Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

235

Ingawa alijua alikuwa amemkosea Bi Mirum, lakini kitendo cha kufukuzwwa alijenga kinyongo.

Kwa Bibi yake Irene kutojihusisha tena na familia ya Regina ilikuwa ndio tamanio lake kubwa.

Ndio hivyo tu mambo yadunia hayawezi kuamuliwa na matumaini pekee, kwasababu kivuli cha asili yake ya bondeni hakikuwa kimempotea.

“Kwa maana hio , Irene ni mdogo wangu wa damu, yaani binamu?”Aliuli8za Regina na wakati akiongea maneno hayo moyo wake ulikuwa katika hali ya kutoeleweka.

Ni masaa machache tu alimwambia Irene asimwite dada nani angedhania baada ya muda angefahamu ni mdogo wake kweli na alistahili kuitwa dada,tena dada wa damu kabisa.

“Lakini mbona inashangaza , hata kama ni ndugu kwanini damu zao makundi yake ni sawa? Mbona ni kama ajabu hivi?”Aliongea Rhoda.

“Nadhani nimesikia kutoka kwa watu wa Bondeni , ukoo wa Dosa damu yake sio ya kawaida ndio maana wali tarajiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuvuna nishati . Lakini licha ya hivyo hakujawahi kutokea mtu mwenye uwezo mkubwa wa mafunzo katika ukoo. Au hili kundi la damu ni la kipekee , kwasababu kwa kumbukumbu zangu Madam na Mzee Dosam wote hawakuwa na kundi la damu kama hilo “Aliongea bibi yake Irene au Bi Tunu.

“Sidhani ni sahihi , kundi hili la damu lipo kisayansi , sidhani kama lina uhusiamo na mafunzo,au unasemeje Bro?”Aliuliza Rhoda.

“Mwili wa binadamu una siri nyingi ambazo hazina mwisho , sembuse kundi la damu, hata seli ndogo tu ya mwili imebeba siri nzito. Pengine kundi hili la damu ni la kisayansi tu na damu ya ukoo wa Dosa ina kitu kingine kikubwa zaidi kinachowindwa na aina hii ya kundi la damu ni udhihirisho wa kitu hicho”

Mara baaada ya kukumbuka uwezo wake wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi ulivyokuwa haraka na uwezo wa kutengeneza baridi alioupata , Regina aliishia kutingisha kichwa chake kukubaliana na Hamza.

“Ila kwanini watu wa Binamu walijaribu kumuua Irene, kwanini sio Regina , sio mimi au Mama? Au hawakujua uwepo wetu mwanzo?”Aliuliza Baba Irene.

“Haiwezekani , Binamu ina kitengo chenye teknoloijia ya intelijensia kubwa chini ya jua. Lazima walijua uwepo wako kipindi kile. Sababu pekee, inaweza kuwa katika kizazi hiki..”Aliongea Hamza na kisha akamwangalia Regina kwa hali ya wasiwasi.

“Damu ya ukoo katika mwili wa mke wangu inaonekana imeshaamka na kuanza kufanya kazi

. Labda wasiwasi wao ni Irene damu yake kuamka pia , hivyo waliamua kuchukua hatua za haraka.”Aliendelea kuongea Hamza.

“Mathias Huge alitaka kumchukua Irene kumpeleka kisiwani , lakini familia ya Dosal ilitaka kumuua Irene. Au ni kwasababu ...”Regina alionekana kukunja sura akihisi kitu katika akili yake na kisha akamalizia;

“Wanataka kumfanya Irene Kikaragosi?”

Hamza aliishia kumwangalia mke wake kwa namna ya kumkubali.

“Wife naona umefikiria kama mimi. Ni sahihi kabisa , Mzee Dosal na mwanae hofu yao ni nyie wawili kurudi na kuchukua nafasi zao . Ila Mathias anataka kuwategemea nyie kama Puppet ili kudili na wazee wa bondeni kuendelea kuwa na mamlaka. Wakati huo huo anataka kuwatumia nyie kupitia uwezo wenu ili kuweza kusoma kitabu kisichokuwa na maandishi. Kama Mathias akifanikiwa kusoma kitabu hicho na kujua kilichopo ndani yake , basi watu wa bondeni hawatojali tena kama kuna familia ya Dosa wala nini. Kwa lugha nyepesi nyie ndio ufunguo wa kusoma Wordless Book. Hivyo kama Mathias hataki kuwaua anachotaka ni kuwakamata ..”Kabla Hamza hajamalizia sentensi yake , ghafla tu sura yake ilijikunja na kumfanya ageuke .

Haikuchukua muda sauti ya kicheko ilisikika katika korido

“Kwa wanaonijua tu mnisikilize, Bro Hamza , ingawa upepo ni mwingi ila mwezi ni angavu. Unaoje ukinipa muda wako tukiongea kidogo , huku tukipata walau kinywaji nilichokuja nacho?”

“Mathias Huge!!”

Hamza macho yake yalichanu, hakutarajia awamu hio mkuu wa kitengo cha Binamu na kiongozi wa Bondeni angetoka kuja mwenyewe mpaka hapo.

Ilionekana umuhimu wa Regina na Irene kwa Binamu na watu wa bondeni ulikuwa mkubwa mno.

“Sina muda , lakini kama ni kukupiga muda nitakuwa nao wa kutosha”Aliongea Hamza katika hali ya ukauzu.

“Haha Bro nakupendea hapo kwenye kunyooka , kama ni hivyo basi nitakusubiri kwenye mgahawa uliopo karibu na hapa”aliongea

Licha ya kwamba sauti yake ilikuwa ikisikika , lakini hakuonekana kabisa na kila mmoja alimsikia akiongea na hata sauti yake kupotelea.

Bi Tunu mara baada ya kusikia jina la Mathias Huge kutajwa alijikuta akifubaa kwa hali ya woga.

“Mathiass Huge! Si ndio kiongozi wa Binamu.

Inamaana ametoka kisiwani mpaka huku kututafuta, tutafanya nini jsmsni kama anataka kutuua”Alionekana kupaniki.

Kama kijakazi wa familia ya Regina mara baada ya kujua , mkuu wa Binamu na bondeni kaja mpaka mjini kwa ajili yao , ilikuwa ni sahihi kupatwa na mshituko kiasi cha kuogopa.

“Mama hebu acha kuzidisha kupaniki? Nimesikia kuhusu Binamu ila mbona sijawahi kusikia chochote kuhusu Bondeni.

Mnamaanisha nini?”Aliongea Baba yake Irene.

Ukweli ni kwamba Binamu ilikuwa iikifahamika kwa watu wengi ambao walikuwa karibu na mfumo wa kitaarifa nyeti , ila wengi wao waliamini Binamu ni kitengo tu ambacho kinatawaliwa na watu wa mataifa makubwa , wasichojua nyuma yake ni kwamba Binamu ni jamii ama kitengo ilioanzishwa na watu ambao wana nguvu ila wakaamua kujificha sehemu ilioitwa Bondeni.

“Usije kukurupuka tu, hii ni Tanzania na upo mwenyewe hapa , ni ngumu kuweza kuanzisha vita na watu wa Binamu wewe peke yako”Alionya Regina aliemwangalia Hamza kwa wasiwasi.

“Mke wangu usiwe na wasiwasi , kitendo cha kuja kunitafuta maana yake ananiogopa. Vinginevyo si angenishambulia tu. Mimi mwenyewe sitaki kulikuza hili suala. Binamu ni jamii kubwa ya Daraja S yenye wafuasi kila kona ya dunia, sio jumuia ambayo unaweza kuifuta katika uso wa dunia kwa urahisi. Nataka kujua mtazamo wake ulivyo , kama tutaelewena basi hakuna haja ya kuwa na ugomvi na Binamu”Aliongea Hamza.

“Kingine wewe ni kama kiongozi wao wanaekusubiria na pengine siku moja unaweza kurudi , sasa akijaribu kupambana na wewe au kufanya chochote si itakuwa sawa na kuharibu misingi iliowekwa na wazee”Aliongea Hamza. “Hata mimi nafikiria hivyo hivyo , kama isingekuwa hivyo sidhani ningekuwa hai mpaka sasa”Aliongea Regina.

“Ndio maana nasema usiwe na wasiwasi mke wangu maana nipo hapa kukulinda . Natoka kwanza , ngoja nikaone anataka kuongea nini. Unaweza pia kumwambia Mjomba Pat kuhusu Bondeni”Aliongea Hamza.

Mara baada ya jina la mjomba kutajwa wote Bi Tunu na Baba Irene walijawa na hali ambazo hazielezeki kwenye nyuso zao.

