Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI YETU.



MTUNZI: SINGANOJR.



SEHEMU YA 106.



The Red sister’s

Ikiwa ni muda wa jua kuzama ndani ya nchi ya Tanzania , hakukuwa na mabadliko ya muda katika maeneo ya bahari ya Hindi yanayopakana na nchi za Somalia , Tanzania na Kenya.

Wakati miale ya mwanga wa jua ikiwa imesambaa juu bahari iliokuwa tulivu na kutengeneza mnunurisho kuvutia , katika meli ya maharamia wa The Shark , alionekana Kapteni Kenny ndani ya chumba akiwa ameloa jasho huku misuli yake kiwa imetuna kutokana na kile alichokuwa anafanya.

Chini yake katika kitanda alikuwepo mwanamke ambae alikuwa ametoa macho kama mfu huku mwili wake wote ukiwa umekufa ganzi na kukosa hisia zozote juu ya kile alichokuwa akifanyiwa.

“Bosi, Bosi”Sauti ya haramia ilisikika kwa nje na kumfanya Kenny kupunguza spidi kwa kile alichokuwa akifanya.

“Kuna nini wewe mshenzi?”Aliongea kwa kingereza.

“Kuna boti ya uvuvi inasogea kwa kasi upande wetu”Aliongea

“Pumbavu , hio boti ina nini mpaka kupaniki na kuniharibia starehe yangu?”Aliuliza Kenny kwa hasira maana siku zote wanakutana na boti nyingi za uvuvi.

“Hapana bosi , hii boti tunaitilia mashaka”Aliongea Haramia huyo na kumfanya Kenny kung’ata meno na kusimama.

“Okey , nimekuelewa natoka nje sasa hivi kuangalia”Aliongea

Baada ya kauli hio haraka haraka alivaa mavazi yake na kisha alimwangalia mwanamke yule aliekuwepo kitandani na kisha kwa kebehi aliongea.

“Huyu mwanamke bado ni mrembo lakini akili yake haifanyi kazi tena ni kama na**mba maiti”Aliongea na Harama aliekuwa mlangoni alicheka.

“Kapteni anahudumia watu zaidi ya nane kila siku na hana muda wa kulala , ni bahati tu mpaka sasa hivi hajakufa bado”Aliongea

“Nyie washenzi muache kutumia nguvu zenu sana kukojoa la sivyo mtajikuta hamna nguvu tukiingia vitani”Aliongea Kenny huku akicheka na kutoka ndani ya boti hio kwenda nje.

Muda huo kulikuwa na maharamia zaidi ya kumi na mbili ambao walikuwa wakikodolea macho boti iliokuwa inawasogelea.

“Bosi angalia ile boti , kuna watu wamekufa ndani yake”Aliongea bwana mmoja huku akimkabidhi Kenny Darubini.

Kenny mara baada ya kuangalia boti ile uso wake ulijikunja , ni kweli aliweza kuona wanaume wawili , mwanamke mmoja na mtoto wakiwa ni wafu.

Kulingana na uzoefu wake wa haraka haraka alijua lazima boti hio itakuwa inamilikiwa na familia ya mvuvi na waliofariki ni familia hio kwani kwa jinsi maiti ya mwanamke ilivyoonekana ni kama alikuwa amefanyiwa ukatili wa hali ya juu wa kijinsia.

“Inaonekana ni boti ya kifamilia na familia nzima wamekufa , nani anaiendesha?”Aliuliza Kenny na kufanya maharamia hao kuongea wao kwa wao wakiamini kuna kitu hakipo sawa.

Muda huo huo mara baada ya boti hio kuwafikia karibu kabisa na meli yao alionekana mwanaume ambae nguo zake zimejikunja huku akiwa na ndevu nyingi na masharubu , uso wake ulikuwa hauna muonekano mzuri kabisa na macho yake yalidhihirisha ukatili, alikuwa ni kama binadamu ambae nafsi yake imetekwa.

Mtu yue aliinua macho yake akiwa kwenye boti ile na kuwaangalia maharamia hao wa kundi la The Shark na alionekana ni kama mtu ambae anawaza jambo.

“Hey , wewe ni nani?, ndio umewaua hao watu wote kwenye boti yako?”Aliuliza moja ya haramia.

Lakini yule mtu mwenye muonekano mbaya hakujbu swali lake badala yake aliruka kutoka katika boti yake na kwenda kutua juu ya meli hio kwa urahisi wa hali ya juu.

Kitendo kile kiliwafanya wale maharamia kuwa katika hali ya tahadhari kwani kutendo cha mtu huyo kuweza kuruka katika meli yao yenye urefu kwenda juu waliamini sio mtu wa kawaida.

Mtu yule aliwaangalia wale maharamia bila hali ya hofu hata kidogo na macho yake yalidhihirisha ukauzu na kejeli.

“Kwanzia leo hii meli ni ya kwangu”Aliongea yule mtu kwa sauti nzito

Maneno yale yaliwashangaza wale maharamia na kumfanya Kapteni Kenny kutoa kicheko kikubwa mno cha masikitiko.

“Unasemaje wewe , nadhani sijakusikia vizuri na kama upo sahihi unanijua mimi nani?”

“Sijali wewe ni nani , kwanzia sasa unapaswa kutii kila ninachoongea kama bosi wako”Aliongea yule mtu

“F*ck huyu kiumbe atakuwa kichaa , Kapteni ngoja tumuue tu”Aliongea Haramia huku akikoki bunduki yake kwa haraka na palepale alimlipua yule mtu .

“Bang!!”

Jeraha liliweza kuonekana katika kifua cha yule mtu na aliinamisha kichwa chake na kuangalia lile jeraha na palepale alivua shati chafu alilokuwa amevalia na aliingiza vidole viwili kwenye lile jeraha na kisha kuchomoa ile risasi.

Kitendo kile kiliwafanya maharamia wote macho kuwatoka wakiwa hawaamini.

“Hii nii…”

Mara baada ya risasi ile kuitoa kilichowashangaza zaidi ni mara baada ya kuona lile jeraha likianza kupona kwa kasi mno mpaka kufunga na kitu pekee kilichobakia ilikuwa ni ushahdi wa damu tu.

Tukio lile lilimfanya Kapteni wa meli hio bwana Kenny kushikwa na kihoro na kumwangalia kwa hofu.

