SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.
MTUNZI: SINGANOJR.
SEHEMU YA 97.
A man from the future , Adam the Obs.
Nje ya ya makao makuu ya kampuni ya Voducum jeshi la zima moto lilikuwa limekwisha kufika eneo la tukio na kuanza kuuzima moto uliosababishwa na mlipuko kwa juhudi kubwa.
Kijana mmoja ambae nguo zake zilionekana kuchanika na kuungua alionekana aktoka nje ya jengo hilo akiwa mweusi usoni , huku mkononi akiwa amembeba mwanaume ambae alionekana kuhema kwa shida.
Polisi waliokuwa ndani ya eneo hilo mara baada ya kumsogelea yule kijana mara moja walionekana kupaniki mara baada ya kugundua aliebebwa ni nani.
“Kamishina?”Wote walijikuta wakiongea kwa namna ya ahueni mara baada ya kumuona mkuu wao alikuwa amesalimika katika mlipuko huo, maana walidhani atakuwa amefariki lakini hakjuwa amefarikiz aidi ya kuumia tu.
Mra baada ya kumkabidhi Afande Maningi kwa polisi hao , Hamza alijikuta akiinua macho yake akiwa kauzu na kuangalia floor ya juu kabisa ya jengo hilo , ilikuwa kitoa moshi mzito.
“Asante sana Hamza kwa kuniokoa , lakini ni habari ya kusikitisha kwa Mzee Mohamedi kupoteza maisha”Aliongea Kamishina mara baada ya kupata ahueni.
Kutokana na kwamba Mzee Mohamedi alikuwa karibu sana na Saidi feki mlipuko ule ulimsababishia kifo palepale.
Lakini kilichomshangaza kamishina ni kwamba Hamza ndio ambae alikuwa karibu zaidi na Saidi feki , lakiini ajabu hakuwa hata na majeraha kwenye mwli wake na sio hivyo tu aliweza kumtoa nje, uwezo wa aina hio aliona sio wa kufikirika kwa akili za kawaida.
“Nilikosea sana kumchukulia poa Saidi , lazima alijua kila kitu ndio maana alijiandaa mapema pindi polisi watakapo fika ofisini kwake , yaani kila tunachofanya anajua , aliandaa mtu feki na kisha akategesha bomu kwenye mwili wake”Aliiongea Hamza huku akikuna kichwa.
“Kwahio kipi tunapaswa kufanya?”Aliuliza Kamishina huyo akijisahau kabisa yeye ni polisi na alimtegemea Hamza ambae ni raia kutoa majibu.
Upande wa Hamza hakujali sana na alionekana kufikiria kwa sekunde na palepale macho yake yalichanua mara baada ya kukummbuka kitu na alitoa smu yake mfukoni lakini aligundua ilikuwa imekwisha kuharibika , hivyo aliomba ya mtu mwingine na mara baada ya ku sync majina kutoka kwenye Email yake aliweza kuipata namba ya Prisla na kupiga.
Lakini sasa baada ya kupiga namba ile ilikuwa ni sauti ya mdada tu iliomwambia mteja anaempigia hakuwa hewani.
“Damn it , I should have thought it”Aliongea Hamza kwa kingereza huku aking’ata meno kwa kujidharau akimaanisha kwamba alipasw akufikiria hivyo mapema.
Aliishia kuchangua nywee zake za kizungu kwa kuchukia huku akijiambia alipaswa kufikiria Saidi alikuwa obssesed na Prsila na kwa namna yoyote asingemkatia tamaa.
“Mr Hamza kuna tatizo lingine tukusaidie?”Aliuliza Afande Maningi na palepale Hamza alimwambia Afande huyo amsaidie kuangalia kamera za barabarani karibu na mtaa ambao anaishi Prisila.
Kwasababu Prisila mtaa aliokuwa akiishi ulikuwa ni wa watu wazito watizo , ulinzi wake wa Kamera ulikuwa ni imara zaidi hivyo haraka haraka Kamishina aliwaagiza vijana wake kuwasliana na makao makuu.
Muda huo Hamza alimsogelea msadizi wa Saidi katika kampuni hivyo na kisha kuanza kumuuliza maswali.
“Katika kampuni ya Said ya utafiti ni projekti gani nyingne anaendelea nayo?”Aliuliza Hamnza na msaidizi yule alionekana kutetemeka kutokana na woga.
“Ni kampuni inayojihusiha na utafit wa baswala ya kibailojia , mathalani uhandisi wa kibailojia katika maswala ya mimea na wanyama”Aliongea.
“Hio taasisi ya utafiti iko wapi na inaitwaje?”
“Tasisi inaitwa S&P na ipo Tegeta Kibaoni mkabara na hospitali ya Rabynsia”Aliongea yule bwana na Hamza hakuuliza swali lingine zaidi na mara baada ya hapo alimuomba Afande Maingi aazimwe gari moja ya polisi ili aelekee katika taasisi hio
Hatua ya kwanza ambayo Hamza alitaka kufanyia kazi ni kutaka kujua kwanini ameweza kubadili muonekano wake kwa kutengeneza kopi na aliona jambo hilo limewezekana chini ya taasisi yake ya utafiti.
Hivyo aliamini akifika hapo anaweza kupata siri nyingi zaidi na ndio namna pekee ambayo anaweza kumkamata.
Kuhusu usalama wa Dina licha ya kwamba alikuwa na wasiwas lakini alijua kabisa hatomdhuru , kama angekuwa na nia hio angemuua muda mrefu tu hivyo hakuwa na haraka.
Kuna kitu kingine ambacho kilikuwa kikimfirisha ukweli ni kwamba aliona kama ni uhasama unaotokana na Prisla kutompenda basi mtu wa kwanza kuonyesha angepaswa kuwa Chriss, kuna kitu kilikuwa kikimwambia pengine kuna ktu kingine ambacho hakuwahi kukifahamu kuhusu Saidi tofauti na kutokuwa kwake kawaida.
