Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

Sharobaro la jf

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
237
Reaction score
325
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : sharobaro la jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA KWANZA-01

"Mwizi mwizii mwiziii..", mayowe yalisikika, mayowe amabayo yalisambaa kwa kasi ya ajabu usiku ule, kitendo ambacho kilipelekea wanakijiji waliokuwa wamelala wakaamka ili kumkimbiza mwizi huyo ambaye alionekana kuwa kasi kukimbia kuokoa uhai wake. Mwizi huyo alifanikiwa kuruka vigingi mbali mbali, akakimbilia nje ya kijiji hicho akatokomea na kuwacha wanakijiji kwenye sintofahamu.

Wanakijiji hao wakajilaumu sana, kila mmoja alikuwa na hamu ya kumkata mwizi yule ili wamuadabishe. Lakini jambo hilo likawa limeenda kinyume na malengo yao. Mwizi aliwapotea.

Baada mwizi yule kuwapotea, wanakijiji waliamuwa kurudi majumbani mwao kulala. Kesho yake asubuhi palipo pambazuka mwenyekiti wa kijiji akamtaka mjumbe wake apige mbiyu kuitisha mkutano wa dharura. Dhumuni kuu la mkutano huo ni kujadili mustakabali wa matukio hayo ya wizi yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara. Wakati mbiyu hiyo ya mgambo inalia, upande wa pili alionekana kijana Zabroni akihesabu fedha alizoiba usiku wa jana. Lakini kabla hajafikia tamati, akasikia sauti ya mama yake akimuita chumbani kwake. Hivyo alisitisha kisha akatii wito. "Naam mama nipo hapa"

"Una nini mwanangu? " Aliuliza mama Zabroni huku akigeuka kwa tabu kumtazama kijana wake. Akakohoa mara tatu mfululizo, kikohozi chepesi. Punde akaendelea kusema "Zabro mwanangu, mama yako tayari nimesha jihakikishia umauti. Huna sababu ya kuendelea kuiba mali za watu ili kuokoa maisha yangu. Tafadhali nakuomba achana na shuguli hiyo, utakufa kingali kijana mwanangu. Sasa fanya kazi za kilimo ili upate fedha za matumizi ya kawaida kwani mama yako sio waleo wala wakesho.. "

"Sikia mbiyu imelia, na hii ni kutokana na tukio lililo tokea jana. Najua fika wewe ndio muhusika, hakuna mwizi mwingine hapa kijijini. Je, unajua kwenye huo mkutano watakuwekea agenda gani? Za mwizi ni arobaini Zabroni, hebu achana na kazi hiyo haufai baba yabgu " Aliongeza kusema mama Zabroni, maneno hayo aliyaongea kwa sauti ya chini iliyojaa hofu na simanzi nzito ndani yake kitendo ambacho kilimpelekea Zabroni kudosha machozi. Lakini yote kwa yote akakubaliana na matakwa ya mama yake ili apate kumlizisha kulingana na hali tete aliyonayo, kamwe hapendi kumuona mama yake akikereka.

"Sawa mama nimekuelewa " Alijibu Zabroni kisha akarudi chumbani kwake kuendelea na zoezi lake la kuhesabu fedha alizoiba usiku wa jana kwanye duka la tajiri kijijini hapo, almaarufu kwa jina Mr. Mashaka.

"Milioni moja na nusu? Aaah pesa nyingi sana hizi, mpambanaji haogopi masikini hachoki, nitaendelea kuiba mpaka nitimize pesa ya kumsafirisha mama akatibiwe Hospitali ya kimataifa" Alijisemea Zabroni mara baada kupata idadi kamili ya pesa alizoiba siku hiyo. Furaha isiyo kifani ikawatawala moyoni mwake, upesi akazikusanya akazihifadhi kwenye mfuko mkubwa wa nailoni kisha akazifukia kwenye shimo maalumu alilokuwa amesha liandaa. Alipomaliza zoezi hilo akatoka ndani, nje akakutana na uso kwa uso na baba yake. Mzee Mwanamalindi. Mzee huyo alikuwa amelowa umande asubuhi hiyo huku uso wake ukionyesha kujaa hofu fulani. "Baba kuna tatizo?.." Zabroni akamuuliza baba yake. Lakini mzee Mwanamalindi hakujibu, aliingia ndani, moja kwa moja mpaka chumbani kwake ambapo huko alimtazama mkewe kwa macho ya huruma, akajisonya sambamba na kuketi kando yake. Akashusha pumzi ndefu na kujiuliza" Nimemkosea nini Mungu? Mbona matatizo hayakauki? Maisha haya nitaishi mpaka lini?.. " Maswali hayo aliyojiuliza mzee Mwanamalindi yaliambatana na machozi mepesi huku kinywa chake nacho kisikauke kujisonya. Kitendo hicho kikamstua mkewe. Mama Zabroni, ambapo aligeuka na kumuuliza mumewe kipi kinacho msibu.

"Loh! mke wangu nahisi kama dunia imenitenga, kila ninalo lifanya haliendi sawa kabisa mpaka muda mwingine najikuta namkufuru Mungu kwa kunileta duniani" Alisema mzee Mwanamalindi.

"Unaamaana gani?.." Akiwa na taharuki alihoji kwa mara nyingine mama Zabroni lakini kabla mumewe hajamjibu, ghafla nje ya nyumba yake ikasikika sauti ya amtu akabisha hodi.

"Subiri nikamsikilize kwanza huyu mtu, nakuja sasa hivi" Alisema mzee Mwanamalindi kisha akatii wito. Hofu na woga ulimjaa baada kufika nje kwani alimkamkuta mzee Fungafunga mdeni wake.

"Habari yako bwana Mwanamalindi" Fungafunga alimsalimu mzee mwenzake. Kwa woga na hofu mzee huyo akainamisha uso wake chini, papo hapo swali likamjia kichwani "Nitamueleza nini leo? Muda nilio muahidi kumlipa pesa zake umewadiwa?.." Alipokwisha kujiuliza swali hilo akaitikia salamu ile "Ni salama tu ingawa sio sana"

"Kwanini? Bado mkewe hali tete?.."

"Ndio bwana hata hivyo nafikiria kukopa pesa nyingine kwa mzee Malila ili niweze kumsafirisha kwenda mbali kidogo na hapa. Nimeambiwa kuna mtaalamu mmoja hivi anaweza kunisaidia "

"Sawa lakini yote kwa yote leo nataka pesa yangu, na sio ngonjera tena.." Alisema mzee Fungafunga huku akiwa amekasirika pasipo mfano.
Mwanamalindi akastuka kumuona mzee mwenzake akiwa katika hali hiyo, moyoni akajua siku hiyo mzee Fungafunga amekuja tofauti kabisa. Hivyo akajikuta hajui lipi la kufanya kwa sababu pesa ndani hakuwa nazo nawala hakujua kama usiku wa jana kijana wake kaiba pesa nyingi ambazo anaweza kulipa deni hilo na nyingine zikabaki.

