Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 57
Kasi ambayo alienda nayo kwake ilikuwa ni nzuri sana lakini kwa mwanaume ambaye alikuwa mbele yake haikuwa nzuri sana hivyo aliishia kukoswa na upanga wa shingo na kupigwa na kisigizo kwenye uso wake. Alirudi nyuma kwa kuyumba yumba na kugundua kwamba kama akicheza vibaya alikuwa anakufa maana watu hao hawakuwa na huruma wala hawakuwa wakiuliza mara mbili kwenye kufanya hayo maamuzi yao ya kutisha sana. Alihema kwa nguvu na kuweza kuutuliza mwili wake kisha akazikunja ngumi ambapo alihesabu mpaka tatu na kusogea taratibu ila kadri alivyokuwa anamsogelea mwanaume huyo mbele yake ndivyo alivyokuwa anazidi kutengeneza ukamakini kwenye ule upanga maana ndipo hatari kubwa ilipokuwepo.
Wakati anafika alijishika kiunoni na kuchomoa bisu kubwa huku akiwa anainama kuukwepa upanga ambao ulikuwa unaitenganisha shingo yake kama ungefanikiwa kumpata na baada ya hapo alilipitisha bisu hilo kwenye tumbo la mwanaume huyo ambalo lililipasua tumbo vibaya sana lakini naye aligeuka vibaya akiwa na uhakika kwamba amemaliza kazi yake kitu ambacho kilimfanya akutane na upanga wa bega ambao ulizamishwa hapo baada ya mwanaume huyo kugeuka na kurusha upanga wake kwa nguvu ili angalau waweze kufa wote.
Alishikwa na hasira sana baada ya upanga kumpatia maumivu hayo makali kwenye bega lake huku mwanaume mwenzake utumbo ukiwa unaonekana maana alichanwa vibaya sana kwenye hilo tumbo lake. Mwanaume aliuchomoa upanga huo kwenye makali kwa kutumia mkono wake mmoja na kisha mkono ambao ulikuwa umebaki aliutumia kuzamisha bisu lake kwenye jicho la mwanaume huyo ambapo alishindilia na ngumi kali mpaka kisu kikatokezea nyuma kisha akakichomoa na kumkita mwanaume huyo na buti zito la kifua ambalo lilimbamiza vibaya sana ukutani huku yeye akiuparamia ukuta na kuishia nje kazi alikuwa ameimaliza huku akiwa na maumivu makali sana kwenye bega lake.
Ted na Kenedy baada ya kumaliza kazi yao kwa wakati mmoja walizunguka mpaka upande wa nyuma na kugundua kwamba hata kijana wao huyo alikuwa amekufa.
“Huyu mmoja amepona, anaweza kuwa tatizo kwa hapo baadae” Kenedy alitamka akiwa anamkagua kijana wao huyo ambaye alikuwa hapo chini.
“Hapana, yule hawezi kuwa hatari, kama amepata nafasi ya kukimbia namna hii basi usitegemee kwamba atarudi ni lazima kuna kitu alikuwa anakiwahi ila nina uhakika hataweza kurudi tena hasa akijua kwamba mtu ambaye alikuwa anamuona kama kiongozi wake alikuwa amekufa”
“Kwahiyo hatuna haja ya kumtafuta kiongozi?”
“Tutamtafuta taratibu usijali ila hana madhara yoyote huyu hivyo kwa bosi tunamwambia kazi imeisha huku tutakuwa tunatafuta uwepo wake sehemu yoyote ile taratibu”
“Sawa mkuu” Ted aliinyanyua simu yake na kuipiga kwa mheshimiwa Denis Kijazo.
“Nipe taarifa nzuri Ted”
“Bosi kazi imeisha, sasa ni muda wako wa kuishi kwa amani kama zamani’
“I’m so proud of you Ted. Hahaha that’s my boy” kiongozi huyo mstaafu aliongea akiwa anacheka kwa furaha sana maana kwake hilo jambo lilikuwa ni hatua kubwa sana kufanikiwa kuwamaliza watesi wake wote hivyo nchi ilikuwa imerudi tena kwenye mkono wake kama alivyokuwa anahitaji mwenyewe toka mwanzo.

Hayo mambo yote ambayo yalikuwa yanatokea, Max alikuwa anayaangalia moja kwa moja kwenye skrini kubwa ambayo ilikuwa mbele yake. Hao ndio watu pekee ambao alikuwa anawatazamia kama tarajio la mwisho baada ya raisi kufa na kugundua kwamba hakuna hata mmoja ambaye alikuwa upande wao. Video ilikomea pale ambapo Bilali aliuawa, mwanaume alichoka sana lakini hakupewa muda wa kutosha zaidi wa kuweza kupumzika.
Muda mchache sana tangu matukio hayo yaweze kufanyika mwanaume aliwekewa taarifa ya habari ambayo alitakiwa kuona ni kipi hasa kilikuwa kinaenda kufanyika. Habari mbaya zaidi ni kwamba mtu ambaye alikuwa anaenda kuongea alikuwa ni Denis Kijazo kwa sababu aliwahakikishia waandishi wa habari ambao walikuwa nyumbani kwake kwamba alikuwa na habari ngumu sana siku hiyo hivyo walitakiwa kusikiliza kwa umakini kwani lilikuwa ni anguko kubwa ndani ya taifa la Tanzania.
Hakuna mtu ambaye alikuwa anafanya kazi muda huo, kila mtu alikuwa anataka kujua kwamba taifa lilikuwa limekumbwa na mdudu gani hasa na ni changamoto gani ambayo ilikuwa imewafikisha huko. Mheshimiwa Denis Kijazo alisimama mbele ya maiki akiwa na huzuni sana, aliwasalimia watanzania kwa jina la nchi ya Tanzania na kukohoa kidogo ili kuweza kujiweka sawa na kuitoa habari hiyo ambayo alidai kwamba lilikuwa ni anguko kubwa sana kwa nchi ya Tanzania.
“Nasikitika sana kutangaza kifo cha mheshimiwa raisi wa nchi yetu, Teodensia Mpanzi” alitulia kwanza kuongea akiweka kituo na kuziangalia kamera kwa utulivu mkubwa ambao ndani yake ulikuwa na mengi sana ya kuweza kuyatoa kisha akaendelea tena.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha mheshimiwa raisi lakini jambo la kusikitisha zaidi ni juu ya mtu ambaye amemuua. Ameuawa na mlinzi wake wa karibu sana ambaye yeye mwenyewe alidai kwamba alikuwa akimuamini sana. Sasa swali la msingi ni kwamba kwanini kamuua? Huenda ni ngumu sana ila hakuna namna wananchi lazima mjue namna nchi yetu ilivyo uhalisia wake na namna mambo yanavyokuwa yanaendeshwa huku juu”
“Siku kadhaa nilipokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania kwamba kuna mienendo ya raisi ni mibaya sana kwa taifa na huenda itakuja kuleta madhara makubwa sana. Mimi kwa sababu nilikuwa nina imani na kiongozi wetu nikamshauri mkurugenzi kwamba ajitahidi sana kuhakikisha kwamba kila kitu kinaenda vizuri ili wananchi na rasilimali za taifa ziwe salama wakati wote jambo ambalo alilifanyia kazi na kuamua kufuatilia zaidi usalama wa raia kuliko kumjali sana raisi na mambo ya nyuma ya pazia ambayo alikuwa anayafanya”
“Lakini baadae tena akanitafuta na kuniambia mheshimiwa fanya kitu nchi inaenda kwenye machafuko makubwa sana nadhani ndio ule wakati ambao watu walianza kufa hovyo hovyo. Kitu ambacho alikifanya raisi wetu ni kuamua kujimilikisha nchi kwenye mikono yake na kuifanya kama yake kiasi kwamba akanijibu mimi kwamba yeye ndiye mtu mkubwa zaidi nchini hivyo anaweza kufanya jambo lolote lile ambalo linampendeza lakini mimi sikukubaliana naye kabisa kwa kile ambacho alikuwa anakifanya kwa kumpa ushauri namna ya kuiongoza nchi kwa sababu hata mimi nimewahi kuwa hapo pia lakini alicho kifanya ni kunipiga marufuku ya kufika Ikulu kabisa mpaka aamue yeye”
“Nimekuja kugundua kwa kuchelewa sana kwamba alikuwa na ajenda zake za siri kuanza kuua kila mtu ambaye aliamua kumkatalia kuihujumu nchi na ndipo alihisi kwamba kuna watu walikuwa kwenye ule ukumbi ambao ulilipuliwa na nyuma ya jambo hilo alikuwepo yeye mwenyewe. Nilijaribu kukaa naye chini kumhoji shida nini akasema yeye ndiye mtu mkubwa zaidi kwenye taifa hivyo anafanya yale ambayo yanampendeza na nisicheze kwenye njia zake ataniua nikaamua kukaa kimya kwa kumheshimu lakini kilicho fuatia baada ya hapo limekuwa ni janga kubwa sana. Alikuwa ameanza kuua kila mtu ambaye aligoma kuungana naye kulifilisi taifa. Gavana mkuu wa benki kuu amemuua, makamu wa raisi amemuua, waziri mkuu alikuwa antaka kumuua bahati nzuri akawa amewahi kwenda Kenya na familia yake. Amemuua mpaka daktari mkuu wa mhimbili kwa sababu alikuwa na siri zake nyingi maana kuna wakati watu hawa wanadaiwa waliwahi kuwa wapenzi wa siri”
“Baada ya kuhakikisha kwamba ameyakamilisha hayo yote alikuwa anataka kumalizia hatua za mwisho ili siri yake ibakie kuwa yake tu na ndipo alipanga kumuua mlinzi wake, sasa kwanini afanye hivyo? Kwa sababu huyo mlinzi ndiye ambaye ametumika kuua watu wote hao ambao Teodensia Mpanzi aliyachukua maisha yao hivyo huyo ndiye ambaye alikuwa na siri zote juu ya kila jambo ambalo amelifanya na alikuwa anaogopa kwamba siku moja anaweza akaja kuujua ukweli hivyo akaona ni bora amuue tena alitaka kumuulia kwenye ofisi yake”
“Alimuita kwa mtego wa kufanya naye mapenzi kwa video na picha za marejeo kama zilivyo onyesha wakati watu wa ulinzi wakiwa wanazipitia na wakafanikiwa kweli kufanya mapenzi ndani ya ofisi kuu ya nchi jambo ambali ni aibu kubwa sana imetufika sisi kama watanzania halafu akahitaji kumtandika risasi mwanaume huyo wakati akiwa amevaa na kutaka kuondoka lakini hakujua kama mtu huyo alikuwa amejihami kwenye mwili wake akiwa na kisu na ni kwa sababu alikuwa ameukataza ulinzi mzima juu ya kumkagua huyo mtu wake ambaye alikuwa anamtumia kwenye kazi zake. Mwanaume huyo hakuzubaa baada ya kuona raisi anataka kumpiga risasi kwa sababu ni mtu mwenye mafunzo ya hali ya juu sana ameutumia uwezo wake kuweza kumchoma choma raisi visu vingi sana kwenye mwili wake ambapo inadaiwa kwamba amemalizia kwenye moyo kama picha za marejeo zinavyo onyesha”
“Wakati raisi akiwa kwenye hali mbaya kwa mahesabu ya wataalamu ni kwamba alifanikiwa kuigusa alamu ambayo ipo chini ya kiti chake ambayo iliwafikia walinzi wa nje na mmoja na mlinzi wake mwingine ambaye walipata mafunzo pamoja na huyu gaidi muuaji wa watu. Kijana huyu anaitwa Karistus Dickson, kwa sababu milango ile ina ulinzi mkubwa sana walitumia muda mrefu kidogo kuuvunja mlango ule na wakati wanamalizia kufanya hivyo mhusika alikuwa ametekeleza tukio lake na kutaka kutoka kwa kasi kwa kuwashambulia walinzi wa Ikulu wakiongozwa na Karistus lakini kwa bahati nzuri sana Karistus alimuwahi na kumpiga risasi zaidi ya sita kwenye mwili wake kutokana na kumjua namna alivyokuwa mtu hatari maana kama angempa nafasi ndogo tu huenda angefanikiwa kuua walinzi wengi sana kitu ambacho ingekuwa hasara kubwa sana kwa taifa ukizingatia walinzi wengi walipata mafunzo nikiwa bado nipo Ikulu”
“Raisi aliwahishwa hospitali lakini daktari mkuu wa Ikulu akawa ametoa taarifa kwamba mpendwa wetu wakati anafika pale alikuwa tayari amekufa muda mrefu sana hivyo tukawa hatuna la kufanya. Huyu gaidi ambaye jina lake anaitwa Donald Daniel yeye baada ya kupokea risasi nyingi kwenye mwili wake alikuwa kwenye hali mbaya sana kwani tuliamini kwamba angetusaidia sana kwenye uchunguzi wetu ila kwa bahati mbaya sana naye akawa amepoteza maisha. Tutamuenzi tu kwa sababu alikuwa ni raisi wa nchi ila matendo yake hayakubaliki kamwe na kwa sasa kama serikali tumekubaliana kwamba waziri mkuu Justin Mtadei ndiye anaenda kuwa raisi wa nchi ya Tanzania kutokana na ujasiri wake wa kuamua kupingana na maovu ya raisi hata kuhatarisha maisha yake kitu ambacho sio watu wote wana huo ujasiri wa kukifanya hivyo tunaamini kwamba ataliletea taifa letu mafanikio makubwa sana”
“Mwisho namaliza kwa kusema Tanzania kuwa na amani inawezekana na hii ndiyo zawadi ambayo tulipatiwa na Mungu hivyo tusiruhusu mtu yeyote aingie kwenye vichwa vyetu na kutaka kutuchukulia hii amani yetu binafsi sitakuwa tayari kumwangalia na kumvumilia mtu huyo. Hivyo natoa rai kwa vijana na watu wote nchini, hakuna mtu atafanya uhalifu kwenye nchi hii akabaki salama, kama unaona wewe ndiye chanzo cha uhalifu basi acha mara moja, kama unaona kwamba wewe uwepo wako imekuwa kero kwa mamilioni ya watu basi acha haraka sana kile ambacho unakifanya kabla haujafikiwa maana hatutakuvumilia na adhabu kali sana zitachukuliwa kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa salama wakati wote. Mungu ibariki Tanzania”

