Apo sawa kaka! Umenena vyemaHapa shida ilipotokea sio coins wala
Kuna kipindi simulizi ilikua bure tulisoma
Ikapelekwa Grupuni kwa wasio na subira ya muendelezo ili waende na kasi yao,Lakini wa bure waliendelea kuburudika hvo hvo pia...mpk leo imehamia fasihinet. Watu wa bure bado walifunguliwa vipande ss ghafla kawatenga watu wa bure kabaki na wale wasio na subira unategemea ukiwacheleweshea na mtu kashalipia atakuelewa??
Wabure mtawasema hawana mchango kwa mwandishi lakini hujui wao ndo mabalozi wazuri kuitangaza simulizi kwa watu wapya
Kwaiyo Singano nakushauri tu endelea na ile ratiba ya kufungua vipande kazaa kwa ajili yao kila week.
Ni kama Kila mtu anapenda mpira lkn sio kila mtu anapenda kubet.
umeeleweka mkuu .... simulizi inaendela hapaHapa shida ilipotokea sio coins wala
Kuna kipindi simulizi ilikua bure tulisoma
Ikapelekwa Grupuni kwa wasio na subira ya muendelezo ili waende na kasi yao,Lakini wa bure waliendelea kuburudika hvo hvo pia...mpk leo imehamia fasihinet. Watu wa bure bado walifunguliwa vipande ss ghafla kawatenga watu wa bure kabaki na wale wasio na subira unategemea ukiwacheleweshea na mtu kashalipia atakuelewa??
Wabure mtawasema hawana mchango kwa mwandishi lakini hujui wao ndo mabalozi wazuri kuitangaza simulizi kwa watu wapya
Kwaiyo Singano nakushauri tu endelea na ile ratiba ya kufungua vipande kazaa kwa ajili yao kila week.
Ni kama Kila mtu anapenda mpira lkn sio kila mtu anapenda kubet.
Hapa shida ilipotokea sio coins wala

AsanteJamii ya muungano wa siri.
SEHEMU YA 220.
Skellidoni mara baada ya kumuona Hamza akimsogelea hofu ilimwingia na kujikuta akirudi nyuma.
“Lucifer wewe kweli ni Gwiji wa kizazi kipya, lakini bado huwezi kunishinda”
“Kizimba cha mfupa!!”
Skellidoni mara baada ya kumaliza kuongea alikuwa tayari kujizingira na nguvu ya kifo kwa mara nyingine. Na wakati huo huo mifupa mingi mirefu ilichomoza kutoka ardhini mmoja baada ya mwingine na kumzingira Hamza kwa namna ya kumtengenezea kizimba(Cage).
Lakini Hamza mara baada ya kuinua ile siraha yake juu ya mfupa na kufyatua ikiambatana na nuio, kibanda chote kilisambaratika.
“Hapana haiwezekani , unawezaje hivi?” Skellidoni ukichaa ulikuwa ukizidi kumvaa. Alimuona kabisa Hamza hakuwa na nishati yoyote ya mbingu na ardhi lakini bado anaweza kusambaratisha nguvu zake bila ya kutumia nguvu nyingi. Alijiuliza kwanini kila akitumia siraha yake kiwepesi tu shambulizi lake linaonekana kuwa na nguvu isio na kawaida.
Ilikuwa ni kama kulikuwa na nguvu ambayo Hamza alikuwa akitoa katika namna alivyokuwa akitumia mfupa ule kama siraha , Skellidoni alionekana kuwa katika hali ngumu kuelewa.
Alijikuta akishikwa na hasira kwa kudhalilika. Alirusha kila aina ya pigo alilokuwa nalo kumsogelea Hamza lakini wapi.
Hamza alikuwa amechachamaa kupunguza umbali aliokuwa nao kati yake na Skelidoni , hivyo aliendelea kupiga hatua kwenda mbele na kutumia kila aina ya sanaa ya mapigano kuendana na spidi yake.
