Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahsante mkuu kwa kuchukua muda wako kutoa maoni. JF wakiruhusu kupost nitaendekea hapa maana walinipiga pini bila kunipa sababu ya msingi.Uandishi wako uko poa Sana Bro pokea maua [emoji253][emoji253][emoji253] yako.
Mi ni mmoja wapo ya wale wanaopenda kusoma threads tofauti tofauti hapa jf na nisi comment sijui kwanin [emoji2369].
***
STRONG FAN BASE
Sijui umejisahau au ndo umelidhika na hili jukwaa mfano simulizi ya roma inaviews kibao huko kwenye entertainment why can't you take advantage of that tyr unawafatiliaji coz simulizi zako ni pendwa tyr mi nimeangalia page ynye jina lako huko fb ni maajbu coz status uliyonayo huk jf ni kubwa ila huko fb ni jau, sometimes inabidi tujifunze kupitia makosa juzjuzi tu hapa ulikuwa locked palikuwa hapakaliki humu kila mtu alikuwa anagwaya coz tulifikiria hatutomsoma tena hamza binafsi nikawa nawaza isijekuwa ndo mazima kama jamaa flani nae alikuwa maarufu hapa jf baadhi watakuwa wanamfahau (t..bold) . Here ur not guaranteed brother kuna terms tu ukikiuka umeyakanyaga je kama usingekuwa unlocked ingekuwaje ???... Ungepoteza audience kubwa Sana coz wengi hatujalipia kwenye grupu
Sio wote tunaweza ku afford price at a certain time kwenye grupu huko Whatsapp coz no body knows tomorrow maybe kesho yangu ndo inaweza ikawa nzuri zaidi hata kulipia full package ya simulizi mda mwingine hata bando tuna tumia VPN ku access free data au public wi-fi.
Tengeneza strong fan base hasahasa fb coz huko ndo kuna watu wengi na waandishi wakubwa wenye fan base kubwa wapo huko .
Ciao .
Tupe link ya fb basi mgosiAhsante mkuu kwa kuchukua muda wako kutoa maoni. JF wakiruhusu kupost nitaendekea hapa maana walinipiga pini bila kunipa sababu ya msingi.
FB kwenye page yangu kule nitaendelea kuna mambo naweka sawa.
Cha kufanya hakikisha hata kama huna hela ya kunifuata watsapp kwa ajiki ya mwendelezo unakuwa na namba yangu ya simu.
Ahsante mkuu kwa kuchukua muda wako kutoa maoni. JF wakiruhusu kupost nitaendekea hapa maana walinipiga pini bila kunipa sababu ya msingi.
FB kwenye page yangu kule nitaendelea kuna mambo naweka sawa.
Cha kufanya hakikisha hata kama huna hela ya kunifuata watsapp kwa ajiki ya mwendelezo unakuwa na namba yangu ya simu.
Big up SinganoSHETANI RUDISHA AKILI ZETU
MTUNZI: SINGANOJR.
WTSAPP:0687151346
SEHEMU YA 111
Namtaka huyo mwanamke
Hamza mara baada ya kutoka nje ya ofisi alikutana na Yonesi ambae ofisi yake ilibadilishwa na kuwa katika floor moja na mkurugenzi.
Yonesi pia alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea na alishikwa na ahueni mara baada ya kusikia Regina ameongezewa muda wa siku moja kwa ajili ya kujiandaa kabla ya watu hao wa kodi kurudi tena na kufanya uchunguzi uliowaleta.
“Wewe ni Kapteni au sasa hivi nikuite mkuu wa idara maana cheo chako kishapanda”Alongea Hamza huku akimwangalia Yonesi usoni.
“Haina haja ya kuhangaika, unaweza kuniita kwa jina langu tu”
“Jamani Yone usiniambie ndio unataka nikuite kwa jina lako kwasababu ukaribu wetu umeongezeka ?”Aliongea Hamza , alikuwa akipenda sana kumchokoza Yonesi.
“Halafu sitaki ufupishe jina langu , hebu niambie kwanza una mpango gani wa kudili na hiki kinachoendelea”Aliongea na kumfanya Hamza kukuna kichwa.
“Sijajua bado maana ni swala ambalo lina mkono mrefu , kama ulivyosema kikosi chenu si kilikuwa kikiwindwa na Mgweno na familia ya Wanyika kwa muda mrefu ,nataka kujua kwanza baadhi ya vitu kabla ya kuchukua hatua”Aliongea Hamza.
“Nashindwa hata mimi kujua kwa hakika kama Mgweno anahusika katika hili au ni mheshimiwa raisi nwenyewe, maana idara zake zote zipo chini yake , licha ya kwamba inaweza kuonekana Raisi Eliasi hana nguvu katika baadhi ya sekta lakini bado nguvu yake kama Raisi inaheshimiika”Aliongea Yonesi.
“Wewe usiwe na wasiwasi najua cha kufanya kutatua hili tatizo”Aliongea Hamza na palepale alianza kupiga hatua kumuacha Yonesi na kuondoka lakini Yonesi alimzuia.
“Hicho unachotaka kwenda kufanya ni nini, kama vipi twende wote”Aliongea Yonesi lakini hamza alitingisha kichwa kukataa.
“Hili ni swala ambalo nataka kwanza kulipatia maelezo ya kina kabla sijachukua hatua , hivyo hatuwezi kuongozana kwasababu hata sijajua ninachoenda kufanya”Aliongea na kisha alimpa ishara ya kwaheri na kutokomea kwenye lift.
Wakati akiwa kwenye lift alitoa simu yake akiwa na nia ya kumpigia Dina lakini kabla ya kufanya hivyo alishangaa mara baada ya kuona kuna ujumbe ambao ulionekana kuingia muda mrefu lakini hakuusoma.
Kutokana na jana kuwa na ubize wa kusherehekea na warembo hakupata muda wa kuangalia simu yake kabisa ndio maana hakuona kama kuna meseji imeingia.
Hamza sura yake ilijikunja palepale mara baada ya kuona ule ujumbe , ulikuwa ni muamala wa kiasi cha pesa kilichoingia katika akaunti yake na mtu ambae ametuma kiasi hicho cha pesa alikuwa ni yule yule wa siku zote,mtu ambae hakuwa akimjua kwa sura zaidi ya kumtambua kwa jina la Mzee.
“Huyu Mzee anajaribu kucheza mchezo gani usio isha kila siku,kama anatuma hela si angalau atume nyingi?”AlijiulizaHamza.
Ukweli ni kwamba sio kama hela hio alikuwa na shida nayo sana , shida ni kwamba tokea aanze kuwa na mahusiano yasiokuwa ya kawaida na Mzee alikuwa akimtumia kiasi cha pesa kila inapofikia mwisho wa mwezi na kiasi hicho hakikuwahi kubadilika hata siku moja.
Haikujalisha yeye ni tajiri ama anao hela nyingi lakini kwa namna yoyote ile lazima hela hio iingie hata kama abadilishe njia za kupokelea pesa.
Muda mwingine Hamza aliamini labda ni kwasababu Mzee huyo anatafuta Attention yake ili isitokee akamsahau lakini bado aliona sio sababu ya kutosha kufikiria hivyo.
Kwasasabu alikuwa na swala la kushughulikia muda huo , aliamua kupotezea swala hilo na kisha aliitafuta namba ya Dina.
“Hatimae nimekumbukwa”Sauti upande wa pili ilisikika , wakati huo Hamza akiwa kwenye maegesho ya magari tayari na alitabasamu kwa uchungu maana aliona ni sahihi kwa mwanamke huyo kuonyesha kulalamika kwani hakuwa akimtafuta mara kwa mara.
“Dina babe kwanini unaongea hivyo , najua sijakutafuta kwenye siku hizi chache lakini upo akilini mwangu muda wote”Aliongea.
“Unachojua ni kuongea tu lakini vitendo aah!”Aliongea na kumfanya Hamza kutamani kucheka.
“Dina natsks uwe mwamnamke mwema maana kuna tatizo na nahitaji msaada wako..”Aliongea Hamza na kisha palepale alianza kumwelekeza kile kilichokuwa kikiendelea na upande wa Dina alionekana kufahamu juu ya jambo hilo kwa muda mrefu kupitia Elisi.
Ilionekana Elisi alifungwa katika gereza la Silo na wakati Mchuku akiwa kama mkuu wa Magereza taarifa za mwanamke huyo ziliweza kumfikia Dina.
Elisi hakuwa kama wafungwa wengine na ndio maana alimvutia Dina tokea mwanzo na kumfanya aanze kufanya utafiti kujua kilichomkuta mpaka kuwa gerezani.
“Kwa staili hii nadhani nitapaswa kuombea kampuni ya Dosam kupatwa na matatizo maana ndio njia pekee ya kukufanya kunikumbuka, maana sio kwa wanawake hao wanaokuzunguka”Aliongea Dina.
“Sio hivyo Dina, nakuahidi hili likiisha nitakupa muda wa kutosha kuwa na mimi”Aliongea Hamza akijitetea na upande wa pili ulivuta pumzi.
“Ukweli nilijua tu utanitafuta na nilishatuma watu kufanya uchunguzi mapema”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa kidogo.
“Kama umefanikiwa kufanya uchunguzi ni kitu gani umepata?”
“Aliempa Presha Kamishina ili kuftuma watu wa kodi kwenye kampuni ni mheshimiwa Napi Pasua”
“Napi Pasua ndio nani?”
“Ni waziri wa Viwanda na biashara lakini pia ni mkwe kwa mheshimiwa Mgweno”
“Kwa maana hio Mgweno katumia nguvu yake kwa mkwe wake kumfanya ampe presha Kamishina wa kodi , kama ni hivi basi ninaepaswa kudili nae ni Mgweno”Aliongea Hamza
“Nadhani uje kabisa tuongee vizuri , pia kuna baadhi ya mambo hayajaeleweka kwa kukosa taarifa”Aliongea Dina na Hamza alimwambia anakuja.
Baada ya kukata simu aliingia kwenye gari na kuianza safari ya kuelekea Kijichi na haikumchukua dakika nyingi aliweza kufika na kwenda moja kwa moja katika ofisi ya Dina.
“Ni kitu gani ambacho umesema hakijaeleweka?”Aliuliza Hamza huku akiwa na shauku.
“Unajua mara baada ya kuniambia Elisi ametoka nimeona haina haja tena ya kuweka mtu kule Gerezani maana ndio aliekuwa shabaha yangu”
“Wewe ulimjuaje?”Aliuliza Hamza maana ingekuwa ngumu kwa Dina moja kwa moja kumjua Elisi na kisha kuanza kumfuatilia.
“Nadhan sijawahi kukuambia lakin mtandao wetu upo mpaka kwenye magereza yote makubwa nchini , miaka kadhaa nyuma niliweza kupata taarifa za uwepo wa msichana mtukutu aliefahamika kwa jina la Elisi , baada ya kufuatilia sikuona hata namna ambavyo aliingizwa gerezani kwani kesi yake haikusomwa , lakini baadae ndio nilikuja kufahamu alikuwa amefungwa kutokana na kuasi jeshi,kwa tabia ambayo alikuwa akionyesha wakati wote akiwa gerezani ilinifanya nijue ilikuwa ni zaidi ya kuasi jeshi na hapo ndio nilianza uchunguzi wangu na nilikuja kugundua nguvu iliotumika kumfunga Gerezani ni familia ya Wanyika , sasa baada ya wewe kuniambia kilichotokea ndio nimepata majibu ya maswali yangu, lakini hata hivyo kuna swala bado halijawa bayana”Aliongea Dina.
“Swala gani hilo?”
“Kwa kipindi ambacho Elisi alikuwa gerezani watu mbalimbali walikuwa wakimtembelea kwa siri na kumhoji na kati ya hao wana uhusiano na familia ya Wanyika, mwanzoni nilijua Elisi alikuwa Gerezani kwasababu ya familia hio kuwa na uadui nae lakini nilikuja kugundua ni tofauti, kulingana na ulichonielezea naanza sasa kuona Familia ya Wanyika hawakumshikilia Elisi kwasababu wanaamini amehusika na mauaji ya Dokta Sindiga bali waliweka mtego wa kujua nani kahusika na mauaji ya familia hio”Aliongea Dina na Hamza kuanza kufikiria.
Kwa lugha nyepesi maana yake ni kwamba , kutokana na Mgweno kuwasiliana na kundi hili la Red Sisters kumuua Yulia na familia yake na wakati huo huo familia ya Wanyika kulitaka kundi hilo kuilinda familia hio na mwisho wa siku mauaji yakatokea , basi moja kwa moja familia hio 0ingefikiria mhusika alietuma watu kumshambulia Yulia na familia yake ni Mgweno na kwa mantiki hio hakukuwa na sabababu ya kumhoji Elisi moja ya maninja wa Red Sisters na kumuuliza nani muhusika, swali hilo moja kwa moja lilimaanisha pengine walikuwa na ushahidi Mgweno hakuwa ndio muhusika.