Baada ya usiku huo familia mbili zenye majina ya baba tofauti zimekuywa ndugu , wawe wanataka au hawataki , ukweli hauwezi kubadilika.Hata hivyo mwanzoni hakukuwa na ugomvi kati ya Mzee Pat na Regina , ukweli ni kwamba Pat alimkubali sana Regina kwa makuzi yake tokea akiwa mdogo na mpaka mafanikio aliofikia, na ni mara nyingi alikuwa akimtumia kama mfano wa kuigwa kwa binti yake Irene.

Kitu pekee ambacho kiliwafanya kutojisikia vizuri , ni kutokana na ukatili wa Mzee Dosam na Bi Mirium waliowaonyeshea.

Lakini hayo yote hayakuwa yakimhusu Regina, isitoshe Regina mwenyewe alitelekezwa mpaka alipokuja kuchukuliwa . ilimchukua miaka mingi kabla ya kurudishwa katika ukoo wa Dosam.

“Najua , unaweza kwenda. Kuwa tu makini”aliongea Regina mara baada ya kusita kidogo kutokana na kauli ya Hamza ya kutaja jina la Mjomba.

“Mtu ambae anapaswa kuwa makini sio mimi bali ni Mathias Huge”

Mara baada ya kuongea maneno hayo Hamza moja kwa moja alitoweka katika korido hio na kwenda nje kuonana na Mathias Huge na kuwaachia upepo pekee.

Jambo hilo liliwafanya Bi Tunui na mwanae kushikwa na mshituko na kujikuta wakiuliza kwa sauti za kitetemeshi.

“Hamza... Huyu Hamza ni nani?”

“Mjomba nadhani kuuliza hilo swali kwasasa sio sahihi. Baadae ndio utakuja kumjua ni nani, ila kwasasa unapawa kujijua wewe ni nani kwanza”

Pat mara baada ya kusikia Regina anamwita kwa jina la mjomba , alijikuta akihisi hali isioelezeka katika moyo wake.

“Mkurugenzi Regina hujisikii vibaya juu yetu?”Aliuliza Bi Tunui.

“Kwaninii nijisikie vibaya juu yenu? Madam huna haja ya kuwa wasiwasi maana hakuna kibaya ulichokifanya. Ni babu yangu ndio wamewafanyia mabaya na sio nyie tu hata mama yangu. Mimi na mama tulitelekezwa kipindi cha nyuma , hivyo najua unachojisikia”

Sababu ambayo Regina hakuwa na hisia mbaya kuhusu ukweli huo ni kwasababu ya uzoefu aliopitia akiwa mtoto.

Katika moyo wake alitamani kuwa na familia na ni kipindi cha nyuma mwanafamilia mmoja baada ya mwingine aliondoka na kutangulia mbele za haki.

Sasa kutokea ndugu wengine ambao alikuwa na uhusiano nao wa damu kabisa , hakufikiria sana zaidi ya kuwakubali. Kitu pekee ambacho kilimfanya kutojisikia vibaya ni uhusiao wa Irene na Hamza.

“Nini! Wewe na mama yako pia mli..?” Bi Tunu alijikuta akishangaa

“Ni ukweli”

“Hivyo haina haja ya kuniita kwa cheo changu , unaweza kuniita tu kwa jina langu , isitoshe ulimzalia babu yangu mtoto hivyo moja kwa moja unakuwa bibi yangu . Lakini nitaendelea kukuita Madam Tunu kwasababu sitaki kuusaliti upendo wa bibi”Aliongea Regina.

“Naelewa hata usiwe na wasiwasi , mimi nitakuita Regina , wewe unaweza kuniita tu Shangazi kama unavyomwita Mariposa. Ukweli mimi na shangazi yako Mariposa wote tulikuwa wafanyakazi wa ndani wa familia yenu huko Bondeni. Mariposa ndio aliekuwa na kipaji hivyo aliweza kujifunza mafunzo ya mapigano , lakini mimi sikuwa na chochote hivyo kubakia kuwa mfanyakazi wa kawaida. Madam Mirium alinifukuza kwenye nyumba yake lakini ninachomshukuru hakunifanya chochote baada ya hapo, hata tulipojikuta kuwa majirani”

Licha ya kwamba Bi Tunu alikuwa na chuki zidi ya Dosam kwa kuwatelekeza na chuki zidi ya Bi Mirium kwa kumfukuza , lakni bado alikumbuka yale mema aliofanyiwa.

Yeye na Marip[osa tokea wakiwa wadogo waliandaliwa kuwa wafanyakazi ndani ya familia ya Mirium na kufanya waamini ndani kabisa ya mifupa yao watakwenda kuwa wafanyakazi maisha yao yote na ilikuwa furaha kwao.

Hivyo kufukuzwa kwake nusu ilikuwa ni sababu yake ya kukubali kuingiliwa kimwili na Dosam mpaka kupata ujauzito.

Sasa muda huo , Regina alikuwa hiari kuwapokea yeye na mwanae , ilikuwa ni furaha kubwa kwa Tunu.

Kwake yeye Regina alikuwa ni bosi wake mpya na kukubaliwa ni kama kurudishwa katika mstari ambao alitoka kwa muda mrefu , ilikuwa ni sawa na kurudishwa kwenye mzizi wa asili yake.

Ingawa Salim alikuwa akijisikia vibaya katika moyo wake , lakini kwa namna alivyomuona mama yake kuwa na furaha alijikuta akigoma kukataa.

Isitoshe Regina alikuwa tajiri kuliko yeye na alikuwa na nafasi kubwa pia huku akiwa na mume kama Hamza , kama angesema hajali nguvu waliokuwa nayo , angeonekana mnafiki tu.

“Basi sawa , kwanzia sasa nitakuita

Shangazi”Aliongea Regina , unaweza ukashangaa kwanini amuite shangazi lakini katika utamaduni wa watu wa bondeni , watu ambao sio wa damu lakini wanaishi ndani ya familia wanapewa cheo cha ushangazi na mara nyingi hao wote ni wafanyakazi wa familia. Shangazi kama Shangazi wa damu haitwi kwa jina hilo bali anapewa cheo cha Mama mkubwa au mama Mdogo.

“Hali kwasasa sio ya kawaida sana . Ngoja niwaelezee kile kinachoendelea ili baadae muwe tayari kukupambana na watu wa Bondeni...”aliongea Regina.

Regina alikuwa hospitalini akiwaambia Bi Tunu na mwanae juu ya hali inayoendelea huko bondeni , na juu ya suala la Bi Mirium kumpa kazi Hamza ili kuwazuia wasimguse.

Upande wa Hamza alifuatisha viashiria ambavyo viliachwa makusudi nyuma na Mathias Huge na kwenda kuingia kwenye mgahawa mmoja mkabala na chuo cha madaktari.

Ukweli ni kwamba mgahawa huo ulikuwa umeshafungwa tayari muda mrefu tu , lakini kama unavyomjua mtu kama Mathias Huge , ilikuwa rahisi kuingia katika mlango wowote ule kwa kufungua kitasa.

Hamza mara baada ya kushika komeo la mlango wa mgahawa huo ulikuwa wazi , hivyo alisukuma na kuingia ndani na kupandisha ngazi mpaka floor ya pili.

Hamza mara baada ya kukanyaga katika floo hio macho yake yalisinyaa mara baada ya kuhisi harufu ya damu , huku akimwangalia Mathias Huge aliekuwa amesimama kwenye Balkoni akiangalia mwezi na nyuma yake kwenye meza kukiwa na boksi.

“Bro hio ni zawadi ya salamu yangu kwako”aliongea mlowezi Mathias Huge akiwa amegeuka na tabasamu.

Hamza alitembea na kisha alifungua kiboksi kile na alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua ni kichwa cha mtu kilichokatwa kutoka kwa mwili wa binadamu.

“Huyu ni nani?”Aliuliza Hamza mara baada ya kutojua sura ya mtu huo.

“Jina lake anaitwa Zabo ni mwamnachama wa familia ya Dosa , ndio mtu aliemjeruhi Irene”Aliongea Mathias Huge.

“Najua Bro Hamza usingemwacha hivihivi tu , hivyo nikaamua kukupunguzia usumbufu kwa kukusaidia kukata kichwa chake”Mara baada ya kuona Hamza bado amenyamaza Mathias aliendelea.

“Bro kama huniamini unaweza kufuatilia mwenyewe na kuruhusu watu wako waliomuona akimjeruhi Irene kumtambua kama ndio yeye”

Hamza aliinua kichwa cha Zabo na kukirushia kwenye sakafu.

“Mkuregenzi mtendaji wa kitengo cha Binamu na mkuu wa watu wa Bonde , huwezi kunidanganya kwa jambo dogo kama hili”Aliongea Hamza na kisha alijimiminia kinywaji kilichokuwa kimeandaliwa juu ya meza na Mathais.

“Ingawa umemkata kichwa huyu ninja , lakini wewe ulituma watu kumteka Irene na watu wa familia ya Dosal walituma mtu kumuua. Hili ni deni ambalo bado halijalipwa”Aliongea Hamza.