Nguvu ya miguu yake ilikuwa kubwa kama vile alikuwa ni ndege anaeogelea angani. Licha ya kwamba alikuwa na uchomvu lakini mwili wake ambao alikuwa akiufunza kwa miaka zaidi ya mitatu ulionyesha miondoko isiokuwa ya kawaida. Hamza alitembea kama vile alikuwa akicheza ngoma na kufanya aonekane ni kama mzimu usio na uzito.
Hamza alizidi kuhisi wepesi na kila sekunde iliokuwa ikisogea alijihisi ni kama kuna vitu vingi ambavyo alizidi kuvielewa. Hamza muda huo alijilaumu kwa kutokuelewa mapema kwamba nishati ya mwili au nguvu ya kiroho ya mwili ni tofauti na ile inayopatikana nje ya mwili. Nishati ya mwili ni kama mazingaombwe , uchawi , au nguvu ya kipekee ambayo inaweza kumlinda mtu kwa namna ya ajabu sana.
Uelewa aliokuwa akipata , kama ingekuwa ni zamanni angekuwa na furaha, lakini muda huo roho yake ilikuwa imamezwa na roho ya kisasi, alichotaka kufanya ni kumlipia Regina kisiasi.
“Arghhhhhhh!!”
Hamza aliruka juu na mwili wake ulikuwa mwepesi kiasi kwamba ulienda mbele bila ya kutumia nguvu kubwa kama mwanzo.
Ndani ya sekunde tu Hamza alikuwa asharuka kutoka alipokuwa na kwenda kutokea mbele yake.
Skellidoni alijikuta akiwa katika hamaki kwani licha ya kila alichofanya kumzuia Hamza asimfikie kilishindwa kuwa na athari kabisa kwake.
Hajawahi kuona mtu akitumia mbinu ambazo hazieleweki kama Hamza maisha yake yote.
Hamza hakuwa na nguvu za kutosha na muda huo aliona atumie pumzi yake ya mwisho iliobakia kutoa shambulizi lake la mwisho lenye nguvu.
“Kufa!”
Hamza alifyatua mfupa uliokuwa kwenye mikono yake na kutengeneza angle 360 wakati wa kumsogelea mwili wa Skellidoni.
Ukipasua kichwa chake anaweza kupona , ukichoma moyo wake anaonekana kuwa sawa. Hamza hakuamini kwamba kama atamgawanya mara mbili anaweza kupona.
Shambulio lake Hamza lilikuwa limejaa upako , lilikuwa jepesi lakini lenye nguvu mno ambayo ilitegemea spidi yake na nguvu ya mwili wake pamoja na muunganiko kamilifu wa mwili wake, na hakika lilionekana kuwa shambulizi lisilokuwa la kawaida.
Kwa mbali Black Fog mara baada ya kuona mashambulizi mengi ya Hamza ya kupangua alijikuta akibung’aa . Lakini mara baada ya kuona siraha ya Hamza ikimfyeka Skellidoni alikuwa katika mshituko mkubwa.
Kwa daraja alilokuwa Black Fog , ilikuwa ni ngumu kuelewa mbinu ya mapigano ya Hamza. Msichana huyo alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa pia , hakuelewa kwanini mapigo mepesi tu yanaweza kutoa nguvu kubwa namna ile ambayo haizuiliki. Licha ya Rhoda kuwa mbali lakini aliweza kuona hali aliokuwa nayo Skellidoni , bwana huyo alionekana kuwa katika hali ya kukata tamaa.
Alionekana kabisa hakuwa na uwezo wa kukwepa , hakukuwepa kabisa shambulizi la Hamza.
Skellidoni aliishia kutoa kilio cha kutia huruma huku akitoa msisimko wa kifo kujaribu kukinzana na shambulizi la Hamza lakini msisimko wake wote ulizimwa mara moja.
