Hamza alijikuta akishangaa mara baada ya kumwangalia Regina , kwa mwonekano wa Regina , ilikuwa ni dhahiri alikuwa akimfahamu huyo mwanaume , lakini mtu huyo hakuonekana kuwa mdogo. Kulinganisha na Regina kulikuwa na utofauti ambao ni zaidi ya mbingu na ardhi , na Hamza alijiuliza inakuwaje wakawa wanafahamiana?.
“Regina! Najua ni wewe , acha kunikimbia baba yako”Aliongea yule mwanaume ambae alionekana kulewa kiasi.
Mara baada ya bwana huyo kuongea hivyo Hamza alijikuta akishikwa na mshangao mkubwa mno na kujiuliza nini maana yake hii?
Baba yake Regina? Lakini mbona nina uhakika Regina ni mtoto wa Mzee Samweli?. Yalikuwa maswali ya Hamza.
“Umenifananisha! Sikujui mimi”Aliongea Regina huku akiwa na macho yaliokuwa mekundu na mara baada ya kuongea alianza kukimbia bila ya kuangalia nyuma.
Hamza alionekana kusita kwa sekunde , lakini hakujali tena kuhusu mwanaume huyo ambae alionekana maisha yamempiga na kuonekana kuchechemea na kumkimbilia Regina aliekuwa akikimbia.
Yule mwanaume aliishia kumfukuza Regina kidogo tu na kudondoka chini kutokana na kulewa kwake na kuoneana kuumia mguu , huku akiendelea kuita kwa nguvu.
“Regina hebu acha kukimbia , wewe m*laya usie na shukrani..”
Watu wengi waliokuwa katika mtaa huo walionekana kushangaa na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja , hawakuelewa ni kitu gani kinaendelea lakini wengi wao walimuona Mzee huyo kuwa kichaa.
Walimuona Regiona ni mwanamke ambae alionekana kuwa wa kishua,inakuwaje kuwa na baba Mlevi, licha ya hivyo wengine walidhani inawezekana , isitoshe kuna matukio mengi ya watoto kuwa matajiri lakini wazazi wanaishi kwenye umasikini.
Yule mwanaume aliendelea kulala ardhini huku akiendelea kulalamika na kumtukana Regina kilevi na kadri sekunde zilivyokuwa zikisogea ndio namna sauti yake ilivyozidi kuwa dhaifu na kunyamaza kabisa .
Baada ya kama dakika tano au sita hivi kupita , mwanaume yule wakati akihangaika kusimama , ghafla tu alisogea mtu na kumnyooshea mkono.
Mwanaume yule aliinua sura yake na kuangalia juu na ndio alipoweza kumuona mwanaume aliekuwa na sura ya kitanashani na alievalia nguo nadhifu zilizoashiria ukwasi, lakini akiwa na tabasamu lililojaa uovu.
“Shika mkono wangu mzee , nikusaidie kusimama”Aliongea yule bwana na hata sauti yake tu ilionyesha hakuwa mtu wa hadhi ya chini.
Yule mlevi alionekana kutetemeka wakati akiwa ameshikana mkono na yule bwana ambae hakumfahamu , huku akijitahidi kusimama.
“Wewe .. ni nani?”
“Hilo swali napaswa kukuuliza wewe .. Wewe ni nani na una uhusiano gani na Regina?”.
*****
Regina alikimbia mpaka kufikia sehemu ambayo walikuwa wameegesha gari , lakini ile anafika aligundua ufunguo alikuwa nao Hamza
Hamza mara baada ya kufikia gari , aliishia tu kufungua mlango na rimoti na Regina aliingia upande wa dereva na yeye pia aliingia upande wa siti na kisha akampatia ufunguo.
“Unaweza kuendesha!”Aliongea Hamza bila ya kuuliza chochote.
Regina mara baada ya kupewa ule ufunguo haraka haraka aliwasha gari kama vile alikuwa akifukuziwa na kuliondoa kwa spidi ndani ya eneo hilo.
