Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR

MHARIRI: ZEROS LITERATURE

SEHEMU YA 133

Mtaalamu​

‘Neema ya tone la maji hulipwa kwa chemchem.’

Staili ya uvaaji wa Yulia ilimpagawisha mno Hamza na kumfanya amkodolee macho kwa sekunde kadhaa.

"Mbona unanikodolea macho? Ijapokuwa mimi ni mrembo, hapaswi kunitamani," aliongea Yulia kimapozi huku akisimama kutoka alipokuwa amekaa na kumsogelea Hamza.

Pua zao zilikuwa zimeachana kwa sentimita chache sana, na Hamza alitumia muda huo kuangalia uso mlaini wa mrembo huyo. Kisha alishuka kwenye lipsi (midomo) pana zilizokuwa zimeiva na kuwa nyekundu, na alitamani kuinamisha kichwa chake na kuzin’gata.

Hata hivyo, Hamza alijua uchokozi na tabasamu la mwanamke huyo yalikuwa ni maigizo tu na hakuwa na hisia zozote kwamba alikuwa akimpenda. Kwenye ulimwengu wake, hisia pekee alizokuwa akizitambua ni hasira na furaha pekee.

"Sio mrembo sana kama mke wangu," aliongea Hamza huku akituliza presha ya damu kutokana na matamanio ya kiume yaliyokuwa yamemshika kwa sekunde kadhaa.

Yulia, mara baada ya kusikia kauli hiyo, palepale uso wake uligeuka na kuwa na ukauzu na ukali, akiwa tofauti kabisa na mwanzo alivyokuwa na alipiga hatua moja kurudi nyuma.

"Shida yako unachukiza sana, kama ungeweza kuendelea kuigiza nisingekuwa na shida kugusanisha lipsi (midomo) zangu na zako," aliongea.

"Kama ni hivyo, kwanini hujaongea mapema?" aliuliza Hamza huku akishika kichwa chake, akijutia kuikosa hiyo nafasi.

"Madam Yulia, una maagizo mengine kwangu? Kama huna, naelekea kupata chakula cha mchana," aliongea Hasina.

"Sina maagizo mengine, unaweza kwenda tu," aliongea, na Hasina alitingisha kichwa kisha akageuka na kuondoka.

"Mkurugenzi wa kitengo cha TIMISA lakini anaonekana kama kijakazi wako. Babe (mpenzi) Yulia, unaonekana wewe ni levo nyingine kabisa," aliongea Hamza, akimaanisha ilikuwa sio kawaida kwa mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha TIMISA kuonyesha unyenyekevu kama kijakazi mbele ya Yulia.

"Sio kijakazi wangu, ni kama bomu ambalo limetegeshwa na serikali kuniua ikitokea nimeisaliti nchi," aliongea.

"Kumbe umeona, ila anaonekana kukubali," aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kisha aligeukia Screen (skrini) iliyokuwa ikionyesha muundo wa manowari, umbo lake la nje na ramani yake ya ndani.

"Sijawahi kudhania utakuwa na uwezo wa kutengeneza kitu kama hiki."

"Tena sio kitu ambacho nilitaka kutengeneza kabisa, ni kutokana na jeshi kuomba nitengeneze. Zikikamilika kama unavyoona hapo kwenye ramani yake, kila moja inao uwezo wa kufyatua

bomu la kusafiri kutoka bara moja kwenda bara lingine."

"Kwa majeshi mengi duniani, kumiliki kitu kama hiki ni ndoto ya usiku," aliongea Hamza huku akichezesha ulimi wake kwa kutoa sauti.

"Kwangu mimi hii silaha naona haina maana kabisa na faida haina. Silaha ninayotamani kuunda ni yenye uwezo wa kuangamiza dunia huku nikiamua ni eneo gani lisiathirike," aliongea huku akiwa na tabasamu la kujivunia.

Alifurahishwa na muonekano wa Hamza wa kuchanganyikiwa ndani ya eneo hilo.

"Vipi, unatamani kuona ni kitu gani ninachofanyia utafiti?" aliuliza huku akiwa na tabasamu lililojaa kejeli.

Hamza asingekataa. Isitoshe, kuja kwake hapo ilikuwa ni kwa ajili ya kuona ni tafiti gani hiyo ambayo mwanamke huyu anaifanyia kazi mpaka kutolewa macho na watu wengi.

Isitoshe Himidu alimwambia kabisa tafiti hiyo inaweza kuwa na msaada mkubwa kwake, na Hamza aliamini ilimradi Himidu anayapenda maisha yake basi asingethubutu kumdanganya kabisa.

"Ndio, natamani sana kujua ni majaribio ya tafiti gani unayofanya. Pengine naweza pata uzoefu mpya," aliongea, na Yulia alitoa tabasamu la kejeli.

"Kama umekuja kutaka kujua ni tafiti gani ninayofanyia kazi, sikwambii."

"What the Fck!*" Hamza alishindwa kujizuia na palepale alimpiga Yulia kibao cha makalioni.

"Hata kama usiniambie maadamu nipo hapa

kisiwani nitajua tu. Sikulazimishi ila ukitaka kuniambia wewe sema."

"Nani kasema utajua? Unadhani ni rahisi hivyo?" aliongea Yulia akiwa na mwonekano wa kumchokoza Hamza.

"Nitahakikisha huoni utafiti wangu na wakati tukifanya majaribio utakaa nje," aliongea.

"Haha... nani wa kuweza kunizuia nikae nje? Wewe unadhani kwanini mmenileta huku, si kwasababu mnaona mimi ni zaidi ya walinzi wenu wote?"

"Ukileta fujo nitaongea na Hasina tu na kisha atafanya mawasiliano kwenda makao makuu ya TIMISA na mkeo Regina atakuwa kwenye matatizo. Kunigusa mimi ni sawa na kugusa taifa na kesi yake ni uhaini," aliongea kwa maringo kabisa na kumfanya Hamza kuvuta hewa nyingi ya ubaridi huku akisaga meno yake. Aliona kabisa mwanamke huyo alikuwa akimtishia makusudi. Lakini hata hivyo aliona kwamba haijalishi ana uwezo kiasi gani ila hana uwezo wa kushindana na nchi.

