Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

mkuu singano amekula ban ya mwaka mzima hvyo cjui tutakuwa na alosto ya muda gani
 
Ingekuwa hekima kama mtu mwingine kwenye group la whatsapp angeendelea kutupia humu wakati Tunasubiri singanojr atoke kifungoni🤔
 
Itaendelea mpaka nitakapoweka mambo sawa na Mods, kwenye grupu kutoa simulizi kuleta huku ni kosa

Mambo gani ya kuweka sawa mghosi kuna niniii tuweke wazi kwani kutupostia story ni kosa? Kwamba unavunja sheria
 


SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI: SINGANOJR

contact watsapp;0687151346



SEHEMU YA 102.


Hamza alimwangalia Amiri ili kuweza kusikia jibu ake, alitaka kujua kwanza ni ushahidi gani ambao unazungumziwa na kisha ndio aanze kutafakari ni mtu gani ambae alimwambia hayo yote na kwa ajenda ipi.

“Hakunipa maelezo ya kutosha , ila kitu alichoniambia ni juu ya Mellisa kuwa mteja wa vyungu kutoka kwa kampuni ya Elix na hapo ndio palipo nichanganya, nilimuuliza kununua vyungu kuna husiana vipi na swala aliloongea lakini hakunipa majibu zaidi ya kuniambia nifuatilie kama nataka kuamini maneno yake.”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kushangaa kidogo , alikuwa akijua kuhusu swala la vyungu.

“Hio kampuni ya Elix unaijua na je wanauza hivyo vyungu?”Aliuliza Hamza maana kidogo kuna kitu ambacho hakuwa amekielewa , aliamini ni Alex na kampuni yake pekee ndio waliokuwa wakisambaza vyungu vile ambapo alipata kujua ni njia ya usafirishaji wa Stimula kama alivyoambiwa na Frida.

“Nimefuatilia kampuni ya Elix, inajihusisha kutengeneza dawa za binadamu, makao yake makuu ni Mikocheni”Aliongea Amiri.

“Ulivyofuatilia uligundua wana huduma ya kutengeneza vyungu?”Aliuliza Hamza.

“Hawana na nimeshindwa hata kuuliza , inakuwaje kampuni ya Elix kuuza vyungu , yule jamaa sikutaka kumwamini maneno yake moja kwa moja na kuonekana mjinga , lakini jambo hili bado linanisumbua akili yangu kulingana na matukio ya Mellisa”Alongea Amiri na Hamza alifikiria kidogo hakutaka kumwambia kuhusu Alex na uuzaji wake wa vyungu kwa kuona anaweza kumuingiza katika hatari.

“Kwanini usimuulize Mellisa?”Aliongea Hamza.

“Lakini kaka, kasema huu ni ushahidi , nikumuuliza Mellisa si itakuwa ni kuharibu ushahidi?”

“Huyo mtu si umesema humjui , basi huna haja ya kufanya kama vile anavyotegemea wewe utafanya , Mellisa ni mpenzi wako , kabla ya kutafuta ushahidi wa nje unatakiwa kupata majibu kutoka kwake,akikudanganya ndio unaweza kuchukua hatua nyingine”Aliongea Hamza na Amiri alifikiria na kuona ni jambo ambalo linaleta maana.

“Inabidi nifanye hivyo kaka”

“Fanya hivyo, akikupa majibu ndio utajua ni hatua gani uichukue , huyu mtu nina uhakika amekuja kwako kwa ajili ya kukuchanganya na kwa ninavyokuona hapa kafanikiwa nusu , ila usiendelee kumpa ushindi , mara nyingi watu wa namna hii wanakuwa na ajenda zao wanataka kuzikamilisha kupitia wewe , hata kama alichosema kinaweza kuwa kweli unaweza kuwa mtego wa kumuingiza Mellisa kwenye hatari au wewe mwenyewe”Aliongea na Amiri aliringisha kichwa.

“Sijakosea kaka kukuchagua kama rafiki yangu”Aliongea Amiri na Hamza alicheka.

“Halafu kaka akili ilikuwa haijatulia na sasa naona ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuwa sehemu kama hii , unafahamiana na huyu mrembo wa hapa nini?”Aliuliza Amiri kisanifu.

“Wewe unamjua?”

“Nani asiemjua , Bro Robert alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wakimfukuzia mno huyu mrembo na kujitamba atakuwa mwanamke wake na sasa kanywea”Aliongea Amiri.

“Robert gani huyo?” Aliuliza na Amiri alishika pua yake na kuona ameongea kitu ambacho Hamza hajui.

“Sijui kama unamfahamu ila ni mbunge wa jimbo la Ukonge , pia ni mtoto wa mheshimiwa Raisi Eliasi”Aliongea Amiri na palepale alimkumbuka Robert kwa kujua ni yule bwana aliebeti nae kulenga shabaha kwa kutumia bunduki huku malipo ikiwa ni kutomsumbua Dina tena.

“Kwahio unafahamiana na huyu Robert?”

“Nafahamiana nae ila sina ukaribu nae , Binamu yangu ni marafiki wakubwa sana , eh tena si umesikia swala la bosi wa kampuni ya Voducum ambae inasemekana alikuwa muuaji mkatili wa wanawake?”Aliuliza Amiri na Hamza alitingisha kichwa.

“Robert na Bosi Side ni marafiki wa karibu sana na imeshangaza jana wakati anahojiwa alisema ni mtu anaefahamiana nae tu ila hawana ukaribu , ila kwa nafasi yake nimeweza kuelewa maana Saidi ameacha makovu kwa watu wengi , hata mimi sikuamini kama ni yeye aisee”Aliongea Amiri huku ule wasiwasi ukimpotea kabisa wakati wa kuanza kuzungumzia swala la Saidi.

Upande wa Hamza aliishia kutabasamu tu maana alikuwa akijua yeye ndio muhusika wa kila kitu aliefankisha tukio la Saidi kukamatwa.

Baadaya maongezi kidogo Dina alijiunga nao na Hamza alimtambulisha Amiri kama Dina ni mpenzi wake jambo ambalo lilimfanya Amiri macho kumtoka asiwe ni mwenye kuamini.

Lakini kadri alivyokuwa karibu yao aliweza kujua ni kweli Hamza hakuwa akitania na aliishia kutingisha kichwa kumkubali.

