NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI SINGANOJR
Mono no aware
SEHEMU YA 669.
Baada ya masaa zaidi ya ishirini na nne ndio waliweza kufika Incheon International Airport , ilikuwa ni mchana wa saa sita wakati wanafika.
Siti Zote walizokuwa wamekaa wakati wote wa safari ni za daraja la kwanza, Roma aliamua kukaa Daraja la kwanza na Clark sio kwamba ana pesa sana lakini ilikuwa ni kuepusha macho kumkodolea Clark kutokana na urembo wake.
Tokea afungue ukurasa wa mapenzi na mrembo huyo alikuwa na wivu pale anapoona wanaume wengine wakimwangalia kwa macho ya kifisi kuliko mwanzo.
Upande wa Clark yeye hakuwa hata na tatizo ni kama amezoea kuangaliwa na wanaume lakini alifurahishwa na vitendo vya wivu vya Roma na alijifanyisha hakuwa akijua kinachoendelea na safari nzima waliongea na kucheka pamoja na pale ambapo walitulia aliendelea kufanya kazi kwa kutumia tarakishi yake ya mapakato.
Ukweli ni kwamba Clark alikuwa akijisikia furaha kutokana na gunduzi hio , ijapokuwa ni gunduzi ambayo haikuwa ya kawaida na ambayo haiwezi kutangazwa kwa jamii lakini bado alijihisi kufanikiwa.
Baada ya kutoka kwenye ndege Roma alikuwa amevalia Jaketi la Leather rangi nyeusi na Clark na yeye alikuwa amevalia koti refu rangi ya Elk na jinsi lilimvyomkaa pamoja na uwepo wa Roma pembeni yake ilifanya wakorea wengi kuwaangalia.
Clark alionekana kama vile ni Star kutoka uzunguni hivyo alivuta attention ya macho ya watu wengi ndani ya uwanja huo..
“Teacher , Teacher I am here”
Sauti ya mwanamke ilisikika kutoka katika kundi la watu waliokuwa wakisubiria wageni na dakika hio hio mwanamke ambaye alikuwa amevalia suti ya rangi nyeupe na sketi ya rangi nyeusi ilioishia magotini alijitokeza.
Alikuwa ni mwanamke wa Kikorea mwenye makadirio ya umri kama miaka therathini hivi akiwa amefunga nywele zake kurudi nyuma , hakuwa amejipaka Makeup yoyote na mwonekano wake ni kama wale wanawake ambao hawajali sana kujipamba na kumfanya kutovutia kwa macho ya haraka haraka labda tu umwangalie kwa muda mrefu ndio utajua kama ni mrembo.
Mwanamke yule hakuwa na aibu na ni kama vile watu wote waliokuwa ndani ya uwanja huo wa ndege walikuwa wamepotea na alimkiimbilia Clark huku akiwa na machozi.
“Teacher Alexander ! Your Are fnally here , I have been waiting for you a longtime”Aliongea yule mwanamke kwa lugha ya kingereza akimwita Clark mwalimu Alexander na kusema alimkumbuka sana.
Ndio Clark jina lake la mwisho ni Alexander na kitendo cha mwanamke huyu kujua jina lake la mwisho basi ilimfanya kweli kuwa mwanafunzi wa Clark.
Zhang Ru ijapokuwa alikuwa kwenye furaha ya kumuona Clark lakini bado alisita sita kukumbatiana nae ni kama alikuwa akimuogopa.
“Zhang Ru Longtime no see, you haven’t changed much”Aliongea Clark kwa tabasamu huku akiwa amemkumbatia.
“Teacher….”Zhang Ru alitaka kuongea neno lakini Clark alimzuia na kumfanya kuchanganyikiwa kwani hakuelewa Clark anataka kumaanisha nini.
“Kama nitakuwa na kumbukumbu nzuri utakuwa na maika zaidi ya therathini sasa hivi , ukiendelea kuniita mwalimu watu watahisi labda nimefanya plastic Surgery ili kuongekana mdogo , hii ni Korea kusini sitaki umaarufu wa ajabu eti”
Ijapokuwa alijua Clark alikuwa akitania lakni Zhang Ru alitingisha kichwa kukubali.
