SEHEMU YA 561.
Hata kwa Faridi mwenyewe alishangazwa na kuhusishwa katika swala hilo na mshangao wake ulimfanya Roma aamini kwamba Faridi hakuwa akijua chochote na hakuwa akiongea ukweli.
“Nadhani mtu ambaye amefanikisha hilo sio mdogo kwako kwa namna ambavyo amefanikisha kukuchezea akili na wewe kushindwa kumfahamu”.Aliongea Farid.
Roma aliona hakika mtu huyo hakuwa wa kawaida kabisa , kama kweli ameweza kutengeneza sura ya udanganyifu na kumuigiza Farid basi kweli mtu huyo ni wa levo nyingine na hapo hapo akili yake ilijiambia huenda aliemfanyia hivyo ni Raphael.
Hermes pekee ndio aliekuwa na uwezo wa kutengeneza Illusion na mtu yoyote asione utofauti, kama ingekuwa ni mtu wa kawaida ambaye alicheza na akili yake basi asingeweza kumdanganya kijinga.
Roma alikumbuka kipindi wakati alipotaka kumuua Denis ni Hermes ambaye aliingilia kwa kumtengenezea udanganyifu kwa kumuona Denisi akimuua mama yake mpaka kughairisha.
Alijiambia kama ni Hermes basi inaleta maana kutokana na uwezo wake kulingana na wa kwake , kwa kutumia siraha yake tu maarufu ya kichawi iliofahamika kwa jina la Caduceus anaweza kuwafanya hata ndugu zake kuwa katika hali ya usingizi wa ndoto.
“Nadhani nishajua nani kafanya hivyo lakini nashindwa kuelewa nia yake halisi”Aliongea Roma na Farid alitingisha kichwa kuelewa .
Balozi Ramadhani aliondoka kuelekea Dodoma na kazi iliokuwa inabaki ni Roma na Edna kutafuta njia ya kusafisha jina la Sophia na kutuliza hali ya hewa.
Mchana wote Edna alikuwa bize kushughulika na swala hilo , Roma ndio ambaye alipaswa kushughulika na swala hilo kama mkuu wa kampuni ya Vexto Media lakini kwasababu yeye amehusishwa na pia lilimuhusu Sophia aliona aingilie majukumu ya Roma kumsaidia.
Ingekuwa rahisi kudili na swala hilo kama watu waliokuwa wakisambaza ni waajiriwa wa kampuni flani , lakini kwasababu ni watu binafsi waliokuwa wakisambaza na kuongezea chumvi ilimfanya Edna kushindwa kuzuia swala hilo mara moja na kukosa kabisa namna ya kudili nalo moja kwa moja.
Kilichomchukiza zaidi watu walitumia uzushi huo kupata ‘attention’ kutoka kwa watu ili kufanya peji zao mtandaoni zifatiliwe kwa wingi.
Roma alijikuta akichukia mno kwa jinsi ambavyo Edna alikuwa akihangaika kudili na swala hilo.
Baada ya muda wa kazi kuisha Roma alimlazimisha Edna kuondoka nae kurejea nyumbani.
Edna alikuwa akipanga kufanya kazi mpaka jioni ili kushugulikia hilo swala lakini alishindwa kumshawishi Roma kumuacha ofisini na mwishowe akaamua kumkabidhi majukumu yote Benadetha kushughulika nayo.
Muda wa kutoka kazini ni kama waandishi wa habari walikuwa wakimsubiria kwani walijaa katika eneo la kuingia ndani ya kampuni hio wakiwa na kamera zao pamoja na vifaa vya kurekodi sauti , walionekana walitaka kusikia chochote kutoka kwa Edna.
Roma alimwagiza Recho kuachana nao na asitokee mfanyakazi yoyote kuongea chochote , hata hivyo hawakuwa na cha kuongea kwani kinachoendelea hakikuwa na ukweli wowote na hata kama wakanushe hakuna ambaye angeamini na wangeendelea kuuliza maswali yasio na msingi , lakini kubwa zaidi Edna hakuwa mtu wa kupenda kuongea ana kwa ana na vyombo vya habari kwani hakupenda sana umaarufu.
Ilibidi wapitie moja kwa moja kwenye Basement katika eneo la maegesiho na baada ya kuingia kwenye gari , Roma aliliondoa na kulipeleka moja kwa moja mpaka nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani Lanlan alikuwa tayari ashatoka shuleni na alikuwa akiangalia katuni , baada ya kuwaona wazazi wake wamefika nyumbani aliwakimbilia na kumsalimia mmoja mmoja kwa kuwakumbatia na kisha akakimbia na kurudi kwenye sofa.
Alionekana kukolea kile ambacho alikuwa akiangalia na Edna na Roma waliangaliana na kuishia kutabasamu.
Edna kidogo alijisikia vizuri mara baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku pamoja na familia yake .
Waliangalia Tv Pamoja mpaka wakati ambao Lanlan alipotelea usingizini na Qiang alimbeba na kumpeleka juu kulala wakati huo Edna alimwambia Roma amfuate hadi kwenye Yadi kuna kitu waongee.
Roma na yeye alikuwa akitarajia Edna kumwambia kile ambacho anafikiria , kwani alimuona wakati wote akiwa ni mwenye mawazo.
Baada ya kukaa kwenye viti maalumu vilivyoweka kwa nje katika Yadi , Edna alivuta pumzi nyingi na kisha kumgeukia Roma.
“Hubby si ulishaniambia utanitimizia chochote na kunisikiliza ili mradi tu sikulazimishi kuachana na wanawake wako?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake na kujiuliza inatokea wapi.
“Nilisema hivyo lakini sikumaanisha katika kila ombi”
“Kwahio unavunja ahadi yako?”
“Kama utaomba kuniacha ulifikiri nitaweza kukubaliana na ombi lako , sijali kama utachokoza mtu mwingine kwani nitakusapoti muda wote”
“Nilijua tu utasema hivyo”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma kwa jicho la pembeni.
“Kama ni hivyo basi naomba nikuulize , je ni kweli kwamba hutonipinga kwa maamuzi yoyote nitakayoyafanya yanayohusiana na kampuni ya Vexto?”
“Bila shaka , kampuni imeasisiwa na wazazi wako na wewe ni urithi wako , sina mpango kabisa wa kuingilia taaluma yako pamoja na uendeshaji wa kampuni”Aliongea Roma bila ya kufikiria na kumfanya Edna kuvuta pumzi nyingi na kuzishsuha.
“Vipi kama nitasema napanga kujiuzuru na kumchagua mtu mwingine kuwa CEO wa kampuni na mimi kumsaidia kwa pembeni? , Je utasapoti maamuzi yangu?”Aliuliza na kumfanya Roma kushangazwa na swali lake hilo.
“Niliweza kuhisia haya ndio maamuzi unayotaka kuchukua , lakini je ndio kitu unachopenda kufanya?”
“Nimechoka , sina nguvu tena za kudili na maswala haya zaidi na isitoshe na mimi ni binadamu, naweza kuonekana mkatili kwa watu wa nje lakini sijui namna ya kudili na marafiki zangu pamoja na familia”
“Unafanya haya yote kutokana na kilichomtokea Sophia, si ndio?”
“Hilo ni moja , iwe ni Dorisi au Nasra wote wanashikilia nafasi muhimu katika kampuni na siwezi kufanya kazi bila wao , lakini kila ninapofikiria uhusiano wako na wao , moyo wangu unakosa utulivu , kwasababu ni wafanyakazi wenzangu najitahidi kujizuia na kujiambia hakuna kitu kibaya kitakachotokea , lakini je unafikiri ni rahisi kwangu?”
Roma alijikuta akikosa neno , alijua Edna ashapotezea mambo hayo muda mrefu kumbe alikuwa akijizuia muda wote huo.
“Pia kama ningekuwa sina uhusiano wowote na Sophia huenda ningeweza kufanya maamuzi ya kumzuia kutoonekana hadharani kwa muda kidogo, lakini siwezi kufanya hivyo kwani mimi ni Bosi wa kampuni na itaonekana namnyanyasa nikifanya hivyo , ukweli sijui namna ya kudili na hili swala nahisi kuchoka…”
Kilichokuwa kikimpa hofu zaidi Edna ni juu ya uhusiano wa Roma na Nasra pamoja na Dorisi , alifikiria je kama itafahamika katika jamii kwamba na wao wana mahusiano ya kimapenzi na mume wake si itamchafua zaidi na zaidi , alichukulia tu kwa mfano tukio la Sophia lilivyokuwa likimuumiza kichwa ndio maana alifikia maamuzi ya kutaka kuachia ngazi.
