Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Mwandishi umetisha unapaswa kupewa tuzo ya noble prize kwa kuleta riwaya Kali sana za kijasusi bongo land
Hahahaha umenipa heshima kubwa sana ambayo sistahili mkuu ila niseme asante sana [emoji122]
 
Hivi GEREZA LA HAZWA naweza kuisoma wapi yotee? Maana nimeishia ukurasa wa sitini na sita kule Facebook, huku JF naona kuna vipande vinamiss, msaada please
Nicheki WhatsApp au kawaida kwa hii namba

0621567672
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

FINAL EPISODE..............
Lakini kwenye kulipigania taifa mwanaume huyo alimpoteza mkewe kipenzi huku akibakia na binti yake wa pekee ambaye ilikuwa kama zawadi bora sana kutoka kwa mkewe ambaye alikufa. Alitaka watu wakaandike vitabu kuhusu shujaa huyo, jina lake liwe alama ya uzalendo kwenye taifa la Tanzania na vijana wote wakaliishi milele iwe kama chachu ya alama bora ya taifa maana bila yeye taifa lilikuwa linaangamia kwa zaidi ya miaka miamoja ijayo wananchi wangezidi kuteseka kila siku lakini pia alisisitiza kwamba alikuwa na ombi moja kwa mtu huyo ambayo angelileta hadharani kama mtu huyo angekubali kulipokea.

