Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR.

WATSAPP:0687151346.

SEHEMU YA 120.

Kama mbwai na iwe mbwai fuwele sitoi

Yule mtu katika vazi la suti ya chuma alimwangalia Hamza kwa dakika kadhaa huku akionekana kama mtu ambae alikuwa akimtathimini na kisha akatoa kicheko hafifu kana kwamba alikuwa akimdharau.

“Mtu uliefanikisha kubadilisha mfumo wote wa ulimwengu wa giza kwa mikono yako , ukayageuza mawimbi na kushinda vita takatifu, mfalme unaeabudiwa mpaka na viumbe wa nje ya sayari , lakini sasa hivi unaonekana katika hali ya kutia huruma kama hio kwasababu tu ya kuiba hazina ya kaburi.. inaonekana hilo kaburi sio la kawaida kabisa”Aliongea yule mtu kwa lugha ya kingereza huku akitingisha kichwa na kumuona huruma Hamza.

Sauti yake haikuwa ya mtu kabisa , ilionekana dhahiri ilikuwa imebadilishwa na vifaa vya kieletroniki ili kusikika kama roboti ndio linaloongea na kumuwia vigumu Hamza kujua alikuwa mwanaume au mwanamke.

Katika kumbukumbu zake hakuwahi kukutana na mtu wa aina hio hapo kabla, lakini alionekana kumjua yeye kwa kila kitu na kumfanya kushikwa na hali ya tahadhari.

“Wewe ni nani?Unaniogopa ndio maana unajificha katika hlo mask lako?”Aliongea Hamza.

“Kukuogopa? Kila siku inanifanya nione binadamu wa huu ulimwengu ni viumbe wa ajabu sana”Aliongea huku akicheka.

“Wewe sio binadamu kwahio?”Aliuliza Hamza akijaribu kumtambua mtu huyo kadri awezavyo.

“Kwasasa ndio lakini sahaau baada ya hapa”Aliongea.

“Unamaanisha nini?”Aliuliza tena Hamza , lakini mtu huyo ndani ya damisi (clown) hakujibu zaidi ya kunyoosha mkono wake wa suti ya chuma kumwelekezea Hamza.

“Haina haja ya kuuliza , kwa hali uliokuwa nayo ni kheri ukatoa ushirikiano na kunipatia vitu ulivyochukua kwenye kaburi”Aliongea.

“Vitu gani nimechukua ilihali kaburi limebaribika na umeona kwa macho yako .. sikuweza kupata chochote mimi”Aliongea Hamza huku akinyoosha mikono yake kumuonyesha kama alikuwa hana kitu.

“Don’t think about hiding it from me. My energy detection system has already discovered you have two good things hidden in your pocket”Aliongea akimaanisha kwamba asifikiri kumficha ili hali mfumo wake wa utambuzi nishati umeweza kuona ana vitu viwili vizuri katika mfuko wake.

Hamza alishangazwa na kauli yake ile na kujiambia inamaana katika hio suti yake kulikuwa na mfumo hata wa kutambua alikuwa na zile fuwele kwenye mfuko wake , alijiambia kama ni hivyo teknolojia iliotumika kutengeneza hio suti imeendelea sana.

Kitu kingine kilichomfanya kuwa na wasiwasi zaidi ni vile bwana huyo ni kama alikuwa akimsubiria atoke kwenye hilo kaburi ili achukue alichopata, aliona haikuwa bahati mbaya kabisa kumkuta hapo nje akisubiri.

“Je wewe ndio uliewapa kazi majambazi Lemur kuja kuchimba hapa?”Aliuliza Hamza.

“Kuna maana gani ya kuuliza hilo swali?Unachopaswa ni kutoa hivyo vitu na kunipatia na kila kitu kitakuwa sawa kwa upande wako”

Hamza mara baada ya kusikia kauli ile moyo wake ulipiga kwa nguvu huku hali yake ikianza kubadilika na kuwa ile ya upambanaji.

“Nadhani sasa naelewa kila kitu , ulichokifanya ni kuwatumia Lemur kuja kujiingiza katika hatari kwa kuingia katika hili kaburi na baada ya kufanya kazi unayotaka na kupata unachotaka ungewaua, hukutaka kutumia makundi yenye utaalamu wa juu na kutumia kundi la majambazi kwasababu hata kama ungewaua usingefuatiliwa, si ndio?”Aliuliza Hamza

“Hata kama upo sahihi kuna maana gani ya kuelezea?. Narudia tena kwa mara nyingine nipatie ulichoshikilia”Aliongea na kumfanya Hamza na yeye kutunisha misuli muda ule akionyesha ishara ya kutotaka kutii maneno yake na kujiambia kama mbwai na iwe mbwai fuwele sitoi.

“Kwasababu unanijua vizuri nadhani pia utakuwa unaelewa mafanikio yangu katika swala zima la mapigano , utakuwa unajua sijawahi kukubali kushindwa kirahisi, hivyo kama unao uwezo wa kunipiga na kunipokonya nilichokuwa nacho fanya hivyo , maana mpaka sasa naona kazi ni majivuno tu nahisi pengine unaniogopa kwa kujua huniwezi”

“Wewe ndio uache majivuno , sitaki kupoteza muda ndio maana , hata kama upo kati ya watu wachache ndani ya dunia hii ambao mna uwezo haimaanishi kwamba huwezekani. Hebu kwanza jiangalie ulivyo namna nguvu zilivyokuishia , kutaka kupigana na mimi kwenye hali kama hio ni kujitafutia kifo tu na kwasababu umetaka mwenyewe sina haja ya kukuchelewa na nitakupa kile unachotaka”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo palepale alipelekea mkono wake mdomoni na kufuta damu iliokua ikimtoka, ni kweli kabisa alikuwa akihisi mwili wake umechoka mno , lakini hakutaka kwa hiari yake kufanya kile mtu huyo anachotaka, hakuwa tayari kutoa fuwele hizo mbili ambazo ametoka nazo kwenye kaburi.

Ijapokuwa hakujua kazi yake , lakini aliamini mpaka mambo hayo yote kufanyika maana yake ni muhimu sana.

Kitu kilichomkasirisha zaidi ni kitendo cha kutaka kutumika kwa manufaa ya wengine , yaani kwa alivyoona mtu huyo ni kama alikuwa akicheza mchezo ili kunufaika bila ya kufanya juhudi yoyote, palepale alikunja ngumi na kumpa ishara ya kusogea kwa ajili ya pambano.

“Sogea utuonyeshe ni kitu gani cha maana unaweza kuonyesha na hizo gamba zako”Aliongea.

“Mjinga wewe kushindwa kujua kuna utofauti mkubwa kati yenu binadamu na sisi”Aliongea na sekunde ileile alipotea alipokuwa amesimama.

Hamza kushituka kwake kulionekana kuwa slow kutokana na majeraha lakini licha ya hivyo aliweza kumuona yule mtu licha ya spidi y ake kuwa kubwa na kufanya asionekane kwa macho.

“Crap!!

Dakika ambayo Hamza alijua yupo kwenye hatari ya kupokea shambulizi alijikuta akipigwa ngumi nzito ya tumbo na kumfyatua kama mpira kwenda hewani.

Hamza alifyatuliwa na kwenda kujingonga kwenye tawi la mti na mpaka kulivunja palepale.

“Arghh”Alikuwa kwenye maumivu makali ambayo sio ya kawaida, tumbo lake lilikuwa ni kama linapasuka kutokana na viungo vyake vya ndani kusagika kwa kiasi kikubwa.

Lile Damisi dakika ileile lilimsogelea Hamza kwa kasi na bila ya kumsubiria asimame alimpiga shambulizi lingine la mgongo.

“Arghhhhhhhhhhh….!!!”

Hamza alijikuta akitoa ukulele mkali wa maumivu huku akivunja tawi lingine la mti na kudondoka chini kwa kuvingirika kwenda chini ya mlima mpaka kusimama mara baada ya kugongana na jiwe.

“My-Prince, bado unadhani nashindwa kukuua?”

Lile damisi liliongea kwa kejeli na kisha lilitembea kumsogelea Hamza na kumwangalia kwa chini na kisha palepale liliinama na kusogeza mkono wake kwenye mifuko ya suruali ya Hamza.

Lakini wakati akitaka kuchomoa zile fuwele Hamza alimshika kwa nguvu mkono wake.

“Wewe…!!”Jitu lile licha ya kwamba halikuonekana sura yake ilivyo lakini sauti yake ilionyesha ni dhahiri ilishikwa na mshituko.

Ukweli ni kwamba kwa kipigo alichompatia Hamza aliamini hana nguvu tena na alikuwa nusu mfu.

“Kama sio kwa majeraha yangu ambayo yamepunguza spidi yangu na uwezo wa kukwepa , unadhani ungeweza kunipiga kirahisi?”Aliongea Hamza na palepale kwa spidi ya hali ya juu alifyatuka na akiwa ameushikilia ule mkono wa lile damisi aliupigisha kwa nguvu zake zote kwenye jiwe.

“Clang!

Mlipuko mkubwa ulitokea baada ya tukio lile na kufanya lile jiwe kupasuka vipande viwili.

Kilichomshangaza Hamza na kumfanya atoe macho ni kwamba mkono wa lile damisi haukuwa umeharibika kabisa , tena sio kutokuharibika tu haukuwa hata na mkwaruzo.

Lakini Hamza kutokana na kuushika aliweza kuhisi malighafi yake ni nyepesi mno , kwani hata mtu huyo alionekana kama vile hakuwa amevaa kitu kizito.

“Ngoja nikuone wewe ni nani”Aliongea Hamza na kisha alipeleka mkono wake kutaka kufungua lile helmeti lakini lile damisi palepale lilikunjua kiganja cha mkono wake wa kushoto na palepale ulitoka moto kama mvuke wa rangi ya bluu na kumchoma Hamza.

Hamza hakujua kutakuwa na shambulizi la namna hio na alikuwa amechelewa kukwepa na moto ule kumchoma kwenye bega lake

“Arghhhhhhhh…..!!!!”

Hamza alitoa kilio kikubwa na bila ya kupenda alimwachia yule damisi.

Jitu lile lilichukulia nafasi hio na kumpiga tena Hamza na kumrusha hewani kwa mara nyingine.

Hamza alikuwa dhaifu lakini licha ya mejeraha alikuwa na uwezo wa kupambana kutokana na kwamba mwili wake ulikuwa na uwezo wa kujiponya kwa haraka, vidonda vinaweza visipone lakini kuzuia damu isimtoke ilikuwa jambo rahisi , lakini kitendo cha kuunguzwa na moto mkali kama huo ilikuwa ngumu kupona kwa haraka na kuendelea na pambano , na kama ataendelea kuunguzwa anaweza kufa kabisa.

Damisi lile lilicheka kwa furaha kubwa ya ushindi na kisha taratibu kama yupo kwenye slow motion alimsogelea Hamza.

“Usije ukafikiri hii suti yangu kazi yake ni kuniongezea spidi na nguvu tu , haha.. wewe ni mjinga , ninazo mbinu mia moja za kukuua, hata kama usingekuwa na majeraha sikuogopi, zaidi sana kwasasa una mejeraha mengi lakini bado unaota kunishinda , endelea kuota”Mara baada ya kuongea vile aliinua mguu wake na kumkanyaga kwa nguvu.

Hamza aliishia kung’ata meno yake na mara baada ya kuona damisi hilo linajiona ni mshindi palepale alishika mguu wake kwa nguvu na kisha kumrusha kwa juu na kumfanya adondoke chini kama furushi,.

Lakini licha ya kumdodosha damisi yule chini hakukuwa na madhara yoyote kwenye ile suti ya chuma zaidi ya pale alipodondokea kutengeneza shimo.

Mara baada ya kushambuliwa vile palepale lilitengeneza tena moto ule wa rangi ya bluu kumlenga Hamza.

Lakini Hamza alikuwa amejiandaa na aliweza kukwepa kwa mara nyingine na palepale aliruka na kwenda kulipiga tena na kulirusha mbali.

“Pumbavu zako hata kama unao uwezo wa kutapika moto na kuvaa gamba lako hilo , kwa uwezo wako mdogo wa mapigano usifikiei kuweza kunishinda mtaalamu kama mimi”

Aliongea Hamza na muda uleule alimsogelea kwa mara nyingine na kisha alilikanyaga kwa nguvu eneo la begani na palepale aliweza kuona kidogo sehemu ile imebonyea na kuona nafasi ya kushinda anayo , hivyo kwa spidi aliandaa tani nyingi za shambulizi lakini kabla hajafanikisha azma yake lile damisi lilifyatua miale mingine ya moto wa bluu kupitia mgongoni

Hamza alijitahidi kukwepa shambulizi lile , lakini licha ya kwamba aliweza kukwepa lakini miguu yake na mikono iliungua.

Damisi lile hatimae lilisimama kutoka ardhini , ijapokuwa hakukuwa na mabadiliko makubwa kwenye sauti yake ya kieletroniki lakini ilikuwa ni dhahiri alikuwa na hasira.

“You dare to damage my armor, I’ll kill you first and take away my thing"Aliongea akisema kwamba anathubhutu vipi kuharibu gamba lake, anakwenda kumuua kwanza na kisha atachukua vitu vyake.

Wakati akiongea hivyo alimsogelea Hamza na mikono yake miwili kwa wakati mmoja ilifyatua miale ya moto wa bluu huku yeye mwenyewe kwa spidi akimsogelea.

Hamza palepale alijua hana uwezo wakupigana na mtu wa aina hio ana kwa ana , hivyo kwa haraka sana alichoona ni kutimua nduki kwa uwezo wake wote kuelekea chini ya mlima na wazo lake alilifanyia kazi na kukimbia kwa mtindo wa nyoka ili kukwepa yale mashambulizi ya moto.

Dakika hio hio sauti ya helicopter iliweza kusikika ikisogelea eneo hilo huku ikiangaza kwa mwanga mkali na kwa wale waliokuwa wakiangalia upande wa mlimani waliweza kushuhdia miale ile ya moto kama vile ni radi.

Hamza alijua pengine helicopter hio ilikuwa ni kwa ajili ya uokozi wa hayo maporomoko feki , alijiambia kama mtu huyo atakuwa kichaa si ataua kila mtu kwenye hio helicopter.

Dakika ambayo Hamza aligeuka na kuhofia swala hilo kutokea , aliona lile damisi halikuendelea kumfukuzia na badala yake likimbilia msituni na ilichukua sekunde kama kumi tu , aliweza kuona likiwa limeshikilia kitu kama sinia lenye tundu la chupa katikati linalofuka moto kwenye mkono wake na kifaa kile kili-mfyatua kwa spidi ya hali ya juu na kupotelea angani.

Hamza alishangazwa na jambo lile na kufikiria sababu ya kufanya vile ni nini na palepale liona au tofauti na kutaka fuwele alizokuwa nazo damisi hilo halikutaka kuonekana kwa watu wengine zaidi yake .