“Bro nilichotaka nikumualika Irene kuja kisiwani kwetu pekee, sikupanga kumzuru wala sikupanga kumteka”Aliongea Mathias na kisha akaendelea.

“Isitoshe watu wangu tayari wamekwisha kuuliwa na watu wako na pia nimempoteza Msukule wa utumwa. Kuhusu Dosal na mtoto wake tokea mwanzo hawajawahi kunikubali kama kionagozi kutokana na asili yangu .. Bro ni kwamba tu hujui ila ni kazi ngumu sana kwangu kama kiongozi wa Bondeni”

“Basi acha kusumbuka , kama unadhani ni kazi kubwa kwako , nitamfanya mke wangu arudi Bondeni , ana damu safi ya urithi na kama akifika wazee hawatoendelea kumsapoti Dosal na mwanae . Na wewe hutopata usumbufu wa kufanya kazi ngumu tena”Aliongea Hamza akicheka.

“Shida Regina hajawa tayari bado na sio mimi tu ambae ni kiongozi ndani ya familia ya Huge, hivyo hivyo kwanzia kitengoni Binamu mpaka katika familia nyingi ndani ya Bonde. Bro nadhani hakuna haja ya kwenda mbali hivyo kwasasa”

“Mathias , ghafla tu ulienda kinyume na wazee wa baraza na kuamua kumteka Irene, Nadhani si kwasababu ya hiki nilichojua sasa hivi , kwa

Irene kuwa na uhusiano na mke wangu sio ndio? Kupitia kitengo chako cha Binamu na teknolojia yenu ya jicho la anga ni ngumu kama haukujua Tunu alikuwa na ujauzito wa mtoto wa Mzee Dosam. Lakini kwa miaka mingi baada ya kimya ghafla tu mnajitokeza na kutaka kumkamata . Ni kwasababu ipi?” Aliongea Hamza akimwangalia Msomi huyo moja kwa moja machoni bila hali ya utani.

Mathias Huge aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha mara baada ya kuona hawezi kumficha Hamza kitu mpaka kufikia hatua hio.

“Bro si nilikusikia ukifikia hitimisho kule hospitalini? Ndio , navutiwa zaidi na uwezo wa familia ya Dosa uliojificha katika damu yao” “Ni kama nilivyotegemea , unadhani Irene ana uwezo wa kipekee uliojificha katika damu yake?”

“Bado haifahamiki , lakini tukifuatilia historia ya urithi wa damu ambayo iliendelezwa miaka na miaka katika ukoo wa Dosa tokea enzi za kale. Inawezekana kabisa kizazi hiki kinaweza kuonyesha uwezo wa kipekee na inaweza kuwa njia ya kuweza kufasiri Worldless Book. Ni jambo muhimu zaidi sio tu kwa watu wa bondeni na wanachama wa kitengo cha Binamu, bali kwa dunia nzima”Aliongea Huge.

“Hebu acha kutaja dunia na Bondeni , hili ni kwa ajili ya familia yako? Ila kwasababu umeweka wazi kwa namna hio , Je unadhani nitakuacha ufanikiwe?”

“Bro naomba tu uniwie radhi , lakini unajua fika kwamba kati yetu hakuna atakaenufaika kama tukianza kupigana . Tutaishia tu kupata hasara na tena hata ushindi wetu unaweza usiwe na thamani yoyote”Aliongea Mathias akiwa na tabasamu ambalo sio tabasamu.

“Vipi kwani kama ikiwa ni hasara ? Wakati naanza vita takatifu kipindi kile sikuwa na tumaini lolote la ushindi. Kupigana na watu wa bondeni na kitengo chenu cha Binamu ni kazi nyepesi kwangu kuliko kupigana na muungano wa Baraza takatifu na watawala wa enzi . Vipi! Unadhani sina huo uthubutu?”
 
Mpango wa Subira.

Wakati Hamza akionyesha hali ya usiriasi, upande wa Mathias Huge hakuwa na nia ya kushindana na Hamza, na aliishia tu kuonyesha muonekano wa kawaida.

“Nadhani, Bro, umepanga kuwalinda Regina na Irene kisawasawa?”

“Kama sitaki kuwalinda, unataka nikupatie mke wangu na shemeji yangu kwa ajili ya kwenda kufunua hayo maajabu yako ya kijinga kuhusu Worldless Book? Mathias, ulikuwa na akili kumuua Zabo kwa kuonyesha uwajibikaji, lakini haimaanishi nakufurahia. Hata kama teknolojia yako ya Jicho la Anga inaona kila kitu, lakini mimi, Hamza, sikuogopi. Halafu, sio kama nyie watu ndio mnajua kila kitu. Vinginevyo, kwa nini mpaka sasa mnahangaika na kitabu kisichokuwa na maandishi?”

“Haha...” Mathias Huge, aliyekuwa kimya kwa muda kidogo, alijikuta akianza kucheka. Alipiga funda moja la kinywaji na kisha akashusha pumzi.

“Bro, kusema ukweli, nilikuwa nikidhani ulitegemea zaidi bahati na uwezo wako wa kuvuna nishati. Lakini sasa hivi nimegundua, akili yako na nafsi yako haijawahi kuwa na woga, na ndio msingi wa mafanikio yako. Wewe ni kati ya watu wachache ambao nahisi siwezi kuwashinda. Ila kwa nini upo kinyume sana na mimi?”

“Mimi sipo kama unavyodhani, na sina mafanikio mengi hayo unayofikiria. Mimi ni mtu wa kawaida tu ambaye nina msimamo wangu. Nitamuua mtu yoyote ambaye yupo kinyume na mimi, na kama mtu hakubaliani na mimi nitampiga mpaka akubali. Huu ulimwengu unaweza kuonekana kuwa na mikanganyiko mingi, lakini hayo mambo mengi yakija kwangu nayachukulia simple tu,” alisema Hamza akimwangalia Mathias Huge na tabasamu hafifu.

“Msomi, nadhani haufikirii nipo hapa kwa ajili ya kuongea na wewe tu?” Aliendelea kuongea, na pale pale Mathias Huge alianza kuhisi msisimko wa ari ya Hamza kuongezeka, ikiashiria kwamba anataka kupigana.

“Bro, hebu subiri kwanza. Hata kama unataka tupimane kidogo, lakini naomba unisikilize kwanza. Nataka tufanye dili.”

“Dili!?”

“Ndio, nina taarifa mbili ambazo ni muhimu sana kwako. Kama, Bro, upo tayari kutoa ushirikiano, nipo hiari kukuambia hizi taarifa zote. Nina uhakika lazima utavutiwa nazo,” alisema Mathias Huge.

“Oh! Zinahusiana na nini?” aliuliza Hamza.

“Ya kwanza inahusiana na maisha yako, Bro.”

“Huyo mtu anayetaka kuniua ana kila dakika na kila sekunde, lakini unajua tofauti ni nini?” alisema Hamza.

“Kama ni hivyo, Bro, hutaki kujua nini kilichompata mama yako mzazi?” alisema Mathias Huge, na kulikuwa na ishara ya fahari kwenye macho yake.

Hamza, kusikia kauli hiyo, moyo wake ulitingishika. Licha ya kwamba hakuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu mama yake, aliikumbuka sura yake.

“Si watu wa Binamu mlisema hamna taarifa yoyote kuhusu wazazi wangu na Mzee?” aliuliza Hamza huku akiwa na usiriasi wa hatari kwenye macho yake.

Alikuwa akikumbuka kabla ya kufika Tanzania, alishalipa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumjua Mzee alikuwa nani na vipi kuhusu mama yake na familia yake. Lakini watu wa Binamu na teknolojia yao ya Jicho la Anga walisema hawakuwa na taarifa yoyote, na ndio maana akaamua kuweka kambi nchini Tanzania.

“Ni kweli hatukuwa na taarifa yoyote wakati ule, lakini, Bro, baada ya kuingia nchini Tanzania, tulijaribu kuwasiliana na baadhi ya watu ambao tuliwapa kazi ya kukusanya ushahidi. Baada ya uchunguzi na upekuzi tukafikia kwenye...”

“Bro, wewe ndio kiongozi wa jamii ya kuogopwa ya INFERNO na vilevile una cheo cha Ugwiji. Kama huwezi kujua taarifa zozote zinazohusiana na wazazi wako, je, utajijua wewe ni nani? Unakubali kuendelea kuishi gizani?”

Hamza, muonekano wake ulikuwa ukibadilika-badilika. Akili yake ilikuwa katika machafuko, na aliishia kukunja ngumi tu na kuiachia. Kisha akamwangalia Mathias Huge na kuvunja ukimya.

“Unataka nini kama mbadilishano awamu hii? Au bado unataka pete?”