“Teacher gari lipo tayari , tafadharii nifuate mpaka eneo la maegesho..”Aliongea na kisha akamgeukia Roma ambaye hakuwa hata na habari nae.
“Wewe ni..”
Ukweli ni kwamba Zhang Ru mara baada ya kumuona Clark akiwa ametangulizana na mwanaume mweusi alijikuta akishangaa na kujiuliza inakuwaje mrembo kama huyo kutangulizana na mwanaume mweusi tena ambaye hana hata muoenekano wa kitanashati , aliona kabisa ni kama hawaendani hivi.
“Mimi ni mwanaume wa mwalimu wako”Aliongea Roma kujitambulisha na palepale Clark alimsogeleaRoma na kumshika mkono.
“Zhang Ru jina lake anaitwa Roma Ramoni , kwanzia sasa unapaswa kumuheshimu kama unavyoniheshimu mmi , hupaswi kumfanya kama mdogo wako kwasababu ni mdogo kuliko wewe sawa?”Aliongea na kumfanya Roma kukunja uso wake na kujiambia ni utambulisho wa aina gani huu.
Zhang Ru macho yake yalionyesha wasiwasi lakini hata hivyo aliishia kutoa tabasamu kwa kulazimisha na kisha akawaomba waondoke.
Upande wa Roma alikuwa ashatumia Koneksheni zake kuandaliwa chumba cha hadhi ya raisi ndani ya hoteli ya Hilton sehemu ambayo ni karibu kabisa eneo ambalo Dhana hio ya mabaki ya kale ya Kibudha ingetangazwa rasmi kwa waumini wanaosalia Buddha..
Wakati wakiwa njiani kwenye gari Zhang Ru alkuwa akipiga jicho kupitia kioo cha nyuma akimwangalia Roma kwa wasiwasi , alikuwa akisikia Clark na Roma wakiongea lugha ambayo hakuwa akielewa na Clark alionekana kuwa katika furaha mno , alijua kabisa pengine wanaongea maswala ya kimapenzi na alijikuta akikunja uso wake na kujiambia mwalimu wake nani kamloga mpaka kutoka kimapenzi na mtu kama huyo mweusi.
“Teacher kwanini umevutiwa na Dhana ya Moyo wa Kibudha, unataka kufanya Research , kama nakumbuka vizuri hukuwa na matamanio kabisa na maswala ya kidini”Aliongea Zhang Ru akivuruga maongezi yao makusudi.
“Oh! ni Roma ambaye alitaka kuja kuangalia mimi nimemsindikiza tu, amevutiwa sana na kifaa hicho”Aliongea Clark na kumfanya Zhang Ru kulazimisha tabasamu.
“Mr Roma kama nitakuwa sahihi ulikuwa ukiongea na Teacher Clark kwa lugha ya kiitaliano , wewe ni raia wa nchi hio?”
“Hapana , nimeishi ndani ya mataifa mengi sana lakini nimerudi rasmi na kuanzisha maisha yangu ndani ya Tanzania sehemu niliozaliwa”Aliongea Roma.
“Oh! Unaishi maeneo gani nchini Tanzania na unafanya kazi gani?”Aliuliza.
“Naishi Dar es salaam na nafanya kazi za vibarua tu , Miss Zhang Ru kwanini unaonekana kama vile ni polisi?”
“Hamna tu ni kwamba nina shauku ya kutaka kukujua ni mwanaume wa aina gani mpaka kuweza kuushinda moyo wa mwalimu wangu , nishawahi kuishi Tanzania wakati baba yangu akiwa balozi wa China , Mr Roma unaonekana kuwa sio wa kawaida”
“Oh! Kama baba yako alifanya kazi katika ubalozi wa China basi utakuwa na wewe ni mchina , nilifikiri kwa muonekano wako ni Mkorea”Aliongea Roma akiwa na mshangao.
“Kwanini , naonekana kama Mkorea?”Aliuliza huku akikunja sura.