Kutokana na kutumia gari ya polisi Hamza alifanikiwa kutosmama njiani na ndani ya dakka kadhaa aliweza kufika Tegeta katika moja ya jengo refu eneo hilo mkabala na hospitali,
Ndani ya eneo hilo kulikuwa na plisi ambao wameweka ulinzi wa kutosha na wafanyakazi wote waliokuwa ndani ya jengo hilo waliondolewa kutokaan na hofu ya kutokea mlpuko kama ilivyotokea kwenye kampuni ya Voducum na hata polisi hao walibakia nje kwa kuhofia pengne kuna mabomu ya metegwa.
Ila Hamza mara baada ya kyfia ndani ya eneo hilo hakuhofia kabisa mlipuko hivyo aliruhusiwa kuingia ndani katika jengo hilo lenye ghorofa nane kwenda juu na alijarbu kufanya ukaguzi kila floo lakini hakuwez akupata kitu chochote cha ziada kinachohusisna na kile ambacho alikuwa akifikiria kichwani.
Lakni sasa baada ya kufika floo ya choni kuna kitu kilimwngia kichwani na palepale alipiga mguu wake chini ya sakafu ya lift na kisha kuanza kupiima mlio unaosikika na palepale alijikuta akigundua lift hio mwisho wake sio floor hio , bali kuna zaidi ya floor kwenda chini ya ardhi na moja kwa moja aljua lazima kuna namna ya kuipeleka Lift kwenda chni kwa kutumia batani zilizokuwa mbele yake.
Hamza hakujali tena maswala ya Pasword kwani palepale aliiharibu na kufanya ianze kuporomoka kwenda chini na mara baada ya kusimama kwa kishindo alilazimisha mlango kufunguka na kisha alitoka nje na kukutana na kile ambacho aliwaza kwenye akili yake.
******
Upande mwingine katika moja ya Ghala sehemu ambayo hakuwa ni wapi, Prisila alijikuta akishituka kutoka usingizini.
“Naona umeamka sasa?”Aliongea Saidi ambae alikuwa amekaa juu ya meza iliokuwa ndefu kama ya kufanyia vikao na juu ya meza hio kulikuwa na vfaa vngi vya kielektoniki ambavyo vilikuwa vnafanya kazi., kulikuwa pia na baadhi ya chupa za mvinyo na pakiti za sigara.
Wakati huo ambao Saidi anaongea mkononni alikuwa ameshikilia chupa ya Moet na alionekana kugida kiasi na kisha kuweka chini na kumwangalia Prisila na monekano uliojaa uovu.
“Saidi unafanya nini hivi , mbona sikuelewi?”Aliongea Prisila kwa kulalamika huku akijaribu kufurukuta kutoka kwenye kiti alichofungwa na kamba lakini alishindwa.
“Kuna tatzo nimeshindwa kulitatua ndio maana”Aliongea Saidi.
“Tatizo gani hilo mpaka uchukue maamuzi ya kuniteka?, hivi unajua unachokifanya hapa ni kitendo cha kihalifu?”Aliongea na mrembo huyo alikuwa na hasira kiasi kwamba mpaka macho yake yalikuwa yamebadilika rangi.
“Unasema kitendo cha kihalifu , unadhani huyo Hamza unaonyesha kumpenda sio mhalifu , ni kwamba tu hujui lakini ni muuaji mkubwa”Aliongea Saidi huku akicheka.
“Kama Hamza amemuua mtu naamini sio kwa makusudi , lazima kuna sababu ya kufanya hivyo na sio kama wewe kichaa?”Aliongea huku akisaga meno kwa hasira.
‘Unajua nini wewe , kwahio unasema Hamza ni bora kuliko mimi , kwanini kila mtu anasema Hamza ni mtu mzuri , ni kwa namna Hamza naonekana kuwa bora kuliko mimi?”Aliongea kwa hasira na namna ambavyo Saidi alivyokuwa akiongea kwa ucungu ilimshgnaza Prisila na kujiuliza imekuwaje akawa na chuki kubwa kwa namna hio ilihali wamekutana mara chache tu.
“Hamza amekuzidigi vitu vingi , ni mtu mzuri kuliko wewe , kwanza ni jasiri , pili ni mkalimu tatu ni mpole na mtu mwenye shukrani , unaweza kuwa tajri kuliko yeye au kuwa na mafanko makubwa kuliko yeye lakini inajalisha nini kama hela zako unatumia kwa ajili ya maonyesho huku ukisahau kuna watu wengi wenye shida na wanahitaji msaada?”Aliongea Prisila na kumfanya Saidi kutoa kicheko cha kebehi.
“Kwaho unamaanisha kitengo cha Hamza kwenda kusaidia watoto Yatima Morogoro ndio inamfanya kuwa mtu mzuri?”Aliongea na kumfanya Oprisila kuonekana kushangaa kidogo.
“Umejuaje Hamza ametoa msaada Morogoro?”Aliuliza kwa mshangao huku akimkodolea macho kwa chuki.
“Unajua nini kinachonikasirisha kuhusu wewe Prisila , ni kitendo cha kutonitambua na ukamtambua Hamza mapema?”Aliongea.
“Unaongea nini wewe sikuelewi?”
“Utanielewa tu ndio maana upo hapa , kama mjomba wako ameshindwa kukuelewesha nitakuelewesha mimi”Alongea Saidi na kumfanya Prisila kuzd kuchanganyikiwa na kumwangalia kwa shauku.
“Prisila hata kama nimebadilika na nimebadilisha jina langu , haikuwa sababu ya kumsahau Adamu”Aliongea Saidi na kumfanya Prisila kuoneysha kuchanganykiwa zaidi kwani hakuwa akielewa anamaanisha nini.
“Adam ndio nani?”
“Kama umeshindwa kumkumbuka Hamza wa utotoni unashindwaje kumkumbuka Adamu wa utotoni?”Aliongea na kauli ile ilimfanya Prisla kushituka.
“Adamu….!!!”Aliongea Prisila huku akimwangalia Saidi kwa mshangao kana kwamba kuna kitu anakumbuka.
“Wewe ni Adamu Saidi Shekhe ?”Aliuliza Prisila na Saidi mara baada ya kusikia jina hilo alitoa tabasamu na kumwangalia Prisila kwa jeuri.