“Kwa maelezo ya Anna inaonekana walichezewa mchezo na Mgweno ili iaminike wao ndio waliokuwa wahusika”Aliongea Hamza.
“Sidhani kama ni kweli , kwa ninavyoona Mgweno aliamua kujimilikisha tukio”Aliongea Dina na kumfanya Hamza macho yake kucheza.
“Kwamba tukio la familia hio kupoteza maisha hakuhusika yeye , lakini kwasababu watu waliohusika hakuwajua akaamua kujimilikisha?, kama ni hivyo anapata faida ipi maana ni kujitengenezea uadui tu?”Aliuliza Hamza.
“Sina uhakika juu ya kila kitu , ila naamini kuna zaidi ya taarifa ambayo tunahitaji kujua”Aliongea Dina
“Hata mimi naamini hivyo maana haileti mantiki kwa Mgweno kutumia nguvu nyingi kwa ajili ya hawa wanajeshi wanawake , wamejitolea kwa ajili ya nchi yao ila akawaundia zengwe na wakaonekana wameasi jeshi , akawapa kazi na ikafeli lakini bado akawatengenezea mazingira waonekane wahusika , lakini licha ya kuwapitisha kwenye hayo yote leo nimewachukua chini yangu bado anatumia nguvu kubwa kunizuia, kama nia yake ni kuwachukua ili wawe chini yake alipaswa kwenda na mpango wa moja kwa moja na sio wa kuzunguka”Aliongea Hamza.
“Kwa upande mwingine mimi naona Mgweno anaonekana kuwahitaji kwa ajili ya kujiimarisha katika ngome yake ya ulinzi lakini hata hivyo pengine kuna ugumu , kama ulivyosema kisasi walichokuwa nacho ni zidi ya Mgweno na kuhusu familia ya Wanyika walikuwa wakitafuta tu namna ya kujisafisha kwamba hawahusiki na mwisho wa siku kuwa huru tena”Aliongea Dina na Hamza aliona ni kweli alichoongea.
Alijiambia hata kama yeye ndio wao basi ikitokea akitaka uhuru wake upande atakaoegamia ni wa familia ya Wanyka na sio kwa Mgweno ambae ndio chazo cha matatizo yao, pengine hio ndio maana ikawa chuki ya Mgweno kuwachukia na kufanya kila namna kuwafanya hawakai hapa nchini na kupata msaada kutoka kwa hio familia.
“Mgweno pia naamini anaogopa wakiwa chini yako , kumbuka pia kama anataka kushikilia hii nchi kama anavyopanga kwa namna yoyote atahitaji kuwa na mkono wake kwenye kampuni ya Dosam”Aliongea Dina na Hamza aliona ni sahihi kabisa , isitoshe haikuwa mara ya kwanza na alijiambia hata kama ana wazo hilo basi kwa namna moja anaona ni swala ambalo linaenda kuwa gumu kutokana na uwepo wake na kuongezeka kwa kundi la Red Sisters kumlinda Regina na Kampuni ilimaanisha ugumu zaidi.
“Tamaa zake za kutaka kujimilikisha nchi zinaonekana kuwa mwiba ndani ya hili taifa kimaendeleo, kama vipi nimsafishe moja kwa moja”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Dina macho kumtoka.
“Huwezi kufanya hivyo Hamza , najua uwezo unao lakini kumbuka Mgweno ni sehemu ya historia ya nchi, bado yupo chini ya ulinzi wa serikali na kwa vyovyote vile kitakachomtokea kibaya itakayoathirika ni taswira ya taifa”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.
“Dina mimi namna yangu ya kudili na tatizo ni tofauti na watu wengi , kwanza inapaswa nionyeshe namna nilivyosiriasi kwa kutoliogopa tatizo na kisha ndio mazungumzo yafuate”Aliongea Hamza.
“Unamaanisha nini?”
“Kama siwezi kumuua kutokana na cheo chake basi nitamng’a meno na kumfanya kuwa Joka la kibisa”Aliongea Hamza na Dina kwa haraka alielewa nia ya Hamza ni nini.
“Unataka kuharibu msingi wote wa nguvu zake si ndio?”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.
“Kwa ninavyojua hapa nchini familia ya Wanyika nguvu yao ipo katika kitengo cha Malibu , ambao ndio wanajeshi wenye uwezo wa juu sana katika jeshi lote, ila upande wa Mgweno yeye ukiachana na Malibu asilimia kubwa ya wanajeshi wa kawaida wapo chini yake kupitia wakuu na waandamizi wao , kama unataka kuua nguvu yake hapa nchini ni kupitia umoja wao wa Makomandoo , awamu ile ulimuua kiongozi wao Kanali Fanueli Yowe ukaacha umoja ukiendelea , mbinu pekee ya kumkata Mgweno Mkono bila hata ya kumgusa ni kuufuta huu umoja hapa nchini, lakini nikutahadharishe tokea siku ambayo ulienda kuwaletea vurugu kwasasa wamejiimarisha sana , sio kwa wanajeshi wa ndani ya nchi lakini kwa wataalamu wa kimapigano wa nje ya nchi , kuna tetesi kipindi hichi akipanga mikakati ya kurudisha nguvu yake ikulu ilioporwa kutokana na kifo cha Jongwe, kawaalika Wachina kwa ajili ya kumlinda”Aliongea Dina na kumfanya Hamza kufikiria , alijua vyema lazima Mgweno kutumia watu wake kumchokonoa moja kwa moja atakuwa amejipanga kupambana nae.
“Ile sehemu bado ndio ngome yao?”Aliuliza Hamza.
“Tegeta haikuwa ngome yao rasmi ,Kibaha ndio ilipo ngome yao lakini ni eneo hatari mno maana lipo karibu na kambi ya jeshi”Aliongea Dina.
“Nataka kwenda huko”Aliongea Hamza , alitaka kumaliza kazi siku hio hio bila ya kuchelewa ili angalau ampoze Regina.
“Hamza itakuwa hatari sana , kipindi hiki cha kuhesabu matokeo ya Kura lazima kutakuwa na vikao vinavyoendelea katika hilo eneo , maana yake ni kwamba ulinzi ni mkubwa mara mbili yake”Aliongea Dina kwa wasiwasi.
“Nitaenda na vijana wako , si kwa kiasi kikubwa wameimarika kulingana na mafunzo niliowafundisha?”Aliuliza na Dina alitingisha kichwa kukubali.
“Uko siriasi juu ya hili?”Aliuliza
“Kama nisipochukua hatua kuhusu hili wataona labda ninawahofia kwasababu ya uwepo wa jeshi , kwangu muda ndio uhai na siwezi kuupoteza, hivyo fanya uwezekano na kusanya vijana nielekee nao”Aliongea Hamza.
Dina licha ya kusita hakuwa na uwezo wa kumpinga , wasiwasi wake aliona pengine maamuzi ya Hamza ni ya kukurupuka lakini hata hivyo alimuamini na kwenda kujiandaa.
Saa moja mbele Dina alirudi na kumpasha habari kwamba maandilizi yamekamilika na yeye pia anataka kwenda huko.
Hamza alishangaa kidogo mara baada ya kuona kuna mabadiliko makubwa kutoka kwa Dina baada ya kubadili mavazi, pengine ilikuwa ni haraka kuja ndani ya hilo eneo ndio maana hakumchunguza uwezo wake, ila mrembo huyo alikuwa amepiga hatua kubwa.
“Bosi Dina Mabadliko yako ni makubwa mno naona umefanikiwa kutambua kiini cha nguvu zako za mwili”Aliongea Hamza huku akijivunia yale aliomwelekeza Dina mpaka kufikia daraja hilo.
Maji ni zao la mbingu ilikuwa ndio mbinu ambayo Hamza alikuwa akimfundisha Dina , mbinu hio maana yake ni kwamba ilianza mbingu na mbingu ikazaa maji, mara nyingi inakuwa ni kanuni tu kwa njia ya kuvuta hisia ili kuelewa siri za ulimwengu na ndio humuwezesha mtu ubongo wake kupanuka zaidi na kugundua siri nyingi za mwili wake kwa wakati mmoja na mwisho wa siku kutumia siri hizo kulandanisha na nishati ya mbingu na ardhi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kabla ya mtu kuweza kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi lazima awe na msingi wa imani yake mwenyewe ambao utamsaidia kugundua kiini cha nishati yake ya mwili kiroho.
“Sifa zikuendee wewe mwalimu mzuri, na tena leo imekuwa kama bahati nitakuonyesha uwezo wangu wa kurusha visu ulivyoimarika”Aliongea Dina akiamini huko wanakoelekea ni kwenye vita.
“Natarajia kuona hizo mbinu”Aliongea Hamza huku akimshika kiuno na dakika hio wote walitoka na kuingia kwenye gari , wao walipanda kwenye gari ndogo ya Mercedenz Benz huku wengine wakiwa kwenye gari mbili nyeusi muundo wa Noah.
Saa moja mbele waliweza kufika eneo husika ndani ya Wilaya ya Kibaha, sehemu ambayo ndio ilipokuwa kambi ya umoja wa wanajeshi wenye vyeo vya juu na wale ambao wamefikia ngazi za ukomandoo.
Licha ya kwamba umoja huo uliitwa wa Kikomandoo haikumaanisha kila mwanachama alikuwa ni komandoo , lakini hata hivyo ilimaanisha kwamba kila mwanachama alikuwa ni mwanajeshi , awe amestaafu ama bado yupo kazini lakini awe anashikilia nafasi kubwa.
Ilikuwa ni akili kubwa kwa upande wa Mgweno kuanzisha umoja huo kwani mengi yameweza kurahisishika kupitia huo umoja lakini pia aliutumia vyema kueneza ushawishi wake katika vikosi mbalimbali vya kijeshi hata baada ya kustaafu.
Hivyo kwa lugha nyepesi kitendo cha wanachama wa umoja hao kuingia kwenye payroll yake , ilimaanisha aliwamiliki wao na wale ambao pia wanamiliki , hivyo alimiliki sehemu ya jeshi.
Eneo lilikuwa kubwa mno , licha ya kwamba kwa njiani haikuonekana nyumba lakini kulikuwa na ukuta mkubwa mno ulioenda hewani na kufanya eneo hilo lionekane kama kuna uwepo wa taasisi.
Ilikuwa ni dhahiri kwa namna gani Mgweno alitumia hela za walipa kodi kujinufaisha yeye na wafuasi wake.
Kama walivyotarajia eneo hilo lilikuwa na ulinzi sio wa kawaida , maana kitendo tu cha kushuka kutoka kwenye magari yao walinzi waliovalia suti za rangi nyeusi waliwazingira wasisogelee geti la kuingilia ndani ya hilo eneo.
Kila mmoja alikuwa ameweka mkono wake kwenye kiuno wakiwa wameshikilia majambia yenye kufanana.
Licha ya kwamba watu hao walikuwa na uwezo wa kutumia siraha kali kama vile bunduki na aina nyingine ya siraha za moto , lakini hawakutaka walinzi wao kutumia aina hio ya siraha kwasababu za kiusalama zaidi na kutoibua taharuki kwa wananchi pindi kunapotokea mapigano.
“Nyie ni wa kina nani?”Alijitokeza mlinzi mmoja akisogea mbele na kuwauliza huku akiwa na sura iliojaa wasiwasi.
Waliweza kuona sura za watu hao walioshuka kwenye gari hazikuwa na nia salama kuja hapo.
Dina aliekuwa hajashuka kutoka kwenye gari aliishia kutoa ishara ya mkono kupitia dirishani na kundi lile la Chatu kwa spidi kubwa sana waliwasogelea wale walinzi kama mbwa mwitu na kuwadhibiti.
Walikuwa wameimarika mno kimapigano , ilionekana mafunzo ambayo wamepewa na Hamza yalileta manufaa makubwa mno na kufanya walinzi hao kutofua dafu mbele yao.
Kilichoweza kusikika ni mlio wa vile visu kudondoka chini na ndani ya sekunde therathini au zaidi wale walinzi wote walikuwa chini wakiwa hawana fahamu.
Dina alikuwa ametoa maelekezo ya kutowaumiza walinzi hao zaidi ya kuwazimisha kwa muda.
Mara baada ya kuona kazi imefanyika vizuri hatimae alishuka kutoka kwenye gari na kisha akatembea kuingia ndani ya jengo hilo baada ya vijana wake kufungua geti.
