NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.
SEHEMU YA 680.
Kila mtu alishangaa mara baada ya Clark kilichompata Yezi ni sumu , hakuelewa sumu hio imetokea wapi na Yezi asingeenda mbali hivyo kunywa sumu kwasababu tu hataki ndoa moja kwa moja kila mtu alijuwa amewekewa sumu.
Clark hakujisumbua hata kutoa majibu kwa Park Juan na watu wengi waliokuwa wakitaka maelezo.
“Hubby mtoe Yezi hapa tumpeleke sehemu tulivu”Aliongea Clark.
Roma hakutaka kujali chochote na palepale alimbeba Yezi na kwenda kumpeleka kwenye moja wapo ya vyumba vilivyokuwa ndani ya eneo hilo huku Clark akimfuata kwa nyuma.
“Kulingana na uzoefu wangu pamoja na uelewa , dalili zinaonyesha sumu ni Pottassium cyanide , ni sumu ambayo ikishaingia mwillini inasharabu maji na Carbondioxide na kudhalisha Hydrogen cyanide , inasababisha mwili kukakamaaa , shida ya kupumua na kuzuia mzunguko wa damu mpaka kupelekea kifo”Aliongea Clark na Roma palepale alimuweka Yezi kwenye Sofa.
Alikuwa akitetemeka pamoja na kukamaa mfululizo na macho yake yalikuwa yamechomoza(.
“Sijali ni sumu ya aina gani , niambie ni kwa namna gani tunaweza kumuokoa”
“Tushachelewa kwa matibabu ya dharula , Hubby kwanini usitumie mbinu yako ya kijini ya andiko la urejesho pamoja na vidonge kumwingizia nguvu ya kijiji ndani ya mwili wake na kuimarisha seli za mwili , ziishakuwa na nguvu itakuwa rahisi kumetabolize na kutoa sumu mwilini”Aliongea Clark.
Rpoma alijua hana muda wa kufikiria kwa wakati huo , alishawahi kumtoa mtu sumu mwilini lakini kuhusu sumu hio ilikuwa kali sana.
Dakika ileile alitoa kidongea alichotengeneza kupitia mifupa ya majini Joka na mimea na kisha akamlisha Yezi.
Kidonge cha aina hio kazi yake ilikuwa ni kuimarisha mwili lakini pia kurahisisha nguvu ya kijini kufanya kazi ndani ya mwli , baada ya kufanya hivyo palepale alianza kumwingizinai nguvu ya andiko kuyeyusha kile kidonge ili kuingia katika mzunguko wa damu/.
Muda huo kundi lote likiongozwa na babbu yake Yezi walikuwa washakifka mlangonni na Clark aliwazuia kwa nje.
“Sir kama unatuamini tafadhari usiingie ndani au vinginevyo utalipia gharama za kumpoteza mjukuu wako”Aliongea kibabe huku akitoa ile Aura ya kuogopeka.
Park Juan alijikuta akirudi nyuma kwa hofu kidogo , lakini alikumbuka uwezo wa Clark katika matibabu pamoja na mbinu za Roma za kimaajabu alijikuta akirulia kidogo na kuizhia kungata meno kwa hasira na kukinga wengine.
“Okey kama dokta alivyosema hakuna anaeruhusiwa kuingia”
Mabodigadi muda uleule walizingira eneo lote kutoruhusu mtu na wageni walianz akuondoka mmoja mmoja.
“Sir natoa ushauri wa kuzuia eneo lote ambalo Yezi alikuwepo , kila
mmoja hapa ni mtuhumiwa , baada ya Yezi kutoka katika hatari tunapaswa kumkamata muhusika”Aliongea Clark na kumfanya Park Juan palepale kuelewa na kutoa maagizo kwa watu wake kufanya kazi hio.
“Dr Clark Yezi ndio uhai wangu… tafadhari naomba muokoeni”
Aliongea Park Juan akiwa amepiga magoti mbele ya Clark na palepale alimzuia na kumfariji.
“Usiwe na wasiwasi , kulingana na nilichoona dosi ya sumu iliompata ni kidogo sana ndio maana hajafa hapo hapo , kuna matumaini makubwa ya kupona”
Clark hakutaka kumpa matumaini makubwa, isitoshe sumu kama Potassium Cyanide na asingeweza kumsaidia kama asingekuwepo Roma.
Inaonekana aliedhamiria kufanya jambo hilo alikuwa amenuia kumuua kabisa.
“Sir nitahitafi vifaa na baadhi ya dawa , najua mtu ndani ya taasisi moja ya kikemia hapa nchini naomba umwagize mtu anisaidie kuvileta”Aliongea na Park Juan hakuuliza mara mbilimbili na alikubali maagizo yake.
Muda nao ulisogea , ile hali ya furaha na shangawe iliokuwa imetegemewa ilikuwa imepotea na wahudumu waliopangwa kuwa ajili ya sherehe hio walikuwa wamejikusanya sehemu moja huku kila mmoja akiwa na mwonekano usiokuwa ukielezeka.
Wageni pia hakuna ambaye aliruhusiwa kuondoka , kuna ambao walikuwa wakiomgea kupona kwa Yezi lakini pia kuna wale waliokuwa wakiombea kutopona kwake.
Lakini wote walionekana kuwa na shauku ya kutaka kupata taarifa ya kile kinachoendelea .
Ndani ya chumba katika Sofa Roma alikuwa bize kuondoa sumu mwilini kwa spidi kubwa, na kila anapofanya mwili wa Yezi uliota vipele vikubwa kwenye ngozi yake ambavyo vilikuwa vimejaa damu nyeusi mpaka anakuja kumaliza raundi ya mwisho alijikuta akivuta pumzi.
Roma alipatw ana ahueni mara baada ya kuona sasa Yezi alikuwa akipumua vizuri na rangi yake ya uso ilikuwa imemrudia ikimaanisha mzunguko wa damu ushaanza kufanya kazi.
Baada ya hatua ya awali kukamilika alimwingizia Yezi nguvu ya kijini na kisha kuibadilisha kuwa maji ya kiroho na yakaanza kusafisha sumu yote mwilini na ndani ya dakika chache tu vile vipele vilianza kupotea.
Clark aliekuwa akilinda mlangponi alijikuta akivuta pumzi yaa hueni mara baada ya kuona mafanikio hayo.
“Asante Mungu ulikuwepo na pia umerudiwa na nguvu zako , la sivyo Yezi angekufa”Aliongea Clark mara baada ya kuona Roma sasa amemaliza.
Roma aliishia kushika mashavu ya Yezi na kurudisha nywele zake nyuma , ilipasw akuwa harusi yake lakini ndio hivyo kidogo tu afe.
Kitendo cha kuhisi kuna mtu ambaye alitaka kumuua Yezi kilifanya macho yake kutokuwa ya kawaida kabisa.
“Ulienda kufanya utafiti katika eneo la tukio?”
“Yeah , nimegunfdua namna tukio lilivyofanyika lakini sijampata muhusika bado”
Hawawezi kufanya hivi bila ya kuhudhuria sherehe , muhsika lazima atakuwa ni mtu ndani ya hili eneo , wachungune zote mmoja mooja nina uhakika tutampata”Aliongea Roma na wote kwa pamoja waitoka.
Baada ya taarifa kutolewa kwambaYezi ametoka katika hatari ya kifo ParkJuan alifurahi sana na kumshukuru Roma kwa kazi yake.
“Mr Roma naruhusiwe kwenda kumuona Yezi?”AliulizaPark Juan.
“Hapana , kila mtu ndani ya hili eneo ni mtuhumiwa mpaka pale tutakapo pata muhusika mwenyewe ,, hiyo nazuia mtu yoyote kusogea karibu na chumba alipo Yezi”Aliongea Roma kwa Kikorea na kufanya kila mmoja hapo ndani kutofurahishwa na kauli yake.
“Wewe ni nani , kwanini tukusikilize?” bwana mmoja alieonakna kama kiongozi aliongea huku akionyesha kejeli , alijiambia kwanini amsikilize mtu mweusi.
“Kama unajiamini sogea uone , nitakukuchukulia kama mtuhimiwa mkuu”Aliongea Roma kibabe na kufanya watu wote kumwangali kwa macho ya wasiwasi.
Yule bwana hakutaka kuleta fujo , pengine aliogopa Roma alivyokuwa akiongea na hakuendelea.
Hakuka mgeni ambaye alitaka kuchukuliwa kama mhalifu hivyo moja kwa moja walitulia katika eneo walioelekezwa.,
Dakiika hio hio Clark alisogea akiwa ameshikilia Shera ambayo alikuwa ameivaa Yezi na kuwaonyesha watu wote.
“Jamani hebu angalieni , hii shera ndio imetumika kumuwekea Sumu Yezi , mtuhumiwa alichokifanya ni kupaka hii shera na sumu aina ya Pottasium Cyanide , wakati Yezi alipokuwa akipumua ule unyevu nyevu wa maji uligusana na Pottasium Cyanide na kugeuka gesi aina ya Hydrogen Cyanide ambayo ni sumu kali inapoingia kwenye mapafu, nimeulizia na kuambiwa gauni la harusi halikupewa ulinzi wala umakini wa ki usalama hivyo kutoa nafasi kwa mgeni yoyote yule kulishika wakati lilipokuwa linapelekwa kwa ibi harusi , hivyo mtu yoyote anaweza akfanya hili tukio , tunaomba ushirikiano wenu”
“Hakuna mtu yoyote ambaye anaruhusiwa kuondoka hili eneo mpaka uchunui ukamilike , wale wote ambao wana kinyongo na familia ya Park aisha ni zamani au sasa hivi naomba msogeee mbele”
“Unatakia wewe katika swlaa muhiu kama hili , kama ni kuanza anza na vijakazi kwanza na wahusika waliompaka Makeu , ndio wahusika wa kimantiki”Alibweka mkorea mmoja.
