Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI:SINGANOJR



SEHEMU YA 115.

Halmashauri ya Giza -Strigoi.

Ndani ya meli mazingira yalikuwa ni yenye kupendeza mno kwa uwepo wa mapambo mengi ya kifahari, huku vito vingi vikiwa ni mkusanyiko wa mabaki mbalimbali ya kale ambayo yailikuwa na thamani kubwa.ikiwemo aina mbalimbali ya ngozi za wanyama adimu.

Muda huo ambao Hamza aliingia aliweza kumuona msichana mdogo kibonge ambae alikuwa akicheza na taji la rangi ya dhababn lililopendezeshwa na madini ya almasi.

Alikuwepo pia mwanamke mrembo mzungu alievalia mavazi ya tamaduni za kikale na kumfanya aonekane ni kama malkia ndani ya ufalme.

“Hatimae nimekutana na wewe , My Prince!”Aliongea yule mwanamke huku akishika gauni lake na kuonyesha heshima kwa kusinyaa.

“Bosi huyu ndio mke wangu , anaitwa Monica na amejiandaa sana kwa siku hii ya kukutana na wewe na unavyomuona hivyo amejipamba kwa nusu siku”Aliongea Levithiani huku akiwa na tabasamu.

“Ngisi hongera sana kwa kuoa mwanamke mrembo kama huyu”Aliongea Hamza huku akitoa kicheko cha dhati.

“Asante sana kwa kunisifia , ukweli ni kwamba kazi yangu kubwa ni uandishi wa habari na navutiwa sana na simulizi zinazohusiana na ulimwengu wa giza.. hususani kuhusu wewe ,licha ya umri wako kuonekana kuwa mdogo lakini unao uzoefu wa miaka mingi , hivyo natamani kupata heshima ya kuandika wasifu wako”Aliongea kwa adabu kubwa huku akijitahidi kuonekana mkarimu.

“Unaonekana kuwa mkarimu san lakini pia sio wa kawaida mpaka kukubali kuolewa na Levithian , kuishi na mjinga kama huyu lazima itakuwa ngumu kwako sana”Aliongea Hamza akitania na kuimfanya Monica kutabasamu.

“Sir naweza kukuuliza swali?”Aliongea Monica huku macho y ake yakiwa na hamu kubwa.

Hamza alitingisha kichwa kumpa nafasi huku akijiambia mwandishi huyo na dada yake Flora wanaonekana kufanana sana kwa vitu vingi.

“Sisi ni kama ndugu hivyo unaweza kuuliza, haina haja ya kuonyesha heshima hivyo”Aliongea Hamza na Monica alitingisha kichwa kukubali.

“Kwa muda mrefu sana nimekuwa na shauku ya kutaka kujua kama unapendelea kuitwa kwa jina lako la msimbo la The Prince KT au unapendelea la Hamza Mzee la sasa?”Aliongea na kumfanya Hamza kushangazwa na swali hilo.

Ukweli ni kwamba alishasahau jina hilo la ufupisho wa msimbo wa KT kwa muda mrefu na kitendo cha kutajwa alijikuta kumbukumbu zikimpeleka mbali.

Upande wa Levithiani aliona Hamza atapandwa hasira , hivyo haraka haraka aliingilia.

“Darling bosi wetu hapendelei kukumbushwa kuhusu maisha yake yalipita hivyo muombe radhi haraka”Levithiani mara baada ya kuongea hivyo, Moninca haraka haraka aliinamisha kichwa chake chini na kuomba radhi.

“Sijawahi kujichukulia kama mtu mkubwa , isitoshe mambo nilioyafanya ni ya kikatili , hakuna cha kujivunia chochote kutoka kwangu”Aliongea Hamza.

“Hupaswi kuongea hivyo , kama sio kujitokeza kwako kipindi kile, pengine rasilimali zote za ulimwengu ambazo zilikuwa chini ya nguvu ya mashirika ya siri zisingeweza kuwa huru kama ilivyo leo, ukiangalia kwa miaka hii mitatu uliopotea , kuna makundi mengi ya ulimwengu wa giza ambayo yamejichipua , sidhani kama yangejitokeza chini ya uangalizi wako”Aliongea Minica kwa maneno ya dhati kabisa na kumfanya Hamza kutabasamu.

“Hivi kumbe nimefanya mambo mengi namna hio? Mbona najihisi kama muuaji niliestaafu”Aliongea Hamza huku akicheka kivivu.

“Bosi nadhani tuachane na hii mada kwanza , kutana kwanza na mtoto wangu Debbie .. haha mwangalie anavyofanana na mimi”Aliongea levithian wakati huo akimbeba msichana aliekuwa akicheza na kumpeleka mbele ya Hamza ambae alinyoosha mkono wake na kushika mashavu yake.

“Hamfananani kabisa , mngefanana asingekuwa mrembo namna hii , halafu ningejua mke wako na mtoto wapo huku ningeandaa zawadi ya kuja nayo”

“Bosi sina ninachokosa hapa , zawadi ya nini tena , kwangu mimi kuwapa nafasi mke wangu na mtoto wangu kukuona ni zawadi tosha”Aliongea huku akicheka.

Hamza alimchukua Debbie kwenye mikono yake na kisha alimkiss kwenye mashavu na kufanya katoto hako kuishia kutoa tabasamu la furaha.

Alimwangalia machoni na alijikuta hali ya joto ikiujaza moyo wake, mtoto huyo kwa namna ambavyo alikuwa mzuri na yeye pia alitamani kuwa na wa kwake.

Ijapokuwa Monica alitamani sana kufanya mahojiano na Hamza lakini alizuiwa na Levithian, kikawaida angemsaidia mke wake ili kufanya mahojiano na Hamza lakini hata hivyo angemsapoti kwa kila kitu lakini likija swala linalohusiana na Hamza alikuwa mkali sana.

Levithiani alijua Hamza hakupendelea maswala yake kuzungumziwa hadharani, kwani licha kwa wengine inaweza kuwa simulizi ya kufurahisha kusikia na ya kishujaa , lakini kwa upande wa Hamza ni simulizi iliojaa maumivu.

“Levithian umesema kuna kitu umegundua , ni kitu gani?”Aliuliza Hamza, aliekaa kwenye sofa akivuta sigara ambayo amepewa na Levithiani.

“Bosi , nimeweza kumuokoa mmoja ya maharamia wa The Shark , ndio aliekuwa na bahati ya kuwa hai baada ya kujirusha majini akiwa na gogo ambalo limemfanya kuelea kwa muda mrefu”Aliongea na muda mfupi mwanaume ambae alionekana kuwa na hali mbaya kutokana na kuungua na jua mwili mzima pamoja na vidonda aliletwa mbele ya Hamza na kupigishwa magoti.

“Mkuu Leviathani!!”Aliongea huku akitetemeka.

“Rudia kuelezea kila kitu ulichoshuhudia siku hio”Aliongea na bwana huyo hakupinga na alianza kuelezea tukio la boti ya uvuvi kusogelea meli yao na mtu wa ajabu ambae mwili wake unaweza kujiponya alivyowashambulia na kuuwa kila mtu ..

Hamza mara baada ya kusikia hivyo , sura yake ilijikunja na alionekana kuwa katika tafakari ya kina.

“Bosi , unadhani wanaweza kuwa watu kutokea Strigoi?”Aliuliza Leviathani.

“Watu wa Halmashauri ya Giza hawana uadui wowote na sisi , tena mara nyingi wanatamani kuwa na urafiki na sisi , kama kweli walikuwa ni Strigoi na wameona chata la Ngisi kwenye bendera,wasingeshambulia”Aliongea Hamza.