"Mzee mwenzangu bado sijapata pesa yako, nimekwama tafadhali njoo kesho basi uhakika upo! Nipo chini ya miguu yako tafadhali " Alijitetea kwa mara nyingine tena mzee Mwanamalindi na wala hakuwa mzito kumpigia magoti mzee Fungafunga ili kudhihilisha kile anacho kisema. Lakini huyo katu hakutaka kuelewa propganda za mzee Mwanamalindi, akacheka kwa sarau sambamba na kuchomoa kibiriti ndani ya mfuko wa koti lake, akachomoa na sigara na kuipachika katika kinywa chake. "Sikia we masikini, ulikuja kwa mikono miwili kuomba msaada lakini malipo unasumbua kulipa. Umenizungusha mara ngapi? Au huna nia ya kuilipa?.." Akafyatua njiti akaiwasha sigara yake kisha akaendelea kusema "Mzee Mwanamalindi, hakuna asiye kuwa na matatizo. Sasa basi nakupa dakika tano tu, unipe pesa zangu la sivyo nachoma kibanda chako" Akamaliza kwa kicheko cha madaha sambamba na kupuruza moshi wa sigara mara mbili mfululizo.

Maneno hayo yalimstua mzee Mwanamalindi, kwa hofu akashusha pumzi ndefu huku akitafakari kipi cha kufanya sababu pesa hakuwa nayo muda huo, hali ya mzee Fungafunga alisimama kidete kutaka pesa zake.

"Nimekuelewa mzee mwenzangu, ngoja nikuletee" Alisema mzee Mwanamalindi na kisha kuingia ndani huku akiwa mnyonge mithili ya kifaranga kilicho nyeshewa na mvua. Moyoni mzee huyo alipania kuchukuwa uamuzi mgumu, kwani aliona dunia imemtenga. Akaingia chumbani kwa Zabroni akakata kamba aliyokuwa akitundikia nguo kijana wake kisha akajinyonga, mbali na kujiona kama dunia imemtenga, lakini pia mzee huyo aliona hana mbinu nyingine ya kujinusuru mbele ya mzee Fungafunga. Mzee asiye na masihara hata chembe pindi anapo dai chake.

Muda ulisonga mzee Fungafunga akimsubiri mzee Mwanamalindi amletee pesa yake. Baada kukatika takribani nusu saa, mzee huyo akaingiwa na imani haba. Moyoni akadhania kwamba mzee huyo kamtoroka kupitia mlango wa uwani na hivyo aliamuwa kuchoma nyumba moto ikiwa ndani yumo mzee Mwanamalindi ambaye tayari marehemu pamoja na mkewe ambaye ni mgonjwa asiye jiweza. Hali hiyo tata ilimpelekea mama huyo kushindwa kupiga mayowe kabisa, na hivyo ajali ya moto ikakatisha uhai wake.

"Jasho la mtu siku zote haliliwi" Akaanza kwa kicheko, mzee Fungafunga alisema maneno hayo kisha akaondoka mahali hapo huku nyuma akiacha moto ukitambaa kwenye nyumba kwa kasi ya ajabu. Punde baada mzee huyo kutokomea, kijana Zabroni naye alikuwa njiani akirudi nyumbani baada kutoka kijiweni kusikilizia watu wanazungumziaje wizi uliofanyika usiku wa ikiwa mwizi ni yeye mwenyewe.

Je, Zabroni atakuwa katika hali gani? KWA msiba huo??
Itaendelea
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi :Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA PILI-02

Moshi mzito ulioambatana na kipupwe cha aina yake ulipaa angani kwa kasi ya hali ya juu ikiwa muda huo kijana Zabroni naye akizidi kuzipiga hatua kurudi nyumbani hata asijue kipi kinacho endelea.

Nyumba ilizidi kupamba moto, punde Zabroni akastuka kuona moshi mkali mweusi ukitanda angani, hofu zaidi ikamjaa baada kugundua moshi ule ukitokea nyumbani kwao. Upesi akatimua mbio ili ajue kipi kinachoendelea. Alipofika, hakuamini kile alicho kiona, alipigwa na butwaa baada kukuta moto ukiishia huku fito zilizoungua nazo zikidondoka chini. Alipagawa, alipasa sauti kumuita mama yake na baba yake lakini harufu ya miili ya wazazi wake iliyoungua ilimfanya Zabroni kuamini kuwa mama yake kaungulia ndani kwani alijua fika kwa hali aliyokuwa nayo mama yake kamwe asingeweza kujinasua kwenye moto huo.

Alilia kwa uchungu, akajiuliza wapi alipo baba yake? Wakati anajiuliza swali hilo miguu yake ilionyesha kukosa nguvu, usongo wa mawazo wa kifo hicho cha mama yake ulimfanya apoteze fahamu bila kutambua kuwa si mama yake tu aliyefariki bali na baba yake pia.

Wakati tukio hilo la Zabroni kupoteza fahamu linatokea, ghafla alionekana mzee Maboso akitokea shamba. Mzee huyo ni jirani wa marehemu mzee Mwanamalindi. Alistushwa na kile alicho kiona, Maboso akastaajabu sana kuona nyumba ya mzee mwenzake ikiwa imeteketea kwa moto lakini pia akapigwa na bumbuwazi baada kusikia harufu ya kuungua kwa mwili, haraka sana akatupa jembe na panga chini akasogea jirani zaidi ili aangalie kama kapona mtu hasa hasa mama yake Zabroni ambaye alifahamu fika mama huyo hajiwezi. Lakini kabla hajasogea zaidi akamuona Zabroni chini akiwa amepoteza fahamu.

"Hili ni zaidi ya balaa" Ndani ya nafsi yake akajisemea sambamba na kusitisha safari yake ya kwenda kujua kama kuna mtu kapona kwenye ajali hiyo ya moto.

"Zabroni Zabroni.. Amka Zabroni. Kwani kuna nini kimetokea?.." Huku akimtikisa Zabroni, mzee huyo alipasa sauti kusema maneno hayo, lakini muda huo huo akagundua kuwa Zabroni amepoteza fahamu. Hakika Maboso akazidi kuchachawa, kijasho chembamba kikiuvagaa mweli wake, akashusha pumzi ndefu wakati huo akaendelea kuzipiga hatua za pole pole mpaka mahali ilipo teketea nyumba.
Akasikitika sana baada kuona mwili wa mama Zabroni ukiwa umeungua, alipo tazama upande wa pili akauona mwili wa mzee Mwanamalindi nao ukiwa hivyo hivyo umeteketea. Akasihisi mwili kusisimka, ni kama wazimu ulitaka kumpanda mara baada kushuhudia vifo hivyo vibaya vilivyo wapata jarani zake. Huku akiwa haamini kile kilicho tokea akatazama kulia na kushoto, ghafla akapata wazo, akatimua mbio za kizee kuelekea kwa Mwenyekiti wa kijiji kutoa taarifa juu ya maafa hayo.

Alipofika hakumkuta Mwenyekiti ila alimkuta mkewe naye alikuwa akijiandaa kwenda kisimani. Mkewe Mwenyekiti alipomuona mzee Maboso akimjia hima hima alisimama, kwa mshangao akamuuliza "Vipi kwema huko?.."

"Hapana sio kwema Siwema" Alijibu mzee Maboso huku akihema haraka haraka.

"Mmh inamaana jina la mwanangu hulijui mpaka unitaje jina langu? Hebu tengua kauli yako halafu ueleze kinacho kusibu"

"Sawa, samahani sana. Yote kwa yote Mwenyekiti nimemkuta?.."