“Sitaki unifundishe ninachofanya , hata wao pia wafanyiwa uchunguzi isitoshe kwanini waweke gauni sumu ilihali watakuwa wahusika wa kwanza?”Aliuliza Roma na kufanya wageni wote kuona ana mantiki.
“Kama unataka kujua ni nani ambaye ana kinyongo na familia ya Park basi itakuwa ni familia ya Gong Gyechung”Alionga mgeni mmoja na kumfanya Gong Gyechung na Gong Woo kumwangalia kwa macho makali.
“Hatuwezi kufanya kitu cha kijinga kama hichi , Yezi anaweza akawa amemkataa mtoto wangu lakini baba yagu alikuwa nni mtu wa karibu na Mzee Park , familia zetu ni kama ndugu”
“Hakuna ambaye anaweza kuamini hivyo , kila mmoja anaua kwamba ulitaka Mzee Park kuendelea kuugua wakati huo ukimfanya mtoto wako kumuoa Yezi”
Muda kama huo kila mgeni alitaka kuondokana na tatizo hilo na kwasababu Park Juan alikuwa amekasirika iliuwa rahisi kubebesa mzigo familia nyingine.
Gong Gyechung na ndugu zake wote walijua kabisa wao ndio washukiw anamna moja kutokana na matukio yaliopita , ilikuwa ni sawa kusema wana sababu za mzingi kufanya tukio kama hilo.
“Hatuhusiki , baba haina haya ya kujibizana nao na hakuna ambaye ana uthubutu wa kutuzuia kutoondoa apa”Aliongea Gong Woo huku akimwangalia Roma kwa hasira.
“Upo sahihi mwanangu , nyie watu hapa wote ni kama mbwa kichaa tu na manchofanya ni kutaka kunibebesha lawama mimi na familia yangu ili kujiokoa , hivi mnadhani tunaogopa?”
“Halafu tunaruhusuje mtu kutoka mataifa yanayoendelea kutuamulia maswala yetu , acheni kuongea upumbavu nitapigia simu polisi waje waweke polisi”
Baada ya kuongea vile kila mmoja alikumbushwa nafasi yake kama jamii , ni kweli waliokuwwpo hapo ndani ni watu kutoka mataifa mbalimbali ndani a Asia ambao wana ukwasi mkubwa wa pesa , kwannini wamsikilize mtu mweusi, isitoshe hata kuhudhuria kwao ni kwa ajili ya heshima kwa Park Juan.
Gong Gyechung na ndugu zake walianza kuomba kupishwa njia kuondoka ndani ya eneo hilo.
Upange wa wageni na wenyewe walianza kujidharau kwa kukubali maneno ya mtu mweusi kama Roma na waliishia kumwangalia Roma kwa macho ya kejeli.
Park Juan mwenyewe alishajua kuhusu hilo kulikuwa na watu wazito ndani ya hilo eneo na matajiri kuliko hata yeye mwenyewe na ni ngumu kukubali kuonyesha ushirikiano
Kundi lote lilianza kutafuta njia ya kuondoka , huku wengine wakianza kupanga mipangyo ya ukutana makusudi kabisa wakionyesha kuchukizwa na Roma
Lakini sasa Roma alionekana kutopendezwa na dharau zao na palepale alienda kuwazuia Gong Gyechung na familia yake.
“Unafanya nini? , hjui kwamba hii ni nchi inayoendeshwa kisheria , tutakufunga kwa kutuingilia ndani ya nchi yetu”Aliongea Gong Gyechung kibabe.
Roma hakujali maneno yake na palepale alisogea mpaka karibu na mlango wa kutokea na palepale alipasua Chandelia kubwa iliokuwa imening’inizwa.
Kwa namna alivyoruka mpaka kuipasua na kuja kutua chini ilifanya wale wageni kurudi nyuma kwa hofu na hata Park Juan mwenyewe alijikuta akipatwa na hofu.
Roma hakuishia kwenye kupasua tu ile Chandelia palepale alianza kusambaza nguvu ya kijini ya kutia watu uoga na kufanya kila mtu kushindwa kupiga hatua na hata wale ambao walikuwa wakimwangalia kwa Dharau walianza kuona woga.
“Nitaanza na nyie”Aliongea Roma na palepale alimshika Gong Gyechung pamoja na Gong Woo na kuwarushia katikati kama mafurushi na kisha alimpa ishara Clark kuwaagiza mabodigadi kuwasachi.
Walisachiwa wote kwa haraka haraka na wale mabodigadi na Clark pia alifanya baadhi ya vipimo vya kikemikali na aliona kila kitu kipo sawa.
“Sio wahusika”Aliongea Clark na palepale Roma aligeukia wagenni wengine.
“Kama nilivyosema wale wote wenye uadui na kinyongo na famili aya Park watoke mbele”Aliongea Roma huku akisambaza hali ya woga na kila mtu hapo ndani alimuona kama Simba na watu zaidi ya kumi na mbili walitoka mbele.
Clark aliwasachi wote lakini hakuna ambaye alkuwa ni muhusika na aliongeaka kushangaa .
“Hii inashangaza , kutokana na muda na namna tukio lilivyofanyika kama kweli walikuwa wakitaka kuweka sumu kwenye shera asi lazima kuna poda ingebakia , au ni wahudumu ndio wamefanya?”
“Wote wapo hapa , hili eneo nimelizingira na nguvu za kijini na hakuna ambaye ametoka , kama hatuwezi kupata ushahidi kutoka kwao basi tutaanza kutafuta eneo lote” Aliongea na Clark alitingisha kichwa na kisha akamwambia Park Juan kuwajumisha na wahudumu.
Lakini na wao wenyewe walisachiwa na kufanyiwa vipimo na kifaa maalumu lakini hakuna ambaye alipatikana.
Muda huo huo Roma aligeuza macho yake kwa Eujung ambaye alikuwa amesimama pembeni ya Park Juan.
“Eujung wewe kazi yako ni kumhudumia Yezi , unapaswa kukaguliwa pia”Aliongea Roma na kumfanya Park Juan na Mzee Km kumwangalia Eujung kwa mshangao ni kama hawakuwamini kama anaweza kufanya tukio la namna hio , itisothe amekuwa kkaribi na Yezi kwa muda mrefu sana na alikuwa akimjali sana.
Eujung aliishia kulamba lips tu kuuvaa ujasiri na kisha alisogea mbele kwa ajili ya kukaguliwa.
Clark palepale kwa kutumia Gloves alianza kumsachi Eujung na kisha akachukua sample flani hivi kwenye nguo zake na kisha akaichanaganya na kimiminika(Solution) chenye rangi ya maji lakini sasa baada ya kutingisha kwa dakika chache tu palepale rangi ilibadilika na kuwa pink na kumfanya Clark kutoa macho.
“Pottassium Cyanide , Ejung wewe ndio muhusika?”Aliuliza Clark kwa mshangao.
SEHEMU YA 681.
Kila mtu alishangazwa na kauli ya Clark na waliishia kumwangalia Eujung kwa mshangao mkubwa kana kwamba alikuwa akitegemea hilo , Eujung aliishia kungata lips zake za chini na kisha akainamisha kichwa chake chini bila ya kuongea neno.
Muda huo wageni wote wlaijikuwa wakipatwa na ahueni kutoka na na kwamba hawakuwa watuhumiwa tena kwasababu mhusika amekamatika.
“Inawezekanaje ,…. Kwanii awe ni Eujung?”Park Juan alijikuta akitetemeka huku akirudi nyuma kwa mshituko na macho yake yalibadilika palepla e a kujawa na hasira.
“Wewe mwanaharamu , nini ambacyo nilikukosea , kwanini ukamuwekea sumu Yezi?”
Kim Yang na Kim Jip waliishia kukunga sura tu huku wakimwangalia , Kim Jip alikuwa ni kama vile atalipukwa na hasira iliokuwa imemvaa.
Roma muda huo aliishia kutulia sasa na kumwangalia Eujung akisubiria maelezo yake.
Eujung macho yake yalimvimba kutokaa na kutoa machozi mengi na palepale aliinua uso wake huku akionyesha tabasamu la maumivu na aliishia kumeza mate huku akimwangalia Park Juan.
“Sir , naomba unisamehe lakini nimeisubiria hii siku kwa muda mrefu”
“Nini?”Aliuliza Park Juan kama vile hajamsikia vizuri.
“Nina uhakika ushamsahau mwanamke uliekutana nae miaka ishirini iliopita , jia lake anaitwa Ho Jiwan”Aliongea Eujung.
Park Juan palepale alijikuta akianza kutetemeka huku akiinua kidole chake akimnyooneysa Eujung.
“Wewe ,,,, wewe ni …”
“Ndio , Ho Jiwo ni mama yangu na mimi naitwa Ho Eujung”
“Hapana , haiwezekani , alisema alisema ,….”Park Juan alikuwa kama mtu ambaye anajaribu kuvuta kumbukumbu.