“Kama ni hivyo ni binadamu gani amewaua ambae anaweza kupona baada ya kushambuliwa na risasi?”

Hamza macho yake yalisinyaa na palepale alionekana kama mtu alieshikwa na wasiwasi kwenye macho yake kwa namna ya kutambua kinachoendelea.

“Inawezekana ikawa ni Biochemical regeneration technology..”Aliongea Hamza akimaanisha inaweza kuwa teknolojia ya kibailojia ya kujiponyesha.

*****

Giza nene lilikuwa limekwisha kutanda wakati Hamza alipoweza kutoka nje ya meli ile , Levithiani alitaka kuagiza watu wake kumrudisha Hamza nchi kavu lakini aliwaambia haina haja kutokana na sababu zake, hivyo kimya kimya alirudi kwenye speedboat aliowaacha wenzake.

Afande Caro na wengine wote mara baada ya kumuona Hamza akirudi , walitamani kujua kile kilichokuwa kimetokea kwenye meli hio.

Hamza alichoishia kuwaambia ni kwamba swala hilo lishapatiwa ufumbuzi na maharamia hao wa Sea Demons wataondoka hapo na kuachia baadhi ya meli walizokuwa wameshikilia na mizigo yake yote pamoja na hela kwa jeshi la Tanzania.

Mara baada ya kuonega hivyo kila mmoja alijawa na ahueni kubwa lakini hata hivyo walibakiwa na shauku ya kutaka kujua ubini halisi wa Hamza mpaka kuheshimika kwa watu hao , lakini wasingemuuliza hivyo na kimya kimya waliweza kurudi nchi kavu.

Hamza wakati anakanyaga ardhi kavu ilikuwa ni usiku kabisa na alijaribu kumpigia Dina ili kumuuliza kama yupo Kijichi lakini Dina alimwambia atakuwa nje ya mji kwa siku kadhaa.

Hamza alipata ahueni , isitoshe licha ya kutaka kutimiza ahadi kwa mrembo huyo , lakini vilevile alikuwa na mpango wa kwenda kumpeti peti Regina mpaka apunguze hasira maana hawakuachana katika hali ya amani, hivyo baada ya taarifa hio moja kwa moja alirudi nyumbani.

Baada ya kuingia ndani aliweza kugundua taa za chumba cha kujisomea cha Regina zilikuwa zinawaka na ilimfanya kusogelea mlango na kujaribu kugonga lakini hakuweza kusikia jibu .

Alijaribu kushika kitasa cha mlango na kusukuma na mlango ulionekana haukuwa umefungwa , hivyo aliusukuma polepole na kuingia ndani na hapo ndio aliweza kugundua Regina alikuwa amelalia meza akiwa amejifunika koti na alikuwa usingizini.

Hamza alipiga hatua kusogelea meza hio na kuona tarakishi ilikuwa inawaka na kuna nyaraka iliosomwa nusu iliokuwa ni Ripoti ya Survey katika soko la Ulaya.

Hamza aliona kumuacha mrembo huyu kuendelea kulala hapo sio vizuri, isitoshe muda ulikuwa umeenda hivyo bila kumuamsha aliamua kumbeba lakini kitendo cha kutaka kumsogelea tu, Regina aliinua kichwa chake na kumwangalia na macho yake ya kirembo yaliokuwa na usingizi.

“Umerudi?”Aliuliza.

Hamza alijikuta akishangaa baada ya kusikia suati hio, haikuwa na hasira kama alivyotegemea wala ilivyokuwa wakati wa mchana.

“Ndio , sorry kwa kukuamsha?”Aliongea.

“Sikuwa nimelala , nimejipumzisha tu..”Aliongea na Mmuda huo alionekana kushituka ghafla na kumfanya Hamza kushangaa.

“Mbona umeshituka , nini kimetokea?”

“Nimedondosha Contact lens yangu?”Aliongea.

“Kumbe unashida ya macho?”

“Acha kujifanyisha hujui basi, inamaana hujawahi kuona macho yangu yana utofauti kutokana na kuvaa lenzi?”

“Kwahio hapo huoni kabisa nikusaidie kuitafuta?”

“Sijasema mimi ni kipofu”Aliongea huku akiokota kilenzi kidogo kwenye nyaraka na kisha alivuta droo na kutoa kikopo cha dawa na kutoa vidonge kadhaa na kumeza, baada ya hapo alirudisha ile lenzi kwenye jicho lake la kushoto na kisha kupepesa macho mara mbili ikionekana imekaa sawa.

Hamza alishindwa kujizuia kutokutabasamu, hakujua kwanini lakini mara baada ya mrembo huyo kumaliza kuweka lenzi hio na kupepesa macho aliona muonekano huo ulivutia zaidi.

“Inakuwaje ukaweka kirahisi namna hio?”Aliuliza Hamza , ukweli hata yeye hakuelewa maana kama ni kuweka angalau angehitaji kioo lakini kwa Regina ilibandikwa haraka haraka.

“Macho yangu ni makubwa ndio maana , nakumbuka wakati nasoma wanafunzi wenzangu wa kike walikuwa wakiyaonea wivu macho yangu”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kuelewa na kujiambia ni kweli kabisa walikuwa na haki ya kumuonea wivu , maana yalikuwa yameendana na muundo wa sura yake kwa asilimia mia moja.

“Wewe ulifikiri wataachaje kuona wivu , kwa urembo uliokuwa nao nadhani wanaume wote walikuwa wanakwangalia wewe tu”

“Hebu acha kunisifia huko , niambie kwanza kama swala limeisha?”

“Litakuwa limeisha na usiwe na wasiwasi , hata kama ikitokea mtu akija tena , nitaenda kushughulikia”Aliongea Hamza na Regina na hakuuliza amelishughulikia vipi.

“Nahisi miguu yangu kukakamaa , kama huna usingizi unaonaje tukienda kutembea tembea huko nje kidogo?”

Hamza mara baada ya kuambiwa hivyo hakutaka kabisa kukataa na kwa haraka haraka , alikubali huku akijiambia itakuwa wasaa mzuri wa kuongeza ukaribu wake na Regina.

Wawili hao kwa pamoja walitoka nje ya geti ya nyumba , hakukuwa na baridi sana hivyo waliweza kutembea pembezoni mwa barabara iliokuwa na mwanga wa taa za sola na kutokana na upepo wa baharini ilimfanya Regina kujisikia vizuri.

Wakati wakiwa wanatembea Hamza aliona kuna kitu kilichokosekana, alimwangalia Regina aliekuwa pembeni yake na kisha akaangalia mikono yake na kushikwa na tamaa ya kuishika.

Lakini sasa baada ya kukumbuka alivyomkasirisha, alipatwa na hali ya kusita kwa kudhania anaweza kuyaanzisha tena.

Baada ya kufikiria zaidi ya mara mbili aliona haina haja ya kuwaza sana na kujiambia siku zote yeye ndio anaepaswa kuanzisha mashambulizi kama mwanaume , kwa namna isiokuwa ikielezeka hata yeye alishangaa likija swala la Regina alipatwa na hofu kubwa na hakujua ni kwanini.

Baada ya kutembea kwa umbali mrefu kama kilomita moja hivi , Regina aligeuka na kumwangalia.

“Mbona huongei chochote , ninavyokujua ni muoingeaji na sio mkimya?”Aliuliza Regina na kumfanya Hamza kutabasamu.

“Ni kwasababu sijui cha kuongea”

“Oh..”Regina aliishia kutingisha kichwa na hakuuliza zaidi na kuendelea kutembea.