“Naelewa unachojisikia lakini hata kama utajiuzuru na kutoa nafasi yako kwa mtu mwingine hawawezi kufanya chochote na watu watasema ulikimbia”
“Najua, ndio maana mpango wangu baada ya kijiuzuru ni kuita waandishi wa habari na kisha nitawalezea uhusiano wangu na Sophia na kuwaambia hahusiki katika uzushi unaosambazwa . ni sababu nzuri kujiuzuru kwa kuwajibika ili kulinda taswira ya kampuni”
“Kwannini unataka kuwajibika , watu walioanzisha huo uzushi ndio ambao wanapaswa kuwajibika”
“Lakini angalau kuwepo na mtu wa kubeba lawama zote , sina mpango wa kuendelea kufanya kazi na kujiuzuru ndio kitu pekee ambacho naweza kufanya kwa ajili ya Sophia”
Roma alona kabisa maamuzi ambayo anataka kuchukua Edna ni ya kijinga na akifanya hivyo kwasababu ya Sophia aliamini kabisa ingemfanya na Sophia mwenyewe kukosa ujasiri wa kujitokeza hadharani tena.
Muda huo wakati wakiongea Bi Wema aliwafuata huku akionekana kuwaita.
“Miss kuna taarifa huku , njooni muone , kuna habari mbaya”Aliongea Bi Wema kwa kupaniki.
********
Muda huo huo ncha ya kaskazini mwa dunia , ndani ya maabara kubwa iliotengenezwa na Yan Buwen, hali ya hewa haikuonekana kuwa nzuri.
Vifaa vyote vya maabara vilionekana kufanya kazi , huku Skrini zikionyesha baadhi ya data ngumu kuelekeweka kupanda na kushuka.
Katika meza kubwa ya kisasa kama zile za hospitalini kulionekana mirija mingi ikiwa imeunganishwa katika mwili wa binadamu.
Upande wa kulia na kushoto wa meza hio kulikuwepo baadhi ya vifaa vilivyokuwa na maumbo ya ajabu ambayo ndani yake kulikuwa na vitu kama maji maji.
Juu kabisa ya mwili wa binadamu uliolazwa kwenye meza hio kulikuwa pia na kifaa cha muundo wa kipekee ambacho ndani yake kulikuwa na mwanga mkali wa kung’aa uliokuwa ukionekana huku ukizunguka zunguka , ilikuwa ni nishati ambayo ilionekana kuunganishwa moja kwa moja na mwili wa binadamu huyo.
Mtu wa ngozi nyeusi alielazwa katika meza alikuwa uchi wa mnyama huku miguu yake ikiwa imebananishwa na kufungwa kwa kamba ngumu maalumu ili kumzuia asisogee.
Alikuwa ni Denisi , ijapokuwa alionekana kuwa na fahamu lakini ilionyesha muda wowote angezimia, yote hayo ni kutokana na kwamba nishati iliokuwa imewekwa juu yake , ilionyesha kujiandaa kuuvamia mwili wake .
“Punguza wasiwasi , utakuwa sawa muda si mrefu , isitoshe hili linafanyika kwa faida yako”
Mwanaume aliekuwa pembeni ya meza hio ya kufanyia operesheni alionekana kutabasamu kifedhuli , alikuwa amevalia koti la maabara ambalo tayari lilikuwa na madoa mengi na alionekana ana muda mrefu hakuwa amenyoa ndevu zake kwani zilionyesha kuota kwa wingi.
Josesph Bikindi muonekano wake ulirudi na kuwa kama ule wa miezi kadhaa nyuma wakati alipokuwa akifahamika kwa jina maarufu la Lekcha.
Nguo pekee ambayo ilikuwa imeusitili mwili wake ni koti la maabara na alikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo , kwani alionyesha kukonda tofauti na alivyokuwa siku kadhaa nyuma kabla ya kuingia katika mabara hio ya marehemu Yan Buwen.
Katika eneo la kifua chake karibu na moyo kulikuwa na kitenesi cha nishati ya Anti- matter ambayo imeshikiliana na mwili wake na huenda Roma angekuwepo moja kwa moja angejua kitenesi hicho cha nishati ni jiwe la kimungu.
Kama ilivyokuwa kwa Yan Buwen , Lckcha alitumia teknolojjia ile ile ilioachwa na kuunganisha jiwe la kimungu na mwili wake , lakini utofauti tu ni kwamba teknolojia hio yeye alikuwa ameindeleza kwa viwango vya juu na kumfanya kuwa na uwezo ambao ni mkubwa zaidi kuliko aliokuwa nao Yan Buwen.
“Unataka kufanya nini?”Alipaniki Denisi mara baada ya Lekcha kuanza kuchezesha lile boksi ambalo lilikuwa limejaa nishati.
“Hehe.. hutaki kuwa na nguvu , hii ni gunduzi yangu mpya nilioweza kuifaikisha kupitia muendelezo wa teknolojjia ya Yan Buwen…”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kejeli kama kawaida yake.
“Hiki ni kifaa nilichokipa jina la ATD(Ant -matter transfomation device) ninachopaswa kufanya ni kukiwasha kwa kutumia jiwe la kimungu na kitaibadilisha nishati yote isio ya maada kwa kuwa na nguvu kwa zaidi ya mara mia moja, kinaweza pia kutumika kufuta Genome za mwili wako na kama kitaonyesha mafanikio kwako basi na kwangu kitafanya kazi na yatakuwa mafanikio ya teknolojia kubwa ya kuwasha link ya vinasaba vya mwili wangu na kuungana na muundo wa viambata vya nishati ya Ant-matter na kwanzia hapo nitakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya ninachotaka”
“Unamaanisha nini?”Aliuliza Denisi kwa hofu.
“How would I know ..,, according to Yan Buwen idea the transformation on the test subject is still unknown . Well no matter how it turned out to be , I’ m sure I will benefit from it ,you won’t understand even if I explain it to you”Aliongea akimaanisha kwamba hawezi kujua kwasababu mchakato wa mabadiliko kwa mtu anaejaribiwa haujulikani , lakini anaendelea kusema licha ya matokeo ya aina yoyote ana uhakika kwamba atafaidika nyao hivyo hata kama amwelezee kila kitu hatoweza kumuelewa.
“Kwahio unataka kunitumia kama chombo cha majaribo , kwanini unataka kunifanyia hivyo , sisi si marafiki?”Aliuliza Denisi kwa wasiwasi mkubwa lakini Lekcha aliishia kucheka sana.
“Umesema marafiki, Wewe?.. wewe ni mbwa tu wangu , unafikiri unafaida kubwa kuliko yule malaya ?”
Baada ya kuongea palepale aliwasha jiwe la kimungu kwa kutmia akili yake tu na palepale mwanga ulizidi kufunika maabara hio baada ya mlipuko wa mng’ao wa mwanga wa ajabu uliotoka katika jiwe la kimungu.
Kila mlipuko wa mwanga ule wa Ant matter unavvyotokea uliakisiwa na kifaa ilichofungwa kwa kuning’inizwa juu ya mwili wa Denisi na kisha palepale kifaa kile cha ATD kilikuza nguvu ya mwanga ule na kisha kumulika katika mwili wa Denisi.
Lekcha alirudia kwa mara ya pili na awamu hio kulitokea mlipuko mkubwa zaidi wa mwanga na kisha ukasharabiwa wote na kile kifaa na kisha ukaelekezewa katika mwili wa Denisi na kumfanya asionekane kabisa kwani kifaa kile kilimulika mwili mzima mpaka kwenye kucha za miguu.
Lekcha alizidi kuinua mikono yake na kuruhusu nguvu ya jiwe la kimungu kumezwa na vifaa na kisha kuelekezewa katika mwili wa Denisi , alirudia mara nyingi mpaka ikafikia wakati sasa mwili wa Denisi ulianza kuonekana kama vile unatoa shoti za umeme wa rangi ya bluu.
Aliendelea vilevile bila kuacha , ilionekana matokeo anayoyataka bado, aliendelea kutoa nishati isio maada kumuingia Denisi huku makelele ya milipuko ya umeme kama vile nguzo inapiga shoti ilisambaa chumba kizima , lakini bado Lekcha hakuacha kufanya anachokifanya alizidi kuruhusu nishati ya ant-matter kuuvaa mwili wa Denisi kwa muda mrefu na ilifikia mwili wa Denisi hakuonekana kabisa.
Ni ndani ya nusu saa tu kulitokea mlipuko mkubwa mno kiasi kwamba kwa macho ya kawaida yasingeweza kuhimiri mn’gao wake kwani ulimkuwa mkali sana wenye wavelength za kuumiza macho.
Lekcha alirudi nyuma na kuacha kile kitendo alichokuwa akiendelea nacho na kisha macho yake yote aliangalia katikati ya maabara hio kama vile mtu anaetegemea mtu kutokea katikati ya mlupuko huo wa mng’ao.