“Nadhani hatimae akili yako imeanza kufanya kazi, ndio mimi ni Adamson Saidi Shekhe , mtoto Yatima ambae alikuwa rafiki yako wa utotoni tofauti na mpuuzi Hamz aunaemuona ni rafiki yako ilihali aliishi kituoni kwa siku chache tu na kuondoka, lakini mimi rafiki yako wa zaidi ya mwaka mzima hukunikumbuka licha ya kusoma hadi Advance wote”Aliongea kwa hasira kubwa sana huku akichukua chupa ya Whiskey na kugida.
Prisila muda huo alijikuta akitoa machozi mengi , haikueleweka yalikuwa machozi ya hatia ama ya hasira , lakini alikuwa akimfahamu kweli rafiki yake wa utotoni alieitwa Adamsoni Saidi Shekhe, hakuwamini yule rafiki yake ndio huyo Saidi aliekuwa mbele yake.
“Machozi ya nini tena , umeshikwa na hatia kwa kutonitambua mapema?”Aliuliza Saidi.
‘Saidi… inakuwaje wewe uwe ndio Adam?”Aliongea Prisila kwa kusita sita.
“Unahisi siwezi kuwa Adam kwasababu ya mafanikio niliokuwa nayo sasa ili hali Adam alikuwa Yatima tu asiekuwa na wazazi si ndio unachomaanisha?”Aliuliza Saidi lakini Prisla alikuwa amekaa kimya.
Ukweli ni kwamba Prisila wakati alipokuwa akiishi kwenye kituo cha watoto Yatima baada ya kuachwa na mama yake aliemkimbia , wakati wote huo aliweza kuwa kama sehemu ya familia ya watoto hao wa kituo hicho na hata wale wageni ambao walitembelea hapo waliamini Prisila alikuwa ni mtoto Yatima , lakini haikuwa kweli ni kwasababu baba yake alikuwa nje ya nchi kikazi na hakuwa na taarifa za kutelekezwa na mama yake na alikuwa kituoini hapo kwasababu ndio nyumbani kwa Baba yake mdogo Mzee Hizza.
Sasa katika kipindi cha mwaka mmoja alichoishi kituoni hapo aliweza kuzoena sana na mvulana mdogo wa rika lake ambae aliitwa Adamsoni ,kilichomfanya kuzoeana na Adamsoni ni kutokana na kwamba alikuwa ndio moja ya watoto wapole zaidi katika kituo kizima na wenzake walimuonea mno , kutokana na Prisla kutopenda kuona mtu akionewa alikuwa akimtetea Adam mara nyingi wenzake alivyokuwa wakimchokoza na kwanzia hapo ndio ukatokea ukaribu wao.
Hata kipndi ambacho Hamza analetwa kituoni hapo na mtu ambae hakujitambulisha , Prisila na Adam walikuwa marafiki tayari , ila kutokana na Prisila kupewa jukumu la kukaa karibu na Hamza ambae alikuwa amepoteza fahamu ilimfanya wafahamiane licha ya kwamba ilikuwa ni kwa muda mchache sana.
Hamza ndio aliewahi kuondoka kituoni baada ya kuja kuchukuliwa na baadae Prisila akaja kuchukuliwa na baba yake na kumuacha Adamsoni kituoni.
Baada ya kipindi cha mwaka kama na nusu wakati Prisila alivyorudi kituoni , baba yake mdogo yaani Mzee Hizza alimpa taarfa kwamba Adamsoni aliweza kupata wazazi ambao walitaka kumuathiri na ni raia wa Canada ambao walikuwa ni wawekezaji mkoani hapo na ndio ikawa mwisho wa Prisila kulisikia jina la Adamsoni tena.
Hivyo kwa lugha nyepesi Prisila alikuwa na ukaribu zaidi na Adamsoni kuliko alivyokuwa na ukaribu na Hamza , kilichomfanya kumkumbuka Hamza kwa urahisi ni kutokana hali aliokuwa nayo alivyofika kituni na hata alivyoondoka.
Sasa baada ya miaka zaidi ya ishirini Prisila hatimae anaweza kulisikia jina la Adamsoni kwa mara nyingina , tena analisikia jina hilo kwa mtu ambae hakumtegemea ambae ni Saidi na swali palepale lilibuka ilikuwaje Adamsoni ambae iliminika alipata walezi wapya ambao ni raia wa kigeni kuwa Saidi.
“Nipe sababu ya kuamini wewe ni yeye kweli , Adam ninaemjua mimi alikuwa mtoto mpole sana”Aliopngea Prisila na kauli hio ilimfanya Saidi kucheka.
“Unakumbuka kipindi cha sherehe za mwaka mpya mwezi mmoja baada ya Hamza kufika kituoni kwetu?”Aliuliza Saidi na kumfanya Prisila kushangaa huku akionekana kukumbuka.
“Unazungumzia kile kilichotokea kati yako na Zigo?”Aliuliza.
“Haha.. kulikuwa na mtoto mwignine mwenye jina baya kama Zigo , ile siku tulitembelewa na wageni na kati ya watoto wote hawakupewa hela ila mimi yule mgeni akanipatia hela lakinni Zigo mara baada ya kuona nimepewa hela akataka kunipokonya… nilikuwa muoga kipindi kle na skutaka ugomvi hivyo nikampa Zigo hela yangu , huku nikijiona mpuuzi nisie na thamani kwa kuacha mtu kama Zigo kunionea huku watoto wote wakinicheka , lakini wewe pekee Prisila hukunicheka zaidi ya kunisaidia, kwa kujiamini ulimfokea Zigo anirudishie hela yangu…”
“Unajua nilikuonaje siku ile , niliona kama malaika ambae ameshushwa kutoka mbnguni kwa ajili ya kunisaidia , sikuwa na wazazi na sikuwafahamu lakini wewe pekee ndio uliekuwa ukinijali na kunisaidia , licha ya kipindi kile kukuzidi umri na pia kulingana na Zigo nilikutegemea msichana mdogo kama wewe kwa ajili ya kunisaidi .. nakumbuka vizuri siku ile Zigo alitaka kukupiga lakini kwa mara ya kwanza baada ya Hamza kutoka kwenye usingizi alikuja kukusaidia na kumpiga Zigo mpaka akamn’goa jino”Aliongea Saidi na kwa maneno hayo Prisila hakuwa na ubisi tena wa kuamini Saidi alikuwa ni Adamsoni maana kama angekuwa anadanganya asingekumbuka tukio hilo, japo ilikuwa utotoni lakini Prisila hakusahau matukio yote yaliomtokea wakati akiwa mtoto , sababu ya kutosahau ndio kipindi ambacho kama mtoto alihitaji zaidi kuwa na mama.
