Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI: SINGANOJR

Saidi hakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa Prisila ambae alionyesha mabadiliko ya ajabu mno, swala ambalo hakuwah kufikiria kwenye maisha yake Prisila angekuwa na uwezo wa aina hio.

Aliishia kumwangalia mpaka anamaliza kujifungua kamba alizomfunga kwa namna rahisi sana na hakuweza kumzuia kwani kumsogelea ilimaanisha kuungua.

Harufu ya kuungua kwa mpira ndio iliogubika eneo hilo na kumfanya Saidi aone anachoangalia ni uhalisia na sio ndoto.

“Haiwezekani , hapana hii sio kweli , inawezekana vipi binadamu wa kawaida kuwa na joto kiasi hichi na macho yake kubadilika”Aliongea Saidi kwa kupaniki huku akitingisha kichwa chake kutokubali kabisa.

Cha kushangaza zaidi Prisila alionekana kuwa sawa, alikuwa ni kama amefunikwa na tabaka la joto kwa nje na kumfanya Saidi asiweze kumsogelea , hata nguo zake hazikupatwa na shida kabisa.

Prisila akili yake ilikuwa kama sio yake , lakini macho yake bado hayakuacha kuonyesha hofu juu ya Saidi aliekuwa mbele yake, hivyo bila ya kuongea neno palepale aligeuka na kukimbilia mlango wa ghala hilo ili kutoka.

Saidi hakutaka Prisila aondoke na alimsogelea kwa kasi ili kwenda kumzuia kwa mbele lakini Prisila kitendo cha kunyoosha mkono na kumsukuma ilimfanya Saidi ashindwe kumsogelea na kubakia pembeni,lakini hata ihvyo hakuwa tayari kumwacha Prisila kuondoka.

“Prisila…!!!”Aliita kwa nguvu huku akiamua kujitoa muhanga na palepale alimshika Prisila mkono wake.

“Arghhhhh…!!”

Saidi alijikuta akipiga ukulele mkali wa maumivu huku mkono wake ukianza kuungua na mvuke wa moto uliokuwa ukimtoka Prisila , lakini hatahivyo aliishia kung’ata meno kwa nguvu huku akikataa kumwachia.

“Niachie…”Aliongea Prisila na palepale alituma mkono wake wa kushoto na kumsukuma Saidi eneo la kifuani.

Kitu kilichomshangaza Said kwa mara ya pili ni kwamba nguvu ambayo alisukumwa nayo haikuwa ya kawaida kwani alirudishwa nyuma kwa nguvu na kwenda kuivaa meza.

Puuh!!

Kitendo kile ni kama kilimfanya Prisila ashituke na kuonekana kama mtu alierejewa na akili zake na aliishia kutoa macho mara baada ya kuona ameweza kumsukumia Saidi mbali hivyo.

Lakini mara baada ya kuona yupo huru , hakujali tena kuhusu Saidi na alikimbia kutoka nje ya eneo hilo kwa mbio zote.

Mara baada ya kutoka nje ndio aliweza kugundua alikuwa ndani ya sheli ambayo imetelekezwa muda mrefu kiasi cha majani kuota kuzunguka eneo hilo, ilionekana mara baada ya barabara kupitishwa upande mwingine ndio maana sheli hio ilifungwa.

Muda huo Prisila aliweza kusikia sauti za gari ya polisi upande mwingine na alijikuta akishikwa na furaha na kukimbilia upande huo.

Walikuwa polisi ambao waliongozwa na Afande Maningi na wote walionekana kushikiria bunduki.

Baada ya kumuona Prisila akikimbia mara moja walisimamaisha gari na kuruka kutoka nje.

“Prisila uko sawa?”Aliuliza Kamishina maana alikuwa akimtambua Prisila.

“Afande , Afande niko sawa lakini Saidi ndio muuaji mliekuwa mkitafuta,yupo ndani kule”Aliongea kwa haraka haraka huku akihema kwa nguvu ,muda huo ile nguvu ambayo alikuwa nayo ilikwisha kumpotea kabisa na alikuwa akitaka kudondoka kutokana na kuishiwa nguvu.

“Prisila uko sawa , mbona jasho linakutoka hivyo?”Aliongea Afande mmoja mara baada ya kuona Prisila alikuwa akitoka jasho kana kwamba alikuwa ameibukia kutoka majini.

“Naombeni mumkatame Saidi , anapaswa kufungwa kwa kumuua Hamza”Aliongea

“Prisila punguza wasiwasi, Hamza hajapata tatizo , ndio alietuambia tuje hapa , muda si mrefu atafika pia “Aliongea Afande Maningi.

“Nini.. Hamza yupo hai?”

Prisila alijihsi ni kama amerudi kutoka kuzimu na kuingia mbinguni kutokana na furaha ya kusikia Hamza hakuwa amekufa.

“Mchukueni mumpeleke hospitalini , hali yake inaonekana sio nzuri sana”aliongea AfandeManingi akiwaamrisha vijana wake.

Prisila bado hakujua kile kilichomtokea mpaka muda huo na aliishia kuingia katika gari ya polisi.

Kitendo cha kuingia katika gar ya polisi hata hakujua nini kinaendelea kwani alianza kuhisi nyota nyota na sekunde zilikuwa nyingi kwake kwani alipoteza fahamu palepale.

Muda huo kabla gari halijaondoshwa Hamza aliweza kufika kwenye difenda na kitu cha kwanza ilikuwa ni kukimbilia katika gari alioingizwa Prisila.

“Nini kimemtokea?”

“Yupo sawa , inaonekana uchomvu ndio umemsababishia kupoteza fahamu , ndio tunampelekea hospitalini”Aliongea na Hamza hakuridhika kwani palepale alimshika mkono kwa namna ya kumkagua msukumo wa damu na aliishia kukunja sura akishindwa kuelewa kwanini amekuwa mdhaifu namna hio ili hai alitekwa muda mchache sana.

Hamza mara aada ya kumkagua na kuthibitisha hakuwa kwenye hali ya hatari alisimama na kisha alianza kupiga hatua kuelekea kwenye ghala lililokuwa mbele yake.

“Nyie nisubirini hapa , nitaenda kuangalia kinachoendelea””Aliongea

“Hakuna shida , tunakupa ushirikiano wote”Aliongea Afande Maningi hakuna ambae alikuwa na ujasiri wa kumkatalia Hamza kile alichokuwa akitaka kufanya , lakini vilevile walikuwa na wasiwasi na ambacho Saidi anaweza kuwafanya.

Uso wa Hamza ulikuwa umejaa ukauzu na hakuwa amevaa viatu wala shati , alichokuwa amevaa ni bukta pekee.

Hamza mara baada ya kuingia ndani ya Ghala alifikiria angemuona Saidi lakini tofaut na kuwepo kwa vifaa vingi vya kielektroniki Saidi hakuonekana kabisa ndani ya eneo hilo.

Hamza aliishia kukunja ndita na haraka alikmbiia upande wa nyuma wa ghala hilo na pale ndio aliweza kuona alama za tairi za pikipiki ambazo zimeelekea usawa wa baharini.

Hamza hakutaka kuchelewa palepale alitimua nduki kuelekea upande wa baharini akiamini lazima Saidi anataka kutoka nje ya nchi kwa njia hio.

Kutoka kwenye ghala la sheri hio mpaka fukwe ya Ndege Mbweni hapakuwa mbali na baada ya kukimba kwa dakika tano tu alikuwa mbele ya bahari na mara baada ya kuangalia baharini aliishia kutoa tusi mara baada ya kumuona Saidi akiwa kwenye Speedboat akielekea katikati ya maji.

Upande wa Saidi pia aligeuza macho yake nyuma kuona alikuwa akifuatiliwa na alishangaa mara baada ya kumuona Hamza akiwa amesimama ufukweni akimtolea macho.

“Haiwezekani , imekuwaje bado hajafa?”Aliongea mwenyewe huku moyo wake ukizama kabisa , mpango wake wakati wa kukimbia ni kwamba hata kama hakuweza kumpata Prisila lakini kwasababu Hamza alikuwa amekwisha kufa mpango wake namba moja umefanikiwa na pengne baadae anaweza kurudi kwa ajili ya Prisila.

Lakni muda huo aliishia kusaga meno kwa hasira mara baada ya kuona hakukamilisha jambo hata moja zaidi ya kujiingiiza kwenye kundi la wahalfu.

Hamza hakutaka kumuona Saidi akikimbia kwa kile ambacho amefanya na palepale alikimbia nduki kuingia majini kama kichaa na kama Samaki aina ya Dolphin alitumbukia kwenye maji na kupiga mbizi kwa sekunde kama kumi tu na kisha haikueleweka amefanyaje bali alifyatuka kama mshale na ile anakuja kutua alikuwa umbali nusu na ilipo boti ya Saidi.

Saidi mara baada ya kuona tukio lile alijikuta akitoa macho na kuongeza spidi, lakini alikuwa amechelewa kwani mara baada ya Hamza kufyatuka mara ya pili kama mshale alienda kutua ndani ya nyuma ya boti yake na kuifanya izunguke kurudi nyuma na kidogo tu igeuke..

Saidi aliishia kutoa macho na hakutaka kuamini Hamza alikuwa ni binadamu mwenye uwezo wa kuruka kama samaki umbali wote huo, hata samaki hakuna wenyewe ni ngumu kuweza kuruka umbali huo.

“Wewe… wewe ni mtu kweli?”Saidi aliishia kubabaika huku akimwangalia Hamza kwa uso uliofubaa.

“Hata kama mimi sio mtu nina afadhali kuliko wewe”Aliongea Hamza.

Saidi licha ya kushikwa na hofu hakutaka kukimbia na alianza kuandaa mpango wa kukabliana na Hamza.

