Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
SEHEMU YA 542.

Yule mjumbe mara baada ya kukubaliana na Roma aliamua kuondoka , huku mpango ukiwa ni kesho kurudi kumwangalia Rose kama bado yupo ili amchukue na kumpeleka katika jamii za kijini kulingana na sheria.

“Hubby unapanga kweli kunipeleka nje ya nchi?”Aliuliza Rose kwa wasiwasi.

“Sina mpango wa kukupeleka nje , nimemtega tu nina mpango nauwazia kichwani”Aliongea Roma na kumfanya Rose kutabasamu baada ya kuona kumbe Roma hakuwa siriasi , hakuwa tayari kwenda kuishi nje ya nchi na kukaa mbali na Roma..

“Kwasasa usiwaze sana kuhusu hili, hebu turudi kuna mtu nikaonane nae”Aliongea Roma na Rose alikubali na wote walirudi na wakati Rose akielekea ndani Roma alimsogelea Raisi jeremy ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka.

“Nadhani uliniambia wewe mwenyewe kama huna mpango wa kumtambua Edna kama mtoto wako?”

“Ni kweli nimesema hivyo , lakini siwezi kubadilisha ukweli kwa maneno , Edna damu yake ni damu yangu “

“Acha kuwa mnafiki na sitaki kukuona karibbu na Edna, kwasasa ni mke wangu na huna haki ya kumsogelea kwasababu ulishamtelekeza , kama kweli ulikuwa ukijitambua kama baba usingekwepa majukumu yako”

“Mr Roma najua kwamba una uwezo mkubwa na una nguvu lakini huwezi kunipangia maamuzi juu ya mtoto wangu na isitoshe taifa langu halikuogopi , eti tu kwasababu una nguvu”Aliongea Raisi Jeremy.

“Unaonekana kujiamini kwasababu umezingirwa na hawa watu , lakini nikwambie ukinichokoza naweza kufanya chochote kile juu yako”Aliongea Roma.

“Kijana unaonekana kuwa imara sana na mwenye ujuzi na umebahatika kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za mbingu na ardhi lakini usiwe na kiburi , mke wako anaweza kuwa mke wako , lakini bado haiondoi ukweli kwamba nyumbani kwao ni Rwanda , Ni kweli Jeremy hapa alifanya makosa lakini sisi jamii ya PANAS tunamsapoti kwenye maamuzi yake, kama unajiona kwamba una uwezo hata sisi tunao pia”Aliongea kibabe na kumfanya Roma kuanza kupatwa na hasira, mawazo yake aliona labda angekuwa na urafiki na jamii hio lakini kwa namna ambavyo hali ilivyo aliona kabisa ni tofauti na alivyofikiria.

Alitamani kuita chungu chake palalepale kiwameze na kuwageuza vidonge vya kijini, lakini hakutaka kufanya jambo lolote kwa muda huo ,kwani hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jamii hio ya kijini na kubwa zaidi alihofia wanaweza kuwa na mbinu kubwa kuliko yeye kutokana na zile tetesi kwamba mbinu yake ya kimaandiko asili yake ni kutoka katika jamii hio.

Ukweli ni kwamba Roma baada ya kuwaangalia watu hao aliona kabisa walikuwa na mitazamo tofauti kabisa na ile ya watu wa China , hawa kidogo walionekana kustaarabika hata katika mavazi yao na alijiambia huenda anachosikia kuhusu jamii hio ni kweli.

Roma alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira na kujituliza , kwa wakati huo aliona kabisa uwezo wake bado ni mdogo kutengeneza maadui wengi wa jamii zisizoonekana hivyo aliamua kuwa mpole

“Nikutahadharishe sijui unachopanga katika akili yako , lakini ni vyema kama nia yako ya kumtambua Edna kama mwanao ni ya dhati la sivyo sitojali ni nguvu gani inayokusapoti , nitahakikisha nakuua”Aliongea Roma na hapo hapo aliingia ndani ya geti la nyuma yake akiwaacha wakiondoka.

“Inatia wasiwasi sana kwa kijana mdogo kama huyu kuwa na uwezo mkubwa wa aina hio , jamii yetu ilikuwa ikimwangalia kwa umakini lakini kwasasa wasiwasi wao juu yake ni mkubwa zaidi “Aliongea yule bwana.

“Mkuu Geni , je hakuna uwezekano wa kuwatumia wakubwa zenu kumdhibiti , nadhani akiendelea kuwa na kiburi hivi mipango yetu haitoenda vizuri kama tulivyopanga”

“Mhmp! , Jeremy hakika wewe ni katili , licha ya yote hupaswi kuongea hivyo kwani bado ni mkwe wako”

“Sina shaka yeye akiendelea kuishi na kuwa mkwe wangu , tatizo ninalohofia ni uwezo wake , unazidi kuwa tishio kwa kila ninachokiwazia na mipango yenu”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , hawezi kuzuia kile tunachopanga kwani lazima kitokee hata kama tusifanye chochote , tunachofanya sasa hivi ni kujiandaa kwa kuweka mazingira sawa ili pale tu fursa itakapojitokeza isitupite”Aliongea bwana alieitwa Geni.

“Mkuu Geni mpaka sasa siamini yale maneno , kama kweli huu utabiri ukatimia kama ulivyosema nashindwa kutabiri nini kitatokea kwa bara lote la Afrika”

“Kama kila kitu kitaenda sawa ndani ya mipango yetu ,Rwanda itakuwa nchi kubwa ki uchumi na katika maendeleo ya teknolojia, kwa nchi nyingine ambazo hazijaweka msingi mzuri lazima watapitia awamu ya pili ya ukoloni wa jamii zote zenye ngozi nyeupe”

“Hiko ndio kinanichanganya zaidi , ukoloni wa mara ya pili?”

“Huna haja ya kuwaza hilo Jeremy , ukiwa mbele ya muda siku zote utakuwa mshindi , ukoloni wa mara ya pili utakaotokea katika bara la Afrika ni ule uliondelea”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuwa katika kimya kidogo kusharabu maneno yake.

“Roma hakuna kitu kibaya kilichotokea wakati wa mauzngumzo yako na Jeremy?”Aliuliza Blandina aliekuwa akionyesha wasiwasi .

“Niliwapa onyo tu kwa kuwatahadharisha kama wana mpngo wenye nia ovu juu ya Edna sitowaacha salama , kuwa na amani hakuna kibaya kilichotokea”

“Wasiwasi wangu ni kwa mkeo nina miaka nusu karne sasa , lakini nashindwa kujua ni kipi ambacho anafikiria”Aliongea na kumfanya hata Roma kujicheka yeye mwenyewe maana haikuwa kwa mama yake tu ,, hata yeye mwenyewe hakuwa akifahamu Edna kile ambacho anafikiria kabisa na mara nyingi aliishia kuingia kwenye mitengo yake bila hata ya kufikiria.

Roma alipanda mpaka juu kwenye chumba cha mke wake , ili kumwangalia anaendeleaje mara baada ya kongea na baba yake mzazi,

“Ongea taratibu Lanlan kalala , kuna kitu unachotaka?”Aliongea Edna mara baada ya kufungua mlango.

“Wife uko sawa , kuna chochote cha kuumiza alichokuambia??”Aliuliza Roma kwa wasiwasi, hakujua Edna aliongea nini na baba yake na huo ndio ulikuwa wasiwasi wake.

“Hapana , hajaniambia chochote cha kuumiza”

“Lakini kwanini unaonekana kama haupo sawa?Niambie kama huyu Jeremy kaongea chochote ambacho kimekuudhi nimfuate sasa hivi”

“Nimesema hajaongea chochote kibaya na sitaki kulisikia jina lake tena”Aliongea Edna kwa kuonyesha kukasirika na Roma alishangaa mabadiliko yake mara baada ya kutaja jina la baba yake, lakini Edna palepale alijishutikia

“Nisamehe .. sio kwamba nakukasirikia , najua una wasiwasi na mimi lakini sitaki kuongea chochote kinachomuhusu kwasasa”.

Roma aliona kabisa Edna hakuwa sawa , lakini hakutaka kumlazimisha kuongea kama hataki , hivyo alitoka na kurudi kwenye chumba chake kupumzika

Dakika chache mbele mlango wa chumba chake uligongwa na alionekana Blandina ambaye alikuwa amebeba sahani yanye bakuli ambalo lilitoa mvuke wa harufu wenye kupendeza pua.

“Mama umebeba nini?”

“Nimekutengenezea supu ya kuku , angalau upashe utumbo joto”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na kitendo hicho , siku zote Blandina alikosa cha kumfanyia Roma kutokana tayari ameshakuwa mtu mzima na kila kitu alikuwa akijifanyia mwenyewe.

Roma alichukua bakuli na kisha akachota kidogo kwa kutumia kijiko”

“Mama mbona kuna harufu kama ya dawa kwenye hii supu, umeweka kitu gani?”

“Sio kitu kikubwa Roma , kuna kajimzizi tu nimechanganya ni dawa nzuri zaidi kwa afya ya mwili wako”

Roma mara baada ya kujua supu imewekwa kijimzizi hakutaka kuendelea kunywa tena.

“Mama siiaki hii supu tena , nitakula tu chakula”

“Roma haina tatizo kwako , najua una nguvu lakini dawa kama hizi zinasaidia , niliongea na mpemba mmoja wa dawa za miti shamba na aliniambia ni nzuri zaidi kwa mwanaume anaetegemea watoto”Aliongea Bloandina bila aibu na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio ya mama yake.

“Mama wanaume wengine ndio wanaopaswa kuwekewa mizizi mimi sihitaji na nishakuambia siwezi kupata mtoto kwa uwezo wangu huu hata kama nitumie miti shamba ya aina zote”

“Najua lakini Rose si tayari ashapanda panda levo na pia anaendelea kupanda , naamini anaweza kuwa mtu sahihi kukupatia mtoto”Roma alishangazwa na kauli ya mama yake , ndio maana tokea juzi muda wote habari za Rose hazikuwa zikiisha kumbe furaha yote ilikuwa kwenye swala la kupata mjukuu.

“Mama ni kweli amepanda levo , lakini bado hayupo na spidi niliokuwa nayo mimi , tayari yupo kwenye levo ya Nafsi na mimi nakaribia mwisho wa levo ya kuipita dhiki , bado nafasi ya yeye kubeba ujauzito wangu ni ndogo”

“Lakini bado nafasi yake ni kubwa kama utamlinganisha na Edna”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa , hakutegemea mama yake kumlinganisha Edna na Rose.

“Mama kwanini unasema hivyo , swala la mafunzo linategemea vitu vingi , Edna ni kweli bado yupo chini lakini siwezi kumfosi kupanda levo kwa haraka na pia siwezi kumpendelea Rose kwasababu kapanda levo kuliko wengine”

“Najua na sitaki kuwa na upendeleo lakini tabia na matendo ya Edna juu yako mimi sikubaliani nayo kwani hayasaidii kitu, nimekuona ulivyotoka kwenye chumba chake ukiwa umenyongea”

“Kwahio ulisikia kila kitu?”

“Sijasikia chochote , lakini mwonekano wako unaongea kila kitu , Kama angalau anatimiza wajibu wake kama mke nisingekuwa na wasiwasi lakini kwanini mpaka sasa mnalala vyumba tofauti , bado nafasi yake ya kupata ujauzito ni ndogo lakini bado anajitenga na wewe , kila nikifikiria swala hili najikuta nakasirika , unapendwa na wasichana wengi wazuri lakini kwanini kuwa na mke ambaye ana akili za kitoto , ashaolewa sasa na anapaswa kufanya kila kitu kulingana na familia, Roma wewe ndio unaekwenda kuendeleza ukoo wa familia na Edna anapaswa kusaidia katika hilo , sitarajii makubwa kutoka kwake lakini angalau aonyeshe matendo ambayo yanaashiria mapenzi kwako”

“Mama haipo hivyo , uadhani wewe mwenyewe unaifahamu tabia ya Edna , ananijali sana lakini kwasababu ya Lanlan sioni kama ni tatizo sisi kuwa hivi na isitoshe hili linarahisisha pia , kwani nina uwezo wa kutoka muda ninaotaka na kuwafanya wengine wasione kama sitimizi wajibu wangu , kuhusu mtoto sidhani kama kuna haja ya kuharakisha”

“Bado tu unamkingia kifgua hata kwenye swala muhimu kama hili, ni mantiki kwake kupata mtoto kwanza kuliko wengine la sivyo mambo hayawezi kuwa mepesi hapo baadae , unafikiri kama wengine wakifanikiwa kupata mtoto, ni yupi utaanza kumjali, mama wa mtoto au mkeo?, sidhani kama mkeo angekuwa Amina , Rose , Dorisi au Nasra wangekubali kulala tofauti na wewe , angalia sasa mtoto wa kuasili anamfanya kutotimiza majukumu yake”

“Mama ni kosa kusema hivyo , Lanlan anaweza kweli ni wa kuasili , lakini kwangu mimi ni binti yangu kabisa , ni mtoto wetu wa kwanza na hilo haliwezi kubadilisha kitu”.

“Sawa hata mimi namuona Lanlan kuwa mtoto mzuri na pia nampenda kama mjukuu wangu lakini tatizo ni msichana na hana damu ya ukoo wenu , babu yako na yeye hana muda mwingi wa kuishi duniani , je unataka atangulie mbele za haki bila kuona mjukuu wake wa kiume”Aliongea na kumfanya Roma ashangae , hakuelewa mama yake tangu lini akaanza kumjali mzee kweka.

“Mama nimekuelewa na pia najua wasiwasi wako , kwanzia leo nitahakikisha wanajifunza kwa spidi ili kupanda levo kwa kasi”

“Roma najua unampenda Edna kuliko wengine wote na mimi kama mama yako najitahidi kumkubali , lakini unatakiwa kuelewa wamama wote ni wabinafsi, Edna ni mkwe wangu, lakini wewe ni mtoto wangu wa kiume , siwezi kuona mwanamke mwingine anakuendesha anavyotaka,inaniuma mimi kama mama yako , una uwezo mkubwa na unapendwa na wanawake wengi , kwanini Edna anakuwa udhaifu wako, kuna siri gani ambayo siijui?”

“Mama usiende mbali sana , nitaongea na Edna na tutayaweka sawa”Aliongea Roma akijaribu kumtuliza maana ilionyesha alikuwa na dukuduku la muda mrefu , pengine kujenga ukaribu na michepuko yake alianza kuona walikua na sifa zaidi za kuwa mke kuliko Edna.

Roma mara baada ya mama yake kutoka , aliona ngoja ataongea na Edna ili kujua namna ya kuishi kama mke na mume zaidi na kuacha kuibua maswali.





SEHEMU YA 543.

Kwasababu alikuwa na kazi ya kudili na mjumbe wa Hongmeng, hakutaka kwanza kudili na mambo yake ya nyumbani ya kuongea na Edna , bali kulivyokucha asubuhi moja kwa moja alienda kazini.

Ilimfurahisha kucheza gemu , kuperuzi kwenye mitandao na kuangalia taarifa za habari akiwa kazini , kwake hakuwa akifika kazini bali alifika kupumzika na muda ukiisha atarudi nyumbani.

Siku hio asubuhi wakati anafika ofisini alishangaa kumkuta Kassimu binadamu yake eneo la maegesho ya magari na alivyomuuliza alikuwa akifanya nini hapo alimwambia amekodisha floor ya nne kwani anafungua kampuni ya maswala ya kuchezesha magemu online.

Roma baada ya kusikia taarifa hio hakushangaa sana kwa Kasimu kukodi sehemu ya jengo hilo kwa ajili ya kufanya biashara ya kuchezesha mage,mu , baba yake Tajiri Azizi alikuwa moja wapo ya matajiri wenye pesa nyingi hivyo ilikuwa sawa kwa Kasiimu kuwa na pesa za kumudu kodi.

Roma alijaribbu kumuulizia Kasimu habari za Donyi na aliambiwa anafanya kazi katika kampiuni ya mama yake katika idara ya ubunifu.

Roma alijikuta akimkumbuka Neema luwazo kwani tokea atoke Korea hawakuwa wameonana, Neema luwazo hakuwa na utofauti na Edna tu wote walikuwa wakipenda kujiweka bize na maswala yao ya kibiashara kuliko kitu chochote kile na hiko kilimfanya kushindwa kupanda muda wa kuwa nao karibu, hususani kwa Neema ambaye alimisi mapenzi ya kiutu uzima.

Ni wakati wa usiku wakati wanafamilia wote wakipata chakula,Blandina ndio ambaye alikuwa ametawala maongezi na muda wote alikuwa akizungumza habari zilizotokea mchana mara baada ya kukutana na mama yake Mage.

Siku hio mchana Roma na mama yake waliweza kushiriki kwa pamoja siku ya kuzaliwa ya Mama T ambaye alikuwa akitimiza miaka arobaini , sasa sherehe hio ilimfanya Blandina kujenga sana ukaribu na mama yake Mage kiasi kwamba waliahidiana mengi na upande wa Mama Mage alijitahidi kumpamba Blandina ili kumpigia debe mtoto wake Mage.

Sasa yale yote yaliokuwa yametokea katika sherehe hio Blandina alikuwa akimhadhithia Bi wema na hali ilio ilimfanya Roma kuona si vizuri kuongea mbele ya Edna, hususani namna ambavyo alikuwa akimsifia Mama T kuwa mtu mzuri sana.

Upande wa Edna hakuwa na taarifa juu ya Blandina na Roma kwenda kushiriki sherehe hio , ukweli ni kwamba Roma alipokuwa yupo kazini aliweza kufuatwa na Mage na kumwambia mama yake anataka ashiriki pia katika sherehe yake ya kuzaliwa na kwasababu ilikuwa ni ghafla sana Roma alikosa muda wa kumtaarifu Edna.,

Hali hio ya Blandina kumsifia Mama T ilimfanya Edna kujihisi mnyonge , lakini pia kwa wakati mmoja kumkumbuka mama yake mzazi, alikuwa akimtegemea mama mkwe wake kuwa kama mbadala wa mzazi wake lakini kinachoendelea hapo ndani ni tofauti na matarajio yake.

“Mama usiongee sana unaonaje ukiweka umakini kwenye kula , utamfanya Edna amkumbuke mama yake”Aliongea Roma baada ya kuona mama yake amepitiliza na Blandina alimwangalia Edna na kumiona akionekana mwenye huzuni.

“Edna nisamehe , sikumaanisha kukufanya mwenye huzuni , usiwe na hasira na mimi, sawa?”

“Usiwe na wasiwasi mama , niko sawa sikukasirikii kumsifia Mama T , hata mimi najua ni mtu mzuri”Aliongea Edna ambaye alikuwa akila chakula kama akilazimishwa.

“Kama ni hivyo hakuna tatizo …”Alijibu na kisha akalazimisha tabasamu na kukaa kimya , hali ya hewa ilionekana kubadilika ghafla na kuwa ya baridi kutoka na kwamba hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuanzisha maongezi, ambaye hakuwa na wasiwasi na kujali kile kinachoendelea ni Lanlan peke yake kwani hakuwa akiifahamu vizuri lugha ya kiswahili.

Roma aliekuwa akifikiria mbinu ya kurudisha hali ya hewa kuwa ya kawaida alijikuta akikunja sura mara baada ya kuhisi msisimko wa nguvu ya kijini ikikaribia nyumba yake, palepale alijua aliefika hapo alikuwa ni mjumbe kutoka Hongmeng, lakini hata hivyo Roma alikuwa na mpango wake kichwani tokea mchana.

Njia pekee ambayo aliamini ingeweza kumbakisha Rose Tanzania nikutoa hongo , alijuwa watu kutoka Hongmeng huendeshwa na tamaa ya vidonge vya daraja la kwanza vya kijini hivyo kama angempa Hongo Mjumbe huyo basi angepiga kimya kuhusu Rose na kumuacha aendelee kubakia Tanzania.

Roma mara baada ya kutoka nje kuonana nae , alimkuta akiwa amekasirika mno na Roma alitegemea hilo lakini hakujali zaidi ya kuanza mauznumzo nae juu ya uwepo wa vidonge ambavyo vingemsaidia kupanda levo kwa haraka.

Bwana yule mara baada ya kuonyeshwa vidonge hivyo alijikuta akishangaaa na kujiuliza imekuwaje Roma akawa na vidonge hivyo na Roma hakutaka kumpa siri yake , lakini alimhamkikishia kwamba kama angefumbia macho swala la Rose basi angempatia kidonge kimoja cha daraja la juu na viwili vya daraja la kati.