“Wewe ni nani haswa?”Aliuliza huku ubaridi wa hofu ukimpitia mgongoni kwake , alifikiria pengine anachokiona ni juu ya zile stori alizosikia juu ya viumbe wanaofanana na binadamu wanaotokea wakati wa jua kuzama.

Yule mtu hakuongea neno na palepale aliwasogelea wale maharamia na kitendo cha wao kutaka kumshambulia walijikuta wamechelewa bada ya kugundua alikuwa na spidi kubwa kuliko isivyokuwa kawaida na kushindwa kabisa kumlenga.

Bwana yule aliishia kuchukua kisu kulichokuwa katika mmoja ya maharamia na kuanza kuwachinja.

Kenny palepale aliweza kuona hali haikuwa nzuri hataa kidogo na anapaswa kuchukua hatua maana ndani ya dakika moja amekwisha kupoteza vijana wake kumi.

Alijikuta hasira kali ikimvaa na palepale alikusanya uwezo wake wote wa nishati ya ndani na kisha kuuwianisha na nishati ya bahari na kumshambulia yule mtu.

Mtu yule ni kama alimuacha Kenny kumshambulia ngumi mbili kifuani kwake na baada ya pale alimshika mikono yake na kisha kichwa chake na kukipigisha kwenye ukingo wa meli na kilipasuka palepale na kuacha uji mweupe , alikuwa ni kama amegongwa na gari.

Bwana yule mara baada ya kumuua yule Mrusi palepale alitumia kisu kilichokuwa chini na kisha alimkata Kenny mkono na kuanza kunyonya damu yake huku akitoa kicheko cha hali ya juu, mara baada ya kuona umekauka aliutupia pembeni na kisha alianza kuchinja maharamia waliokuwa wamebakia katika ile meli , waliosalimika walikuwa ni wachache sana ambao waliamua kurukia majini ili kuepukana na kuchinjwa , lakini zaidi ya mahaatamia mia moja walipoteza maisha palepale ndani ya dakika chache tu na kufanya meli hio kujaa damu nyingi ambazo zilitirika na kuingia majini.

Mara baada ya kuona amekwisha kumaliza kazi aliishia kutabasamu akifurahishwa na damu na viungo vya watu hao na palepale alipiga hatua na kuingia ndani ya kibanda cha meli hio.

Na kitendo cha kuingia tu aliweza kumuona mwanamke ambae amejificha kwenye kona akitetemeka.

Mwanamke huyo ngozi yake ilionekana kuwa na makovu mengi kutokana na kufanyiwa ukatili na alikuwa akitoa harufu kali hata kwa umbali wa mita kadhaa.

Yule mwanaume wa kutisha alimwangalia yule mwanamke ambae alikuwa ni kama mnyama aliengia kwenye mtego wa mwindaji na hali ya tamaa ilimvaa palepale.

Mwanamke yule mwili wake wote pamoja na hisia vilikuwa vmekufa ganzi kabisa na alitumia macho yake kumwangalia yule mwanaume kwa umakini lakini palepale macho yake yalionekana kuchanua kama mtu ambae alikuwa kwenye giza muda mrefu na hatimae ameweza kuona mwanga.

“Sa.. sa.. Saidi!?”Aliita kwa nguvu akiwa ni kama haamini.

Mwanaume yule mara baada ya kusikia jina lake likiitwa alisimama na kuacha kusogea huku muonekano wake ukitoka katika hali ya ukatili na kuwa ya mtu wa kawaida.

Kitendo cha kusikia jina lake feki la Saidi badala ya Adamu ilimfanya abadilike palepale na kujihisi binadamu.

“Wewe ni nani… unanijua mimi..?”Aliuliza Saidi huku mikono yake ikianza kumtetemeka , alikuwa ni kama mtu ambae ametoka kwenye ndoto ya kutisha.

Upande wa yule mwanamke ilikuwa ni kama amemuona mwokozi wake na palepale alianza kutambaa kutoka alipokuwa na kwenda kuikumbatia miguu ya Saidi.

“Mimi ni Lamla , mke wa Wilsoni Dosam , familia inayomiliki makampuni ya Dosam , tuliwahi kuonana kwenye tafrija ukiwa na James, wewe ni Saidi ndio sijakufanansha.. tafadhari nisaidie,.. siwezi kuendelea kuvumilia zaidi huu ukatili nitakufa mimi nisaidie…. Uwiiiii”

Lamla alikuwa ni kama sasa amepata uhai na kuanza kulia kama binadamu , zile hisia zake ambazo zilikuwa ni kama zimempotea kama binadamu zilimrudia.

Saidi palepale alianza kumwangalia kwa umakini mwanamke huyo na palepale kumbukumbu zake zilimkumbuka vizuri.

“Wewe nakujua , imekuwaje ukawa hapa , hii pia ni kazi ya Hamza?”Aliuliza Saidi.

“Hamza!”

Lamla mara baada ya kusikia jina la Hamza hofu ilimwingia palepale , jina hilo kwake ni kama jina la shetani.

“Hamza ni shetani … sitaki kulisikia hata jina lake”Aliongea huku akiendelea kulia.

“Hahaha.. ni kweli kabisa yule ni shetani kwa namna alivyotufanya na kuwa katika hali hii , umesema unataka nikusaidie wakati na mimi nipo kama hivi na sijui hata ni wapi napaswa kwenda, unataka nikusaidie vipi au unataka turudi Tanzania na kuendelea na maisha ya kujificha?”Aliuliza Saidi.

“Hapana siwezi kurudi Tanzania , mtoto wangu yupo Australia kimasomo, nikiweza kumpata nitaweza kupata hela ambayo itanifanya kuwa na maisha mapya”

“Unamaanisha Frank?!”Aliuliza Saidi na Lamla alitingisha kichwa na kumfanya Said kucheka kwa nguvu.

“Kama ni hivyo basi twende zetu Australia na hii meli”Aliongea na kurudia hali ya kucheka kwa nguvu na palepale Lamla alisimama na kuanza kucheka lakini upande wake baadae kicheko kiligeuka kuwa kilio cha uchungu huku akionekana kama mtu ambae kisasi kimeujaza moyo wake.

“Hamza na Regina nitarudi”Alijiwazia Lamla huku akisaga meno kwa hasira.

*******

Siku iliofuata Hamza hakuweza kuota kabisa ile ndoto licha ya kulala usingizi mzito, ukweli alitamani kuota tena ili ajue nini kinaendelea lakini upande wake hakutaka kulazimisha kuota kwa kuutumia ule mshumaa ambao Frida alimwambia autumie, hakujua tu ni kwanini lakini bado alikuwa mzito mno kutumia kifaa kile ili aweze kuota.