“Naona umeshindwa kuongea , basi nitakusaidia , kipindi kile wakati mama yangu akiwa msaidizi wako ulimtongoza ili kuwa mpenzi wako na mara baada ya kukubalia na kumpa mimba ulimwmabia aitoe kwasababu uliogopa ingekuhabiria taswira yako , mama hakutaka kuitoa hivyo alikudanganya na mimba ile ndio nilizaliwa mimi , mwanzoni alipanga baada ya mimi kuzaliwa kuja kukubembeleza ili unikubali lakini wewe ukampatia hela na kumfukuza tu ili kuzima uvumi ndani ya kampni , hivi unajua hajawahi kutabasamu tokea siku ambayo amenizaa , alikuchukia kwasababu ulimtelekeza na alikuwa akiinipita kila saa na kunifokea akinilazmisha kupiga magoti na kuniongelea maneno ya laana , alikuwa ni mlevu wa kupindukia mpaka anakuja kupta saratai ya ya ini daraja la nne , nilikuja kugundua wewe ndio baba yangu wakati akiwa ndio anakaribia kufa ndio aliniambia kila kitu na kuniomba msamaha lakini sikutaka kumlaumu , mtu amaye namchukia ni wewe”
Aliongea Eujung huku akitoa kilio , kitendo cha kuzuia hisia zake na kuzitoa wakati huo ilimfanya kutikisika mabega kwa kulia.
Park Juan alijikuta akijikalia chini ila kujilwa , ni kama amezeeka na hajiwezi au ni kwasababu ya hatia ya matendo yake.
“Kwahio ,,, kwahio ulikuja ndani ya familia yangu kwa ajili ya kulipiza kisasi?”Aliongea Park Juan huku akimwagalia mtoto wake wa kumzaa ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kihudumu.
Mpaka hapo ilimaanisha kwamba ndio mtoto wake wa mwisho , Park Jiyeon ni wadogo zake walikuwa katika hali mchanganyiko kwani hawakutegenea kijakazi wao amegeuka kuwa mdogo wao.
“Upo sahihi , nilijifuza Taekwondo na maswala ya kihudumu na ndio nikaingia kwenye familia yako , nilikuangalia siku zote na sura yako ya kinafiki na nimefikia hatua ya kumtaka mjukuu wako unaempenda kufa kwenye harusi yake , ninataka ilimpie gharama kwa dhambi zako..”Aliongea kwa kufoka.
“Park Cheon mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno na kama sio kutumia vidonge vya Roma basi presha inempanda.
“Mtoto wangu …. Eujung naomba nisamehe”Aliongea na kufanya kundi lote kushangaa kutokana na kitendo cha Pakr Juan kukubalii .
“Eujung nimeshi kwa majuto sana kwa makosa ambayo nilifanya miaka migi liopita , nilitamani kumtafuta mama yako na kumwomba msahama lakini niliogopa amna ambavyo angeniangalia ,,, Eujung naomba unisamehe mimi baba yako , nipo tayari kukupokea na kulipa fidia kwa miaka yote ambayo sikukutambua… Eujung mwannangu nipatia nafasi”Aliongea Park Juan.
“Acha kuwa mnafiki, uaniombaje nikupe nafasi ilihali nilitaka kumuua mjukuu wako na sumu?”Aliogea na ni kama Park Juan alishasahau na palepale alimgeukia Roma.
“Mr Roma tafadhari muachilie Eujung , alifanya hata yote kwasababu ananichukia sio kwasababu anamchukia Yezi , kwasababu Yezi yupo salama naomba hili liishe na nakuhidi hiki kitendo hakitotokea tena….Ejung ni binti yangu na siwezi kuruhusu kumuona akifa mbele yangu”Aliogea kama vile alishajua mpango wa Roma ni kumuua muhusika.
“Mimi sitaku unafiki wako , nipo tyari kufa , naomba umuache Mr Roma anue hapa hapa , hhio ndio njia pekee ya kunifanya nisikuone tena , nina shtahili”
“Wewe , Eujung acha kuwa mjinnga …”Alifoka na akaendelea kumuomba Roma Eujung asamehewe.
“Mr Roma nitakubali chochote utakachohitaji ili mradi utamuacha Eujung”
“Mimi sijali kama ni mtoto wako , anapaswa kufa kwa kumdhuru Yezi”Aliongea Roma kibabe na kufanya jopo lote la watu kupatwa a ubaridi na waliona Roma alipaswa kuacha lipite , isitoshe Yezi amwksiha kupna na Eujung alikuwa akitia huruma.
“Nitakufa kwa niaba ya Eujung , Mr Roma niue mimi , hata hivyo imeishi maisha marefu lakini Eujung bado ni mdogo”Aliongea Park Juan na kwa wakati huo hakuonekana kama tajiri bali alionekana kama baba.\
Roma aliishia kukosa uvumilivu na palepal e alimsukuma Park Juan mbali na kisha akampa ishara Clark kumuondoa
“Hebu acha kunichukiza , mtu ninaemua hapa ni binti yako na sio wewe”Aliongea Roma na palepale alimsogelea Eujung.
Eujung aliishia kufumba macho yake akikisubiria kifo , alikuwa akijua uwezo wa Roma hivyo aliamini hata kama akileta ukinzani asingeshinda.
“Huwezi kumuua”Sauti ya kikauzu na ya kibabe ilisikika na palepale Kim Jip alikuwa ashamkingia Eujung kwa mbele akimwangalia Roma kwa macho makali kama Cobra.
“Unadhani unaweza kunizuia?”Aliuliza Roma.
“Siwezi”
“Kama ni hivyo unafanya nini?”
“Nimesimama hapa sio kukuzuia bali kukuambia ukweli wote”
“Ukwel?”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kifedhuli
“Hapana”Eujung alimvuta Kim Jip kumtoa mbele yake.
“Sogea mbele yangu , anania mimi na sio wewe , unafanya nini”Aliongea Eujung na palepale Kim Jip alimkumbatia kwa nguvu Eujung na kisha akamwagalia Roma.
“Mimi ndio nimemuwekea sumu Yezi na sio Eujung”Aliongea na kumfanya Eujung kuanza kutoa kilio na kumpiga piga Kim Jip kifuani.
“Kwanini unafanya hivi , nilitaka kufa mimi , kwanini…”Aliogea Eujung.
Waliokuwa wakiangalia igizo hilo ni kama walishajua nini kiaendelea kati yao
Kim Yang baba yake Kim Jip alijikuta akipauka uso baada ya kusikia maneno ya mtoto wake , alikuwa katika kiwango cha juu cha hasira na dani ya dakika hio hio alijikuta akipoteza fahamu na kusaidiwa na mabodigadi.
“Roma huwezi kumuua mtu asie na hatia , , ninakuamini na nipo hapa kukuambia kwamba mwanamke ninaempend akweye maisha yangu ni Ho Eujung , ndio mwanamke ambaye napend akusihi nae maisha yangu yote , ninaweza kumuua Yezi tena naweza kwenda mbali zaidi na kumua raisi Park kwa ajili yake , najua sio fair kwa Yezi lakin sikuw ana chaguo lingine , ninaweza kuwa kichaa au mwanaharamu”
“Lakini ukaguzi na majaribio ya kisayansi yameonyesha yeye ndio kamuwekea sumu unaongea vipi hapo?”Aliuliza Roma.
“Wewe mwenyewe huoni inashangaza kama kweli ni muhusika basi angehakikisha aabadilisha mavazi a haachi ushihid wa aina yoyote , lakini Eujung pengine alipata kichupa ambacho kilikuwa na sumu wakati akiweka sawa suti yangu”Aliongea na kisha alimwangalia Eujung kwa macho ya kimahaba.
“Wewe mwanamke mjinga kwanini ulifanya hivyo , yalikuwa ni maamuzi yagu hivyo nipo tayari kufa lakini nimefurahi , siku zote nilidhania hukuipenda kweni lakini imeondakana nilikudhania ivbaya , upo tayari kufa kwa niaba yangu ,,, nimefurahi”Aliongea
“Mimi sitaki ufe ,,, sitaki ufe”Aliongea Eujung.
Wageni waliokuwa wakiangalia waliishia kuwaonea huruma hao wenza, ile hofu waliokuw anayo ilishapotea na sasa walishangaa drama hizo.
Roma muda huo ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kutoa tabasamu la ushindi na kisha akamgeukia Clark.
“Babe unaonaje maigizo yangu , nadhani ninastahili tuzo…”Aliongea Roma na kumfanya Clark kutoa tabasamu na palepale alimkumbatia Roma na kumpiga busu.
“Upo vizuri ,,, maigizo yako ni ya viwango”
“Hehe… ni kwasababu na script ulizoniandikia mwenyewe”
Baadhi ya waliokuwa wakielewa kingereza walishangazw ana maneno yao a walionekana kutaka kusikia maelezo yao kwani ni kama vile tukio zima wlaikuwa wakilifahamu.
Clark palepale alitoa chupa yenye kimiminika cha ragi ya pink na kisha akaweka kwenye test tube.
“Nyie watu hamjui Chemistry , hivi mnadhani sumu aina ya Pottasium Cyanide inaweza kugudulika na jaribio la nama hii..”
Maneno yake yaliwashangaza kundi lote ikiwemo Kim Jip na Eujung wlaiokuwa wakibembelezana.