Roma sio kwamba alikuwa akiogopa kupigana nae , alichokuwa akihofia kama atamuua na mjumbe huyo mwingine wa Hongmeng basi angejitengenezea tatizo ambalo angeshindwa kulitatua kwa kipindi hicho ambacho alihitaji kuweka umakini kwenye kufunza warembo wake kupanda levo, lakini na yeye pia kujiimarisha zaidi.

Ijapokuwa mwanzo Balozi huyu wa Hongmeng kujifanyisha mgumu wa kukataa Rushwa lakini mwisho wa siku alikuwa na udhaifu uleule tu ambao binadamu wa kawaida wanao , hivyo Roma alifanikisha kumhonga vidonge na Balozi kumuhakikishia kwamba hakuna mtu kutoka Hongmeng ambaye atajua uwepo wa Rose nchini Tanzania.

Baada ya Roma kukamilisha swala hilo alienda kwa Rose na kumpa taarifa juu ya kumtafutia suluhisho la muda la kuendelea kukaa nchini , ndio lilikuwa suluhisho la muda kwani aliamini siku zijazo lazima Rose atafahamika na huenda sio Rose tu , kwasababu wengine wote walikuwa wakijifunza basi wangefikia katika levo ya nafsi na kuanza kuandamwa.

Roma mara baada ya kumweleza Rose jambo hilo na kuona amefurahi alirudi nyumbani , Blandina na Qiang Xi walikaa kwenye runinga kangalia tamthilia na Edna yeye alikuwa bize kumsaidia Lanlan kukamilisha Homework yake aliopewa shuleni.

Roma alijiunga nao , ijapokuwa Lanlan kwenye mwandiko alikuwa vibaya sana , lakini alikuwa na uelewa wa juu sana hivyo haikumpa shida kwenye kumuelekeza baadhi ya mambo.

Lanlan alikuwa na uwezo mkubwa lakini alikuwa na tabia ya uvivu na hakuwa anapendelea kabisa kufanyia kazi anazopewa shuleni na ni mpaka alazimishwe na hilo ndio jambo pekee ambalo lilimfanya Roma asione ni wakati nzuri wa kumfundisha mbinu za kijini , kwani akili yake bado haikuwa imetulia na alikuwa ni mtoto mwenye mambo mengi na kama angemfudisha asingepata faida zaidi ya kumuweka kwenye hatari.

Roma aliangalia namna Lanlan alivokuwa akiumba herufi, zilikuwa kubwa mno kama vile ni vikatuni na aljikuta akijichekea , hata yeye mwenyewe alikuwa na mwandiko mbaya hivyo hakumshangaa sana Lanlan , lakini kwa Edna alipatwa na wasiwasi na kujiambia sku za baadae Lanlan ataandika sana kwa kuchapa kuliko kuandika kwa mkono.

Roma baada ya kukaa hapo kwa dakika kadhaa , alimpa ishara Edna kumfuata mpaka juu kwenye Lounge ili kuongea na Edna alishangaa na kujiuliza Roma anataka kuongea nini , lakini aliishia kufuata hadi juu na kumwachia Qang Xi kazi ya kuendelea kumsaidia Lanlan kumalizia homework yake.

“Kuna kitu gani unachotaka kuongea?”Aliuliza Edna na Roma aliamua kumwelezea Edna juu ya malalamishi ya mama yake , alijitahidi kuweka maneno yake namna ambavyo hayamkwazi Edna bali kumuelewesha.

“Usimlaumu sana mama , ushakuwa mama tayari lazima utakuwa unajua hisia ambazo wazazi hupitia , mimi sina tatizo na najua wewe ni mwenye hasira za haraka, lakini mama anachotaka ni sisi kuishi kama mume na mke”Aliongea Roma na Edna alionyesha kuelewa na aliishia kung’ata lipsi zake.

“Nimekuelewa, nitamfudisha Lanlan kulala peke , nipe angalau hata wiki moja na baada ya hapo tutaanza kulala chumba kimoja”

“Ni sawa kufanya hivyo lakini usione kama nalazimisha tulale pamoja , na isitoshe nina furaha na huu utaratibu”

“Najua ndio unafuraha , unajua kabisa kulala na mimi itakuwia ngumu kutoka nje usiku kulala na wanawake wako wengine , unafikiri sijui kuhusu hilo , nadhani utaratibu anaotaka hauwezi kukupa furaha ya moja kwa moja, mimi sina tatizo kama unataka rulale pamoja , kwani tayari sisi ni mume na mke”

“Edna nadhani swala analozungumzia mama zaidi sio kuhusu kulala pamoja tu, babe Edna anachomaanisha ni wewe angalau kuwa mpole na mnyenyekevu unapoongea na mimi na kunijali anapokuwa mbele yetu, nadhani ndio namna ya kumfanya kuwa na furaha na atakupenda zaidi”Aliongea na kumfanya Edna kukosa furaha.

“Najua nina madhaifu katika sehemu nyingi kama mke lakini hata kama nije kuwa mpole na mnyenyekevu mbele yako sifanyi kwasababu ya mama , wewe unadhani ni sawa mimi kuigiza kukujali?”

“Hicho sio ninachomaanisha , ninachotaka ni wewe na mama kuwa na mahusiano mazuri , yeye ndio mama yangu wa pekee na wewe ni mke wangu , sio sawa mimi kuwasaidia kuelewana, na kati yenu siwezi kuwalinganisha kwani wote nyie ni muhimu kwangu , Najua mama anakupenda lakini kuna vitu hamvimridhishi hivyo angalau wewe nifanyie unachotaka tukiwa wenyewe lakini mbele yake jaribu kuwa makini”Aliongea na kumfanya Edna kujisikia vibaya ila aliona ana pointi.

“Honey , je nimekuwa mjinga kiasi kwamba imekufanya kuwa na wasiwasi juu ya haya yote kwa ajili yangu..”

“Usichukulie hivyo , isitoshe mimi ndio nakufanya uwe na hasira za mara kwa mara kwani matendo yangu hayaridhishi , wasiwasi wangu ni furaha ya nyumba kupotea na mimi hii ni kazi ngumu sana kwangu kuifanya kuliko kuua , hivyo mke wangu naomba unisaidie katika hili, sawa babe?”Aliongea Roma kwa tabasamu huku akibembeleza.

“Kwanini kila mtu anaona labda na kuchukulia kama sehemu ya kutolea hasira zangu , lakini kila kitu kipo wazi wewe ndio mchokozi..”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu na kumfanya Roma kujikuta akipata ahueni.

*****

Siku iliofuata baada ya Roma kufika kazini , alitakiwa kwenda kuhudhuria kikao na idara ya uhusiano na masoko makao makuu ya kampuni ya Vexto.

Baada ya kuendesha gari mpaka katika jengo hilo alishangazwa kuona kuna watu wanaume kwa wanawake waliokuwa wameshikilia mabango nje ya jengo hilo , na kwa macho yake ya haraka alijua ni watu ambao walikuwa wakifanya mgomo.

Hawakuwa watu wengi hivyo haikusababisha barabara kuwa na msongamano na hata wau hawakuwajali , lakini upande wa Roma alipatwa na wasiwasi na palepale alitoa simu na kumpigia Edna.

“What is it Mr Roma Ramoni..”Sauti upande wa pili ya Edna ilisikika na kwa kauli hio alijua tu lazima atakuwa kwenye kikao .

“Nini kimetokea , mbona naona kuna watu wapo chini ya jengo wakiwa na mabango ya shinikizo na wanapiga makelele?”Aliuliza Roma na Edna alikaa kimya kidogo kabla ya kijibu.

“Usiwajali , acha wapige makelele wakavyo wakichoka wataondoka, hata hivyo hali ya hewa kwasasa ni ya mvua sidhani kama watadumu muda mrefu”Aliongea Edna kikauzu na baada ya kumaliza kauli yake alikata simu.

Roma alijikuta akipata mamivu ya kichwa kwani ni jana usiku tu alikuwa akimwambia aonyeshe upole na unyenyekevu wakati wakuongea nae , lakini asubuhi hio matokeo yalikuwa tofauti.

Roma aliamini mtu pekee ambaye anaweza kumpatia majibu ni Daudi, aliamini lazima atakuwa akifahamu kinachoendelea katika makao makuu ya kampuni , hivyo baada ya kurudi katika kampuni yake alimwita ofisini.

“Director didn’t president tell you anything Aren’t you husband and wife?”Aliongea Daudi kwa kingereza akimaanisha je Edna hakumweleza , kwani wao si mume na mke.

“Upuuzi , ningekuuliza kama najua kinachoendelea?”Aliongea Roma huku akiona kidogo aibu kwani Daudi alikuwa na maana , ila asichokijua tu ni kwamba Edna hakuwa akimshirikisha mtu maswala yake ya kibiashara na Roma hakujali maswala ya kushirikishwa pia.









SEHEMU YA 544.

Uapnde wa Daudi alionekana kupatwa na aibu kidogo kuuliza maswali ambayo hayakuwa ya msingi.

“Mkurugenzi hao ni waajiriwa wa kampuni ya maduka ya Beseli(Beseli department store) , wanafanya maandamano baada ya kuona kampuni ya Vexto imenunua kampuni yao kwa njia zisizo halali”

“Beseli Department Store , sijawahi kuisikia?”

“Ndio mkurugenzi , Beseli ni kampuni ya muda mrefu sana iliojikita ndani ya Tanzania, mwanzilishi wake , Mzee Kakolanya pia ni mjasiriamali aliejijengea jina kwa muda mrefu , katika miaka ya hivi karibuni CEO Edna alikuwa akijipanua zaidi na zaidi kibiashara na karibia asilimia hamsini ya Department Store(Maduka makubwa) zote znazopatikana katika eneo la Kibaha zipo chini ya menejimeni ya kampuni ya Vexto, mpango wa kampuni ya Vexto ni kubadilisha mpangilio wa kibiashara katika eneo la Kibaha kwa wa kisasa ili kuvutia zaidi wapangaji katika eneo la Mji wa kisasa , lakini kampuni ya Beseli ambayo inaendesha asilimia sabini ya biashara zake katika wilaya ya kibaha walikuwa wakileta ugumu kuchukuliwa na kampuni ya Vexto , sio tu jina la kampuni yao lakini pia eneo la ardhi katika biashara yao hawapo tayari kuuza , kampuni ya Beseli inalenga wateja wa chini zaidi katika maswala ya fasheni na vyakula lakini staili yao ya kibiashara haiendani na mikakati ya kampuni ya Vexto katika kubadilisha mwonekano wa mji hivyo licha ya viongozi wa kampuni kujaribu kumshawishi Mzee Kakolanya kuuza biashara yake na eneo lote kwa bei kubwa mbali na thamanni ya kampuni yake licha ya kuendesha biashara kwa hasara na kuwa na madeni mengi lakini aligoma”

“Kama ni hivyo kwanini wafanyakazi hawa wanafanya maandamano nje ya jengo la kampuni?”

“Kwanzia wiki iliopita kulizuka taarifa mitandaoni na katika vyombo vya habari juu ya kampuni ya Beseli kuuza bidhaa feki kwa bei ya bidhaa orijino ,Mzee Kakolanya alipandwa na ghadhabu mno kwani taarifa hio ilikuwa na athari kubwa kwa kampuni,

Benki nao walianza kuharakisha Beseli kulipa deni wanalodaiwa au wakubali kuuza hatimiliki kwenda kampuni ya Vexto , hivyo Mzee Kakolanya anaamini Edna ndio ambaye alihonga vyombo vya habari pamoja na watu wa mitandao kuchafua jina la kampuni yake, hivyo wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hio walishawishiwa na Mzee Kakolanya kufanya maandamano mbele ya kampuni ya Vexto”Aliongea Daudi na sasa Roma aliweza kuelewa tatizo lote , lakini bado ilikuwa ngumu kwake kuamini juu ya swala hilo kama kampuni ya Vexto imehusika.

Lakini Roma bado alikuwa na mashaka , alikuwa akijua staili ya kuendesha biashara kwa Edna na muda mwingine anachukua hatua za kikatili zaidi.

“Daudi , je unaamini kampuni ya Vexto imewahonga watu na vituo vya habari kutoa taarifa ya uzushi?”

“Kama nitakuwa mkweli kwako Mkurugenzi naamini hili ni swala ambalo kampuni ya Vexto inahusika ukiangalia na mpango wa muda mrefu wa kutaka kuinunua kampini hio ya Beseli , ninaweza kusema kilichofanyika ni kuhonga wanahabari ili kuzusha taarifa hizo na wakati huo huo benki iliwalazimisha kulipa deni ambalo lilikuwa kubwa kutokana na malimbikizi , hivyo Beseli mwisho wa siku itabakiwa na chaguzi mbili , aidha wajitutumue kulipa deni ambalo hawana uwezo nalo au wakubali kuuza kampuni yao kwa Vexto”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba mke wangu anawanyanyasa wengine si ndio?”

“Mkurugenzi usinifikirie vibaya , lakini biashara ni vita na siku zote mwanajeshi hawezi kuacha kufanya njia za mikato kupata ushindi , kama ni mpango wa Boss Edna basi nitasapoti maamuzi yake”

“Okey nimekuelewa , unaweza sasa kuondoka”Aliongea Roma na Daudi alitoka kwenye ofisi ya Roma.

********

Katika siku chache zilizofuata Edna alifanikisha kumlazimisha Lanlan kulala katika chumba chake na yeye akahamia katika chumba cha Roma.

Blandina mara baada ya kuona wanalala pamoja , alijikuta sasa akiridhika na tabasamu kwenye uso wake kila alipokuwa akiongea na Edna liliongezeka maradufu.

Blandina alionekana na yeye kuanza kuzeeka vibaya , kwani mara nyingi alikuwa akikaribisha marafiki zake nyumbani na kupiga soga muda mrefu na hata kucheza karata.

Edna kila alipokuwa akirudi kutoka kazini aliweza kukutana na kundi la wanawake wakiwa eneo la sebuleni wakipiga makelele na kugongesheana viganja , kutokana na tabia yake ya kupenda utulivu na maisha ya kujitenga hakufurahishwa na ustaarabu wa mama mkwe wake , lakini aliishia kuvumilia na kuhakikisha kila wanapoongea anajitahidi kuonyesha tabasamu kwa kadri awezavyo.

Muda wa usiku katika chumba chao , Roma hakutaka kupoteza fursa hata siku moja, alikiwasha kila siku na kilichosikika ni milio ya Edna kuomba apumzishwe, lakini Roma hakusikiliza hoja yake na isitoshe mke wake huyo hakuwa na uwezo wa kwenda raundi ya pili..

Hiki kipande kitaendelea …Subiri uone kiakachotokea wataachana tu.







SEHEMU YA 544B

Sheria moja tu ambayo Roma aliwekewa na mke wake ni kwamba hakuna kurudia mara mbili na Roma kwasababu alikuwa akimsikiliza Edna kwa kila anachomwambia alikubali.

Lakini sasa upande wake alihakikisha hio mara moja inakuwa kama ni mara tatu kwa mtu wa kawaida.

Muda huo wa usiku kilikuwa ni kilio kwake , Roma aliekuwa amemlalia kwa juu hakumpa nafasi ya kusogea hata nchi moja, Edna hakujua hata kinachoendelea katia mazingira yanayomzunguka , lakini kwa muda huo ni kama vile yupo juu kileleni mawinguni.mwanaume wake alikuwa na nguvu kiasi kwamba alimfanya kupanda mlima na kushuka mara nyingi iwezakanavyo na kumfanya kila kiungo cha mwili wake kama vile kimepalalaizi.

Ni zaidi ya lisaa limoja na nusu tokea amwingine mkewe , lakini bado alijihisi yupo mbali kabisa kumaliza , alijua hakuwa wa kawaida lakinni alijitahidi kupunguza muda ili isije kutokea mke wake kuchoka haraka kabla ya yeye mwenyewe kumaliza , ukizingatia kulikuwa na mashariti hivyo alitumia akili kwenye kuridhisha mwili wake.

“Huwezi hata kupumzika siku moja ,hiki kitendo unakipenda sana?”Edna alilalamika huku akihema kama mbwa mara baada ya Roma kumwachia.

“Mpenzi , kwanini unaongea kama vile wewe huhusiki isitoshe sijapanda mlima kama ilivyokuwa kwako”

“Hapana usiongee…kwanini huna aibu kuongea mambo hayo”Aliongea Edna huku akiona aibu kama mtoto wa darasa la saba na kumfanya Roma ampige kibao kiwili wili cha chini.

“Mama amesema unatakiwa kuweka juhudi kupata ujauzito wa mtoto wetu wa kwanza ,hapa si ndio nakusaidia?”

“Lakini hata kama sio jambo ninaloweza kuamua na isitoshe kama nni mtoto ninae tayari”

“Wazee wetu wa familia wanataka wajukuu wengi , hivyo unapaswa kuelewa hisia zao”

“Kama nitaendelea kujali kile wanachojisikia , vipi kuhusu mimi?”.

“Unamaanisha nini kuhusu wewe?”Aliuliza Roma alieashangazwa na kauli yake.

“Honey , tutafute muda tuongee na mama kualika watu wengi wa uswahilini kujaa hapa nyumbani , wale mashangazi wana sauti kubwa mno na hawana hata ustaarabu kwenye kuongea, nashangaa kwanini mama ametengenza nao urafiki”

“Mama anajisikia vibaya kukaa mwenyewe muda wote na isitoshe maisha yake karibia yote yalikuwa ni yeye mwenyewe , kwanini tusimuache afanye anachotaka?”

“Kama nni hivyo angalau atafute watu wastaarabu kwa mfano maa yake Nasra hana shida , lakini wale wengine siwajui hata wanatokea wapi “

“Kama ni hivyo kwanini kama vile unataka miimi ndio niongee nae , kwanini usimfate na kumwambia kistaarabu wewe mwenyewe , isitoshe sisi ni wanafamilia na mama amestaarabika”

“Ninaogopa nitamfanya awe na hasira na mimi , siku za hivi karibuni amekuwa akinijali , lakini kama hutaki kunisaidia sahau kama nimeomba”Roma kuona mke wake anaomba kwa sauti ya kubembeleza alishindwa kumkatalia , ijapokuwa aliona sio jambo zuri yeye kuingilia , lakini anapaswa kufanya.

Siku iliofuata katika meza , wanafamilia wakiwa wanajipatia kifungua kinywa Roma aliona aweke wazi dukuduku la Edna mbele ya mama yake apate kulisikia.

“Mama , je unaweza kunisaidia kitu?”Aliongea Roma baada ya kufikiria gia ya kuanza nayo.

“Kitu gani unataka nikusaidie , unafikiria nini wewe toto korofi”Aliongea Blandina kwa furaha.

“Sio jambo kubwa , ni kwamba umekuwa ukialika watu kuja nyumbani kupiga soga na hata kucheza karata , nadhani sio jambo zuri kwa Lanlan, unaonaje ukiacha kuwaita?”Aliongea Roma.

Blandina ambaye alikuwa akibandua maganda ya yai la kuchemsha ailiweka chini ya sahani na tabasamu ambalo lipo kwenye uso wake lilipotea palepale .

“Roma mwanangu , je inakufanya ujisikie vibaya mimi mama yako kualika hao wanawake kuja hapa nyumbani?”

“Sijamaanisha hivyo, Mama yake Nasra yupo pia , siwwezi kusema ni jambo la aibu kwangu”Alijitetea na kummfanya Blandina kutoa tabasamu hafifu na kisha kugeuza macho yake kwa Edna .

“Najua likija swala la kustaarabika tabia na mengineyo wale wamama hawakufikii kwani hawajasoma kama ilivyo kwakko , hawajui hata taratibu za familia zenye kipato cha juu , labda kwa macho yen nyie watoto wa siku hizi , ni watu wa kupotezewa, lakini katika maisha yangu ndani ya miaka kadhaa iliopita nilijifunza mambo mengi wakati nazunguka katika nchi nyingi za Afrika kufuatilia maendeleo ya vito vya Yatima nilivyovianzisha katika kuomba taisi udhamini wa michango , nishawahi kukutana na aina ya wato wa aina zote , wakati nilipokuwa mdogo hata mimi vilevile niliona wamama kama hao wamekosa ustaarabu kwa namna ambavyo wanaongea kama wanafoka , namna wanavyokunywa vinywaji kama vile ni wanaume na kweli haipendezi kwa mwanamke”Alipozi kidogo na kisha akamwangalia Edna.

“Edna naamini hata wewe pia unawaona kama hawajastaariabika na tabia ao hazivumiliki si ndio?”