Hamza aliishia tu kumwangalia mwanamke huyo , alivyokuwa mkavu kwenye macho yake , ingawa alikuwa na maswali mengi , lakini hakutaka kuuliza. Aliona Regina alihitaji muda wa kutulia kwanza.
Mara baada ya kuendesha gari kwa nusu saa nzima uelekeo wa nyumbani aliingiza gari katika geti linaloingia fukweni na kisha akasimamisha pembeni.
Mara baada ya kushuka kwenye gari , Regina alisogelea upande wa fukwe na kuanza kuvuta hewa nyingi huku akimwangalia Hamza aliekuwa akishuka kutoka garini taratibu.
“Kwanini huulizi yule mtu ni nani?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutingisha mabega.
“Kama unaona unaweza kuniambia , basi utaniambia tu..”
Regina alionekana kunyamaza kwa sekunde kadhaa na kisha aliangalia upande wa minsupermaket ya masaa ishirini na nne na palepale alianza kutembea kuelekea uelekeo huo.
Hamza aliishia kumfuata nyuma nyuma mpaka ndani ya min-supermaket ile na alimuona Regina akisogelea friji na kutoa maji na kunywa kiasi.
Hamza mara baada ya kuona Regina alipanga kunywa na yeye pia alisogelea friji na kutoa bia ya kopo na kisha kusogea karibu na Regina.
“Ngoja tunywe wote”Aliongea Hamza akicheka kidogo na Regina aliishia kutembea mpaka kwenye viti na kukaa chini huku akiendelea kunywa maji yale mdogo mdogo akiangalia upande wa baharini.
Hamza pia aliendelea kushusha bia yake taratibu na korosho huku na yeye pia akiwa ameangalia uelekeo wa baharini.
Mkao huo ulimkumbusha Hamza kipindi kila mwenzao anapofariki katika harakati za vita angekaa hivyo na washikaji zake na kunywa wakiwa wameangalia baharini.
“Jina lake anaitwa Madilu…”Aliongea Regina baada ya kimya cha muda mrefu.
Hamza aligeuka na kumwangalia Regina ambae alioneakna katika hali ya mawazo huku nywele zake zikiwa zinapeperushwa na upepo, kulikuwa na ishara ya machozi kwenye macho yake pia.
“Kwanini kasema wewe ni baba yake?”
Hamza mara baada ya kuona mwanamke yupo tayari kuongea , aliona aulize maswali ili kumjuia zaidi.
“Kama hutaki kuongea , unaweza kuacha tu. Hata hivyo sijali sana..”
“Kwanini usijali! Ukiweza kujua ukweli , pengine hisia zako juu yangu zinaweza kubadilika kabisa”Aliongea Regina huku akitoa tabasamu lililojaa huzuni.
“Kitu pekee kitakachobadilika ni kwamba nitakujua zaidi ya mwanzo ila kubadilika kwa hisia zangu kwako”Aliongea Hamza huku akicheka kidogo.
“Vipi kama ukijua mimi ni mtoto wa changudoa?”
Hamza kauli hio ilimshangaza na palepale alikumbuka kipindi wale wazee Regina akiwafukuza kwenye kampuni walikuwa wakimtukana kwa kumuita mtoto wa kahaba na sio hao tu hata Lamla alishawahi kusikia akiongea na alijua ni hasira tu , ila kumbe mama yake alikuwa akifanya kazi maalumu.
Hakujali mwanzo , ila baada ya kumsikia Regina akiongea alijikuta akianza kujali sasa. Ila Hamza hakujali sana kwani kutokana na uzoefu wake alikuwa akielewa baadhi ya mambo. Ili kuendelea kuishi ilikuwa ikieleweka baadhi ya watu kufanya maamuzi magumu.
Hamza alijikuta akiinua mkono wake na kumshika Regina kichwa na kumwangalia usoni.
“Inua kichwa chako na niangalie usoni”Aliongea na Regina aliinua kichwa chake na kumwangalia Hamza usoni na kufanya amcho yao kukutana.