“Bro unajua moja ya sifa yangu kubwa nini ?”Aliuliza Amiri wakati Hamza akiagana nae na Hamza alitingisha kichwa kukataa.

“Ni macho ya rohoni”Aliongea.

“Unamaanisha nini?”

“Unajua tokea siku ambayo nilikuona ukiwa umempigia magoti Anitha kule chuoni niliona kitu ambacho wengne hawakukiona ndo maana nilitaka kuwa rafiki yako”

“Ah.. kitu gani hicho mbona unanitisha?”

“Niona sio kama ulikuwa ukimpenda yule Anitha mpaka kumpigia magoti vile mbele ya watu , bali ulikuwa ukiigiza tu , mimi nakuambia hivyo kwasababu nishawahi fanya tukio kama lile , ila utofauti wangu na wako mimi nilifanya nikiwa na dhamiri ya dhati ila wewe yalikuwa maigizo hivyo ilikuwa ni rahisi kukuelewa”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kukunja sura kidogo huku akikuna kichwa chake.

“Kwanini unasema hivyo bro wakati uliona kabisa hata chozi liliniitoka?”Aliongea Hamza huku akikumbuka tukio lile.

“Wewe ni jasusi kaka , mimi nina macho ya kuwajua majasusi siku zote , lile tukio tafsiri yake ni kama kuna watu ulitaka waone tukio lile na ndio maana hata baada ya kukataliwa hukuwa na wasiwasi, ulionekana kama vile hakuna kilichotokea na chuo ukawa unakuja kama kawaida , Bro nakuambia shida zangu kwasababu najua wewe ni mtu ambae unaweza kunisaidia , wewe ni jasusi na majasusi mna upeo mkubwa wa mambo”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kucheka.

“Uko vizuri kwenye kusoma watu , huenda ikawa kweli mimi ni jasusi”

“Huna haja ya kuongea Bro nazijua sheria, halafu tukiachana na hayo Anitha ananisumbua sana haha…”Aliongea Amiri.

“Anasemaje?”

“Sijui kapatwa na macho ya rohoni kama mimi au vipi , lakini ghafla anaonekana kukuulizia mno kwa kukudadisi”Aliongea na kumfanya Hamza kukumbuka mwanamke huyo alikuwa akimtumia meseji nyingi.

“Sirudii mwanamke alienikataa mbashara , si itakuwa dharau bro , heshima ni kutafuta chombo kizuri kuliko yeye kumkomesha”

“Upo sahhi na kwa hilo umefanikiwa asilimia mia moja , Bosi Dina ni mwanamke mrembo sana ambae hata mimi kwa ujanja wangu sidhani ninaweza kumsogelea , Kama Robert kashindwa ila wewe umefanikiwa, Saluti kwako Bro”Aliongea na kumfanya Hamza asijue acheke ama alie ila aliishia kuagana tu na Amiri.

Ukweli ni kwamba alichoongea Amiri kilikuwa sahihi kwa asilimia mia moja , tukio la Hamza kumpigia Anitha magoti na kuanza kumtongoza sio kama alimpenda sana ila kuna watu waliokuwa wakimfuatlia na alitaka kuwaaminisha tofauti na kile walichokuwa wakimuwazia ndio maana alifanya vile.

Hata kwa Anitha pengine alishangaa maana Hamza hakuwahi hata kumomba namba na ghafla tu siku mwanaume anatokea na Ua mbele yake na kumpigia magoti na kumtaka wawe wapenzi , ila kwasababu Anitha ni mwanamke wa kawaida asingefikiria mbali kama alivyofanya Amiri, yalikuwa maigizo ya Hamza kujificha zaidi asigundulike hakuwa wa kawaida.

Saa tisa kamili za mchana Dina alipokea simu kutoka kwa Zabi na Regani wakimtaarifu waelekee eneo la tukio kwa ajili ya pambano.

Dina hakutaka Hamza kwenda peke yake hivyo aliingia kwenye gari moja na kuelekea huko.

Mara baada ya kufika , kwasababu Hamza haikuwa mara yake ya kwanza kufika hivyo hakupata shida sana kama ilivyokuwa siku ile alivyofika akiwa na Eliza.

Mara baada ya kuingia katika ukumbi huo wa mapigano chini ya ardhi, waliweza kukutana na bosi Laizer ambae alikuwa na muonekano usiokuwa ukielezeka lakini alijitahidi kuonyesha tabasamu.

“Hamza usione upo salama kwa kumuua mtoto wa Mzee Azimu?”Aliongea Laizer akiwa na tabasamu feki lakini upande wa Hamza hata hakuzingatia sana alikuwa akichunguza eneo hilo ambalo lilikuwa tofauti siku hio kwa kukosa watu.

“Mbona leo hakuna watu kabisa hapa au mmefunga biashara?”Aliuliza Hamza na kauli yake ilimfanya Laizer hasira kumpanda.

“Hasara ulionitia siku ile ndio imesababisha haya yote?”Aliongea Laizer.

Ukweli ni kwamba mara baada ya Hamza kumshinda Maddog siku ile ni kama wateja wote walikosa hamu tena ya kuja kumwangalia Maddog akipigana , moja ya sababu ambayo iliwafanya kuvutiwa nae ni kutokana na kutoshindwa ulingoni na mpinzani yoyote lakini baada ya kushindwa na Hamza hawakuja tena.

Hata wale ambao walikuwa wakija walikuwa wachache sana na pia Maddog alitoweka na kumfanya kuzidi kupata hasara , kwa ufupi mauzo yake yalipungua sana na kutokana na hilo alianzisha ratiba maalumu za maonyesho.

Muda huo huo macho ya Laizer yalichanua kwa furaha pamoja na uovu ndani yake mara baada ya kuona watu wakiingia ndani ya eneo hilo.

“Hamza mpinzani wako amekwisha kufika”Aliongea

Hamza hata yeye aliweza kuhisi uwepo wa askari mwenye nguvu za ziada akisogelea eneo hilo , aligeuza kichwa chake palepale na kuangalia upande huo na aliweza kumuona mwanaume mwenye muonekano wa kihindi na msisimko wake wa nguvu za kichawi ulikuwa kama uleule wa Regani.

Mwanaume huyo alikuwa na nywele ndefu nyeusi ambazo zimechanwa kurudishwa nyuma , alikuwa amevalia nguo kama gagulo na ilikuwa ngumu kujua alikuwa amevaa sketi au suruali.