"Hapana kaenda kukagua mashamba yake ila muda sio mrefu atarudi, siunajua leo kuna kikao? Kulikoni mzee Maboso? "

"La! Hili ni balaa asikwambie mtu mzee Mwanamalindi na mkewe wamefariki kwa ajari ya moto"

"Mungu wangu weee! Imekuwaje sasa jamani!?.." Mke wa mwenyekiti aliuliza huku akisikitika. Mzee Maboso akaishusha pumzi yake kisha akajibu.

"Doh we acha tu! Ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni. Zabroni naye amepoteza fahamu yani hata sijui ni kitu gani kimepita kwenye familia ile"

"Sawa acha mimi nikamwambie mjumbe apige mbiyu ya msiba ", Aliongeza kusema mzee Maboso na mara moja akaelekea kwa mjumbe kumpa taarifa.
Alimkuta mjumbe akitengeneza baiskeli yake, baada ya salamu akamueleza kila kitu kilichojili kijijini hivyo punde. Mjumbe alimtazama mzee Maboso kwa jicho la husda kisha akasema. "Kwahiyo nikishatoa taarifa wewe utafaidika nini?.."

"Unamaana gani sasa? Mbona sikuelewi!.."Akistushwa na maneno hayo makali aliyoyasema mjumbe, mzee Maboso alimuuliza. Lakini mjumbe hakujibu zaidi aliacha zoezi lake la kutengeneza baiskeli akaingia ndani. Punde akatoka na mbiyu mkononi mwake, akaitupa mbele ya mzee Maboso kisha akasema
"Mbiyu hiyo hapo tangaza mwenyewe, toka zamani mimi na mzee Mwanamalindi ni maadai kwahiyo siwezi kupoteza muda wangu mimi. Kwani hata nikitoa taarifa atapona? "

"Afe tu, hana faida yoyote hapa kijijini. Wamekufa manabii sembuse yeye" Mjumbe aliongeza kusema aliongea kwa hasira punde akaendelea na kazi yake ya kutengeneza baiskeli hata asijali msiba huo mzito. Mzee Maboso akaona hakuna haja ya kumbembeleza akaondoka zake. Ila kabla hajafika mbali,mara ghafla nyumbani kwa mjumbe akaja mzee Fungafunga. Mzee huyo akacheka sana kisha akasema "Mzee mwenzangu wewe ni mwanaume na unamsimamo wa kiume"

"Kwanini bwana" Alihoji mjumbe.

"Kukataa kupiga mbiyu hapo upo sawa kabisa, Mwanamalindi hafai abadani "Alijibu Fungafunga, maneno hayo aliyaongea kwa furaha kubwa sana. Mjumbe akafurahi sana kupata ujiko kwa mzee Fungafunga na wala asijue kwamba Fungafunga ndio muhusika mkuu wa tukio la mauaji ya mzee Mwanamalindi pamoja na mkewe.

Kikao cha viongozi wa kijiji ulifanyika siku hiyo, waliopata taarifa ya msiba huo walifika na ambao hawakupata hawakufika. Mazishi yalifanywa na wanakijiji wachache sana siku hiyo, hakuna aliyekuwa na taarifa harisi kuhusu msiba huo, lakini pia mjumbe wala mwenyekiti hawakufika msibani Jambo hilo lilimuumiza sana mzee Maboso akajiaminisha kuwa huwenda vifo hivyo ukawepo mkono wa mtu. Wakati mzee Maboso akiwaza suala hilo upande wa Zabro naye aliamini kama vile ambavyo mzee Maboso alivyokuwa akiamini.

Baada ya msiba, mzee Maboso akamtaka Zabroni aishi nyumbani kwake, lilikuwa pigo baya sana katika maisha yake. Jambo hilo liliweza kumfanya asitishe zoezi la kuendelea kuiba, kwani aliyekuwa akimfanya aibe ameshapoteza maisha. Lakini licha ya kuamuwa kuacha zoezi hilo, ndani ya moyo wake kuna kitu alipania kukifanya mbadala. Roho ilimuuma sana, aliona hatolizika endapo kama kitu hicho hatokitekeleza.
"Wazazi wangu wamekufa kikatili sana, hivyo nitahakikisha kila siku iendayo kwa Mungu nyumba moja inateketea kwa moto mpaka kijiji chote kiwe jangwa" Aliweka nadhiri kijana, maneno hayo alijisemea kwa uchungu ndani ya nafsi, chozi halikusita kutiririka kunako mboni za macho yake. Akaona uamuzi wa kuchoma nyumba kila siku iendayo kwa Mungu ni uamuzi mzuri na sahihi pia.

Uamuzi huo hakutaka kuufanya pasipo kumshirikisha mzee Maboso ambaye upande wake alimchukulia kama ndugu, mzee huyo naye alipo sikia nadhiri hiyo akamsifu sana kwa kuamua kuchukuwa uamuzi wa kiume. Akaachia tabasamu bashasha kisha akasema "Safi Zabroni, upo sahihi. Samaki mmoja akioza, wote wameoza. Ukweli nina mashaka na uongozi wa juu kwenye kijiji hiki hususani juu ya suala hili la kuwaawa kwa wazazi wako. Mimi nipo nyuma yako kijana wangu. Kesho nitakupa mzizi utautafuna, ni dawa ambayo itakufanya upotee katika mazingira yoyote pindi utakapo nuia maneno ambayo nitakwambia hapo kesho. Natamani lengo lako litatimia Zabroni. Na hakika Mbuyuni yote inageuka jangwa" Zabro akatabasamu, tabasamu ambalo lilionekana usoni mwake kupitia mwanga hafifu wa koroboi (Kibatali) bada tabasamu hilo akajibu. "Nitakushuru sana mzee wangu, na mimi sitikuangusha nitachoma nyumba moja baada ya nyingine usiku usio julikana. Vile vile mtu yoyote yule atakaye jaribu kunifuatilia, kichwa chake kitakuwa halali yangu"

"Naam Zabroni! Jasiri haogopi " Aliunga mkono mzee Maboso kisha akamtaka Zabroni atie unga kwenye maji waliyoinjika jikoni, wasonge ugali wale ili kesho wagange yajayo.

Itaendelea.

UPELE UMEPATA MKUNAJ.. BALAA LINATARAJI KUZUKA,
Usikose sehemu ya 03
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA TATU-03

Palipo pambazuka,mzee Maboso ndio alikuwa wa kwanza kuamka ambapo kabla ya yote alitoka nje kujisaidia kisha akarudi ndani na kisha akamuamsha Zabroni "Mimi naenda kukagua mitego yangu nikirudi tupukuchue mahindi ili twende nashineni sionaona unga umetuishia?.." Mara baada Zabroni kuamka, mzee Maboso akamwambia maneno hayo.

"Usijali hii kazi niachie mimi,wewe nenda kaangalie mitego yako babu " Alijibu Zabroni sambamba na kukurupuka kutoka kitandani.

Mzee Maboso akichukuwa panga na mkuki akaelekea porini kukagua mitego yake wakati huo huo Zabroni aliamka akanawa uso na kisha akaingia kwenye ghala kuchukuwa mahindi. Lakini kabla hajaanza kuyapukuchua, akafika mpenzi wake aitwaye Tina. Wawili hao ni wapenzi wa siku nyingi sana, siku hiyo Tina alienda kumuona Zabroni baada kuona muda mrefu hajaonana naye na wala hana taarifa naye.

