FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #121
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 51
“Mlijua kwamba nitakuja hapa?”
“Yeah”
“Kivipi?”
“Tulikuwa tunabeti tu kama ikitokea mtu huyo akahojiwa basi akuelekeza wewe hivyo ili uje tukukamatie huku na huko ulikotoka watu wako wanauawa bila wewe kuwepo kisha unapewa kesi na kutangazwa kama gaidi na baada ya hapo utakuwa hauna kazi tena tunakuua”
“Hahahah hahahaha” Max alicheka kwa hasira sana kwa sababu alikuwa amechezewa mchezo wa kitoto sana.
“Unamaanisha Brandina hayupo huku?”
“Huyo yupo lakini kwa bahati mbaya hauwezi kumpata” mwanaume huyo aliongea huku akiwa anaichomoa bastola na kulenga tenki la mafuta la gari ambapo gari la Max lililipuka hivyo ikawa hakuna njia ya kumfanya yeye kurudi haraka ndani ya Dar es salaam.
“Ulitakiwa kuniua ukiwa na nafasi bado, umefanya kosa kubwa sana kuniacha hai wakati ambao ulikuwa unanishambulia”
“Hata mimi nilitamani sana kukuua ni kwa sababu tu siruhusiwi kukuua ndiyo maana mpaka sasa upo hai” wakati mwanaume huyo anamalizia kuongea Max alinyanyua buti lake na kuanza kuja kwa kasi kali mno. Alijirusha chini ya mchanga na wakati ananyanyuka hapo kasi ambayo alisimama nayo akiwa ameirusha michanga juu ilikuwa ngumu sana kwa mwanaume yule kuweza kuihimili hivyo akajikuta anapiga hewa na mwanaume alizunguka nyuma yake na kuliachia shoka lake kwa nguvu huku akiwa ameshikilia kwenye mpini.
Shoka hilo lilitua kwenye mgongo wa huyo mwanaume na kuupasua vibaya mno, alivutwa kisha shoka hilo likawekwa shingoni, alichinjwa mithili ya kuku wa pasaka. Aliachiwa chini akiwa mfu kama wa miaka mia nane iliyokwisha kupita. Max akiwa amesimama hapo alishangaa kuona geti likiwa linafunguliwa kama alama ya kumkaribisha aingie ndani, alishangaa sana na kuangalia pembezoni mwa geti hilo ndipo aligundua kwamba kulikuwa na kamera kila mahali kumaanisha kwamba watu ambao walikuwa ndani ya jengo hilo na pengine ambao walikuwa wapo nje ya jengo hilo walikuwa wanaangalia kile ambacho kilikuwa kinaendelea moja kwa moja.
Aliingia akiwa makini sana kuweza kuangalia mazingira ya ndani jinsi yalivyokuwa, ndani ya jengo hilo alikutana na sura ngumu saba za wanaume ambao walionekana kwamba walikuwa wanamsubiri kwa hamu kubwa sana. Akiwa anawahesabu kwa umakini wanaume hao alisikia sauti ya mtu akiwa anapiga makofi juu ya ghorofa, kwenye balcony alikuwa amesimama Brandina akiwa amevaa bikini huku nyuma yake akiwa amefunikwa na gauni ambayo mbele ilikuwa wazi na kuvifanya viungo vyake vilivyo nona sana kuonekana kwa usahihi.
