Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

Kaka hiki kisa ungekiuza kitengenezewe movie ingekua bonge Moja la dudeee an 🙌
Daaah mkuu umewaza mbali sana....

Hizo hesabu huwa zipo sema nasoma upepo kwa sababu kama ni movie labda upate outsiders ndo wawekeze kwa sababu budget zake nina uhakika bongo hakuna mwenye uwezo wa kuweka pesa .......

Ni ndefu kimtindo kwa sababu ina hadi season 2 yake ambayo ilisha kamilika tayari....

Shukrani kwa maoni yako 🤝
 
Tunapokuja tujitahidi kutag na wengine Uzi uende chap ili tuanze na sehemu inayo fuata ✅

Tuna mengi sana ya kuyafurahia kwenye maisha ya hicho kiumbe cha kuitwa GAVIN LUCA......

Bado haujaona maajabu ya huyo binadamu hatari....

Kuna mambo ya kutisha na ya kufurahisha na ya hatari yanakuja huko mbele mpaka utaanza kumuogopa huyo bwana GAVIN LUCA
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
SONGA NAYO................

Kwahiyo ili kuzuia hilo wewe na familia yako mnatakiwa kufa lakini kama unavyo vijua vyombo vyetu vya habari, taarifa itakuwa ni kwamba muuaji wa mke wa raisi aamua kujiua yeye na familia yake kwa ujumla ili kukwepa adhabu ambayo ingemkuta mbele yake. Yaani jina lako litabakia kuwa moja kati ya wanajeshi wa hovyo zaidi kuwahi kuwepo Tanzania Sarah na kwa bahati mbaya sana hakuna mtu ambaye atajali kuhusu hilo
Kwa sababu watu wote wataamini kwamba ni kweli, hii kesi ya mke wa raisi itaishia hapo na maisha mengine yataendelea. Bila shaka umeelewa ni kwa namna gani maisha yanaenda kasi, unakufa huku ukibebeshwa dhambi za watu wengine” mwanaume huyo aliongea kwa kutamba huku akiwa anacheka kwenye mkono wake akiwa anakizungusha kisu.

“Why umekuwa hivi Nickson?”
“Mimi nafanya haya yote ili niishi, kuna wakati inabidi uwapunguze baadhi ya watu ili uwe na nafasi ya kutosha ya kuweza kuishi kwa amani”
“Una uhakika hili litakupa amani?”
“Hakuna anaye jua hilo na sitaki kujua hilo, ni wakati wa wewe kushuhudia vifo vya wapendwa wako” alinyanyuka na kumsogelea mama yake Sarah, aliishika shingo yake mithili ya mtu ambaye amelishika jogoo la pasaka, alitaka kumuua kikatili mbele ya mwanae.
“Tafadhali usifanye hivyo, naomba yachukue maisha yangu uwaache waende, hawahusiki kwa lolote hao na hawajui lolote” alikuwa analia Sarah mpaka udenda unamtoka mdomoni, hakuwa tayari kushuhudia mauji ya mama yake hadharani namna hiyo, aliona kama ulikuwa ni ukatili ambao ulikuwa umevuka mipaka. Hakuwa hata na nguvu za kunyanyuka, alikuwa anajivuta sakafuni huku akiwa analia, nani alimjali Sarah? Maskini binti wa watu.

Nick alikipitisha kisu shingoni, wakati anahitaji kukivuta ili kumuua kwa kumchinja huyo mama, ghafla umeme ulikatika. Alishtuka kwani ilikuwa ni ghafla na hakutegemea kukutana na jambo kama hilo, alikuwa ana uhakika kwamba hilo eneo hakuna mtu mwingine ambaye alikuwa anaishi na wakati kama huo hakuna mtu ambaye alipaswa kuwepo kwenye nyumba hiyo. Alimuachia mama huyo na kwenda kuchungulia dirishani, nje kulikuwa kimya mno ila alihisi kama kuna kivuli kimepita nje kwa kasi, hapo alikumbuka kwamba kuna kosa walilifanya, lipi? Mlango bado ulikuwa wazi, alisonya na kurudi mlangoni kwa kasi akiwa anaitoa bastola yake.

