Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

singanojr hebu toa hata offer kwa mashabiki wa Yanga basi, tumechukua ubingwa, top scorer uko kimya tu hata hujitikisi[emoji471]
 
Haya singano jr,singano, singano nakuita Mara tatu watu wako wanalialia jukwaani
 
SEHEMU YA 46.

Regina mara baada ya kuisikia hio kauli uso wake ulipata moto kwa aibu maana ni kama kitu ambacho hakutegemea.

“Bibi unaongea nini , mimi siwezi kuolewa nae?”Aliongea Regina

Hamza hata yeye alikuwa kwenye kuchanganyikiwa , hatua hio aliona ni ya haraka sana , isitoshe hata mwezi haujaisha tokea afahamiane na Regina.

“Hutaki kuolewa nae , kwahio umetafuta boyfriend wa kucheza na akili yangu ili niridhike au ni kama alivyosema Lamla, Hamza ni mpenzi wako feki”

“Sio hivyo bibi , mimi na Hamza ni kweli ni wapenzi”Aliongea Regina kwa kusita sita.

“Kama ndio hivyo nataka muone , sio lazima ya sherehe , kwasababu Hamza ni muislamu na wewe ni mkristo mnaweza hata kwenda kuandikisha ndoa yenu bomani na kuanza kulala pamoja , mkishaona nimekufa mnaweza kuachana kama hampendani”Aliongea

Regina alishikwa na wasiwasi mkubwa mno na aligeuka na kumwangalia Hamza lakini kwa bahati mbaya alikutana na uso uliokuwa na tabasamu zito na kujiambia hili lipuuzi mbona linatabasamu, au ndio mpango wake kutaka kunioa kwa muda mrefu, Regina alijihisi kichaa kinakwenda kumshika.

“Bibi hali yako sio nzuri kwasasa , kwanini tufunge ndoa wakati wewe unateseka , tusubiri ukishapona tutaanza kufikiria swala la ndoa”Aliongea Regina akijitahidi kutafuta kisingizio cha aina yoyote ile ili kumtuliza bibi yake.

Ukweli ni kwamba hakuwahi kuwaza kuolewa na Hamza na sio hivyo tu hakuwaza ingekuwa mapema hivyo baada ya bibi yake kuija Dar kitu cha kwanza anachotaka ni kuona ndoa, yaani ilionekana mzee huyo hajaja kupona bali kumuozesha.

“Hivi unadhani na huu uzee wangu pamoja na kuumwa akili yangu haifanyi kazi , usisahau ni mimi na babu yako tuliopigania kampuni ya Dosam imesimama, hata kama nimekuwa mzee huwezi nidanganya kirahisi”Aliongea na kumfanya Regina kuonyesha muonekano wa kukosa kujiamini.

“Bibi nathubutu vipi kukudanganya?”

“Regina usisahau hisa asilimia hamsini na moja unazoshikilia therathini na mbili ni za kwangu na kumi na tisa ndio zako , hisa zangu ni nyingi hata uunganishe na saba za baba yako”Aliongea.

“Bibi najua hilo..”

Upande wa Hamza ndio kwanza alianza kushangaa , ukweli siku zote alijua Regina ndio mwenye hisa nyingi ndani ya kampuni lakini kumbe ni bibi yake ndio mmiliki mkubwa wa kampuni , sasa ndio anajua bosi mwenyewe wa kampiuni ya Dosam ni Bi Mirium.

“Asilimia kumi na tisa jumlisha asilimia 32 ya hisa zangu jumla yake ni hamsini na moja , hii ndio maana halisi ya kuwa bosi wa kampuni ya Dosam na kuwa na nguvu , wakati babu yako anafariki aliweka wazi katika wosia wake ukiweza kuolewa na kuanzisha familia yako ndio nitakukabidhi moja kwa moja asilimia zangu zote , sasa kama hutaki kuolewa nitampatia baba yako hisa zote therathini na mbili na ndio atakuwa mmiliki halali”Aliongea.

“Bibi!!?”

Regina alijikuta akishangazwa na maamuzi ya bibi yake na kuishia kukunja sura.

“Bibi sio kama nina tamaaa sana lakini wewe mwenyewe unajua baba hana uwezo wa kuiendesha kampuni , isitoshe kama akisikia hivi nina uhakika mtu mwenye nia mbaya atazikwapua hisa zote na kampuni kutoka nje ya umiliki wa familia”

“Unadhani kwa umri huu najali sana hela , kwangu vitu na hela havina maana sana , ukifikia umri wangu utajua ninachomaanisha , sababu babu yako kuacha wosia ule ni kwasababu anataka uwe na familia, kwasababu ndio kitu pekee ambacho kinaweza kukufanya kuwa na furaha na kuvumilia yote, wewe mtoto kwanini huelewi , kila kitu ni kwa ajili yako lakini unashindwa kukubali , babu yako anachotaka ni familia kuongezeka na amenisisitizia hilo na ndio ninachotaka kuona kabla sijaaaga”Aliongea na kumfanya Regina kushangaa , hakuamini babu yake Dosam alikuwa na mpango huo kichwani.

“Sikutaka kukulazimisha swala la kuolewa kwasababu nilitaka wewe mwenyewe utafute mtu unaempenda bila ya kujali hali yake ya kimaisha wala dini , ndio maana hata baba yako aliposema anataka uolewa na mtoto wa mzee Benjamini sikuongea chochote , sasa Hamza huyu hapa umemtafuta mwenyewe lazima nihakikishe mnafunga ndoa, au nimekosea, mimi sijakulazimisha kuolewa na mtu usiempenda , si umesema mwenyewe Hamza ni mpenzi wako ?”Aliongea mzee huyo , ilikuwa ni kama vile ndio misheni yake ya mwisho anayotaka kuikamilisha kabla ya kufunga ndoa,

Regina alijikuta akikosa neno la kuongea , alitamani kusema Hamza sio mpenzi wake lakini hakuwa akiweza kufanya hivyo na kumfanya kutamani kulia , isitoshe alijua Hamza ana mpenzi wake hivyo asingemlazimisha kuolewa nae.

“Halafu ili uelewe vizuri kabla ya kufanya safari ya kuja hapa nishaongea na mwanasheria kwa ajili ya kuandaa nyaraka za kusaini , muda wa kupoteza sina ni aidha iwe sahihi yako au ya baba yako , kila kitu kinategemeana na maamuzi yako na Hamza mtakayoamua”

Mara baada ya kuongea kauli hio alifumba macho yake na kujifunika vizuri shuka akionekana kabisa hakutaka kuendelea kuongea.

Regina kihasira hasira alienda mpaka kwenye chumba chake cha kujisomea na Hamza alifuata nyuma nyuma.

“Regina inamaana ni kweli tunakwenda kufunga ndoa?”Aliuliza Hamza kizembe.

“Ndio unachotaka?”

“Sijamaanisha hivyo , siwezi kufunga ndoa na wewe mimi,, nadhani unajua hilo vizuri”Aliongea Hamza lakini maneno hayo hayakuwa na radha nzuri kabisa kwenye masikio yake, alijihisi kuumia kuona Hamza hakuwa hata na wazo la kumuoa.

“Kwannini unaongea hivyo , unaonekana kutonipenda kabisa, nachukiza sana?”Aliongea Regina huku akizidi kuwa kauzu.

“Sio hivyo , unajua wewe ni mrembo sana na pia ni mwanamke tajiri , ni bahati sana kuweza kupata mwanamke wa aina yako..”

“Hebu acha kuongea , mpaka sasa hata sijui nani ni rajiri zaidi kati yetu”Aliongea , Regina hakusahau Hamza alikuwa akivaa mavazi ya bei ghali mno ambayo hajawahi kuyavaa kwenye maisha yake licha ya kutambulika kama mwanamke tajiri.

“Isitoshe hata huyo Master Alex fundi wako simfahamu vizuri , bado kuna Dokta Ronica ambae siwezi hata kula nae sahani moja”

“Bosi Regina hebu acha kunishangaza , mimi nipo chini yako ?”

“Nani unamaanisha haswa?”

“Utajua mwenyewe kama hujaelewa “Aliongea Hamza , hakuwa kabisa na mpango wa kujibishana nae , lakini kwa wakati mmoja alijikuta akifurahia ndani kwa ndani , sio kwamba alifurahia kwasababu ya pendekezo la Bibi Mirium , ila ni kwasababu hakujua ni maauzi gani ambayo Regina na ukauzu wake atayachukua, alitaka kusoma mchezo hadi mwisho utakavyokuwa.

“Hebu ondoka kwanza nataka kufanya kazi”

“Bado unataka kufanya kazi , umekuwa bize siku nzima kwanini usipumzike”

“Jali mambo yako , Tokaa!”

Hamza alishia kujisikitikia na kutoka kisha akafunga mlango , ukweli ni kwamba kila ambacho alikisioma mtandaonni kuhusu Regina alikuwa akikishuhdia katika mazingira halisi.

Regina alitambulika mtandaoni kama mfanyabishara katili likija swala la kutengeneza pesa na ndio ambacho alikuwa akiona na wengi walitafsiri hivyo na kuna wengine ambao walienda mbali na kuwaza Labda Regina alikuwa ametengenezwa na Mzee Dosam kuwa roboti la kutengeneza pesa.

Hamza aliishia kumuonea huruma na kujiwazia kama kampiuni itakuwa katika mikono ya baba yake moja kwa moja itamilikiwa na Lamla na familia ya James na ikifikiria hatua hio Regina atakuwa katika hali gani.

*****

Upande wa chumba cha Bibi Mirium , Shangazi alikuwa akimfunika vizuri

“Madam natoka kwenda kupumzika sasa , uwe na usiku mwema”Aliongea.

“Mariposa hebu niambie , unadhani Hamza anao uwezo wa kumlinda Regina?”Aliuliza na kumfanya Shangazi kugeuka.

“Ndio nina uhakika asilimia mia , ijapokuwa sijui ametokea nchi gani na ni nani haswa lakini kwa kipindi chote nilichomfuatilia , sio mtu mwepesi”

“Kwa uzoefu wako tokea ukiwa kitengoni mpaka sasa , kama umesema sio mtu mwepesi basi naaamini asilimia mia, mimi ndio nishazeeka hivyo , wasiwasi wangu Wilsoni na Regina watapata shida sana , wakati Mzee Dosam ananiambia nisije kumchagulia Regina mume na mtu wa kwanza atakaemchagua nihakikishe wanafunga ndoa nadhani naanza kuamini alichokuwa akimaanisha , huu ni muongozo alionipatia na naona umekuja nikiwa siku zangu za mwisho”

“Lakini madam licha ya kwamba Hamza anaonekana kuwa na uwezo lakini anaonekana kuwa na matatizo kidogo , labda ila sina uhakika..”Aliongea Shangazi akisita sita.

“Unamaanisha nini?”

“Kwa uchunguzi wangu wa kimya kimya nilioweza kufanya nimeweza kugundua yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Eliza , mpaka sasa nashindwa kujua kama Regina anafahamu hilo”

“Unamaanisha huyu Eliza mtoto wa mzee Mlowe?”

“Ndio”

“Haha.. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Eliza amekuwa vizuri licha ya changamoto alizopitia , huyu Hamza inaonekana ana jicho la kuona mbali yule mtoto anafiti kila idara, lakini kama anataka kuendelea kuwa na Hamza lazima akubali baadhi ya ndoto zake kutotimia”Aliongea.

“Madam unamaanisha..”

“Wanaume siku zote ambao wana uwezo mkubwa , hawajawahi kuwa waaminifu , Dosam mpuuzi yule alinisaliti mchana kweupe bila hata ya kujutia , nadhani unajua ninachomaanisha Mariposa”Aliongea lakini kauli ile ilimfanya Shangazi kupiga magoti mara moja.

“Madam samahani sana haikuwa nia yangu…”

“Inatosha sasa , wote tushazeeka sasa , japo mimi ndio naonekana kizee wewe bado kijana , mbinu yako imefanya kazi nadhani ndio maana Dosam alikupenda , lakini hayo yamepita kwasasa tumekuwa kama dada, huna haja ya kuomba msamaha wakulaumiwa ni Dosam sio wewe,ila bora alikupenda wewe ndio maana sikuwa na tatizo , ingekuwa ni mwanamke mwingine ningeachana nae mara moja”Aliongea Bi Mirium.

“Asante sana kwa kuniona mtu mzuri”

“Kuhusu huyu Eliza muda si mrefu nitaonana nae na kumfanya anitambue mimi ni nani , kuhusu Hamza kama uwezo anao sio kosa lake kuwa na wanawake wawili watatu, isitoshe unajua fika Regina sio rahisi kudii nae hususani ugonjwa wake ukiamka, kama akikubali kuolewa na Hamza naamini atakuwa na njia zake za kudili na michepuko ya Hamza, hili ni swala ambalo sisi tulioishi muda mrefu hatupaswi kuingilia”

“Madam upo sahihi , na mimi naona hivyo hivyo kwasababu ni watu wazima watafanya maamuzi yao wenyewe”

“Mariposa hebu simama acha kuendelea kupiga magoti , nakutegemgea siku za usoni wewe ndio utakuwa mlinzi wa mtoto wangu na mjukuu wangu , najua ni misheni yako kumlinda Regina kwasababu ya nafsi yake nyingine lakini mimi awe Regina au yule mwingine wote ni wajukuu wangu.. nakuomba uhakikishe Regina anakuwa salama , ndio namna pekee ya Wilsoni kuwa salama pia”

“Madam mimi Iris nitaulinda ukoo wako mpaka hatua ya mwisho ya uhai wangu”Aliongea Shangazi akijiita Iris huku akikakamaa kama mwanajeshi.

****

Hamza mara baada ya kurudi kwenye chumba chake alimtafuta kwanza mpenzi wake Eliza na kumuulizia swala la mama yake lilivyoenda.

Eliza alionekana kuwa na furaha mno akisema kwamba Dr Ronica kamhakikishia mama yake anaweza kupona na kurudi katika hali ya kawaida na mtu ataagizwa kuja Tanzania kwa ajili ya kusafiri nae kwenda nje ya nchi.

Eliza pia alikuwa ashafanya utafiti wake na kujua Dr Ronicas anatokea Mayo Medical Center kutoka Rochester Minnesota , akiwa kama daktari namba moja katika hospitali hio yenye matawi Marekani nzima lakini pia namba moja dunnia nzima.

Sasa mara baada ya kujua Dokta Flora Ronicas ndio Dean wa hospitali hio ya chuo na pia CV yake kwa ujumla alijikuta akishangaa na hakuwaza kabisa siku moja mama yake anaweza kutibiwa na mtu mzito kama huyo , ilimfanya kujawa na shauku ya kutaka kumjua Hamza mara moja.

*******

Hakujua hata ametumia masaa mangapi tokea apoteze fahamu , lakini mara baada ya kushituka aliweza kujua alikuwa katika chumba ambacho kilikuwa ni kama hospitali.

Amosi alijikuta akivuta kumbukumbu zake vizuri na kujiuliza ni nani ambae amemkamata kwa kumzimisha na kumleta katika eneo hilo ambalo lilionekana kama hospitali lakini kwa upande mwingine lilionekana kama maabara.

Alikuwa amefungwa katika kitanda ambacho mara nyingi aliviona katika filamu za kisayansi , juu yake kulikuwa na kitu kama helmeti ambalo lin vidole vilivyokuwa katika muundo wa chuma , ilikuwa ni kama roboti na ni harufu hafifu tu ndio iliompa nafasi ya kuona eneo hilo sio la kawaida hata kidogo.

Kutokana na kufungwa vizuri hakuweza kukagua eneo lote kwani hakuweza kuangalia nyuma , vitu ambavyo aliweza kuona ni mbele yake na kulia na kushoto kwake.

Alijaribu kufurukukta lakini ilikuwa ni ngumu mno kujitoa, alikuwa amefungwa na chuma na sio pingu.

Alijikuta akiishia kutoleta ukinzani na hio ni mara baada ya kuona kuna Kamera ambazo zilikuwa zikimmulika na moja kwa moja alijua kabisa kila anachofanya kinaonekana.

Na kweli ndani ya dakika chache alisikia mlango kuslide , ijapokuwa hakuweza kuona kutokana na kwamba hawezi kuangalia vitu vya jyuma yake lakini alihisi uwepo wa mtu.

Dakika ileile akiwa na matarajio makubwa ya kumuona mtu alieingia na kumuuliza kwanini amefungwa hapo alishangaa baada ya kuona sura ya mwanamke mrembo alievalia Hijabu , macho yake hayakuwa yakimdanganya mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa ni Sister kutokana na mavazi yake.

“Sister naomba unifungue , hapa ni wapi?”Aliuliza Amosi huku akiwa na wasiwasi, ukweli ni kwamba alijihisi hayupo Tanzania na kuna hisia zilimwambia pengine amelala muda mrefu akiwa hajitambui.

“Kuwa mtulivu Mr Amosi , kadri unavyohangaika ndio unavyojiumiza , isitoshe kidonda bado hakijapona vizuri”Aliongea Yule Sister na kumfanya Amosi kushangaa.