“Kama unakumbuka yote hayo , unapaswa kumshukuru Hamza kwa kukusaidia kipindi kile na sio kumchukia”Aliongea Prisila.
“Sijawahi kumpenda yule mpuuzi tokea siku ambayo aliletwa pale kituoni , kwa jinsi ulivyokuwa ukimwangalia kwa macho ya huruma sikumpenda , nilijua tu lazima utaniacha mimi na kujenga nae urafiki na nilishukuru sana alivyoondoka , sikupenda kiherehere chake , siku ile nilipanga kumshikisha Adabbu Zigo lakini akajichukulia pointi mbele yako”Alongea kwa hasira sana kiasi cha kutupa chupa ya Whiskey ukutani.
“Imekuaje ukawa Tanzania , ilihali ilijulikana wazazi waliokuasili walikuwa raia wa Canada?”Aliuliza Prisila.
“Huna haja ya kujua kwanini nilirudi ila mimi sio Adam unaemjua , yule mpole mpole”Aliongea na baada ya pale alisogelea Kontena kubwa la kampuni ya Evegreen lililowekahapo ndani na kisha alifungua mlango wake , ndani ya kontena hilo kulikuwa ni kama chumba kilichotengenezwa kwa namba ya vijikabati vidogo vidogo vya glasi za kioo kama vifriji na kulikuwa na mwanga mweupe ndani yake ulioonyesha kila kitu ndani.
Prisila mara baada ya kuangalia kilichokuwa ndani ya vijikabati hivyo vya kioo , palepale alijikuta akishikwa na kichefu chefu akitaka kutapika.
“Wewe …”
Alishindwa hata kuongea mara baada ya kugundua ndani ya vifriji hivyo kulikuwa kumejazwa viungo vya binadamu , ngozi pamoja na nywele, kila kitu kilikuwa cha wanawake wa umri mdogo.
“Prisla unaonaje hapa , kila kitu kilichopo hapa ni kutoka kwa wanawake wachanga na warembo , nikimuona mwanamke ni mchanga na mrembo namuwinda na kisha nakata baadhi ya viungo vyake vya mwili vnavyonivutia”Aliongea huku macho yake yakiwa yamejaa uwendawazimu.
“Wewe ndio yule muuaji anaetafutwa?”Aliuliza Prisila kwa mshangoa.
“Haha.. ndio , lakini haya yote ni kwa ajili yako Prisila”
“Kwa ajili yangu , ni lini nilikuambia uue mtu?”Aliuliza huku akilia.
“Sio hivyo Prisila , hujanielewa , ukiachana na watu kunifahamu kama mfanyabiashara lakini sijawahi kusomea ufanya biashara , unadhanai wale Wacanada walijiasili bila sababu?, waliona kabisa mimi ni jiniasi na kweli hawakuwa wamekosea , nilikuwa na akili nyingi na nilizigtumia vyema na kusomea uhandisi wa kibailojia
Nina uelewa mpana kuhusu Gene za binadamu na ukuaji wake wote , kwa lugha nyepesi mimi sio wa miaka hii , unaweza kuniita ‘ A man from the future’ , unachoona hapa ni mimi kukusanya specimen ili kuweza kupata seli na Genes changa kutoka kwa wanawake wazuri sana kwenye sunia hii , malego yangu ni kutumia seli zao kutengeneza mwanamke mwingine mrembo mno ambae hajawahi kutokea katika dunia hii na mtu ambae napanga kumtengeneza ni wewe Prisila , ukikubari ni ufanyie mwili wako maboresho , utakuwa mwanamke mzuri uliekamilika kila idara dunia nzima na hakuna ataeweza kukufikia kwa uzuri, Prisla unakwenda kuwa Malaika”
“Prisila sikutaka kujitambulisha kwako kwa muda mrefu kwasababu nilikuwa nikikuandalia hii zawadi , hii ni surprise kwako , ni namna ya mimi kuonyesha ni kwa kias gani nakupenda”Aliongea Saidi huku akicheka kwa furaha na palepale alisogelea kiboksi kidogo kabisa na alikibeba na kumsogelea nacho Prisila.
“Prisila angalia huu mdogo ni wa Salma , sijaukata kwasababu nataka kutumia seli zake , ila alikuwa akiongea sana huku akisema humzidi kwa urembo ndio maana nikaukata mmi , Salma nilimchukia sana ila kwangu wewe Prisila ni malaika na mrembo zaidi”Aliongea huku akicheka kwa nguvu.
Kwa jinsi alivyokuwa Prisila fahamuz ake zilimwambia kwa asilimia mia moja aliekuwa mbele yake sio Saidi , pengine kuna roho imemvaa na licha ya kushikwa na kichefu chefu kikali aliishia kutoa machozi kama mfereji pekee huku akifumba macho.
“Wewe sio binadamu , hapana wewe sio Adam ninaemjua mimi , wewe ni chizi na mwendazmu , unamauuajie mwanamke kwasbabu ya kukupenda?”Aliongea Prisila huku akitoa kilio cha kwiki , hakuamini kwenye maisha yake anaaweza kukutaana na kitu kama hicho.
“Prisila unalia nini sasa , Salma sio mtu wa kumlilia na kupoteza machozi yako , ninakupenda na wanawake wote ndani ya dunia hi ni takataka”Aliongea huku akitema mate chini kudharau wanawake wote na muda uleule alibadiilika na kisha alipiga magoti mbele ya Prisila huku muonakneo wake ukibadlina na kuwa wa kubembeleza.