Alikuwa na uso uliopauka mno na ilikuwa ngumu kukadiria umri wake , lakini macho yake yalikuwa yakionyesha ni mtu ambae ana uzoefu wa kutosha.

Kulikuwa na wanaume wawli aliotangulizana nao , mmoja Hamza alimjua alikuwa ni Regani na mwingine alikuwa Chotara wa kihindi alievalia suti nyeupe ya Armani , alikuwa akionekana kama mwanaume ambae ana mafanikio makubwa kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana.

“Hamza ngoja nikutambulishe watu hawa , huyu ni Mdogo wake Marehemu Farhani anaitwa Majid na huyu ni Master Jagani kutoka Hansii na ndio mkuu wa Shiriki yetu”Aliongea Regani.

“Wewe ndio umemuua kaka yangu?”Aliuliza yule bwana aliefahamika kwa jina la Majid akimwangalia Hamza kwa macho makali.

Hamza aliishia kutoa kejeli ya ndani kwa ndani , aliona ijapokuwa bwana huyo alikuwa na hasira kwa nje lakini moyoni alikuwa akichekelea.

Ilionekana dhahiri yeye kama mtoto wa pili ndani ya familia yake , kifo cha kaka yake ilimaanisha yeye ndio anaekwenda kurithi utajiri wa baba yake.

“Ni mimi ndio , unauliza kwasababu unataka kulipiza kisasi?”Aliongea Hamza.

“Leo aliefika hapa kwa ajili ya kulipiza kisasi ni mkuu wetu kutoka nchi ya Asili , Mkuu wetu yupo mwishoni mwa levo ya Kabla ya mbingu katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , kama una neno la mwisho la kuongea ongea kabla ya kifo chako”aliongea yule bwana lakni Hamza aliishia kutingisha mabega.

Levo ya mzunguko kamili maana yake ni levo kabla ya mbingu , mara nyingi Askari au shujaa wa mapigano wa levo hio anakuwa na uwezo wa kuubusti mwili wake kinguvu kwa kukusanya nishati ya ndani ya mwili wake na kuiwianisha na nishati ya mazingira na kumfanya kuwa na uwezo mkubwa mno katika kushambulia.

“Hebu tuache porojo , ni muda wa kupambana na kumaliza hili swala haraka iwezekanavyo , napanga kuwahi kurudi nyumbani baada ya hapa”Aliongea Hamza

“Unaongea sana ilihali huna nishati yoyote ya nguvu kwenye mwili wako , ngoja nione ni kwa muda gani utaendeleza majigambo yako”Aliongea yue bwana na mara baada ya kauli hio aliruka na kwenda kutua kwenye ulingo, lakini kilichomshangaza Hamza ni kwamba sauti ya bwana yule ilibadilika na kuwa ya kizee ghafla licha muonekano wake mwanzoni ulikuwa ni wa kijana.

“Nini kinaendelea katika Shirki yenu , yaani sauti inasikika ya kizee lakini mwili wake unaonekana kama ni wa kijana?”Aliuliza Hamza

Hamza kwa uelewa wake wa haraka haraka wa sautilcha ya kuongea kihindu alijua bwana huyo lazima atakuwa katika miaka kati ya sitini au sabini hivi lakini kwa nje alionekana kama vle alikuwa na miaka therathini au hamsini.

“Acha maneno mengi”Aliongea na palepale kwa staili ya kungfu alimsogelea Hamza na kumpiga kibao cha kifua ambacho ameunganisha na nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi.

Lakini licha ya kumpiga Hamza kwa nguvu eneo la kifua chake hakusogea hata inchi na kilichosikika ni kishindo kikubwa.

Bam!!

Hamza aliishia kumwangalia mzee huyo kwa macho ambayo hayakuelezeka.

Jagani alijikuta akishikwa na mshangao mara baada ya kuona licha ya kutumia nguvu kubwa kumshambulia Hamza lakini hakukuwa na madhara alioyapata na mbaya zaidi hakusogea hata kidogo , alikuwa akijua nguvu ya shambulizi lake hata kama mtu ana mafunzo ya nishati za mbinug na yupo levo ya mzunguko kamili hawezi kupokea shambulizi hilo bila ya kupata shida lakini Hamza hakuwa na ishara yoyote ya kuwa na nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi, ilimfanya ajiulize maswali mengi.

“Wewe mwanaharamu ni mbinu gani ya mafunzo ya mapigano unajifunza?”Aliongea huku akionyesha kuwa na hasira na muda ule alimsogela Hamza kwa pigo la karate akitaka kumlenga eneo la kichwani.

Lakini kabla hata hajamfikia Hamza na kumshambulia mkono wake ulidakwa hewani na kilichoweza kusikika ni mifupa ya mkono kuvunjika.

“Crack.. Crackk”

“Arghhhhhh!!”

Ukulele wa maumivu kutoka kwa Jagani uliweza kusambaa eneo lote na kufanya kila mtu alieshuhudia tukio lile kushikwa na mshituko.

“Inawezekaneje.. mkuu wetu na yeye amepi..”Regani alishndwa kuzuia mshituko wake, alitamani sana kuona Hamza akishindwa lakini hakuamni mkuu wake ndio anaenekana kuchezea kichapo.

Laizer na Majid na wenyewe walijikuta wakikunja ndita na waliishia kuangaliana na palepale walionyesheana ishara ya tabasamu la uovu ndani yao kama kwamba wanafurahia kile ambacho Hamza anamfanyia yule mhindi.

Katika ulingo Jagani kwa hasira sana alimwangalia Hamza na alijitahidi kadri awezavyo kuvumilia maumivu na kwa mara nyingine alitoa shambulizi akirudia mpango wake uleule wa kumshambulia Hamza kichwani , lakini mara baada ya kumsogelea, Hamza alisogea pembeni na kisha akaudaka mkono wake wa kulia na kuupindisha tena na kuvunja mifupa yake.

“Ni kama nilivyootea…, unaonekana kutumia toniki kwa ajili ya kupunguza kasi ya kuzeeka ndio maana unaonekana mdogo kuliko umri wako si ndio?”Aliongea Hamza na bwana yule hakumjibu na Hamza aliendelea kuongea.