“Kidonda , unamaanisha kidonda gani?”Aliuliza Amosi huku akijaribu kudhibiti mwili wake kujihisi kama kuna maumivu sehemu , lakini hata sehemu ambayo alipatwa na jeraha la risasi palikuwa pashapona na hakusa na maumivu.

Sister yule alionyesha kutoa tabasamu na dakika ileile alipiga makofi mawili na kitanda alicholalia Amosi kilianza kubinuka taratibu na kumfanya akae kitako na baada ya pale kiti kile kiligeuka kama kiti cha saluni na kumgeuzia upande mwingine.

Hakukuwa na kitu cha kushangaza zaidi ya Runinga iliokuwa mbele yake, ki ufupi alikuwa wodini , utofauti ni kwamba wodi aliokuwa ilikuwa imeendelea zaidi .

“Hello Mr Amosi , naitwa Dokta Maya Thema kutoka kitengo cha tiba ya fahamu ilioendelea chini ya Sinagogu , unachokwenda kuona ni hatua kwa hatua za operesheni ya kupandikiza Chip kwenye ubongo wako bila kufungua kichwa chako , tunatumia teknolojia maalumu ambayo ina uwezo wa kutengeneza Chip ndani ya ubongo wako kwa kukuingizia mionzi isiokuwa na madhara ambayo huambatana na madini maalumu , kazi kubwa ya chip hii ni kuushitua ubongo wako na kutengeneza daraja la kimawasiliano kati ya ubongo wako na vifaa vyetu vya kielektroniki..”Amosi alijikuta akishangazwa na kauli ile , sauti iliokuwa ikisikika ndio ya Sister aliekuwa ndani ya chumba hicho japo kwenye Skrini alionekana kuvalia barakoa na PPE.

“Sister nani anakwenda kufanyiwa hio operesheni ya kupandikizwa Chip?”Aliuliza Amosi huku akiwa na hali ya kuchanganyikiwa.

“Mr Amosi operesheni imekwisha kufanyika , unachopaswa ni kuangalia na majibu ya maswali yako yote utayapata”Aliongea yule Sister na kumfanya Amosi kugeuza macho yake kwenye Runinga.

Hazikupita dakika chache Skrini ilianza kuonyesha taaarifa za mgonjwa ambae amefanyiwa operesheni, kitu cha kwanza ambacho kilimfanya Amosi kushikwa na mshituko ni mara baada ya kuona jina lake , Amosi Sembe..”.

“Hapana , haiwezekani”Aliongea Amosi na kuanza kufurukuta kwa nguvu akitngisha kile kitanda na kumfanya yule Sister kumwangalia kwa macho ya masikitiko na palepale aliangalia Kamera na kutoa ishara flani na ni ndani ya sekunde tu Amosi alishikwa na usingizi na kulala tena.

“Tutaendelea baadae akionyesha kuukubali ukweli ,ninachowahakikishia upasuaji umeenda vizuri kwa asilimia mia moja na baada ya hapa atakuwa Agent mahili na kukamilisha misheni zenu zote”Aliongea yule Sister huku akionyesha ishara ya heshima kwa kuangalia zile Kamera , ilionyesha ni dhahiri kuna watu ambao walikuwa wakiangalia, haikueleweka Amosi alikuwa wapi.

*********

Siku iliofuata Regina na Hamza hawakuenda kazini bali walimchukua bibi yao kumpeleka hospitali ya chuo ya Muhimbili .

Kwasababu Ronicas alitarajiwa kukutana na wanafunzi wote wanaosomea udaktari na kutoa hotuba yake ilibidi wapelekwe kabisa katika upande wa wodi za watu mashuhuri kwa ajili ya kusubiri.

Bibi Mirium alitumia nafasi hio kumuuliza Hamza kuhusu maisha yake kwa ujumla wapi alipotokea na familia yake ilipo , lakini alishia kutunga uongo ulioenda shule lakini upande wa Bibi huyo alionekana kuamini na kuishia kufurahi.

Wakati wakiendelea kusubiri mlango ulifunguliwa na akaingia mwanaume mrefu alieenda hewani alievalia shati la mikono mirefu, alikuwa mweusi aliependeza kwa kufuga nywele zake na kuwa ndefu.

Mara baada ya kuingia tu alionyesha hali ya furaha katika uso wake na kumsogelea Bibi Mirium.

“Grandma , I missed you so much”Aliongea kwa sauti laini isiokuwa ikiendana na muonekano wake , ukweli Hamza alidhania bwana huyo angekuwa na sauti nzito lakini alivyoongea alionekana kama aina ya wale watoto walioharibiwa na wazazi wao kwa kudekezwa.

“Naona hatimae umezileta ngula zako hapa Frank”Aliongea Bibi Mirium huku akitabasamu.

Upande wa Regina kwa namna ambavyo alionekana ilikuwa ni dhahiri kabisa hakuwa na mpango wa kusalimiana na Frank.

Hamza pia ilikuwa mara yake ya kwanza kuonana na mdogo wake Regina na kwa kumwangalia tu bwana huyo licha ya kubarikiwa mwili mzuri lakini alikuwa dhaifu mno kiasi kwamba ilionyesha alikuwa akifanya sana ngono.

Frank mara baada ya kusalimiana na bibi yake alisimama na kumwangalia Hamza huku akiweka tabasamu bandia.

“Kwahio huyu ndio boyfriend wa dada yangu , Shemeji yangu sio?”Aliuliza.

“Habari yako mzee”Aliongea Hamza huku akionyesha kutotaka kuendelea zaidi kuongea nae.

“Wewe Frank ni lini utaanza kufanya intership yako ndani ya kampuni , ongea na dada yako akupatie nafasi uanzie chini kabisa”Aliongea bibi lakini kauli ile ilimfanya Regina kukunja sura , ilionyesha dhahiri hakupenda.

“Bibi mimi pia ni mwanafamilia , sidhani kuna haja ya mimi kufanya intership , unaonaje ukinikopesha bilioni mbili napanga kuanzisha kampuni ya Mutual fund

“Yaanni huna hata uzoefu wa kufanya kazi ndani ya kampuni unataka kuanzisha kampuni?”Aliongea Bibi Mirium huku akimkodolea macho Frank.

“Lakini tayari Dada ashakuwa CEO , sihitaji uzoefu kwani nina uwezo wa kuajiri watu wazoefu ambao wanaweza kuniongoza , bibi nadhani unanijua mwenyewe mjukuu wako ninaweza kujifunza haraka , sihitaji uzoefu kabisa”

“Usinione kichaa wewe mtukutu , ni aidha ukatafute kazi au ukaanze kufanya kazi ndani ya Dosam katika ngazi ya chini kabisa, unadhani dada yako amekuwa CEO kwa kupendelewa , wakati akiwa chuo ashaanzisha kampuni yake na kuipa thamani mpaka akafanikiwa kuiuza kwa Bilioni kumi na ndio tulitumia nafasi hio kushawishi wakurugenzi kumpigia kura kuwa CEO, lakini wewe ni tofauti , unachoweza ni kucheza tu na hutaki hata kutumia ujuzi na akili halafu unataka nikupe hela yote hio uongoze kampuni , unadhani mimi kichaa”Aliongea na kumfanya Frank kutabasamu kwa kufosi.

“Basi bibi yaishe , mwakani namaliza chuo , utanipa hisa zako lini?Aliongea na kumfanya Bi Mirium kumpiga konzi.

“Yaani mimi nikosiriasi unaanza kufikiria kuhusu hisa zangu , ni lini utajifunza , kama nikitoa hisa zangu itakuwa ni aidha kwenda kwa baba yako au kwa dada yako, sio zamu yako”

“Bibi unachofanya ni upendeleo , Dada anakwenda kuolewa muda si mrefu na mimi ndio mtu pekee wa kuendeleza ukoo , Da Regina tayari ana hisa kumi na tisa ila mimi hata hisa moja sina”

“Hela ya matumizi unayopewa ni zaidi ya bilioni moja , unataka hisa za nini?”Aliuliza Bi Mirium huku akionyesha hana furaha.

“Bibi..”Frank alijikuta akishindwa kuendelea kuongea zaidi na alikuwa na hasira mno kiasi cha kusugua meno yake kwa hasira.

“Basi bibi haina shida nitakusikiliza kwasasa chochote unachoongea”Mara baada ya kauli hio alimsogelea Hamza.

“Shem , unaonaje tukienda kuongea kidogo hapo nje?”Aliuliza na kumfanya Hamza kushangaa na kujiuliza huyu bwana anataka nini.















SEHEMU YA 47.

Regina pia alishangaa na kumwangalia Frank kwa ukauzu.

“Frank unachotaka ni nini?”

“Sister hakuna ninachotaka , nataka kuongea na shemeji yangu sidhani ni tatizo , isitoshe siku zote kuna mazungumzo ya kiume huwa yanafanyika”Aliongea huku akicheka

“Hamza unaweza kuondoka , Frandk anataka kuongea na wewe sio mbaya , isitoshe Dokta Ronica hajafika bado”Aliongea Bibi huku akijilaza vizuri kwenye kitanda.

“Wapi tunaenda kuongea?”Aliuliza Hamza.

“Wewe nifuate tu”Aliongea na kisha alianza kuongoza njia.

Regina alikuwa na wasiwasi , baada ya wote wawili kutoka alimsogelea bibi yake na kumuongelesha kwa sauti ya chini

“Bibi umemuona Frank alivyo katika macho yake anachokiwazia ni hisa zako , haonekani kujali afya yako kabisa”

“Najua.. lakini vyovyote vile ni mdogo wako na ni mjukuu wangu”Aliongea na kumfanya Regina kujawa na hisia zisizoeleweka na aliishia kugeuka na kunyamaza.

Upande mwingine Frank alimchukuaHamza mpaka eneo la kuegeshea magari .

“Shem vipi tena , kwanini umenileta kote huku?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.

“F*ck you , nani shemeji yako?”Aliongea kwa hasira huku akimtolea Hamza macho.

“Wewe ndio ulieniita Shemeji wala sijakulazimisha?”

“Unakichaa , unadhani mpuuzi kama wewe masikini masikini unaweza kuwa shemeji yangu?”Aliongea huku akiingiza mkono wake mfukoni.

Hamza aliishia kumwemwesa midomo huku akijiwazia huyu Frank anaonekana kuwa na akili ndogo mno , licha ya kwamba alikuwa na undugu na Regina alijiuliza imekuwaje kuna utofauti mkubwa wa akili baina yao.

“Kwahio umeniita hapa kwa ajili ya kuongea huu upuuzi?”

“Nimekuja kukuambia Dada yagu ataolewa na James na si vinginevyo , lazima aolewe na familia ya Mzee Benjamini , hivyo kama unajielewa ni bora ukaondoka ndani ya hili jiji mapema na kupotea nisikuone tena”

“Kama niliependana nae ni dada yako wewe kinachokuuma nini , unadhani naweza kusikiliza pumba zako?”

“Wewe huwezi kunielewa kabla ya kufanywa kiwete”Aliongea na muda uleule alipiga simu na kwa sauti kubwa alionekana kuita watu.

Ilionekana kuna watu ambao alikuwa tayari ashawaandaaa kwani ndani ya nusu dakika wanaume wawili warefu na waliojazia waliingia huku wakiwa na vifaa flani vya mawasiliano kwenye masikio yao , walionekana kama wanausalama .

“Hawa wote ni mabodigadi wangu , wamepitia jeshi kabisa , nikitaka kukupiga ni swala la dakika tu , vipi ushaanza kuogopa?”Aliongea na ilionekana alitegemea mabodigadi hao kumuogopesha Hamza.

“Yaani unataka mabodigadi wanipige , huogopi nikikusemea kwa dada na bibi yako?”

“Hio ni baada ya kukugeuza kiwete , unadhani najali ukiwaambia wala kunishitaki , hawawezi kunifanya chochote kwa ajili ya mtu usie na undugu kama wewe”Aliongea huku akicheka.

“Naamini hujawa mjinga kiasi cha kufanya haya maamuzi?”

“Mpuuzi wewe yaani mtu huna mbele wala nyuma lakini unataka kuvunja undugu tunaotaka kutengeneza kati ya familia yetu na ya Mzee James , mimi mrithi wa mali za familia siwezi kuona hili likitokea kwasababu ya wewe na mjinga mwenzako Regina , hivyo nakupa onyo mara ya mwisho unaondoka au huondoki?”

“Umesema huwezi kuruhusu mtu kama mimi lakini kwanini unamwingiza na dada yako?”

“Kwahio nini sasa au ndio unategemea mwanamke kuja kukusaidia hapa, wewe ni..”Kabla hata hajamaliza sentensi yake alijikuta macho yake yakiingiwa na ukungu.

Frank alijikuta akipiga ukulele huku mikono yake ikiwa mdomoni kwake kutokana na maumivu makali ambayo alikuwa akiyasikia.

Ilikuwa ni pigo kutoka kwa Hamza alilomlenga usoni , ijapokuwa hakutumia nguvu lakini ngumi yake ilitosha kumletea maumivu makali mtoto wa kudekezwa kama huyo.

“Takataka kama wewe unajilinganisha vipi na mimi , ushukuru tu sina mpango wa kukuua”Aliongea Hamza huku akimwangalia Frank ambae ashaanza kulia.

“Mpigeni huyu mshenzi , mpigeni mpaka afe”Aliamrisha mabodigadi wake.

Mabodigadi wale walijikuta wakianza kumshambulia Hamza kulia na kushoto lakini Hamza hakuongea chochote ilikuwa ni teke lake moja na ngumi yake moja aliwafurusha wale mabodigadi kama vifurushi na kwenda kujigonga kwenye magari.

Kitendo kile kiliwafanya waanze kumwangalia Hamza kwa hofu , ukweli ni kwamba hawakujua hata wamepigwa vipi kwani walijikuta tu wakiogelea hewani.

Hamza baada ya kuwapatia kipigo cha kushitukiza wale mabodigadi alimsogelea Frank na kisha alimshika kola na kumning’iniza hewani na kuanza kumwangalia na macho yasiokuwa ya kawaida , kitendo kile kilimfanya Frank kuanza kushikwa na ubaridi wa hali ya juu mno kiasi kwamba kidogo tu angejikojolea.

“Bro.. hapana shemeji naomba unisamehe sitorudia tena , nimekosea usinipige”Aliongea huku akilia kama litoto jinga.

“Kumbuka hakuna dawa ya majuto kwenye maisha , ukichagua kufanya jambo baya basi ni kosa lako la maisha, lakini hata hivyo mimi ni mvumilivu sana , hivyo leo nakupa onyo lakini kumbuka kwenye maisha yangu sijawahi kumpatia mtu nafasi mara mbili”

Frank alikuwa ni kama amechanganyikiwa , hakuweza hata kumsikia Hamza vizuri kwani alikuwa akiogopa mno.

Hamza aliishia kumtupa Frank kama furushi kwenye lami na kisha alitoa gomba mfukoni na kuitoa karatasi na kuanza kuitafuna bila ya wasiwasi huku akirudi alikotoka.

Mara baada ya kufika katika wodi , kulikuwa na watu wengi wamesimama mlangoni na karibia wote walikuwa ni viongozi wa hospitali.

“Ilikuwa ni dhahiri Ronica ashafika na kuanza matibabu , Hamza hata hakujali watu hao na alijiminya minya na kuingia ndani na hatimae aliweza kumuona Regina akiongea na Dokta Ronica na Flora mara baada ya kumuona Hamza alimkonyeza huku akitabasamu.

“Well , do you want a CT?”Aliuliza Hamza akimaanisha je anahitaji vipimo vya CT scan.

“No need , I‘ve already seen them all , there are migratory thrombophlebitis and arterial thrombosis..”Aliongea

“Duuh , ndio ipo hivyo…”Aliongea Hamza huku akionyesha kukunja sura.

Mara baada ya Regina kuona Flora na Hamza wanaongea kingereza huku wakitumia maneno ya kitabibu alijikuta akizidi kujiambia Hamza anazidi kutokuwa mtu wa kawaida.

Isitoshe mtu wa kawaida asingelewa maneno ya kitabibu lakini Flora aliongea kama vile Hamza anamuelewa.

“Dokta Ronica unaweza kuelezea shida yake , sijaelewa kitu”

“Wewe niite tu Flora , ni mpenzi wa Hamza hivyo haina haja ya kuonyesha heshima kiasi hicho mbele yangu”Aliongea na kumfanya Regina kuona aibu huku akitaka kuelezea yeye sio kama anavyofikiria lakini alishindwa kutokana na uwepo wa bibi yake.

“Miss Regina , ijapokuwa naweza kuonekana mkatili kwa kauli yangu , lakini naomba niseme tu kwamba huna haja tena ya kupoteza nguvu na pesa zako kutafuta madaktari , kitu pekee unachoweza kufanya ni kumuandaa mgonjwa kwa ajili ya saa yake ya mwisho”Aliongea na kauli ile ilimfanya Regina sura yake kujikunja.

“Dokta hata wewe huwezi kufanya chochote?”