“Hapana ni kwamba kwangu unaonekana kama Mkorea hususani na huo mwonekano wako wa dharau”Aliongea Roma huku akionyesha kutoridhishwa na Zhang Ru tabia yake.
Zhang Ru palepale aliona aibu na hofu ya kuogopa kutomkasirisha Clark.
“Hapana Mr nilikua na shauku tu ya wapi ulipotokea , sitouliza tena”Aliongea akijitahadhari.
Upande wa Clark alikuwa kimya na alimuona Roma kama vile hakuwa akitaka kuonekana mbele ya Zhang Ru kama wa kawaida hivi.
“Mpenzi , Zhang Ru alikuwa ni msichana mzuri sana na wakati anaanza chuo pale Imperial College London miaka mitatu iliopita ilimchukua mwaka mmoja tu kuweza kuingia katika darasa la Vipaji maalumu ambalo ndio niliweza kukutana nae kwani nilikuwa nikifundisha hapo , maksi zake zilikuwa za juu mno”
“Asante sana mwalimu kwa kunisifia?”
Upande wa Roma alikuwa kwenye mshangao tu miaka mitatu iliopita msichana wa kawaida pengine angekuwa High School lakini Clark alikuwa tyari ni Profesor kwenye vyuo vikubwa ndani ya Uingereza na Marekani , ukiachana na hilo pia alikuwa akifundisha wanafunzi wa vipaji maalumu kwa mtu wa nje ambaye hakuwa akimjua Clark pengine angeishia kushangaa na kutokukubali.
“Ukiachana na hayo, Zhang Rhu nakumbuka mara ya mwisho uliniaga kwamba unarudi China kwa ajili ya kazi , nimeshangaa kukuona kwenye tangazo hapa nchini Korea kama mtafiti”
“Nimeingizwa kwenye Project maalumu ya ubadilishanaji wa walimu kati ya Korea na China , nimekubali kuja Korea kwasababu ya kutaka kupata ujuzi wa kufanya kazi katika Project za kimataifa”
Ijapokuwa walikuwa wakisikia kabisa maneno yake hayana ule udhati ndani yake lakini Clark na Roma hawakutaka kuuliza zaidi isitoshe ni maswala yake binafsi.
Roma ili kuhakikisha swala ambalo limemleta Korea ni siri hakutaka kufanya watu wengi wajue yupo nchini hapo.
Zhang Ru ndio mtafiti ambaye alikuwa akihusika na Dhana iliopewa jina la Moyo wa Kibuddha hivyo kwao ingekuwa rahisi kuhusika katika Consecration hivyo hatua ya kwanza ya uthibitishaji ilikuwa rahisi.
Baada ya kupitia hatua za mwanzo mara baada ya kuingia hotelni Zhang Ru aliweza kugundua Roma na Clark wamechukua chumba kimoja na swala hilo lilionyesha kabisa kutomridhisha na alimuomba kuongea nae pembeni.
“Unataka kuongea nini Zhang Ru”Aliuliza Clark ambaye alikuwa kidogo kwenye sintofahamu ya kile ambacho Zhang Ru alitaka kumwambia.
“Teacher kwanini unataka kulala nae kwenye chumba kimoja?”Aliuliza .
“Tatizo liko wapi , ni mpenzi wangu”
“Hapana hata kama ni boyfriend wako kwanini mwanamke kama wewe ulale nae bila taratibu maalumu , hata kama mnalala kwenye kitanda kimoja bila ya kufanya chochote hairuhusiwi , Teacher mimi nimeolewa na nina uzoefu mzuri kwenye maswala ya kimahusiano , utaharibu taswira yako kama ukilala nae kabla ya ndoa”Aliongea huku akiwa na uso uliojaa usiriasi lakini ajabu ni kwamba clark alishindwa kujizuia na kuishia kutoa kicheko.