“Kama nipo sahihi India kuna sheria ambayo inakataza watu kutumia toniki ambayo inawafanya kuonekana wadogo ilihali uhalisia ni wazee, kama nyie mnatumia basi nina uhakika dhehebu lenu sio kubwa kama nilivyowafikiria”Aliongea Hamza.

Kwa uelewa wa Hamza ni kwamba zipo mbinu za kichawi na za kiroho ambazo mtu hutumia nguvu yake ya ndani kunyonya kitomvu cha mtu mwingine ili kujipatia hali ya uhai wake huku anaenyonya kuongeza hali ya uhai wake na kumfanya kuonekana kuwa kijana, ilikuwa sawa kabisa na namna ambavyo watu hunyonya nguvu ya ukike ama ukiume kwa njia ya kufanya mapenzi , ilikuwa ni mantiki hio hio ya kunyonya kitomvu cha mwingine ili kuchukua ile hali ya ujana wa mtu huyo.

Lakini sasa licha ya kwamba hizi mbinu ni za kichawi na zinafanyika haikumaanisha kwamba mtu akishanyonya anakwenda kuishi maisha marefu , bali kinachobadilika ni muonekano wake tu pekee, utajiuliza kwanini fulani hazeeki kumbe kazi yake ni kunyonya watu vitomvu kichawi.

Miaka kadhaa ya nyuma serikali za mataifa mengi kama vile Brazli , India na China kulikuwa na kasumba ya mambo haya ya kichawi, licha serikali haikutangaza wazi wazi kutambau uzushi huo lakini kupitia vitengo vyao vya kupambana na nguvu za giza vilipiga marufuku mambo hayo ya kishirikina.

Katika ulimwengu wa kawaida kiongozi wa nchi anaweza kukuambia serikali haiamini katika maswala ya uchawi lakini kiongozi huyo huyo ni muumimi mkuu wa kafara za kichawi.

Sasa Hamza kutokana na uzoefu wake alikuwa akifahamu hilo na alijua pia kuna makundi ambayo yalikuwa pia yakitumia hii mbinu kujitengeneza kuoekana vijana na moja ya makundi hayo ni Black Trinity, licha ya watu kutumia mbinu ya mapenzi kujiongezea uwezo wa nguvu za kiroho lakini vlevile walitumia mbinu hio ya mapenzi kuongeza mvuto na muonekano wao wa nje.

“Unaongea ujinga gani , muonekano wangu hautokani na unachongea wewe bali ni mbinu ambayo dhehebu letu limeigundua”Aliongea kujitetea na Hamza alitoa tabasamu.

“Kama unachoongea ni sahihi , kwa vile ninavyojua mimi viongozi wa haya makundi ya wavuna nishati mara nyingi wanatembea na mbinnu zao ili zisiibiwe na makundi mengine , hivyo kama unachoongea ni sahihi kwanini usinionyeshe hio mbinu nithibitishe”aliongea Hamza

Na bwana yule mara baada ya kusikia kauli hio alianza kupaniki na kutaka kuondoka ndani ya hilo eneo maana alishajua atashindwa lakini Hamza asingempa hio nafasi hivyo aliishia kuhangaika kujipapasa na kisha alitoa karatasi lililokunjwa kunjwa kwenye kifua chake na kumpatia Hamza.

Kitendo kile kilimfanya Regani na Majid kupaniki , hawakutegemea mkuu wao angekuwa dhiafu kiasi kile tofauti na walivyotegemea.

“Hamza kuangalia siri za mapgano za kundi lingine sio sheria katika ulimwengu wa sanaa ya mapginano”Aliongea Regani.

“Sijali maswala ya mbinu yenu mnayofanya , ninachotaka kujua hapa ni kama mnachojifunza kimepigwa marufuku au ni halali”Aliongea Hamza.

Regani mara baada ya kusikia vile aliishia kufubaa na kwa hasira aliruka na kuingia kwenye ulingo kwa dhamira ya kumshambulia Hamza , lakini kabla hata shambulizi lake halijamfikia mguu wake ulikwisha kukamatwa na alirushwa nje ya ulingo kama furushi.

Mara baada ya kuona upande wake hakuna ambae anamuweza Hamza , Majidi alimpa ishara Laizer na palepale bwana huyo alitoa simu yake na kufungua upande wa app ya vidio call na kuongea.

“Hamza acha kabisa kutaka kugusa siri ya mafunzo yetu la sivyo mpenzi wako Eliza kuna kitu kitamtokea”Aliongea Laizer.

Hamza aliishia kumwangalia Laizer na tabasamu ambalo halikuwa tabasamu .

“Oh! nini kimetokea Eliza?”

“Angalia mwenyewe utajua tunachomaanisha”Aliongea Laizer na kumsogelea Hamza akimpatia ile simu , lakini dakika ambayo alikuwa akitaka kuongea alisikia sauti ya mtu na kufanya aangalie simu ile na ndipo alipoweza kuona sura ambayo haikuwa ya watu wake.

“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa hasira.

“Naitwa Afande Mwiba , wewe si ndio tajiri Laizer nani kakupa ruhusa ya kuvunja sheria za nchi na kuagiza watu wako kuteka raia?”Aliongea yule Afande.

“Afande Mwiba ndio jina gani mbona sikujui mimi”Aliongea kwa kubabaika kutokana na bwana yule kutovaa gwanda na upande wa pili Afande yule alitoa badge inayomtambulisha na kisha kumuonyesha.

“Malibu!!?”

Wa kwanza kuongea hivyo alikuwa ni Majidi na alionekana kuwa na hofu baada ya kujua ni mwanajeshi kitengo cha Malibu.

“Ni vizuri mnajua kitengo chetu , hebu mpatie Hamza simu”Aliongea Afande Mwiba.

Tajiri Laizer na Majidi walikuwa na hofu mno , licha ya kwamba familia yao kwa nje ilikuwa ikionekana kama familia ya kawaida lakini ni watu ambao walikuwa wakijihusisha na mambo ya ulimwengu wa giza tena kwa kutumia nguvu za giza na kuvuna nishati , sasa siku zote makundi hayo ambayo yalikuwa yakivuna nishati yalikuwa yakiogopa kitengo cha Malibu kwani kuingia kwenye lada zao ilimaanisha uhalifu , hata upande wa Laizer alikuwa ameonywa na mheshimiwa mara zote aepuke kitengo cha jeshi cha Malibu kwani hakifuati maagizo ya kisiasa zaidi ya kufanya vile wanavyoona ni sahihi kwa ajili ya usalama wa nchi na hakuna wa kuwazuia hata kama awe raisi.