Ni ndani ya dakika kama kumi na tano tu , ule mng’ao ulianza kujikusanya taratibu taratibu na kuanza kupungua na mpaka wote unaisha Denisi hakuweza kuonekana wala ile meza haikuonekana, ni kama vile imeyeyuka na kitu pekee kilichobakia ni mpira wenye kung’aa uliobakia sakafuni, ulikuwa ni mpira wa nishati , huenda ni nishati ya nguvu ya Ant-Matter.
Lekcha alijikuta akijawa na mshangao huku uso wake ukiwa katika hali ya tabasamu pana na alisogea kwa haraka.
Na kwa kutetemeka mikono aliunyanyua ule mpira wa nishati wenye mwanga uliokuwa ukicheza.
Baada ya kuusihikilia mkononi aliuachia hewani na palepale hakudondoka chini bali ulielea na kisha ukamsogelea katika eneo la kifua chake upande wa jiwe la kimungu.
Ilikuwa ni kama lile jiwe la kimungu lilikuwa likiuvuta kwani baada ya mpira ule wa nishati kufika katika kile kifua ulimezwa wote na kupotelea ndani ya mwili wa Lekcha.
“Haha.. I did it … I did it”Aliongea kwa furaha huku mwili wake ukianza kutetemeka , alikuwa akihisi kabisa seli za mwili wake zilikuwa zikicheza na ngozi yake alihisi ikiwa na muwasho usio kuwa wa kawaida , ni kama vile mwili wake umegeuka kuwa kidonda na sasa ulikuwa ukipita katika hatua ya kupona.
Palepale alitupa koti lake chini na kubakia uchi , lakini baada tu ya kutoa lile koti alidondoka chini na kuanza kutetemeka kwa kurusha miguu kama vile alikuwa mgonjwa wa kifafa na ghafla tu jiwe lililokuwa katika kifua chake lilitoa mwanga mkali kwa sekunde tu na kisha ukapotea na palepale mwili wa Lekcha ulianza kupitia mabadiliko kwa kasi kubwa mno kama vile ni kiumbe cha ajabu kwani hata nywele zilianza kubadilika..
Baada ya dakika tano Lekcha mwili wake ulibadilika na alifanana kwa kila kitu na Denisi , alikuwa ni Denisi mtupu.
Baada ya kutulia kabisa na kuhisi mwili wake haupo kwenye maumivu na ule muwasho wa mwili umeisha palepale alisimama na kisha akakisogelea kioo.
“Denis”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli huku akiwa uchi , na alianza kujikagua mwili mzima akiwa kama mtu asieamini kama ameweza kubadilika na kuuvaa mwili wa Denisi.
Lekcha muda uleule hakusubiri tena hata sekunde kwani alipotea ndani ya maabara ile kama jini na alipokuja kutokezea ni nje kabisa juu ya barafu na ile anatua tu , vivuli vya watu wawili vilivyoakisiwa na mwezi vilionekana,Alikuwa ni Kizwe pamoja na Desmond.
“Denisi..!”Aliita kizwe kwa mshango na kisha alimpita Lekcha kwa mbele na kumkagua.
“Little Cripple dear , you finally succeded should I call You Denis Senga now?”
“Mpenzi wangu kilema naona umefanikiwa , vipi nikuite Denisi Senga sasa?”Aliongea Kizwe kwa kingereza.
Lekcha palepale alimsogelea kwa spidi na kabla hata Kizwe hajaelewa alijishutikia akiwa kwenye mikono ya Lekcha mwenye muonekano wa Denisi.
Kizwe alikuwa ashazoea namna ambavyo Lekcha alikuwa akimfanyia kila anapotaka huduma kutoka kwake na palepale hakuleta ubishi na alimsogezea mdomo mwanaume huyo na wakaanza kubusiana.
Desmond alisimama bila hata ya kujali kile kinachoendelea , hata hivyo licha ya kwamba mama yake alifufuliwa lakini hakuwa mama yake anaemjua , alionekana ni mtu mwingine kabisa na hakuwahi kumkubali.
“Mmefanikuwa kupata chochote?”Aliuliza Joseph Bikindi au ukipenda mwite Lekcha.
“Ni kama nilivyotarajia Jeremy ameita ndugu zake kutoka ujinini , kuna mwanaume mmoja anaeitwa Nix pamoja na Gesha , wote wana uwezo wa mafunzo ya mbingu na ardhi”Aliongea Kizwe.
“Vizuri .. tutachukulia swala hilo kwa manufaa kwetu”Alijibu Lekcha.
“Lekcha kwanini usiuvae mwili wa Jeremy na ukawa raisi wewe?”Aliuliza Kizwe.
“Acha ujinga wewe mwanamke , unafikiri hao majini ni rahisi kushindana nao , ninaweza kuwamaliza ndio lakini vipi kuhusu huko wanakotokea , unafikiri nitaweza kuwashinda wakija duniani kupambana?, kwasasa mimi ni Denisi na lazima nichukulie mwonekano wangu kama fursa”
“Unamaanisha …”Kizwe alitaka kuongea lakini palepale alijikuta akitoa tabasamu pana kama vile taa imeweshwa kwenye akili yake na kugundua anachopanga Lekcha .
“Kilema , hakika wewe ni mwenye akili sana”Aliongea Kizwe huku akitoa kicheko cha kebehi na Lekcha alimwangalia kwa kejeli mwanamke huyo na kisha akanusa nusa shingo yake lakini hakuonyesha tamaaa ya kumuhitaji Kizwe tena
“Clelia Allisanto” Jina hilo lililipuka kwenye akili yake na palepale alimtua chini Kizwe na kuonyesha tabasamu.
“Tumetumia muda mwingi sana kukaa huku Ncha ya Kaskazini…. Kituo chetu cha kwanza ni nchini Tanzania, Tuondokeni kazi ya kulipa kisasi imeanza rasmi”Aliongea Lekcha na palepale wote kwa pamoja walipotea.
Ilionekana hata Desmond alikuwa na mabadiliko makubwa kwani hakuwa wa kawaida tena.
Muda wote ambao Lekcha alikuwa akijibadilisha kuwa Denisi alikuwa akiangaliwa na mtu alievalia Mask na mavazi meusi , alikuwa ni bwana yule ambaye alipigana na Roma nchini Korea na Australia.
Lekcha hakuweza kumuona bwana huyo kutokana na kwamba alikuwa akitumia nguvu za kijini kujificha na hata baada ya Lekcha kuondoka ndani ya maabara alimfuata kwa nyuma.
Muda uleule wakati Lekcha na wenzake walivyoondoka , akitaka kugeuka na yeye kuondoka hilo eneo , kivuli cha mtu mwingine kilionekana nyuma yake .
“Your Highness Athena , you’re here”Aliongea kwa heshima huku akiinamisha kichwa chake na Athena alitingisha kichwa tu na kisha akaongea.
“He did it..”Aliongea kwa sauti yake ya kike akimaanisha , Amefanikiwa?
“Yes as you said , he activated the genetic link technology and ate Denis .He Transfomed into Denis and his power had improved greatly”Aliongea akimaanisha kwamba ameweza kufanikiwa kuwasha teknolojia ya Genetic Link na kummeza Denis, Amebadilika na kuwa Denis na nguvu zake pia zimeimarika sana.
“He is still slower , looks like he’s not as good as Yan Buwen”Aliongea akimaanisha kwamba bado yupo taratibu , na inaonekana hayupo vizuri zaidi kama Yan Buwen.
Kwa kauli yake hio ilionyesha kifo cha Yan Buwen kilikuwa hasara kubwa kwake.
“Kwa maoni yangu , Yan Buwen anaweza kuwa na kipaji na uwezo mkubwa wa akili lakini Joseph ana tamaa kubwa halafu ni mkatili , nina uhakika anaweza kuwa tishio kwetu muda si mrefu , sijui kwanini unamuacha afanye atakavyo , si tayari amefanikisha misheni ya kuendeleza utafiti wa namna ya kuwasha teknolojia ya Genetic link?”Aliuliza Bwana mwenye Mask.
“I need the results from his research but he still has values , stop asking about it”
“Nilihitaji matokeo kutoka kwa tafiti yake lakini bado ana thamani , acha kuuliza kuhusu hilo”Aliongea Athena.
“Yes Your Highness”Aliongea bwana mwenye Mask.
“Hamisha vifaa vyote ndani ya maabara katika sehemu salama na haribu kila kitu , baada ya hapo nenda nchini Tanzania na endelea kumfatilia , hakikisha Roma hakuoni asije kukumeza maana sitoweza kukukoa tena”Aliongea na kumfanya Bwana mwenye Mask kukakamaa mwili, baada ya kukumbuka tanuru la Maafa(Chaos Cauldron).