“I am so sorry , I am a doctor not a God”Aliongea kwa sauti ya radhi huku akimwambia kwamba yeye ni daktari na sio Mungu.

“Ukweli ni kwamba mara nyingi nakutana na wagonjwa ambao kesi zao zinakuwa ni ngumu sana kimatibabu na katika utaalamu wangu ni asilimia therathini tu ya wagonjwa waliopona , asilimia sabini wengi wao hawatibiki”Aliongea.

Ijapokuwa Regina alikuwa amejiandaa kwa taarifa hio lakini ilikuwa ni huzuni kwake kusikia hakuna tumaini lolote kabisa na alijikuta machozi yakimtoka.

Bibi nae alikuwa akisikia kila kitu juu ya afya yake na mara baada ya kuona namna mjukuu wake alivyokuwa na huzuni aliishia kumwambia asogee karibu yake.

Ukweli ni kwamba tokea jana mara baada ya Ronica kupokea taarifa ya kimatibabu ya Bibi Mirium alishajua anakufa na ni swala la muda tu ila kufika kwake ni kwa ajili ya kumheshimisha Hamza pekee.

Lakini yeye kama dokta alishakutana na hali kama hizo mara nyingi na huwa hampi mgonjwa matumaini hewa.

Baada ya hapo Dokta aliaga na kisha alimpa ishara Hamza kuongozana nae nje na waienda kusimama kwenye balkoni.

“Unaondoka leo?”

“Ndio , nitaondoka mchana lakini kabla ya kuondoka nimesikia taarifa inayokuhusu”Aliongea.

“Nini?”

“Kuna mtu alivunja katika maabara ya Profesa na aliweza kupata anuani ya mahali unapoishi kwa sasa , hivyo ni sawa na kusema inajulikana unaishi Dar es salaam”

“Umeshachelewa kuniambia mbona , watu tayari walishatumwa na kuanza kuniletea matatizo”Aliongea na kumfanya Flora kushangaa.

“Mapema hivyo?”

“Doctor Genesha amejua kuniletea matatizo mno , nataka ukifika ukusanye kila kinachomuhusu na uchome moto , ndio namna pekee ya kuniepushia na matatizo”

“Vipi kuhusu tafiti ya Mti Wa uzima , unataka na zenyewe zichomwe moto?”

“Bado tu unazo hizo tafiti , zitakuletea mtatizo mno , ijapokuwa hatujapiga hatua yoyote kwenye kutafsiri lakini huwezi zuia shauku na matamanio ya watu wenye tamaa”

“Lakini tafiti ile ndio maisha ya Mwalimu na alikufa kwa ajili ya kuilinda”Aliongea Flora kwa kusita.

“Utafiti wake haujakamilika na Tembo wa Trishaza ameshakufa , chukulia tu kama ndoto nzuri na baada ya kuamka sio uhalisia”Aliongea Hamza akiwa siriasi.

“Sidhani kama ni kweli , taarifa za siri nilizosikia ni kwamba kabla ya Profesa kupoteza maisha alishafanikiwa na matokeo ya tafiti yake alimpatia rafiki yake wa karibu , kwa ninavyojua Profesa hajawahi kuwa na rafiki wa karibu tofauti yako”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia Flora na macho yaliojaa usiriasi.

“Inamaana hata wewe huniamini?”

“I am Sorry my Prince , I‘m just curios”

“Curiosity is sometimes not a good thing”Aliongea akimaanisha kwamba shauku muda mwingine sio nzuri na Flora alitingisha kichwa kumwelewa.

“Nitaondoka kwanza , napaswa kwenda kuangalia kinachoendelea”Aliongea Hamza na Flora alitingisha kichwa.

Wakati Hamza anakaribia mlango ulifunguliwa na Regina alitoka , ukiachana na macho yake kuwa mekundu lakini alikuwa amerudi katika hali yake ya kikauzu.

“Nipeleke kazini”Aliongea.

“Hutaki kuongozana na bibi kurudi nyumbani?”

“Nitaongozana na wewe, isitoshe napaswa kukujua kidogo kwa muda haina haja ya kuwa na haraka sana , vipi au huoni unapaswa kujiandaa?”

“Kujiandaa na nini?”Aliuliza Hamza akimwangalia Regina kwa mshangao,

*******

TEL AVIV- ISRAEL, 13;25.

Ni saa saba dakika ishirini na tano katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tel Aviv Israeli , katika eneo la maegesho ya magari ziliingia gari tatu mbili zikiwa gari ndogo za kifahari na moja ilikuwa ni gari ndefu ya kifahari aina ya Cadillac escalade ESV isiopitisha risasi.

Baada ya gari zile kusimama gari iliokuwa mbele kabisa walishuka vijana wakiyahudi waliovalia suti na miwani pamoja na vifaa vya mawasiliano.

Haikuhitaji akili kujua kuna mtu mzito ambae anapokewa ndani ya eneo hilo na ilikuwa kweli kwani ndani ya dakika chache baada ya ndege ya kifahari kutua , alitoka mwanaume katika mlango wa watu mashuhuri mzee wa makamo ambae ameongozana na watu wanne kati yao mmoja alikuwa mwanamke na kwa tembea yake ilipaswa kuonekana wale wote walikuwa ni wasaidizi wa yule mzee aliekuwa na mvi wa umri kama wa miaka sabini hivi.

Dakika ileile mara baada ya mzee yule kutoka nje kabisa wale watu ambao walikuja na gari la kifahari walimsogelea yule mzee na kumzingira huku kiongozi wa msafara akijitambulisha kwa dakika chache na baada ya pale walioekana kuelewana na kusogelea lile gari la milango mingi na bwana yule aliingia pamoja na yule mwanamke na bwana mwingine na kisha waliobakia mmoja aliingia katika gari ya nyuma huku mwingine akiingia katika gari ya mbele.

Ilichukua dakika chache tu gari zile zilikwenda kusimama katika jengo la hoteli ya David Kempisky na kupokelewa na wahudumu waliokuwa nadhifu na kumuelekeza moja kwa moja kuingia ndani.

Lakini Mzee yule mwenye nywele zake nyeupe kadri alivyokuwa akipiga hatua ni kama kuna hali ya wasiwasi iliokuwa ikionekana katika macho yake, mara nyingi kwa kufika hotelini alipaswa kuwa na hali ya utulivu kwa kuelekea sehemu ya kupumzikia lakini kulikuwa na wasiwasi.

Yule mwanamke wa makadirio ya miaka kama therathini hivi mwenye nywele zake nyeusi ni kama aliona hali aliokuwa nayo bosi wake na alitoa kitu kama bublish kutoka kwenye mkoba na kumpatia na kisha akampatia na maji na mara baada ya dakika moja tu alijikuta akivuta pumzi na kutulia na hatimae lift ilifunguka na safari ya kuingi katika korido ilisonga huku wakipokelewa na Maneja na walienda kusimama katika mlango uliokuwa na maandishi makubwa ya VVIP na kwa nje alionekana kuwepo mwanamke mlinzi ambae alikuwa amekakamaa mwili na baada ya kupewa kadi na yule mwanamke, alionekana kuelewa na kisha aliongea kupitia kifaa cha mawasiliano na mlango uifunguka palepale.

“Welcome Mr Alfonso!!”

Sauti ya kike iliongea na kumfanya yule mzee kupagawa na mara baada ya kuangalia mtu aliekuwa mbele yake sura yake ilianza kujikunja na hata ule wasiwasi kupotea.

“Frida kwanini ni wewe hapa?, yupo wapi Prince?”Aliuliza na swali lake lilimfanya Frida kutoka katika tabasamu na kuwa na uso uliojaa usiriasi na kuanza kupiga hatua kiasi cha kufanya bwana alieitwa Alfonso kurudi nyuma kwa hofu.

******

Upande mwingine katika makazi ya Raisi Mstaafu Mzee Mgweno Mandia kulikuwa na kikao kilichokuwa kikiendelea , kikao hiki kilikuwa kikihusisha kamati ya kampeni ya Mheshimiwa Jongwe pamoja na wadhamini wake wakuu.

Moja ya watu ambao walikuwa wakitambulika kwa sura alikuwa ni MzeeBenjamini mmiliki wa kampuni ya Zena.

Watu wote walikuwa wamekaa kwenye masofa ya gharama na mtu ambae alionekana kukosekana ni Mzee Mgweno mwenyewe , ilikuwa ikionyesha ni yeye pekee ambae alikuwa akisubriwa.

“Mzee Benjamini misheni yako naona inazidi kuchukua muda , imekuwaje ukashindwa kuimeza kampuni ya Dosam , unarudisha nyuma juhudi za mheshimiwa katika ujenzi wa ngome yake , umeshakuwa ufa tofauti ya gundi”Aliongea.

“Kwavava unaongea nini? , kitu pekee ambacho una mchango katika ujenzi wa ngome ya mheshimiwa ni cheo chako cha umakamu ndani ya kitengo cha MALIBU , ukivuliwa hicho cheo wewe sio tofali tena unabakia kuwa tope”Aliongea Mzee Benjamini na kauli ile ilifanya baadhi ya watu kutabasamu na baadhi ya watu kuingiwa na wasiwasi.

“Acha kujipa umuhimu ambao hujapewa , mtu mwepesi kama wewe huwezi hata kutofautisha kati ya seruji na tope ndio maana huwezi kuona umuhimu wangu , Shame on you”Aliongea na kumfanya Benjamini kutaka kupandisha lakini alizuiwa na bwana aliekuwa karibu yake.

“Kwavava hivi ni lini mtakuja kukaa meza moja bila ya kugombana , sisi wote ni familia moja maswala yenu binafsi hapa hayana nafasi , kwa nje Afande Kwavava unaaminiwa kuwa na busara lakini mbele ya Benjamini unashindwa kujizuia ni kipi kinaendelea kati yenu?”Aliongea na kuwafanya wote wawili kunywea.

“Mzee Jongwe kama kawaida yako , nadhani mheshimiwa hakukosea kukupigia chapuo mpaka sasa unapeperusha bendera ya chama , neno lako moja tu kelele kwisha”Aliongea na kauli yake ilimfanya Mzee Jongwe kutoa tabasamu hafifu.

“Mheshimiwa Lughalila huna haja ya kwenda mbali kwenye kunisifia , kama nilivyosema nafasi yako baada ya kushinda ipo wazi”Aliongea Jongwe na kumfanya jamaa alieitwa Lughalila kutoa tabasamu.

Dakika ileile mlango ulifunguliwa na msaidizi wa Mheshimiwa mstaafu na aliingia kana kwamba yeye ndio anaeongoza nchi , maana watu waliokuwa hapo ndani kila mmoja alikuwa na cheo , kama sio mwanajeshi basi ni mwanasiasa.

Mheshimiwa Jongwe licha ya kwamba ni mstaafu lakini bado afya yake ni imara kabisa , ndio mstaafu pekee ambae alikuwa hai mara baada ya watangulizi wake wote kutangulia mbele za haki.

“Nafasi ya Gabusha mbona ipo wapi?”Aliuliza mara baada ya kusalimiana na viongozi hao na kauli ile ilimfanya kila mtu kumwangalia Mzee Benjamini.

“Gabusha yupo mkoani Kigoma kujiimarisha?”Aliongea Benjamini na kumfanya Mstaafu kukunja sura.

“Ina maana mambo yake na yule mwanamke hayajakaa sawa mpaka kwenda kujitoa fidia?”

“Mheshimiwa mambo hayakuwa mepesi , kizingiti kilichomkuta Gabusha kimenikuta na mimi?”Aliongea.

“Benjamini unamaanisha nini , usiniambie umeshindwa kutimiza kazi yako mpaka sasa?”Aliuliza na kumfanya Mzee Benjamini kukunja sura.

“Mheshimiwa mpango ulikuwa ukienda vizuri , lakini mara baada ya huyu bwana anaeitwa Hamza kujitokeza kila kitu kimeenda ndivyo sivyo , kila tunalopanga linaenda Kombo”Aliongea kwa namna ya kujitetea huku akisimama na kumfanya Mheshimiwa kumwangalia kwa kutoridhika.

“Unaweza kukaa chini tuanze kikao chetu , isitoshe Ajenda yetu pia inahusiana na huyu anaeitwa Hamza , nilimpotezea mwanzo ila naona anaanza kuwa tatizo”Aliongea na kumfanya Mzee Benjamini kupata ahueni na baada ya hapo alianza kupitia sura ya kila mmoja aliehudhuria na alikuja kusimamisha macho yake kwa Mheshimiwa Jongwe.

“Jongwe hali ya mwitikio katika kampeni zako kwa wananchi zinaendaje?”

“Mheshimiwa kampeni zinaendelea vizuri sana na nimerudi Dar es salaam kwa ajili ya kufunga kampeni , kwani mwezi ujao tunaingia moja kwa moja katika upigaji kura”

“Una uhakika wa kushinda, vipi kuhusu mpinzani wako?”Aliuliza na kumfanya Mzee Jongwe kusita kidogo lakini alianza kuongea.

“Kuhusu Msemakweli amekuwa tatizo na hivi baada ya tukio la kupotea kwa Tajiri wa Kenya na Balozi wa Rwanda na jambo hili kulihusisha na mtandao wa Panyaroad ameanza kuteka fikra za wananchi, mheshimiwa kwannini nisitangaze moja ya nia yangu ni kuitokomeza Chatu?”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa kukunja ndita kidogo.

“Uko juu juu sana Jongwe kimawazo , ndio kitu ninachokupendea na kutokukupenda kwa wakati mmoja kwani inakufanya kuwa dhaifu, mpaka sasa kushinda kwako kwa uchaguzi kupo katika mikono ya mtu mmoja , inategemea na namna utakavyomshawishi katika kikao hichi , la sivyo tutatumia nguvu nyingi sana kukuweka Ikulu au Waangalizi watushitukie kuiba kura na kuhatarisha amani ya nchi”Aliongea na kufanya watu wote hapo ndani kutoelewa kauli yake inamaanisha nini , lakini dakika ileile walielewa alichomaanisha kwani mlango ulifunguliwa na hapo ndipo walipojua Mheshimiwa alikuwa akimaanisha nini.

“Nadhani wote mnajua huyu , sina haja ya kuwatambulisha , lakini kabla hajaenda kuongea na kuanza kikao nataka kutoa maelekezo kwamba tukio la kupotea kwa balozi , kifo cha Kamishina msaidizi na wengine linahusiana na yeye”Aliongea na kisha alilazimisha tabasamu na kumwangalia Dina kwa namna ya kumkaribisha.

“Siwezi kuhatarisha mtandao wa Chatu kuteteleka , ndio msingi wa ngome yangu , nitakutumia kuimarisha na kuvuta kipindi hiki cha mpito na baada ya hapo nitakutoa kwa ulazima”Aliwaza mheshimiwa huku akimwangalia mrembo huyo kwa macho yaliojaa ufeki na matamanio.
 
SHETANI RUDISHA AKII ZETU



MTUNZI:SINGANOJR





SEHEMU YA 47.

Ilikuwa ni dhahiri kwa mwanaume aliefahamika kwa jina la Mr Alfonso kutokutarajia mtu ambae alipaswa kuonana nae kwa kufanya safari ya kufika Israeli kuwa Frida, kwa muonekano wake wa haraka haraka ilionyesha alikuwa akimfahamu fika Frida na macho yake yalionyesha hofu na wasiwasi kiasi cha kurudi nyuma na kurudia mlango akitaka kutoka.

Mara baada ya kupalamia mlango akihitaji kuufungua haukufunguka na alijikuta akigonga kwa nguvu lakini bado hakuweza kusikia watu kutoka nje na akili yake ilimwambia walinzi wake na wasaidizi wapo chini ya ulinzi wa Frida.

“Mr Alfonso sifa zako haziendani na kile ambacho watu wengi wanaongea kuhusu wewe , sidhani ni sahihi kumuogopa mwanamke ambae hana siraha yoyote”Aliongea Frida huku akitoa sura ile ya usiriasi na kuuvaa ukarimu huku akipiga hatua kumsogelea.

“Wewe ni shetani .. usinisogele?”

“Mimi ni nani?!. Kama kweli mimi ni shetani sidhani unapaswa kuogopa, kwa sifa za cheo chako wanaokufuata wakisikia kiongozi wa Sinagogu anamuogopa mwanamke aliemwita Shetani ni dhahiri haitokuwa taswira nzuri kwako?”Aliongea Frida na kumnyooshea mkono Mr Alfonso.

“Unataka nnini kutoka kwangu , mpaka kuniwekea mtego kwa kujitambulisha wewe ni Prince?”Aliuliza.

“Sina chochote ninachotaka kutoka kwako , bali sisi ni watu wenye malengo sawa ndio maana umefika kwa haraka bila ya kufanya uhakiki wa ki usalama?, sipo hapa kama adui bali kwa niaba ya Maadam”Aliongea na kumfanya Mr Alfonso kuvuta pumzi nyingi huku bado akimwangalia Frida kwa wasiwasi.

