HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 48
“Ulikuwa sahihi kusema kwamba wamekushtukia na muda wowote huenda wamekuweka kwenye mtego na wanaweza kukukamata kuanzia sasa kwa sababu tayari wameshakuwa na uhakika kwamba wewe sio mwenzao tena”
“Kwahiyo natakiwa kufanya nini?”
“Makamu wa raisi umempata?”
“Ndiyo”
“Vijana wanakupeleka uwanja wa ndege saivi ambapo utakutana na familia yako maana kuna vijana wengine pia nimewatuma wakaichukue familia yako, ukifika pale kuna ndege binafsi ambayo itakusafirisha wewe na familia yako mpaka Kenya. Huko utakaa mpaka nitakapo kupigia simu ya kukutaka urudi kwani siwezi kuruhusu ukaingia kwenye matatizo kwa sababu baada ya hili nataka nikufanye uwe raisi”
“Mheshimiwa una uhakika na hili? Naona kama inaweza kuwa hatari zaidi”
“Fanya kama navyo kuelekeza kwani kila kitu kipo ndai ya mipango yangu”
“Sawa mheshimiwa” waziri mkuu alihema kwa nguvu baada ya kuikata simu hiyo, mpango ulikuwa ni kwamba yeye alitakiwa kuishi na sio kufa kwa sababu alikuwa anahitajika sana kwa hapo baadae. Aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ilianzia pale.
Asubuhi na mapema sana mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Tanzania, mheshimiwa Philipo Tibaigana alipigiwa simu yake na raisi kwamba afike ofisini kwake kwani alikuwa na maagizo yake ya mhimu sana. Taarifa hiyo ilikuwa ni ghafla sana na ilimshtua kwa kiasi kikubwa sana kiongozi huyo wa usalama hivyo baada ya simu hiyo kukatwa alimpigia Denis Kijazo kumpa taarifa hiyo ili aone kama kulikuwa na umuhimu wa kwenda au asiende.
“Mheshimiwa nahisi kabisa huko sio salama kwenda”
“Kwahiyo unataka kujionyesha hadharani kwamba rasmi unamgeuka raisi? Yule anasikilizwa na kila mtu anaweza kuandaa mkutano wa vyombo vya habari akatangaza kwamba umeiasi nchi unahisi sisi tutakua kwenye hali gani?”
“Kwahiyo nifanye nini mheshimiwa?”
“Nenda kamsikilize”
“Mheshimiwa”
“Fanya nilivyokwambia halafu huyu binti amekuja kwangu muda sio mrefu sana”
“Brandina?”
“Ndiyo”
“Kwa sababu gani?”
“Gavana ameuawa”
“How?”
“Wameshajua kila kitu na sisi tumejua kila kitu hivyo kilicho baki na kutafuta nafasi ya kumuua raisi tu”
“Brandina yupo salama?”
“Hapana”
“Kwanini?”
“Nina uhakika huu utakuwa ni mtego kumtuma yeye kuleta mwili kwangu, nadhani walitaka kujua kama yupo kwao au yupo kwangu”
“Watajuaje?”
“Kama binti akirudi akiwa mzima watajua ni mmoja wetu”
“Usiniambie kwamba umepanga kumuua?”
“Hapana, hilo lipo juu yako wewe, nimemuacha aende”
“
Where We Dare To Talk Openly
“Nenda kamsikilize huyo changudoa kisha ukitoka nambie kilicho endelea, mpango wote unafanyika leo usiku”
“Una uhakika gani?”
“Huwa naishi mbele ya mu dasana”
“Unamaanisha nini?”
“Yule bwana mdogo Bilali ambaye alikuwa anajifanya anaishi kwa kificho sana leo usiku anakufa na wenzake hivyo raisi anabaki na kijana mmoja tu Max ambaye baada ya kifo cha raisi anapewa kesi ya kifo kisha na yeye anakufa”
“Utawapata vipi watu ambao hata hawajulikani walipo?”
“Kuna kifaa amewekewa kwenye mwili wake wakati anasalimiana na waziri mkuu, nijua sehemu yoyote ile atakayokuwa na wenzake”
“Naomba hili liishe haraka sana mheshimiwa kabla mambo hayajaharibika sana”
“Go” mheshimiwa aliikata simu hiyo baada a kuhakikisha kwamba amemaliza maagizo yake kwa mkurugenzi huyo. philipo Tibaigana alikuwa na hofu sana kitu ambacho kilifanya apige simu kwa pupa sana kwa Brandina na simu hiyo ilipokelewa baada ya muda mfupi tu.
“B upo salama?”
“Sijui”
“Upo wapi kwa sasa?”