“Shaaa!!”
Siraha yake alioshikilia ilidondoka chini huku mwili wake ukitenganishwa mara mbili.
Skellidoni joho lake lilichia wazi , ndani yake kuliikuwa na vipande vya mifupa iliovunjika.
Hatimae mwili halisi wa Skellidoni ulionekana. Hamza na Black Fog walijikuta wakishangaa mara baada ya kuona ndani ya mskeletoni kulikuwa na mwili mwingine wa kizee uliosinyaa mno na wenye muonekano usiokuwa wa kawaida kutokana na uzee wake.
Pengine ni kutokana na kujifunza nguvu za giza ndio maana mwili wake halisi ukasinyaa na matokeo yake ilibidi atumie skeletoni kwa ajili ya kutengeneza udanganyifu kwamba hawezi kuuliwa kumbe ni mtu halisi aliejificha ndani ya mbavu za skeletoni.
Kitendo cha Hamza kushambulia eneo la katikati kwa namna ya kumfyeka bila kujua alikuwa ameshambulia kichwa halisi cha Skellidoni.
“Nini..imeku..”
Gwiji huyo mpaka anapoteza uhai hakujua ni kwa namna gani Hamza ameweza kumdhibiti wakati alikuwa amechoka mno.
Hamza mara baada ya kushinda , mwili wake wote ulianza kukumbwa na uchomvu mkali na akili yake ilianza kuingiwa na hali ya ukungu.
Mfupa aliokuwa ameshikilia katika mkono wake ulidondoka chini ardhini. Alikuwa akisikia hali ya sumu ya umauti ndani ya mwili wake ikiendelea kumtafuna kwa kasi kubwa.
Licha ya kwamba Hamza aliweza kushinda lakini hakufanikiwa kutoa sumu iliokuwa ndani ya mwili wake na aliona bila ya kuwa na mbinu ya mgawanyiko hakujua ataweza vipi kuihimili.
Mara baada ya kutingisha kichwa chake kwa namna ya kujaribu kujiweka sawa hatimae midomo yake ilitoa tabasamu la afadhali akiangalia maiti ya mke wake.
“Wife nimekulipia kisasi.. nakufuata huko ulipo”Aliongea Hamza na palepale alidondoka chini na kufumba macho.
Lakini muda huo kiumbe kilichofunikwa na moto wa dhahabu kilishuka kutoka angani na kwenda kutua mbele ya Hamza.
“Hamza! Wewe kichaa hebu acha kuniogopesha hivyo”
Mtu aliekuwa amefika hapo , alikuwa ni Nyakasura . Mwanzoni hakujua hata kwanini alikuwa akija upande huo , alikuwa na hasira na ni kama hakuwa akiamini Hamza amempotezea kwa sababu ya Regina.
Hakutaka kujihisi kuchanganyikiwa kwa kukosa majibu ndio maana aliamua kuja hapo kwa ajili ya kutaka maelezo kutoka kwa Hamza kwanini alimdharau . Na alijiambia kama Hamza asipoomba msamaha wake basi atampotezea kwanzia hapo na kisha ataunguza nyumba.
Lakini ile alipokuwa akisogelea karibu , aliweza kuhisi nguvu kali ya msisimko wa kifo.
Nyakasura hakufikiria tena na palepale aliegesha gari na kutumia nguvu zake na kusogea haraka. Lakini alifika akiwa amechelewa kwani ndio pambano lilionekana kutamatika na Hamza kupoteza fahamu.
Black Fog mara baada ya kumuona Nyakasura ni kama akili ilimrejea na kusota huku akipiga makelele.
“Madam naomba muokoe Bro, Msaidie apone”
Nyakasura aliishia kukunja sura , hakujua imekuwaje Skellidoni kutokea hapo na kupigana na Hamza.
Ile anataka kuangalia mapigo ya Hamza , ghafla sura yake ilitua katika maiti ya mtu mwingine , ulikuwa ni mwili wa Regina na alijikuta akishangaa mno.