Macho ya Mathias Huge yalichanua mara baada ya kusikia kauli hiyo ya Hamza, na haraka sana alijiweka sawa na kuongea kwa sauti ya chini:

“Kwanza kabisa, nahitaji pete. Pili, nahitaji umuache Mkurugenzi Regina kufuatana nami kwenda kisiwani kwa muda wa mwezi mmoja.”

“Kumbe! Kwa hiyo hata mke wangu anapaswa kuchukuliwa awamu hii?”

“Sio kama napanga kumdhuru. Ninachotaka ni kuthibitisha baadhi ya vitu. Isitoshe, Wazee wa Bondeni hawawezi kuruhusu Regina kupatwa na shida yoyote, hivyo, Bro, unaweza kuwa na amani kabisa. Ukweli, Bro, haya mabadilishano hayawezi kukufanya upoteze chochote, maana hata hivyo pete haina msaada wowote kwako, au nakosea?” alisema Mathias Huge.

Hamza aliinamisha mwili wake kwenda mbele, akaweka mikono juu ya meza, kisha akamwangalia Mathias Huge kwa macho makavu.

“Msomi! Hivi bado haujaoa, si ndio?” aliuliza Hamza.

“Nilishaoa tokea miaka nane iliopita na nina watoto wawili sasa hivi, kwanini unauliza?”

“Oh! Basi nina uhakika ndoa yenu ilikuwa ni ya kupangiwa. Namaanisha wewe na mke wako lazima mtakuwa mlikutanishwa , si ndio ?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.

“Familia yangu ina sheria kali sana na pia mimi ni mtu bize sana , sina muda wa kufikiria masuala ya mahusiano baina ya mwanamke na mwanaume? Kutumia muda wangu kama ndege na upepo kufikiria masuala ya nani nimuoe sio jambo sahihi kwa mwanaume kufanya. Mke wangu na mimi tumekuwa pamoja kwa miaka nane na siku zote tumekuwa tukiheshimiana. Amenizalia watoto wawili , sioni dosari yoyote kutoka kwake”Alijitetea.

“Kwangu sijali kama unaona ni jambo zuri, kwangu mimi swali muhimu ni je mke wangu ana maana gani kwangu..”Aliongea Hamza huku sura yake ikizidi kukunjamana.

“Yaani bila wasiwasi kabisa unasema nikuazimishe mke wangu kwa mwezi mmoja , tena unaongea bila ya woga wowote? Kwa maneno yako pekee unastahili kifo...”

Kitendo cha kumaliza kauli hio iliambatana na mpasuko wa meza waliokuwa wameweka vikombe vyao na kipande kimoja kilienda kumvaa Mathias Huge kifauni.

Hata hivyo Mathias Huge alikuwa ni Gwiji na siku zote alikuwa makini sana anapokuwa mbele ya mtu kama Hamza , hivyo tukio lile haraka sana lilimshutua na kufyatuka kama mshale kurudi nyuma na kwa wakati mmoja alitumia nishati za mbingu na ardhi kupasua kioo cha dirisha na kupotelea nje.

Kama ingekuwa rahisi kumuua kiongozi wa Binamu na mkuu wa Bondeni , basi kitengo cha Binamu pekee kisingepewa hadhi ya daraja S.

Hamza nae hakuchelewa, kupitia dirisha lilelile alifyatuka na kupotelea nje.

Chini ya mwangaza wa mwezi , Mathias Huge alielea kama vile anavutwa na kamba na kwenda kutua katika paa la jengo lingine.

“Hamza hutaki kumjua Mzee ni nani , hutaki kumjua kwa undani Naomi Lindsey?”Aliongea Mathias mara baada ya kumuona Hamza ametua kwenye kingo ya paa la ghorofa alilokanyaga.

“Hata kama nataka kujua, nitafanya uchunguzi mimi mwenyewe . Siwezi kumuuza mke wangu kwa taarifa ?”

Aliongea Hamza na kisha palepale alikandamiza sakafu kwa nguvu na mguu kisha alifyatuka kama mshale kumsogelea Mathias Huge.

Mathias Huge aliishia kukunja sura tu , hakujua kwanini lakini alihisi kuna kitu hakipo sawa kutoka katika maneno ya Hamza na ilimfanya kujikuta akihisi hasira kutokana na tabia ya Hamza ya ugomvi.

“Kwasababu Bro umezidi ukorofi basi mimi mdogo wako sina jinsi zaidi ya kupambana na wewe kwa raundi kadhaa mpaka utakapotulia”

Mathias Huge aliekuwa amesimama juu ya ghorofa akimwangalia Hamza anaemsogelea , ghafla tu mwili wake wote ulifunikwa na mlipuko wa nishati yenye kutoa rangi nyeupe inayoelekea kuwa kijivu. Ilikuwa ni kama nishati ila ilikuwa ni kama jua lililokingwa na kifaa ambacho kiliakisi mwanga wake na kubadilika rangi.

Uwezo wa Mathias Huge wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ulikuwa katika levo ya ukamilifu. Kilichozingira mwili wake ilikuwa ni nishati ya kiroho ambayo ilikuwa na nguvu zaidi ya upako wa kawaida au nishati ya mbingu na ardhi ya kawaida inayotokana na asili ya elementi nne za ulimwengu .

Mbinu na sanaa yake ya kimapigasno ilikuwa bora na kufikia ukamilifu kutokana na daraja la kinishati alilokuwepo.

Mara baada ya kuona Hamza amemkaribia na anataka kumshambulia haraka sana aliinua mkono wake na kama vile anapunga upepo , nishati ilisikika katika sauti ya mluzi na kwenda kumvaa Hamza.

“Boom!!”

Kutokana na mlipuko huo , Hamza alihisi ni kama vile kuna bomu limelipuliwa mbele yake na presha ya mlipuko huo kumfyatua kwenda mbali.

Kama isingekuwa utimamu usiokuwa wa kawaida wa mwili wa Hamza, mtu wa kawaida angeshageuzwa vipande vipande vya nyama.

“Nishati kubwa sana hii !”

Aliongea Hamza huku akiangalia mavazi yake ambayo yalikuwa yameshachanika na kubaki vipande vipande na kufanya mwili wake uliojengeka kuonekana.

“Bro hata wewe uwezo wako sio wa kawaida , ni adimu sana mtu kuhimili shambulizi langu la presha ya nishati ya mbinu na ardhi”Aliongea Mathias Huge na kisha palepale alinyoosha mkono juu na ghafla tu feni la kujipepea lilionekana katika mkono wake .

Feni lile lilionekana kutengenezwa na malighafi ambazo si za kawaida kuhimili presha ya mlipuko wa nguvu alioachia.

Hamza palepale alihisi kama asipogawanyisha mwili wake , anaweza asiwe na uwezo wa kuhimili mashambulizi ya Mathias. Lakini ilikuwa ni kwa bahati kwamba alikuwa amegundua jambo muhimu sana hivi karibuni juu ya uhusiano ulipo kati ya nishati ya ndani ya mwili na nishati ya mbingu na ardhi.

Muda huo alitaka kutumia ufunuo aliokwisha kupata zidi ya Mathias Huge kuona kama anaweza kumdhibiti.

Hamza palepale alifikiria mbinu nzuri zaidi ya kutumia uwezo wake na palepale wazo lilimjia na kumwemwesa maneno kwa lugha ya kingereza ‘Long Fist’.

Long Fist ni aina ya sanaa ya kimapigano ya kale, ilikuwa na vigez o vyake na mazingatio, mosi ili kutumia ngumi ya mbali au Long Fist unapaswa kuweka umakini katika mjongeo wa mikono na miguu yako , sio mbinu kubwa sana katika mapigano lakini ilikuwa ya kuonyesha msingi wa kawaida kabisa katika sanaa ya kupigana. Kwa ufupi ni mbinu ambayo hutumiwa na wacheza ndondi katika harakati za kujihami bila ya kuwa karibu na mshindani.

Sasa mpango wa Hamza ilikuwa ni kutaka kutengeneza koneksheni kati ya nishati za mbingu na ardhi na nguvu ya ngumi yake ili kumdhibiti adui bila ya kumsogelea karibu. Hakuhitaji aina ya mapigano ya juu sana, alichotaka ni kutumia uelewa aliokuwa nao kuonyesha nguvu yake.

Kadri aina ya shambulizi linavyoonekana kuwa la kawaida ndio njia rahisi ya kuficha nia ya shambulizi.

Hamza alikunja miguu yake ili kushusha kituo cha uzito wa mwili wake na kisha akaituliza akili yakee. Palepale alipiga hatua pana kwenda mbele na kisha akairusha ngumi yake.

Hamza mara baada ya kurusha ngumi hio ya mbali hakuwa na mawazo mengi , ila alikuwa na wazo moja tu la upekee, ambalo ni nia ya kumharibu adui yake.