Hamza aliishia kujidharau kwenye moyo wake kwa kujiambia alipaswa kuendeleza topiki hapo hapo na sio kuikatisha , pengine kutumia muda huo kuomba msamaha, swala la Anna lilikuwa la kukurupuka kwa upande wake na aliona alipaswa kuyamaliza na Regina kwa kuomba kusamehewa.

Wakati akiwaza nini cha kuongea , dakika hio hio mvua nayo ambayo haikuweleweka imetokea wapi ilianza kunyesha kwa kasi.

“Turudi zetu , naona ishaanza kunyesha”Aliongea Regina huku akikunja sura.

Hamza aliona umbali mpaka wafike nyumbani ni mrefu , hivyo bila ya kufikiria mara mbilimbili alivua koti lake la suti na kumfunika kichwa,Regina alishangaa mara ya kwanza na bila ya kupenda alimwangalia Hamza usoni.

“Unafanya nini?”

“Nafanya hivi ili usinyeshewe kichwani”

“Utaloana sasa shati lako ni jepesi na nimevaa koti pia”

“Mvua kidogo sana hii haiwezi kuniloanisha”Aliongea Hamza na Regina alichojisikia moyoni kilikuwa cha tofauti , hakuwahi kuwa cared namna hio hapo kabla.

Upande wa Hamza alikuwa mbishi na alipanua mikono yake na kumkinga Regina asinyeshewe na mvua , Regina alishikwa na wimbi la hisia za ajabu kwenye moyo wake na aliishia kutokumzuia.

Wawili hao walijikuta wakiongeza spidi kurudi , lakini mvua ilizidi kuwa kubwa.

“Wife kwa staili hii tutafika tumeloana kabisa , unaonaje nikikuweka mgongoni ili iwe haraka”

“Kwani nikiloana kuna shida gani? , mimi sio katope”Aliongea Regina

“Ninachomaanisha sio wewe kuloa bali kuwahi kurudi kabla haijazidi kuwa kubwa”

“Kama unataka nikimbie nakimbia basi”Aliongea na palepale alianza kukimbnia kurudi uelekeo wa nyumbani.

Alikuwa amevalia visendo na kadri vilivyokuwa vikiloa maji machafu ya barabara ndio miguu yake ilivyoanza kuteleza na ilikuwa ni kama Hamza alivyowaza atate;eza kwani ile anaruka shimo katika barabara alijikuta akiteleza na kupiga kelele , lakini sekunde ambayo alijua anakwenda kudondoka , hatimae mikono yenye nguvu ilimshikilia.

Maji ya mvua yalishuka kutoka katika nywele ndefu za Hamza na kumwagikia usoni.

“Acha kuwa mbishi, kwa majukumu ulionayo unapaswa kulinda afya yako”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu hafifu na baada ya kuongea hivyo hakujali ubishi wa Regina tena kwani palepale alimbeba na kukimbia nae kurudi nyumbani.

Regina hata hakujua nini kilichotokea , kwani mvua ilikuwa ikimnyeshea na kulikuwa na baridi lakini alikuwa akihisi joto ambalo halikuwa likielezeka.

Dakika chache tu wote waliweza kufika nyumbani na Hamza aliingia chumba cha wageni na kutoka na mataulo mawili na moja kumpatia Regina ajifute.

“Kama ningejua itanyeshe ningechukua mwamvuli”Aliongea Hamza.

Regina sura yake iliishia kushikwa na haya na hakuongea chochote na kufanya eneo hilo la sebuleni kuwa kimya na hali kutokuwa ya kawaida.

“Regina si unaenda kuoga na kisha upumzike?”Aliuliza Hamza na Regina ndio alikumbuka muda ulikuwa umeenda sana.

“Ndio , mimi natangulia kwenda juu,usiku mwema”Aliongea na kisha kuanza kuzikwea ngazi kwenda juu.

“Regina Am sorry”Aliongea Hamza kwa sauti ya chini na kumfanya Regina kusimama na kugeuka nyuma.

“Kuhusu nini?”

“Kuna lingine lipi zaidi ya lile swala la mimi na Anna”Aliongea Hamza.

“Natamani kukwambia uachane nao wote , ila haiwezekani na pia sijali,siku nyingine kuwa tu makini”Aliongea na kumfanya Hamza asielewe Regina anmaanaisha nini kusema hajali na siku nyingine awe makini, lakini kwa namna alivyoongea Regina kidogo alipatwa na ahueni.

“Wife kwahio huna hasira tena na mimi?”Aliuliza.

“Ukiendelea kuongea ujinga nitakuwa na hasira kweli”

As you command”Aliongea Hamza kwa lugha ya kingereza na Regina mara baada ya kumwangalia alivyo mdogo mbele yake midomo iliishia kumcheza.

“Anna na wenzake nimekubali kuwaajiri kutokana na usalama wa kampuni , usije ukadhani nimekubaliana na wewe kwa ajili yako”Aliongea Regina.

“Ndio ,sitofikiria hivyo”Aliongea Hamza huku sauti yake ikionyesha alikuwa na hofu asije kuongea kauli yenye utata maana kiswahili chake mara nyingi kiliishia kumkasirisha mwanamke huyo.

Regina licha ya kusikia hivyo aliamini kabisa Hamza atafanya kosa hilo tena , maana maneno yake ni kama hayakuwa ya dhati.

Kwa sababu zisizoeleweka alijikuta akichukia , alijua Hamza alikuwa amezoea maisha ya kuwa huru katika eneo hilo , lakini aliona kama asipomuwekea ngumu kidogo itakuwa ni simulizi ya kufikirika.

Aliishia tu kukubali huku akizingatia maneno ya mwisho ya bibi yake , akimwambia kwamba kama anataka kuwa na mtu kama Hamza basi akubali hawezi kuwa kama wanaume wa kawaida.

Isitoshe aliona Hamza ni mtu ambae anafanya vitu ambavyo mwanaume wa kawaida hawezi kufanya , hivyo aliona ni sawa tu na ule msemo wa ukipata huku unapoteza kule.

Lakini muda huo hakuacha kufikiria namna ambavyo Hamza alionekana kuwa mwepesi mbele ya wanawauke na hata kulala nao baada tu ya kukutana , kufikiria tu hivyo aliona hata swala la wao kuwa mume na mke lilikuwa linashangaza na mtu wa nje pengine angeona ni kituko juu ya kile kinachoendelea.

Anyway , vyovyote vile ni juu yako”Aliongea Regina na kisha alipandisha juu kuingia kwenye chumba chake.

Hamza aliishia kujikuna nywele zake zilizoloa na kujiuliza imekuwaje huyu mwanamke anabadilika badilika ,asubuhi alionekana kukasirika kutokana na kuwa na mwanamke mwingine lakini dakika hio ni kama alikuwa akimruhusu kufanya anavyojisikia ila tu awe makini.

Hamza hakuelewa kabisa ni kitu gani alichokuwa akifikiria Regina, lakini hakutaka kulipa kipaumbele sana na palepale alitembea na kurudi kwenye chumba chake.

Baaada ya kutoka bafuni wakati akijiandaa kulala muda ule alikumbuka ule muamala wa kiasi kidogo cha pesa ulioingia katika akaunti yake ya simu na palepale mawazo ya swala la Mzee yaliibuka.

Ukweli ni kwamba licha ya mpango wake tokea mwanzo ni kumfahamu Mzee lakini aliona ni kama anachukua muda mrefu kufanikisha hilo kutokana na kudili na mambo mengi ambayo hayahusiani na misheni yake.