Baada ya kutingisha kichwa kuitikia palepale aliondoka hapo na kuelekea katika maabara kufanyia kazi maelekezo aliopatiwa , kwa uwezo wake ilikuwa rahisi sana kuhamisha baadhi ya vitu muhimu vyote katika sehemu salama ndani ya muda mfupi tu.
Lakini hata hivyo alizidi kumuogopa Athena , hio yote ni kutokana na kwamba mipango yake ilikuwa ipo kimahesabu zaidi .
Licha ya kuwa na uzoefu wa karne lakini alishindwa kabisa kufahami ni kipi anafikiria na mpango wake unaofuata ni upi.
SEHEMU YA 562.
Hakika ilikuwa habari mbaya sana kwa Edna na Roma kulingana na juhudi kubwa ya kumfanya Sophia kuwa maarufu.
Taarifa ambayo ilikuwa ikiwasilishwa katika runinga ilionekana ni ambayo Sophia alikuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Kitendo cha Sophia kufanya ‘Press conference’ bila ya kushirikisha kampuni inayomsimamia kilimshangaza Edna na Roma kwa wakati mmoja , mbaya zaidi haikuwa kikao na waandishi wa habari kukanusha tu uvumi bali alienda mbali zaidi kutangaza jambo kubwa zaidi.
Katika kikao hicho kwanza kabisa alikiri kwamba Edna ni dada yake na hata kuanzishwa kwa lebo ya kusimamia wasanii chini ya Vexto media ilianzishwa kwa ajili yake.
Baada ya kuongea hivyo waandishi hawakuonyesha hali ya kuridhika na kutaka kujua ukweli wote kuhusu yeye na Roma kama wana uhusiano wowote na hapo ndipo Sophia aliharibu kabisa kwani alikiri kwamba alikuwa na hisia za kimapenzi na Shemeji yake , lakini hakuwahi kuweka hisia zake wazi wala kujihusisha nae kwani ni mume wa dada yake.
Kauli ya Sophia ilimshutua mno Edna na hakutaka kabisa hata kuendelea kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea kwani palepale aliondoka na kusema anaenda kulala.
Roma alishindwa kuongea chochote kutokana yeye ndio chanzo ya kila kinachoendelea hivyo alimwangalia mke wake kwa huzuni akipandisha ngazi kwenda juu kwa ajili ya kulala.
Sophia mara baada ya kutoa kauli yake hio alitoa tangazo Rasmi kwamba anaachana na maswala ya Mziki na Usanii.
Ilikuwa kauli ambayo ilishangaza kila mmoja ambaye alikuwa ni shabiki yake na hata waandishi wa habari waliokuwa wakiuliza maswali walitaka kujua kwanini Sophia kaamua kufanya maamuzi makubwa ya namna hio ilihali alishatolea swala la uhusioano wake na Shemeji yake, waliuliza je kuna sababu nyingine ya kufanya maamuzi ya kuachana na mziki, lakini licha ya maswali hayo Sophia hakutaka kujibu na alifunga mkutano huo.
Roma aliekuwa sebuleni akiangalia na Bi Wema alijikuta akiwa kwenye mshangao na kushindwa kujua kitu cha kufanya kwa wakati mmoja, alitamani kupotea hapo hapo na kwenda mpaka Dodoma.
Lakini aliona hata kama akianzisha safari hio na kufika Dodoma hakuna ambacho angeweza kufanya kama tu Sophia kaamua mwenyewe kufanya kikao bila kumshirikisha , kuna hisia zilimwambai kabisa Balozi atakuwa amehusika katika hilo.
Mjuda uleule Roma akiwa ni mwenye kuwaza cha kufanya simu yake ilianza kunguruma ikishiria ilikuwa ikiita na alipoangalia namba ambayo inampigia ni mpya na alipokea palepale na alipoweka sikioni na kusikia sauti ya mwanaume aliejitambulisha hapo hapo alijua ni nani ambaye alikuwa akiongea, alikuwa ni Balozi baba yake Sophia.
“Hades nadhani mpaka sasa umeona taarifa?”Sauti ya Balozi ilisikika.
“Nimeona taarifa ndio , lakini kwanini mmefanya maamuzi bila ya kutushirikisha mnajua ni kwa nguvu kiasi gani ambayo Edna mke wangu aliwekeza ili kumfanya Sophia kuwa maarufu”
“Hayo yalikuwa maamuzi yake , nadhani mpaka sasa unaelewa ni upi msimamo wa Sophia”
“Naelewa vipi msimamo wake ilihali sijaongea nae tokea tukio litokee”Aliongea Roma huku sauti yake ikianza kukosa uvumilivu.
“Sophia mpaka sasa hataki kuendelea na maswala ya mziki tena na ninarudi nae Japan, ukitaka kumjumuisha sehemu ya wanawake wako mfuate Japan, nilimleta Sophia kwako sio kwasababu nilitaka umfanye kuwa maarufu bali nilitaka umfanye mke wako wa pili”
“Lakini mziki ni kitu ambacho Sophia alikuwa akipenda , hatukukurupuka kumuingiza katika ulimwengu wa kistaa”
“Una uhakika ndio kitu anachokipenda au unausemea moyo wake?”
“Unataka kumaanisha nini?”
“Hades wewe ni mwanaume kwanini unazunguka zunguka ilihali unaujua ukweli , kama unahitaji kuonana na Sophia kwa mara nyingine umfuate Japan”Aliongea Balozi kitemi na palepale alikata simu yake na kumfanya Roma akijikune kichwa chake na kukosa kabisa cha kufanya.
Siku iliofuata wakati wakipata kifungua kinywa , Roma alionekana kabisa kukosa raha zote , ukweli ni kwamba usiku mzima hakulala kutokana na maamuzi alioyafanya Sophia.
“Sophia karudi Japani?”Aliuliza Edna.
“Umejuaje?”
“Kanitumia meseji jana ya usiku ya kuniomba msamaha kwa kila kitu na kuniambia kaachana na mziki”Alijibu Edna na kumfanya Roma kushangaa .
“Kwanini mimi hajaniambia chochote hata kunitumia tu ujumbe?”Aliongea Roma huku akicheka kicheko cha kukata tamaa.
“Unapanga kwenda kumfuata?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kuwa katika hali ya mshangao kidogo na kushindwa kujibu swali lake.
“Kama unataka kwenda sitokuzuia”
“Najua huwezi kunizuia kwasababu ni Sophia lakini hio ndio sababu pekee ambayo inanifanya nisiende”Aliongea na kumfanya Edna kutoa tabasamu hafifu.
“Hapa hata sijui napaswa kukasirika au kuwa na furaha”
“Usifikirie sana , hakuna ambaye amefanya kosa, baadhi ya vitu katika maisha haviendi kama tunavyopanga lakini haimaanishi kwamba haiwezekani kwa sisi kutosahau , Sophia bado ni mdogo anaweza kusahau kila kitu wakati akiendelea kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi”
Ndio hata Sophia alikuwa akifanya mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na Ardhi ili asizeeke kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine.
Hivyo Roma aliaminig nishati ya akili ambayo ageweza kuipata Sophia moja kwamoja ingemfanya kusahau yaliopita na kuanza maisha mengine.
Roma alivyokuwa akifikiria ni tofuati na Sophia alichokuwa akifikiria , Sophia alifanya mziki kwasababu tu ni sehemu ya kitu anachopenda kwasababu hakuwa na kitu kingine ambacho angeweza kufanya , malengo makuu ya Sophia ni kuwa katika mahusiano na Roma na kadri siku zilivyokuwa zikisonga alikuwa kabisa akikosa uvumilivu wa kuzishinda hisia zake , huenda hata maamuzi ya kuondoka bila kumuaga Roma ilikuwa ni sababu maalumu ya kumfanya Roma kuweza kumkumbuka.
Edna kuna kitu alichokuwa akikiona kutoka kwa Roma na alijua fika hiko ndio kilichomfanya kuwa na mwonekano wa kukosa furaha asubuhi hio.
Baada ya kula kidongo tu aliweka uma na kijiko chini na kisha akamshika Lanlan nywele na kumpa maagizo Qiang Xi kumuwahisha shule na kisha alichukua mkoba wake na kuaga anaenda kazini.
“Kwanini haraka hivyo , kuna jambo la muhimu huko kazini?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Nina miadi na lakini pia kuna vitu vya kuandaa kabla ya kikao”
“Wife ni kweli unapanga kustaafu”
“Ndio , nilishakuambia tayari jana na natarajia utasapoti maamuzi yangu”
“Lakini hauna haja ya kuharakisha kwasabu lazima kwanza uchague nani anakwenda kurithi nafasi yako , Vexto ni kampuni ya kimataifa, sio rahisi kupata mtu mwenye uwezo na ambaye ataweza kuongoza kwa ufanisi kama wewe”Aliongea Roma kushauri na kumfanya Edna kutabasamu.