Muda ambao Mathias Huge alikuwa akijiuliza kwanini Hamza anataka kushambuliana nae kwa mbinu ya kawaida ya kurusha ngumi ya mbali na kuona ni kama Hamza amemdharau , alijikuta akigundua mara baada ya ngumi ile kurushwa hewani. Alihisi nguvu isiokuwa ya kawaida kama ya vichomi iliokuwa ikiusogelea mwili wake kumshambulia.

“Nini hiki!”Alijikuta akipaniki na palepale haraka sana alifyatua nishati ya mbingu na ardhi na kupambana na nguvu ile isionekana.

“Bam!”

Kwa mlipuko mkubwa, nishati yake ililipuka mara baada ya kumtoka na kugusana na ile ya Hamza isionekana.

Sasa kabla hata hajafikiria, ghafla tu Hamza huyu hapa mbele yake kwa kuruka sarakasi ndefu kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.

Ngumi mfyeko , ngumi mcharazo , ngumi mpasuo na kuendelea...

Hamza urushaji wake wa ngumi ulikuwa ni kama vile amegeuka na kuwa kivuli , ukijumlisha na nguvu ya miguu yak, yalikuwa ni mashambulizi ya ngumi ambayo yalikuwa yakitoa wakati mgumu sana kwa adui.

Mathias Huge aliishia tu kukwepa ngumi zile na hata kutumia feni alioshikilia mkononi kujikinga, lakini mashambulizi yalimzidia na kujikuta akirudi nyuma.

Alijikuta akishangaa kwa kuona siku zote nishati yake ya mbinu na ardhi imefikia katika ukamilifu , lakini ajabu hakuweza kumshambulia Hamza kwa pigo lolote zaidi ya kupangua mashambulizi.

Wawili hao walijikuta wakipigana kwa kufukuziana kutoka jengo moje kwenda kwenye paa la jengo lingine. Spidi yao ilikuwa kubwa mno na kufanya waonekane kama vivuli pekee vilivyokuwa vikiruka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi na nguvu isioonekana ya ngumi ya Hamza ilikusanya upepo mwingi na kusababisha eneo lote kuonekana kama vile limekumbwa na kimbunga.

Ilikuwa ni kwa bahati tu walikuwa wakichagua majengo ambayo ujenzi wake ulikuwa ukiendelea , la sivyo ingewaogopesha watu na kufanya hata polisi kuwahi katika eneo hilo .

Hamza aligundua , ingawa ameweza kupanda katika daraja ambalo anaweza kutumia nguvu ya mbingu na ardhi bila ya kuivuna, licha ya kwamba ni kidogo lakini ilimtosha kabisa kupambana na mtu kama Mathias Huge ambae mafunzo yake yalikuwa ya juu sana.

Uzuri pia ni kwamba kwa wavuna nisahti wengi , mafunzo yao yalitegemea ufunuo wa shambulizi la aina moja , hivyo ilimpa nafasi ya kupangilia mashambulizi yake bila ya kuhofia adui yake kuwa na shambulizi la ajabu la kumshitukiza.

Hamza alitumia mbinu za kawaida kabisa za mapigano kutengeneza nishati isioonekana kumshambulia Mathias.

Upande wa Mathias Huge ambae pambano alilichukulia kama utani mwanzo, aliacha kufikiria hivyo tena na kuwa siriasi, na kuanza kuwa katika umakini mkubwa wa kuita na kutumia uwezo wake. Ingawa kwa mtu kama yeye kwa wakati huo hakuonekana kama vile anapigana kwa ajili ya kuua , lakini haikumaanisha uwezo wake ulikuwa mdogo.

Mathias Huge alisifika kwa kuficha uwezo wake na alionyesha kidogo tu siku zote.Pengine ni kwasababu hajawahi kupigana na mtu ambae ana uwezo mkubwa kuliko wake au wa kulingana nae ki uwezo.

Ingawa hakuweza kufahamu Hamza amefanikiwa vipi kuzuia mashambulizi yake bila ya kuwa na nishati yoyote ya mbingu na ardhi , lakini hakuwa na muda wa kufikia mpaka kufikia hapo.

Hata hivyo aliona ni ngumu kwa mtu ambae hakuwa na mafunzo ya nishati ya mbinu na ardhi kuzuia mapigo yake kwa muda mrefu , hivyo alikuwa akijiamini kushinda.

Palepale Mathias Huge alificha lile feni mkononi mwake na kisha alichanua mikono yake yote juu huku akikanyaga chini ya sakafu na vidole na kunesa nesa kama vile anacheza ngoma

“Maumbo nane akisi , muundo wa ndege anaepaa”

Mathias Huge muonekano wake ulianza kubadilika badilika kadri alivyokuwa akinesa nesa kwa kumzunguka Hamza. Miondoko yake ilichukukua sekunde moja tu spidi ilizidi kuongezeka kwa kasi kubwa sana na palepale kadri alivyokuwa akiongeza spidi muonekano wake ulianza kujigawa katika maumbo mengi.

Ghafla tu Mathias Huge aligawanyika mara nane kwa kutengeneza udanganyifu wa macho na kumfanya mtu kutokujua halisi ni yupi.

Hamza palepale alionyesha na yeye staili kama vile miguu yake ilikuwa ikididimia ardhini huku akijizungusha kama pia , ilikuwa mbinu maalumu ya kupunguza umbali kati yake na Mathias Huge halisi haraka iwezekanavyo.

Kadri alivyokuwa akizunguka kwa spidi alionekana kufuta yale maumbo ya Mathias Huge na aliendelea kwa spidi zaidi na hatimae alionekana Mathias Huge peke yake na palepale alipiga kibao hewani kumlenga.

Nguvu iliotoka katika kibao kile ilikuwa ni kama dhoruba kubwa ya upepo ambayo ilikuwa ikimsogelea.

Mathias alijikuta akihisi ubaridi katika moyo wake , mara ya mwisho kukutana na Hamza hakudhania angeweza kuwa na uwezo wa nguvu isionekana kama hio. Ingawa kulikuwa na taarifa ilioonyesha Hamza uwezo wake umepanda na kumuua Skellidoni lakini hakuona uwezo huo wa Hamza uliozungumziwa kwa macho yake.

Lakini hata hivyo sio kama hakuwa na chakufanya, nishati yake ya mbingu na ardhi ilikuwa ikimzunguka mwili mzima, kupitia matundu makubwa ya jasho na vituo maalumu vya bahati vya utendaji wa mwili wake , viliongeza kwa kiasi kubwa nguvu yake.

“Mbavu za Chui!!”Aliongea kwa nguvu na kisha yeye pia alirusha kiganja cha mkono wake kama vile alikuwa akikinga mwanga usiumize macho yake na palepale kulitokea mlipuko mkubwa wa nishati ya mbingu na ardhi uliokwenda kugongana na nguvu aliotuma Hamza na kisha wote wawili waliruka kwenda nyuma na eneo nguvu zile zilipokutana katika jengo ambalo ndio floor inamwagiwa zege ilititia.

“Binam Eight Diagram Arrys!!”

Hamza alishawahi kusikia , kuna mbinu ya mapigano huko Bondeni ambayo ilikuwa ikitumika. Mbinu ambayo ilikuwa ikimgawanya mtu na kuonekana mara nane kwa kutegemea spidi yake pekee ya mzunguko.

Alisikia mbinu hio sio tu kwa ajili ya kumfanya mpiganaji kuwa na uwezo mkubwa , lakini vilevile ilikuwa ni mbinu ambayo iliazima nguvu kwa wanajeshi wengine katika uwanja wa mapigano.

Inasemekana tokea mwanzo watu wa Bondeni ambao walihitaji cheo katika ulinzi , kama vile kuwa majenerali na kuendelea walipaswa kuweza kutengeneza maumbo nane , ilikuwa ni kama kigezo na ilitumika nguvu kubwa na miaka mingi mpaka kufanikiwa kutengeneza maumbo nane, wengi waliishia kaitka maumbo mawili au manne pekee.

Kama sio mbinu hio Hamza angeweza kufanikisha kumuadhibu Mathias kisawasawa na shambulizi lake, lakini hata hivyo Hamza aliridhika katika moyo wake. Kwasababu kupitia ufunuo aliopata ameweza kufuta maumbo yote nane na kisha kushambulia na nguvu kubwa ambayo ilionekana kulingana na nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi aliokuwa nayo Mathias Huge.

Hamza aliona alikuwa na nafasi kubwa ya kupanda levo ya juu kabisa ya kuelewa muunganiko uliopo kati ya nguvu yake ya ndani na nishati za mbingu na ardhi, pengine bila ya kuvuna nishati hizo anaweza kufika daraja la juu la kutumia nishati hio kwa uhuru kabisa, labda kwa kulingana na mtu wa daraja la juu kabisa la mafunzo au kwenda mbali zaidi katika madaraja ambayo hajawahi kufikiwa na binadamu.