Edna ambaye alikwa akipeleka kikombe cha maziwa mdomoni alijikuta akiishia njiani na akikosa ujasiri wa kutoa jibu kwa kutingisha kichwa au kuitikia , lakini kwa Blandina ni kama alijuwa Edna asingemjibu.

“Katika vitu ambavyo nimejifunza , kamautalinganisha wanawake wenzangu ambao wameolewa katika familia za kitajiri na pengine kukulia katika familia hizo na hawa wa mtaani , wale wa kitajiri licha ya kwamba wamestaarabika na pia ni wasomi lakini wengi wao hawana moyo wa kusaidia ni kama sio binadamu na hili limenifanya niwachoke mno, wakati nikikaa na kubadilishana mawazo na wanawake wa kitajiri mara nyingi lazima nifikirie kile ambacho naongea …ninachotaka kumaanisha ni kwamba licha ya kwamba wamebarikiw vitu vingi ambavyo katika macho ya wengi ni vya kutamani lakini wengi wao ni wanafiki na maisha yao mengi ni ya kushindana na wivu , lakini ninapokuwa na hawa wa uswahilini wengi wao sio wanafiki na hawatangulizi hela na usomi wao kwenye kusaidiana mambo ya kijamii, mimi kwangu ni watu wazuri zaidi licha ya kwmaba nyie mnawaona kamasio wastaarabu , najisikia huru zaidi kuongea nao”Aliongea Blandina huku macho yake yote yakimwangalia Edna.

Katika meza yote ni kama aliekuwa akiongeleshwa ni Edna na sio mwingine na Edna mwenyeewe hakujuwa kwanini mama yake alikuwa akimwangalia yeye katika kuongea, lakini palepale alikisia kwamba huenda mama mkwe wake kashajua kwamba yeye alimtumia Roma kungea nae .

Upande wa Roma hakuwa ameelewa mamabo na isitoshe hata yeye hakujichanganya sana na watu wa kawaida katika makuzi yake na mahusianyo yake na jamii ni kitu ambacho hakukiweka akilini , lakini maneno alioongea mama yake yalimgusa.

“Hata mimi naunga mkono hoja , ijapokuwa kweli ni wa maisha ya chini na hawajastaaranbika wala kuwa na elimu ya juu lakini inaleta amani wakati wakuongea nao , mara nyingi nikifika sokoni wananichagamkia mno , wanawake wenye pesa na utajiri wengi wamejaa maringo”Aliongezea Bi Wema ambaye kila siku anawahi hapo kufanya usafi na kupata kifungua kinywa.

“Mama sio kwamba niliwadharau hao mashangazi ni kwamba nyumba inakuwa na makelele sana , kama itawezekana unaonaje mkatafta mahali pazuri kwa ajili ya maongezi”

“Roma najua hayo sio maneno yako , bali Edna ndio kakuambia unje uongee na mimi , si ndio?”

“Mama kwanini..”Roma alijikuta akikosa usemina kujiuliza mama yake amejuaje kuhusu hilo.

“Usishangae , ulivyorudi Tanzania uliweza kufanya kazi ya kubeba mizigo na kuishi maeneo ya uswahilini na familia za kawaida , kwanini uchukie wanawake wachache waliokuja nyumbani kunitembelea na kuongea kwa sauti , kama sio mke wako je ungelalamika?”

Ilileta mantiki , Roma ni kweli aliishi mazingira ya kawaida sana wakati alivyorudi Tanzania lakini hakuona tatizo kabisa na alifurahia maisha na kupta uzoefu mpya , alikula chakula hata kwenye migahawa ambayo usafci wake ulikuwa wa kubabaisha, sasa anakerwa vipi na wamama wanaopiga makelele na kucheka nyumbani kama sio Edna.

Edna mpaka hapo alionekana kabisa amekamatika., aliona mama yake alikuwa na pounti ya msingi kwa kile alichoongea.

“Edna kumtumia mumeo kama siraha ya kumshambulia mama mkwe wako sio jambo zuri”

“Mama .. sikumaanisha hiyyo.. “Edna alishindw akabisa kujitetea

“Edna je unaniona kama vile mtu ambaye naweza kufoka au kukasirika bila sababu , au mimi mama mkwe wako sijastaarabika , kuna haja gani ya kumtumia mume kuongea na mimi , unaweza kuniambia nyumba ina maekele sana na inamuathiri Lanlan, Au unaniogopa?”

“Hapana”

“Sisi ni wanafamilia , na unaweza kuongea chochote na mimi ambacho hakikuridhishi , kama niliweza kuruhusu wewe kuasili mtoto kwanini unaniona kama mtu ambaye naweza kukasirika bila sababu?”Aliongea kwa kufoka na kumfanya Edna machozi kuanza kujitengeneza kwenye macho yake na Roma aliona hilo.

“Mama acha sasa kumfokea na naahidi siwezi kuwa mjumbe wa Edna tena , anakuheshimu ndio maana alipatwa na wasiwasi kuongea na wewemoja kwa moja”

“Sawa nimeacha na nitakusikiliza ewe , isitoshe mkeo ndio mtu muhimu zaidi kwenye moyo wako”Aliongea Blandina na kisha akakaa kimya na kuchukua yai lake na kuendelea kulibabua maganda.

Roma alikosa usemi , alijikuta akimwangalia Edna na kisha akamgeungia na Bi Wema na kukosa cha kufanya , alitamani kuongea maneno machache ili kuweka hali hio sawa lakini alikosa ni neno gani la kuongea , lakini Bi Wema alimwangalia na kumuonyeshea tabasamu bila ya kuongea chochote.

Upande wa Lanlan hakujali malumbano hayo ya asubuhi kati ya bibi yake na mama yake , yeye kwanza hakuwa akisikiliza na isitoshe kiswahili kilimpiga chenga.

Baada ya kumaliza maziwa yote aliowekewa na mama yake kwenye kikombe , aligusha tumbo lake na kuona sasa limeshiba.

“Nanny !Lanlan want to go to the school”Aliongea akimwambiaQiang Xi kwamba anataka sasa kwenda shule.

Qiang xi alikuwa ashajiandaa , hivyo alichukua kijibegi cha rangi ya pingi chenye maua maua cha Lanlan na kumshika mkono naLanlan aliaga kwa furaha kwa kila mmoj.

“Tumekuwa kichekesho asubuhi asubuhi mbele ya mtoto”Aliongea Blandina mara baada ya kumwangalia Lkanlan akitokomea nje.

“Mama naahidi sitofanya hivyo tena , nisamehe nimekosea”Aliongea Edna

“Ulichokusudia ni sahihi , mama yako sikufikiria mara mbilimbili nilitii hisia zangu bila kuzingatia mnajisikiaje kama wanafamilia , lakini haikuwa sahihi kumfanya Roma ndio aongee na mimi kwaniaba yako , hivyo siku nyingine uniambie wewe mwenyewe sawa?”Aliongea na Edna alitingisha kichwa kukubali.

Muda huo huo gari lilisikika likisimama getini na kupiga honi , kwasababu nyumba ilikuwa kimya waliweza kusikia /

“Kuna kitu Lanlan kasahau?”Aliuliza Bi Wema maana Edna alikuwa ashambadilishia Lanlan utaratibu wa kwenda shule kwa kutumia gari ya shule na Qiang Xi ndio alikuwa na jukumu la kumpeleka na gari na kumrudisha.

“Ni gari nyingine , nadhani kuna tuna mgeni”Aliongea Roma na muda huo huo kengele ya ndani iligonga.

“Mh ni nani anakuja nyumbani asubuhi asubhi yote hii?”Aliongea Bi Wema kwa mshangao huku akinyanyuka kutokta nje kujua mgeni ni nani.
Ni sawaaa
 
SEHEMU YA 549.

Edna alijikuta akimeza maneno yake aliotaka kuongea kutokana na namna Roma alivyomwangalia.

Maneno yale aliongea Roma ni kama yaligeuka na kuwa jiwe ambalo limetua moja kwa moja kugonga katika moyo wake uliokuwa kama barafu.

Alimwangalia machoni kwa muda mrefu kabla ya kuvuta pumzi na kuzitoa na kisha akalamba lipsi za midmo yake na kuongea.

“Wewe ni mbinafsi sana”

“Nakubali mimi ni mninafsi , ndio maana sitokubali sisi kutalakiana . siwezi kukuruhusu ukaondoka kwenye maisha yangu ,siwezi kupiga magoti pia na kukuomba tena wala sitoomba msamaha , unayo kila haki yakubakia hapa lakini wewe ni wangu na hilo haliwezi kubadilika”

“Unaongea mambo ambayo hayana sababu ya msingi”Aliongea huku akishikilia kwa nguvu nguo yake ya kulalia.

“Nataka uone uhalisia ulivyo , wewe unadhani mama amekukera sana kwa kualika wale wanawake nyumbani , unafikiria sisi wote tulikuwa tukikuchokoza kwa kukushuku , mbona unakuwa mwenye kutukandamiza , unaweza kuwa na kisirani chako kwangu utakavyo na naweza kuvumilia lakini hasira zako za haraka zilifanya kila mtu kukosa furaha , je unadhani wewe ndio unaepaswa kufanya tu hivyo , kwanini unataka kushindana na mimi? , mimi ni mume wako na uyle ni mama mkwe wako na sisi ni wanafamilia , kwanini unataka kutuletea tabu”

“Wewe… nilijua tu hujawahi kunionea huruma”

“Naongea ukweli”

“Inaniuma kwasababu kila kitu ulichoongea ni ukweli”Baada ya kumaliza kauli hio aliingia ndani na kufunga mlango wa balkoni na Roma aliishia kumwangalia lakini hakuwa na sababu ya kumsogelea tena kuingia ndani , aliamua zake kupotea na kurudi nje.

Alijikuta akisimama nje kwa muda akivuta upepo mkali unaotoka baharini na baada ya dakika tano aliingia kwenye gari , lakini ile anataka tkuliwasha simu yake ilianza kuita na aliekuwa akimpigia ni Neema Luwazo.

“Kipenzi changu , uko wapi?”Sauti ya kichokozi ya kumnyanyua nyoka pangoni ilisikika kwenye ngoma zake za masikio.

“Sauti yako inaonyesha kama unajua kinachoendelea”

“Wewe hujui wafanyabiashara mtaji wetu ni taarifa na isitoshe ni swala linalokuhusu , nasikia umekosana na mkeo na amehama kabisa nyumbani?”

“Umesikia wapi , Nasra ndio kakuambia?”

“Ah..,! Nasra sio mtu wa kuongea ongea umbea nadhani hata wengine hajawaambia , nilienda nyumbani kwenu nikakuta hakuna mtu ndio nilipofanya maamzui ya kumpigia Bi Wema na akaniambia kinachondelea , kwanini unajaribu kutuficha , haujui mtu kama mimi ambaye siku zote nina ajenda za siri nilikuwa nikisubiria hii siku itimie kwa hamu zote , namchukulia Edna kama mshindani wangu hata hivyo”Aliongea huku akicheka na kumfanya na Roma pia kucheka kutokana na utani wake.

“Inakupasa usubiri muda mrefu, kwani kisheria haturuhusiwi kupeana talaka angalau tuwe tumeishi pamoja miaka miwili”

“Haha.. Naamini atarudi tu ndani ya siku chache zijazo , nadhani sina haja ya kuendela na mpango wangu , unaonaje ukinisindikiza twende Shopping, hutujaonana muda mrefu”

“Si kwasababu muda wote unasema upo bize wewe , uko wapi nije sasa hivi kukuchukua”

“Nipo nyumbani kwangu , Donyi kaondoka leo asubuhi kulekea Los Angels na mchumba wake Kasimu nipo mpweke mno”

Baada ya kuambiwa hivyo moja kwa moja aliendesha gari kurudi uelekeo wa nyumbani kwa ajili ya kumfuata Neema.

Ndani ya madakika kadhaa Roma aliweza kufika na kusimamisha gari nje ya geti na Neema Luwazo alikuwa ashatoka nje na kumpokea kwa kumbatio , alionekana ashajiandaa tyaari kwa ajili ya kuondoka, aikuwa amevalia blauzi na suruali ya jeans ambayo ilimpendeza na kuchora umbo lake namba nane.

“Unaangalia nini , ingia kwenye gari tuondoke”Aliongea kwani Roma alikua akiangalia mtetemno kwa nyuma huku akiwa ameweka tabasamu a kifedhuli , aliishia kucheka na kungia ndani ya gari.

“Mh! Jamani mbona hili gari linanuka sigara”Aliuliza lakini Roma hakujibu zaidi ya kuguna na kumfanya Neema kumwangalia.

“Kwahio mawazo yamekuwa mengi , sijawahi kukuona ukivuta sigara , nilidhani mwanaume wangu ni wa kipekee lakini inaonekana kumbe hauko imara kudhibiti mawazo yako”Aliongea huku akivuta mdomo na kumfanya Roma kucheka.

“Okey kwanzia leo nitaacha, Wapi unataka kwenda?”

“Mimani City , tunaweza pia kula huko huko chakula cha mchana , unaonaje?”Aliuliza na Roma hakubisha kwanza hata hivyo asingerudi nyumbani na kukaa peke yake wikiend yote hio , hivyo aliona huenda ingekuwa afadhali.

Baada ya kufika Mlimani walianza kupita kwenye kila duka kwasababu Neema hakuwa na kitu kichwani anachotaka kununua hivyo alijaribisha kila kitu kilichomfurahisha , lakini mwisho wake hakuridhika na wakaishia kwenda kwenye Brand maarufu za Balenciarga , Dr Martens, Luis Vuiton na lancome.

Roma aliishia kumsindikiza maana wafanyakazi walikuwa wakimsaidia kushika kila ambacho anachagua , lakini Roma kwenye upande wa nguo hakuona kwanini Neema anachagua aina hizo za nguo kwani hazikuwa zikimvutia.

“Hey , kama unataka kununua nguo nadhani ulizopita kule nyuma ndio zinakufaa zaidi , hizi nguo nadhani ni kwa ajili ya maonyesho ya fasheni, hakuna maana kuziangalia”Aliongea Roma.

“Wewe mwanaume huelewi kama nisipovaa nguo ambazo ni za brand kubwa nikienda kwenye vikao wataniona kituko , sisi wanawake siku hizi tunajali sana kile ambacho tunavaa kuendana na wakati”

“Kuna haja gani ya kujali watu wanasemanini , kwani hakuna anaeweza kuipima thamani yako kupitia mavazi”.

“Hehe ndio dunia inavyoenda , kama sio hivyo unadhani makampuni kama haya yangekuwa maarufu , kampuni ya mkeo ukiachana na upande wa kampuni zake ndogo ndogo za ujenzi na mambo ya mafuta lakini pia upande wa fasheni umemuinua sana kiuchumi”

“Inaonekaa hufatilii sana kile ambacho kinaendelea kwenye kampuni , hivi majuzi tu aliweza kuingia ubia wa kibiashara na kampuni zenye majina makubwa makubwa kuomba haki ya kusambaza bidhaa zinazotokana na malighafi mpya , kampuni alizoingia nazo mkataba ni kama Prada , Hermes na Burberry , faida alizopata kwenye ubia na kampini hizo ni mara mbili yake anayopata kwenye kampuni zake za ujenzi ukiachana na mafuta pamoja na viwanda vya utengenezaji wa bidhaa za ndani”

“Ana kipaji cha kufanya biashara , lakini nadhani anapaswa kujifunza namna ya kuwa mke bora”Aliongea lakini Neema alicheka.

“Mbona unacheka?”

“Ni hivyo uliposema ana kipaji cha biashara lakini kwa mtazamo wangu naamini ni kinyume chake , ameweza kufanikisha yote hayo kutokana na ukweli kwamba baba yake ni mtu mzito na ana ushawishi mkubwa kwa Raisi Senga na nchi zote za Afrika ya mashariki na kati

“Unamaanisha nini?”

“Wafanyabiashara kama sisi siku zote tunapaswa kufanya vitu kwa wakati sahihi , sehemu sahihi na watu sahihi , kuwa na watu sahihi sio kitu kigumu kwasababu unachotakiwa ni kuwa na ushawishi tu na maipo mazuri , kuhusu sehemu sahihi inategemeana na bahati yako katika biashara , kama sio kampuni ya Vexto kuchagua maeneo sahihi katika kufanya biashara basi siamini ingeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa nchi kama hii ya kwetu ambayo ndio kwanza inaendelea , kitu kigumu katika biashara ni kufanya vitu kwa wakati sahihi kwasababu kikawaida inategemnea sana na sera za nchi , kadri utakavyofanya vitu ndani ya sera za serikali basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu fursa za kibiashara , kama sera haiendani na biashara yako hata uwe na mtaji mkubwa kiasi gani huwezi kufanikiwa na ndio maana wawekezaji wanapoenda kuwekeza kufanya biashara katika mataifa ya nje wanachoangalia ni Sera”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Raisi Jeremy alikuwa akimsaidia Edna katika maswala ya sera ndio maana kampuni yake inafanya vizuri?”

“Ndio maana nakushauri kuwa makini na Raisi Jeremy , ijapokuwa hakuwahi kumtambua Edna waziwazi kama mtoto wake, lakini amesaidia sana kampuni ya Vexto kufikia pale ilipo, huenda kama atakuja kumwambia Edna mambo ambayo amefanya Edna moja kwa moja ataguswa”Aliongea Neema na kumfanya Roma kukumbuka kuna siku Edna ashawahi kumwambia kuhusu mtu anaefahamika kwa jina la the Protector ni kama maneno ya Neema yamemkumbusha kuhusu hilo jina kwani alikuwa amesahau kwa muda mrefu.

“Kwanini unaniambia haya ghafla tu, unadhani kwanini Jeremy anaushawishi mkubwa ndani ya Afrika mashariki na kati?”

“Kuna kitu sikukuambia kwasababu nilikuwa bize na kazi , lakini katika moja ya vitu ambavyo niliweza kugundua katika baadhi ya nyaraka alizoacha mstaafu Kigombola ni juu ya raisi Jeremy na siri zake”

“Siri zake!”

“Ukweli kama ningeona taarifa hizo miaka ya nyuma kabla ya kukutana na wewe nisingezielewa wala kuamini , lakini kwa kipindi ambacho tumekutana na nikajua mengi ambayo hayaonekani katika huu ulimwengu ndio maana nimefanikiwa kuelewa kile alichoandika”

“Umegundua nini?”

“Kwa maelezo ya Kigombola ni kwmaba Raisi Jeremy ana nguvu kubwa nyuma yake ambayo inamlinda na inahusiana na viumbe wasioonekana(majini) , katika nyaraka nilizoweza kupata kusoma jamii hio inafahamjka kwa jina la Panas kama sikosei”Roma alishangaa maneno ya Neema.

“Amejuaje kuhusu hii jamii kuwa nyuma ya Jeremy , mwenyewe nilianza kufikiria hili swala mara baada ya kuona watu wawili kutoka Panas ambao tayari wapo katika levo ya Nafsi wakimsindikiza kama mabodigadi”

“Nini!!, kwahio nilichosoma ni kweli jamii hio ipo, kama ndio hivyo inamaanisha kwamba wametoka katika maficho yao sasa wanataka kuingilia amswala ya kawaida ya dunia?”Aliongea Neema Luwazo kwa mshangao.

“Siwezi kujua, lakini uwepo wao hapa nchini ulinipa maswali mengi ambayo sijayapatia majibu bado na kama uliosema ni kweli basi naanza kupata picha lakini pia shauku yangu kuzidi kuongezeka , je hakuna kitu kingine ambacho uliweza kupata katika maelezo uliosoma?”

“Maelezo niliosoma ni hayo pekee na ndio nguvu kubwa ya Raisi Jeremy nchini Rwanda , ilionekana Kigombola bado hakuwa na majibu ya kutosha na hata alichokiandika hakikuwa na ushahidi , lakini baada ya wewe kusema wameonekana hapa Tanzania sasa naamini maneno yake”Roma alifikiria kidogo na kuona huenda kuna sababu ambayo watu wa Panas wakaamua kuja upande wa duniani , lakini kama ni hivyo kwanini Aphrodite na wenzake hawakumweleza kuhusu hii jamii maana kama na wao walikuwa wakitumia nguvu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi basi wangewalaetea mtafaruku wakati walipokuja duniani.

“Kama ni hivyo je unadhani swala hili linaweza kumuhusu Edna?”

“Lazima liwe linamuhusu , nadhani mpaka sasa huna taarifa, ukweli ni kwamba mpaka sasa mtoto wa pekee wa Raisi Jeremy hafahamiki alipo , ijapokuwa taarifa hio ni ya siri lakini hawezi kuificha kwa watu kama sisi ambao tunahusiano wa moja kwa moja na serikali, kama hisia zangu zitakuwa sahihi basi naamini anataka kumfanya Edna kuwa mrithi wake”Aliongea na kumfanya sasa Roma kuelewa kitu.