“Mr Roma ,Dr Clark kwahio unaseme ,,, hiki kilichofanyika ni kwa makusudi maalumu?”Aliuliza na kumfanya Eujung nae akili yake kujirudia.
“Kwahio hukugudua chochote wakati wa kuisachi?”
“Ndio , unadhani ni rahisi kuinasa sumu ya Pottasium Cyanide , ukweli ni kwamba Eujung alijimwagia poda , nilitaka kumsachi Kim Jip kwa mara ya mwisho lakini mpango wangu ulienda vizuri”
“Kwahio ulijua mimi ndio muhusika tokea mwanzo?”Aliuliza Kim Jip.
“Sikujua kwa uhakika kwani hata Ejungun pia nilimdhani …”Aliongea Roma.
“Niliweza kugundua kuna kitu kinachoendelea nyie wawili kwa muda mrefu , pengine mlijua mmejificha vizuri lakini kuna vitu mmeshindw akuficha , mara ya mwisho wakati nikiishi ndani ya familia ya Yezi , mara baada ya Park Juan kusema anataka umuoe Yezi a wewe kutoonyesha ishara yoyote ya kutomtaka kabisa na hukutaka kumwangalia kabisa usoni lakini wakati alipoiwa akipandisha kwenda juu uligeuza shingo na kumwangalia , nilijiuliza kwanini ugeuze shingo lakini mara baada ya mimi kunagalia nilijua ulikue ukimwangalia sio Yezi bali I Eujung…..”Roma aliendelea kuongea ishara ambazo aligundua kuhusiana na Eujung na Kim Jip kupendana , alikuwa gwiji kwenye mapenzi hivyo ilikuwa rahisi kuusoma mchezo muda mrefu.
Roma mara baada ya kugundua viashiria vya kimapenzi kati ya Kim Jip na Eujung palepale aliwapa kazi watu wake kufatilia taarifa zinazomuhusu Eujung a ndipo alipokuja kugundua mapema kabisa kwamba Eujung ni mtoto wa Park Juan wa nje ya ndoa
“Eujung nilifahamu wewe ni mtoto wa nje ya ndoa wa Park Juan kwa muda mrefu sana ..”Alimalizia Roma na kufanya kila mtu kushangazwa na maneno y ake yalivyonyooka na kuwa katika mpangilio wa kimatukio.
Hawakuamini mtu mweusi na mkatili kama Roma anaweza kujega hoja pamoja na kunyaka viashiria vidogo namna hiyo na vikawa ukweli.
Ukweli ni kwamba pengine ni kutokana na ubize wa Park Juan ndio maana alishindwa kugundua lakini Kim Jip alikuwa katika penzi nzito na Eujug kwa muda mrefu sana na hata baadhi ya vijakazi walikuwa wakijua hilo lakini walikaa kimya.
“Kama yote hayo uliyajua kwanini bado ukataka nimuoe Yezi , ulipaswa kujua kwmaba nisingeweza kumpenda na kumpa furaha”AluongeaKim Jip.
“Kwasababu Roma alikuamini wewe kama wewe”Alijibu Clark.
“Mimi kama mimi?”
********
Siku kadhaa mbeleKim Jip na Eujung walifunga ndoa rasmi mara baada ya kusamehewa kile walichokifanya na Yezi.
Roma alitaka kumuadhibu Kim Jip kwa kile kilichotokea lakinin Yezi aliingilia kati na kuomba Kim Jip kusamehewa.
Upande wa Yezi alitumia nafasi hio kuweka hisia zake wazi kwama aampenda Roma kimapenzi na anataka kwenda kuishi nae , maneno ya Yezi yalishangaza kila mmoja na hata Roma mwenewe.
Park Juan alikataa Yezi kujihusisha kimapenzi na Roma kwani tayari amekwisha kuoa lakini Yezi aligoma huku akitumia tukio la mama yake na baba yake lilivyowakuta mpaka kumfanya kuwa yatima na Park Juan mara baada ya kukumbushwa namna alivyovuruga mapenzi ya mtoto wake Park Jooncheni baba yake Yezi alijikuta akijawa na hatia na aliishia kukubali mahusiano ya Yezi.
Yezi aligoma kabisa kufanywa mrithi wa familia na alichokuwa akitaka ni kuishi karibu na Roma na Park Juan hakutaka kumlazimisha na mwisho wa siku aliamua kumfanya Eujung kuwa mrithi wake ajae..
Park Juan hakujari sana watu watakavyomuongelea , ukweli ni kwamba licha ya kwmaba hakuwa tayari kumwachia Yezi kuwa mwanamke wa Roma lakini aliamini kuna faida kubwa sana kwa familia yake uwa a undugu.
Roma aliweza kuodoka Korea kabla ya harusi ya Kim Jip na Eujung a hakurudi Tanzania moja kwa moja bali alielekea visiwa vya wafu.
Roma kabla ya kuanza safari aliambiwa Neema Luwazo , Najma, Amina na Lanlan walishafika Visiwa vya wafu kasoro Rufi tu ambaye alikataa kondoka Tanzania kwa ajili ya kutaka kukaa na mama yake.
Roma mara baada ya kusikia sababu ya Rufi alioa ipo kimantiki kwani Bi Wema alikuwa mpweke sana na kama kila mtu aliodoka basi angekuwa peke yake , isitoshe Edna alikuwa mtu bize sana hivyo hakutaka kumalizimisha Rufi kwenda visiwa vya wafu.
Upande wa Yezi yeye alibakia Korea na alipaswa kuhudhuria harusi ya shangazi yake Eujung na baada ya hapo kuagana rasmi na familia na kuja kuungana na Roma katika visiwa vya wafu na kuanza kuvua nishati ya mbingu a ardhi kama wengine.
SEHEMU YA 682.
ISLAND X
Ni ndani ya kisiwa X katika makao makuu ya kambi ya kisayansi ya shirika la siri la Zeros Organisation.
Ni siku kumi na mbili tokea kwa Naira kurudi ndani ya kambi hii rasmi baada ya kuondoka kwa takribani mwaka mmoja.
Katika siku zote kumi na mbili Naira alikuwa amepewa uhuru wa kuchagua idara yoyote ambayo atapenda kujiunga nayo kwendeleza misheni za kisayansi ambazo ziaendelea ndani ya hilo eneo.
Kambi hii ilikuwa na maajabu yake , ukichana na kwamba wafanyakazi wote wanaongia ndani ya eneo hilo hawakuwa wakiruhusiwa kutoka lakini vilevile watafiti wote wlaiokuwepo ndani ya hio ngome muda wote walikuwa waiifanya vitu ambavyo vinawapa ubongo wao maairfa mengi zaidi na zaidi.
Inasemekana kwamba asilimia sabini ya wafanyakazi wote ndanni ya hio kambi hawana wazazi wala ndugu katika ulimwfengu wa kawaida na walikuwa ndugu wao kwa wao.
Unaweza ukashangaa hili linawezekana vipi lakini ndio utaratibu uliowekwa tokea kuanza kwa kambi hio, kuna binadamu walipo ndani ya eneo hilo ambao walizaliwa hapo hapo kwa njia za kisayansi zaid lakini kuna wale pia ambao walizaliwa nje ya eneo hilo ambao walionekana kuwa na uwezo mkubwa wa akili.
Kwa mfano Naira alikuwa ni moja ya watafiti ambao wamezaliwa nje ya eneo hilo na kuonekana kuwa na akili zaidi lakini yeye akiwa tofauti kidogo na wenzake yeye amezaliwa kwa misheni maalumu ya kisayansi ambayo ilipewa jia la Misheni Pro Human iliofanyika nchii Bolivia miaka mingi iliopita.
Unachopaswa kuelewa hii ni Kambi tu ya kisayansi ambayo ipo chini ya Zeros Organisation.
Kikawaida Zeros organisation haina kabisa makao makuu kwani ni jumuia ya siri ambayo sio ya rasmi kama ilivyo kwa umoja wa kimataifa bali kama vikao vikifanyika basi ni kutoka na mpangilio maalumu wa kizamu katika nchi za kila mwanachama ni kama ilivyo kwa G7 au G20.
Katika siku zote kumi na mbili tokea kufika kwake kila idara ya kitafiti alitumia siku mbili mpaka tatu kusoma taratibu na kujifunza mambo mapya , ilikuwa ni fursa kubwa sana kwa Naira kuliko mfanya kazi yoyote wa kambi hio na yote hayo ni kutokana na kupata ruhusa ya kutembelea kila idara kutoka kwa mkuu wa kambi.
Hatimae siku ya kumi na tatu mara baada ya kutembelea idara zote alikuja kutua katika idara ya ufuataliaji wa maendeleo ya Mpango LADO, idara ambayo husimamiwa na Dyan pamoja na Carlos kama wakuu wa kambi.
Naira licha ya kwamba mwanzo alikuwa aifanya kazi chini ya kambi hio lakini alitaka kuifanya kuwa ya mwisho kabla ya kupitia idara zote.
Kila mwana idara ambaye alifanya kazi na Naira alikuwa amefurahi sana kumuona kwa mara ya pili , tena sio kufurahi kila mmoja alikuwa akimsubiria kwa hamu kupitak kwenye idara yao.
Unaweza ukashangaa kwa nini kusumbiaria kwa hamu ili hali wapo katika kambi moja ila ukweli ni kwaba kuna sheria maalumu za eneo hilo ambazo hufanya watu wa idara moja kwenda nyingine kutoonana kwa muda wa kila siku ishirini na nne.