Kitendo cha wao kupita kwenye geti tu ni kama wamekanyaga mtego kwani kin’gora cha ajabu kilianza kusikika katika majengo yote yote yaliokuwa ndani ya hilo eneo.
Na ilichukua sekunde kadhaa tu walinzi wengine walitokea kila pande na kuwazingira , kilichomfurahisha Hamza baada ya yeye pia kuingia ni kuona kulikuwa na baadhi ya sura ambazo ni dhahiri hawakuwa raia wa kitanzania.
Muda uleule baada ya kuzingirwa sauti ya mwanaume ilisikika kutoka nyuma yao na kufanya watengeneze njia ili mtu huyo anaengea kuonekana .
“Dina hakika una ujasiri wa kipekee mno , yaani msichana mdogo kama wewe unapata ujeuri na kukanyaga katika hili eneo takatifu, wewe huogopi?”
Muda uleule mwanaume mweusi aliweza kuonekana , alikuwa mkubwa makadirio ya miaka kama therathini hivi kwenda arobaini, aliekuwa na uwararaza na alikuwa amevalia suti ya rangi ya damu ya mzee na saa ambayo ilionekana kuwa ya gharama, alikuwa ameongozana na mabodigadiu wawili warefu wenye miili mikubwa , pembeni yake pia kulikuwa na mwanaume mwingine ambae alionekana kuwa kijana zaidi na watu wote hao Dina alikuwa akiwafahamu.
Mwanaume aliekuwa na umri wa makamo alifahamika kwa jina la Afande Konzu ndio ambae alipokea nafasi ya Kanali Fanueli Yowe mara baada ya kuuliwa na Hamza na kijana mdogo alikuwa ni mtoto wake pia ambae alikuwa ni mwanajeshi akifahamika kwa jina la Nassani Konzu
“Kuja ama kutokuja hapa sio tatizo la kuunganisha na ujasiri wangu , nimemsindikiza mpenzi wangu”Aliongea Dina na palepale Mzee Konzu , Nassani na wengine wote walimwangalia Hamza na mwonekano ambao haukua ukielezeka , walikuwa wakimfahamu fika Hamza ndio ambae alihusika kwa kumuua Fanueli Yowe mkuu wao , ni kwamba tu wakati tukio hilo likitokea Mzee Konzu hakuwepo ila habari zake zilitosha kumtia woga.
“Hamza tunajua ujasiri wako hauna mfano, lakini hili eneo ni tofauti na ilivyokuwa kule Tegeta”Aliongea huku akimwangalia kwa macho yaliojaa umakini kama vile alikuwa akitafuta kuona Hamza akitishika.
“Sentensi yako ya kunisifia naipokea na mimi nasema angalau mnao uwezo kiasi lakini kuna vitu mnafanya vinanikosesha uvumilivu ndio maana nimefika”Aliongea Hamza kwa sauti ya upole tu.
“Wewe ndio Hamza uliemuua Kanali Yowe?”Aliuliza Hassani mtoto wa Mzee Konzu.
“Mimi ndio Hamza ulienisikia na sikumbuki hata kusikia nimemuua mtu wa hilo jina ulilotaja”Aliongea Hamza na kumfanya bwana huyo mdogo kujitahidi kuonyesha ujasiri mbele ya kila mmoja lakini kwenye moyo wake alikuwa na hofu kubwa.
“Hamza wewe ni kijana mdogo na mimi kama mtu mzima nadhani ni vyema nikikupatia ushauri , ukifanya chochote hapa kutugusa matokeo yake yatakuwa mabaya sana , ni busara kujiepusha na matatizo ya kujitakia”Aliongea
“Kama ni matatizo mshaanza kunisababishia kuna haja gani ya kuogopa hayo zaidi ambayo kwanza sina uhakika yanaweza kunipata, ninachotaka kujua ni uhusiano gani uliopo kati ya hili kundi lenu la wanajeshi na familia ya kisiasa ya Mgweno?”Aliongea Hamza.
“Umoja wetu unaundwa na wanajeshi waliostaafu kwa ajili ya kushauri jeshi , tupo chini ya sheria za nchi hii , Mstaafu Mgweno licha ya kuwa raisi mstaafu lakini vilevile ni mwanajeshi mwenzetu , hivyo ni sawa tu kuwa katika umoja wetu, nadhani swali lako nimekujibu. Lakini wewe Hamza na kampuni ya Dosam mnavunja sheria wazi kwa kutaka kuwalea wahalifu ni vyema kuangalia makosa yako kuliko kuyapotezea na mwisho wa siku kuwa makubwa zaidi , hili ni taifa linalolendeshwa kwa sheria na sisi kama wazee inatupasa kutoa ushauri wa kipi kifanyike”
“Unaongea ujinga kwa mtu kama wewe kujiita mzee , kama nia zenu ni za dhati kwanini mnatumia njia za kuzunguka kudili na mimi , kama nimewalea wahalifu kama ulivyosema , vifungu vya sheria vilipaswa kusomwa na mkanishitaki lakini sio kutoa maagizo watu waingilie biashara za kampuni, kwanza naona hata kuongea na mzee kama wewe ambae umelewa rushwa ni kujipotezea muda.”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kufanya mzee yule kukunja ndita.
“Kwahio kilichokuleta hapa ni kitu gani?”
“Nimekuja kupata suruhu ya matatizo yangu na sio vinginevyo”Aliongea
“Baba anamaanisha nini?”Aliuliza Hassani akimwangalia baba yake.
“Ninachomaanisha ni kutaka kuongea na Mgweno kupitia umoja wenu, kwa ulinzi uliopo hapa kama nipo sahihi basi lazima na yeye atakuwepo na anaangalia tu kinachoendelea hapa “Aliongea Hamza na kuweka mkazo wa macho yake kwa Hassani na hisia zake zilikuwa kweli ,ilionekana na mstaafu Mgweno alikuwa ndani ya hilo eneo.
Hata Dina aliweza kugundua hilo lakini tofauti na Hamza ambae alionekana kuridhika upande wake yeye aliingiwa na hofu kwa Hamza kuchukua hatua ambazo zinaweza kumletea matatizo.
“Unaonekana kuwa na akili , lakini kwa bahati mbaya akili yako haiwezi kukusaidia kujilinda , huwezi kumuona mstaafu kirahisi hivyo , kwa vigezo gani kama sio kuota ndoto ya mchana”Aliongea Hassani huku akicheka.
“Asante kwa kuwa mkweli , ili mradi nimembahatisha hapa basi naamini kufunga safari yangu kuja mpaka huku sio bure”Aliongea na palepale macho yake yaliingiwa na usiriasi.
“Unaonekana kuwa kijana usiekuwa na hofu kabisa licha ya kuwa kwenye kizimba cha Chui , nimepatiwa taarifa ya namna ulivyoweza kumzibiti mkuu wa kundi la Hansii, Master Jaggani , ila usione kwamba na uwezo huo unaweza kudili na mimi kirahisi, hata ikitokea nimekuua leo hii serikali haiwezi kunilaumu maana namlinda mstaafu”Aliongea yule mzee kwa kujiamini , licha ya kusikia Hamza alikuwa na uwezo wa ajabu aliamini bado ni binadamu hivyo anacho kikomo cha uwezo wake na hapo ndio wakati at atakaoweza kushinda.
Afande Nassani mara baada ya kuona namna ambavyo baba yake amekuwa siriais na Hamza na yeye mara moja alisogea mbele na kuamrisha vijana wake.
“Wanaumee!!”Aliongea kwa nguvu kwa kupiga makofi na dakika ile wanaume wanne waliokuwa na mwonekano mkubwa na wa kutisha walitoka , walikuwa sio raia wa Tanzania kwa muonekano wao na mmoja alikuwa ameshikilia siraha iliokuwa ikifanana na Bazooka.
Walinzi wa Dina mara baada ya kuona wanaume hao hali za wasiwasi ziliwavaa palepale , walikuwa wakijiamini kutokana na uwezo wao kuongezeka lakini mara baada ya kuona siraha ile iliofanana kwa kila kitu na roketi ya kurusha kwa mkono hofu iliwaingia.
“Acheni woga ile sio RPG ni siraha tu inayotumia umeme kutengeneza bomu la shoti”Aliongea Hamza na kisha akamgeukia Dina.
“Unaonaje nikianza kuona uwezo wako?”Aliuliza na Dina palepale alitoa tabasamu na kisha aliruka sarakasi na ile anakuja kujiimarisha kwenye ardhi visu vilikuwa vimeshamtoka mkononi kuwalenga wale wachina wanne.
Kwa jinsi visu hivyo vilivyokuwa vikizunguka na kasi yake ilikuwa ngumu kuona vinaenda kumlenga nani na kilichoweza kusikika ni sauti ya kukata pepo.
Wale wanaume wanne wa kichina walikokuwa wameshikilia bomu la shoti walikuja kugundua limeshaharibiwa kwa kuchomwa na vile visu vilivyotoka kwa Dina.
Walinzi wa Dina mara baada ya kuona tukio hilo walijikuta angalau sasa wakipata amani baada ya kujua wanaume wale hawakuwa wameshikilia siraha ya moto bali ni bomu la kutengeneza shoti kasma alivyosema Hamza.
Hamza alishangazwa na uwezo ule wa Dina na alisogea mbele huku akimwangalia Mzee Konzu na mwanae.
“Chukulia visu hivyo vimerushwa kulenga huo mtambo wenu wa plastiki na umeharibika , vipi kama vikilengwa kwa watu wako , unadhani watasalimika?”Aliongea
Mzee Konzu na mwanae walionyesha hali ya hofu , ukweli ni kwmaba walikuwa wamejiandaa kwa muda mrefu kwasababu walimtegemea Hamza kufika ndani ya hilo eneo , lakini hawakuamini shambulizi la Dina moja tu limeharibu kabisa mtego wao.
Chaguo la kutumia siraha za moto pia haikuwezekana , kwani watu walikuwa wengi mno na ikitokea hivyo ilimaanisha pia wangejeruhi watu wao , isitoshe pia taarifa za Hamza kuweza kukwepa risasi walikuwa nazo
“Kila mtu na aosgee mbele na kumzuia huku tukisubiria jeshi , kumbukeni mnachofanya hamvunji sheria bali tunamkamata muhalifu”Aliongea na kumfanya Hamza sura yake kujikunja , ilionekana uwepo wa Mgweno ndani ya eneo hilo unaweza kuwaleta wanajeshi na kuwashambulia, isitoshe alikuwa ni mstaafu wa nchi.
Kwanza kwa namna moja ama nyingine aliona kabisa kuja eneo hilo ni kama alitarajiwa na mpango ulionekana ni kumkamata.
Hamza aliamini pengine hata swala la Anna kutaka kumteka Regina na kumlazimisha ajiue ulikuwa ni mpango uliokuwa na mkono wa Mgweno.
Lakini muda huo aliona sio swala la kufikiria kwani alikuwa amezungukwa na watu wengi ambao walionekana kuwa tayari kuitoa roho yake.
Kitendo cha Hassani kutoa ishara ya kushambulia na Dina hivyo hivyo aliwapa kazi vijana wake kushambulia , lakini wale walinzi walionekana kuwa mabaunsa pekee na wamekosa ujuzi maalumu wa kimapambano hivyo walianza kuangushwa na walinzi wa Dina mmoja baada ya mwingine.
Hamza palepale alisogelea mabodigadi waliokuwa wakimlinda Mzee Konzu na kisha aliwazimisha na kumshika Mzee huyo kwenye Kola na kumning’iniza hewani.
“Mgweno yupo sehemu gani kwenye haya majengo ?”Aliuliza Hamza akiwa siriasi kama vile alikuwa amefika hapo kwa ajili ya kumkamata Mgweno , haikueleweka hata alikuwa akipanga nini baada ya kumpata.
“Kama unao uwezo wa kuniua wewe niue , lakini je unajua nini kitakupata kwa kumuua mwanajeshi?, unadhani kwa kutumia nguvu katika dunia hii unaweza kutatua kila tatizo?”
“Nimekuuliza swali lakini bado unaongea ujinga , kwasababu umekitaka kifo basi kufa”Aliongea Hamza na palepale alimrusha kwa nguvu na akaenda kujipigiza kwenye ukuta.
Bam!!
Kilikuwa ni kishindo kikubwa na mzee yule aliishia kuacha alama ya damu kwenye kuta huo wa rangi nyeupe na kudondoka chini.
“Baba..!!!”
“Afande!!”
Walinzi wa eneo hilo mara baada ya kuona tukio hilo macho yaliishia kuwatoka , wakiwa kama hawaamini Kamanda huyo amepoteza uhai kwa namna hio.
