nergomafioso
Senior Member
- Apr 3, 2024
- 109
- 284
🙏🙏 Hasta el fuegoUsiku leo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🙏🙏 Hasta el fuegoUsiku leo
Asante sana mkuuSHETANI RUDISHA NAFSI ZETU
MTUNZI:SINGANOJR
MHARIRI: ZEROS LITERATURE
SEHEMU YA 133
Mtaalamu
‘Neema ya tone la maji hulipwa kwa chemchem.’
Staili ya uvaaji wa Yulia ilimpagawisha mno Hamza na kumfanya amkodolee macho kwa sekunde kadhaa.
"Mbona unanikodolea macho? Ijapokuwa mimi ni mrembo, hapaswi kunitamani," aliongea Yulia kimapozi huku akisimama kutoka alipokuwa amekaa na kumsogelea Hamza.
Pua zao zilikuwa zimeachana kwa sentimita chache sana, na Hamza alitumia muda huo kuangalia uso mlaini wa mrembo huyo. Kisha alishuka kwenye lipsi (midomo) pana zilizokuwa zimeiva na kuwa nyekundu, na alitamani kuinamisha kichwa chake na kuzin’gata.
Hata hivyo, Hamza alijua uchokozi na tabasamu la mwanamke huyo yalikuwa ni maigizo tu na hakuwa na hisia zozote kwamba alikuwa akimpenda. Kwenye ulimwengu wake, hisia pekee alizokuwa akizitambua ni hasira na furaha pekee.
"Sio mrembo sana kama mke wangu," aliongea Hamza huku akituliza presha ya damu kutokana na matamanio ya kiume yaliyokuwa yamemshika kwa sekunde kadhaa.
Yulia, mara baada ya kusikia kauli hiyo, palepale uso wake uligeuka na kuwa na ukauzu na ukali, akiwa tofauti kabisa na mwanzo alivyokuwa na alipiga hatua moja kurudi nyuma.
"Shida yako unachukiza sana, kama ungeweza kuendelea kuigiza nisingekuwa na shida kugusanisha lipsi (midomo) zangu na zako," aliongea.
"Kama ni hivyo, kwanini hujaongea mapema?" aliuliza Hamza huku akishika kichwa chake, akijutia kuikosa hiyo nafasi.
"Madam Yulia, una maagizo mengine kwangu? Kama huna, naelekea kupata chakula cha mchana," aliongea Hasina.
"Sina maagizo mengine, unaweza kwenda tu," aliongea, na Hasina alitingisha kichwa kisha akageuka na kuondoka.
"Mkurugenzi wa kitengo cha TIMISA lakini anaonekana kama kijakazi wako. Babe (mpenzi) Yulia, unaonekana wewe ni levo nyingine kabisa," aliongea Hamza, akimaanisha ilikuwa sio kawaida kwa mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha TIMISA kuonyesha unyenyekevu kama kijakazi mbele ya Yulia.
"Sio kijakazi wangu, ni kama bomu ambalo limetegeshwa na serikali kuniua ikitokea nimeisaliti nchi," aliongea.
"Kumbe umeona, ila anaonekana kukubali," aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kisha aligeukia Screen (skrini) iliyokuwa ikionyesha muundo wa manowari, umbo lake la nje na ramani yake ya ndani.
"Sijawahi kudhania utakuwa na uwezo wa kutengeneza kitu kama hiki."
"Tena sio kitu ambacho nilitaka kutengeneza kabisa, ni kutokana na jeshi kuomba nitengeneze. Zikikamilika kama unavyoona hapo kwenye ramani yake, kila moja inao uwezo wa kufyatua
bomu la kusafiri kutoka bara moja kwenda bara lingine."
"Kwa majeshi mengi duniani, kumiliki kitu kama hiki ni ndoto ya usiku," aliongea Hamza huku akichezesha ulimi wake kwa kutoa sauti.
"Kwangu mimi hii silaha naona haina maana kabisa na faida haina. Silaha ninayotamani kuunda ni yenye uwezo wa kuangamiza dunia huku nikiamua ni eneo gani lisiathirike," aliongea huku akiwa na tabasamu la kujivunia.
Alifurahishwa na muonekano wa Hamza wa kuchanganyikiwa ndani ya eneo hilo.
"Vipi, unatamani kuona ni kitu gani ninachofanyia utafiti?" aliuliza huku akiwa na tabasamu lililojaa kejeli.
Hamza asingekataa. Isitoshe, kuja kwake hapo ilikuwa ni kwa ajili ya kuona ni tafiti gani hiyo ambayo mwanamke huyu anaifanyia kazi mpaka kutolewa macho na watu wengi.
Isitoshe Himidu alimwambia kabisa tafiti hiyo inaweza kuwa na msaada mkubwa kwake, na Hamza aliamini ilimradi Himidu anayapenda maisha yake basi asingethubutu kumdanganya kabisa.
"Ndio, natamani sana kujua ni majaribio ya tafiti gani unayofanya. Pengine naweza pata uzoefu mpya," aliongea, na Yulia alitoa tabasamu la kejeli.
"Kama umekuja kutaka kujua ni tafiti gani ninayofanyia kazi, sikwambii."
"What the Fck!*" Hamza alishindwa kujizuia na palepale alimpiga Yulia kibao cha makalioni.
"Hata kama usiniambie maadamu nipo hapa
kisiwani nitajua tu. Sikulazimishi ila ukitaka kuniambia wewe sema."
"Nani kasema utajua? Unadhani ni rahisi hivyo?" aliongea Yulia akiwa na mwonekano wa kumchokoza Hamza.
"Nitahakikisha huoni utafiti wangu na wakati tukifanya majaribio utakaa nje," aliongea.
"Haha... nani wa kuweza kunizuia nikae nje? Wewe unadhani kwanini mmenileta huku, si kwasababu mnaona mimi ni zaidi ya walinzi wenu wote?"
"Ukileta fujo nitaongea na Hasina tu na kisha atafanya mawasiliano kwenda makao makuu ya TIMISA na mkeo Regina atakuwa kwenye matatizo. Kunigusa mimi ni sawa na kugusa taifa na kesi yake ni uhaini," aliongea kwa maringo kabisa na kumfanya Hamza kuvuta hewa nyingi ya ubaridi huku akisaga meno yake. Aliona kabisa mwanamke huyo alikuwa akimtishia makusudi. Lakini hata hivyo aliona kwamba haijalishi ana uwezo kiasi gani ila hana uwezo wa kushindana na nchi.
"Hehe... vipi bado unataka kuona tafiti yangu hata kwa kulazimisha?" aliuliza Yulia mara baada ya kuona Hamza kanywea, na kumfanya Yulia kushikwa na furaha ya ajabu.
Hamza aliishia kunyamaza huku akiangalia prototype ya manowari iliyokuwa ndani ya maji. Alijiambia kwamba Yulia sio tu kwamba alikuwa mwanasayansi, bali sio mwanasayansi wa kawaida, na kila kitu kilikuwa kikimwambia kuwa utafiti ambao anaufanyia kazi utakuwa sio wa kawaida pia. Kama ataondoka hapo kisiwani bila kuona utafiti huo, itakuwa hasara kubwa sana kwake.
"Madam Yulia, kama unakitu unataka kuongea na mimi, ongea. Isitoshe nimekuokoa zaidi ya mara mbili. Ikiwa kuna tatizo baina yetu, unaonaje tukikaa chini na kuongea kuyamaiza?"
"Kwahiyo unadhani kwa sababu uliniokoa nitakuwa na shukrani? I am sorry, sina mpango huo kabisa. Isitoshe si uliniokoa baada ya kuniona ni mrembo, na tamaa zako ndio zilikusukuma. Nyie wanaume ni viumbe ambao hamjawahi kufikiria na kichwa cha juu mbele ya mwanamke mrembo."
"Siwezi kukataa, navutiwa sana na umbo lako, sura yako. Lakini hata hivyo, mimi kitaaluma ukiachana na kusomea uchumi, vilevile mimi nimesomea udaktari. Hivyo, nimekuokoa kama daktari."
"Huna haja ya kujieleza mwanaume. Unachopaswa kufanya ni kuniahidi kitu kimoja, na nitakuruhusu kuangalia majaribio hayo kesho."
"Kitu gani?"
"Kuwa mpenzi wangu."
Aliongea bila ya kuuma maneno na kumfanya Hamza kuvuta pumzi ya baridi, na kisha alianza kucheka kwa kukosa ujasiri.
"Mbona spidi hivyo? Nawezaje kuwa mpenzi wako kwa kuniamrisha?"
"Sio kama unaenda kuwa mpenzi wangu halisi, unakwenda kuigiza kuwa mpenzi wangu. Nataka tucheze mchezo wa kuwa wapenzi."
"Mchezo wa kuwa wapenzi, ili kumuonyesha nani?"
"Kuna mwanaume ananisumbua sana, na imefikia hatua ananichukiza," aliongea Yulia akikosa kabisa subira ya kupata jibu kutoka kwa Hamza.
"Vipi, unakubaliana na sharti langu? Mbona unafikiria sana swala rahisi namna hiyo?" Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kukunja sura. "Kama sikosei, mtu ambaye anakufukuzia lazima sio mtu wa kawaida. Kwanini usinikubali ukawa demu wangu kabisa na sio kuigiza?" Aliongea Hamza.
"Ushaoa tayari, utakuwaje mpenzi wangu?"
"Basi nipatie sharti lingine? Unajua, mimi kuigiza kuwa mpenzi na mwanamke mrembo kama wewe kunanipa wakati mgumu sana."
"Kama hutaki, acha na kuwa tu bodigadi wangu," aliongea Yulia huku akigeuza kichwa chake na kuangalia pembeni.
Yulia aliishia kung'ata meno yake kwa hasira na aliona aliamini Hamza anakataa kwa kuogopa kugombana na vigogo wa nchi. Ndiyo maana hakutaka kulazimisha sana.
"Basi hakuna shida. Kwa jinsi ulivyo mrembo, nakubali kuigiza kuwa boyfriend wako," aliongea Hamza huku akijiambia atatumia nafasi hiyo kumchokoza na huenda akapewa tunda.
Yulia, mara baada ya kusikia kauli hiyo, aligeuka akiwa na tabasamu murua kabisa kama vile ni ua linaloanza kuchanua. Uzuri wake uliongezeka zaidi ya isivyokuwa kawaida.
"Babe, kwa sababu umekubali, unaonaje ukinisindikiza kwenda kupata chakula cha mchana kwanza?" aliongea kimadaha na kumshika Hamza mkono huku akimvutia kuelekea kwenye lifti.
"Yulia, naomba nikuambie kabisa, ni leo tu ndio naenda kuigiza na sio siku nyingine," aliongea Hamza akiwa siriasi, lakini licha ya usiriasi wake alishindwa kuzuia macho yake kukikodolea kifua cha Yulia.
"Usiwe na wasiwasi. Isitoshe nakujua ni mtu wa aina gani," aliongea Yulia huku akiwa na uso uliojaa dhihaka.
Wawili hao waliingia kwenye lifti ambayo iliwachukua moja kwa moja mpaka ghorofa ya ishirini. Mara baada ya kutoka, walikuwa katika mgahawa mkubwa ndani ya hoteli hiyo. Mapambo yalikuwa na umaridadi wa hali ya juu na kupendeza macho, na kuashiria ufahari mkubwa tofauti na chini kwenye vyumba vya ardhi.
Walitembea kuingia katika mgahawa huo uliokuwa angavu kutokana na mwanga wa jua uliobadilishwa na vioo kupendeza mandhari ya ndani, na kufanya mtu yoyote anayeingia hapo ndani mudi yake kuimarika haraka.
Kulikuwa na watu wengi tayari ndani ya eneo hilo, na juu ya meza zao zilikuwa zimechafuka kwa aina mbalimbali ya vyakula vya kutamanisha. Asilimia kubwa walionekana kama wasomi wa maswala ya sayansi. Hawakuwa wamevalia sare kama ilivyokuwa kwa wanausalama wengi bali walivalia kama vile walikuwa watalii. Hakukuwa na ngozi nyeupe hata moja, asilimia kubwa walikuwa weusi tupu na baadhi tu ndio walikuwa machotara kama ilivyokuwa kwa Hamza.
Mara baada ya kumuona Yulia akiingia hapo akiwa ameshikana mikono na Hamza, kila mtu aliishia kutoa ishara ya heshima kumsalimia Yulia huku kwa wakati mmoja wakiwa na maswali mengi juu ya Hamza ni nani.
“Bosi Yuli ..”
“Hello!.”