Yaanii wana idara wote hujumika mara moja tu dani ya mwezi ambapo ni kila baada ya siku ishirini na nne , haikueleweka kwanini kuna utaratibu wa aina hii lakini ndio kanuni ilivyokuwa.
Sasa tokea Naira kufika ndio kwanza siku chache zilizpita ndio wana Kambi wote walikutana kwa mara ya kwanza ikimaanisha kwamba baada ya siku ishirini na nne wangekutana tena.
“Welcome back Naira” Aliongea Dr Dayana mara baada ya Naira kufika kwenye idara yao, asubuhi hio na wana idara wote walikuwepo akiwemo Carlos msaidizi pamoja na wanasayansi wengine.
Naira alikuwa amebadilika sana kiumbo , alikuwa amekuwa mtu mzima haswa na alikuwa na zaidi ya miaka therathini kwa wakati huo hivyo ni rahisi kusema alikuwa amekomaa kiakiri.
“Thank you Madam Dayana”Aliongea Naira kwa tabasamu hafifu huku akikumbatiana na mwanamama huyu aliefahamika kwa jina la Dayana mkuu wa idara ya kituo cha ufuatiliaji wa Mpango LADO.
“Naira tulikumisi sana, karibu sana kwenye idara yetu , siku kumi na mbili tokea kusikia uwepo wako ndani ya kambi imekuwa kama mwezi mzima kukusubiri”
“Nashukuru sana Evans niliwamisi sana”Aliongea Naira kwa lugha ya kingereza na palepale mara baada ya kusalimiana na kila mmoja aliongozwa na Carlos na Dayana mpaka kwenye chumba maalumu cha miutano ambacho kimejaa mitambo ya mawasiliano.
Ijapokuwa Naira alikuwa mwenyeji ndani ya idara hio lakini kutokana na kutokuwepo kwa zaidi ya mwaka mzima basi alipaswa kupewa ushirikiano wa kitaarifa kwa kile kilichojili tokea kuondoka kwake.
Utaratibu ambao ulifanyika katika kila idara ambayo amepita , basi ulipaswa pia kufanyika hata katika idara hio.
Idara ya ufatiliaji Mpango LADO ndio ambayo ilikuwa ikihusika na kufatilia maendeleo ya Agent Code name 13 yaani kwa lugha nyingine ni kwamba nni idara ambayo inamfatilia wakala aliekuwa chini ya mpango LADO ambaye hufahamika kwa jina la Ajent namba kumi na tatu ,. Huyu ndio Roma Ramoni.
“Evans leo utachukua jukumu la kuwakilisha ripoti ya mpango LADO ulifipofikia na unapoelekea , tunakuamini katika kuongea kwako na kujenga hoja hivyo naamini uwakilishi wako utamfanya Naira kuchangua idara yetu na kufanya kazi na sisi kwa mara nyingine”Aliongea bwana mweusi ambaye ni kiongozi , huyu ni director msaidizi ambaye jia lake ni Carlos .
Muda huo Naira alikuwa na mchecheto mkubwa , ijapokuwa misheni nyingi ambazo zilikuwa zikifanyika ndani ya kambi hio zilimshangaza lakini alikuwa na mchecheto wa kujua maendeleo ya mpango LADO.
Miaka michache nyuma ndio alietoa pendekezo la namna ya pekee ya kumfanya ajent 13 kurekebisha tabia yake ya kikatili na kuishi maisha ya kawaida , pendekezo ambalo lilileta matokeo makubwa chanya mpaka leo hii , hivyo ni kwamba Naira aliheshimika.
Naira ndio ambaye alitoa pendekezo la Seventeen kiondolewa katka maisha ya Thirteen ili kupunguza ile tabia yake ya kimauji , kupunguka kipindi hicho Ajent 13 alikuwa ni kama nyama na ilikadiliwa kwa mwezi alikuwa akiua binadamu kwa wastani wa watu therathini ambayo ni idadi kubwa sana.
Tabia ya ajent 13 kuua watu ilikuwa ni athari za kisaikolojia ambazo zimetokeana na sayansi iliopo ndani ya mwili wake pamoja na ugonjwa uliokuwa ndani ya ubongo wake. Viongozi wa Zeros waliwapanikisha wanasyansi hao kuhakikisha njia mbadala inafanyika ili kumfanya Ajent 13 kuacha mauji na ukatili wake na mbinu nyingi zilipendekezwa na hakuna ambayo ilifanya kazi na katika mbinu zote hizo zilikuwa ni zile za kumrudisha Roma katika maabara na kumwingizia Chipu kwenye ubgogo na wazo hiloo lilipingwa vikali kwani lilikuwa na athari kubwa na hapo ndio Naira pekee alipokuja na wazo tofauti kabis ana wenzake wote na wazo hilo ndio ambalo lilikuwa ni la kumtumia ajent 17.
“Miss Naira mpaka sasa kuna mabadiliko makubwa sana yametokea chini ya mpango LADO , wakati unatoka mpango LADO ulikuwa kwenye Pase ya tatu na mpaka sasa umefikia Phase namba nne”Aliongea Evans na kumfanya Naira kumwangalia kwa umakini kwa macho ya kutarajia maelezo zaidi.
Katika phase namba moja hapa ilihusisha mwanzo kabisa mwa mpago LADO yaani kipindi ambacho ndege ya shirika la M Airline inapotea hii nndio ilikuwa phase namba moja au hatua ya kwanza kabisa , hatua ya pili ilikuwa ni ya kimaabara zaidi na hiii ilifanyika katika visiwa vya madagascar na Phase hii ilifanyika mara baada ya Phase namba moja ya kirusi kumalizika , hatua hii ya pili ilihusisha kuwamulika Ajent 13 na Ajent 17 na mwanga wa jiwe la kimungu na hatua hii ilikuwa katika mgawajo wa steji mbili ya kwanza kabisa ni mazoezi ya kijeshi na kininja pamoja na ya kumulikwa , hatua ya tatu sasa ndio ambayo Ajent 13 na Ajent 17 walipewa uhuru wao huku tabia zao sikifatiliwa kwa ukaribu.
“Nadhani kila mmoja anaelewa mafanikio ya mpango LADO si tu kwenye kufanikiwa katika majaribio ya kisayansi lakini pia afaniklio yanaandaliwa katika ujumuishi wa matokeo baada ya majaribio ya kisayansi..”
“Evans nadhani ungeenda moja kwa moja katika hatua ambayo mpango LADO umefikia kwa sasa na ni malengo gani yanatarajiw aktika mpango huu”Aliongea Naira na Evans alitingisha kichwa.
“Mpaka sasa mpngo LADO umevuka katika hatua ya ufatiliaji wa moja kwamoja kupitia mitambo mpaka kuwa katika ufatiliaji wa kijasusi”
“Unamaanisha kwamba hakuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Ajent 13 na kituo chetu cha ufuatiliaji?”Aliuliza Naira kwa kingerez.
“Ndio”Aliongea na palepale aliwasha mtambo ambao siku zote ulikuwa ukitumika kumfatiliaji utendaji kazi wa mwili wa Ajent 13, siku za nyuma mtando huo ulikuwa ukionyesha data ambazo zinacheza cheza lakini kwa kipindi hicho hakukuwa na dalili yoyote yaani kwa haraka haraka ni kwamba mtando uliandika ‘No Signal’
Jambo lile lilimfanya Naira macho yake kuchanua na alionyesha tabasamu hafifu.
“Madam hatua hii inatafsirika vipi?”Aliuliza Naira akimwangalia Mama mtu mzima ambaye hufahamika kwa jina la Dyana.
“Mpaka sasa hatua hii inatafsirika kwamba PLMC hiana access ya moja kwa moja na Ajent 13 na swala hili linahamia moja kwa moja chini ya kitengo maalumu kilichopo chini ya Dhoruba nyekundu , kama aliyyosema Evans Mpango LADO kwasasa upo katika hatua ya kijasusi zaidi kuliko remote monitoring”
“Kama mpango huu upo katika hatua hii ni kazi gani ambayo imebakia chinni ya PLMC?”Aliuliza Naira.
PLMC ni kifupi cha Project Lado monitoring center
“Ijapokuwa kwasasa mpango LADO upo katika hatua ya kijasusi zaidi kuliko ya kisayansi haimaanishi kwamba idara yetu ndio iafungwa kutokana na kukosekana kwa majukumu , kama alivyokwisha kusema Evans kwa sasa tupo katika hatua ya nne lakini kuna hatua ya tano na ya sita, katika hatua hizi kinachongojewa ni kizazi kinachofuatia”
“Unamaanisha watoto watakaozaliwa na Ajent 13?”
“Ndio Naira hio dio itakuwa hatua ya tano ya mpango LADO ambayo mpaka sasa ipo nusu kufikiwa”
“Unamaanisha nini kusema nusu kufikiwa?”Aliuliza Naira huku akionyesha shauku na palepale Carlos alimpa ishara Evans kuendelea.
“Dr Naira , huyu ni Lanlan Ramoni Kweka ni mtoto wa kwanza wa Ajent 13 na Ajent 17, hizi ndio taarifa ambazo zinamuhusu Lanlan mpaka sasa kuanzia maendeleo ya ukuaji wake tabia yake na ukuaji wake”Aliongea na kisha alipatiwa kishikwambi kilichokuwa na chata ya Zero na kuanza kusoma na Naira alijikuta akisimkwa na mwili.