“Wewe ni moja kati ya wanaume wajinga sana, you were too smart sikufikiria kama unaweza kuingia kwenye mtego wa kitoto ule kisa uchi wa mwanamke. Uchi umekufanya umewasaliti wenzako kwa kuiweka wazi mipango ambayo inaenda kuwateketeza wote kwa pamoja”
“Umeniangusha sana, kwenye nyumba yako ulikuwa unajifanya kwamba ulikuwa makini sana hasa kwenye kufanya maongezi yako lakini ulishindwa kutambua kwamba nilikuwa nimeweka vifaa vya mawasiliano kila sehemu hivyo kila ambacho ulikuwa unakiongea na kila ambacho kilikuwa kinaendelea mle nilikuwa nasikia lakini sio mimi tu na watu wengine wengi walikuwa wanasikia kirahisi sana ndiyo maana iliturahisishia kuweza kuzisoma alama zenu ambazo zilikuwa zinafuata” “Mpaka unafika hapa najua Philipo huenda umemuua kwa hasira na sijali kuhusu yeye hata kama ndiye mwanaume ambaye amenifikisha hapa ila huwa najali maslahi yangu binafsi tu. Kuna muda sikulaumu sana kwa sababu niliwahi kufundwa kabisa kuhusu kitanda ndio maana mwanaume yeyote ambaye anauona uchi wangu na kunipanda kamwe hawezi kuniacha ila kwa wewe, you were too smart for that sijajua kama ni ushamba wako wa mapenzi ambayo hata hauyajui ndo umekufanya ukawa zuzu kiasi hiki? Hebu fikiria kama taifa lilikuwa limekutuma kufanya kazi nyeti nje ya nchi si ndo ungekuwa umesha liingiza taifa hasara wewe? Na ukumbuke kwamba huko nje ya nchi kuna wanawake warembo na wanawake watamu sana hata zaidi yangu, hahahahah hahahaha”
“Kosa ambalo umelifanya ni kukurupuka kuja huku bila kupiga hesabu kwamba ukishakuja huku ni kipi ambacho kinabaki kinatokea huko ulikotoka, unajua kinacho endelea? Ulipaswa kwanza kujiuliza kwamba Karistus yuko wapi ambaye wewe umemzoea kwa jina la Dax. Hapo unaona kosa la kwanza ambalo umelifanya kukurupuka? Dax alikuwa pale pale Ikulu kwenye ofisi ya katibu akiwa amejificha kwa sababu yule katibu pia ni kijana wetu, maskini raisi wa watu changundoa yule hana msaada wowote kwa sasa”
“Umekuja hapa ukiwa umemuacha raisi wako anakufa bila msaada wala kutoa wosia wake wa mwisho kwako na kwa wenzako pia, hii ni mbaya sana kwa upande wako lazima. Lakini pia hao vijana wa DRAGON BOYS ambao bila shaka ulihisi watakuwa msaada mkubwa sana kwako, kule kwa Madilu wametengenezewa mtego wanaenda ni kufa tu na hakuna hata mmoja ambaye anaweza kutoka akiwa hai”
“Inanisikitisha sana, wewe upo kwenye wakati mgumu sana namna hii, wewe unakamatwa saivi kusubiria muda wako wa kuuawa ufike, raisi wako muda wowote kuanzia sasa anakufa lakini hata wale vijana watatu ambao unawategemea kwa sasa nao wanaweza kufa kuanzia wakati huu. Unahisi utafanya nini maskini?” Brandina alikuwa anampa somo Max namna walivyokuwa wameicheza michezo yao huku akiwa anamskitikia kinafiki sana mwanaume huyo ambaye alikuwa anamsikiliza mwanamke huyo kwa umakini sana wakati huo.
“Unataka kujua baada ya haya kutokea kitafuata nini? Unataka kujua kipi kitafuata baada ya raisi kufa, baada ya wenzako watatu kufa na wewe kuwa hai? Kiukweli ni kwamba nilikuwa nataka nikuue huku huku ni basi tu unatakiwa kufika kule ukiwa mzima wa afya. Sababu ya wewe kuwa hai ni kwamba raisi akifa utakamatwa ukiwa haujadhurika kabisa ili kuwe na ushahidi kwa watu kuhusu wewe kumuua raisi na picha nyingi sana zitapigwa ukiwa karibu na mwili wa raisi lakini baada ya hapo wewe utauawa na taarifa zitachapishwa kwamba umeuawa ukiwa unataka kuwashambulia makomando ambao walikuwa eneo la tukio kukudhibiti Max. unataka kujua tena nini kitafuata baada ya wewe kufa?”