Kulikuwa na watu waliomuita Yulia kama Mkurugenzi, kuna wengine walimwita mwenyekiti na wengine pia walimwita Injiniia. Kila cheo alionekana kuwa nacho mwanamke huyo na kumfanya Hamza kuweza kuona heshima iliyojificha nyuma ya sura ya mrembo huyo. Aliona hakika Yulia hakuwa wa kawaida.
“Mbona unaninishangaa, unadhani naheshimika sana kwa watu sio? Mimi sio levo yako kabisa, nifuate na kunitii kama bosi wako,” aliongea Yulia kumchokoza Hamza.
Hamza, upande wake, hakubughuziwa na uchokozi wake. Badala yake, alimuuliza swali nje ya topiki.
“Uwanasayansi wako ndio uliosababisha ukataka kuuliwa nje ya nchi wewe na familia yako kupoteza maisha?”
“Ndio, tokea wakati ule nilivyorudi nchini sikuwahi kusafiri kutoka nje ya nchi, naboreka mno kutokana na kukosa uhuru,” aliongea Yulia.
Kaka yake na wazazi wake wote waliuliwa wakiwa ughaibuni wakiwa Vacation na sababu ya kupoteza kwao maisha ni kwa sababu yake.
Mara baada ya kuongozwa mpaka kwenye ukumbi binafsi wa kupatia chakula, walipokelewa na meza kubwa ya mahadhi ya kimagharibi.
Hamza kabla hata hajaingia alikuwa ashahisi watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo wote walikuwa ni watu na ziada. Baada ya kuingia kabisa hatimaye aliweza kumuona mwanaume aliyekuwa amevalia shati la Versace, alikuwa na nywele ndefu ambazo zimechanwa vizuri, alionekana pia kuwa mtanashati mno na alikuwa bize kula steki ya nyama.
Mwanaume yule mara baada ya kuhisi kuingia kwa Yulia katika eneo hilo aliinua na kuonyesha sura yake iliyojaa uhandsome na alimwangalia Yulia kwa sekunde kadhaa na kisha macho yake akayageuzia kwa Hamza na akatoa tabasamu lililojaa upole na uungwana.
“Yulia karibu sana, huyo mwanaume pembeni yako ndio nani?” aliuliza.
“Ni mpenzi wangu, anaitwa Hamza, ndio mtu aliyekoa uhai wangu nje ya nchi na kwa bahati nzuri tumekutana kwa mara nyingine hapa nchini na tumeanza mahusiano yetu,” aliongea Yulia akiwa na mwonekano wa uitikiaji.
Hamza aligundua mwanaume huyo alikuwa na nguvu za ziada kwenye mwili wake na sio hivyo tu, watu waliokuwa pembeni yake wote walikuwa na uwezo wa ziada na walionekana walikuwa wakimlinda. Kushoto kwake kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na kipara, hakuwa mrefu sana lakini alikuwa na mwonekano wa ujasiri na aliashiria ukali. Alikuwa siriasi hata wakati wa kula, ni kama vile alikuwa na kinyongo na chakula kwa staili yake ya ulaji.
Kulia kulikuwa na mwanamke ambaye ana mwili wa miraba minne, alikuwa na nywele fupi kiasi zilizopakwa dawa , hakuwa mrembo kabisa hususani kwa namna alivyoonekana kukomaa, tofauti na wenzake yeye hakuwa akila chakula badala yake alikuwa ameshika kioo kidogo mkononi na alikuwa akijiremba kwa mapozi ambayo yalimfanya Hamza aone ni kama vile anataka kupiga chafya.
Yule mwanaume ambaye alionekana kama ndio bosi ndani ya eneo hilo alisimama na kisha alimpa Hamza mkono na kumsalimia kwa kingereza.
“Nimefurahi kukutana na wewe, naitwa Herbert Kijazi, mtoto wa kwanza wa Mzee Kijazi na mchumba wa Yulia,” aliongea.
Hamza mara baada ya kusikia jina la Kijazi moyo wake ulidunda kwa haraka na kujiambia Yulia ni mshenzi sana kwa kutaka kumgombanisha na mtoto wa Mzee Kijazi.
Hamza licha ya kuishi kwa muda mfupi nchini Tanzania, kutokana na kuingia sana mitandaoni alikuwa akiifahamu familia ya Mzee Kijazi kuwa na mahusiano ya ukwe na Mheshimiwa Mgweno na familia ya M,zee Azim. Maana kwamba kutokana na kuwa na uhasama wa chini chini na familia ya Mgweno basi moja kwa moja pia familia ya Kijazi alikuwa na uhasama nao. Sasa kitendo cha kutambulishwa na Yulia kama mpenzi kilikuwa ni kama kuchochea moto.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi, nilichokuwa nikimaanisha Yulia ashawahi kuwa mchumba wangu, lakini baada ya kurudi nchini aliongea kuna mtu ametokea kumpenda na moja kwa moja uchumba wetu ulikoma,” aliongea kwa kujielezea mara baada ya kuona Hamza alikuwa amekumbwa na wasiwasi.
“Yupo sahihi Hamza, Hebert ni mpenzi wangu wa zamani na hakuna kinachoendelea kati yetu, naomba usije ukakasirika,” aliongea Yulia kwa kujibebisha akijitetea mbele ya Hamza.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo alihisi kuna kitu hakipo sawa na hiyo yote ni kutokana na kwamba aliona hali ya Hebert kuwa na hisia za kimapenzi kwa Yulia lakini alijifanyisha kutokasirika wala kuwa na wivu.
“Bro karibu uketi, wewe hata usinijali kabisa, nipo hapa kama moja ya timu ya utafiti na sio kwa sababu ya Yulia,” aliongea kwa upole akimkaribisha Hamza kukaa.
Muda ule mara baada ya wote kuketi chini, Hasina alikuja akiwa ametangulizana na wahudumu wa hoteli ambao walikuwa wameshaandaa chakula tayari. Haikuwa na haja ya kuulizwa unakula nini kwani kulikuwa na kila aina ya chakula na wewe kuchagua unachotaka.
Licha ya chakula hivyo kupendezesha macho, upande wa Hamza ni kama hamu ilimpotea ghafla kutokana na kujihisi kuna kinachoendelea hapo.
“Babe mbona unaonekana kama huna hamu ya kula, usije kuhisi vibaya, Hebert ni mwanajeshi idara ya utafiti na uhandisi ndio maana yupo hapa,” aliongea Yulia.
Hamza alijiambia kuna haja gani ya kujitetea ilihali bwana huyo inaonekana ni dhahiri amejishikiza katika kitengo hicho ili kuwa na ukaribu nae, kwa uzoefu wake Hamza aliamini kadri mtu anavyoonyesha kutokujali maana yake anajali sana.
“Hehe.. Unaonaje tukienda kisheria sheria mpenzi, unatakiwa kunikiss kwanza ndio nile,” aliongea Hamza huku akijiambia kwa sababu mambo yamefikia hatua hiyo basi kama mbwai na iwe mbwai, ni mwendo wa kujifaidisha.
Mwonekano wa Yulia wala haukubadilika kwa ombi hilo, lakini macho yake namna yalivyokuwa yakicheza cheza ilionyesha dhahiri hakuwa amefurahishwa na Hamza kuongea hivyo.
“Yaani wewe sijui nakufanya nini...”
Yulia aliigiza na kisha aliinama kutaka kumkiss Hamza shavuni, lakini kabla hata lipsi zake hazijaligusa shavu lake, Hamza alipindisha mdomo wake kwa kugeuka na kisha alimshika Yulia kiuno na kumpiga busu la kwenye lipsi.
“Ugh...!!”
Yulia macho yake mazuri yalikodoka mara baada ya kuona mpango wa Hamza ni kutumia fursa vizuri. Licha ya kwamba hakupendezwa na shambulizi hilo, lakini vilevile asingeweza kujiondoa haraka kwa kuamini lazima Herbert angeona kinachoendelea. Hivyo alikosa jinsi na kuishia kutoa ushirikiano wa kupanua mdomo wake na kumruhusu Hamza kumwingizia ulimi.
Hamza alikuwa akifurahia mno kinachoendelea, alijiambia si amejileta mwenyewe basi hana budi kutumia fursa hiyo vizuri, alikuja kuacha baada ya mhudumu kuingia katika eneo hilo na kumpelekea Yulia kushikwa na haya za kike.
Hamza aliishia kufurahishwa na muonekano wa kuzubaa wa Yulia.
“Babe ni muda wa kula sasa, tutaendelea baadae tukiwa wenyewe,” Aliongea Hamza huku akimkonyeza.
Yulia aliishia kumwemewesa lipsi zake na kutingisha kichwa huku akilazimisha tabasamu. Hakujua kwanini, lakini kwa mara ya kwanza katika maisha yake moyo wake ni kama kuna mdudu alielala na anajaribu kuamka. Alihisi hisia ambazo hazikuwa za kawaida na mpaka hatua hiyo hakujua ni kitu gani kinamtokea.
Herbert aliishia kuangalia tukio hilo lote bila ya kuongea neno zaidi ya kuupamba uso wake na tabasamu.
“Bro Hamza kama sikosei utakuwa tayari na mke si ndio?” Aliuliza Herbert akiwa na tabasamu usoni. Hakujali kabisa kama alikuwa amemzidi Hamza kwa zaidi ya miaka kumi ila alimwita Hamza Bro.
“Upo sahihi, naona ushafanya utafiti wako kabisa na kujua kila kitu kuhusu mimi, kwanini unauliza ilihali majibu unayo?”
“Mkeo ni Regina Dosam, mmiliki na Afisa mtendaji mkuu wa makampuni ya Dosam, lakini pia mwanamke anaye sifika kwa kuwa na urembo wa ajabu. Kwa hiki unachofanya hawezi kupatwa na wivu?”
“Mke wangu ni muungwana sana na anaamini mimi kama mwanaume kuwa na wanawake angalau watatu sio tatizo,” Hamza alitunga pumba na kujibu bila ya kuwaza sana.
“Oh! Unaonekana kumjua sana mkeo?” Aliongea Herbert huku akiwa na mwonekano wa kushangaa.
“Hahaha…Braza naamini hautoenda kunisnitch kwa mke wangu kwa kinachoendelea hapa,” aliongea Hamza akionyesha hali ya kuwa na mashaka na Herbert.
“Haha... Bro wala usiwe na wasiwasi kabisa, mimi ni mwanaume na siwezi kufanya hivyo, nimeuliza tu kutokana na kuwa na shauku... Bro wewe kula maisha na warembo siri zako zipo salama.”
“Nimemjua Hamza kwa muda sasa na ni mtu alienisaidia na kutokana na hilo nipo tayari kumpa chochote. Hata kama Regina atafahamu kuhusu uhusiano wetu sidhani anaweza kufanya chochote,” Aliongea Yulia lakini upande wa Hamza alikuwa akiwaza tofauti.
Alijiambia ilikuwa bahati Regina hakuwa katika eneo hilo, vinginevyo angekasirika mpaka kutapika nyongo. Regina alikuwa akimchukia mno Yulia.
“Hehe... kwanza kabisa mke wangu ni mtu muungwana sana na kingine anajua nina
michepuko mingine tofauti na Yulia, kiufupi ni mwelewa mno.”
“Nakubali bro, isitoshe wewe ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana. Nasikia binamu yangu Farhani alifanya vitu vya ajabu na ukaishia kumuua... kama sehemu ya familia nakushukuru sana kwa kutuondolea yule kichaa,” Aliongea na kauli hiyo ilimfanya Hamza kuona kweli Herbert alikuwa na uvumilivu wa hali ya juu mpaka kwa kufikia hatua ya kumshukuru kwa kumuua ndugu yake.
Farhani alikuwa ni bwana aliemuua Mliman City mara baada ya kuanza kumtaka Eliza , alikuwa ni mjukuu katika familia ya Mzee Azim na mama yake Farhani ni shangazi kwa Hebert.
Wakati akiwa anawaza hivyo, palepale yule mwanaume aliekuwa siriasi sana na chakula alipiga kofi meza kwa hasira.
“Bosi hata kama binamu yako alikuwa na makosa bado anabakia kuwa ndugu yako, hajaishia tu kuvunja uchumba wako na bosi Yulia lakini pia ndio aliemuua bosi Farhani na Master Jagani mkuu wa Shirki ya Hansee,” Aliongea.
“Hey, Pima, unapaswa kukubali pale unapoteokea umekosea, hatuwezi kujiona tupo sahihi muda wote kwasababu ya ukubwa wa familia ya Azimu na uhusiano wa familia ya Kijazi na ya mstaafu Mgweno,” Aliongea Herbert.
Yulia macho yake yaliishia kusinyaa na alimwangalia Hamza na kisha akatabasamu.