“Zhang Ru asante sana kwa wasiwasi wako juu yangu lakini ukiachana na mwonekano wake wa kawaida ambao unakuchanganya ambao kwangi n wa thamani lakini ninachoweza kusema ni kwamba nimemjua kwa zaidi ya miaka kumi , sio kwamba nimekurupuka tu kumchagua kama mpenzi wangu , hivyo kuwa na utulivu wa nafsi , mapenzi kwangu hayanishangazi”Aliongea
“Miaka kumi! , kama ni miaka kumi si wakati huo mtakuwa wote ni watoto , unajua nini kuhusu mapenzi kwa wakati huo , Teacher hata kama umempenda kupitiliza ukweli hauwezi kubadilika na hakuna ambaye anaweza kuamini maneno yako”
Ijapokuwa Zhang Ru alishawahi kuwa mwanafunzi kwa Clark lakini ukweli ni kwamba hawakuhi kukutana mara nyingi ni kama mara moja au mbili kwa wiki na mara zote ni wakati wa kipindi chake tu , ukiachana na kwamba alikuwa akimkubali Clark kama Clark lakini hakuwa akimjua ki undani zaidi.
Alikuwa akijua Clark alikuwa ni Princess wa Wales na ndio maana hakutaka kuona analala na mwanaume yoyote ambaye hana mwelekeo kama Roma.
Alikuwa ni mtu mzima kuliko Clark na alijua wasichana wa sasa hivi mara nyingi wanapotea linapokuja swala la mapenzi na Clark Stephanie Alexander ni mmoja wao.
Zhang Ru aliishia kuwaangalia Roma na Clark wakitembea pamoja kuingia kwenye Lift kwenda kwenye chumba chao na hali ile ilizidi kumtia mawazo na kujiambia kwanini asiwe hata ni mzungu wa kawaida lakini mwafrika wa kawaida kwake ilikuwa ni kituko cha mwaka.
“Hata mimi nishawahi kupenda mwanaume mweusi lakini hakuwa wa kawaida kuliko wa Clark”Aliwaza na palepale mawazo ya namna ile yalimtengenezea kukumbuku na macho yake yalichanua na kisha alitoa simu yake na kuingia kwenye mtandao wa Watsapp na kutafuta jina la mwanaume ambaye amemsahau kwa miaka mingi tokea kuachana nae kwa muda mrefu , unaweza kusema ni X wake wa muda mrefu.
“Zhang Ru..!! ni wewe kweli , siamini ”Sauti upande wa pili ilizungumza kwa kingereza.
“Nani mwingine kama sio mimi?”
“Haha,,, ni kweli ni wewe na kisauti chako , sijawahi kuwaza kuna siku utanikumbika na kunipigia simu , unaendeleaje , vipi kazi yako?”Sauti upande wa pili ilisikika na kumfanya Zhang Ru kutoonyesha tofauti yoyote.
“Asante kwa kuwa na wasiwasi na mimi Mr X , nilisikia ulipandishwa cheo mara ya mwisho, ila sijakupigia simu kukupongeza , nitaenda moja kwa moja kwenye sababu yangu ya kukupigia , nahitaji msaada wako , upo tayari au haupo tayari?”Aliongea kibabe.
“Nilijua tu huwezi kunipigia bila sababu”
“Kwahio unaniona msumbufu si ndio , basi nakata simu”Aliongea huku akiigiza kukasirika.
“Hapana usikate , nilikuwa nikiongea tu , haya niambie ni nini unataka msaada wangu , ili mradi ni halali nitakusaidia”Aliongea yule mwanaume.
“Looh hajabadlika kabisa huyu mwanaume”Aliwaza Zhang Ru kwenye kichwa chake huku akitoa tabasamu la kejeli..
“Nataka unisaidie kumchunguza mwanaume anefahamika kwa jina la Roma Ramoni ambaye anaishi hapo Dar es salaam , ana miaka kama ishirini na tano hivi kupanda na ameishi sana nje ya nchi , amerejea nchini kwenu hivi karibuni”
“Nini !?Roma Ramoni?”
“Una tatizo gani , mbona umepaniki kusikia hilo jina , una mfahamu?”
“Ndio namjua, kama kweli umekutana nae huko Korea , kwanini unataka nimchunguze?”