Denis Kijazo alitumia saa zima kuweza kuichambua na kuielezea habari hiyo, habari ambayo iliwaacha wananchi kwenye mshangao mkubwa sana, habari ambayo iliwafanya wananchi washindwe wachague lipi la maana zaidi ya kumuamini mtu ambaye alikuwa ni raisi wao mstaafu na waliwahi kumpenda sana. Mambo ambayo yalitokea yalikuwa ni mazito sana ambapo walipaswa kusikitika kumpoteza raisi wao lakini kwa yaliyokuwa yanaendelea watu walijikuta wanaanza kushangilia mwanamke huyo kufariki.
Mijadala ilianza kuzuka kila sehemu usiku huo watu wakiwa wanatukana huku wengine wakidai kwamba wao walikuwa wajuvi zaidi na walizijua tarihi za mababu zilivyokuwa zinaelezea juu ya mambo hayo. Max alipewa ugaidi na taifa ambapo picha yake ilianza kusambaa kwa kasi sana huku baadhi ya watu wakiwa wanamlaani na kutamani kwamba serikali ni bora isingefanya jambo lolote kwake wangemuacha akiwa hai kabisa kisha wawakabidhi wananchi waweze kumalizana naye wenyewe.

57 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 58
Lakini kuna baadhi ya wananchi walimsifia sana mwanaume huyo kwamba alikuwa ni miongoni mwa malegendi wa kukumbukwa kwa kutaka kumuua raisi ndani ya ofisi yake hivyo wananchi walichaguliwa cha kuamini nao wakawa wameingia kwenye huo mtego wa mchezesha kamali maarufu Denis Kijazo kwa udanganyifu mkubwa sana wa tabasamu lake ambalo mara nyingi alikuwa analionyesha hadharani anapokuwa na watu.
“Nadhani umeona kinacho fanyika ndugu yangu wewe mwenyewe ukiwa unahesabu dakika zako za kuwa hai. Una lipi la kuniambia labda?” Dax aliongea kwa sauti yenye kicheko ndani yake akiwa anamgeukia Max kwenye kiti ambacho alikalishwa huku akiwa anavuja damu kila sehemu maana litobolewa sehemu nyingi kwenye mwili wake na risasi. Mwanaume hakuwa na uwezo wa kuanza kubishana nao kwa yaliyo tokea basi alikubali kwamba kila kitu kilikuwa kimeishia pale hivyo hakuna kitu angeweza kufanya zaidi ya kuishia kucheka kwa hasira na uchungu mkubwa sana.
“Pole sana Max hivyo ndivyo siasa inavyofanya kazi ndugu yangu, watu wanachaguliwa cha kuamini na inakuwa hivyo na wale ambao mnajifanya wazalendo wananchi wale wale ambao mlijitoa kwa ajili yao ndio wanataka wewe upelekwe kwao waweze kugawana vipande vidogo vidogo na hilo litaishi milele kila wakiona picha yako au kusikia jina lako basi watakuwa wanakutamani sana au kutamani mno kukuua. Bosi anakuja saivi atakuwa kwenye helikopita hivyo ni dakika kadhaa tu Max ila nataka nikuhakikishie kwamba sura yangu ndicho kitakuwa kitu cha mwisho wewe kukiona kwenye maisha yako” Dax aliongea huku akiwa anamtwisha Max ngumi nzito sana ya mbavu kwenye kiti ambacho alikuwa amefungwa kiasi kwamba mwanaume alipoteza fahamu.
Alikurupuka kwa sauti kali ya maumivu baada ya kumwagiwa maji yenye barafu nyingi sana ndani yake kiasi kwamba iliamsha maumivu ya risasi ambazo alikuwa nazo kwenye mwili wake. Baada ya kukurupuka akiwa anagugumia kwa maumivu makali, sura yake ilikutana na mwanaume ambaye hawakuwahi kupata bahati ya kukutana tangu mwanzo ana kwa ana wakazungumza Denis Kijazo. Kigogo huyo alikichukua kiti ambacho kilikuwa pembeni yake na kukisogeza mbele ya mwanaume huyo kisha akakaa na kutoa sigara yake ya bei ghali sana na kuiwasha wakiwa wawili tu humo ndani.
“Ni jambo la kusikitisha sana maana nasikia umegoma kabisa kufa. Licha ya mwili wako kuweza kupokea risasi sita lakini bado unaishi na hauna hata dalili za kufa kwa sasa hiyo inaonyesha kwamba nafsi yako imegoma kabisa kufa japo mwili unataka lakini mimi naweza kukupa nafasi nyingine ya dhahabu kama utakuwa tayari” mwanaume huyo alikohoa kidogo kumpa mtu wake nafasi ya kumsikiliza na kumuelewa kile ambacho alikuwa anajaribu kumaanisha.
“Nataka nikufanye kuwa muuaji, uue kila mtu ambaye ataonyesha dalili mbaya kwangu na kunipinga mimi hata kama hana hatia au hata kama anacho kisema ni cha kweli. Nataka wewe ndiye uifanye kazi hii tena kwa moyo wote na sio kwamba sina watu wa kufanya kazi kama hiz, wapo wengi sana ila nataka nikupe nafasi ya mwisho kama unaweza kunifanya nikakuamini basi utakuwa kijana wangu. Nimekupa hii nafasi ya upendeleo kwa sababu najua wewe ni kijana bado damu inakuchemka sana hivyo naamini kuna maamuzi ulikuwa unayafanya sio kwa akili yako na kingine una kipaji kikubwa sana cha mapigano ndani yako nahisi nitajisikia vibaya sana mtu kama wewe kukuua kirahisi sana namna hii wakati unao uwezo wa kutengeneza pesa nyingi sana. Ukisema ndiyo nakuacha uishi na kukuitia madaktari bingwa wakupe huduma kubwa na bora sana ila kama ukisema hapana basi nitaagiza ukazikwe ukiwa hai unapumua” alipewa machaguo ya kwenda nayo na sasa uamuzi ulikuwa kwenye mkono wake kuamua kama angeamua kuwa mbwa wa mzee huyo au kuamua kufa kishujaa kama walivyokufa wenzake.
Kitu ambacho Max alikifanya ni kumtemea mate yenye damu mzee huyo usoni kwake kitu ambacho kilimfanya asimame na kwenda kwenye kona moja ya chumba hicho ambako kulikuwa na nyundo nzito sana, aliishusha kwenye goti la mwanaume huyo ambapo goti liliteguka vibaya sana ni basi tu kwa sababu hakuwa na nguvu za kutosha kwenye mkono wake ila nyundo hiyo kama ingetua kwenye mikono ya mtu ambaye alikuwa na nguvu sana kwenye mikono yake basi lazima goti hilo lingesagika vibaya sana.
“Kuna kitu ambacho watu wengi huwa hamjui kuhusu mimi bwana mdogo. Unavyo iona picha ya mtu hautakiwi kumpima kwa macho bali hakikisha una taarifa zake hata asilimia sabini ndipo ufanye maamuzi sahihi namna ya kukabiliana na mtu huyo kwa sababu hizo asilimia zinavuka wastani ila kama mihemko itakuendesha na ukaamua kujichukulia maamuzi yako mwenyewe kwenye akili yako basi asilimia hizo sabini zinageuka na kuwa hatari kubwa sana kwenye maisha yako” alimpa somo la maisha bwana mdogo kwa kufanya chaguo ambalo lilikuwa ni baya sana.
“Una bahati mbaya sana umenikuta kwenye mood mbaya na sina muda mrefu wa kukaa hapa kwa sababu natakiwa kwenda kuanza kurudisha pesa zangu ambazo zimepotea muda huu sasa hivi” aliongea akiwa anacheka kwa sauti sana na kutoka humo ndani ambapo alimkuta Dax akiwa nje na vijana wengine wakiwa wanasubiri amri kutoka kwake.
“Nendeni mkamzike akiwa hai kabisa hivyo hivyo”
“Sawa mkuu” ilikuwa furaha sana kwa Dax ambaye aliingia ndani na kuwapa ishara vijana hao kumbeba Max ili wakamzike akiwa bado anapumua.
Wanaume hao hawakuwa na muda wa kuremba, walipanda kwenye magari usiku huo huo huku mvua ikiwa inaendelea kunyesha. Safari yao ilienda kuishia huko Mpiji Magohe ndani ya kata ya Mbezi kwenye msitu mmoja mdogo ambao ulikuwa unaaminika kwamba ilikuwa maskani ya wahuni wengi na majambazi ambao walikuwa wanateka watu ambao walikuwa wanapita maeneo hiyo mida mibovu.
Huko ndiko ambako walienda kumzika Max ambapo wanaume hao walichimba kaburi kwa haraka sana usiku huo na ndani ya nusu saa kaburi lilikuwa tayari kabisa kwa ajili ya mazishi. Dax alimsogelea mwanaume wa kazi Max na kuongea kwa majivuno sana.