“Kwasababu bomu limeshindwa kukuua , nitakuua mwenyewe awamu hi”Aliongea na palepale kwa nguvu zote alimrukia Hamza na kumlenga ngumi za kifua mfululizo pamoja na shingo , lakini licha ya kutumia nguvu zake zote Hamza hakusogea hata kidogo na ngumi zake zilikuwa ni kama za mwanamke mwenye hasira juu ya mwanaume anaempenda katika mwili wa Hamza.

Alijitahidi kurusha ngumi nyingi kwa kadri alivyokuwa akiweza lakini Hamza aliishia kumwangalia tu bila kuonyesha ishara yoyote ya kuumia.

“Hapana.. haiwezekani , kwanini huumiii?”Said alijikuta akianza kutingisha kichwa kutokubaliana na matokeo na kujiambia siku hio nini kinamtokea kwanzia kwa Prisila na hatimae kwa Hamza.

“Umemaliza kupiga?”Aliuliza na Saidi aliishia kukosa neno na kumeza mate mengi.

“Nimekuacha utoe toe hasira maana sijui hata ugomvi wetu umeanza lini”AliongeaHamza na baada ya pale alimshika Saidi shingo.

“Arghhh”

Saidi aljikuta akifurukuta mara baada ya kuning’inizwa hewani lakini licha ya kujitahidi alishindwa kujitoa katika mkono wa Hamza uliomshika.

“Haijalishi unanichukuliaje , unaweza kunifanya chochote lakini huwezi kuumiza watu wasio na hatia kwa tamaa zako”Aliongea Hamza.

“Huwezi kunishinda , siwezu kukuruhusu , kafie mbali”

Aliongea na palepale ghafla tu alichomoa sindano kwenye mfuko wake wa suruali na kisha alimchoma nayo Hamza kwenye shingo na alianza kucheka kwa ushindi.

“Hahaha.. ulidhani utaniweza kirahisi hivyo , nilikuwa na mbinu yangu pia , hio ni sumu inayotokana na kirusi niliotumia kuua walezi wangu, haina tiba dunia hii na hakuna wa kuweza kujua umekufa kwa namna gani , Hamza hakuna wa kushindana na mimi juu ya mwanamke ninae mpenda”Aliongea kwa nguvu lakini sasa alijikuta akianza kushangaa mara baada ya kugundua Hamza yupo vilevle na haonyeshi kuathirika na ile sindano ya sumu.

Palepale aliona kuna kitu ambacho hakipo sawa huku akiwa ashamaliza kimiminika chote cha sumu , alijikuta akishikwa na mshituko na haraka sana aliinua lile bomba la sindano na kuangalia na hapo ndipo aliposhikwa na mshangao mara baada ya kugundua sindano ilikuwa imetoka kwenye bomba na haikumchoma Hamza.

“Kama bomu limeshindwa kuniua , unadhani unaweza kuniua kwa kijisindano kidogo kama hicho “Aliongea Hamza na muda ule ndio sasa Saidi anajua hakuwa na namna nyingine ya kumshinda Hamza.

Katika macho ya Saidi , Hamza hakuwa binadamu kabisa zaidi ya kuwa jitu ambalo hawezi kulifkia kwa uwezo, alijihisi kuwa pakacha kwa wakati huo .

Hisia za kutokubali na kudhalilika zilimvaa na kumfanya ajihisi vibaya zaidi ya kifo.

“Wewe ni shetani , kama sio wewe Prisila angenipenda , kwanzia tukiwa wadogo mpaka sasa umekuwa kikwazo kwangu”Aliongea Saidi na kumfanya Hamza amwangalie kwa macho ya mshangao kidogo.

“Unamaanisha nini tukiwa wadogo?”

“Hahaha.. huwezi kukumbuka chochote kuhusu mimi hata nikikuambia, sijui hata ulikuwa ukielewa lugha yetu wakati ulivyoletwa pale kituoni ukiwa hujitambui”Aliongea Saidi.

“Unamaanisha kituoni cha kulelea Yatima Morogoro?”Aliongea Hamza kwa mshangao kidogo na Saidi aliishia kuonyesha dharau za kukubali swali la Hamza.

“Unamjua alienileta kituoni?”Aliuliza kwa mara nyingine.

“Hata kama nikijua utaniacha hai?”Aliongea Said kwa kejeli.

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha najua ila sikwambii kwani najua utaisha kuniua tu”Aliongea na kumfanya Hamza macho yake kuzidi kuonyesha ukauzu, licha ya kwamba kuna hisia alizokuwa akizihisi muda huo lakini hakutaka kuyanunua maneno ya Saidi.

“Hamza wewe ndio umenifanya niende mbali namna hii , umemchukua Prisila malaika wangu tokea siku ulioletwa pale kituoni na sio hivyo tu hata baada ya kurudi ukanipokonya na kuharibu mipango yangu yote,Prisila alikuwa kila kitu kwangu kwanini unipokonye”aliongea kwa hasira.

Hamza alijikuta akimwangalia Saidi ambae alikuwa akilia , alikuwa akijiuliza amuache hai ili akamhoji kuhusana na maswala ya kituoni au ni hila za zake za kumchezea akili, lakini mara baada ya kukumbuka mauaji aliosababisha aliona ni mtu ambae hastahiri pumzi.

“Sijamchukua Prisila kutoka kwako mimi bali ni kwasababu hajawah kuwa wako”Aliongea Hamza.

Muda ule Saidi mara baada ya kutafakari maneno hayo picha ya Salma ilimjia akilini na hakushindwa kujizuia na kutamka jina lake.

Upande wa Hamza hakujali kitu chochote , kutokana na mambo ambayo Saidi amefanya aliona hata sheria haiwezi kumhukumu kisawa sawa,hivyo bila ya kufikiria alimpiga ngumi nzito ya tani kadhaa tumboni.

“Puchh!!”

Ngumi ile ilikuwa nzito kiasi kwamba ilipita moja kwa moja na kuingia ndani ya tumbo na kufanya damu zianze kumtoka mfululizo , Saidi hakuhisi hata maumivu zaidi ya mwili wake wote kufa ganzi.

Hamza hakutaka hata kuendelea kujisumbua nae , alijua mpaka hapo Saidi hawezi kupona tena hivyo alimwachia na akatumbukia baharini na kitu pekee kilichoweza kuonekana ni damu nyingi kusambaa eneo ambalo amezamia.

“Kwaheri ya kuonana Saidi”Aliongea Hamza.

*****

Saa mbili kamili za usiku Prisila alikuwa ameketi kwenye kitanda akiangalia taarifa ya habari dakika chache baada ya kumaliza maongezi na baba yake aliekuwa nje ya nchi.

Kamishina wa uchunguzi wa makosa ya jinai Kanda ya Dar es salaam, Afande Sospeter Maningi alikuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya jeshi la polisi kufanikiwa kumkamata muaji aliesababisha vifo vingi vya wanawake.

Taarifa hio ilikuwa gumzo kwani kabla ya kukamatwa kwake ilifanya wanawake wengi kuishi kwa hofu kubwa mno. Sasa kitendo cha jeshi la polisi kufanikiwa kumkamata muhusika kwanza iliondoa hofu kwa wananchi na pili kamanda huyo alijizolea umaarufu pale aliposema yeye mwenyewe aliongoza kikosi maalumu cha uchunguzi na kumbaini mhusika , licha ya kutangaza muhusika kupoteza maisha hakuna aiejali hata kidogo juu ya kifo chake.

Hamza ndio aliefanya kazi yote ya kumkamata Saidi lakini hakutaka kuhusishwa na kumkamata muuaji huyo hivyo alimpa ruhusa Kamanda Maningi kubeba sifa zote.

Kilichowakasirisha na kuwashangaza wetu wengi ni mara baada ya kujua mhusijka alikuwa ni mtu maarufu kabisa aliekuwa akiaminiwa na kusifiwa na watu wengi.

Wananchi walienda mbali na kuanza kulaumu shirika la mtandao wa simu la Voducum kwa kuajili mtu kichaa.

Lakini licha ya hivyo kampuni hio ilikanusha kuhuska kwa njia ya moja kwa moja na tukio hilo la kikatili na hata wao wenyewe wamesikitishwa na kuguswa mno na kuahidi watatoa fidia kwa familia zilizoathirika na matendo ya Saidi aliekuwa Mkurugenzi.

Licha ya taswira kuchafuka lakini kama shirika kubwa lenye wafanyakazi wengi waliamini swala hilo muda si mrefu litapotea katika vichwa vya raia na kusahaulika kabisa hivyo hawakutaka kukataa kuwajibika ndio maana wakaona watoe fidia.

“Prisila unaendeleaje?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuingia katika wodi ya daraja la kwanza aliolazwa Prisila ndani ya hospitali ya jeshi.

Macho ya Prisila yalichanua mara baada ya kumuona Hamza hakuwa na majeraha yoyote mwilini tena akiwa amebadili kabisa nguo.

“Niko poa.. Hamza unajua nilikuona kabisa ukilipuka , nilishikwa na mshituko nikajua umekufa kweli”Aliongea akiwa haamini na Hamza alishia kutoa tabasamu pekee na kwenda kukaa karibu yake kwenye kitanda na kisha alimshika mkono wake na kuanza kusikiliza mapigo ya msukumo wa damu.

“Mapigo yako ya msukumo wa damu yamekaa sawa , hatimae umeimarika”Aliongea na kumtoa Prisila kwenye mshangao maana hakujua Hamza anajaribu kufanya nini.

“Prisila nilisikia kutoka kwa Polisi uliweza kutoka mwenyewe kwa kukimbia kwenye ghala , uliwezaje kumtoroka Saidi?”Aliuliza Hamza akiwa na macho ya shauku maana hakujua kama Saidi anaweza kufanya kosa la namna hio na kumruhusu Prisila kutoroka.