“Sijui ni kitu gani unakwenda kuongea , ila nadhani kupitia macho yangu unaona sijali chochote”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
“Kweli!” Aliuliza Regina huku macho yake mazuri yakichanua.
Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo , bado alikuwa na wasiwasi, palepale macho yake yalikumbuka kitu na kumfanya arudishe kumbukumbu nyuma.
“Wife ngoja nikuambie kitu, kuhusu maisha yangu yaliopita , pengine baada ya kunisikiliza unaweza kunielewa”Aliongea Hamza.
“Mh.. ni kitu gani?”
“Wakati nikiwa na miaka kumi na tisa , miezi miwili kabla ya vita takatifu kuanza. Ukweli ni kwamba sikuwahi kuwaza kama nakwenda kupigana vita vikubwa , sikuona kabisa nafasi ya kushinda.
“Unapaswa kujua mtawala wa Zama ,Mr Black sio tu kuwa peke yake lakini vilevile alikuwa na mwanamke niliekuwa nikimwita Madam , yule White Queen. Sio hivyo jamii nyingi za siri zilikuwa chin yao na kulikuwa na zaidi ya watu sita ambao walikuwa wanakaribia levo ya ugwiji ….”
Regina alionekana kushangaa na kuchanganyikiwa na alijikuta akiuliza;
“Kama ni hivyo nini kilikupelekea ukaingia vitani licha ya kujua hautoshida?”
“Kwasababu .. mtu muhimu kwangu aliuliwa kwa sumu na kiongozi mkuu wa Madhabahu takatifu. Ndio mtu ambae alinisaidia nikatoka katika giza na kuona kuna vitu vingi katika ulimwengu ambavyo ni sahihi kufanya , sio kuua tu , ijapokuwa nilikuwa nimeaua sana, lakini mikono yangu pia ilikuwa na uwezo wa kuokoa watu…”
Regina muda huo alijikuta akikukumba kipindi walipokuwa kwenye Baraza la maksi , mshereheshaji wakati wa kumtambulisha Hamza alielezea stori kubwa ambayo ilikuwa ikimuhusu , mpaka kuelezea namna Hamza alivyobadilika kutoka kuua na kuanza kuokoa watu.
“Ni kwasababu ya huyo mtu ndio maana ukaamua kuacha kuua na kuokoa watu?”Aliuliza Regina.
“Ndio, bila yeye pengine ni ngumu kudhania ni wapi ningekuwa sasa hivi, labda ningekuwa nishakufa tayari.. hata hivyo nilikuja kugundua amewekewa sumu na kufariki, nilihisi maumivu kiasi kwamba niliona labda ulimwengu umekuwa giza tena. Sikujua ni wapi niende , sikujua nini nifanye. Nilijiuliza nipambane na watu wa Madhabahu kulipa kisasi , nitaweza kushinda vipi mashetani kama wao? Kufikiria kuingia katika vita ya kulipa kisasi , ilimaanisha kuacha nafasi niliokuwa nayo kipindi hicho ndani ya umoja , kwa maneno mengine, ilikuwa ni kwenda kinyume na taasisi mbili za daraja S .. na nguvu ambazo wanamiliki wanaweza kuigeuza dunia nzima na kuwa uwanja wa vita..”
“Lakini bado si ulienda kulipa kisasi?”
“Ndio! Nilijua kuingia ndani ya Baraza la watu wa madhabahu ni sawa na kujitoa muhanga , hivyo nilimtega kiongozi aliemuua kwa sumu kutoka nje na kisha nikamuua. Ni baada ya hapo na kuendelea watu niliokuwa nikifahamiana nao waliamua kutoka chini ya uongozi wa watawala wa zama na kunifuata na tukaannzisha vita kwa zaidi ya miaka miwili…….”
“Nini kilichokufanya ukaamua kuingia vitani licha ya kuwa na wasiwasi wa kutoshunda?”Aliuliza Regina.
“Sikuamua tu, bali kuna mtu nilikutana nae kwa bahati nzuri au mbaya”
“Nani?”Aliuliza Regina na kumfanya Hamza kucheka.