“Jina lake anaitwa Pima ni mhitimu wa mafunzo ya kimapigano kutoka shirki ya Hansee India, yupo vizuri sana hivyo kuwa makini,” Yulia alimwambia Hamza.
“Pima na Farhani sio tu kwamba walikuwa ni mtu na bosi wake lakini pia walikuwa marafiki wakubwa sana, kutokana na kuhusika kwako na kifo cha rafiki yake ndio maana anaonekana kukuchukia, naomba ujaribu kumwelewa na umsamehe,” Herbert aliongea akimwambia Hamza.
Hamza aliishia kujiuliza na kujiambia kuna haja gani ya kumtetea ilihali ni msaidizi wake tu.
Hamza ni kama ambavyo alitegemea, kwani Pima hakuonekana kabisa kumchukulia bosi wake kwa umakini, na palepale alisimama na kumnyooshea Hamza kidole huku akiwa na uso uliojaa hasira.
“Hamza, kama kweli wewe ndiye uliemuua Master Jagani, basi utakuwa ni mtaalamu wa hali ya juu katika mapigano. Unaonaje tukipimana? Ukishinda nitaondoa kinyongo changu dhidi yako.”
“Pima, hebu acha ujinga. Braza Hamza yupo hapa kwa mwaliko maalumu kutoka kitengo cha Malibu. Yupo hapa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Kwanini unaanza kujilinganisha naye? Isitoshe, utulivu katika eneo hili ndio kitu muhimu zaidi.”
“Bosi, mimi kama Falsafa Pima bado siamini kama
Hamza ndiye aliemuua Master Jagani. Hata kama Mzee Azim hakutaka kulikuza hili suala, bado huoni hii ni dharau kwa familia ambayo imetoa mchango wa kusaidia taifa kupata wanajeshi wengi chini ya Hansii?”
“Pima…” Herbert alitaka kuongea lakini alikosa neno na aliishia kumwangalia Hamza.
“Bro, unaonaje kuhusu hili suala?”
“Sitaki kushindana naye. Kama ni suala la kumuua bosi wake, sijutii kufanya vile maana alinichokoza makusudi kwa kujigamba mbele ya mpenzi wangu. Kwanini nishindane naye kupigana ilhali sina kosa?”
“Tuone kama hutoshindana,” aliongea, na palepale mwili wake ulituna na kukusanya nguvu yake yote ya ndani huku akikunja vidole vyake katika staili ya kucha za mwewe. Kwa spidi ya hali ya juu bila kujali walikuwa hotelini, alimshambulia Hamza palepale kwa kulenga shingo yake.
SEHEMU YA 134.
Hamza, mara baada ya kushambuliwa vile, haraka sana alirudi nyuma na hata kiti alichokuwa amekalia kilipinduka. Mara baada ya kufanikiwa kumkwepa, alirusha mkono na kupangua shambulizi la Pima.
Pima, mara baada ya kuona shambulizi lake la kwanza limefeli, hakupoa. Palepale alifyatuka na sarakasi mtelezo na kufyatua kiti kwa ustadi wa hali ya juu kama mpira, kisha alikisukumiza kwa nguvu kumlenga Hamza kichwani. Hamza aliishia kukwepa kwa ustadi wa hali ya juu sana kiti kile, na kilienda kuvaana na ukuta na kupasuka pasuka.
Kwa haraka haraka, mashambulizi ya Pima yalimshangaza kiasi kutokana na uwezo wake na vilevile alivyokuwa na shabaha ya kushambulia. Lakini hata hivyo, ilikuwa ngumu sana kumshinda Hamza na mbinu yake hiyo ya mapigano.
Mara baada ya Pima kuleta shambulizi lingine, Hamza hakumsubiria sana kwani palepale alisogea kidogo pembeni na kisha aliweka mkono wake wa kulia katika staili ya karate na kupangua shambulizi lake kwa mara nyingine.
Pima hakutaka kumpa nafasi ya kupumua kwani aliendeleza kumpelekea Hamza mashambulizi, lakini yalipagunguliwa kwa ustadi mkubwa mno. Alijaribu mpaka kubadili mbinu ya kushambulia lakini hakuweza kabisa hata kugusa mwili wa Hamza kwani mashambulizi yake yaliishia juu juu.
Baada ya kuona anashindwa kabisa kumwingia Hamza, alijikuta akishikwa na hali ya wasiwasi na kumchunguza.
“Ni mbinu gani ya mafunzo unatumia, kwenye kuvuna nishati za mbingu na ardhi? Kwanini sihisi chochote kwenye mwili wako?” aliuliza.
Yeye mwenyewe alikuwa katika levo ya mzunguko kamili katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
“Umekosea swali maana sijifunzi mbingu za nishati za mbingu na ardhi, ndiyo maana hujahisi chochote kutoka kwangu.”
Ukweli ni kwamba Pima, mwanzoni mara baada ya Hamza kuingia na Yulia katika eneo hilo, alimchukulia kuwa binadamu wa kawaida kutokana na kutokuwa na nishati zozote za mafunzo ya mbingu na ardhi kwenye mwili wake. Ndiyo maana alikuwa na ujasiri wa kupigana naye, lakini baada ya kuona ameshindwa kufua dafu mbele ya Hamza, wasiwasi ulimwingia.
“Haiwezekani, kama hujifunzi mafunzo ya mbingu na ardhi umewezaje kuzuia mashambulizi yangu ya nguvu ya mzunguko kamili?” Aliongea na pia hakutaka jibu kwani palepale alibadilisha mbinu na alianza kuchezesha vidole vyake angani kwa namna ya ajabu. Mbinu hiyo Hamza aliifahamu fika; ilikuwa ni kitendo cha kupoteza nguvu nyingi za mwili kwenda kwenye ardhi huku ukiruhusu nishati nyingi za mbingu kuuvaa mwili ili kuongeza wepesi. Mbinu hii ndiyo inayowezesha wavuna nishati kuweza kupaa kwa kubatilisha kani mvutano kwa kuupoteza uzito wa mwili kwa kuzidanganya kanuni za anga.
Alifanya mjongeo ule kwa sekunde chache tu na akaanza kuwa mwepesi mno, hali iliyomfanya Hamza kutoa macho. Dakika ileile, bila ya Pima kumgusa, Hamza alihisi kama vile amefungwa kamba kwenye kiuno na shingo na anavutwa na ile nguvu kumkaribia Pima. Kama isingekuwa na nguvu nyingi za kuhimili ile nguvu inayomvuta, angeweza kushambuliwa kirahisi sana na Pima.
Mara nyingi hali kama hii hutokea si kwamba umefungwa, bali mbinu hiyo inacheza na akili yako na kukufanya uhisi kuvutwa. Kwa hali halisi, mtu anajichawia mwenyewe na kujiweka karibu na adui, sawa na jinsi mtu anavyoshikwa na jinamizi. Kitendo cha kuendelea kuchezesha nguvu kwa kuonyesha mjongeo, Pima alipotea aliposimama kichawi na kuwa kivuli, huku akizidi kumfanya Hamza kujihisi anavutwa pande zote.
Hamza alikuwa akijua mbinu hizi vizuri. Ukweli ni kwamba, neno uchawi ni nguvu iliyo ndani yetu wenyewe na si kwamba wachawi wanatuloga; wanachofanya ni kukuadhibu na nguvu yako iliojificha katika mwili wako. Hivyo, Hamza kitu cha kwanza alikuwa ni kuushinda uchawi wake mwenyewe kwa kufumba macho na kutumia hisia na sauti za masikio.
Hebert hakuwa akijali kabisa kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea na aliendelea kukata vipande vya steki ya nyama huku akitafuna kwa kasi. Upande wa Yulia, baada ya Pima kutoweka kwa macho, alishikwa na wasiwasi. Hakushangaa kwa sababu mambo haya yalikuwa ni kawaida sana tangu elimu ya mafunzo ya nishati za mbingu kueleweka kwa watu wengi.
“Bertha, hebu acha kushangaa hapo na msaidie
Hamza,” aliongea Yulia. Sio kwamba alihisi labda Hamza amezidiwa, lakini kama mwenza alitaka kuonyesha kujali. Bodigadi wake Bertha, mwanadada mwenye sura ngumu, aliishia kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho la kushoto, sababu ya kufanya hivyo ilikuwa kupima ukubwa wa hatari. Katika mafunzo ya kimapigano, hasa kwa wale wanajeshi wanaosomea kudili na nguvu za ziada, endapo wakikutana na adui na wanashindwa kuona mjongeo wake na nguvu zake, tofauti na kutumia hisia, wanashauriwa kutumia jicho moja kuangalia hatari kwa msingi wa falsafa kwamba kuichunguza hatari kwa macho yote mawili ni kuukaribisha udanganyifu. To perceive danger with
both eyes is to invite illusion; true clarity arises when one employs a singular focus and embodied awareness to dispel the shadows.
“Bosi, Yulia, nipo hapa kwa ajili ya kukupatia ulinzi. Mpenzi wako hana tatizo mbona?” aliongea Bertha mara baada ya kufumbua jicho moja, huku akiendelea kujirembesha sura yake kupitia kioo.
Muda uleule, hatimaye Hamza alifanya shambulizi kwa kusogea kwa kasi kubwa, na ghafla mkono wake ulionekana ukiwa umemshika Pima, ambaye alionekana kama ameinuka kichawi. Ilikuwa kama vile Hamza alikuwa akivua na kumtoa Pima kutoka majini kwa ndoano. Hamza hakutaka kutumia nguvu kubwa sana kwa sababu angeweza kumuua, hivyo alipiga ngumi kidogo tu kumwadabisha.
Baada ya Hamza kuzimisha mazingaombwe ya Pima, Herbert alianza kupiga makofi huku akiwa amesimama na kucheka.
“Hamza, sijakosea kabisa kukuita bro; uwezo wako si wa nchi hii,” aliongea, lakini Hamza wala hakujali sifa zake. Badala yake, aliangalia shati lake ambalo lilichanika katika harakati ya kuzima mazingaombwe ya Pima.
Hamza, mara baada ya kumtaitisha Pima, aliachana naye kisha alichukua kiti kingine na kukaa mezani na kuendelea kula.
“Nadhani nishashida, ole wako usinisumbue tena,” aliongea.
Muonekano wa Pima haukuwa sawa kabisa; alikuwa na hali ya hofu na kujikuta akiwa katika hali ya kuzubaa. Ukweli ni kwamba aliona kabisa Hamza hakutumia nguvu kubwa kumdhibiti, na kama angemtumia nguvu kubwa, angekufa. Kuwa mpiganaji ulieiva maana yake ni kuweza kumsoma adui yako kwa haraka na kujua kama una uwezo wa kushindana naye. Alijua fika Hamza alivuta muda si kwa sababu hakujua namna ya kushambulia bali alikuwa akijifunza mjongeo yake.
Ilikuwa sahihi kabisa. Hamza alijua fika kwamba mpiganaji mzuri ni yule anayejua kushambulia bila ya kumwonyesha adui mbinu zake. Kitendo cha Pima kupotea kilikuwa ni sehemu ya kuonyesha kuwa anaficha mbinu zake, na Hamza hakuhitaji macho kuona alichokifanya, bali alitumia hisia zake.
“Bosi, nisamehe kwa kukudhalilisha,” aliongea Pima.
“Hebu acha kuongea ujinga. Licha ya kwamba unaniita bosi, sisi ni marafiki, hivyo haina haja ya kuona aibu kwa kushindwa na Hamza. Shida yako tu ni kwamba unakurupuka sana,” aliongea Herbert.
“Asante sana, bosi, kwa kunionyeshea uvumilivu,” alijibu Pima.
“Hamza, majaribio yatafanyika kesho. Leo siku nzima hakuna cha maana tunachofanya. Kwa uzuri wa hiki kisiwa, unaonaje tukijumuika pamoja kula bata?” aliongea Hebert mara baada ya chakula cha mchana.
“Shati langu limechanika, napanga kwenda kwenye chumba changu kwanza kubadili,” aliongea Hamza akiwa hana hamu ya kula bata anazoongelea Hebert.
“Usiwe na wasi wasi. Naagiza mtu sasa hivi akuletee shati lingine kabisa,” aliongea Hebert na mara moja alimpa ishara muhudumu na aliondoka akiwa ameelewa maagizo.
“Hebert, unaonekana kuwa na shauku ya kutaka kumfahamu kiundani mpenzi wangu?” aliuliza Yulia, akimwangalia Hebert.
“Yulia, sio kama ulivyosema. Unaweza kuwa na muda wa kuwa pamoja na mpenzi wako, lakini leo ndio kwanza nimekutana nae. Nataka tuongee mawili matatu kufahamiana kidogo,” aliongea Hebert akiwa na tabasamu.