Hamza mara baada ya kufikiria kwa umakini aliona ni kitu kinachowezekana , lilikuwa likiogopa kugundulika kwa kuonwa na macho ya watu wengi .

Hamza aliona inaleta maana , isitoshe Damisi lile lilionekana kutokuwa na nguvu za kutosha na kama ikitokea uwepo wake ukaingia kwenye rada za jeshi la Malibu ingekuwa hatari zaidi.

Hamza alijua hakuna uwezekano Damisi lile limekata tamaa ya kutopata fuwele alizokuwa nazo , moja kwa moja alijua lazima litarudi , licha ya hatari iliopo lakini hakutaka sana kufikiria juu ya hilo , alikuwa amechoka sana na kama sio kutunza nguvu kidogo angekuwa ashadondoka na kuzima

Hamza alishuka kwa spidi mpaka chini ya mlima na aliweza kuona watu ambao walionekana kufika hapo kumuokoa.

Baadhi ya watu wa jeshi la uokoaji kumuona alikuwa ameloa damu haraka sana walimsogelea na kumbeba kisha wakamwingiza kwenye ambulance.

Chini kabisa Yonesi alikuwa akizunguka huku na huko kumsubiria Hamza kwa wasiwasi , lakini mara baada ya kuona watu wa jeshi la uokoaji wamefika nae akiwa na majeraha kibao alijikuta akishituka mno na macho yake kuwa mekundu na kumsogelea.

“Nini kimekutokea mpaka ukaumia kiasi hichi?”

Katika macho ya Yonesi alimuona Hamza ni mtu ambae hakuna wa kumshinda hivyo hakuwahi kudhania Hamza anaweza kujeruhiwa namna hio.

“Ni ngumu kukuelezea ukaelewa , twendeni kwanza hospitalini nipate dawa maumivu yapungue”Aliongea Hamza kwa kujikaza.

Saa moja na nusu baadae Hamza alipelekwa hospitali ya halmashauri ya wilaya na kufungwa mabendeji kadhaa baada ya huduma ya kwanza , ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya vidonda vyake vilikwisha pona ,ila baadhi yake vilionekana kuona taratibu mno.

Kama sio kuwa katika levo ya Kukaidi mbingu na asili na kuwa mtu wa kawaida angekuwa amekwisha kupoteza maisha ndani ya lile kaburi kabla hata ya kupigana na Damisi.

Asilimia kubwa ya wafanyakazi wote wa Dosam walikuwa salama na ni baadhi yao tu walikuwa na majeraha kidogo ya migu na michubuko kwenye mikono.

Ilibidi safari ya kuendelea na utalii ighairishwe na wafanyakazi wote walipakiwa kwenye basi kurudi hotelini na baadhi yao waliokuwa na majeraha makubwa walibakia hospitali , upande wa Yonesi hakutaka kuondoka na kubakia wodini na Hamza.

Mwanamke huyo alimuuliza Hamza kama kuna kitu alichoweza kupata kwenye lile kaburi na Hamza alimwelezea kile alichoona kwa ufupi sana huku akiacha kuelezea sehemu ya kuwa na fuwele, alimwambia tu aliona kuna kitabu kilichokuwa na majina ya ukoo yaliokuwa kwa lugha isioeleweka basi.

Saa tano za usiku Regina aliweza kufika kwa kutumia helicopter ya kampuni na kujulia hali wafanyakazi walioumia na kitendo hicho kilifanya wafanyakazi hao kuguswa.

Lakini Regina akili yake haikuwa kwao kabisa na kwa haraka sana alienda katika wodi aliokuwa amelazwa Hamza.

“Unaendeleaje?”Aliuliza haraka haraka huku akimwangalia Hamza

Aliweza kumuona Yonesi aliekuwa pembeni ya kitanda huku macho yake yakiwa ni kama anataka kulia.

Kwa namna isioelezeka ni kama hali ndani ya wodi hio ilibadilika na kuwa isioelezeka hususani kwa upande wa Regina kumkuta Yonesi akimwangalia Hamza kimahaba.

******

Wakati hayo yakiendelea muda wa saa nne za usiku , alionekana mwanaume alievalia suti ya Zambarau akiingia katika kanisa la Wabrazili na kwenda kukaa nyuma kabisa ndani ya kanisa hilo.

Alikaa nyuma kwasababu muda huo ibada ilikuwa ikiendelea ndani ya eneo hilo na waumini walikuwa ni wafuasi wa Lucifer(Shetani) au maarufu kama devil worshipers.

Ilikuwa ni ibada ya kutisha mno kwa wale ambao hawakuwahi kuona , mbele ya kila muumini kulikuwa na bilauri nyekundu ya kumeremeta na kisu kidogo cha rangi ya dhahabu na kifimbo cha mshale kama pembe tatu sawa, kulikuwa na sinia la madini ya kung’ara lenye kuonekana kuwa na kimiminika na pembeni kulikuwa na kitaulo.

Hakukuwa na waumini wengi wala hawakuwa wachache vilevile na mbele kabisa ya madhabahu alikuwepo mwanaume alievalia kinyago cha nembo ya tone la damu na joho lenye mchoro usioelezeka ulikuwa ni kama wa pembe tatu zilizozungushwa mara kumi na mbili katika kichwa cha mtu.

Kiongozi yule alikuwa ameshikilia kitabu kikubwa mkononi ambacho kava lake lilionekana kupambwa na madini, alisikika akiongea kwa namna ya kusoma kitabu kile na kisha wale waumini walikuwa wakitamka kwa kunawa uso katika bakuli na kisha kunywa kilicokuwa katika bilauri lakini lugha yao haikuelezeka.

Bwana yule aliekaa nyuma kabisa zilipita kama dakika chache alifuatwa na mtoto mdogo alievalia nikabu na kiremba kichwani na kisha alimpatia kifaa kidogo kama kishikwambi na kisha yule bwana aliweka mkono juu ya kile kishikwambi kwa sekunde.

“Mr Christopher Gabusha unaweza kunifuata sasa, maandalizi ya tohara yako yamekamilika”Aliongea yule mtoto na Chriss mtoto wa Gabusha hakuonekana kushangaa sana kwani alisimama na kumfuata yule mtoto nyuma nyuma na kuingizwa kwenye chemba.

END OF SEASON 4.
NAPATIKANA WATSAPP 0687151346
Kiongozi

Kiongozi siku hizi umetutupa sana n siku ya Monday bana😉😉
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR

SEASON 5

SEHEMU YA 121.

Lugha ya malaika na Karama ya uzao wa damu.

(Enochian language)

Yonesi pia aliweza kuhisi jambo lile , isitoshe wenzake wote walikuwa wamekwisha kuondoka , kama mkuu wa kitengo cha ulinzi alipaswa kuangalia usalama wa wafanyakazi na sio kukaa katika wodi ya Hamza.

Sasa kitendo cha kumuona Regina akiwa ameingia hapo alijikuta akishangaa huku akikosa utulivu kwa wakati mmoja .

“Mkurugenzi.. kwasababu umefika nitawaacha sasa”Aliongea kwa kubabaika kama mwanamke aliekamatwa akimtega mume wa mtu.

“Vipi umeumia?”Aliuliza Regina swali hilo likimlenga Yonesi.

“Sikuumia , nipo sawa”Aliongea na hakutaka kusema kama kidogo tu angekufa kama sio Hamza kumuokoa.

“Basi kesho litawachukua kuwarudisha mjini asubuhi , nadhani ni vizuri ukienda hotelini kuoga na kupumzika”Aliongea na kumfanya Yonesi kushangaa maana alikuwa amechafuka na hakuwa amepata muda wa kujisafisha na muda ulikuwa umeenda kweli.

“Asante pia kwa kumuangalia kwa kujali Hamza”Aliongea akimshika begani lakini Yonesi alihisi kauli ile ni kama ilikuwa na zaidi ya maana na kumfanya ajishitukie.

“Mkurugenzi sijafanya chochote, usije ukanielewa vibaya”Aliongea huku sura yake ikianza kuwa nyekundu na kutokana na mwoneknao huo Regina alihisi kuna kitu kinachoendelea baina yao maana hakumzoea Yonesi kukosa kujiamini namna hio mbele yake na aliishia kumwangalia Hamza aliekuwa amelela kitandani akijifanya hajui kinachoendelea na alianza kushikwa na hasira katika moyo wake.

Lakini kutokana na bendeji kubwa ambalo Hamza amefungwa kwenye bega lake na miguuni aliishia kuzima hasira zake.

Ukweli ni kwamba alisikia habari kwamba kama siio Hamza wafanyakazi wengi wangepatwa na majeraha makubwa na pengine hata kupoteza maisha na swala kama hilo lingetoka kwenye vyombo vya habari maswali mengi yangeibuka.

Kwa mantiki hio Regina kama mkurugenzi alipaswa kumsifia Hamza kwa ushujaa aliofanya lakini alikasirika mara baada ya kuona alikuwa ashaanza kumteka na Yonesi kihisia..

Bila hata ya kuambiwa alijua tu lazima Hamza atakuwa amemuokoa Yonesi katika janga hilo la sivyo isingemfanya mwanajeshi huyo wa kike kuonyesha mahaba ya waziwazi kwa Hamza.

Regina alijihisi kukosa nguvu na udhaifu kwenye moyo wake , siku zote alikuwa vyema katika kudili na matatizo yanayohusiana na kazi yake lakini matatizo ya kimahusiano na familia yalikuwa magumu mno kwake.

“Unaweza kutembea?”Aliuliza mara baada ya kusogea karibu zaidi na Hamza.

“Ndio naweza kutembea , unaonaje tukienda nje kutafuta chakula maana nahisi njaa kali”Aliongea Hamza maana hakupata chakula tokea mchana na aliingia kwenye mapambano makali na masanamu na kisha akakutana na lile damisi.

Regina aliishia kukunja sura , baada ya kumsikia aliona Hamza alikuwa akitia huruma hivyo bila ya kubisha aliishia kutingisha kichwa kukubali.

Hata Yonesi hakuwa amekula chochote hivyo wote watatu walitoka nje na kutafuta mgahawa pembezoni mwa hospitali , ijapokuwa ilikuwa ni kimgahawa kidogo sana kutokana na kufungwa lakini hawakujali.

Walianza kuagiza mishikaki, mihogo na chai huku wakisubiria ugali na samaki uandaliwe kama Hamza alivyoagiza.

Haikuchukua muda wakati wakisubiria chakula mwanamke mrembo wa kuvutia alievalia koti la suti aliingia katika mgahawa huo , ijapokuwa nywele zake zilionekana kuchanguka kidogo lakini haikuathiri urembo wake.

“Lizzy!!, unafanya nini huku?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.

Eliza mara baada ya kusikia sauti ya Hamza macho yake yalichanua lakini mara baada ya kumuona Regina na Yonesi , tabasamu lake lilififia na kuwa katika hali ya wasiwasi.

“Mkurugenzi , Yonesi! Kumbe na nyie mpo huku?”Aliongea kwa kushangaa huku akishindwa kupiga hatua kama vile amegandishwa , lakini hata hivyo aliishia kuingia ndani.

Yonesi mara baada ya kuona Eliza amefika alijihisi akipatwa na amani na wala hakujua kwanini.

“Ndio umefika au ulikuwa huku?”Aliuliza Regina maana alijua Eliza alikuwa Dodoma makao makuu ya nchi kikazi.

“Nilipokuwa Dodoma niliona nipitie Moshi kupitia maendeleao ya kiwanda chetu cha ngozi na wakati najiandaa kutoka ndio nilisikia taarifa za kilichotokea ndio nikaona nipitie kujulia wafanyakazi hali zao”Aliongea Eliza akijitahidi kujitetea na kisha alisogea na kumwangalia Hamza na kumuuliza kama yupo sawa.

“Niko sawa , kaa kwanza chini nina njaa kweli hapa , vipi ulikuwa ukiendesha mwenyewe au ulikuwa ukiendeshwa?”Aliuliza na Eliza alitingisha kichwa na kujibu alikuwa akiendesha mwenyewe.

Ukweli ni kwamba mrembo huyo hakuwa na mpango wa kupanda gari kusafiri mpaka Dar , wakati akiwa Moshi alipanga kurudi KIA na kisha apande ndege kurudi Dar es salaam , lakini baada ya kusikia habari hizo haraka haraka alichukua gari ya kampuni na kuendesha kwa zaidi ya masaa matatu kuja kufika Lushoto.

Hamza aliguswa kwa namna wanawake wote wanavyomjali na aliishia kucheka kwa furaha huku akimwangalia mmoja mmoja na kisha amcho yake yakaishia kwa Regina.

“Mke wangu hebu angalia , kila mtu ana wasiwasi juu yangu , hii ndio maana halisi ya kuishi na watu vizuri , nimeguswa mno”Aliongea

“Umeguswa au unahisi kujivunia?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kushikwa na aibu.

“Kidogo tu… lakini si imekuwa vizuri kwa mara ya kwanza tunakaa chini na kula pamoja?”Aliongea lakini Regina aliishia kuangalia pembeni huku akinywa taratibu chai ya maziwa kupoza baridi huku akimpotezea .

Baada ya muda mfupi wa kusubiri ugali na samaki aliwekwa mbele yao na Hamza hakuongea zaidi ya kujiweka bize kuushughulikia , mwanzoni wakati anafika bongo hakupenda sana ugali lakini mara baada ya kuuzoea aliona ni chakula kizuri sana katika kurudisha nguvu.

Baada ya kula wote walitoka nje ya mgahawa na palepale Regina alimgeukia Yonesi.

“Eliza utaondoka na Yonesi kwasababu umekuja na gari, maana mnaelekea njia moja”Aliongea

Yonesi na Eliza waliishia kuangaliana kwa sekunde kadhaa na kisha waliishia kutingisha vichwa kukubali.

Regina mara baada ya kuona hawakupinga wazo lake alijihisi kuridhika na kisha alimgeukia Hamza na bila ya furaha alimwambia waondoke na Hamza alimpa ishara ya kutangulia na baada ya kuona Regina amemuacha kwa hatua kadhaa haraka sana alimsogelea Eliza na kumpiga busu la shavu na akahamia kwa Yonesi na spidi yake ilikuwa kubwa mno kwani kabla hawajashituka tukio hilo lishafanyika tayari na Hamza ashaondoka na kuendelea kutembea kumfuata Regina Regina.

Regina alihisi kitu kimetokea nyuma yake lakini baada ya kugeuka aliona Hamza alikuwa nyuma akimsogelea kwa adabu na Hamza mara baada ya kuona anaangaliwa alijishutukia.

“Wife kuna tatizo?”

“Kuna ujinga umefanya sio?”Aliuliza huku akikunja sura.