“Historia na kanuni za imani yangu zinanikataza kufanya hivyo, kwanini nikuamini wewe uliekengeuka , haijalishi nini unachohitaji kwangu , kutumia hila kunisafirisha mpaka hapa ni kosa kwa upande wako na sio kwa upande wangu?”Aliongea.

“Kama ni hivyo basi malengo yenu hayawezi kufanikiwa na hili unalijua ndio maana taasisi yako ikanichomesha kwa viongozi wangu , ili nichukuliwe hatua , lakini ajabu malengo yenu hayakutimia na sasa nipo hapa kwa niaba ya jumuiya”.

“Tulichofanya sio kukuchomesha , huwezi kusema hivyo ilihali umeingia katika dhehebu letu kama Double agent na haukuwahi kuwa mmoja wetu, wewe ni msaliti na doa kwa imani yetu na hatuwezi kukaribisha tena”Aliongea na kumfanya Frida kutabasamu.

“Basi nadhani ni muda sahihi wa sisi kukaa chini na kuongea, kama nilivyosema nipo hapa kama muwakilishi wa Wiccan , siku zote hii ndio njia yetu ya kuwasiliana ili kuficha mienendo yetu , hivyo huna haja ya kukasirika na unapaswa kuuliza kwanini umeletwa Israeli kutokea Brazili”Aliongea Frida na muda ule hakutaka kuongea nae tena akiwa amesimama kwani alirudi katikati ya chumba hicho chenye samani za gharama na kisha akakaaa kwenye sofa.

Mr Alfonso licha ya kuwa na wasiwasi alijikuta akivuta pumzi na kisha kusogea taratibu na kwenda kukaa kwenye masofa mbele ya Frida.

“Utapendelea kinywaji?”Aliuliza Frida huku akimimina mvinyo kwenye glasi.

“Hapana nashukuru , nadhani ni vyema ukienda moja kwa moja kwenye dhumuni lako”Aliongea na kumfanya Frida kutabasamu ki uchokozi.

“Nahitaji nafasi yangu ndani ya taasisi” Aliongea Frida.

“Hilo haliwezekani hatuajiri panya”Aliongea kwa kingereza.

“Taasisi yenu inanihitaji zaidi ya ninavyowahitaji ,sina haja ya kuelezea hili zaidi , isitoshe misheni zenu zote zinategemeana na tafiti zangu”Aliongea Frida.

“Unamaanisha hatuwezi kuishi bila wewe , Miss Frida kama hicho ndio unachowaza umoja wetu haupo tayari kukupokea , wewe ni dosari kwa misheni zetu na hatuwezi kuruhusu makosa kwa mara nyingine”Aliongea Mr Alfonso.

“Vipi kama nikikuambia siri ambayo ni watu wachache mpaka sasa wanaijua , siri ambayo umoja wangu haujawahi kuifahamu?”Aliongea Frida.

“Una siri ya namna hio , najua kila binadamu ana siri lakini kuwa na siri kama gia ya mazungumzo sidhani inaweza kuwa na ushawishi wa kutosha wa kukurudisha kwenye taasisi”Aliongea Mr Alfonso huku akijitahidi kuonekana ni mwenye kujiamini.

“Umeshawahi kusikia Agent mwenye jina la msimbo(Codename) 2FcommaG?”

“Unataka kusema nini , hilo ni jina la Ajenti ambae umoja wetu umekuwa ukimfatilia kwa muda mrefu na ni taarifa nyeti zaidi ya daraja la juu, unafahamu vipi hii taarifa?”Aliuliza Mzee Alfonso huku akionekana ishara ya kuchangayikiwa.

“Kwasababu mimi ndio Ajenti 2FcommaG maana ya jina hili ni Frida Franklin Genesha”

“Quee!!!”(What!)

Mzee Alfonso alijikuta akimaka huku akisahau kutumia lugha ya kingereza na kuongea kireno, macho yake yalianza kumwangalia Frida kama kwamba kaona mzimu.

“Vipi?, siri yangu imeweza kukupagawisha kiasi hicho?”

“Najua vipi wewe ni kweli ni Ajent 2F tumeweza kukufuatilia kwa muda wa miaka saba mpaka sasa bila ya kukufahamu , umewezaje kujificha kwa muda wote huo mbali na teknolojia yetu?”

“Sikujificha , miaka saba iliopita niliachana moja kwa moja na jina hilo , mlikuwa mkitafuta mtu ambae amekufa na hayupo kwenye ramani hivyo ni sahihi kwenu kushindwa kumpata licha ya kutumia rasilimali nyingi na wanachama wote wa Wiccan tunaishi kwa sura nyingi”Aliongea na muda uileule alichukua kishikwambi kilichokuwa kwenye mkoba wake na kukiweka mezani huku picha ikionekana.

“Najua malengo yenu ya kufungua taasisi ya Haliz foundation nchini Tanzania , pamoja na Dhehebu la kidini , ni kwa ajili ya kutafuta hii alama iliowahi kuwepo miaka mingi na ikapotea..”Aliongea Frida na kumfanya Mzee Alfonso paji la uso wake kutoa jasho.

“Who are you!?”Aliuliza akimaanisha yeye ni nani.

“Wewe ni nani , kwanini unajua siri za juu za dhehebu letu?”Aliuliza na Frida muda huo alikuwa na tabasamu pana.

“Mimi ni mtu pekee ambae nahitajika katika taasisi yenu kukamilisha tafiti zangu , najua mpaka sasa mpo njia panda kuthibtishia waumini wenu juu ya ushahidi wa kiimani wa kuzaliwa upya ili kujipatia wafuasi wapya na kuwa na msingi wa kiimani baada ya kujitoa katika Kanisa kuu huku mkijua muda ukiwa si rafiki kwenu , lakini haya yote hayawezi kufanikiwa bila mimi , mimi ndio ufunguo aliouacha Dokta Genesha , ufunguo wa kuthibitisha nguvu ya kiroho inaweza kuthibitishwa kisayansi, mimi ndio ufunguo wa kuwaonyesha ni nani haswa katika maisha haya anabeba alama yenu iliopotea katika unabii”Aliongea Frida huku wakati huo akiwa amesimama na alionekana kuwa siriasi.

“Umejielezea kuhusu wewe , juu ya kitu unachohitaji , vipi kuhusu Wiccan , wanataka nini kutoka kwetu , sidhani kama ulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kujitoa katika adhabu ya kukiuka sheria za umoja wenu wa kipagani?”Aliongea Mr Alfonso na kumfanya Frida kutabasamu na alirudi kwenye sofa na kukaa chini na kumwangalia usoni.

“Hilo ni swali zuri kwa upande wako Mr Alfonso , kama nilivyosema sisi wote tunatafuta kitu kimoja?”

“Unamaanisha hata nyie wapagani mnahitaji kujua nani amebeba alama iliopotea katika maisha haya? , mnataka kujiaminisha nini kupitia alama hio?”

“Mr Alfonso unajua ni kitu gani ambacho dunia inashindwa kutafsiri maana halisi ya neno Wiccan?”

“Ni rahisi , kwasababu hamuamini uwepo wa Mungu zaidi ya nguvu za giza?”

“Hilo ndio kosa kubwa , sisi sio Wapagani kama watu wanavyojaribu kututafsiri , sisi pia tunaamini uwepo wa Mungu”

“Hilo ni jipya kwangu kusikia kutoka kwa mpagani?”

“Tunaamini Mungu ni nguvu iliopo katika umoja wakati wa kujitetea na udhihirisho ila sisi tunasimama kwa kuamini katika vitu vingi ambavyo hutengeneza kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana ikiwemo Mungu”Aliongea Frida na kumfanya Mr Alfonso macho kuwaka.

“Unaonekana kuwa muumini mtiifu wa Wiccan kwa namna unavyoilezea imani yako , sio jambo baya kwangu kuona unaitetea imani yako , lakini swali langu linasimama palepale mnataka nini kutoka kwetu na ili mdhihirishe nini?”

“Kuijua lugha ambayo imewashinda binadamu wote kuitafsiri mpaka leo ili tuweze kupata vitabu vyote vilivyoelezea uchawi kutoka kanisa kuu”Aliongea na kumfanya Mzee Alfonso macho yake kuchanua.

“Wakati nikihudumu kama Kardinali niliwahi kusikia uzushi mwingi juu ya uwepo wa Manucript za kale zilizohifadhiwa katika maktaba za siri ndani ya makao makuu ya kanisa kuu ,nyaraka ambazo lugha yake haijaweza kutafsiriwa na kujulisha watu zinahusiana na nini , isitoshe sijawahi kuona huo ushahidi wa uwepo wa hizi nyaraka , unachosema wewe kinanifanya niamini pengine ilikuwa kosa upande wangu kupotezea uzushi ule”Aliiongea

“Yapo maandiko mengi sana ambayo yametumia lugha ambayo haijawezekana kutafisirika mpaka leo , kutokana na kanisa kuepusha hatari waliamua kuzificha wakati huo wakizifanyia utafiti, moja ya maprofesa wa kiimani waliopewa kazi hio mmoja wapo ni Dokta Genesha na ndio mtu pekee ambae alipata kufahamu uwepo wa andiko lililojaa siri katika simulizi fupi ya Njiwa juu ya mti wa uzima, tulipeleka mapendekezo kwa kanisa kuu kutupatia hizi nyaraka lakini waligoma , Dokta Genesha alipendekeza njia pia ya kutafsiri nyaraka hizi lakini aligoma vilevile na ndio kilichochangia mauaji yake”Aliongea.

“Dokta Genesha alipendekeza kitu gani kwenda kanisa kuu kilichompelekea kupoteza maisha na vipi kuhusu hii simulizi ya Njiwa juu ya Mti wa Uzima?”

“Askofu sidhani ni sahihi kujua kila kitu , isitoshe kuna kichwa cha habari juu ya simulizi hio lakini kilichoandikwa ndani yake hakifahamiki kwani lugha yake haitafsiriki , lakini kwa mtazamo wa Dokta Genesha ni siri kubwa ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa binadamu”

Aliongea na kumfanya kuanza kuonekana kama mwenye kutafakari , hakueleweka alikuwa akifikiria nini.

“Wiccan wanataka kusaidiwa vipi katika hili , hili likifahamika kwa waumini tutapoteza msingi wetu wote wa kiimani na nguvu tuliotumia kupigania uhuru wetu kwa miaka mingi ili kusimama kama kanisa itakuwa ni bure , siwezi kushirikiana na wapagani kirahisi , hata kukutana na wewe hapa ni kosa?”Aliongea Mr Alfonso.

“Ndio maana tumechukua kila tahadhari , tumemtumia mtu ambae unatamani sana kukutana nae , mtu anaefahamika kwa jina la Prince , Mr Alfonso nadhani huwezi kutuchukia katika hili , ilikuwa ni mbinu ya kuweza kufunika mienendo yetu, kuhusu namna ya kutusaidia sisi ni rahisi sana , napaswa kurudi na kuendelea na tafiti zangu ndani ya Haliz foundation siku yoyote nitakayotia mguu nchini Tanzania , sisi kama Wiccan tumetoka mbali shabaha yenu ni shabaha yetu, nataka kuendelea na misheni na wewe kama Askofu mkuu wa Sinagogi B unapaswa kunirudisha kazini”

“Bado sijashawishika kukubali ombi lako , isitoshe wewe ni muumini tu wa chama cha wapagani wanaoamini katika uchawi , wa kuzungumza hili kiitifaki ni mkuu wako na si vinginevyo”

“Nadhani unapaswa kuniambia unachohitaji , huwezi kuonana na mkuu wangu , kama nilivyosema mimi ni mwakilishi , kama una nia ya kuonana na mkuu wetu ni lazima ukubali kutii mila na desturi za Kiwiccan ili kupata jicho la ziada la kuonana nae”Aliongea na kumfanya Mzee Alfonso sura kujikunja.

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha ili uweze kuwa na uwezo wa kuonana nae , unapaswa kuwa na uwezo wa tofauti kidogo na binadamu wa kawaida , na ili kupata hio nafasi lazima upitie ibada ya kuondoa ukungu wa macho”

“She is Shadow who speaks to me through you?”Aliongea akimaanisha kwamba Frida anatumika na Kivuli kuongea nae.

“Unaamini uwepo wetu!!?”Aliuliza Frida.

“The abundunce of informations relating to the existence of so called Night Shadows has been a long-standing topic , we conducted our research to validate the truth”Aliongea akimaanisha kwamba kuna taarifa nyingi zinazozungumzia kuhusu uwepo wa Night Shadows kwa muda mrefu na walifanya utafiti kuujua ukweli”

“Na kipi mlipata kupitia utafiti wenu?”

“Tulipata ushahidi wa uwepo wa nguvu ya ziada kwa watu wote waliosema walitawaliwa na kivuli kisichokuwa cha kwao lakini utafiti wetu ulikuwa wa kiroho zaidi , jamii za wanasayansi duniani wamekataa uwepo wenu kutokana na kukosa ushahidi unaonekana”

“Basi wewe ni kiongozi wa kwanza mkubwa kuongea na sisi , muda wangu wa kutawala kivuli cha Frida umekaribia mwisho , kama tulivyoongea unapaswa kukubali kila nilichoongea kama unataka kufanikiwa na sisi kufanikiwa, ili uwepo wetu kuwa wazi tunahitaji kuwafundisha lugha yetu na matumaini yetu yapo katika tafiti ya Frida”Aliongea Frida na muda uleule mlango wa kuingilia katika chumba hiko ulifunguliwa na mtu wa kwanza kuingia ni msaidizi wa Mr Alfonso na alionekana kuwa na ahueni mara baada ya kumuona bosi wake akiwa mzima.

“Mr Alfonso upo sawa?”

“Niko sawa Pretta”Aliongea huku akimwangalia Frida usoni.

“Umeondoka?!”Aliuliza Mr Alfonso alionekana kuwa na swali lingine.

“Unamaanisha mimi au Madam?”Aliongea Frida huku akiwa na tabasamu na kumfanya mzee huyo kushngaa.

“Ulikuwa ukijua anakutumia?”

“Ndio, lakini ndani ya Israeli pekee”Aliongea Frida huku akitabasamu.

“Unamaanisha nini?”Aliongea na kumfanya Frida kumwangalia Pretta msaidizi wa Mr Alfonso.

“Pretta subiri nje kwanza , namalizia maongezi”Aliongea na Pretta alikubali na kutoka nje.

“Shadows wapo kila mahali ni viumbe wasionekana lakini wenye ufahamu , udhaifu wao mkubwa hawawezi kusafiri kuvuka bahari hata kwa vifaa , hivyo Shadows waliopo bara la Afrika hawawezi kuwa bara la Australia au Amerika lakini haimaanishi hakuna mawasiliano baina yao”Aliongea na kumfanya Mr Alfonso kushangaa.

“Kwanini wapo katika hali ya kivuli na malengo yao ya mwisho ni nini , sidhani swala la Lugha linaweza kuwa mwisho?”

“Kuhusu malengo yao ya mwisho sina uhakika , lakini nina hisia juu ya kile ambacho wanahitaji, naamini wanataka kuonekana kama sisi tunavyoonekana”Aliongea na kumfanya kukunja ndita.

“Hilo haliwezi kuwezekana”

“Kama nakumbuka vizuri ni wewe ambae ulipinga vikali juu ya imani ya kuzaliwa upya”Aliongea Frida huku akitoa tabasamu.

*******

Lawrence alionekana kuwa na wasiwasi akiwa ameketi katika eneo la kusubiri , wasiwasi wake ni kile ambacho kinaendelea ndani alikoingia bosi wake , hakujua kama Dina anaweza kuwa salama na alitamani kumpigia Hamza kumjulisha kile kinachoendelea lakini aliona akifanya hivyo angemkasirisha bosi wake , isitoshe alimwambia amuamini katika hilo.

“Madam hili eneo ni miliki ya mheshimiwa na lolote linaweza kutokea , kwasasa una maadui wengi kwanini nisiongee na Bro kwanza tumfahamishe kinachoendelea?”Aliuliza Lau dakika kadhaa kabla ya kuingiza gari katika makao makuu ya mheshimiwa mstaafu.

“Wewe ndio ulieniletea taarifa yupo bize na CEO wa Dosam lakini unataka kumsumbua , Lau najua unawasiwasi juu yangu lakini Hamza amekwisha kutusiadia vya kutosha na alisema nidili na hili mwenyewe , niamini nitalimaliza , siwezi kuruhusu juhudi za babu kupotea”Aliongea.

“Wasiwasi wangu ni huyu mzee , alikuwa ni moja ya adui mkubwa kwa bosi wetu aliepita , ni ngumu sana kumuamini”

“Hata mimi nimekuja hapa sio kwasababu namuamini , nimekuja kwasababu nina kete ya kucheza na kwa vyovyote vile hawezi fanya chochote”Aliongea na Lau kishingo upande aliingiza gari katika makazi hayo ya kifahari.

Makazi ya mstaafu Mgweno kwa barabarani unaweza kudhani ni ya kawaida , lakini ndani yake ilikuwa ni hekalu la kifalme ambalo limejengwa kwa mtindo wa kitamaduni wa nyumba za kirumi.