Yulia hakutaka kuendelea kukaa karibu na Hebert kwa sababu alijua akiendelea kuigiza na Hamza kama wapenzi, bwana huyo hashindwi kuchukulia hiyo kama fursa ya kumchezea. Mpango wake ulikuwa kumgombanisha Hamza na Hebert tu na sio vinginevyo. Hata hivyo, kwa sababu Hebert ndiye aliyeshawishi, asingekataa moja kwa moja ikiwa hana cha kufanya, aliona ngoja alipe gharama ya kumgombanisha Hamza na Hebert.
“Babe, naona hakuna tatizo kwa alivyopendekeza.
Twende tukacheze cheze, tuchangamke,” aliongea Hamza huku akiminyaminya paja la Yulia makusudi kabisa.
Hamza alijua kabisa hakuwa na haja ya kuigiza kuwa mpenzi wa Yulia tokea mwanzo. Aliona kabisa nia ya Yulia kupendekeza kuigiza ni kumtengenezea uadui na Hebert tu ili achukue maamuzi ya kijinga na mwisho wa siku pengine amuue Hebert na kujiingiza kwenye mgogoro na familia yake.
“Kama unataka, twende kucheza. Nipo tayari tukacheze,” aliongea Yulia akiwa na tabasamu usoni lakini moyoni alikuwa akitamani Hamza limkute jambo.
Baada ya kundi hilo kukubaliana, waliingia kwenye lift iliyowashusha mpaka nje kabisa na walianza kutembea katika bustani zilizokuwa kando ya fukwe.
Hebert mara baada ya kuona motorboat mbele yake, macho yalichanua.
“Bro, unaonaje tukishindana kuendesha motorboat?” aliuliza lakini Hamza alimkatalia. Alikuwa amezoea sana kutumia boti hizo za pikipiki wakati alivyokuwa nje ya nchi, na mara nyingi kipindi hicho akiwa anaendesha boti hizo, lazima nyuma yake awe na mrembo alievalia bikini. Sasa kutokana na eneo hilo kukosa warembo waliovaa bikini, hakuwa na hamu kabisa ya kucheza kwenye maji na boti hizo.
“Bro, ushashuka mpaka huku tayari. Sidhani kama ni vizuri kutofanya chochote. Pima licha ya kuwa na uwezo mdogo kwenye mapigano, ameshiriki mara nyingi katika mbio za boti. Unaonaje ukimpa nafasi ya kushindana tena?” aliongea Hebert, na kauli hiyo ilimfanya Pima kushangaa kwa sababu hakutarajia kama bosi wake angemtaka kushindana na Hamza kuendesha boti.
“Unadhani ninaweza kufanya kila kitu kwa sababu tu umeongea?” aliuliza Hamza.
“Bro, sijasema unashindana bure. Kama ukishinda, sitakuwa tena na kinyongo na Yulia kwa kuvunja uchumba wetu na nitawatakia maisha mema.”
“Uwe na kinyongo ama usiwe nacho, huwezi kubadilisha chochote. Yulia ni mpenzi wangu tayari,” aliongea Hamza na kisha alimgeukia Yulia.
“Si ndiyo babe?”
“Nimezaliwa kuwa mpenzi wako,” licha ya Yulia kusema hivyo, mwonekano wa Hebert haukubadilika.
“Inaweza isiwe kweli lakini, ijapokuwa nyie ni wapenzi, sidhani kama familia ya Yulia wakisikia kuhusu mahusiano yenu watakubali kirahisi.Watapinga kwa nguvu zao zote. Kunikataa
mimi na kisha kuwa na mahusiano na mwanaume aliyeoa siyo tu tusi kwa familia ya Yulia, bali pia ni tusi kwa familia yetu,” aliongea Hebert.
“Kwahiyo unaniogopesha au inakuwaje?” aliuliza Hamza kwa hasira.
“Haha… Bro, huko sio kukuogopesha. Naomba usinifikirie vibaya. Nilikuwa najaribu kuonyesha mtazamo wangu juu ya mahusiano yenu basi,” alijitetea Hebert.
“Kama kuna mtu anataka kupinga mahusiano yangu na Yulia, ajaribu aone,” aliongea Hamza akiwa na hali ya kuwa siriasi.
“Bro, sijasema hivyo kwa nia ya kukutishia,” alijitetea Hebert.
Hamza alikuwa mvivu wa kuongea zaidi na kumkomoa Hebert. Alimsogelea Yulia na kumkumbatia kwa nyuma, akiogelea umbo lake. Lakini dakika hiyo hiyo walianza kusikia sauti za mtu akipaza sauti akitokea baharini akiomba msaada.
Alikuwa mwanamke alievalia koti la maabara, akiwa amefungwa kwenye boti na mwanaume alievalia mavazi meusi na walikuwa wakielekea baharini.
“Si Dokta Sarah yule!!” aliongea Hebert kwa kuhamaki.
Yulia licha ya kutomtambua Dokta Sarah vyema, lakini mavazi ya mtu ambaye alikuwa amemfunga Dokta Sarah aliyatambua vyema.
“Hamza, yale mavazi ni wale Ninja waliotaka kuniua!” aliongea Yulia kwa kuhamaki.
“Inaonekana wanataka kupata taarifa ya tafiti zetu ndiyo maana wamemteka. Imekuaje wakaweza kujipenyeza hapa kisiwani?” aliuliza Yulia.
“Pima, acha kuzubaa na fanya jambo kumuokoa Dokta Sarah kabla hajapotelea baharini,” aliamrisha Hebert.
Pima mara baada ya kupokea maagizo hayo, haraka sana alikimbilia boti na kuanza kuwafukuzia. Lakini sasa dakika ambayo yule ninja aligundua alikuwa akifukuziwa kwa nyuma, mita kama mia mbili kutoka ufukweni, alichomoa kisu na kumchoma Dokta Sarah ambaye alidondokea majini huku damu nyingi zikimtoka.
Hamza ambaye alikuwa ufukweni mara baada ya kuona tukio hilo, haraka sana alivamia boti akitaka kuingia majini.
“Unafanya nini?” aliuliza Yulia.
“Naenda kumuokoa,” alijibu Hamza wakati huo akiangalia mwili wa Dokta ukiwa anaelea juu ya maji na kusukumwa na mawimbi. Aliona kama asipookolewa mapema nafasi ya kupona itakuwa ndogo sana.
“Kuna haja gani ya kwenda kumuokoa ilihali tayari amekwisha kufa?” aliuliza Yulia akionyesha kutojali kabisa na kumshangaa Hamza kuona kwamba anataka kujisumbua kwenda kumuokoa mtu ambaye hana uhusiano wowote naye.
Kutokana na ugonjwa wake, Yulia aliamini mtu anayepaswa kusaidiwa katika hali kama hiyo ni yule pekee anayemfahamu vizuri.
alivyokuwa akikaribia, alihisi kuna kitu hakipo sawa. Ilikuwa ni kama akili yake ilianza kufanya kazi. Kwa ulinzi mkali wa kisiwa hicho, wanajeshi walipaswa kumfukuzia yule Ninja. Lakini tofauti na Pima, wote walikuwa wamesimama tu bila kufanya chochote.
Muda huo, Hebert aliyekuwa amesimama kwenye fukwe alitoa tabasamu na palepale alitoa simu yake ya kisasa. Kwa kutumia kalamu ya simu ile, alionekana kama vile alikuwa akichora kitu.
“Yulia, kwanini huwezi kunielewa siku zote? Kitu nisichoweza kupata mimi, hakuna mwingine anayeweza kukipata,” aliongea Hebert huku akicheka.
“Hebert, unataka kufanya nini?” aliuliza Yulia huku akihisi baridi usiokuwa wa kawaida.
Hebert alikuwa na tabasamu lililojaa uungwana, lakini nyuma yake alikuwa mkatili mno, alieogopwa na kila mtu. Baada ya kumwangalia Yulia kwa tabasamu, aliinua simu hiyo juu na kama vile anabadilisha chaneli, aligusa kitufe kilichokuwa kwenye simu hiyo:
BOOM!!!
JUMAMOSI INAENDELEA-WATSAPP 0687151346
Uzi mkalisana huu congratulationAsante sana mkuu
Shukran San [emoji120][emoji120][emoji120]SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

Umaskini wa akili mpaka mali huwa unapelekea mtu kuwa na hasira za kipumbavu sana,, ukichanganya na situation unayopitia ukiwa kwenye siku zako ndo kabisaaaa 😎Kwani tulikutuma utoe Mbili.
mhm!! polepoleUmaskini wa akili mpaka mali huwa unapelekea mtu kuwa na hasira za kipumbavu sana,, ukichanganya na situation unayopitia ukiwa kwenye siku zako ndo kabisaaaa
😂😂 Muda zake ni zile za wanga kueni wapole
ShukranSHETANI RUDISHA NAFSI ZETU
MTUNZI:SINGANOJR.
SEHEMU YA 137
The Earth Axis.
“Ndege mzuri huchagua mti mzuri kutengeneza kiota”
Ilikuwa ni siku ya kwanza tokea rais huyo kustaafu, kutokana na kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya uapisho wa Rais mpya, Mheshimiwa Abubakari Kassim Kunambi. Kanali alikuwa katika makazi hayo akiitikia wito wa Mheshimiwa huyo. Tokea mara ya mwisho kuonana naye Ikulu, akielekea nchini Malaysia, hakuonana naye kabisa.
Mara baada ya kufika getini na kufuata itifaki za kiusalama, hatimaye alipita na kuingia katika jumba hilo. Ilikuwa ni muda wa saa mbili hivi kwenda saa tatu, na aliweza kumuona Mheshimiwa aliyekuwa amevalia bathrobe juu ya balkoni, akimwangalia kutoka juu.
Kanali aliangalia juu na pale pale Mheshimiwa alimpa ishara ya kupandisha juu.
"Mheshimiwa, habari za jioni?" alisalimia Kanali, na kumfanya Eliasi kutoa tabasamu hafifu ambalo halikutafsirika liliashiria nini.
"Nishakuwa mstaafu sasa, Dastani."
"Hongera kwa kustaafu, Mheshimiwa."
"Huna haja ya kunipongeza, nimestaafu kicheo tu lakini mambo mengine yanaendelea, ndiyo maana na wewe upo hapa," aliongea na kisha alitoka kwenye balkoni na kwenda kukaa kwenye kiti cha straw, na alimpa ishara Kanali kukaa.
"Vipi kuhusu kazi niliokupatia, kazi ya kutafuta ile rekodi ya sauti, umefanikiwa?" aliuliza.
"Ndio, Mheshimiwa, nilifanikiwa."
"Ulifanya kama nilivyoagiza au kama kawaida yako ulikiuka maagizo yangu?"
"Mheshimiwa, nimefanya ulivyoagiza. Baada ya kuipata, nimemkabidhi mstaafu Mgweno," aliongea akiwa siriasi na kumfanya Rais Eliasi kucheka kidogo. Pale pale alichukua glasi aliyokuwa akitumia, akamimina kinywaji kidogo na kumpatia Kanali.
Kanali alionekana kusita, lakini mstaafu Eliasi alimpa ishara ya kupokea. Baada ya kupokea, alikunywa yote na kumfanya Elias kutabasamu.
"Nishakuonesha ukarimu sasa, ni wakati wako wa kuniambia kilichokuwa kwenye hiyo rekodi," aliongea na kumfanya Kanali kuwa kama mtu ambaye hajui, lakini alipoangaliana na Mheshimiwa kwa jinsi alivyomkazia macho, aliishia kusafisha koo na kumwambia.
"Mheshimiwa, nimepata kusikiliza kilichokuwa ndani ya sauti. Tofauti na kujua Chindez kuwa jasusi aliyezamia nchini kama mhalifu, hakuna cha ziada nilichoweza kupata, isipokuwa tu kuna maneno ya sauti aliyokuwa akiongea na wazungu lakini lugha yake nimeshindwa kuitafsiri mpaka sasa," aliongea.
"Unamaanisha Chindez alikuwa jasusi? Kama ni hivyo, kwanini alikuwa gerezani?" aliuliza na kumfanya Kanali kushangaa.
"Mheshimiwa, nilitaka kukuuliza wewe hili swali," aliongea Kanali.
"Sikuwahi kupata ripoti ya kesi yake. Wakati anafungwa, Mheshimiwa Mgweno ndiye aliyekuwa madarakani. Nilichoweza kusikia ni kwamba ana uhusiano na kesi iliyotokea miaka mingi iliyopita, lakini nilishindwa kuelezewa undani wa kesi yake," aliongea na kumfanya Dastani aonekane kama mtu ambaye hakuwa akiamini na kujiuliza inawezekanaje Mheshimiwa asijue kuhusu hilo, ilihali alikuwa mfungwa wa kidiplomasia.