Nyakasura alizidi kushangazwa na mkuki uliotoboa kifua chake na kujikuta kuhamaki bila ya kupenda.
“Nini kimemtokea?”
“Dada Regina kwa , kwa ajili ya kumsaidia Bro kukinga shambulizi , aliishia kuuliwa” Aliongea Rhoda huku akitoa kilio cha kwikwi.
“Nini!”
Nyakasura sura yake ilifubaa , uhalisia alioweza kushuhudia ulimfanya kushindwa kujua cha kufanya. Mwanzoni wakati akimwambia Regina hakuwa na thamani ya kuwa na Hamza , ilikuwa ni kutokana na kwamba alitamani uwezo wa Hamza , alikuwa akitaka kutumia uwezo wa Hamza kujinufaisha . Lakini muda huo sasa ndio anajua Regina amejitoa kafara kwa ajili ya Hamza alijisikia tofauti.
Nyakasura moyo wake ulikumbwa na majuto makali na kujilaumu. Ndio sasa anajua hakufanya sahihi , alijikweza sana na kumshusha Regina.
“Ms Nyakasura , Sister Regina ameshindwa kumuokoa licha ya kusalimisha uhai wake , haraka naomba ufikirie namna ya kumsaidia bro”
Black Fog alikuwa akitembea pia kwa maumivu makali na asingeweza kufanya chochote kwa hali aliokuwa nayo zaidi ya kumtegemea Nyakasura kufanya maajabu.
Nyakasura hisia zake zilirudi na palepale alimwangalia Hamza ambae alikuwa amepoteza fahamu.
“Nguvu yangu ya moto wa mbingu ya tisa unaweza kupambana na kila aina ya uovu . Nitaweza kumuokoa” aliongea Nyakasura na palepale alimkalisha Hamza na kuweka mkono wake nyuma ya mgongo wake na kuanza kumuingizia nishati ya mbingu na ardhi.
Hamza mwili wake pia ulikuwa na nguvu , nguvu yake haikuwa kwenye misuli tu lakini vilevile ilikuwa kwenye seli za mwili wake , hivyo alikuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na sumu.
Sababu ya kwamba sumu iliweza kunyong’onyesha mwili wake kiasi hicho ni kutokana na kwamba alipoteza nguvu nyingi sana , hivyo kinga yake ilipotea pia.
Hivyo mara baada ya nishati ya moto wa nyakasura kuingia katika mwili wake , ni kama mwili wake ulishtuka na kuanza kushindana na sumu iliokuwa ndani yake.
Haikuchukuwa muda mrefu , rangi ya Hamza iliweza kurudi na kuwa kawaida na pumzi yake ilizidi kuimarika sekunde hadi sekunde.
Dakika nne mbele Hamza aliweza kushituka , ijapokuwa kichwa chake kilikuwa kizito lakini alikuwa sawa.
“Bro upo sawa!?” Aliongea Black Fog.
Hamza aliishia kutingisha kichwa chake tu. Hakuwa hata na haja ya kujua nani aliemsaidia , alikuwa na uelewa mkubwa sana likija suala la nishati ya mbingu na ardhi.
“Nyakasura , asante sana”
Ijapokuwa Hamza hakuwa tayari amemsamehe Nyakasura kwa maneno yake , lakini kama isingekuwa yeye kumsaidia , pengine uhaii wake ungekuwa hatarini. Hiivyo shukrani yake ilikuwa ni ya dhati.
Nyakasura alionekana kushangaa , ilikuwa ni mara ya kwanza Hamza kuongea akiwa na sauti hio, ijapokuwa haikuwa ya upole sana lakini ilisikika tofauti.
“Mh! Sikutaka mshenzi kama wewe ufie kwenye mikono ya watu wengine”Aliongea kwa maringo.