Lau mara baada ya kuegesha gari alipokewa na moja ya mtumishi wa nyumba hio na kupitia maelekezo Lau aliambiwa asubiri katika eneo maalumu la wageni huku Dina akipelekwa moja kwa moja katika chumba cha mikutano.

Sasa nusu saa zilikuwa zimepita bila ya Dina kutoka na jambo hilo ndio lilimfanya Lau kuzidi kuwa na wasiwasi , alitamani kuingia alipoingia bosi wake lakini walinzi walionekana wapo tayari kumfanyia chochote akifanya fujo.

Hatimae mara baada ya kujishauri kusubiri dakika kumi na tano nyingine bosi wake alitoka na kujikuta akihema kwa ahueni.

Upande wa Dina hakukuwa na ishara ya utani katika macho yake na mara baada ya kumfikia Lau alimpa ishara ya kuondoka na alitii haraka haraka na kuingia ndani ya gari.

“Tukitoka hapa fanya utaratibu wa kuaachilia huru Balozi , Debora na yule mzee”Aliongea Dina.

“Madam kwanini umefikia haya maamuzi?”

“Nimempa alichokitaka na nikapata nilichokitaka lakini mzani umelemea kwangu hivyo naweza kusema kilichonileta kimefanikiwa”Aliongea Frida huku akionyesha tabasamu hafifu na Lau alitabasamu na kisha akaliondoa gari.

“Katika kipindi hiki chote nitahitaji utulivu ndani ya mtandao wetu , hakikisha vijana wetu hawatumiki bila ruhusa yangu , dawa ya msema kweli imeshapatikana lakini kosa kidogo linaweza kuifanya ikose nguvu , umenielewa ninachomaanisha?”

“Ndio Madam”Aliongea Lau huku muda huo akiitoa gari katika makazi hayo ya mheshimiwa.

*******

Licha ya Kanali Dastani kuwa katika uchunguzi ndani ya kitengo kwa muda haikumaanisha alikuwa ametolewa katika kitengo cha MALIBU , nafasi yake ndani ya kitengo hicho ilikuwepo na alikuwa akifika kazini , isitoshe hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumthibitisha alikuwa msaliti wa taifa.

Saa saba na nusu mchana alikuwa katika ofisi yake na alionekana kuegamia kiti chake kama kawaida huku akiwaza hili na lile.

Moja ya kitu ambacho kilikuwa kikimfanya kuwaza ni juu ya Afande Mchuku na Amosi, alimuwaza Afande Mchuku kwa kuamini kitendo chake cha kuwasiliana nae kupitia simu kimemponza na kumfanya kukumbwa na umauti.

Alikuwa akimuwaza Amosi kwa kuwahi eneo la tukio sehemu ambayo ndio kifo cha Afande Mchuku kimetokea.

Swali lilikuwa ni moja tu , imekuwaje Amosi akawahi eneo la tukio kabla yake , maana kwa mahesabu ya muda aliona kabisa Amosi sio muhusika wa kifo cha Mchuku bali ni mtu mwingine ila kuna hisia zilimwambia Amosi alikuwa akijua kitu ambacho Mchuku alikuwa amebeba.

“Au Mchuku aliwasiliana na Amosi pia?”Aliwaza Kanali lakini swali hilo pia liligoma , alimjua Mchuku kwa muda mrefu isingekuwa rahisi kuwasiliana na Amosi.

“Kesho napaswa kwenda kuhudhuria mazishi Ikwiriri ninaamini nitapata pakuanzia”Aliwaza kanali , ukweli licha ya kwamba kifo cha Afande Mchuku kimetoka bado aliamini rekodi ya sauti ambayo alikuwa nayo Mchuku mpaka kuuwawa bado haijaingia katika mikono ya mtu mwingine.

Wakati akiwaza simu yake ilimtoa katika mawazo kwa kuanza kuita, baada ya kuangalia jina la anaepiga ni katibu wa mheshimiwa raisi na hapo hapo tumbo lilianza kumchemka , alikumbuka misheni ambayo mheshimiwa alimpatia kuikamilisha na akashindwa , misheni ya kumuua Hamza.

“Habari za saa hizi Mr Dastani?”Sauti upande wa pili ilisalimia mara baada tu ya Kanali kupokea simu.

“Salama katibu habari za mchana”

“Ni njema Kanali , mheshimiwa anakuhitaji ofisini saa nane kamili”Aliongea Katibu na kumfanya Kanali kuangalia saa ya ukutani na sura yake ilijikunja mara moja.

“Sawa katibu nitakuwa hapo ndani ya muda”Alijibu huku simu ikikatwa upande wa pili , alikuwa na dakika kumi na tano kutoka hapo mpaka kufika Ikulu , uzuri ni kwamba kitengo chao hakikuwa mbali sana na ilipo ikulu.

Kwa cheo chake hakuhitaji kuomba ruhusa zaidi ya kutoa taarifa hio kwa Sekretari na moja kwa moja aliingia katika gari lake na kuelekea Ikulu.

Baada ya kupitia itifaki zote za ki usalama hatimae aliweza kuongozwa na katibu moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi ya Mheshimiwa.

Katika kipindi hicho ambacho Raisi Eliasi Mbilu alikuwa akimalizia muda wake kichwa chake hakikuwa kikiwaza kuwatumikia wananchi kabisa , alikuwa akiwaza maisha yake baada ya kutoka Ikulu , sio kama kiinua mgongo kulingana na katiba hakikuwa kikimtosha , ukweli ni kwamba hata baada ya kustaafu serikali inamlipa lakini pesa hizo aliona hazikumtosha , hivyo mikataba mbalimbali ya kumnufaisha ambayo hakuikamilisha ndio ulikuwa wakati wake na kumfanya kuwa bize sana na wageni wengi waliingia na kutoka Ikulu.






“Dastani sitaki hata kuanza kuongea kilichotokea juu ya kazi niliokupatia , naelekea Nchini Malaysia masaa mawili yajayo hivyo nipo bize , kuna swala moja nataka ulifanyie kazi na nahitaji majibu ya haraka”Aliongea Mheshimiwa huku akivuka hatua ya salamu.

“Nipo tayari mheshimiwa”

“Sio tu upo tayari Dastani , kwa miezi hii miwili sijaona matokeo ya kuridhisha kutoka kwako , naweza kustaafu hata kesho lakini kumbuka nguvu yangu serikalini haiwezi kuisha mara moja, kama unataka kuendelea kupata kinga kutoka kwangu unapaswa kunifurahisha, una maadui wengi wanaosubiria nikupe mkono wa kwaheri”Aliongea na kumfanya Kanali kutingisha kichwa.

“Nadhani umezisikia habari za kifo cha mkuu wa Gereza la Silo na sababu ya kifo chake unazijua , sitaki kujua umeanza lini biashara na Afande Mchuku hayo ni makandokando yako na ni sehemu ya ubinadamu , ninachotaka ufanyie kazi ni kupata rekodi alioacha Afande Mchuku mara moja , fanya juu chini uipate, ina taarifa ambayo haipaswi kumfikia mtu yoyote ni swala la kidiplomasia, umeleewa Afande?”

“Mheshimiwa unamaanisha Afande Mchuku….”

“Unataka kuuliza kilichomkuta Afande Mchuku kinahusiana na mimi? , sidhani ni swala la kushangaza , Mchuku alikiuka miiko yake ya kazi na kilichompata kastahili, baada ya tukio Mchuku alikuwa na USB drive na tuliamini ndio yenye maongezi ya wageni waliofika kuonana na mfungwa lakini kwa hila za Mchuku kilichokuwa kwenye USB drive ni picha za nyumba yake anayojenga”Aliongea Mheshimiwa na kumfanya Kanali kushangaa lakini kutabasamu ndani kwa ndani baada ya kujua wazo lake lilikuwa sahihi Mchuku hakupoteza kitu muhimu.

“Mheshimiwa nitalifanyia kazi hili ndani ya muda mchache nitapata majibu na kukupatia taarifa?”

“Ukishapata faili haina haja ya kuja moja kwa moja kwangu wasiliana na wasaidizi wa Mgweno na ukabidhi”Aliongea na kumfanya Dastani kushangaa kidogo.

“Sawa mheshimiwa?”Aliongea

“Sikia Dastani nakupa onyo, hakikisha ukipata hio flashi hufanyi kitu kingine tofauti na kukabidhi , sitokuwa na namna yoyote ya kukulinda ukienda kinyume na maagizo yangu”Aliongea Mheshimiwa huku akimkazia Dastani macho.

“Mheshimiwa kama hutaki nikisikiliza kilichomo kwanini unanipatia hii kazi mimi?”Aliuliza na kumfanya mheshimiwa kumwangalia kwa sura iliojaa uchunguzi.

“Naitambua tabia yako Dastani ndio maana unafaa katika hii kazi , kumbuka maelekezo yangu pekee , watu wanaohitaji hii kazi kumalizika wana nguvu kuliko unavyodhani, hawapo kama sisi, wanachotaka ni kuficha kile walichoongea na mfungwa basi”Aliongea na Kanali aliishia kutingisha kichwa kukubali.

Dakika chache mbele Kanali Dastani alikuwa ndani ya gari lake , ukweli bwana huyo alianza kujifikiria na kuona kazi nyingi ambazo anafanya sio za kitengo cha MALIBU bali ni za kitengo cha TISA.

“Mheshimiwa anajua kuongea kwa lugha mbili kwa wakati mmoja , anachotaka ni kujua kilichopo katika rekodi alioacha Afande Mchuku , hii inaniambia moja kwa moja sio yeye alietoa ruhusa ya hao wazungu kuonana na mfungwa , lazima kuna mkono wa mheshimiwa Mgweno , lakini kama ni hivyo wameongea nini? , kwanini hawakuchukua tahadhari mpaka wakaruhusu Mchuku kuweza kuwarekodi, hii kesi ya huyu mwanamke ina siri gani kubwa mpaka watu kuwa makini namna hii??”

Ni maswali ambayo Kanali alikuwa akijiuliza lakini kadri ambavyo aliona anazidi kupiga hatua kuisogelea kesi hio kwa ukaribu ndio usalama wake unavyopungua.

Wakati akiwa ashatoka nje kabisa ya geti la ikulu simu yake ilianza kuita na mara baada ya kuangalia anaepiga alijikuta akitabasamu kijeuri na kuipokea.

“Kuna nini Tresha!!?”

“Uko wapi?”Sura ya Kanali ilijikunja.

“Kwanini haraka hivyo? , kuna kilichotokea?”

“Nadhani Amosi kafanya kile tulichokuwa tukijilinda nacho muda mrefu, nimeangalia Kamera za ulinzi na kumhoji Mwanaidi amekubali Amosi alikuwa ndani ya pub na vifaa vya kusikilizia sauti na Kamera..!!”Kanali mara baada ya kusikia taarifa hio alifunga breki mara moja huku kichwa kikianza kuwaka moto.

“Sikia Dastani huna haja ya kufikiria sana , nadhani ameamua kutumia nyendo zako kufanya uchunguzi wake kwa hilo nampa credit, lakini haipaswi hii kuendelea , Amosi atavuruga mipango yetu yote , hebu fikiria picha zikifika kwa Eliasi atachukua maamuzi gani?”

“Tresha unazunguka zunguka, unataka nitafanye nini?”

“Kwahili hata mimi nimechangia , lakini ukweli hauwezi kupingika haukuwa makini Dastani , tabia yako ya kumdharau Amosi itakuletea matatizo , nimempa kazi mtu kumtafuta Amosi popote pale na kumuua, hili swala lishakuwa binafsi tayari”

“Tresha hebu subiri….”Kanali alijikuta akipiga usukani wa gari mara baada ya simu kukatwa , dakika ileile alipiga tena simu kwenda kwa Tresha lakini simu ilikuwa haipatikani hewani.

“Tresha ataniingiza kwenye matatizo huyu Ma*ya kwa kukurupuka, nakiri nilikosea kumdharau Amosi lakini namjua Amosi nje ndani sio mtu wa kukurupuka na hachukulii vitu kuwa binafsi, sio mwepesi kuvujisha picha”Aliongea chini chini huku akikanyaga pedeli na kusogeza gari lake makao makuu ya kitengo huku wazo namba moja ni kumtafuta alipo Amosi kabla hajafikiwa na Tresha.

********

“Hukujumuishwa?”Aliuliza Regina huku akimwangalia Hamza kwa macho makavu.

“Mbona unauliza kimkato mkato sio tabia yako hii?”Aliongea Hamza akilalamika.

“Ninachomaanisha leo kuna mashindano ya Basketball , mbona katika taarifa ilionifikia wewe pia umejumuishwa kama mchezaji?”Aliongea Regina na sasa kumfanya Hamza kukumbuka.

Siku kadhaa nyuma anakumbuka alifuatwa na moja ya wafanyakazi aliefahamika kwa jina la Aroni wa kampuni na kumuomba kujiunga na timu yao ya kampuni kwa ajili ya mchezo wa basketball, kilichomfunga Hamza ni mara baada ya wafanyakazi hao kumuuliza kama anaujua mchezo huo na aliitikia kama anaujua na moja kwa moja wafanyakazi wale walimwambia ashiriki kama mchezaji lakini kwake Hamza alisema anaujua na sio kujua kucheza.

Ukweli katika mambo ambayo hayakuwa na umuhimu katika kichwa cha Hamza hilo lilikuwa namba moja ndio maana alisahau kabisa na hata kwenda kwenye mazoezi hakukumbuka.

“Waliniandika kama mchezaji bila ridhaa yangu, waliniuliza kama naujua mchezo wa Basketiball nikawaambia naujua nadhani wamenielewa vibaya nani asieujua mchezo wa Basketball , halafu kwani kuna umuhimu wa kushiriki?”Aliuliza Hamza huku akikuna kichwa.

“Kwako wewe inaweza isiwe na umuhimu kwasababu umejiunga na kampuni juzi , lakini huu umekuwa utaratibu wa muda mrefu wa wafanyakazi wa kampuni mbalimbali kushindana katika michezo mbalimbali ikiwemo mpita wa miguu, Marathon na Basketball, nikuambie tu leo Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine wamealikwa hivyyo wewe kama mchezaji nahitaji ushindi”Aliongea Regina.

“Lakini sijasema mimi ni mchezaji kwanini unaniamrisha nikupe ushindi?”

“Iwe jina lako limeandikwa bila ridhaa yako au kwa hiari wewe ni mchezaji na majina yashatolewa tayari , unapaswa kuelewa kampuni yetu haina wafanyakazi wa kiume wengi hivyo endesha gari kurudi kazini , mchezo unaanza mchana”Hamza alijikuta akishindwa kujua alie au acheke , licha ya kwamba ni kweli anajua mchezo huo lakini hakuwa na mpango wa kucheza kabisa na alitamani kumpigia simu Aroni msimamizi wa mchezo huo na kumwambia hakuwa tayari kuhusika.

“Regina hebu subiri kwanza , kwahio haya mashindano mshindi anazawadiwa nini au ndio mnacheza kujifurahisha?”

“Hujakubali hata kuwa mchezaji unaanza kuuliza zawadi utakayopewa , hebu tuondoke muda unaenda”Aliongea Regina huku kwa wakati mmoja akitamani kumpiga Hamza teke, alishindwa kujielewa kwanini muda wote anahisi kukerwa na Hamza lakini kwa wakati mmoja akiifurahia kampani yake, kilichokuwa kikimuuzi zaidi Regina ni maigizo ya Hamza alijua sio mtu masikini lakini muda wote anawaza pesa.






Lisaa limoja mbele Hamza na Regina waliwasili katika uwanja wa Basketi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

Sehemu hio ilikuwa imezingirwa na polisi waliokuwa wameshikilia siraha na hio yote ni kutokana na uwepo wa viongozi wa kiserikali ambao walialikwa kushuhudia mchezo huo.

Ijapokuwa ni mashindano ambayo yalihusisha wafanyakazi wa jiji lote lakini yalifanyika siku moja tu.

Mpira huo wa kikapu sheria zake sio kama za mpira wa miguu , raundi zilikuwa ni kila dakika ishirini ishitini.

Kulikuwa na timu jumla kumi na sita ambazo zinashiriki , kimsingi mashindano hayo huanza mchana mpaka usiku na ndio hufikia mwisho , ilikuwa hivyo kwasababu viongozi ambao wamealikwa hawawezi kuhudhuria kila siku kwa ajili ya mechi kadhaa , kingine wachezaji karibia wote ni wafanyakazi wa makampuni hivyo muda wao wa kucheza mechi hizo kila siku ni mdogo.

Moja ya sababu kubwa kwa mashindano hayo na kwa timu ambayo inaweza kushinda ni kujitangaza bila ya kutumia pesa kwa kupiga picha pamoja na viongozi wa kiserikali , ukweli ni kwamba tuzo ya mshindi sio kitu kinachotafutwa sana hapo.