“Unaweza usiamini hata nikikuambia , ila simjui hata alikuwa nani , ila ilikuwa ni nchini Urusi , sehemu moja inaitwa Siberia ndani ya club ya pombe”
Regina mara baada ya kusikia kauli hio , alijikuta akikunja ndita na kujisikia vibaya.
“Unamaanisha alikuwa ni ka…”Aliuliza Regina na Hamza alikuwa muwazi.
“Wife hata nikuambie kwamba kipindi changu nikiwa nje huko nilikuwa na mwanamke itakuwa uongo , tulichokuwa tukifanya kama wanaume ni kutafuta sehemu ya kumaliza haja zetu tu ..”
Regina alijikuta akiishia kung’ata lipsi zake tu , ingawa alijua Hamza alipokuwa nje ya nchi huko alicheza sana na wanawake , lakini kumwambia ukweli ilimfanya kutokuwa na furaha.
Regina alijikuta akivuta tu pumzi , huku akiondoa mawazo mabaya yaliokuwa yakimjia kichwani.
“Endelea kuongea , huyo mwanamke , amewezaje kukufanya ukafikia maamuzi?”Aliuliza na Hamza alicheka kidogo.
“Mpaka muda huo nilikuwa nishajikatia tamaa , nilikaa Siberia kwa muda wa nusu mwezi na ilikuwa ni kunywa kila siku na sikuwa hata nikijua nichukue maamuzi gani au ni kipi nifanye. Baada ya kukutana na huyu mwanamke na kumaliza haja zangu , ghafla tu aliniuliza nini kinanisumbua na mimi bila ya kujali nikaamua kumwambai juu juu tu. Baada ya kumwelezea nikamuuliza swali , je atachukua maamuzi gani kama akijikuta yupo katika hali ambayo hawezi kuchagua zaidi ya kuikubali?”
“Baada ya kumuuliza hivyo alianza kucheka kwanza na kisha aliniangalia kama kituko na kuniuliza nimefikiria nini mpaka kumuuliza mwanamke anaejiuza kama yeye swali siriasi hivyo…” Regina mara baada ya kusikia hivyo , alijikuta akijawa na shauku.
“Usiniambie , alisema nenda kalipe kisasi na wewe ukafanya hivyo ?”
Hamza alitabasamu na kisha palepale alikunywa kinywaji chote alichoshikilia mkononi kwa mkupuo mmoja.
“Sikumwambia kwa kina kinachonisumbua hivyo asingeniambia hivyo , na yeye hakuniambia ni kitu gani napaswa kuchagua. Aliniambia maneno kadhaa ambayo nayakumbuka mpaka leo vizuri kabisa…”
“Alisema , ukijaribu kuepuka mambo ambayo yanakufanya kuhisi kuwa hai lakini pia yanakutisha na kukuhuzunisha , mwishoe utajikuta umepoteza hisia zako zote na moyo wako kubakia mtupu. Kama unajihisi hisia zako zimevurugika na huelewi ni maamuzi gani ufanye , tafuta sehemu tulivu na ya wazi na fikiria kwa makini. Uhusiano baina ya mwanamke na mwanaume hochochewa na utashi wa kiasili na sio maadili pekee wala akili , mahusiano ndio kitu kinachomrudisha mtu katika uhalisia wake wa asili.Muhimu zaidi haijalishi unapitia wakati mgumu namna gani , ila jua nafasi ya kuishi maisha ya maana bado unayo , haina haja ya kupoteza muda katika eneo kama hili na mtu kama mimi ila kama unahisi hapa ndio mahali pakukufanya kufikiria kwa usahihi unakaribishwa kwangu muda wowote”Aliongea Hamza kwa hisia kali huku akifinyanga kopo la bia alilokuwa ameshikilia mkononi na kumwangalia Regina usoni.