“Nadhani ndio maana alionekana kuwa na haraka ya kumtaka Edna kumtambua kama baba”

“Unamaanisha alishaanza kuongea na Edna?”

“Siku ambayo niliwaona hao watu kutoka Panas ndio wakati ambao alifika nyumbani kwetu kwa ajili ya kuongea nae , lakini inaonyesha Edna hakuwa tayari kukubali”

“Wasiwasi wangu ni kwamba ataishia kukubali na kama hilo litatokea mkeo anaweza akakuingiza kwenye mtego , mpaka sasa naamini Hongmeng ni maadui zako na hata jamii hio ya Panas sidhani kama wanakuchukulia kama rafiki au adui, Jeremy ndio mtu pekee ambaye atafanya kila kitu kwa faida yake na mawazo yake yote ni kuona Rwanda inakuwa kimaendeleo kwa kunyonya rasimali za nchi zinazomzunguka kupitia njia za kijasusi”Roma alijikuta akianza kuwa na wasiwasi, alijua msimamo wa Edna ulivyo likija swala la familia.

“Lakini sidhani Edna anaweza kuwa mwepesi namna hio”Aliongea Roma.

“Hata mimi natumaini asiwe mwepesi wa kukubali kila kitu”

“Okey, nimekuja kurelex sio kuongea mazungumzo haya , hebu tuendelee na kilichotuleta”Aliongea Roma na kisha waliendelea kufanya shoping.

Ni muda wa saa saba wakati wakiwa kwenye mgahawa wakipata chakula cha mchana Roma aliweza kupata msisimko wa kuongezeka kwa mtu mwenye nguvu za kijini na kujikuta kugeuza shingo yake kuangalia upande wa kulia na palepale aliweza kumuona Omari Tozo akiingia eneo hilo.

Omari alikuwa amevalia mavazi ya suti na kwa mwonekano wake ni kama vile amekuja hapo ndani kwa ajili ya kuonana na mtu , baana ya kukagua baadhi ya watu palepale aligeukia upande wa aliposimama Roma na kisha akatabasamu na kupiga hatua kumsogelea.

Tokea siku ambayo waliweza kuhudhuria harusi yake hawakuwahi kuonana tena.

“Madam Neema nadhani hutonilaumu kwa kuingilia muda huu mzuri kwenu wa chakula cha mchana nikimchukua kwa dakika huyu kiumbe , si ndio?”Aliongea Omari huku akiweka tabasamu.

Kwa muonekano wa Omari alivyo alijua tu kuna kitu anahitaji kuongea nae.

“Nadhani ndoa tamu , naona una mabadiliko makubwa ya kiafya”Aliongea Neema kwa utani na kumfanya Omari kutoa cheko kama kawaida yake.

“Nadekezwa mwenzenu , nashindwaje kunenepa sasa”Aliongea na kisha wakasogea meza ya pembeni kwa ajili ya kuongea,.

“Kwa muonekano wako nadhani hatujakutana hapa kwa bahati mbaya si ndio?”

“Upo sahihi , nipo hapa kwa niaba ya serikali chini ya TSS kukuuliza maswali kadhaa ya kiusalama”

“Maswala ya kiusalama , tangu lini serikali ikaniuliza maswala ya kiusalama wakati mimi ni rais mwema?”Aliuliza Roma kwa mshangao.











SEHEMU YA 550.

Roma alijua sio rahisi kwa Omari kumtafuta na kutaka kuongea nae maswala ya kiusalama , lazima kutakuwa na kitu ambacho kinaendelea ambacho yeye hakifahamu , imepita wiki kama tatu tokea The Eagles kuondoka Tanzania na kurudi visiwa vya Mediterranian hivyo hakuwa na chanzo sahihi cha taarifa.

Aliwaondoa kwasababu ya kwamba tishio la kiusalama lilishaisha kutokana na kumuua Yan Buwen na washirika wake akiwemo Mzee Longoli.

“Kwa muonekano wako naamini huna taarifa ya makundi ya watu waliongia Tanzania hivi majuzi?”

“Ndio sina taarifa nadhani mnafahamu The Eagles project yao hapa Tanzania imesitishwa na kurudi, kwasasa nipo mwenyewe tu hapa Dar es salaam”

“Ndio maana hujaweza kupata taarifa”

“Kuna nini kinachoendelea?”

“Intellijensia ya usalama wa taifa imeweza kubaini kikosi cha giza cha Siraha Kwenye Jiwe(SIS) kutoka Scotland ,Bunge la Kiza likijumuisha wanachama wao wa kundi la Camarilla na Sabbat wapo hapa nchini , kuna pia baadhi ya makundi madogo ya watu wanaotumia nguvu za giza pia wamefika”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa.

“Wamekuja hapa Tanzania , kwasabau gani , kama ni jiwe la Kimungu nadhani wanajua halipo chini ya umiliki wangu?”

“Nadhani hawajaja kwa ajili yako na isitoshe sidhani kama wana uwezo wakupigana na wewe”

“Kama sio hivyo kwanini wamefika?”

“Intellijensia tulioweza kuvujishiwa kutoka nje ya nchi ni kwamba wapo hapa kwa ajili ya siraha ya kichawi ifahamikayo kwa jina la Magical Girdle”Aliongea Omari na kumfanya Roma kushangaa kwani neno la Magical Girdle ashawahi kusikia.

“Unamaanisha siraha iliopo kwenye hadithi za miungu ya kigiriki ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Aphrodite?”

Katika hadithi za miungu ya kigiriki na kiroma , mungu wa urembo aliefahamika kwa jina la Venus kwa kirumi au Aphrodite kwa kigiriki alikuwa na siraha ya mvuto ya mshipi wa kichawi wa dhahabu ambao uliwafanya miungu mingine kuvutiwa nae sana kimapenzi.

Inasemekana alitumia siraha hio kuwapumbaza miungu na kutawala akili zao kihisia , alifikia hatua ya kushindana na Athena pamoja na Hera katika kujiongezea mvuto kwa kutumia siraha hio na alifanya miungu yote kumchagua yeye kama mrembo zaidi.

Lakini hata hivyo ni hadithi tu , kitu ambacho kilitungwa na binadamu wakiwa wamedhibiitwa kiakili ili kufanya binadamu wengine kuwaabudu viumbe hao waliovamia dunia na kuona Binadamu ni kiumbe dhaifu.

Sasa Roma hakuwahi kusikia kutoka kwa Christen kama kweli alishawahi kuwa na siraha hio ya kichawi ifahamikayo kwa jina a magical Girdle lakini kama ilivyokuwa kwa Hades wa zamani kutokumuambia kuhusu siraha yake ya Helmeti of Invisibility(Helmet la kutokuonekana) wakati alivyomuachia urithi basi aliona huenda ni sawa kwa Christen pia.

Siraha za aina hio hata hivyo hazikuwa na maana sana kwa viumbe hawa wa sayari nyingine ambao wameishi hapa duniani kwa muda mrefu , kutokana na kwamba wanakosa miili yao halisi.

Na Roma aliona kama Christen kweli alikuwa na huo mshipi kwa alivyokuwa akimtamani huenda angeshaidhibiti akili yake na kumfanya alale nae au kufanya zaidi ya hivyo na hana uhakika kama angeweza pia kutawala akili ya Zeus na wengine.

“Kama ni hivyo unamaanisha wanatafuta huo mshipi hapa Dar es salaam ,unamaanisha mshipi huo umeonaka hapa Tanzania?”

“Hata sisi hatuna uhakika pia , na tumeshindwa kuweza kujua taarifa kamili”

“Kama ni hivyo wamejuaje kama Mshipi huu wa kichawi upo hapa Tanzania?”

“Kuna mtu ambaye ametumia Mshipi huo wa kichawi kuwadhibiti wanajeshi wa kitengo maalumu na aliweza kuonekana kwenye Rekodi ya Vidio , hio Vidio ndio ambayo imesambazwa kwa Kundi la SIS , Bunge la Kiza na baadhi ya makundi madogo madogo, Eneo ambalo limeonekana kwenye Vidio hio ni katika kambi yetu ya kijeshi ya Ruvu”

“Kama unayo hio vidio unaweza kunionyesha?”Aliuliza Roma huku akianza kuwa siriasi na Omari alionekana alishajiandaa kabla ya kufika hapo na alitoa simu yake na kuchezesha kicha akamkabidhi Roma.

“Kwenye Vidio hio ilionyesha kivuli cha mtu mwenye ngozi nyeusi yaani muafrika akijaribu kutawala akili za wanajeshi waliokuwa katika Demo ya mazoezi ya siraha na kwa kutumia Mshipi wa Dhahabu palepale wale wanajeshi waligeukana wao wenyewe na kupigana risasi.

“Ni Vidio fupi sana , tukio hili mpaka sasa ni siri ya serikali na limetokea wiki iliopita , baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na kivuli cha mtu kinachoonekana kwenye hio Vidio kutotambulika Serikali ilipanga kikao kuzima swala hili ili kubakia siri , lakini ajabu ni kwamba hio Vidio ilisambaa nje ya nchi kwa makundi hayo ya watumiaji wa nguvu za giza”

“Inasemekena pia mtu ambaye anatumia hio Dhana ametangaza kwamba ameipata kwabahati mbaya na anashindwa kufahamu namna ya kuitumia hivyo anapanga kuiachia kwa watu wengine wenye uwezo na ameificha ndani ya jiji la Dar es salaam na mtu ambaye atabahatika kuipata ndio atakuwa mmiliki”Roma alijikuta akiwaza kidogo kusharabu maneno hayo.

“Nadhani sio sawa ,kama kweli hio dhana ni yenyewe sidhani Aphrodite angeshindwa kuinasa kihisia, lakini mpaka sasa hakuna hatua aliochukua na isitoshe siraha hio haiwezi kutumiwa na mtu yoyote kwani inahitajika kuwa na nguvu ya kiuungu ndani yake, Kwahio hamjatambua kabisa hiko kivuli cha mtu ni nani na nia yake ya kufanya hivyo?”

“Bado hatujaweza kufahamu , ni swala ambalo ucunguzi wake unaendelea kwani mpaka sasa linaumiza vichwa vya wakuu wa majeshi , maana tukio la kupigana risasi wanajeshi kwa wanajeshi ni la kuogofya sana kwa usalama wa nchi”Aliongea na kumfanya Roma aanze kufikiri.

Kuna kipindi wakati alipokuwa Ufaransa watu walikusanyika kwa ajili tu ya kutaka kuipata siraha ya Thanatos , lakini sio hivyo tu hapa Dar es salaam ni kama tukio hilo linajirudia , kwani mara ya kwanza Dhana ya Holly Grail ilionekana Tanzania na makunndi ya nguvu za giza na za Nuru walifika na kuanza kupigana kuipata.

Roma mara baada ya kuwaza aliishia kucheka , alijua hata kama inaweza kuwa halisi , hakuna uwezekano kwamba wanaweza kuitumia kupumbaza watu kwani ni siraha inayomjua mmiliki.

“Lakini kwanini hili swala naona kama ni mtego , nadhani nyie watu msijisumbue , ngoja wafanye wanachoweza kufanya na sisi tuone”Aishauri Roma,

“Bro unapaswa kutusaidia katika hili , hawa watu kama itatokea wakahatarisha usalama wa nchi vikosi vyetu vya idara ya uchawi sidhani kama wanaweza kufanikisha kuwadhibiti na isitoshe wewe pi ni mtoto wa raisi na familia yenu imeweka mizizi katika usaama wa taifa”

“Ohoo!, siwezi hata kumdhibiti mke wangu mwenyewe, halafu nijihusishe katika haya mambo . kwanini niingilie?”Aliongea Roma akijaribu kukataa.

“Kama huwezi kuingilia tunalo ombi moja kwa sasa , wewe unafahamiana na miungu wenzako mathalani Aphrodite mungu wa urembo, kama kutakuwa na uwezekano wa kujitokeza na kutusaidia , maana kama watu hao wataanzisha vurugu mambo yanaweza kuwa nje ya uwezo wetu”Roma alifikiria kidogo.

“Okey nitampigia simu baadae”

“Mpigie sasa hivi Bro wakuu wanasubiri majibu muda huu”Aliongea kwa msisitizo na kumfanya Roma kukosa neno la kuongea na palepale aliamua kutoa simu yake na kutafuta namba ya Christen na kupiga na iliita kwa muda mrefu kidogo lakini Roma hakukata tamaa kwani alijua muda huo Los Angeles itakuwa ni usiku kukikaribia kupambazuka.

“Hades , are you calling to ask me about Magical Girdle too?”Aliuliza akimaanisha kwamba je anampigia kwa ajili ya kuulizia mshipi wa kichawi pia.

“Ndio”Alijibu Roma.

“Mshipi wangu wa thamani kubwa haujaibiwa , ninao siku zote hivyo naomba usiulizie tafadhari , Mshipi ambao umeonekana kwenye vidio unafanana sana na wa kwangu lakini ni feki , kuna wachawi wengi wa kiroho dunia hii, kwa mfano kundi la kichawi la Siraha kwenye Jiwe wanaweza kutengeneza udanganyifu , hivyo kwanini iwe dhana yangu ya Mshipi wa dhahabu”Aliongea kwa namna ya kujitetea na kukereka kwa wakati mmoja na kumfanyaRoma kukunja sura.

“Kwanini sasa unaonekana kuwa na hasira , miimi nimepiga simu kwa niaba ya jeshi la Tanzania kitengo cha wachawi kwani hawana uwezo wa kukuuliza moja kwa moja na isitoshe nilijua usingeshindwa kunasa kihisia pale mtu anapotumia dhana yako”

“Tatizo mnanisumbua , muda si mrefu Poseidon ,Hermes na Artemis wamenipigia na kuniamsha kwenye usingizi , naomba usijihusishe , waache watafute kama wanavyoamani lakini kama utagundua muhusika wa kuzusha uongo huo ni nani niambie nitahakikisha namchuna ngozi akiwa hai”

“Sawa lakini kwa nilivyosikia kundi la Sabbat pia lipo hapa nchini , nadhani chuki zako uzielekezee kwa Raphael kwani ndio kiongozi wa kundi hilo ambae ameagiza watu wake kuja hapa nchini na wakafatia kundi la Camarilla”

Raphaeli ndio kiongozi wa kunti la Tzimisce ambaye anatumia mwili wa Vampire , ni kiumbe kutoka sayari nyingine ambaye alifanya watu duniani wamuabudu kwa kumuita Hermes mchunga kondoo.

“Hermes ni mtu wa ajabu na sipendi kuongea nae, nadhani amefanya hivyo kutokana na kuficha uhusika wake, mpaka sasa hakuna Vampire anaemfahamu kwa jina la Hermes, Hades nitakuw amkweli kwako kila dhana ambayo tulikuja nayo imeunganishwa na roho zetu kuna zile zilizopotea na tulizobakiwa nazo , ndio maana hata Artemis aliweza kuhisia uwepo wa Selene nchini Korea kusini licha ya kwamba alikuwa umbali wa takribani nusu ya dunia, mpaka sasa dhana pekee ambayo imepotea na na imeshindikana kufahamika imepotelea wapi ni Helmeti la kutokuonekana ambalo ni siraha yako , kama hujui, Helmet hilo ni kama taji na nitofauti sana na dhana tulizokuja nazo kwani teknolojia yake ilikuwa ni ya hali ya juu sana na Hades wa dhamani kwasababu alikuwa ni mwanasayansi ndio anajua siri yake”

“Ndio maana Hades wa zamanni sikuwahi kumuona nalo , kumbe ni dhana ambayo haionekani”

“Nadhani umeelewa sasa narudi zangu kulala , kama utakuwa na muda naomba uniangalizie nani kaanzisha huo uvumi , niambie na nitakuja kumuua mwenyewe , anadhani kujificha Tanzania siwezi kumpata na kumuua”

“Kuhusu hilo usijali nitakusaidia ,lakini na mimi utanisaidia kujibu maswali yangu yote ya kile kilichotokea Korea kusini bila kunificha kitu”Aliongea Roma na kauli yake ilimfanya Christen kuwa kimya.

“Nilishakujibu tokea muda mrefu hukuzingatia ndio maana , mimi nalala”Aliongea na kisha akakata simu na kumfanya Roma kukuna kichwa chake na kujiambia atajua tu ukweli wote kuliko mambo nusu nusu wanayomwambia.

Roma ilibidi amwelezee Omari juu ya alichoweza kupata na wote walijikuta wakiwa na ahueni na aliwathibitisha hakuna mgogoro unaoweza kutokea baina ya wageni hao kama tu Mshipi huo hautakuwa halisi.

“Asante sana Bro , nadhani napaswa kuondoka sasa nikuache na shemeji, tutakutaarifu tukimpata muhusika”

“Haina haja ya kunifahamisha , hilo ni swala ambalo halinihusu”Aliongea na Omari aliaga na kuondoka.

Neema hakumuuuliza sana maswali Roma juu ya kile ambacho alikuwa akiongea na Denisi , kwani mara baada ya kurudi kwenye meza walikula chakula kama wapenzi huku wakishushia na mvinyo.

Wikiend nzima Roma alimalizia kwa Neema Luwazo na walipika na kupakua na alimsaidia pia kwenye kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Siku ya jumatatu mara baada ya kuamka mawazo ya Edna yalianza kukisumbua kichwa chake na wakati alipokuwa akipata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Neema alimkumbuka na alijiambia kutokana na anavyo mjua Edna muda huo atakuwa hajapata chochote , hivyo alimwambia Neema amwandalie vitu vya kuondoka navyo kwani anampelekea mke wake, aliongea bila ya kupindisha kauli.

Neema baada ya kuambiwa hivyo alimuonea wivu Edna lakini aliishia kuandaa kwani alijua yeye ni mchepuko tu na ili aendeee kufurahia penzi na kijana huyo mdogo basi ni kuhakikisha anamfurahisha na kumsapoti kwa kila kitu na isitoshe anapata faida kubwa ya kuvuna nishati kitu kitakachompeekea kuwa mrembo muda mrefu.

Roma asubuhi hio mara baada ya kufika nje ya ofisi ya Edna aliweza kukutana na Recho ambaye alikuwa akitoka katika ofisi ya Edna na kwa haraka haraka alijua huenda alikuwa akisafisha na kuweka mazingira sawa lakini aligundua sio hivyo mara baada ya kuona amebeba mabakuli na juisi kwenye mfuko wa plastiki.

Hakuwa amemuona Recho kwa muda mrefu kidogo ni kama zaidi ya miezi mwili , lakini alionekan hakuwa amebadilika sana zaidi ya kwamba kipindi hiko alionekana ni mwanamke mwenye kujiamini sana kuliko alivyokuwa mwanzo na ni kama urembo wake umeongezeka zaidi.

“Ni wewe .,… nikajua Boss ndio amefika”Aliongea huku kidogo akionyesha hofu.

Tokea kitendo kilichotokea miezi kadhaa iliopita ilifanya wao kujihisi vibaya kila pale wanapokutana .

“Edna yuko wapi , bado hajafika kazini?”Aliuliza Roma na kumfanya Recho kushangaa kidogo.

“Kuna chochote kilichotokea kati yako na Boss? Kwanini amehamia Msasani?”

“Nadhani haina haja ya kuongelea hilo kwasasa”Aliongea Roma maana hakutaka kutanganza matatizo ya ndoa yake hadharani.

“Ulichobeba ni kifungua kinywa kwa ajili ya Edna?”Aliulizia Roma kupotezea mada.

“Ndio , amenipigia simu nimwandalie ..”Aliongea Sekretari Recho huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza chini , alikuwa na aibu za kike kwani alishindwa kumwangalia Roma usoni.

Ukweli ni kwamba Recho licha ya kwamba alikuwa na maisha mazuri na kule kukataliwa na wanaume kuisha , lakini akili yake haikufuta tukio la kufanya mapenzi na Roma , ni tukio ambalo muda mwingine hujirudia hata wakati anapofanya mapenzi na mpenzi wake mpya na kadri siku zinavyozidi kuendelea ndio ambavyo tukio lilizidi kutawala akili yake lakini hakupata ujasiri wa kumsogelea Roma tena kwani ni mke wa bosi wake na aliogopa ikija kugundulika , kwani maisha yake wakati huo na familia yake yalikuwa mazurri kutokana na mshahara mnono pamoja na posho anazopata kutoka kwa Edna.