"Hehe... vipi bado unataka kuona tafiti yangu hata kwa kulazimisha?" aliuliza Yulia mara baada ya kuona Hamza kanywea, na kumfanya Yulia kushikwa na furaha ya ajabu.

Hamza aliishia kunyamaza huku akiangalia prototype ya manowari iliyokuwa ndani ya maji. Alijiambia kwamba Yulia sio tu kwamba alikuwa mwanasayansi, bali sio mwanasayansi wa kawaida, na kila kitu kilikuwa kikimwambia kuwa utafiti ambao anaufanyia kazi utakuwa sio wa kawaida pia. Kama ataondoka hapo kisiwani bila kuona utafiti huo, itakuwa hasara kubwa sana kwake.

"Madam Yulia, kama unakitu unataka kuongea na mimi, ongea. Isitoshe nimekuokoa zaidi ya mara mbili. Ikiwa kuna tatizo baina yetu, unaonaje tukikaa chini na kuongea kuyamaiza?"

"Kwahiyo unadhani kwa sababu uliniokoa nitakuwa na shukrani? I am sorry, sina mpango huo kabisa. Isitoshe si uliniokoa baada ya kuniona ni mrembo, na tamaa zako ndio zilikusukuma. Nyie wanaume ni viumbe ambao hamjawahi kufikiria na kichwa cha juu mbele ya mwanamke mrembo."

"Siwezi kukataa, navutiwa sana na umbo lako, sura yako. Lakini hata hivyo, mimi kitaaluma ukiachana na kusomea uchumi, vilevile mimi nimesomea udaktari. Hivyo, nimekuokoa kama daktari."

"Huna haja ya kujieleza mwanaume. Unachopaswa kufanya ni kuniahidi kitu kimoja, na nitakuruhusu kuangalia majaribio hayo kesho."

"Kitu gani?"

"Kuwa mpenzi wangu."

Aliongea bila ya kuuma maneno na kumfanya Hamza kuvuta pumzi ya baridi, na kisha alianza kucheka kwa kukosa ujasiri.

"Mbona spidi hivyo? Nawezaje kuwa mpenzi wako kwa kuniamrisha?"

"Sio kama unaenda kuwa mpenzi wangu halisi, unakwenda kuigiza kuwa mpenzi wangu. Nataka tucheze mchezo wa kuwa wapenzi."

"Mchezo wa kuwa wapenzi, ili kumuonyesha nani?"

"Kuna mwanaume ananisumbua sana, na imefikia hatua ananichukiza," aliongea Yulia akikosa kabisa subira ya kupata jibu kutoka kwa Hamza.

"Vipi, unakubaliana na sharti langu? Mbona unafikiria sana swala rahisi namna hiyo?" Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kukunja sura. "Kama sikosei, mtu ambaye anakufukuzia lazima sio mtu wa kawaida. Kwanini usinikubali ukawa demu wangu kabisa na sio kuigiza?" Aliongea Hamza.

"Ushaoa tayari, utakuwaje mpenzi wangu?"

"Basi nipatie sharti lingine? Unajua, mimi kuigiza kuwa mpenzi na mwanamke mrembo kama wewe kunanipa wakati mgumu sana."

"Kama hutaki, acha na kuwa tu bodigadi wangu," aliongea Yulia huku akigeuza kichwa chake na kuangalia pembeni.

Yulia aliishia kung'ata meno yake kwa hasira na aliona aliamini Hamza anakataa kwa kuogopa kugombana na vigogo wa nchi. Ndiyo maana hakutaka kulazimisha sana.

"Basi hakuna shida. Kwa jinsi ulivyo mrembo, nakubali kuigiza kuwa boyfriend wako," aliongea Hamza huku akijiambia atatumia nafasi hiyo kumchokoza na huenda akapewa tunda.

Yulia, mara baada ya kusikia kauli hiyo, aligeuka akiwa na tabasamu murua kabisa kama vile ni ua linaloanza kuchanua. Uzuri wake uliongezeka zaidi ya isivyokuwa kawaida.

"Babe, kwa sababu umekubali, unaonaje ukinisindikiza kwenda kupata chakula cha mchana kwanza?" aliongea kimadaha na kumshika Hamza mkono huku akimvutia kuelekea kwenye lifti.

"Yulia, naomba nikuambie kabisa, ni leo tu ndio naenda kuigiza na sio siku nyingine," aliongea Hamza akiwa siriasi, lakini licha ya usiriasi wake alishindwa kuzuia macho yake kukikodolea kifua cha Yulia.

"Usiwe na wasiwasi. Isitoshe nakujua ni mtu wa aina gani," aliongea Yulia huku akiwa na uso uliojaa dhihaka.

Wawili hao waliingia kwenye lifti ambayo iliwachukua moja kwa moja mpaka ghorofa ya ishirini. Mara baada ya kutoka, walikuwa katika mgahawa mkubwa ndani ya hoteli hiyo. Mapambo yalikuwa na umaridadi wa hali ya juu na kupendeza macho, na kuashiria ufahari mkubwa tofauti na chini kwenye vyumba vya ardhi.

Walitembea kuingia katika mgahawa huo uliokuwa angavu kutokana na mwanga wa jua uliobadilishwa na vioo kupendeza mandhari ya ndani, na kufanya mtu yoyote anayeingia hapo ndani mudi yake kuimarika haraka.

Kulikuwa na watu wengi tayari ndani ya eneo hilo, na juu ya meza zao zilikuwa zimechafuka kwa aina mbalimbali ya vyakula vya kutamanisha. Asilimia kubwa walionekana kama wasomi wa maswala ya sayansi. Hawakuwa wamevalia sare kama ilivyokuwa kwa wanausalama wengi bali walivalia kama vile walikuwa watalii. Hakukuwa na ngozi nyeupe hata moja, asilimia kubwa walikuwa weusi tupu na baadhi tu ndio walikuwa machotara kama ilivyokuwa kwa Hamza.

Mara baada ya kumuona Yulia akiingia hapo akiwa ameshikana mikono na Hamza, kila mtu aliishia kutoa ishara ya heshima kumsalimia Yulia huku kwa wakati mmoja wakiwa na maswali mengi juu ya Hamza ni nani.

“Bosi Yuli ..”

“Hello!.”