“Prisila hujui tu kilichonitokea.. ni kweli nililelewa na kafahamika nilikuwa Canada lakini ukweli wale walezi wangu hawakuwa watu wa Canada , walikuwa ni wa Marekani na hawakunichukua kwenda kunilea bali walinichukua ili nikawe mbwa wao , walinipiga mno hadi kunigunga kamba shingoni kama mbwa,, walikuwa wakikosana wao kwa wao wanakuja kutolea hasira kwangu .. nniliishi kwa mateso makubwa sana na nilikuwa na hofu ya kila siku , kitu pekee kilichoniweka hai ni kukumbuka wewe wewe Prisila malaika wangu na muda mwingine niliamini utajitokeza na kuja kuniokoa , hiv unajua ni kiasi gani nilikungojea , lakini hawakujua mmi nina akili nyingi , nilichokifanya ni kuwaibia hela zao kariba zote na kisha nikawawekea sumu, ilikuwa mbinu mujalabu kabisa na hakuna hata alieweza kujua walikufa kwa sumu niliowaekewa mmi , baada ya kuona wamekufa niliondoka kimya kmya na kurudi Tanzania , lakini hata nilivyokuja kwenye shule uliokuwa ukisomea hukuweza kunitambua tena , niliumia lakini sikutaaka kujitambulisha kwako , hivyo nilijibidiisha kwenye masomo na mara abaada ya wote kumaliza nikaenda Canada kuendelea na msomo huku nikiamini nikpata kitu cha kujifunia mbele yako ndio siku nitakaayojiitambulisha kwako na kisha kukuoa , motisha iliokuwa ndani ya moyo wangu ilifanya kazi nnilisoma kwa bidi na nlitumia kiasi cha hela nilichowabia walez wangu na kuwekeza hela nyingi na hatimae kurudi nchini nkiwa tajiri , lengo lilikuwa moja tu kukuoa wewe malaika wangu wa moyo”Alliongea huku akimshika Prisila sura yake.
Prisila aliishia kuishia kuwa kimya tu huku uso wake ukiwa umefubaa , hakuamini Saidi alikuwa ni Adam na hakuamini mwanafunzi alieibbuka kinara katika masomo ya kidato cha tano na sita Tanzania nzima alikuwa ni huyu kichaa wa sasa hivi , kila kitu kilikuwa tofauti.
“Prisila unaonya nilioyafanya haya yote kwa ajili yako tu ili uelewa ninachojiskia moyoni , Hamza ni takata yule na hana vigezo vya kuwa na wewe”Aliongea.
“Unafanya nini?”Aliuliza Prisila maana wakati huo wakati akongea alikuwa amepeleka mkono wake hadi kwenye shingo , na kumfanya Prisila kupaniki asijue Saidi anataka kufanya nini.
“Kama nilivyosema , nataka kukufanya uwe malaika wa ndoto zangu”Aliongea huku akimeza mate meng.
“Naomba uache Said unachotaka kufanya , stop please”Aliongea Prisla huku machozi mengi yakimtoka , hakuwa tayari kufanyiwa kitendo cha namna hio, lakini dakika ile sauti ya kubim kama alamu iliskka nyuma ya Saidi na kumfanya aache na kisha kusimama kwenda kuangalia nini kimetokea na mara baada ya kuangalia klichokuwa kikionekana kwenye tarakishi ya mapakato alijikuta akitoa tabasamu la furaha.
“Haha.. huyu mpuuzi wako Hamza naweza kusema ni mtu mwenye bahati sana , naona ameweza kuifuata Zawadi niliomwandalia”Aliongea ka furaha.
“Unasemaje?, unataka kumfanyia nini Hamza?”Aliongea Prisila huku akifurukuta na Saidi alichukua ile tarakishi na kisha akamgeuzia Prsila ili aweze kuona kinachoendelea
Hapo sasa ndio aliweza kuonekana Hamza akiwa ndani ya maabara ambayo imefunikwa na mwangaa mweupe na wa rangi ya kijivu kwa mbaali , Hamza alionekana kulanda landa ndani ya vifaa hivyo vya kisasa katika hio maabara akionakan akuna kaitu mbacho anatafuta
Hamza aliweza kufungua mafrji ambayo yaimfanya kukunja sura mara baada ya kuona kumejazwa ngozi za sura za watu , viungo vya kila aina vya wanaume na wanawake.
Wakati akiwa ndani ya maabara hio sauti iliweza kusikika katika spika.
“Hamza unaonaje , nashangaza eneo kama hilo kuwa hapa nchini sio?”Aliongea Saidi au Adam
Hamza mar abaada ya kusikia kauli ile palepale aligeuza macho yake na kuangalia Kamera zilizokuwa zikimmulika.
“Kwahio hiki ndio ulichokuwa ukifanyia utafti , kwahio umefanikiwa kuendeleza kivitendo nadharia ya 3D ya kuprint geni za kibailojia?”Aliuliza Hamza.
“Eti 3D haha .. hilo ni jina la kizamani lakini nadhani linafiti , lakini kwa bahati mbaya sio kama unavyofkiria na hataa nikikuambia huwezi kunielewa , kitu pekee ninachoweza kukuambia ni jina langu , Naitwa Adam a. k. a Adam the Obs, the new creator of this world, my wisdom is not something a normal person like you can imagine”
SEHEMU YA 98.
Hamza hata yeye hakuweza kuelewa imekuwaje mtu wa kawaida kama Saidi kufanikisha kutengeneza sura feki , hakuelewa kwasababu hakuwa na ujuzi wowote katika swala zima la teknolojia za kihandisi za mwili wa binadamu.
Hamza alijiambia mtu ambaea angeweza kujua ambacho amefanikisha Saidi pengine ni Dokta Genesha peke yake lakini kwa bahati mbaya alikuwa amekwisha kufariki.
“Umemfanya nini Prisila , umemwachia huru?”Aliuliza Hamza akipotezea viungo vya miili ya watu vilivyokuwa ndani ya maabara hio.
“Haha.. kwanini nimwachie , huyu ni malaika wangu , mke wangu mtarajiwa na wewe unakwenda kufa leo”Aliongea na muda huo kupitia speaker za maabara hio aliweza kusikia kicheko cha uovu kutoka kwa Saidi , lakini ni muda huo huo alipoweza kusikia sauti ya Prisila.