Kilichowapa hofu wakati huo ni kutokujua Hamza alikuwa na mawasailiano ya karibu na kitengo hicho na walienda moja kwa moja na kudhania pengne Hamza pia ni mwanajeshi maana siku zote walikuwa wakijua wanajeshi wa kitengo hicho uwezo wao ulikuwa mkubwa na hata Hamza uwezo wake ulikuwa mkubwa pia hivyo ilileta maana kufikiria hivyo.

Laizer aliishia kulazimisha tabasamu na kisha akampatia Hamza simu.

“Haha.. inakuwaje ni wewe Afande?”Aliuliza Hamza huku akiwa ni mwenye kucheka lakini dakika ileile iliongezeka sura ya mtu mwingine,alikuwa ni Afande Caro maarufu kama afande Barafu.

“Hamza kuwa na amani mpenzi wako Eliza yupo salama”Aliongea Afande Caro huku akiwa na tabasamu na Hamza mara baada ya kusikia kauli ile alijikuta akijihisi ni mwenye shukrani.

“Haha.. asanteni sana , nikirudi nadhanti tutakaa tutaongea vizuri nitawapa ofa pia ya chakula cha usiku”Aliongea Hamza

“Hamza .. usiwe na wasiwasi hawa wamejitambulisha kwangu ni wanajeshi na watanilinda , vipi huko uko salama?”aliongea Eliza alijitokeza kwenye skrini.

“Niko sawa , wewe endelea kukaa nao na usitoke leo”

“Sawa”

Hamza mara baada ya kukata simu aliitupa chni na ikapasuka vipande vipande na kisha aliwapotezea watu hao waliokuwa wakitetemeka na kisha alifungua ile karatasi na kuanza kusoma kilichokuwa kimeandikwa.

Kila kitu kilikuwa katika maandishi ya lugha ya kitamil lakini kwa bahati nzuri Hamza alikuwa akielewa lugha hio vizuri

Kilichomshangaza ni kwamba andiko hilo lilionekana kuwa la muda mrefu mno na kadri ambavyo alikuwa akisoma macho yake yalizidi kuonyesha hali ya mshangao.

“Mmetoa wapi hili andiko”Aliongea Hamza.

















SEHEMU YA 103.

Jagani hakuamini Hamza alikuwa akijua lugha hio na aliishia kumeza mate mengi huku akijibu.

“Ni andiko lililoachwa miaka mingi na mababu zetu , niliiba kwenye maktaba ya siri ya India”Aliongea yule bwana kwa hofu akijua kabisa kama Hamza ni mtu wa kitengo basi hana haja ya kuficha kwani zipo mbinu nyingi za kufanywa aongee.

Ukweli ni kwamba dunia nzima kulikuwa na ushirikiano wa kijeshi katika kudili na maswala yanayohusiana na nguvu za ziada na ikitokea tukio limetokea Tanzania na kitengo cha Tanzania kikahitaji maelezo India basi moja kwa moja watajua na ushirikiano utatolewa.

Sasa Jagani kwasababu andiko hilo lilikuwa muhimu na aliliiba katika Maktaba ya nyaraka za siri za nchi yake maana yake kama taarifa zitafka atakuwa mhalifu wa kitaifa kwa kuiba nyaraka za serikali.

“Nani mwingine anajua uwepo wa hili andiko?”Aliuliza Hamza.

“Ukiachana na mkutubi wa Maktaba ya India mmi na Regani ndio tunafahamu siri yake”Aliongea.

“Kuna siri kubwa ya mafunzo kwenye hili andiko na wengi waliamini ni kitu ambacho kilipotea duniani mara baada ya maktaba ya Great Britain kuungua, lakini nashangaa muda wote mlikuwa nalo na mnachofanya pekee ni kutumia kujifanyisha kuwa vijana”Aliongea Hamza.

“Mr Hamza kama unaona lina thamani kwako lichukue ila usije ukatoa siri yetu juu ya kuliiba”Aliongea yule mzee.

“Hiki ni kipande chake tu , sehemu yake nyingne iko wapi?”aluliza Hamza

“Ni kipande , hatuna uelewa huo”Aliongea na kumfanya asijue acheke ama alie , ilionekana licha ya kushikilia nyaraka hio muhimu lakini bado hawakujua kama haijakamilika.

“Basi hakuna shida nitapokea hili andiko”Aliongea Hamza na Jagani alijikuta akifurahi , alijiambia hakuna hasara hata akipoteza andiko hilo maana ni zaidi ya miaka ishirini tokea aanze kulisoma hivyo anao uwezo wa kuandika alichokariri upya, lakini kwasababu uhai wake muda huo ni muhimi alijitilisha huruma mbele ya Hamza.

“Mr Hamza tuna macho lakini tumeshindwa kukufahamu wewe una uwezo kuliko sisi , tafadhari pokea andiko letu na uniachie niendelee kuwa hai na sitolalamika kwa kulichukua”Aliongea.

“Ndio huwezi kulakamikamaana hapa ndio mwisho wako”Aliongea Hamza na kabla hata hajashangazwa na maneno ya Hamza alikuwa tayari ashashikwa shingo yake na ikazungushwa na palepale akapoteza uhai.

“Mkuu..!!”

Walijikuta wakipiga kelele huku Regani akijikuta akifubaa baada ya kuona tukio hilo , palepale akili yake ilimwambia akimbie lakini alikuwa amechelewa kwani Hamza tayari alikuwa mbele yake.

Hamza hakutaka hata kumchelewesha mara baada ya kumfikia alimtandika teke ambalo lilimfyatua kama mpira na kwenda kujigonga kwenye ncha ya kingo za jukwaa na kuishia kuachia damu tu na kudondoka chni akiwa hana uhai tena.

Laizer na Majidi waijikuta wakitetemeka na hawakuamini Hamza alikuwa na uwezo wa kumshinda mkuu wao , siku zote familia yao iliotapakaa dunia nzima ikifanya biashara walikuwa wakijivunia uwepo wa dhehebu lao la Hansii na kurahisisha mambo mengi kwa kujenga koneksheni na wanasiasa lakini leo hio ni kama wameamshwa kutoka kwenye usingizi.