Ukweli ni kwamba, ni kweli Eliasi alikuwa akijua kuhusu mfungwa huyo kuwa wa kidiplomasia. Licha ya kutopata kesi yake kwa undani, lakini alikuwa na taarifa nusu yake. Kitu pekee ambacho hakuwa akijua ni kuhusu mfungwa huyo kuwa jasusi.
"Ila niseme kwamba nilikuwa na mashaka yangu juu ya huyu mfungwa. Ndiyo maana baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani alivyoniletea taarifa ya uwepo wa wageni kutaka kuongea naye, nilitoa ruhusa huku nikitaka kujua kinachoongelewa ni nini," aliongea Eliasi.
"Mheshimiwa, unataka kusema wewe ndiye uliefanikisha marehemu Mchuku kurekodi sauti!?" aliuliza Kanali akiwa na mshangao kidogo.
"Mwanzoni sikutaka kumtumia Mchuku, lakini mara baada ya kugundua alikuwa na vifaa vya siri tayari, kijana niliyemwagiza kukamilisha kazi hiyo nilimwambia aweke mazingira ya Mchuku kurekodi bila ya kushitukiwa! Niseme tu kijana alizembea na kuzidiwa akili na Mchuku, ndiyo maana rekodi iliyonifikia ilikuwa haina kitu ndani," aliongea na Dastani alielewa. Pale pale alitoa flash na kumpatia Mheshimiwa.
"Kama nilivyosema Mheshimiwa, nimefanikisha kusikiliza rekodi ya sauti na nimeweza kutafsiri maneno ya sauti zao. Kwani walitumia lugha ngeni, lakini neno la mwisho nimeshindwa kulifahamu maana yake. Nilijaribu kwenda kwa mtaalamu wa lugha na ameweza kutafsiri, lakini bado hana uhakika. Anasema anahitaji muda zaidi," aliongea Dastani.
"Vipi, hujampelekea hiyo rekodi Mgweno! Wala kujadiliana naye, pengine anajua maana alionekana kuzuia sana hiyo rekodi isivuje," aliongea.
"Nimefanikiwa kumpatia na hakukuwa na maelekezo mengi kutoka kwake. Aliniambia tu napaswa kuwa makini kama nimekiuka maagizo," aliongea na kumfanya Mheshimiwa kutoa tabasamu, na pale pale wazo lingine liliuvamia ubongo wake.
"Mtaalamu wa lugha amekuambia nini kuhusu hilo neno?" aliuliza.
"Neno ni gumu, lakini kwa kulinganisha na muktadha wa maana ya maongezi, inaonekana lugha hiyo ni juu ya kitu ambacho Chindez anafuatilia juu ya aliyekuwa nacho. Nimekazia kuelewa hivyo kulingana na namna ambavyo alikuwa akibadili magereza. Inaonekana ni kama kuna mtu aliyekuwa akimtafuta gerezani," aliongea na kumfanya Mheshimiwa kumwangalia Dastani kwa tanabahi.
"Unamaanisha nini kubadili magereza?"
"Nimeweza kupata taarifa nyeti, inaonekana Silo ni gereza lake la kumi kufungwa hapa Tanzania. Ameishi katika magereza yote makubwa, alianza na Silo na kisha akarudishwa. Ukijumlisha na tafsiri aliyoishauri mtaalamu wa lugha, ni sahihi kusema Chindez kuwa mfungwa ilikuwa ni cover tu, bali alikuwa jasusi anayefuatilia mtu anayejua kitu ambacho lugha yake nimeshindwa kupata kuelewa," aliongea na Eliasi shauku ilimjaa.
"Nina uhakika Mgweno anajua kuhusu hili. Ndiye mtu aliyenipa maagizo ya kutoa ruhusa kwa Chindez kukutana na wale wazungu kwa siri. Sijui kinachoendelea ila nataka nikupatie kazi nyingine muhimu zaidi ya hii kwanza na kisha endelea na uchunguzi. Tunapaswa kujua kila kitu," aliongea.
"Nipo tayari kwa kazi yoyote, mstaafu," aliongea na Mheshimiwa mstaafu,pale pale alitoa simu yake na kumpatia Kanali.
"Soma huo ujumbe," aliongea na Kanali aliusoma ujumbe ule haraka haraka.
"Unaonekana kutoka kwa mstaafu Mgweno, lakini kwa nini inaonekana kama anakutishia?" aliuliza.
"Swali zuri. Kazi yako ni kujua kwanini anaonekana kunitishia katika huu ujumbe. Nadhani unajua kilichotokea katika uchaguzi uliopita. Sina haja ya kukuelezea kuhusu hili. Ila tokea juzi kutokee tukio la ugaidi Morogoro, kuna hisia zinaniambia Mgweno kuna anachopanga, tena tukio zima la kupindua nguvu yangu, pengine na Wanyika," aliongea na kumfanya Kanali macho kuchanua.
"Kama ni kweli, mheshimiwa, hili swala linaweza kuwa gumu. Nadhani unajua ni kwa namna gani mstaafu alivyo msiri kwenye taarifa zake," aliongea.
"Hilo lisikupe shida. Ngoja nikuambie kitu muhimu sana ambacho kitakusaidia katika uchunguzi. Nadhani unamkumbuka Mzee Masai?" Aliongea na Kanali alitingisha kichwa kumkumbuka.
"Vizuri. Moja ya watu waliosaidia kwa hatua kubwa Mstaafu Mgweno kujimalisha kwa ushawishi hapa Tanzania ni Mzee Masai. Ila kabla ya mimi kuingia madarakani, Mstaafu alimgeuka Mzee Masai baada ya kwenda nje ya ahadi na kunichagua mimi kuingia Ikulu. Na kuanzia pale, Masai akawa haelewani kabisa na Mstaafu," aliongea na Kanali alikuwa akiyajua yote hayo.
"Lakini mheshimiwa, Mzee Masai alifariki juzi tu hapa. Kuna chochote kutoka kwake?" Aliuliza na Mstaafu alikunja nne.
"Baada ya kifo cha Jongwe, mgombea chaguo la Mgweno kufariki kwa ile ajali, Mgweno baada tu ya kutoka katika kikao cha chama na Abubakari kuchaguliwa kuwa mbadala wa marehemu kuwania kiti cha urais, alimtembelea Mzee Masai hospitalini na kwa taarifa nilizopata walitumia zaidi ya masaa matatu kuongea," aliongea na kauli ilimfanya Kanali kutoa macho.
"Mstaafu alimtembelea Mzee Masai kabla ya kufariki!?"
"Ndio, hata familia yake haijui kama alimtembelea na wakaongea. Mpango ulikuwa wa siri sana ila taarifa zilinifikia. Ninachotaka ufanyie kazi ni kujua waliongea nini. Najua ni ngumu kujua ila kuna huyu mtu nataka ukamhoji," aliongea na kisha alienda upande wa majina na kumuonyesha picha.
"Madam!!!" Aliongea kwa mshituko Kanali.
"Ndio, huyu ndio anajua kila kitu, maana ndiye alicheza kwa nafasi kubwa kuruhusu kikao hiki kufanikiwa," aliongea.
Kanali alishangaa kwa sababu kwa kipindi kirefu sana Madam na Mstaafu Mgweno walikuwa na uhasama mkubwa, uliotokana na kupotea kwa mtoto wake Sedekia miaka ishirini iliyopita wakati Mstaafu Mgweno akiwa chini ya wizara ya ulinzi kabla ya kuwa raisi.
Madam alikuwa akiamini Mgweno ndio aliyempoteza Sedekia, ilishangaza kuona kwamba Madam alishirikiana na Mgweno ili aongee na Mzee Masai kwa siri.
"Mheshimiwa, mwezi uliopita niliweza kusikia taarifa za Madam kumtembelea Mzee Masai, ina maana hii siku Madam alitumika kama kivuli tu?"
"Mpaka hapo ushanipata Dastani, na wewe ndio unafaa kwa hii kazi kutokana na ukaribu wako na yeye. Najua kwa muda mrefu amekuamini na kukupa kazi ya kumtafuta mwanae. Kama nipo sahihi, lazima Mgweno ametoa taarifa iliyomfanya akatoa ushirikiano," aliongea na Dastani aliona kabisa maneno ya Mstaafu yalikuwa sahihi kabisa.
"Kanali, nina uhakika asilimia mia moja hawa watu watatu hapa nchini kuna mpango wanauandaa Mzee Kijazi, Mzee Azim na Mgweno. Njia ya kujua kuhusu mpango wao ni kupitia huyu Madam wa Taifa," aliongea na Kanali jasho lilianza kumvaa pale pale baada ya kuona ni kazi ngumu sana anayokwenda kufanya.
Madam hakuwa mtu wa kawaida sana, kama angekuwa wa kawaida asingepewa cheo cha 'Madam wa Taifa'. Lakini swali liliibuka katika kichwa chake, Madam alikuwa akimwamini kwa muda mrefu sana na kumwambia mambo yote. Imekuwaje akamficha swala la Mgweno mpaka analisikia kwa mheshimiwa Eliasi.
“Nataka tuongee ni kwa namna gani ninaweza kuwa kiongozi mkuu wa familia ya Wanyika,” aliongea huku macho yake yakiwa yamechanua.
“Au ulikuwa ukimaanisha nini? Si ulisema unataka kuazima nguvu ya familia yangu? Kama unataka hilo linitimie, ni lazima niwe mrithi pekee. Na kufanikisha hilo, unapaswa kuwafukuza warithi wengine wanaoitamani hii nafasi, na nitakubali kiroho safi kilichotokea leo. Ila kama huwezi na ulikuwa ukijisifu tu, ni bora ukaniua sasa hivi. La sivyo, nitakufanya ujue nini maana ya kisasi cha mwanamke mwenye ugonjwa wa akili.”
“Babe, mbona unaonekana kuwa na wasiwasi sana mpaka kuanza kuzungumzia malengo yako muda huu? Bado tu hujapona hapo chini lakini unaanza kuongea yanayoendelea katika familia yenu.”
“Wewe huna unachokijua kuhusu familia ya Wanyika, lakini unajitutumua na kusema unataka kutumia nguvu yake?”
“Ndio, sijui. Lakini ukinieleza wewe nitajua,” aliongea huku akimwangalia mwanamke huyo ambaye alianza kuonyesha kukasirika.
“Niondokee huko. Sitaki kukuona tena. Ondoka kwenye chumba changu!” Alifoka kwa nguvu.
Mwanzoni, alifikiria alikuwa na mpango kichwani wa kumfanya kiongozi wa familia ya Wanyika, ndiyo maana akalegea na aliwe. Lakini muda huo aliona kabisa alikuwa akimdanganya tu ili kumlegeza, na hakuwa na kitu chochote alichopanga kichwani. Kufikiria hivyo, hasira zilimpanda na hakutaka kumuona. Alitaka kukaa chini na kufikiria ni uhusiano wa namna gani kuanzisha nae kulingana na kilichomtokea.
“Acha kuwa mwepesi wa kukasirika. Kama kuna kitu unataka tuongee, tukae chini tuongee.”
“Nishasema sitaki kuongea na wewe, na ondoka. Usipoondoka, nitapiga makelele na kusema umenibaka.”
“Unaongea nini wewe? Si wewe uliekuwa ukitoa ushirikiano kwa raha nilizokuwa nakupa?.”
Hakutaka kuendelea kusikiliza, alimsogelea na kumshika kola ya shati kisha akamsukuma kumtoa nje.
Alipanga kupumzika kidogo, lakini kwa bahati mbaya alijikuta akiingia katika ugomvi na mrembo huyo. Baada ya kuona amepandisha mzuka, hakuona haja ya kuendelea kukaa hapo maana hapatakuwa na amani.
“Hebu acha makelele! Siwezi kupita mlango wa mbele. Mpaka sasa, nafahamika nimekufa. Nikitoka nje wataniona, na yule mpuuzi Herbert lazima atapanga njama tena za kudili na mimi. Mimi ndio natakiwa kufikiria namna ya kumuua na sio yeye,” aliongea akiwa amesimama, hataki kutoka, na aliposikia hivyo Yulia aliacha kumsukuma na kumwangalia kwa macho yenye maswali.
“Unapanga kweli kumuua Herbert?”
“Nisipomuua, unadhani ataniacha salama?” aliongea huku akiwa amekunja ndita.