Waliamini Hamza asingekuwa kichaa kwa kwenda mbali na kumuua mwanajeshi , maana kwa kufanya hivyo angejiingiza katika uadui na jeshi moja kwa moja.
“Umemuua baba!?, leo sikuachi lazima ufe na wewe hapa”Aliongea Hassani kwa hasira kubwa.
Hamza upande wake hakutaka kujali sana maada wao wenyewe ndio wamemuwekea mtego licha ya kujua tabia yake , kama wangekuwa wanataka amani basi Mgweno aliejifichna ndani ya eneo hilo angejitokeza.
Alijiambia kama maongezi yana uwezo wa kutatua matatizo kwenye ulimwengu basi kusingetokea vita , muda mwingine kuua ni namna ya kutatua tatizo ili lisijitokeze tena.
Hamza palepale akiwa hana utani hata kidogo kwenye macho yake alipiga hatua kumsogelea Nassani lakini walinzi waliamua kujitoa muhanga na kumziba kwa mbele.
“Nakupa nafasi ya mwisho kuniambia wapi alipo Mstaafu Mgweno, kama kuna uwezekano mwambie ajitokeze pengine tutaongea tu na kufanya hili liishe”
Hassani aliishia kushikwa na hofu kubwa mno , alikuja kugundua Hamza hakuwa akiogopeshwa na wingi wao kabisa.
“Yupo kule nyuma wanaendelea na kikao?”Aliongea kwa kutetemeka , licha ya baba yake kupoteza maisha hakutaka pia kupoteza uhai wake kwa kupambana na kichaa Hamza.
Hamza aliishia kutoa tabasamu na kabla hata hawajajua nia yake Nassani alikuwa ameshakwisha kushikwa shingo yake na mkono ulichezeshwa kidogo tu na kilichosikika ni mvunjiko wa koromeo na akapoteza maisha palepale.
Hamza hakuona haja ya kumuacha Nasani hai maana lazima angeandaa mpango mwingine wa kutaka kulipiza kisasi na ingezidi kumuongezea usumbufu.
Hamza muda ambao alitaka kuondoka ndani ya hilo eneo kwa ajili ya kukutana na Mgweno alijikuta mwili wake ukimsisimka baada ua kuhisi uwepo wa mtu mwenye nishati ya mbinu na ardhi akisogea kutokea upande aliokuwepo na hakutaka kumsubiri amfikie bali alimfuata hukohuko.
SEHEMU YA 112
Hamza mara baada ya kuangalia kwa umakini aliweza kumuona mtu huyo na alishangaa baada ya kugundua alikuwa ni mzee wa miaka kama hamsini hivi.
Baada ya kumsogelea Hamza karibu zaidi aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali na kisha alitoa miwani na kuivaa.
“Kijana ujasiri wako sio wa kawaida , kitendo cha kuingia katika eneo la hatari kama hili na kuleta vurugu sijawahi kushuhudia aina hii ya ujasiri”Aliongea huku akionyesha meno yake ya rangi ya njano.
“Mzee Joeli haina haja ya kuongea nae , naomba tu umuue maana huyu ni kichaa ambae anaona kuua sio shida” Sauti hio ilikuwa ya mwanaume kijana alievalia suti ambae alionekana kusogelea eneo hilo.
Hamza alimfahamu huyo bwana na alishangaa kumuona ndani ya hilo eneo na alijiambia inamaa siku ile hawakukoma bado.
Hisia zake zilikuwa sahihi Mzee Joeli alikuwa ni mlinzi wa mstaafu Mgweno kwa muda mrefu sana , alisifika kwa uwezo wake wa juu mno likija swala la mapigano na uwepo wa mzee huyo kwenye maisha ya Mgweno ilimfanya kujiamini mno.
“Kama nyie ndio mmejitokeza pekee , basi naamini Mgweno amenikimbia , sikudhani atakuwa muoga hivyo lakini naamini ujumbe wangu ameupata”Aliongea Hamza.
“Acha porokjo na kwa taarifa yako wanajeshi wapo njiani kufika ndani ya hili eneo”Aliongea Majidi na Hamza hakutaka kujibishana nae maana alimpa nafasi ya kuwa hai yeye na Laizer lakini akajileta tena.
Lakini kitendo cha Hamza kutaka kumsogelea, alizuiwa kwa mbele na yule mzee mwenye nishati za mbingu na ardhi na kumshambulia kwa staili kama anataka kumpapura na makucha na Hamza alimkwepa mara moja.
“Hio mbinu ni maarufu kama Makucha ya Dragoni”Aliongea Hamza akiuonyesha mshangao kidogo maana mbinu hio ni adimu sana kuona mtu akiitumia tena akiwa katika ardhi ya Tanzania.
“Haha.. upo sahihi , wewe mtoto inaonekana uelewa wako juu ya mbibnu za kimapigano sio mbaya sana , upo sahihi , kwa jina naitwa Joeli Ninga , nimepata mafunzo yangu ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi kutokea China kwenye dhehebu maarufu la Azura.
“Inaonekana nguvu ya Mgweno sio ya kawaida mpaka kukupata mwanafunzi kama wewe kutokea Azura”Aliongea Hamza , alikuwa akilijua vyema dhehebu hilo na sheria zao.
Kutokana na jambo hilo Hamza aliona nguvu ya Mgweno haikuwa ndogo hata kidogo , kitendo cha kulindwa na askari wa Azura halikuwa jambo rahisi.
Azura ni moja ya taasisi chache za mafunzo ya kimapigano zinazopatikana katika taifa la China , ambazo zinachukua wanafunzi wachache sana duniani l akini wenye uwezo wa hali ya juu , sababu ya kuwa na wanafunzi wachache ni kutokana na kwamba sheria yao kubwa ni undugu(Brotherhood)
Maana yake ni kwamba ikitokea ukakutana na mwanafunzi wa Azura na ukapambana nae na kumuua moja kwa moja utakuwa umemuua ndugu wa kundi la Azura na kwa mantiki hio unajitengenezeda uadui na dhehebu lote na watakutafuta popote pale kulipa kisasi cha mwenzao , hio ndio sheria yao ambayo ilifanya kuogopeka kwani walikuwa kama watu wanaoweka vinyongo moyoni.
“Kama unajua nimetokea Azura basi utakuwa unajua kwamba ukipambana na mimi moja kwa moja umejitengenezea uadui na ndugu zangu wote”Aliongea
“Sijawahi kuogopa kiumbe chochote ndani ya dunia hii kwanini niogope kikundi cha watu wachache wanaojiita Majoka ya Azura?”Aliongea Hamza na kumfanya yule mzee kukunja sura.
“Kijana ujivuni wako naona unavuka mipaka , hebu tuone ni uwezo gani uliokuwa nao kukufanya kuwa na kiburi namna hio”Aliongea na palepale alianza kukusanya nguvu zake za mbingu na ardhi na ilimchukua dakika chache tu mwili wake ni kama umegeuka na kuwa kivuli cha rangi ya bluu na kwa haraka sana alimsogelea Hamza kumshambulia.
Mikono yake miwili ilionekana kama vile imegeuka kutoka kuwa ya binadamu na kuwa makucha ya Dragoni.
“Licha ya hio mbinu kuwa na nguvu kubwa kwa watu walioweza kuibobea lakini niseme tu uwezo wako wa kuitumia bado ni mdogo sana”Aliongea Hamza.
“Haha.. l;evo ya uwezo wangu wa kutumia hii mbinu imevuka rangi ya bluu na sio rahisi kuweza kujua ni levo ipo nimefikia”Aliongea mzee huyo kwa kujisifia.
“Onja kwanza radha ya mjeledi wa mkia wa Dragoni”Aliongea kwa nguvu na palepale alianza kuchezesha mikono yake na vidole kwa spidi na kadri alivyokuwa akifanya vile kile kivuli cha rangi ya bluu kilionekana kuongezeka nguvu yake maradufu na kutengeneza upepo wa kisulisuli.
Hamza licha ya kuona mbwembwe zile hakusogea wala kuonyesha wasiwasi , ukweli ni kwamba kwa levo aliofikia Mzee huyo aliona amejitahidi sana ni hivyo tu umri ulikuwa sio rafiki kwake.
Hamza alichokifanya ni kufanya mwondoko maridadi sana na shambulizi lile lilimpita lakini dakika hio hio alikuwa ashamsogelea Mzee Joeli na kushika vidole vyake na kisha kuviminja kwa nguvu.
Moja ya mbinu ya kushindana na mtu mwenye uwezo wa kushambulia kwa nishati za mbinu na ardhi kwa kutumia mbinu hio ya makucha ya Dragoni ni kushambulia vidole vyake , ukivisdhambulia moja kwa moja u umemuweza, hio inatokea kwasababu asilimia kubwa ya askari wa namna hio wenye mafunzo wanadhibiti nishati ya mbingu na ardhi kwa kuwianisha na nishati ya mwili wao kwa kutumia vidole.
Kitendo cha vidole vyake kuvunjwa bwana huyo alijikuta akiwa haamini na alipiga ukulele mkubwa kutokana na maumivu makali, hakujua hata amefikiwaje lakini alivyokuja kugundua alikuwa kwenye maumivu makali mno.
“Wewe ….”Bwana huyo alijikuta akishindwa kuongea huku akimwangalia Hamza kwa wasiwasi na uchungu mkubwa.
“Ni kama nilivyokuambia , hii mbinu kwa mbobezi ni hatari sana ila kwa upande wako ni dhaifu mno na nimekuonyesha udhaifu wako upo wapi?”
“Lakini hukuwa na nishati yoyote ya mbingu na ardhi , umewezaje kuepuka shambulizi langu?”Aliongea kwa staili kama vile anamlalamikia Hamza.
“Sina haja ya kuwa na nguvu ya nishati za mbingu na ardhi kudili na mtu mdhaifu kama wewe”Aliongea Hamza na kumfanya bwana yule kuchemka kwa hasira , lakini ilikuwa ndio muda ambao gari zilisikika zikiingia ndani ya eneo hilo kwa kasi.
“Haha ni wanajeshi , ni wanajeshi tuliowaita, Afande Yasini nipo hapa”Aliongea Majid kwa furaha na dakika ile ile Hamza aligeuza uso wake na kuweza kumuona mwanajeshi alievalia kombati , alionekana kuwa na cheo cha Meja.
“Majidi tumepata taarifa kwa kuchelewa kidogo lakini afadhali tumekuja ndani ya muda, unaweza kutulia kwa uwepo wetu hakuna wa kukugusa na tutahakikisha tunaondoka na hawa wahalifu”Aliongea Kamanda huyo huku akimwangalia Hamza kwa macho yaliojaa sumu.
Lakini kabla hata hajavuta pumzi ya kumaliza kuongea , Hamza alikuwa amekwisha kutoka aliposimama na ile anakuja kuibukia alikuwa mbele ya Majid na vidole vyake vilitua katika shingo na kuiminya kwa nguvu na Majidi aliishia kutema damu na kudondoka chini.
Meja Yasini uso wake uligeuka mweusi palepale kwani hakuweza hata kuona namna Hamza alivyotoka alipokuwa amesimama na kuja kutokeza mbele ya Majidi na kumfanyia shambulizi lile.
“Umemuua?”Aliuliza mzee Joeli kwa hali ya kupaniki.
Hakujua angeenda kuongea nini kuhusu kifo cha Majidi kwani ni yeye mwenyewe alietoa ahadi kumlinda na kutoka katika hilo eneo akiwa salama na haikuwa haja ya kuondoka na mheshimiwa Mgweno.
“Wewe ni nani wa kuua mtu mbele yangu?”Aliuliza Meja huyo.
Kwa muda mrefu sana alitamani kujiunga katika u moja huo wa makomandoo ili kuwa sehemu ya watu wanaofurahia mema ya nchi na ndio maana baada ya kupokea simu kufika eneo hilo na kikosi cha jeshi hakusita hata mara moja zaidi ya kuitikia ndio , huku akiahidi kwamba atamtoa Bosi Majidi akiwa salama salimini, sasa kitendo cha Hamza kumfanyia shambulio Majidi na kumuua palepale kitumbua kimeingia mchanga.
Baada ya kuona Hamza amemharibia mpango wake , palepale alitamani kumpiga risasi amuue.
“Huyu kifo chake nilikichelewesha tu , kama ni kufa alipaswa kufa muda mrefu .. watu waliopangiwa kufa ni wasumbufu sana ukiwakwepa wanakufuata wenyewe”Aliongea Hamza.