“Hamza nipo nae hapa kwenye ghala ..”Haikueleweka alitaka kuendelea kuongea nini lakini sauti yake ilikatishwa mara moja.
Hamza sasa alijua Saidi alikuwa amemteka Prisila na kumpeleka kwenye Ghala ila hakujua ni ghala lipi maana jiji la Dar lilikuwa na maghala mengi , hivyo alitoa simu yake ili kumtafuta Afande Maningi ili aanze utaratibu wa kutafuta ni uelekeo upi walipo.
Lakini sasa muda ambao alikuwa akisubiria simu ipokelewe alichoweza kusikia ni milipuko iliokuwa ikitokea kwa kumzunguka na zilichukuwa sekunde chache tu kilichosikika ni:
“BOOOM!!
Alikuwa amekwisha kuchelewa, sekunde ambayo alijua maabara hio ilikuwa imetengenezwa na uwezo wa kujilipua yenyewe pale mmiliki akitaka kufanya hivyo ilikuwa tayari imelipuka.
Alichoweza kuhisi ni wimbi kubwa la moto likimfunika kuanzia juu mpaka chni na kufanya asionekane kabisa.
BOOOM!
Upande wa nje na kwenyewe polisi waliokuwa wakilinda jengo hilo baadhi yao hata hawakupewa nafasi ya kusikia mlio kwani walipoteza maisha mara moja mara baada ya jengo lote kulipuka na kuwadondokea
Ulikuwa ni mlipuko mkubwa ambao pengine umewasababishia wagonjwa wa moyo waliokuwa karibu katika hospitali kupatwa na hali za dharula.
Ardhi yote kuzunguka eneo hilo ilitetemeka huku wafanyabiashara wa migahawa wakipga mayowe ya mshituko huku wale majasiri wakiangalia wasiamini kile kinachotokea.
Jengo lote lilidondoka na kilichoweza kuonekana ni kifusi kikubwa ambacho kimefunika eneo hilo huku Hamza akiwa chini ya vyumba vya ardhi.
******
“Nooooo!!!!”
Ulikuwa ni ukulele wa aina yake alioweza kutoa mrembo Prisila akiwa si mwenye kuamini kile kilichomtokea Hamza , alichoweza kujisikia muda huo ni kama ghafla tu akili yake imevamiwa na ugonjwa wa ukichaa , ndio dakika ambayo mrembo huyo alijua ni kwa jinsi gani Hamza hakuwa Hamza tu kwake bali alikuwa zaidi ya jina lenyewe.
Macho yalifunikwa na machozi huku akiendelea kulia kwa kwikwi
“Haahaha…”
Adam kama Said alivyojipambanua alicheka kama kichaa huku akiruka ruka juu na kukamatia chupa cya vodka na kunywa mfululizo.
“Wewe ni nani mpaka unipokonye mwanamke ninae mpenda , hahaha.. kufa mwanaharamu wewe, shenzi kabisa hahaa..”Aliongea kwa furaha kubwa.
Pengine Prisila angehuzunnika tu kwasababu hakuwa na mahusiano yoyote na Hamza lakini wakati huo hakuweza hata kuelewa kinachoendelea katika mwili wake , alianza kujihisi kama vile mwili wake umevamiwa ghafla na watu ambao wameanza kumchoma visindano vidondo vidogo kwenye mwili wake na kutemtengenezea maumivu makali.
“Saidi wewe ni mnayana na unakwenda kufa kifo cha kinyama…”Aliongea kwa nguvu
“Vyovyote vile unavyotaka kusema , knachokusumbua wewe ni hali ya kuchanganyikiwa tu kutokana na huyu Hamza lakini ukishaamka kutoka kwenye ndoto utajua hakustahili kabisa machozi yako”
Mara baada ya kuongea kauli ile alivua tisheti yake na kuacha mwili wake wazi na kutunisha misuli ambayo ilimkubali na kuvimba kisawa sawa na palepale alimsogelea Prisila kisha akamshika kidevu na kumwangalia na macho ambayo yamejaa tamaa za kingono.
“Malaika wangu hatimae nimekupata..ijapokuwa huu mchakato ni tofauti na nilivyopanga mwanzoni lakini hata hivyo matokeo ni yaleyale tu”
Mara baada ya kuongea hivyo aliinama na kutaka kumbusu kwenye lipsi zake lakini kilichomtokea ni kutemewa mate ya uso.
“Mimi sio malaika wako na ole wako uniguse uone , nitageuka kuwa kiumbe wa ajabu na nitamlipizia Hamza”Aliongea kwa kuonya.
Saidi aliishia kutumia vidole vyake na taratibu sana alifuta yale mate katika uso wake na kisha akayalamba yote.
“Bado tu unaendelea kumkumbuka mtu ambae nina uhakika hata nafsi yake haijapona , huwezi kuja kumuona hata ugeuke mzimu, huwa najiuliza amekupatia nini mpaka ghafla tu ukabadlika kwa ajili yake na kuwa kama mtumwa?”Aliongea Saidi na swali lile lilimfanya hata Prisila mwenyewe kujiuliza Hamza kampa nini maana hata hajawahi kumtakia anampenda zaidi ya kujua alikuwa mume wa bosi na rafiki yake Regina.
“Huwezi kuelewa hisia za bnadamu zilivyo kwasabbau wewe sio binadamu , wewe ni mtu ambae umeamua kuupoteza utu wako kwa ajili ya kuukwepa uhalisia”
“Unajua nini wewe , hebu kaa kimya”Aliongea na pale pale alishindwa kujizuia na kumpiga kibao Prisila.
Kilikwa kibao kikubwa mno na kama sio kiti hicho kutengenezwa kwa chuma pengine angedondoka nacho, ukubwa wa nguvu ya kibao kile ilimfanya aanze kutokwa na damu puani.
Saidi mara baada ya kuona hilo aliona alizidsha kumpiga na kumfanya apatwe na wasiwasi na harahara alimpatia kitambaa na kutaka kufuta zle damu.