“Kwaninin Athena hakunielezea kuhusu kuwepo kwa Lanlan?”Ni swali ambalo liliibuka palepale katika kichwa cha Naira.
“Umesema hatua ya tano ipo nusu kufikiwa , nataka maelezo ya kutosha kuhusu hili”Aliongea na palepale Evans ni kama alisubiria swali hilo kwani alitoa tabasamu na kuanza kuelezea maisha ya Roma kuanzia kufika chini Tanzania nama ambavyo amekutana na Edna na wanawake wengine.
Ilikuwa ni taarifa ambayo alikuwa akiijua nusu yake lakii alishangazwa mara baada ya kuona Roma alikuwa na kundikubwa la wanawake tena akiwemo rafiki yake wa utotoni Dorisi.
Naira alisisimkwa na mwili palepale na alishajua ni kipi ambacho kilikuwa kikitarajiwa kwa haraka haraka kilichokuwa kikisubiriwa katika mpango huo ni watoto ambao Roma atapata kupitia wanawake hao.
“Manaamii vipi watoto watakaopatikana kupitia hawa wanawake wataweza kuwa na uwezo mkubwa kuzidi huyu Lanlan?”
“Matarajio yetu ni makubwa sana kupitia watoto watakaopatikana, mpaka sasa tuliweza kufatilia kwa karibu sana namna ambavyo Ajent 13 alivyoweza kujiondoa katika mifumo yetu ya kiufatiliaji , ijapokua hakuna maelekezo sahihi lakini inaonekana mbinu ambayo amejifunza chini ya Master Tai Chi ndio sababu kubwa , mpango wetu mwanzoni ni kumfanya kuweza kuzielewa kanuni za anga lakini akachagua mbinu nyingine ajabu ni kwamba mwili wake umepitia steji ya purification na ndio iliosababisha kukosa mawasiliano nae ya moja kwa moja, hizi ni taarifa za mwisho ambazo tuliweza kufatilia kuhusu mwili wake”Aliongea na kisha palepale alitoa ripoti nyigine na kumpatia Naira.
“Virusi ambao waliingizw akatika mwili wake walikuwa na kazi kubwa ya kupitia mabadiliko pale anapokuwa ni mwenye hasira lakini tokea mwili wake kutawaliwa na nguvu isiokuwa ya kawaida, virusi wote wamekosa utawala wa seli za mwili na kubakia kama chembe chembe ndani ya mwili wake , dalili pekee ambayo inafanya kazi katika mwili wake ni nguvu ya mwanga wa kuungu amao alimulikwa nao na huu hujidhihirsa kupitia macho yake”
“Naona hapa faida kubwa ambayo ameipata kupitia mpango LADO kwasasa ni kuwa na mwili usio wa kawaida lakini nguvu zake hazitegemeanni kabisa na mpango LADO ni hatua nzuri ambayo amefikia , vipi lakini kuhusu uvimbe ulipo kwenye ubongo wake?”
“Mpaka sasa hatuna taarifa zake kutokana na mtu ambaye huhusia katika kumpiga ni princess Clark Stephanie na kutokana na teknolojia kubwa ya kimitambo anayotumia tumeshindwa kudukua taarifa zake”Aliongea na kumfanya Naira kuvuta pumzi kidogo na kuwaza jambo.
“Sio Ajent 13 tena bali ni Roma Ramoni kwa jina lake , amepiga hatua kubwa lakini je anaelewa mipango ya Athena, ninapasw akufanya namna ya kufanya nae mawasiliano kwa namna yoyote ile hii sio kwa ajili yake tu lakini pia kwa ajili yangu na kila mmoja aliepo hapa ndani , nahitaji kuwa huru”
“Kwanza niseme kwamba nimferahishw ana kazi kubwa ambayo idara ya PLMC imefanya kwa kipindi chote ambacho sikuwepo hii inanipa shauku ya kutaka kujua nini kinafuatia katika hatua ya tano na sira ya mpango LADO ila niseme kwasasa nimevutiwa zaidi na Project ya Quantam Nexus and Horizon”Aliogea na kufanya kila mmoja kuwa katika mshangao lakini kwa wakati mmoja wakiingiwa na huzuni.
Quantum Nexus na Horizon ndio idara kubwa za kitafiti ambazo pia zilikuwa zikiendelea chini ya Zeros organisation.
Kauli ya Naira iliwafanya kujawa na huzuni kwani ilimaanisha kwanzia siku hio hatokuwa tena chini ya idara ya PLMC bali anakwenda kujiunga na idara ya utafiti wa kisayansi wa teknolojia ya Quantam mechanic.
SEHEMU YA 683.
Warembo wa Roma waliokuwa wakiishi ndani ya visiwa hivyo ndio waliokuwa na jukumu la kuwapokea wenzao katika uwanja wa ndege.
Ilikuwa ni kipindi cha hali ya hewa ya unyevunyevu ndani ya eneo lote la mwambao wa bahari ya Mediterranian hivyo ilifanya kisiwa kupendeza zaidi kwani ni hali ambayo ipo katikati haikuwa ya joto sana wala ya baridi sana kwa mwezi huo wa kumi na mbili kuelekea mwezi wa kwanza.
Roma alikuwa amemmisi sana Rose na warembo wengine kwani hakuwaona kwa kipindi kirefu na mara baada ya kufika alijikuta akiwakumbatia na kuongea nao maneno ya kuwafurahisha.
Upande wa Rose na Magdalena walkuwa wamepiga hatua kubwa sana katika mafunzo ya mbinu hizo za kijini walikuwa katikati mwa levo ya Nafsi na hata mahusiano kati na hata ile hali ya ashiki ya kimapenzi ilikuwa imebadilika mno.
Kadri ambavyo uwezo wa mwanake anavyopanda levo na tamaa ya kimapenzi hushuka zaidi na zaidi na upendo unaobakia sio ule wa kingono zaidi bali ni ule ambao hauelezeki kwa maana nyepesi.
Roma ni kama vile amejiandika katika mioyo ya wanawake hao kwa karabu ambayo wino wake ni ngumu kufutika.
Ilikuwa ni kwa ghafla sana tayari kisiwa kilikuwa na wanawake kumi wa Mfalme Pluto , hali hio iliwafanya wakazi wa eneo hilo kuvutiwa sana na picha hio , hakukua na sheria ya kitamaduni ndani ya hivyo visiwa na kilichohesabika ni kwamba wanawake hao ni wa mfalme Pluto na wanapaswa kuheshimiwa , huo ndio ukweli ambao raia wa visiwa hivyo walipaswa kuelewa.
Ilikuwa ni kwa bahati nzuri kwamba wanawake hao hakuna ambaye alikuwa na tabia mbaya au hasira za kutumia nguvu ya Roma vibaya , kwa zaidi sana ni Mage ambaye alikuwa mtu wa vitendo zaidi kwani ndani ya muda mchache aliofika alikuwa ashaanza kufahamina na wakuu wote waliiokuwa chini ya Roma na kujua ngazi zao na madaraka yao lakini hata hivyo wote walimpa heshima yake na hawakuchukizwa na maswali yake mengi.
Ujio wa Lanlan ndio ambao ulikuwa ni wa kivutio zaidi ndani ya visiwa hivyo kwasababu kila mtu alijua huyo ndio mtoto wa Seventeen na Roma na uzuri ni kwamba asilimia kubwa walikuwa wakimjua Seventeen kwani alishaishi ndani ya visiwa hivyo na wakampa heshima yake na alikuwa na mchagao mkubwa lakini pia walijua ni nafasi gani aliokuwa nayo katika maisha ya Roma.
Hivyo kils mmoja alipenda kumuona Princess Lanlan na kujenga nae ukaribu kwa kumsifia hivi na vile.
Lanlan alijikuta kwa muda mfupi sana anakuwa na wajomba , mashangazi na mababu na alishindwa kujizuia na kujikuta ni mwenye furaha kwani wale aliowaita mababu walimfurahisha zaidi kutokana na aina ya chakula walichokuwa wakiandaa na pia burudani waliokuwa wakimuonyeshea.
Ki ufupi Lanlan ndio aliekuwa bize zaidi kuliko wote na ilimfanya kusahau kwa muda kufanya mazoezi kiasi cha kuhofia baba yake kumfokea.
Lakini kitu kungine ambacho kilimfurahisha Lanlann ni uwepo wa bahari ambayo hakuwa akiona mwisho wake , bahari ambayo ilimruhusu kuongelea muda wote na kulikuwa na watoto wengi ambao alikuwa akicheza nao bila ya kumhofia.
Watoto waliokuwa akicheza nao wazazi wao wenyewe hawauwa wa kawaida na walikuwa na vyeo hivyo ni kama ujasiri wao wameridhisha watoto wao na hawakuwa wale watoto legelege , walikuwa ni watoto ambao wana aina ya mazoezi kulignana na umri wao,
Tanzania watoto ambao Lanlann alitkuana nao shuleni asilimia kubwa ni wale wadhaifu wadhaifu na wazembe ambao wamekaa ki uwoga woga na kumuogopa lakini watoto wa kisiwa hicho walikuwa ni wa tofauti sana na hili ndio ambalo lilimfurahisha Lanlan na alifurahi hata pale alipopigwa makofi mara baada ya kumuua Papa na kumburuza mpaka nchi kavu.