Nick alikimbilia mlangoni haraka wenzake wakiwa gizani hawaelewi kinacho endelea, walikuwa wanaulizana tu lakini mpaka wakati huo hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anatoa majibu kamili juu ya kilichokuwa kinaendelea. Lengo lake la kuwahi kwenye huo mlango alitaka kwanza aufunge ndipo aanze kufanya utafiti kwamba ni nani alifika ndani ya eneo hilo wakati kama huo.
Alikishika kitasa cha ule mlango wa mninga na kuhitaji kuubamiza ila wakati anaanza kuusukuma kwa nguvu, aliuachia na kuguna kwa sauti kubwa akiwa anarudi nyuma. Alihisi kapigwa na kitu kizito kwenye paji lake la uso kiasi kwamba alipitia maumivu makali mno isivyo kawaida. Aliona kivuli kinapenya ndani hivyo alishambulia kwa risasi kwenda kwenye huo mlango ila risasi ziliishia kwenye mlango, wakati anaangaza kila kona kwenye kiza kinene alipokea buti la shingo hata bastola hakuweza kuishika tena ilidondokea mbali.
Umeme ulirudi ghafla mno na ilionekana kwamba hawakujiandaa kuweza kuupokea hivyo walifumba macho, walipokuja kuyafumbua Nick hakuamini kile alichokuwa anakiona. Wale wenzake wote walikuwa wamekufa kwa kuchinjwa vibaya na kitu chenye ncha kali huku mwanaume aliyekuwa ameingia humo ndani akiwa mbele yake amesimama na nguo nyeusi mwili mzima. Licha ya kujifunika sana mwilini ila bado kwa nyuma, rasta zilizo tunzwa vizuri zilikuwa zimetaradadi.
Hata Sarah hakuwa anaamini kile ambacho alikuwa anakiona mbele yake, ni msaada ambao hakuutarajia wala hakujua ni nani ambaye alikuja kumpatia huo msaada wenyewe. Kwake alishukuru Mungu kumletea malaika wa kuisaidia familia yake kwa wakati huo japo hakuwa na uhakika kama mtu huyo alikuja kumsaidia yeye au alikuwa na dhumuni lake lingine, jambo pekee ambalo kidogo lilimpa imani ni kuona mama yake na mdogo wake hawajafa kwa hiyo dakika, aliamini mengine yangejileta yenyewe huko mbeleni.

Mwanaume huyo hakuwa akiongea neno lolote, kwenye mkono wake alikuwa na chuma kidogo ambacho kwa mbele kilikuwa kimetanduliwa na kutengenezwa kama misumari, ndicho alikitumia kuitandaza miili ya wanaume waliokuwa humo ndani kwa muda mfupi uliokuwa umepita. Nick alinyanyuka kwa sarakasi ya hewani na kujigeuza akatua akiwa ameupanga mkono wake ambao ulikuwa na kisu, alitembea kwa zigzaga kumfuata yule mwanaume, aliuachia mguu wake huku mkono wenye kisu akiurushia upande wa ubavu wa kulia wa yule mwanaume.
Ule mguu mwanaume yule hakuukwepa, aliukutanisha na mkono wake ambao ulikuwa na kile kifaa, kilizama kwenye mguu wa Nick ambapo alikivuta kifaa kile kikaitandua sehemu kubwa ya mguu wake. Nick ile hali ilimfanya asiwe na nguvu ya kuufikisha ule mkono wenye kisu kwenye ule ubavu. Alirudi nyuma kidogo bwana yule akamtisha, alirudi nyuma kwa uoga na hofu lakini mwenzake alikuwa na hesabu za ziada, baada ya kuhakikisha mtu huyo amerudi nyuma alimjia kwa kasi kubwa ambapo alimtishwa ngumi nyingi na kumshindilia na kisu tumboni kisha akakitoa kwa nguvu. Aligeuka na buti ambalo lilitua kwenye mbavu ya Nick, alipiga makelele, alikutana na kiganja cha kichwa.