“Ujinga gani wakati nilikuwa nikiutukuza uzuri wako kwa nyuma , au hata hilo ni la kijinga?”

Regina mara baada ya kusikia kauli hio aliishia kugeuka maana alihisi ghafla uso wake kushikwa na joto.

“Nani wa kukuamini wakati muda wote haupo siriasi”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la kumchokoza.

Aliona mbinu ya kumpeti peti mrembo huyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri sana na alijiambia atakuwa anatupia tupia maneno ya mtego kila anapopata nafasi ili kumlainisha.

Kwasababu Hamza alikuwa na bendeji ilibidi kurudi kwanza wodini na kupumzika na Regina pia alirudi nae, lakini Hamza hakuwa na usingizi hivyo mara baada ya kukaa chini kwenye kitanda na Regina kuvamia sofa akionekana kuangalia kitu kwenye kishikwambi chake ,Hamza alimwambia Regina anaomba kalamu na karatasi yoyote na Regina licha ya kushangaa aliishia kutoa karatasi na karamu na kumpatia Hamza.

Hamza mara baada ya kupewa karatasi ile alianza kuandika kwa namna ya kuchora, ubongo wake ulikuwa na uwezo wa kukumbuka kila kitu hivyo alichochora herufi ,zilikuwa ni zile ambazo aliona kwenye kile kitabu , hakujua maana yake lakini muonekano wa lugha ile alikuwa akijua vyema.

Baada ya nunsu saa aliweza kuchora nusu ya ukurasa wa kile kitabu na kumfanya atingishe kichwa kukubali uwezo wake wa kuwa na akili yenye uwezo wa kupiga picha.

Baada ya pale alivuta hisia juu ya kitabu alichopewa na Ganesha kuona kama kuna hali ya kulandana kwa asilimia ngapi kwa meneno hayo alioandika chini na kila kitu kilikuwa sawia kabisa..

Baada ya kufanya vile alitafuna karatasi ile na kisha akatupiua kwenye dustbin na mara baada ya kumaliza hivyo , aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa nje zile fuwele.

Kitendo cha kuzishika mkononi mwanga wake ulibadilisha chumba na kumfanya Regina kushituka na kumwangalia Hamza kwa mshangao na mrembo huyo palepale alisogea kutoka kwenye sofa na kuja karibu ya Hamza.

“Hamza hivyo ni nini!?”Aliuliza kwa mshangao mkubwa mno.

“Mimi sijui , ila ni vitu ambavyo vingesababisha nipoteze maisha”Aliongea.

“Nini , kwani kulitokea nini?”Aliuliza kwa mshangao mkubwa.

Hamza alifikiria kwa dakika kadhaa na kuona kutokana na Regina mwenyewe familia yake kuwa na muunganiko mkubwa na ulimwengu wa giza basi ni swala la muda tu kujua mambo mengi, hivyo swala kama hilo hakuona haja ya kumficha pia na alianza kumwelezea kutoka mwanzo hadi mwisho kwanzia habari za Kaburi na mpaka swala la kupigana na Damisi mpaka kuamua kukimbia.

Regina mara baada ya kusikia maelezo hayo kutoka kwa Hamza alishituka mno akiwa ni kama hakua akiamini kile alichosikia, lakini kutokana na kusikia mambo mengi ya kushangaza pamoja na fuwele hizo za ajabu alijikuta akiamini.

“Au ni za viumbe kutoka sayari nyingine , si umesema hayo masanamu yalionekana kama maroboti yenye teknolojia kubwa , kama kweli ni ya Zamani wewe unaona imewezekana vipi zamani wakawa na teknolojia ya aina hio?”Aliuliza Regina

“Hata mimi nashindwa kuelewa , isitoshe sijawahi kukutana na maroboti ya namna ile ambayo yanajua mapigano , kuhusu kuwa Alien nashindwa pia kupata pointi ya kuunganisha”

“Mimi hata kama uniambie ni Alien siwezi kushangazwa na hilo?”

“Kwanini unaongea hivyo?”Aliongea Hamza huku akimwangalia Regina kwa shauku.

“Hebu jaribu kufikiria kuhusu historia ya ulimwengu ilivyo , kila mtu anasema la kwake , tunaambiwa washawahi kuwepo viumbe kama Anunnaki waliokuja duniani kwa ajili ya kupata rasilimali za dunia , lakini vile tunaambiwa washawahi kuwepo kwa viumbe wenye miili mikubwa maarufu kama Ma’giant waliotengeneza vitu vya kustaajabisha kama Mapiramidi na mambo mengine ya kushangaza ambayo mpaka leo hii hayana majibu, ukifuata watu wa sayansi wenye kufuata ukweli watakuambia ni hadithi tu na hakuna ukweli , ukiwaambia waelezee ukweli kuhusu ushahidi fulani wanatunga kweli ya kuendana na ushahidi na kwasababu wanao ushawishi wa kusikilizwa inakuwa kitu ambacho binadamu tunamini ndio ukweli, kama mambo mengi yametokea kipindi cha nyuma sana , je ni rahisi sisi binadamu wa kizazi cha sasa kuelewa historia yote? Tunajua viumbe wote waliokuwepo duniani katika enzi hizo?.Nina uhakika kuna mambo mengi ambayo yalitokea katika enzi ya kale ambayo historia yao ilipotea na kufanya mambo mengi yawe ni ya kusadikika tu”Aliongea Regina kwa kirefu.

Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo alishindwa kujizuia na kuishi kutingisha kichwa kukubaliana nae.

“Hata mimi nadhani hivyo , maana mwisho wa siku binadamu tunaamini kile ambacho kina ushahidi”

“Kusema jambo flani halipo au halikuwahi kuwepo inatokana na pale utashi wetu wa akili unapoishia , kwa mfano tunajifunza kuna uelekeo wa Kusini , Kaskazini , Mashariki na Magharibi , lakini katika anga nje ya dunia hakuna kitu kama hicho , mwisho wa utashi wetu ndio ukomo wa uhalisia, tunachoona kwa macho tunaamini ndio uhalisia kwa kuupa sababu za kimantiki ujinga wetu juu ya kile kilichokosa ushahidi. Wewe mwenyewe si ndio ulisema kuna zaidi ya asilimia tisini na nane ya ulimwengu ambao hauonekani kwetu binadamu , kwanini sasa hivi unaongea kama vile huamini maneno yako?Kama ulichoona kwenye hilo kaburi ni sahihi basi ni theluthi moja ya ushahidi wa kuonyesha kwamba kuna vitu vilikuwepo ila tunaamini havikuwepo kwa kukosa ushahidi”.

Hamza aliishia kutoa tabasamu baada ya kuona Regina anatumia maneno yake kumwelekeza, lakini hata hivyo alichoongea kilikuwa na mantiki.

“Kinachonipa wasiwasi ni juu ya hilo Damisi, ni nani na ana nia gani ya kutaka kuchukua hizo fuwele?”Aliongea Regina akionekana kuwa na wasiwasi.

“Hata mimi sijui chochote , ila nitafanya uchunguzi kupata majibu na kuhusu hizi fuwele ni hatari nikitembea nazo, napaswa kutafuta sehemu na kuzificha, Yule mtu Suti yake ina mfumo wa kunasa nishati za hizi fuwele , kama nikiendelea kutembea nazo , itakuwa rahisi kunipata”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Regina macho yake mazuri kuchanua.

“Kuna sehemu naijua ni salama labda unaweza kuficha”Aliongea

“Wapi au unataka kusema kwenye Vault za benki , kama ni huko itakuwa rahisi sana”Aliongea Hamza.

“Unaniona mjinga, kesho nitakupeleka”Aliongea Regina na Hamza licha ya kushangaa alikubali.

Siku iliofuata Hamza aliondoa mabendeji aliokuwa nayo , licha ya daktari kumwambia apumzike kidogo lakini alikataa na kumwambia itakuwa mbele kwa mbele, isitoshe dokta huyo alikuwa akitaka kuchukulia faida uwepo wa Regina katika hospitali yao.

Regina ndio aliekuwa akiendesha gari , wafanyakazi wengine walipanda basi huku Eliza na Yonesi wakipanda gari pamoja na kurudi mjini.

Regina mara baada ya kufika Dar es salaam , hawakuelekea nyumbani bali walielekea upande mwingine na dakika kadhaa walikuja kutokea Msasani na alienda kusimamisha kwenye jumba kubwa ambalo lilikuwa na geti jeusi nje.

Regina alishuka kwenye gari na kisha baada ya kusogelea lile geti alipachua sehemu kwa namna flani ya kipekee ya kuzungusha na kisha palepale alisogeza kitu kama ufuniko na kulionekana kitu kama kijisimu na aliweka kiganja cha mkono na dakika ileile geti lilianza kujifungua lenyewe taratibu na akampa ishara Hamza aingize gari ndani.

Hamza aliingiza gari mpaka ndani na alishangazwa na jumba kubwa la kifahari lililokuwa mbele yake.

“Hapa ndio nilipokuwa nikiishi kabla ya kuhamia kule Kigamboni , ndio nyumba ambayo baba alikuwa akiishi”Aliongea Regina na palepale Hamza alijua sehemu hio ndio ambapo familia nzima ya Regina ilikuwa ikiishi hapo kabla , sasa kwasababu ya baba yake kupoteza maisha na Lamla, hakukuwa na mtu anaekaa na moja kwa moja Regina ndio mwanafamilia ambae anaimiliki.

Hamza mara baada ya kuingia ndani aligundua kulikuwa ni kusafi mno , ilionekana kuna mtu ambae anafanya usafi kila siku.

Regina alimpa ishara Hamza kumfuata juu na kuingia katika chumba kikubwa kilichojaa vitabu kama maktaba.

“Hii ndio ilikuwa kama ofisi ya babu na baada ya babn kufariki baba aliirithi”

“Kwahio unataka nizifiche hapa?”Aliuliza Hamza lakini Regina hakuongea chochote na kutembea mpaka kwenye shelf ya vitabu na kuvitoa kisha alibonyeza ubao uliokuwa nyuma ya shefl hio na sauti za kitu kusogea zilianza kusikika na hatimae eneo lile liliacha uwazi na kufanya mlango uonekane.

“Kuna sehemu inayoelekea ndani?”Aliuliza Hamza kwa kushangaa.

“Hata mimi sikujua mwanzo , baada ya swala lile la maswala ya bondeni na jicho la anga , shangazi aliniambia kwenye hii nyumba kuna sehemu ya siri ambayo hata baba hakuwa akiifahamu ,sehemu ambayo babu alikuwa akificha vitu vyake vya siri, nilikuja hapa mara moja na sikuona vitu vingi lakini kwa namna sehemu ilivyo naona ni sehemu sahihi kuficha hizo fuwele zako”Aliongea Regina.

Hamza alivutiwa na bila kuuliza sana alimfuata Regina kuingia ndani na kitendo cha kuingia katika kijichumba hicho ilikuwa ni kama lift kwani walishishwa mpaka chini na hatimae walienda kusimama kwenye mlango wenye kuta za mawe.

Mara baada ya kuingia Hamza aliweza kuona picha nyingi ambazo zilikuwa zimening’nizwa , ikiwemo picha zisizoeleweka pamoja na majina yake kwa chini na Hamza aliamini lazima utakuwa ni ukoo wa Regina.

Kilikuwa chumba cha ardhini ambacho hakikuwa na vitu vingi lakini kuna sehemu ambayo ilionekana kama sehemu ya kusali ama kuswali kwa namna ilivyowekwa.

“Babu yako alikuwa dini gani , mbona kama hii sehemu alitumia kama mahali pa kusalia?”Aliuliza Hamza.

“Babu alijitambulisha kama mkatoliki , lakini sijawahi kumuona hata akienda kanisani na hakuwahi kuniambia niende kanisani vilevile”Aliongea Regina bila kufikiria sana na kisha alimuonyesha Hamza kijiboksi maalumu lilichochongwa kwa jiwe juu ya kiango .

“Hii sehemu inafaa kabisa kuhifadhi hivi vitu , kwa namna palivyotengenezwa sidhani kama atakuwa na teknolojia ya kunasa uwepo wake hapa”Aliongea Hamza.

“Ndio, mimi nilikuja kuangalia na sikukuambia kwasababu sikuona cha maana tofauti na hizi picha na majina yake na karibia zote zinazungumzia watu wenye historia kubwa duniani na kuzungukwa na uzushi wa kila aina”Aliongea Regina

Hamza hata yeye hakufikiria sana na baada ya kufanya vile moja kwa moja aliweka zile hadhina kwenye boksi lile

“Ijapokuwa sijui vitu hivi ni nini , lakini nitachukulia kama mahali yangu kwako”Aliongea na kumfanya Regina kuvuta mdomo kwa kejeli.

“Unataka kufanya hivyo vigoroli vyako kuwa mahali yangu,unanichukualiaje kwa mfano?”.

“Hehe.. kwasababu nyie ni matajiri tayari , hata nikitoa hela haitokuwa na maana , ila kuna hisia zinaniambia hizi fuwele thamani yake ni zaidi ya hela”Aliongea na Regina hakumbishia.

“Tuondoke sasa nataka ningie kazini mchana”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa kukubali, lakini wakati akitaka kuondoka macho yake yalitua kwenye karatasi kubwa iliokunjwa kama ramani na Hamza haraka haraka alisogea na kuichukua na kuifungua ndani.

“Unafanya nini tena?”Aliuliza Regina huku akisogelea kuangalia kile alichoshika Hamza.

“Hii mbona inaonekana ni kama ramani ya kisiwa .. hapana hii kwa nje inaonekana kama ramani ya kisiwa cha BINAMU lakini kwa nje ni lugha ya ufunuo”

“Lugha ya ufunuo unamaanisha nini?”Aliuliza Regina kwa mshangao maana alishaona karatasi hio na hakuelewa na kuona labda ni kitu tu cha zamani chenye thamani kilichohifadhiwa hapo.

“Lugha ya ufunuo unaweza kuita kwa jina lingine kama Lugha ya Malaika au Enochian langauge , ijapokuwa ukiangalia hivi unaweza kuona ni kama mchoro lakini kuna maana kwenye herufi zake, mtu wa kawaida huwezi kuelewa lakini mimi niliejifunza vitu vingi nimeweza kugundua mara moja hii ni ramani lakini vilevile ni mafunzo maalumu ya kufungua nguvu za mwili yalioandikwa kwa lugha ya kimalaika, sio watu wote wanaoweza kuitafsiri hii lugha kutokana na maajabu yake , uwezo wa kuitafsiri unazaliwa nao na nadhani hiki ndio kitu alichokosa babu yako na kuishia kuhifadhi hapa , lakini swali linaibuka amewezaje kushika kitu cha thamani kama hiki”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushangaa

“Ndio maana nilikuwa nikijiuliza maswali mengi , inakuwaje babu kujenga eneo kubwa kama hili na hajaacha kitu cha thamani , inaonekana hiki ndio kitu cha thamani sana alichoacha”

“Ni zaidi ya thamani ya hela , lakini hilo sio la kuzingatia , nina uhakika amekuachia hapa makusudi baada ya kuona hawezi kutafsiri nadhani aliona utaweza kufanya hivyo, kwa usalama wako nadhani ni vizuri ukianza kutafisiri ili upate uwezo wa kujilinda baadae”Aliongea Hamza.