“Nimekuahidi Max kwamba sura yangu ndicho kitakuwa kitu cha mwisho wewe kukiona kwenye maisha yako maana baada ya hapo utakumbana na mchanga tu kisha kiza kitatawala na utahangaika sana kujitoa humo lakini kwa bahati mbaya hautaweza pumzi itakuwa inakata taratibu na baada ya muda mfupi utaanza kuvimba na mishipa kukutoka tena, utatamani uje kuomba msamaha lakini ndo hivyo tena ushachelewa na wakati huo mimi nitakuwa juu ya kiuno cha yule mrembo ambaye alikuwa katibu wa raisi Ikulu maana ni mpenzi wangu hahaha hahahah hahaha Max hii dunia inatisha sana ndugu yangu. Uliniambia KAMALI YAKO YA MWISHO NDIYO KAMALI YANGU YA KWANZA lakini mimi nakwambia kwamba KAMALI YANGU YA KWANZA NDIYO KAMALI YAKO YA MWISHO” alitamka kwa majivuno huku akiwa anamsukumia mwanaume huyo ndani ya kaburi hilo kwa buti kali sana na baada ya hapo vijana wale walianza kulifukia kwa haraka sana ambapo ndani ya dakika mbili walikuwa wamemaliza.
Dax alipanda na kusimama juu ya kaburi hilo kisha akalishindilia vizuri sana na kutoweka hilo eneo haraka sana maana ilikuwa ni siku ya kwenda kushagilia ushindi kwa kufanya mapenzi siku nzima. Kijana Max mpambanaji, kijana ambaye alijitoa kwa ajili ya kulipambania taifa lake, kijana ambaye alikuwa ana ndoto ya kufanya mambo makubwa sana kwa ajili ya wananchi wa Tanzania safari yake ilikuwa imekomea huko kwenye msitu tena akizikwa kwa aibu kubwa sana.
Baada ya kufika kwenye gari Dax alipiga simu kwa kiongozi wake na kumpa taarifa hiyo.
“Kazi imeisha bosi”
“Kazi nzuri sana kijana wangu hakikia nitakufanya kuwa moja kati ya vijana wakubwa na wenye maisha mazuri sana hapa nchini. Ndani ya dakika kadhaa tu kwenye akaunti yako unaingiziwa pesa nyingi sana ambazo utachagua mwenyewe namna ya kuzitumia na utapumzika nchi yoyote ile duniani kwa mwezi mzima maana ushakuwa shujaa wa ulimwengu sasa”
“Asante sana kwa kila kitu bosi, sitakuangusha siku zote” alijibu kwa furaha sana huku simu hiyo ikikatwa. Nafasi kubwa ambayo alikuwa anaitaka tayari alikuwa ameiweka kibindoni na ulikuwa muda wake wa kula maisha kadri atakavyo kwa mazuri ambayo alikuwa amemfanyia Denis Kijazo.

KIBITI, PWANI.
Ndani ya mkoa wa pwani katika sehemu ambayo inajulikana kama Kibiti, sehemu ambayo inadaiwa kwamba ina wale wahuni asilia wa mtaani kutokana na asili ya maisha ya huko lakini ni sehemu ambayo inalima sana mihogo. Jioni hiyo wakati mheshimiwa raisi anatoa hatuba yake mzee mmoja alikuwa akisikiliza redio na mjukuu wake mkubwa wa kiume, ni taarifa ambayo aliisikiliza kwa umakini mkubwa sana mpaka inaisha.
Alitoka nje na kwenda kuketi huku akiwa anainamisha kichwa chake kwa masikitiko makubwa sana ambayo alikuwa nayo, mjukuu wake hakuelewa kabisa kwamba babu yake alikuwa amekumbwa na tatizo gani mpaka kuwa kwenye hiyo hali ilibidi amfuate nje kwenda kumuuliza kile ambacho kilikuwa kinamsibu babu yake.
“Babu mbona umebadilika ghafla badala ya kuwapongeza kwa kufanya maamuzi sahihi ya kumuua mtu ambaye alikuwa anahitaji kuiharibu amani ya nchi yetu?”
“Una miaka mingapi Hamisi?”
“Ishirini na tano sasa”
“Unamjua baba yako?”
“Hapana, kwanini?”
“Ndiyo maana haumjui”
“Kwa sababu ipi?”
“Hizo hizo siasa”
“Sasa hiyo inahusiana vipi na hiki kinacho endelea?”
“Nisikilize mjukuu wangu mimi na baba yako au niseme familia yangu nilihitaji wawe watu wa amani muda wote, nilihitaji familia yangu iwe moja ya sehemu kubwa sana ya kulinda na kuihamasisha amani ya taifa hili lakini unajua ni kipi kilitokea?”
“Hapana babu’’
“Nilimpoteza mwanangu ambaye ni baba yako pamoja na mkwe wangu ambaye ni mama yako”
“Babu?”
“Nisikilize kwa umakini sana. Mimi nimezaliwa nikiwa mwanajeshi tena ambaye nilijitoa haswa kupambana kwa ajili ya nchi hii kiasi kwamba nilipokuja kuvunjika mguu nikampeleka mwanangu jeshini kwa niaba yangu mimi nikawa mtu wa nyumbani tu ambako huko alikutana na mama yako mzazi ambaye alikuwa anafanya kazi ya kuwapikia huko jeshini na yeye hakuwa mwanajeshi ni bahati tu ya mtende ilimuangukia kupata nafasi huko. Baada ya muda mrefu wa kwenye mahusiano ndipo mama yako akaja kupata mimba yako na ndio muda ambao baba yako alikuja kumtambulisha nyumbani na kuamua kumuacha hapa kwangu na yeye akaenda kuendelea kuyapambania maisha kwa kutenda haki haswa kama nilivyokuwa mimi baba yake mzazi”

58 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 59
“Mwanangu alikuja kugundua genge moja la kihalifu ambalo lilikuwa linauza viungo vya watu hususani watoto wadogo kwenda nje ya nchi ambapo watu hao walikuwa wanafanya upotevu wa watoto kuwa mkubwa sana mtaani lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye aliweza kujali kabisa jambo hilo ndipo akaamua kuanza kupambana nao. Alichukua wiki moja tu tangu aanze kuwafuatilia watu hao na kilichorudi hapa ni maiti, mama yako baada ya kumuona baba yako naye alikufa pale pale na ni bahati nzuri sana tayari ulikuwa umezaliwa maana yake kama ungekuwa bado ungefia tumboni kwa mama yako”
“Baadae sana nilikuja kugundua kwamba watu hao walimuua kwa sababu kwenye kuitafuta haki aliyagusa maslahi yao moja kwa moja na ndivyo jinsi siasa inavyofanya kazi. Mimi niliamua kuyasahau yote kwa sababu nilikuwa na wewe hapo, niliichagua amani ushindi nikawaachia wao maana kama ningejaribu hata kupaza sauti basi hata wewe ningekukosa pia. Nacho jaribu kukwambia kwenye maisha yako siku zote ukiona mwanasiasa anatumia nguvu nyingi sana kutaka kuonekana yeye ni mwema basi asilimia tisini na tisa huyo ni mhalifu na ni bazazi ambaye hatakiwa kubakia kwenye uongozi au kwenye nafasi yoyote ya serikali kwani kinakuwa ni kirusi ambacho kinasambaa taratibu”
“Denis Kijazo mimi namjua kwenye siasa kabla wewe haujazaliwa, ni mwanaume mwenye tamaa kubwa sana ya madaraka na mali, ni mtu ambaye yupo tayari kufanya jambo lolote lile ambalo anahisi linafaa ili tu mambo yake yaweze kwenda kama anavyotaka yeye. Amewatapeli watu wengi sana maslahi yao, ameua watu wengi sana kuja kuwa raisi wa nchi hii lakini akiwa madarakani amefanya ufujaji wa mali nyingi sana za serikali kitu ambacho kimeliweka taifa hili kwenye hali ngumu sana. Yule mwanamke nina uhakika aliamua kupambana naye ndiyo maana siku kadhaa nyuma ulisikia habari juu ya uozo ambao alikuwa anaufanya leo hii anakuja kujitanabaisha kwamba yeye ndiye shujaa wa taifa? Hilo ni jambo ambalo haliwezekani ila hakuna cha kufanya kwa sababu yeye ndo mwenye nguvu na yeye ndo mwenye kisu kikali hivyo anakata nyama kadri yeye anavyo ona inafaa”
“Huyo kijana ambaye inadaiwa ameuawa ndiye ambaye alikubali kupigana nao ndiyo maana wameamua kumuondoa haraka kwa sababu angekuja kuwa hatari sana kwao na hao wote ambao wamekufa kutoka serikalini ambao walikuwa kinyume naye ni lazima amewaua mwenyewe ili kuhakikisha siri zake zinabakia hadharani na kwa namna anavyopenda kucheka akiwa mbele za watu basi hakuna mtu hata mmoja atakuja kujua lolote juu yake mpaka kizazi chote hiki kinaisha ila lenye mwanzo huwa halikosi kuwa na mwisho siku zote, inaweza kuchelewa ila ipo siku haya yatafika mwisho na tutapata mtu wa kuja kulikomboa taifa hili kwa mara nyingine”
mzee huyo alitoa shule kwa mjukuu wake na kutoa yale mengi ambayo alikuwa ameyahifadhi kifuani kwa muda mrefu sana maana nchi alikuwa anaijua vyema sana kwa sababu aliwahi kuwepo huko miaka hiyo akiwa bado kijana. Aliondoka hapo akiwa amemwacha mjukuu wake kwenye mwazo mazito sana maana aliambiwa mambo mengi na magumu sana na hakuwahi kuyajua kabla ya kupewa habari hizo siku hiyo.