Mara baada ya kupigana na Jagani ndani ya ulingo wa NunguNungu alijua Majidi na mwenzake Laizer wamekoma , ila hakuamini kama angejitokeza mbele yake, tena akiwa na kiburi.
“Unaongea kama vile unacheza maigizo , hivi unajua mtu uliemuua ni nani?, hebu mkamateni mara moja na ikitokea akileta ukinzani mpigeni risasi “Aliongea palepale kwa hasira na wanajeshi walioshikilia mitutu ya bunduki mara baada ya kupokea oda hio walisogea mbele kwa kazi.
“Hili ni jeshi ambalo kazi yake ni kulinda usalama wa nchi , lakini kundi la watu wachache wala rushwa wanatumia hawa wanajeshi kwa ajili ya kutimiza matendo yenu ya uovu, hii nchi inachezewa sana”Aliongea Hamza.
“Tupo hapa kwa ajili ya kupambana na jambazi kama wewe na unachoongea hakina msingi wowote kwa haya ulioyafanya”Aliongea.
“Kama ni hivyo unaonaje ukisogea kwanza wewe mwenyewe kuliko kuwatanguliza wanajeshi wako?”Aliongea Hamza akiwa hana wasiwasi hata kidogo lakini kauli yake ilimuogopesha Meja Yasini.
“Afande Yasini asikutishie huyo , hana mtu wa kumpa msaada zaidi ya hao majambazi wenzake , mkamateni akafie jela”Aliongea Joeli ambae maumivu yalionekana kupungua.
Meja Yasini mara baada ya kusikia maneno hayo ni kama alipandwa na morali upya na palepale , aliiwamrisha wanajeshi wake kumlenga Hamza na akileta ukinzani awashambulie.
Lakini sasa wanajeshi wale wakati wakimlenga walishangaa Hamza amekwisha kutoweka mbele ya macho yake na ile wanataka kujua ametowekea wapi walishangaa akiwa nyuma ya Mzee Joeli.
“Nilikuvunja vidole vya mkono wako mmoja , lakini naona unataka kifo kabisa”Aliongea Hamza na sekunde ileile mkandamizo usiokuwa wa kawaida ulimtoka na kisha aliishika shingo ya yule mzee na kilichotokea ni kulegea kwa shingo yake na akadondoka chini akiwa hana uhai tena.
“Mzee Joeli!!!”
Hakuna ambae aliamini mlinzi wa mheshimiwa Raisi wa muda mrefu, aliekuwa akiogopwa mpaka na makomandoo alikuwa amepoteza maisha namna ile.
“Meja wewe unatokea Kambi ipi , unaonaje kabla ya kuruhusu wanajeshi wako kushambulia ukawasiliana na wakuu wako kwanza”Aliongea Hamza akiwa hana wasiwasi.
“Kupiga simu ama kutopiga haikuodolei sifa ya uhalifu , wewe ni muaji kwanini nikusikilize”Aliongea.
“Mimi nimekushauri tu ili kukuepushia usumbufu baadae”Aliongea Hamza na muda huo Dina na vijana wake walisogea upande waliokuwepo.
Kwa muda wote walikuwa bize kudili na walinzi wa eneo hilo na walifanikiwa.
“Hamza tunafanya nini kuhusu hawa wanajeshi?”Aliuliza Dina kwa wasiwasi maana alijua hata kama walikuwa na uwezo wa kushambulia hao wanajeshi , lakini kupigana nao ni kama kutangaza vita na serikali na pengine ndio Mgweno alichokuwa akitegemea.
SEHEU YA 113.
Hamza mara baada ya kuona wanajeshi hao walikuwa ni wa kutii maagizo bila ya kuuliza sababu alitoa ishara ya kutofanya chochote.
“Haina haja ya kushambulia ,hawa wanajeshi hawana kosa zaidi ya kufuata maagizo ya wakuu wao , ngoja nimpigie Himidu simu”Aliongea Hamza.
Ukweli ni kwamba Hamza angemaliza swala hilo tokea mwanzo kama angeongea na Himidu na hata kesi za Anna na wenzake zingeweza kumalizwa kimya kimya , lakini kutokana na Mgweno kuanza mwenyewe alitaka kumuonyesha ni umbali kiasi gani anaweza kwenda kama tu ikitokea amechokozwa , isitoshe hakuwa akifanya kosa kwani wanajeshi wale walikuwa wamesingiziwa tu makosa kutokana na hila za kisasa.
Lakini dakika ambayo alikuwa akitoa simu yake kwa ajili ya kumpigia Himidu , alishangaa kuona yeye ndio aliekuwa akipiga na alipokea palepale.
“Himidu naona hakuna linalokupita kwenye nchi hii”Aliongea Hamza huku akiwa na tabasamu.
“Bosi hata wewe una taarifa?”Aliiongea Himidu upande wa pili.
“Taarifa ya nini?”
“Wewe si ndio umesema hakuna kinachonipita , nilijua unaongea kuhusu maharamia wa kundi la The Shark”Aliongea Himidu
“The Shark!!, Wamefanya nini kwani?”Aliuliza Hamza huku akiwa amekunja sura kwa mshangao.
“Bosi kama hukuwa ukiwaongelea hao ulikuwa ukilenga kitu gani?”Aliuliza Afande Himidu na kumfanya Hamza kucheka na baada ya hapo alimwambia kilichotokea.
“Dah , Bosi kwa kusababisha matatizo una kipaji kikubwa sana”Aliongea Himidu huku ikionyesha ni dhahiri alikuwa akisikitika
“Ila bosi haina shida , wewe angalia mwenyewe namna ya kudili nao ,isitoshe mimi pia nipo upande wa familia ya Wanyika na kwa maslahi ya nchi tulitamani kulikomesha lakini tuliepusha migongano ndani ya jeshi”Aliongea Himidu.
Hamza hata yeye tokea mwanzo alikuwa akijua Himidu anatokea katika familia gani na namna ambavyo walikuwa wakishindana na baada ya hilo kupita alirudi kwenye topiki ya kundi la The Shark.
“Ulikuwa ukiongelea kuhusu The Shark , ni kitu gani kilichowakuta?”Aliurudi kwenye topiki ya mwanzo.
“Maharamia wote wa kundi la The shark wamepoteza maisha kwa kuuliwa , yaani meli yote iliokuwa na maharamia zaidi ya mia wamepoteza maisha na baadhi yao kukimbia”
“Nini , nani kafanya hivyo?”Aliuliza Hamza huku akionyesha mshangao.
“Sijui ni nani amehusika , zamani swala kama hili lisingesumbua sana kwasababu ni kundi la Daraja B , lakini kutokana na kujiunga na Sea Demons tatizo limekuwa kubwa , Levithian anatushutumu wanajeshi wa Malibu ndio wamehusika , anasema katika ukanda wa Afrika mashariki tofauti na kitengo chetu hakuna jeshi lenye uthubutu wa kufanya mauji ya aina ile , hata baadhi ya makundi mengine ya Alshababu , Boko Haram hawana sababu ya kuwashammbulia na kuwamaliza kwa siku moja tu , leo ili kuonyesha mkazo wa msimamo wake amesogeza meli yake mpaka mpakani mwa Tanzania na amekamata meli kadhaa za mizigo ambazo zilikuwa zikiingia bandarini kwetu , anasema bila maelezo ya kutosha hawezi kuachia meli hizo , kama hili likiendelea wasiwasi wangu litakuwa swala kubwa na haijalishi ana uwezo kiasi gani hawezi kushindana na nchi”Aliongea akionekana kabisa hakutaka Levithiani aingie katika matatizo.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo kichwa kilianza kumuuma na kujiuliza ni nini hiki kinachotokea, palepale alimsogelea Lau na kumwambia ampe sigara na kiberiti na baada ya kupewa aliwasha na kuvuta moshi huku akijikuna kichwa.
“Huyo Ngisi kwasababu mpaka sasa hajaua mtu basi atakuwa anajali urafiki wetu, kwanini usimuelezee wewe mwenyewe kilichotokea?”Aliongea Hamza
“Nimefanya mawasiliano kwa siri kumwelezea nchi yetu haihuski katika shambulizi hilo lakini yule bwana anashindwa kabisa kuniamini na anasema kama sio sisi basi tutafute nani amehusika , lakini mimi peke yangu najuaje muhusika sasa bila kushirikisha vitengo vya usalama? , najaribu kuwa makini ili watu wasije kufahamu nilichokuwa nikifanya nje ya nchi la sivyo inaweza kuleta shida”Aliongea Afande Himidu.
Hamza mara baada ya kusikia maelezo hayo aliweza kuelewa rafiki yake huyo anachomaanisha
“Wewe mwanaharamu kwahio unaongea hayo yote , unachotaka ni msaada wa kutumia sura yangu?”
“Haha… bosi ninachotamani ni sura yako kumzima huyu mshenzi maana anakusikiliza zaidi kuliko mimi , nikisema niende mwenyewe kuna uwezekano akanifanya chakula cha samaki”Aliongea na kumfanya Hamza macho yake kusinyaa , hakuona haja ya kutokumsaidia rafiki yake kutatua tatizo hilo , isitoshe aliona sio vizuri kwa Levithian na Himidu kugombana ilihali walikuwa ni marafiki wa kitambo.
Upande wa Hamza pia aliona swala la Kundi la maharamia wa the Shark kufa ghafla tu aliona kuna kitu hakipo sawa na hawezi kuchukulia rahisi na anapaswa kwenda kuchunguza yeye mwenyewe.
“Unaonaje tukifanya hivi hivi , wewe andaa usafiri na nikitoka huku nilipo nitaanza safari ya kuelekea huko ili nikaangalie klichotokea”Aliongea Hamza.
“Bosi najua nakusumbua lakini asante sana , maana hii hali nimeshindwa hata kuielezea kwa wakubwa wangu”
“Hebu acha porojo na maliza na hili kwanza maana kuna mitutu imeelekezewa kwangu”Aliiongea Hamza na kumfanya Himidu kucheka na ksha kukata simu akimwambia ampe dakika mbili.
Muda ule Meja Yasini , alionekana kupokea simu na aliongea kwa heshima.
“Jambo Afande …Ndio ndio Afande…. , nitahakikisha misheni inakamilika”
Mara baada ya Afande Yasini kukata simu alimwangalia Hamza kwa heshima ,uso wake ulikuwa umejawa na hali ya kumkubali.
“Mr Hamza nimekukosea kwasababu sikuweza kufahamu kama wewe ni mwenzetu , tafadhari naomba uingie kwenye gari tukusindikize mpaka bandarini”Aliongea Afande Yasini.
Kauli hio iliwafanya Dina na wenzake kushusha pumzi za ahueni maana walijua ingekuwa ngumu mno kupambana na wanajeshi bila kuibua matatizo makubwa mbeleni.
“Kwanini unataka wakusndkize mpaka bandari ya jeshi?”Aliuliza Dina
“Kuna swala nakwenda kulishughulikia kwa ajili ya rafik yangu , tangulia kurudi kwanza na nitakuja kwako kama nilivyokuahidi , siwezi kwenda kinyume na ahadi yangu”Aliongea Hamza na Dina baada ya kusikia hivyo alishikwa na furaha.
“Basi kuwa makini huko uendako”Aliongea na Hamza alimshika kidevu kimahaba na kisha akampita
Hamza ndio aliekuwa wa kwanza kuondoka na gari za kijeshi na kumfanya Dina kumwangalia Hamza akiondoka huku akiwa na hisia zisizoeleweka , kwa kile ambacho amefanya hapo ilipaswa kuwa swala kubwa lakini limeisha kiwepesi sana.
“Madam unadhani nini kitatokea baada ya hapa , ijapokuwa tumefanikiwa lakini moja kwa moja tumeingia katika mgogoro na Mgweno?”Aliuliza Lawrence,
“Tuliopambana nao hapa ni walinzi pekee na karibia wanachama wote hawapo, hata kama kiongozi wao amekufa haimaanishi umoja huu umekoma lakini nina uhakika hauwezi kuwa kama mwanzo , mambo kama haya hayahitaji tuhusike kwa asilimia mia moja , tunahitaji kuanza na baada ya hapo watu sahihi watakuja kumalizia kazi”Aliongea Dina.
“Unamaanisha baada ya habari za hapa zitasambaa na kufikikia wanajeshi na kutengeneza msimamo tofauti?”