“Kwanzia pale nilikuja kuelewa jambo moja tu , maisha hayana haja ya kuumiza kichwa ni njia gani uchague. Bali ni njia ambayo ipo mbele yako ndio ya kuendelea nayo. Kitu unachopaswa kufanya ni kuendelea kusonga mbele mpaka ufike mwisho au ufie njiani. Yule mwanamke mtoa huduma ndani ya bar hakuelewa kuhusu kanuni za maisha zinazofundishwa kila siku wala hakunijua mimi ni nani , lakini licha ya hivyo alionekana kuwa huru zaidi kuliko nilivyokuwa mimi. Aliamua kukubali maisha yaliokuwa mbele yake na kuendelea kusonga mbele huku akijitahidi kuifanya kazi bila majuto”Aliongea Hamza na kisha aliweka mkono wake kwenye bega la Regina.
“Wife unadhani alichokuwa akifanya huyo mwanamke kilikuwa cha kishenzi au alikuwa akijikosea. Nina haki ipi ya kuanza kumhukumu kutokana na aina ya maisha yake?”
Reegina alionekana kushangaa kwa sekunde kadhaa na kisha aliishia kuongea kwa sauti ya chini.
“Kwasababu utashi wa binadamu ni kuishi na kutamani katika mioyo yao.. Mama yangu pia alikuwa akifanya hayo yote kwa ajili ya kuishi”
“Nadhani sasa unaelewa , sikuwa na nia ya kukudharau , wewe ni wewe na mama yako ni mama yako , haijalishi ni kipi alifanya ila yeye ndio amekuleta duniani”
“Usifikirie vibaya , ijapokuwa mama yangu amefanya kazi Bar lakini alikuwa ni mtu mzuri , ni kwamba tu aliingia kwenye mtego wa Madilu , lakini hakuwa na jinsi na kukubali kwasababu alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kujifungua. Watu waliokuwa karibu na mama ndio waliongea kabisa na wengi walikuwa wakimheshimu kabisa”
“Yule Madilu ni baba yangu wa kambo , mara baada ya mama kupoteza uhai baada ya kunizaa , yeye ndie alinichukua na kunipelekea kituo cha kuletea watoto yatima”
“Kumbe ndio ilikuwa hivyo! Ndio maana nilishangaa inakuwaje mtu mwenye damu ya watu wa bondeni kuwa na baba anaeitwa Madilu . Kumbe ndio alikuwa baba yako wa kambo..”
“Mama yangu baada ya kubeba ujauzito na kufukuzwa, alianza kufuatishana na Madilu kwasababu hakuwa na mtu wa kumtegemea hapa jijini na asingeweza kwenda popote. Mwanzoni Madilu alikuwa ni tajiri na alimiliki kampuni ya ujenzi , na mama alitamani nikizaliwa kuwa na baba ndio maana alikubali kuolewa. Baada ya kampuni yake kufirisika kutokana na kujiingiza kwenye kamari , alijikuta akipoteza msingi wa maisha na kugeuka kuwa mlevi , na ndio alianza kumtishia mama yangu kama asipoenda kujiuza na kumpatia hela, basi atampiga mpaka mimba itoke. Mama hakuwa na jinsi aliamua kwenda kujiuza akiwa amenibeba tumboni , hayo yote sikuyajua , ila baada ya kufikisha miaka sita ndio nilianza kuambiwa taratibu. Inasemekana mara baada ya mama kujifungua hospitalini , alipoteza damu nyingi iliompelekea kupoteza uhai kotokana na kumchelewesha kumleta hospitalini, huyo Mzee Madilu ndio alikuja kuniacha kituoni mpaka nilipofikia umri wa miaka sita, ndio alikuja kunitembelea na kujitambulisha yeye ni baba yangu na kutaka kunichukua , lakini viongozi wa kituo ndio walikataa na alikasirika sana na siku moja ndio akajaribu kuniteka tukiwa nje ya kituo. Baada ya tukio hilo alitishiwa kufunguliwa kesi ndio akapotea mazima. Nikiwa na miaka saba ndio nilikuja kugundua sababu ya kutaka kuniteka alitaka kwenda kuniuza kwa babu, ila nia yake haikufanikiwa. Baadae ndio babu akajua nipo kituo gani na kuja kunichukua. Hata baada ya hapo alijaribu kumsumbua babu na kudai yeye ndio alinilea hivyo anataka alipwe fidia. Lakini babu hakumpa hata mia na alituma watu wamfanyizie na kuanzia hapo hakuwahi kuonekana tena mpaka leo”
“Kwahio sasa hivi , unataka afe?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina kushangaa kama vile alikuwa amesikia vibaya.