Ukweli hata yeye muda wote alikuwa akiwazia tukio lile na alitamani kumtafuta mtu wa kongea nae ili amsaidie kupata majibu, hivyo alimwelezea Hamza kile kilichotokea.

Upande wa Hamza kadri alivyokuwa akisikiliza maelezo ya Prisila hakuonyesha mshangao lakini alizidi kuwa siriasi kwenye uso wake na mwisho wa stori aliona ni kitu ambacho hakikuwezekana.

Licha ya uzoefu wake hakuwahi kusikia kuna mtu duniani anaweza kuwa na uwezo wa ajabu namna hio

“Hamza nimesikia na kusoma katika vitabu vingi eti mtu akiwa katika hali ya kifo na uhai , anaweza kuonyesha uwezo wake wa ajabu uliojificha, hio inaweza kuwa sababu ya mimi kuwa vile?”Aliuliza .

“Hata kama uwezo wako wa ajabu unaweza kujionyesha lakini inawezekana vipi kuwa na joto la kuweza kumuunguza mtu kama chuma,Prisila hata mimi sina majibu ya kuelezea hali yako , vipi kuna hali nyingine uliojisikia?”

“Sikujisikia chochote , kitu pekee nilichoweza kuhisi ni kama nimekuwa mtu mwingine na ninao uwezo wa kufanya chochote , ila baada ya kupoteza fahamu na kuamka sasa hivi sina chochote ninachojisikia cha tofauti”Aliongea.

Upande wa Hamza hakuweza kupata tafsiri sahihi ya kile ambacho kimemtokea Prisla , kitu pekee ambacho alihisi pengne kuna kitu ambacho Prisila hakuwa akikijua yeye mwenyewe , zilikwa ni hisia tu , lakini hakuwa na uhakika huo na kama ni kupata majibu aliona aidha ni mzazi wake Prisila au mjomba wake.

Hamza alikaa hosptali kwa muda mrefu kidogo mpaka Prisila alivyolala na ndo alichukua safari ya kurudi nyumbani kupumzka.

Mara baada ya kufika, nyumba ilikuwa tupu na alijisikia vibaya kukaa mwenyewe kwenye nyumba yote hio kubwa na pia hakuwa kwenye mudi nzuri na alitaka kupata mtu ambae anaweza kuongea nae, hivyo palepale alimkumbuka Eliza ambae hakuwa ameonana nae kwa siku kadhaa tokea aende msibani.

Kwakuwa alikuwa amemkumbuka sana, alimpigia palepale simu na kumuuliza kama yupo nyumbani lakini alisema bado yupo kazini , kitu ambacho kilimshnagaza Hamza.

Ukweli ni kwamba Eliza kwa muda wote alikuwa akikamu nafasi ya Regina ndani ya kampuni na kutokana na majukumu mengi kichwa kilikuwa kikiwaka moto na muda wote alikuwa bize na hata nyumbani alichelewa kurudi.

Hamza mara baada ya kujua mrembo huyo alikuwa kazini , moja kwa moja aliendesha gari kuelekea huko na ilimchukua dakika chache sana mpaka kufika.

Eliza alikuwa amekwisha kutoka tayari kurudi nyumbani na usiku huo licha ya kuonekana kuchoka , ila alikuwa amependeza mno , alikuwa amevalia shati refu la rangi ya kijivu na Jeans ya rangi ya bluu , huku nywele zake akiwa amezifunga kwa kuzirudisha nyuma na kumfanya aonekane mtoto zaidi kuliko mtu mzima.

“Mbona unaniangalia hivyo wakati ni siku chache tu ambazo hatujaonana?”Aliongea Eliza huku akimwangalia Hamza aliesimama akimkodolea macho.

“Eliza umepanda cheo na uzuri wako pia umeongezeka , nadhani nikitaka kuwa mtanashati na mimi nipandishwe cheo , nakuonea wivu eti”Aliongea Hamza na kumfanya Eliza kucheka.

“Hebu tuondoke muda umeenda, utafanya la maana kama tukipitia mgahawani maana nina njaa”Aliongea na Hamza alitingiisha kichwa huku akimuonea huruma mrembo huyo kwa kutokula mpaka muda huo.

Hamza hakuona haja ya kwenda mbali , mara baada ya kumtoa katika makao makuu hayo moja kwa moja aliendesha gari na kwenda kusimamisha kwenye mgahawa wa Paparotti Mlimani City.

Licha ya muda ulikuwa umeenda lakini kulikuwa na wateja wengi kiasi,ambao wengi wao walionekana kuwa Wenza.

Kutokana na mgahawa kuwa na watu wengi mhudumu aliwasogelea na kuwachukua mpaka kwenye meza iliokuwa wazi na kisha wakakaa na kuagiza chakula na kilevi. Hamza licha ya kwamba alijua ataendesha gari aliagiza pombe, huku akijiambia polisi wa barabarani wakimkamata atakachokifanya ni kumpigia simu Afande Maningi na kutatua tatizo hivyo hakuwa na wasiwasi.

Upande wa Eliza mchana wote alikuwa na furaha na hio ni mara baada ya kutumiwa taarifa na Dokta Ronicas ikimwelezea maendeleo ya mama yake yameimarika mno na kuna zaidi ya aslimia hamsini za mama yake kuweza kutembea tena.

Ilikuwa ni taarifa kubwa na ndio iliomfanya kutaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii mpaka kuchelewa kutoka kazini.

Wakat Eliza akimpatia habari hizo Hamza alifika muhudumu alieshikilia glasi ya Blood Mary na kumpatia Eliza

“Hamza kwani umeniagizia Cocktail?”Aliuliza Eliza kwa mshangao mara baada ya kuakabidhiwa ile Blood Mary Cocktail.

“Hamna sijaagiza”Alijibu Hamza huku akimwangalia yule muhudumu kutaka maelezo

“Kuna yule mkaka upande ule ndio kaniagiza nikuletee , kaniambia pia nikupatie hii”Aliongea yule Mhudumu huku akionyesha noti za elfu kumi kumi kama ishirini hivi na kuziweka kwenye meza mbele ya Eliza.

Wote wawili yaani Hamza na Eliza walishindwa kujizuia na kugeuza macho kuangalia upande wa mwanaume huyo na pale ndipo walipoweza kumuona mwanaume wa kihindi mtanashati alievalia miwani ya rangi ya kahawia na alikuwa ameangalia upande wao..

SEHEMU YA 100

Eliza alitoa kikaratasi kilichokuwa kimeambatanishwa na zile hela na kisha akakisoma na aliishia kukunja tu sura.

“Naomba uchukue umrudishie vitu vyake sina shida navyo “Aliongea Eliza kwa hasira na mhudumu yule haraka haraka alichukua kila kitu na kurudi kwa aliemtuma.

“Lizzy umekataa kwasababu hazitoshi nini?”Aliuliza Hamza huku akiweka muonekano wa matani kwenye uso wake .

“Unaongea nini na wewe , kanionaje mpaka kuniletea hela ili hali anatuona tupo pamoja, kanidharau mno”Aliongea Eliza kwa kukasrika mno , aliona kabisa mwanaume yule alimuona kama malaya ambae anaweza kuacha mwanaume aliekuwa nae na kwenda kwake kwa dau kubwa.

“Nimekutania tu na wewe kipenzi , halafu watu kama hawa haina haja ya kukufanya ukasirike unapaswa kuwazoea maana wapo wengi”

“Kaniharibia mudi yangu nzuri niliokuwa nao , najihisi ni kama nimekula mdudu”Aliongea Eliza.

Lakini muda ule wanaume wawili wenye miili iliojazia waliovalia suti nyeusi walisogelea meza yao , huku mmoja kati yao akiwa na sigara mdomoni.

“Mrembo, bosi wetu pale anataka kupata kinywaji na wewe kwa usiku huu , tunaomba usimpuuze basi maana ni mtu mzito” Waliongea wakiwa siriasi.

“Sitaki , naomba muondoke”Aliongea Eliza kwa kufoka.

“Acha maringo mrembo , jione kuwa na bahati kwa bosi wetu kukutamani , ni mtu wa hadhi ya juu ambae hawezi kutamani mwanamke kiholela, kama wasiwasi wako ni huyu kapuku hata usiwe na wasiwasi bosi wetu ametuambia tumpatie kitita cha pesa ya kumridhisha”

“Mnaongea ujnga , huyo bosi wenu ni mfalme?”Eliza hasira zilizidi kumpanda na hakutaka kuendelea kukaa na alisimama huku akimpa Hamza ishara waondoke.

Hamza upande wake hakuwa na mpango wa kujibishana na watu usiku huo , isitoshe mrembo wake asingepatwa na chochote ili mradi yupo.

Lakini sasa kitendo cha wao kutaka kuondoka wale wanaume waliwakinga kwa mbele na mmoja wapo alitoa kisu cha kufyatuka na kumnyooshea Hamza kulenga tumbo lake.

“Ukisogea tu hatua moja nitaumwaga utumbo wako chini”Aliongea mmoja ya wale mabwana huku wakiwa siriasi mno kwenye macho yao na kwa haraka haraka Hamza aliona watu hao haikuwa mara yao ya kwanza kuua mtu.

Hamza aliishia kuhema kwa nguvu na kujiambia kwanini siku hizi Dar es salaam limekuwa jiji ambalo lina matukio ya ajabu namna hii kama vile sheria hazikuwa zikifanya kazi.

Alifikiria kwa muda na aliona isingeleta picha nzuri kama akiwashughulukia mbele ya watu waliokuwa wakiangalia.