Hamza alitaka kutumia ule mshumaa , lakini bado alikuwa akisita kuutumia kutokana na kukosa maelezo ya kina , licha ya kwamba Frida alimshauri kuutumia , lakini bado hakuwa akiamini watu kirahisi mpaka kuchukua hatua.

Kwa namna moja ama nyingine alijiambia anao uwezekano wa kukutana na Mzee tu na kuhusu swala la kumiliki kumbukumbu zake kupitia ndoto, hakutaka pia kulifikiria sana na kuijiambia ikitokea jambo hilo kuwa kweli atalikabali.



















SEHEMU YA 116.

Siku iliofuata Hamza alienda kazini na wakati akiwa ndani ya ofisi yake Anna alieambatana na Mima , Yonesi pamoja na wenzake wote waliingia katika ofisi yake.

“Hamza asante sana , tumesikia ulivyoyatibua kuhusiana na swala letu”Aliongea Anna na ilionekana kila mmoja alikuwa ameguswa na kile Hamza alichofanya.

“Sisi wote ni wafanyakazi wa kampuni moja , hivyo lazima nifanye kile ambacho nimewaahidi .hakuna haja ya kuwa hivyo mbele yangu”Aliongea Hamza na kumfanya Anna kulainisha lipsi zake na mate na kisha akamwangalia kimapozi.

“Kama utakuwa na shida yoyote hakikisha unaniambia”

Hamza mara baada ya kusikia sentensi hio , aliweza kuelewa mwanamke huyo ni kitu gani alichokuwa akimaanisha, lakini hakuwa na mpango tena wa kumgusa Anna hapo baadae , mpango wake wa kuwa na ukaribu wa zaidi na wanajeshi hao aliuweka pembeni kwanza kwasababu ya Regina.

Mara baada ya walinzi hao wa kampuni kutoka , simu ya Hamza ilianza kuita na alivyoangalia aliekuwa akipiga aligundua ni Irene.

Hakuwa ameongea na msichana huyo kwa muda kidogo tokea tukio la kulala nae hotelini na asubuhi kuja kuchukuliwa na baba yake.

“Hey! wewe mtoto hujaenda shule tu?”Aliongea Hamza mara tu baada yqa kupokea.

“Swali gani hilo sasa Hamza , hata salamu hakuna unaniita mtoto?” Sauti ya kulalamika upande wa pili ilisikika.

“Ulitaka niulize swali gani ilihali wewe ni mwanafunzi, haya niambie uko poa?”

“Niko poa , ila nina shida?”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura na kujiambia isije huyo mrembo mchanga anamwandalia mtego tena.

“Baba yako anavyokupenda , una shida gani?”

“Nimepata leo leseni yangu ya udereva, nataka unisindikize nikanunue gari”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura kidogo.

“Baba yako amekuruhusu kununua gari?”Aliuliza.

“Hehe..baba nilimuomba mwanzo hela akakataa, ila juzi tu kaja na furaha na kunipa hela nikanunue ninalotaka. Leo asubuhi nimegundua majibu ya vipimo vya DNA yametoka na kunikuta ni mtoto wake”Aliongea na namna ambavyo Hamza alisikia sauti hio alitamani kucheka.

Ilionekana baada ya baba yake Irene kusalitiwa mara kibao na mke wake aliamua kwenda kupima vina saba vya damu na kugundua Irene alikuwa mtoto wake , hata Hamza aliona mzee huyo anapaswa kuwa na furaha baada ya wasiwasi kumtoka.

Lakini kilichomchekesha ni namna ambavyo sauti ya Irene ilikuwa ikisikika.

“Hamza kubali basi , nataka nikamkomoe kwa kunidhania mimi sio damu yake wakati tunafanana vitu vingi”Aliongea kwa kubembeleza.

“Wewe bado mwanafunzi , gari unayotaka ni ya nini?”Aliuliza Hamza.

“Wewe hayakuhusu , kama unanipeleka nipeleke kama hutaki basi”Aliongea kibabe.

“Sitaki”

“Jamani Hamza mbona upo hivyo wewe kila siku?, kama unamuogopa Regina mkeo useme?”

“Wewe umejuaje Regina ni mke wangu?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.

“Baba kaniambia, kasema Regina ni mzuri na ana hela kuliko wewe hivyo unamuogopa asije kukuacha, inaonekana kila alichosema baba ni kweli, unamuogopa ATM?”

“ATM!?”Hamza alijikuta akikuna kichwa chake huku akikunja sura na kutoa tabasamu lililojaa kejeli , ilionekana alikuwa akijaribiwa ili kumtoa kwenye msimamo wake.

“Ndio ATM yako ya hela si Regina”Aliongea na kumfanya Hamza asijue namna gani amjibu , lakini muda uleule alimuona Aroni akiingia ndani ya ofisi yake na alijua lazima kuna swala lililomleta hivyo alihold simu ya Irene.

“Bro upo tayari?”Aliongea Aron mara baada ya kumuona Hamza ametoa simu sikioni.

“Tayari na nini bro?”

“Kwenda Tour , kila mtu ashajiandaa na wapo tayari kwa kuondoka”Aliongea Aroni na kumfanya Hamza macho kumtoka na kugeukia karatasi aliopewa na Regina inayohusiana na Tour hio ambayo ameitupa pembeni.

Alijikuta akitamani kucheka maana alikuwa amesahau kabisa kuhusu swala hilo ni siku hio.

“Japo hata sijajiandaa , ila twende zetu”Aliongea Hamza na kisha alikimbia kwenda kwenye ofisi ya Regina kwa ajili ya kumuaga kama anaondoka , lakini aliambiwa na Linda, Regina katoka kwenda kwenye kikao hivyo aliishia kutuma ujumbe pekee.

Kila baada ya nusu mwaka kampuni ya Dosam inao utaratibu wa kutoa majina ya baadhi ya wafanyakazi ambao wanaenda Tour kutoka katika matawi yote na baadhi ya wanaofanya kazi makao makuu.

Moja ya sababnu kubwa ya safari hii ya kitalii ni kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa baina ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi mzuri zaidi wa utendaji katika kampuni , asilimia kubwa ya kampuni nyingi zina utaratibu wa kuwalipia wafanyakazi wao gharama zote za usafiri na maradhi kwa ajili ya safari ya kimatembezi kama hio.

Lakini sio hivyo tu pia inawapa motisha wafanyakazi kufanya kazi kwa juhudi ili kila awamu inayofika waweze kupata bahati ya kuwa moja ya wafanyakazi wanaosafiri.

Jambo la kufurahisha ni kwamba , kutokana na asilimia kubwa ya wafanyakazi wa kampuni ya Dosam kuwa wanawake , kwa wanaume wachache ambao wanakuwa katika safari hio walikuwa wakifurahia sana , maana asilimia kubwa ya wanawake walikuwa ni warembo.

Katika awamu hio ya kusafiri Dosam Bank ndio walioshinda nafasi ya kuchagua ni wapi Tour hio ifanyikie na walichagua Wilayani Lushoto mkoani Tanga , huku sababu kubwa ilikuwa ni kutaka kwenda kuona kilele cha Mlima Joto katika safu za milima ya Usambara.

Utalii wa Kwenda Mlima Joto ulikuwa moja ya utalii maarufu sana kwa siku za hivi karibuni , moja ya umaarufu wake ni kutokana na kwamba, Mlima unaopatikana katika Wilaya ya Mlalo , kijiji cha Kisange ulikuwa ukipandisha joto kila nyakati za usiku bila kujalisha mvua ilikuwa ikinyesha ama haikuwa ikinyesha.