Upande wa wanawake wa Roma walijua kabisa mume wao amewaltea katika visiwa hivyo sio kula bata bali kujifunza hivyo hawakutaka kumkatisha tamaa , walifikia hadi hatua ya kushindana wao kwa wao.
Isitoshe Rose , Magdalena na Sophia walikuwa na levo za juu zaidi katika mafunzo hayo na ndio ambao walishindana zaidi wao kwa wao na kila mmoja alitaka kumshinda mwenzake na ndio maana walitumia kila maelekezo ambayo Roma huwapatia.
Katika siku ya kwanza ambayo Roma alifika hakutaka hata kwenda kutembelea marafiki na alijichimbia katika chumba cha ardhi katika ngome yake na kuanza kutengeneza vidonge vya kijini.
Alikuwa na lile tunda moja tu la damu na hakujua ni vidonge vingapi ambavyo angetengeneza hivyo alitumia umakini mkubwa sana katika utengenezaji hili asije kuharibu.
Roma alitumia kila mbinu ambayo ilikuwa kwenye andiko la malkia wa tushani alilopatiwa na Aoiline katika ulimwengu wa majii pepo na aliishia kujawa na shukrani kubwa.
Kitendo cha Roma kufanikiwakutengeneza kidongea daraja la kwaza kiliwafanya hata Rose na Magdalena na Sophia waiokuwa wakivuna nishati katika kilele cha mlima Volcano kuhisi nguvu yake na kukimbilia ndani ya ngome.
Roma ile anatoka katika chumba cha siri cha utengenezaji vidomge aliwatuka warembo hao wakisubiria kwa shauku kubwa na aliishia kutoa kicheko kutokana na macho ao yalivyojaa shauku na tamaa.
“Naomba mmekuja kwa haraka sana lakini siwezi kuwapatia hivi vidongea , ni vya watu ambao wanataka kuingia katika levo ya Nafsi na nyie tayari hivyo mkae pembeni”
“Shiii.. mimi na Magdalena hatuhitaji sana , tulitaka kuona tu”Aliongea Rose ambaye urembo wake umeongezeka mara tano zaidi , ni dhahiri kama angetia mguu ndani ya Tanzania wanaume wangepanga mstali kuomba hata namba alikuwa sio wa kawaida na kama una nguvu kidogo sana za kiume basi ukimwangalia ni kama vile uso wake unabadilika badilika kutokana na kuzingirwa na nguvu ya mbingu na ardhi.
Haikuwa kwa Rose tu hata kwa Magdalena alikuwa na mabadiliko makubwa saa ya kimwili na moja wapo ya faida ya nguvu za kijini ni kwamba zinakuja na aina ya marashi asili ambayo hayaelezeki , yaani I aina ya marashi ambayo haihitaji kujipuliza.
“Umepauka uso , unaonekana umechoka sana kwa kutumia nguvu ya mtoto mweupe kutengeneza vidonge kwa siku tatu mfululizo”Aliongea Rose huku akishika shavu la Roma kimahaba huku macho yake ni kama yamejaa machozi lakini ukweli nin kwamba hayakua machozi bali nguvu ya kijini ndio ilifanya macho kuwa kama yamejaa maji.
‘Nimepoteza nguvu kidogo tu lakini nitakuwa sawa kama utaniruhusu ninyonye asali yako kwa dakika kadhaa babe Rose”Aliongea Roma kama kawaida yake huku akitoa tabasamu la kifedhuli.
“Hebu achianeni kwanza , nataka kujua ni vidonge vingapi umetengeneza”Aliongea Magdalena huku akimvuta Rose kwa nguvu.
“Haha.. Magdalena wako ni wivu kama na wewe unataka si ujiunge upigwe busu”Aliongea Roma akimtania Magdalena na kumfanya kupotezea.
“Nimetengeneza vidonge kumi tu kwa kutumia lile tunda la damu la finiksi , nyie wawili pamoja na Sophia hampaswi kupewa , nnitawapa ambao wanapasw akuingiakatika levo ya Mzunguko kamili a kuingia levo ya nafsi”
“Vinatosha hivyo kabisa na vinaonekaa kuwa na nguvu kubwa kutokana na msisimko wake , sisi hatuna tatizo ukiwapa wengine”Aliongea Magdalena lakii akiwa na sura ya huzuni.
“Magdalena kwani kuna utamu gani kuhusu vidonge , hupaswi kuwa na huzuni , mimi mwanaume wako nitakulisha kitu kingine tofauti na vidonge…”Aliongea Roma huku akikodolea kifua cha Magdalena kwa macho ya kifisi na kauli yake ilimfanya kuwa na aibu na kumwagalia Roma kwa macho ya hasira.
Baada ya kuongea a Magdalena na Rose kwa muda Roma aliwaita wanawake wote kurudi katika ngome hio , ilikuwa ngome kubwa mo na kila mmoja alikuwa na chumba chake kikubwa tu lakini ajabu ni kwamba licha ya Roma kuwaachia uhuru wa kuchagua hakuna ambaye alichagua chumba kikubwa zaidi cha hadhi ya juu ambacho Roma mara ya kwanza alijaribu kualla na Edna na akagoma.
Roma mara baada ya kuwakusanya kwenye meza alitoa kifaa ambacho amehifadhia vile vidonge.
Neema Luwazo , Amina , Mage, Najma , Nasra , Dorisi na Clark wote walichukua kimoja kimoja na kwasbabu Yezi ndio kwanza ameanza kujifunza basi hakupaswa kuchukua na Roma alimuhifadhia hivyo katika vidonge kumi vilibaki viwili tu ambavyo Roma alipanga kimoja kingekuwa ni cha Edna.
Lakini Roma hakuwa na mpango wa kumpa Edna kwa haraka kutokana na vita baridi inayoendelea.
“Kwa taarifa yenu tu , hiki kidongea ijapokuwa kina nguvu sana lakini lazima kutakuwa na maumivu makali sana ya kuvumilia baada ya kukimeza hivyo kama unaogopa basi usimeze isitoshe mimi sio kama wale Master wakali , nataka kuwaona mkiwa salama hivyo haina haya ya kuharakisha , kama ukishaingia levo ya mzunguko kamili haina haja ya kuharakisha kuingia levo ya nafsi”
“Unaongea kama vile unatuona sisi ni watoto wa miaka mitatu , hivi unajua ni maumivu gani wanawake wanapitia wakati wakifanya upasuaji wa sura na shepu ili kuwa warembo , mwanamke yoyote anaweza kuvumiliv magumu yote ili mradi tu matokeo awe mrembo”Aliongea Neema.
“Sio hivyo , ninachomaanisha ni kwamba ijapokuwa ni kweli kuna maumivu mtapata lakini sijui ni maumivu ya aina gani kwani mwenyewe sijawahi kujaribu ., sitaki kuona mkipitia wakati mgumu”
“Angalau una dhamiri ya kueleweka , hivyo hebu nikutoe wasiwasi kwa kukuambia mimi nitakuwa wa kwanza kujitoa kafara kumeza hiki kidonge”Aliongea Afande Mage na palepale alichukua kidonge chake na kukimeza palepale.
Alitaka kuwa wa kwanza katika majaribio na alikuwa jasiri kiasi cha kuwafanya wengine kuonyesha kumpenda.
Magdalena alitaka kumzuia dada yake lakini alikwua amechelewa kwani kishapita kwenye koo tayari na aliishia kuwa na wasiwasi tu ya kile ambacho kinakwenda kumtokea na hakutaka endelee kubakia hapo kwani alimbeba na kuondoka nae na kwend akujificha ndani ya vyumba vya chini ya ardhi.
Roma na yeye alifatisha huko huki akitaka kujionea kama Mage atafanikisha kutumia nguvu yote ya kidonge hicho na kupanda levo.
Ndani ya chumba Mage alikwua amekalishwa kwenye Sofa na alikuwa akitokwa na jasho ambalo sio la kawaida huku mwili wake ukito mvuke ambao harufu yake haikuwa nzuri kabisa ilikuwa nni kama vile hajaoga muda mrefu lakini Roma aliweza kugundua ni hatua ya kwanza ya kidonge hicho kusaficha mwili kabla ya kurhusu nguvu nyingine kumvaa akini wakati huo mishipa ya damu ilikuwa imetanuka sana kwani hata uso wake ulikuwa ukionekana mishiririzi ya mishipa ya damu.
Wakati huo alikuwa ashapoteza fahamu na Magdalena alitaka kumsaidia dada yake lakini Roma alimzuia.
“Usimguse kabisa na umuache , hatua ya kwanza ya kusafisha mwili ni ngumu kidogo na ndipo maumivu yalipo , kama asipofanikiwa kuvumilia yeyemwenyewe basi itakuwa rahisi kupoteza uwezo wake huko mbeleni”
Mage alikuwa kama taa ya balbu ambayo inakaribia kupasuka kwani alikuwa akirejewa na fahamu na kisha zinapotea tena pale maumivu yanapomzidia na mara ya mwisho kabisa mara baada ya fahamu kumrejea hakupoteza fahamu tena na aliishia kungata meno na kukunja ngumi huku akitokwa na mguke wa ajabu mno na kubadilisha hali ya hewa ya chumba.
Nusu saa mbele alianza kuota vipele vikuwba ambavyo vilikuwa na damu nyeusi na hapo ndio maumivu yalipozidi kiasi cha kumfanya kutetemeka lakini hakupoteza fahamu tena na vipele vle vilikuwa vikiota na kupasuka vyenyewe.