Mkuu wa majeshi Steven Mwilonga alikutwa akiwa amejiua ofisini kwake akiwa ameacha barua ya kuomba msamaha kwa familia yake na watanzania kwa kushindwa kuwa mzalendo na kuamua kuwatumikia watu. Alikuwa anajutia sana jambo hilo hivyo hakuona sababu ya kuweza kuishi kwa kuchangia machufuko kwenye nchi yake mwenyewe.
Mwanasayansi ambaye alikuwa anatumiwa na Denis Kijazo aliitwa mbele ya vyombo vya habari na kuelezea namna alivyokuwa anatumika kuitengeneza sumu hiyo kali kwa miaka mingi sana ambayo alifanya kazi kwa lazima chini ya mtu huyo huku akifurahia sana kuweza kurudi tena kwa mara nyingine kuungana na familia yake na alilaani sana kile ambacho alikifanya huko ila hakuwa na namna kwa sababu alifanya ili kuweza kuilinda familia yake. Alichaguliwa kuwa mwanasayansi bora wa mwaka na aliahidi kutengeneza dawa madhubuti kwa ajili ya sumu hiyo ambayo ilikuwa imesambazwa tayari kwa watu wenye pesa ili kama kuna tatizo lingekuwa kutokea basi iwe rahisi kuweza kuwatibu watu.
Dawson Nduka, mwandishi wa vitabu alielezea mambo mengi sana kwa uchungu mkubwa, alielezea sababu ambayo ilimfanya kuishia kule kwa mtu yule na kutumika kuandaa makala ambazo zilikuwa zinamfanya Denis Kijazo aandikwe kama kiongozi bora sana. Mwanaume huyo alikuwa anajutia kufanya hayo ila alifanya kwa ajili ya familia yake ambayo mkewe alikuwa anamsaliti na moja ya mlinzi wa kutegemewa na Denis Kijazo huku akijua kabisa kwamba mtu huyo ndiye ambaye alileta matatizo kwenye familia yake.
Mtu huyo hakuishia hapo tu licha ya kutoka na mkewe ambaye aliishia kupata mimba bado alitoka na mtoto wake wa damu kitu ambacho kilifanya kuzaa nao wote wawili bila wao kujua kwamba walikuwa wanachanganywa na mwanaume mmoja hali ambayo ilimuumiza na kumfanya kuishi kwa maumivu makali sana kiasi kwamba alitamani hata kujiua ila aliamua kuishia kwa sababu ya watoto wake na alidai kwamba alishamsamehe mkewe na alikuwa tayari kuwalea watoto hao wote kama wake.
Aliomba msamaha kwa familia nzima ya mwandishi wa habari ambaye alimponza baada ya kuhitaji kumtumia kukitangaza kitabu chake ambacho kingeongea ukweli wote na kusema kwamba hakuna na maana mbaya bali alitaka kuwaumbua watu hao juu ya kile ambacho walikuwa wanakifanya nchini ila kwa bahati mbaya sana akaishia kwenye mikono ya watu hao kwa miaka mingi sana. Almshukuru sana Donald Daniel kwa kuweza kuwaokoa huko Arusha na kuwafanya wazione familia zao kwa mara nyingine tena.
Mwandishi huyo rasmi alikiachia kitabu chake cha MAITI INAYO ONGEA ambacho kiliandika udhalimu ambao ulikuwa unafanywa na kiongozi. Kilichukua tuzo ya kitabu bora duniani baada ya kutafsiriwa kwa lugha la Kiingereza na kumfanya kuwa mwandishi namba moja duniani kikiuza zaidi ya kopi biliona moja na kumfanya kuwa mwandishi wa vitabu tajiri zaidi ulimwenguni Dawson Nduka akipewa na tuzo ya heshima na umoja wa mataifa.
Mkewe alijiua kwa kujiona mwenye hatia sana kwa yale ambayo alioyafanya na binti yake alibakia na sonona kubwa sana kwenye moyo wake lakini mzee huyo alikubali kuwalea watoto wa Ted kama wake.
Mmiliki wa THE UNTOLD, Fabian the real ndiye alikuwa mwandishi wa habari maarufu zaidi duniani, huku video yake ikitazamwa mara bilioni saba kwenye mtandao wake kwa muda mfupi sana kitu ambacho kilimuingizia pesa nyingi sana na kumfanya kuwa tajiri mkubwa sana akiwa na umri mdogo. Alifanya mahojiano mengi sana na vyombo vikubwa duniani huku kila mtu akiwa anataka kujua ni kwa namna gani alikutana na shujaa bora duniani Donald Daniel mpaka akamwamini yeye na kumpatia ushahidi huo na zawadi ya kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho alisema hakupewa yeye tu bali kwa mashujaa wote ambao walipambana mwanaume huyo aliwapatia pesa hizo na kusaidia watu wengi sana wenye uhitaji nchini kote na Afrika kwa ujumla.
Gavana wa zamani Laurent Mande jina lake liliandikwa mbele ya benki kuu ya Tanzania kama heshima kwa kazi bora ambayo aliifanya baada ya taarifa kutoka kwamba alikuwepo ndani ya lile jengo la Morogoro na familia yake ilipewa maisha bora sana lakini sio yeye tu bali kwa mashujaa wote familia zao zilipewa maisha bora sana kuwaenzi watu wao kwa namna walivyo jitoa kulisaidia taifa lao.
Watu wote ambao walifahamika kwamba kwa namna moja walikuwa wanajihusisha na Denis Kijazo, wote walikamatwa na kufungwa hivyo nchi ilibaki safi kabisa. Kutokana na kufanya kazi iliyo tukuka mkurugenzi Chuki Steward aliapishwa kuwa raisi mpya wa Tanzania kwani watu waliona kwamba mwanamke huyo ndiye pekee alikuwa anaweza kuwapeleka nchi ya ahadi.
Baada ya kuapishwa na kuwa raisi alikutana na Max Ikulu wakiwa wameongozana na mwanae Naima.
"Donald sijajua ni kwa namna gani napaswa kukushukuru kwa hili, nchi inatakiwa kujivunia sana kuwa na mtu kama wewe"
"Sioni haja ya kunishukuru kwa sababu mimi nilitengenezwa kuwa hivi nadhani nilikuwa natimiza majukumu yangu kiongozi"
"Sijawahi kukutana na mtu mzalendo kama wewe, nasikia kwamba yaliyokuwa maeneo ya mke wako huko Sinza na salasala baada ya kuondoka baadae serikali ilikuja kujibinafsishia baada ya wafanyakazi kuripoti kwamba bosi wao amepotea na akaunti za benki zilizuiliwa"
"Yeah, ilichukua muda mrefu sana na aliondoka bila taarifa kwa sababu za usalama hivyo hakuwaaga wafanyakazi wake"
"Kila kitu kimerudi kwenye mikono yako na akaunti za benki zinafanya kazi nitakutumia taarifa zote nadhani ni mali sahihi kabisa kwa Naima"
"Nashukuru sana kwa hilo, itakuwa kumbukumbu bora sana ya mwanamke ambaye nilimpenda sana"
"Amekuachia zawadi ya mtoto huyo ndiye atakuwa furaha yako kwa sasa"
"Ni kweli, nadhani natakiwa kwenda kupumzika na mwanangu sasa"
"Justin umemsamehe?"
"Hapana, nimemchoma sindano ya sumu ambayo itayachukua maisha yake taratibu"
"Bora wameisha na kila kitu kinaisha ila nina ombi moja kwako Donald"
"Nakusikiliza mheshimiwa"
"Nafasi yangu ya kuwa raisi nahisi bado haijakamilika kabisa na niliwaahidi raia kwamba nina ombi kwako"
"Kwanini?"
"Najua kwa sasa utakuwa unapitia mengi sana ila nakuomba sana uwe mkurugenzi wa shirika letu la kijasusi"
"Hapana mheshimiwa, kwa sasa nataka nikapumzike na mwanangu, nataka mwanangu awe na muda wa kutosha na baba yake na isitoshe naenda mbali sana na Tanzania"
"Sio amri bali ni ombi langu, hata kama utaenda kupumzika kwa miaka miwili naweza kukupa hiyo ruhusa kisha utakaporudi utaendelea na majukumu" mwanaume alitabasamu na kumwangalia mwanae ambaye alikuwa anacheka na kumpa baba yake ishara ya tano kumaanisha kila kitu kilikuwa sawa japo Kiswahili hakuwa anaelewa sana maana alizaliwa Marekani na alikuwa akikisikia kidogo tu pale walipokuwa wanaongea wazazi wake.
"Nitafanya hivyo" Mwanaume alikubali ombi hilo ambapo walikumbatiana na mheshimiwa raisi kisha akaondoka eneo hilo akiwa na ulinzi wa kutosha. Safari yake iliishia nyumbani kwa komando James ambapo baada ya kuwakuta watu hao wakiwa wamerudi kwenye furaha yao aliaga na kuondoka kabisa Tanzania kuelekea ndani ya Malaysia katika jiji la KUALA LUMPUR.

MWISHO.











Naam, tulikuwa wote ndani ya simulizi hii ya kusisimua yenye visa na mikasa ya kutosha na sasa tunafika tamati na mimi naamua kutoka ndani ya chumba ambacho nilijifungia mwenzi mzima kuandaa andiko hili.
Niseme asante sana kwa kuwa pamoja na mimi mwanzo mpaka mwisho, panapo majaaliwa tutakutana ndani ya simulizi nyingine ambayo inafuata. Sio mzuri sana wa kuahidi ila tunaweza kukutana ndani ya simulizi ya GEREZA LA HAZWA CHAPTER 2.
Langu jina naitwa FEBIANI BABUYA, wao wanapenda kuniita BUX THE STORYTELLER. Nyuma ya kalamu nilikuwa ni mimi mwenyewe till next time.
Tchao.
asante sana mkuu na hongera sana kwa muda na nguvu zako nyingi kwenye hii story ya kusisimua, nimeumia sana mke wa max kufa ange enjoy maisha mapya na familia yake
 
Back
Top Bottom