“Huenda hii ndiyo sehemu mbaya zaidi ambayo hautaipenda kwa sababu naenda kuwa waziri mkuu wa nchi hii kwa kazi kubwa ambayo nimeifanya lakini waziri mkuu atarudishwa nchini kisha wananchi watatungiwa uongo mwingine wa kupewa, unataka kusikia huu uongo utakuwaje Max?”
“Magazeti yataandikwa kwa ukubwa kwamba Gaidi namba moja aliye muua raisi auawa eneo la tukio na kuwapongeza mshujaa ambao wamelifanikisha hilo. Kisha Denis Kijazo atasimama kwenye vyombo vya habari na kukanusha habari ile mbaya ambayo raisi aliisema kwamba yeye ndiye mbaya wa nchi ni kwa sababu tu raisi huyo alikuwa na mipango miovu sana juu ya taifa hili na Denis Kijazo alisimama ili kupingana naye ndipo akaanza kumchafua na kumtishia kifo huku wewe ukionekana kama mtu ambaye ndiye ulikuwa unatumwa na raisi Teodensia Mpanzi kufanya shughuli zake haramu na baada ya kufanya kazi zake nyingi alitaka kukuua ili kulinda siri zake ila kwa bahati mbaya sana ukamuwahi na kumuua”
“Nadhani hii itakuwa habari mbaya sana pale ambapo kila mtu atajua kamba wewe na raisi pamoja na kundi lako mlikuwa magaidi. Kuhusu wananchi wao huwa wamwamini kiongozi muongo zaidi na anayewapa uongo ambao unawafurahisha kisha wataahidiwa kushushiwa kodi kidogo na kupatiwa malipo kwa usumbufu wa vitisho ambavyo walivipata na vinguo kidogo na watasahau kila kitu ambacho kilitokea na wakati huo unajua wewe na wenzako mtakuwa wapi?”
“Mtakuwa mmekufa, watu ambao mlijitoa kulipigania taifa hili kwa hali na jasho, historia itawaandika kama magaidi na watu wataishi wakiwa wanawachukia sana wakiamini nyie ndio watu ambao kwa kiasi kikubwa mlichangia kuimomonyoa amani ya taifa hili. Waziri mkuu atatangazwa kuwa raisi rasmi wa Tanzania na nchi itarudi kwa Denis Kijazo and we don’t give a https://jamii.app/JFUserGuide Max kwamba who is the owner kikubwa sisi tunaangalia maslahi yetu tu basi mengine hayatuhusu.”
“Nadhani kwa sasa umetambua kwamba ni nani mwenye karata ya ushindi. Unahisi utaweza kujisaidia na kuwasaidia wengine ambao umewaacha huko Dar es salaam? Upo nje ya muda, labda jaribu bahari yako kwani ninajua kwamba wewe ni mtu hatari sana ila pia unatakiwa kutambua kwamba najua uhatari wako ndiyo maana nimekuandalia hawa wanaume ambao ni zaidi yako. Mimi naenda kusikiliza muziki ndani, good luck DONNY” Alipewa shule haswa mwanaume na kila ambacho aliambiwa kilikuwa kinamuingia moja kwa moja kwenye moyo wake mpaka alijihisi kwamba alizingua sana, B aliiangalia saa yake na kutabasamu kisha akaingia ndani na kuwaachia wanaume uwanja waweze kufanya yale ambayo yalikuwa yanawahusu.
Mwanaume mmoja alimrushia pingu na kumtaka ajifunge mwenyewe bila kuumizwa ili wawahi kutoweka ndani ya hilo eneo, mwanaume aliona kama hiyo ilikuwa ni dharau kubwa sana ukizingatia alikuwa kwenye hasira kubwa sana. Alimsogelea mwanaume huyo ambaye alimrushia hiyo pingu akiwa ameiokota na kuishika mkononi, mwanaume huyo naye alimsogelea pale alipokuwepo akiwa anazikunja ngumi zake maana hakuwa akiruhusiwa kuweza kutumia silaha ambayo ingeweza kuyatoa maisha ya Max.