Kulikuwa na watu waliomuita Yulia kama Mkurugenzi, kuna wengine walimwita mwenyekiti na wengine pia walimwita Injiniia. Kila cheo alionekana kuwa nacho mwanamke huyo na kumfanya Hamza kuweza kuona heshima iliyojificha nyuma ya sura ya mrembo huyo. Aliona hakika Yulia hakuwa wa kawaida.

“Mbona unaninishangaa, unadhani naheshimika sana kwa watu sio? Mimi sio levo yako kabisa, nifuate na kunitii kama bosi wako,” aliongea Yulia kumchokoza Hamza.

Hamza, upande wake, hakubughuziwa na uchokozi wake. Badala yake, alimuuliza swali nje ya topiki.

“Uwanasayansi wako ndio uliosababisha ukataka kuuliwa nje ya nchi wewe na familia yako kupoteza maisha?”

“Ndio, tokea wakati ule nilivyorudi nchini sikuwahi kusafiri kutoka nje ya nchi, naboreka mno kutokana na kukosa uhuru,” aliongea Yulia.

Kaka yake na wazazi wake wote waliuliwa wakiwa ughaibuni wakiwa Vacation na sababu ya kupoteza kwao maisha ni kwa sababu yake.

Mara baada ya kuongozwa mpaka kwenye ukumbi binafsi wa kupatia chakula, walipokelewa na meza kubwa ya mahadhi ya kimagharibi.

Hamza kabla hata hajaingia alikuwa ashahisi watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo wote walikuwa ni watu na ziada. Baada ya kuingia kabisa hatimaye aliweza kumuona mwanaume aliyekuwa amevalia shati la Versace, alikuwa na nywele ndefu ambazo zimechanwa vizuri, alionekana pia kuwa mtanashati mno na alikuwa bize kula steki ya nyama.

Mwanaume yule mara baada ya kuhisi kuingia kwa Yulia katika eneo hilo aliinua na kuonyesha sura yake iliyojaa uhandsome na alimwangalia Yulia kwa sekunde kadhaa na kisha macho yake akayageuzia kwa Hamza na akatoa tabasamu lililojaa upole na uungwana.

“Yulia karibu sana, huyo mwanaume pembeni yako ndio nani?” aliuliza.

“Ni mpenzi wangu, anaitwa Hamza, ndio mtu aliyekoa uhai wangu nje ya nchi na kwa bahati nzuri tumekutana kwa mara nyingine hapa nchini na tumeanza mahusiano yetu,” aliongea Yulia akiwa na mwonekano wa uitikiaji.

Hamza aligundua mwanaume huyo alikuwa na nguvu za ziada kwenye mwili wake na sio hivyo tu, watu waliokuwa pembeni yake wote walikuwa na uwezo wa ziada na walionekana walikuwa wakimlinda. Kushoto kwake kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na kipara, hakuwa mrefu sana lakini alikuwa na mwonekano wa ujasiri na aliashiria ukali. Alikuwa siriasi hata wakati wa kula, ni kama vile alikuwa na kinyongo na chakula kwa staili yake ya ulaji.

Kulia kulikuwa na mwanamke ambaye ana mwili wa miraba minne, alikuwa na nywele fupi kiasi zilizopakwa dawa , hakuwa mrembo kabisa hususani kwa namna alivyoonekana kukomaa, tofauti na wenzake yeye hakuwa akila chakula badala yake alikuwa ameshika kioo kidogo mkononi na alikuwa akijiremba kwa mapozi ambayo yalimfanya Hamza aone ni kama vile anataka kupiga chafya.

Yule mwanaume ambaye alionekana kama ndio bosi ndani ya eneo hilo alisimama na kisha alimpa Hamza mkono na kumsalimia kwa kingereza.

“Nimefurahi kukutana na wewe, naitwa Herbert Kijazi, mtoto wa kwanza wa Mzee Kijazi na mchumba wa Yulia,” aliongea.

Hamza mara baada ya kusikia jina la Kijazi moyo wake ulidunda kwa haraka na kujiambia Yulia ni mshenzi sana kwa kutaka kumgombanisha na mtoto wa Mzee Kijazi.

Hamza licha ya kuishi kwa muda mfupi nchini Tanzania, kutokana na kuingia sana mitandaoni alikuwa akiifahamu familia ya Mzee Kijazi kuwa na mahusiano ya ukwe na Mheshimiwa Mgweno na familia ya M,zee Azim. Maana kwamba kutokana na kuwa na uhasama wa chini chini na familia ya Mgweno basi moja kwa moja pia familia ya Kijazi alikuwa na uhasama nao. Sasa kitendo cha kutambulishwa na Yulia kama mpenzi kilikuwa ni kama kuchochea moto.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi, nilichokuwa nikimaanisha Yulia ashawahi kuwa mchumba wangu, lakini baada ya kurudi nchini aliongea kuna mtu ametokea kumpenda na moja kwa moja uchumba wetu ulikoma,” aliongea kwa kujielezea mara baada ya kuona Hamza alikuwa amekumbwa na wasiwasi.

“Yupo sahihi Hamza, Hebert ni mpenzi wangu wa zamani na hakuna kinachoendelea kati yetu, naomba usije ukakasirika,” aliongea Yulia kwa kujibebisha akijitetea mbele ya Hamza.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alihisi kuna kitu hakipo sawa na hiyo yote ni kutokana na kwamba aliona hali ya Hebert kuwa na hisia za kimapenzi kwa Yulia lakini alijifanyisha kutokasirika wala kuwa na wivu.

“Bro karibu uketi, wewe hata usinijali kabisa, nipo hapa kama moja ya timu ya utafiti na sio kwa sababu ya Yulia,” aliongea kwa upole akimkaribisha Hamza kukaa.

Muda ule mara baada ya wote kuketi chini, Hasina alikuja akiwa ametangulizana na wahudumu wa hoteli ambao walikuwa wameshaandaa chakula tayari. Haikuwa na haja ya kuulizwa unakula nini kwani kulikuwa na kila aina ya chakula na wewe kuchagua unachotaka.

Licha ya chakula hivyo kupendezesha macho, upande wa Hamza ni kama hamu ilimpotea ghafla kutokana na kujihisi kuna kinachoendelea hapo.