“Prisila naomba unisamehe , sikumaanisha kuku…”
Prisila hakutaka kuguswa tena na Saidi na alitingisha kichwa chake kwa nguvu zote kukataa.
“Niondokee mbele yangu , usije kunigusa”Aliongea na kumfanya Saidi kutupa kile kitambaa pembeni huku kama kichaa akianza kujikuna kichwa chake na shingo huku akitembea kwenda mbele na kurudi nyuma.
“Kwanini hakuna mtu hata mmoja anaetokea kunielewa , mimi sio kichaa, mimi ni mshindi kwa kuua kila mtu ambae anaenda kinyume na mimi , mimi nina busara kuliko mtu yoyote, walitonitelekeza , walionidharau , walioninyanyasa na waliojiona wana uwezo na kutaka kushindana na mimi wote wanapaswa kufa… nasema nitawapeleka kuzimu”
Aliongea kwa sauti kubwa huku macho yake yakitoka yale yanayoashiria uhai na kubadlika na kuwa yale ya ushetani, akili yake ilikuwa imempotea na hakuwa tena Said , hakuwa tena Adam mtoto mpole.
“Prisila ukiwa wangu nitakuonyesha ni kwa namna ganai mimi nina nguvu , sasa hivi umechanganyikiwa tu baada ya kujua Hamza alikuwa ni yule mpuuzi aliekuwa akitia huruma akiwa mdogo , naamini ukinijua vizuri utajua pia kuisoma akili yangu”
Mara baada ya kuongea kauli hio alimsogelea Prisila na kuacha kujali kila kitu , kitendo kile kilimfanya mwanamke huyo kupiga makelele ya kupaniki na kuanza kufurukuta lakini kwa bahati mbaya hakukuwa na uwezo wa kujiachia huru.
Palepale ni kama picha zilianza kujitengeneza katika kichwa chake ,alianza kuona picha ya Hamza akimezwa na wimbi la moto , alianza kuona wasichana wakikatwa viungo vya mwili na kuchunwa ngozi , kila alichoweza kufikiria kilimfanya kuzidi kutishika na kile ambacho Saidi anakwenda kumfanyia.
Dakika ileile ni kama moyo wake umepigwa kiberiti cha moto , tokea akiwa mdogo hakuwahi kuhisi kiwango cha juu cha hasira namna hio.
Ni muda ule sasa alianza kusikia sauti ikibisha hodi kwenye akili yake , sauti ile ilikuwa ni kama vile inamfokea kwa kukubali kufungwa kwenye kiti na mtu kichaa kama huyo, sauti ile ilimpigia makelele kuchukua hatua ya kujiokoa.
Kitendo cha Sadi kupeleke mkono wake kutaka kumgusa Prisila alijikuta akishituka kama mtu ambae ameshika chuma cha moto na kurudisha mkono wake nyuma huku macho yakiwa yamemtoka.
Prisila akili yake ilianza kupoteza uwezo wa kudhibiti mwili wake licha ya kwamba aliweza kuhisi kila kitu kilichokuwa kikiendelea , alihisi ni kama mwili wake unaingiziwa damu ambayo imechemshwa kwa moto mkali, dakika ile eneo lote lilifunikwa na hali ya joto kali mno.
Saidi alijikuta akishikwa na mshituko mkubwa asipate kuelewa nini kinatokea , alijikuta akikaa mbali na Prisila huku akiwa ameshikilia kidole chake ambacho ni kama kimeungua na moto wa volcano.
“Nini kinaendelea”Alijikuta akibweka kwa mshangao huku akianza kumhofia Prisila.
Kilichomfanya azidi kuogopa ni pale alipoona macho ya Prisila yakibadilika kabisa na kutoa miale mikali ya jua huku mwili wake wote ukianza kumeta kwa mwanga mkali wa kuunguza.
*******
Upande mwingine wa dunia haikueleweka ni wapi mara moja , lakini alionekana mwanaume mweusi ndani ya jengo moja ambalo ilikuwa ngumu kuelezea lilikuwa ni kanisa , Sinagogi , Tempo au Sinagogi, hiyo yote ni kutokana na namna lilivyojengwa, hakukuwa na benchi hata moja ndani ya jengo hilo wala hakukuwa na zuria, chini kwenye sakafu kulikuwa na michoro ya nyayo za miguu za rangi nyeupe ziliozopangiliwa kwa mstari karibia eneo lote.
Michoro ile ilikuwa ni kama ikielekeza mtu aneingia ndani ya jumba hilo anapaswa kusimama kwa kujilandanisha na nyayo hizo.
Eneo hilo lilikuwa na mwanga hafifu na alionekana yule mwanaume akiingia huku akiwa kifua wazi na amejifunga kaniki ya rangi nyeusi.
Bwana yule licha ya kwamba alikuwa hajavaa kitu chini miguuni lakini hatua zake zilikuwa zikisikika waziwazi kama mwangwi kwa namna zilivyokuwa zikijirudia rudia.
Alitembea taratibu mpaka akafika eneo la mbele kabisa la eneo hilo na akasimama kwa kujilandanisha na mchoro wa nyayo na palepale ule mwangi wa hatua ulipotea.
“Profesa umegundua nini?”Sauti ya mwangi ilisikika.
“Uzito wa hatua zangu umeongezeka”
“Hahah.. ndio, maana yake cheo chako kimepanda pia kulingana na kishindo cha hatua zako”
“Naweza kujua ni mchango gani nimeweza kufanya na kujiongezea kishindo cha hatua zangu?”
“Nakwambia safi sana profesa , hatimae amefanikiwa kwa mara ya kwanza”Sauti ile iliendelea kujirudia rudia.
“Unamaanisha nini madam?”Aliongea mwanaume yule mweusi alieitwa Profesa.
“Namaanisha binti yako Prisila amefanikiwa kwa mara ya kwanza, ameweza kuamsha nguvu zake za kichawi hahaha..”
Naam mwanaume yule aliekuwa amevaa kaniki alikuwa ni Profesa Singano na haikuweleweka alikuwa eneo gani, lakini kauli alioweza kusikia ilimfanya kuonyesha hali ya kuchanganyikiwa.