Alifurahi sana kumuona mpenzi wake kwa mara nyingine, alizipiga hatua za kunyata ilihali Zabroni naye akionekana kuandaa mahali pakupukuchulia mahindi, ghafla akajikuta akizibwa macho na mtu ambaye hamkujua, lakini punde Tina akatoa viganja vyake kwenye macho ya Zabroni kisha akaangua kicheko.

Zabroni akatabasamu kidogo na kusema "Habari za siku Tina"

"Safi Zabro, kwanza pole na matatizo. Lakini pia naomba unisamehe kwa kutokufika msibani. Wazazi walinikataza kufika mpenzi wangu" Aliongea Tina kwa sauti ya chini huku akimtazama Zabroni kwa haibu.

"Huna sababu ya kuniomba msamaha Tina,hayo ni mambo ya kawaida sana kwahiyo furahi kunikuta mzima" Alijibu Zabroni, maneno hayo aliyaongea kwa sauti yenye simanzi nzito ndani yake. Mara baada kusema hayo wawili hao waliketi chini wakaanza kazi ya kupukuchua mahindi huku wakipiga zogo la aina yake. Wapenzi hao walitaniana wakacheka sambamba na kupanga mikakati kabambe juu ya penzi lao ambalo lilizidi kukomaa mizizi kila kukicha.

Lakini wakati hayo yanajili, upande wa pili nyumbani kwa Mwenyekiti alifika mzee Fungafunga. Fungafunga alionekana anamazungumzo na mwenyekiti siku hiyo ,kwa maana hiyo ilimbidi Mwenyekiti aache kazi aliyokuwa akiifanya muda huo na kisha kumpa sikio lake mzee mwenzake. Alikuwa akitengeza mipini ya jembe, sasa akamsikiliza mzee huyo ana jambo gani anataka kumwambia. Mzee Fungafunga akapewa kigoda akakaa, akakohoa kidogo kisha kusema

"Naona kajua kanawaka"

"Mmh kiangazi hii bwana, kulikoni mbona leo hujaenda shamba"

"Nilikuwa namaongezi juu yako,ndio maana siku hii nimeamua iwe kwa ajili yako" Alijibu mzee Fungafunga.

"Mmh sawa nakusikiliza"

"Kabla sijaingia kwenye jambo lanyewe hivi mipini huwa unatengeneza kwa shilingi ngapi?.."

"Aah bei poa tu kwa wewe elfu tatu tu"

"Anhaa. Sawa. Jambo lanyewe sasa ni kuhusu huyu kijana huyuuu.. Zabroni "

"Huyu mtoto wa marehemu mzee Mwanamalindi? .."

"Huyo huyo, ujue tangu wazee wake wafariki tabia ya wizi imetoweka hapa kijijini"

"Kwa maana hiyo wanataka kusema yeye ndio alikuwa mwizi?". Fungafunga alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Ndio maana yake! Au unaonaje?.."

Jibu hilo la mzee Fungafunga, likamfanya Mwenyekiti naye akakaa kimya muda mfupi halafu akasema "Bila shaka naweza kuungana na wewe, sasa unanishauri nini?.."

"Mimi sina cha kukushauri ila nataka nikuulize swali! Vipi ukimfahamu muhusika wa tukio la kuchoma moto nyumba ya mzee Mwanamaalindi? .." Mwenyekiti akashusha pumzi kwanza, akakohoa kisha akajibu "Kwa jinsi yule mzee nilivyokuwa simpendi, kiukweli nitampatia zawadi huyo muhusika. Unajua yule mzee tangu kipindi kile aninyime baiskeli yake nilimchukia sana na ndio maana hata msibani sikwenda, sio mimi hata barozi wangu naye hakwenda sijui wewe mwenzangu " Fungafunga aliposikia maneno hayo ya Mwenyekiti alicheka sana, alipo katisha cheko lake akajibu "Wala sikwenda, kwanza mimi ndio muhusika wa tukio lile. Ukweli mzee yule nilimuazima pesa kwa niaba ya matibabu ya mkewe lakini wakati wa malipo akaanza kunizungusha. Sikuwa na sababu nyingine mimi"

"Ulisikia wapi jasho la mtu linaliwa?" Akaongeza kusema mzee Fungafunga mara baada kuweka wazi kuwa yeye ndio muhusika mkuu wa tukio lile alilofanya.

Mwenyekiti alipigwa na butwaa kwa muda lakini mwishowe akarudi katika hali yake wakati huo huo mzee Fungafunga akaangua kicheko sambamba na kusema "Nipe zawadi yangu sasa"

"Baadaye tukutane kwa mama Ziada kuna gongo pale njoo tuburudike mzee mwenzangu kwani umekuwa shujaa wa kijiji chetu" Alijibu Mwenyekiti, mzee Fungafunga akafurahi baada ya hayo akaaga na kuondoka zake hujuy nyuma akimuacha Mwenyekiti akilitafakari tukio lile akijiuliza kwanini baada wazazi wa Zabroni kuuwawa matukio wizi yametoweka kijijini hapo.

Kwingineko Zabroni na mpenzi wake walikuwa wakiendelea kupukuchua mahindi wakati huo wakipiga zogo la hapa na pale. Baada kumaliza Tina aliaga kuwa anarudi nyumbani,Zabroni akamsindikiza lakini walipokuwa Zabroni akamwambia Tina jambo ambalo lilimstua.

"Tina najua ipo siku mimi nitafungwa jela"

"Kwanini unasema hivyo?" Alihoji Tina kwa taharuki. Zabroni akashusha pumzi ndefu kwanza kisha akajibu "Kwa sababu nahitaji kulipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wangu"

"Kisasi sio kizuri mpenzi wangu, kwanini usimuachie Mungu?"

"Unajua Zabroni mimi nimeshakuzoea, istoshe nakupenda sana. Je, unafikiri ukifungwa mimi nitakuwa katika hali gani? Hebu muachie Mungu ndio ataweza kukulipia" Aliongeza kusema Tina.

"Dawa ya moto ni moto, acha nilipe kisasi Tina? Lakini pia..." Kabla Zabroni hajaendelea kusema,mara ghafla mzee Fungafunga akatokea. Tina alipo muona baba yake aliogopa, mara moja akatimua mbio wakati huo huo Zabroni naye aligeuka kurudi nyumbani ila njiani alikutana uso kwa uso na mzee huyo.

Fungafunga akamtazama Zabroni kwa jicho ngebe kisha akasema "Sitaki mazoea na mwanamgu mwana haramu wewe"

"Ukiendelea, tutaonana wabaya" Aliongeza kusema kwa msisitizo mzee huyo. Lakini Zabroni hakujibu neno lolote, alimtazama tu kisha akaishia zake. Lake rohoni juu ya nadhiri aliyojiwekea kuhusu nyumba za kijiji hicho. Kamwe hakuamini kama anaweza tokea mtu yoyote anayeweza kubadilisha dhamira yake.

"Kisasi lazima" Moyoni akajisemea maneno hayo huku akiendelea na safari yake ya kurudi nyumbani.

Usiku ulipo fika, mzee Maboso alimkumbusha Zabroni kuhusu mzizi ambao utamfanya apotee mahali popote pindi atakapo nuia na kisha kugusa kitu chochote.