“Mabraza sioni kama ni vizuri tukipigana hapa maana ni biashara ya mtu hii, au mnaonaje?”Aliongea Hamza

“Kwahio unasema unataka kupigana na sisi , kama una ujasiri huo twende chooni kule tukakufanyizie akili ikukae sawa”Aliongea na kumfanya Hamza kuchanua mikono yake kukubaliana na wazo lile.

“Hakuna shida wakuu ,siku hizi matatizo mengi huwa yanamalizikkia chooni”Aliongea na palepale alimwambia Eliza amsubiri anakuja.

Eliza hakuwa na wasiwasi na Hamza kabisa kwani alikuwa akijua uwezo wake , ila hata hivyo wasiwasi alikuwa nayo kwani hakujua Hamza anakwenda kudili nao vipi.

Hamza alijikuta akivuta pumzi mara baada ya kuona choo hakikuwa na mtu , hivyo mara baada ya kuingia, mmoja alifunga kabisa mlango wa kwa ndani.

“Dogo leo tutakufanya ulale hapa wakati bosi wetu akimshugulikia ipasavyo demu wako”Aliongea mwamba mmoja mwenye mwili mkubwa na kisha alimsogelea Hamza akitaka kumrushia ngumi kwa kumlenga kichwani , lakinn Hamza aliidaka ngumi yake.

Yule mtu alianza kuhangaika kutoa mkono wake ulioshikiliwa na Hamza na aligundua alikuwa akishindwa kujitoa na kuishia kukunja sura.

“Naona mna kiu ya maumivu?”Aliongea Hamza na palepale kwa spidi kubwa alimshika yule bwana shingo na kumsukumizia kwenye ukuta na kuupigisha uso wake.

“Ooochiiiii!!”

Baunsa yule akili yake ilizunguka mara baada ya paji lake la uso kugonganishwa na ukuta , yule mwingine mara baada ya kuona mwenzake akishughulikiwa haraka haraka alitoa kisu na kutaka kumchona nacho Hamza mgongoni.

Lakini alikuwa amechelewa maana kabla hajamfikia Hamza teke lilisharushwa na kwenda kumpiga kwenye korodani na alijikuta akipiga ukulele mkubwa wa maumivu makali.

Hamza wala hata hakujali , kwa mikono yote miwili aliwashika wote shingo na kisha alienda na akazilengesha sura zao kwenye masinki kukojolea kwa nguvu.

“Bang , Bang , Bang…!”

Mara baada ya kugonganisha vichwa vyao na masinki kwa zaidi ya mara kumi , damu ziliwatoka kwa wingi na kupoteza fahamu palepale.

Baada ya kuona hawajitambui alifungua milango miwili ya chooni na kisha aliwapigisha magoti na kutumbukiza sura zao kwenye masinki yake ya vyoo vya kukalia.

Ukiwaangalia utasema wanakunywa maji ya choo kwa namna walivyokuwa wakionekana.

Hamza mara baada ya kuona kazi imeisha vizuri , alinawa mikono na kuweka shati lake vizuri pamoja na nywele kwa kujiangalia kwenye kioo na baada ya hapo alirudi alikomuacha Eliza bila wasiwasi.

Eliza mara baada ya kumuona babe wake anatoka tena kwa kudunda aliishia kutoa tabasamu na kusimama kumlaki.

“Upo tayari tuondoke sasa?”Aluliza Eliza.

“Ndio , halafu vipi leo naweza kulala kwako?” Aliuliza Hamza huku akimkonyeza.

Eliza alionekana kama mtu ambae anataka kuongea kitu lakini alijisikia aibu , aliishia kuvimbisha mashavu huku akitingisha kichwa kukubali.

Wawili hao waliondoka katika mgahawa huo na kuelekea walipoegesha gari yao , lakini dakika ambayo wanatoka Hamza aliweza gundua kuna mtu aliekuwa akiwafatilia nyuma.

Lakini kilichomshangaza zaidi ni kwamba mtu yule hakuwa na uwezo wa kawaida.

Hamza mara baada ya kufika kwenye maegesho kitu cha kwanza ilikuwa ni kumwingiza Eliza kwenye gari na kisha aligeuka na kumwangalia yule mwanaume.

Yule mwanaume alikuwa mtu mzima wa makadirio ya miaka kama arobani hivi , alikuwa mweusi tii huku akiwa amevalia mavazi ya mahadhi ya Kinaigeria , alikuwa na uchebe ulioning’ninia.

“Kuna kitu unataka?”Aliuliza Hamza.

“Dogo nataka kujua ni familia gani unatokea hapa nchini?”Aliuliza

“Sina familia ni mimi mwenyewe”Aliongea Hamza

“Oh… kama huna familia nadhani nikushauri acha kujifanya jasiri , huyo mwanamke uliekuwa nae ni hadhina kwa bosi wangu”Aliongea huku akitabasamu.

Muda ule mwanaume ambae alimtumia Eliza hela na kimemo aliweza kutoka akiwa ameambatana na wale mabodigadi wawili ikionekana fahamu zimewarudia ila damu zinawatoka.

“Mzee Regani unasubiri nini mzimishe haraka na nimchukue huyo mwanamke kabla ya muda kutimia”Alongea huku akimwangalia Hamza kwa macho ya uovu.

“Mtu yoyote anaejaribu kunichokoza maana yake hajui vizuri maana ya neno kifo”Aliongea Hamza.

Upande wa Eliza ndani ya gari alikuwa akiona mambo yote hayo na kumfanya kushikwa na wasiwasi na hasira kwa wakati mmoja , kama sio Hamza kumzuia angekuwa ashaita polisi tayari.

“Bosi Farhani , huna haja ya kuwa na wasiwasi , kilicho chako kitakuwa chako siku zote”

“Kama ni hivyo mbona hufanyi kazi nikiona matokeo?”Aliongea Farhani na kumfanya yule bwana aliefahamika kwa jina la Regani kumsogelea Hamza.

“Dogo unaijua thamani ya huyo mwanamke kiroho , kwanini unachukuwa mwanamke aliebeba nyota ya bosi wangu?” Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura na kujua palepale kinachotafutwa kwa Eliza sio mapenzi tu ila ni nishati ya kiroho ya kike aliokuwa nayo, nishati ambayo mara nyingi humfanya kuwa shabaha ya wavuna nishati wengi wa ulimwengu wa giza.

“Huyu ni mwanamke wangu na bosi wako ndio anaetaka kumuiba kwangu , lakini kwanini imegeuka na kuwa kinyume chake?”

“Katika ulimwengu wa watu wenye nguvu kuongea kimantiki hakuna maana , kigezo pekee cha kumiliki ndio maana”Alongea na palepale alitoa tabasamu lililojaa uovu na alimsogela Hamza na kumrushia kiganja cha mkono.

Kwa mtu wa kawaida angejua alichokuwa akifanya ni shambulizi la kawaida la kimapigano kama la Karate lakini haikuwa hivyo.

Kwani mara baada ya mkono ule kufika usawa wa macho ya Hamza kutoka kwenye mkono wa shati lake kulitokea moshi kama poda uliochanganyika rangi ya bluu na kijivu na kusambaa.

Hamza aliishia kukunja sura mara baada ya kuona rangi ya moshi ule wa poda ulikuwa na sumu isiokuwa ya kawaida na haraka sana alirudi nyuma ili usimpate.

Regani mara baada ya kuona shambulizi lile limefeli , palepale alitoa kijichupa kidogo na kufungua ufuniko wake kwa juu na wadudu aina ya Buibui walionekana kutoka kwa kasi.

Buibui hao walionekana kuwa weusi tii , huku wakiwa na ukijani flani hivi kwenye mabawa yao , ijapokuwa walikuwa wadogo sana lakini walikuwa na uwezo wa kusogea kwa kasi mno na kufanya kuwa ngumu kuwakwepa.

Regani ni kama hakujua kushambulia na mara baada ya kuwaachia wale Buibui alichezesha mikono yake kimazingara na ghafla tu walimsogelea Hamza na kuanza kumshambulia kwa kumng’ata.

Corpse Spider!!”Hamza alimaka.

Hatimae alikuwa ashajua nini kilichokuwa kikiendelea , Buibui hao walikuwa wakiitwa Corpse Spider au Buibui Nyamafu , sababu ya kuitwa Buibui Nyamafu ni kwasababu chakula chao kikubwa ni nyama ya maiti iwe ni binadamu au mnyama wa mwitu.

Kulikuwa na aina nyingi sana za Buibui na wengine kuna uwezekano wa watu wachache sana kuwafahamu kwani wanaonekana kwa shida sana wengine wakijitokeza usiku tu.

Baadhi ya Mamajusi(Magi) na wachawi(Mages) ndio watu pekee wenye uwezo wa kuongea na kuwapa maelekezo aina hawa ya Buibui nyamafu lakini pia baadhi ya wataalamu wa mapigano ya mbinu za kikale(Ancient Martial Artist) wana ujuzi wa kimafunzo wa kutumia aina ya hawa Buibui Nyamafu kama siraha kumshambulia mtu, ni kama vile mchawi anavyokuwa na uwezo wa kutumia nyuki kushambulia hivyo hiivyo kwa baadhi ya watu kuwa na uwezo wa kutumia aina hio ya Buibui kushambulia.

Buibui hawa nyamafu ni adimu mno na mara nyingi wanaonekana usku pekee na ikitokea umeng’atwa na aina hi ya buibui matokeo yake mwili wako utaanza kufa kutoka nnje kwenda ndani na hakuna dawa inayoweza kukuponyesha na hata kama usife kwa kuwahi matibabu utaishia kuwa nusu mfu.