Wakati akifikiria pia juu ya lugha iliokuwa kwenye kitabu alichopewa na Genesha ilimfanya kukumbuka pia swala la Amiri na palepale alitoa simu yake na kuwasiliana na Sally na haikuchukua muda mrefu kumpata mwanamke aliefahamika kwa jina la Sally na kumwambia ampe matokeo ya kazi.

Lakini Hamza alichoweza kusikia hakikuwa cha kuridhisha kabisa mara baada ya kuambiwa lugha hio bado imekuwa ngumu kujulikana ni lugha gani lakini utafiti bado unaendelea mara kwa kuhisia pengine ni lugha ya kikabila.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakutaka kufikiria zaidi na kumwambia Sally kama atapata kitu ambacho kitarahisiha kazi hio atamjulisha.

Siku nzima ya jumapili hakuna kilichotokea zaidi ya kukaa nyumbani akichati na mrembo Irene ambae alianza kwa kumlaumu Hamza kwa kuoa bila ya yeye kuwa na taarifa na Hamza alimjibu kwani yeye ni nani mpaka amwambie , mrembo huyo licha ya kuambiwa hivyo hakukasirika na kumtaka Hamza atimize ahadi yake, akimaliza masomo lazima wawe wote hata kama ameoa. Kauli hio ilimfanya Hamza asijue acheke ama alie maana ilikuwa ya kijinga lakini kwa Irene alioneana kuwa siriasi.

Upande mwingine Kanali Dastani na Amosi waliweza kuingia dili na Dina , ijapokuwa mwanzoni walitaka kujua kwanini Dina aliwapatia rekodi ya sauti ambayo inadhihirisha Sedekia hakufariki lakini Dina aliwaambia hawezi kuwapa sababu mpaka watimize masharti yake yote ambayo aliwawekea mezani.

Dastani na Amosi hawakuwa na namna , kwa namna flani waliweza kuhisi kuna kitu kikubwa kiliendelea kama kweli Sedekia atakuwa bado yupo hai na jambo hilo liliwatia shauku na kutaka kujua zaidi nini kinachoendelea , hivyo waliona kwa namna yoyote wanapaswa kutimiza masharti ya Dina ambayo ni kuruhusu mtu mwingine kukaa katika Gereza la Silo kurithi nafasi ya Mchuku na vilevile wapate taarifa zote zinazohusiana na familia ya Wanyika.

Sharti la mrithi wa Mchuku halikuwa gumu sana kwa upande wa Kanali , lakini shari la taarifa za familia ya Wanyika ilikuwa ngumu mno kwani kwa kipindi kirefu siri juu ya nguvu ya familia hio ilikuwa ni kama siri ya taifa na hakuna aliekuwa akijua na hata wale waliokuwa wakijua hawafahamiki ni wa kina nani kwa majina au faili lake linapatkana wapi , lakini Dastani aliamini kwa namna moja ama nyingine lazima kuna namna ambayo famila hio itakuwa inafahamika na faili lake lipo ndio maana wanakuwa na nguvu sana ndani ya Tanania , hivyo kete yake ya kwanza aliamini ni kumtumia raisi anaekwenda kustaafu mheshimiwa Eliasi na akikwama katika hilo ndio atatumia mpango mwingine.

Upande wa Amosi hakuwa na haraka sana , alipanga kufuata nyayo zote za Dastani na ataweza kufanikisha misheni yake aliopewa kwa njia hio, kila kitu kilimwambia tukio la Ex wake Jasmine na juu ya mkufu aliowahi kuona lazima kuna muunganiko na kesi ya Sedekia pamoja na ya tukio la ajali ya radi lililotokea miaka mingi huko Mkoani Rukwa Wilaya ya Sumbawanga , hivyo licha ya kwamba hakuwa akimwamini Dastani aliamini hio ndio rahisi kufanikisha mipango yake kwa kuamini pia Dastani hakuwa akimwamini yeye na kwa namna moja ama nyingine lazima atakuwa na mpango wa kutompatia taarifa.

Kwa Akili hio Amosi alikaa macho na kuona kila hatua ambayo Kanali atachukua.

*******

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa ya mwanzo wa wiki , wiki ambayo kwa Tanzania ilikuwa wiki ya Uchaguzi wa kuchagua raisi mpya wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Polisi kwa kushirikiana na idara nyingine za ki usaama walihakikisha hali ya amani ndani ya maeneo yote ya Tanzania inadumishwa ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa ukamilifu mkubwa bila ya dosari.

Wakat wananchi wengi wakijali juu ya Serikali inayoingia madarakani upande wa Regina ni kati ya watu ambao hawakuwa wakijali nani atachaguliwa au nani alikufa na nani akamrithi mwingine , kwa namna yoyote ile alijua kampuni yake haiwezi kuathirika na hata kama ikitokea, mbinu za kukabiliana na sera mpya ya serikali wanazo kama walivyofanya kazi kwa miaka mingi chini ya maraisi tofauti tofauti.

Kama mwenyekiti na Afisa mtendaji mkuu wa kampuni , siku hio ya Jumatau rasmi alirudi kazini.

Wakati akiingia ndani ya jengo hilo la makao makuu ya kampuni zote za Dosam wafanyakazi walikuwa wametengeneza bango kubwa pamoja na maua ya aina mbalimbali kumkaribisha pamoja na kumpa pole , ilikuwa ni ishara pia ya kumpa heshima yake kama Mmiliki mkuu wa makampuni yote nje na ndani ya nchi.

Na Hamza ili kuwapa nafasi wafanyakazi kumkaribsha alimuacha Regina nje ya geti ili aingie kwa miguu kupitia lift ya kawaida.

Regina alikuwa kama malkia akipita katikati ya watu waliojipanga mstari ambao wengi wao ni wafanyakazi wakubwa katika kampuni hio na wengine wakiwa ni wakurugenzi katika kampuni Tanzu.

Siku hio kulikuwa na kikao cha bodi ya wakurugenzi ndio maana kila aliekuwa na cheo kikubwa katka kampuni hio aliwasili.

Regina licha ya udogo wake alionyesha kujiamini kusiko kuwa kwa kawaida huku akiwapa ishara baadhi ya mabosi hao kuwasalimia.

Hamza aliekuwa ndani ya gari aliisha kuangalia tukio lote na kwa jinsi ambayo Regina alionekana kujiamini , aliishia kukunja mdomo na kutoa tabasamu ambalo halikuelezeka alikuwa akiwaza nini.