Kusogea kwake alikutana na pingu ambayo ilirushwa kwa nguvu sana ikiwa inakuja upande wake, alijaribu kuinama ili asipate madhara lakini alishindwa kutokana na ukaribu sana ambao walikuwepo hivyo ilimpasua kwenye pua yake hali ambayo ilimfanya afumbe macho yake na wakati anafumbua alikuwa amechelewa sana. Shoka lilipitishwa kwenye uso wake na kuuchana chana uso wake vibaya mno hali ambayo iliwafanya wenzake kuja kwa kasi sana maana waliona kumchukulia kimzaha mwanaume huyo ingewaletea madhara makubwa sana isivyo kawaida.
Walikuwa wanakuja kwa kujizungusha maana walikuwa wengi, Max alijaribu kurudi nyuma kwa nguvu ili kuweza kupishana nao wote lakini asingeweza kuzikwepa ngumi kumi na mbili kwa pamoja. Alipigwa mabuti na ngumi kali sana japo hata yeye alifanikiwa kuwapiga wanaume wawili, kipigo kizito ambacho kilitua kwenye mwili wake kilimbeba kwa umbali kidogo na kumfanya ajivute huku akilichomweka shoka chini ambalo lilimpa balansi ya kutulia vizuri. Alisimama kwa nguvu kupitia shoka lake kisha akadunda kwenye mpini ambapo aliruka sarakasi na kulirudia shoka lake ambalo lilikuwa chini na wakati anafanikiwa kunyanyuka aliachia shoka hilo kuelekea kwa wale wanaume huku yeye mwenyewe akiwa anakuja kwa kasi mno.
Shoka lilitua kwa mwanaume mmoja kwenye kiuno chake, hali ambayo ilimfanya kupiga kelele kwa nguvu sana maana alipata maumivu makali lakini wakati huo huo mwanaume alikuwa amefika akiwa anachomoa visu viwili kwenye kiuno chake. Alijirusha kwa sarakasi ya hatua ndefu ambapo alipishana nao wakiwa wanamfuata maana yeye aliruka kwa juu na kutua karibu na mwanaume ambaye alikuwa mwishoni.
Alimdaka mwanaume huyo kwenye kola ya shati yake na kumguzia kwake, hakuwa na hadhithi za kumsimulia zaidi ya kuzamisha visu vyake kwenye shingo na kuichana chana huku akiwa anamsukumia mwanaume huyo pembeni maana hakufaa kabisa kuwepo ulingoni tena. Wanaume hao walianza kuingiwa na wasiwasi sana maana walikuwa saba lakini mpaka wakati huo wanne tu ndio walikuwa wamesimama mbele yake akiwa anawaangalia kwa hasira sana. Aliangalia saa yake mkononi, muda haukuwa rafiki kabisa kwake kwani aliambiwa kwamba alitakiwa kuwahi Dar es salaam kwa ajili ya kuwaokoa wenzake akiwemo mheshimiwa raisi ambaye alikuwa kwenye hatari kubwa sana.
Alivizungusha visu vyake akiwa anawasogelea ambapo walikuwa wamesimama, alidunda kwa buti moja kwa sarakasi ya mbele kisha akajivuta nyuma, wanaume wawili walidanganyika na ile sarakasi hivyo wakawa wamemfuata kwa pupa pale ambapo alikuwepo lakini kujivuta kwake kuliwafanya wakutane na hewa tupu huku yeye wakiwa wamemkosa. Baada ya kumkosa aliwasogelea mwenyewe ambapo mmoja alimpiga na kiganja eneo la sikio lake akaacha kabisa kusikia na mwingine alizamisha kisu kwenye moyo wake na kukishindilia kwa ngumi nzito sana kisha kwa kasi akamgeukia yule ambaye alikuwa bado anazunguka kwa maumivu ambayo aliyapokea kwenye sikio lake.
51 inafika mwisho.