Regina mara baada ya kusikia kauli hio alishangaa na kuhisi hali ya wasiwasi katika akili yake , kwa maelezo ya Shangazi alimwambia watu wa Bondeni wana mbinu zao za mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na kuwafanya kuwa kama majini na kuthibitisha hilo ni kama Mzee Suwi alivyojitokeza na kutaka kuwapokonya pete , mbinu aliotumia ilikuwa ni ya nishati za mbingu na ardhi.

“Kama siwezi kutafisiri nitawezaje kujifunza , siamini kama naweza kuwa na uwezo wa ajabu”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutabasamu na kujiambia angejua kwa kipindi kirefu kulikuw ana vita kati ya Vatican na kundi la watu wanaojiita Wiccan kutafuta hili andiko asingeongea kirahisi namna hio.

“Moja ya maajabu makubwa ya lugha ya malaika haipo kwenye kusoma kama unavyoangalia herufi , bali kwenye maana akili yako inayopata kwa kuangalia tu hizo herufi zake, hii inaifanya kila mtu aliezaliwa na karama ya kuitafsiri kwa namna yake na kubwa zaidi, hii ni lugha inayomtambua msomaji”

“Unamaanisha nini ni lugha inayomtambua msomaji”

“Maana yake ni kwamba maandiko yenyewe ya hii lugha ndio yanajifunua kwako na kupata maana na sio wewe kuyatafsiri na kupata maana , labda nikupe mfano moja ya watu ambao walibahatika kuweza kutazama maandiko haya wakiwa na karama mmoja wapo ni John Dee kutoka karne ya kumi na sita , huyu bwana pamoja na Edward Kelley maandiko yalivyojifunua kwao yaliwafanya kuwa wachawi wakubwa ambapo mbinu za uchawi walizopata zinatumika mpaka katika uchawi wa kisasa wa leo hii na wamekuwa msingi mkubwa sana wa imani ya Wicca”Aliongea Hamza.

“Kwahio unachomaanisha kama mimi pia ninayo karama naweza kugeuka kuwa mchawi?”Aliuliza Regina kwa wasiwasi.

“Japo ni kweli maandiko haya yanajifunua kwa mtu na kupata maana , lakini sio kweli kwamba yanamfanya mtu kuwa mchawi . hata mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi pia zilipatikana kutokana na tafsiri ya lugha hizi hizi lakini kwa namna tofauti ndio maana leo hii kuna mbinu kibao za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi, mafunzo yanasema Karama ni one-time blood generation, maana yake ni kwamba kunaweza kutokea kizazi cha kwanza , cha pili na cha tatu katika ukoo na hakuna mwenye Karama licha ya kizazi cha kwanza alikuwepo mtu mwenye karama , lakini baada ya kizazi cha nne ndio ule urithi wa karama uliotokea katika kizazi cha kwanza ukaja kuibukia kwenye kizazi hicho, sasa kulingana na karama yako ya kuelewa lugha ya malaika itatokana na karama ya urithi wa uzao wa damu katika ukoo wako na sio nje ya hapo”

“Kwahio unasema kama kuna historia ya mchawi kwenye familia yetu na mimi nitapata tafsiri ya uchawi kwa kuangalia lugha ya malaika?”

“Hakika, ndio maana nikasema lugha hii inamtambua mtu mwenyewe kulingana na uzao wake , hivyo kama una Karama ya kuitafsiri na kuipata maana haitokuwa nje na historia ya familia yako , kwa machache niliojua kuhusu babu yako inaonekana yupo mbali sana na kinachoitwa uchawi , rejea historia aliyozungumzia Shangazi juu ya namna mama yake alivyobakwa kupewa pete na alivyozaliwa, inanifanya niamini pengine unaweza kupata maana halisi ya maandiko ya lugha hii tofauti na watu walivyoweza pata tafsiri kadri walivyofunuliwa”Aliongea Hamza na Regina alionekana kuelewa.

Kwa lugha nyepesi alichokuwa akimaanisha Hamza ni kwamba Enochian Language au lugha ya malaika ni andiko ambalo linampatia mtu ufunuo wa kutafsiri ikiwa tu huyo mtu amebarikiwa Karama ya upekee , sasa hizi karama zinatokana na urithi wa uzao wa familia husika ambao hutokea kwa hali ya uadimu sana kama kurithi, hivyo kama familia ina urithi wa karama ya uchawi basi andiko hilo linampatia tafsiri ya itakayomfanya kuwa mchawi na kama Karama urithi wake ni kuwa na nguvu za kijini basi tafsiri itampatia nguvu za namna hio , kama Karama ni ile ya kujua siri za malaika basi nguvu utakazopata katika andiko hilo ni maana halisi ya nguvu za kimalaika.

Yaani kuna familia ambazo ni wana Karama ya uchawi bila kujitambua na kuna familia wana Karama ya majini na kuendelea.

Unadhani ni sahihi kwa Hamza kumuamini kwa asilimia mia moja kumpatia Regina zile Fuwele ilihali ni mtu mwenye nafsi mbili?

Nani kamshambulia Hamza , utaona katika vipande vinavyofuatia kwa dokezo tu Dokta Genesha yupo hai na anasuka mipango yake kimya kimya akimtumia Hamza.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR .

SEHEMU YA 122.

Dokta Ganesha na Elementi za Nuru

(Nactivagus Umbraeus)

Hamza alimwelekeza Regina kuhusu maana ya lugha hio mpaka pale alipoona ameelewa na kuhusu namna ya kutafisiri na kujifunza nguvu ya maandiko hayo alimwambia atamwelekeza wakifika nyumbani.

Kesho yake Hamza alianza kumwelekeza Regina taratibu taratibu mpaka ilipofikia mahali Regina alijikuta akishangaa kwani alikuwa akiona maana iliokuwa katika maneno hayo.

Hamza mara baada ya kuona mafanikio hayo alimuacha na kumwambia atumie msingi aliomwelekeza na kila kitu kitajifunua kwake na Regina hakubisha aliamua kumwamini Hamza na kuanza kujifunza ili kupata maana katika lugha hio ya kimalaika.

Siku ya kwanza ilipita na ya pili yake Regina alikuwa ni kama amepata kitu kingine cha kufanya kila aliporudi kwani kazini aliendelea na kazi hio.

Ukweli hata yeye Hamza hisia zilimwambia kabisa kitu ambacho Regina atapata katika andiko hilo pengine inaweza kuwa sawa na yeye , isitoshe hata yeye mafunzo yake yalitokana na ufunuo wa lugha hio hio japo maana tofauti.

Mwanzoni Hamza alidhania akirudi tu lile Damisi litarudi na kumshambulia lakini hakukuwa na tukio lolote la kutilia shaka, ijapokuwa hakujua sababu ni nini juu ya ukimya huo , lakini aliendelea kuongeza umakini.

****

Chini ya anga juu ya bahari ilionekana boti kubwa sana ya kifahari ikielea.

Ndani ya boti hii kubwa , katika chumba kikubwa chenye mwanga hafifu sana alionekana mtu ambae amekaaa kwa kuegeamia kiti huku akitingisha glasi kwa namna ya kuizungusha iliokuwa imejaa champagne.

Ghafla tu chumba hicho kiliwaka kwa kujaa mwanga na vilionekana vitu kama skrini za vioo zilizoning’inizwa angani , zilizokuwa zikionyesha alama za kufanana kama nembo hivi na ghafla tu palepale yalionekana maumbo kama ya mshale ambayo yaliungana na kisha yakatengeneza umbo la pembe sita(Hexagram).

Dakika ileile skrini zile zilifuta zile nembo na kisha kama vile ni sinema inaanza palepale walionekana watu tofauti tofauti katika skrinni hizo , wengine wakiwa wamevalia suti , wengine wakiwa katika mavazi ya kijeshi, wengine katika mavazi ya kidini na wengine wakiwa katika mavazi ya kulalia, wanaume kwa wanawake , watoto kwa wakubwa.

“Now because everyone is here , time is precious so let’s not waste anymore time”Aliongea mwanaume ambae alionekana kuwa na umri wa miaka kama hamsini hivi kwenda sitini , alievalia mavazi ya kijeshi huku akiwaangalia kila moja.

“Dokta Ganesha tunataka kusikia maendeleo ya mpango wako mkubwa”Mmoja aliongea.

Ganesha alikuwa ndio mwanaume ambae alikuwa amekaa kivivu kwenye kiti na baada ya kuambiwa hivyo alikaa vizuri kitako na kisha aliinua juu glasi yake huku akitoa kicheko.

“General Robnson kwanini una haraka hivyo? Ni muda mrefu sana hatujaonana unaonaje tukianza na kinywaji kwanza?”

“Jenerali kwa muda mrefu ameacha kunywa pombe , Dokta acha kuzunguza zunguka , muda wetu ni mdogo sana na majukumu ya kitaifa yanatusubiri”Mwanamke wa makamo mzungu alievalia Trench coat na miwani aliongea.

“Sawa Madam Tiffanny, ukweli ambao nataka kuwaaeleza mpaka kuitisha kikao hiki ni kwamba utafiti wangu juu ya uwepo wa chumba cha nuru umetbibitika na kuwa kaburi la nuru kama ambavyo nimeweza kusoma katika kitabu, ni kama muongozo ulivyo kwani ndani yake kulikuwepo na hazina mbili ambazo zinahitaji utafiti zaidi , sina uhakika lakini kama nipo sahihi katika tafsiri yangu zitakuwa ni elementi za Nuru ambazo nilikuwa nikizitafuta kwa muda mrefu”

“Kweli? Hio ni taarifa njema sana , utachukua muda gani mpaka kukamilisha huo utafiti?”Jenerali Rob aliuliza.

Ganesha aliinamisha kichwa chake chini kama mtu ambae anafakiria na kisha akakiinua na kutabasamu.

“Ijapokuwa nimeweza kuzigundua lakini kuna mtu ambae amezichukua mapema kabla yangu na ili nisije kugundulika na jeshi la Tanzania kitengo cha Malibu ilibidi nijifiche kwanza”Aliongea.

“Nini! Ganesha unafanya nini, unajua tumetumia kiasi gani cha pesa kukutengenezea hio Mecha yako ya kibailojia , halafu unatuambia elementi ulizipata na zikachukuliwa na mwingine?”Mwanaume mwenye misharubu na kipara alievalia kanzu aliongea huku akipiga mkono juu ya meza, lakini hakumshitua Genesha kwani aliinua mkono wake na kuanza kutoa kicheko cha uovu.

“Shekh Hassani punguza presha ,uwekezaji wako wa hela za mafuta haziwezi kupotea, ni kwa muda tu hizi elementi zitakuwa katika mikono yake lakini nitafikiria mbinu ya namna ya kuzichukua , nishamdanganya mara kibao kwanini anishinde awamu hii?”Aliongea

“Nini! Unamaanisha ni yeye?”

Mara baada ya kusikia hivyo watu wote waliokuwa wakionekana kwenye hizo skrini walionyesha hali ya wasiwasi.

“Una uhakika hakujua ni wewe?”Mwanamke aliefahamika kwa jina la madam Tiffanuy aliongea na kumfanya Ganesha kutoa kicheko hafifu.

“Kama angejua mtu niliekuwa ndani ya Mecha ni mimi asingeamini, msiwe na shaka hawezi kunijua”Aliongea.

“Ni vizuri basi kama ndio h ivyo , huyu mtu kudili nae ni ngumu na uwepo wa Malibu mambo yanaweza kuleta mkanganyiko”

“Pumbavu zake sana huyu mtu , kila saa anapotokea lazima baya litokee , hatujamaliza swala la vita takatifu lakini anataka kuvuruga mpango wetu mwingine, halafu si nimesikia amejiondolea uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi na kuamua kustaafu?”Aliongea Mzee Hassan mwarabu kwa hasira.

“Inawezekana kweli ameua uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi lakini kumbuka ndio huyu huyu ambae ilimchukua miaka michache kuwa mfalme wa ulimwengu wa giza , kuna uwezekano anatumia mbinu nyingine ya mafunzo ambayo hatuifahamum ,nilivyomuona sio dhaifu kama mwanzo”Aliongea Genesha.

“Mbinu nyingine! Unamaanisha hii hii ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi au tofauti , hata kama ni hivyo ni mtu wa aina gani kufanikisha ndani ya miaka mwili tu?”Aliongea mwanaume mzungu mwenye nywele nyeupe ambae kavalia pajama.

“Mr Brandon tokea siku alipotambulishwa kama mwanamfalme wewe ulidhani ni wa kawaida?”

“Huyu mtu siku zote nawaambia ni mnyama hamnielewi, nadhani ni vizuri kukaa nae mbali la sivyo mipango yetu yote itakwama”

“Jini mmoja haogopeshi kinachoogopesha ana watu wake wengi ambao wapo nyuma yake , kama akijua mipango yetu yote mambo yatakuwa magumu sana kwetu”Aliongea Afande Rob.

“Genesha unapaswa kuwa makini sana na kutumia akili nyingi kuhakikisha unazipata hizo elementi za nuru bila kuathiri mipango yetu”

“Usiwe na wasiwasi General, lakini kwa tahadhari kwanini usiniunganishe na wanajeshi wa Nactivagus Umbra, nikiwa nao hawa sitokuwa na wasiwasi kabisa hata kama wawe ni makafiri inatosha”Aliongea Genesha huku akicheka.

“Usifikirie kabisa juu ya hilo, kama unataka wanajeshi wa Umbra kukulinda unatakiwa kupata heshima yao kwanza na si vinginevyo, ijapokuwa umefanikiwa kutengeneza hio Mecha yako ya kibailojia huna uwezo mkubwa kihivyo wa kuwafanya Umbrasi wafuate unachowaambia , unapaswa kufikiria namna ya kuhakikihsha uwekezaji wetu kwako haupotei”

“Naunga mkono hoja ,ukishindwa kutekeleza ahadi yako kwetu , basi jua ghadhabu ya night shadows itakuwa juu yako”Aliongea Hassani.

“Naombeni muwe na utulivu kila mmoja na nawaahidi sitowaangusha kabisa nyie kama wawekezaji wakuu wa mpango huu”Aliongea Genesha huku akitoa tabasamu la kujiamini na watu wale walionekana kumuamini.

Dakika chache kikao kiliisha kwa upande wa wengine lakini kwa Genesha aliunganisha mawasiliano na upande mwingine na hazikuchukua hata dakika nyimgi alionekana mwanamke mrembo mwafrika kwenye skrini.