“Babe mbona unaonekana kama huna hamu ya kula, usije kuhisi vibaya, Hebert ni mwanajeshi idara ya utafiti na uhandisi ndio maana yupo hapa,” aliongea Yulia.

Hamza alijiambia kuna haja gani ya kujitetea ilihali bwana huyo inaonekana ni dhahiri amejishikiza katika kitengo hicho ili kuwa na ukaribu nae, kwa uzoefu wake Hamza aliamini kadri mtu anavyoonyesha kutokujali maana yake anajali sana.

“Hehe.. Unaonaje tukienda kisheria sheria mpenzi, unatakiwa kunikiss kwanza ndio nile,” aliongea Hamza huku akijiambia kwa sababu mambo yamefikia hatua hiyo basi kama mbwai na iwe mbwai, ni mwendo wa kujifaidisha.

Mwonekano wa Yulia wala haukubadilika kwa ombi hilo, lakini macho yake namna yalivyokuwa yakicheza cheza ilionyesha dhahiri hakuwa amefurahishwa na Hamza kuongea hivyo.

“Yaani wewe sijui nakufanya nini...”

Yulia aliigiza na kisha aliinama kutaka kumkiss Hamza shavuni, lakini kabla hata lipsi zake hazijaligusa shavu lake, Hamza alipindisha mdomo wake kwa kugeuka na kisha alimshika Yulia kiuno na kumpiga busu la kwenye lipsi.

“Ugh...!!”

Yulia macho yake mazuri yalikodoka mara baada ya kuona mpango wa Hamza ni kutumia fursa vizuri. Licha ya kwamba hakupendezwa na shambulizi hilo, lakini vilevile asingeweza kujiondoa haraka kwa kuamini lazima Herbert angeona kinachoendelea. Hivyo alikosa jinsi na kuishia kutoa ushirikiano wa kupanua mdomo wake na kumruhusu Hamza kumwingizia ulimi.

Hamza alikuwa akifurahia mno kinachoendelea, alijiambia si amejileta mwenyewe basi hana budi kutumia fursa hiyo vizuri, alikuja kuacha baada ya mhudumu kuingia katika eneo hilo na kumpelekea Yulia kushikwa na haya za kike.

Hamza aliishia kufurahishwa na muonekano wa kuzubaa wa Yulia.

“Babe ni muda wa kula sasa, tutaendelea baadae tukiwa wenyewe,” Aliongea Hamza huku akimkonyeza.

Yulia aliishia kumwemewesa lipsi zake na kutingisha kichwa huku akilazimisha tabasamu. Hakujua kwanini, lakini kwa mara ya kwanza katika maisha yake moyo wake ni kama kuna mdudu alielala na anajaribu kuamka. Alihisi hisia ambazo hazikuwa za kawaida na mpaka hatua hiyo hakujua ni kitu gani kinamtokea.

Herbert aliishia kuangalia tukio hilo lote bila ya kuongea neno zaidi ya kuupamba uso wake na tabasamu.

“Bro Hamza kama sikosei utakuwa tayari na mke si ndio?” Aliuliza Herbert akiwa na tabasamu usoni. Hakujali kabisa kama alikuwa amemzidi Hamza kwa zaidi ya miaka kumi ila alimwita Hamza Bro.

“Upo sahihi, naona ushafanya utafiti wako kabisa na kujua kila kitu kuhusu mimi, kwanini unauliza ilihali majibu unayo?”

“Mkeo ni Regina Dosam, mmiliki na Afisa mtendaji mkuu wa makampuni ya Dosam, lakini pia mwanamke anaye sifika kwa kuwa na urembo wa ajabu. Kwa hiki unachofanya hawezi kupatwa na wivu?”

“Mke wangu ni muungwana sana na anaamini mimi kama mwanaume kuwa na wanawake angalau watatu sio tatizo,” Hamza alitunga pumba na kujibu bila ya kuwaza sana.

“Oh! Unaonekana kumjua sana mkeo?” Aliongea Herbert huku akiwa na mwonekano wa kushangaa.

“Hahaha…Braza naamini hautoenda kunisnitch kwa mke wangu kwa kinachoendelea hapa,” aliongea Hamza akionyesha hali ya kuwa na mashaka na Herbert.

“Haha... Bro wala usiwe na wasiwasi kabisa, mimi ni mwanaume na siwezi kufanya hivyo, nimeuliza tu kutokana na kuwa na shauku... Bro wewe kula maisha na warembo siri zako zipo salama.”

“Nimemjua Hamza kwa muda sasa na ni mtu alienisaidia na kutokana na hilo nipo tayari kumpa chochote. Hata kama Regina atafahamu kuhusu uhusiano wetu sidhani anaweza kufanya chochote,” Aliongea Yulia lakini upande wa Hamza alikuwa akiwaza tofauti.

Alijiambia ilikuwa bahati Regina hakuwa katika eneo hilo, vinginevyo angekasirika mpaka kutapika nyongo. Regina alikuwa akimchukia mno Yulia.

“Hehe... kwanza kabisa mke wangu ni mtu muungwana sana na kingine anajua nina

michepuko mingine tofauti na Yulia, kiufupi ni mwelewa mno.”

“Nakubali bro, isitoshe wewe ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana. Nasikia binamu yangu Farhani alifanya vitu vya ajabu na ukaishia kumuua... kama sehemu ya familia nakushukuru sana kwa kutuondolea yule kichaa,” Aliongea na kauli hiyo ilimfanya Hamza kuona kweli Herbert alikuwa na uvumilivu wa hali ya juu mpaka kwa kufikia hatua ya kumshukuru kwa kumuua ndugu yake.

Farhani alikuwa ni bwana aliemuua Mliman City mara baada ya kuanza kumtaka Eliza , alikuwa ni mjukuu katika familia ya Mzee Azim na mama yake Farhani ni shangazi kwa Hebert.

Wakati akiwa anawaza hivyo, palepale yule mwanaume aliekuwa siriasi sana na chakula alipiga kofi meza kwa hasira.

“Bosi hata kama binamu yako alikuwa na makosa bado anabakia kuwa ndugu yako, hajaishia tu kuvunja uchumba wako na bosi Yulia lakini pia ndio aliemuua bosi Farhani na Master Jagani mkuu wa Shirki ya Hansee,” Aliongea.