Watu wote walikuwa wakimwangalia mpaka lisaa linapita walijikuwa wakishangazwa na nguvu za mbingu na ardhi ambazo zlikuwa zikimtoka Magdalena na jambo hilo liliwashangaza wote na Roma alijiabia alifanya la maana kuwaleta huku kufanyia mazoezi kwani nguvu hio kwa hakia lazima ingewaamsha majini.
Baada ya maumviu yaliodumu kwa saa moja na nusu hatimae mvuke uliisha kwenye mwili wa Magdalena na ngozi yake ilianza kujiotesha upya na kubakia na magamba magamba ambayo yalikuwa yakimtoka kwa kugusa tu na mkono , ilikuwa ni ajabu kweli.
“Haha… Mage tayari amefanikisha kunyonya nguvu ya kidonge na kilichobakia hapo ni kuingia katika tafakari nzito ya kuweza kupata ufunuo wake na kuingia katika levo ya Nafsi”Aliongea Roma huku akijipongeza na mara baada ya kuona ufanisi wa vidonge hakiona haja ya kuwazuia wengine kutokuvimeza.
Usiku chakula kiliandaliwa kama kawaida na mpidhi wa kimataifa ambaye alipewa ajira kabisa kwa ajili ya kazi hio.
Lanlan alikuwa akila zaidi ya vle alivyokuwa akila alipokuwa Tanzania na mashavu y alizidi kumtoka lakini licha ya hivyo Roma aliamini kadri ambavyo atajifunza basi mafuta ya mwili wake yangejiwianisha kwenye mwili wake na kuwa na mwonekano mzuri zaidi.
“Daddy lini tunarudi?”Aliuliza Lanlan ambaye alikuwa amekaa pembeni.
“Umechoka kukaa huku?”
“Sijachoka lakini Lanlan anataka kwenda shule”
Ukweli ni kwamba licha ya mzingira ya hapo kuwa na marafiki wengi ambao anacheza nao lakini kuna aina ya michezo hawakuwa wakicheza kwani wengi wao walikuwa ni wasichana ambao wamekaa kitomboy kitomboy na waliishia kumwita Princess tofauti na Lanlan jina ambalo hakuwa akilipenda.
Bado siku tatu mpaka likizo kuisha , nitakurudisha kabla ya hio siku”Aliongea Roma.
‘Hata mimi pia”Aliongea Nasra lakini muda huo huo wote waikarishwa na kuingia kwa Mage ambaye alikuwa bado hajatoka kwenye chumba cha ardhi , muda huo alikuwa amebadilika na ngozi yake mpya ilishajitengeneza na yale mabaka mabaka kama nyoka anaejichna yashaisha na sasa alikuwa ameoga na kupendeza.
“Yuko mwishoni mwa levo ya Mzunguko kamili”Aliongea Roma na kuwafanya Roma na Rose kuangaliana , ufanisi wa kidogea ulikuwa mkuwba kuliko walivyotarajia.
Mage hakujali walivyokuwa wakimwangalia na alikimbilia chakula na kuanza kukifakamia na alipiga sahani tatu mfululizo
Usiku Roma alijaribu kutafuta sasa watoto kwa Magdalena na Rose lakini hata hivyo hakuwa na matarajio makubwa kwani kulikuwa na gepu kubwa hivyo ilikuwa ni kwa kubahatisha tu.
Siku iliofuata Najma , Clark , Amina , Neema , Nasra na Dorisi wote walimeza vidonge kwa wakati mmoja na mpaka inafika mchana wote wlaiweza kupita hatua ya maumivu ya mwili kujisafisha kasoro Clark tu ambaye alikuwa amejifungia kwa muda mrefu sana kiasi cha kuwafanya wengine kuwa na wasiwasi na kutaka kumshitua lakini Roma aliwazuia.
Siku ya kwanza ilipita bila ya Clark kutoka na Roma hakumgusa ili mradi alijua mwili wake upo sawa na Roma alishangazwa na jambo hilo lakini alijiambia angefahamu zaidi atakavyoshituka.
Roma siku iliofuata alianza uwafundisha warembo hao mapigano ya kisjehi wakisaidia na wanajeshi The Eagles.
Kwa jinsi ambavyo walikuwa wakijifua ni kama vile muda wowote Roma anakwenda kuingia vitani baada ya kufanikisha.
Mpaka inakuja kufika usiku ndio sasa Roma aliweza kuhisi msisimko usio wa kawaida na hakuwa yeye tu hata Magdalena na Rose wote waliweza kuhisi msisimko huo na hapo ndipo walipojua Clark alikuwa ameingia kwenye levo ya nafsi jambo ambalo lilishangaza kila mmoja , ilikuwa ni maajabu kwani Clark alikuwa ameingia levo ya Nafsi ndani ya masaa ishirini na nne tu na nusu.
Ijapokuwa Sophia aliingia ndani ya levo ya Nafsi kwa spidi lakini yeye alikuwa na msaada kutoka ka Aoiline lakini Clark peke yake aliingia katika levo ya nafsi kwa msaada wa kidonge tu.
Wakati Clark alipotoka nje alikuwa I kama vile ni Aphrodite mungu wa kizazi , labda ni kwasababu alikuwa ndio mzungu pekee katika kundi la wanawake wa Roma.
Kila mmoja alitaka kusikia siri ya Clark kuweza kutoboa ndani ya siku chache na hapo ndipo walipomsikilza kwa umakini kuhusu ufunuo aliopata na kwa maelezo yake anasema alijaribu kulinganisha nadharia ya Einstein kati ya anga na muda , yaani kwa lugha nyepesi ni kama Clark alikuwa ameiga namna kanuni za anga zinavyotumika na ndio alipoweza kupatwa na uelewa wa haraka.
Mbinu ya Clark ilikuwa ni ya ajabu mno na hata \Roma mwenyewe alishindwa kuielewa na alijua Clark anaweza kuwa tishio zaidi kuliko wengine wote.
Siku chache mbele Sophia ambaye alikuwa Itally kwenye show aliungana na Roma katika visiwa vya wafu na iliandaliwa tafrija ndogo ya kumpongeza kila mmoja kwa mafannikio, wakati wengine wote wakiwa wamefikia levo ya mzunguko kamili Clark , Sophia , Rose na Magdalena walikuwa washaingia katika levo ya mwishoni mwa mzunguko kamili na muda wowote wangeweza kutoboa , ilikuwa ni juhudi kubwa.
Baada ya tafrija hio Roma aliwaambia wanaotaka kurudi bongo waongozane nao na wanaobaki wabaki lakini wote hakuna ambaye alitaka kuondoka kabla ya kufikia levo ya nafsi.
Roma sasa mara baada ya kuona mafanikio ya warembo hao ukweli ni kwamba alifikiria muda wa kutafuta mbinu ya kufanya wawe huru licha ya kuwa nguvu za kijini na aliona mbinu pekee ni kuzidi kuvuna nishati ili kuwa na nguvu kubwa ya kwenda kubadilisha sheria walizoweka majini na kuwafanya warembo wake wawe huru kwenda wanapotaka.
Najma akiwa visiwani alijulishwa kuteuliwa na kuwa afisa habari na msemaji mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na alipaswa kuripoti Dodoma siku kumi zijazo hivyo aliungana na rafiki yake Nasra na Roma kurudi Tanzania.
Roma ijapokuwa alishangazwa na chaguo la Najma kujiingiza kwenye siasa lakini hakutaka kutoa dukuduku isitoshe hakuona tatizo kwa mtu kutaka kuwa na nguvu ya kimadaraka , alijiambia ili mradi atakuwa na furaha basi atamsapoti.
Roma mara baada ya kufika Ununio ilikuwa ni usiku tayari na walishangaa kukuta nyumbani kwa Nasra taa inawaka kwa ndani.
Roma alijiuliza ni nani yupo ndani na wakati huo alikuwa amemshikilia mkono Nasra kwamkono wa kushoto na Lanlan mkono wa kulia.
“Roma mwanangu naona hatimae umerudi”Sauti iliwez akusikika mara baada ya mtu kutoka nje na palepale Roma aligundua alikuwa ni mama ake Blandina.
Na alimwangalia Roma kwa umakini kama vile kuna kitu anatafuta na aliridhika kuona hana tatizo lolote.
“Mama kwanini upo huku , umefika lini?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Kwannini unaniuliza hivyo au siruhusiwi kuja sehemu anayoishi mwanangu ?”Aliongea Blandina akionyesha hali ya kutoridhishwa na swali la Roma na palepale alimsogelea mjukuuw ake na kumbeba juu juu.
“Jamani Lanlan ulikuwa ukila nini huko visiwani , mashavu yameongezeka”Aliuliza na Lanlan aliishia kucheka cheka na kuishia kuita bibi tu.
Baada ya kuingia ndani Blandina aliongea kidogo na Nasra kisha akakaa chini na kuongea na Roma.
“Mama umemaliza maswala yako , uliniambia kuna mamabo unashughulikia nje ya nchi mara ya mwisho?”
“Ndio maana nimerudi , nimeamua kurudi sasa kuishi huku , Roma nimesikia habari zako nikiwa huko , niliambiwa uliweza kupunguza nguvu ya familia ya mzee Sharif”Aliongea
“Umesikia wapi