“Unaweza ukaja makao makuu kama una shauku , nishachagua tayari mrithi wangu na mtu huyo atafika ndani ya kampuni baadae”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa , ijapokuwa alikuwa na hisia kwamba tayari Edna ashachagua mtu wa kumrithi lakini bado ilimfanya kama vile kawekwa gizani kwa mara nyingine.
Ukiachana na mchakato, taarifa ambayo anakwenda kutoa Edna huenda ingewashangaza wengi kwani ni ya ghafla sana , kubadilika kwa CEO wa kampunni kubwa kama hio ni jambo kubwa sana.
Edna alikuwa ashakusanya wafanyakazi wote wa juu wa kampuni siku ya jana kwa ajili ya kikao siku hio na baada ya kufika ofisini aliweza kupewa taarifa na Recho watu wote wamekusanyika katika ukumbi kwa ajili ya kikao.
Dorisi ,Nasra , Recho na Benadetha wote walikuwepo na baadhi ya wafanyakazi waliuliza sababu ya kikao hicho ni nini , lakini hawakuwa na majibu sahihi ya kuwapa kwani hawakuwa wakielewa pia kinachoendelea.
Saa nne kamili Edna aliweza kuingia katika ukumbi wa mikutano, kama kawaida yake akiwa na mwoneknao wa kujiamini na watu wote walisimamama kuonyesha ishara ya kumkaribisha .
Baada ya miaka mingi ya kufanya nae kazi pamoja na licha ya kuwa mdogo ki umri lakini alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa wafanyakazi wake.
Roma hata yeye alikuwepo , hakuhudhuria kikao kama mfanyakazi wa kampuni lakini yeye alisimama nje ya mlango wa kuingilia akitaka kujua nani anakwenda kuwa mrithi wa Edna.
Recho ambaye muda wote alikuwa akimsaidia Edna katika majukumu yake akili yake ilikuwa kwenye wasiwasi , yeye ndio aliekuwa akijua kinachoendelea kwani siku ya jana yote ndie aliekuwa na jukumu la kupigia simu viongozi wa juu wote wa kampuni Tanzu kufika makao makuu kwa ajili ya kikao.
Sasa alijiambia kama Edna anakwenda kustaafu vipi kuhusu yeye kazi yake , inamaana na yeye anapaswa kuacha kazi kwasababu hatokuwa msaidizi tena wa Edna.
“Have a seat”Aliongea Edna kwa kingereza akiwaambia wafanyakazi hao wote kukaa chini.
Chumba chote kilibakia kuwa chini ya ukimya wa hali ya juu sana na macho yao yote walikuwa wameyaelekezea kwa Edna.
Edna upande wake alitulia kwa dakika kadhaa na kisha akaonyesha tabasamu ili kuondoa hali ya hewa ya wasiwasi kwa wafanyakazi hao.
“Najua mna wasiwasi mkubwa na kama mmechanganyikiwa na kujaribu kufanya makisio na kupelekea kuwa katika hali ya wasiwasi lakini yote hayo hayatozuia mimi kutoa tangazo langu , Ninaachia ngazi katika nafasi yangu kama raisi wa makampuni yote ya Vexto”Aliongea Edna na kufanya watu wote kuwa katika hali ya mshangao na kauli yake.
“Raisi Edna nini kinaendelea , kampuni yetu inafanya vizuri tutawezaje kuendelea bila ya wewe?”Aliuliza mmoja ya wafanyakazi alieshindwa kuzuia mshangao wake.
“Ndio CEO, tuambie matatizo yako, tumepitia magumu mengi kuifikisha kampuni katika hatua hii tukiwa pamoja , hakuna lingine la kutuogopesha”Alichangia mwingine na mwingine akadiakia hivyo hivyo na mwishowe likaibuka Zogo la wafanyakazi wote kutaka Edna atengue kauli yake na Edna alisimamia katika msimamo wake.
“Ninajiuzuri kama CEO lakini haimaanishi kwamba naitelekeza Vexto , Bibi yangu na mama yangu waliyatoa maisha yao kwa ajili ya maendeleo ya kampuni hii na ishakuwa kama sehemu ya familia yangu , siwezi kuitekeleza familia yangu , ninachosema ni kwamba najiuzuru katika nafasi yangu lakini bado nitakuwa na asilimia hamsini za hisa zote za kampuni na nitaendelea kubakia kama mwenyekiti wa bodi .. sababu ya mimi kujiuzuru ni kwasababu ya maswala binafsi , siwezi kfuanya kazi kila siku kama nilivyokuwa nafanya kipindi cha nyuma”Aliongea na wafanyakazi hao walijikuta wakipata ahueni kidogo kwa maneno yake lakini bado walikuwa katika hali ya mshangao na kutoridhika.
“Raisi Edna unataka kubakia kama mwenyekiti wa bodi kwasababu umechoshwa na kazi?”Aliuliza mwanamke mmoja.
“Kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea kufanya maamuzi haya , naamini wote mnajua kwamba nimeolewa na pia nina mtoto tayari , ninataka kutumia muda mwingi kuwa na binti yangu ili kumwangalia kwa ukaribu akiendelea kukua na isitoshe mume wangu hapendi nikifanya kazi kwa muda mrefu, nadhani ni wakati wa mimi kuwa karibu na familia yangu , nimechoka sana na nadhani napaswa kujipa muda wa mapumziko , ninaweza kabisa kustaafu hata uwenyekiti na kumpa mtu mwingine kushika nafasi yangu”Aliongea na kufanya chumba chote kuwa kimya na watu kuangaliana .
“Madam , kama unajiuzuru nani anakwenda kushika wadhifa wako , mrithi lazima awe na uelewa wa namna kampuni ya Vexto inavyoendeshewa pamoja na sera zake ili kuwa na ufanisi , lazima awe pia na uwezo wa kutushawishi na sisi tumkubali kama kiongozi wetu”Aliongea mwingine na kumfanya Edna kuangalia saa ya ukutani.
“Mrithi wangu atakuwa hapa muda si mrefu , tafadhari subirini kwa muda kidogo”Aliongea.
Muda huo Roma aliekuwa nje ya mlango akitaka kujua nani anakwenda kuwa mrithi wa Edna , alijikuta akipatwa na mshangao mara baada ya kuona sura za watu wawili zikitokea kwenye Lift .
Alikuwa ni mwanaume ambaye amevalia suri safi ya bei ghali na tai nyekndu na kumpelekea kuonekana ni mtaaluma maridadi na kwa upande wa mwanamke alionekana kuwa na sura ya kawaida lakini alikuwa ni mwenye tumbo kubwa akiashiria ni mjamzito , lakini licha ya hivyo alitembea kwa muondoko wa kuonyesha kujiamini huku akitoa Aura kama ya mfanyabiashara mkubwa.
“Ernest Komwe na Monica !!?”Roma alijikuta akiongea katika nafsi yake kwani hakutegemea watu hao ndio ambao Edna alikuwa akizungumzia kwenda kumrithi.
“It’s been a while Mister Roma , I hope you are not irked by our appearance”
“Imekuwa kipindi kirefu Mr Roma , natumaini hujakerwa na kuonekana kwetu?”Aliongea Ernest Komwe akiweka tabasamu huku akionyesha heshima mbele ya Roma , alikuwa makini sana na ni kama mtu ambaye aliogopa kumkosea Roma.
Upande huo wafanyakazi wote waliweza kumuona Ernest akisalimiana na Roma walijikuta wakishangaaa mno.
Hawakushangaa kumuona Ernest Komwe tu , bali pia walishangaa kumuona Monica kwani taarifa walizokuwa nazo ni kwamba watu hao walihamia Marekani.
Nasra, Dorisi na Benadetha mara baada yakumuona Ernest walijikuta sura zao zikikunjamana.
Roma aliishia kuangalia mkono wa Ernest Komwe na kumfanya Edna kumwangalia Roma kwa mwonekano wa kuomba asifanye chochote kibaya.
Roma hakupokea hata mkono wa Ernest zaidi ya kutoa tabasamu la machungu na kisha aligeuza na kuondoka kuzifuata Lift na kupotelea ndani.
Kutokana na yaliotokea hakuwa kabisa na hamu ya kuongea na Ernest wala kuendelea kusikiliza kikao hicho ndio maana akaondoka.
Alijiambia ndio maana Edna alikuwa akimuomba kumsapoti kwa maamuzi yoyote kumbe mtu ambaye aliona anafaa kumrithi ni binamu yake Ernest.