Mwanzoni wananchi wa kata hio mara baada ya kugundua eneo hilo kupandisha joto nyakati za usiku walishikwa na hofu kwa kudhania ni Volcano inachemka , lakini Serikali ilituma watalaamu kufika ndani ya hilo eneo ili kupima kama hali hio ya kilele kupata moto ilikuwa ikisababishwa na Volcano.

Baada ya utafiti wa kina ulioongozwa na Profesa George Adrin kutoka chuo Kikuu cha SUA kwa kushirikiana na wanafunzi wa chuo cha Bristol Uingereza walikamilisha utafiti wao na kutoa majibu eneo hilo kupandisha joto kwake hakusababishwa na mlipuko wa Volcano bali ni mchakato wa kijilojia unaofahamika kitaalamu kama Radiative cooling, wakaelezea kwa kumaanisha kwamba eneo hilo kutokana na kilele chake kuwa na mawe mengi , nyakati za usiku mawe hayo yanapoa na kusababisha eneo hilo kuwa na hali joto.

Sasa kutokana na hali hio ya kijio;ojia kampuni kubwa ya African Maple inayojihusisha na biashara za mahoteli iliona ni fursa na kujenga hoteli ya kitalii pembezoni mwa mlima huo na kuwapa watalii nafasi ya kufanya Hiking na Camping juu ya kilele hicho na kufurahia mandhari nzuri ya misitu ya asili, huku wengine wakilitumia eneo hilo kiimani zaidi, wakiamini ni joto linaloondoa nuksi.

Sasa hapo ndio wafanyakazi wa benki ya Dosam walichagua kwa ajili ya kwenda kutembelea katika trip hio.

Hamza mwanzoni hakuvutiwa na safari hio kabisa , lakini mara baada ya kuingia kwenye basi la kisasa la kampuni alijiambia hakika Regina alikuwa akimpenda kwa kupendekeza kusafiri kwenda Tour na wanawake warembo namna hio.

“Mambo Hamza!”

“Hamza njoo ukae hapa jamani”

“Jamani Hamza wewe ni Handsome”

Wafanyakazi kibao ndani ya basi hilo hasa wa kike walianza kumsalimia Hamza kwa bashasha huku wengi wakimwangalia kwa macho ya mitego kwa kuyalegeza.

Hamza alikuwa mtanashati sana na mwili wake umejengekea kimazoezi huku akiwa ameenda hewani , jambo ambalo lilifanya kuwa ugonjwa wa wanawake wengi , kuchanganya rangi ilikuwa sifa ya ziada kwa wanawake kutamani tu kumzalia, lakini hilo halikuwa kubwa ambalo lilimpatia sifa na umaarufu, moja wapo ya swala lililompa umaarufu ni tukio la kushinda Tuzo katika mashindano ya Basketball.

Hamza alikuwa maarufu kwanzia ngazi ya kampuni Tanzu mpaka makao makuu na ndio maana wengi wa wafanyakazi walikuwa wakimfahamu.

“Bro unashobokewa sio poa, usipoangalia utawala wote ndani ya hili basis”Aliongea Aroni huku akijitahidi kutembelea nyota ya Hamza.

Hamza aliishia kutoa tabasamu , ukweli hakuamini kampuni ilikuwa na wanawake warembo namna hio.

Muda huo Hamza alipewa taarifa na Aroni kwamba kwasababu yeye alikuwa akienda kwa niaba ya Regina basi ndio kiongozi wa msafara wa wafanyakazi hao zaidi ya mia nne, hivyo alipanda cheo ghafla pia.

Kwa jinsi alivyokuwa akishobokewa na Warembo alijihisi ni kama vile anaogelea angani na hakuna wa kumshusha na hata kama akitokea malaika angemkatalia.

Baada ya kusalimiana na kila mtu , hatimae alienda zake na kukaa mbele kabisa , lakini ni muda huo aligundua siti ambayo iliachwa kwa ajili yake pembeni alikuwepo kapteni Yonesi.

“Kapteni.. ah! sorry namaanisha Mkuu wa idara, kwanini na wewe upo hapa?”Aliuliza Hamza.

Yonesi tofauti na wafanyakazi wengine wa kike ni yeye pekee aliemwangalia Hamza kwa macho ya ukauzu ,ilikuwa ni kama vile hakupenda namna ambavyo alikuwa akishobokewa.

“Mimi pia ni kiongozi wa huu msafara, wewe ni kiongozi wa wanaume na mimi ni kiongozi wa wanawake , hujaelewashwa kuhusu hili?”Aliongea kikauzu.

“Mimi sikujua bwana , nilijua mimi ni kiongozi wa wote, ila huu utaratibu unanifanya niamini imeandikwa kabisa kwenye vitabu tukutane, tumeanza kula pamoja na sasa tunaenda Tour pamoja”Aliongea

“Wewe ndio ulijipendekeza kuja kwenye meza yangu na sio kuandikwa, sawa?”Aliongea huku akiishia kujisikitikia kwa ndani maana hakuwahi kukutana na mwanaume asie na aibu kama Hamza.

“Naona ulivyojaa sifa kwa ulivyokuwa ukisalimiana na hao warembo huko nyuma , kwanini usiende ukakae nao kabisa?”

“Yonesi mbona nahisi kama unaona wivu?”

“Kichaa wewe, sitaki kuongea na wewe mimi”Aliongea na kisha aligeuzia sura yake upande wa dirishani huku akihisi ni kama joto lishaanza kumvaa.

Hamza hakujali hata hivyo maana kulikuwa na warembo kibao waliokuwa wakitaka kuongea nae , hivyo alijikuta akiwa bize mwenyewe safari nzima.

Kutoka Dar es salaam mpaka Tanga Wilaya ya Lushoto iliwachukua zaidi ya masaa sita na mawili kwenda Mlalo.

Safari ilikuwa ya kuchosha sana kwa Hamza lakini kwa upande wa wafanyakazi wenzake , kila mmoja alionekana kufurahi mno na wengi walipiga picha katika vituo walivyosimama kwa ajili ya chakula na mambo mengine.

Hamza alikuwa bize kweli kupiga picha na warembo na kuwachekesha , upande wa Yonesi alikuwa kimya huku akiwa amevaa Earpods zake akionekana hakutaka kabisa usumbufu.

Walifikia kwanza hotelini na kisha baadhi yao waliotaka kwenda kulala kwenye mehema katika Kilele cha joto walianza safari na asilimia kubwa walielekea huko.

“Mbona hakuna watu kabisa ndani ya hili eneo ?”Waliuliza baadhi ya wafanyakazi maana mpaka katika geti la kuingilia msituni kupanda mlima mlinzi hakuonekana.

“Naona hata walinzi hakuna , tunalipaje hapa?” waliendelea kuuliza.

“Acheni ujinga , kwani hamjui kampuni imlipia kila kitu kwa ajili yenu?, gharama za hoteli ni mpaka huku”Aliongea Yonesi kibabe kama kawaida yake.

Kundi hilo la wafanyakazi waliishia kuelewa na hakuna ambae alijali tena kwanzia hapo na ilileta mantiki hata hivyo.

Kutokana na kuwa na furaha kubwa , wengi walipiga picha mbalimbali katika mandhari hayo ya kuvutia , muwekezaji wa eneo hilo alikuwa amefanya kazi kubwa mno ya kulipendezesha na likawa la kitalii kweli.

Hamza mara baada ya kuona Yonesi anazubaa zubaa alimvutia kwake na kuanza kupiga nae Selfie.

“Yonesi hujaja huku kufanya kazi bali kula bata , hebu acha kutukasirikia bwana na jilegeze”Aliongea Hamza baada ya kuona picha alizopiga nazo hakuna hata moja ambayo Yonesi alikuwa akicheka.