“Unaongea nini!Unataka kumuua Mzee Madilu?”
“Ndio. Kwa aliomfanyia mama mkwe , anastahili kifo”
“Usije kufanya hivyo. Kumuua hakutabadilisha chochote na hawezi kutufanya chochote pia , mtu kama yule anaweza kutufanya nini? Na kingine si kumuacha aendelee kuteseka mtaani ni kisasi pekee zaidi ya kufa?”Aliongea Regina akiwa amekunja sura
“Wife upo sahihi , isitoshe una moyo mwepesi mno , vinginevyo usingeweza kumsamehe Lamla”Aliongea Hamza .
“Pengine kwenye ulimwengu wenu wa siri kuua ndio njia rahisi ya kutatua tatizo , ila mimi kwangu ni njia ya mwisho kabisa. Kama kuua mtu ni kitu rahisi , tuna utofauti gani na majambazi? Hamza nataka uniahidi kitu kuanzia sasa hivi, siku nyingine usije kutamka kauli kama hio. Yaani unasema unataka kuua mtu kirahisi , unaniogopesha ujue”
Hamza mara baada ya kuona hali ya wasiwasi aliokuwa nayo Regina,alijikuta akicheka kivivu .
“Basi mke wangu kama hutaki niongee hivyo , sitofanya hivyo siku nyingine. Tatizo tu nahisi kukuonea huruma , pengine huyu mtu aliacha kovu kwenye maisha yako. Vinginevyo usingekuwa na wasiwasi vile baada ya kumuona..”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kutoa tabasamu hafifu.
“Ni mambo ya zamani hayo yashapita , huna haja ya kujali sana..”
“Kwanini nisijali sana? Wife mimi ndio naogopa wewe kutokujali na kunikimbia?”Aliongea Hamza akiwa na sura ya utani.
“Anaeongea hapo ndio mtukufu mfalme wa kuzimu na gwiji kabisa , hata nikukimbie nitajifichia wapi.Unavyosema ulikuwa ukipita na kila mwanamke kutoa hamu zako kipindi cha nyuma ni kama unamaanisha ni sawa kuwa na wanawake wachache sasa hivi na sina haja ya kujali sana , si ndio?”
“Wife mawazo yako yanaenda mbali sana , kwanini niwe na mawazo hayo?”Aliongea Hamza huku jasho likianza kumtoka.
“Kweli!”
“Kabisa!”
“Ni kheri kama ni kweli , ila jaribu tena kwenda kwenye hivyo vilabu kwa ajili ya kukidhi haja zako , uone kama nitakuruhusu uniguse mwili wangu” Regina alionya.
“Siwezi kufanya hivyo , usiwe na wasiwasi kabisa mke wangu”
Regina macho yake yalichanua na alionekana mudi yake kurudi upya na palepale alisimama.
“Tuondoke sasa , muda umeenda”
“Wife hii ni fursa adhimu sana kwetu , unaona lile bonge la hoteli pale , unaonaje tukichukua chumba?”
Mzee Madilu kakutana na nani pale? Unadhani rafiki wa Regina ni nani?
Soma sura ya 'SEHEMU YA 242' kutoka riwaya 'Shetani rudisha akili zetu Africa' kwenye FasihiNet.
fasihinet.com
Ukitaka kuendelea kusoma, ingia fasihinet chapu, unaweza kununua coins moja kwa moja kupitia mtandao wa simu ama, nitafute mwenyewe watsapp nikupe pass ya bei nafuu.. episode 50 unasoma kwa elfu tatu tu. watsaap namba 0687151346