“Ndio , hivyo Mgweno kwasasa hata kama bado anayo nguvu ya kisiasa lakini ni ya Muda , familia ya Wanyika wakifanikiwa kushikilia Ikulu kwa asilimia mia moja maana yake nguvu yake muda wowote itazima na kama hilo likitokea mbinu pekee ni kujiimarisha katika ulimwengu wa Giza, anaweza kukimbilia Binamu kuomba sapoti lakini siku zote Binamu ni shirika ambalo halijawahi kushirikiana na mtu mdhaifu, isitoshe Eliasi aliekuwa rafiki yake amemsaliti kwa kuikabidhi Ikulu kwa Wanyika”
“Kwa maana hio kitu pekee atakachofanya ni kuhakikisha anajiimarisha kwenye ulimwengu wa Giza na kama ni hivyo si ndio tutakuwa shabaha yake?”
“Ni kinyume chake , sisi ndio tunakwenda kumlenga kama shabaha , kwanzia sasa tunapaswa kujipanua zaidi ili asipate nafasi ya kujilimbikizia nguvu, na imekuwa rahisi sana kwa tulichofanya leo”
“Ndio madam , kwa leo lazima taarifa zetu zitasambaa na pengine muda si mrefu tunaweza panda daraja kimataifa”Aliongea Lawrence na Dina alitabasamu huku akijiambia yote hayo yamewezekana kwa uwepo wa Hamza na ataendelea kumshikilia kwa kumpa mapenzi yake yote hata kama mara nyingi anaonekana kumsahau akiwa na wanawake wengine na kumkumbuka wakati mke wake Regina akiwa katika matatizo , lakini alijiambia kama Hamza kumkumbuka kwake ni kwasababu ya Regina basi atahakikisha anafanya mambo mazuri kwa siri kwa ajili ya Regina.
Lisaa limoja mbele Hamza aliweza kufikishwa katika bandari ya jeshi Bagamoyo na aliweza kuwakuta watu kadhaa aliokuwa wakifahamu , alikuwa ni Afande Mwiba na Afande Barafu.
Kilichomshangaza Hamza ni baada ya kutambulishwa kwa mkuu wa kitengo cha Malibu Brigedia Doswe ambae ndio alikuwa akienda kama mwakilishi wa kutatua swala hilo ili kuongeza uzito kwa Levithian ionekane kweli kitengo chao hakikuhusika.
Brigedia Doswe licha ya kwamba alikuwa akizisikia habari nyingi za Hamza na baadhi yake hata kushuhudia, lakini alikuwa na kinyongo na Hamza , sio kwasababu alikuwa na uwezo bali ni kwasababu Hamza alikuwa na ukaribu na Himidu.
Doswe na Himidu wa kwanza kujiunga na jeshi alikuwa ni Doswe , lakini ajabu baada ya Himidu kujiunga alipanda cheo haraka haraka na kumpita hata yeye na hata nafasi ya Ushauri ukuu ilikuwa ni yake na aliamini Himidu alitumia Koneksheni ya Wanyika kuikwapua nafasi yake na yeye kubakia kama mkurugenzi wa Malibu.
Ili kuwatuliza maharamia wa kundi la Sea Demons kutokushambulia ndio maana waliamua kutumia Speedboat ya kawaida kwenda maji ya kimataifa kuonana na Levithian,
Wakati jua likizama hatimae meli tatu za kivita zilionekana kwa mbali , kwa jinsi meli zao na vifaa vyao vya kimashambulizi vilivyoonekana , ilikuwa ni ngumu kudhania watu hao walikuwa ni maharamia , ilikuwa ni kama vifaa vya kivita kutoka taifa dogo.
Mara baada ya maharamia kuona boti ndogo inawakaribia , palepale miluzi na firimbi za kutoa ishara ilianza kusikika kama vile ni mbwa wanaobweka baada ya mtu asiejulikana kuingia kwenye himaya yao.
Hazikuchukua hata dakika mbili mwanaume mwenye ngozi nyeusi tii na misuli mikubwa kama Goliati alitembea kibaunsa mpaka mbele ya meli hio , alikuwa amevalia koti la kijeshi ambalo ni urithi wa Admiral mmoja wa jeshi la majini la Uimgereza katika vita ya pili ya dunia.
“Yule sio ndio Levithian?”Aliuliza Afande Doswe akimwangalia mwanaume wa miraba minne aliekuwa amesimama kwenye meli
Afande Mwiba na Afande Barafu waliokuwa wamekaa pembeni wote mwonekano wao ulibadilika , licha ya kwamba walikuwa katika umbali lakini hofu yao iliongezeka kutokana na kuhisi mkandamizo wa nishati za mbinu na ardhi usiokuwa wa kawaida.
Levithian ndio mtawala wa bahari wa maharamia wote , unaweza kumuita mfalme wa bahari ambae anaongoza kundi namba moja la kiharamia maarufu kama Sea Demons , huku yeye akibatizwa jina la Sea Monster.
Kulikuwa na makundi makubwa ya kiharamia duniani , ikiwemo kundi maarufu la Whaler of the Arctic ocean , lakini kama utalinganisha na kundi hilo ambalo linaongozwa na Levithian walikuwa na vifaa vizito vya kimashambulizi ambavyo sio tu teknololijia yake kuwa kubwa lakini vilevile maharamia wake walikuwa wabobevu kwenye kuvitumia na hio yote ni kutokana na maharamia hao kuwa wanajeshi wastaafu na waliotoroka jeshi na kuungana na Levithian katika biashara ya kuuza siraha.
Moja ya sababu ambayo inafanya kundi la Sea Demons kuogopwa na kundi la Malibu ni kutokana na madaraja yao , Sea Demons wenyewe walikuwa daraja S huku kikosi cha Malibu cha kupambana na nguvu za ziada kipo katika daraja A , kulikuwa na vikosi vichache pekee vya kijeshi ambavyo vilikuwa katika daraja S kama vile Kitengo cha China maarufu kama Dragon Soul na The Wolfpack kutoka Marekani.
Sababu nyingine ya Sea Demons kuheshimiwa na mataifa mengi ni kutokana na kwamba kitendo cha wao kuwa na nguvu kubwa baharini ilidumisha usalama wa meli nyingi za mizigo kwa kuepuka mashambulizi kutoka kwa maharamia wadogo wadogo ambao wanataka kuiba , hivyo kwa lugha nyepesi kundi h ilo ndio lilikuwa likimiliki makundi mengi madogo ya kiharamia na kuhakikisha hawavunji sheria zilizowekwa na kuhatarisha usafiri wa baharini.
Sasa unaweza kushangaa kwanini kundi la ulimwengu wa giza la Sea Demosn kupambanishwa na kundi la kijeshi la ulimwengu wa kawaida , ukweli ni kwamba vigezo ni vilevile , kikosi cha Malibu kilipanda daraja kutoka chini mpaka kufikia hapo na kushinda vitengo vingi vya mataifa ya nje ni kutokana na wingi wa misheni ambazo zilifanywa na kikosi hicho huku Sea Demons wao walipanda daraja kutokana na kuangusha kundi lingine kubwa la kiharamia ambalo ni mara kumi zaidi ya misheni ambazo zimefanywa na kitengo cha Malibu , maana yake inakuja kuwa sawa tu kwa wale wanaopanga madaraja kwasababu wingi hufidiwa na uwezo wa mtu au taasisi hata kama ni moja.
“Brigedia nadhani ni vizuri kama tutasubiri na kuangalia hali kwanza kabla ya kuwasogelea”Alishauri afande Caro.
“Usiwe na wasiwasi , hawezi kutufanya chochote , isitoshe tupo hapa kama wawakilishi wa taifa”Aliongea Afande Doswe na kisha aliwaamrisha wanajeshi wake wapunguze mwendo na kunyanyua bendera inayoashiria amani.
Kikosi hicho cha wanamaji walifanya haraka kama walivyoamrishwa na upande wa meli ile ya maharamia na wenyewe waliinua bendera yao wakiwaashiria kwamba wanaweza kusogea karibu zaidi.
Upande wa Hamza alikuwa amekaa zake nyuma kabisa ya boti akiwa hana habari na alikuwa akivuta sigara mfululizo ambazo alichukuwa kutoka kwa Lawrence , alimwangalia Levithian aliekuwa juu ya meli na kumfanya macho yake kusinyaa kama mtu ambae alikuwa akikumbuka mbali.
Ilikuwa ni nje ya mategemeo , Ngisi huyo kama alivyopendelea kumuita alikuwa akimfuata nyuma yake kwa miaka mingi lakini wakati huo amekuwa kiongozi wa kundi kubwa duniani la kiharamia mpaka kuhenyesha nchi.
Mara baada ya boti ile kukaribiana na meli ya kivita , hatimae ngazi ya kamba ilishushwa.
Afande Doswe mara baada ya kuona ngazi hio alitoa tabasamu kwa hali ya juu ya kujiamini .
“Mnaona sasa , hata hatujaongea neno lolote lakini tayari wametukaribisha tupande juu , hivi mnadhani kundi la kiharamia wanao ubavu wa kushindana na nchi kama yetu?”Aliongea Afande Doswe.
Upande wa Afande Mwiba na Afande Caro pia walishangaa maana hawakujua mambo yanakwenda kuwa marahisi namna hio , wote walionekana kupatwa na ahueni.
Afande Doswe ndio aliekuwa wa kwanza kutangulia na kushikilia ngazi hio na kupanda kijeshi kwenda juu huku ujivuni wa kuwa mwakilishi wa kitengo cha Malibu ukiwa umemvaa.
Wakati anakaribia kufika juu ghafla tu alizuiwa na mwanaume goliati kama kifusi na kumfanya asiweze kuona hata mbele.
Alikuwa ni Levithian aliemkinga kwa mbele asipande kuja juu kabisa , kitendo kile kilimfanya Afande Doswe mwili wake kukakamaa na alimeza mate mengi akijitahidi kujituliza.
“Levithian mimi ni…”
“F*ckk off”Aliongea Levithian kwa sauti nzito na kumfanya Afande Doswe kurudi nyuma kwa hofu maana hakuona dalili za kukaribishwa kukanyaga juu ya meli hio.
Kwa mtu anaetisha kama Levithian akikwambia ondoka unajikuta ukiondoka mwenyewe bila ya kupinga , lakini kwa Doswe mara baada ya kukumbuka chini yake ameacha vijana wake ambao wanamwangalia kama kongozi hakutaka kukata tamaa kirahisi.
“Naitwa Brigedia Doswe , nipo hapa kama kiongozi wa kitengo cha Malibu..”Aliongea kwa Kingereza lakini alivyojitambulisha uso wa Levithian ulizidi kukufunikwa na weusi wa ukatili.
“Idon’t care who you are idiot”Aliongea akimaanisha hakuwa akijali yeye ni nani mjinga.
Kitendo cha kusikia akiitwa mjinga , alijikuta akipandwa na hasira mno na alishindwa kuvumilia aina hio ya udhalilishaji na palepale aliamua kutumia nguvu ili kupanda juu , lakini Levithian alinyoosha mkono wake na kisha akamsukuma kwenye kifua na kumrudisha chini na kwa kutokana na kutumia nguvu za mbingu na ardhi , Kamanda Doswe hakuweza kujizuia na ilikuwa bahati kwake na yeye alikuwa pia na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi hivyo baada ya kuanza kukosa balansi aliweza kujizuia kwenye ngazi asidondoke.
Palepale hakutaka kushindwa , alitaka kuonyeysha ubavu mbele ya Levithian hivyo mara baada ya kupata balansi kwenye ngazi ile alikusanya nguvu zkae zote na kisha kwa spidi kubwa alipanda juu.
Lakini ni kama Levithan alijua Doswe anachokwenda kufanya kwani aliachia mkandamizo mkubwa wa nishati ya mbingu na ardhi kuliko hata aliokusanya Doswe na kitendo cha kutaka kumfikia alijikuta akikutana na wimbi kubwa la upepo ambalo lilimrudisha kwa kumzungusha hewani kwenda chini.
“Kamandaa…!!”
Afande Caro alijikuta akipiga yowe mara baada ya kumuona mkuu wake akipokea shamblizi lile , lakini kwa bahati nzuri alidondokea kwenye boti yao , lakini alikuwa tayari ashaumizwa viungo vya ndani kutokana na shambulizi lile na kumfanya kutema damu nyingi.
Doswe mara baada ya kusimama alijikuta akimwangalia Levithian kwa macho yaliojaa hofu mno na mshangao , uwezo wake ambao ulikuwa umefikia mwishoni mwa levo ya nafsi haukuwa kitu mbele ya uwezo wa Levithian.
Kutokana na hofu yake alioweza kuonyesha kundi lile la maharamia walianza kumcheka kwa nguvu kwa kile alichofanyiwa , huku wengine wakimwita mjinga kwa kujaribu kushindana na hosi wao.