“Profesa hatimae umenitafuta baada ya kimya cha muda mrefu , ila bado sijategemea kuongea na wewe mapema hivi”Aliongea kwa lugha ya kingereza na kumfanya Genesha kutoa tabasamu.

“Ni kama nilivyosema , wengi wenu mtaniona kwasababu maalumu pekee, nilipata taarifa ulikuwa kikaangoni na umeweza kutoka na kisha umekutana na Kuhani , kazi nzuri Frida kwa upande wako”

“Asante Profesa”

“Nipe maendeleo ya kazi yako kwa ujumla , sijaona Signal zozote juu ya mshumaa kutumika”Aliongea Genesha na kumfanya Frida kuonyesha hali ya wasiwasi.

“Profesa nipo chini ya tishio la Nightshadows kwa muda sasa , nimejitahidi kumfanya aniamini lakini bado imekuwa ngumu”Aliongea na kumfanya Genesha kutoa tabasamu la kutoridhika.

“Maneno pekee yasingeweza kumfanya akuamini ,naona hili lipo nje ya uwezo wako, nadhani napaswa kuingilia mwenyewe”Aliongea na kumfanya Frida kutoa macho.

“Profesa unataka kuingilia kivipi? Inaweza ikasababisha tulichokianzisha kukosa kabisa maana kama atajua uwepo wako”Aliongea.

“Hilo lisikuumize kichwa , ninachotaka kwasasa kutoka kwako ni ripoti kamili ya utafiti wako ndani ya Haliz Foundation , nikikuhitaji tena nitakutafuta”Aliongea na kumfanya Frida kutingisha kichwa lakini wasiwasi haukutoka kwenye macho yake lakini Genesha hakumpa nafasi kwani palepale alikata mawasiliano yale.

Baada ya kurudi kwenye benchi ndani ya maabara yake kubwa ya kisasa katika boti hio ya kifahari alisogelea skrini iliokuwa ikionyesha baadhi ya data ambazo hazikueleweka na alionekana kama mtu ambae alikuwa akifikiria chakufanya kutokana na data hizo kutomridhisha.

“Kupata pekee elementi za nuru haitoshi , napaswa kujua namna ya kuzitengeneza na njia ya kufanikisha hili ni kupata tafsiri yote ya kilichomtokea katika maisha yake ya awali kwa kile anachoota”Aliongea huku akisugua meno kwa namna ya kuonyesha kazi anayoenda kufanya ni ngumu.

*****

Ijumaa Regina alisafiri kwenda South Africa kikazi na alimwambia Hamza kuwa makini na sio kucheza huku na kule na kusababisha matatizo.

Hamza aliitikia kwa furaha kwasababu alijua kauli hio ilimaanisha Regina alikuwa na wasiwasi akimuacha atatembea na wanawake wengine , dalili za wivu wa Regina zilimfurahisha na kumhakikishia atakuwa mpole wakati wote ambao yupo safarini.

Hamza baada ya kumfikisha Regina Airport yeye aliendesha gari mpaka kazini , lakini wakati akiwa njiani alipokea simu kutoka kwa CR wa chuo akimtaarifu saa nane anapaswa kuwepo chuoni, ijapokuwa Hamza hakuambiwa kuna nini kinachoendelea ila wiki za field zilikuwa zishaisha.

Ukweli ni kwamba alikuwa ashaanza kushikwa na uvivu wa kurudi chuo kabisa na alijikuta akijiuliza ilikuwaje kwanza akawa mwanachuo, ila kwasababu ni swala ambalo amelianzisha aliona alimalize na alimwabia CR atafika muda huo.

Baada ya kufika kazini kama kawaida aliingia kwenye ofisi yake na alipoteza muda mpaka saa tano tano na baada ya hapo alitoka na moja kwa moja alielekea katika ofisi ya Eliza.

Eliza kama Kaimu mkurugenzi mkuu wa kampuni ofisi yake ilikuwa imebadilishwa na kupandishwa hadhi , ilikuwa ofsi kubwa iliosheheni hadi masofa ya kukaa watu watano, ijapokuwa haikuywa kubwa kama ya Regina lakini ilikuwa imependeza mno.

Kitendo cha Hamza kugonga na kuruhusiwa kuingia katika ofisi hio aliishia kutoa tabasamu huku akimwangalia namna mpenzi wake alivyopendeza.

Mwonekano wake tu na namna alivyokuwa akijiamini katika utendaji wake wa kazi ilimfanya Hamza kujivunia na kujiona kidume mpaka kumfanya mwanamke mrembo kama huyo kufa kuoza kwake licha ya kujua alikuwa na mke.

“Mhona umeingia tu na kuanza kuniangalia na huongei chochote?”Aliongea Eliza huku akionekana kumshangaa.

“Kwa jinsi ulivyopendeza leo , inanifanya nione ni kama umelenga kunitia ukichaa”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu.

“Kukutia ukichaa kivipi wakati haya ni mavazi ya kazini ya siku zote”Aliongea huku akijitahidi kuzuia moyo wake ulioanza kudunda kwa kasi.

“Haya sio mavazi ya kawaida , yananipa hamasa ya kuku’kiss’”Aliongea na kisha alimsogelea kwa kasi kutaka kumbusu lakini mrembo huyo alikwepesha.

“Hamza hapa ni kazini , vipi kama mtu akiingia na kuona tunachokifanya”

“Mimi jiniasi wewe nimefunga mlango kwa ndani”Aliongea na kisha palepale alimvuta Eliza kwenye kifua chake na kuanza kupeana busu nyevu na kadri dakika zilivyokuwa zikienda wote akili zilianza kuhama.

Walichokuwa wakifanya ni kama walikuwa wakiichukulia nafasi ya Regina kutokuwepo kazini kwani hawakuishia kwenye kubusiana tu bali dakika chache mbele sketi aliovaa Eliza ilikuwa imepandishwa hadi kwenye kiuno huku surali ya Hamza ikiwa miguuni na kilichosikika ni miguno ya kimahaba, kama ofisi hio isingekuwa na soundproof walioko nje wangeweza kusikia.

Nusu saa mbele Hamza alikamatia suruali yake na kuivaa huku akifunga vifungo vya shati lake akimwangalia Eliza ambae amejawa na aibu kwa kile ambacho kimetokea ndani ya ofisi.

“Umeona sasa umenichania nguo yangu ya ndani na nguvu zako”Aliongea kwa kulalamika.

Ukweli mwanamke huyo alijitahidi kumzuia Hamza asiende mbali mpaka kusex ndani ya ofisi lakini nguvu kidogo alizokwua nazo hazikumtosha kumzuia Hamza ambae alikuwa ni kama Simba aliejeruhiwa.

“Kwani lazima uvae chupi, ukitoka hapa moja kwa moja upo kwenye gari unaelekea nyumbani nani atajua hujavaa?”Aliongea Hamza akiwa hana hatia kabisa ya kile alichokifanya, pupa yake ilimfanya kurahisisha mambo na kuishia kuichana.

“Nina kikao Posta saa nane na meneja wa matawi ya benki”Aliongea

“Kwahio tunafanyaje au nimwagize Yonesi akuletee”Aliongea Hamza bila ya wasiwasi.

“Yonesi!Unataka ajue kilichotokea hapa”.

“Akijua kuna nini wakati mpo kundi moja”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la kifisi.

“Halafu wewe!”Eliza aliishia kunyoosha kidole asijue hata aongee nini, kukosa maneno huko ni kwasababu alikuwa ashajua kuna kinachoendelea kati ya Hamza na Yonesi na aligundua wakati wakirudi Dar es salaam pamoja lakini hakuwa na cha kumfanya.

Wakati akijua Hamza anatania alikuwa ashapiga simu tayari na imepokelewa na Yonesi na Hamza hakuzunguka na kumwambia Yonesi bosi wake anataka nguo ya ndani kwani aliokuwa nayo imepata matatizo ya kiufundi.

Upande wa Yonesi mara baada ya kusikia kauli hio aliishia kunyamaza kimya na kisha akatoa jibu.

“Sitaki”Alijibu kikauzu.

“Kweli! Basi hakuna shida ngoja nifikirie njia nyingine ya kumsaidia”Aliongea Hamza

“Njia gani unaweza pata kujishaua tu , naenda kumnunulia na kumletea”Aliongea na kisha alikata simu palepale bila ya kuuliza saizi ila kutokana na umbo la Eliza na Yonesi kulingana Hamza aliamini hawezi kukosea saizi.

Hamza mara baada ya kumwambia Eliza shida yake imeisha na Yonesi ameenda kununua alijikuta akiziba mdomo kwa aibu .

“Yaani ni aibu ya aina gani hii, unataka Yonesi anione ni mwanamke muhuni ambae siwezi kujizuia”

“Si umesema una kikao wewe , au ungeenda hivyo hivyo , mimi nimerahisisha kazi”

“Nisingeenda mpaka nivae , kwanza mwanamke usipovaa nguo ya ndani mbele ya watu wa heshima unakosa kujiamini” Mara baada ya kusikia hivyo Hamza palepale alimshika kiuno kwa mara nyingine.

“Saivi sina kazi za kufanya tukiendelea kumsubiria Yonesi unaonaje tukipanda mlima haraka haraka”

“Hamza jamani usiwe hivi… argh..sii”

Nusu saa baadae Yonesi alifika akiwa ameshikilia mfuko wa duka la nguo na alikuwa akificha ficha ili wafanyakazi wengine wasione , baada ya kufikia ofisi ya Eliza aligonga mlango.

“Kaimu ni mimi”Aliongea Yonesi na muda ule mlango ulifunguliwa na Hamza

“Wewe! kwanini bado upo ndani?”Yonesi alionyesha hali ya kushituka lakini palepale alishikwa mkono na Hamza na kuvutiwa ndani.

Kitendo tu cha kuingia ndani aliweza kuhisi kaharufu kalikomfanya vinyweleo kusimama na kuona aibu kiasi , aliweza kumuona Eliza aliekuwa nyuma ya meza akionekana kama mtu ambae hakuweza kusimama vizuri.

“Wewe mshenzi ulikuwa ukifanya nini mchana yote hii?”Aliongea Yonesi kwa kufoka lakini Hamza aliishia kumkonyeza.

“Unauliza wakati ushajua kilichokuwa kikifanyika”

“Fu**ck!”Yonesi alijikuta akishikwa na hasira na alichokifanya ni kupeleka mkono mpaka kwenye meza na kumpatia.

“Eliza nimekuletea”Aliongea.

“Asante sana , Yonesi usi…”Alitaka kujitetea lakini Yonesi aliingilia.

“Najua uko bize , hivyo nitaondoka na huyu mtu”Aliongea na kisha palepale alimshika Hamza mkono akimvutia nje.

“Yones haina haja ya kuwa na haraka hivyo tukae kidogo kwanza”

“Wewe na bichwa lako , unataka kubakia hapa uendelee kufanya nini, Eliza hana mafunzo yoyote na ukiendeleza ushenzi wako unadhani ataweza kuhimili , mtu unaonekana sio wa kawaida lakini unataka kwenda nae sambamba..”Aliongea wakati wakiwa nje.

“Inaonekana mna mahusiano mazuri sana wewe na Eliza mpaka kuanza kumtetea”

“Nimefahamiana nae kwa miaka mitatu na tuliishi kwenye jengo moja kwanini tusiwe marafiki”

“Basi usiwe na wasiwasi siwezi kwenda mbali , pale hajachoka sana bali ni aibu tu ya kukuangalia ndio maana”

“Huna haja ya kunielezea ushenzi wako mimi , unaonekana kuwa muhuni sana, kaa na mimi mbali kwanzia leo”Aliongea na kisha aliondoka bila ya kugeuka nyuma.

Hamza aliishia kusimama akimwangalia mwanamke huyo na kujiambia kama ni Yonesi wanaweza kusumbuana kwa masaa mengi bila kuchoshana.

Wakati akipanga kuelekea mgahawani kwa ajili ya chakula cha mchana simu yake ilianza kuita na alipoangalia aliekuwa akimpigia aliona ni Dina, kuona tu hivyo tumbo lilianza kuingiwa na joto maana alishajua alikuwa ameshamsahau Dina kwa mara nyingine.

“Babe Dina vipi umesharudi , siku ile uliniambia utakuwa nje ya mji kwa siku kadhaa”Aliongea Hamza akiwahi kujihami.

“Nilisharudi muda mrefu tu , ila nimesubiri utimize ahadi yako lakini wapi , Hamza kama hunipendi ni bora uongee tu kuliko kunitesa”Aliongea.

“Dina si…”Hamza kabla hata hajaongea chochote simu ilikatwa palepale na kumfanya akunje sura.

Mpango wake wa kwenda kula chakula ulivurugika palepale na kuona cha kufanya kwanza ni kwenda Kijichi kumpoza mrembo huyo na kisha ndio alekee chuo , muda alikuwa nao na aliona masaa mawili yalikuwa yakimtosha sana.

Baada ya kuingia kwenye gari yake kwasababu ilikuwa mchana hakukuwa na foleni na nusu saa tu alikuwa ashafika na kupokelewa na Lawrence.

“Bro madam kaniambia hataki kukuona tena , sijui itakuwaje maana kaniambia ukija nisikiruhusu”Aliongea Lau kwa upole .

“Ndio maana upo hapa nje?”Aliuliza na alitingisha kichwa kukubali.

“Lakini lazima nionane nae , unaonaje nikikuzimisha kwanza ndio niingie”Aliongea.

“Hapana bro , hata kama kanikataza usiingie lakini njia ipo wazi”Aliongea Lawrence maana alijua Hamza sio mtu wa utani.

Hamza alienda moja kwa moja mpaka katika chumba anacholala Dina na aliweza kumkuta akiwa amejilaza kitandani kama mwanamke ambae ameachwa ghafla.

“Dina!”Aliita Hamza huku akisogea karibu na kitanda chake akitaka kumshika lakini muda uleule Dina alifyatuka na mguu mmoja na kwenda kumpiga kifuani.

“Arghhh… umenipiga nilipoumia na kutonesha kidonda”Aliongea akiigiza maumivu.

“Acha maigizo , kwa mwili wako unadhani sijui hupati maumivu wewe”

“Mimi ni binadamu kwanini nisipate maumivu?”

“Ndio wewe ni binadamu unasikia maumivu ndio maana hujali ya kwangu”Aliongea.

“Dina mpenzi najua nimekosea kutokukutafuta siku hizi chache , nisamehe na kwanzia sasa nitakutafuta kila siku”Aliongea Hamza huku akijaribu kumkumbatia Dina lakini mrembo huyo alikunja sura palepale.

“Unanukia harufu ya mwanamke na kama sikosei hii harufu itakuwa ni ya Eliza si ndio?”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Hamza kukaa kimya na lilikuwa jibu tosha kwa Dina.