Hamza hakujali sana na palepale alisimama , uso wake haukuwa na hisia zozote , lakini macho yalikuwa yamejawa na majonzi makubwa na upweke.
Kinyonge sana alijikuta akisogelea maiti ya mke wake Regina na kupiga magoti pembeni yake na kisha aliinamisha kichwa chake chini na kupapasa kichwa cha Regina kwa upole.
“Mke wangu , nitakurudisha nyumbani nikupumzishe”
Hamza mara baada ya kusema hivyo aliweka mkono wake kwenye ule mfupa na aling’ata meno kwa nguvu na kisha akauchomoa kwenye kifua cha Regina.
Damu nyeusi ilitoka katika shimo lile kama vile ilikuwa ikitoka na uhai wa Regina uliobakia.
Hamza mara baada ya kuona tundu hilo kubwa katika kifua cha Regina, alijikuta akishindwa kujizuia na machozi kumtoka.
Katika akili yake alijikuta akianza kukumbuka siku ambayo anakutana na Regina kwa mara ya kwanza , hatua walizochukua kufahamiana mpaka kufunga ndoa na hatimae kupendana na kuendelea.
Ukweli ni kwamba licha ya kwamba ilikuwa mara ya kwanza kukutana na Regina lakini siku ambayo alikutana nae alijihisi ni kama alishawahi kukutana na Regina kabla.
Kutoka kuwa bosi kauzu , mwanamke mpenda donati , baadae mtu mwenye hila nyingi mpaka muda huo ambao amejitoa uhai wake kwa ajili yake , Hamza hakujua ni upande upi wa Regina ni halisi, lakini kwa vyovyote vile uhalisia wake haukujalisha tena. Tayari alishayatumia maisha yake ili kuthibitisha hisia zake hazikuwa feki.
“Bro Sister Regina amekufa kwa ajili yako. Tutamzika pamoja, ulishamlipia kisasi nina uhakika atakuwana furaha kuona upo salama”Aliongea Black Fog akimsogelea Hamza kumfarij.
Hamza aliishia kuvuta pumzi nyingi sana na kisha alijitahidi kujituliza kiume na kutingisha kichwa.
“Nipo sawa , kwasasa nataka kumchukua na kumrudisha Tanzania”
Ile Hamza anataka kumbeba tu Regina mara mwanga wa bluu usiokuwa wa kawaida ulitokea katika mwili wa Regina na kumzingira.
“Eh!!?”
Nyakasura , Rhoda na Hamza wote walijikuta wakijawa na mshangao baada ya kuona jambo la ajabu lilikuwa likitokea katika mwili wa Regina.
Ilikuwa ni miale ya baridi sana ya rangi ya bluu ilikuwa ikitoka kwenye mfuko wa koti lake, mara baada ya Hamza kufungua ilikuwa ni ile pete ya watu wa bondeni ambayo ilichoropoka na kuelea juu angani na kummulika Regina.
“Naona vibaya ama! Hio si pete ya watu wa Binamu , imekuwaje akawa nayo Regina?”Aliuliza Nyakasura akiwa na mwonekano wa kushangaa. Bila shaka hata yeye alishawahi kusikia ama kuiona pete hio katika vitabu.
Hamza hakujisumbua hata kulezea mara baada ya kuona pete ile ilikuwa ikitoa nishati ya ajabu.
Nishati hio ya blue ilikuwa na hali ya ubaridi mkali mno, huku mwanga wake ukiwa wa kuwaka waka kama vile ni nyota wa angani.
Upande wa mwili wa Regina , jeraha lake lilionekana kuganda , ule mng’ao na ubaridi uligandisha lile jeraha na barafu kusamba mwili mzima.
“Bro , hicho ni kitu gani?”Aliuliza Black Fog akiwa na uso uliojaa hali ya kuchanganyikiwa.
“Hata mimi sijui..” Hamza alijikuta akihamasika kwenye moyo wake kwasababu alihisi ni kama ishara ya tumaini kwake.