Licha ya Hamza kutumia mbinu ya ngumi na kiganja cha mkono kwenye kushambulia , mbinu hio kwa asilimia mia moja haikupaswa kuitwa nia ya siraha , ilikuwa ni mbinu ya kawaida tu ya mapigano iliojaa makusudio.

Mbinu ambayo ilikuwa ni ya kisiraha kwa asilimia moja ni ileile ambayo aliitumia kumshinda Skellidoni na kumuua , nia ya siraha au manuio ya kisiraha.

Hamza macho yake yalicheza na palepale aliinua mkono wake na kuweka katika staili ya karate huku ncha ya vidole vyake vikiangalia juu angani kama ameshikilia kitu na kisha palepale alifanya shambulizi la kawaida kama vile anajaribu kuigizia upanga unavyokata.

“Nia ya kisiraha!!”

Mathias Huge alihisi kuna kitu hakipo sawa mara baada ya kumuona Hamza akiwa ameinua mkono wake juu angani kwa staili kama vile alikuwa ameshikilia upanga kwenye mkono wake. Lakini kwa wakati mmoja hakujua kwanini , ila alihisi ni kama Hamza ameshika upanga kweli ambao haukuwa ukionekana katika mikono yake.

“Bro ni mbinu gani hio unayotumia. Hakika una bahati sana”Aliongea Mathias akishindwa kuzuia hisia zake na kukubali tu.

Hamza mwonekano wake ulikuwa hauelezeki , muda huo ni kama vile hakuwa katika mazingira ya dunia na alikuwa kwenye ulimwengu mwingine ambao alikuwa akifanya mawasiliano baina ya siraha yake ya kiimani kwenye mikono yake na nishati za mbingu na ardhi.

Miguu yake ilisogea kwa muunganiko wa kila kiungo katika mwili wake. Ile anafyeka kwa kuchezesha mkono wake kama vile anaigiza, ilikuwa ni kama vile ghafla umetokea upanga usioonekana mkubwa sana na wenye makali na kukata hewa.

Hewa yenyewe ilitoa mlio wa ‘ swiii’ kama vile ilikuwa ikilalamika Hamza kuachia shambulizi la namna hio na kuiumiza.

Mathias Huge hakuhisi mabadiliko yoyote ya kinishati katika mazingira, wala hakuhisi kabisa nguvu zozote zinazotoka kwa Hamza , ila aliweza kuhisi kuna kitu kilichokuwa kikimsogelea na kinakwenda kumtenganisha vipande viwili.

“Uchawi wa muundo wa nyoka!!”

Mathias Huge mwili wake ulififia na kuruka kwa kujitoa katika usawa wa shambulizi la siraha isionekana.

“Boom!”

Ulikuwa ni mtikisiko mkubwa wa jengo , huku nguzo ambazo zilikuwa zimesimamishwa katika floor hio zikisambaratika na kubakisha nondo pekee zilizoinama.

Mathias Huge alijikuta akigeuka na kuangalia kile kilichotokea na alijikuta mwili wake ukikakamaa. Jambo ambalo lilimwogopesha sio ukali wa shambulizi la Hamza , bali ni kutokuelewa namna shambulizi lake lilivyo aa alivyolifanikisha.

Alijikuta akijiuliza kwa hamaki kubwa ni kitu gani kimetokea , sio nishati , sio miujiza wala sio uchawi , ni nishati gani yenye nguvu Hamza anatumiua?.

Hamza hakuishia pale , kwani aliruka huku upepo ukimfukuza kama vile unamsindikiza wakati akimsogelea Mathiasi Huge.

Mathias Huge mara baada ya kuhisi hali sio shwari kwake, alijikuta akiruka majengo mawili mfululizo na kwenda kutua katika paa la jengo la Apartment.

“Bro subiri kidogo!”

Aliongea kwa nguvu mara baada ya kuona Hamza alikuwa akimfukuzia , huku akihisi hali sio shwari kwake.

“Mimi mdogo wako nina jambo nataka kuongea.
 
“Sitaki kulisikia”

Hamza hakujali bwana huyo anataka kuongea nini , yeye alikuwa akifurahia hisia nzuri za kupigana hivyo hakutaka pambano lisitishwe. Pia hakuwa na uhakika kama anaweza kumuua ila alihisi itakuwa vizuri kama akimpa kibano cha kueleweka.

Mathias Huge uso uligeuka wa kijani , hajawahi kuona mtu mpuuzi kama Hamza anaetaka kupigana bila sababu , yaani yeye kama mkuu wa Binam,Bondeni na Gwiji mwenzake hataki hata kumpa nafasi ya kuongea neno moja?.

Kabla hata Mathias Huge hajajua cha kufanya , Hamza alikwisha fika mbele yake. Mathias alijikuta hana jinsi zaidi ya kung’ata meno yake kwa hasira na kisha palepale aliita nishati ya mbingu na ardhi na kuizungusha katika mwili wake ili kutengeneza kinga.

“Mlima wa nishati!”

Aliongea kwa sauti kubwa na paleplae nguvu kubwa ya nishati ilitokea mbele yake na kutengeneza mlima wa kuzuia shambulizi la Hamza. Mpaka kufikia hapo aliona kwanza ajilinde na kushambulia ni swala la pili.

Hamza mara baada ya kushambulia, Mathias alifanikiwa kukwepa shambulizi lile huku akikimbia kwa wakati mmoja.

Hamza mara baada ya kumuona Mathias anakimbia na yeye hakubakia nyuma alianza kumfukuzia , nguvu ya miguu Hamza aliojifunza ilimpa uwezo wa kuwa sambamba na mtu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.

Muda mfupi walijikuta ndani ya msitu mkabala na fukwe na waliendelea kushambuliana mpaka kwenye maji na kisha kurudi kwenye maegesho ya magari ya club za pembeni ya fukwe.

Watu waliokuwa karibu na njiani walijikuta wakishituka , mara baada ya kupitiwa na upepo mwingi , lakini hawakuweza kuona kitu zaidi ya kuhisi ni hali ya kawaida ya mabadiliko ya hewa baharini.

Baada ya kufukuzana na Mathias Huge kwa muda, hatimae Hamza aliweza kupata uelewa wa juu zaidi kati ya nguvu yake ya ndani na nguvu ya nje yaani nishati ya mbingu na ardhi.

Mara baada ya kurudi tena usawa wa miti , alivunja tawi na kuligeuza kama siraha na kisha alimnyooshea Mathias Huge aliekuwa akimwangalia Hamza kwa macho ya kutia huruma.

Mathias Huge aligundua ni kama Hamza alikuwa akifanyia majaribio kitu kipya kupitia yeye na amekigundua , hivyo kufanya ukaribu wao kuzidi kupungua sekunde na sekunde.

“Shaa !Shaa! Shaa”

Hamza alifyatua lile tawi kulenga uelekeo wa Mathias kwa mara tatu kwa angle zote. Mathias Huge aliishia kuhisi nguvu ya ajabu ikimshambulia na alijikuta akikosa jinsi na kuamua kuacha kukimbia na kupambana na Hamza ana kwa ana.

Palepale alibadilisha mbinu ya mashambulizi na kutumia mbinu yake yambavu za chui, aliamua kuweka nguvu zake zote katika kazi ili kupambana na Hamza.

Nishati ya rangi ya kijivu iliokuwa ikimzingira , ilikuwa ni kama mafuriko ambayo yalitaka kumvaa Hamza.

Hamza alishangazwa na ukubwa wa nguvu aliokuwa akionyesha Mathias Huge mara baada ya kusimama , lakini hakuwa na hofu ya kupambana nae, alitumia tawi aliloshikilia mkononi mwake kulivika nguvu yake ya ndani na kwa wakati mmoja akiwianisha na nishati ya nje ya mwili wake.

Hamza mara baada ya kuhisi shambulizi zito kutoka kwa Mathias Huge palepale kwa siraha yake alipanga kugeuza shambulizi lile uelekeo kwenda juu na haraka sana alipiga sarakasi na kuachia shambulizi lingine mcharazo kwa chini na kumlenga Mathiasi kama vile anataka kumkata miguu.

Mathias alijikuta akipatwa na mshituko , hakuwahi kuona mtu ambae hakuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kuwa na uwezo wa kutumia nishati hio na kisha kuitumia kubadilisha uelekeo wa shambulizi lake tena kwa kutumia tawi la mti pekee.

Kama isingekuwa yeye mwenyewe ndio anaepigana , basi angependezwa zaidi awe yeye ndio anaangalia , ili kuona kwa uwazi kile Hamza anachofanya na pengine angejifunza kitu.