Licha ya hivyo Roma alikubali maamuzi ya Edna , kwanza kabisa Ernest ashafanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto kwa muda mrefu na ana uelewa na maswala yote ya kampuni lakini pia alikuwa ni mwenye uwezo mkubwa , pili ingekuwa ngumu kwa Ernest kumsaliti Edna kutokana na kwamba alishuhudia uwezo halisi na ukatiri wa Roma , mwisho kabisa uwepo wa Monica pembeni yake ungeongeza ufanisi mkubwa kwani Monica alihudumu katika kampuni ya Vexto kwa vipindi vya mabosi wote wawili yaani Rahel pamoja na Edna mwenyewe hivyo uzoefu wake ulikuwa mkubwa.
Lakini jambo la umuhimu sana Ernest alikuwa ni binadamu yake , huenda aliona ngumu kuchagua mtu wa nje ya familia kuongoza kampuni.
Roma aliona pia mpaka Edna kufikia maamuzi hayo huenda alikuwa na mawasiliano ya karibu na Ernest , kwani isingekuwa kitendo cha kufanya maamuzi jana na baada ya hapo kumrihisha kampuni.
Baada ya Roma kuondoka Edna alionyesha hali ya wasiwasi , lakini aliweza kujizuia na kisha akawakaribisha Monica na Ernest kungia ndani ya chumba hicho cha mikutano.
Monica na Ernest walijisikia vibaya kutokana na Roma kuondoka bila kuonyesha furaha ya kuwaona , lakini na wao walijitahidi kutoonyesha hali ya kuathirika na kusalimia kila mmoja aliekuwa ndani ya ukumbi huo.
Baada ya muda wa kusalimiana kwa wale waliokuwa wakimjua Ernest na Monica hatimae Edna aliamua kuwatuliza ili kuendelea na kikao.
“Jamani mpo sahihi huyu ni Ernest , alikuwa ni CEO Msaidizi , jina lake la mwanzo la ukoo alikuwa akiitwa Komwe lakini sasa hivi anafahamika kwa jina la Ernest Kayage, nadhani kila mmoja anafahamu uwezo wake katika kazi hivyo kurudi kwake akiwa ameambatana na Bi Monica ni jambo la bahati sana , Baaada ya kustaafu kwangu nafasi yangu itachukuliwa na Ernest Kayage na Monica atakuwa msaidizi wake , Recho msaidizi wangu atachukua nafasi ya Benadetha kama mkuu wa kitendo cha idara ya uhusiano na masoko na Benadetha atapandishwa cheo na kuwa CEO msaidizi namba mbili akisaidiana na Nasra”Aliongea Edna na kufanya kila mmoja kushangazwa na taarifa hio ya ubadilikaji wa vyeo.
Nasra, Dorisi , Benadetha na Recho walipatwa na mshangao , aliekuwa kwenye mshangao zaidi wa kutokuamini ni Recho baada ya kusikia kwamba anapandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara, kila kitu kwake kilikuwa kama ndoto.
Edna muda wote aliaminika katika maamuzi yake na hata baada ya kutamka mabadiliko hayo madogo hakuna ambaye alipinga kwani walimuamini.
Baada ya mkutano kuisha Dorisi na Nasra walimsogelea Edna haraka haraka wakionekana kuwa na maswali.
“Edna ulimwambia Roma kabla ya kufanya haya maamuzi?”Aliuliza Nasra.
“Aliniambia atanisapoti kwa kila maamuzi nitakayochukua lakini nadhani sasa hivi amekasirika”
“Ndio lazima akasirike , unajua kabisa kilichotokea kati yake na Ernest na sasa hivi..”Aliongea lakini muda huo huo na Ernest aliwasogelea na alioekana kusikia maongezi yao.
“Samahani sana Makamu Nasra , najua tunaonekana kama tumekosa aibu kwa kitendo cha sisi kurudi licha ya mabaya tulioyafanya”
“Vizuri kama unaelewa , Edna anakuchukulia kama binamu ndio maana Roma alikuacha hai , la sivyo tusingekumbuka jina lako muda huu”Aliongea Dorisi akionyesha hajafurahishwa, Monica na Ernest waliangaliana wakikosa neno la kuongezea kupinga kauli yake.
“Hayo yote ni mambo yaliopita na tuachane nayo , hakikisha unafanya vizuri kusimamia Vexto wakati ambao sitokuwepo , sikutaka tu kuona ndugu wa mama yangu wakiishi uhamishoni kwa muda mrefu bila msaada”Aliongea na kumfanya Nasra na Dorisi kuangaliana kwa ishara.
“Edna kama wewe unaondoka na mimi sina sababu ya kubakia hapa kuendelea na kazi , nitatafuta mtu wa kumpendekeza kurithi nafasi yangu”Aliongea Nasra.
“Nilijua tu utaongea hivyo , vipi na wewe Dorisi una mpango wa kuacha pia?”Aliuliza Edna na Dorisi alitingisha kichwa.
“Nitaondoka baada ya kukamilisha majukumu yangu , sitaku kuachwa hapa peke yangu na kuwa nyuma ya mazoezi”Aliongea akimaanisha kwamba hawezi kuendelea na kazi na kushindwa kuendeleza mazoezi ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Monica na Ernest walishindwa kuelewa Dorisi amemaanisha nini kwani kauli yake ilionekana kuwa na zaidi ya maana.
“Juu ya yote Monica Hongera , naona unatarajia mtoto”Aliongea Dorisi.
“Asante sana Dorisi”Alijibu Monnica huku akiweka tabasamu na Nasra na yeye pia alimpa hongera.
SEHEMU YA 563.
Ni muda wa mchana baada ya kikao , Roma hakuwa ameondoka bado ndani ya jengo la kampuni na hata wakati wa Dorisi , Nasra na Edna wanashuka katika Kantini ya kampuni kwa ajili ya chakula waliweza kumkuta.
“Hubby unaonaje ukiungana na sisi kwa ajili ya chakula cha mchana , unaweza kuchagua chochote utakachopenda na sisi tutakula hicho hicho”Aliongea Edna mara baada ya kukutana na Roma njiani lakini Roma hakutaka kuongea nae na kuanza kupiga hatua za kutaka kuondoka akionyesha hali ya kukasirika.
Edna alionyesha kuwa na hofu kwenye macho yake na jambo lile liliwashangaza wafanyakazi waliokuwa wakiona kinachoendelea na hawakutegemea kuona mwanamke mrembo kama Edna kumuogopa mume wake, Edna hakutaka kumpa nafasi Roma ya kuondoka na alimzuia kwa kumshika mkono.
“Unafanya nini , si ulisema wewe mwenyewe siku zote utakuwa ni mwenye kunisapoti? Sikukuomba kuachana na wanawake wako kama tulivyokubaliana lakini kwanini … na isitoshe hili haliwezi kutuletea matatizo , unadhania naweza kumuacha binamu yangu kuzurula huko ugenini bila msaada wowote licha ya yaliowatokea?”Aliuliza Edna na upande wa Roma alijifanyisha kutoridhika.
“Kama nilijua utawarudish kwanini nilitumia juhudi kubwa kuwafukuza kwenda nje ya nchi , naona kabisa binamu wako ni muhimu zaidi kuliko mimi mume wako”Aliongea Roma na kumfanya Edna kukamatika maana alikuwa akimjaribu kuishi ndani ya ahadi yake lakini ilishindikana
“Basi sawa , nakubali nimefanya kosa na sijakutendea vizuri , ni kipi naweza kufanya ili unisamehe?”Aliongea Edna na kumfanya Roma moyo wake kutabasamu ndani kwa ndani , ukweli ni kwamba hakuwa na hasira ila alikuwa akitaka kutumia nafasi hio kuweka mpango wake wazi.
“Okey kwasababbu unaonyesha kubembeleza basi kitu unachopaswa kunifanyia ni kuniruhusu kwenda Cicilly kuwasindikiza Rose na Magdalena wiki ijayo … hivyo sitopata muda wa kukaa na wewe pamoja na Lanlan…”Aliongea Roma lakini palepale sura ya Edna ilijikunja na aliishia njiani kutokumalizia sentensi yake.
“Lakini kama hukubaliani na pendekezo langu , bado tunaweza kujadiliana.. si wewe umesema ni kipi unataka ufanye ili nikusamehe”Aliongea Roma huku akibadili sauti yake.
“Okey hakuna shida unaweza kwenda , hatuwezi kufa au kupotea kwasababu haupo na isitoshe ninaweza tu kumwambia Lanlan baba yake amechagua kusindikiza shangazi zake bada ya yeye”
“Kwanini unataka kumwambia mtoto hivyo ? Nina uhakika Chubby wangu lazima atatafsiri vibaya”
“Hakuna cha kutafsiri vibaya , unaenda kusindikiza wanawake wengine”Aliongea huku akimwangalia kwa macho makali na kumfanya Roma ayakwepeshe ya kwake.
