli na ilikuwa ikitafutwa tu sababu”Aliongea Afande mwingine mwenye kitambi na kumfanya Roma kumgeukia babu yake.
“Mzee ni kipi kinapaswa kufanyika?”
“Unamuuliza ni kipi cha kufanyika? , wanachotaka ni kitu kimoja aidha kuwepo na marekebisho ya vipengele vya muungano au ufikishwe mbele ya sheria, lakini hilo bado hatujaliafiki,. tulichoona kinafaa ni wewe mwenyewe kwenda kuonana na Raisi wa Zanzibar na kumtuliza kwa muda huku tukiendelea na uchunguzi , Afande kashasema kuna sababu iliokufanya kuchukua maamuzi ya kumuua Haruni hadharani na tuna taarifa ya uchunguzi uliofanyika hospitalini mara baada ya mwili wa marehemu kufikishwa mochwari , hivyo tukiendelea na ufumbuzi zaidi wewe ndio unaepaswa kwenda nyumbani kwa mheshimiwa na kumuomba msamaha na hata wakikuzuia itakuwa ni kwa muda tu, ilimradi maandamano yakome na vipengele vya muungano kundelea kubakia kama vilivyoasisiwa”Aliongea Brigedia mmoja ambaye Roma hakumfahamu.
“Kwahio unashauri kwamba mimi nijitoe kafara niende mpaka Zanzibar bila ya kujali uhatari wote na nikaombe msamaha? , yaanni unaniambia nikaombe msamaha kwa mtu ambaye ananichukulia kama muuaji? , unadhani atakubali kuutoa huo msamaha?”Aliongea Roma akipandisha sauti na kufanya watu wote kuangaliana.
“Nadhani kipaumbele kwasasa ni kujua kwanini Afande Razaq kaamua kuchagua upande wa Zanzibar na kukiuka sheria za muungano na isitoshe anao udungu wa mbali na mzee wetu Afande Kweka”Aliongea Afande Tozo lakini muda huo huo zilisikika purukushani kutoka nje na mlinzi wa Raisi Senga alimsogelea na kumwambia jambo na kumpa ishara ya ndio na kisha akatoka na muda uleule aliingia Afande Maeda .
“Afande Kuna nini?”Aliuliza Afande Tozo na Afande Maeda ambaye hakuwa kwenye Kombati za jeshi alitoa salamu kwa maafande kwa kukakamaa mwili bila sauluti na baada ya salamu yake kuitikiwa aligeuza macho yake yenye wasiwasi upande wa Roma.
“Jana usiku tumepokea taarifa ya kifo cha Aloni Sauli Shabibu kutoka kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa”Aliongea na kufanya watu wote akiwemo Roma kuwa katika hali ya mshangao, lakini aliendelea kuelezea namna ya kifo hicho kilivyotokea na matokeo ya uchunguzi wa Awali na kwa maelezo yake ni kwamba kifo hicho kimetokea nje ya hoteli ya Pink Lady katika maegesho ya magari na mtu alieonekana kufanya hivyo ni Mr Roma Ramoni kwa staili ileile ambayo alimuua Haruni , yaani kupasuliwa kichwa kama tikiti.
Akaendelea kusema uchunguzi wa awali umethibitisha alama za vidole ni za Roma Ramoni bila ubishi na akaenda mbali kusema habari hio imeweza kumfikia baba yake Aloni yaani Shabibu ambaye ni kaka wa Afande Razaq na huenda ndio sababu ambayo imemfanya kukubali kuungana na Raisi wa Zanzibar kuwapa ushirikiano Raia.
Roma alijikuta akishangaa sana na haikuwa kwake tu kila mmoja hapo ndani alimgeukia yeye mwenyewe na kumwangalia kwa macho makali mno , upande wa Afande Kweka na yeye alimwangalia Roma kwa wasiwasi mkubwa , waliamini ndio wanaongea kumaliza tatizo lakini ndio mwanzo wa tatizo lingine.
ITAENDELEA.