Hamza mara baada ya kufika tu alisogelewa na Aronni ambae alionyesha furaha kumuona , Hamza alilalamika kama sio mchezaji lakini Aroni alimwambia anapaswa kushiriki kwani idadi yao ni ndogo na kutokana na macho ya Regina yalivyokuwa siriasi ilimfanya Hamza kutingisha kichwa kukubali.

Kabla ya mashindano kuanza kulikuwa na sherehe za ufunguzi na kitu ambacho Hamza aliweza kusikia ni sauti za watu asiowafahamu wakiuongea juu ya jukwaa.

Baada ya hotuba kutoka kwa viongozi na wakuu wa kampuni husika Hamza na wachezaji wengine waliokuwa wakishiriki walienda moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vya kubadilishia

Lakini kitendo cha kuingia ndani ya korido ya vyumba hivyo aliweza kukutana na sura ya mtu ambae anamfahamu.

Aliekuwa mbele yake alikuwa ni James na Chriss wote wakionekana ni mabosi kutoka timu tofauti , Chriss akiwakilisha kampuni yao na upande wa James akiwakilisha kampuni yao.

Chriss alikuwa na kundi la wachezaji nyuma yake huku James pia hivyo hivyo, licha ya timu kuwa tofauti lakini kulionekana ukaribu kati yao.

“Hamza!!”Aliita James huku akisogea kiswaga kumsogelea Hamza , mara baada ya Chriss kusikia jina la Hamza na yeye macho yake yalichanua na kusogea.

Ukweli ni kwamba Chriss hakuwa akimjua Hamza vizuri zaidi ya kumsikia tu na alitamani kuonana nae , sasa ilikuwa ni kama bahati maana alikuwa na hasira sana na bwana huyo kwa kujihusisha na Prisila.

Ki ufupi James alikuwa na hasira na Hamza kwasababu ya Rregina , huku Chriss akiwa na kisasi na Hamza kwasababu ya Prisila.

Upande wa timu ya Hamza mara baada ya kuona kundi la James walionekana kama vile walikuwa wameona maadui wakubwa.

“Na nyie mpo hapa kwenye mashindano?”Aliuliza Hamza.

“Unauliza au umejijibu , unadhani kampuni kubwa kama yetu inakosaje nafasi ya ushiriki ,sisi ndio waasisi wa mashindano haya”Alionge na kisha alimgeukia Chriss.

“Chriss huyu boya ndio Hamza ambae anatusumbua” Aliongea James huku akimwangalia Chriss.

Ukweli upande wa Chriss hakumwangalia Hamza kwa macho ya dharau alikuwa katika hali ya kumtathimini, kimwonekano hawakuwa wamezidiana sana ni kwamba Hamza alikuwa na asili ya kizungu huku Chriss akiwa na asili ya kiarabu.

Kitu pekee kinachowatofautisha ni kwamba Hamza anaonekana kuwa mkakamavu zaidi kuliko Chriss wakati huo Chriss akionekana aliestaarabika zaidi kuliko Hamza.

“Chriss mbona huongei chochote? Huyu boya ndio alietambulishwa na Prisila?”Aliongea James na kumfanya Hamza kushangaa kidogo.

“Mimi kutambulishwa na Prisila kuna tatizo gani mpaka kutaka mshikaji hapo aongee?”

“Mimi ndio mpenzi wa Prisila , naitwa Chriss Gabusha”Aliongea Chriss akiwa katika hali ya tabasamu.

Ukweli ni kwammba asubuhi mara baada ya Chriss kuamka hasira yake zidi ya Hamza ni kama ilishuka mara baada ya kuongea na Prisila.

Upande wa Prisila hakujua kama Hamza alikuwa akifahamika kwa Chriss sasa ili kulinda siri ya Regina ilibidi aseme Hamza sio mpenzi wake bali jana alimsindikiza tu kama rafiki wa rafiki yake yaani Regina.

Upande wa Hamza hakutaka mambo kuwa mengi hivyo alipokea salamu ya Chriss isitoshe hakuwa na mahusiano na Prisila hivyo hakutaka kuingilia sana maswala yake, maana Regina alimpa tahadhari kutofanya chochote ambacho kinaweza kumfanya James kuona mahusiano yao ni feki.

“Hamza na wewe upo hapa kwa ajili ya mashindano?”Aliuliza Chirss.

“Ndio na nyie vipi?”

“Unataka kujilinganisha na mimi , kwanini nishindane mwenyewe wakati wafanyakazi kama wewe wapo?”Aliongea James akiingilia maongezi.

“Upo sahihi , nadhani kutokana hata kupigana hujui mwili wako ni dhaifu hivyo ni ngumu kwako kucheza mpira wa kikapu?”Aliongea Hamza.

“Wewe mpuuzi unajikuta nani kuniita dhaifu , labda hujui ila mwaka jana kampuni yetu ndio ilishinda na tunataka na mwaka huu kushinda pia, tukikutana kama timu nitahakikisha nakuabisha mbele ya Regina”Aliongea kijeuri , alikuwa akimchukia mno Hamza kiasi kwamba alitamani kuongea kila neno baya lakini muda hakuwa nao.

Hamza na yeye alimpotezea na kwenda kubadilisha mavazi , mwanzoni hakuwa na mudi kabida ya kucheza mchezo huo lakini uwepo wa James ni kama umempa motisha.

“Bro imekuwaje ukawa na uadui na James , wale wachezaji wa kampuni yake licha ya kuwa wachezaji lakini pia ni walinzi waliopitia mafunzo maalumu na wanajua mno kucheza rafu hivyo uwe makini”Aliongea Aroni.

“Haina haja ya kuwa na wasiwasi tunaenda kushindana kurusha mpira na sio kupigana”Aliongea Hamza na kumfanya Aroni na wenzake kuwa na sura ziliozokunjamana.

Asilimia kubwa ya wachezaji wenzake Hamza hakuwa akiwajua vizuri kwasababu walikuwa wakifanyakazi nje na makao makuu .

Nusu saa mbele mechi ilianza katika viwanja vyote vinne , Hamza mara baada ya kuingia katika Court aligundua wafanyakazi baadhi kutoka makao makuu wamefika pia na walikuwa wakishangalia kwa kutaja jina lake kitendo kilichomfanya kuhisi damu kuanza kumsisimka na kuona ni mahali pake pakujichukulia pointi kwa warembo hao.

Wafanyakazi hao walikuwa ni kutoka idara ya mauzo walioambatana na Eliza na mara baada ya mrembo huyo kukutanisha macho na Hamza aliishia kutoa tabasamu huku akimpungia mkono , alikuwa na macho yaliojaa matamanio kana kwamba anajaribu kuwaambia watu kupitia hisia yule ni mpenzi wangu.

Upande wa Regina kama bosi wa kampuni alikuwa ameungana na mabosi wengine wa kampuni na walikuwa wamekaa kwenye jukwaa la VIP.

Sasa kitendo cha kumuona Hamza akipungiana mkono na Eliza na namna Eliza alivyokuwa akitabasamu uso wake na macho yake yalijawa na hali ambayo haikutafsirika.

Muda huo James akiwa na tabasamu zito alisogea na kwenda kukaa pembeni ya Regina.

“Mrembo , nadhani hutojali nikikaa pembeni yako?”Aliongea lakini upande wa Regina hakuwa na hisia zozote katika macho yake na hata hakujisumbua kumjibu.

James alijikuta akijisikia aibu kidogo kutokana na macho ya watu wengi yalikuwa yakimwangalia, alijikuta akijitafuta mwenyewe na kukaa chini na hazikupita dakika tano lazima ageuze macho kumwangalia mrembo Regina.

Hatimae kipenga kilipulizwa na mechi zote nne kwa wakati mmoja zilianza

Upande wa Hamza timu waliokuwa wakishindana nayo ilikuwa imejaa wachina na baadhi ya watanzania wachache na kwa muonekano wao walionekana ni wataalamu wa mchezo huo kwa namna miili yao ulivyojaa mazoezi.

Kwa macho yao walionekana kuwadharau wafanyakazi wa Dosam , licha ya kwamba ni kweli hata upande wa Hamza wachezaji wake walionekana kuwa na miili iliojengeka kimazoezi lakini kutokana na uzoefu wao mchezo wa kikapu sio swala la kuwa na nguvu bali ni swala la nguvu , ujuzi na muunganiko kitimu.

Lakini licha ya hivyo walishangaa kukutana na ukinzani mkubwa wa kimashambulizi kutoka kwa timu ya Hamza.

Timu ya Dosam haikuonyesha kujali sana kuonyesha mbwembwe zaidi ya kurushiana mpira mpaka eneo la pointi tatu na mtu wa mwisho kupata mpira kama mwanariadha aliruka na kwenda kuutumbukiza mpira kwenye kikapu

“Suui!!!

Mpira uliingia na kelele kama zote na hatimae Dosam kujikuta wakianza na kupata pointi mbili.

Kampuni ya Dosam ilikuwa imebarikiwa na wanawake warembo na walikuwa wakishangilia kwa shangwe na sauti tamu mara baada ya kuona timu yao imeshinda.




“Hamza tupo nyuma yako , twende kazi, tuheshimishe baba!!!”Wakina Asha na Mirium walipiga kelele na wengine wote waliunga na kuanza kulitaja jina la Hamza.

Eliza alikuwa na tabasamu kama lote , alijihisi kuwa na furaha kumuona mpenzi wake akicheza mpira wa kikapu kama hivyo.

“Pumbavu wana bahati hawa”

Wapinzani wao walijikuta wakisemezana wao kwa wao wakiwa na mshangao na hatua iliofuata waliingai katika pambano la kuzuia na kushambulia kwa wakati mmoja.

Upande wa Hamza ni kama alikuwa akitalii , ukweli ni kwamba alikuwa akitembea kurudi nyuma na kwenda mbele na hata uwezo wake wa kuzuia ulionekana mdogo.

Upande wa Aroni na wenzake mara baada ya kudaka mpira wa Rebounds palepale walimrushia Hamza na hakurembesha kwani kwa jicho lake la kichawi alisogea mpaka eneo la pointi tatu na kisha akarusha mpira na uliingia bila kugusa kigo za gori na kilichosikika ni mkwaruzano tu wa nyavu.

Mpaka dakika ishirini zinaisha Hamza alikuwa ameonyesha uwezo wa kurusha mpira kwenye kikapu wa hali ya juu mno , hakuonekana kama mchezaji wa basketbal ila alionekana kama mtaalamu wa kulenga shabaha.

Matokeo ya mwisho Dosam iliishinda kampuni ya kutengeneza rangi kwa pointi 43 kwa 25.

Jambo hilo lilifanya wanawake wa kampuni ya Dosam kumpigia kelele Hamza huku kila kilichowakalia mdomoni waliongea , ukweli ni kwamba hata Aroni na wenzake walikuwa wakimshangaa Hamza kwa uwezo wake wa kulenga kikapu na mpira.

Na wakati wa kucheza kwao kote ni kama wameona namna ya kushinda hivyo kila wakipata mpira walikuwa wakimpelekea Hamza ili kutupia.

Hakuna alietegemea kampuni ya Dosam inaweza kuvuka hata mechi ya kwanza na kwenda hatua inayofuata , maana siku zote Dosam ndio iliokuwa ikiongoza kwa kuwa wa mwisho katika mchezo huo.

“Haha.. Bro aisee umenishangaza sana , uwezo wako wa kulenga sio wa kawaida ni kama sio binadamu vile”Aliongea Aroni.

“Aroni wakati unasema huyu ni moja ya mchezaji nilijua umetupiga na kitu kizito na tunaenda kuonyesha tu tumeshiriki, Bro una heshima yangu katika mchezo wa Basktetball”

Wachezaji walianza kumsifia Hamza kutokana na uwezo wake , mpaka hapo walijiona hawakuwa na hofu tena ya kushinda mechi zinazofuatia.

Hamza alienda mpaka pembeni ya uwanja na kisha akachukua chupa ya maji na kunywa kidogo huku akijiambia anapaswa kupunguza namna anavyoshinda la sivyo watamuona sio wa kawaida , ili mradi timu ishinde basi haina haja ya kuonyesha kupatia kulenga kila dakika anayopata mpira.

Upande wa Regina alijikuta akipata ahueni na mara baada ya kusikia mabosi wenzake wanavyojadili namna Hamza alivyokuwa na uwezo wa kulenga kikapu alijikuta akijihisi furaha moyoni mwake.




“Regina timu yako inacheza vizuri , lakini usiombee ikutane na timu yetu”Aliongea James

Regina aliishia kumwangalia kwa ukauzu tu huku akishikwa na wasiwasi , hofu yake ni kwamba James anaweza akawa na kitu kibaya anapanga.

“Mr James nimesikia kampuni yenu imekuwa katika ushindani mkali na Dosam hivi karibuni, sidhani pia kama mkikutana utakuwa mchezo rahisi, ninachoona hapa kila timu inacheza kwa ajili ya kuheshimisha kampuni yake”Aliongea Mkuu wa mkoa Mheshimiwa Chamali Ngala mara baada ya kusikia maneno ya James kwenda kwa Regina

“Mheshimiwa kumbe na wewe una wasiwasi na kampuni zetu pia , niwie radhi kama maneno yangu yameonekana sio mazuri kwa mpiuzani”Aliongea James huku upande wa Regina pia akitingisha kichwa kukubaliana na Mheshimiwa.

“Zena na Dosam ni moja ya kampuni kubwa zinazolipa kodi kubwa ndani ya Tanzania , mimi kama kiongozi ni swala la kawaida kujua kinachoendelea , matumaini yangu ni kuona kampuni zote zinakuwa na kustawi vizuri kwa manufaa ya taifa zima , mashindano kama haya ni kawaida lakini hata kama kampuni ni kubwa vipi haiwezi kuwa juu ya sheria za nchi”Aliongea Mheshimiwa.

“Ni kweli kabisa mheshimiwa , tutazingatia maelekezo yako”Aliongea James huku akitabasamu kinafiki ni kama yeye ndio aliekuwa akisemwa.

Upande wa Regina hakuongea chochote zaidi ya kutoa tabasamu hafifu.

Kwa bahati nzuri Mheshiimiwa Chamali na Jopo la Mameya wa jiji hilo walikuwa wakiijua fika tabia ya Regina na washamzoea sio mtu wa kuongea neno , hivyo ni kama walijua kumvumilia.

Ilikuwa tabia ya Regina hata mara baada ya kuombwa na wagombea wa kiti cha uraisi kufadhili kampeni lakini Regina alikuwa na jibu moja tu kwamba hatofadhili upande wowote maana hakutaka kuiingiza kampuni yake na maswala ya kisiasa.


Baada ya kumpumzika kwa dakika kadhaa hatimae raundi ya pili ilianza na Hamza aliongea na wenzake na kuwaambia wakipata mpira wampasie, Hamza aliona iwe hivyo kwasababu hakuwa na mbinu nyingine ya kuonyesha zaidi ya kuujaza mpira kwenye kikapu.

Hatimae mara baada ya dakika kumalizika upande wa Hamza ulishinda tena kwa faida ya Hamza kurusha mpira kutoka mbali na kuujaza na hatimae raudi tatu zilipita na ikafikia hatua ya nusu fainali.

Na sasa ilikuwa ni zamu ya kampuni ya Zena kushindana na kampuni ya Dosam.

Aroni na wenzake alikuwa wameloa jasho lakini walikuwa na morali kubwa mno ya kushinda mechi.

Hasa pale walipokuwa wakitajwa majina yao na warembo wa kampuni yao hali ya kujiamini iliongezeka huku wakiamini wakishindwa itakuwa rahisi kuwaopoa hao warembo.

“Bro Hamza kama tukifanikiwa kushinda hii timu nina uhakika tutaweza kuwa bingwa , hii ndio timu ngumu pekee hivyo tunakutegemea”Aliongea Aroni.

“Ndio Bro tutahakikisha tunausaka mpira kwa namna yoyote na wewe ndio utakuwa kete yetu ya ushindi”

Walishauriana huku wakimuona Hamza kama shujaa wao wa mchezo ambae amewatoa katika mateso ya kuonewa kila mashindano hayo yakianza.

Hamza licha ya kwamba hakuwa amezoeana na watu wengi lakini kupitia mechi hio ni kama ameweza kupata marafiki ndani ya kampuni kwa haraka sana.

“Haina noma , nyie nipasieni mpira nitatupia”Aliongea Hamza na kisha waliwekeana mikono ya kitimu na kisha kujipanga kusubiria kipenga cha refa.



Nadhani moja ya sababu ya wachezaji wa kampuni ya Zena kushinda ni urefu wao , walikuwa wameenda hewani mno, wote walikuwa katika makadirio ya mita moja pointi tisa ki urefu, hivyo iliwapa faida ya kushambulia na kushinda kwa uharaka.

Mara baada ya mchezaji wa Dosam kupata mpira alimpasia Hamza na lijamaa lirefu la upande wa Zena lilimsogelea haraka na kumzuia kwa mbele akinyoosha mikono yake.

Lakini ajabu Hamza aliruka juu zaidi kwenda angani kiasi cha kumzidi kimo yule mwamba na kuurusha mpira kirahisi.