DAR ES SALAAM
Denis Kijazo alikuwa anajipongea kwa kazi kubwa sana ambayo alikuwa ameifanya. Ni kazi ambayo kama angeifanyia utani ilikuwa inaondoka na maisha yake maana ilifanyika kwa weledi mkubwa na kufanya hata yeye kuwapoteza baadhi ya watu wake kama mkurugenzi wa shirika la kijasusi pamoja na gavana wa benki kuu.
Alikuwa ndani ya jumba lake la kifahari kwenye vyumba vyake vya siri ambavyo mara nyingi alikuwa anavitumia kwa ajili ya mikutano au kama alikuwa anataka kukutana na watu wake wa siri. Alikuwa amesimama akiwa anakunya wine yake taratibu na sigara kubwa mkononi, pembeni yake walikuwa wameketi wanaume wawili wakiwa ndani ya suti za bei ghali sana.
Kazi ya watu hao ilikuwa ni kuhamisha kiwango cha pesa ambacho kilikuwa kinatunzwa benki kuu kwa mgongo wa gavana maana gavana hakuwepo hivyo hiyo pesa ilitakiwa kutolewa haraka sana huko. Wanaume hao walikaa kwa nusu saa wakiwa bize sana na komputa mpakato zao na baada ya hapo ambaye alionekana kuwa kiongozi wa mwenzake aliivua miwani yake na kuiweka pembeni kisha akakohoa kama kumshtua mtu ambaye alikuwa anatakiwa kumsikiliza.
“Umemaliza kazi?”
“Hapana kuna tatizo kubwa sana”
“Kivipi?”
“Hakuna pesa yoyote kwenye hii akaunti”
“Umelewa sio?”
“Nina miaka kumi nafanya kazi na watu wakubwa sana duniani na kwa bahati mbaya sana huwa sio mnywaji wa pombe hivyo nacho kwambia ndio ukweli ambao upo hapa” aliongea akiwa anamgeuzia Denis Kijazo ili aone kwa macho yake maana alianza ubishi na kugoma. Jambo ambalo alilishuhudia lilimfanya ashuke mpaka chini akakaa akiwa anacheka kwa sauti kali sana ila ambayo ilikuwa ya kutia huruma na hasira kali sana ndani yake.
“Whaaaaat?”
“Pole sana nafikiri ni muda wa kutupa malipo yetu sisi tuweze kuondoka kazi iliyotuleta tumeifanya kuliko feli ni wewe na watu wako” Denis Kijazo bado alikuwa haamini hicho kitu hivyo alisogea karibu zaidi na kuanza kuangalia akaunti namba moja moja tena kwa kuhesabu mpaka tarakimu.
Akaunti ilikuwa ni yenyewe kabisa lakini salio lilikuwa linasoma sifuri.
“Kipi kimetokea?”
“Baada ya kuangalia ni kwamba siku chache tu nyuma kiwango cha pesa kikubwa sana kiliweza kuhamishwa kwenda kwenye akaunti zaidi ya miambili. Akaunti hizo nimejaribu kuweza kuzihaki lakini umepita muda mrefu sana hivyo haiwezekani labda kama ingekuwa siku ile ile japo napo tungefanikiwa kurudisha pesa ndogo sana maana hizo akaunti ni za nchi tofauti tofauti duniani. Kinacho fanyika kama ukifanikiwa kuzihaki basi unaanza na nchi moja moja ambapo kila dakika inarudi shilingi elfu kumi sasa mpaka uje ufikishe hata bilioni moja unaye mfuatilia atakuwa ameshtuka muda mrefu sana ila kwa hapa ilipo fikia hakuna namna unaweza ukafanya kuweza kuzipata tena hizo pesa labda kama unamjua mhusika umtafute moja kwa moja” mwanaume huyo alimaliza maelezo yake akiwa anakabidhiwa begi la pesa na mlinzi.
Hao walikuwa ni watu wa kukodiwa ambao walikuwa wana uwezo wa kuhamisha pesa nyingi sana mtandaoni kwa njia salama kabisa na mtu yeyote yule asiweze kushtuka hata kama anaibiwa lakini pia walikuwa ni wadukuzi hatari mno ndiyo maana wafanya biashara wengi wakubwa walikuwa wakifanya nao biashara. Kazi zao walikuwa wanazifanya kwa masaa kadhaa tu na baada ya hapo walikuwa wanapokea malipo makubwa sana kwa hiyo kazi yao. Denis Kijazo aliwalipa watu hao pesa kibao na bado yeye hakuambulia hata mia ya kubahatisha kwenye matirioni ya fedha”
“Msafiri Kigoti mshenzi mkubwa wewe, kwanini ulinifanyia usaliti mkubwa sana namna hii?” aliongea kwa hasira sana huku akitoa bastola na kumimina risasi zote kwenye kioo ambacho kilikuwa mbele yake. Alichukia sana kwa kile ambacho kilikuwa kinafanyika kwani aligundua moja kwa moja kwamba ambaye alifanikisha watu hao kuzipata pesa hizo lazima alikuwa ni huyo gavana kwani ndiye ambaye alitekwa na watu hao na hakuna mtu mwingine ambaye alikuwa ana uwezo wa kuzipata pesa hizo zaidi yake na gavana mkuu wa benki kuu.
Alikuwa anahangaika sana humo ndani huku asijue ni kitu gani ambacho alikuwa anatakiwa kukifanya.
“Inatakiwa nimpate mtu mmoja miongoni mwao wale ambao walikuwa upande wa raisi Teodensia Kijazi” aliongea akianza kucheka cheka mwenyewe bila mpango maalumu lakini aligundua kwamba watu ambao alikuwa anawataka kwa wakati huo walikuwa wamekufa hivyo hakuna kitu ambacho kingefanikiwa. Alichukia sana mheshimiwa tajiri.
“Niitie Ted hapa haraka sana” aliongea kwa sauti ya juu kwa mlinzi wake ambaye hata hakujibu zaidi ya kutoka nje, dakika moja tu alirudi na mwanaume huyo ambaye alionekana kwamba hakuwa mbali wakati mambo hayo yanatokea.
“Yule kijana yupo hai?”
“Unamaanisha Max?”
“Ndiyo”
“Hapana mkuu, ulisema auliwe na kuzikwa na imefanyika hivyo”
“I need one of them” kauli yake ilimfanya mheshimiwa ageuke kwa mshangao kana kwamba hakuwa anaamini kile ambacho kilikuwa kinaongelewa.
“Mmoja wao anaishi”
“Whaaaaat?”
“Ndiyo bosi”
“How”
“Wale vijana wa DRAGON BOYS waliokuwa wapo chini ya Francis Mboye mmoja wao amefanikiwa kuondoka akiwa hai pale na nimeamua kutomtafuta kwa makusudi” mheshimiwa licha ya kuweza kufurahishwa sana na taarifa hiyo lakini bado alihitaji kujua sababu ya msingi hasa ya mwanaume huyo kuweza kumuacha mtu huyo hai na kudai kwamba alikuwa na sababu za msingi za kuweza kufanya hivyo.
“Unaweza kunipa sababu ya msingi ya wewe kufanya kitu cha hatari kama hicho?”
“Ndiyo mkuu”
“Nakusikiliza”
“Nilimuacha hai ili kujua kama wameisha wote au kuna watu wengine zaidi ya wale ambao tumewamaliza. Sikutaka tufanye kosa la kuamini kwamba tupo salama moja kwa moja ndiyo sababu kubwa ambayo imenifanya nicheze hii kamali na kama hivi tumeanza kuwahitaji tena. Lengo kubwa nlijua kwamba kama atakuwa na wenzake kwa yale ambayo umeyazungumza basi lazima ataenda kuwapa taarifa zote na hawatakubali mpaka Teodensia Mpanzi anazikwa lazima watakuwa wamejitokeza kuleta madhara au kuhitaji kukuchafua kwenye mitandao hivyo tutafanikiwa kuwaua wote na kama walikuwa wameisha basi yule kwenye maisha yake yote ataenda kujificha mbali sana na maisha ya wanadamu wa kawaida kwa sababu anajua kabisa kwamba atatafutwa sana”

59 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 60
“Hahahah hahaha namhitaji” mheshimiwa alicheka sana akiwa anasogea kwenye kiti na kukaa
“Lakini hii sio garantii mheshimiwa kwa sababu ni Kamari tu hivyo tunatakiwa kuendelea na mipango mingine tukiwa tunasubiria kama hili litafanikiwa”
“Nalijua hilo na nahitaji nchi hii ilipe gharama zangu zote, waziri mkuu anatakiwa kukopa pesa nyingi sana nje na kusaini mikataba ya pesa nyingi sana kupitia jina langu ili nirudishe hasara yangu na kama isipopatikana hii pesa basi kuna watu lazima nitawaua na watakao umia sana ni wananchi na sio mimi kama walivyokuwa wanadhani kwamba watanikomoa. Kwa sasa nataka nitafutiwe malaya mrembo kuzidi wote nchi hii nadhani unajua ni wapi pa kumpeleta nitakaa naye kwa siku kadhaa”
“Sawa bosi” maagizo yalikuwa yanajitosheleza hivyo mwanaume alitoka nje kwenda kuanza kuyakamilisha.