Pete ya watu wa kondeni, binamu , Jicho la Anga , kitabu kisichokuwa na maandishi na damu ya familia , kuna kitu kisicho cha kawaida kuhusu hivi vitu? Hamza alijiwazia.
“Hii nishati kwanini ni ya baridi hivyo lakini pia yenye nguvu?”Aliongea Nyakasura.
Haikuwa rahisi kumfanya Nyakasura kuongea namna hio , kusema kwamba nishati hio ina nguvu sana . Lakini kuwazia kwa kina kama pete hio isingekuwa na nguvu ya ziada basi watu wa bondeni na Binamu wasingekuwa wakiiwinda namna hio.
Hamza alijikuta akishangaa zaidi mara baada ya kuona jeraha la Regina lilikuwa limefunikwa na mwanga ule wa bluu na kuliponja kwa kasi kubwa mno kutokea ndani.
Kwa macho ya kawaida kabisa jeraha lile lilionekana kuanza kupungua ukubwa wake na kuwa dogo. Nyama na damu yake ni kama imepokea uhai mpya.
“Huku mbona ni kuzaliwa kwa moto! Anawezaje kufanya hivyo?”Aliongea Nyakasura kwa mshangao.
“Kuzaliwa kwa moto kivipi , moto umeuona wapi hapa?”Aliongea Hamza.
Nyakasura mara zote ambazo akipata majeraha ili mradi awe karibu na moto basi anaweza kuyaponyesha kwa kuogelea kwenye miale yake. Ili mradi isiwe ni majeraha makubwa basi anaweza kupona kabisa na moto ndani ya muda mfupi. Hio ilikuwa nguvu ya damu yake.
Lakini Regina aliekuwa mbele yao , hakuwa kabisa na damu ya kifoeniksi kama Nyakasura . Kingine zaidi , hakuwa akitoa moto , hivyo kwanini azaliwe upya kwa moto.
“Najua sio moto lakini kinachomtokea ni kama ambavyo inanitokea mimi! Au hii ndio inaitwa kuzaliwa na barafu?” Nyakasura alitunga jina mwenyewe kulingana na nguvu ya ubaridi alioweza kusikia ikimtoka Regina.
Tumaini la Regina kufufuka lilionekana. Hamza furaha ilimrudia kiasi cha kutaka kuruka ruka , lakini hakuthubutu kabisa kuugusa mwili wa Regina .Aliishia kushika mikono yake kwa wasiwasi akiangalia kile kinachoendelea.
Black Fog na Nyakasura mara baada ya kuona mabadiliko ya Hamza , walijikuta wakiwa na hali zisizoelezeka. Wanawake hao walielewa nini kinaendelea katika moyo wa Hamza.
Lakini hawakuwa na la kusema kwasababu Regina alitumia uhai wake kuthibitisha hisia zake. Hakuna ambae aliweza kuwa na wivu wala kumuonea husuda.
Mara baada ya dakika kumi , hatimae mwili wa Regina kimiujiza uliweza kupona kabisa. Jua la asubuhi na lenyewe liliangaza vizuri na kufanya barafu yote iliokuwa imefunika mwili wa Regina kuyeyuka na kumfanya aonekane ni kama mtoto amezaliwa kwa mara nyingine.
Mara baada ya mwanga kupotea , ile pete ni kama ilikuwa imepoteza nguzu zake zote na kudondoka chini.
“Inaonekana hakupoteza pumzi muda mrefu tu , ni kama hio pete ilikuwa na kazi maalumu ya kulinda uhai wake na kusubiria wakati sahihi wa kuanza kumponyesha”Aliongea Nyakasura.
Hamza hata yeye alishindwa kujua nini kinaendelea mara baada ya kuona Regina mapigo yake ya moyo yakidunda huku kifua chake kikipanda na kushuka kama vile alikuwa amelala usingizi mzito, alikuwa na furaha isioelezeka kumuona Regina anapumua tena.