“Inakuhusu nini , kama unataka mtu wa kucheka cheka , piga na wengine”

Mara baada ya kuongea hivyo aliungana na kundi lingine la mbele walioanza safari ya kupanda kileleni kwenda kuonja joto la Mlima , hakuna ambae alikuwa na mpango wa kulala hotelini , wengi walitaka kwenda kulala katika kilele hicho katika mahema ili kutoa nuksi kama walivyosikia tetesi ya nguvu ya eneo hilo.

Hamza aliishia kutoa tabasamu tu lakini hata hivyo hakuwa na haraka sana , hivyo taratibu taratibu alianza na yeye kuanza safari ya kwenda juu ya mlima na wanawake wengine na baadhi ya wanaume.

Ilikuwa ni Tour ya siku tatu tu , hivyo usiku huo wangelala katika mlima huo na kesho jioni wangeanza safari ya kwenda kutalii eneo lingine na kisha kuanza safari ya kurudi.

Baaada ya kupandisha katika kilima hicho kwa lisaa kama moja hivi , wengi wao walianza kuchoka na kupumua na midomo.

Mara baada ya kuona Yonesi na Hamza hawakuwa na dalili kabisa za kuchoka walishangaa na kuwakubali kwa wakati mmoja .

Yonesi mwenyewe alijishangaa , ijapokuwa alikuwa mtu wa mazoezi lakini hakwa hivyo zamani , kwa umbali aliopanda lazima angekuwa na dalili za kuchoka lakini matokeo yake ni kama alikuwa akitembea kwenye tambarare.

Baada ya kufikiria kwa umakini alijua lazima ni mbinu ambayo Hamza amemfundisha na kuifanyia mazoezi kila siku , kutokana na hilo alijikuta akimpenda Hamza na kumchukia kwa wakati mmoja . alimuona ni mtu mwenye uwezo sana lakini anafanya vitendo ambavyo vinamfanya amchukie.

Kipande cha mwisho kuelekea eneo hilo la Joto hapakuwa mbali sana na ilihitajika kutembea kwa kuzunguka.

Baada ya kutembea taratibu walijikuta wakigeuza macho yao nyuma na kuangalia upande wa chini na waliweza kuona vilele vingi vya milima katika eneo hilo , lakini pia bonde lililokuwa chini yao liliwaogopesha na wengine mara baada ya kuona wanazidi kwenda juu walianza kushikwa na hofu.

Lakini sasa wakati huo wakipiga kelele za malalamishi ya kuchoka , tukio la ajabu lilitokea.

Zilikuwa ni sauti za kuporomoka kwa mawe kutoka juu kwenda chini yalioambatana na mchanga , mawe hayo yalikuwa spidi sana kutokana na mteremko mkali.

“Ni mmomonyoko?!”Walijikuta wakishangaa maana hakukuwa na mvua ilionyesha kabisa.

Mawe hayo yalishuka mfululizo na hata chanzo chake hakikuonekana kabisa.

“Kimbieni upande huu msije kuumia?”Aliongea Yonesi kwa nguvu baada ya kuanza kusikia makelele ya wafanyakazi wenzake.

Mawe yaliendelea kushuka na kusababisha hata kingo za njia zilizojengwa kwa chuma kugongwa na kupinda.

Hamza alijikuta akinyoosha mkono wake na kuzuia moja ya jiwe lililokuwa likisogea upande wake kwa kasi huku akionekana kukunja sura.

Hamza aliona jambo hilo ni la kushangaza kwasababu eneo hilo limejengezwa vizuri na ilikuwa ngumu kutokea kwa maporomoko kwani kulikuwa na msitu mkubwa na vichaka ikionyesha ardhi yake ilikuwa ngumu , sasa alijiuliza sasa maporomoko hayo yametokea wapi ghafla maana hata kama ni volkano haikuwa ikiripuka kwa staili hio.

Kwa mtu mzoefu kama Hamza aliona kabisa hayo sio maporomoko ya kawaida , lazima kuna kitu , ila hakujua ni kitu gani.

Kilichomfanya pia kuona sio maporomoko ya kawaida ni kutokuonekana kwa mtalii yoyote katika mlima huo na hata kule hotelini watalii walionekana ni wachache na getini hawakukuta mtu, hata kama hoteli hio imekodiwa yote ilikuwa ngumu kutokuwepo kwa watalii.

“Wote kimbieni kuelekea chini ya mlima , msiangalie juu nyie kimbieni kwa uwezo wenu wote”Aliongea Hamza kwa sauti kubwa akiwaamrisha wenzake.

Wakati huo akiwahimiza watu kukimbia aliweza kusikia baadhi ya vi,lio kwa baadhi na hio yote ni kutokana na mawe kuzidi kuporomoka.

Hamza aliona kwa ukubwa wa mawe hayo kama ikitokea mtu kugongwa basi anaweza kufa hapo hapo au kuvunjika kabisa.

“Nyie kimbieni tu kurudi chini , nitayazuia yanayowakaribia”Aliongea.

Mara baada ya kusikia hivyo na Yonesi aliruka kuja mbele na kuyazuia akiacha kujali usalama wake.

Alipanga kutumia mwili wake kuzuia mawe hayo ili wafanyakazi hao wasidhurike.

Hamza alijikuta ni kama kichaa kinamvaa na kujiambia huyu mwanamke anajaribu kufanya nini , au amekuwa chuma ghafla.

Mara baada ya kuona bonge la jiwe linamshukia Yonesi kwa kasi , kwa spidi ya chui aliruka na kwenda kumkinga kwa mbele , na muda huo hakujali mawe mengine yaliokuwa yakishukia wengine na alichofanya ni kukinga yale ambayo yalikuwa yakimsogelea Yonesi, lakini hata hivyo alihakikisha pia wote wanakimbia kushuka chini bila kupata majeraha.

Yonesi mara baada ya kutarajia kugongwa na jiwe kubwa na ghafla akatokea Hamza , alihisi ni kama Mungu ameshuka na kumuokoa lakini baada ya hapo hakujua kilichoendelea.

Mawe hayo kwa namna yalivyokuwa yakishuka , ilikuwa ni kama vile ni makombora ya kifo, ijapokuwa asilimia kubwa walifanikiwa kukimbia lakini baadhi yao walipatwa na majeraha.

Vilikuwa ni vilio kutoka kwa wanawake wakipiga makelele wakati wakikimbia na hakuna hata mmoja aliekuwa na ujasiri wa kuangalia nyuma wala kusikilizia maumivu, kila mtu alikimbia akidhania kuna jiwe lililokuwa likimsogelea na kufanya hata wale waliokuwa wamechoka kupata nguvu na kukimbia kama wanariadha.

Giza na lenyewe halikusubiria kwani lilianza kutanda ndani ya eneo hilo

Hamza alijikuta akivuta pumzi na kuitoa kwa nguvu , kwani alikuwa amefanya kazi kubwa kwa spidi ya hali ya juu ya kuyabadilisha uelekeo mawe hayo huku mengine akiyazuia kabisa.

Muda huo wakati mawe yanapungua alijikuta akigeuka nyuma na aliweza kuimuona Yonesi akiwa amepoteza fahamu , huku eneo la paji la uso pakitoka damu.

Haraka sana alimsogelea na kumpima mapigo ya moyo na aligundua alikuwa amepoteza fahamu tu , hivyo kwa haraka haraka , alishitua kituo cha nguvu zakena kumfanya ashituke.

Alijikuta akiangalia kulia na kushoto na kuona namna uchafuzi uliotokea

“Naona hujapata majeraha makubwa, sio mbaya”Aliongea Hamza.