“Hey, Pima, unapaswa kukubali pale unapoteokea umekosea, hatuwezi kujiona tupo sahihi muda wote kwasababu ya ukubwa wa familia ya Azimu na uhusiano wa familia ya Kijazi na ya mstaafu Mgweno,” Aliongea Herbert.

Yulia macho yake yaliishia kusinyaa na alimwangalia Hamza na kisha akatabasamu.

“Jina lake anaitwa Pima ni mhitimu wa mafunzo ya kimapigano kutoka shirki ya Hansee India, yupo vizuri sana hivyo kuwa makini,” Yulia alimwambia Hamza.

“Pima na Farhani sio tu kwamba walikuwa ni mtu na bosi wake lakini pia walikuwa marafiki wakubwa sana, kutokana na kuhusika kwako na kifo cha rafiki yake ndio maana anaonekana kukuchukia, naomba ujaribu kumwelewa na umsamehe,” Herbert aliongea akimwambia Hamza.

Hamza aliishia kujiuliza na kujiambia kuna haja gani ya kumtetea ilihali ni msaidizi wake tu.

Hamza ni kama ambavyo alitegemea, kwani Pima hakuonekana kabisa kumchukulia bosi wake kwa umakini, na palepale alisimama na kumnyooshea Hamza kidole huku akiwa na uso uliojaa hasira.

“Hamza, kama kweli wewe ndiye uliemuua Master Jagani, basi utakuwa ni mtaalamu wa hali ya juu katika mapigano. Unaonaje tukipimana? Ukishinda nitaondoa kinyongo changu dhidi yako.”

“Pima, hebu acha ujinga. Braza Hamza yupo hapa kwa mwaliko maalumu kutoka kitengo cha Malibu. Yupo hapa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Kwanini unaanza kujilinganisha naye? Isitoshe, utulivu katika eneo hili ndio kitu muhimu zaidi.”

“Bosi, mimi kama Falsafa Pima bado siamini kama

Hamza ndiye aliemuua Master Jagani. Hata kama Mzee Azim hakutaka kulikuza hili suala, bado huoni hii ni dharau kwa familia ambayo imetoa mchango wa kusaidia taifa kupata wanajeshi wengi chini ya Hansii?”

“Pima…” Herbert alitaka kuongea lakini alikosa neno na aliishia kumwangalia Hamza.

“Bro, unaonaje kuhusu hili suala?”

“Sitaki kushindana naye. Kama ni suala la kumuua bosi wake, sijutii kufanya vile maana alinichokoza makusudi kwa kujigamba mbele ya mpenzi wangu. Kwanini nishindane naye kupigana ilhali sina kosa?”

“Tuone kama hutoshindana,” aliongea, na palepale mwili wake ulituna na kukusanya nguvu yake yote ya ndani huku akikunja vidole vyake katika staili ya kucha za mwewe. Kwa spidi ya hali ya juu bila kujali walikuwa hotelini, alimshambulia Hamza palepale kwa kulenga shingo yake.







SEHEMU YA 134.

Hamza, mara baada ya kushambuliwa vile, haraka sana alirudi nyuma na hata kiti alichokuwa amekalia kilipinduka. Mara baada ya kufanikiwa kumkwepa, alirusha mkono na kupangua shambulizi la Pima.

Pima, mara baada ya kuona shambulizi lake la kwanza limefeli, hakupoa. Palepale alifyatuka na sarakasi mtelezo na kufyatua kiti kwa ustadi wa hali ya juu kama mpira, kisha alikisukumiza kwa nguvu kumlenga Hamza kichwani. Hamza aliishia kukwepa kwa ustadi wa hali ya juu sana kiti kile, na kilienda kuvaana na ukuta na kupasuka pasuka.

Kwa haraka haraka, mashambulizi ya Pima yalimshangaza kiasi kutokana na uwezo wake na vilevile alivyokuwa na shabaha ya kushambulia. Lakini hata hivyo, ilikuwa ngumu sana kumshinda Hamza na mbinu yake hiyo ya mapigano.

Mara baada ya Pima kuleta shambulizi lingine, Hamza hakumsubiria sana kwani palepale alisogea kidogo pembeni na kisha aliweka mkono wake wa kulia katika staili ya karate na kupangua shambulizi lake kwa mara nyingine.

Pima hakutaka kumpa nafasi ya kupumua kwani aliendeleza kumpelekea Hamza mashambulizi, lakini yalipagunguliwa kwa ustadi mkubwa mno. Alijaribu mpaka kubadili mbinu ya kushambulia lakini hakuweza kabisa hata kugusa mwili wa Hamza kwani mashambulizi yake yaliishia juu juu.

Baada ya kuona anashindwa kabisa kumwingia Hamza, alijikuta akishikwa na hali ya wasiwasi na kumchunguza.

“Ni mbinu gani ya mafunzo unatumia, kwenye kuvuna nishati za mbingu na ardhi? Kwanini sihisi chochote kwenye mwili wako?” aliuliza.

Yeye mwenyewe alikuwa katika levo ya mzunguko kamili katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.

“Umekosea swali maana sijifunzi mbingu za nishati za mbingu na ardhi, ndiyo maana hujahisi chochote kutoka kwangu.”

Ukweli ni kwamba Pima, mwanzoni mara baada ya Hamza kuingia na Yulia katika eneo hilo, alimchukulia kuwa binadamu wa kawaida kutokana na kutokuwa na nishati zozote za mafunzo ya mbingu na ardhi kwenye mwili wake. Ndiyo maana alikuwa na ujasiri wa kupigana naye, lakini baada ya kuona ameshindwa kufua dafu mbele ya Hamza, wasiwasi ulimwingia.

“Haiwezekani, kama hujifunzi mafunzo ya mbingu na ardhi umewezaje kuzuia mashambulizi yangu ya nguvu ya mzunguko kamili?” Aliongea na pia hakutaka jibu kwani palepale alibadilisha mbinu na alianza kuchezesha vidole vyake angani kwa namna ya ajabu. Mbinu hiyo Hamza aliifahamu fika; ilikuwa ni kitendo cha kupoteza nguvu nyingi za mwili kwenda kwenye ardhi huku ukiruhusu nishati nyingi za mbingu kuuvaa mwili ili kuongeza wepesi. Mbinu hii ndiyo inayowezesha wavuna nishati kuweza kupaa kwa kubatilisha kani mvutano kwa kuupoteza uzito wa mwili kwa kuzidanganya kanuni za anga.