Ukweli Hamza jana na asubuhi hio Regna alikuwa tofauti na yule aliekuwa akicheza nae siku nzima ya jumamosi , alikuwa amerudi katika hali yake ya kawaida na hakuwa hata na chembe ya utani kwenye macho yake.

Mara baada ya kuegesha gari katika maegesho moja kwa moja alienda mpaka ndani ya ofisi yake na alikuta kazi zilizowekwa azifanyie kazi lakini kabla ya kuanza kazi aliingia kwenye soko la sarafu ya Bitcoin kuona ametengeneza faida kiasi gani.

Na baada ya hapo alimalizia kazi haraka haraka na Linda katibu muhtasi mara baada ya kukuta kazi ambayo ameacha imekwisha kumalizwa aliishia kuridhika na hakuwa tena yule mwanamke ambae alikuwa akimwangalia kwa chuki.

Alimheshimu Hamza mara baada ya kugundua kuna uhusiano uliokuwa ukiendelea na bosi wake, hivyo licha ya kumpa kazi lakini alijitahidi kutovuka mipaka , isitoshe alkuwa akiipenda kazi yake mno na aliogopa kumkasirisha Regina kama alivyofanya mara ya mwisho , licha ya elimu yake kutokuwa kubwa sana lakini mshahara wake ulikuwa ni zaidi ya wa daktari bingwa..

Muda wa chakula cha mchana kama kawaida Hamza alishuka mpaka katika mgahawa wa kampuni na kuchukua chakula chake na kwenda kukaa katika meza aliokuwepo Yonesi.

“Dahh. Kapteni leo unaonekana vizuri mno , vipi mazoezi?”Aliuliza Hamza.

Yonesi hakuwa ameonana na Hamza kwa zaidi ya wiki moja au zaidi na katika muda wote huo alikuwa akichukua mazoezi ya kile alichomwelekeza.

“Nimejitahidi kuchukua mazoezi ya miondoko ulionionyesha lakini nashindwa kufikia mara mia moja , mpaka sasa nimeishia mara tano tu”Aliongea Yonesi.

“Wewe usiharakishe , uzuri ni kwamba una msingi mzuti wa kimwili na kadri nguvu zako za ndani znavyojikusanya utapiga hatua , mimi kwa mfano uwezo wangu miaka kadhaa iliopita ilinifanya maadui wasinisogelee kabisa , lakini baada ya kutelekeza nishati za mbingu na ardhi na kuanza kujifunza kitu kingine sikufanikiwa haraka , nilitumia muda mwingi kuwaza , kujaribu na kufeli mpaka nilipopata ujuzi mpya”

Hamza aliongea hivyo ili kumtia moyo Yonesi na aendelee kujitahidi kuchukua mazoei kadri awezavyo

“Kwahio wewe mpaka sasa hivi , hii mbinu imekufikisha levo ya ngapi?”Aliuliza Yonesi huku akimwangalia Hamza na muonekano ambao ilikwa ni ngumu kuelewa.

“Mimi ni pacifist hivyo siwezi kujua nipo levo ya ngapi , sio mtu wa kupigana mara kwa mara”Aliongea Hamza.

“Sio kama wewe ni pacifist hutaki tu kuniambia, nadhani kujuana kwako na mtu kama Mshauri mkuu huwezi kuongea kila kitu na mtu wa chini kama mimi, wewe endelea kunichezea”Aliongea Yonesi kwa kulalamika.

“Kapteni unamaanisha nini kukuchezea?, hatujawah kuchezena ujue”Aliongea Hamza na kauli ile ilimfanya Yonesi kuanza kuwa mwekundu maana ilikuwa na utata..

“Unaongea ujinga gani sasa, sijamaanisha hicho unachowaza”

“Mimi mbona naona hujakosea , wewe niambie kama unataka tuchezeane?”Aliongea Hamza.

Shida sio kuongea, tatizo ni kwamba Hamza sauti yake likuwa ni ya juu mno na wafanyakazi waliokuwa ndani ya mgahawa walivyosikia maneno hayo waligeuka kwa mshangao.

Huku wengi wakijiuliza inamaana mwanamke mgumu kama Yonesi anataka kuchezeana na Hamza.

“Yaani wewe usivyokuwa na aibu , kuwa makini kabla sijakufanya kitu kibaya”Aliongea Yonesi huku akiwa na hasira baada ya Hamza kumfanyia makusudi watu wamwangalie kwa nyuso za kumcheka.

“Usiwe hivyo Yonesi au hujapenda staili yangu ya maneno, naweza yabadlisha yanyooke kabisa moja kwa moja kwenye pointi”Aliongea na kauli hio ilimfanya Yonesi ukichaa kutaka kumvaa lakini hata hivyo simu yake iliotoa mlio ilimfanya kutulia.

Mara baada ya kusoma ujumbe ulioingia kwenye simu yake palepale alionekana kuwaza kidogo na kisha kumwangalia Hamza kwa macho makali.

“Tufanye siku nyingine na lazima nikushikishe adabu , mimi naondoka zangu”Aliongea haraka haraka na alisahau kuondoa sahani yake kutokana na haraka.

Hamza hakujua nini kinachoendelea mpaka mrembo huyo mwanajeshi kuwa na haraka namna hio.

Mara baada ya Yonesi kuondoka Hamza alibakia mwenyewe na hakukuwa na mtu mwingine wa kuweza kutaniana nae , hivyo baada ya kumaliza chakula aliingia kwenye mafriji na kukusanya matunda boksi mbili na safari ya kwanza ilianzia kwenye ofisi ya Eliza lakini hakumkuta na alimuuliza Marium na kuambiwa yupo katika ofisi ya Bosi.

Hamza alijiambia kwasababu anakwenda kuunganisha familia ya Eliza na Regina kwa wakati mmoja , ngoja akawape chakula chao kwa wakati mmoja ili waanze kuzoeana.

Baada ya kuingia katika ofisi ya mkurugenzi Eliza alikuwa mbele ya meza ya Regna huku akionekana kuwa na mawazo hivi.

“Nini kinaendelea hapa jamani?”Aliuliza Hamza bila aibu yoyote wala wasiwasi

Eliza mara baada ya kugeuka na kumuona Hamza aliishia kung’ata lips zake huku akiangalia chini.