James, mmoja wa memba wa kundi hatari la DRAGON BOYS alifanikiwa kutoroka na kutoka akiwa mzima wa afya kabisa lakini ilikuwa tofauti kwa wenzake wawili ambao walipoteza maisha yao pale pale sehemu ambayo walikuwa wanapambana na Ted na Kenedy. Mwanaume huyo kuishi kwake alikuwa anatakiwa kuhakikisha kwamba Max anaishi tena na kuwa hai na ndiyo majukumu ambayo aliachiwa na kiongzi wake Bilali Rikardo.
Baada ya kufanikiwa kutoka pale alienda moja kwa moja mpaka ndani ya jumba lao ambalo lilikuwa karibu kabisa na shirika la msalaba mwekundu na kuingia ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na mashine moja ya mionzi na mashine moja iliyokuwa na makali mithili ya sindano. Aliingia kwenye mashine hizo ambazo zilikuwa zimeunganishwa, ile mionzi iliwashwa kuelekea ulipokuwa mwili wake na baada ya sekunde kadhaa alikuwa anapiga makelele sana kwa maumivu makali ambayo alikuwa ameyapata.
Baada ya dakika moja tu mashine ambayo ilikuwa na sindano kali na kubwa ilichana sehemu ya mwili wake na kutoa kitu ambacho kilikuwa kama laini ya simu lakini kilikuwa kidogo sana. Kilikuwa ni kifaa cha mawasiliano ambacho kilikuwa kimepandikizwa kwenye mwili wake na alijua kwamba hicho kingemfanya yeye akamatwe kirahisi sana. Mwanaume alipitia maumivu makali sana kiasi kwamba alidondoka kabisa chini huku mashine hizo zikijizima zenyewe baada ya kazi hiyo kuisha. Alikaa hapo kwa dakika kama tano akiwa nahema kwa nguvu sana maana ile mionzi ilikuwa na nguvu kubwa mno na mwili wake haukuwa bado umetulia vizuri lakini hakuwa na muda wa kupoteza.
Akiwa kifua wazi alisimama kwa kusaidiwa na ukuta akaanza kujivuta kuelekea kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana, aliziwasha na kutaka kubahatisha jambo moja japo kwenye nafsi yake hakuwa na imani kama jambo hilo lingeweza kufanikiwa ila aliamua kuziamini hisia zake na kukisia hivyo hivyo. Wakati wanafanya mawasiliano ya mwisho na Max alikuwa na simu kwenye mwili wake, hata wakati anakamatwa na Dax mwanaume alitolewa shati na koti tu pekee, suruali yake nzito ya kazi ilikuwa kwenye mwili wake na hata buti lake ilikuwa hivyo lakini moja kati ya makosa ambayo waliyafanya ni kushindwa kumkagua mtu huyo kwenye mifuko yake kwa sababu walijua ni siku yake ya mwisho hivyo hawakuwa na huo umakini zaidi ya kutoa kifaa cha mawasiliano tu kwenye mwili wake.
Hiyo ndiyo simu ambayo ilikuwa kwenye mifuko ya Donny ndiyo James alikuwa anahitaji kuitumia ili kujua kama mwanaume huyo alikuwa wapi majira hayo ya usiku ili kama atakuwa hai awahi kuweza kumsaidia. Ilikuwa ni kama bahati nasibu tu kwa mdukuzi hatari sana huyo ambaye alikuwa anategemewa sana na kundi lake kwa hiyo kazi. Alikaa kwenye komputa hizo na kubonyeza kwa muda kidogo ambapo simu hiyo aliipata tena ikiwa hewani na location yake ilikuwa inasoma Ikulu.
Alisubiri kuona kama inaweza kupotea hapo na kweli baada ya muda aliona inaanza kusogea na kuonekana inatoka kabisa ndani ya hilo eneo. Mwanaume alisogea kwenye kabati moja na kutoa vidonge akiwa anayumba yumba kwa sababu bado mwili wake ulikuwa na maumivu makali sana. Vidonge alivyotumia vilikuwa ni hatari sana kwa uhai wa seli kwa sababu vilikuwa vinaupa mwili nguvu kwa lazima hivyo ilikuwa ni hatari kwa upande wa afya yake ila hakuwa na namna kazi ambayo ilikuwa mbele yake kuliokoa taifa ilikuwa ni mhimu sana kuliko hata maisha yake.
Baada ya kunywa dawa hizo alilia kama mtoto mdogo akiwa ameshika kichwa maana zilimletea maumivu makali sana na baada ya dakika tatu alitulia kwa dakika moja kisha akaamka akiwa sawa kabisa mwili ukiwa umelowa kwa jasho.
“Max wewe ndiye pekee ambaye unaweza kuja kulisaidia taifa hili tafadhali sana naomba usife, nakuja kwa ajili yako” aliongea kwa msisitizo sana akichukua nguo zake za kazi na bastola kwenye kiuno chake kisha akatoweka kwa gari ndani ya hilo eneo.
Simu hiyo ilikuwa inamuelekeza wapi pa kwenda kulingana na namna ilivyokuwa inahama, alitembea akiwa umbali kidogo baada ya kuziona gari ambazo zilionyesha kwamba ndimo simu hiyo ilimokuwemo. Hakuwa na uhakika kama simu hiyo alikuwa nayo bado Max ila hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake ya pekee kabisa maana hakuona tobo lingine la kuweza kufanya hivyo. Safari ya wanaume hao iliishia msituni ambapo hata yeye mwenyewe alisimama na kuligeuza gari lake na kulipenyeza ndani ya miti baada ya kuona watu hao wanamtoa mtu kwenye gari na kuanza kuelekea naye ndani msituni huku wengine wakiwa wameshika majembe na koleo kadhaa wakiwa na haraka sana mvua ikiwa inaendelea kushuka.
Mwanaume aliwafuatilia kwa umakini sana mpaka walipofika pale na kuanza kuchimba kaburi ambapo walichimba na kisha kwa muda mfupi mwanaume huyo alirushiwa ndani ya kaburi hilo na kuanza kufukiwa. James kwa hali ambayo alikuwa ameiona alikuwa amekata tamaa kabisa kwamba mtu huyo mpaka anazikwa maana yake ni kwamba alikuwa ameshauawa hivyo alikata kabisa tamaa lakini kuna kitu kimoja ambacho kilimshtua na kuhisi kwamba kuna kitu huenda hakikuwa sawa kabisa. Ni baada ya kumsikia Dax akiwa anamkumbushia mwanaume huyo kwamba sura yake ndicho kitu cha mwisho kabisa yeye kuweza kukiona kisha utafuata mchanga na giza halafu pumzi itaanza kukata na baada ya hapo utakufa vibaya sana.
Tambo za Dax ndizo ambazo zilimhakikishia kwamba mwanaume huyo alikuwa mzima bado ila huenda kuna kitu kibaya alifanyiwa. Hayo yote alikuwa anayashuhudia akiwa amejibanza sehemu kwenye mti mmoja mkubwa ambao ulikuwa na matawi mengi sana. Aliwashuhudia wanaume hao wakifukia kaburi hilo mpaka walipomaliza kisha Dax akalishindilia vizuri na kuanza kuondoka lakini kitu ambacho walikosea ni baada ya kuona vifaa vyao vina tope sana waliamua kuvitupia porini na kuvitelekeza huko huko.
James alikuwa makini sana kuwaangalia watu wale walivyokuwa wanatokomea mpaka kufika kwenye magari yao na kuanza kuondoka. Mwanaume alisogea hiyo sehemu akiwa na wasiwasi sana, alishika koleo moja na kuanza kufukua kwa kasi ya ajabu mno kwenye kaburi hilo ambalo lilimchukua muda mfupi sana kuweza kuukuta mwili wa mwanaume huyo wa kazi tena ukiwa kifua wazi kabisa. Alimtoa nje na kumgusa puani, mwanaume hakuwa akitoa pumzi yoyote ile, alimgusa kwenye moyo palikuwa kimya sana na mwisho akagusa shingo, hakuhisi kitu chochote kile kama mtu yule alikuwa hai.
“Hapana Max huwezi kufa kwa staili hii, hii nchi inakuhitaji sana” aliongea akiwa na wasiwasi sana, alimjazia pumzi sana kwenye mdomo lakini wapi hakuona chochote, alimbeba akiwa anakimbia na kuelekea alipokuwa amepaki gari yake kwa kasi mno kisha aliitoa hapo kama vile ana kichaa kuwahi kwenye makazi yake akaangalie kama anaweza kumsaidia mtu huyo maana nafsi yake ilikuwa inagoma kabisa kuamini kwamba mtu huyo alikuwa amekufa.
Akiwa anapita njiani kwa kasi alikutana na ule msafara wa akina Dax, wao hawakuwa wamemuona maana aliwapita kasi sana ila alifanikiwa kumuona mwanaume huyo kupitia dirishani akiwa anajipongeza kwa pombe kali, alimwangalia kwa hasira sana lakini hakuwa na cha kufanya muda huo ulikuwa ni wakati wa kujaribu bahati yake kama anaweza kumsaidia huyo mwanaume ambaye aliambiwa kwamba ndipo tumaini la nchi lilipokuwa.
Alifanikiwa kurudi nyumbani, ambapo yalikuwa ni makao makuu ya DRAGON BOYS na kumuweka Max kitandani akiwa bado ana tope kwenye mwili wake, alimsafisha vizuri kisha akajaribu kupampu moyo na mashine lakini hakuona chochote. Alijitahidi sana kumuwekea mpaka vifaa vya kupumulia lakini bado ilikuwa kama ni kazi bure na dalili za kuamini kwamba mtu huyo hakuwa hai na alikuwa amekufa zilikuwa zinaanza kuja hasa baada ya kumsafisha na kuona kwamba mwanaume huyo alikuwa na risasi za kutosha kwenye mwili wake.
James alisogea kwenye komputa yake na kuingia kwenye mtandao wa madaktari, alikuwa anahitaji kumpata daktari wa kukodisha kwa muda. Alitengeneza jina feki ili liweze kumsaidia kwenye kuaminina na akafanikiwa kumkuta daktari mmoja ambaye alikuwa anajulikana kama daktari hodari sana lakini alikuwa ni mtu mpenda rushwa sana kwenye huduma yake hiyo. Aliwasiliana naye na kumuahidi kiasi kikubwa sana cha pesa ila kikubwa yeye alikuwa anataka tu mtu wake aweze kupona na daktari huyo hakuwa na tatizo kikubwa ambacho yeye alikuwa anajali ni pesa kuingia kwenye akaunti yake tu.
Dakatri huyo alifika ndani ya dakika arobaini tu usiku huo huo wa manane maana dau ambalo aliwekewa mezani lilimfanya hata usingizi wake kuisha baada ya kupokea simu. Kukutana na James alimkuta mwanaume huyo akiwa na wasiwasi mkali sana hivyo akajua kabisa kwamba hapakuwa pema. Bila kuongea walipeana mikono na mwanaume huyo akamuongoza daktari huyo ambaye alikuwa anawaza pesa tu kwenye kichwa chake mpaka ndani ya chumba ambacho alikuwa amelazwa Max. alishtuka sana baada ya kuiona sura hiyo kwa sababu kila sehemu ya nchi zilikuwa zimesambazwa taarifa kwamba mwanaume huyo alikuwa ni gaidi na alikuwa amekufa, sasa ilikuwaje awe hapo na awe hai? Alihisi hakuwa salama.
“Huyu si gaidi?”
“Vyombo vya habari ndo vinasema hivyo”
“Unataka mimi nimtibu mtu aliye muua raisi wa nchi? Unataka mimi nimtibu mtu ambaye dunia nzima inajua kwamba ni msaliti kwa taifa lake? Unahisi kitanikuta nini watu wakijua kwamba mimi ndiye niliyaokoa maisha yake?”
“Hakuna atakaye jua kuhusu hili”
“Unajuaje kwamba itakuwa hivyo?”
“Kwa sababu hakuna namna ya wewe kuweza kuongea” kauli za James daktari alishindwa kabisa kuzielewa ila kama angezielewa huenda angetafuta mapema njia ya kuweza kuyaokoa maisha yake.
“Hata kama ni hivyo bado siwezi kumtibu mimi”
“Nakulipa bilioni moja kwa kazi ya usiku mmoja tu. Pesa ambayo huenda haujawahi kuishika mkononi hapo hapo na huenda hautakuja kuishika milele mpaka unakufa, wewe ni mtu smart sana dokta usitake kuikataa hii ofa ambayo ninaweza kumpatia daktari yeyote yule na akaja muda huu” dau lilikuwa ni kubwa mpaka yeye mwenyewe anavyotajiwa alishtuka sana maana hakutegemea huko, aliishia kuguna na kuiweka tai yake sawa huku akilitua begi lake la kazi mezani. Hiyo ilikuwa ni ishara ya kukubali kazi.
“Huyu mtu ni nani hasa kwako mpaka unaweka pesa nyingi sana kiasi hicho kwa ajili yake?”