Upande wa Hamza sababu ya kumuua Regani na Jagani ni kwasababu ya andiko hilo , maelezo yake yaliokuwa humo ndani aliona ni ya hatari sana kama yatasambaa kwa mtu ambae ana uelewa mkubwa na nia ovu, hivyo ili kujibakisha ni yeye tu anaejua ndio maana aliwapoteza palepale.

“Ndio naondoka zangu , kuna mwenye pingamizi?”Aliuliza Hamza akimwangalia Majidi na Laizer.

“Hakuna pingamizi , Mr Hamza ondoka kwa amani na naomba unisamehe pale nilippokukukosea”Aliongea Majidi akishindwa kujua hata amemkosea wapi Hamza.

“Ndio Hamza tunaomba radhi kwa yote yaliotokea , sikujua kama wewe ni mtu wa kitengo cha Malibu , tafadhari tunaomba upotezee hili lililotokea leo”Aliongea Laizer huku awamu hio akiwa na heshima tofauti na siku ile.

Hamza wala hakujali ,baada ya kumaliza alimchukua Dina na kisha waliondoka kwenye jumba hilo , upande wa Dina licha ya kwamba aliona Hamza amedili na swala hilo kirahisi lakini lazima kuna uwezekano kujenga chuki kwa watu wa ulimwengu wa giza isitoshe makundi mengi yanapenda sana kununua ugomvi.

“Hamza ni kitu gani kilichoandikwa kwenye hio karatasi ?”Aluliza Dina.

“Hata mimi nataka kwenda kuelewa kilichomo ndani licha ya kwamba najua ni kitu ambacho sio cha kawaida , wale watu wametumia andiko hili kujifunzia ila licha ya kuonekana vijana hawakuimarika kinguvu , kuna namna walikuwa wanakosea”Aliongea Hamza

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba andiko hilo linaelezea mbinu ya kutozeeka?”

“Sina uhakika lakini ipo hivyo , ngoja nisome nielewe maana lugha yake ni ya zamani sana na nikishapata uelewa wake nitakuambia wewe kwanza”Aliongea Hamza na kumfanya Dina kutoa tabasamu kama lote.

“Basi tubadilishe mada na tuongee kuhusu Eliza kwanza , unaonaje ukinikutanisha nae nimfahamu , si leo haendi kazini?”Aliongea Dina.

“Unataka kuonana na Lizzy?”

“Haiwezekani?”

“Sijamaanisha hivyo”

“Kama hujamaanisha hivyo naona ni vizuri kama nikifahamiana nae mapema , ili tuwe na maelewano”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria kidogo na aliishia kutoa kicheko.

“Nadhani upo sahihi , kama vipi nitawakutanisha”Aliongea Hamza huku akijiambia ikitokea Dina akifahamu ameshamla kitumbua Eliza kabla yake sijui atasema nini,isitoshe ni Dina ambae alikuwa akililia dudu kwa muda mrefu kabla ya Eliza ambae alikutana nae baada ya kufahamiana na Regina.

*****

Hamza mara baada ya kurudi Dar na kwenda nyumbani kwa Eliza aliweza kuwakuta Afande Mwiba na Afande Caro wakiwa bado hawajaondoka.

Hamza hakutegemea kama angewakuta wakiendeea kusubiri na alijua pengne kuna kitu kingine walichokuwa wakitaka , isitoshe hakujua ilikuwaje mpaka wakaamua kumlinda Eliza wakati yeye akienda kupambana.

Kwasababu muda ulikuwa umeenda Hamza aliwaalika kuelekea mgahawani kwa ajili ya kupata chakula cha usiku.

Hivyo Hamza , Eliza na Dina pamoja na maafande hao walielekea katika moja ya mgahawa uliokuwa ukipatikana ndani ya eneo hilo hilo la Kigamboni maarufu kwa kuchoma nyama ya mbuzi.

Kitendo cha Eliza kukutana na Dina kidogo ilimfanya Eliza kukosa utulivu lakini Dina alitumia ukubwa wake na kuanza kuongea na Eliza na dakika chache mbele walionekana wakipiga stori kwa kuanza kuzoeana.

Upande wa Hamza aliagiza kilo za kutosha za mbuzi na kuwaambia maafande hao wale tani wanazotaka na atalipa lakini ni muda huo Afande Caro alichukua nafasi ya kuongea.

“Hamza vipi umeridhika na kazi tulioifanya leo?”Aliongea Caro na kumfanya Hamza aone lazima wanajeshi hao kuchukua hatua ya kumsaidia kumlinda Eliza kuna kitu wanataka pia kutoka kwake.

“Sio mbaya , ndio maana nimeamua leo kuwanunulia msosi”Aliongea huku akitabasamu

“Tusimruhusu Hamza kutulipia ,Mwiba hebu nenda kalipie”Aliongea Caro akimwamrisha Afande Mwiba.

Afande Mwiba licha ya kutopenda aliishia kusimama na kwenda kulipia kwa maagizo ya mkuu wake.

Upande wa Hamza aliishia kukunja tu sura na kujiambia hawa maafande wanaonekana wana mbinu za kuongea kivitendo , kulipa chakula chao maana yake ilimaanisha licha ya kwamba wamemsaidia lakini sio rahisi hivyo kuwashukuru kwa msosi pekee.

“Hamza sisi kama jeshi tumeona ni vyema kama tukiwa na ushirikiano nt mtu mwenye uwezo kama wewe , isitoshe pia una urafiki wa karibu na mshauri mkuu wa jeshi , hivyo tunatamani kama utatupigia debe”Aliongea .

“Lakini si jeshi la Tanzania linapandisha watu vyeo kulingana na mchango wao jeshini , kwanini niwapigie debe kwa Himidu, Au hata yeye alipigiwa debe sio kwamba alipanda vyeo kwa uwezo wake?”Aliongea Hamza na wanajeshi hao walionekana kukamatika.

“Nyie niambieni ni kitu gani mnachotaka niwasaidie msizunguke sana ilihali nyie ni wanajeshi”Aliongea Hamza na kumfanya mwanamama Caro kutabasamu.