“Sio kama unavyofikiria , marafiki zangu wengi waliopo Cicilly wanataka niende nikaangalie , siwezi kuwapotezea , nipe angalau wiki moja tu na nitawahi kurudi haraka iwezekanavyo baada ya kumaliza kazi yangu”
“Kama ni hivyo kwanini ni Rose na Magdalena ambao wanaweza kwenda huko na sio mimi na Lanlan?”
“Edna haiwezekani , unajua mwenyewe kinachokwenda kutokea huko ni kama vita kati ya wanajeshi na wanajeshi na nadhani mwenyewe unajua tabia ya Lanlan”Aliongea Roma na kumfanya Edna angalau kuelewa maana yake na kujituliza lakini bado hakuridhika.
Wakati Roma akiendelea na maongezi yake na Edna mara palepale simu yake ilianza kuita na alivyoangalia mtu anaepiga ni mama yake mzazi.
Roma palepale alipokea kutaka kujua tatizo ni nini maana mama yake hakuwa na tabia ya kupiga muda kama huo na isitoshe jana usiku tu aliwasiliana nae.
Baada ya kusalimiana ndio muda ambao Blandina alimweleza Roma kuhusu Najma kupata kazi katika wizara kama Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam.
Roma alifurahishwa na taarifa hio , lakini ilimshangaza kwa wakati mmoja mara baada ya kusikia mtu aliewezesha Najma kupata nafasi hio ni raisi Senga na kwa namna ambavyo mama yake alikuwa akisikika ni kama alikuwa na maelewano mazuri na baba yake mzazi, ijapokuwa alikuwa na hisia za aina hio , lakini bado alishangaa kuona mama yake amepiga hatua , lakini hata hivyo alifurahi kwa ajili yake
“Roma baba yako anajitahidi kuanza kujenga ukaribu na wewe , nadhani itakuwa jambo zuri kama utampigia simu na kumshukuru kwa kumsaidia Sophia , isitoshe ni mwanamke wako pia”Roma alifikiria kidogo maelezo yake na kutaka kumuuliza mama yake ni lini akawa na mahusiano ya karibu na Senga lakini alijizuia.
“Mama ni jambo dogo kama hilo amefanya na halihusiani kabisa na mimi kumsogelea , yeye ndie aliekuwa wa kwanza kunikataa kwanini nimfuate na kujipendekeza kwake”Aliongea Roma.
“Najua ndio , lakini ni hasira tu , Senga baba yako amepitia magumu mengi kukuomboleza, huwezi jua lakini alikuwa akikupenda sana wakati ulivyokuwa mdogo na alifanya kila kitu kukuona una furaha, isitoshe ni jambo zuri kama atakutambua , naamini pia uhusiano wako na Denisi utaimarika, ni muda sasa alikuwa na mawazo juu ya Denisi na amekwisha kurudi nyumbani, Roma nakushauri kuepuka ugomvi na Denisi”
“Mama umesema Denisi amerudi?”
“Ndio amerudi baada ya kutokuonekaan kwa mwezi mmoja”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kuhisi kitu cha hatari lakini alipotezea.
Baada ya maongezi ya muda mrefu kidogo Roma alikata simu na Edna alionekana akitaka kujua nini walikuwa wakiongea mara baada ya kusikia jina la Denisi.
“Nimesikia kuhusu Denisi , vipi amerudi?”Aliuliza Edna , alikuwa akijua kutoweka kwa Denisi kupitia Ashley ambaye alikuwa akiongoza projekti yake ya dawa aliongia nayo mkataba na Profesa Clark.
Ashley alikuwa na mwezi mmoja tokea arudi nchini Tanzania na aliteuliwa rasmi kama mkemia mkuu wa serikali na baba yake na kutokana na mafanikio yake hakuna mtu aliepinga nafasi yake, lakini licha ya hivyo Roma hakuwahi kukutana na Ashley tokea arudi nchini , huenda ni kwasababu ya ubize wake ndio maana.
“Mama amesema kwamba Denisi amerudi na kwa maelezo yake anasema hatoondoka tena na mpango wake ni kubadilika na kuwa mtoto mwema na ameweza hata kwenda nyumbani kwa Afande Kweka na kumuomba amuunganishe na jeshi kwani anataka kulitumikia taifa”Aliongea Roma.
“Kama ni hivyo kwanini uso wako upo hivyo , je una kwenda kumuua?”Aliuliza Roma na alishindwa kujibu swali lake , ukweli ni kwamba Roma hakuwa kabisa na mpango wa kumua tena Denisi tena , na hakujali pia makuzi yake yalikuwaje na isitoshe kwa muda huo hakutaka mitafaruku zaidi kwani alipenda amani ndani ya familia yake.
Lakini licha ya hivyo alihisi kuna kitu kinaendelea kuhusu kuonekana kwa Ghafla kwa Denisi na kuanza kutaka kujiunga na jeshi, ijapokuwa hakuwa na sababu ya msingi ya kujisikia hivyo lakini hisia zake zilimwambia kabisa kuna kitu hakipo sawa kuhusu Denisi.
“Tutaona pia namna itakavyokuwa , si unakumbuka mzee Kweka alituhitaji tukusanyike Iringa siku zijazo kama familia , nadhani nitapata fursa ya kujua mchezo anaopanga kucheza., siwezi kuogopa kumuua kama kuna kitu kibaya anachopanga lakini siwezi kufanya hivyo mbele ya Lanlan na kuja kufahamu kwamba nilimuua mdogo wangu”Aliongea Roma.
Roma siku ambayo alienda kumchukua Lanlan mara baada ya kurudi Dubai aliweza kuambiwa na Afande Kweka kufika Iringa mwanzo wa mwezi unaokuja.
Afande Kweka alikuwa akihamia rasmi Iringa na kufanya makazi ya kudumu, alitaka angalau kukaa karibu na mifugo yake na kuufurahia uzee wake, Roma hakuuliza sana juu ya safari hio ya kwenda Iringa.
Ukweli ni kwamba siku hio ilipangwa maalumu na Afande Kweka kuwakutanisha rasmi Raisi Senga na Roma ili kumaliza tofauti zao na hio ni mara baada ya Raisi Senga kufika nyumbani na kuweka nia yake wazi na kuomba baba yake mzazi kumsaidia katika kuirudisha familia yake katika mstari.
Edna aliridhishwa na kauli ya Roma kwamba hawezi kumruhusu Lanlan kushuhudia yeye mwenyewe akimuua mdogo wake.
“Naona mume wangu umezidi kuwa na busara”Aliongea Edna huku akitoa pumzi ya ahueni lakini kauli yake ilimfanya Roma kuona aibu kidogo za kiume , tokea aoe na hatimae kuwa na mtoto alianza kuzingatia mambo mengi .
“Turudi kwenye topiki yetu mke wangu , naomba uniruhusu niondoke angalau kwa siku saba , ninakuahidi nitarudi mapema na wote kwa pamoja tutaenda Iringa, nyie wawili mtachceza mtakavyo mara baada ya kufik, sawa babe?”Aliongea kwa kubembeleza.
“Ole wako uchelewe kurudi na kutumia siku nyingi na kututelekeza mimi na mtoto , nakuambia hutoweza kuvumilia matokeo yake”Aliongea Edna , hata hivyo alijua asingeweza kumzuia , alifurahi kwamba alikuwa akiombwa ruhusa hivyo hakutaka kuleta mambo mengi.
******
Katika siku zilizofuata Edna tayari alianza taratibu za kuhamisha uongozi wake kwenda kwa Ernest na kumkabidhi kila kitu.
Upande wa Roma na yeye baada ya kuona Edna kaacha kazi na yeye hivyo hivyo aliacha na nafasi yake akampatia Daudi.
Edna rasmi akawa sio CEO tena wa kampuni ya Vexto na maswali mengi katika vyombo vya habari yaliibuka lakini kampuni iliishia kutoa maelezo kwa ufupi kwamba Edna alijiuzuru kwa sababu za kifamilia.
Ilikuwa ikishangaza kwani Edna alikuwa amejijengea jina kubwa sana katika ulimwengu wa kibiashara ndani na nje ya nchi.
Upande wa Edna alionekana kufurahia maamuzi yake na alitumia muda mwingi nyumbani kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi huku akipewa maelekezo na Rufi kutokana na uelewa wake ulioambatana na uzoefu.
Bi Wema alifurahi sana kuona namna ambavyo Edna alijenga ukaribu na Rufi mtoto wake, hata ile hali ya uzee aliokuwa nayo ilianza kutoweka na sasa alianza kuwa kijana zaidi , huenda mawazo ya kumkumbuka mwanae yalimtesa miaka na miaka na baada ya kurudi alijisikia vizuri zaidi.