“Nitajuaje kama unachoongea ni kweli au sio kweli? Hata hujui familia ya Kijazi ilivyo na familia yetu pia. Una ujasiri kweli wa kufanya kama unavyopanga?”
“Ikiwa Herbert atatoka katika hiki kisiwa akiwa hai, nabadilisha jina,” aliongea na kisha alitembea mpaka upande wa dirisha na kulifungua na upepo mwingi uliingia ndani.
“Unafanya nini? Usiniambie unataka kuruka kutoka ghorofa ya 24 mpaka chini?” aliongea akihamaki.
“Babe Genius, usiku mwema.”
Mara baada ya kuongea kauli hiyo, aliruka na kutokomea chini.
Yulia lijikuta akishikwa na mshituko, na alikimbia kuchungulia chini huku roho ikitaka kumtoka,akijiambia mshenzi huyo hana hata mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na anaruka umbali wote huo. Alivyoangalia kwa umakini chini, alijikuta akishangaa baada ya kumuona akitua salama kwenye nyasi za bustani kwa miguu yake na kisha alipotea palepale ndani ya lile eneo.
Aliishia kufunga dirisha taratibu huku akishika kifua chake eneo la moyo na kufumba macho. Mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio mno. Kama ingekuwa ni mwanajeshi ambaye ana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ndiyo alieruka kutoka ghorofa hiyo, asingeshikwa na tahamaki. Lakini Hamza hakuwa kabisa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, lakini ameweza kuruka na kutua bila ya kuumia. Alijikuta akijiuliza, Hamza ni nani hasa kuwa na uwezo wa ajabu?.
Hamza hakwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Herbert sio kwamba alikuwa akimuogopa, lakini ni kwa sababu bado hakuwa ameona utafiti na majaribio yaliomfikisha hapo kisiwani. Alikuwa na wasiwasi kwamba, ikiwa atamuua Herbert mapema, mambo yanaweza kubadilika na wale ambao wanamuunga mkono wangewekeza umakini wao katika kushindana naye na sio kwenye majaribio tena.
Hata hivyo, kwa sababu ilikuwa ni usiku, Hamza hakupanga kulala. Isitoshe, alikuwa amekuja hapo kama mlinzi, hivyo aliona sio mbaya akipiga doria kwenye kisiwa hicho akisubiria kupambazuke. Kingine, hakutaka kulala kwenye chumba chake kwa sababu alitaka kuendelea kujificha ili asitambulike kama alipona kwenye lile bomu.
Ijapokuwa kulikuwa na wanajeshi wengi waliokuwa kwenye doria, lakini ilikuwa rahisi kwake kuwakwepa wasimuone. Hamza, mara baada ya kutembea mpaka ufukweni, aligundua kulikuwa na mtu aliyekaa kwa kuegamia jiwe huku akiota moto akiwa pia ameshikilia chupa ya whiskey.
Hamza alisogea kwa tahadhari mpaka eneo hilo na mara baada ya kumjua ni nani, aliachia kicheko.
“Ni wewe, haha… nilikuwa na wasiwasi nitakuwa mpweke kwa kukosa cha kufanya, kumbe umeshaweka mambo sawa na hizo wine kibao," aliongea Hamza na kukaa chini.
Mwanaume yule, mara baada ya kumuona Hamza, uso wake ulibadilika palepale kwa mshituko.
"Ahhh! Wewe ni mzimu au binadamu?" Aliongea yule mtu.
Mwanaume huyo alikuwa ni Pima, mwanajeshi na mwanafunzi wa Shirki ya Hansii kutoka India. Kitendo cha Pima kukataliwa na Herbert maana yake alikuwa amekataliwa na familia yake yote na kutokana na machungu ya kudharauliwa, aliishia kuja kukaa hapo na kunywa ili kupunguza mawazo.
"Mimi ni mzimu ndio," aliongea Hamza na kisha alichukua chupa ya mvinyo, akafungua na kuanza kuigugumia.
"Naona una kivuli, inamaanisha hukufariki?" Aliongea kwa mshangao. Alijua siku zote jini au mzimu hauna kivuli kama ilivyo kwa binadamu; ukitaka kujua mtu ni jini au mzimu nyakati za usiku, angalia kama kuna kivuli. Ukiona anatembea bila ya kivuli licha ya mwezi, kimbia au sali.
"Naona unataka sana kuona nikifa. Una kinyongo gani na mimi kwani?"
"Unajua nguvu ya lile bomu? Ni yale mabomu maalumu yanayotumika kwenye manowari. Unataka kuniambia hata bomu la ukubwa ule haliwezi kukuua?" Aliongea huku akifadhaika kwa jambo hilo.
"Ukweli ni kwamba nilishikwa na uziwi kutokana na sauti ya mlipuko wake, lakini kuhusu ngozi yangu ni ngumu. Na ukizingatia nilikuwa kwenye maji, kwangu bomu kama lile haliwezi kuniletea matatizo."
"Kama ni hivyo, ngoja nikamwambie bosi wangu," aliongea akitaka kwenda kumwambia Herbert juu ya kuwa na uwezo uliopitiliza fikra za kibinadamu. Aliona mpaka hapo bosi wake alikuwa hatarini.
Hata hivyo, baada ya kupiga hatua, alijikuta akisimama huku uso wake ukijikunja na kuhisi maumivu kwenye moyo wake. Hamza wala hakuwa na wasiwasi kwa bwana huyo kuondoka, na aligeuka kumwangalia baada ya kuona amesimama.
"Mbona umesimama, au umeghairi? Unaweza kwenda tu, siwezi kukufanya chochote," aliongea, na bwana huyo alijikuta kivivu sana akigeuka na kukaa chini.
“Hata kama nikienda kumwambia upo hai hawezi kuniamini yule, siku zote anapenda kuamini kile anachoona kwa macho yake na sio vinginevyo.”
“Kuna msemo unasema; ‘ndege mzuri huchagua mti mzuri kutengeneza kiota’. Imekuwaje ukawa chini ya mtu kama Hebert kama bosi wako? Unaonaje ukiwa chini yangu, naweza pia nikakuunganisha na ukawa mlinzi katika kampuni ya mke wangu,” aliongea Hamza na kumfanya Pima kuinua uso wake na kumwangalia Hamza.
“Moja ya sababu kubwa ya sisi Watanzania kuweza kwenda kujifunza mapigano nchini India chini ya shirki ya Hansii ni kutokana na ushirikiano mkubwa wa familia ya Mzee Azim na Kijazi. Nadhani unajua ni kwa namna gani shirki za India zilivyo na ubaguzi kuruhusu watu wa nje ya taifa lao kujifunza mbinu zao? Kuna wanajeshi wengi ambao wamejifunza chini ya Hansii na yote hayo yamewezekana kutokana na familia ya Mzee Azim ambaye ni mkwe wa familia ya Kijazi, mpaka sasa ndio wafadhili wakubwa. Nilikuwa na miaka kumi na tisa tokea nipewe kazi ya kumlinda bosi Hebert na imepita miaka saba mpaka sasa,” aliongea.
“Alipanga kukuua kwa lile bomu na wewe pia, lakini bado unataka kuwa mtumwa wake?”
“Huna haja ya kuniambia maana najua, ila napanga kuendelea kuwa mtiifu chini yake, hata kama akiniua, sitokuwa na majuto.”
“Acha kuwa siriasi namna hiyo, nilikuwa nikijaribu kuulizia uwezekano wa wewe kuwa chini yangu basi.”
“Niseme tu una uwezo wa ajabu sana kwa mtu ambaye huna hata ishara yoyote ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Nikijaribu kufikiria kuhusu hili naona ndio maana wakuu wamekuleta kuwa mlinzi wa Bosi Yulia,” aliongea lakini Hamza hakuwa na hamu ya kuendelea na aina hiyo ya mazungumzo na alisimama palepale.
“Nishaanza kuboreka kunywa bila kuwa na cha kutafuna, ngoja nikatafute samaki kadhaa tuje tuwachome,” aliongea Hamza.
Pima aliishia kumwangalia Hamza bila ya kuongea neno, hata yeye hakuwa amepata chakula cha usiku bado, baada ya Hamza kutoa pendekezo hilo ni kama njaa ilishituka.
“Unaenda kuwapatia wapi, au unataka kuchukua hotelini?” aliongea akiwa ni kama hajaelewa Hamza alichokuwa akimaanisha.
“Baharini hatukosi kamba wadogo wadogo, hakuna haja ya kwenda hotelini kuchukua,” aliongea.
“Usiniambie unataka kuingia baharini kwenda kuvua! Huwezi kupata kamba huku karibu na ufukweni, mpaka kwenye kina kirefu kidogo na lazima pia uwe na vifaa ambavyo hatuwzi pata muda huu,” aliongea Pima akiwa katika hali ya mshangao.
Hamza hakutaka kupoteza muda kuongea nae na palepale alivua nguo zake zote na kubakiwa na boksa tu na kisha alianza kukimbia kuelekea baharini na mara baada ya kufika kwenye kina kirefu alipiga mbizi na kupotea.
Pima alishindwa kuelewa Hamza anataka kufanya nini na alijikuta akikimbia upande wa majini bila kujali alikuwa amevaa suruali akitaka kujua Hamza anafanya nini.
Ndani ya dakika kama bili na nusu hivi Hamza aliibukia akiwa ameshika samaki ambao hata hawakueleweka ni aina gani ya samaki na kumrushia Pima.
“Kaanze na hao, ngoja nikakamate wengine,” aliongea na kisha palepale alipiga mbizi bila kujali mshangao aliokuwa nao Pima.
Alitumia dakika kumi na alifanikiwa kukamata kamba wadogo wadogo, kaa na samaki wadogo na kisha akarudi ufukweni na kuvua hata poksa aliokuwa amevaa kutokana na kuloa.
“Hukuwa hata na vifaa lakini umeweza kupiga mbizi kwa muda mrefu kiasi hiki?”
“Kina ni kifupi sana, vifaa vya nini, ninao uwezo wa kupiga mbizi mpaka zaidi ya mita mia moja chini ya bahari bila shida yoyote, hapo nimeenda mita kumi tu,” aliongea Hamza.
“Mita mia bila kifaa!!? Wewe ni nani hasa?”
Alishangaa kwa sababu alikuwa akijua, binadamu wanaopiga mbizi mara nyingi wanaishia mita mia tatu hivi kwenda chini tena wakiwa na mitungi ya gesi na vifaa maalumu vya kujilinda, lakini Hamza anasema anao uwezo wa kwenda mita zaidi ya mia bila ya kifaa, hata hizo kumi alizoenda na kukamata samaki haikuwa kawaida kabisa. Maana yake ni kwamba spidi yake ya kuogelea ilikuwa kubwa mno kuzidi samaki ikionyesha haathiriwi kabisa na presha ya maji.
“Nilikuchukulia poa sana, ila sidhani hata kama wewe ni binadamu,” aliongea.
“Hebu acha porojo na kaa chini tule samaki bwana, unaonekana kuna mambo mengi kuhusu dunia huyajui kama na hili linakushangaza,” aliongea.
Pima alijikuta akinywea, hata ile hali ya kujiamini mbele ya Hamza ilimpotea na aliishia kukaa huku akiwa na haya usoni.
Baada ya kuanza kula, stori nazo zilichukua nafasi yake, walianza kuongea vitu vingi sana ambavyo vilikuwa nje ya mada ya yale yaliyojiri mchana wa siku hiyo.
Hamza alionekana kuridhika sana wakati wa kutafuna samaki na kushushia na mvinyo, ilionekana ni dhahiri kwamba alikuwa na uwezo wa kuishi katika kila aina ya mazingira.
“Kama bosi wako amekukataa, unapanga kurudi jeshini au India, najua unaweza kuwa mwanajeshi lakini pia unaweza kuishi chini ya shirki uliojifunzia na kupata uraia kabisa,” aliongea Hamza.
“Napanga kurudi mafunzoni kwa muda, bado uwezo wangu sio mkubwa sana.”
“Haina haja ya kuharakisha kurudi mafunzoni, unaonaje ukikaa kwanza Dar kwa muda kupumzika, tunaweza kukutana mara kwa mara na kula bata.”
“Mr. Hamza, nashukuru kwa mwaliko, lakini…”
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi, sijakualika kwa ajili ya kuwa chini yangu. Najua kulingana na sheria huwezi kubadilisha shirki, nimekuona tu kama mtu mzuri usiye mnafiki ndiyo maana nimeona tunaweza kuendana vizuri tukiwa marafiki. Kama unaona ni ombi kubwa sana kwako, potezea.”