Kadri mechi ilivyokuwa ikiendelea ilionyesha ni namna gani urefu wao na ukubwa wa miili haukuwa na athari zote mbele ya Hamza kwani wakimzuia hivi Hamza anafanya hivi na kushinda.

Ijapokuwa hata wao walikuwa wakishinda lakini ilikuwa ni pointi mbili kwa tatu , yaani wakishinda mbili Hamza anashinda tatu.

“CEO Regina yule bwana wa pointi tatu tatu naona sio wa kawaida kabisa”Aliongea Mheshimiwa huku akipiga makofi.

Regina upande wake mdomo wake ulicheza kwa tabasamu na kujiambia asije akajitia aibu kutokana na furaha yake hivyo alijitahidi kujizuia kutoamka kushangilia.

“Yupo vizuri”Aliongea .

‘Upande wa wafanyakazi wa Dosam walikuwa na furaha , kuishinda kampuni ya Zena ilikuwa na msisimko mkubwa kuliko kushinda timu yoyote ile.

“Eliza , Hamza ameshinda tena”

“Jamani jamani na alivyo Handsome , lazima nijishobokeshe kwake , sijui atanipenda”

“Hebu acheni kujishebedua , Hamza ni wa kwetu na haendi popote..”Aliongea Mirium na Aisha wakishindana na wafanyakazi wa benki ya Dosam katika kundi hilo alikuwepo Mellisa mpenzi wake Amiri ambae alionekana kuwa tofauti kidogo na wenzake licha ya kuwa na furaha, alikuwa mrembo haswa , ilikuwa haki kwa Amiri kulilia penzi.

Upande wa Eliza alikuwa na furaha kwasababu ya uwezo wa Hamza , lakini mara baada ya kusikia kila mwanamke alikuwa akimtaka Hamza wasiwasi ulimvaa.

Alikuwa na wasiwasi kutokana na umaarufu Hamza aliojipatia ni lazima warembo wa kampuni watamshobokea.

Kutokana na Hamza kushinda mara kwa mara James wasiwasi ulimvaa mara moja na aliangaliana na Chriss ambae alikuwa amekaa upande wa nyuma akimwangalia Hamza kwa mshangao na palepale James alitoa simu na kuonekana akituma meseji na hali ya uovu ilionekana kwenye macho yake.

Baada ya awamu ya pili kuanza wachezaji wa kampuni ya Zena walikuwa na mwonekano wa kikatili na ilionekana mpango wao ni kucheza rafu na ndio kilichotokea , wakati wa kushindania Rebounds mchezaji wa kati aliruka na ghafla tu alimpiga Aroni kwenye kifua kwa kiwiko cha mkono

Kitendo cha Aroni kupiga ukulele kwa rafu ile yule mchezaji alishuka chini na kumkanyaga kwenye enka ya mguu.

“Arghhhh..!!!”

Ukulele wa Aroni ulishitua baadhi ya watu na Refa aliwahi kupuliza filimbi akionyesha kuwa ni faulu.

“Aroni vipi hali yako?”

“Refa hawachezi kushinda ila ni rafu”Aliongea Aroni akiwa na maumivu na wachezaji wenzake mara baada ya kuona hilo walianza kugombana na wachezaji wa upande wa Zena.

Lakini upande wa timu ya Zena walionyesha hali za upole wakiashiria kwamba faulu hio haikufanyika makusudi.

Kitendo kile Regina alishindwa kukivumilia na kumgeukia James akimwangalia kwa macho makali.

“James wachezaji wako wanafanya makusudi kuumiza wachezaji wetu””

Ukweli ni kwamba James alitoa maelekezo ya Hamza asiguwe maana atawadhalilisha kwa kujua mapigano hivyo alitoa maelekezo kwa wachezaji wenzake ndio waumie

“Regina hatimae umeanza kuniongelesha mwenyewe , lakini mbona unanisingizia , tukio kama lile ni la kawaida kwenye mchezo wa kikapu”

Regina alijikuta akisugua meno kwa hasira , alijitahidi kujizuia kwasababu alikuwa amezungukwa na watu wa heshima , hivyo aliachana na James na pamoja na Linda walishuka mpaka chini kwenda kumwangalia Aroni.

“Vipi hali yako , umeumia sana?”Aliuliza Regina .

Aroni mara baada ya kumuona bosi amekuja kumwangalia alijitahidi kusimama ili aongee nae lakini alijikuta akidondoka bila ya kupenda chini kutokana na maumivu makali

“Bosi Regina una mchezaji mwingine wa hakiba kwenye timu yako?”Aliuliza Refarii huyo wa kike

“Mchezaji mwingine!?”

Regina alijikuta akishindwa kuongea mara baada ya kujua hakuna mchezaji mwingine

“Refa kwani kuna ulazima wa kucheza watu watano ili kuendelea na mechi?”

“Ndio , hatuwezi kupindisha sheria ya mchezo”Aliongea Refa na kumfanya Hamza kufikiria.

“Kama ni hivyo unaonaje Aroni akiendelea kubakia uwanjani hata kwa kukaa?”Aliuliza na kufanya kila mtu kushangazwa na pendekezo lake.

“Unachomaanisha aendelee kubakia mchezoni?”











SEHEMU YA 49.

“Namaanisha tumeanza pamoja hivyo tutamaliza pamoja”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la kawaida lakini macho yake yalionyesha namna gani alikuwa siariasi.

Refa hakufikiria sana na aliishia kumuuliza Regina kama anakubaliana na wazo la Hamza na Regina upande wake aliishia kukubali na mechi ikaanza lakini kwa sura tofauti.

Wachezaji wanne upande wa Dosam huku Aroni akiwa amekaa pembeni kana kwamba anasubiria kuangalia kinachokwenda kutokea.

“Sikia nipasieni mpira mimi , hakikiisheni mnaeupka kufanyiwa rafu”Aliongea Hamza na wachezaji watatu wote walitingisha kichwa kukubaliana nae.

Upande wa wachezaji wa Zena waliamua kutumia uwezo wao wote wakiwa wengi uwanjani , isitoshe waliona ingekuwa ni aibu kama watapoteza shindano kwa timu iliopo na wachezaji pungufu.

Lakini mwishowe mara baada ya mpira kumfikia Hamza walijikuta wakitamani kuzimia , Hamza alikuwa katikati kabisa ya court na bila kusema chochote alirusha mpira mpaka kwenye kikapu na ukaingia na kuwapatia pointi tatu.

Kitendo hicho cha ushindi wa Hamza kutokea mbali uliamsha hata mashabiki wa kampuni ambazo zimekwisha kutolewa na kuanza kuishangilia kampuni ya Dosam.

“Mungu wangu , Jamani Hamza weweee..!!”

“Wewe kaka jamani..!!”

“Kama angekuwa na urefu hata sentimita kadhaa nadhani anavigezo vya kushiriki NBA”

“Haha.. umeenda mbali sana lakini ni kweli yupo vizuri”

Watu walianza kuongea wao kwa wao huku kelele zikiwa zimejaa , katika kipindi chote cha mashindano pengine siku hio ndio mchezo huo umekuwa na hisia kubwa kwa wanaoangalia.

Wachezaji wa Zena waliona ni ngumu kumzuia Hamza kutoshinda hivyo walitumia mbinu ya kumzunguka kuhakikisha hapati mpira.

Lakini sasa Hamza ni kama anawapotea kimazingara na wanapotaka kumzunguka ashapotea na kuwa sehemu nyingine na kukamata mpira na hakujali eneo alilosimama akiupata hakufanya mbwembwe na kuutupia golini huku akijikosesha mara kadhaa huku mara nyingi akipatia.

Hamza hakutaka kuonyesha vitendo ambavo sio vya kawaida , alihakikisha mbinu zake zote zinaonekana katika macho ya wanaomwangalia kwa kuhakikisha namna ambavyo anakwepa wapinzani wake.

Ndani ya muda chache ubao ulisoma hamsini na moja kwa ishirini na tatu na Hamza pekee alishinda pointi arobani, hivyo matokeo ya mchezo yalionekana wazi.

Mpira wa mwisho mara baada ya kumfikia Hamza aliamua kuonyesha ujuzi sasa alikimbia na mpira kwa kuudunda dunda mpaka pembeni ya uwanja na kisha kwa umakini mkubwa sana alirudi kati na kugonganisha katika ubao wa gori na kisha kwa uwezo wa juu ali’dunk’ na kwenda kuujanza mpira kwenye kikapu na mkono mmoj.

“Damn! anajua hata Ku’slum dunk?”

“Nilijua anachojua ni kulenga kikapu tu”

“Hii inakwenda kuwa aibu kwa upande wa itmu ya Zena kushindwa na wachezaji wanne”

Watu walikuwa wakiongea kila walichowaza huku wengine wakishangalia kwa ujuzi wa ku’dunk’ alioonyesha Hamza.

Upande wa timu ya Zena sura zilikuwa nyeusi tii , moja ya mfanyakazi wa kampuni hio alikuwa ni mchezaji mkubwa sana wa mpira huo ndani ya jiji la Dar na alishangazwa na uwezo wa Hamza.

Aroni aliishia hata kusahau maumivu yake na alijikuta akiungana na wengine kushangailia

Baada ya kuona hamasa hio ya mashabiki wapya kila mfanyakazi wa kampiuni ya Dosam alijawa na furaha.

Eliza aliishia kuruka ruka kwa furaha , alitamani kutoka alipo na kwenda kumbusu Hamza lakini kariba yake haikumuwezesha kufanya hivyo.

Regina aliishia kumwangalia Hamza na macho yaliojaa hisia , kwa jinsi Hamza alivyokuwa akijiamini na mwili wake wa mazoezi ulivyo mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi mno.

Linda ambae hajawahi kumkubali Hamza alijikuta akionyesha ishara ya kumheshimu.

Viongozi waliohudhuria walijikuta wakisimama na kuanza kupiga makofi , walikuwa pia na furaha japo wengi wao walijilazimisha kuja kutokana na mashindano hayo kukosa msisimko lakini kwa kilichotokea kiliwafurahisha.

Chriss alikuwa na wasiwasi kwenye macho yake , ukweli ni kwamba licha ya kampuni yake kushindana hakuwahi kuitilia mkazo kushinda , kilichompa wasiwasi ni kwamba licha ya Prisila kujitetea asubuhi lakini bado alikuwa na wasiwasi , aliona kuna kila dalili ya Prisila kumpenda mwanaume kama Hamza ambae ana uwezo mkubwa.

Katika macho yake hakumuona Hamza kama mwanaume mwenye pesa bali mwenye uwezo na kunasababu iliomwambia ndio maana Prisila alimchagua ku’fake’ nae kuwa boyfriend wake , isitoshe habari za Hamza kufahamiana na Yulia alizisikia pia.

James yeye alijikuta akibadilika sura kutokana na hasira , aliishia kuinamisha kichwa chake chini na taratibu alitoka kwenye jukwaa na kuelekea upande wa parking na kisha kuondoka.

Hakuaka kuendelea kukaa hapo , alikuwa amemsahau hata rafiki yake Chriss aliekuja nae.

Kutokana na uwezo wa Hamza timu nyingine ilikataa kuingia uwanjani hivyo timu ya Dosam ilipewa ushindi moja kwa moja na kuwa mabingwa.

Hakuna timu ambayo ilipenda kudharirishwa na Hamza maana ni kama alikuwa akicheza peke yake uwanjani.

Hamza alikabidhiwa cheki ya pesa kiasi cha shilingi milioni mia na mara baada ya kuona tarakimu hizo alijikuta akijawa na majuto na kujiambia kwanini hakufikiria hili kabla , pengine mara baada ya kuja bongo angejiingiza kwenye mchezo wa basketball na ingekuwa rahisi mno kwake kujipatia pesa za haraka.

Mara baada ya kupokea kitita hicho kama mchezaji bora hakuwaza kuzitumia yeye , alijua fika ni wapi anapaswa kuzipeleka . sehemu ambayo anakumbukumbu nayo wakati wa utoto wake.

Jioni mara baada ya mashindano kuisha Regina aliandaa tafrija ndogo katika hoteli ya Dosam V kwa ajili ya kuwazawadia timu yote ilioshiriki katika mashindano hayo.

Tokea aanze kufanya kazi kama kiongozi wa kampiuni hajawahi kuona morali ya wafanyakazi wake kuwa juu namna hio na aliona ni swala la kusherehekea.

Lakini hata hivyo jina la Hamza halikusahauliwa maana ndio liliipatia heshima kampuni.

*****

Upande mwingaine wakati wafanyakazi wa kampuni ya Dosam wakisherehekea ushindi kwa furaha kubwa , nyumbani kwa mzee Benjamini wingu zito lilikuwa limetanda kuzunguka nyumba yao tu.

Ndani ya jumba la kifahari la Mzee Benjamini katika eneo la sebuleni Mzee Benjamini na James walikuwa wamekaa kwenye masofa huku chupa kadhaa za whiskey zikiwa zimeenea.

Walionekana walikuwa wamekunywa mno , macho yao yalikuwa mekundu na yamevimba kama ya nguruwe.

“Kulingana na uchambuzi .. taarifa ya habari ikitoka hisa za kampuni ya Dosam zitapanda kwa asilimia tatu na hisa zetu zitazidi kuporomoka kwa asilimia mbili”Aliongea Mzee Benjamini.

“Kushuka tena , nimeweka juhudi kubwa kuzipandisha na zinakwenda kushuka tena?, F*ck him, haya yote ni kwasababu ya huyu mpuuzi Hamza , huu ndio ulikuwa mpango pekee wa kuirudisha taswira ya kampuni yetu lakini tumeshindwa tena”Aliongea James kwa hasira huku akipasua glasi ukutani.

“James usiwe na wasiwasi tulikuwa kwenye kikao kizito na mstaafu Mgweno na ajenda kubwa ilikuwa ni namna ya kumuondoa Hamza hapa Tanzania , mheshimiwa kupitia umoja wa Makomandoo ametoa agizo Master Konki kufika mara moja nchini na watalaamu wa mapigano, mawasiliano yashafanyika na muda si mrefu atafika na kumshikisha adabu”

“Baba hata kama hao watu kutoka kundi la Mwewe mweusi wakifika sidhani kama wanaweza kumjeruhi Hamza na hata kama wafanye hivyo hawawezi kubadilisha chochote ndani ya kampuni yetu ni raia wa kigeni sidhani watakuwa na ujasiri wa kumuua Hamza”Aliongea James na kumfanya Mzee Benjamini kuwa kimya , hata yeye pia alikuwa akifikiria juu ya swala hilo.

“Baba si ulisema mara ya mwisho kama hatuwezi kumpata Regina kwa njjia za kawaida tutatumia njia nyingine , huoni huu ni muda sahihi wa kutafuta maninja hatari ili kumuua Hamza na Regina”

“Kuwaua wote kutarahisisha changamoto zetu nyingi , lakini kwa maelekezo ya mstaafu huu ni mpango wa mwisho kabisa kama mbinu zote zikishindikana, isitoshe pia tuna watu wetu ndani ya familia ya Regina”Aliongea na dakika hio hio anamaliza aliweza kusikia kelele za mwanamke kutoka nje.

“Waueni , kama msipo waua sasa hivi tunaweza kuchelewa kabisa”

Baada ya kauli hio kusikika iliwafanya James na baba yake kugeuza vichwa.

Alikuwa ni Lamla mke wa mzee Wilsoni na Regina mama yake wa kambo.

“Rebe nini tatizo , kwanini umekuja ghafla ghafla?”Aliuliza mzee Benjamini.

“Madam , nini kimetokea?”Aliuliza James

Lamla ambae aliitwa Rebeka na Mzee Benjamini kama vile yupo kwake alitupa mkoba wake kwenye sofa na kisha alijimiminia kilevi kwenye glasi na kupiga mkupuo mmoja.

“Kama nisingekuja kukuelezea kinachoendelea pengine ningechelewa”

“Nini kimetokea?”

“Si yule Ajuza amekuja Dar jana kwa ajili ya matibabu na inaonekana hana muda wa kutosha kuendelea kuishi na mpango wake ni kumrithisha Regina hisa zake zote”Aliongea kwa hasira

“Nini!!?, Amekuwa kichaa , kwahio anaacha kumpaitia mtoto wake Wilsoni na kumpatia mjukuu wake?”

“Kinachokasirisha zaidi , Benjamini yule kizee hana mpango kabisa wa kumpatia mtoto wetu Frank hata hisa moja na ameenda mbali kumwambia aende eti akafanye kazi katika nafasi ya chini, yaani nimeitumikia ile familia kwa muda mrefu na bado wananidharau”Aliongea Lamla huku aking’ata meno kwa hasira lakini upande wa James alikuwa na mshituko.

“Baba.. madam , mnaongea nini, Frank ni mtoto wenu?”Aliuliza kwa hamaki na kumfanya Mzee Benjamini kunywea.

“Benjamini inamaana hujamwambia James bado?”Aliuliza na kumfanya Mzee Benjamini kumwangalia mtoto wake.