"Hapa kila kitu kitakuwa sawa kijana wangu", Aliongea mzee Maboso huku akiutoa mzizi huo kwenye kitambaa alichotumia kuhifadhia. Akaketi kwenye kigoda, akamtazama Zabroni kwenye mwanga hafifu wa kibatali, akaendelea kumueleza uwezo wa mzizi huo na maneno anayotakiwa kuyaongea pindi atakapo hitaji kupotea kwenye mazingira husika.

"Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nikishaongea maneno hayo halafu nikagusa kitu chochote iwe nyasi au ukuta napotea?.." Aliuliza Zabroni kwa umakini zaidi.

"Naam! Hii dawa sio ya mchezo" Alijibu mzee Maboso kisha akamkabidhi. Zabroni akaupokea mzizi huo, akautafuna. Alionekana kukunja uso wake, kwa namna gani mzizi huo ulivyokuwa mchungu. Baada kukamilika suala hilo, sasa akahitaji kufanya jaribio usiku huo huo ili awe na uhakika kabla hajaanza kazi rasmi ya kukibadilisha kijiji kuwa Jangwa.

Kwenye jaribio hilo, alichoma moto nyumba tano usiku wa siku hiyo. katika nyumba hizo hakubahatika kupona mtu hata mmoja. Kesho yake asubuhi, kijiji kikakubwa na majonzi ya msiba mkubwa kuwahi kutokea, jambo ambalo lilipelekea wanakijiji kumnyooshea kidole Mwenyekiti ikiwa wakati huo Mwenyekiti naye akimtilia shaka mzee Fungafunga kuhusu tukio hilo tata alilozua kijana Zabroni katia jaribio lake.

Itaendelea..

Balaa kijiji, USIKOSE MUENDELEZO.. Lakini pia unaweza kumaliza uhondo kwa kulipia vipande vyote shilingi 2,500/= tu
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : sharobaro la jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA NNE-04

Mwenyekiti wa kijiji alimuhisi muhusika wa tukio hilo huwenda akawa ni mzee Fungafunga kwa maana jana alimwambia kuwa yeye ndio aliyehusika kuchoma nyumba ya mzee Ndalo,sasa hatimaye tukio hilo hilo limejitokeza tena. Istoshe limesababisha maafa mkubwa sababu ndani ya hizo nyumba tano zilizochomwa moto hakufanikiwa kutoka mtu hata mmoja,kitu ambacho kiliwasikitisha walio wengi ni familia ile iliyokuwa na watoto Saba pamoja na wazazi wao wawili. Familia yote ikawa imekufa kwa pamoja,huzuni kila pande ya kijiji wakati huo huo mzee Fungafunga akijiuliza "Nitaificha wapi sura yangu mimi mbele ya mwenyekiti? Sijui kwanini nilimwambia jambo lile",alijiuliza mzee Fungafunga huku akionekana kujilaumu jambo lile kumuelezea mwenyekiti ilimradi tu apate ujiko. Katika umati wa watu uliokusanyika katika nyumba ile ya familia saba,mwenyekiti akamtazama mzee Fungafunga kisha akamuita faragha. Mzee Fungafunga akionekana kuwa na hofu alitii wito wa Mwnyekiti.
"Mzee mwenzangu, nini sasa umefanya?" Mwnyekiti akamuuliza Fungafunga huku akionekana uso wake kana kwamba anataka kudondosha machozi,wakati huo huo mzee Fungafunga akashusha pumzi na kisha akajibu "Walaa sio mimi ndugu mwenyekiti, unafikiri kwa utu wangu huu naweza kufanya maafa kama haya? Hapana siwezi mwenyekiti labda tufanye uchunguzi atajulikana tu muhusika" alijibu mzee Fungafunga macho akiwa ameyatoa mfano wa chura aliyebanwa na mlango. Baada ya maelezo hayo mwenyekiti akajikuta akishindwa cha kuongeza kusema zaidi aliyafuta machozi yake yatokanayo na uchungu wa kupoteza baadhi ya wanakijiji wake, maana hali kijiji hapo ilionekana kutisha sana.
Wakati hayo yanaendelea, upande wa pili mzee Maboso na Zabroni walikuwa wakielekea shambani. Walipo kuwa njiani mzee Maboso akamwambia Zabroni "Nadhani umeona hiyo dawa ilivyokuwa noma"
"Dah! wewe acha tu,kwanza nilipofika kwenye nyumba ya kwanza nilichoma kumbe kwa mbali kuna mtu alikuwa anakuja maeneo hayo,bila shaka yule alikuwa mlevi maana usiku wote ule sio wa kutembea tembea hovyo. Basi bwana baada kumuona nikasema hapa haonwi mtu haraka sana nilinuia yale maneno halafu nikagusa ukuta wa nyumba hiyo hiyo nikawa nimepotea " Zabroni akacheka kwanza kisha akaendelea kusema "Nikasema kweli hii dawa ni moto wa kuetea mbali,na kwakuwa ni moto wa kuotea mbali? Hakuna budi kukamilisha methali ile isemayo dawa ya moto ni moto"
"Naam upo sahihi Zabroni", aliunga mkono mzee Maboso na kisha wakagongena mikono wakacheka sana na zogo nyinginezo zikaendelea. Walifika shambani wakafanya shughuli zao mpaka mida ya saa nane mchana waliweza kurejea nyumbani kwao ambapo wakati walipofika tu nyumbani akaja mzee Adenel, mzee huyo alionekana anajambo moyoni mwake lakini pia mzee huyo hana uenyeji na kijiji hicho bila shaka alikuwa mgeni ingawa mzee Maboso alimfahamu fika na ndio maana alipomuona alionyesha kutabasamu.
"Karibu sana wanyumbani",alisema mzee Maboso huku akimlaki mgeni wake. "Nimeshakaribia,habari za siku nyingi ", alijibu mzee Adenel, mzee Maboso akaitikia "Salama sana ngoja nikachukue kigoda ili tukae tuongee zaidi ", baada kusema hayo mzee Maboso alizama ndani akachukuwa kigoda kisha akatoka nacho nje. "Enhe nipe habari hivi ni wewe kweli?..", alihoji mzee Maboso akionekana kutoyaamini macho yake lakini mzee Adenel akamjibu "Ndio ni mimi ujue miaka mingi sana nimekuacha hapa naona sasa tayari umekuwa mwenyeji wa Tanzania. Mmh sasa habari ni kwamba unatakiwa kurudi nyumbani. Familia inakuhitaji kwa vyovyote vile", aliongea mzee Adenel akimtaka Maboso arudi nyumbani kwao nchini Nigeria,mzee huyo alikuwa kiutafutaji kijijini hapo na hivyo mtafutaji ambaye alikuwa naye miaka ya nyuma kabla hajarudi nchini kwao leo hii kaja kumchukuwa. Hakika mzee Maboso alionekana kupoa huku sana mithiri ya maji ya mtungini, akawaza "Miaka mingi nipo nchi ya watu kiutafutaji sasa leo hii nirudi nyumbani sina kitu? Hakuna kilicho badirika Je, haibu yangu nitaificha wapi mimi?", aliwaza mzee Maboso kitendo kilicho pelekea ukimya kidogo kutawala lakini mwishowe kimya hicho kilitoweka baada mzee Adenel kumuuliza kwa lugha ya kikwao "Unawaza nini?"
"Hapana ila najiuliza nauli nitatoa wapi?.." alijibu mzee Maboso naye vile vile alijibu kwa lugha yao.
"Usijali kila kitu kipo cha muhimu wewe jiandae kesho turudi nyumbani"
"Sawa"
"Lakini mbona kuna mahala nimepita nimekuta watu wanaomboleza kulikoni kuna msiba?.." aliongeza Adenel. Mzee Maboso akamjibu "Ndio"
"Sasa kwanini hamjahudhulia",kabla mzee Maboso hajajibu,Zabroni alileta chakula maongezi hayo kuhusu misiba yakawa yamekomea hapo.
Usiku ulipoingia kesho yake ikiwa ndio safari ya mzee Maboso kurudi Nigeria, aliamwambia Zabroni kuhusu ujio na dhumuni la mzee Adenel. Zabroni aliumia sana kwani aliamini swahiba wake kuonana naye tena ni majaliwa hivyo alijiuliza amlipe nini? Ndipo akakumbuka kuwa alifukia fedha aridhini,fedha alizoiba zamani kwenye moja ya maduka kijijini hapo! Fedha hizo aliiba kwa kudhumuni ya kwenda kumtibia mama yake nje ya nchi, ndoto ambayo ilitoweka mithiri ya mshumaa uzimikapo unapokubwa na upepo. Haraka sana alikwenda kuzifukua kwa kuangalia ramani kilipokuwepo chumba chake, alifanikiwa kupaona. Aliachia tabasamu na kisha mara moja akaanza kuzifukua. Zoezi hilo lilikamlika, fedha zilikuwa kwenye mfuko wa gunia. Kwa mara nyingine tena akaachia tabasamu, akaona fedha hizo ni fadhila tosha kwa mzee Maboso aliyeamua kumuunga mkono juu ya hatua ya kulipa kisasi aliyochukuwa. Ni fedha nyingi mno.