Muda huo ambao hawakuwa wakijua ni topiki gani waendelee nayo kuongea wakimsubiria Bosi hatimae Edna alitokea kwenye lift na kuingia eneo hilo na alijikuta akipatwa na ubaridi mara baada ya kumuona Roma mbele yake.

Jicho moja tu kwa Recho ni kama aliona lazima kuna kitu kilichotokea kati ya Roma na sekretari wake na hapo hapo alizidi kuongeza ukauzu wake.

“Boss karibu kazini , nimekuandalia ulichoniagiza”Aliongea Recho kwa mtindo wa heshima kwa bosi huku akiwa na afadhali.

Edna alimpita Roma kama hamjui na kisha alimsogelea Recho na kuchukua mfuko alioshikilia mkononi na kisha akatingisha kichwa kama ishara ya kushukuru na kupiga hatua kuingia ofisini kuingia kwake , lakini kabla hajafikia mlango Roma alianzisha maongezi.

“Edna na mimi nimekuletea kifungua kinywa mke wangu, niliju tu muda huu utakuwa hujapata chochote”Aliongea huku akimwonyeshea mfuko alioshikilia na Edna alijikuta akitoa kicheko hafifu cha kukera.

“Una uhakika umeleta kwa ajili yangu?”











SEHEMU YS 551.

Upande mwingine nyumbani kwa Afande Kweka mara baada ya Lanlan kufika nyumbani hapo akiwa ametangulizana na Qiang , aliweza kupokelewa kwa furaha na wazee wawili ngozi tofauti ,mmoja akiwa ni Mzee Kweka mwenyewe na mwingine alikuwa ni Pastor Cohen.

Pastor Cohen mara baada ya kumuona Lanan alimwangalia Afande Kweka kwa tabasamu kubwa na kutingisha kichwa kuonyesha ishara ya kukubali jambo.

Ukiachana na maswala mengi ambayo Afande Kweka na Pastor Cohen waliweza kuzungumza lakini kubwa zaidi ni swala la Lanlan kuwa mtoto wa Seventeen pacha wa Edna ambaye aichanganywa na Roma kwenye mpango LADO.

Pastor Cohen na Afande Kweka ndio watu ambao walioratibu mchakato wa kumuingiza Roma na Seventeen katika mpango LADO na moja wapo ya matokeo hayo ni uwepo wa Lanlan duniani.

“Komredi nikiri hapa hakuna ubishi , lakini nashindwa kuelewa inakuaje Roma kushindwa kumfahamu binti yake mwenyewe”

“Komredi hilo ni swali gumu kwangu , najua nilihusika kuwaingiza kwenye mpango LADO lakini uendelevu wake sikuhusika”

“Sio wewe tu ambaye hukuhusika , wote hatukuhusika, mpango LADO kumbuka ulikuwa chini ya Zeros organisation na sisi tulichokifanya ni kufuata maagizo ya kuchomeka watu ambao hawakuwa katika mpango ili kutengeneza mafanikio”Aliongea na Afande Kweka alionekan kutopinga.

“Nadhani imekuwa ngumu kutokumfahamu mtoto wake kutokana na kilichomtokea Seventeen”

“Nakuunga mkono , lakini bado kuna kitu nashindwa bado kuelewa , kama wewe umeweza kumfahamu mjukuu wako kwanini yeye baba ameshindwa hilo”

“Ukiniuliza hilo nitasema ni uzoefu lakini nikikujibu kwa niaba yake nitasema licha ya mengi ambayo yametokea lakini bado mtoto wake ameweza kurudi nyumbani kumfuata , damu ni nzito kuliko maji”

“Ningetamani kujua kila kilichotokea , nadhani mzee mwenzangu una shauku ya kujua pia nini kilitokea baada ya kupotea kwa ile ndege , kwani mpaka sasa ni mpango wa siri ambao ni watu wachache sana duniani wanaoufahamu”

“Ninatamani sana , lakini kwa uzee huu nadhani naweza kuangulie mbele za haki bila kujua kile kilichotokea”Aliongea na kumfanya Pastor Cohen kutingisha kichwa.

“Wewe ni mimi Komredi hatuna haja ya kuwa na huzuni ilimradi tulichokifanya kinakwenda kuisaidia dunia , kwasasa nadhani shauku yangu imetimia sasa , nimemwona kitukuu chako, nadhani ni muda wa mimi kuondoka , lakini kabla ya yote nataka kukueezea kile kinachoendelea ndani ya umoja”

“Nakusikiliza Komredi”

“Kwasasa ndani ya kundi , kuna ‘interval’ kubwa ya tarehe katika kalenda kwa kile ambacho wanachana wanapaswa kufanya”

“Unamaanisha nini Komredi?”

“Ukiachana na taratibu za kawaida ambazo zinaendelezwa kufanywa na wanachama kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya kwanza ya mvua ya theluji kwa bara la Afrika”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushangaa.

“Mvua ya kwanza ya Theluji katika bara la Afrika , unamaanisha Tanzania Mvua ya Theluji itawezekana kunyesha?”

“Hakika , ndio ishara kubwa inayosubiriwa “

“Ishara hii inamaanisha nini?”

“Katika umoja wetu ishara hii inamaanisha ule wakati uliosubiriwa umetimia ni kama unabii umetimia , kwa upande wa Illuminat na Allien kwao ni ishara ya utawala wao duniani kuanza”

“Nini kitatokea baada ya hapo?”

“Kwasasa hakuna majibu sahihi ,mpaka itakapojulikana ni kipi kingine kinapaswa kufanyika kulingana na Kalenda , lakini mpaka sasa tunaweza kufanya makisio, nadhani unajua nini kinasababisha Theluji?”

“Najua ni Baridi?”

“Sahihi kabisa, makisio ni kwamba kuna uwezekano joto la dunia kushuka katika viwango vya chini sana kiasi cha kupelekea bara la Afrika kuweza kupitia vipindi vya majira ya mvua ya Theluji”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushika kidevu , ijapokuwa hakuonyesha mshangao wake waziwazi lakini ilikuwa dhahiri taarifa hio ilikuwa ya kumshangaza.

*****

Roma alijikuta akishangazwa na swali la mke wake kwani hakuwa amemulewa kabisa , alimbebea yeye kifungua kinywa lakini tena anatilia mashana nia yake ya kumletea.

“Edna unamaanisha nini?”

“Nadhani Recho hajapata kifungua kinywa bado , usipoteze hela zako kwa mtu kama mimi , nitajifanya sijaona chochote”Aliongea na Roma palepale aliweza kuelewa anachomaanisha na kushindwa kuzuia hasira zake .

“Edna hata kama unataka kuonyesha hasira zako hupaswi kwenda mbali hivyo , ndio nimefika sasa hivi na kukutana na Recho hapa , hata kama unadhani sina jema lakini huwezi kuongea hivyo kwa kumsingizia msaidizi wako”

“Nimeonyesha wapi hasira? , au umeelewa vipi kauli yangu , kwanini unajishtukia kama huna hatia?”Aliongea na kumfanya Roma kuwa katika mtego wa maneno.

Alikuwa na hasira na kauli ya Edna lakini alishindwa kukataa wala kukubali , kwani ni kweli kuna dhambi ambayo alishawahi kufanya na Recho.Aliona kama angekataa asingeweza kuituliza roho yake yenye dhamira ya kuhukumu.

“Madam , tafadhari naomba usituelewe vibava Mr Roma amenikuta hapa na amekuletea kifungua kinywa , hakuna chochote kinachoendelea baina yetu naomba usifikirie hivyo tafadhari”Aliongea kwa uwoga huku akiangalia chini.

Roma baada ya kumuona namna ambavyo Recho anajitetea ilimfanya amuonee huruma , kwani alikuwa kwenye hali ya taharuki mno , alikuwa kama mtu ambaye amekamatika katika jambo na sasa anahofia kibarua chake kuota nyasi.

“Recho wewe unaweza kutumia hiki kifungua , kama mtu hataki haina haja ya kumlazimisha ilihali wahitaji wapo”Aliongea Roma na kuweka kwenye miguu ya Recho ule mfuko na kisha aliondoka hilo eneo na kuzisogelea lift.

Recho mara baada ya kuona ameachiwa msala alitamani kupiga magoti , lakini palepale aliushika ule mfuko kwenye sakafu na kisha akamnyoshea Edna aupokee.

“Madam naomba usimfikirie vibaya , Mr Roma kakuletea hiki kifungua kinywa kwa ajili yangu naomba ukichukue..”

Edna aliangalia ule mfuko aliopewa na Recho ulivyotuna na kisha alimsogelea Recho na kuuweka chini.

“Unaweza kuchukua na hiki pia , sina hamu ya kula chochote leo”Baada ya kusema hivyo aliingia ofisini kwake.

Recho aliona siku hio imeanza vibaya sana kwake , alijikuta akiangalia ile mifuko yote miwili , alioleta Roma na alioleta yeye mwenyewe na kujikuta akikosa cha kufanya kwani aliishia kusimama katika sehemu moja bila ya kusogea.

**********

Upande mwingine katika ofisi ya Raisi Senga asubuhi hio , Raisi wa nchi ya Tanzania akiwa ofisini kwake akiendelea na majuku yake , aliweza kufika Kabwe nje ya ofisini huku ameshikilia faili mkononi na baada ya kuruhusiwa kuingia ndani moja kwa moja alimsalimia Mheshimiwa.

“Vipi kuna jipya , kuna chochote ambacho mmefanikiwa kupata?”Aliuliza Raisi Senga kwa shauku.

“Mheshimiwa mpaka sasa hatujapata mwanga wowote wa kumpata Denisi , lakini vijana wamejjitahidi kutafuta taarifa ambazo kwa kiasi flani zinatupa tafsiri ya kile kinachoendelea”Aliongea Kabwe.

“Nipe taarifa”

“Kuna baadhi ya watu hapa nchini tuliweza kuwahoji , mmoja wapo ni Abubakari Hamadi mtoto wa Mzee Alex mmiliki wa kampuni ya JR na mwingine ni Elvis Temba mtoto wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma”

“Na mlichogundua ni kitu gani?”

“Nadhani Denisi alikuwa na mpango anaoendeleza yeye na Yan Buween kwa siri hapa nchini kwani kwa maelezo tuliokusanya ni kwamba aliwaambia marafiki zake wote kwamba kuna kitu ambacho wanapanga kumfanyia Roma”

“Lakini Yan Buwen si ameshakufa?”

“Hili ni tukio ambalo limetokea miezi takribani mitano nyuma Mheshimiwa kabla hata ya mheshimiwa Kigombola na Yan Buwen kufariki”

“Kama usemayo ni sahihi basi hayapingani na taarifa tulioweza kupata ya Denisi kuwa na uwezo wa ajabu si ndio?”

“Ndio Mheshimiwa”

“Kama ni hivyo kapotelea wapi?, mwezi wa pii na nusu huu haonekani nyumbani na mbaya zaidi kakomba hela zangu zote zilizokuwa chini ya jina lake katika visiwa vya Shelishei , kapeleka wapi pesa zote hizo?”

“Mheshimiwa nadhani swala hili linahusiana na kinachoendelea nchini Rwanda kwani kati ya marafiki wa karibu wa Denisi ni Desmond mtoto wa Raisi Jeremy”

“Nimejaribbu kumuhoji Jeremy lakini anakuwa mgumu wa kufunguka , lakini chanzo kinaanzia katika kifo cha mke wake, sijui nini ananificha kwasasa inanipa wasiwasi kuhusu Denisi mahali alipo kama yupo salama”

“Mheshimiwa kwanini usifanye kama ambavyo Madam anapendekeza , nadhani Mr Roma atakuwa na majibu sahihi zaidi”Alipendekeza Kabwe na kumfanya Raisi Senga kusimama akitoka kwenye kiti chake.

Ukweli ni kwamba Raisi Jeremy familia yake haikuwa na amanni hata kidogo na yote hayo ni juu ya swala la kupotea kwa Denisi , lakini vile vile kuwa na uwezo wa ajabu ambao alikuwa na uhakika ni uwezo ambao amepewa na Yan Buwen.

Mama yake Denisi yaani Damasi alikuwa na mawazo sana na muda wote ni mwenye kumbebesha Lawama mume wake kwa kutokuwa makini na mtoto mpaka kufikia katika hatua ya kupotea.

Ilikuwa ni miezi miwlii imepita sasa , tokea Denisi alivyopotea ghafla mara baada ya kuweza kukwapua kiasi kikubwa cha pesa cha baba yake alichokificha katika visiwa vya Shelisheli.

Hofu ya Damasi ni kwamba alijua fika kuna uwezekano kuna jambo baya ambalo Denisi analiandaa na hilo linaweza kumuweka katika hatari ya kuuliwa na Roma kwani kwa muda mrefu alishaweza kufahamu kinyongo cha Denisi kwenda kwa kaka yake , hivyo hofu yake ilikuwa ni kubwa mno huku akimlazimisha mume wake kuchukua hatua za haraka kuweza kunusuru hali hio kabla kubwa zaidi halijatokea.

Kilichomshangaza zaidi Senga ni kwamba tukio ambalo linamtokea yeye mwenyewe ni kama linalomtokea rafiki yake Jeremy raisi wa Rwanda, kwani wote watoto wao wa kiume ambao wanaamini kuwa warithi wao hawaonekani walipo na kila dalili inaonyesha hawawezi kuwa sawa tena.

Ilikuwa ni afadhali kwa Raisi Senga kwani alikuwa na Ashley ambaye ni mkubwa na angemrithisha kila kitu chake , lakini bado sheria za ukoo wako zinampa nafasi kubwa mtoto wa kiume.

“Kabwe nadhani kwasasa sina jinsi , ni muda sahihi wa kumkubali Den.. namaanisha Roma kama mtoto wangu”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Kabwe kidogo kutoa macho ya mshangao.

“Mheshimiwa unataka nifanye nini?”

“Blandina aliniomba nimsaidie yule msichana Najma nafasi serikalini kama hatua ya kwanza ya kujenga uhusiano wangu na Roma nadhani kwanza nitekeleze hilo”

“Ndio mheshimiwa nitakuletea faili lake”

“Haina haja, fanya utaratibu wa kuangalia nafasi gani itaweza kumfaa katika Wizara ya elimu”

“Sawa mheshimiwa”

“Kingine nitaenda nyumbani kuonana na mzee jioni ya leo na nitapata chakula cha usiku huko huko”

“Sawa mheshimiwa nitaandaa itifaki?”Aliongea na kisha akampa ruhusa ya kuondoka na kumfanya Raisi Senga kuonekana kuwa katika mawazo.

“Huenda uamuzi wangu ukawa sahihi , nikirudisha ukaribu na Roma na kuzuia hatari yoyote kumtokea Denisi nitaweza kupata faida nyingine , naweza kuushinda udhaifu walionitengenezea Freemason na naweza kurudi kwenye mstali kama kiongozi wa taifa hili”Aliwaza mheshimiwa Senga lakini muda ule ule katibu Muhtasi aligonga mlango na kumshtua katika mawazo na aimruhusu kuingia.







SEHEMU YA 552.

Ilikuwa ni saa moja za jioni , haikueleweka Roma alishinda wapi lakini muda huo alionekana ndio kwanza anarudi kuelekea Ununio nyumbani, alikuwa na haraka kwani alikuwa na miadi na Rufi siku hio kwenda kula chakula cha usiku nyumbani kwa Bi Wema , kwani tokea Bi Wema anunue nyumba ambayo anaishi na Rufi mtoto wake wa kike hakuwahi kufika.

Sasa wakati akiwa Tegeta aliweza kupokea ujumbe wa meseji ambao ulimfanya atabasamu kifedhuli ulikuwa ni ujumbe unaotoka kwa namba ambayo hajaisajili kwenye simu yake lakini kutokana na kilichotokea dakika chache zilizopita alijua nani katuma ujumbe huo na alishangaa kwa kuona kwamba mtu huyo hakuwa amekata tamaa , kwani ilikuwa ni kama mwezi mmoja umepita huenda na zaidi tokea akutane nae.

Dakika chache nyuma wakati akiwa anatokea Mbagala akiwa anapita uwanja wa taifa aliweza kugundua kuna gari inamfuatilia nyuma na licha ya kugundua hilo hakutaka kwanza kumchezea mchezo mtu aliekuwa akimfuatilia , kwani aliendesha gari kusonga mbele bila wasiwasi lakini alipokuja kupita katika daraja la Kijazi interchange Ubungo ndio alipanga namna ya kumpotezea mtu ambaye alikuwa akimfatilia nyuma nyuma.

Mtu aliekuwa anemfuatilia alikuwa ashamtambua na ilionekana pia hata mtu huyo ashajua kama ashajulikana kutokana na kwamba alikuwa akisambaza nguvu za kijini na kwa kufahamu uwezo wa Roma alijuwa atakuwa amehisi uwepo wake, lakini haikumkatisha tamaa kutimiza dhamira yake.

Roma mara baada ya kuingia katika barabara ya Sam Nujoma sehemu pekee ambaye aliamini anaweza kumpoteza mtu anaemfatilia ni eneo la Mwenge Mataa na kweli aliweza kufanikisha hilo kwani alihakikisha alikuwa mbele kabisa anagalau mbele ya magari mawili kutoka kwa mtu anaemfatilia na hio alilifanikisha na wakati tu ambao anakaribia Mwenge taa za kijani zilimruhusu kupita lakini kitendo cha kupita tu taa za rangi nyekundu ziliwaka na kuzuia magari yaliokuwa nyuma yake kupita.

Ilikuwa ni tukio la kushangaza kwani ilionekana kwa wale wanaoendesha magari kama taa hizo zilikosea kimahesabu katika kupitisha magari kwani taa iliwaka kwa sekunde sita tu na kuzima na kisha ikawaka nyekundu.

Mtu aliekuwa akimfatilia Roma katika gari aina ya Toyota Camry alitoa tusi kwa lugha ya kichina huku akigonga usukani kwa hasira na kujiapiza.

Sasa Roma alipokuwa katika eneo la Mbuyuni akikaribia Tegeta aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa namba ambayo hakuwahi kuisevu lakini alikuwa akiikumbuka ilikuwa ikimtumia meseji za ajabu ajabu.

Roma licha ya kwamba aliweza kumpoteza mtu huyo lakini wasiwasi wake ni kwa Rufi kwani aliamini kama mtu huyo ataendeea kumfuatiia na kujua anapoishi na kuja mara kwa mara basi nafasi ya kumuona Rufi ingekuwa kubwa.

Ndio alikuwa ni msichana wa kichina afahamikae kwa jina la Xiao Xiao ambaye kwa maelezo ya Rufi alikuwa anatokea katika familia ya wakwe zake katika ulimwengu wa jamii za watu wasionekana za kichina.

Roma alipotezea kwanza swala hilo na kuwa na umakini katika kuendesha gari kwani muda umeenda, ndani ya dakika chache tu aliwea kufika nyumbani kwake na laishangaa kumkuta mtu akiwa amesimama nje ya geti na alipoangalia kwa umakini alikuwa ni Rufi na ilionyesha alishindwa kuingia ndani kwani alikuwa amefunga geti kabisa wakati wa kutoka.

“Rufi kwanini umenisubiri hapa, ungekaa nyumbani kwenu tu ningekukuta”Aliongea Roma mara baada ya kusimamisha gari.

“Ni sawa tu , nilikuwa nikipata hewa safi ya bahari”

“Msichana mjinga , huwezi kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mishipa yako ya damu ni myembaba kwasasbu ya kiwango kikubwa cha nishati ya Yin, unatakiwa ujali afya yako upepo kama huu unakuumiza”

“Kweli?”

“Ndio”

“Nilipatwa na wasiwasi maana sikukuona siku zaidi ya tatu zote , nilikuwa na shauku kubwa ulivyosema utakuja kuungana na sisi kwa ajili ya chakula cha usiku, niishindwa kuvumilia ndani ndio maana nikaja kukusubiri hapa”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na matedo yake na kumwambia aingie kwenye gari waelekee nyumbani kwao , kwani ilikuwa ni upande wa pili.

Baada ya kufika na kuingiza gari ndani Roma alishuka na kumfugulia Rufi mlango na kisha alimshika mkono na kumfanya mrembo huyo kutoa tabasamu na kuona aibu kwa wakati mmoja.

Bi Wema alikuwa amenunua nyumba nzuri , ijapokuwa haikuwa kubwa kama ya kwao , lakini ilitosha familia ya watu saba na mazingira yake yalikuwa mazuri pia kufanya watu wanaoishi hapo kuonekana wa kipato cha juu , lakini ajabu kwake ni kwamba hakuwahi kuingia ndani , licha ya kwamba alipafahamu.