“Hamza naomba uondoke sioni haja ya kuendelea kukulazimisha kuwa na mimi ilihali naijua nafasi yangu kwenye moyo wako”

Mara baada ya kauli ile mrembo huyo alikimbilia bafuni na kufungulia shower.

Hamza aliishia kusimama huku akikuna kichwa na kujiuliza inamaana Dina anaoga , ila kwasababu hakutaka kuondoka bila kutatua tatizo, dakika ileile alivua nguo zake zote na kisha alizama bafuni.

“Wewe unafanya nini toka…”

Hamza hakumpa nafasi ya kuongea na kumshika kiuno kwa nyuma wote wakiwa uchi na sekunde chache mbele kilichoweza kusikika ni miguno ya kimahaba kutoka kwa Dina.

Zilipita dakika arobaini na tano Hamza ndio alimtoa na kwenda kumkalisha kitandani mrembo huyo akiwa amechoka na hasira zote zikiwa zimemuishia na kumwangalia Hamza kwa jicho la kulegea.

Alijiona ni mdhaifu sana kwa Hamza na yote hio ni kutokana na namna ambavyo alikuwa akimpenda , alipanga kumkalia kimya muda mrefu ili kumpa fundisho lakini matokeo yake yeye ndio alipewa fundisho.

“Babe njoo ukae hapa nikukaushe nywele basi nataka tuondoke”Aliongea Hamza.

“Tuondoke kwenda wapi?”

“Nimeambiwa niwasili chuo saa nane na sasa hivi ni saa saba hii , tunaenda Date ila tunaanzia chuo”Aliongea Hamza na kauli ile baada ya Dina kuifikiria alikubali mara moja huku furaha ikimwingia , alijua nini ilimaanisha kwenda na Hamza chuoniu, watu wengi wangewaona na Hamza angemtambulisha pengine kwa marafiki zake.

Nusu saa mbele alikuwa ameshavaa na staili yake ya uvaaji ilikuwa ni ile ya kuendana na mazingira ya chuo kabisa , alikuwa ni pisikali haswa na kumfanya Hamza kufikiria chuoni siku hio kutachimbika.

Baada ya kutoka hata Lawrence alishangaa kumuona bosi wake na uvaaji wake.

“Bosi mpaka nimekusahau”Aliongea Lawrence na kumfanya Dina kucheka.

“Lawrence tutaonana baadae naelekea na huyu mrembo matembezini”Aliongea Hamza na kumfanya Lawrence kupiga saluti na kisha alimwingiza kwenye Maybach na wakaondoka.

Nusu saa mbele Hamza aliweza kufika chuoni na wakati gari hio inaingia chuoni hapo kila mwanafuzi aliekuwa karibu na maegesho aliwaangalia kwa matamanio makubwa , isitoshe hata magari ya maprofesa waliokuwepo hakuna lililokuwa na thamani kuzidi Maybach alioingia nayo Hamza.

Kitendo cha Hamza kushuka katika gari hio na Dina kufuatia kwa wale wanafunzi wachache waliokuwa wakimjua Hamza walimshangaa mno ni kama hawakuwa wakiamini ni yeye.

“Ulikuwa ukijua kutakuwa na wanafunzi wengi namna hiii nini?”Aliuliza Dina.

“Hehe .. sikujua ila si ndio vizuri nakwenda kuwaringishia , sidhani kuna ambae anakuzidi kwa uzuri”Aliongea na kumfanya Dina kujikuta kama malaika, ule ubosi wa kumiliki mtandao wa Chatu ulipotea kabisa na hapo alikuwa kama msichana ambae anategemea kila kitu kwa mwanaume wake, hisia hizo zilimfanya kujisikia vizuri sana.

“Hamza Bro..”Sauti iliita nyuma yao na kumfanya Hamza kugeuka na palepale aliweza kumuona Amiri alievalia shati la mikono mirefu , ilionekana na yeye pia alikuwa chuo.

Amiri mwanzoni hakumjua mwanamke aliekuwa nae ni Dina na mara baada ya kumuona macho yalimtoka kiasi na kupotezea mshangao wake.

“Madam shemeji tunakutana tena”Aliongea Amiri na kumfanya Dina kutabasamu.

“Uko poa Amiri?”

“Niko poa kabisa Madam , karibu chuoni kwetu”Aliongea.

“Nimemleta shemeji yako leo kidogo aangaze aangaze macho”

“Haha.. kaka umejua kumleta kweli , umetisha sana”

“Unamaanisha nini?”

“Wewe huoni macho ya watu wanavyokuangalia”

“Hawaniangalii mimi , wanamwangalia Dina mwanamke mrembo kuliko wote hapa chuoni”Aliongea Hamza na kumfanya Dina kumfinya.

“Baada ya hapa unachukua uelekeo gani bro, unaonaje tukijumuika pamoja jioni ya leo wewe na Madam na mimi na Mellisa , halafu sijawahi hata kukutambulisha kwa Mellisa”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kuona sio mbaya.

“Unaonaje?”Alimuuliza Dina na alitingisha kichwa kukubali.

“Itakuwa vizuri zaidi , pia naweza kusikiliza ulipoishia kwenye lile swala”Aliongea Hamza na Amiri aliishia kutoa tabasamu la furaha na kisha kuwaacha wakikubaliana jioni hio walekee Kidimbwi.

Hamza alimchukua Dina na kwenda kumuacha kwenye bustani na kumwambia amsubiri anaelekea ofisini kuonana na mkuu wa chuo.

“Nikajua unaongana na wenzako , si umesema kuna kikao sijui?”Aliuliza.

“Ndio lakini nimekuja kutokana na sababu nyingine leo”Aliongea Hamza na kumfanya Dina kuhisi sababu ya Hamza kuja chuoni hapo..

Nusu saa mbele Hamza alirudi lakini baada ya kusogea sehemu aliomuacha Dina aliona kuna mwanaume aliekuwa amekaa pembeni yake na alionekana alikuwa akimbembeleza Dina kumpa namba yake.

“Oya kaa mbali na mpenzi wangu , ashachukuliwa huyu”Aliongea Hamza kibabe.

“Ni mpenzi tu huyu kwako acha kupaniki bro , kama hujamuoa nafasi na mimi pia ninayo”Aliongea huku akiangalia mapaja ya Dina yaliokuwa wazi , maana mrembo huyo na yeye ni kama alikuja kukomoa wanachuo marijali, maana gauni alilovalia halikuwa refu sana.

“Kwahio hutaki kuondoka na unaleta ngumu?”

“Nikipata mawasiliano yake nitaondoka , kuwa muungwana basi nimalizane nae”Aliongea yule bwana kwa kujiamini na kumfanya Hamza akunje sura palepale na hakutaka kumchelewesha kwani alimshika kola ya shati kwenye shingo na kumvutia nyuma yake na kutokana na Hamza kutumia nguvu kiasi ilimfanya yule bwana kwenda kujigonga kwenye kimbweta na damu kuanza kumtoka palepale.

Tukio lile lilishihudiwa na watu wengi na mmoja wapo alikuwa ni Anitha , mwanamke ambae alishaanza kumtaka Hamza kwa kasi , haikuwa sahihi kumpenda kwasababu alimuona Hamza ni wa hadhi kutokana na kumuona na warembo kadhaa wa hadhi ya juu ikiwemo Irene na leo hio Dina.

Hamza hakutaka kupoteza muda wala kuangalia yule bwana hali yake ipoje kwani alimshika Dina mkono na kisha kumuondoa eneo hilo mpaka kwenye maegesho ya magari.

“Hakukuwa na haja ya kumfanyia vile Hamza”Aliongea Dina huku akitabasamu.

“Alitaka kuniletea ujuaji mbele ya mpenzi wangu , unadhani ni kipi ambacho alistahili , halafu na wewe imekuwaje ukakaa nae halafu mimi kidume wako nipo”

“Alikuwa king’ang’anizi nilimwambia mpenzi wangu anarudi ila hakutaka kunisikia”Aliongea.

“Ni kwasababu ya jinsi ulivyovaa , lazima atakuwa amepagawa , ole wako uvae hivi tena”Aliongea.

“Inamaana hukuona nimevaa hivi wakati tunatoka?”

“Nimekuona ndio , ila jinsi ulivyokaa nae vile si kama ulikuwa ukimtega halafu unaniuliza”Aliongea Hamza na kumfinya kwenye mapaja yake na kumfanya Dina kucheka.

Alikuwa akifurahia maisha ya kuwa msichana wa kawaida na sio bosi ndio maana alimtengenezea Hamza mazingira ya kushikwa na wivu lakini hakutegemea italeta shida.

“Nina njaa tukale kwanza , au unaonaje?”Aliuliza na Dina alitingisha kichwa kukubali.

“Heka heka naona zimekuwa nyingi mjini”Aliongea.

“Ni maandalizi ya uapisho wa rais”Aliongea na kumfanya Hamza kukumbuka zoezi la kutangaza matokeo limekwisha kumalizika.

“Nani kashinda?”

“Kuna haja hata ya kuuliza ni Abubakari”

“Huyu ndio alierithi nafasi ya yule aliefariki sio”

“Ndio , halafu hata hukuniuliza nini kiliendelea baada ya pale”Aliongea Dina.

“Ulisema utabakia kule kwa siku kadhaa , kuna kilichotokea?”

“Mtoto wa mstaafu Mgweno alinitafuta baada ya kuondoka tu akihitaji kuongea na mimi”

“Mtoto wa Mgweno! Alikuwa akitaka nini?”Aliuliza Hamza na muda huo alikuwa akiingiza gari Peacock hoteli na kuegesha.

SEHEMU YA 123.

Ilibidi wasitishe maongezi yao kwanza na kuingia ndani ya mgahawa na kwenda kukaa.

Hamza alikuwa mzoefu ndani ya hilo eneo na alichagua siti ileile ambayo alikaa na baba yake Prisila wiki kadhaa zilizopita.

Baada ya kuketi waliletewa menu na kila mmoja aliagiza chakula alichopenda na kuandaliwa.

“Kitendo cha Wanyika kuweza kuingiza mtu wanaemtaka ikulu imemuathiri sana Mgweno katika harakati za kuitawala Tanzania nje ya ikulu, ndio maana anaonekana kuwa desparate kutaka kurudisha ushawishi wake upya, kitendo cha kuyumbisha umoja wa makomandoo lilikuwa pigo kwake , kwani wanajeshi wengi ambao walikuwa ndani ya ule umoja wanaamini yanayoendelea na kutochukuliwa siriasi na serikali kwasababu Mgweno nguvu yake imeshuka mno serikalini na amebakia kuwa mstaafu mfanyabiashara na sio mwanasiasa mwenye ushawishi”

“Unamaanisha nilichokifanya kilileta matokeo makubwa?’”

“Licha ya kwamba siku ile wanachama hawakuwa wote lakini lile tukio limetengeneza mgongano mkubwa serikalini , kwa intellijensia ilionifikia kuna waliokuwa wakishinikiza uchukuliwe hatua , ila upande mwingine uliokuwa ukiongozwa na mshauri mkuu uliweka ngumu , kilichomshangaza Mgweno mwenyewe ni kwamba wale ambao alikuwa akiwaaamini walihamia upande mwingine na kumsaliti”

“Sishangai sana , watu wapo na wewe wakiwa na cha kufaidika, kwahio wamehamia upande wa familia ya Wanyika?”

“Wengi wamesema wapo neutral lakini mioyo yao ipo upande huo, tukio lile limempunguzia sana Mgweno ushawishi wake ndani ya jeshi na kuongeza ushaiwishi kwa upande wa familia ya Wanyika na kitendo cha kumuweka Abubakari Ikulu maana yake sasa hivi wana udhibiti wa kitengo cha Malibu na Ikulu , ni sawa na kusema wameshikilia nchi nzima”Aliongea Dina.

“Kwahio huyo mtoto wake alitaka nini kutoka kwako?”Aliuliza.

“Anataka kuunganisha nguvu zake na mimi , yaani biashara zao zote ambazo hazikuwa zikipita kwenye network yetu zipitie na kunipa maeneo ambayo yalikuwa chini yao kwa masharti ya kumsapoti kwenye harakati zake za kisiasa”

“Harakati za kisiasa?!”

“Ndio anasema baba yake amekosea kukuchokoza wewe na kampuni ya Dosam na makosa ya baba yake yanafifisha ndoto zake za kuwa rais na njia pekee ya kurekebisha ni kusalimisha kila kitu upande wetu, wakiamini kwamba kujisalimisha kwangu ndio kujisalimisha kwako”Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu.

“Inaonekana nafasi yako inazidi kuimarika katika ulimwengu wa giza ndani ya Tanzania , kama amejisalimisha kwako inamaana waliokuwa wafuasi wake si watakuwa chini yako pia?”

“Ndio licha ya kwamba Mgweno amepoteza nguvu nyingi katika upande wa siasa lakini upande wa biashara yupo vizuri , kampuni nyingi ana hisa zake kwa majina tofauti tofauti na kama unavyojua hakuna kampuni inayoendesha biashara zake kwa kutegemea ulimwengu wa kawaida pekee, lazima kubalansi na ulimwengu wa giza , sasa hivi nimekuwa kama mmiliki wa barabara , wakitaka kupita wanalipia ushuru kwanza, nisipotaka wasipite hata ushuru wao sipokei”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa na kumnyooshea dole gumba.

“Inabidi nikuite Queen of undewoild”Aliongea na kumfanya Dina amwangalie na jicho la pembeni na walijikuta wakiishia kucheka.

“Kwahio sasa hivi hawawezi kumsumbua tena Regina na wale wanawake walinzi si ndio?”

“Rafiki yako anahakikisha kila kitu kinaenda sawa , unawasiwasi gani?Sidhani kama watapata shida tena”Aliongea na kumfanya Hamza kuridhika.

Baada ya kufanya shopping ya nguvu Hamza alimchukua Dina na kukutana na Amiri na safari ya kwenda Kidimbwi ilianza.

Mellisa mpenzi wake na Amiri alionekana kumfahamu Hamza lakini upande wa \Hamza Hamza alimuona mwanamke huyo kupitia picha pekee.

Alikuwa mrembo haswa kwa macho ya karibu , ilikuwa haki kwa Amiri kufa na kuoza kwa mpenzi huyo.

“Ulifanikiwa kukaa nae chini?”Aliuliza Hamza mara baada ya Mellisa kuonekana kuwa bize akiongea na Dina.

“Niliongea nae kaka, kuna vitu ambavyo ameniambia na vimenishangaza kidogo, kasema nisimwambie mtu lakini kwasababu wewe ni rafiki yangu sidhani kuna haja ya kukuficha”

“Ni vitu gani?”