“Basi ni vyema kama unamfahamu , ninachotaka ni taarifa zinazomuhusu”
“Xiao Ru sitaki kukufaicha chochote kwa makusudi lakini huyo mwanaume … siwezi kukuambia ni nani haswa na hata kama nikikuambia jua tu kwamba nakudanganya”
“Basi poa , mimi nilijua tu hujawahi kunipenda na ulikuwa ukinionja tu kubalisha radha , tokea tulivyokuwa kwenye mahusiano yetu ulikuwa msiri sana mpaka tukaachana … nilijua tu tokea mwanzo upo kwenye mfumo ., hebu niskilize kama hutaki kunisaidia basi acha nitajua mwenyewe kupitia ubalozi”Aliongea kwa kukasirka .
“Ru habu kwanza nisikilize sio kwamba sitaki kukuambia chochote lakini huyo mwanaume ni hatari, usije ukamchokoz…”Kabla hata hajamaliza kuongea Zhang Ru alikata ile smu kihasira hasira.
“Eti hatari , kila mwanaume ambaye ataweza kuwa karibu na Clark lazima awe ni hatari ndio kama sio jasiri “Aliwaza.
Aliendela kuwaza au pengine ni mhalifu kutoka huko Tanzania ambae anaogopeka , kama sio hivyo kwanini anaogopa kutoa taarifa zake.
Baada ya Zhang Ru kujifikiria kwa muda alianza kupatwa na hofu na kujiambia au yupo karibu ya Clark kutokana na ubini wake.
“Yeah nimekumbuka , Moyo wa Kibudha , Teacher Clark alisema huyu Roma yupo hapa Korea kwa ajili y a moyo wa Kibudhha …. Inamaana anajaribu kutumia ukaribu wake na Clark kutaka kuiiiba?”
Zhang Ru aliona utakuwa ni ujasiri wa aina yake kama kweli Roma atakuwa na mawazo hayo.
“Profesa Zhang unafanya nini hapa?”
Sauti kutoka nyuma yake ilimshutua na palepale aliweza kuona sura ya mwanamke Polisi alievalia gwanda za jeshi la polisi la Korea akiwa anaingia ndani ya hoteli hio.
Huyu mwanamke wa Kikorea alionekana kama alikuwa kwenye miaka arobaini hivi lakini ni aina ya wanawake ambao wanajipenda , alikuwa na lipsi nyekundu mno huku akiwa mwembamba na umbo lake tatanishi.
“Kapteni Hwang ..”Aliita Zhang Ru huku akiwa katika tabasamu .
Hwang Sooyeon ni polisi katika idara ya ulinzi ya jeshi la polisi ndani ya jiji la Seoul , alikuwa ndio mkuu wa idara ya ulinzi na alifahamiana na Zhang Ru sana tu.
“Profesa unafanya nini hapa?”Aliuliza Kapteni.
“Oh,,,Mwalimu wangu , Profesa Clark , Mkuu wa Royal Academy of Sciences kutoka Uingereza yupo hapa , amekuja kwa ajili ya kuangalia mabaki ya moyo wa Kibudha na nimemleta hotelini”Aliongea
“Mkuu wa idara ya Royal Acadamy? , basi inaonekana atakuwa mtu mzito mno kiasi cha kukufanya Profesa kama wewe kuja mpaka hapa , sishangai ndio maana umeweza kuongoza utafiti wa kuchunguza moyo wa Kibudha kwa umri huo mdogo… kama sikosei basi utakuwa ni mwanafunzi mwenye akili wakati anafundisha …”Aliongea huku akitabasamu
Upande wa Hwang Sooyeon palepale wazo lilimjia na kujiambia au akaripoti swala hilo kwa chifu , pengine Clark kama ataalikwa kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Consecration italetea taifa umaarufu”
NB:Consecration Ceremony mara nyingi ni sherehe za maonyesho ya kuweka Wakfu kitu flani , kwa mfano hao waumini wa Budha wanafanya sherehe ya kuweka wakfu moyo huo wa Kibudha.