Aliyumba yumba akachotwa kwa nguvu na kubaki anaelea hewani, mwanaume yule aligeuka na mateke yote mawili akayatua kwenye kifua cha Nick ambapo wakati mateke hayo yanatua hapo, alisikika akihema kwa nguvu huku akitapika damu nyingi. Yale mateke yalimbeba mbali mpaka nje baada ya kuvunja dirisha la kioo ambalo lilikuwa ukutani, wakati anakaribia kulifikia dirisha alisindikizwa na kile kifaa ambacho kilitua kwenye kifua na kuzama ndani. Kilisikika kilio nje ya dirisha hilo na mwanaume huyo alipo sogelea hilo eneo aligundua kwamba bwana yule alikuwa anakimbia kuelekea kwenye fensi akiwa kwenye hali mbaya, alipanda na kudondokea nje, hakuwa na muda wa kuanza kumfukuzia kwa sababu sicho ambacho kilimpeleka hilo eneo.

Alikitoa kitambaa usoni na kugeuka, Sarah kama angekua na uwezo angekimbia ila hakuwa na huo uwezo na hata kama angekuwa nao basi huenda asingefanya hivyo kwa sababu ya familia yake. Ila kitu alicho kiona kilimtisha na kumfanya aogope sana, alikuwa anamuona mwanaume ambaye siku kadhaa nyuma alipata taarifa kwamba alihusika kwenye mauaji ya waziri wa mambo ya ndani tena mchana wa jua kali maeneo ya Kariakoo. Hakuwa mwingine, alikuwa ni mtaalamu Othman Chunga.
“Nakuomba usije ukaiua familia yangu tafadhali” alijua kabisa huyo bwana ni muuaji na hakuwa na huo ubavu wa kumzuia, kitu pekee alicho ona kinafaa ni kuweza kuomba lakini bwana huyo alimsogelea pale alipo na kumpatia kidonge kimoja ili akimeze aweze kupata nguvu.
“Sijaja hapa kukuua, nimeagizwa nije nikuchukue kwa sababu tulitegemea hili lingetokea baada ya wewe kujiingiza kwenye lile tukio la mauaji ya mke wa raisi”
“Mlijua kwamba itatokea kivipi?”
“Nasikitika kukwambia kwamba mimi huwa sio mtu ambaye napenda kuulizwa maswali ila huwa napenda zaidi kuuliza maswali”
“Nani amekutuma hapa uje kunipa msaada wakati hatujuani?”
“Bibie nimekwambia kwamba mimi sipendi kuulizwa maswali hususani na wageni. Muda sio mrefu watakuja watu wengi hapa ambao watanichelewesha na naweza shindwa kuwapa msaada. Kwa sasa unaenda kuwa miongoni mwa watu ambao wanatafutwa zaidi ndani ya taifa hili kwa kuhusika na mauaji ya mke wa raisi kwahiyo inatakiwa tuondoke haraka na familia yako kabla mambo hayajaharibika” Sarah alitamani kuendelea kuuliza maswali mengi lakini alijua kabisa kwamba bwana huyo hakutaka hilo jambo. Baada ya kumeza kidonge kile alipata nguvu hivyo wakaichukua familia yake ili kuondoka na bwana huyo ambaye hata hakuijua japo nukta ya maisha yake na hakuwa na imani kama alikuwa hapo kwa ajili ya msaada wa moja kwa moja au alikuwa na malengo yake mengine lakini hakuwa na namna kwa wakati huo zaidi ya kumumini kwani bila yeye mpaka wakati huo yeye na familia yake yote wangekuwa wamekufa tayari.


Sehemu ya 53 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
Back
Top Bottom