“Alikiri alikuwa ni mteja wa muda mrefu wa dawa wanayoita viungo vya akili , alinielekeza kila kitu kaka mpaka nikajua kuhusu swala la vyungu na mambo megine , inaonekana kuna dawa mpya kama madawa ya kulevya ambayo watu hutumia kujitoa ufahamu”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia Amiri kwa udadisi zaidi.

“Ulimuuliza ilikuwaje mpaka akajiingiza kwenye mambo kama hayo?”

“Anasema ilianza kumtokea nje ya nchi alipokuwa akisomea masters yake, alikutana na msichana mmoja raia wa Ukraine ndio aliemfundisha kutumia , baada ya masomo aliacha kabisa kutumia lakini wakati akiwa hapa nchini rafiki yake huyo alimwambia kama anataka kupata udhoefu wa kujitoa ufahamu na kuona ulimwengu uliopo nje ya mawazo yetu anaweza kumuunganisha na mtu ambae anaweza kumpatia huduma.anasema mwanzoni alikataa lakini baada ya muda aliishia kukubali na ndio alianza kuletewa Delivery

“Na nani?”

“Hawajawahi kujitambulisha kwake , yeye alikuwa akipokea tu Delivery mara mbili kwa wiki na alikuwa akipata bure, baada ya kumuuliza rafiki yake alimwambia anaweza kupata bure kabisa ila ratiba za kupokea mzigo zitakuwa zinabadilika badilika”Aliongea

Hamza alifikiria kidogo na kuona ni swala ambalo linawezekana , ila alishindwa kujua kwanini hakuwa akilipia ilihali Frida alionekana kununua kwa kiasi kikubwa cha pesa.

“Kwahio umepanga kufanya nini , unaacha atumie au mnaendeleza?”

“Kaka hata bado nashindwa kuwa na msimamo , akiacha anashikwa na ndoto mbaya sana usiku na kushindwa kabisa kulala , ni kama kilekilichokuwa kikimtokea tulivyokuwa nje ya nchi”Aliongea na Hamza aliona hapo kuna kasheshe.

“Inabidi kwanza uchunguzi ufanyike kuna makusudio gani yanalengwa mpaka kupewa ratiba maalumu na dawa hizo bure’

“Mimi kuna kitu nimegundua kaka , unakumbuka ile sauti niliokusikilizisha siku ile?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa.

“Sasa ukisikiliza ile sauti ni kama Mellisa anaongea na mtu , juzi wakati napitia pitia mitandaoni nilikutana na bandiko linalohusiana na viumbe ambao wanavumishwa wanaofahamika kama nightshadows”

“Umepata nini?”

“Kaka mwandishi alichoandika mtandaoni licha ya kuonekana uzushi kwa watu wengi , ila hili swala la Melisa vinaendana sana , anasema ni dawa za kufanyia mawasiliano kati ya roho na roho , kwasababu nightshadows ni viumbe kutoka sayari nyingine ambao hawana miili na wapo kama roho , wakitaka kuwasiliana kutoka umbali mrefu kuja umbali mwingine ndio hutumia njia hii , nimejaribu kufikiria nikaona ni kweli na pengine hizi ratiba za Mel;lisa kuletewa vyungu ni kwasababu hio”Aliongea Hamza na hata yeye alikumbuka siku moja alishawahi kusoma kitu kama hicho mtandaoni lakini hakumaliza.

“Inawezekana lakini inahitaji uchunguzi zaidi”

“Najua kaka , lakini uchunguzi naanzia wapi kama hili ni kweli, nimejaribu kufuatilia ile kampuni na majibu pia sikupata na kwasasa nahisi kama nimestuck na nashindwa kumsaidia mpenzi wangu”Aliongea kwa kutia huruma huku akimwangalia Mellisa aliekuwa mbele yake.

“Ngoja nitakusaidia , kama unavyosema ni kweli nahisi ukimwambia aache mara moja haitowezekana na ataishia kushikwa na hizo ndoto na mfumo wake wa maisha unaweza kubadilika mara moja , kwanza nitafanyia uchunguzi na nikipata majibu nitakuambia cha kufanya”Aliongea Hamza huku akijiambia kama watu wa binamu ndio wanahusika katika hili basi haina budi kuingilia isitoshe ni swala ambalo lilionekana kuathiri watu , mtu ambae aliona anaweza kumsaidia kupata majibnu yake yote ni Alex hivyo anapaswa kumbananisha.

Baada ya kufurahia pamoja kwa kunywa na kula, usiku Hamza alirudi moja kwa nyumbani kwa Dina na waliendeleza walipoishia mchana.

Usiku ulikuwa mfupi sana kwa Hamza lakini upande wa Dina alionekana kuridhika na wakati ikiwa ni saa mbili asubuhi simu yake ilianza kuita na alisimama na kumsogeza Dina pembeni.

Hamza mara baada ya kushika simu ile alishangaa baada ya kugundua ni Regina ambae anapiga.

“Dina ni mke wangu anaepiga usipige kelele”Aliongea Hamza kwa tahadhari kwani hata yeye alishitushwa na mwito wa simu hio.

Dina wala hakujali alichokifanya ni kukumbatia kiuno cha Hamza na kisha akaendelea kulala.

“Wife kuna kilichotokea asubuhi asubuhi huko kwa Madiba?”Aliongea Hamza akijitahidi kusafisha koo.

“Ushaamka?”Regina aliuliza na Hamza kwasababu alijua Regina yupo nje ya nyumbani kikazi alikuwa hana hofu kabisa.

“Nipo kitandani bado , vipi umenimiss?

“Mh.. kidogo, vipi jana ulienda kazini?”

“Ndio nilienda na nilifanya kazi vizuri”Aliongea na upande wa pili ulinyamaza kidogo , ilionekana ni kama Regina kuna kitu alichokuwa akinywa.

“Upo nyumbani?”

Hamza mara baada ya kusikia swali hilo aliishia kumwangalia Dina aliekuwa pembeni yake na kutoa tabasamu la uchungu .

“Ndio nipo nyumbani nikimsubiri mke wangu kwa hamu zote arudi”

Hamza hakuwa na hofu kwa kudhania Regina anaweza kumuuliza Shangazi , alijua shangazi ni mtu mzima na asingemchomesha kwa namna yoyote ile kama hakurudi kabisa..

“Kama upo nyumbani fungua droo ya meza kulia kwako”

“Kuna nini ?”Aliuliza Hamza akiwa katika hali ya mshangao.

“Nimeweka hela za dola kwenye droo , nataka uziangalie na unitajie namba tatu za mwisho kwenye noti ya juu kabisa”Aliongea

Hamza mara baada ya kuingia kwenye mtego huo mwili wake ulishikwa na baridi , maana aliona ni kama Regina alikuwa akimchunguza na alijikuta akishindwa kujua namna ya kujibu.

“Unanidanganya si ndio?”

“Hapana , ukweli ni kwamba jana niliziona na nikazibeba zote kutokana na kuboreka kukaa mwenyewe nilienda kunywa mvinyo, Regina mke wangu unaonaje ukiwahi kurudi , nishaanza kukuzoea unajua”Aliongea Hamza huku akijambia staili hio hawezi kukamatika kwa namna yoyote.

Regina aliishia kuwa kimya kwa dakika kadhaa

“Sijaweka hata mia kwenye droo zako”

“Eee…!”

Hamza alitamani kujichapa ngumi ya shavu , alikuwa amesahau Regina alikuwa ni mwanachama wa watu wenye IQ kubwa duniani, ilikuwa hasara kwake kujifanyisha ana akili zaidi yake.

Dina alikuwa amejifanyisha kulala tu ila baada ya kusikia maongezi hayo na namna Hamza alivyobadilika alishindwa kujizuia na kuachia kicheko kikubwa.

Regina upande wa pili hakukuwa na namna ashindwe kusikia kicheko hiko.

“Nadhani nimepiga muda mbaya , samahani kwa usumbufu ..”

Kauli hio ilimfanya Hamza kuhisi ubaridi wa mifupa na aliishia kukubali kusihndwa maana hakukuwa na namna.

“Regina .. nimekosea…”

“Tii.. tii”

Hakutaka hata kuendela kusikia kile ambacho Hamza anataka kuongea kwani alikata simu mara moja.

Hamza alijikuta akijaribu kupiga tena lakini alichosikia ni simu iko bize na alijua palepale alikuwa amelimwa tofari.

“Sh*** keshanipiga tofari”Aliongea Hamza aking’ata meno yake kwa wasiwasi.

“Usije kunilaumu tu wakati mmenichekesha wenyewe , haikuwa na haja ya kudanganya kama angeuliza wewe ungemwambia upo nje mazoezini na sio kujifunga”

“Sikutegemea atanipa mtihani wa maswali ndio maana , kwasasa sina namna zaidi ya kusubiri arudi mchana nitajua namna ya kumbembeleza”Aliongea

“Unapanga kwenda kumpigia magoti kuomba msamaha?”Aliuliza Dina kwa shauku kubwa.

SEHEMU YA 123.

Hamza aliishia kumshika Dina pua kwa namna ya kumfinya.

“Naonekana kama mwanaume ambae naweza kumpigia mwanamke magoti kirahisi?”

“Unaonekana kama mtu ambae utaenda kupiga magoti , mwonekano wako wakati ukiongea nae sijawahi kukuona nao tokea nikujue”

Kauli hio alihisi ni ya uchokozi na alitaka kugeuka na kumpiga kibao cha makalio lakini alikuwa ashajihami kwa kujifunika na shuka na kusogea mbali.

“Usinisogelee tena siwezi kufanya tena nimechoka”Aliongea na Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijihisi kidume , ukweli hakuwa akipanga kupoteza muda kucheza na Dina tena kwani jana alimuahidi Irene atamsindiza kwenda kununua gari.

Alijua msichana alikwisha kununua gari mara baada ya k umkatia simu siku mbili zilizopita lakini jana aliomba tena kwenda nae na aliishia kukubali.

Hamza aliona atamaliza mapema miadi hio na Irene na kisha mchana Regina lazima atakuwa amerudi maana South Africa hapakuwa mbali , ukweli alijiona alikuwa na kazi kubwa sana siku hio.

Baada ya kuoga na kuvaa nguo zake alimuaga Dina na kisha aliingia kwenye gari lake na kuondoka, wakati akiendesha simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaempigia alikuwa ni Prisila na Hamza alipunguza mwendo kidogo huku akikumbuka hakuongea na mwanamke huyo kwa muda mrefu.

“Niambie mrembo , umenikumbuka leo”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.

“Nikajua baada ya kunifahamu kama rafiki yako wa utotoni utakuwa unanikumbuka , nadhani mimi ndio ninaekukumbuka peke yangu”Sauti ya kulalamika iliongea na kumfanya Hamza kukunja uso.

“Nakukumbuka sana tu ila mishe mishe zimekuwa nyingi”

“Mh..!Uko wapi kwanza, mbona kama unaendesha?”

“Ndio niko barabarani?”

“Njoo Palm Village hapa basi unichukue kama haupo bize”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria na kujiambia kuna nini mpaka ampigie simu na kumwambia amfuate lakini hakutaka kuwaza sana , kwasababu ndio uelekeo anaoenda aliona akubali tu.

“Sawa nakupitia ndani ya dakika chache zijazo”

“Okey”

Hamza mara baada ya kukata simu aliona kwanza ampigie Irene simu ili kujua yupo wapi na mrembo huyo alimwambia yupo Kinonfoni B anamsubiri , Hamza hakujua anafanya nini hapo ila aliendesha uelekeo huo na alichukua dakika chache sana mpaka kufika na kumkuta Irene akisubiria pembezoni mwa kituo na baadhi ya watu wanaosubiria daladala.

“Ingia basi , safari inaendelea hii”Aliongea Hamza akiwa ameshusha kioo.

“Niambie kwanza kama nimependeza niingie”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka na hata baadhi ya watu waliokuwa nyuma yake waliishia kutabasamu kwa utoto aliokuwa akifanya.

“Haya umependeza”Aliongea Hamza kuepusha shari na Irene alizunguka haraka haraka na kuingia.

“Ulivyoongea ni kama sifa hazitoki moyoni vile”

“Unamaanisha nini?”

“Mkeo anaweza kuwa mrembo kunizidi , lakini mimi tabia yangu ya U’cute inanifanya nipendeke kirahisi”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka.

“Nani kakuambia unatabia ya U’cute”

“Watu wengi tu ,wazazi wangu na ndugu zangu na hata wanaume wanaonitaka , halafu umechelewa nimeombwa sana namba ya simu”

“Na ukawapa?”

“Sio wote wakaka wawili mmoja anaendesha BMW na Caddilac nimewapa “

“Kwanini umewapa sasa unataka wakusumbue?”

“Unasikia wivu kuwapa namba yangu?”

Hamza aliishia kukaza macho barabarani maana alijua hawezi kumshindwa msichana huyo kwenye maneno.

“Huko kuna showroom ya magari , kwanini tusielekee Posta nasikia Slipway kuna magari mazuri ya Mjerumani”Aliongea.

“Unataka magari ya Mjerumani , hela unayo lakini?”

“Sikosi la bajeti yangu”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa kumwelewa.

“Kuna mtu namchukua hapo Palm Village na kisha tutageuza”Aliongea na Irene alionekana kuelewa.

Hamza mara baada ya kuendesha gari kwa dakika kadhaa aliweza kufika chini ya majengo ya Palm Village na kabla hata hajapeleka gari yake maegeshoni waliweza kumuona Prisila akiwa amesimama nje huku pembeni yake kukiwa na mwanaume mtanashati hivi alievalia suti akiwa ameegamia boneti ya gari.

“Unaemchukua hapa ni dada Prisila?”Aliuliza Irene na kumfanya Hamza kumwangalia.

“Unafahamina na Prisila?”Aliuliza Hamza lakini muda ule ni kama Prisila pia aliwaona Hamza na Irene kwani aliwapungia mkono na kumfanya mwanaume ambae ameegamia kwenye gari kugeuka na kuangalia upande wao na Hamza palepale aliweza kujua kwanini mwanamke huyo alimwita.

Alikuwa ni Chriss , ijapokuwa alikuwa amehisi ni yeye tokea mwanzo lakini hakuwa na uhakika.

“Nisubiri kwenye gari nakuja”Aliongea Hamza na kisha alishuka.

Upande wa Prisila alionekana kuwa na ahueni mara baada ya kumuona Hamza amefika lakini upande wa Chriss hakufurahishwa na ujio wa Hamza pale.

“Prisila umemuita?”Aliuliza Chriss.

“Nilikuwa na miadi nae asubuhi ndio maana”Aliongea na kumfanya kukunja sura.

“Prisila unajua ni kwa kiasi gani nimekuwa nikipenda tuwe wapenzi, ukaribu wako na Hamza unanifanya nihisi kuna kinachoendelea kati yenu, ni kheri uniambie nijue moja”Aliongea na muda huo Hamza alikuwa ashakaribia tayari lakini hata licha ya kuwa mbali aliweza kusikia anachoongea.