Baada ya kuingia ndani aliweza kuona ubunifu wa mapambo ya ndani haukuwa na utofauti na nyumbani kwake , kitu kidogo kiichotofatiana ni kwamba nyumba hio haikuwa na mapambo mengi eneo la sebuleni , ubunifu wake ulikuwa ni ule wanaoitwa Simple enterior design.

Bi Wema alitoka akiwa ameshikilia mabakuli akionekana alikuwa jikoni akiandaa chakula.

“Sir ushafika , karibu sana ndio naandaa chakula na kuna vitu vichache naendelea navyo muda si mrefu chakula kitakuwa tayari , karibu uketi”Aliongea Bi Wema kwa ukarimu.

Ukwei Bi Wema hapo alikuwa akimchukulia Roma kama Mkwe wake sio kwa Edna bali kwa mtoto wake wa kike Rufi.

“Halafu nimesahau kwenye gari nimenunu samaki , ngoja nikawalete”Aliongea Roma akitaka kutoka lakini Bi Wema alimzuia na kumpa kazi hio Rufi aifanye na Roma alitingisha kichwa kukubali na kumwachia Rufi ufunguo.

Muda wa saa mbili wakati Roma aipojikaribisha Mezani kwa ajili ya kushambulia chakula mlango wa kuingiia ulifunguliwa na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia mgeni aliefika.

“Aisee, kunanukia vizuri jamani , naona nimechelewa , Bi Wema , Rufi nimekuja tena”Ilikuwa ni sauti ya Amina na kiswahili chake kisichonyooka na alijikuta akishangaa baada ya kumuona Roma pia yupo kwenye meza.

“Mpenzi kwanini uko hapa , na wewe umekuja kwa ajili ya chakula cha usiku?”Aliuliza kwa kingereza.

“Kwannini inaonekana kama vile unakuja mara kwa mara?”Aliuliza Roma huku akiwa ameupamba uso wake na tabasamu kwa furaha ya kumuona huyo mrembo na alishangazwa siku hio kumuona Amina akiwa amevalia Shungi kichwanni na kumfanya kupendeza zaidi.

“Anasema hajisikii kula peke yake , lakini pia anapenda mapishi ya Mama , amekuwa bize kwenye siku hizi chache hatujaonana kwa muda”Aliongea Rufi.

Amina kutokana na baba yake kusafiri kwenda nje ya nchi kimatibabu kwa mara nyingine alijikuta akiishi peke yake , kutokana na kwamba hakuwa na uzoefu na maswala ya biashara za baba yake ilimchukua muda mrefu kukaa kazini na kukamilisha majukumu yake.

“Mr unaweza ukawa hujui , ukweli ni kwamba Amina na Rufi ni marafikii wakubwa na kipidi ulipokuwa nnje ya nchi walikuwa wakitoka mara nyingi pamoja kufanya shopping na aimfundisha pia namna ya kujiremba”Aliongea Bi Wema.

“Yeah mimi sio kama nakula bure nafanya juhudi pia”Aliongea Amina na kisha aliweka chini mifuko aliokuja nayo na kusogea mezani.

Roma aligundua hakuwa makini na hawa wanawake, hakuwa na uelewa kwamba Rufi na Amina wamekuwa marafiki kama iivyokuwa kwa Dorisi na Rose kuwa marafiki, lakini ilileta maana , ukiachana na kwamba wote hawakuwa wakielewa vizuri kiswahili lakini pia walikuwa na tabia zinazoendana.

Muda wote wa chakula Amina alikuwa akipiga stori na Rufi ambazo hazikuwa na miguu wala kichwa na Roma hakutaka kuingilia zaidi ya kuweka umakini wake kwenye kula.

“Halafu sikukuona wiki nzima , ulikuwa umeenda wapi?”Aliuiza Rufi na kumfanya Amina kushika shingo yake kuizungusha kuonyesha ishara ya kuchoka.

“Nimekuja kugundua kuongoza kampuni sio mchezo , tokea nirithi nafasi ya baba yaani mambo ndani ya kampuni ni mengi , wakurugenzi wa bodi kazi yao ni kunilalamikia hili halipo sawa lile halipo sawa khaa”

“Nini kimetokea kwani?”

“Washindani wetu wa kibiashara wanahati hati ya kupata tenda ya kufunga mitambo ya gesi kwenye baadhi ya hoteli na majumbani hio ni mara baada ya kupata uwekezaji mkubwa kutoka nje ya nchi , nadhani unajua tunajihusisha zaidi katika uwekezaji wa nishati , sasa kama zabuni hio tukikosa hisa za kampuni zitaporomoka maana washindani wetu wanasapoti kubwa serikalini”Aliongea huku akitia huruma.

“Lakini kampuni yenu si ilifanya Merge na baadhi ya biashara zilizokuwa chini ya Tajiri Khalifa Tanzania , bado kuna kampuni inayoweza kuwaletea ushindani?”

“Hakika ipo , mambo kwasasa yanabadilika sana tena kwa haraka sana , ni rahisi kujenga kampuni yenye msingi mzuri wa kibiashara kadri utakavyokuwa na rasilimali watu wenye talanta kubwa ya ubunifu lakini pia wenye ushawishi wa juu , Washindani wetu inapokea sapoti kubwa kutoka serikaini hivyo kazi lazima ifanyike kwa umakini katika kudili nao , najihisi muda mwingine kuzimia nikiwa ofisini”

“Hubby tafadhari msaidie Amina anatia huruma , wewe si una hela nyingi kwanini usinunue hio kampuni?”Aliongea Rufi.

“Ujinga , kwanini nifanye hivyo wakati hawajafanya hila yoyote , wameonyesha ushindani wa haki na kama nitaingilia kwasababu tu mimi tajiri itanifanya nionekane muhun na sina maadilii, hata kama nikifanikiwa kununua vipi kuhusu makampuni mengine lazima na yenyewe niyanunue ili kumuondolea ushindani, haina haja ya kuwa na wasiwasi , Amina hata kama kampuni yako ikifilisika nitakuwa na pesa za kuwatunza wote”

“Okey nimeelewa , lakini sipendi kuona akipoteza kampuni ambayo ndio kwanza amepewa kuongoza”

“Nilishawahi kujiambia kuongoza kampuni sio jambo gumu sana lakini tokea nilivyopewa majukumu yote na baba , niligundua ni kazi ngumu mno , kuna baadhi ya vitu najikuta kwenye Dilemma hata kuvitolea maamuzi , nimejikuta nikimkubali Dada Edna , Ameweza kuwa CEO wa kampuni katika umri mdogo lakini anazidi kung’ara tu”Aliongea kwa kulalamika , lakini mara baada ya kmtaja Edna moyo wa Roma ulishituka tena na hata hamu ya chakula ikapungua palepale.

“Sir sijawahi kukuuliza , Je ulienda kumtafuta Edna nakuongea nae kwenye siku hizi mbli , amekubali kurudi nyumbani?”Aliuliza Bi Wema mara baada ya kusikia jina la Edna, kwa wakati huo Bi Wema alikuwa akijua kingeereza licha ya kwamba alikuwa na ugumu kwenye kuongea lakini aliweza kusikia baadhi ya maneno na alijifunza kwa ajili ya Rufi.

Amina na Rufi walimwangalia Roma wakitaka kusikia jibu kutoka kwake kuhusu Edna, lakini swali hilo lilimfanya Roma kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Bi Wema nafikiri Edna hatorudi nyumbani hivi karibuni?”

“Kwanini unaongea hivyo , nini kimetokea?”Aliliza Bi Wema kwa wasiwasi na Roma hakuona haja ya kuwaficha na aliwaeleza mambo alioyafanya katika siku zote alizoenda kuongea na Edna na kuchomolewa.

“Bi Wema nashindwa kujua ni namna gani naweza kumaliza tatizo , nilimpelekea kifungua kinywa kwasababu nilikuwa nikimuwazia lakini badala ya kunipoktea alinishuku na Recho ambaye nilimkuta ofisini akiwa yeye hajafika kazini, kwanini akaanza kupandisha jazba na kutaka ugomvi?”Aliongea kwa kulalamika na kumfanya Rufi na Amina kiumwangalia kwa huzuni na walishindwa kuongea chochote.

“Mr Najua umekasirika namna ambavyo Edna anakufanyia lakini naamini anajua unafanya hayo yote kumbembeleza , lakini muda mwingine wanawake wanapofikiria kitu hawazingatii kipi ni sahihi na kipi sio sahihi wala kujali nani anatakiwa kuwajibika “

“Kwahio anataka nini sasa?”

“Mtazamo wako”

“Mtazamo wangu?”

“Ndio wanawake wanajali sana mtazamo wa mwanaume kwao , inaweza ikaonekena labda napindisha lakini hata kama amefanya makosa kukufanyia hivyo , mtazamo wako ndio tatizo , kwa mfano ulienda anapoishi kuomba msamaha lakini hukumtaarifu kwamba unaenda na ulienda kama vile atakusikiliza na kukusamehe hapohapo, nadhani hicho kimemfanya ajisikie vibaya zaidi , Edna anatabia ngumu sana kuzoeleka lakini ni mtu mkarimu na mwenye moyo mzuri, angekusamehe kama ungeongea nae vizuri , kuhusu kifungua kinywa cha leo nadhani usingemjibu wala kuonyesha kukasirika , alikuwa anajaribu kutafuta sababu tu ya kukukasirikia , sidhani kama alifikiria kweli kuna kitu kinaendelea kati yako na Recho”Aliongea Bi Wema na Roma aliona ni sahihi , alikuwa akijiamini sana mambo yangekuwa marahisi kwake kusamehewa , ijapokuwa aliomba msamaha kwa dhati lakini hakuonyesha uhatari wa kuona kwamba hatosamehewa alionyesha mwonekano ambao ni kama vile ni haki yake Edna kumsamehe na hapo ndio alipoona amekosea..

“Bi Wema upo sahihi , lakini bado naweza kusema mpaka sasa hatua ambayo tumefikia sidhani mambo yatakuwa marahisi na sioni sababu yake ni hasira zake juu yangu kumshuku au kuna mengine , sina mpango wa kumtafuta kwa sasa”Aliongea Roma.

“Unaonaje mimi nikienda na kuongea nae?”Amina aliongea na kumfanya Roma kucheka.

“Amina humuogopi Edna ?”

“Namuogopa ndio lakini sidhani kama atakataa kuonana na mimi , kwasababu siku zote ananichukulia mimi ni mwepesi kwake .. ninaweza kwenda na kumuuliza baadhi ya mbinu za kibiashara pia”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria.

Ijapokuwa aliona sio wazo zuri kwani lingemkasirisha zaidi Edna , ila aliona ni kheri Amina na yeye kwenda kujaribu maana yeye amekwama.
ITAENDELEA - MAWASILIANO 0687151346
Watsapp tunaelekea mwishoni mwishoni mwa hii simulizi... tunaelekea sehemu ya 700 wiki hii nicheki kama unahitaji mwendelezo
[emoji373][emoji2923][emoji373][emoji2923]
 
Imagine Toka 2022 August 10 mpaka leo tupo hapa na haijaisha, hata Ottoman kule Azam imeisha na sasa tupo na Barbarossa, mtaalam Kama anatuchora ivi eeh
 
SEHEMU YA 556.
Kitendo cha mtu aliefahamika kwa jina la Heinholtz kuonyesha msimamo wake , kundi la wanywa damu kutoka Lasombra na Brujah walianza kungurumiana.
Kucha zao zilianza kurefuka wakionyesha upande wao ambao unatisha pale binadamu wa kawaida anapowaangalia , mara nyingi wakionyesha hivyo jua wapo katika hasira.
Edna kuona kitendo kile alipatwa na kihoro cha aina yake na alichokifanya ni kukaa chini kwenye sakafu na kisha akafumba macho yake asione kile kinachoendelea.
Kwenye maisha yake hakuwahi kuangalia muvi za kutisha , sasa anapata wapi kuangalia vitu vya kimaajabu kama hivyo ambavyo vipo kwenye macho yake kabisa katika uhalisia.
“Mshipi wa kichawi bado haujaonekana lakini bado mshaanza kugombana”Aliongea mwanaume aliefahamika kwa jina la Udinese.
“Acha maigizo Udinese , darubini yetu ya ulozi haiwezi kukosea , kama tusipo upata kwenye hii nyumba basi naamini labda ni chini ya ardhi”Aliongea Heinholtz na palepale kwenye mkono wake kulijitengeneza panga refu la mita moja lenye rangi kama ya damu
“Move! Blood Bursting Slash”
Heinholtz aliongea kwa nguvu na palepale aliinua lile panga lake juu na kisha akalipigiza kwenye sakafu kwa mtindo wa kukata na palepale ulitokea mlipuko ambao haukuwa wa moto bali ni mwanga flani hivi ulichonganika na moshi wenye harufu kama vile matairi ya gari yanapochomwa na mpaka moshi unakuja kupotea palepale eneo la katikati lilijitengeneza shimo kwenda chini.
Edna alijikuta akitoa macho mara baada ya mlipuko huo na alipoangalia kwa umakini katika shimo lile lilichochimbwa kimaajabu alijikuta akihema kwa taabu ya woga mkubwa na mshangao na kuzidi kujibanza kwenye kona.
Baada ya mpasuko ule watu wale vampire wa kizungu waliangalia ndani yake na waliweza kushuhudia kitu kama mkanda flani hivi wanaovalishwa wale washindi wa kimasumbwi au wacheza mieleka, lakini mkanda huo wenyewe ulikuwa na michoro ya kizamani sana ambayo haikuwa ya kueleweka.
“Haha…. nilijua tu upo chini , Marigic Girdle!!!”Aliongea Heinholtz huku akionyesha furaha lakini hakuwa peke yake ambaye alikuwa kwenye mchecheto , Udinese pia alikuwa na mchecheto pia .
“Unacheka nini , huo sio wa kwako”
“Udinese najua wanajeshi wa Brujah ni majasiri lakini sisi tunanguvu zaidi kulinganisha na watu wenu wenye fikra finyu”
“Heinholtz hatutaogopa kupambana na wewe lakini kabla ya hapo kwanini tusiwamalize hao binadamu wa maisha ya thamani ndogo kwanza?”
“We shall see of your underlings are faster or if my peaple are crueller..”Aliongea akimaanisha kwamba wataona kama watu wake wapo na spidi au watu wake yeye ni wakatili zaidi.
Palepale walitoa ishara maalumu ya kichawi ambayo ilifahamika kwa watu wa kundi la mwanywa damu waliokuja nao na muda uleule baada ya watu hao kupata ishara kutoka kwa wakubwa wao ,mita kadhaa kutoka katika nyumba ya Edna yalisikika malalamishi ya maumivu kutoka kwa watu.
“Wametuona, waueni watu wote wa jamii ya wanywa damu haraka , pambaneni” Sauti ya mtu aliekuwa kwenye gari aina ya Noah ilisikikana palepale watu walishuka kwa haraka kutoka katika magari na kuvamia wale wa kabila la wanywa damu.
Ilionekana walikuja wengi lakini baadhi yao ndio waliongiia katika nyumba ya Edna.
Binadamu kutoka katika makundi mbaimbali ya kichawi walianza kupigana na kundi la wanywa damu , wao wenyewe walikuwa wametulia kwenye gari kwani waliamini Mshipi huo ukishapatikana kundi la Sabatt na Camarilla lazima wangeanza kugombana wao kwa wao na wangetumia mwanya huo kuchukua mshipi wa kichawi na kupotea , lakini ilionekana mpango wao sio kama walivyotegemea kwani Udinese wa kundi la Camallira aliungana kwanza na Heinholtz wa kundi la Sabbat kupigana ili kuwamaliza kwanza binadamu hao wachawi.
Uwezo wa mamwinyi(Dukes) pamoja na Makwisi (Marquises) wa kundi la wanywa damu ulikuwa ni mkubwa sana , sasa binadamu hao wangewezeaje kushinda na hapo tu Udinese na Heinholtz hawajaingilia.
Ni ndani ya dakika chache tu binadamu wote wa kawaida wa kichawi waliweza kuangamizwa na watu wa kundi la wanywa damu
“Three Dukes , eight marquises and earls Udineses is Camarila so afraid of Sabbat? Is there a need to bring so much elite over?”
“Mamwinyi watatu , Makwises nane na Udineses nyie wote ni Camarila , je mnatuogopa sana Sabbat mpaka kuleta watu wote hawa wa viwango?”Aliongea Heinholtz.
“Kuwaogopa!? , unaongea upuuzi gani , Heinholtz si wewe pia umewaleta Lashrac na Saka , wanao uwezo mkubwa kuliko mamwinyi wangu watatu”Aliongea Udineses kwa utani na kumfanya Heinholtz kumgeukia Edna aliejikunyata kwenye kona akitetemeka.
“Huyu mwanamke inaonekana anaweza kuwa chakula kizuri..”Aliongea Vampire Heinholtz huku akilamba midomo yake kwa tamaa lakini Udinese palepale alipotea na kuja kuibukia mbele ya Edna.
Edna aijikuta akihisi kitu cha baridi katika shingo yake, alikuwa ni Udinese ambaye tayari amekwisha kushika shingo yake kwa nyuma na kuipindisha kidogo na kuangalia kwa matamanio mshipa wa kijani wa damu unaopita damu kwenda kwenye ubongo.
Edna alijikuta akikosa ujasiri wa kufanya chochote , machozi tu ndio ambayo yalimtoka , ijapokuwa alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko lakini asingeweza kupambana na aina ya watu hao wanaoishi kwa kutegemea damu.
Alijikuta akikosa msaada kabisa na hakujaribu hata kujitetea na aliishia kusubiria shingo yake ikipasuliwa.
Katika wakati kama huo watu wawili ndio waliijaza akili yake , alimuwaza Roma na kujiuliza maswali je itamchukua siku ngapi kuomboleza kifo chake , vipi kuhusu Lanlan je atalia kwa muda gani pale atakaposikia mama yake amepoteza maisha, Je kama ningepunguza ujuaji nisingekuwa nyumbani muda huo nikipata chakula cha usiku na familia yangu?, maswali mbalimbali yalipita katika kichwa chake.
“Ah ..she smells so good , I haven’t smelled blood as sweet as hers , Heinholtz, this woman … I call dibs on her , I’ll enjoy the meal after I kill you”
“Ah ananukia vizuri mno .. sijawahi kuona damu inanukia utamu hivi, Heinholtz , huyu mwanamke nishamuwahi , nitafurahia damu yake baada ya kukuua”Aliongea Udinese na kumfanya Heinholtz kucheka sana.
“Kama ni hivyo basi tutaona kama utakuwa hai muda huo”Baada ya kumaliza kauli yake palepale pepo la rangi ya damu liliamka kama vile ni moto kwenye mikono yake , kutokana na kuwa katika kizazi cha tatu katika koo za wanywa damu alikuwa na uwezo wa kuita pepo mwenye nguvu wa damu ya moto.
Yule pepo wa damu ya moto alikuwa akicheza cheza kama shetani na kufanya eneo kama ni vile vyumba vya joto vya kufanyia masaji kutokana na mvuke wake.
“Saka , Leshrac hebu wadhibitini hao ndugu zetu kutoka Camarilla , nitadili na Prince Udinese..”Aliongea Heinholtz.
“Yes your Highness”
Wachawi waliokuwa ni binadamu wa kawaida walikuwa tayari washauliwa na vita iliobaki ilikuwa ni kati ya makundi mawili ya wanywa damu yaani Camarilla na Sabbat.
Baada ya Heinholtz kutoa maagizo palepale wale mamwinyi walijiandaa kushambulia.
Vita ilianza na kilchoonekana sio watu bali ni vivuli vya watu vinavyotembea kwa kasi sana kuzunguka katika jengo zima nje na ndani huku mbinu mbali mbali za kichawi zikitumika katka kupambana.
“Udinese , hebu chukua hili pepo lenye kiu ya damu ya moto”Aliongea na palepale alipotea aliposimama na alipokuja kuibuka alikuwa mbele ya Udinese na alimpiga ngumi katika uso.
Muda ule Udinese alikuwa tayari ashamtupa Edna pembeni ili asije kushambuliwa na Heinholtz na kufa kabla hajamnyonya damu.
Edna alidondoka vibaya kwa kuzunguka zunguka kwenye tailizi na ilikuwa bahati kwake kwani hakujigonga kichwani lakini wakait mmoja akihisi maumivu makali kama vile kuna mtu kakata mifupa ya mbavu zake , yaani kitendo cha watu hao kumdharau mno kilimfahya kuhisi kudhauraulika sana.
Alijitahidi kusimama huku akimkazia macho Udinese kwa hasira kali .
Udinese hakumjali Edna alichojali muda huo kwanza ni kushinda pambano, palepale alipoletewa shambulizi hakutaka kuendelea kusimama mbele ya adui yake bali alisogea upande wa kushoto kidogo na pigo likapita na aliita nguvu za kichawi na palepale kilionekana kivuli cha mbwa mwitu na kuanza kumng’ata Heinholtz, lakini bwana huyo hakuhofia hata kidogo zaidi ya kuachia shambulio lingine na kumueekezea Udinese.
“Haha.. unadhani unaweza kunikimbia , likija swala la spidi hata Sargaras hawezi kushindana na mimi , kubaliana na majaliwa yako”Aliongea na kumfanya Udinese kuzidi kujawa na wasiwasi kwani kila akisogea upande wowote Heinholzt alikuwa mbele yake na alishajua hawezi kumzidi likija swala la spidi.
“Acha kujiamini sana kama umeshinda, ngoja nikuonyeshe mshenzi wewe”Aliongea Udinese na palepale alitoa chupa kama vile ni zile za spray au manukato na kuanza kumpulizia Heinholtz na kitendo kile kilifanya pepo la Heinholtz kukosa nguvu likionyesha kuathirika.
“Dhana ya Chupa ya Sumu hio , Pumbavu kabisa”Aliongea Heinholtz kwa hasira baada ya kuona nguvu ya pepo lake likimezwa na ule moshi wa sumu ya kichawi.
Kila mwanafamilia katika jumba la kifalme anamiliki dhana maalumu na inasemekana Dhana zote takatifu za kale duniani zipo jumla yake therathini.
Hivyo mojawapo kati ya Dhana hizo ni chupa ya sumu ya kichawi ambayo harufu yake humeza kila aina ya shambuio la kiroho kwa kutumia moshi wake tu.
“Unajaribu kunishinda kwa kutumia pepo la damu , umenidharau sana , nitakufanya uonje utamu halisi wa pepo lako mwenyewe”Aliongea Udinese na palepale aliminya ile chupa kwa wingi na ikaanza kutoa moshi wa rangi nyeusi ambao ulianza kumsogelea Heinholtz kwa spidi.
Heinholtz aijua kabisa akishaguswa na ule moshi moja kwa moja angekosa nguvu na kuwa kama mtu aliepalalaizi hivyo alitumia juhudi zote kuukwepa na palepale alifyatuka na kwenda kutua eneo la juu ya nyumba hio.
“Udinese inaonekana upo siriasi sana na hili pambano , sasa ngoja nikuonyeshe , huwezi kunishinda kizembe hivyo”Aliongea na palepale kwenye mikono yake kulionekana ufunguo wenye umbo la ajabu lakini wa madini ya dhabahu na kumfanya Udinese kushanga.
“Huo si ufunguo wa Shetani , kwanini upo nao?”
“Hahaha… surprise..!!! , Raphael alijua nini kingetokea, alijua tu lazima ungebeba chupa ya sumu ndio maana akanipatia ufunguo wa shetani”
“Pumbavu zake Raphaeli”Aliongea Udinese kwa hasira na Heinholtz hakutaka kuongea chochote bali palepale aliirusha funguo ile kwenye hewa na palepale ilitengeneza kitu kama shimo kwenye anga na ule moshi uliokuwa ukimfuata palepale ulimezwa na shimo lile , likuwa kama vile ni Shimo jeusi.
Katika historia kuna uwepo wa dhana therathini ukiachana na kopo la sumu kuna uwepo ufunguo wa shetani ambao kazi yake kubwa ni kufungua geti la kuzimu.
Kwasababu nguvu zote wanazotumia zinatokana na asili ya ushetani basi palepale geti la kuzimu linapofunguka nguvu zote za giza za kiroho humezwa na kurudi kwenye koloni lake.
Kitendo cha Heinholtz kutoa ufunguo wa shetani na kufungua geti la kuzimu ilimpelekea Udinese kuanza kukosa nguvu.
Edna alikuwa kwenye kiwewe kwani kila alichokuwa akiangalia hakikuwa kikieleweka kwa akili zake za kawaida , alikuwa ni kama yupo ndatoni na alikuwa akiona maluwe luwe.
Heinholtz baada ya kuona Udinese ashaanza kukosa nguvu alimwangalia kwa tabasamu la kejeli na pale pale alimsogelea Edna na kumshika shingo.
“Hey mrembo usiogope , huwezi kuwa na wasiwasi tena wakati nikinyonya damu yako yote”Aliongea na kisha palepale aliruhusu kucha zake kurefuka.
Mkono mmoja uliomshikilia ulimfanya kumchoma kwenye kiuno na akaanza kutokwa na damu licha ya kwamba hakuwa ametumia nguvu kumdhuru.
Edna alijikuta akihisi maumivu makali huku akijaribu kufurukuta kujitoa katika mikono yake lakini hakuweza na ilimfanya kuhisi maumivu zaidi kwani Heinholtz alizidi kukaza mkono wake na kuruhusu kucha kuzama vizuri.
“Nilikuambia huyu binadamu ni kwa ajili yangu usiku huu Udinese, hebu angalia sasa ninavyoenda kumnyonya damu mbele yako na kisha nikuue”Aliongea na palepale alimshika Edna na mkono wa kulia kwenye shingo kwa ajili ya kukata mshipa wake mkubwa wa damu , Edna mpaka hapo alijuwa anakwenda kufa muda ambao kucha hizo zitaingia ndani kwenye ngozi yake ya shingo.
Alijikuta akifumba macho akiwa amekosa kabisa tumaini na kusbiria kifo chake kwani hakuwa na namna ya kujiokoa mpaka hapo.
Wale wengine mara baada ya kumuona anachotaka kufanya , walikaa pembeni na kumwangalia Heinholtz kwa macho ya kutamani kile anachokifanya wawe ndio wao, lakini sasa kabla hata hajazamisha zile kucha zake kwenye shingo ya Edna, ghafla tu kulitokea kivuli ambacho kilipita na mkono wake na kuunyofoa palepale na kumpelekea kumuachia Edna kutokana na maumivu makali.
“Wewe ni nani .. kwanini upo hapa?”Aliuliza huku akivumilia mkono wake ambao ulianza kujiponyesha kurudi katika hali yake ya kawaida.
Vampire kama hao hawakuwa na woga wa kupoteza mkono kutokana na kwamba walikuwa na uwezo mkubwa wa kupona na kuwa kawaida.
Lakini kilichomuogopesha ni kwamba alishambuliwa kwa namna ambavyo hata yeye mwenyewe hakuelewa na alijiuliza mtu huyo aliefika imekuwaje akaweza kuficha Aura yake na asionekane.
Roma palepale aligeuka na kumwangalia Heinholtz aliekuwa kwenye mshangao na maumivu.
Edna mara baada ya kugundua aliefika hapo ni Roma alijikuta akipoteza nguvu zake zote na kujidondokea kwenye sakafu na kumwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida , ikishindikana kuelezea kile ambacho anajisikia katika moyo wake.
Ijapokuwa alikuwa akihitaji Roma atokee kama muujiza na kumuokoa katika hali aliokuwa nayo kama alivyokuwa akifanya tokea wakutane lakini sasa hivi ameweza kutokea hisia zake zilikuwa katika hali ya kutoeleweka, ni hisia za mshituko , furaha na kutokuamini.
Alishindwa hata kujielewa na ule ujasiri aliokuwa nao muda mchache uliopita ulimpotea na palepale alianza kutoa kilio kama mtoto mdogo.
Roma hakujali machozi yake kabisa na hata hakujihangaisha kumzuia wakati alivyokuwa akidongoka chini.