Kulingana na maarifa ya Hamza kulikuwa na mashirika matatu pekee duniani aliokuwa akiyajua yanatoa mafunzo ya kichawi ya kutumia wadudu na moja wapo ilikuwa ni kutokea China , India , Brazili na Slovakia, nchi za kiafrika hakukuwa na maatumizi hayo ya wadudu labda itokee mwafrika kusafiri kwenda kwenye mashirika hayo kujifunza, hivyo hata mtu aliekuwa mbele yake hisia zake zilikuwa zkimwambia ni mwanafunzi kutoka kati ya mashirika hayo.

“Naona unawatambua hao wadudu , lakini kwa bahati mbaya huna uwezo wa kufanya kuokoa maisha yako”Aliongea yule bwana

Hamza upande wake aliacha wale wadudu kumshambulia mwili wakekwa kumng’ata huku akitumia mikono yake na kuanza kuwaua mmoja baada ya mwingine.

“Haha…. hata kama uwaue huna uwezo wa kumsaidia mpenzi wako , kwanini unahatarisha maisha yako kwa ajili tu ya kumlinda huyu mwanamke , ninni kinakufanya uteseke kwa ajili yake?”Aliongea Regani huku akicheka lakini Hamza wala hakumjali.

“Kama sikosei unatokea dhehebu la kichawi kutoka India maarufu kama Nishaali Hansii?”Aliongea Hamza.

“Wewe unajuaje Dhehbu letu la Nishaali , wewe ni nani halafu mbona hufi baada ya kung’atwa na Buibui Nyamafu?”Aliongea Regani kwa mshangao.

“Unashangaa kwanini Sumu yake haijanidhuru , labda nikuambie tu Sumu ya Buibui Nyamafu inamuathiri binadamu wa kawaida pekee , ila kwa taarifa yako mimi sio wa kawaida”Aliongea Hamza kijivuni.

Regani palepale aliona hali sio nzuri hata kidogo na bila kujitambua aliishia kupiga hatua kadhaa nyuma na kukaa pembani ya mkuu wake.

“Bosi tunapaswa kuondoka hapa , huyu mwanaharamu simwelewi”

“Wewe mpuuzi mbona unanitia aibu , hii si inamaanisha dharau na pia mbele ya Tosha si ni kuvunja masharti huku kwa mara nyingine, hujui nini kitatokea swala hili likifeli kwa mara nyingine, tutajitetea vipi?”aliongea yule bwana kwa hasira.

Baada ya kuongea vile , dakika ileile alitoa siraha yake ya bastora na kisha akafyatua risasi kumlenga Hamza.

Hakuna alieamini bwana huyo angetumia risasi muda huo karbu na mgahawa , ijapokuwa ilikuwa ni usiku na maegesho hayo hayakuwa na watu wengi lakini mlio wa risasi ilikuwa ni rahisi kusambaa.

Regani alikuwa amechelewa kumzuia bosi wake kwani risasi ilikwisha kutoka tayari na muda huo aliona cha kufanya pekee ni kuwasliana na familia yake la sivyo swala hilo halitaisha kirahisi mbele ya vyombo vya usalama , isitoshe alijua Hamza anakwenda kufa.

Lakini sasa Hamza alikuwa amesimama katika eneo lileile bla kusogea huku akiwa ameshikilia risasi mkononi akicheza nayo , tena kwa mkono wa kushoto.

“Hapana , haiwezekani , kawezeje?”Aliongea Farhani huku akitoa macho kana kwamba ameona mzimu.

Yule Regani aliishia kumeza mate mengi huku wasiwasi ukimshka.

“Kwahio tokea mwanzo alikuwa ni mtaalamu wa hali ya juu , Bosi tuondoke hapa”Aliongea kwa kumkazania bosi wake.

Reganni alijua mtu ambae ana uwezo wa kudaka risasi basi hawezi kuwa mtu wa kawaida hata kidogo kama alivyosema.

“Kuna haja gani ya kumuogopa ilihali ashakuambia hata familia hana”Aliongea Farhani kwa macho ya kejeli akionyesha kutoogopeshwa kabisa na kile ambacho Hamza amefanya.

Upande wa Hamza hakutaka kabisa kuona mtu kama huyo anaendelea kuvuta pumzi , hakujali kama alikuwa akitokea wapi ama famlia yake ina nguvu kiasi gani lakini alichoona adhabu inayomtosha ni kifo pekee.

“Puuch!!

Haikueleweka Hamza alitumia uwezo gani lakini risasi alioishikilia mkononi aliirusha kwa nguvu na kumlenga nayo Farhani na ilienda kumtoboa eneo la kichwani.

“Bosiii…!!1”

Regani na wale mabodigadi walijikuta wakimkimbilia bosi wao kwenda kmdaka wakati akidondoka chini huku damu nyingi zikimtoka.

Eliza upande wake alishangazwa na tukio lile na aliona Hamza alikuwa na uwezo mkubwa mno ambao haukuwa ukielezeka kwa mancno ya kawaida , hakuweza hata kumfananisha Hamza na mwanajesh kwani alichokuwa akionyesha ni zaidi ya uanajeshi.

Hamza hakujali bwana huyo kama amekufa ama laah , kwani palepale aliingia katika gari na kisha kuliondoa ndani ya eneo hilo, huku Regani akiishia kumwangalia Hamza kwa macho yasioweza kueleweka anachokiwaza ni kitu gani.

“Amekufa?”Aliuliza Eliza kwa wasiwasi.

“Itakuwa”Aliongea Hamza.

“Utafanya nini sasa kama amekufa?”Aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

“Unazungumzia kuhusu sheria au familia yake?”Aliuliza.

“Vyote?”

“Itajulikana mbele ya safari , ila kwa ninavyojua mimi, lazima familia yake imejifungamanisha na maswala ya utajiri wa kishetani na hata kukutaka wewe kwa nguvu ilikuwa ni mpango kama wa Mzee Gabusha wa kutimiza masharti”Aliongea Hamza.

“Unamaanisha alitaka kunitumia kuninyonya nguvu zangu za kike kupitia mapenzi?”Aliuliza Eliza , alikuwa akikumbuka vyema Hamza alichomwambia walipokuwa Morogoro.

“Ndio , Eliza kama nilivyokuambia wewe kwenye macho ya watu wa ulimwengu wa giza wewe ni hadhina kwao ya kujinufaisha kiroho”

“Sasa bado hujaniambia nini kitatokea kama wakijua wewe ni uhusika , umejiingiza kwenye matatizo”

“Kuna sheria ya madhehebu ya watu wanaotumia nguvu za giza , we ni kwa mapgano ama kujipatia utajiri , moja ya sababu kama ikitokea mtu amepewa masharti ya kuivuna nguvu ya kiroho au nyota ya mtu na akafia wakati akiwa katika misheni ya kutimiza masharti maana yake yeye ndio alikuwa mlengwa wa kafara”Aliongea Hamza na macho ya Eliza yalitoka kodo.

“Kwamba amekuja kunipata mimi lakini akafeli , hiyo kufeli kwake gharama yake ni yeye kutolewa Kafara?”

“Umeelewa vizuri sana mpaka hapo, hivyo nina uhakika ameletwa kwako nimuue tu kutimiza masharti ya kidhehebu lao , nina uhakika na familia yake watakuwa wanajua hilo”

“Inakuwaje inakuwa hivyo?”

“Inatokea mara nyingi, kama umeshndwa kutimiza masharti zaidi ya mara tatu , Mfano Mzee Gabusha yule nina uhakika kifo chake hakikuwa cha kawaida , pengine ulikuwa misheni ya sharti lake la mwisho na akakukosa ndio maana kifo kikampaata , lakini licha ya hivyo katika mazingira ya kawaida ukiondoa imani zao familia yake lazima haitolchukulia hili kiwepesi na kuacha lipite”

“Unamaanisha watataka kulipiza kisasi?”

“Ni zaidi ya kulipiza kisasi , ila usiwe na wasiwasi hili nitajua namna ya kudili nalo”Aliongea Hamza kwa kujiamini na kumfanya Eliza kuvuta pumzi ya ahueni lakini bado alikuwa na wasiwasi licha ya kwamba hakujua huyo Farhani anatokea familia gani .

Upande wa Hamza alijua familia yake haiwezi kuwa nyepesi , kama Farhani alikuwa akilindwa na mtaalamu mwenye uwezo wa kutumia Buibui Nyamafu basi lazima mizizi yao katika ulimwengu wa giza imeenda mbali sana.

Kutokana na Hamza kuguswa na wale Corpse Spider , hakutaka kumgusa Eliza bila ya kujisafisha , hivyo alikimbilia bafuni kuoga .

Eliza muda huo alikuwa ameketi kwenye sofa na alikuwa akijitahidi kujituliza ili kutofikiiia maswala ya Farhani , wakati akisikilizia maji ya shower yakidondoka chini mwili wake ulianza kukamakaa.

Ijapokuwa walishawahi kulala kitanda kimoja lakini hawakuwahi kufanya lile tendo , lakini muda huo alikuwa akiwaza atakataaje kama Hamza akiomba kitumbua chake, hakutaka hata kufikiria kitakachotokea.

“Eliza mbona hakuna taulo huku?”Sauti ya Hamza ilisikika kutoka bafuni na Eliza mara baada ya kumsikia alikumbuka taulo ambazo amenunua hakuziweka bafuni na haraka haraka alichukua moja na kuipeleka.

“Nakuachia hapa mlangoni , toka uchukue”Aliongea lakini dakika hio hio mlango wa bafuni ulifunguliwa wote na Hamza aliekuwa uchi bila wasiwasi alionekana mbele ya mrembo huyo

“Ahhhh…!!”

Eliza mara baada ya kuliona dudu kwa macho yake alijikuta mwili wote ukipata moto huku aibu ya kike ikimshika na kugeuka pembeni.