Regina yeye mara baada ya kuona maboksi mawili kwenye mikono ya Hamza macho yake yalionyesha hisia flani lakini kwa sekunde kadhaa tu.

“Unaweza kuweka kwanza hayo matunda chini na uondoke kuna jambo tunaongealea hapa”Aliongea.

Hamza alikubali mara baada ya kuona hali ya hewa hapo ndani kidogo ilikuwa nzito na moyo wake ulikuwa ukisukuma damu kwa haraka, lakini licha ya hivyo hakutaka kuondoka, baada ya kuyaweka chini alienda kukaa kwenye sofa.

Upande wa Regina mara baada ya kona Hamza amekaa chini bila kuondoka aliishia kukunja sura na kisha akampotezea.

“Eliza haina haja ya kumjali kama una cha kuongea ongea tu nakusikiliza””

“Mkurugenzi nilichotaka kuongea ni kwamba naona kabisa sina vigezo vya kuwa Vice President wa kampun kutokana na ukubwa wake”Aliongea Eliza

“Eliza kikao cha bodi kishapitsha tayari hili na nishatangaza juu ya wewe kukubali kushikilia wadhifa huo , kipi kinakufanya kusita sita?”

“Ni kwasababu sijaingia kwenye hii kampuni kwa muda mrefu na hata kama nikisema hivyo hakuna ambae anaweza kuniamini , nina wasiwasi ninaweza kukuangusha juu ya matarajio yako kwangu”

Hamza mara baada ya kuskia maneno ya Eliza hatimae alijua nini kinaendelea , ilionekana ni swala la Eliza kutojiamini kuwa Makamu rais wa kampuni na sio ugomvi wa mambo yao binafsi.

Lakini hata hivyo Hamza alikuwa na hamu ya kuona ni kwa namna gani Regina atamshawhi Eliza kushikilia wadhifa huo wa Vice Presindent.

Ukweli ni cheo kikubwa kulingana na ukubwa wa kampuni ndio maana kwa mwanamke mpole kama Eliza lazima aone uzito wake , isitoshe pia kuna maafisa waandamizi wengi ndani ya hio kampuni ambao walifika hapo kabla yake hivyo swala hilo lingempa mzigo wa kisaikolojia.

Regina alionekana kufikiria kwa muda huku akimwangalia Eliza na baada ya dakika tatu alionekana kupata cha kuongea.

“Sawa Meneja Eliza , nitakuuliza maswali kadhaa hivyo unapaswa kuyajibu kwa uaminifu’Aliongea na Eliza alitngisha kichwa kukubali.



















SEHEMU YA 107

“Ni faida kiasi gani idara yenu iliingiza katika robo ya kwanza ya mwaka huu?”Aliuliza Regina na kumfanya Eliza kupepesa macho akiwa haelewi kwanini Regina anauliza swali la namna hio na yote ni kutokana na kwamba taarifa hizo zote Regina alikuwa nazo , isitoshe akili ya mkurugenzi huyo ilikuwa ni kama komputa kwenye kukariri.

“Katika Robo ya kwanza ya mwaka faida tulioweza kuingiza kupitia idara yetu ni bilioni 370 za Kitanzania” Aliongea Eliza.

“Na mlipata nafasi ya ngapi kama idara ndani ya kampuni?”

“Ya kwanza”Alijibu Eliza bila ya wasiwasi.

“Niambie tena katika robo ya mwisho ya huu mwaka faida mliongiza ni kiasi gani kama idara ya mauzo?”

“Bilioni 250”

“Nafasi yenu katika kampuni ni ya ngapi?”

“Ya kwanza bosi”

“Vipi mwaka uliopita wote mliingiza faida kiasi gani na mlikuwa wa ngapi?”

“Tuliingiza bilioni mia tisa kwa mwaka mzima na kushikilia nafasi ya kwanza”

“Vipi kuhusu mwaka juzi mlikuwa wa ngap?”

“Wa kwanza pia bosi”Aliongea Eliza kwa kujiamini kabisa na muda huo ni kama ile ari ya upambanaji ilirejea upya na unyonge kumtoka , alianza kufikiria timu yake ya mauzo ambayo aliongoza tokea aingie ndani ya kampuni na changamoto zote alizopitia na namna alivyozikabili, alijikuta akijivunia yeye mwenyewe kwa mafanikio”

Regina aijikuta akimwangalia Eliza na palepale tabasamu lilipamba uso wake.

“Meneja Eliza unadhani nani anastahili hii nafasi tofauti na wewe?”Aliuliza.

“Bosi ni kwamba..”Eliza alitaka kusema hawezi nafasi hio lakini mara baada ya kukumbuka maswali alioulizwa na pia katika kpindi hicho idara yake kufanya vizuri miaka zaidi ya mitatu mfululizo aliona kabisa Regina hakufanya upendeleo bali ni kazi kubwa aliofanya na hakuna aliemzidi, aliona sio kama hakuwa na vigezo , alichokuwa amekosa ni kutokujiamini tu.

Aliishia kumwangalia bosi wake kwa namna ya heshima na kumhusudu na aliishia kujicheka mwenyewe.

“Hakuna bosi”Alibadilisha jibu lake na Regina alitingisha kichwa kukubali.

“Kama ni hivyo unaweza kuondoka na ukaandae hotuba kwa ajili ya kikao baadae”

“Sawa Mkurugenzi”Aliongea na kugeuza kuondoka

Muda ambao alitaka kutokomea nje , Regina alimsimamisha .

“Eliza chukua boksi moja la matunda tusimfanye mtu wa watu kupanda na kushuka kwenye lift”Aliongea na Hamza alietulia aliweza kusikia maneno hayo lakni aliendelea kukaa vile vile akijifanyisha hajasikia.

Mara baada ya Eliza kutoka Regina alikunja mikono yake huku akimwangalia Hamza kwa macho yaliojaa uchokozi.

“Ulidhania nataka kumfokea mpenzi wako?”Aliuliza Regina.

“Sio hivyo , nilitaka kukaa hapa kujifunza namna unavyoendesha kampuni , Wife unaonekana upo vizuri sana kusoma akili za wafanyakazi wako, unaonaje siku moja ukaja chuoni na kutupiga pindi?”

“Hebu acha unafiki na ondoka nina kazi za kufanya”Aliongea huku akimkazia macho.

Hamza hakuwa na tatizo na aliweka boksi la matunda kwenye meza.