Hamza alijikuta akifuta machozi haraka kwa kuhofia kumdondokea Regina na haraka sana alimbeba juu juu na kumpeleka ndani ya nyumba na kumlaza kitandani.
Mara baada ya kumuweka Regina kitandani , alitoa simu y ake na kupiga na sio muda mrefu simu hio iliunganishwa na sauti ya heshima kutoka kwa mwanaume upande wa pili ilisikika.
“Sire , umeniita asubuhi , kipi naweza kufanya kwa ajili y ako?”
“Mzee Pino , nataka unitafutie hospitali nzuri ndani ya Paris , na haraka sana andaa madaktari bingwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kimwili”
Aliekuwa akiongea nae Hamza ni Tajiri Pinalt wa Kering corporations.
“Sire hujisikii vizuri?”
“Sio mimi , ni mke wangu anaekwenda kufanyiwa uchunguzi”
“Oh , basi nitafanya hivyo sasa hivi , nipe dakika tatu nitakutumia ujumbe”Aliongea Mzee Pino bila ya kuuliza sana.
Haikuchukua muda Mzee Pino alituma ujumbe wa meseji ulioambatana na anuani ya hospitali husika na madaktari watakaompokea.
“Hey ! Usiniambie unampeleka Regina hospitali ?”
“Kwani siwezi?”
“Sio kama huwezi , ni kwamba tu hajaamka lakini hali ya mwili wake inaonekana kuwa sawa”Aliongea Nyakasura.
“Lazima nihakikishe mke wangu yupo salama kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya hali ya juu sana . Nikishathibitisha kupitia vipimo kama hana shida ndio nitatulia sasa”
“Lakini vipi kuhusu mdogo wako! Hata yeye anayo majeraha?”
Hamza palepale ndio alikumbuka Black Fog na yeye aliumia na aliishia kuongea kwa kubembeleza.
“Sorry nilikuwa nimechanganyikiwa na sikukujali kabisa, unaonaje ukiongozana na sisi kwenda hospitali?” Aliongea Hamza lakini Black Fog alikuwa ni mwelewa.
“Usijali Bro , majeraha yangu hayawezi kulingana na aliopata Sister”
“Jamani , muone anavyotia huruma sasa kaka yake kamtelekeza . Ni zamu yangu kuhakikisha unakuwa sawa mdogo wangu”Aliongea Nyakasura akimshika Black Fog kichwa na palepale hakujali kile ambacho Black Fog alikuwa akiwaza kwani alimkandamiza chini na kisha akaweka kiganja cha mkono wake nyuma ya mgongo na kuruhusu nishati ya moto kumuingia.
Haikuchukua muda , Black Fog alianza kuhisi hali ya joto katika mwili wake na ndio alijua Black Fog alikuwa akimsaidia kuponyesha majeraha yake , alijikuta akishangaa na kuguswa kwa wakati mmoja.
Isitoshe tabia ya Nyakasura kwenda kwa Rhoda haikuwa nzuri katika siku chache zilizopita . lakini dakika hio kuanza kumjali ilimgusa mno.
Nyakasura uwezo wake ulikuwa mkubwa sana , hivyo nishati yake ilitosha kabisa kutibu majeraha ya kawaida ya mwili, hivyo alichofanya kilimsaidia sana Rhoda na ingemchukua siku mbili tu kuwa sawa kabisa.
Muda mfupi mbele Hamza alimchukua Regina na kumuingiza kwenye SUV na safari ya kuelekea hospitalini ikaanza mara moja.
Kwasababu ilikuwa ngumu kwa Black Fog na Nyakasura kuendelea kubaki hapo shamba , hivyo waliondoka pamoja kwenda hospitalini.Na ndio muda ambao Hamza alikumbuka kumuuliza Nyakasura swali.