“Nadhani ni kweli hatuwezi kukuficha na kuzunguka zunguka , ukweli ni kwamba tuna jambo tunaomba msaada wako”

“Hakuna shida nawaona ni kama mmekuwa marafiki zangu , kuomba msaada sio dhambi, nitawasadia hata kama ni swala linaloenda kinyume na sheria za nchi”Aliongea na kumfanya Caro kulaani ndani kwa ndani na kujiambia ni yeye ndio mtu anaeweza kufanya vitu vinavyoenda kinyume na sheria kwanini anataka kuwaambukiza.

“Ukweli ni kwamba sio swala gumu sana , ni kwamba tu sisi kama kitengo tunakosa nguvu kazi ya watu na kuna misheni ambayo inaendelea hapa nchini ambayo tunahtaji mtu mwenye utaalamu zaidi wa kimapgano ambae anaweza kutusaidia kwa ukaribu, ipo hivi tumepewa misheni kutoka kwa wakubwa zetu kumlinda moja ya mwanasayansi muhimu sana ambae tafiti zake zimevuja kupitia mashushu kwenda nje ya nchi, hivyo ndani ya kipindi hiki kuna majasusi wengi wametumwa kuzamia ili kumuua asikamilishe majaribio ya huo utafiti”Aliongea

“Kama kuna watu wametumwa kwanini msitumie jeshi kumlinda?”Aliuliza Dina.

“Shida sio swala la ulinzi tu , ukweli ni kwamba swala kama hili halikupaswa kuwa chini ya kitengo chetu lakini kutokana na ukubwa wake na watu waliotumwa kuwa na uwezo wa juu wa kuua , ndio maana limekuwa chini yetu , hivyo tunaweza kutuma watu wa kawaida kutoa ulinzi lakini wakashindwa kudhibiti baadh ya mbinu za kimauji , swala ambalo ni muhimu ni kwamba huyu mwanasayansi mwezi huu ataingia katika majaribio makubwa ya tafiti yake na kama atafanikiwa inamaanisha hatua kubwa katika utafiti huo , hivyo serikali ipo makini kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa bila dosari yoyote”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria kwa dakika kadhaa na aliona kama ni swala la kumlinda mtu halitakuwa swala kubwa sana kwake.

“Hakuna shida nitamlnda huyo mwanasayansi lakini niwaambie tu sitomlinda kwa muda mrefu”

“Bila shaka , tunachotaka ni usalama wake kabla na wakati wa majaribo na baada ya hapo jukumu tutalibeba , lakini majaribio hayo yatafanyikia nje ya maabara na ndio maana hatari ni kubwa , hivyo ili mradi ukikubali kusafiri na sisi kwa hizo siku tatu za majaribio tutashukuru sana”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakuona ni ombi kubwa , isitoshe pia kufanya hivyo ni kusapoti Tanzania katika nyanja ya sayansi na teknolojia.

“Huyo mwanasayansi anaitwa nani , ni mtu maarufu sana au ndio hawa wanaochipukia?”Aliuliza Hamza huku akinywa pafu la bia kiasi. Afande Caro alionekana kusita kumwambia kidogo lakini aliongea.

“Nadhani hakutakuwa na tatzo hata tukikuambia ukweli ni mtu unaemjua anaitwa Yulia..”

Kitendo cha Hamza kusikia jina hilo alijikuta akishindwa kuzuia mshituko na kumtemea kwa bahati mbaya pombe alioweka mdomoni Afande Caro.

“Wewe!”

“Hamza unafanya nini?”

Dina na Eliza ambao walikuwa wamesimama pembeni walijikuta wakishangazwa na kile kitendo cha Hamza na kujiuliza nini kinaendelea katika kichwa chake mpaka kumtemea mwenzake pombe.

Afande Carlo alikuwa ametemewa pombe mpaka uso wake wote ukaloa

“Samahani Afande Caro , jifute na hii tishu”Aliongea Eliza akimkabidhi tishu , hata hivyo alikuwa mwanajeshi na hakujali sana muonekano.

“Hamza nini kimetokea?”Aliuliza mara baada ya kumaliza kujifuta.

“Yulia inakuwaje akawa mwanasayansi , si mfanyabiashara yule?”Aliuliza Hamza.

Eliza na Dina pia walishikwa na shauku , ukweli ni kwamba Yulia alikuwa mwanamke maarufu katika biashara ndani ya Tanzania

“Haha.. wewe unamjua hivyo tu lakini sio taaluma yake kabisa , Yulia ni kiumbe mwenye akili sana , amepewa cheo cha ufanyabiashara kwasababu za ki usalama pekee , ndio hivyo tu sasa hivyo taarifa zake zimevuja”Aliongea Afande Carolline.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo ilibidi kwanza asogee pembeni na kisha kumpigia Afande Himidu simu.

“Bosi vipi , mambo yameenda sawa?”Sauti upande wa pili iliongea huku mtu huyo akicheka.

“Himidu mambo gani haya , mbona naona kama unaniingiza kwenye matatizo?”Aliongea Hamza

“Ah..! bosi unamaanisha nini , hata kama nipate ujasiri wa ziada mara elfu moja siwezi kukufanya chochote”

“Kama ni hivyo kwanini unataka mimi ndio nimlinde Yulia , hivi hujui ukorofi wa Yulia au ndio unanitafutia tu matatizo “

“Ah tena bosi usingeniambia kuhusu hili nisingekumbuka ila niliwaambia kwamba wakualike kama mlinzi kwasababu nyingne kabisa , isitoshe sikuona uhusiano wako na Yulia unaweza kuwa tatizo hususani kuhusiana na tafiti zake , ukiwa wewe kama msaada kwake nitakuwa na amani zaidi”Aliongea Hamza.

“Ni tafiti gani hizo kwanza?”

“Bosi hii ni taarifa ya siri ya daraja la juu kabisa , siwezi kukuambia kupitia simu , ukweli hata majasusi waliotumwa nchini kwa ajili ya kumuua Yulia hawajui hata ni tafiti gani anafanyia kazi , ila kama ukiwa nae katika majaribio hayo nina uhakika utaelewa ni tafiti gani”Aliongea Afande Himidu.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijihisi muwasho kwenye moyo wake.

“Himidu kwahio umewaagiza wanitafute mimi niwe mlinzi kwa malengo ya kuona hio tafiti ya Yulia si ndio?”Aliuliza

“Hahaha.. bosi nadhani umenielewa sasa , ipo hivyo kama ingekuwa ni kwa ajili ya kumlinda Yulia tu nisingekusumbua kabisa , ningemlinda mimi mwenyewe au ningempa kazi mtaalamu mwingine na hakuna ambae angeweza hata kumsogelea, nilitaka kukupa fursa ya kuona kinachoendelea na angalau kujua kwanini familia yake iliuwawa kipindi kile kule Sweeden mpaka ukajitolea kumuokoa”Aliongea Himidu akiwa siriasi.