SEHEMU YA 557.
Roma alianza kujisambazia nguvu za kijini na kufanya wale watu wote kuanza kuwa na hofu isiokuwa na kifani , ilikuwa ni nguvu kubwa zaidi kuliko nguvu iliokuwa ikisambazwa na geti la mlango wa kuzimu.
Kitendo cha kuwasambazia nguvu za kijini wale watu wote walijikuta wakijawa na woga wa ajabu ambao kwa maisha yao yote hawakuwahi kukutana nao na ilikuwa ni kama wanakiona kifo chao kabla hakijatekelezwa.
Walianza kujiuliza maswai mtu huyu ni nani ambaye amewavamia ghafla na palepale walianza kuunganisha doti na wote kwa pamoja walijikuta wakipatwa na kihoro mara baada ya kuelewa sasa hali ilivyo.
Walikuwa wakisikia habari za miungu watu na kati ya miungu hio mmoja wao aliefahamika kwa jina la Pluto ni mtu mwenye ngozi nyeusi yaani Mwafrika.
“Mama maa ni P…Pluto!!!?”
Udinese ndio aliekuwa wa kwanza kukumbuka na alivyotaja hilo jina ndio kila mmoja alitoa macho.
Jasho lilijitokezea kwenye uso wa Heinholtz huku akiwa mwekundu kutokana na ngozi yake nyeupe , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa mkubwa kutokana na kutawaliwa na nguvu ya shetani lakini mtu aliekuwa mbele yake hakuwa na uwezo wa kushindana nae.
“Mfalme Pluto sijui kwanini umeunvunja mkoni wangu lakini ninachojua hakuna chuki kati ya Sabbat na miungu yote , si ndio?”Aliuliza Heinholtz lakini Roma hakumjibu zaidi ya kusimama katika sehemu moja huku koti lake la suti lilikipepesuka na upepo.
Roma baada ya kukagua mazingira alimnyooshea kidole Heinholtz akimuonyesha ishara ya kusogea
“Njoo na ufe”Aliongea Roma kwa sauti ya chini na kumfanya Heinholtz kuwa katika hali ya wasiwasi a kusimama.
“Mfalme Pluto tafadhari usifanye utani wa namna hio , kukuheshimu kwetu haimaanishi kwamba Sabbat ni wepesi , sisi sio wajinga na lazima kuwe na sababu ya wewe kuanza kunishambulia na kama sio hivyo labda na wewe upo hapa kwa ajili ya Mshipi wa kichawi , na kama ni hivyo upo hapo hapo kwenye hilo shimo , tunaweza kukupatia hivyo hakuna haja ya sisi kupambana na wewe”
“Njoo hapa na ufe”Alirudia Roma maneno yake akimwambia Heinholtz na palepale aliachia mkandamizo wa hewa ambao ulizidi kumfanya aogope na hata wale wengine ambao walikuwa wamesimama mbali waliweza kuhisia na hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na ujasiri wa kusogea licha ya kwamba waliona jambo hilo kwao ni kama udhalilishaji.
Heinhloltz alijikuta akitetemeka kwa hasira nyingi na akaachana na swala la kuona uoga na kuvaa ujasiri na pale pale alimsogelea Roma kwa ajili ya kumshambulia.
“Umezidi , ngoja nikuonyeshe”Aliongea na palepale spidi yake ilikuwa ya juu mno kiasi kwamba hata kivuli chake hakikuweza kuonekana na alipomkaribia tu aliita nguvu ya kizimu ambayo ilikuwa kama wingu la moshi wa rangi ya majivu.
Roma alikuwa amesimama palepale na hakusogea na hata Heinholtz alivyomvaa hakuonekana kwa upande wa mbele na kuwafanya wale wengine kutoona kinachoendelea lakini kile kiwingu kilivyotoweka walijikuta wakiwa katika kiwewe mara baada ya kumuona Heinholtz akiwa amening’inia hewani ameshikwa na mkono mmoja kwenye shingo.
“Nilikuambia uje hapa ufe na sijakuambia unishambulie kwanini unaleta usumbufu”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na kumfanya Heinholtz kufurukuta ili ajitoe lakini hakuweza kabisa na alijikuta akipagwa kwani muda huo alikuwa ameruhusu mwili wake kutumiwa na nguvu ya kishetani kwa asilimia mia moja lakini licha ya hivyo hakuwa na uwezo kabisa hata wa kujitetea mbele ya Roma.,
Roma mara baada ya kuona amemshikilia vyema palepale aliita chungu chake cha kijini.
Katika kitu ambacho alikiwaza ni kwamba kama chungu hiko kilikuwa kikitumika kumeza watu wenye nguvu za kijini , itatokea nini kikimeza watu wa jamii ya Vampire.
Udinese na wenzake walijikuta wakitetemeka kwa woga mara baada ya kuona jungu la kichawi mbele yao na kushindwa kuelewa maana yake nini kwani hawakuwahi kuona mtu ambaye anatumia aina hio ya uchawi.
“Hongera kwako , umekuwa mtu wa kwanza kukufanyia majaribio”Aliongea Roma na kisha alinuia maneno na Caulron ya maafa ilikuja chini ya Heinholtz.
Na kilivyomfikia chini ya miguu yake aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikimvuta na kadri alivyojaribu kupiga piga miguu kujiondoa alishindwa kabisa.
“Hapana..!!”
Ile anamaliza kauli yake alimezwa mzima mzima na Caulrdon na akawa haonekani tena kwa nje.
Roma palepale hakujali , aliita moto wa rangi nyeupe na kisha aliutumbukiza kwenye Caudron, huku mpango wake ni kujaribu kutengeneza kidonge cha kijini kwa kutumia mwili wa Vampire.
Wale wanywa damu waliobakia walichoweza kusikia ni upepo tu wa Heinholtz kumezwa na kile chungu na baada ya hapo kikatulia tuli na hata lile geti la kuzimu lilijifunga palepale kutokana na kufa kwa Heinholtz.
Roma aliweza kuhisi nguvu ya kichawi ikitoka kwenye kile chungu mara baada ya Vampite kuyeyuka na aliona huenda ni kwasababu pepo liliouvaa mwili wake limeshindwa kutoroka ndio maana kuna furukuto ndani yake la nguvu za kichawi.
Roma alijikuta akiona hakuna cha maana alichofanya kwani hakuna kitu chochote kilichotokea nje ambacho kingeongeza nguvu ya chungu chake.
Ikumbukwe Dhana ya Caulron ilikuwa na uwezo wa kupanda levo pia kadri Roma anavyopanda levo , lakini pia kama chungu hiko kitameza mtu yoyote mwenye nguvu za kijini moja kwa moja zile nguvu zake zingejigawa kati ,zingine zingebakia kwenye Caudron na zinazobakia zingekuja kwake hivyo angekuwa ameongeza uwezo wake , lakini kwa Vampire hao hakukuwa na aina ya nguvu zozote zilizotoka zaidi ya msisimko wa nguvu za kichawi pekee ambao ulimvaa na kmfanya kaunza kuona vitu visivyo vya kawaida.
Roma alijikuta akipatwa na hisia ambazo zilimpa ufunuo wa aina yake na kugundua huenda hayupo mbali na kuingia katika levo ya kudhibiti elementi za maji , yaani oksijeni na haidrojeni na kutengeneza maji ya kiroho(Ultra purity spiritual water).
Kama angefanikisha hivyo basi moja kwa moja angefanikisha kuwa na siraha ambayo ingekuwa na uwezo wa kumwagia kiumbe chochote na kukiondolea uwezo wake kwa kukisafisha.
Inasemekana katika miliki za kijini Maji ya kiroho yanaogopwa sana kwasababu yanabeba nguvu ambayo ina uwezo wa kusafisha uwezo wa mtu wa nishati za mbingu na ardhi, na sio hivyo tu hata kwa wachawi wa kawaida pia walikuwa wakiogopa sana Maji ya kiroho.
Kwa upande wa Roma hio ilikuwa ni levo ya mwanzo ya kudhibiti elementi za maji kabla ya kufikia levo ya kugandisha au kugeuza mtu kuwa barafu.
Roma akili yake ikiwa inapambana na msisimko wa nguvu za kichawi uliokuwa ukitoka kwenye kile chungu palepale aliita nguvu za kimaandiko na kuzielekezea katika mikono yake, nalifanya hivyo bila hata ya kujielewa ni kama moyo wake ulikuwa ukimwambia cha kufanya na baada ya kukusanya nguvu zake katika kiganja cha mikono palepale aliita na nguvu ya mbingu na ardhi na kisha akauganisha na mvuke wa anga na kulitokea vitu kama mapovu yakielea hewani.
Udinese na wenzake mara baada ya povu lile kutokea walijikuta roho zao zikifurukuta na ilikuwa ni kama kuna kitu kinawavamia rohoni.
“Hahaha… Pure water , Maji ya kiroho”Aliongea Roma akionyesha kufurahi mara baada ya kufanikisha kugundua mbinu ya kutengeneza povu la maji ya kiroho.
“Mfalme Pluto asante sana kwa kuokoa maisha yetu , tutaondoka hapa haraka ili tusikusumbue”Aliongea Udinese baada ya kuona anashindwa kuvumilia msisimko ambao ulikuwa ukipingana na nguvu zao.
“Msisogee , hili halijaisha bado”Aliongea Roma na kumfanya Udinese kutetemeka na kumwangalia.
“Je una maaagizo yoyote kwetu?”Aliongea lakini Roma hakuwajibu na kuangalia Cauldron yake ya maafa.
“Nataka majibu ya maswali yangu , huyu mwanamke ambaye amekaa chini nani ambaye amemgusa?”Aliuliza na kumfanya Udinese kujawa na kihoro kutokana na swali lake na kumfanya Roma kugundua kitu katika macho yake na alianza kupandwa na jazba.
“I… I”Alijikuta akitaka kuongea ila alisita lakini mmoja wa wale watu wa kundi la Sabbat waliingilia.
“Your Majesty Pluto , it’s Udinese he is the first person to hurt this lady , he is culprit”Aliongea akimaanisha kwamba ni Udinese na ndio mtu ambaye ni wa kwanza kumgusa Edna na yeye ndio mshukiwa.
Vampire Lasombra alijitahidi kuongea ili kujiokoa katika hali hio baada ya kushuhudia kifo cha mtoto wa mfalme Heinholtz na mpaka hapo waliona chaguo la pekee ni Roma kumuua Udinese na kuwaacha wao.
“Unaongea ujinga ,Heinholtz ndio ambaye amemuumiza huyu mwanamke , alitaka kumnyonya damu wala sio mimi”Aliongea na wale walimrudishia kwamba yeye ndio aliekuwa wa kwanza na upande wa kundi la Bruja waliwaambia Heinholtz ndio alimuumiza Edna, walianza malumbano ya kurushiana mpira wao kwa wao kila mtu akivutia kwake.
“Acheni kelele , kwanza kabisa haina haja ya nyie kulumbana wenyewe kwa wenyewe”
“Mfalme Pluto sio mimi kweli “Aliongea huku akitingisha kichwa kwa woga.
“Haijalishi ni nani kati yenu , wote nyie mnastahili kifo”Aliongea Roma akiwa kwenye tabasamu .
“Mfalme Pluto huwezi kufanya hivi , si wewe ni mshrika na kundi la Camarilla je haumkumbuki rafiki yako Marquess Lilith"Aliongea Udinese akijaribu kubembeleza.
“Rafiki!! , kama nyie ni marafiki kwanini mmeshindwa kumfahamu mke wangu na kutaka kumnyonya damu , halafu bado mnajinasibu na urafiki”
“Ah…”Udinese alishindwa kuongea neno zaidi ya kupanua mdomo wake kwa wasiwasi baada ya kujua Edna kumbe alikuwa mke wa Pluto.
Wale Vampire waliangaliana na palepale walipeana ishara ya kukimbia , walijiambia kama Heinholtz ameweza kuuliwa wao ni nani hadi waachwe hai.
Lakini bahaii mbaya ni kwamba Roma hakurudisha chungu chake na wakati ambao wanapanga kukimbia palepale lile jungu kama tanuru liliwageuzia mdomo upande wao na kuaanza kuwavuta wote kwa pamoja.
Roma palepale alitengeneza maji mengi ya kiroho na kuyalekeza aliposimama Udinese na ile yanamkaribia , ni kama vile ameguswa na tindikali kwani alianza kubadilika ngozi na ikaanza kuyeyuka.
Dakika mbili tu hakukuwa na mtu yoyote aliebakia katika hilo eneo akiwa hai kwani wote walimezwa na chungu cha maafa hivyo amani ikarudi upya.
Roma baada ya kurudisha chungu chake palepale alimgeukia Edna na kumwangalia na Edna na yeye alimwangalia mume wake kwa macho yasioelezeka.
*******
Ni juu kabisa ya kilele cha mlima kilimanjaro muda huo huo ambao Roma alikuwa akipambana na Vampire..
Sasa basi juu kabisa ya eneo la kilele ambalo limefunikwa na barafu , alionekana mwanamke mmoja mrembo akitembea peku peku akikanyaga barafu bila ya kuathirika na ubaridi.
Mwanamke huyo alikuwa kama vile ni mchoro wa kizamani kutokana na aliivyokuwa akionekana , alikuwa amevaa gauni refu la rangi ya kijani la kitambaa cha hariri , ni gauni ambalo lilikuwa ni kama yale yanayovaliwa na wanawake wa kiarabu maarufu kama Abaya.
Alikuwa mrembo haswa na shepu yake ilionekana waziwazi licha ya kwamba alikuwa amevalia gauni hilo kuu kuu ambalo halikuwa na udarizi wa kibunifu.
Alikuwa na nywele ndefu mno kama vile ni wale wanawake wa Korea kusini wanaoneana katika filamu za kihistoria akiwa amezibana kwa kuchomeka pini ambayo ilmetengenezwa kwa kunakshiwa na Lulu.
Ki ufupi mwanamke huyo ni wa rangi nyeupe mwenye macho yake yenye kiini kama vile ni rangi ya anga.
Baada ya mwanamke yule kusimama kwa muda kidogo , kivuli cha mtu alievalia nguo nyeusi kilionekana na kutua karibu na yule mwanamke .
Alikuwa ni mwanaume ambaye amevalia koti refu la rangi nyeusi, huku nywele zake zikiwa ni nyeupe maarufu kama Blonde hair , alikuwa ni kijana mno na uso wake wa kuvutia.
Mwanaume yule hakuwa mwingine bali ni kiongozi wa kundi la Tzsimisce ambae anafahamika kwa jina la Raphaeli lakini pia akifahamika kwa jina la siri la Hermes.
Hermes mara baada ya kumwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake kwa dakika kadhaa alionyesha tabasamu hafifu.
“I like how you’re dresssed today”Aliongea Hermes akimwambia yule mlimbwende kwamba amependa namna ambavyo amevalia, lakini licha ya kutoa sifa hizo , yule mwanamke alimwangalia kwa macho makavu.
“Mpango wetu umeendaje?”Aliuliza kwa kingereza yule mwanamke.
“Mpango umefeli , hata kwa kutumia mbinu ya kilozi ya Athena ya unabii bado tu imeshindikana kutabiri muonekano wa mkanda ule wa kipekee wa hali ya chini lakini bado ni mzuri kuliko wa kwetu”
“Mhmh , nadhani ni bahati tu”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli na kumfanya Hermes kucheka.
“Vipi lakini kuhusu wewe , je tayari umemkamata yule mtu?”
“That man is extremely cunning , it’s easy to win him over but to get him .. its quite arduous .. but I will get him soon or later”Aliiongea akimaanisha kwamba yule mwanaume ni mjanja sana lakini ni rahisi kumshawishi lakini kumpata ni ngumu , lakini nitampata tu mapema au baadae.
“Kama ni hivyo basi unapaswa kuharakisha , Athena tayari ashapata moyo wa Gaia , ijapokuwa mpango wake una hatua nyingi lakini yeye ndio kaanzisha kwa haraka , kama tutasubiri mpaka akianzisha kila kitu yeye mwenyewe hatutokuwa na nafasi”
“Je unafikiri mpango wake utaendelea vizuri? Ana asilimia therathini tu ya uwezo wake na uwezo wake wa kinabii bado una shida nyingi , vinginevyo asingeingilia kuweka mambo sawa”
“Nina wasiwasi kama mpango wake utafanikiwa, si ataendelea na tabia yake ile ile ya kutaka kutawala akili zetu kwa miaka mingi kama alivyokuwa akifanya katika sayari yetu?”
“Unaogopa nini , kiwango cha uwezo wake kinaweza kuwa kikubwa lakini haitokuwa ngumu kwangu kuimarika, lakini hata hivyo uwezo wangu ni wa tofauti kabisa na wa kwake tokea mwanzo lakini siwezi kuwa na wasiwasi kwasababu mbinu zinazotumika katika miliki za kijini ni nzuri zaidi na pia wana dhana ambazo wamerithi kutoka vizazi vilivyopita ambazo zina uwezo mkubwa , dhana ambazo ni ngumu kushidana nazo, kitu kingine mimi na yeye tunao utofauti, yeye anahitaji moyo wa Gaia kurudisha nguvu zake zote na kutawala upya lakini kwangu mimi hakutakuwa na athari zozote “Aliongea na kumfanya Hermes kutabasamu vibaya.
“Nadhani upo sahihi , kwanini usimfanye yule mtu akatengeneza tena dhana feki kwa mara nyingine ili niendelee kufurahia kamchezo”
“Haina haja, ijapokuwa hawezi kukuua lakini anao uwezo wa kukulazimisha upitie hatua ya kuzaliwa upya kama alivyofanya kwa Hades wa zamani na ukiangalia uwezo wako naamini itakuchukua miaka sita au kumi , nadhani mpaka hapo utakuwa umechelewa sana”Aliongea na kumfanya Hermes kukunja sura na kukosa neno la kuongea.
“Ukiachana na hilo , vipi kuhusu Apollo , Poseidon na wengine ni kipi wameweza kusema?”Aliuliza yule mwanamke.
“Kuhusu wao! Mhmh... , kundi lote hilo linamuogopa Athena na hawana ujasiri wa kumpiga kwa lolote , hatuwezi kuomba msaada kutoka kwao kwani haiwezekani nadhani tujifanyishe hatujui kitu kwa sasa na tuendelee kuangalia nini kinaenda kutokea”
“Basi ni sawa , hata kama Athena ni kama shetani ambaye anastahili kifo lakini bado ni ndugu yetu… mimi sina tatizo na mpango wake wa kufufua moyo wa Gaia lakini kama ndugu zetu roho zao zitaamka siamini kama tutaweza kuwa kama ilivyokuwa kwenye sayari yetu”Aliongea na kumfanya Hermes kutabasamu kisiri siri na palepale alijikuta akitoa macho kama mtu ambaye ana furaha.
Unafikiri mwanamke anaeongea nae Hermes ni nani , kuna mpango gani wanapanga na kwanini anasema mbinu za kijini ni nzuri , je na yeye ni sehemu ya miungu ambaye amechagua kujifunza mbinu za kijini? Kumbuka kati ya miungu ambayo iliweza kutawala roho za binadamu jumla yao ni kumi na mbili ukimuondoa Zeus na Hades wa Zamani ambao haijulikani walipo , kuna Apollo ambaye tushamjua , yupo Artemis , Aphrodite , Poseidon ,Hermes na Athena ambao jumla yao ni saba kama ni hivyo watano wako wapi?
ITAENDELEA.
[emoji2923][emoji373][emoji120]
 