******
Sauti 1: “Kwanini ulichukua maamuzi ya kumuua wakati ulipewa kazi ya kumkamata?”
Sauti 2: “Nani nimemuua”
Sauti 1: “Hujui uliemuua , unafanya nini hapa kama hujui uliemuua?, Ongea ukweli wote wazi ndio namna pekee ya kukusaidia”
Sauti 2: “Nimeua watu wengi, unamaanisha nani nimemuua?”
Sauti 1: “Mwandishi wa habari Sedekia”
Sauti 2: “Sijamuua mwandishi yoyote aneitwa Sedekia, kwanini unanisingizia kesi?”
Sauti 1: “Nani aliekutuma?”
Sauti 2: Kunituma kufanya nini , hakuna alienituma”
Sauti 1: “Ulimuua ila hakuna aliekutuma?”
Sauti 2: “Sijamuua mtu”
Sauti 1: “Umemuua ila hujui aliekutuma?”
Sauti 2: Sijatumwa na sijamuua mtu”
Sauti 1: Ndio hujatumwa?”
Sauti 2: Ndio”
Sauti 1: “Ndio umemuua ila hujatumwa”
Sauti 2: “Nimesema sijamuua mtu”
Sauti 1: “Mwili wa Sedekia uliutupa wapi , sema ukweli wako?”
…………..
“Mbona sielewi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Amosi mara baada ya kumaliza kusikiliza kile ambacho Dina aliwapatia.
“Usisikilize kuelewa?”Aliongea Dastani.
“Kwanini nisisikilize kuelewa?”
“Sikiliza maana ya matamshi , haya ni mahojiano hizi sauti mbili zote ni za Watanzania”Aliongea Kanali huku akijishika kidevu.
“Ndio maana nimesema sielewi , hio sauti ni ya polisi wa Kitanzania hio bila shaka na mtuhumiwa , lakini kwanini anamhoji hivi , si huyu mfungwa tunaemfuatilia ndio alimpoteza Sedekia au kuna kingine?”Aliuliza na kumfanya Dastani kufikiria kidogo.
“Sedekia alikufa ama amepotea?”Aliuliza na swali lile lilimpa uelewa flani Amosi.
“Ulisema alitoweka”
“Kutoweka ndio kupotea wewe , kama alitoweka inamaanisha hakuna ushahidi kama alikufa , kwanini tunaamini Mad dog alifungwa kutokana na kutoweka kwa Sedekia?”
“Alifungwa kwasababu iliaminika alikufa , lazima kwa namna yoyote alikiri”Aliongea Amosi.
“Na huyu anaehojiwa hapa ni nani?”Aliuliza na swali hilo lilimfanya amwangalie kanali.
“Kanali wewe ndio umesema nisikilize kuelewa , nimechanganyikiwa na hii sauti na sioni kama ina chochote cha maana”Aliongea na palepale Kanali alionekana macho yake kuchanua.
“Sedekia hajafa?”Aliongea.
“Unamaanisha nini?”Aliuliza Amosi kwa mhangao.
“Sikiliza tena kisha niambie unasikia nini , usielewe maneno elewa sauti”Aliongea na kumfanya Amosi kuchanganyikiwa na alianza kusikiliza upya.
“Amosi ulikuwa na ukaribu na Sedekia lazima uelewe ninachomaanisha”Aliongea na kauli yake ilimfanya Amosi kuingiwa na shauku na kuanza kusikiliza sauti zile kwa umakini.
“Hii saut…!!!”Amosi macho yalimtoka.
“Ndio hio sauti ni kama ya Sedekia , sio ya mtuhumiwa”Aliongea Dastani huku akionyesha hali ya kuwa na furaha kuona Amosi kagundua kitu ambacho amekigundua.
“Sema bado ni muda mrefu , nahisi kama ni yake ila sio ya kwake kwa wakati mmoja, nadhani tunaweza kuithibitisha kwa kusikiliza sauti yake upya au mtu aliekuwa karibu yake zaidi , mke wake au mama yake”Aliongea Amosi.
“Unataka tukamsikilizishe hii Madam?”
“Ndio mtu wa karibu anaeweza kututhibitishia hili , hatuwezi kuamini moja kwa moja kama hii ni sauti ya Sedeka na hajafa?”
“Hapana Amosi, hiki sio kitu ambacho Dina alipaswa kutupatia, namaanisha huu sio Mzigo ambao Mchuku alitaka tuuchukue kwake , unahisi kuna maana gani imejificha kwa Dina kutupatia kitu kama hiki na kuacha kutupatia mzigo halisi”
“Siwezi kujua kuhusu hilo?”
“Hilo ndio swali la kujiuliza kwanza kabla ya kuchukua hatua zote, kama hili ni kweli basi kuna swali kubwa litajitokeza hapa , kwanini Mad Dog yupo gerezani ilihali hii sauti ya anaehojiwa ni Sedekia mwenyewe , inamaana alihojiwa akiwa ameandikiwa
script au vipi huku akirekodiwa, kama ni hivyo ni kwasababu gani?, na kama yote haya ni kweli basi inatupa jibu rekodi ya Mchuku ina uzito mkubwa kuliko sisi kujua Sedekia yupo hai”Aliongea Dastani na alikuwa ni kama anajifkiria yeye mwenyewe.
“Kwahio tunafanyanye baada ya hapa?
“Hakuna namna , kabla ya kwenda kuonana na madam kwanza tunapaswa kujua alichoacha Mchuku ni kitu gani na baada ya hapo tutaweza kuchukua hatua nyingne tukiwa na majibu yote , hivyo tunapaswa kumpa Dina kila alichohitaji”
“Lakini masharti ya Dina ni magumu kutekelezeka Dastani?”
“Najua , lakini hi kesi usiichukulie ya kawaida , hii ni mwanzo wa kujua mambo mengi yaliojificha , kuna mtu atatusaidia katika hili lazima , wewe niachie mimi”Aliongea na kisha alitoa tabasamu akionekana kuna kitu amekumbuka.
ITAENDELEA.
CONTACTS: 0687151346 WATSAPP ONLY