Kesho palipokucha saa kumi na mbili safari ilianza,Zabroni akaambatana na wazee hao kuwasindikiza mpaka stendi ya magari yaendayo mjini,ikiwa kama hatua ya kwanza ya safari ya kuelekea Nageria Dakika tano nyingi gari ikawa imewadia maeneo hayo,mzee Maboso akamuaga Zabroni lakini kabla hajapanda gari, Zabroni alimpatia mfuko mdogo mweusi wenye fedha ambazo mzee Maboso hakuweza kutambua ni kiasi gani. Maboso akapanga gari na neno la mwisho alimwambia Zabroni "Mzee Fungafunga ndio muuwaji wa wazazi wako,nakutakia kazi njema kijana wangu ",kwisha kusema hivyo gari iliondoka pole pole mpaka kasi ilipoongezeka. Huku nyuma kijana Zabroni akionekana kupigwa na butwaa akajiuliza "Yani inamaana kwamba baba yangu mkwe mtarajiwa ndio kafanya kitendo hiki Mzee Maboso hajawahi kunidanganya, acha nitembeze moto sasa mpaka kijiji kiwe jangwa. Tina utanisamehe maana hili ni pigo lisilo saharika katika maisha yangu" kwisha kuwaza hayo Zabroni akidondosha machozi ya hasira.
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la jf
CONTACT:0765168293

SEHEMU YA TANO-05

Zabroni alirudi nyumbani baada kutoka kumsindikiza mzee Maboso,akiwa njiani aliwaza kipi afanye sasa baada kumtambua mbaya wake. Je, aendelea kuchoma nyumba ama adili na mbaya wake? Akili ya fasta ikamjia kwamba bora aendelea kuchoma nyumba ikiamini kuwa maumivu aliyonayo moyoni mwake huwenda yakatulia kama sio kupotea kabisa.

Yote hayo kijana Zabroni alikuwa akiyawaza huku akirejea nyumbani mikono nyuma kichwa chini,alipo fika nyumbani alikuta karatasi ndogo kwenye meza iliyokuwepo sebuleni. Zabroni alionekana kustuka huku moyo wake ukihitaji kufahamu kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo,hatimaye aliichukuwa na kuanza kuisoma "Kijana wangu Zabroni, mjukuu wangu mwanangu pia. Nimekupa dawa hii ili uweze kulipa kisasi juu ya kile ulicho fanyiwa,hakuna ubishi mzee Fungafunga ndio muhusika mkuu wa vifo vya wazazi wako. Alifanya kitendo kile baada kuona baba yako anamzungusha kumlipa deni lake alilokuwa akimdai. Zabroni Zabroni lipa kisasi kijana unyama huo kamwe huwezi kuupuzia abdani,mwanaume haogopi. Yote kwa yote nikutakie maisha marefu kijana wangu,mimi narudi nyumbani ila najua ipo siku tutakuja aonana tena", Zabroni aliyasoma hayo kwa umakini na uchungu mkubwa, aliyafuta machozi, punde akaendelea kusoma "Kwisha kusema haya napenda kukwambia kuwa dawa hiyo unaweza kujigeuza kiumbe chochote chini ya jua,sharti moja tu ambalo inakubidi utekeleze, usithubutu kufanya mapenzi"

Zabroni alishusha pumzi ndefu,mwili wake ukasisimka hasira zisizo na mfano zikatawala ndani ya moyo wake akatamani kumfuata mzee Fungafunga muda huo huo lakini akajitahidi kuzizuia hasira zake ambapo aliamuwa kulala mpaka jioni saa kumi na moja hata hivyo aliamka baada kusikia Tina akigonga hodi.

Siku hiyo Tina alikuja na chakula kwa niaba ya mpenzi wake. Zabroni alionyesha kufurahia kitendo kile cha Tina ila moyo wake ulikuwa na kiza kinene,alipiga moyo konde akamkaribisha Tina ndani wakapiga zogo mbali mbali huku akiendelea kula chakula alicholetewa na mpenzi wake.

"Kulikoni mpenzi,mbona babu simuoni?.", aliuliza Tina huku akionekana kumfuta futa vumbi uzushi kijana Zabroni kunako shati yake.

"Babu kasafari,karudi kwao"

"Kwao? Kivipi yani"

"Ndio, hakuwa mtanzania kwahiyo jana alikuja ndugu yake kumchukuwa amerudi nchini kwao", alijibu Zabroni.

"Anha kwahiyo karudi Nigeria ? Jamani babu alikuwa mkarimu yule! "

"Ndio hivyo" alihitimisha Zabroni wakati huo sasa ameshamaliza kula chakula alicholetewa na mpenzi wake,baada kumaliza Tina alihitaji kutulia faragha na Zabroni siku hiyo na ndio maana alimjia saa ya jioni. kwa sauti ya upole na yamahaba alimwambia Zabroni asimame , naye akasimama bila kupoteza muda Tina alimshika mkono moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa dhumuni ya kufanya yao.

Walipofika chumbani Tina akamsukuma Zabroni kwenye kitanda cha telemka nikaze,Zabroni alianguka chali, muda huo huo Tina akampanda na kuanza kumpapasa kifuani huku pole pole akitaka kupitisha ndimi yake kwenye kinywa cha Zabro.