Alifanya mjongeo ule kwa sekunde chache tu na akaanza kuwa mwepesi mno, hali iliyomfanya Hamza kutoa macho. Dakika ileile, bila ya Pima kumgusa, Hamza alihisi kama vile amefungwa kamba kwenye kiuno na shingo na anavutwa na ile nguvu kumkaribia Pima. Kama isingekuwa na nguvu nyingi za kuhimili ile nguvu inayomvuta, angeweza kushambuliwa kirahisi sana na Pima.

Mara nyingi hali kama hii hutokea si kwamba umefungwa, bali mbinu hiyo inacheza na akili yako na kukufanya uhisi kuvutwa. Kwa hali halisi, mtu anajichawia mwenyewe na kujiweka karibu na adui, sawa na jinsi mtu anavyoshikwa na jinamizi. Kitendo cha kuendelea kuchezesha nguvu kwa kuonyesha mjongeo, Pima alipotea aliposimama kichawi na kuwa kivuli, huku akizidi kumfanya Hamza kujihisi anavutwa pande zote.

Hamza alikuwa akijua mbinu hizi vizuri. Ukweli ni kwamba, neno uchawi ni nguvu iliyo ndani yetu wenyewe na si kwamba wachawi wanatuloga; wanachofanya ni kukuadhibu na nguvu yako iliojificha katika mwili wako. Hivyo, Hamza kitu cha kwanza alikuwa ni kuushinda uchawi wake mwenyewe kwa kufumba macho na kutumia hisia na sauti za masikio.

Hebert hakuwa akijali kabisa kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea na aliendelea kukata vipande vya steki ya nyama huku akitafuna kwa kasi. Upande wa Yulia, baada ya Pima kutoweka kwa macho, alishikwa na wasiwasi. Hakushangaa kwa sababu mambo haya yalikuwa ni kawaida sana tangu elimu ya mafunzo ya nishati za mbingu kueleweka kwa watu wengi.

“Bertha, hebu acha kushangaa hapo na msaidie

Hamza,” aliongea Yulia. Sio kwamba alihisi labda Hamza amezidiwa, lakini kama mwenza alitaka kuonyesha kujali. Bodigadi wake Bertha, mwanadada mwenye sura ngumu, aliishia kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho la kushoto, sababu ya kufanya hivyo ilikuwa kupima ukubwa wa hatari. Katika mafunzo ya kimapigano, hasa kwa wale wanajeshi wanaosomea kudili na nguvu za ziada, endapo wakikutana na adui na wanashindwa kuona mjongeo wake na nguvu zake, tofauti na kutumia hisia, wanashauriwa kutumia jicho moja kuangalia hatari kwa msingi wa falsafa kwamba kuichunguza hatari kwa macho yote mawili ni kuukaribisha udanganyifu. To perceive danger with

both eyes is to invite illusion; true clarity arises when one employs a singular focus and embodied awareness to dispel the shadows.

“Bosi, Yulia, nipo hapa kwa ajili ya kukupatia ulinzi. Mpenzi wako hana tatizo mbona?” aliongea Bertha mara baada ya kufumbua jicho moja, huku akiendelea kujirembesha sura yake kupitia kioo.

Muda uleule, hatimaye Hamza alifanya shambulizi kwa kusogea kwa kasi kubwa, na ghafla mkono wake ulionekana ukiwa umemshika Pima, ambaye alionekana kama ameinuka kichawi. Ilikuwa kama vile Hamza alikuwa akivua na kumtoa Pima kutoka majini kwa ndoano. Hamza hakutaka kutumia nguvu kubwa sana kwa sababu angeweza kumuua, hivyo alipiga ngumi kidogo tu kumwadabisha.

Baada ya Hamza kuzimisha mazingaombwe ya Pima, Herbert alianza kupiga makofi huku akiwa amesimama na kucheka.

“Hamza, sijakosea kabisa kukuita bro; uwezo wako si wa nchi hii,” aliongea, lakini Hamza wala hakujali sifa zake. Badala yake, aliangalia shati lake ambalo lilichanika katika harakati ya kuzima mazingaombwe ya Pima.

Hamza, mara baada ya kumtaitisha Pima, aliachana naye kisha alichukua kiti kingine na kukaa mezani na kuendelea kula.

“Nadhani nishashida, ole wako usinisumbue tena,” aliongea.

Muonekano wa Pima haukuwa sawa kabisa; alikuwa na hali ya hofu na kujikuta akiwa katika hali ya kuzubaa. Ukweli ni kwamba aliona kabisa Hamza hakutumia nguvu kubwa kumdhibiti, na kama angemtumia nguvu kubwa, angekufa. Kuwa mpiganaji ulieiva maana yake ni kuweza kumsoma adui yako kwa haraka na kujua kama una uwezo wa kushindana naye. Alijua fika Hamza alivuta muda si kwa sababu hakujua namna ya kushambulia bali alikuwa akijifunza mjongeo yake.

Ilikuwa sahihi kabisa. Hamza alijua fika kwamba mpiganaji mzuri ni yule anayejua kushambulia bila ya kumwonyesha adui mbinu zake. Kitendo cha Pima kupotea kilikuwa ni sehemu ya kuonyesha kuwa anaficha mbinu zake, na Hamza hakuhitaji macho kuona alichokifanya, bali alitumia hisia zake.

“Bosi, nisamehe kwa kukudhalilisha,” aliongea Pima.

“Hebu acha kuongea ujinga. Licha ya kwamba unaniita bosi, sisi ni marafiki, hivyo haina haja ya kuona aibu kwa kushindwa na Hamza. Shida yako tu ni kwamba unakurupuka sana,” aliongea Herbert.

“Asante sana, bosi, kwa kunionyeshea uvumilivu,” alijibu Pima.