“Chriss nadhani tushaongea hili na tumemaliza na matarajio yangu nikunielewa , siwezi kuijilazimisha kukupenda Chriss”

“Prisila hilo sio jibu ninalotaka?, Ninachotaka kujua ugumu unaoniwekea ni kwasababu ya Hamza au vipi, umebadilika sana tokea atokee kwenye maisha yako”

“Niwape nafasi au tunaondoka Prisila?”Aliongea Hamza.

“Jiongeze tu”Aliongea Chriss , ijapokuwa alikuwa akimchukia lakini alikuwa akimhofia vilevile alishazipata habari ndio aliehusika na kifo cha Saidi na James hivyo alikuwa na tahadhari kubwa.

“Hapana nishamaliza kuongea nae tunaondoka , Saidi safari njema huko uendako nakutakia baraka ya kupata mwanamke utakaempenda mzuri zaidi yangu”Aliongea Prisila na kisha alianza kupiga hatua kusogea ueleko wa gari ya Hamza.

“Prisila subiri..”

“Safari njema kaka”Aliongea Hamza asijue hata ni safari gani anaelekea, ukweli sio kwamba alikuwa akimuwekea kiwingu ila alionekana kama usumbufu kwa Prisila na alifanya hivyo kumsaidia , isitoshe Prisila alisumbuliwa na Saidi na mwisho wa siku akaingia kwenye matatizo , hakutaka na Chriss kuja kumwingiza kwenye matatizo , isitoshe alikuwa akijua mwanaume akionekana kumn’gang’ania mwanamke ambae hampendi hayo sio mapenzi bali ni tamaa tu.

Chriss aliishia kung’ata meno yake kwa hasira huku akiwaangalia wakiondoka mbele yake.

Nitarudi”Aliongea kwa kusaga meno na kisha aliingia kwenye gari yake na kuiondoa kwa hasira.

Upande wa Prisila mara baada ya kumuona Irene ndani ya gari ya Hamza alionyesha kushangaa.

“Irene!Unafanya nini kwenye gari ya Hamza?”Aliongea kwa wasiwasi maana alihisi pengine Hamza anatembea na Irene.

“Irene alikuwa mwanafunzi wangu huyo, sikujua kama mnafahamiana”Aliongea Hamza na kisha alizunguka upande wa dereva na kuingia garini.

“Tangu lini ukawa mwalimu?”

“Dada Prisila usiwe na wasiwasi , alikuwa akinifundisha twisheni nyumbani kipindi”Aliongea Irene na kumfanya Prisila kuvuta pumzi ya ahueni.

“Unaonekana ulikuwa na kazi nyingi sana?”Aliongea Prisila akimlenga Hamza.

“Ukiwa huna hela kila kazi unaweza kufanya”Aliongea na kumfanya atabasamu.

“Kwahio mlikuwa mkienda wapi, naona kama ni mtoko huu?”

“Dada Prisila naenda kununua gari , nimemuomba Hamza anisindikize?”

“Kununua gari , una leseni tayari?”

“Ndio ninayo”

“Mnafahamina vipi kwanza , wewe na Irene?”Aliuliza Hamza.

“Baba yake Irene rafiki yake mkubwa ni baba , wakati Irene anazaliwa tulikuwa majirani nilimpenda sana Irene wakati akiwa mdogo na kufanya mama yake muda wote aniachie niwe namwangalia”

“Dada Prisila unaongea kama vile hunipendi sasa hivi”

“Wakati ukiwa mdogo ulikuwa kazuri mno , kila mtu alikupenda na kutamani kukubeba”

“Inaonekana ulijipatia mdogo wako wa hiari ulivyokuwa mdogo”

“Sio nilikuwa, hata sasa hivi , Irene ni mdogo wangu na ukae nae mbali”Aliongea Prisila akiwa siriasi.

“Nikae mbali kivipi , kama Irene ni mdogo wako na mimi ni kaka yake”Aliongea Hamza lakini kauli hio ilimfanya Irene kuvuta mdomo.

“Da’Prisila umemuacha kaka Chriss anatia huruma jamani”Aliongea Irene.

“Nimemuacha vipi, wewe umeonaje?”

“Anatia huruma ndio , amekufuatilia kwa muda mrefu sana nilikuja kudhania utakuja kuolewa nae”

Kauli hio ilimfanya Prisila kumwangalia Hamza kupitia kioo cha mbele

“Chriss ni rafiki yangu tu na atabakia kuwa hivyo , halafu na wewe mama yako anajua unakuja kununua gari?”

“Nimetoka kwa mama Kinondoni mbona na anajua kabisa Hamza ndio ananisindikiza”Aliongea na kwa namna ambavyo Irene alikuwa akitaja jina la Hamza aliona kabisa Irene alikuwa akimtaka Hamza na moyo wake ulishikwa na wasiwasi na kujisikia vibaya kwa wakati mmoja na kujiambia kwanini Hamza kila mwanamke anampenda.

“Mnaishi Kinondoni!Kwani mmehama Masaki siku hizi?”

“Baba na mama wametengana, Mama anaishi Kinondoni”

“Oh!!”

Prisila hakutaka kuuliza zaidi maana alikuwa akijua mgogoro mkubwa wa familia hio , hata kwa Hamza baada ya kuona namna Prisila alivyoitikia ilionekana alikuwa akijua ni yeye tu ambae mwanzoni alimuona Mama Irene kama mtu mwema sana.

Dakikika chache mbele waliweza kufika showroom na haikuwa Slipway kama ambavyo Irene alipendekeza bali Prisila aliwaelekeza upande mwingine ambapo na yeye huagizia magari yake kupitia kampuni hio.

Kampuni ya Vexto ilikuwa kampuni kubwa zaidi , ikitoka hio ndio inakuija Dosam , lakini hata hivyo makao makuu yake yalihamishwa kutoka Tanzania ilipoanzishwa na kupelekwa Italy lakini Tanzania ilikuwa ndio nchi iliobeba viwanda vyake vingi.

Kwasababu walikuwa na ushirika wa kibiashara na kampuni kubwa za kutengeneza magari, ilikuwa ni rahisi kupata gari mpya kabisa.

Ilikuwa ni kama Prisila alivyoongea kwani Irene aliweza kupata gari kwa haraka , ijapokuwa alipenda gari ya kwanza ilioonyesha lakini ilikuwa ghali sana kulingana na bajeti yake na Prisila alimwambia achukue BMW 118i ya rangi ya bluu metallic na aliridhika.

Irene alionekana kuwa na mchecheto mno baada ya kupewa ufunguo wa gari yake , hakutaka hata kuendelea kubakia na Hamza na aliendesha kuitoa akirudi nyumbani na kumfanya Hamza na Prisila kuangaliana na kutabasamu.

“Ameridhika?”

“Ni kweli , pale marafiki zake wanaenda kukoma”Aliongea Prisila na kucheka.

“Nisindikize basi hadi Mlimani city, au uko bize”Aliongea Prisila.

“Kuna nini Mlimani?”

“Dalali wa nyumba yetu Mbweni kanipigia simu na kuniambia kapata mpangaji na kapenda nyumba , naenda kuonana nae ili kusainishiana kwa niaba ya baba , tumepanga kukutana Mlimani City”Aliongea na Hamza hakukataa.

Baada ya dakika kama therathini hivi waliweza kufika Mlimani City na kuingia katika Mgahawa wa Instabul, baada ya kuketi Prisila alimpigia Dalali simu na kumuulizia kuhusu mpangaji na aliambiwa anakuja hapo muda si mrefu.

Muda ule wakati Hamza akiletewa kahawa aliweza kumuona mwanamke wa kizungu wa makamo ya miaka kama therathini na tano hivi kwenda arobaini , mwanzoni alihisi ni kam kamfananisha na kusubiria ageuke maana alionekana kuongea na simu.

Muda uleule simu ya Prisila ilianza kuita na aliona ni namba mpya na alipokea na palepale aliweza kusikia sauti ya kingereza na aliongea maneno ambayo Hamza aliyaelewa na palepale yule mwanamke aligeukia upande wao na Hamza palepale alimjua.

Haikuwa kwa Hamza tu hata yule mwanamke mara baada ya kugeuka upande alipo Prisila macho yake yalichanua kana kwamba ameona mtu ambae anamfahamu na hakutegemea kumuona hapo, alipiga hatua kusogelea upande huo kwa haraka.

“Serena!!”

Hamza ndio aliekuwa wa kwanza kumwemwesa maneno hayo huku akimwangalia huyo mwanamke akisogea.

“Unamjua?”Aliuliza Prisila kwa mshangao na Hamza alitingisha kichwa na alitoka kwenye meza na kumsogelea kabla hajamkaribia.

“Serena ni wewe kweli , Niite Hamza jina langu jipya”Aliongea Hamza mara baada ya kuona Serena anataka kumuita kwa jina lake la mwanzo na mwanamke huyo alielewa haraka haraka .

“Hamza ni wewe!Unaishi kweli Tanzania?”Aliongea yule mwanamke kwa kingereza baada ya kukumbatiana huku wakisogea kwenye meza aliokuwa amekaa Prisila.

“Ndio , umekuja lini Tanzania?”Aliuliza.

“Nimekuja tokea juzi , nimefikia hotelini lakini nilipanga kukaa hapa muda mrefu kidogo hivyo natafuta nyumba ya kupanga”

“Wewe ndio ninaepaswa kuonana nae hapa? , Hamza huyu ni mpenzi wako ,what coincidence?”Aliongea baada ya Prisila kutingisha kichwa.

“Hapana, Prisila ndio jina lake , ni rafiki yangu wa utotoni “Aliongea na mwanamke yule alimpa mkono Prisila akimwambia amefurahi kuonana nae na imekuwa baraka pia amemkutanisha na mtu anaefahamiana nae.

Prisila alikuwa na mshangao kwa wawili hao kufahamina na aliona ni kweli ni kama bahati ya mtu anaekuja kukutana nae kufahamiana na Hamza.

“Serena upo Tanzania kwa ajili ya Tembo wa Trishaza?”Aliuliza.

“Ndio nimeona nimsamehe ndio maana nimekuja kuona hata kaburi lake”Aliongea.

“Vipi kuhusu kazi yako?”

“Nishaacha kazi , nina mambo mengi kichwani ya kufanyia utafiti , hivyo nataka kuwa mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja”Aliongea Serena.

“Hamza unafahamiana nae vipi?”Aliuliza Prisila kwa kingereza

“Huyu ni mjane wa rafiki yangu wa kitambo”Aliongea Hamza

Ukweli ni kwamba asingeweza kusema mwanamke huyo ni mke wa Dokta Genesha maarufu kama Tembo wa Trishaza kwani watu wengi duniani hawakuwahi kujua kama Genesha alikuwa na mke.

Ijapokuwa Serena alikuwa na umri mdogo kuliko Genesha lakini walikuwa wakipendana mno na wote walikuwa ni wanasayansi ambao walijaribu kufanyia utafiti wa kitabu cha Mti wa uzima au Ankh.

Sasa kutokana na Genesha kuwa bize sana kufanyia utafiti kitabu hicho ilimfanya kukosa muda wa kuwa karibu na Serena na uhusiano wao ndio ulivyoanza kuyumba mpaka ukaja kuvunjika.

“Serena najua hizi ni taarifa mbaya kwako , lakini Trishaza hana kaburi, nilimzika kwa namna ya kuunguza mwili wake na kusambaza majivu baharini , kabla ya kifo chake kauli yake kubwa ilikuwa ni kutaka kukuona kwa mara ya mwisho”Aliongea Hamza na kumfanya mwanamke huyo macho yake kuwa mekundu palepale.

“Jamani hata sikujua, nadhani hii ni adhabu kutoka kwa Mungu., ila haina shida, Hamza mimi sina haraka nitachukulia safari yangu ya kuja hapa Tanzania kama Vacation na nitaendelea na mpango wangu wa kupanga nyumba , angalau wewe upo sidhani kama nitakuwa mpweke sana , au unasemaje?”Aliongea na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.

“Mimi kwasasa tayari nimekwisha oa , mke wangu asipoweka pingamizi basi sina tatizo”Aliongea

“Wow! Umeoa , hizi taarifa zikisambaa sijui ni watu wangapi watashikwa na shauku ya kutaka kumuona mkeo, Naomba unipeleke nikamuone nafasi ikiwepo”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa kumkubalia.

Prisila licha ya kwamba alikuwa akijua kingereza vizuri lakini alishindwa kuelewa wanachoongea kutokana na topiki yenyewe hivyo aliendelea kukaa kimya huku akifurahia chakula kilichowekwa mezani.

“Dokta alikufa akiwa na majuto makubwa sana , aliona hata kama misheni ya Ankh ikifanikiwa haitakuwa kitu kizuri , Kuishi kunaweza kuleta furaha lakini pia huja na maumivu na mateso makali.. kama asingeondoka pengine ningehisi ananiiingiza kwenye mtego , isitoshe Ankh ni kama simulizi tu lakini watu wengi mpaka sasa wanaamini ni kitu ambacho kipo na wameanza kunisumbua sana”Aliongea Hamza na kauli ile ilitengeneza dalili ya chuki kwenye macho ya Serena.

“Kaka yake ndio msababishi wa yote haya… Nissa alimsaliti kaka yake , vinginevyo asingejiua kutokana na msongo wa mawazo , hata mimi pia ni wa kulaumiwa, nilikuwa nikijua anachopitia lakini nikaachana nae”Aliongea.

ITAENDELEA.
WAtsapp 0687151346
 
Hapa nafkiria yaani mke ni km huyo regina.
Akiamua kunipa mapande huwa nasanda.
Baada ya masaa kadhaa utaskia uko wapi?😁
Unaona ebo,si ndo wewe ulisema hutaki kuniona? Ni amri
'rudi hapa usiniletee ujinga"
Unabaki mame,tate,nene🙆‍♂️.
Ukute bahati mbaya we ushakamata uno jingine.
 
Hapa nafkiria yaani mke ni km huyo regina.
Akiamua kunipa mapande huwa nasanda.
Baada ya masaa kadhaa utaskia uko wapi?[emoji16]
Unaona ebo,si ndo wewe ulisema hutaki kuniona? Ni amri
'rudi hapa usiniletee ujinga"
Unabaki mame,tate,nene[emoji2297].
Ukute bahati mbaya we ushakamata uno jingine.
Hahaha...Hawa Viumbe
 
Hongera sana brother singano jr kiukweli hii series ni kali kinoma ndo maana ikichelewa kupostiwa watu huanza kulalama na arosto wanaanza kumwambia shunie akuite [emoji1787][emoji23][emoji28][emoji2]
 
I'm your number 1fan
 
Respect mkuu
 
Respect kamanda

Back
Top Bottom