“Kula usiendelee kuumwa njaa”

“Haina haja ya kunipeti peti , nikwambie tu mimi sio mtu wa kuchukulia mambo binafsi , hata kama ikitokea wewe na Eliza mkapata watoto siwezi kumnyanyasa kazini , halafu pia nikwambie sijali chochote kuhusu wewe”Aliongea na kumfanya Hamza uso wake kujikunja kama katafuna mdudu.

“Mke, mbona kama umeenda mbali sana , mimi ni mtu ambae najali mila na desturi za kitanzania , mpaka kumbebesha kitumbo lazima kuna taratibu zifuatwe, angalau kwanza upate kitumbo ndio italeta mantiki”

“F*ck you, shut up”Regina alishindwa kujizuia kutokutukana kwasababu ya maneno hayo

“Haya nimenyamaza isitoshe mimi kama mwanaume sitakiwi kuongea sana zaidi ya kuonyesha vitendo”Aliongea na kumfanya Regina kuishia kumwangalia tu maana aliona hata kama akijibishana nae anaweza asishnde , aliishia kuchukua nyaraka zilizokuwa pembeni yake na kisha kumrushia.

“Hebu angalia kwanza hizo nyaraka , sina mpango wa kwenda kushiriki lakini wewe kama msaidizi wangu ukienda kuniwakilisha haitakuwa jambo baya na ninavyokujua unavyopenda hio michezo nadhani tukio linakufaa sana”Aliongea Regina na Hamza aliinua nyaraka zile na kuangalia kilichokuwa kimeandikwa.

Lilikuwa tukio la kampuni kwa wafanyakazi wote kwenda tour ya pamoja kwa ajili ya kuzoeana na kuongeza ufanisi kikazi.

Ni kweli kabisa alivyoongea Regina alikuwa akipenda mambo kama hayo kuliko kukaa ofisini muda wote.

“Hehe.. Babe Regina asante sana kwa kunijali , naomba niseme itakuwa heshima kubwa kukuwakilisha”

Hamza hakuamini wale warembo wa kampuni ambao mara nyingi aliishia kuwaona kwa mbali wanakwenda kujumuka pamoja kwenye Tour, aliona ni muda mzuri wa kwenda kuzoeana nao .

“Najua ujinga unao waza hapo , ila ujue sijakupa nafasi ya kwenda ili ukacheze , nataka ukahakikishe usalama wao na sifanyi kukuonyesha nakujali ili unipende , hilo futa katika akili yako”Aliongea na kumfanya Hamza kushikwa na soni.

“Mke wala usijali kabisa kuhusu hilo najua ninachokifanya , halafu kwanini muda wote unakuwa kama mnyoo tumboni kwangu?”

“Kwahio Hamza mimi ni mnyoo?”Aliongea Regina kwa hasira huku akipiga mkono wake kwenye meza kwa hasira.

Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo muda si mrefu atalipuka alichukua kila kilichokuwa chake na kukimbia ndani ya ofisi hio.

Dakika chache tu baada ya kutoka simu yake ilianza kuita na alivyoanglaia jina la mpigaji alikuwa ni Yonesi.

“Kapteni unaniwazia sana , si tumeoana muda si mrefu?”Aliongea Hamza kimatani.

“Hebu acha ujinga , una kazi sasa hivi , kama huna njoo”

“Nije wapi , usiniambie unataka tutoke out muda wa kazi , mimi nipo siriasi sana likija swala la kazi ujue Yonesi”

“Yaani wewe… hebu njoo hapa mgahawa wa Yam kuna Komredi wangu anataka kuonana na wewe”

“Komredi wako?”Aliuliza Hamza akishangaa na kujiuliza iweje Komredi wake atake kukutana nae.

“Kapteni hebu acha utani bwana , mimi na Komredi wako wapi wapi?”

“Alikuwa ni kiongozi wa kikosi chetu jeshini wakati tukiwa mafunzoni anasema mshawahi kukutana , hivyo acha porojo na njjoo haraka kama wewe ni mwanaume kweli”Aliongea na kauli hio ya kuambiwa kama ni mwanaume kweli ilimfanya Hamza kukuna kichwa asiweze kukataa.

Mara baada ya kutoka alitembea upande wa kushoto wa barabara kulisogelea jengo la kampuni ya mawasiliano ili kuweza kuufikia mgahawa maarufu wa Yam , ulikuwa mgahawa mzuri mno ndio maana aliweza kuujua kwa haraka.

Baada tu ya kuingia ndani aliweza kumuona mwanamke mwenye umbo la kuvutia(Buxom shape) akiwa amekaa kwa kuangaliana na Yonesi,alikuwa na nywele ndefu mno zilizofika mgongoni na Hamza hakujua ni bandia au ni asili mpaka aliposogea karibu zaidi na kuona ni asili.

Mwanamke huyo alikuwa amevalia koti la Cashmere na kijisweta cha rangi nyekundu ndani , alionekana kuwa sio wanawake wa kawaida kawaida na alikuwa mrembo kama alivyokuwa Yonesi.

Kilichomfanya Hamza kushangazwa nae ni kwamba mwanamke huyo alikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kufikia levo ya Mbingu(Nafsi) na mara baada ya kukumbuka Yonesi alimtambulisha kama kamanda wake wa kikosi aliamini basi Yonesi alitokea kikosi ambacho sio cha kawaida.

Mwanamke yule mwenye shingo ndefu iliodhihirsha unyarwanda mara baada ya kumuona Hamza alimkazia macho huku akitoa tabasamu hafifu.

“Hamza huyu alikuwa mkuu wangu wa kikosi , wakati nilipokuwa mwanajeshi , anafahamika kwa jina la Anna , vipi unafahamiana nae?”Aliuiza Yonesi lakini Hamza sura ya mrembo huyo wa rangi ya chocolate ilikuwa ikija na kupotea potea.

“Nimefurahi kukufahamu Anna , hivi tushawahi kukutana kabla?”Aliuliza Hamza.

“Da’ Anna huyu ndio Hamza au ulikosea sio yeye unaemtafuta?”Aliuliza Yonesi na Anna alitoa tabasamu lililomfanya kuzidi kuwa mrembo na meno yake yaliokuwa meupe mno.

“Hatujawahi kwa ukaribu , tulionana kwa mbali .. ila nakufahamu wewe ni Hamza na ndio muhusika wa vifo vya dada zetu sita”Hamza na Yonesi mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakikishangaa, upande wa Hamza hakujua ni dada gani hao anawazungumzia.