60 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 10
Aliyekuwa mbele alipigwa kwenye shingo na kiganja alikata moto hapo hapo hakuweza kuongea tena alidondoka chini, buti la mwanaume wa pili lilikuwa linakuja kwenye shingo yake alibendi kwa nyuma huku visigino vyake pekee ndivyo vilikuwa chini. Kwa namna alivyo jizungusha ilikuwa ni ngumu kwa mtu wa kawaida kubaki amesimama zaidi ya kudondoka vibaya lakini kwa mwanaume huyo lilikuwa zoezi rahisi sana wakati anasimama vyema alirudi na ngumi mbili ambazo zilitua kwa mwanaume mmoja lakini na yeye pia alipokea mateke ya mbavu mawili kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye alitokea pembeni akateleza chini kwa miguu yake na kusimama kisha na yule mwanaume ambaye alikuwa amedondokea mbele yake akiwa ananyanyuka na kudondoka tena kwa ngumi ambazo zilikuwa zimetua kwenye kifua chake lakini alifanikiwa kusimama vyema.

Mwanaume huyo baada ya kuona watu hao wanazidi kumchukulia muda wake alijiviringisha kwa chini na kuinukia pale walipokuwepo huku kwenye mkono wake akiwa na cheni ambayo ilikuwa imeandikwa B13 na cheni hiyo alikuwa akiikunjua kinakuwa kisu kikali sana hivyo wakati anasimama hapo mguu wa mwanaume mmoja ambaye alikuwa anahitaji kumtwisha nao hapo alipokuwepo aliudaka na kuzamisha cheni hiyo ambayo ilitoboa toboa vibaya sana hilo buti hali ambayo ilimfanya mwanaume huyo ajivute nyuma ili asije akapata madhara ya cheni hiyo lakini kurudi kwake nyuma kulimfanya mwanaume ambaye alikuwa kwenye hayo manguo ya magunia kuinamia kwa mbele kisha akampiga mwanaume mwenzake vibaya sana na kisigino cha mdomoni ambacho kilimtoa damu nyingi sana na kumfanya arudi nyuma akiwa anaguna kwa maumivu.

Mwenzake alikuwa anakuja kwa haraka sana lakini hatua zake hazikuendana na mtu ambaye alikuwa anashindana naye mpaka aliposhtukia cheni ipo kwenye shingo yake, mwanaume huyo alihitaji kuifungua cheni hiyo ili kuipoteza shingo ya mtu huyo ila alighairisha zoezi lake baada ya kusikia mlio wa gari ukifika hilo eneo kwa kasi sana.
“Stop” ni sauti ambayo ilisikika kutoka kwa mzee ambaye alikuwa anashuka ndani ya gari hiyo ambapo mwanaume huyo alimzunguka mwenzake kwa nguvu na kumpiga mtama mkali kisha akamkita na goti kwenye kifua chake ambapo alienda kudondokea kwenye miguu ya yule mze ambaye alikuwa ameshuka akiwa na walinzi wawili.

“Bosi?” mwanaume huyo ambaye alikuwa amevamiwa hilo eneo akiwa kwenye hayo manguo yake aliita kwa mshangao huku akiwa anainama kutoa heshima kwa kiongozi wake huyo.
“Ni vizuri haujamuua hata mmoja maana kama ningechelewa kidogo ningewapoteza vijana hawa ambao hawana hatia yoyote ile”
“Sikujua kama ni wewe uliwatuma hapa ila washukuru sijataka kuwaua haraka maana nilitaka niwajue kwanza kwamba ni akina nani ila bila hivyo ningewaua muda mrefu sana”

“Panda kwenye gari” mzee huyo alitoa amri moja tu kisha gari hiyo ikatolewa hapo kwa kasi sana huku wale wanaume watatu ambao walikuwa wamevamia hapo wakikokotana na kutoweka haraka sana hilo eneo kwani maagizo ambayo walikuwa wamepewa na kiongozi wao walikuwa wameyatakeleza vizuri. Gari hiyo ilienda kusimamishwa maeneo ya mzambarauni pembezoni mwa reli ya treni na mzee huyo akawataka walinzi wake wawili watoke ndani ya hiyo gari alihitaji kubaki na kijana wake tu pekee na taa zote zikazimwa pakawa kimya sana ndani ya hilo eneo.

“Bilali nadhani unatakiwa kuwa makini sana, usipende sana kuitoa toa cheni yako hiyo kwa sababu ina utambulisho wa kifupisho cha jina lako, kuna watu ambao ni wataalamu sana wa kuunganisha doti hivyo inaweza kupelekea wewe ukajulikana haraka sana sehemu ambayo unakuwa upo mwisho wa siku ukaja kupotea kizembe sana. Kwenye kikosi cha DRAGON BOYS kumbuka wenzako wawili wanakutazama wewe hapo hivyo hautakiwi kufanya ujinga wowote ule ambao unaweza ukafanya wenzako wakaingia kwenye hatari”
“Nimekuelewa bosi, naomba unisamehe sana kwa hilo”
“Hayo yameisha nipe ripoti kamili”
“Hawa watu nimewafuatilia kwa umakini sana lakini kiufupi ni kwamba mheshimiwa raisi yupo kwenye hatari kubwa sana ya kuweza kuuawa”
“Hilo nalijua, nahitaji unipe taarifa kamili kwamba ni nani yupo upande wetu na ni nani hayupo upande wetu na nahitaji kujua sana kwamba ni akina nani ambao Denis anawaamini sana na kuwatumia sana kwenye hizi kazi zake”
“Watu wengi ambao wapo kwenye mfumo wa serikali ni wake na wanamtii yeye, kuanzia jaji mkuu wa serikali, mwanasheria mkuu wa serikali, spika wa bunge, waziri mkuu ambaye mpaka sasa hajatolewa, makamu wa raisi ambaye amemaliza naye utawala na watu wengi sana Ikulu wapo upande wake lakini jambo la hatari zaidi hata mkurugenzi wa shirika letu la kijasusi ni mtu wake wa karibu sana na kila habari nyeti huwa anampatia”
“Whaaaat?”
“Ndiyo bosi iko hivyo lakini pia kuna watu wachache sana ambao hawapo upande wake”
“Ni akina nani hao?”
“Kuna kiongozi mmoja wa upinzani lakini kwa wale ambao wapo ndani ya chama chake kuna DCI na IGP, hawa tunaweza kuwatumia kama silaha kwetu”
“Kwa namna ipi?”