“Wewe .. unafanya nini sasa?”

“Njoo tuoge wote basi”

“Hapana.. nguo zangu zitaloa”

“Zivue sasa .. ngoja nikusaidie”Aliongea Hamza ila Eliza alitaka kukimbia lakini kabla hata hajapiga hatua alikuwa ameshashikwa vizuri na kuzibwa mdomo na kuvutiwa bafuni na nguo zote kuondolewa mwilini.

Dakika chache baadae ilikuwa ni miguno mingi ya kimahaba iliokuwa ikisikika kutokea chumbani , huku sauti tamu ya Eliza akilalamikia utamu wa dudu ilisambaa chumba kizima huku mwenyewe akijihisi yupo dunia nyingine kabisa..

SEHEMU YA 101.

Familia ya Mzee Mpoki kutoka Bagamoyo ni moja ya familia ambazo zinasifika sana kwa uvuvi kwa muda wa zaidi ya miaka therathini.

Mpoki ambae ndio baba wa familia yote ni kama alikuwa akitaka wanafamilia wake wote wajue maana halisi ya uvuvi licha ya kwamba watoto wake walikuwa waajiriwa na wenye biashara za kuwakidhi kimaisha.

Kila ifikiapo mwanzoni mwa mwezi wa kumi huchukua familia yake yote katika boti na kwenda kuvua samaki pamoja kama sehemu ya kukumbukia enzi ya safari ya biashara zake za kuvua samaki.

Ikiwa ni saa tano za usiku katikati ya bahari ndani ya boti mke wake pamoja na mke wa mtoto wake wote walikuwa wamekwisha kulala na yeye na mtoto wake walikuwa nje ya boti wakijipatia mvinyo kidogo kuchangamhsa miili yao huku wakiendelea na uvuvi , stori kubwa walizokuwa wakizungumzia ni nyakati za raha na shida walizopitia kama familia mpaka kufikia wakati huo.

Lakini ghafla tu wakati wakiwa bize kuongea sauti ya hatua za mtu zikitokea nyuma ya boti zilisikika.

“Nani kaamka?”Aliongea Mzee Mpoki.

“Nadhani kuna anaenda kujisaidia”Aliongea kijana ambae sio mwanafamilia ila mara nyingi huambatana na familia hio.

Mtoto wa Mzee Mpoki alishangaa maana alijua namna mke wake na mama yake walivyokuwa waoga wa giza la bahari , hata kama walikuwa wakiamka kwenda kujisaidia ilikuwa ni ngumu kutoka nje kabisa ya boti.

Dakika hio wakati wakijiuliza , kivuli cha mtu kiliweza kuonekana , mtu yule alikuwa ni kama mzimu ulioibukia kutoka baharini , alikuwa ameloa nguo zake zote huku akiwa ametapakaa mimea ya baharni , mbele ya shati upande wa tumboni palikuwa pamechanika lakini mwili wake ulikuwa sawa.

“Wewe ni nani?”

Baba na mwana walijikuta wakisimama kwa hamaki huku wakishangazwa na mtu huyo aliekuwa akifanana na mzimu.

Lakini sasa licha ya kuuliza swali hilo , mtu yule aliwapotezea bila ya kuwajibu na mara baada ya kuona Korosho na samaki wakuchoma juu ya meza , ni kama ukichaa ulimvaa na alisogea kwa haraka na kukwapua korosho zile na kuzipeleka mdomoni

“Huyu ni binadamu au ni Mzimu?”Mtoto aliwaka kwa hasira na alinyanyua kibenchi kilichokuwa karibu yake na kumpiga nacho yule mtu mgongoni.

“Bang!!”

Kibenchi kile kiliharibka lakini mtu yule hakuonekana kuwa na maumivu hata kidogo na aliishia kugeuka tu na kumwangalia yule mtoto wa Mvuvi kwa macho ya kutisha yaliokuwa mekundu kama yamevilia damu kwa ndani.

Mtoto alijikuta akishikwa na hofu huku akimwangalia yule mtu kama mzimu.

Yule Mzimu mtu alisimama na kisha kumsogelea yule mtoto wa mvuvi na kisha akamkaba shingo kwa nguvu na kuizungusha, kilikuwa kitendo cha sekunde chache tu mtoto yule wa kume wa mvuvi alikufa palepale huku uso ukigeukia mgongo.

Baba alijikuta akishitushwa na swala lile na alipiga kelele kama mnyama akimsogelea yule mtu kwa kasi akitaka kupigana nae , lakini yule mtu hakutishika hata kidogo na kwa nguvu ya ajabu yule Mvuvi alipigishwa kichwa chake chini na kupoteza maisha palepale.

Kitendo kile cha kuona baba na mwana kupoteza uhai , kijana aliekuwa ni msaidizi wa familia ile hakutaka kuuliwa kikatili na palepale alijirusha majini.

Yule mtu Mzimu wala hakujali na aliendelea kufakamia chakula kilichokuwa mbele yake kwa namna ambayo ni kama kichaa na alionekana alitaka kukidhi njaa yake kwa dakika chache iwezekanavyo.

Dakika ileile mke wa yule mvuvi alitoka kuja uelekeo wa alipokuwepo mume wake na mtoto wake mara baada ya kusikia purukushani , lakini kitendo cha kujitokeza na kuona kile kilichokuwa kikiendelea alijikuta akipiga ukulele na kumfanya yule Mtu Mzimu kugeuka na kumwangalia mwanamke huyo aliezeeka kwa macho yaliojaa uovu na palepale alionekana kutamka maneno.

“Ninachotaka kula lazima kilike”

Yule mwanamke alikuwa katika hofu kubwa mo na kitu pekee alichoweza kurusha kujitetea ni ndoo ya maji kutaka kumpiga nayo mtu yule na kitendo kile ni kama kilimuongezea ukichaa yule Mtu Mzimu na alimsogelea kwa kasi na kisha alimshika kwa nguvu na kumtupia baharini.

Alitoa kilio kikubwa mno cha kuomba msaada asaidiwe asizame na kumpelekea mke wa mtoto wake kutoka usingizni.

Mara baada ya Mke mwana aliejaaariwa sura ya urembo kutoka nje ya Cabin ya boti ile na kukutana na sura ya mtu huyo aliekuwa kama mzimu,hakuwa hata na muda wa kujitetea kwani alikamatwa palepale.

“Ahhhhhhhhhh…niachee!!”

Mwanamke yule aliishia kupiga kelele za kuomba kuachiliwa na jitu lile , licha ya mwanamke yule kutokuwa mrembo sana lakini nguo aliovalia ilimfanya kumchoresha vizuri umbo lake na kulifanya lile jitu kushikwa na joto la moyo na kutaka kulitolea kwake.

Mara baada ya kuona mwanamke huyo anajaribu kumletea ukinzani alimchapa vibao vitatu vya nguvu na kisha palepale alichana gauni lake na kumuacha uchi na hakuchukua muda mrefu mwanamke yule alionekana kupiga yowe kwa nguvu la maumivu ya kubakwa.

“Mamaaaaa.. !!!!”

Sauti ya mtoto wa kiume iliokuwa kwenye mshituko mkubwa kwa kile alichokuwa akifanyiwa mama yake iliweza kusikika kutoka nyuma ikiita kwa nguvu huku ikiambatana na kilio kikali , lakini lile jitu bahari halikumwachia kabisa yule mwanamke na kuendeleza kile alichokuwa akifanya.

******

Asubuhi hatimae miale ya jua ilipenyeza katika chumba na kumwamsha Hamza ambae alikaa kitako na kumwangalia mwanamke ambae alikuwa amelala unono pembeni yake.

Shuka lote jeupe lilikuwa limeufunika mwili wake mzuri huku ngozi laini ya mebega yake ikionekana wazi kiasi kilichopelekea mapigo yake ya moyo kuanza kwenda mbio.

Hamza alishindwa kujizuia na kupeleka mkono kwenye nyusi za Eliza na kuzipitishia kidole na kitendo kile kilimfanya mrembo huyo kutingishika kana kwamba amehisi kitu na kumfanya afumbue macho yake.

Eliza alijikuta akiangalia mwili wake uliojifunika nusu na shuka na mara baada ya kuangalia sura ya mwanaume iliokuwa na tabasamu mbele yake hakushituka hata kidogo , lakini mara baada ya kukumbuka kile kilichotokea usiku ghafla tu alivuta shuka lote na kujifunika gubigubi akikataa kumwangalia Hamza

“Haha.. nini tena sasa?”

“Usiniangalie..”

“Kwanini nisikuangalie”

“Nikiamka nakuwa mbaya”Aliongea akiwa ndani ya shuka na kumfanya Hamza kukosa neno la kuongea na kushangazwa na kauli yake

Kwa mtazamo wa Hamza, Eliza hakuwa na mabadiliko makubwa awe amejipodoa ama bila kujipodoa na hio yote pia ni kwasababu Eliza sio mtu wa kuvaa makeup, lakini bado alihisi kuwa mbaya kwasababu ndio ameamka kutoka usingizini.

“Eliza nimeona kila kona ya mwili wako tayari , hebu jifunue basi ni kukisi kidogo”

“Wee sitaki , hujapiga mswaki”

Hamza hakujua acheka ama alie , kulikuwa na maelezo mengi kwa hali kama hio lakini kadri alivyokuwa akimwangalia aliona ndio inamfanya azidi kuvutia na hakuweza kujizua na kujikuta akizidi kumpenda.

Dakika kumi mbele Hamza alitoka bafuni na kumwangalia mrembo huyo ambae alikuwa akionyesha aibu zake za kike na alimsogelea na kumbusu kwenye lipsi zake.