“Dada Anna nini kinaendelea , unamaanisha nini kusema Hamza ndio muhusika?”Aliuliza lakini yule mrembo alimwangalia Hamza kwa macho makali.

“Mr Hamza nadhani ushawahi kusikia kuhusu kundi la wanawake maninja wanaojiita Red Sisters , najua unafahamu hilo jina na wewe ndio uliewaua wenzetu sita nchini Sweeden huku mmoja wetu ukisababishwa akamatwe na Interpool, hivi unajua ulitukosea sana ilihali hatukua na uadui na wewe”Aliongea yule mwanamke na Hamza palepale alijua kinachoendelea , lilikuwa ni tukio ambalo alimuokoa Yulia katika mikono ya watekaji baada ya kukuta familia yake imekwisha kuwawa , watu ambao aliwakuta wamemshikilia Yulia walikuwa ni wanawake sita na aliwaua wote na kumchukua Yulia, baadae mara baada ya kutafuta taarifa zao alisikia ni kundi la kininja la wanawake linalojita Red Sisters, sasa anaelewa kinachoendelea

“Kwahio wewe ndio ulikuwa kiongozi wa kundi la Red Sisters?”Aliuliza Hamza

“Red sisters!!. Dada Anna mnamaanisha nini ?”Yonesi hakuelewa tena kilichokuwa kikiendelea, ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia jina la Red Sister’s.

“Yonesi sidhani kuna haja ya kukuficha tena , baada ya tukio lile na wewe kuja kuchukuliwa na familia yako ambayo ina nguvu ilibidi tutoroke kambini . ule ulikuwa uonevu kwetu sisi na hatukutaka kurudi Tanzania na kufungwa gerezani kwa kosa la usaliti ambalo hatukufanya , baada ya kutoroka na wenzangu tulikimbilia nchini Haiti na huko tulijifua kimazoezi huku roho ya kisasi ikiwa motisha kwetu , katika harakati zetu ndio tukaunda kundi la kininja ambalo tulijiita Red Sisters na kwanzia hapo kazi yetu ikawa ni kuua kwa hela, samahani kwa kukuambia sasa hivi haya, lakini tulikuwa na wakati mgumu sana , tulitumia hadi miili yetu kufanikisha kila misheni tuliopata , hata baadhi yetu zile ndoto za kuja kuolewa na kuwa na familia zilipotea kabisa”Aliongea yule mwanamke kwa uchungu.

Yonesi licha ya kutokujua kilichotokea baina ya Hamza na Anna , lakini mara baada ya kusikia Anna hakuwa mwanajeshi tena bali ni ninja alipatwa na mshituko mkubwa.

“Da’ Anna kwahio unasema umekuja hapa Tanzania kwa ajili ya kulipa kisasi?”

“Unaweza kusema hivyo na nitaanza na Hamza , samahani unajua hili sasa hivi”Aliongea .

Upande wa Hamza hakuonyesha ishara ya kupaniki na aliishia kumwangalia mwanamke huyo mrembo kwa muonekano usioelezeka.

“Anna kama kweli umekuja hapa kuniua kwa ajili ya kulipa kisasi basi nadhani unajua huniwezi peke yako”Aliongea Hamza na yule mwanamke alitingisha kichwa kukubali.

“Ijapokuwa siwezi kujua uwezo wako ulivyo lakini hisia zangu znaniambia kabisa sikuwezi”

“Utashi wako upo sahihi kabisa , kama sio eneo hili kuwa mgahawa na watu kuwepo ningekuwa nishaivunja shingo yako”Aliongea Hamza huku akizungusha macho yake na baadhi ya watu walionekana kumwangalia na aliwaonyeshea tabasamu kuwaashiria mazingira ni shwari, lakini sasa licha ya kusema hivyo alisambaza msisimko uliomlenga Anna na kumfanya Yonesi aliekuwa mbele yake kuhisi woga huku moyo wake ni kama unataka kumtoka.

“Hamza niseme kweli wewe ni mwanaume Handsome na mcheshi mno, kama kusingekuwa na mgogoro wa damu kati yetu ningefanya lolote lile kuhakikisha nalala na wewe , huwa napenda mwanaume ambae ni mkatili kama wewe ila mtanashati”Aliongea yule mrembo huku akiweka muonekano wa uchokozi.

“Hata mimi pia napenda warembo ambao wana shepu matata kama yako na wenye shingo ndefu kama Twiga”Aliongea Hamza huku akipitisha macho yake kuangalia mapaja ya mrembo huyo yaliofunikwa nusu na sketi kutokana na kuwa fupi mno.

Mwanamke huyo alionekana ni aina ya wanawake ambao walikuwa ni wa wazi sana kwa kile wanachojiskia , ilikuwa kawaida hata hivyo kwa maninja wote wa kike, mara nyingi wanatumia mbinu zote za kishushushu kuhakikisha wanaihadaa shabaha yao ili kuingiza mtegoni.

“Sijapanga kupigana na wewe ana kwa ana hapa”Aliongea yule mwanamke akimwangalia Hamza ambae amehamia na kukodolea manyonyo yake lakini Anna hakujali macho ya Hamza na aliendelea kuongea.

“Mdogo wangu na mwenzetu anaefahamika kwa jina la Elisi ana miaka zaid ya mitatu tokea kuletwa Tanzania na kushikiliwa katika moja ya Gereza na mtu ambae ametumia nguvu nyingi kuhakikisha Elisi hafahamiki yupo Gereza gani na kwanini kafungwa ni Raisi Mstaafu Mgweno , ninachotaka kutoka kwako ni kuhakikisha Elisi anaachiwa huru”Aliongea.

“Mbona swala dogo sana hilo, kwa msaada wa Kapteni hapa ninaweza kutumia koneksheni na kuhakikisha ndugu yenu anaachiwa huru”Aliongea na kumfanya yule mwanamke kutabasamu.

“Baada ya Elisi kuwa huru na salama , nataka ujiue mwenyewe ili kulipa fidia ya nafsi sita za dada zetu peponi”Aliongea akiwa hana utani hata kidogo .

“Nini!!!”Yonesi alijikuta akishituka.

“Da’Anna inawezekanaje ..?”

“Kwamba haiwezekani?.. inawezekana kwasababu mpaka sasa hivi mke wake yupo kwenye mikono yetu”Aliongea na palepale muonekano wa Hamza ulibadilika.

“Kwahio umemtumia Yonesi anipigie simu nitoke nje ya kampni kwa ajili ya kumteka mke wangu?”Aliuliza Hamza na moyo wa Yonesi ulisinyaa palepale.