Zabroni naye baada kufanyiwa hicho kitendo,mwili wake ulianza kupata hisia mawazo yake yote yakazamilia kuvunja sharti. Lakini kabla kitendo hicho hakijatokea akakumbuka maneno ya ile barua,haraka sana akang'atuka akamsukuma Tina kisha akatoka ndani. Tina alishangazwa na kitendo hicho alichokifanya Zabroni.

"Kwanini lakini", wakati anajiuliza swali hilo akazipiga hatua kumfuata Zabroni nje. Zabroni muda ulionekana akiwaza na kuwaza jambo akilini mwake. Punde tu Tina akamfikia, kwa sauti ya upole akasema "Zabroni una nini mpenzi wangu? "

"Hakuna tatizo Tina, ila siku ya leo siko poa kabisa kufanya kitendo hicho"

"Unatatizo gani?..", aliongeza kuhoji Tina huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kinacho msibu mpenzi wake. Lakini bado Zabroni hakuwa tayari kumwambia Tina ukweli alionao moyoni mwake. Ni jambo ambalo lilimpelekea Tina kukasirika, akamuwa kurudi nyumbani ingawaje moyo wake bado ulikuwa na mashaka juu ya kitendo kile alichokifanya Zabroni kwani haikuwa kawaida yake.

Baada Tina kuondoka, Zabroni alirudi ndani moja kwa moja akazama mpaka chumbani kwake. Alisimama wima huku akitazama ile karatasi iliyosoma muda mchache ulio pita, kwa mara nyingine tena akaishusha pumzi ndefu kisha akajiuliza "Hivi ni kweli naweza kujigeuza kuwa kiumbe chochote?.."

"Hebu ngoja nijaribu, nijigeuze kuwa mzee nione kama kweli itawezekana", aliongea baada kujiuliza, kwisha kuongea maneno hayo akanunia na punde si punde akaonekana katika hali ya uzee. Alistaajabu sana, akanyoosha mikono yake kuitazama ngozi ya mwili wake, bado hakuyaamini macho yake, upesi akatoka ndani akaelekea nje kwenye mwanga. Napo bado alishuhudia kitendo kile kile, "Ahahahaha hahahahah", aliangua kicheko ndani ya moyo wake kisha akajisemea "Kweli huu ni moto wa Nigeria. Sasa kwa hali hii nipo salama kila idara. Hawa watu wamekwishaaaaaaa".

Lakini wakati yupo kwenye hali hiyo ya furaha, upande wa pili kijijini anaingia mzee mmoja wa makamo. Mzee huyo alionekana kubeba begi kukuu, pasipo na hofu alijikongoja huku akionekana ni mgeni kijijini hapo. Hakuwa peke yake mzee huyo, kando alikuwa sambamba na Mwenyekiti wa kijiji. Taharuki baadhi ya wanakijiji inazuka, wale waliomfahamu mzee huyo walionyesha nyuso za furaha, na wale ambao hawakumfahamu waliishia kuzama kwenye taharuki.

"Huyu mzee Baluguza amefuata nini huku?..", moja ya vijana waliopata wasaa wa kumuona mgeni huyo aliuliza.

"Mmmh kiukweli haujui lakini nahisi amekuja kumsaka huyu kirusi wa matukio haya", alijibu kijana wa pili, mtu wa tatu akaongeza kusema "Ya ngoswe tumuachie ngoswe na kwa jinsi ninavyo mfahamu huyu mzee ukweli lazima atajulikana tu huyu mtu aliyeanziasha zahma la kuchoma nyumba hovyo hovyo", yote hayo yalikuwa ni mazungumzo kilingini.

Upande wa pili napo zogo baina ya mwenyekiti na mgeni wake liliendelea. Mwenyekiti alikuwa akimpa habari namna kijiji kinavyo karibia kuwa jangwa na hata mfanyaji wa matukio hayo asijulikane. Mzee Baluguza alihuzunika sana hasa familia ile ya watu saba iliyokufa kwa pamoja, kwa kinywa chake akamthibitishia Mwenyekiti kuwa mtu huyo atajulikana, na atathubutu kumpoteza sehemu isiyojulikana. Mwenyekiti alifurahi sana kusikia maneno hayo, wakati huo huo mbele yao alionekana kijana Zabroni. Hapo mzee Baluguza akasita kidogo baada kumuona, alistuka wakati huo mwili wake ukimsisimka. Mwishowe alitikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, akaishusha pumzi ndefu kisha ndani ya moyo wake akajisemea "Naam! Kazi imekwisha"

JE, mzee Baluguza atamuweza Zabroni? ikumbukwe tayari Zabroni anauwezo wa ajabu. Tukutane sehemu ijayo
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA SITA-06