Mara baada ya kuona Hamza amemshambulia kwa mara nyingine, alichokifanya ni kuruka hewani na kukaa kama anaogelea na kufanya shambulizi lile kupita katika tumbo lake, lakini sasa licha ya kwamba amefanikiwa kukwepa shambulizi hilo, lakini mkondo wa upepo uliombatana na vichomi , uliipitia sura yake na kumfanya uso wake kuchanika na kutokwa na damu.

“Arghhhhh!”

Mathias Huge aliona hali si nzuri hata kidogo na palepale , hakutaka kupigana na Hamza tena na alitimua nduki bila ya kuangalia nyuma, aliona angekuwa mfu kama angekosea kidogo tu kukwepa shambulizi lile. Aliishia kujiuliza inamaana huyu mshenzi Lucifer alikuwa siriasi kumuua na sio kama wanapimana nguvu tu?

Hamza alijikuta akicheka kwa nguvu , nani angedhania mtu ambae hana mafunzo yoyote ya nishati ya mbingu na ardhi angemfanya mtu aliejifunza nishati kwa miaka mingi na kufikia levo za juu kukimbia kama hivyo , tena gwiji , kiongozi wa watu wa Bondeni na Binam?.

Jambo hilo lilimfanya Hamza sasa kujiamini kwa asilimia mia moja , njia ambayo amechagua hakukosea kabisa, hakuhitaji kuvuna nishati ili kutumia nishati ya mbingu na ardhi , alichohitaji ni kuboresha mwili wake na nia yake ili kuweza kumiliki kila kitu.

Palepale alijikuta akiingiwa na wazo lingine mujarabu , alihisi kama atamuua Mathias Huge moja kwa moja angepelekea machafuko ndani ya Binam na Bondeni na ingekuwa namna rahisi ya kumfanya Regina kuwa kiongozi. Kwa mahesabu hayo Hamza aliona ni muda sahihi wa kumuua Mathias Huge moja kwa moja , lakini ile anapanga kumfukuzia ili kumshambulia , ghafla tu watu wawili walitokeza mbele yake na kumkinga Mathias kwa mbele.

“Mzee Elish! Mzee Elkim!”

Mathias Huge mara baada ya kuhisi uwepo wa wazee hao haraka sana aligeuka na kuwagundua ni wakina nani na alijikuta akipatwa na ahueni na kuacha kukimbia na kwenda kutua kwenye jengo lingine akifuatiwa na wale wazee.

Hamza mara baada ya kuona wanaume hao waliovalia mavazi ya suti tupu , alijikuta akilaani ndani kwa ndani kwani wazee hao walionekana kutokuwa wa kawaida kabisa , wote walionekana kuwa katika levo ya nafsi mkandamizo na palepale hisia nyingine zilimwambia pengine kuna wengi zaidi waliokuwa wakisogelea eneo hilo.

Mathias Huge mara baada ya kuona msaada umefika , alijikuta akirudiwa na kujiamini kwake.

“Bro Hamza! Bado tu unataka kuendelea?”

Hamza hakuwa mjinga , tayari alishawafanya wazee hao wa Bondeni kuja mpaka hapo , hivyo aliona apunguz ujeuri wake kidogo.

Isitoshe watu hao waliofika hapo , walikuwa na mafunzo ya juu ya nishati za mbingu na ardhi na walionekana wapo kwa lolote kumlinda Mathias Huge na pia ilionyesha ni dhahiri wana mbinu ya kuwasiliana na wenzao kama wakizidiwa.

Kilichomshangaza Hamza ni kwamba wazee hao wote walikuwa ni weusi maana yake walikuwa ndio Wazawa. Hamza aliona ndio maana kwa muda mrefu Regina alikuwa salama na familia nzima haikuguswa kumbe kulikuwa na wazawa kama hao wenye mafunzo ya juu tena weusi ambao wamejichimbia tu bila kujionyesha.

Unachopaswa kuelewa ni kwamba Bondeni familia ya Huge pekee ndio ilikuwa ya kizungu na ndio familia iliochukuliwa ya kufikia tofauti na weusi wenyewe ambao walijichukulia wazawa au waasisi.

Licha ya kwamba familia ya Huge ilikuwa na madaraka ya ki uongozi , lakini hawakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwasababu hawakuwa na nguvu za kutosha kuzidi wazawa.

Hamza alijikuta akiwaangalia wazee hao waliofika hapo na alijiktua akipatwa na wasiwasi akihisi hatokuwa na uwezo wa kuwadhibiti, walionekana sio wazee wa umri mchache, hivyo uzoefu wao ungekuwa mkubwa zaidi na inaweza kuwa hasara kwa upande wake.

“Haha.. nilichotaka ni kushindana na mtu kama wewe pekee”Aliongea Hamza na kumfanya Mathias mara baada ya kusikia hivyo kutaka kutapika unafiki wa Hamza.

“Bro huku ni kushindana kwa aina gani? Nilihisi kabisa unataka kuniua ili kufanya Bondeni na Binamu kupatwwa na machafuko”Aliongea

“Nini! Lucifer kivipi kuwa na mawazo ya namna hio! Sisi watu wa Binamu tupo kwa ajili yako hapa , lakini wewe unakejeli msaada wetu kwa kutaka kumuua kiongozi wetu?”Aliongea Mzee mmoja kwa ukali.

“Hata kama umeweza kushinda vita takatifu , haimaanishi unao uwezo wa kushindana na watu wa jicho la ufunuo”Aliongezea mwingine.

“Acheni kupaniki! Sikuwa na mpango mnao waza , nilichotaka ni kuwafikishia ujumbe tu”aliongea Hamza

“Nini! Ujumbe gani?”

“Siku nyingine msije kunichokoza , wala kuwa na mipango yoyote juu ya mke wangu. Sijali ni wanawake wangapi wana uhusiano na asili yenu, kwa kufupisha tu , hili lililotokea leo likijirudia tena nawaahidi mtajuta”

“Unakiburi sana Lucifer! Kama usingemuoa Regina na ukamuumiza kiongozi wetu tungekuadhibu vikali. Unatoa wapi uthubutu wa kujibishana na sisi?”

“Haina haja ya kumuingiza mke wangu hapa. Mimi sina asili yoyote na watu wenu wa Bondeni , halafu msijifanye mpo juu mkidhani sijui nyie wote wawili hamna uhusiano wowote na familia ya Dosa na hampo upande wao , kwanzia mwanzo mpaka sasa hamjahawahi kuwa na nia nzuri juu yangu kwasababu ya mke wangu na lazima mtakuwa mnatamani lolote linikute , si ndio”

“Unaongea ujinga! Wazee wetu ni wamoja , kwanini kuwe na mgawanyiko kwasababu ya majina ya kifamilia?”Aliongea Mathias.

“Kama ni hivyo basi sitaki kuendelea kuongea. Nyie ndio mnajua mnachofikiria na mimi nishaongea na nimemaliza , kama mnataka kumsaidia Mathias , mnakaribishwa muda wowote kushindana na mimi”

Hamza hakuongea neno lingine zaidi na palepale alifyatuka mara mbili na kupotelea ueleko wa hospitalini.

Mara baada ya kuona Hamza ameondoka , wazee hao waliokuwa katika mavazi ya suti waliishia tu kukunja sura zao.

“Mkuu wa ufunuo wa jicho , vipi tumfukuzie?”Aliuliza mmoja wao.

“Haina haja , lazima atakuwa na mbinu nyingine ameificha,hata kama sisi wote watatu tushirikiane kushambuliana nae tunaweza tusimshinde”

“Lakini amekuumiza na ameharibu taswira ya fahari ya jamii yetu”

“Watu ambao wamepangwa kuwa muhimu hawana haja ya kujali mambo madogo madogo zaidi ya kukubali kuharibiwa kwa nje. Nikifanya uficho mdogo sana wa nilipoumia , hakuna wa kuweza kuona , haikuwa na haja ya kwenda mbali na kumchokoza”Aliongea.

“Huyu Lucifer mbona ana nguvu hivi, yaani ameweza kumuumiza mkuu wetu. Kulingana na intelijensia yetu , si alikuwa dhaifu kuliko wewe miaka mitano iliopita?”Aliuliza

“Mzee Elkim , wewe pamoja na mzee Elish ni miaka ishirini sasa lakini mpo hatua ya awali tu ya mkandamizo wa nafsi?”

“Upo sahihi .. ndio kwanza tupo katika daraja la mkandamizo wa nafsi , lakini ni wazee namna hii na hata uwezo wetu wa akili pia unapungua na pia inatuwia vigumu kuweza kuhimili uwezo wetu , sembuse kwenda mbele zaidi”Aliongea Mzee Elkim.

“Mkuu kwanini umekumbushia hili?”Aliuliza Mzee Elish.