Mwanzoni Hamza alitaka kumuuliza mrembo huyo kama anampenda na wanaweza kuendelea lakini mara baada ya kutoka bafuni na kukutana na jicho legevu la mahaba , aliona kabisa hakuna hata haja ya kuuliza maana kila kitu kinajielezea.

Eliza alipoteza bikra yake hajitambui wakati akiwa mdogo mara baada ya mpenzi wake kumuwekea dawa za usingizi kwenye kinywaji na kumuingilia , hivyo hakuwahi kuhisi utamu wa penzi ulivyo , lakini usiku wa jana yake mara baada ya kuona utamu halisi wa dudu alijikuta akijishangaa na kujiuliza inakuwaje dunia ikawa na kitu kitamu namna hio cha kufurahisha moyo, japo mwanzoni aliona ni kama kinyaa kwa Hamza kumlamba sehemu zake za siri lakini akikumbuka utamu wake alishindwa kuzuia msisimko wa mwili wake.

“Umetembea na wanawake wa ngapi kabla yangu , kwanni upo vizuri sana?”Aliuliza na kumfanya Hamza kucheka kivivu.

“Zamani wanawake ndio waliokuwa wakinihudumia na sio mimi kuwahudumia”aliongea Hamza.

“Kwahio unasema mimi ndio wa kwanza kunifanyia vile?”

“Ndio”Aliongea Hamza akiwa siriasi lakini ajabu mrembo huyo alijikuta akiangua kicheko.

“Wewe ni muongo Hamza , hebu lione”Aliongea kwa sauti ya puani huku akicheka.

Hamza upande wake aliishia kucheka , ilikuwa ni mara yake ya kwanza kula mbususu tokea akanyage ardhi ya Tanzania , kuhusu kuwa mzoefu hakutaka kufikiria sana.

“Nahisi maumivu huko chini , umeyasababisha yote haya halafu mimi natakiwa kwenda kazini , unataka wanioneje nikionekaa natembea kwa kuchechemea”Aliongea.

“Basi haina haja ya kwenda kazini , tutakaa wote nyumbani”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la uchokozi.

“Wewe siaki , ulivyonichosha jana sitaki uendelee kukaa hapa”

“Kwanini sasa mpenzi , Lizzy unajua nimejizuia sana mbele yako, kwanini unataka kunikatiri baada ya kunionjesha”

“Wewe muone nakutania tu , halafu kwanza najua Regina akisharudi hutopata hata muda wa kulala na mimi hapa”Aliongea na Hamza hakuongea chochote zaidi ya kufikira na kuona hana cha kuogopa maana hakuwa akilala na Regina.

“Nataka kwenda kukutengenezea kifungua kinywa , unataka kula nini?”Aliuliza Eliza.

“Wewe si ndio umesema unaskia maumivu hapo chini , au ndio mbinu zako za kivita?”

“Unaongea ujinga gani , kwanini unachowaza ni hayo mambo tu?”

“Ni kwasababu sijali kifungua kinywa ila najali wewe kuwa kifungua kinywa changu”Aliongea Hamza na ile anataka kumshika tena ili kupata cha asubuhi simu yake ndio iliomzuia kuendelea baada ya kuanza kuita.

Sasa Hamza mara baada ya kuangalia anaepiga na kugundua ni Dina alijikuta akishangaa na kujuliza mwanamke huyo anataka nini mpaka kumpigia simu asubuhi asubuhi.

“Dina kuna tatizo?”Aliongea Hamza mara tu baada ya kupokea.

“Wewe, jana umeua mtu?”Aliuliza.

“Umejuaje haraka hivyo nimeua mtu?”

“Umemuua mtoto wa Mzee Azimu halafu unaongea kawaida hivyo , yaani Hamza wewe utakuja kunipa mshituko wa moyo”

“Azimu ndio nani?”Aliuliza Hamza.

“Azimu ni mfanyabishara ila nguvu yake kubwa inatokaa na kupata msaada mkubwa kutoka nchi ya asili yake”Aliongea Dina

“Kama unamaanisha India najua hayo yote , ila nimemuua huyo Farhani kwasababau alivuka mpaka , yaani mtu anichokoze halafu nimuache hivi hivi tu bila ya kufanya chochote , na hasira zangu namaliza vpi?”Aliongea Hamza huku akiona Dina anayakuza ili hali ni mambo madogo sana.

“Shida umeniletea hawa watu kwangu , wenye ndugu yao wapo hapa na wanataka mimi ndio nitoe taarifa zako na wamemhusisha mstaafu Mgweno katka hili ili kukulipizia kisasi”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura na kuona ni kama alivyotarajia ila hakushikwa na hofu hata kidogo.

“Kwahio unasema mstaafu Mgweno anahusika katika hili?”

“Sijajua ila Azimu na Mheshimiwa Mgweno ni marafiki wakubwa sana , tena wa muda mrefu hivyo ni sawa tu kumuunga mkono Azimu kama anataka kulipa kisasi, taarifa zilizonifikia ni kwamba Familia ya Azimu wameomba msaada kutoka India kwa ajili ya kuleta wataalamu wa mapigano Tanzania kumuongezea mstaafu nguvu ili kupambana na Eliasi na familia ya Wanyka ambao wameunganisha nguvu kuondoa utawala wake wa muda mrefu”Aliongea Dina.

“Ndio maana jana nilikutana na mtu anaetumia nguvu za kichawi kutoka dhehebu kubwa la mafunzo kutoka India , kumbe knachoendelea ni hiki?”Aliongea Hamza.

“Hamza hebu fikiria kwanza namna ya kumaliza hili swala, kabla ya mambo hajawa magumu”Aliongea Dina kwa wasiwasi lakini Hamza alicheka.

“Dina acha woga , huyo Azimu sidhani ana nguvu kiasi cha kuniogopesha , hata kama anapata msaada kutoka nchi ya asili yake haimaanishi kwamba anaweza kufanya chochote ndani ya ardhi ya Tanzana hata kama aungane na Mgweno ni bure kama anapambana na familia ya Wanyika”Aliongea Hamza.

“Sio kama nakuwa muoga , ni kwamba kwasasa nchi licha ya kuonekana kutulia lakini kuna mengi ya chinni chini yanaendelea hususani haya mabadilishano ya kmadaraka baada ya uchaguzi wiki ijayo , hata kama unaweza kuwa na nguvu ikionekana una hatarisha usalama wa nchi itakuwia ngumu kwako kuendelea kubakia hapa nchini”Aliongea.

Japo kauli ya Dina ilionekana nyepesi lakini Hamza alijua anachomaanisha , alijua hata kama ananguvu kiasi gani serikali ni serikali tu na wenye nguvu wakiamua kufanya kitu itakuwa ngumu kudili na kila kitu yeye mwenyewe huku akilinda wapendwa wake.

“Hao watu waliokuja kwako kama bado wapo hapo wasubirishe nakuja”Aliongea Hamza na kisha alikata simu.

“Vipi ni wale watu wa usiku sio?”Aliuliza Eliza kwa wasiwasi.

“Usiwe na wasiwasi , ngoja niende nikaweke mambo sawa na nitarudi”Aliongea Hamza mara baada ya kutingisha kichwa

Eliza alitaka kuongea kitu lakini alionekana kusita.

“Eliza unakumbuka nlichokuambia wakati tukiwa kule Morogoro?”Aliuliza Hamza na Eliza aitngisha kichwa kukumbuka.

“Chochote kitakachotokea unatakiwa kuamini uwezo wangu basi na kila kitu kitakuwa sawa”Aliongea kumkumbushia.

“Kama ni hivyo naomba tu uwe makini , ukifanikiwa kuweka mambo sawa nipigie simu”Aliongea na Hamza alitabasamu na kumbusu kisha akavaa nguo zake na kuondoka.

Wakati akiwa njiani simu yake ilianza kuita kwa mara nyingine na mara baada ya kuangalia jina la mpgaji alikuwa ni Amiri na alipokea.

“Vipi kaka?”

“Kaka hujarudi tu , kuna tatizo nataka unisaidie , jana nimegundua kitu kisicho cha kawaida kuhusu Mellisa”Aliongea Amiri kwa kupaniki na kumfanya Hamza kukunja sura kidogo.

“Kuna mgahawa wa kuuza chai maeneo ya Kijichi si unaufahamu?”Aliuliza Hamza.

“Ndio kaka na ufahamu japo sijawahi kuingia hapo?”

“Saa tano tano njoo hadi hapo tutaongea”

“Sawa kaka , Asante sana kaka , mambo ni magumu hata sielewi”

“Hakikisha unafika huo muda tutaongea”Aliongea Hamza na kisha alikata simu na kuwasha gari na kuliondoa.

Dakika chache tu Hamza aliweza kufika Kijichi na kuingiza gari katika mgahawa wa Dina.

Nje alonekana Lawrence ambae ni kama alikuwa akimsubiria na mara baada ya kumuona alimsogelea na kisha alimzungusha kwa nyuma na kumpeleka sehemu ambayo wageni wake walikuwepo.

Mara baada ya kuingia tu ndani aliweza kumuona yule bwana wa jana aliepambana nae , anaefahamika kwa jina la Regani akiwa na baadhi ya wanaume wengine ambao hakuwa akiwafahamu lakini wote walikuwa na muonekano wa kihindi.

Dina alikuwepo ndani ya ofsi hio na mara baada ya kumuona Hamza amefika alionyesha wasiwasi huku akilazimisha tabasamu.

“Hamza umefika, karibu wanakusubiria”Aliongea na Hamza alitngisha kishwa na kukaa chini.

Regani bado alikuwa na wasiiwasi katika uso wake kana kwamba alikuwa akikumbuka kile kilichotokea jana.