“Okey nimekuelewa mkuu , sitouliza sana na nitaenda kumpa ulinzi”Aliongea Hamza na kisha aliagana nae.

Hamza alijikuta akivuta pumzi na kukumbuka siku ile alivyomuokoa kwa wale Stray Ninja’s kule Msat na kwa namna flani alianza kuelewa kinachoendelea.

“Afande mtanitaarifu tu siku na muda wa kuondoka kufanya hayo majaribio na tutaongozana”Aliongea Hamza mara baada ya kurudi kwenye nafasi yake

Afande Carolline hakuwa na tatizo baada ya kuacha namba za mawasiliano waliondoka yeye na Afande Mwiba.

Mara baada ya kumaliza kula , Hamza alitoa wazo kwa warembo hao kwenda Mlimani City kwa ajili ya kuangalia filamu mpya pamoja na ombi lake kidogo lilileta kashikashi kwa warembo hao kutokana walikuwa wawili lakini walikubali.

Mara baada ya kuondoka kwenda huko na kufika , waliweza kupata tiketi na kuingia ukumbini na hakuchukua muda mrefu movie ya kimarekani ambayo inazinduliwa katika kumbi zote kubwa duniani za Cinema ilianza kuonyeshwa.

Hamza alikuwa kama mfalme , alikuwa akijiamini vilivyo na aliwavuta wote wawli na kuwaegamiza kwenye mabega yake na warembo hao hawakuleta pingamizi na walikaa hivyo hivyo wakiendelea kuangalia filamu hio.

Wanaume baadhi waliokuwa wakishuhudia kitendo hicho waliamini lazima Hamza na warembo hao ni ndugu , maana hakuna mwanaume jasiri duniani wa kutembea na wanawake wawili wakati mmoja kama hivyo na wakawa wapenzi wake.

Lakini sasa starehe ya Hamza haikudumu muda mrefu mara baada ya simu yake kuanza kuita.

Mara baada ya kutoa na kuangalia anaempigia , aligundua alikuwa ni Regina na alijiuliza alikuwa akimtafutia nini au kagundua alikuwa na warembo katika ukumbi huo.

Hamza hakuwa na jinsi na alitoka nje haraka haraka kwenda kupokea .

“Wife kuna tatizo ?”Aliongea Hamza kwa sauti ya chini.

“Uko wapi?”

“Nipo ukumbini kwenye Movie.. namaanisha nje”

“Na nani?”Aliuliza mara baada ya kusikia kauli hio na Hamza alisita kidogo lakini kabla hata hajajibu Regina aliongea tena.

“Au achana na hilo , wewe endelea kuangalia tu filamu”Aliongea.

“Regi hebu acha kuwa na haraka , niambie kwanini umenitafuta?”Aliuliza Hamza na Regina alikaa kimya kwa muda mrefu na kisha kuongea.

“Gari imeniharibikia njiani”Aliongea kwa sauti ya kinyonge na kumfanya Hamza kushangaa na kujiuliza kwanini hakupigia fundi kwanza na kumtafuta yeye , lakini aliona kama asingempigia yeye inamaanisha Regina angeonyesha hakuwa akijali uwepo wake hivyo kwa namna moja alifurahi pia, alijiambia pengine Regina alitaka mume wake ndio aende akamsaidie.

“Niambie ulipo , nitakuja haraka hapo?”Aliongea Hamza na Regina alimwambia alipo na ilikuwa mbali mno nje ya Dar es salam.

Hamza ilibidi arudi ukumbini na kuwaambia kuna dharula imempata Regina na warembo hao hawakuwa na shida na kumwambia aende.

Hamza licha ya kuwa mnyonge kuwaacha warembo wake japo ndio aliemua kuwaleta hapo ila aliona Regina akikaa zaidi barabarani anaweza kupatwa na shida ya ki usalaama hivyo anapaswa kuwahi.

Hamza aliendesha gari yake kwa dakika kama arobaini mpaka kumfikia Regina umbali mfupi kutoka kiwanda cha sukari Bagamoyo.

Na baada ya kufika aliweza kuona BMW M6 ya rangi ya bluu ikiwa imeegeshwa pembeni huku vioo vyote vikiwa vimefungwa.

Mara baada ya kuegesha gari pembeni alishuka na kwenda kugonga kioo.

Regina mara baada ya gari yake kugongwa kwanza alishituka lakini alivyogundua ni Hamza alishikwa na ahueni na kufungua mlango.

“Reg.. kwanini ni wewe tu , Shangazi yupo wapi?”

“Shangazi kasema kuna mchungaji anaenda kuonana nae ili aje kufanya ibada nyumbani na nitangulie lakini nilivyofika hapa ghafla tu gari ikazima na nikiiwasha inawaka na kuzima”Aliongea Regina na Hamza alimwambia atoke ajaribishe kuliwasha na kweli kila linapowaka lilikuwa likijizima.

Ilibidi aangalie kiasi cha mafuta kilichopo na hapo ndio alijikuta akisikitika maana gari haikuwa na mafuta kabisa.

“Yaani gari haina mafuta na unataka iendelee kutembea kweli?”

“Lakini Dashboard hapo inaonyesha ninaweza kuendesha umbali wa kilomita hamsini?”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa kukataa.

“Haya ni makadirio tu lakini sio sahihi , ukiona hii alama ya taa ya mafuta imewaka mana yake unapaswa kujaza na sio kuendesha, una uzoefu mdogo mno na magari , au haijatokea gari kukuishia mafuta tokea uanze kuwa dereva ?”Aliongea Hamza.

“Sasa mimi najuaje hayo yote wakati sio fundi”Aliongea Regina huku akivuta mdomo mara baada ya kuona Hamza anamzodoa kwa kushindwa kuelewa kitu kidogo kama hicho.

Regina akijua Hamza anaenda kumlinda Yulia atatapika damu.

NB:Unazeeka zako kwa kasi kumbe kuna mwamba ananyonya kitomvu chako usiku kila siku

ITAENDELEA.
 
Back
Top Bottom