Simulizi ya Kijasusi: Salamu Kutoka Kuzimu

Roho ya Paka
 
Umenikumbusha mbali sana. Inspekta Kombora na kachero lililokubuhu, Joram Kiango.

Kwa uandishi wa kazi hizi za Riwaya za upelelezi hapa nchini Tanzania, Ben Mtobwa anamfuatia Msiba ambaye yeye ameandika Riwaya za kachero maarufu Willy Gamba. Na ukiangalia vizuri zaidi, Mtobwa anaweza hata akamzidi Msiba kwa sababu yeye Msiba riwaya zake zinaonekana kama kuiga uandishi wa James Hardley Chase, na hivyo inaonekana kama alikuwa anamuiga Chase kwa kuandika riwaya za Kiswahili.

Nimesoma sana hivi vitabu O-level Nilikuwa na jamaa yangu tulikuwa tuko darasa moja, stream moja, alikuwa anatumia jina la Nyanda Petro (sasa hivi alishabadilisha jina). Huyu bwana alikuwa ana roho nzuri sana. Yeye alikuwa ana uwezo wa kununua vitabu hivi ila mimi sikuwa nao, lakini alikuwa kila akinunua, lazima anipe na mimi nisome. That man was a very nice. Magazeti ya Sani pia vile vile alikuwa anafanya hivyo hivyo
 

[emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji1374] asante mkuu
Mtobwa anajua sana.. Kipaji hiki hakuna mfano wake
 
Na sasa kitabu hiki kweli kilikuwa na mambo ya kuzimu... 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…