“Kwa sasa mheshimiwa raisi anatakiwa kumteua waziri mkuu ambaye anamwamini sana kwa sababu tutamhitaji sana hapo baadae lakini pia anatakiwa kumpata makamu wa raisi ambaye ataweza kumuamini sana ndiye ampe hii nafasi na kwenye baadhi ya vitengo vikubwa tuwapenyeze wapelelezi wetu wa kuaminika ambao watakuwa wanakusanya taarifa za watu hao na kutupatia na hapa inatakiwa tuwapate watu ambao wapo nje ya mfumo ndio itakuwa rahisi zaidi kuweza kuwamudu kwenye kuwaendesha ila asimtoea mkurugenzi wa taasisi ya kijasusi”
“Kwanini asitolewe?”
“Huyu atatusaidia sana kwenye ukamilisho wa kuzipata taarifa za ndani sana za watu hao”
“Mtu ambaye hayupo upande wetu anatupaje taarifa za watu hao?”
“Nadhani unajua kuhusu yeye kumpa mheshimiwa raisi wale walinzi wawili na unajua kabisa kwamba wamelekwa pale kwa kazi maalumu?”
“Hilo nalijua, endelea”

“Sasa kwa wale vijana wawili ambao wamepewa ile kazi kuna walakini kwamba mmoja ni mzalendo na mwingine ni mtu wao ambaye wamemtuma kwa kazi maalumu pale Ikulu ndiyo maana nasema kwamba maisha ya raisi yapo hatarini muda wote kwa sababu muuaji yupo naye anamlinda muda wote vipi kama akipewa maagizo ya kuweza kumuua? Ni suala la dakika moja tu kutekeleza amri ya kiongozi wake ila sisi tutaitumia hii nafasi kuwaingiza wao kwenye shimo” mwanaume huyo ambaye alijulikaan kama Bilali alikohoa kidogo kujiweka sawa ili ampe mheshimiwa mpango mzima juu ya kile ambacho walitakiwa kukifanya hapo kuwatia watu hao kwenye mifuko yao.

“Nimefuatilia kwa undani sana taarifa za wale vijana tangu wanaanza kupatiwa mafunzo hapa Tanzania mpaka wanafikia hatua ya kumlinda mheshimiwa raisi ila mmoja wao kuna tatizo kidogo kwenye rekodi zake ndiyo maana ndiye ambaye naweza kusema kwamba ni msaliti na anafanya kazi zao wale watu. Anaitwa Karistus Dickson ni mzaliwa wa jiji la Mwanza huko, huyu kwenye rekodi zake alikuwa ni mtu ambaye kila baada ya siku kadhaa alikuwa akipotea kwenye kambi na baada ya muda kama wa dakika kumi angeonekana anarudi na kujumuika na wenzake na kwa huo muda ambao aluikuwa anapotea inaonekana alikuwa anafanya mawasiliano kwenye simu na baadhi ya watu jambo ambalo kiitifaki halikutakiwa kufanyika hivyo hilo limeleta uwalakini kwamba lazima alikuwa anaendelea kufanya kazi yake hata akiwa mafunzoni ya kuripoti kila ambacho kilikuwa kinaendelea kwa viongozi wake hivyo huyu ndiye hatari kubwa zaidi ambayo ipo kwa upande wa raisi na haitakiwi huu mpango ubadilike haraka sana namna hii maana inaweza kuwa hatari huyu anatakiwa kuendelea kuwepo pale ili kutimiza kazi yetu kwa usahihi”

“Lakini huyu mwingine ambaye anaitwa Donald Daniel, yeye ni kijana ambaye sina uhakika ila anaonekana ni mzalendo sana na ndiye ambaye tunatakiwa kumpata haraka sana kwa namna yoyote ile maana jina lake ni safi zaidi hata ya Obama kwa sababu hana historia yoyote ile mbaya wala kukutwa na tatizo au dosari yoyote ile kwenye maisha yake hata alipokuwa huko kwenye mafunzo lakini pia ni mwanaume wa shoka sana. Rekodi zake zinaonyesha kwamba alikuwa amepata alama za juu sana za mapigano na upelelezi kwenye kila sehemu ambayo alikuwa amepita hivyo naweza kusema anatufaa moja kwa moja”

“Na huyo kijana tunampataje?” mzee huyo aliingilia meongezi hayo baada ya kuonekana kwamba alikuwa amemuelewa sana kijana wake.
“Mtu pekee ambaye anatakiwa kufanya naye haya mazungumzo ni mheshimiwa raisi bosi”
“Hilo ni jambo gumu sana, tunaweza kujiingiza kwenye shimo sisi wenyewe, vipi kama akimmwagia hizo siri halafu akawa tofauti na unavyo mdhania huoni kama raisi atakuwa amejiteketeza yeye mwenyewe?”
“Bosi hii ndiyo njia ngumu lakini ndiyo njia pekee. Nina uhakika na taarifa zangu hivyo kwa asilimia sabini nina imani nipo sahihi na kama sipo sahihi basi ni kwa asilimia thelathini tu ambazo haziwezi kuathiri mpango wetu na kama tukimpata huyu tayari tutakuwa na mtu wa mhimu wa kumwamini kwenye mkono wetu ambaye anaweza kutusaidia sana kutekeleza majukumu haya ya mhimu”
“Na baada ya kumpata mpango wako ni upi?”

“Huyu atatusaidia kumchunguza kwa ukaribu sana mkurugenzi wa taasisi ya kijasusi kwa sababu yeye anaweza kukutana naye muda wowote ule hivyo kupitia yeye tutaweza kupata taarifa nyingi na kumbuka ukimtoa raisi yule ndiye mtu mhimu zaidi ndani ya taifa kwa sababu ana taarifa za siri ambazo zinaweza kuliteketeza taifa au kulikomboa taifa”
“Mpango wako mwingine ni upi?”

“Wakati kazi hiyo inafanyika ndio muda ambao raisi anatakiwa kuufungia ukumbi ule kama tulivyokuwa tumekubaliana mwanzo na muda huo mimi nitakuwa nimeingia kwenye upelelezi ili kuweza kuwajuia washirika wake wengine wa siri ambao huenda wanampa nguvu kuliko hawa wanasiasa maana lazima kuna wawekezaji wakubwa ambao wapo nyuma yake sasa tunatakiwa kuwapata hao na kama tutafanikiwa kuwapoteza ndipo tunaweza kumfuata yeye moja kwa moja itakuwa kazi sio ngumu sana kuliko kumfuata yeye bila kuwajua ambao wapo nyuma yake hapo hakuna jambo la maana ambalo tutakuwa tumelifanya zaidi ya kupoteza muda tu”

“Good, umefanya kazi nzuri sana lakini kuna jambo lingine ambalo ulisema kwamba ulikuwa unahitaji sana kuniambia kwa haraka mno”
“Ndiyo bosi ndiyo maana nikataka tuonane moja kwa moja”
“Lipi hilo”
“Unamkumbuka Laurenti Mande?”
“Ndiyo, aliwahi kuwa rafiki yangu kwa kipindi fulani, huyo si gavana ambaye alipoteaga kwenye mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa inaaminika kwamba alifia baharini?”

Naweka nukta sehemu ya 10 panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Tchao.
Hongera mkuu kazi nzuri
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 60
“Hahahah hahaha namhitaji” mheshimiwa alicheka sana akiwa anasogea kwenye kiti na kukaa
“Lakini hii sio garantii mheshimiwa kwa sababu ni Kamari tu hivyo tunatakiwa kuendelea na mipango mingine tukiwa tunasubiria kama hili litafanikiwa”
“Nalijua hilo na nahitaji nchi hii ilipe gharama zangu zote, waziri mkuu anatakiwa kukopa pesa nyingi sana nje na kusaini mikataba ya pesa nyingi sana kupitia jina langu ili nirudishe hasara yangu na kama isipopatikana hii pesa basi kuna watu lazima nitawaua na watakao umia sana ni wananchi na sio mimi kama walivyokuwa wanadhani kwamba watanikomoa. Kwa sasa nataka nitafutiwe malaya mrembo kuzidi wote nchi hii nadhani unajua ni wapi pa kumpeleta nitakaa naye kwa siku kadhaa”
“Sawa bosi” maagizo yalikuwa yanajitosheleza hivyo mwanaume alitoka nje kwenda kuanza kuyakamilisha.