“Levithiana kama umeshusha ngazi kwanini bado hutaki nikiingia melini kwako?, Au ni ishara kwamba hutaki maongezi na sisi wawakilishi wa kitengo cha Malibu?”Aliongea Afande Doswe na kauli yake ilikuwa sahihi kwani hata wanajeshi alioambatana nao walikuwa katika hali ya mshangao pia , waliamini kitendo cha kushushiwa ngazi ilikuwa ni ishara ya nia njema katika mazungumzo hayo lakini baada ya mkuu wao kupanda akamshambulia , walijiuliza kuna mantiki ipi kufanya hivyo kama hakukuwa na nia nzuri kwa kuwashushia ngazi.
“Nimeshusha ngazi sio kwa ajili ya wewe mjinga , nimekushambulia kwasababu huna thamani yoyote ya kukanyaga juu ya meli yangu”Aliongea
“Kama hujashusha kwa ajili yangu umeshusha kwa ajili ya nani?”Aliuliza Afande Mwiba na Caro bila ya kupenda aligeuza macho yake na kumwangalia Hamza ambae alikuwa akitupa kipisi cha sigara majini ikionyesha amemaliza.
“Nawashauri mwendelee kubakia ndani ya boti , msije kunilaumu mkiuliwa kama mkinifuata”Aliongea Hamza huku akipita kutoka nyuma na kisha akashikilia ngazi na kuanza kupanda.
Kadri Hamza alivyokuwa akipanda juu ile hali ya ukatili kwenye macho ya Levithian ilianza kushuka taratatibu na kuonyesha muoenekano wa kukumbuka mbali.
Dakika ileile Levithian alirudi nyuma na pamoja na watu wake waliikunja viuno vyao na kuinama chini kuonyesha heshima ya kumkaribisha mfalme kwenye meli yao.
Tukio hilo lilikuwa tofauti kwasababu ya kile ambacho Kamanda Doswe alifanyiwa , iliwafanya wanajeshi wa kitengo cha Malibu pamoja na mkuu wao kushikwa na hali isiokuwa ikielezeka.
Hamza mara baada ya kukanyaga juu ya deki ya meli hio maharamia wote walibakia kimya huku wakimwangalia kwa nyuso zilizokuwa na kila aina ya hisia , wengine wakiwa na wasiwasi , wengine wakiwa na hali ya msismko na wengine walimwangalia kama shujaa alierudi kutoka vitani.
Dakika ileile wote kwa pamoja waliongea kwa hali ya juu .
“My Prince!!”
Mara baada ya kauli ile wakiongozwa na Levithian wote walipiga magoti kwa mguu mmoja kijeshi.
Kitendo hicho ni kama anga libebadilika ghafla , hususani namna sauti zao zilivyosambaa na kusikika kwa wakati mmoja bila kuachana, kwa wale waliokuwa wakiangalia ni kama walisikia sauti hizo zinajirudia rudia kwenye masikio yao kutokana na mwangwi.
Ni mtu wa aina gani ambae anaweza kumfanya Levithian Goliati wa bahari kupiga magoti bila ya ukinzani tena kwa heshima kubwa namba hio, ki ukweli kulikuwa na maswali mengi.
Upande wa Hamza aliishia kukuna kichwa chake asijue acheke ama alie, mwanzoni mpango wake ni kuja kumaliza mambo kimya kimya bila kujionyesha lakini mambo yalikuwa nje ya matarajio yake
“Mnaweza kusimaa sasa , nilishastaafu muda mrefu kwanini kila siku ni kama mnataka kunirudisha kazini”Aliongea.
Hamza mara baada ya kuongea hivyo Levithian alikuwa wa kwanza kusimama na akafuatiwa na wenzake.
“Ngisii bwana na mambo yako yaliopitwa na wakati!!”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu akimsogelea Levithian kwa bashasha.
‘Haha.. bosi nimesikia habari zako kutoka kwa Mafii umepoteza uwezo wako wa nishati za mbingu na ardhi , bado kweli unaweza kuwa kama zamani?”Aliuliza Levithian.
“Unaweza kujaribu uone”Aliiongea Hamza.
“Kama ni hivyo bosi , basi sina haja ya kujizuia” Aliongea.
Wanajeshi wa Malibu hawakujua ni kitu gani Hamza na Levithian wanaongea , lakini kilichofuatia baada ya hapo kiliwafanya wasimame juu ya boti kw amshangao mkubwa.
Yule Levithiani ambae mwanzoni alionekana kama binadamu wa kawaida aliongezeka ghafla ukubwa wake kwa zaidi ya mara mbili huku rangi ya weusi kwenye mwili wake ikimpotea na kuwa ya kijani.
Kama Simba alibweka kwa hali ya juu na kisha alimsogelea Hamza kwa kasi na kumpiga kwa kumlenga kifuani.,
Ngumi ile haikuwa na haja hata ya kumpiga mtu , upepo ambao ilikusanya ulitosha kusaga maini yalioko tumboni kwa binadamu wa kawaida.
Wanajeshi wale walishituka na kudhania pembeine Levithian anataka kumuua Hamza.
Lakini maajabu yake Hamza aliweka shambulizi la mkono wake na kisha aliruka juu na teke la sarakasi na kumpiga Levithian juu ya kifua
“Bam!!
Mwili wa Levithiani ni kama uligongwa na nyundo kubwa kwani ulirudishwa nyuma kama jiwe na kwenda kujipigiza kwenye keria ya meli.
Kwa jinsi ambavyo alirushwa utadhani mtu huyo alikuwa puto ambalo ndani yake ni upepo na sio nyama.
Maharamia waliokuwa juu ya meli hio wote walishikwa na bumbuwazi wasiamini bosi wao waliekuwa wakimuogopa mno ndio aliepigwa na teke na kurushwa umbali mrefu namna hio , lilikuwa ni tukio ambalo halikuwezekana kwa macho ya kibinadamu.
Upande wa wanajeshi wa Malibu mara baada ya tukio hilo walijikuta wakikumbuka namna ambavo Kamanda wao alishambuliwa mpaka kushushwa chini na kisha wakaunganisha na tukio la Hamza kumshambulia Levithian na teke moja tu, utofauti ulikuwa ni kama wingu na tope.
Kamanda Doswe uso wake ulikuwa ukiungua kama vile amekula kinyesi cha mende , palepale alikunumba neno alilomwambia Hamza alivyosema anataka kuja nae hapo na alianza kujiona ni kwa namna gani alikuwa mjinga.
Afande Caro na Mwiba wenyewe muda huo waliishia kutabasamu kwa uchungu katika moyo yao , waliona mtu kama Doswe kushindana na Hamza ni kuwa mjinga.
Katika meli hio Maharamia karibia wote walikuwa wakimwangalia Hamza kama vile wanaaangaliana na mtu maarufu ambae wanataka kupiga nae picha.
Levithian mara baada ya pigo lile alirudi katika hali yake ya kawaida na kuanza kukohoa huku akitema damu chini akishika tumbo na kumwangalia Hamza kwa tabasamu lilojaa wasiwasi.
“Bosi ni mbinu gani unatumia , kwanini bado unaonekana sio wa kawaida licha ya kupoteza uwezo wako?”
“Ngisi ni mara ngapi nakuambia kukusanya nguvu za ndani na kujigeuza puto ni udhaifu mkubwa kwako , una bahati sijatumia nguvu ile ungekuwa baharini unaogelea”;AliongeaHamza.
“Haha.. bosi mtu asiekuwa wa kawaida atajua vipi udhaifu wangu , wewe ndio bosi ndio maana unanifahamu vizuri”Aliongea Levithian na palepale alimsogelea Hamza akiwa hana maumivu na kumkumbatia kama vile amekumbatia mdoli kutokanna na udogo wa Hamza.
“Naona unafanya kazi nzuti kijana , yaani umeamua kuchukua meli tatu na kuja karibu na Tanzania kwa ajili ya kuwajambisha tu , Murhpy amefura huko na kukuona ni mtu ambae hufikirii vizuri , amekushauri lakini hata hukutaka kumsikia”
“Huyo mpuuzi Murphy Stophhillius anachojua ni kutoa ripoti yake ya maneno machache , bosi nadhani unanijua mimi mwenyewee ninavyopenda kuwa muwazi , yaani vijana wangu wameuliwa kikatili lakini yeye anaona kuja hapa kutoa maelezo ni kupoteza muda, isitoshe sijafanya hata mambo makubwa ya kumkosesha heshima , nilizuia vimeli viwili tu vya bidhaa kwa ajili ya kunichukulia siriasi”Aliongea akilalamika.
“Kama ni hivyo vipi umeweza kupata taarifa ya kilichotokea , ijapokuwa The Shark ni kundi la daraja B lakini sio rahisi kulishambulia kwa wepesi na kuuwa watu wote”Aliongea Hamza.
“Bosi ukweli ni kwamba kabla hata hujafika hapa nimeweza kupata viashiria muhimu”
“Viashiria?”
“Ndio , nadhani twende ndani ya Cabin ili tuongee vozuti , halafu pia mke wangu na binti yangu pia wanataka kukutana na wewe , wamekuwa mashabiki zako kwa muda mrefu”aliongea Levithian na kumfanya Hamza kucheka.
“Kwahio ndio maana ukaja mpaka huku nia yako ni kutaka familia yako wanione, ila sio mbaya ngoja nionane na shemeji yangu na mtoto wake”aliongea
Mara baada ya kuona Hamza alikuwa akikaribishwa ndani ya meli hio na Levithian , wanajeshi wa Tanzania waliokuwa kwenye boti waliishia kutulia , hatimae waliweza kuelewa kwanini Mshauri mkuu alitaka Hamza aongozane nao , kama isingekuwa Hamza Goliathi huyo wa baharini asingewaangalia usoni hata kwa sekunde.
“Hivi wamemaanisha nini kwa kumuita Hamza my Prince au isijekuwa Hamza ni mtoto wa mfalme kutoka taifa lingine na hatujui?”Aliongea Afande Caro.
“Tunajuaje , lakini hisia zangu zinaniambia mtu ambae anaweza kufahamiana na mshauri mkuu hawezi kuwa wa kawaida , tunapaswa kumpa heshima yake kwanzia sasa hivi”Aliongea Afande Tito mwanajeshi wa majini alieambatana nao.
“Nishawahi kusikia Levithian anatokea kutoka kwenye umoja flani wa siri lakini taarifa za huo umoja zilizuka mara moja na kupotea, sijui kama bado atakuwa ni mwanachama?”Aliongea Afande Mwiba.
“Hata mimi nishawahi kusikia huo umoja lakini taarifa yake ilikuwa ya siri mno na ni watu wachache katika vitengo yva usalama wanajua juu ya huu umoja , ila nina uhakika Mshauri mkuu atakuwa na taarifa zote”Aliongea Afande Caro.
SEHEMU YA 114.
Australia, Sydney,
Ilikuwa ni usiku wa kiza kinene ndani ya jiji la Sydney katika nchi ya Australia ndani ya bara linalofahamika kwa jina hilo hilo la nchi , katika eneo la makazi karibu kabisa na chuo kikuu cha Sydney , ilionekana gari aina ya Aud A7 ikisimamishwa kando ya nyumba kubwa yenye muonekano wa kifahari.
Mara baada ya gari ile kuzimwa mlango ulifunguliwa na aliweza kuonekana kijana mdogo(Generation Z) wa rangi nyeusi akishusha na kisha akafuatia mwanamke mzungu aliekuwa na nywele za rangi ya kahawia.
Kijana yule aliweka mkono katika kiuno cha mlimbwende yule wa kizungu na kisha walizipiga hatua kuusogelea mlango wa nyumba hio.
“My dear is this where you live , you rented a house ?”Aliuliza yule mlimbwende kwa lugha ya kingereza akimuuliza yule kijana kama sehemu hio ndio anayoishi.
“Haha . hii ni nyumba yangu , niliinunua kipindi flani nyuma huko na hili eneo lote ni la kwangu”Aliongea yule kijana kwa namna ya kujivunia akimjibu yule mwanamke kwa kingereza.
“Jesus , inakuwaje mwanaume wa kiafrika kama wewe kuweza kununua nyumba kubwa kama hii halafu bado ukawa mwanafunzi na gari yako vilevile ni ya kifahari?”Aliongea yule mwanamke akishanga maana haikuwa rahisi kununua nyumba kama hio kwa jiji ghali kama la Sydney.
“Kama umepapenda basi lala usiku wa leo”Aliongea yule kijana akiwa na tabasamu lililojaa hila na yule mwanamke alipendezwa na ukaribisho huo na palepale bila ya kujizuia alianza kumkisi kwa pupa yule kijana huku akisogelea mlango kuingia.