“Hamza, majaribio yatafanyika kesho. Leo siku nzima hakuna cha maana tunachofanya. Kwa uzuri wa hiki kisiwa, unaonaje tukijumuika pamoja kula bata?” aliongea Hebert mara baada ya chakula cha mchana.

“Shati langu limechanika, napanga kwenda kwenye chumba changu kwanza kubadili,” aliongea Hamza akiwa hana hamu ya kula bata anazoongelea Hebert.

“Usiwe na wasi wasi. Naagiza mtu sasa hivi akuletee shati lingine kabisa,” aliongea Hebert na mara moja alimpa ishara muhudumu na aliondoka akiwa ameelewa maagizo.

“Hebert, unaonekana kuwa na shauku ya kutaka kumfahamu kiundani mpenzi wangu?” aliuliza Yulia, akimwangalia Hebert.

“Yulia, sio kama ulivyosema. Unaweza kuwa na muda wa kuwa pamoja na mpenzi wako, lakini leo ndio kwanza nimekutana nae. Nataka tuongee mawili matatu kufahamiana kidogo,” aliongea Hebert akiwa na tabasamu.

Yulia hakutaka kuendelea kukaa karibu na Hebert kwa sababu alijua akiendelea kuigiza na Hamza kama wapenzi, bwana huyo hashindwi kuchukulia hiyo kama fursa ya kumchezea. Mpango wake ulikuwa kumgombanisha Hamza na Hebert tu na sio vinginevyo. Hata hivyo, kwa sababu Hebert ndiye aliyeshawishi, asingekataa moja kwa moja ikiwa hana cha kufanya, aliona ngoja alipe gharama ya kumgombanisha Hamza na Hebert.

“Babe, naona hakuna tatizo kwa alivyopendekeza.

Twende tukacheze cheze, tuchangamke,” aliongea Hamza huku akiminyaminya paja la Yulia makusudi kabisa.

Hamza alijua kabisa hakuwa na haja ya kuigiza kuwa mpenzi wa Yulia tokea mwanzo. Aliona kabisa nia ya Yulia kupendekeza kuigiza ni kumtengenezea uadui na Hebert tu ili achukue maamuzi ya kijinga na mwisho wa siku pengine amuue Hebert na kujiingiza kwenye mgogoro na familia yake.

“Kama unataka, twende kucheza. Nipo tayari tukacheze,” aliongea Yulia akiwa na tabasamu usoni lakini moyoni alikuwa akitamani Hamza limkute jambo.

Baada ya kundi hilo kukubaliana, waliingia kwenye lift iliyowashusha mpaka nje kabisa na walianza kutembea katika bustani zilizokuwa kando ya fukwe.

Hebert mara baada ya kuona motorboat mbele yake, macho yalichanua.

“Bro, unaonaje tukishindana kuendesha motorboat?” aliuliza lakini Hamza alimkatalia. Alikuwa amezoea sana kutumia boti hizo za pikipiki wakati alivyokuwa nje ya nchi, na mara nyingi kipindi hicho akiwa anaendesha boti hizo, lazima nyuma yake awe na mrembo alievalia bikini. Sasa kutokana na eneo hilo kukosa warembo waliovaa bikini, hakuwa na hamu kabisa ya kucheza kwenye maji na boti hizo.

“Bro, ushashuka mpaka huku tayari. Sidhani kama ni vizuri kutofanya chochote. Pima licha ya kuwa na uwezo mdogo kwenye mapigano, ameshiriki mara nyingi katika mbio za boti. Unaonaje ukimpa nafasi ya kushindana tena?” aliongea Hebert, na kauli hiyo ilimfanya Pima kushangaa kwa sababu hakutarajia kama bosi wake angemtaka kushindana na Hamza kuendesha boti.

“Unadhani ninaweza kufanya kila kitu kwa sababu tu umeongea?” aliuliza Hamza.

“Bro, sijasema unashindana bure. Kama ukishinda, sitakuwa tena na kinyongo na Yulia kwa kuvunja uchumba wetu na nitawatakia maisha mema.”

“Uwe na kinyongo ama usiwe nacho, huwezi kubadilisha chochote. Yulia ni mpenzi wangu tayari,” aliongea Hamza na kisha alimgeukia Yulia.

“Si ndiyo babe?”

“Nimezaliwa kuwa mpenzi wako,” licha ya Yulia kusema hivyo, mwonekano wa Hebert haukubadilika.

“Inaweza isiwe kweli lakini, ijapokuwa nyie ni wapenzi, sidhani kama familia ya Yulia wakisikia kuhusu mahusiano yenu watakubali kirahisi.Watapinga kwa nguvu zao zote. Kunikataa

mimi na kisha kuwa na mahusiano na mwanaume aliyeoa siyo tu tusi kwa familia ya Yulia, bali pia ni tusi kwa familia yetu,” aliongea Hebert.

“Kwahiyo unaniogopesha au inakuwaje?” aliuliza Hamza kwa hasira.

“Haha… Bro, huko sio kukuogopesha. Naomba usinifikirie vibaya. Nilikuwa najaribu kuonyesha mtazamo wangu juu ya mahusiano yenu basi,” alijitetea Hebert.

“Kama kuna mtu anataka kupinga mahusiano yangu na Yulia, ajaribu aone,” aliongea Hamza akiwa na hali ya kuwa siriasi.

“Bro, sijasema hivyo kwa nia ya kukutishia,” alijitetea Hebert.

Hamza alikuwa mvivu wa kuongea zaidi na kumkomoa Hebert. Alimsogelea Yulia na kumkumbatia kwa nyuma, akiogelea umbo lake. Lakini dakika hiyo hiyo walianza kusikia sauti za mtu akipaza sauti akitokea baharini akiomba msaada.

Alikuwa mwanamke alievalia koti la maabara, akiwa amefungwa kwenye boti na mwanaume alievalia mavazi meusi na walikuwa wakielekea baharini.

“Si Dokta Sarah yule!!” aliongea Hebert kwa kuhamaki.

Yulia licha ya kutomtambua Dokta Sarah vyema, lakini mavazi ya mtu ambaye alikuwa amemfunga Dokta Sarah aliyatambua vyema.

“Hamza, yale mavazi ni wale Ninja waliotaka kuniua!” aliongea Yulia kwa kuhamaki.