James, mmoja wa memba wa kundi hatari la DRAGON BOYS alifanikiwa kutoroka na kutoka akiwa mzima wa afya kabisa lakini ilikuwa tofauti kwa wenzake wawili ambao walipoteza maisha yao pale pale sehemu ambayo walikuwa wanapambana na Ted na Kenedy. Mwanaume huyo kuishi kwake alikuwa anatakiwa kuhakikisha kwamba Max anaishi tena na kuwa hai na ndiyo majukumu ambayo aliachiwa na kiongzi wake Bilali Rikardo.
Baada ya kufanikiwa kutoka pale alienda moja kwa moja mpaka ndani ya jumba lao ambalo lilikuwa karibu kabisa na shirika la msalaba mwekundu na kuingia ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na mashine moja ya mionzi na mashine moja iliyokuwa na makali mithili ya sindano. Aliingia kwenye mashine hizo ambazo zilikuwa zimeunganishwa, ile mionzi iliwashwa kuelekea ulipokuwa mwili wake na baada ya sekunde kadhaa alikuwa anapiga makelele sana kwa maumivu makali ambayo alikuwa ameyapata.
Baada ya dakika moja tu mashine ambayo ilikuwa na sindano kali na kubwa ilichana sehemu ya mwili wake na kutoa kitu ambacho kilikuwa kama laini ya simu lakini kilikuwa kidogo sana. Kilikuwa ni kifaa cha mawasiliano ambacho kilikuwa kimepandikizwa kwenye mwili wake na alijua kwamba hicho kingemfanya yeye akamatwe kirahisi sana. Mwanaume alipitia maumivu makali sana kiasi kwamba alidondoka kabisa chini huku mashine hizo zikijizima zenyewe baada ya kazi hiyo kuisha. Alikaa hapo kwa dakika kama tano akiwa nahema kwa nguvu sana maana ile mionzi ilikuwa na nguvu kubwa mno na mwili wake haukuwa bado umetulia vizuri lakini hakuwa na muda wa kupoteza.
Akiwa kifua wazi alisimama kwa kusaidiwa na ukuta akaanza kujivuta kuelekea kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana, aliziwasha na kutaka kubahatisha jambo moja japo kwenye nafsi yake hakuwa na imani kama jambo hilo lingeweza kufanikiwa ila aliamua kuziamini hisia zake na kukisia hivyo hivyo. Wakati wanafanya mawasiliano ya mwisho na Max alikuwa na simu kwenye mwili wake, hata wakati anakamatwa na Dax mwanaume alitolewa shati na koti tu pekee, suruali yake nzito ya kazi ilikuwa kwenye mwili wake na hata buti lake ilikuwa hivyo lakini moja kati ya makosa ambayo waliyafanya ni kushindwa kumkagua mtu huyo kwenye mifuko yake kwa sababu walijua ni siku yake ya mwisho hivyo hawakuwa na huo umakini zaidi ya kutoa kifaa cha mawasiliano tu kwenye mwili wake.
Hiyo ndiyo simu ambayo ilikuwa kwenye mifuko ya Donny ndiyo James alikuwa anahitaji kuitumia ili kujua kama mwanaume huyo alikuwa wapi majira hayo ya usiku ili kama atakuwa hai awahi kuweza kumsaidia. Ilikuwa ni kama bahati nasibu tu kwa mdukuzi hatari sana huyo ambaye alikuwa anategemewa sana na kundi lake kwa hiyo kazi. Alikaa kwenye komputa hizo na kubonyeza kwa muda kidogo ambapo simu hiyo aliipata tena ikiwa hewani na location yake ilikuwa inasoma Ikulu.
Alisubiri kuona kama inaweza kupotea hapo na kweli baada ya muda aliona inaanza kusogea na kuonekana inatoka kabisa ndani ya hilo eneo. Mwanaume alisogea kwenye kabati moja na kutoa vidonge akiwa anayumba yumba kwa sababu bado mwili wake ulikuwa na maumivu makali sana. Vidonge alivyotumia vilikuwa ni hatari sana kwa uhai wa seli kwa sababu vilikuwa vinaupa mwili nguvu kwa lazima hivyo ilikuwa ni hatari kwa upande wa afya yake ila hakuwa na namna kazi ambayo ilikuwa mbele yake kuliokoa taifa ilikuwa ni mhimu sana kuliko hata maisha yake.
Baada ya kunywa dawa hizo alilia kama mtoto mdogo akiwa ameshika kichwa maana zilimletea maumivu makali sana na baada ya dakika tatu alitulia kwa dakika moja kisha akaamka akiwa sawa kabisa mwili ukiwa umelowa kwa jasho.
“Max wewe ndiye pekee ambaye unaweza kuja kulisaidia taifa hili tafadhali sana naomba usife, nakuja kwa ajili yako” aliongea kwa msisitizo sana akichukua nguo zake za kazi na bastola kwenye kiuno chake kisha akatoweka kwa gari ndani ya hilo eneo.
Simu hiyo ilikuwa inamuelekeza wapi pa kwenda kulingana na namna ilivyokuwa inahama, alitembea akiwa umbali kidogo baada ya kuziona gari ambazo zilionyesha kwamba ndimo simu hiyo ilimokuwemo. Hakuwa na uhakika kama simu hiyo alikuwa nayo bado Max ila hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake ya pekee kabisa maana hakuona tobo lingine la kuweza kufanya hivyo. Safari ya wanaume hao iliishia msituni ambapo hata yeye mwenyewe alisimama na kuligeuza gari lake na kulipenyeza ndani ya miti baada ya kuona watu hao wanamtoa mtu kwenye gari na kuanza kuelekea naye ndani msituni huku wengine wakiwa wameshika majembe na koleo kadhaa wakiwa na haraka sana mvua ikiwa inaendelea kushuka.
Mwanaume aliwafuatilia kwa umakini sana mpaka walipofika pale na kuanza kuchimba kaburi ambapo walichimba na kisha kwa muda mfupi mwanaume huyo alirushiwa ndani ya kaburi hilo na kuanza kufukiwa. James kwa hali ambayo alikuwa ameiona alikuwa amekata tamaa kabisa kwamba mtu huyo mpaka anazikwa maana yake ni kwamba alikuwa ameshauawa hivyo alikata kabisa tamaa lakini kuna kitu kimoja ambacho kilimshtua na kuhisi kwamba kuna kitu huenda hakikuwa sawa kabisa. Ni baada ya kumsikia Dax akiwa anamkumbushia mwanaume huyo kwamba sura yake ndicho kitu cha mwisho kabisa yeye kuweza kukiona kisha utafuata mchanga na giza halafu pumzi itaanza kukata na baada ya hapo utakufa vibaya sana.
Tambo za Dax ndizo ambazo zilimhakikishia kwamba mwanaume huyo alikuwa mzima bado ila huenda kuna kitu kibaya alifanyiwa. Hayo yote alikuwa anayashuhudia akiwa amejibanza sehemu kwenye mti mmoja mkubwa ambao ulikuwa na matawi mengi sana. Aliwashuhudia wanaume hao wakifukia kaburi hilo mpaka walipomaliza kisha Dax akalishindilia vizuri na kuanza kuondoka lakini kitu ambacho walikosea ni baada ya kuona vifaa vyao vina tope sana waliamua kuvitupia porini na kuvitelekeza huko huko.
James alikuwa makini sana kuwaangalia watu wale walivyokuwa wanatokomea mpaka kufika kwenye magari yao na kuanza kuondoka. Mwanaume alisogea hiyo sehemu akiwa na wasiwasi sana, alishika koleo moja na kuanza kufukua kwa kasi ya ajabu mno kwenye kaburi hilo ambalo lilimchukua muda mfupi sana kuweza kuukuta mwili wa mwanaume huyo wa kazi tena ukiwa kifua wazi kabisa. Alimtoa nje na kumgusa puani, mwanaume hakuwa akitoa pumzi yoyote ile, alimgusa kwenye moyo palikuwa kimya sana na mwisho akagusa shingo, hakuhisi kitu chochote kile kama mtu yule alikuwa hai.
“Hapana Max huwezi kufa kwa staili hii, hii nchi inakuhitaji sana” aliongea akiwa na wasiwasi sana, alimjazia pumzi sana kwenye mdomo lakini wapi hakuona chochote, alimbeba akiwa anakimbia na kuelekea alipokuwa amepaki gari yake kwa kasi mno kisha aliitoa hapo kama vile ana kichaa kuwahi kwenye makazi yake akaangalie kama anaweza kumsaidia mtu huyo maana nafsi yake ilikuwa inagoma kabisa kuamini kwamba mtu huyo alikuwa amekufa.
Akiwa anapita njiani kwa kasi alikutana na ule msafara wa akina Dax, wao hawakuwa wamemuona maana aliwapita kasi sana ila alifanikiwa kumuona mwanaume huyo kupitia dirishani akiwa anajipongeza kwa pombe kali, alimwangalia kwa hasira sana lakini hakuwa na cha kufanya muda huo ulikuwa ni wakati wa kujaribu bahati yake kama anaweza kumsaidia huyo mwanaume ambaye aliambiwa kwamba ndipo tumaini la nchi lilipokuwa.
Alifanikiwa kurudi nyumbani, ambapo yalikuwa ni makao makuu ya DRAGON BOYS na kumuweka Max kitandani akiwa bado ana tope kwenye mwili wake, alimsafisha vizuri kisha akajaribu kupampu moyo na mashine lakini hakuona chochote. Alijitahidi sana kumuwekea mpaka vifaa vya kupumulia lakini bado ilikuwa kama ni kazi bure na dalili za kuamini kwamba mtu huyo hakuwa hai na alikuwa amekufa zilikuwa zinaanza kuja hasa baada ya kumsafisha na kuona kwamba mwanaume huyo alikuwa na risasi za kutosha kwenye mwili wake.
James alisogea kwenye komputa yake na kuingia kwenye mtandao wa madaktari, alikuwa anahitaji kumpata daktari wa kukodisha kwa muda. Alitengeneza jina feki ili liweze kumsaidia kwenye kuaminina na akafanikiwa kumkuta daktari mmoja ambaye alikuwa anajulikana kama daktari hodari sana lakini alikuwa ni mtu mpenda rushwa sana kwenye huduma yake hiyo. Aliwasiliana naye na kumuahidi kiasi kikubwa sana cha pesa ila kikubwa yeye alikuwa anataka tu mtu wake aweze kupona na daktari huyo hakuwa na tatizo kikubwa ambacho yeye alikuwa anajali ni pesa kuingia kwenye akaunti yake tu.
Dakatri huyo alifika ndani ya dakika arobaini tu usiku huo huo wa manane maana dau ambalo aliwekewa mezani lilimfanya hata usingizi wake kuisha baada ya kupokea simu. Kukutana na James alimkuta mwanaume huyo akiwa na wasiwasi mkali sana hivyo akajua kabisa kwamba hapakuwa pema. Bila kuongea walipeana mikono na mwanaume huyo akamuongoza daktari huyo ambaye alikuwa anawaza pesa tu kwenye kichwa chake mpaka ndani ya chumba ambacho alikuwa amelazwa Max. alishtuka sana baada ya kuiona sura hiyo kwa sababu kila sehemu ya nchi zilikuwa zimesambazwa taarifa kwamba mwanaume huyo alikuwa ni gaidi na alikuwa amekufa, sasa ilikuwaje awe hapo na awe hai? Alihisi hakuwa salama.
“Huyu si gaidi?”
“Vyombo vya habari ndo vinasema hivyo”
“Unataka mimi nimtibu mtu aliye muua raisi wa nchi? Unataka mimi nimtibu mtu ambaye dunia nzima inajua kwamba ni msaliti kwa taifa lake? Unahisi kitanikuta nini watu wakijua kwamba mimi ndiye niliyaokoa maisha yake?”
“Hakuna atakaye jua kuhusu hili”
“Unajuaje kwamba itakuwa hivyo?”
“Kwa sababu hakuna namna ya wewe kuweza kuongea” kauli za James daktari alishindwa kabisa kuzielewa ila kama angezielewa huenda angetafuta mapema njia ya kuweza kuyaokoa maisha yake.
“Hata kama ni hivyo bado siwezi kumtibu mimi”
“Nakulipa bilioni moja kwa kazi ya usiku mmoja tu. Pesa ambayo huenda haujawahi kuishika mkononi hapo hapo na huenda hautakuja kuishika milele mpaka unakufa, wewe ni mtu smart sana dokta usitake kuikataa hii ofa ambayo ninaweza kumpatia daktari yeyote yule na akaja muda huu” dau lilikuwa ni kubwa mpaka yeye mwenyewe anavyotajiwa alishtuka sana maana hakutegemea huko, aliishia kuguna na kuiweka tai yake sawa huku akilitua begi lake la kazi mezani. Hiyo ilikuwa ni ishara ya kukubali kazi.
“Huyu mtu ni nani hasa kwako mpaka unaweka pesa nyingi sana kiasi hicho kwa ajili yake?”

60 inafika mwisho.
001. Apone aendelee kuokoa taifa
James anatia huruma
Sana
 
Back
Top Bottom