“Nawaza kama nirudi Ikulu au niende wapi maana watu hao wameshanijua”
“Sasa nisikilize kwa makini, nenda safe house kule kisha usiku majira ya saa sita nitakuja kukutoa nikusafirishe kwenda nje ya nchi. Hiyo simu itupe saivi kwa sababu huenda sio salama na usimwamini mtu yeyote kwamba upo wapi hata hiyo gari iache hapo hapo ulipo na uondoke haraka sana”
“Sawa naomba usiniache kwenye hili bosi”
“Nipo kwa ajili yako siku zote. Fanya nilivyo kuelekeza utakuwa salama mpenzi, siwezi kuruhusu kukupoteza nikalikosa lile penzi ambalo sijawahi kulipata kwingine kolote” Brandina alikata simu akiwa anacheka kicheko cha hofu lakini chenye imani ndani yake baada ya mtu ambaye alikuwa anamtegemea kuonekana kwamba hakuwa tayari kumsaliti hata wakati wa shida bado angekuwa naye sambamba na jambo hilo wangelimaliza pamoja.
Lakini simu hiyo ilikuwa inasikilizwa upande wa pili, Bilali na Max walikuwa Ikulu kwenye chumba cha mawasiliano wakiwa wanasikiliza watu hao ambao moja kwa moja walikuwa ni wapenzi.
“Pole sana ndugu yangu” Bilali aliongea akiwa anakunywa kahawa kidogo
“Pole ya nini?”
“Najua kila kitu kuhusu wewe na huyo binti. Mimi nikitaka kufanya kazi na mtu huwa namfuatilia hadi namna anavyo ishi, nadhani haukutegemea mwanamke ambaye ulikuwa umeanza kumpenda sana anaweza kuwa msaliti na alikuja kwako kwa kazi ambayo mpaka sasa amefanikiwa kwa asilimia tisini”
“Nimefanya kosa kubwa sana ambalo limetuingiza wote mpaka sasa kwenye matatizo mazito sana”
“Unatakiwa kukosea ili ujifunze kwenye haya maisha bila hivyo ni ngumu sana kufanya mambo sahihi. Kitu cha mhimu ni kuhakikisha kwamba hautarudia tena kosa la namna hiyo kwenye maisha yako na usiku wa leo huo muda wewe ndiye unatakiwa ukakutane na huyo binti na hakikisha sura yako ndiyo inakuwa sura yake ya mwisho kuiona kwenye maisha yake. Twende naona mtu wetu amefika kwenye kamera hapo” hakumtuhumu vibaya bali alimpatia ushauri na siku nyingine namna ya kuchukua tahadhari hususani kwenye matukio ya hatari kama hayo kisha akamtaka waende sasa kukutana na mkurugenzi.
Philipo Tibaigana alikuwa anaingia Ikulu akiwa ndani ya suti kali sana, moyoni mwake alikuwa na hofu kubwa sana isivyokuwa kawaida. Alitembea taratibu mpaka kwa katibu wa raisi ambaye alikuwa ofisi ya nje, alikaa hapo akiwa na mawazo sana kiasi kwamba alisahau hata kusalimia mpaka alipokuja kushtuliwa kwamba raisi alikuwa akimsubiri ndani, aliiweka tai yake vizuri na kuhema kisha akaingia ndani ya ofisi kubwa na mhimu zaidi nchini.
“Karibu sana mheshimiwa Tibaigana”
“Asante mheshimiwa, ni heshima kubwa sana kuitwa na wewe hapa”’
“Unajisikiaje kuwa kwenye nafasi kubwa kama hiyo?”
“Najisikia fahari kubwa sana kuwa moja ya sehemu ya watu ambao wanahakikisha taifa hili linakuwa salama”
“Una uhakika taifa lipo salama kweli?”
“Nahisi hivyo mheshimiwa”
“Lakini kumbuka kwamba kuna matatizo mengi sana yanatokea, kuna mauaji yanatokea kila siku na wananchi wanahitaji majibu ila kwa bahati mbaya haujawahi kuniletea ripoti hata moja hapa”
“Mheshimi……”
“Hata usijali, haya nitawajibu wananchi mwenyewe kwa sababu walinichagua mimi na sio wewe hivyo naona hili halikuhusu”
“Bado sijakuelewa mheshimiwa”
“Usijali utanielewa tu muda sio mrefu, hapo mezani kuna laptop ambayo nadhani umeiona, hilo ni shirika lako ambalo nahitaji taarifa zake uziweke wazi kwa kutoa hizo codes za kufungulia kwenye mafaili ya siri ambayo mimi siyajui na nywila wewe ndo unazo’’
“Hili ni jambo la hatari sana”
“Ni hatari kwa raisi kulijua kuliko watu ambao hawahusiki kulijua?”
“Sijamaanisha hivyo”
“Unahisi labda nakuomba?”
“Hapana mheshimiwa”
“Basi fanya hivyo” hakuwa na namna zaidi ya kufungua akaunti za siri za shirika hilo na raisi alikuwa makini sana kumwangalia kwa kila ambacho alikuwa anakifanya.
“Siku nyingine hautakiwi kuwa mbishi sana bwana hasa unapo ongea na mtu ambaye amekufanya umeendelea kuwepo kwenye hiyo nafasi”
“Mheshimiwa kuna jambo lingine labda?”
“Ndiyo, ndiyo lipo hata usiwe na haraka, nadhani unamfahamu vizuri sana Denis Kijazo”
48 inafika mwisho.