Hamza, licha ya kuona bwana huyo sio mtu mbaya sana, lakini vilevile mpango wake ulikuwa ni kutaka kupata taarifa za kutosha kuhusu Azim na washirika wake, lakini vilevile anaweza kujua nini kinaendelea chini ya Hansii. Kwa hisia zake, aliamini familia hiyo kupeleka Watanzania kwenda kujifunza mapigano sio bure, lazima kuna mpango wanapanga.
“Kama kweli unanialika basi nitakuja kukutembelea,” aliongea, na Hamza alitoa tabasamu na kumpa ishara ya kugonga cheers, huku wakiendelea kupata mvinyo.
Lakini dakika hiyo hiyo, wote walijikuta wakishituka mara baada ya kusikia mlipuko mkubwa.
Boom! Boom!
Hamza alijikuta akigeuza kichwa chake na aliweza kuona mlipuko huo umetokea uelekeo wa hoteli. Aliweza kusikia mfululizo wa milipuko ikigonga katika hoteli na kusababisha moto mkubwa na moshi huku jengo likianza kulia king’ora.
Pima naye hakuishia kuangalia tu bali alitoa macho akiwa haamini kile anachoona.
Hamza hakuwa na muda wa kuongea neno tena; palepale aliamka na kuanza kukimbia kuelekea hotelini.
Pima alijikuta akishituka mara baada ya kuona Hamza amepotea mbele yake, na pale ndipo alijua spidi ya Hamza haikuwa ya kawaida.
“Hili ni tatizo, bosi Hebert,” Pima alijikuta akikumbuka bosi wake pia alikuwa ndani ya hoteli, na licha ya kutukanwa mchana hakutaka kumuona akipoteza maisha, na palepale alikimbilia uelekeo huo.
Kitendo cha hoteli kulipuka bomu kilikuwa kimeshitua wanajeshi wote waliokuwa wakilinda katika kisiwa hicho. Makamanda wa vikosi vya ulinzi walitoa maagizo haraka kukimbilia hoteli kuanza zoezi la kuzima moto.
“Hakikisheni mnawaokoa watafiti, okoeni kila mmoja asitokee kufa mtu!”
Sauti za makamanda zilisikika huku wengi wakikimbilia hoteli kwa haraka.
Hali ilikuwa mbaya mno kwa sababu kila floor ilikuwa imeshika moto. Jengo hilo lilikuwa imara, ndio maana halikudondoka, lakini haikumaanisha lilikuwa na uwezo wa kujilinda na moto.
Wanajeshi wengi walioletwa ndani ya kisiwa hicho walikuwa makomandoo na hakuna aliyeogopa moto. Ngazi maalumu za kupanda juu zilifunguliwa na walianza kuingia kwa kasi kufanya zoezi la uokozi.
Kamanda Luvanga, aliyekuwa nje ya jengo hilo akitoa maelekezo ya uokozi, alijikuta akishangaa baada ya kuona kundi la wanajeshi waliovaa mavazi ya kujikinga na moto na mahelmeti usoni wakiingia ndani ya jengo kwa kukimbia. Hawakuonekana hata ngozi zao zilivyo wala sura, na pia walikuwa na spidi sana.
“Hii timu ya wanajeshi wanaoingia ni kutoka kikosi gani, na imekuwaje wakawa na vifaa vya zima moto kwa muda mfupi?” aliuliza kamanda mwingine akiwa ameduwaa.
“Haina maana kuuliza sasa hivi, ngoja uokozi uendelee kwanza,” aliongea kamanda akipotezea wanajeshi wale.
Walikuwa wengi, takribani wanajeshi kumi waliongia kwenye hoteli hiyo wakiwa na vifaa maalumu vya kujikinga na moto pamoja na mahelmeti. Wanajeshi waliwapisha bila kuwajali kama walikuwa wenzao au la.
Lakini mara baada ya kutaka kuingia kwenye lift, walizuia na kapteni mmoja aliyeongoza kikosi chake alionekana kuwashangaa wakitaka kutumia lift badala ya ngazi.
“Nyie mmetokea kikosi gani? Hamuelewi maelekezo, tumieni njia ya dharura. Mnataka kujitafutia kifo kupanda lift?” aliongea kamanda yule aliyeongoza na wanajeshi wenzake watatu.
Lakini sasa hawakujibu kwa sauti, kwani mmoja wa wale wanajeshi alitoa bomu la rangi ya silver kwenye mfuko wake na kuwarushia.
Wanajeshi wa Kitanzania hawakuwa hata na muda wa kujiandaa kukabiliana na bomu lile. Hawakujua kwanini wenzao waliwarushia bomu, kilichosikika ni ‘peng’; wanajeshi wote watatu walilipuka palepale.
“Hey! Jason! First, open the passage to the military laboratory! Ignore these Tanzanian! Otherwise we will be exposed!” [“Hey! Jason! Kwanza fungua mlango wa kuelekea maabara ya kijeshi! Puuza hawa Watanzania! Vinginevyo tutagundulika!”] Sauti ya Kizungu ilisikika kutoka kwa wale wanajeshi waliokuwa wamevaa mavazi ya kujikinga na moto na mahelmeti usoni.
“Kleig, tatizo lako unafikiria sana. Hawa wanajeshi wa Kitanzania wapo kwenye mfadhaiko kudili na moto. Kama hawajatushutukia, nani ataweza kutugundua?” mwanaume aliyeitwa Jason aliongea.
“Captain Cleig! Disintegrating laser rifle is ready!” [“Captain Cleig! Risasi ya laser ya kupasua tayari!”]
“Safi sana! Tengeneza njia sasa,” Cleig aliongea.
Mwanajeshi mmoja alivua gloves zilizokuwa zimefunika mikono yake, na palepale mkono wa chuma ulionekana. Haikueleweka kama lilikuwa roboti au mtu amevaa suti ya kiroboti, lakini mbele kwenye mkono wake kulikuwa na slot yenye kutoa nishati ya moto wa laser.
Miale ya nishati hiyo ya moto mara baada ya kugusana na chuma cha lift ilikuwa kama kisu kinakata kile chuma, na kutengeneza shimo kubwa kwenye sakafu ya lift hiyo.
“Kazi nzuri, Jason. Wewe baki hapa, nitaongoza vijana kwenda chini,” aliongea.
“Hakuna shaka, Cleig. Unapaswa kufanya haraka; vinginevyo, naweza kuua kundi la wanajeshi watakao kuja upande wangu,” aliongea.
Cleig aliishia kuonyesha sura ya tabasamu la kejeli, kisha baada ya vijana wake kuruka kwenye lile shimo, naye aliruka na kwenda kudandia kamba za lift na kutua mpaka chini.
Ijapokuwa wanajeshi hao wa Kizungu hawakuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, lakini kwa namna walivyoruka mpaka kutua chini, hakuna aliyejiumiza hata kidogo.
Mara baada ya kufika katika maabara hiyo kubwa ya kijeshi, Cleig aliangalia kifaa kama simu alichovaa kwenye mkono wake na palepale ramani ya maabara hiyo yote ilionekana kwenye kijiskrini kile kilichokuwa kama saa, na kisha aliwapa ishara vijana wake kumfuata.
“Nifuateni, ni uelekeo huu,” aliongea.
Wote wanne haraka sana walielekea upande wa kaskazini wa maabara hiyo kwenye moja ya jengo.
Ndani ya maabara hiyo sio kama hakukuwa na watu. Afande Makwela alikuwa ndiye amepewa jukumu zima la ulinzi ndani ya maabara, na mara baada ya kupewa taarifa kwamba kuna uwezekano wa kambi hiyo kuvamiwa na adui, haraka sana aliwahimiza wenzake kuhifadhi taarifa zote za kisayansi.
“Haraka sana, hifadhini taarifa zote muhimu!” aliamrisha huku akipiga makofi kuwahamasisha, akienda mbele na kurudi nyuma akihimiza wanasayansi hao na watu wa maswala ya IT kuhakikisha kabla ya adui hajafika wawe wamehifadhi data na kisha kufuta kila kitu kabla ya kuchukuliwa na adui.
Lakini sasa wakati akihimiza watu wake kufanya kazi hiyo, hatimaye wanajeshi wanne waliovaa mavazi ya kujikinga na moto pamoja na risasi walikuwa wakiingia ndani ya maabara hiyo, na makomandoo waliokuwa wakilinda mlango wa kuingilia ndani ya maabara waliuliwa mara moja na bunduki za mionzi.
“All of you, let go of your work! Hands up! Face the wall!” [“Wote acheni mnachokifanya! Mikono juu na angalieni ukuta!”] Kapteni Cleig aliongea kwa kuamrisha.
Afande Makwela alijikuta akikunja uso na macho, akishangaa kuwa wamevamiwa ndani ya maabara na vilevile alishangaa baada ya kumgundua adui.
“Wanajeshi wa Kimarekani! Mnafanya nini kwenye ardhi yetu?” aliuliza Afande Makwela, akimfanya Cleig kumwangalia eneo la bega lake kujua cheo chake.
“Inaonekana wewe ndio kiongozi hapa. Waambie wanajeshi wako wanyooshe mikono juu na kuangalia ukuta. Hatupo hapa kuua mtu; tutachukua tunachotaka na kisha tutaondoka,” aliongea.
“Mmeingia katika eneo la nchi yetu halafu unatuamrisha? Mnataka kuanzisha vita?”
“Wajinga nyie Watanzania! Mlionywa mara ya kwanza, acheni ushirikiano wenu na Urusi, mkakaidi. Tukawaonya acheni kutengeneza silaha za maangamizi, mkaendelea kufanya hivyo. Mnadhani hatujui kinachoendelea hapa ndani? Silaha mnazotengeneza ni tishio kwa usalama wa dunia, na ni jukumu letu kuwazuia,” aliongea Kapteni Cleig, na palepale alitoa mkono wake wa roboti.
Mwili wake ulikuwa kama wa simba, alisogea kwa spidi na kwenda kumvaa Afande Makwela, akishika shingo yake.
“Speak! Where is the experimental device!?” [“Ongea! Kifaa cha majaribio kiko wapi!?”] aliamrisha akimwambia aonyeshe kifaa cha majaribio.
Afande Makwela uso wake ulikuwa hauelezeki kwa hofu, lakini ujasiri haukumuondoka mwilini.
“Mimi ni mwanajeshi, siwezi kusaliti kiapo changu, acha kunigopesha,” aliongea.
“Mhmh, unadhani usipoongea hatutoweza kukipata?” aliongea na kisha aligeuza macho yake upande wa kulia na kisha alitoa tabasamu hafifu.
“Professor Ndiswe, it has been hard on you this time. Do you know where the experiment apparatus is located?” [“Profesa Ndiswe, umepata shida sana. Unajua kifaa cha majaribio kilipo?”] aliongea akianza kumpa pole Profesa Ndiswe kwa suruba iliompata njiani kabla ya kufika hapo na kumuuliza kama anajua kilipo kifaa cha majaribio.
“Profesa Ndiswe kumbe ulikuwa ni shushu wao!?” aliuliza Afande Makwela akiwa haamini.
Muda ule ndio sasa anajua kwanini wale magaidi hawakumuua zaidi ya kumuumiza mkono pekee licha ya wanajeshi waliokuwa wakimlinda kufa wote. Kumbe walimuacha hai makusudi, zilikuwa hila za kuonyesha kwamba alikuwa akiwindwa ila kumbe ni kiini macho.
“Watanzania asanteni kwa ujinga wenu, ijapokuwa bado sijaelewa vizuri kuhusu kifaa na majaribio yake, lakini nimepata taarifa zote muhimu,” aliongea.
“Vizuri sana Ndiswe, General kawasalimie kuzimu,” aliongea Cleig na palepale ule mkono wake wa roboti ulifyatua visu na kumchoma Afande Makwela shingoni na ikawa ndio mwisho wake.
“Jeneralii!!”
Kundi hilo la wanasayansi wa kijeshi waliishia kupiga makelele wasiamini Afande Makwela amekufa namna hiyo.
“There's not much time left. I'll now bring you all to that laboratory, and the Earth Axis is also there”aliongea Profesa Ndiswe, akimaanisha kwamba muda hautoshi na atawaongoza kwenda katika maabara ambapo pia kifaa Earth Axis kimehifadhiwa.
“What!? The earth's axis is also here!? That is an unexpected surprise!” [“Nini!? Earth Axis pia iko hapa!?]” Afande Craig alishanga kusikia Earth Axis pia ipo hapo, kitu ambacho hawajategemea kukikuta hapo ndani wala kukijia.
“Ndio Kapteni, lakini ulinzi wake ni mkubwa mno, tunapaswa kuharakisha la sivyo hatuwezi kufanikisha ndani ya muda,” aliongea Profesa Ndiswe.