Lakini sasa yule kijana alishutka mara kwani wakati alipotaka kufungua mlango ulifunguliwa kwa ndani na mwanamke na pale macho yake yalichuanua akiwa kama kaona mzimu.
“Mama .. mama usije ukawa…”
“Frank ni mimi mama yako na sio Mzimu , hatimae umerudi”Aliongea Lamla huku akimsogelea Frank na kumkumbatia kwa nguvu.
Kijana huyo alikuwa ni Frank lakini hata hivyo hakuwa akifahamika kwa jina la Frank kwani alibadilisha jina mara baada ya taarifa za familia yake kuuwawa.
Ukweli ni kwamba kabla ya Lamla kufanya mchakato wa kutaka kumuua Regna ili kupora kampuni alianza kuchukua tahadhari ya kumpeleka mtoto wake nje ya nchi kwa Visa ya kimasomo , ilikuwa rahisi sana kutokana na kwamba Balozi wa Tanzania nchini Australia alikuwa akifahamiana nae.
Hata swala la Frank kununua nyumba hio Lamla alikuwa na taarifa na pengine ndio sababu Frank alimkuta mama yake akiwa tayari ndani ya nyumba.
“Mama si nilisikia …nilisoma kwenye taarifa ukitangazwa ume…”Aliongea kwa kubabaika , alikuwa na uhakika mama yake amekwisha kufa na amekuwa yatima ndio maana alimuona kama mzimu.
“Mama yako nipo hai , mama yako nimeokolewa katika mikono ya mateso , nimekuja hapa Australia kwa ajili ya kukutafuta mwanangu ili tuanze maisha pamoja”Aliongea.
“Lakini mama kama serikali ikisikia upo huku si watakuja kukukamata , unadhani Regina na Hamza wanaweza kukuacha uendelee kuishi?”Aliongea kwa wasiwasi.
“Acha wasiwasi , kwanza hawajui hata bado tupo hai , ni stori ndefu sana juu ya kilichotutokea ila kuwa na amani mimi mama yako siwezi kukusababishia matatizo”Aliongea na kisha alimwangalia yule msichana mdogo ambae hakuwa akielewa wanachoongea kutokana na kutumia lugha ya kiswahili.
“Mwambie huyo malaya wako aondoke , uingie ukaonane na mjomba wako”Aliongea
“Nikaonane na mjomba gani?!”Aliuliza kwa mshangao.
“Huyo mwanamke asiondoke” Sauti ya mwanaume ilisikika kutoka ndani.
Muda uleule Saidi alievalia shati la rangi nyeupe na suruali alitoka, alikuwa msafi kasoro tu bado hakupunguza ndevu zake , alikuwa na tabasamu la uovu huku akiwa ameshikilia glasi yenye pombe.
Frank alijikuta akipepesa macho kama vile anajaribu kuoana vizuri , dakika ileile aliweza kumtambua Saidi na jasho lilianza kumtoka.
“Sa.. Saidi?”Uso ulimpauka huku akipiga hatua kurudi nyuma
“Ni wewe muuaji kichaa?” Aliuliza kana kwamba hakuwa akifahamu kweli, Lamla mara baada ya kuona hofu ya mtoto wake haraka sana alimsogelea na kumzua.
“Frank hebu acha wasiwasi na usiongee kwa kuropoka , hebu tuingie ndani kwanza nitakuelezea kinachoendelea”Aliongea
“Mama kuna kipi kingine cha kunielezea ilihali kila kitu kipo wazi huyu ni muuaji… mimi napigia simu polisi”
Frank alikuwa na hofu mno na aligeuka akitaka kukimbia.
Mwanafunzi mwenzake wa kike hakujua hata kinachoendelea kwasababu walikuwa wakongea lugha ya kiswahili , lakini mabadliko ya Frank yalimjulisha kinachoendelea.
“What happened , what are guys talking about, what language is this?”aliuliza kwa kubabaika.
“Hurry up come with me”Aliongea Frank na kumshika yule msichana mkono ili kuondoka nae , lakini kabla hata hawajasogea Sadi alikuwa tayari amesimama mbele yao.
Saidi uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu , lakini hata hivyo tabasamu lake halikuwa lile la urafiki bali lilojaa uovu.
“Ni vizuri ukimsikiliza mama yako na kuingia ndani”Aliongea Saidi kwa sauti nzito.
Frank jasho lilikuwa likimtoka mfululizo , woga uliomvaa kwenye moyo wake ulimlazmisha kupiga hatua bila ya kupenda na kuingia ndani.
Yule mwanamke wa Ki’Australia alijikuta kama kachanganyikiwa asijue nini kinachoendelea na kutaka kuondoka , lakini kabla hata hajapiga hatua Saidi kwa kiganja alimshika sura yake.
Ughh!!”
Mwanamke yule alitaka kupiga kelele na kukimbia lakini alishikiliwa vyema na Saidi na kuvutwa ndani lakini bado aliletea ukinzani na hakupewa tena huruma kwani palepale alipigwa teke la tumbo na kumfanya agugumie maumivu huku akipiga maekele ya chini chini maana amezibwa mdomo.
Saidi wala hakujali na alimshika mkono kwa nguvu na kisha alianza kumvuta kumwingiza ndani kama vile anavuta mzigo
Frank mara baada ya kuona tukio hilo alijikuta akishindwa kujizuia na kutamani kumsaidia yule msichana lakini hakuweza.
“Unataka kumfanya nini?”
“Wewe ulikuwa ukipanga kumfanya nini kumleta nyumbani?”Aluliza Saidi.
“Nili.. nili”
“Ulichopanga kufanya ndio ninachoenda kufanya”
Mara baada ya kuongea hivyo hakujisumbua tena na palepale alishika gauni la yule msichana na kulichana chana na kisha akamwacha uchi na akamuweka begani na kupanda nae juu.
Dakika chache mbele sauti za kilio cha maumivu ziliweza kusikika kutoka kwa yule mwanamke na dakika kumi mbele sauti haikusikika tena.
Saidi alimbaka yule mwanamke akiwa amemkaba shingoni na ilionekana alikosa pumzi wakati wa kitendo hicho na kupoteza maisha palepale.
Frank na mama yake baada ya kupanda juu na kuona tukio hilo alijikuta akianza kutetemeka kiasi cha kujikojolea palepale.
Upande wa Lamla hakuonyesha mshangao zaidi ya kuchukia tu kwa kitendo kile.
Saidi wala hakujali ameua na alisimama kama shetani na kisha aliupiga ule mwili teke.
“Kum**mba mama yako kila siku kwenye meli kumenichosha na nilitaka radha mpya , nakushukuru kwa kumleta huyu mwanamke nyumbani’”Aliongea Saidi.
Bwana mdogo huyo mara baada ya kusikia maneno hayo alijikuta akimwangalia mama yake kwa mshangao.
Lamla uso wake ulikuwa umegubikwa na haya nyingi usoni , ilikuwa ni aibu kwa mtoto wake kusikia maneno hayo lakini hakujua kwanini , lakini baada ya kukumbuka matukio yote kwenye meli mwili wake ulishikwa na muwasho wa kutamani tena.
“Frank mshukuru mjomba wako , mimimama yako nimeweza kuwa ha kwasababu yake , kwanzia sasa nitaishi na wewe hapa na kuanza maisha yetu upya”Aliongea Lamla.
“Yaani unataka kuishi na mimi?”
“Ndio nitaishi na wewe hapa , sitaki tutengane tena”
“Mama umekuwa kichaa , hela nilizobakiwa nazo ni milioni kadhaa tu na sidhani kama zitatutosha wote , kama mnataka kukaa hapa hela mnazo?, halafu tena unaongea hivyo unataka pia niishi na huyu muuaji”Aliongea kwa hasira.
“Usiwe na wasiwasi , Saidi mjomba wako uwezo anao na atajua namna ya kupata hela”
“Hapana nataka kuishi mwenyewe , siwezi kuishi na watu kama nyie , nilikuwa na maisha yangu ya amani hapa lakini mmeniharibia baada ya kujitokeza , kama unanijali mimi kama mtoto wako naomba upotee kwenye maisha yangu”Aliongea kwa uchungu mkubwa na maneno yale yalimfanya Lamla kushikwa na huzuni.
“Frank mimi ni mama yako na nakujali sana na ndio maana nimekuja mpaka hapa kukutafuta , kwanini nikuumize , kwanini nipotee kwenye maisha yako”
“Siwezi kuwa na mama mshenzi na asie na aibu kama wewe , kama unataka kuwa na huyu mhuni ni maisha yako na uhuru wako na usiniingize mimi”Mara baada ya kuongea hivyo , Frank aligeuka ili kukimbia ili asije kujingiza kwenye hali ya hatari kama hio lakini Saidi kama pepo alimsogelea na kumkinga kwa mbele na kitendo kile kilimshutua Lamla.
“Frank!!”
Kitendo kile pia kilimuogoesha Frank kwa kuamini pia anaweza kuuliwa na Saidi hapo hapo, hivyo alitaka kutumia mbinu ya aina yoyote kujiokoa.
Lamla alimsogelea mtoto wake kumkinga na Saidi , lakini Frank alijikuta mbishi na kumsukuma mama yake pembeni ili atoke lakini Saidi alikuwa amekinga njia.
Aliangala pembeni na palepale aliweza kuona mtalimbo wa baseball pembeni na aliuchukua akimpa ishara Saidi kutaka kumpiga nao kama atamgusa.
Baada ya kumtishia aliondoka mlangoni na kukimbilia upande mwingine na kushuka chini kwa haraka ili atoroke kupitia mlango wa nyuma.
Lakini ilitia huruma kwani dakika ambayo anafika chini na Saidi alishamfikia na kumzuia.
“Mama yako ameteseka sana kwa ajili ya kuja kukutana na wewe halafu unachukulia rahisi?”Aliongea Saidi.
“Kama ameokoka kwa ajili yangu kwanini amekuleta hapa?, naomba unipishe nipite”Aliongea kwa hasira huku akimrushia Saidi ule mjeledi kutaka kumpiga nao.
Kitendo kile kilimfanya Saidi kuonyesha ukauzu wa ghafla na aliudaka na kisha akautupa pembeni kwa nguvu na palepale akamshika Frank shingo.
Lamla ambae alikuwa akikimbia kushuka chini , baada ya kuona tukio haraka sana alipiga magoti chini na kuanza kumbembeleza Saidi.
“Saidi tafadhari naomba usimuue , nitakulipa unachotaka ukimuacha hai , Frank ni mtoto mjinga asiejua anafanya ujinga”Aliongea.
Frank na yeye mara baada ya maji kumfika shingoni alianza kuonyesha muonekano wa kuomba kuachwa hai licha ya kwamba hakuwa akipumua vizuri kutokana na kukosa pumzi na alimgeukia mama yake akimuomba amsaidie.
“Mama Sitaki kufa naomba unisaidie”Aliongea
Lamla hakujali tena maneno ya mwanae na palepale alijirusha katika miguu ya Saidi na kuanza kuikumbatia huku kilio kikiwa kikubwa.
“Saidi tafadhari kwa huduma niliokupatia wakati wote naomba umsamehe mtoto wangu , ndio tumaini langu la mwisho lililobakia”Aliongea.
“Kwangu ulikuwa mbwa wa kike niliekuokota na huna haki ya kujadiliana na mimi kwa masharti yoyote”
Mara baada ya kuongea hivyo palepale Saidi alikaza mkono na misuli ya shingo ililegea na Frank alipoteza maisha.
“Frank.Nooooo!!!”
Kilikuwa kilio cha aina yake kwa mwanamke huyo kumshuhudia mwanae akifa mbele ya macho yake.
ITAENDELEA WASILIANA NAMI WATSAPP KWA MAONI NA MWENDELEZO; 0687151346
Kwahiyo shule ndiko wanafundisha jinsi ya kuzielewa hadithi.? Sasa bwamdogo hali hiyo una elimu hiihii ya kipuuzi sasa je ungebahatika kusoma harvard hali ingekuwaje?Duh yaani kama uliikimbia shule nakupa pole maana hii simulizi inahitaji akili kuielewa,huyu mwandishi ni balaa,tumpe maua yake🎉🎉🎉
I think you misunderstood me brother, but why have I studied in the UK if it is an American university because there are no idiots?🤣Kwahiyo shule ndiko wanafundisha jinsi ya kuzielewa hadithi.? Sasa bwamdogo hali hiyo una elimu hiihii ya kipuuzi sasa je ungebahatika kusoma harvard hali ingekuwaje?
Hakuna aliesoma vyuo vya UK akawa na akili za mavi kama weweI think you misunderstood me brother, but why have I studied in the UK if it is an American university because there are no idiots?🤣