Kwisha kujisemea maneno hayo aliachia tabasamu bashasha huku akimsindikiza kwa macho Zabroni kitendo ambacho kilipelekea mwenyekiti kuingiwa na hofu akajiuliza maswali mengi ambayo aliyakosa majibu yake,ilihali upande wa pili Zabroni o naye aligeuka kumtazama mzee Baluguza ambaye kwa macho yake ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona. Alistuka baada macho yake kugongana na macho ya mzee Baluguza ila hakujali zaidi aliendelea na safari yake kama alivyofanya mzee Baluguza.
"Huyu ni nani?..", ndani ya kichwa chake Zabroni alijiuliza. Upande wa pili mwenyekiti alimkalibisha nyumbani mzee Baluguza kwa furaha huku akimpa tumaini kwamba ajisikie yupo nyumbanin,Baluguza akakaribia kwa bashasha ya hali ya juu. Baada ya maongezi mawili matatu,mwenyekiti akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mzee Ngurumo ambaye ndio balozi wa nyumba kumi. Alimkuta. Akamwambia nia na dhumuni ya ujio huo,mzee Ngurumo alimuelewa vema tena akampongeza kwa hatua aliyochukuwa ya kumleta mzee Baluguza mganga mashuhuli aliyefamika kwa huduma yake maridadi isiyokuwa na utapeli.
"Ama kweli wananchi waliokuchagua hakika hawakukosea,kiukwe hili ni tatizo tena sugu. Tusipo chukuwa hatua mapema tutajikuta tukipoteza mpaka familia zetu", aliongea mzee Ngurumo huku akifunga mlango wa nyumba yake. Mwenyekiti alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Ni kweli ,si unajua tusipo ziba ufa tutajenga ukuta? .."
"Kabisa ndugu mwenyekiti"
"Basi hima twende tukazungumze naye tujue hili tatizo atalikomesha vipi" aliongeza kusema mwenyekiti wakati huo tayari wameshatoka nyumbani hapo kwa mzee Ngurumo na sasa walionekana kuanza safari kurudi nyumbani kwa mwenyekiti. Ila kabla hawajafika,Ngurumo akatoa wazo akasema "Unaonaje tukamuone na mzee Fungafunga? Maana hili suala kama linamuhusu na yeye?.."
"Sawa hakuna shida twende ingawa sidhani kama atakuwa karudi kutoka shamba,nasikia ngedere wanasumbua sana shambani. Wami unamsumbua sana"alijibu mwenyekiti.
"Loh. Nikweli lakini tukajaribu"
"Sawa twende"
Mwenyekiti na mzee Ngurumo walielekea kwa mzee Fungafunga, bahati nzuri walimkuta akiwa tayari ametoka shamba alionekana kuchoka sana.
"Hodi! Hodi! Bwana Fungafunga " Ngurumo alisema.
"Anhaa KARIBU bwana,karibu sana. Mama Tina leta vigoda haraka", alijibu mzee Fungafunga kwa tabasamu bashasha ,na punde si punde Mama Tina alileta vigoda. Mzee Ngurumo na mwenyekiti wakapata kuketi kisha soga zikaendelea.
"Naam! mzee mwenzangu,pole sana nasikia ngedere wanamsumbua sana huko", aliongea mzee Ngurumo. Wakati mzee Fungafunga akajitayarisha kumjibu Ngurumo. Upande wa pili kijana Zabroni alionekana kasimama kando kando ya nyumba,alitazama kulia na kushoto hakuona mtu. Giza tayari lilikuwa limeanza kutanda kwa maana hiyo kijiji kilianza kupoa zaidi zilisikika kelele za vijana wa kijiji kijiweni wakibishana mambo mbali mbali,gumzo ilikuwa ni ujio wa mzee Baluguza kijijini hapo. Wapo waliombenza kwamba mzee huyo si chochote si lolote,lakini pia wapo walimnadi ya kwamba huyo mzee ni moto wa kuotea mbali. Hivyo hali hiyo ndiyo iliyoweza kuleta ubishi katika kijiji hicho eneo la kijiweni. Kelele zilipasa kila kona hakuna aliyegusia masuala ya siasa abadani bali wote waliongelea ujio wa Baluguza. Lakini pindi mada hiyo ikiwa imepamba moto, mara ghafla ulionekana mwanga mkali angani ulio ambatana na moshi. Kwa maana hiyo tayari nyumba ya mtu ilikuwa inateketea kwa moto mapema tu saa moja usiku. Taharuki ilizuka, soga la kumnadi mzee Baluguza upesi zilikatishwa ,hima wakakimbia kuelekea kule kunako fuka moshi na moto. Pindi vijana hao walipokuwa wakielekea huko,upande wa pili nyumbani kwa mwenyekiti walionekana mzee Ngurumo,mzee Fungafunga pamoja na mwenyekiti wa kijiji bila kusahau mzee Baluguza. Nao walikuwa wakijadili namna gani ya malipo yatakavyo fanyika pindi mzee Baluguza atakapo kamilisha kazi iliyo mleta, ila makubaliano hayo yaliingia dosari baada mama Tina kupasa sauti ya mayowe alipoona moshi mkali ulioambatana na kipupwe cha moto. "Unaona sasa?..mapema tu leo" alisema mzee Ngurumo huku akinyoosha kidole kule ilipokuwa nyumba inateketea.
"Nadhani hapo mzee mwenzangu utakuwa umeamini kuwa hata zile nyumba za awali sio mimi niliyezichoma moto", alidakia mzee Fungafunga akijitetea mbele ya mwenyekiti ambaye hapo awali baada kuchomwa nyumba tano,Mwenyekiti alimuhisi yeye kwamba ndiyo muhusika kwani aliwahi kung'atwa sikio na mzee huyo kuwa yeye ndiyo aliyechoma nyumba ya mzee Ndalo baba yake Zabroni kwahiyo Mwenyekiti akawa hana imani na mzee Fungafunga lakini siku hiyo alimuamini baada kuona nyumba ikiteketea kwa moto. Wazee hao waliazipiga hatua kuelekea kwenye ajali hiyo,walipo fika waliwakuta vijana wakishughulika kuuzima moto lakini hawakuweza kufanikiwa. Nyumba iliungua yote huku ndani akiwemo mzee Kadili mchongaji nguli wa mipini kijijini hapo,mzee ambaye aliishi yeye peke yake, hakuwa na familia

Kwa mara nyingine tena yanatokea majonzi kijiji hapo,kila mwanakijiji roho juu ilihali huzuni nayo ikitawala mioyoni mwao. Walihofia usalama katika kijiji chao, lakini wakati wanakijiji hao wakiwa katika hali hiyo,mara ghafla mzee Baluguza akamuita kando mwenyekiti kisha akasema "Hivi yule kijana tuliyepishana mude ule yupo hapa? ", Mwenyekiti hakujibu upesi, alikaa kimya huku akijaribu kumkumbuka. Akamkumbuka na ndipo alipo tazama upande ule waliosimama vijana wengi akamuita mmoja wao, naye alitii wito wa mwenyekiti "Zabroni yupo hapa? ..", kijana huyo aliyetii wito wa mwenyekiti aliulizwa.
"Hapana ", alijibu kijana huyo,jibu hilo alilisikia na Mzee Baluguza.Akalizika nalo akatikisa kichwa halafu akamuuliza tena Mwenyekiti "Unapajua anapoishi?..", lakini kabla Mwenyekiti hajamjibu Baluguza, ghafla ilionekana mwanga mkali angani na moshi mwingi. Kiashiria hicho kilimanisha kuwa tayari kuna nyumba nyingine inateketea,Mwenyekiti aligeuka akatazama kule akaona mwanga ule unatokea mahali ilipo nyumba yake. "Lahaulla nyumba yangu", alitaharuki mwenyekiti huku akiweka mikono kichwani alijua fika nyumba yake inateketea. Haraka sana vijana wa kijiji wakajigawa magundi mawili, kundi moja liliendelea kuuzima moto kwenye nyumba hiyo inayoteketea, na kundi lingine lilielekea kule inapoungua nyumba nyingine ambayo mwenyekiti aliamini kuwa ni nyumba yake. Mzee Baluguza aliposikia maneno ya mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti, haraka sana akapotea eneo hilo akaibukia nyumbani kwa Mwenyekiti. Alikuta nyumba ya mwenyekiti ipo salama, ila nyumba nyumba ya jirani yake ndiyo iliyoonekana ikiteketea. Mzee Baluguza akastaajabu kumuona mchomaji akiendelea kufyatua njiti. Mtu huyo hakuwa mwingine ni Zabroni ambaye baada kuchoma nyumba hiyo aliamua kujibadilisha umbile lake akachukuwa umbile la mzee Ngurumo. Hivyo alipokuwa katika umbile hilo la mzee aliendelea kufyatua njiti kuchochea moto wakati mzee Baluguza akimtazama mara mbili mbili mwishowe akakumbuka mtu huyo kamuacha kule alipotoka, aliingiwa na hofu akaona ni mchezo mchafu anachezewa. Aliguna kisha akajisemea "Nimekupata ila siku zako zinahesabika nitakukomsha"., maneno hayo mzee Baluguza alijisemea ndani ya moyo wake huku Zabroni naye akiwa na umbile la mzee Ngurumo alionekana kuishia zake kwenye giza totoro akiacha nyumba ikiteketea vile vile akimuacha mzee Baluguza akiishia kumsindikiza kwa macho tu wakati huo akifahamu fika kijana huyo anauwezo wa ajabu sana. Na pindi Zabroni alipokuwa njiani akitembea kwa kujiamini katika umbile la mzee Ngurumo, mbele yake walionekana wazee wa wawili wakitembea kuelekea kule anakotokea yeye wazee hao ni mwenyekiti wa kijiji sambamba na mzee Ngurumo mwenyewe!

ITAKUAJE HAPO? tukutane sehemu ijayo! Je, Baluguza atauweza moto wa Zabroni?
 
Back
Top Bottom