“Nyakasura kipi kilikuleta tena huku shamba?”
“Nini! Yaani nimekuokoa halafu unaniuliza nini kimenileta?”
“Nimeuliza tu , wasiwasi wa nini sasa? Si nilishakushukuru kama haitoshi unataka nifanye kitu kingine?”
“Hata usijisumbue . Nilikuja kwasababu nilipanga kuunguza nyumba yenu mkiwa mmelala, nani kakuambia unikasirishe. Lakini mara baada ya kuwaona mpo katika hali ya kusikitisha namna ile , hasira yangu iliisha mara moja”
Hamza aliishia kushangazwa na hasira za mwanamke huyo , yaani katoka hotelini anakolala mpaka shamba kwa ajili tu ya kutaka kuwaunguza kwa sababu alikasirika?.
“Tukiachana na hayo , imekuwaje mpaka ukashambuliwa na Skellidoni asubuhi asubuhi? Si aliuliwa na Silvia?”
Hamza hakuona kuna haja ya kudanganya , hivyo alimwambia Nyakasura kila kitu. Nyakasura mara baada ya kusikia stori hio alijikuta akikunja sura.
“Kama hivyo basi hili suala sio la kawaida. Nina uhakika ni Silvia aliemtuma Skellidoni kuja kukuua ili kuficha ukweli. Hii haiwezi kuendelea hivi napaswa kumwambia Simba na wengine kama Silvia ndio aliekuwa fundi wa kila kitu na mpango wake ulikuwa ni kuitawala Set Association”
“Hata ukiongea nani atakuamini sasa , Skellidoni amekwisha kufa tayari na ushahidi huna”Aliongea Hamza.
Ukweli ni kwamba Hamza hakujali sana . Hakujali Silvia alikuwa akipanga kufanya nini na uhusiano wake na Sinagogu ukoje , ili mradi haitokuwa na athari kwa Hamza na watu wanaomzunguka , Hamza hakupanga kujali sana. Lakini kama Sinagogu watakataa kumuacha na kuendelea kumchokoza , Hamza alijiambia hawezi kuwa mwema tena na yupo tayari kutoka mafichoni na kuanzisha vita takatifu tena.
“Bro ni aina gani ya mafunzo uliotumia kumuua Skellidoni ? Ilikuwa na nguvu mno? Nilijua umekosa jinsi kabisa ya kupambana nae lakini kumbe ulikuwa umeficha mbinu hatari namna ile?”aliongea Rhoda.
“Nawezaje kuficha sasa katika hatari kama ile? Ni kitu ambacho sijawahi kufikiria hapo kabla. Ni aina tu ya mbinu imenjijia na naweza kusema ni kama nguvu ya kimungu”
“Ni mbinu gani hio , hebu niambie haraka”aliongea Nyakasura.
“Nitawaelezea , ila subirini kwanza mpaka mke wangu afike hospitalini na ndio nitawaambia kila kitu”Aliongea Hamza na wanawake hao mara baada ya kusikia hivyo walionekana kumuelewa.
soma sehemu ya 221 mpaka 223 bure kabisa, unachopaswa kufanya ni kujisajili na google, utaweza kufungua sehemu hizo. Nimeziwekea sarafu sifuri. Hapa jukwaanin itaendelea sehemu ya 224 siku ya jumanne hapa.. fuata link:- SEHEMU YA 221
Hatuna deni na ww 🙌Jamii ya muungano wa siri.

Mtaalam singanojr uliahidi muendelezo Jumanne, leo ni Jumatano bado hujawekaJamii ya muungano wa siri.

singanojr ni Bora tu aanze kuweka miendelezo huku, kwenye group lake la Whatsapp anaharibi vibaya, kwa kuwapoteza washabiki wake. Hana tabia ya kuwa mkweli.Mtaalam singanojr uliahidi muendelezo Jumanne, leo ni Jumatano bado hujaweka