Upande wa Amina baba yake alikuwa akiendelea vizuri na hio ni mara baada ya kupewa kidonge cha kijini na Roma, ijapokuwa ugonjwa wake haukuwa umepona lakini hali yake iliimarika kidogo lakini licha ya hivyo hakuweza kurudi kwenye kampuni tena.
Amina mara baada ya kusikia Edna kajiuzuru na yeye alitamani kufanya hivyo lakini hakuwa na mtu wa kumrithisha hivyo aliachana na mawazo hayo na kuendelea kufanya kazi huku akifanya mazoezi ya kuvua nishati za mbingu na Ardhi.
Upande wa Qiang Xi na yeye alikuwa na wasiwasi mara baada ya Edna kujizuru kwa kugopa kwamba kazi yake ya kumlea Lanlan moja kwam moja ingehamia kwa Edna , lakini Edna alijua wasiwasi wake na kumwambia hana haja ya kuwa na wasiwasi na Edna alimwambia kama atakuwa na mpango wa kutaka kurudi nchini China basi atahakikisha anamsaidia namna ya kwenda kuanza maisha , lakini mrembo huyo wa kichina aligoma na kusema anataka kubakia Tanzania kwa muda.
Kauli yake hio ni kama ilieleweka , walijua tu lazima Qiang Xi alikuwa akitegemea Master wake atarudi Tanzania kumuona Lanlan na yeye ndio maana hakutaka kuondoka , isitoshe pia aliogopa kwamba kuna baadhi ya majukumu hakuwa ametimiza kwa ajili ya Lanlan kama alivyoagizwa na Master wake.
Siku ya jumapili ndio siku ambayo Roma alianza safari yake ya kuelekea katika visiwa vya wafu.
Magdalena na Rose licha ya kwamba walisuburia kwa wiki tu , lakini kutokana na shauku yao ilimwafanya kuona kama wamesubiri muda mrefu na hawakuamini siku ya kesho ndio hio ambayo wanatarajia kuona mkutano huo wa kaisari au Baraza la kaisari ambalo hukutanisha vikosi vya wanajeshi wa kulipwa kutoka makundi mengi duniani.
Siku walizoishi katika visiwa vya wafu , ukiachana na kufanya mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini pia waliweza kuzoeana na raia wanaoishi katika visiwa hivyo.
Ijapokuwa walikuwa wakipata shida ya kuwasiliana kutokana na baadhi ya wengi wao kujua kitaliano , lakini kutokana na kwamba walikuwa katika levo ya Nafsi uwezo wao wa kujifunza lugha mpya ulikuwa mkubwa mno.
Lakini pia asilimia kubwa ya wakazi wa visiwa hivyo kuwa ni wanajeshi wastaafu basi ilikuwa rahisi kwao kupata watu ambao walikuwa wakizungumza lugha ya kingereza na kuelewana, walichofurahi zaidi hawakuonyeshewa ubaguzi kutokana na rangi zao.
Ron kwasababu ndio aliekuwa ana kwenda kuwa mwenyeji katika kipindi chote watakachokuwepo Cicily basi aliweza kufanya maandalizi yote ya safari.
Baada ya Roma kufika tu Ron tayari amekwisha kuandaa Ndege binafsi iliokuwa ikimsubiri yeye na wanawake wake kupanda na kuondoka visiwani hapo.
Kutoka Visiwa vya wafu mpaka Cicilly ulikuwa ni umbali wa nusu saa tu na kama wangependa kusafiiri kwa mbinu za kijini basi ingekuwa ni kufumba na kufumbua , lakini kutokana na kwamba ilikuwa kama safari ya kimatembezi basi waliona watumie ndege.
Cicilly kilikuw ani kisiwa cha watu wengi na kilikuwa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.
Kama ilivyoelezwa katika historia , Ugiriki ya kale , Warumi , Wabzantine(Byzantines), Vikings(Norman) na wengineo ndio ambao walitawala kisiwa hicho hapo kabla , baada ya mgawanyiko wa tawala ya kifalme ya Cicily wahispania na wao walikitawala na baada ya hapo ndipo utawala wa Italy ulikichukua na kuanzia hapo ndipo Cicily ilipoweza kujiendesha yenyewe.
Ni sehemu katika Italy ambayo ni maarufu sana kutokana na kwamba ndio mahali ambapo makundi ya Kimafia duniani yalitokea kwa wingi na kutawala eneo lote ,
Familia za kimafia walikuwa ni kama serikali kivuli ndani ya miji ya visiwa hivyo na walienda sambamba na serikali na hawakuweza kutokomezwa kutokana na makundi hayo kupandikiza watu wao serikalini.
Katika eneo hilo sheria ya kiserikali haikufanya sana kazi au kufuatwa na sheria ambazo zimetungwa na makundi hayo ya kimafia ndio ambazo zilikuwa na nguvu.
Familia ya Constantine ndio familia ambayo anatokea Ron na ndio moja wapo ya familia ambayo ilikuwa ikiogopeka kwa kumiliki kundi kubwa la Mafia Gang.
Lakini hata hivyo Ron alikuwa tayari ashaachia ngazi kama kiongozi wa familia hio na kuhamishia maisha yake katika visiwa vya wafu lakini licha ya hivyo ukubwa wake ndani ya familia bado ulikuwa ukichukuliwa siriasi na alikuwa akiheshimika.
Wakiwa katika ndege Magdalena na Rose waliweza kushangazwa na tamaduni nyingi ambazo Ron aliwaambia kuhusiana na watu wa Cicily lakini shauku yao yote ilikuwa kwenye umoja wa makundi ya kimafia ufahamikao kwa jina la Mafia Alliance.
“Mr Ron nimeweza kusikia kutoka kwa watu kule kisiwani kwamba ulikuwa raisi wa Mafia Allianace? Tuambie ni kwa namna gani uliweza kupata cheo hicho , inashangaza sana?”Aliongea Rose kwa shauku kubwa , kundi lake la Tembo lilikuwa kama chawa kwa makundi ya kimafia ya Itali, watu wa huko walikuwa ni Ma’gangstar wa kihistoria.
“Lady Rose hayo yote ni kwasababu ya Mfalme Pluto , ukweli ni kwamba kama asingetusaidia huenda makundi yote ya kimafia ndani ya Cicily yangetokomezwa”
“Roma ndio kafanya hivyo ?”Aliuliza Magdalena kwa shauku.
“Ukweli ni kwamba wale watu waliokuwa na nguvu ndani ya makundi yetu walikuwa wakipungua siku hadi siku hivyo kupunguza ukubwa wa shughuli zetu na zaidi ya yote watu wa dunia walianza kutuchoka na kipindi hicho serikali ilichukulia jambo hilo kama fursa na wakasambaza wanajeshi wa vitengo maalumu kupambana na sisi , ijapokuwa kipindi hicho tuliweza kupata taarifa mapema ya mpango wa serikali lakini ilikuwa ngumu kwetu kuweka ukinzani , unachotakiwa kuelewa ni kwamba kama serikali ikiamua lake hawachukui tahadhari za aina yoyote, kipindi ambacho tunakaribiwa kushindwa kwa kukosa siraha na watu wa kupambana ndio kipindi ambacho Ghafla tu mfalme Pluto alitokeza”Aliongea huku akionyesha hali ya kukumbuka kipindi kilichopita.
“Nakumbuka kabisa kipindi hicho Mfalme Pluto alitokeza mbele ya maadui zetu na kuharibu siraha zao na kuharibu magari yao ndani ya muda mfupi tu , wanajeshi waliotumwa kipindi hicho walikuwa ni kutoka kambi ya kijeshi ya Uingereza iliokuwa pembeni ya Rome na walisifika kwa uhodari wao lakini Mfalme Pluto aliweza kubadili hali ya hewa kwa kumuua Kamanda wao na mkono mmoja tu , baada ya tukio hilo kundi letu lote lilipata nguvu upya na tuliweza kupambana mpaka tukashinda na baada ya machafuko kuisha ndio nilivyoweza kupata cheo cha uraisi wa Mafia Alliance kama hsehima , lakini ukweli ni kwamba sikufanya chochote..”Aliongea huku akimwangalia Roma kwa namna ya kumkubali, Rose na Magdalena na wao walimwangalia kwa macho ya kiulizo
Muda huo Roma hakuwa ni mwenye kujali stori zao kwani alikuwa bize kula matunda ya zabibu yaliokuwa kwenye sahani na baada ya kugundua anaangaliwa aliwasogezea sahani.
Upande wa Magdalena na Rose waliweza kuona kuna utofaut mkubwa kati ya matarajio yao na uhalisia wanao uona na pengine wanaokwenda kuushuhudia.
Kuna nini huko kwenye Kaisari Conference , je unadhani wanaenda tu kuangalia mapambano tu na Roma anawasindikiza tu warembo hao , jibu linakuja.