Imagine Toka 2022 August 10 mpaka leo tupo hapa na haijaisha, hata Ottoman kule Azam imeisha na sasa tupo na Barbarossa, mtaalam Kama anatuchora ivi eeh
Barbarossa ipo pia DSTV,ni hiyohiyo au kuna nyingine?
 
Imagine Toka 2022 August 10 mpaka leo tupo hapa na haijaisha, hata Ottoman kule Azam imeisha na sasa tupo na Barbarossa, mtaalam Kama anatuchora ivi eeh
Kuna wahusika wengine hadi nimeshaanza kuwasahau ikiwemo Clelia Allisanto, wale wazungu majirani wa msaidizi/ mke mwenza wa Edina yule alokuwa na black card ya benki. Halafu kaanzisha story nyingine wakati hii bado episodes Kama 200 hivi ndo iishe. Maana kule group walishafika ep700+ na bado gaijaisha.
 
kuhus nadia nakumbuk aliwah kupokea sim akifokewa kua kapew kz aifanye kuhus roma ila bado hajaikamilisha na boss wake alikasirik sana, nadhan bos mwenyew alikua ni apollo fek
Mule mule, umepatia. Hata hivyo, Edna naye sio wa kawaida maana alitakiwa kutenganishwa na Roma ili kufanikisha malengo ya Appolo feki. So kuna ka chain si ka kawaida katika hii riwaya. Hadi utulie sana ndo unaweza kuelewa kwa mbaaaaaliiiii.
 
Barbarossa ipo pia DSTV,ni hiyohiyo au kuna nyingine?
Sijui mkuu lakin hii ya Azam ni muendelezo wa Otugrral na Othoman, Kama hiyo inausu maudhui hayo ya Waturuki huenda ikawa yenyewe
 
SEHEMU YA 238.
“Kabla sijaendelea kuelezea naomba kuuliza swali?”Aliongea The First Black kwa wasiwasi.
“Unaweza kuuliza , lakini ni swali moja tu nakuruhusu”Ilisikika sauti ya Athena ndani ya chumba hiko cha hoteli na The First Black alivuta pumzi.
“Kwa miaka mingi nimekuwa nikiishi chini yako na kukutii kwa kila maelekzo uliokuwa ukinipatia na kuhakikisha nakupatia majibu ambayo yanakuridhisha , lakini pia niliamini katika kichwa changu unao uwezo wa kujua kila kitu ndani ya dunia hii na kutokana na hilo nimekuwa nakuheshimu sana , lakini kazi hii ya kuwafuatilia wanachama wote wa Illuminat imenishangaza, hivyo swali langu ni kutaka kujua kwanini unawatafuta hawa wanachama?”Aliuliza The First Black.
“Nikitaka kujibu swali lako kwa ufahasa , lazima uelewe historia yangu ya nyuma miaka mingi tokea kufika kwetu ndani ya uso wa dunia, nadhani unakumbuka mara ya mwisho nilikueleza kuwa sikufika kwenye dunia hii peke yangu?”
“Ndio nakumbuka?”
“Basi jibu ni kwamba nawatafuta ndugu zangu niliokuja nao na naamini kwa asilimia mia moja wamejificha chini ya hili kundi la Illuminat, nina mpango unaoendelea na ili kufanikiwa kwa mpango wangu nikuhakikisha nakuwa na kila jina la mwanachama wa Illuminat ndani ya dunia hii”Aliongea Athena.
“Asante kwa jibu lako”
“Huna haja ya kunishukuru , nimekujibu kwakua nataka majibu yangu kukusaidia katika kazi yako , hivyo huu ni wakati wako wa kunielezea Illuminat ni kundi lipi na Freemason ni kundi lipi”Aliongea .
“Mimi ni mwanachama wa Illuminat , naomba unisaheme kwa kukuficha juu ya hilo”Aliongea The First Black kwa wasiwasi mkubwa lakini muda ule ule aliijikuta akikosa hewa na kuanza kukohoa mfululizo huku akiwa ameshikilia shingo yake kama mtu anaekabwa.
“Nao..mba uni..sa.. mehe , nilikuwa na sababu ya kutokukueleza”Aliongea huku akilala kwenye sofa kwa namna ya kurusha rusha miguu kama mtu anaekata roho na tukio hilo lilidumu kwa muda wa dakika chache tu na alimuachia.
“Biuadamu tabia yenu ya kusema uongo inaniudhi sana na inanipelekea kuwachukia kila siku”Ilisikika sauti ya kike , licha ya kwamba ilikuwa ikiashria hasira , lakini bado ilikuwa nyororo.
“Nitakueleza ninachokijua kuhusu Illuminat , naomba unisamehe kwa kukuficha”Aliongea The First Black na kisha akavuta pumzi na kuweka akili yake sawa.
“Illuminat kama nilivyosema kiasili sio waanzilishi wa kundi la Freemason , bali Illuminat waliomba hifadhi ya kujificha ndani ya kundi hili la Bavarian la wajenzi huru , ambao enzi hizo walikuwa na utajiri mkubwa, sababu iliowafanya wajifiche chini ya kundi la Freemason ni kutokana na kwamba walikuwa wakiwindwa sana na serikali ya Kirumi… “Aliongea na kisha akaendelea.
Kwa maelezo yake ni kwamba Mwaka kati ya 1700 kuendelea ndani ya mamlaka ya Rumi kuliibuka wanasayansi wengi ambao walikuwa wakifanya gunduzi mbalimbali , kulikuwa na wanasayansi wabobezi katika maswala ya hesabu , kuna waliokuwa wamebobea katika maswala ya biolojia na mashine lakini pia kulikuwa na wanasayansi walibobea katika maswala ya anga.
The First Black anaelezea kwamba baada ya gunduzi hizi kufikia serikali ya kirumi ambayo ilikuwa ikiongozwa kwa misingi ya dini, walikasirishwa na baadhi ya gunduzi za wanasayansi hao kutokana na kwamba zilikuwa zikipingana na maandiko matakatifu na hili liliibua uhasama sana kwa watu wa dini na kuona wanasayansi hao wanapingana moja kwa moja na dini kutokana na tafiti zao ,na hapo ndipo serikali ilipoanza msako wa kukamatwa kwa watu waliokuwa wakijiita wanasayansi , na serikali iliwakamata na kuwatesa huku ikiwataka wanasayansi hao wabatilishe baadhi ya kauli zao.
Sasa basi baada ya serikali kuzidi kutesa na kuua wanasayansi wengi , ilipelekea hofu kwa wanasayansi wengine ambao hawajafikiwa na serikali na kupitia hofu yao iliwafanya wakusanyike kwa siri sana kwa ajili ya kuzungumza mustakabali wao wa kuendeleza sayansi na teknolojia, baada ya kufanikiwa kukutanika kwa siri waliamua kujipatia jina kwanza ili kujiongezea hamasa na ujasiri ,na ndipo walipojipatia jina la ‘Enlightened ones’ yaan Illuminat.
The First Black anaelezea kwa kusema kwamba dhumuni ambalo liliwafanya wanasayansi hawa kukutana ni kwa ajili ya kutaka kuanzisha vita na watu wa dini kutokana na tabia yao ya kuwakamata na kuwatesa , jambo ambalo lilipingwa vikali na mwanasayansi mmoja maarufu ambaye pia alikuwa ni mtu wa dini kindakindaki , mwanasayansi ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Galilei Galilleo.
Gallileo aliwapinga wenzake kwa mpango wao wa kuanzisha vita kwa madai ya kwamba sayansi na Dini ni vitu viwili vinavyotegemeana na kwamba Sayansi ipo kwa ajili ya kuimarisha na kuipa nguvu dini , hivyo akawaasa wanasayansi wenzake wasifanye fujo bali yeye yupo tayari Kwenda kuzungumza na watu wa dini juu ya kwamba sayansi haipingi uwepo wa mungu Zaidi ya kwamba inaipa nguvu dini kimaarifa.
Sasa kwasababu Gallileo ndio aliependekeza swala hilo , wanasyanasi wakaona wajaribu kuongea na watu wa dini.
Kabla ya hapo Gallieo alikuwa tayari ashagundua kwamba dunia ilikuwa ni duara lakini pia Dunia ndio inazunguka jua na sio jua kuzunguka dunia na aliweza kugundua kutumia darubidni yake.
Sasa gunduzi yake ilikuwa ikipingana na watu wa dini waliokuwa wakiamini kwamba dunia ni tambarare na haiwezi kuwa duara na jua ndio linaiuzunguka dunia, sasa Baada ya Gallieo kutangaza gunduzi yake alianza kuwindwa na watu wa dini na alionekana kama kichaa na mtu anaeenda kinyume na mafundisho ya dini , hivyo akaingia kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na watu wa dini.
First Black anaelezea kwa kusema kwamba kundi lote la Illuminat ambao sasa ni wanasayansi , walipendekeza Galileo Kwenda kuongea na watu wa dini juu ya pendekezo lake, na Gallielo hakupinga kwanza alikuwa akipenda sana dini licha ya kuwa mwanasayansi hivyo alifanya maamuzi ya Kwenda kuongea na watu wa dini, na alipoweka swala lake wazi , palepale alikamatwa na kuingizwa kwenye chumba cha mateso huku akilazimishwa kubatilisha kauli yake ya kwamba dunia ni duara, lakini Galileo hakuwa tayari kubatilisha kauli yake na alisimamia msimamo wake , jambo ambalo liliwaudhi watu wa kanisa na kuamua kumfunga ndani ya chumba cha gereza lenye giza mpaka umauti wake.
Sasa huku wa kundi la illuminat baada ya kuona mpango umebuma walianza kutoroka nje ya mamlaka ya kirumi na Kwenda mbali Zaidi nje ya mkono wa serikali , wakitafuta eneo zuri Zaidi kwa aijili ya kujunda upya, na katika heka heka zao ndipo walipokuja kukutana na kundi lingine linalofahmika kwa jina la Freemason na Kundi la Illuminat ndipo walipamua kujiunga nao kwa kuomba hifadhi ndanni ya kundi hilo.
Na kwanzia hapo kundi hilo la wanasayansi walitumia jina la Freemason kuendeleza Imani yao ya kuamini katika sayansi na kipindi ambacho wanakubaliwa kuingia , kundi la Freemason lilikuwa na wafuansi wengi mno kuanzia Amerika yote mpaka kufikia baadhi ya nchi za Ulaya na walikuwa washajenga mpaka Lodge za kufanyia ibada zao.
“Kwa maelezo yako Illuminat waliamua kutumia jina la Freemason kuendeleza mipango yao ya maendeleo ya kisayansi?”Aliuliza Mrembo The Doni.
“Ndio na baada ya wao kujiunga na Freemason kundi lao lilipote na kuwa Dormant”
“Kwa maelezo yako ni Dhahiri kwamba huwezi kutenganisha Freeason na Illuminat?”
“Ndio kwasababu Freemason , licha ya kwamba hatuamini uwepo wa Mungu , lakini pia Freemason tunaamini Zaidi katika utajiri na huo ndio msingi wa dunia hii”
“Kwenye vikao vyenu mnazungumza nini kuhusu mimi?”
“We Believe you are one of us”
“Tunaamini wewe ni mmoja wetu”Aliongea The First Black.
********
Mheshimiwa Senga alimkaribisha Kigombola kwa tabasamu la kinafiki mtangulizi wake mara baada ya kufika ndani ya ukumbi wa ikulu wa kuonana na wageni na kwa upande wa Mheshimiwa Kigombola , alikuwa akijua kuwa tabasamu la Senga ni la kinafiki kwasababu Mheshimiwa Kigombola hakuwa chaguo lake katika kumrithisha uongozi , ni hivyo tu kwamba wazee wachama ndio waliokuwa na nguvu Zaidi , hivyo kumfanya ashindwe kushindana nao na kuweka mtu anaemtaka yeye.
Baada ya kusalimiana kwa dakika kama kumi na tano huku vicheko vya kinafiki vikiendelea, Mheshimiwa Kigombola alienda kwenye jambo ambalo limemfaya kuja hapo ikulu.
“Nina uhakika ushapata taarifa juu ya mimi kuonana na baadhi ya viongozi wakubwa wa ulinzi , akiwemo jenerali Tozo?”Aliongea Mheshimiwa Kigombola na kumfanya Senga kushangaa kidogo na kushindwa kufahamu nia ya mtangulizi wake.
“Ndio nimeipata na imenichanganya sana mimi kama mkuu wa Nchi kuona viongozi wa chini yangu wanafanya mambo pasipo kunishirikisha”Aliongea Senga na kumfanya Mheshimiwa Mstaafu kutabasamu.
“Nazifahamu hizo hisia kwasababu hata mimi nishawahi kuwa katika nafasi yako, niende moja kwa moja , kwanza kabisa mimi ndio niliowaita kwa ajili ya kuzungumza nao na swala ambalo tumezungumza ni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa hili”
“Wiki kadhaa nyuma nilipokea ugeni kutoka taifa la China na sikuelewa kwanini Jenerali wa jeshi la wananchi wa China aliagiza mgeni kuja moja kwa moja kwangu, lakini naweza kukisia dhumuni lao”Mheshimiwa Senga alishangaa maana hakuwa na taarifa hio.
“Mheshimiwa Senga kuna siri ambayo sikukuambia baada ya kuachia madaraka na leo hii nipo hapa kwa ajili ya kuiweka wazi”
“Siri!!!”Mheshimiwa Senga alishangaa .
ITANDELEA JUMAPILI MCHANA

0687151346 .WATSAPP NICHEKI TUONE NAMNA YA WEWE KUENDEKEA KUBURUDIKA
238
SIRI
 
Sijui mkuu lakin hii ya Azam ni muendelezo wa Otugrral na Othoman, Kama hiyo inausu maudhui hayo ya Waturuki huenda ikawa yenyewe
Kwa hiyo Othman Bay bado sterling huko Azam? DSTV Hakuna Othman Bay
 
bado episodes Kama 200 hivi ndo iishe. Maana kule group walishafika ep700+ na bado gaijaisha.
Kule kwa group ni mwendo was kuliwa buku 5 tu 😂

Group lilishatelekezwa ila ukilipa unaungwa ili uvisome hivyo vi episode vilivyotolewa then unaachwa kwenye mataa 😂😂
 
Back
Top Bottom