“Da’Anna inamaana umemkamata bosi Regina?”

“Yonesi naomba unisamehe kwa hili , napaswa kumuokoa Elisi na kisha nimuue Hamza , hii ndio namna pekee tunayoweza kukamilkisha hili , nisamehe kwa kukutumia”Aliongea na Yonesi aliishia kutoa machozi pekee.

“Komredi Anna nilidhani mmenisamehe kwa kuwatelekeza.. kumbe najidaganya tu , kukuamini kwangu kumenifanya kusababishia matatizo watu wengine”

“Huna haja ya kutoa machozi Yonesi , ukweli hatukuwahi kukulaumu ka kutuacha, haukuchagua kuzaliwa katika familia yenye nguvu, badala yake sisi ndio tumekufanya umsaliti mfanyakazi mwenzako”Aliongea

Hamza muda huo alianza kuchukia lakini alijua ni chuki za kipuuzi tu muda huo ambao mke wake ameshikiliwa.

“Kwahio mke wangu yupo wapi sasa hivi?”Aliuliza

Anna palepale alitoa simu yake na alifungua upande wa Vidio call na palepale ofisi ya Regina iliweza kuonekana.

“Da’ Anna kila kitu kipo tayari”

Mwanamke mwingine rika la Yonesi alionekana katika kioo cha simu, alikuwa amevalia sare maalumu za walinzi wa kampuni ya Dosam , muda huo alikuwa amemshikilia Regina huku akiwa amemuwekea kisu shingoni

Regina alikuwa na ukauzu wa hatari, alikuwa na woga na hasira kwa wakati mmoja , hakuwahi kufikiria mtu anaeonekana kama mlinzi wa kampuni yake ghafla tu ameingia ofisini kwake na kumteka.

“Safi sana Mima , usimuumize Regina, ndio kete yetu ya kumuokoa Elisi”Aliongea Anna kwa ridhiko.

“Regina usiogope nitahakikisha nakuokoa”Aliongea Hamza na Regina alitingisha kichwa kidogo bila ya kuongea neno.

“Mkurugenzi ni makosa yangu kutokuwa makini …. Anna nitakuua”Aliongea kwa hasira , alikuwa na huzuni kuliko watu wote.

Aliona kila kitu kimeanza na yeye kwa kitendo chake cha kumuita Hamza kupitia simu.

Upande wa Anna hakuwa na wasiwasi kabisa japo alimsikitikia Yonesi lakini alihitaji mpango wake kufanikiwa kwa namna yoyote ile nafasi hio waliitafuta kwa miaka mingi sana.

“Hamza unaonaje tukianza na kupiga simu?”Aliongea Anna.

“Hakuna shida, unataka nimpigie nani?”

“Mshauri mkuu , taarifa zinasema una ukaribu nae sana , tunaamini lazima atakuwa na taarifa ya wapi alipo Elisi na hata kama hana anajua namna ya kumtafuta”Aliongea Anna na Hamza hakuwa na shida palepale alitoa simu yake lakini kabla ya kupiga Anna aliichukua na kutafuta namba mwenyewe na kisha akapiga.

Baada ya simu kupokelewa Hamza alienda moja kwa moja kwanini anapiga na mara baada ya kutaja Red Sisters , Afande Himidu alionekana kuwa na taarifa hio, lakini hakujua kwanini Hamza anaulizia.

Hamza alienda moja kwa moja kwa kile alichokuwa akitaka na alitoa agizo bila kuzunguka zunguka na kumwambia Himidu afanye mpango Elisi popote pale alipo aachiwe huru.

Afande Himidu hakujua kwanini bosi wake wa zamani anaomba ombi kama hilo lakini simu ilikuwa imekwisha kukatwa tayari baada ya kuambiwa anasubiria majibu.

Walisubiri kama dakika nne na simu ya Hamza ilianza kuita na ilipokelewa haraka na Anna.

Afande Himidu palepale alimwambia Hamza ametumia koneksheni yake na taratibu za kutolewa kuachiwa huru kwa Elisi zimeanza mara moja.

Hamza hakutaka kumhusisha Himidu kwenye matatizo yake na alimwambia tu safi kwa kazi nzuri na ataongea nae baadae kidogo.

Simu pale ilikatwa na Anna tabasamu liliupamba uso wake.

“Nimependa namna ambavyo una nguvu hapa nchini Mr Hamza , sikutarajia mambo yatakuwa marahisi hivi, kinachobaki ni wewe kutimiza sharti la mwisho, ukijiua wewe mwenyewe bosi Regina ataachwa”Aliongea Anna akiwa siriasi

Upande wa Regina mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akifubaa..

“Hamza usije kufanya kitu cha kijinga , hawezi kunifanya chochote”Aliongea Regna na yule ninja wa kike aliefahamika kwa jina la Mima alikandamiza kisu shingoni kwa Regina.

“Kaa kimya ninaweza nisikuue lakini ninao uwezo wa kuharibu sura yako kwa kuichana chana”Aliongea na Regina aliufyata.

“Da’ Anna , Mima jamani , naomba msiende mbali hivi , hamuwezi kutatuta tatizo mlilokuwa nalo kwa njia hii”Aliongea Yonesi kwa kubembeleza akiwa hajui nini kitatokea , ni kweli alikuwa na uchungu wa kutaarifiwa wenzake sita walifariki lakini hakuwa tayari kumuona Hamza akijiua ili kumuokoa Regina , alijiuliza atamwangalia vipi Regina usoni.

“Yonesi hili halikuhusu kabsia , wewe kaa pembeni”Aliongea Anna akiwa siriasi

Muda ule Yonesi aliibuka na kisu kwenye meza na kukiweka shingoni huku machozi yakimtoka.

“Da’ Anna sipo tayari kuhushudia mume wake Regina akifariki mbele yangu huku mimi nikiwa msababishaji , nipo tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili ya Hamza , naomba tusimwingize mtu mwingine kwenye machungu , Regina hastahili hili kabisa…”Aliongea akiwa siriasi.

Unadhani wana stori gani hao wanaojiita Red Sisters mpaka kutoroka kambi na kuwa maninja, Lamla na Saidi wamekutana na kuungana, unadhani watafanikiwa kurudi na kulipa kisasi.

Tuendelee kula mtori nyamza zipo chini.

ITAENDELEA PANAPOMAJAALIWA.
watsapp 0687151346
 
Back
Top Bottom