“Inaonekana wanataka kupata taarifa ya tafiti zetu ndiyo maana wamemteka. Imekuaje wakaweza kujipenyeza hapa kisiwani?” aliuliza Yulia.

“Pima, acha kuzubaa na fanya jambo kumuokoa Dokta Sarah kabla hajapotelea baharini,” aliamrisha Hebert.

Pima mara baada ya kupokea maagizo hayo, haraka sana alikimbilia boti na kuanza kuwafukuzia. Lakini sasa dakika ambayo yule ninja aligundua alikuwa akifukuziwa kwa nyuma, mita kama mia mbili kutoka ufukweni, alichomoa kisu na kumchoma Dokta Sarah ambaye alidondokea majini huku damu nyingi zikimtoka.

Hamza ambaye alikuwa ufukweni mara baada ya kuona tukio hilo, haraka sana alivamia boti akitaka kuingia majini.

“Unafanya nini?” aliuliza Yulia.

“Naenda kumuokoa,” alijibu Hamza wakati huo akiangalia mwili wa Dokta ukiwa anaelea juu ya maji na kusukumwa na mawimbi. Aliona kama asipookolewa mapema nafasi ya kupona itakuwa ndogo sana.

“Kuna haja gani ya kwenda kumuokoa ilihali tayari amekwisha kufa?” aliuliza Yulia akionyesha kutojali kabisa na kumshangaa Hamza kuona kwamba anataka kujisumbua kwenda kumuokoa mtu ambaye hana uhusiano wowote naye.

Kutokana na ugonjwa wake, Yulia aliamini mtu anayepaswa kusaidiwa katika hali kama hiyo ni yule pekee anayemfahamu vizuri.

alivyokuwa akikaribia, alihisi kuna kitu hakipo sawa. Ilikuwa ni kama akili yake ilianza kufanya kazi. Kwa ulinzi mkali wa kisiwa hicho, wanajeshi walipaswa kumfukuzia yule Ninja. Lakini tofauti na Pima, wote walikuwa wamesimama tu bila kufanya chochote.

Muda huo, Hebert aliyekuwa amesimama kwenye fukwe alitoa tabasamu na palepale alitoa simu yake ya kisasa. Kwa kutumia kalamu ya simu ile, alionekana kama vile alikuwa akichora kitu.

“Yulia, kwanini huwezi kunielewa siku zote? Kitu nisichoweza kupata mimi, hakuna mwingine anayeweza kukipata,” aliongea Hebert huku akicheka.

“Hebert, unataka kufanya nini?” aliuliza Yulia huku akihisi baridi usiokuwa wa kawaida.

Hebert alikuwa na tabasamu lililojaa uungwana, lakini nyuma yake alikuwa mkatili mno, alieogopwa na kila mtu. Baada ya kumwangalia Yulia kwa tabasamu, aliinua simu hiyo juu na kama vile anabadilisha chaneli, aligusa kitufe kilichokuwa kwenye simu hiyo:

BOOM!!!
JUMAMOSI INAENDELEA-WATSAPP 0687151346
Daaah
Singano asante sana
 
Unavyomshukuru leo last ametuma last week ujue anajua ametuma ndefu sana na itatosha na week hii, ebu fanya maarifa yako ya la dada shunie sta boy atupie ma jambo leo aseee
Daaah
Singano asante sana
 
Hizi Hadithi za kupima bwana taabu kweli kweli,mwanza kuna bahari Au ziwa.
 
Mkuu hata mwakani Sawa tu kikubwa goma liendelee, wewe pia binadamu Una mambo yako mengi tu ya kufanya sio tu kuleta story hapa. Unapopata muda tupia mwendelezo ukikosa muda fanya yako
 
Mkuu hata mwakani Sawa tu kikubwa goma liendelee, wewe pia binadamu Una mambo yako mengi tu ya kufanya sio tu kuleta story hapa. Unapopata muda tupia mwendelezo ukikosa muda fanya yako
eeh waaah!!! ila asiwe anapotea sana..maana simulizi zake n zaid ya darasa..kuna vitu tunajifunza kupitia yeye, ndio maana tunamind pale anapotusahau...
 
eeh waaah!!! ila asiwe anapotea sana..maana simulizi zake n zaid ya darasa..kuna vitu tunajifunza kupitia yeye, ndio maana tunamind pale anapotusahau...
MNASHINDWAJE KUMSUPORT KWA KUSUBSCRIBE GRUP LAKE KWA KUMCHANGIA ILE 3000NA AKUKUPA EPSD ZOTE MPAKA NAE ANATAKIWA AKIKAA KUUMIZA KICHWA RESEARCH UJUE ANAHITAJI MUDA.no no wonder africa tunakua maskin sana
 
MNASHINDWAJE KUMSUPORT KWA KUSUBSCRIBE GRUP LAKE KWA KUMCHANGIA ILE 3000NA AKUKUPA EPSD ZOTE MPAKA NAE ANATAKIWA AKIKAA KUUMIZA KICHWA RESEARCH UJUE ANAHITAJI MUDA.no no wonder africa tunakua maskin sana
it's due to the lack of money..ndio maana tunasubilia huruma yake2..tungekuwanazo tungemfuata hukohuko kwenye magroup yake..
 
it's due to the lack of money..ndio maana tunasubilia huruma yake2..tungekuwanazo tungemfuata hukohuko kwenye magroup yake..
ila kwenye viti virefu aaa na kuwapiga watoto ofa . kumsuport mwana 3000 anaumiza kichwa. ku andika fiction based on realities. au unafikiri hao kina athena ni uongo? wapo kweli kwenye ukimwengu wa history athena, ares sijui hermes ingawa napinga kwamba wao ni miungu ila majina hayo yapo huko kwneye greek. anyway nilichotaka kusema support ni muhim
 
MNASHINDWAJE KUMSUPORT KWA KUSUBSCRIBE GRUP LAKE KWA KUMCHANGIA ILE 3000NA AKUKUPA EPSD ZOTE MPAKA NAE ANATAKIWA AKIKAA KUUMIZA KICHWA RESEARCH UJUE ANAHITAJI MUDA.no no wonder africa tunakua maskin sana
Kuna vitu viko nje ya uwezo wetu mkuu ndo maana tunasubiria hapa hapa
 
Back
Top Bottom