“Sikia James ukweli ni kwamba Frank ni damu yangu .. hivyo ni mdogo wako”Aliongea MzeeBenjamini na kauli ile ilimwamsha James

“Nini!!, nyie watu mekuwa vichaa ?”

“Wewe mtoto hebu kaa chini , cha kushangaza nini hapo , unadhani ningejisumbua vyote hivyo kupambania ndoa yako na Regina na kushirikiana na baba yako ili tuichukue kampuni ya Dosam, unadhani nimefanya bure, ni kwasababu mimi na baba yako tunahistoria”

James alikuwa ameshikwa na bumbuwazi bado hakuwa ameamini kinachoendelea.

“James sisi ni familia”Aliongea Lamla.

“Wilsoni ni mwanaume mpuuzi puuzi , kwa miaka yote hio ameshindwa hata kujua Frank sio mtoto wake , ni hivyo tu Mzee Dosam aliwahi kumleta Regina kipindi kile na kumfanya kuwa sehemu ya familia na mpango kuvurugika … kama sio Regina tungeweza kuichukua kampuni ya Dosam muda mrefu sana”

“Mzee Dosamu yule hakuwajhi kuwa mtu mwepesi na hata kwa mke wake ni hivyo hivyo , sina uhakika kama yule kikongwe hajui Frank sio damu ya mtoto wake , mimi nadhani anajua ndio maana yupo tayari kumpatia Regina hisa zake zote”

“Tunapaswa kuhakiksiha Frank anaendelea na mafunzo ya kivitendo ndani ya kampuni ili kuonyesha uwezo wake , ninaamini yule kikongwe anaweza kuishi kwa muda mrefu kidogo kabla ya kutoa hisa zake na Frank atakuwa na uwezo wa kuthibitisha uwezo wake”

“Unadhani atabadilika , ana hisa asilimia 32 yule na yupo tayari kumpatia Regina zote?”

“Nimeulizia idara ya sheria na nilichoambiwa wosia wa Mzee Dosam utafuatwa kama kawaida , Kama Regina ataoana na Hamza ndio atawapaitia hisa zake”Aliongea Lamla.

“Huu ni upuuzi yaani kumpa mtu hisa kwasababu kaolewa , yaani sijawahi kuona sababu kichaa kama hii”

“Hata mimi nimewaza hivyo hivyo , ninachoona yule kikongwe anachotaka kuona ni Regina kuolewa kabla ya kufa , lakini maamuzi ya kumpatia hisa Regina yashafanyika muda mrefu na anafanya maigizo tu”Aliongea Lamla kwa chuki.

“Vipi kuhusu Mzee Wilsoni, hana pingamizi lolote katika hilo?”

“Pingamizi alitoe wapi , mwenyewe bado anamuogopa mama yake na hataki kumpinga kwa kuogopa atapokonywa asilimia saba anayomiliki, yaani hana analojua kichwa maji kabisa , nachukia kipindi kile kukubali kuolewa nae”

“Lamla ni makosa yangu kipindi kile , kama sio wazazi wangu usingekuwa katika hali hii”Aliongea MzeeBenjamini huku akimpeti peti na kumfanya Lamla kulegea

“Baba unamaanisha nini , usiniambie ulilazimishwa kuoana na mama yangu?”Aliuliza James.

“Ah, sijamanaisha hivyo ni kwamba baba alichanganya mambo , ni makosa ya baba”Aliongea Benjamini huku akijitetea.

“Sitaku kuhusika kwenye maswala yako mzee , nimezdhalilishwa vya kutosha na Regina na yule mwanaharamu Hamza , ninachotaka ni wao kufa sio kingine”

“James yupo sahihi , hatuna muda wa kupoteza , ikitokea Bi Mirium kumpatia Regina hisa zake moja kwa moja hatuna cha kufanya tena , tunapaswa kuchukua hatua sasa hivi”

“Huna haja ya kuongea sana , ninajua mtu ambae anaweza kuniunganisha na muuaji mbobevu hapa Dar , awamu hii nitatumia pesa yoyote kuhakiksiha namuua Regina na Hamza”Aliongea James na kwa hasira aliondoka.

Kitendo cha James kuondoka ni kama wamepewa uhuru kwani Lamla alimbusu mdomoni Mzee Benjamini na kisha kuegamia kifua chake.

“Benja .. unadhani James hatonichukia?”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , umekuwa msaada mkubwa kwake kwa muda mrefu , nina uhakika mambo yakienda sawa ataelewa tunachokifanya sio kwa ajili ya Frank pekee”

“Upo sahihi kwa ajili ya Frank na James tumeshirikiana kwa muda mrefu kwa siri sana kukamilisha mipango yetu , hatuwezi kuruhusu tulichopanga miaka kumi na tano nyuma kupotea hivi hivi na kampuni kuchukuliwa na Regina”Aliongea Lamla na kumfanya Mzee Benjamini kugida kilevi chote kilichobakia na kisha alisimama na kumshika Lamla kiuno.

“Leo hakuna kurudi , nimekumisi kwa muda mrefu , hebu twende chumbani kwanza”Aliongea na kumfanya Lamla uso wake aliojichubua kuwa mwekundu.

“Yaani wewe , kila ukiniona unachowaza ni ngono tu , miaka yote hio ni kazi ya kukupa tu huchoki wewe mwanaume “

“Hehe , kama umechoka wewe sema , mimi naiweza shoo kuliko yule goigoi wako, au nasema uongo?”

“Tena hata usimtaje huyo mjinga , hebu twende zetu tukaliamshe”

******

Siku iliofuata katika bahari za michezo ni juu ya ushindi waliopata kampuni ya Dosam na namna ambavyo Hamza alionyesha uwezo wake.

Ilikuwa ni habari ambayo ina taswira chanya kwa kampuni hivyo hisa zake zilipanda kama ilivyotabiriwa

Wakati wa chai ya asubuhi Regina aliona habari hio na alijikuta akifurahi mno.

Baada ya kumaliza kula walipokea Delivery kutoka kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya kimataifa na mzigo huo ulikuwa ni wa Hamza.

Hamza alisaini na kisha akapoktea mzigo wake , ulikuwa ukitokea London Uingereza na ilionekana Master Alex alikuwa ashamaliza kazi yake ya kuandaa mavazi ya Hamza ya kuvaa.

“Aiii.. huyu mzee inaonekana ametumia juhudi kubwa sana kukamilisha kazi sio kwa uzito huu”Aliongea Hamza na kisha alilitupia boksi lile kwenye ngazi akiwa hana haraka ya kulipeleka juu kwake.

Regina aliishia kuangalia lile boksi na macho yake yalionekana alikuwa na shauku ya kutaka kuona nguo alizoletewa Hamza.

“Vipi Regina unataka na wewe kuona nguo zangu za ndani?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina uso kuanza kupata joto kutokana na kauli ya Hamza , maana ni kama anamwambia baada ya kuona nguo yake ya ndani siku ile basi ni zamu yake na yeye kuona zake.

“Sina shida , hebu fanya haraka tuondoke”Aliongea Regina huku akinywa juisi yote kwa mkupuo mmoja.

“Nimeheshimisha kampuni kwa kushinda , hujaniambia ni zawadi gani unanipatia?”

“Nitakupa muda wowote , haraka ya nini , kwani huna kitu kingine cha kuongea kisichohusisha hela?”

“Kama ni hivyo basi nitaongea kitu kingine kisichohusisha hela , eti Regi ni lini tunafunga ndoa kama bibi alivyosema?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina kuzidi kubadilika na uso wake wa kirembo kuwa mwekundu.

“Sifungi ndoa halafu nani anataka kufunga ndoa na wewe?”Aliuliza na kumfanya Hamza kucheka , hata hivyo alikuwa akitania tu.

Tokea bibi yake Regina ataje swala la ndoa , Regina alikuwa sensitive sana na neno ndoa , ukimtajia ni kama Simba aliekanyagwa mkia.

“Nimeuliza tu , hasira za nini sasa?”

“Ukiniuliza hilo swali la kipuuzi tena nitahakikisha sio zawadi tu ambayo utakosa bali ni mpaka mshahara wako”Aliongea kwa hasira na alitamani kumwagia Hamza maji ya uso.

Shangazi ambae alikuwa bize jikoni aliishia kusikiliza mtafaruku huo na kujikuta akitingisha kichwa chake kwa masikitiko.

Ilikuwa ni bahati tu bibi yake Regina alikuwa hospitalini bado la sivyo angecharuka kusikia makelele hayo.

Muda huo huo simu ya Regina ilianza kuita na Regina alimwangalia Hamza kwa sekunde na kisha kuipokea.

“Linda kuna nini?”

“Bosi mambo sio mazuri huku , yule mtu aliekuja mara ya mwisho anaejiita Konki amerudi tena akiwa na kundi la wathailland na wameingia mpaka floor ya pili idara ya walinzi na Gym, inaonekana wamekuja kulipa kisasi”Aliongea Linda.

“Nini!!?”

“Kapteni Yonesi anajaribu kuwazuia lakini sina uhakika kama ataweza , vipi nipigie simu polisi?”Aliuliza na kumfanya Regina kufikiria kwa muda , alijua fika mpaka wakafika katika kampuni yake kuna mkono kutoka kwenye jeshi la polisi hivyo haiwezi kuwa na maana.

“Mwambie Yonesi asifanye kitu chochote , tunakuja muda si mrefu”

“Sawa bosi”

Regina mara baada ya kukata simu hakuweza kumuona Hamza mbele yake tofauti na ngurumo ya gari na hakutarajia Hamza angekuwa mshapu kiasi hicho , alitoka haraka haraka na kuingia kwenye gari

“Tunaelekea…”

Regina kabla hata ya kuongea gari ilinguruma kama simba na kupiga msele huku ikiacha moshi kana kwamba inataka kupaa.

“Ahhhhhh.., wewe wewe unafanya nini?”

“Funga mkanda vizuri , leo barabara inaweza isiwe nzuri”Aliongea Hamza huku akikunja sura.

Regina alitaka Hamza kuendesha gari kwa haraka lakini hakutaka Hamza kuchafua hali ya hewa kwa kuendesha gari kama kichaa , lakini mara baada ya kukumbuka kinachoendelea kwenye kampuni hakutaka kumzuia.

Aliishia kufumba macho na mara baada ya Hamza kuliingiza gari barabarani kama mshale alilitoa nduki na walichukua dakika ishirini na tano mpaka kufika makao makuu , ilikuwa bahati kwao hakukuwa na msongano.

Mpaka gari linakuja kusimama ndani ya maegesho ya kampuni Regina alijihisi tumbo la kuhara lakini aliamua kujikaza na kuvuta pumzi na kisha kushuka na kuingia ndani.

“Linda hali ipoje?”Aliuliza Regina mara baada ya kupokelewa na Linda.

“Mkurugenzi wapo katika floor ya mazoezi , Yonesi anabishana nao , anang’angania kushindana nao”Aliongea Linda na mara baada ya Regina kusikia hivyo kwa haraka sana aliingia kwenye lift pamoja na Hamza na kwenda juu.

Mara baada ya kuingia katika floor hio waliweza kumuona Master Konk na kundi la wanaume nane, watano wakiwa ni weusi huku watatu wakiwa sio raia wa Tanzania na kulikuwa na wafanyakazi wengine wa kampuni ambao wamefika pia kuangalia.

“Hakikisha wafanyakazi wote waliofika hapa kuangalia wanaondoka na kuendelea na majukumu yao”Aliongea Regina akimpatia Linda maagizo na ndio muda ambao Linda anagundua wafanyakazi wengi walikuwa wamefika kuangalia kinachoendelea na kwa haraka aliwaambia waondoke wakaendelee na kazi.

“Yonesi hebu shuka kwanza hapo?”Aliongea Regina akimtaka Yonesi kutoka kwenye ulingo, hakutaka kukurupuka maana alikumbuka mara ya mwisho alimshindwa Master Konki na kama sio Hamza angeumizwa.

“Mkurugenzi wamekuja kutafuta tu matatizo hapa , kama tusipowapa sababu ya kuondoka watarudi tena”

“Wewe msichana hivi unadhani unaweza kuwazidi hawa , yaani unishindwe mimi uweze kushindana na hawa wataalamu wa sanaa ya mapigano”Aliongea Master Konki alikuwa bado na Bandeji kwenye mkono wake na alichukua nafasi ile kumtambulisha Mthalland mmoja aliekuwa mrefu wa mita kama moja na nusu hivi , ambae amevalia mvazi ya kitamaduni ya Thailland ,ni kama amevaa shuka halafu akalitengeneza suruali

“Mimi ni makamu kiongozi mkuu wa dhehebu la Black Eagle nafahamika kwa jina la Chekani , mwanafunzi wetu mzee Konk alitoa taarifa ya kukutana na mtu anaemzidi kwa kutumia msingi wa sanaa ya kimapigano wa mbinu yetu ya vidole vya Tai , hivyo kwa shauku nimesafiri na kaka zangu hawa wawili kujionea wenyewe, ni maagizo pia kutoka kwa baba yangu”

“Mzee mara ya mwisho sikuwa makini na sikutarajia kama una mafunzo yale lakini awamu hii hata tukutane sina uhakika kama utaniweza”Aliongea Yonesi huku akimsogelea yule bwana aliejitambulisha lakini bwana yule aliefahamika kwa jina la Chakeni alimwangalia Yonesi kwa dharau.

“Sina mpango wa kupigana na mwanamke , usiniambie wanaume mliopo hapa hakuna mwenye uwezo wa kupigana na mimi”Aliongea Chekani huku macho yake yakitua kwa Hamza.

“Hili sio swala la nani kuwa mwanamke au mwanaume bali ni swala la uvunjifu wa sheria , kampuni ya Dosam ni kubwa na kuingia ndani kuleta taharuki ni kuvunja sheria , serikali inatulinda pia, sijui uhusiano wa kundi lenu la mapigano na serikali ukoje lakini usije kuona hatuwezi kufanya chochote”Aliongea Regina kwa hasira na Mzee Konki macho yake aliyageuzia kwa Hamza.

“Haina haja ya kutumia sheria kutuogopesha na hatujaja hapa kuvunja sheria , sababu ya kuja ni kwa ajili ya kupambana na huyo mtoto . hili swala halina uhusiano wowote na kampuni yako”Aliongea Mzee Konki.

“Yaani mmekuja ndani ya kampuni halafu mnasema hili swala halina uhusiano wowote na kampuni?”Aliuliza Yonesi.

“Hakuna shida , kama hamtaki tukitumia eneo hili basi tunaweza kutafuta sehemu nzuri ya kupigana ,sidhani tukiondoka na Hamza hili litakuwa na uhusiano na kampuni”Aliongea Master Konki na kumfanya Regina kumwangalia Hamza.

“Una maamuzi gani?”Aliuliza , Regina hakuwa na uelewa mkubwa sana kuhusu sanaa ya mapigano hivyo alikuwa na wasiwasi Hamza anaweza kumshindwa Kachani.

Upande wa Hamza wasiwasi wake ni kuogopa walinzi wa kampuni akiwemo Yonesi watapigwa lakini mara baada ya kukuta hakuna kilichotokea alijikuta akipumua.

“Sijachukua mazoezi ndani ya muda mrefu kidogo , nadhani sio mbaya kama nikienda nao”Aliongea Hamza

“Subiri kwanza , unamaanisha nini , unadhani wanaweza kunishinda?”Aliuliza Yonesi akizuia na hakuwa na furaha baada ya Hamza kutokumuuliza chochote.

“Kapteni Yonesi hawa wapo hapa kwa ajili yangu , sidhani kuna haja ya wewe kujihusisha”

“Mimi ndio kapteni wa timu ya ulinzi , nina kila sababu ya kulinda usalama wa wafanyakazi wote , sitaki kuonekana kama sina thamani na kazi yangu siiijui”Aliongea Yonesi na kisha akamwangalia Regina.

“Mkurugenzi tafadhari naomba uniamini mimi , awamu hii siwezi kushindwa”Aliongea Yonesi kwa namna ya kubembeleza na ilimfanya Regina na Hamza kushangaa kwani hawakuamini Yonesi atakuwa siriasi mno kuhusu swala hilo, ilionekana ni dhaihiri kabisa Yonesi hakukubali kushindwa kirahisi.

“Basi haina haja ya kuondoka mtapigana hapa hapa , Hamza muachie Yonesi pambano”Aliongea Regina.

“Asante sana Mkurugenzi kwa kuniamini nakuahidi sitokuangusha”Aliongea huku akionyesha shukrani za dhati kabisa kwa Regina.

Muda huo Chekani hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia kwenye ulingo kwa ajili ya kupigana na Yonesi licha ya kuona msichana huyo hana chochote cha kumtishia”

Unadhani Yonesi atashinda au atadundwa mpaka maji ayaite mma.

ITAENDELEA WIKIEND
EPUKA AROSTO KWA KUNICHEKI WATSAPP 0687151346
 
Duu huyu Hamza huyu!! Ndugu Mtunzi huyu nae ataenda hongomen au ataishia ukerewe na gambosh kule bariadi😅😅😅
 
Back
Top Bottom