“Halafu Kapteni huyu binti Yulia ni jiniasi sana, tunapaswa kuondoka naye au hata kumuua la sivyo hata kama tuweze kuipata Earth Axis hatuwezi kuizuwia Tanzania kuendeleza majaribio,” aliendelea kuongea Profesa Ndiswe.
“Usiwe na wasiwasi juu ya hilo, Kanali Bird yupo kwenye kazi hyio. Ongoza njia,” aliongea na kisha aligeuka na kuwapa ishara vijana wawili.
You guys stay here! Anyone who enters this base will be killed”aliongea akiamrisha kwamba wabakie hapo na yoyote atakaeingia auawawe.
“Boom! Boom!”
Ulikuwa ni mwendelezo wa milipuko iliokuwa ikisikika katika kila floor na kusababisha moto kuendelea kusambaa kwa kasi ndani ya hoteli hiyo.
Ndani ya chumba cha Yulia, mwanamke huyo alikuwa akiwaza juu ya siku ya kesho katika majaribio ya kwanza, lakini baada ya mlipuko wa ghafla na jengo hilo la hoteli kushika moto, alijikuta akipaniki na kutaka kukimbia.
Lakini dakika ambayo anataka kukimbia kuomba msaada alikumbuka floor hiyo ilikuwa ikilindwa na wanajeshi wachache sana, na wote walikuwa wakikimbilia kwenye ngazi maalumu za dharura kujiokoa.
Daklika hiyo hiyo sauti ya Yulia kuitwa ilisikika, alikuwa ni Bertha bodigadi wake.
“Betha, milipuko imesababishwa na nini?” aliuliza Yulia.
“Acha kwanza kuuliza juu ya milipuko, usalama wako ndio kipaumbele kwa sasa,” aliongea lakini muonekano wa Yulia ulibadilika.
“Haiwezekani kuwa kirahisi hivi, lazima kutakuwa na mpelelezi aliyezamia katika hiki kisiwa mapema, vinginevyo isingekuwa rahisi kutega mabomu ndani ya hoteli.”
“Ishatokea tayari na hatuna tunachoweza kufanya, muhimu ni kujiokoa kwanza,” aliongea Bertha.
Yulia alikuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa, alitamani kukimbia kwenda kwenye kambi ya maabara kuona kinachoendelea, lakini alijua asingeweza kufanya hivyo.
“Okey, nichukue tutoke hapa kwanza ndio nitajua cha kufanya,” alisema akianza kupiga hatua kuelekea upande wa lift.
“Mkurugenzi hatuwezi kutumia lift, kama uwezo wangu usipotosha nitakuchukua kukushusha kupitia njia ya dharula.”
“Sawa, ongoza njia.”
Bertha hakutaka kupoteza muda na alitembea kuelekea njia ya dharula.
Kutokana na urefu wa jengo na upepo kutoka baharini, moto ulisambaa kwa kasi sana, ijapokuwa baadhi ya mifumo ya hoteli hiyo haikuwa imeharibika lakini haikuwa na maana kutumika katika muda huo.
Wawili hao hawakutembea umbali mrefu baada ya kuona bahari ya moto mbele yao ikiwazuia kupita upande wa pili na kama wangetaka kufika katika njia ya dharula ya kujiokoa kwenda nje, iliwaruhusu kupita kwenye moto huo.
“Kapteni una bahati mafunzo yangu nimeyapata katika Shirika la Holly Fire la sivyo tungekwama hapa,” aliongea Bertha huku akicheka.
Na palepale mwili wake ulianza kujitutumua na nishati za mbingu na ardhi zilianza kujikusanya katika mwili wake, huku kwenye mkono wake uliibuka moto wa rangi nyeupe ambao alianza kuuzungusha kwa kutengeneza mzingo na kisha palepale aliusukumizia kwenye lile dimbwi la moto na ajabu ni kwamba ule moto wa kawaida ulisogea pembeni na kutengeneza njia katikati.
Palepale alimshika mkono Yulia aliyeonekana kuwa na mshangao .
“Mbinu ya mafunzo ya nishati ya Holly Fire inaweza kukinga moto wa kawaida?” aliuliza.
“Kikanuni moto mweupe una nguvu zaidi kuliko moto wa njano, huu moto ni wa kawaida na katika mpangilio wa miale ya moto ndio wa mwisho. Unadhani kwanini kitengo cha Malibu wanalipa hela nyingi kutupeleka makomandoo kujifunza mbinu hii? Ni kwa sababu ya kudili na hali kama hizi,” aliongea Bertha.
“Acha maelezo mengi, tuondoke joto kali,” alisema Yulia lakini ile anamaliza kuongea palepale alisikia sauti ya mtu ikiita kutoka mbele yao.
Palepale waliweza kumuona mwanaume alievalia kombati za kijeshi, bwana huyo alikuwa mweusi lakini kombati zake hazikuwa za jeshi la Kitanzania.
Ajabu zaidi ni kwamba mwanajeshi yule jicho lake la kushoto halikuwa la kibinadamu, lilikuwa jicho la kielektroniki na lilikuwa na mstari wa mwanga katikati uliokuwa ukizunguka.
“Reporting to Colonel Bird, we have confirmed the target, would you like to take action!?” aliongea kwa Kingereza akitoa ripoti kwamba shabaha imeonekana na je achukue hatua.
“Yes!” alijibiwa achukue hatua.
Mara baada ya kuruhusiwa, palepale bwana yule alimsogelea Yulia kwa spidi bila kuogopa ule moto na hata ulipomuunguza hakuathirika kabisa.
“Ahhh!, Huyu ni shetani!” alihemka Afande Bertha palepale mara baada ya kumuona yule bwana akitembea kwenye moto bila shida yoyote na palepale alimrushia ule moto wa kitakatifu uliokuwa kwenye mikono yake.
Sauti ya Bang, ndiyo iliweza kusikika ule moto wa Bertha ulivyotua katika kifua cha yule mwanajeshi.
Argghh!
Yule bwana mweusi aligunguruma huku akikinga mashambulizi ya ule moto na mkono wake wa kulia, lakini nguo zake zote ziliunguzwa na palepale mwili wake ulionekana ukiwa sio wa kawaida, ilikuwa ni kama ngozi yake imeshonewa na chuma tupu kwa ustadi wa hali ya juu mno.
Yulia mara baada ya kuona mwanajeshi yule na kile chuma mwilini, macho yalimtoka huku hali ya hofu ikimkumba.
“Bertha ni mwanajeshi wa Zero Delta huyo, Daah! Wamewaleta hadi hawa?”
“Zero Delta Squadron! Hivi kumbe ni kweli wapo?” Aliongea Bertha macho yakimtoka.
Yulia alikuwa akifahamu sifa za kikosi hicho kutoka nchi ya Washington. Kikosi hicho kilikuwa kikiaminika kipo lakini hakikuwahi kuonekana hadharani.
Miaka kadhaa nyuma, jeshi la Kimarekani lilipigwa marufuku na Umoja wa taifa kuacha mara moja kutengeneza wanajeshi hao, lakini ilikuwa ni kauli hewa tu, isitoshe umoja huo ulikuwa chini ya mkono wa Mmarekani. Kwa nje taarifa ilitolewa nchi hiyo imeacha kuunda hilo jeshi lakini ilikuwa geresha tu, zilikuwa ni moja ya siraha za kimaangamizi zilizoandaliwa na nchi hiyo kwa siri, huku kwa raia ikifahamika kama fununu tu.
“Unashangaa ujinga, kama ilivyo kwa jeshi letu kuwa daraja A na kuunda siraha za siri, Delta Zero pia ni kikosi ambacho kipo na cha siri. Ni kwa sababu tu sikuwahi kutarajia wamefikia maendeleo ya namna hii,” aliongea Yulia.
Yulia alikuwa akijua mataifa makubwa duniani kama China na Marekani walikuwa na siraha zao za siri ambazo hazionyeshwi hadharani hata siku moja. Kama sio kwa ukubwa wa kile ambacho anafanyia utafiti, kikosi kama hicho kisingetumwa na hata kama wangetuma wanajeshi wa kawaida kwa ulinzi uliowekwa, wangetumia kiasi kikubwa cha rasilimali.
“Huyu mwanajeshi mwili wake umeunganishwa na chuma, ndiyo maana anao uwezo wa kutembea kwenye moto bila shida yoyote,” aliongea Bertha kwa mshangao.
Yule mwanajeshi hakuongea neno, alikuwa kama roboti kwa namna alivyokuwa akionekana na pale alifyatua miale ya laser yenye kiwango kikubwa cha joto kumlenga Bertha.
Bertha hakusubiri kushambuliwa kizembe kwani palepale na yeye alikusanya nishati za mbingu na ardhi na palepale duala la ngao ilijitokeza mbele yake.
“Holy fire shield!”
Ile miale ya laser ilisambaratishwa na kumfanya yule mwanajeshi kutamka maneno hayo kwa mshangao kiasi na palepale alirusha shambulizi lingine lenye nguvu zaidi na kumfanya Bertha kuruka pembeni kwani licha ya ngao yake kuzuia lile shambulizi, lakini haikuzuia mionzi yote.
Yulia alipiga kelele mara baada ya kuunguzwa katika mkono wake.
“Bosi Yulia!!” aliita Bertha kwa hamaki mara baada ya kuona hana uwezo wa kukinga mashambulizi hayo kwa asilimia mia moja hivyo yangemuumiza Yulia.
“Kimbia kwanza kurudi nyuma, nitamuua kwanza ndio tuondoke,” alisema Bertha na pale palepale alimsogelea yule mwanajeshi na kupambana naye ana kwa ana baada ya kuona kitu pekee kitakachomuua ni uzito wa ngumi zake zenye kuimarishwa na nishati.
Lakini licha ya kutupa ngumi kwa ustadi mkubwa ilikuwa ni kama bure kwani yule mwanajeshi wa Delta Zero mwili wake umetengenezwa kwa chuma kigumu sana (Alloy).
Uwezo wake wa kukinzana na uzito wa ngumi na joto ulikuwa mkubwa sana, hata baada ya kupokea ngumi na mateke mazito hakuathirika hata kidogo.
“Go to hell! Warrior” alikoroma yule mwanajeshi kwa sauti na pale palepale aliunganisha mikono yake kwa pamoja na palepale katika kwenzi za vidole vyake kulichomoza mionzi tofauti na ile ya mwanzo.
Bertha kwa spidi ya ajabu palepale alitengeneza ngao takatifu kufyatua pembeni ile mionzi, lakini ile mionzi ni kama iligonga kila pande kwa spidi ya ajabu mno na kushindwa kuizuia.
Palepale alijikuta akifubaa, alijua mwanajeshi huyo alichokuwa akifanya ni kumzubaisha upande mmoja ili kupata mwanya wa kumshambulia Yulia aliye nyuma yake.
Yulia alijikuta akianza kutetemeka, ukuta ulianza kuporomoka kutokana na nguvu ya shambulizi lile na kumfanya aone mwisho wake umekaribia.
Kitendo cha Bertha kuzubaa palepale shambulizi lilipita ile ngao yake kumsogelea Yulia.
“Yuliaa!!”
Bertha aliita kwa nguvu huku akikosa namna ya kwenda kumsaidia Yulia, ikiwa imebakia kidogo tu palepale kivuli cha mtu kilitokeza na kuruka juu na Yulia na shambulizi lile likapita na kuporomosha mawe upande wa pili na kubomoa korido hiyo.
“Damn! Damn…” Bertha alijikuta akipatwa na ahueni na hasira kwa wakati mmoja na alitumia fursa ya kumshambulia yule mwanajeshi aliyezubaa baada ya shambulizi lake na kutokana na kutumia nguvu nyingi alimpiga kwa nguvu na kumfanya aende kujigonga ukutani kama furushi.
“Genius! Bado tu hutaki nikiwa karibu yako!” aliongea Hamza aliyeukinga mwili wa Yulia asiathiriwe na matofari yanayoporomoka.
Yulia aliishia kumwangalia Hamza bila ya hisia zozote, muda huo sura yake ya kirembo ilikuwa imechafuka na vumbi na kumfanya aonekane kutia huruma. Alikuwa akionyesha ni kwa jinsi gani alishukuru Hamza kutokea na kumwokoa maana alikiona kifo.
Unadhani Earth Axis ni kitu gani? Simulizi ina mambo sana hii, tuendelee kula rojo , nyama na mifupa yake ipo chini.
SEE YOU UNTILL NEXT.
NICHEKI WATSAPP 0687151346 UPUNGUZE AROSTO , niwaibie siri Hamza yupo PAris , ufaransa na Regina mambo ni moto sana.
AsanteSHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

CoolSHETANI RUDISHA NAFSI ZETU