“Wengine wako wapi , kuna alieumia?”Aliuliza kwa wasiwasi huku akiangalia chini ya mlima.

“Siwezi kujua , nadhani turudi kwanza chini tukaangalie kama kuna aliepata majeraha”

Muda huo Yonesi alijikuta akigeuza macho yake na kumwangalia Hamza na kukumbuka tukio lililotokea kabla ya kupoteza fahamu , ilikuwa ni kidogo tu akutane na jiwe lakini Hamza alitokea na kumkinga kwa mbele.

Kwa namna Hamza alivyomsaidia alijikuta akihisi hisia za tofauti sana katika moyo wake.

“Kwanini ulifanya vile?”Aliuliza.

“Unadhani ningefanya nini?”

“Hukujua ni hatari kiasi gani kukurupuka namna ile , kama ungeumia unadhani ningemwangalia vipi Regina usoni?”Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu.

“Unafikiria sana , unadhani naweza kufa kirahisi hivyo , lakini ni mjinga sana, unadhani mafunzo niliokuipatia yamekufanya kuwa chuma na kutaka kukinga mawe, kwa uwezo wako jiwe la kilo tano tu linatosha kukupeleka magharibi, lakini hebu ona ujinga uliojaribu kufanya, kama nisingekuwahi je?”Aliongea Hamza kwa kupandisha sauti na ilimfanya aanze kutoa machozi.

Alikuwa amechafuka mno na vumbi na muda huo alikuwa kama mtoto mdogo anaegombezwa, tokea mwanzo alimuona Hamza kama mtu mchokozi ambae kazi yake ni kuyafanya maisha yake kutokuwa na amani akiwa kazini, lakini katika hatari kama hio alionekana mtu siriasi mno ambae hakutaka kuona akidhurika.

Hamza mara baada ya kuona Yonesi anatoa machozi aliona pengine ameenda mbali kwenye kumfokea lakini hakuacha.

“Hey Yonesi najua wewe ni mwanajeshi lakini punguza ujasiri usiokuwa na maana, kwenye hali kama hii ulipaswa kujilinda mwenyewe na sio kulinda wenzako , ulichofanya hakikuwa na utofauti kabisa na kujiua?,halafu mbona unaniangalia tu na machozi yako , endelea tu kukaa kimya ila huo ndio ukweli wewe sio jabali..”

Hamza alishindwa kuendelea kuongea sentesi nyingine baada ya kuvamiwa na kupewa busu nyevu , halikuwa busu la shavuni bali la mdomoni kabisa , ki ufupi ni kwamba alipigwa busu bila ya kupenda na Kapteni Yonesi.

Hamza aliweza kuhisi mlipuko wa hisia za mwanamke huyo ni kama ua waridi linalochanua.

Mara baada ya nusu dakika , Yonesi alijikuta akitetemeka na kumsukuma Hamza na kumwangalia kwa macho makavu , alikuwa na aibu lakini hakutaka kuzionyesha.

“Hio ni asante ya kunisaidia na uache kunifokea”Aliongea na ndio muda ambao Hamza akili yake ilianza kufanya kazi sasa na kugusa lipsi zake zilizobusiwa kijeshi na alijikuta akitoa tabasamu ambalo halikueleweka maana yake.

“Yonesi ulikuwa ukinishukuru au kujaribu kuniogopesha , busu gani hili la kutaka kuning’ata mdomo?”Aliongea Hamza

“Wewe… unaongea ujinga gani…Ah embu niache unafanya nini?”

Yonesi alitaka kujitetea , lakini Ghafla tu Hamza ashamshika na kwenda kumkandamiza kwenye mti.

Hamza hakumchelewesha , baada ya kumkandamiza kwenye mti palepale aliinamisha uso wake na kumpiga denda la muda mrefu.

Alimpiga kiss la uhakika mpaka alipohakikisha ameanza kuishiwa na pumzi ndio alimwachia.

Hamza aliishia kutoa tabasamu la kifisi akimwangalia mrembo huyo namna ambavyo alikuwa amebung’aa kwa kile alichofanyiwa.

“Kama ulinikisi kwa ajili ya kunishukuru ulipaswa kunikiss vizuri sio juu juu la sivyo siku nyingine usije kuwaza kunisaidia maana sijakuomba”

“Muhuni sana wewe ..”Yonesi alijikuta akiinamisha kichwa chake chini , alijihisi ni kama vile moyo wake unakwenda kumtoka kutokana na namna ulivyokuwa ukidunda.

“Yonesi najua ushaanza kunipenda muda mrefu , au sio kweli ?”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Furahi kadri unavyoweza , ila mimi sijui unachoongea ni kwasa..”Alitaka kujielezea lakini Hamza mara moja alimsogelea na kumziba mdomo na kumfanya kufurukuta.

“Tulia kimya kuna sauti nimeisikia , kuna swala halipo sawa tokea mwanzo”Aliongea Hamza na kuanza kusikiliza sauti kwa umakini kabisa na aligundu hazikuwa hatua za mtu bali vilikuwa ni vishindo kama kuna watu waliokuwa wakichimba kitu.

“Ni nini?”Aliuliza Yonesi maana yeye hakuweza kusikia hata kidogo.

“Nilikuwa nikijiuliza inakuwaje kukatokea haya maporomoko ghafla tu , hata wewe huoni kuna kitu hakipo sawa baada ya sisi tu kuanza kupanda kwenda juu ndio maporomoko yalianza?”Aliongea Hamza.

“Unamaanisha kuna watu waliokuwa wakitushushia mawe na sio maporomoko?, lakini kama ni hivyo kwanini mtu anataka kuuwa wafanyakazi wa kampuni ya Dosam?”Aliongea Yonesi akionekana kuamka kutoka usingizini.

“Inaweza sio swala la sisi kuwa wafanyakazi wa kampuni ya Dosam na kuna sababu nyingine au pengine imetokea kiasilia wakati tukiwa tunafika hapa”Aliongea

“Kama ni hivyo ni kitu gani tunapaswa kufanya ?”

“Kwa sauti nilizosikia lazima nipande juu na kwenda kuangalia nini kinaendela , wewe shuka kwenda chini na ukaangalie hali za wenzetu zipoje , pia uwatoe hofu pengine wanajua tumekufa”Aliongea Hamza.

“Hapana , na mimi nataka kwenda kuangalia pia”Aliongea Yonesi akiwa na wasiwasi na kumfanya Hamza kufikiria kwa sekunde na aliona kama atamruhusu Yonesi kushuka mwenyewe inaweza kuwa hatari zaidi, hivyo ni salama akipanda nae kwenda juu.

“Sawa twende wote lakini hakikisha unasikiliza kila ninachokuambia na usifanye vitu vya kijinga”Aliongea Hamza na Yonesi macho ya shauku yalichanua huku akitingisha kichwa kukubali.

Wawili hao kwa umakini mkubwa walianza kupandisha kwenda juu kabisa kileleni huku wakiruka mawe na udongo uliokuwa umeporomoka.

Hawakuwa na muda wa kujali wenzao waliokuwa chini huko na kuendelea kusonga mbele.

Upande wa Hamza wakati huo hakuacha kukumbuka kivutio cha mlima huo kuwa na joto nyakati za usiku na alijiuliza au kilichotokea kina uhusiano na jambo hilo , lakini hata hivyo hakutaka kujipa maswali mengi ilihali anaukaribia ukweli.

Baada ya muda mfupi tu waliweza kufika katika kilele ambacho eneo lake lote lilikuwa tambarare lakini kadri ambavyo walikuwa wakisogea karibu waliweza kusikia sauti za watu wakichimba na kumwanga mchanga.