“Nasikia mnanitafuta , mnapanga vpi kudili na mimi?”Aliuliza Hamza

“Mr Hamza ijapokuwa unaonekana kama mtu ambae una uwezo mkubwa lakini huwezi kudharau ukubwa wa familia yetu, kwasababu ya kuwa mshirika na Dina mkuu wa mtandao wa Chatu nadhani unajua mpaka hapa swala hili hatutaki kudli nalo kisheria maana haliwezi kutupa majibu tunayoyataka”Aliongea bwana ambae alitwa Zabi.

“Farhani ndio mtu ambae alitaka kumchukua mwanamke wangu na baada ya kushindwa akafyatua risasi , lakini kwanini ninachoona hapa ni kama mmejaa chuki na mimi ilihali alieanzisha ni ndugu yenu?, kitu kingine inaonekana alikuja kulazimisha kuwa na Eliza kwasababu ya imani zenu za kichawi?”Aliongea Hamza

“Hata kama amekukosea haikuwa sawa wewe kumuua , tumekuja hapa ili kupatamaelezo ya kutosha la sivyo taswira yetu itaharibika”

“Mnataka nni sasa? , maana naona ni kama mmemtoa kafara ndugu yenu na mnaanza kunishutumu mimi niliewasaidia”Aliongea Hamza.

“Tumesikia wewe ni mtaalamu wa mapigano ya hali ya juu sana na unazo mbinu nyingi , tumewasiliana na Mkuu wa dhehebu letu kutoka India na ili kulinda heshima ya familia zetu zilizotapakaa dunia nzima unapaswa kupambana na mtu atakaechaguliwa kuja Tanzania”

Hamza alifikiria kwa muda na aliona sio wazo baya , isitoshe licha ya kujua Farhani ametolewa kafara kichawi na yeye kukamilisha kafara hio , lazima abebe uwajibikaji wa kukamilisha jambo hilo katika macho ya watu wa kawaida ili walinde heshima yao.

“Hakuna shida nakubali , mnapanga kumleta nani na wapi tunaenda kufanya hayo mapigano?”

“Mkuu alisema usafiri kwenda India lakini baada ya majadiliano mkuu kaamua kuja mwenyewe Tanzania na pambano litafanyikia Singida makao makuu ya Familia ya Mzee Azimu”Aliongea.

“Haiwezekani yafanyikie Singida, mnataka aende Singida kwasababu ni miliki yenu na kuna uwezekano mkawa na hila nyingne”Aliongea Dina

“Dina kwahio unataka mtu wetu aende wapi , kama akija kupambana hapa si inamaanisha pia wamekuja kwenye miliki yako na watakuwa hatarini?”Aliongea Zabi.

“Kwanini tusitumie ulingo wa Nungunugu ndani ya jumba la Tajiri Laizer?”Aliongea Regani na Dina alitaka kukataa pia lakini Hamza alimzuia.

“Hakuna shida , tutaenda kumaliza kazi hapo , sina muda wa kupoteza hivyo mtu wenu akishatua nchini nipeni taarifa”Aliongea Hamza.

Mara baada ya Hamza kukubaliana na masharti yao Regan na wenzake walianza kujadiliana na kisha walifanya mawasiliano moja kwa moja kwa kile walichoafikia kwenda kwa wakuu wao.

“Kwaninni umekubali kwenda kutumia ulingo wa Tajiri Laizer, hivi hujui pale ni eneo la Mgweno ila anamtumia Laizer tu kama mwakilishi?”Aliongea Dina kwa hasira

"Cha msingi ni kushinda , kwanini nijali wapi naenda kupambania?”Aliongea Hamza.

“Shida hujui huyo mtu anaetoka mbali kotea huko India ana uwezo gani , lakini unakubali kirahisi rahisi , Hansii licha ya kuaminika kuwa na watu wenye mapigano ya hali ya juu lakini vilevile ni walozi wakubwa Asia yote”Aliongea Dina.

“Sikia Dina , kwenye maisha yangu nishawahi kupoteza pambano mara moja tu na siwezi kupoteza kwa mara ya pili”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Dina kukumbuka Hamza alishawahi kumsimulia tukio la kushindana na mwanamke na akamchakaza vibaya mno.

“Unamzungumzia yule mwanamke uliewahi kuniambia?”

“Ndio na ile ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho , siwezi kuruhusu kufeli tena kwa mara ya pili”Aliongea Hamza na kumfanya Dna kuishia kutingisha kichwa pkeee.

“Sijui hata kujiamini kwako kumetoka wapi namna hio”Alongea.

Upande wa Dina licha ya hivyo alipata ahueni mara baada ya kuona mambo yamemalizika namna hio , Hamza akishinda maana yake hakuna uhasama tena

Upande wa Hamza alijua kabisa mtu ambae anasafirishwa kutoka India kuja kupamaban nae anaweza asiwe wa kawaida hata kidogo , kitendo cha Regani kuona uwezo wake na kwenda kuusimulia ni lazma watakuwa wapo makini.

Hansee licha ya kwamba lilikuwa dhehebu kubwa ndani ya India lakini mambo yao yalikuwa ya siri mno ,isitoshe ni maswala yanahohusiana na ulimwengu wa Giza.

Kawaida ilikuwa ni kwamba licha ya Hamza kumuua Farhani ambae alikuwa katika misheni ya masharti ya imani yao ,swala ambalo linatafsiriwa kama ajali kazini , lakini siku zote kwa nje ili kulinda heshma yao lazima watume mtu ambae ataendeleza ukubwa wa taswira yao.

*****

Saa nne kamili wakati Hamza akiwa mgahawani kwa Dina , Amiri aliweza kufika na gari yake ya Aud Q8 na alionekana kuwa na haraka mno.

Kwasababu Hamza alikuwa ametoa maagizo juu ya ujio wa Amiri haraka alielekezwa mpaka alipo.

“Mzee mbona presha hivyo?”Aliongea Hamza mara baada ya kusalimiana nae.

“Kaka mambo sio shwari”

“Kivipi?”

“Ukiachana na kile nilichopanga kukuambia kuhusu kilichotokea tukiwa safarini , ila nilichosikia jana mpaka sasa hata sijaelewa”

“Ongea ni kipi ulichosikia?”

“Jana nilikuwa Cask Bar na washikaji wa Kenya waliokuja kunitembelea , wakati tukiendelea na stori za hapa na pale alikuja jamaaa hivi ambae anaonekana kutokujua kiswahili na akaniambia ana maongezi na mimi”

“Washikaji walishangaa hata mimi pia nilishangaa maana jamaa hata simfahamu , ila alionekana kunifahamu vyema na aliponiambia ni swala linalohusiana na Mellisa hata sikutaka kumkatalia”

“Enhe .. baada ya kuongea amekuambia nini?”

“Kaniambia anajua kila kitu kuhusu wasiwasii wangu juu ya Mellisa”

“Alikuambia hivyo?”

“Ndio , lakini kubwa zaidi ambalo limenishangaza ni pale aliposema Mellisa ni wakala wa Night Shadows”Aliongea Amiri na jambo lile lilimshangaza Hamza.

“Wakala wa Night Shadows!!”

Muda ule ni kama Hamza alianza kukumbuka alishawahi kukutana na makala Jamiiforum ikizungumzia uwepo wa viumbe wanaojionesha kwa binadamu kama vivuli na hakuwahi kuamini kuhusu habari hizo.

“Ndio kaka , kaniambia hivyo , kasema wasiwasi wangu juu ya Mellisa unatokana na sababu ya Mellisa kukubali nafsi yake kutumika kama njia ya mawasiliano na moja kwa moja kuwa wakala wa Night Shadows”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kushangaa zaidi.

“Umesema huyu mtu hakuwa akijua kiswahili? , vipi alikuambia ametokea wapi?”

“Ndio amesema ni msharika wa kanisa la Wabrazili . ndio kasema kama siamini maneno yake ushahidi wa kunithibitishia anao”Aliongea Amiri kwa mchecheto mbele ya Hamza kana kwamba alijua Hamza atamsadia kila kitu.

Upande wa Hamza aliamini pengine inaweza kuwa kweli na palepale alikumbuka juu ya kazi aliompatia Sally ya kufuatilia ile lugha aliokuwa akiongea Mellisa na alipaswa kuifatilia jana ileile lakini kutokana na swala la Saidi alisahau na aliona muda huo ni mzuri wa kufatualia.

“Huo ushahidi upo wapi na unahusiana na nini?”Aliuliza Hamza kwa shauku ya kuaka kujua.

ITAENDELEA.
contacts 0687151346
 
Upande wa Hamza aliamini pengine inaweza kuwa kweli na palepale alikumbuka juu ya kazi aliompatia Sally ya kufuatilia ile lugha aliokuwa akio🔥🔥🔥ngea Mellisa na alipaswa kuifatilia jana ileile lakini kutokana na swala la Saidi alisahau na aliona muda huo ni mzuri wa kufatualia.

“Huo ushahidi upo wapi na unahusiana na nini?”Aliuliza Hamza kwa shauku ya kuaka kujua.

ITAENDELEA.
contacts 0687151346
🔥 🔥🔥🔥
 
Thanks Mr Singano the great, Hadi lini tena
 
yan hata mim mwenyew nashangaa wakuu zangu ujue hii mara ya pili amekula ban
Dah hii nchi n ngumu sana kuendelea, sasa kazi kubwa ya mods n kupiga watu ban badala ya kutatua changamoto kibao kwenye forum..
Hivi kweli mitandao kikubwa kama FB, X na Instagram wangekua na mentality za Mods kusoma kila stori na kufungia watu ingekua mikubwa hivo???
 
zaidi ya kutoana kwenye malengo tu
 
Back
Top Bottom