“Kwa nyie wote wawili kuweza kufikia daraja la mkandamizo wa nafsi mnachukuliwa kama watu wenye vipaji , lakini hebu fikiria huyu Lucifer akiwa tu na miaka kumi na nane alikuwa amekwisha ingia katika levo ya Mkandamizo wa nafsi , ni tofauti zaidi ya miaka sitini na nyie. Kipaji chake likija suala la mafunzo ,uvumilivu na uimara wa kuvumilia upweke ni kitu ambacho hamuwezi kudhania. Miaka mitano iliopita ilikuwa ni kweli ni dhaifu kuliko mimi , lakini kwa kipaji chake haishangazi anaweza kunipita mbali ndani ya miaka mitano ijayo…”

Mzee Elkim na Elish waliangaliana na kuona alikuwa ameongea kimantiki.

“Kulingana na historia ya maandishi yaliorekodiwa katika maktaba zetu vizazi na vizazi , wanajeshi wengi waliowahi kuwa na nguvu na kuutawala ulimwengu , wote wanatabia moja ambayo ni ‘Wewe tangulia, mimi nakuja mdogo mdogo’.

Ukiwafuatilia hao wataalamu , utagundua wote hawana mbinu za kuchanganya sana , kinyume chake kila muda unavyoenda wanazidi kuimarika, ni kama vile hawajali kile kinachowatokea katika maisha yao na kuacha asili iamue , hivyo kufanya iwe ngumu sana kwa wengine kuwaiga ama kuwakadiria.

Huyu Hamza wasasa ananikumbusha stori za magwiji wengi katika vitabu vya historia.. yaani anaonekana yupo yupo tu , hayupo siriasi lakini uwezo wake unaimarika kwa hali ambayo inashindikana kueleweka”

“Kwa bosi kama wewe kuweza kumkadiria kwa daraja la juu inaonekana kweli sisi wote watatu hatumuwezi”Aliongea Mzee Elish.

“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi , msingi wa jamii yetu sio kumiliki kila kitu kwa nguvu. Ubongo ndio muhimu zaidi kuliko ngumi”Aliongea Mathias.

“Leo , nyie wazee wawili mmekuja mpaka huku na mimi , na nawashukuru sana , nilikuwa na wasiwasi Hamza atakuwa mgumu kunielewa , ni kwa bahati nzuri tumefanikiwa kulizuia hili”

“Unakaribishwa kiongozi wa jicho la ufunuo muda wowote, lakni vipi , una mpango gani?Inaonekana haitokuwa rahisi kuwakamata hawa wanafamilia wawili wa damu ya Karama?”Aliongea Elkim.

“Mpango wangu ni neno moja tu na ni; Subira”

“Subira!”

“Ndio mpango wetu kwa sasa. Haitochukua muda mrefu , mtu mwingine atakuja kupambana na Lucifer na kumalizana nae. Ikifikia muda huo atajuta kwa kukataa kufanya dili na mimi”Aliongea Mathias.

********

Upande wa Hamza aliweza kurudi hospitalini na mara baada ya kutembea kusogelea mlango wa wodi , aliweza kugundua watu aliowaacha kwenye korido hawakuwepo tena na haraka sana aliongeza hatua na kwenda kuingia ndani.

Mara baada ya kuingia ndani , aliweza kugundua , Bi Tunui , Black Fog na Regina na wengine walikuwa wamekizunguka kitanda cha Irene na alijikuta akishindwa kuzuia shauku yake na kusogea karibu.

“Nyie mnaangalia nini?”

Mara baada ya kuona Hamza amerudi , kila mmoja alirudiwa na fahamu na wakwanza kuvunja ukimya alikuwa ni Black Fog.

“Bro hebu njoo uangalie , hiki si kama kile kilichotokea Paris?”Aliongea Rhoda na kumfanya Hamza kutembea mpaka kando ya kitanda na kuangalia na alijikuta macho yake yakiganda.

Kulikuwa na barafu iliokua imetanda katika tumbo la Irene , karibu na eneo la jeraha lake.

Mwanzoni jeraha lile walikuwa wamelishona lakini muda huo ni kama nyuzi hazikuwa na umuhimu tena kwani eneo lote lilikuwa lishapona muda huo ambao Hamza anaingia, ikionyesha hali hio ilianza muda.

“Ni muda mfupi tulivyoingia kwa ajili ya kuona hali yake , tulihisi chumba kikiwa na baridi kali na ile tunamfunua ndio tukaona amefunikwa na barafu”Aliiongea Rhoda.

Hamza alijikuta ghafla akimwangalia Regina , ambae alikuwa akiangalia pia na mwonekano usioelezeka.

“Wife sio kwasababu ya damu yako?”

Kwasababu Regina amempatia Irene damu yake, Hamza alihisi pengine ni kwasababu hio.

“Hata mimi sijui pia , hii ndio kama ilivyokuwa kwangu?”Aliuliza Regina na Hamza aliishia kutingisha kichwa chake kukubali.

“Hakika damu yenu ya urithi ni ya ajabu mno, nashindwa kuelewa ni kwasababu umempatia damu yako au ni uwezo wake mwenyewe kutokana na damu yake”

“Vipi! Binti yangu atakuwa sawa?”Aliuliza Baba yake Irene aliekuwa kimya muda wote

“Sio tu kuwa sawa. Kama kila kitu kikienda sawa, basi bahati itakuwa upande wake. Akishapona kabisa nitamfanya na yeye pia kujifunza Andiko la malaika. Tena huyu ana umri mdogo kuliko mke wangu , kama ataweza kujifunza kwa bidii anaweza kufanikiwa kwa urahisi zaidi”

“Una andiko la Karama ya uzao wa damu!?”Aliuliza Bibi yake Irene kwa mshangao.

“Ndio, Nimeshaanza kujifunza”Alijibu Regina.

“Lakini itakuwa sahihi kumfanya Irene kujifunza , isitoshe ni wa nje..”Madam Tunui aliinamisha kichwa chake chini akionyesha ni wa daraja la chini.

Alikuwa sahihi kulingana na sheria , Irene alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa kutoka kwa baba yake na kisheria hakupaswa kujifunza.

Hamza upande wake hakujali sana masuala ya sheria , hivyo alimwangalia mke wake ambae ndio mwenye kauli ya mwisho.

“Mke wangu unaonaje?”

“Kwasababu watu wa Binam , wanataka kumkamata , hatuwezi kuangalia tu wakifanikiwa. Babu na Bibi wana deni kwa Madam na mwanae , kumruhusu Irene kujifunza nitakuwa nimelipunugza deni walau kidogo”

Kauli ya Regina ilimfanya Bi Tunu kushikwa na hisia nzito , ingawa hakujua sana kuhusu mbinu za mapigano na mafunzo ya nishati , wala kuhusu Andiko la kuamsha karama ya damu , lakini alijua ni jambo zuri sana kama Irene atajifunza. Kwani ingemsaidia kujilinda hapo baadae.

“Regina, asante sana..”Aliongea huku akifuta machozi kwa furaha.

Unadhani Subira ya Mathias utafanikiwa?

nicheki watsapp kama unahitaji mwendelezo, namba ni 0687151346
 
Hapa shida ilipotokea sio coins wala
Kuna kipindi simulizi ilikua bure tulisoma
Ikapelekwa Grupuni kwa wasio na subira ya muendelezo ili waende na kasi yao,Lakini wa bure waliendelea kuburudika hvo hvo pia...mpk leo imehamia fasihinet. Watu wa bure bado walifunguliwa vipande ss ghafla kawatenga watu wa bure kabaki na wale wasio na subira unategemea ukiwacheleweshea na mtu kashalipia atakuelewa??
Wabure mtawasema hawana mchango kwa mwandishi lakini hujui wao ndo mabalozi wazuri kuitangaza simulizi kwa watu wapya
Kwaiyo Singano nakushauri tu endelea na ile ratiba ya kufungua vipande kazaa kwa ajili yao kila week.
Ni kama Kila mtu anapenda mpira lkn sio kila mtu anapenda kubet.
Exactly
 
Wikiendi hii usiiishi kinyonge sana...njoo nikupe episode 20 bure nicheki namba 0687151346 watsapp...hakikisha umejisajili tayari fasihinet.
 
Wengine tunatumia kiswaswadu cha opera mini inakua ngumu
Tutaendelea kupost mwendelezo hapa mdogo mdogo mkuu, usiwe na wasiwasi kabisa, tatizo kuna watu humu nikiweka mwendelezo wanachukua na kwenda kuuza kwenye magroup na channel zao......
 
Hii simulizi kwa wanaotaka kuendelea nayo, tuko mbali sana sehemu ya 600 na zaidi, .. tuko mbali Hamza tayari ana mtoto wa kike na Regina... kama unataka kusoma kwa watsapp au fasihinet nicheki 0687151346
 
Back
Top Bottom