“Fanyeni haraka tumalize usiku huu huu la sivyo watu watatumwa kuja kuchunguza”Sauti ya kingereza kilichojaa lafudhi ya kiafrika iliweza kusikika.

“Najua bosi ndio maana vijana wanaharakisha , kama sio kupoteza muda wetu kudili na yule shombeshombe tungekuwa tunamalizia kazi sasa hivi”

“Tuna bahati mbaya sana , kama tungejuwa kuna watu watapandisha leo hii katikati ya wiki tungekuja siku nyingine”Aliongea mwingine.

“Hebu acheni ujinga na endeleeni na kazi , amesema tukifikisha mita kama saba hivi kwenda chini lazima tutaona ishara”Walisikika huku wakionekana kuchanganya kingereza na kilugha.

“Wanaongea nini mbona nawasikia nusu nusu?”Aliuliza Yonesi huku akiangalia fusi la mchanga lililokuwa limechimbwa , ilionekana yale mawe yote yalioporomoshwa walikuwa wameyachimba.

Hamza hata yeye aliweza kusikia wakiongea vizuri na kutokana na lafudhi zao , haikuwa ngumu kuwatambua hawakuwa raia wa Tanzania, walionekana kuwa kama Wanaijeria ama Waghana hivi.

“Wanachimba madini au, kama vipi tuondoke tu tukawaripoti”Aliongea Yonesi.

“Hebu subiri kwanza tuone wanachochimba ni kitu gani . si itakuwa vizuri zaidi kuwaona wanachochimba kabla ya kuondoka au wewe huna shauku?”Aliuliza Hamza.

“Wewe walivyo wengi vile hata huogopi , vipi kama wakituona na kutushambulia?”

“Acha woga hata kama wakituona hawaniwezi”Aliongea Hamza kwa kujiamini na muda ule alimshika Yonesi kiuno.

“Unaoinaje tukipoteza muda kwa kuendelea pale tulipoishia pale chini..”Aliongea Hamza na hakutaka kumchelewesha kwani alimvutia kwake na kumfosi kumpiga denda kwa mara nyingine.

Yonesi licha ya kushitushwa na shambulizi hilo , hakutaka kutoa mlio kwa kuogopa kuwashitua wale wachimbaji.

Alijikuta akilainika mwenyewe na kuhisi msisimko wa ajabu mara baada ya Hamza kushika nyash yake na kusahau kabisa kile kinachoendelea.

Baada ya dakika kumi za kumpiga kiss na kumshika shika vimanyonyo vyake alimwachia na kumwangalia kwa tabasamu la ufedhuli.

Yonesi jicho lilikuwa limelegea mno na alishindwa hata kumwangalia Hamza usoni .

“Nitakushuhulikia tukirudi..”Aliongea Yonesi kwa kumung’unya maneno na kumfanya Hamza kutamani kucheka , alijiambia kati yake na yeye nani anakwenda kumshughulikia mwenzake.

“Tumeona ,bosi tumeaona , kuna sauti ya chuma inasikika , unasikia?”Sauti za wale watu zilianza kuongea kwa hamasa na kuwafanya Hamza na Yonesi kuangaliana na hawakutaka kusubiri kwani palepale Hamza alimshika mkono Yonesi na kukimbilia sehemu watu wale walipo akaangalie na yeye.

Hatimae waliweza kuona watu waliokuwa na sura nyeusi tii wakiwa wamesimama kwa kuzunguka shimo huku ndani yake ikionekana kuna watu waliokuwa wakichimba , jumla yao walikuwa kama tisa hivi na shimo ambalo wamechimba lilikuwa refu mno kama choo.

Pembeni ya wale watu kulionekana maiti za watu kama sita hivi na kwa haraka haraka Hamza alitambua lazima watakuwa ni wafanyakazi wa eneo hilo na wameuliwa nyakati za mchana.

Hamza hatimae alielewa kwanini hakukuwa na mtu yoyote kwenye geti la kuingilia.

“Nyie ni wakina nani?”Sauti ya kingereza iliweza kusikika kutoka kwa bwana ambae hakuonekana kuchimba kabisa , alionekana kuwa ndio kiongozi wa kundi hilo na alikuwa amevalia koti la ngozi na glovusi nyeusi mikononi , huku akiwa ameshikilia kiko cha kuvutia sigara,.

“Sisi ni wapitaji tu wakuu ila baada ya kuona mnachimba , tulitaka kuona kama mmepata mali”

“Bora mngekimbia kuliko kujileta hapa , Vijana wauweni waungane na wenzao”Aliongea yule bwana na wanaume wale wenye sura ngumu palepale walichomoa visu vyao kwenye viuno na kumsogelea Hamza na Yonesi kwa ajili ya kuwshambulia.

ITAENDELEA
0687151346
 
Story ni nzuri sana ila huu uhusika wa Regina storyline yake haieleweki, kuna kipande kilifika nilijua Regina kashaanza kumtii Hamza kwa kuhofia competition na yule demu aliyekuja nyumbani kwake.

Mpaka Regina alikubali kabisa kuliwa mzigo na Hamza kwa kuzingatia wosia wa bibi yake, yaani alikuwa anakwenda kwenye mstari.

Lakini sasa naona mambo yamerudi tena nyuma kwenye ukauzu, hapa naona kama hii character ya Regina umeiweka so complicated yaani.
 
Story ni nzuri sana ila huu uhusika wa Regina storyline yake haieleweki, kuna kipande kilifika nilijua Regina kashaanza kumtii Hamza kwa kuhofia competition na yule demu aliyekuja nyumbani kwake.

Mpaka Regina alikubali kabisa kuliwa mzigo na Hamza kwa kuzingatia wosia wa bibi yake, yaani alikuwa anakwenda kwenye mstari.

Lakini sasa naona mambo yamerudi tena nyuma kwenye ukauzu, hapa naona kama hii character ya Regina umeiweka so complicated yaani.
Enyewe ila Mimi nikama muandishi nmemuelewa,muandishi alieleza hisia za Regina mapema sana,kwa sasa Regina haja amua na yote ni sababu ya kushindwa kumutabiri hamza Aka the son of Hades, Pia Regina ni wale viumbe ambao hawajui kijishusha ama kwa maana ingne asiependa kushindwa.
 
Story ni nzuri sana ila huu uhusika wa Regina storyline yake haieleweki, kuna kipande kilifika nilijua Regina kashaanza kumtii Hamza kwa kuhofia competition na yule demu aliyekuja nyumbani kwake.

Mpaka Regina alikubali kabisa kuliwa mzigo na Hamza kwa kuzingatia wosia wa bibi yake, yaani alikuwa anakwenda kwenye mstari.

Lakini sasa naona mambo yamerudi tena nyuma kwenye ukauzu, hapa naona kama hii character ya Regina umeiweka so complicated yaani.
vile vile regina anamatatizo kidogo ya akili yenye kumfanya awe na uhusika katika pande mbili. Alieleza mwandishi.
 
Story ni nzuri sana ila huu uhusika wa Regina storyline yake haieleweki, kuna kipande kilifika nilijua Regina kashaanza kumtii Hamza kwa kuhofia competition na yule demu aliyekuja nyumbani kwake.

Mpaka Regina alikubali kabisa kuliwa mzigo na Hamza kwa kuzingatia wosia wa bibi yake, yaani alikuwa anakwenda kwenye mstari.

Lakini sasa naona mambo yamerudi tena nyuma kwenye ukauzu, hapa naona kama hii character ya Regina umeiweka so complicated yaani.
Kula Mtori kijana Nyama zipo chini
 
Back
Top Bottom