Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi :Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA SIBA-07

Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.
Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.
Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. "Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"
"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.
"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. "Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.

ITAKUAJE HAPO tukutane sehemu ijayo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA NANE-08

Moto ule uliokuwa unawaka kwenye nyumba ya mzee Ngurumo uliwastua sana wanakijiji,pia hata mzee Baluguza naye alionyesha kustuka ingawa sio rahisi kutumbua endapo kama ukimtazama usoni kwa pupa. Ngurumo alitaharuki baada kuona nyumba inaungua, alipasa mayowe huku akijing'atua eneo alilokuwa amekaa akitaka kwenda walau kuokoa baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani,lakini kabla hajaondoka,Mwenyekiti alimshika mkono akamvuta karibu yake kisha akasema "Hata ukiondoka hutaweza kuokoa kitu chochote mzee mwenzangu, kwahiyo nakusihi hebu punguza jazba ili leo tumtambue kirusi wa kijiji hiki" alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Ngurumo ambaye muda huo alikuwa akilia kilio cha mtu mzima. Mke wake alisimama akilia machozi mithili ya mke aliyefiwa na mumewe,mwanamke huyo akamkumbatia mumewe huku akiangua kilio. Kitendo hicho kilitia simanzi mkutanoni hapo,baadhi ya wakina mama na wakina baba wenye hekima walijaribu kuwatuliza wazee hao,nao kila mmoja alitulia kwa muda wake ingawa mioyoni mwao wakiwa wamefura hasira zisizo na mfano.
Utulivu ulipo tawala,mzee Baluguza akaanza kufanya mambo yake akiwa na nia ya kumuweka hadharani kirusi huyo wa kijiji,kwenye mti mnene kiasi alibandika kitambaa cheupe huku akiimba nyimbo zake za asiri. Alipo maliza aliwaambia wanakijiji wawe makini kukitazama hicho kitambaa umakini na utulivu ukaongezeka kwa wanakijiji hao ilihali kijana Zabroni naye akiwa hajui chochote ila aliamini kuwa huyo mzee hawezi kitu chochote juu yake. Na wakati akijiaminisha hayo ndani ya nafsi yake,Ghafla kwenye kile kitambaa cheupe alionekana Zabroni akiwa anafanya kile kitendo kwenye Nyumba ya mzee Ngurumo. Wanakijiji walitaharuki kila mmoja alionekana kushungaa, ilihari Zabroni naye alijikuta akijishangaa na kujiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya kile kilicho kuwa kikiendelea kwenye kitambaa kile cheupe. Aliingiwa na hofu pasipo kuchelewa alisimama akaanza kunuia maneno yake ili apate kupotea maeneo hayo lakini kabla hajatamka chochote,kundi la wanakijij likaanza kumvagaa na kisha kumpiga. Zabroni alichezea kipigo cha mbwa mwizi ila baadaye kidogo alifanikiwa kupotea katikati ya umati wa watu,ajabu aliwaachia nguo zake tu. Kitendo hicho kiliwastua wanakijiji,hapo sasa kila mmoja akajawa na hofu huku maswali yaliyokosa majibu yakitawala akili mwao. Ni kitendo ambacho kilimshangaza sana mzee Baluguza, alijiuliza uwezo gani alio nao kijana huyo, Na baada kumaliza shughuli hiyo aliona hakuna haja ya kuendelea kukaa kijijini hapo kwani kwa maono yake aliona kamwe hatoweza kufua DAFU kumkabili Zabroni, ili kulinda uhai wake aliamua kufunga safari usiku wa manane kurudi kijijini kwao. "Nayapenda maisha yangu", alijisemea mzee Baluguza ndani ya nafsi yake huku akiandaa vilago vyake. Hatimaye kila kitu kilikaa sawa, na sasa alianza safari wakati anatoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alipokuwa amefikia,punde si punde Zabroni alitua maeneo hayo. Akiwa na lengo moja tu ambalo ni kutekeleza ahadi yake aliyojiwekea. Pasipo kupoteza muda Zabroni alichukuwa kamba yake akaitambalika kisha akachoma moto. Moto ambao ulianza kutembea pole pole kuelekea kwenye nyumba wakati huo yeye tayari ameshapotea eneo hilo,nia kuu ya kijana Zabroni kuwahi kuchoma moto nyumba ya Mwenyekiti ni kumuuwa mzee Baluguza ili apate kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi bila kubuguziwa na mtu yoyote, aliona kama mzee huyo anataka kuharibu mkakati wake.
"Kufa tu hakuna namna mwanaharamu mkubwa wewe", aliongea Zabroni na hata asijue kuwa tayari amechelewa kwani mzee Baluguza alishafungasha vilango vyake na kuondoka zake. Ule moto uliendelea kutembea kwenye kamba ile kwa kasi ya ajabu ila kabla haujanasa kwenye nyasi za nyumba,zilisikika kelele za mbwa wakibweka kwa nguvu kiasi kwamba mkewe Mwenyekikiti ilimfanya aamke na kisha kumwamsha mumewe ili atoke nje akatazame ni nini kinacho endelea huko. Kumbe wakati Zabroni anaondoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alijibadilisha akawa katika umbo la kutisha liliacha harufu mbaya ambayo iliwafanya mbwa kubweka kuashiria nje kuna kitu cha hatari, Mwenyekiti akamsikiliza mkewe haraka sana akatoka nje ambapo alizunguka nyuma ya nyumba akakuta moto tayari umeshika nyumba. "MOto moto motoooo" alilalama Mwenyekiti usiku ule wa manane, mkewe akiwa ndani akastuka alipotaka kukimbia akajikuta anazima kibatali kilichokuwa kinawaka. Hapo sasa aliukosa mlango wa kutokea kwamaana ndani palikuwa na giza nene,upande wa pili napo Mwenyekiti alikuwa akihaha japo kuuzima kwa mchanga lakini alipoona moto unazidi kukolea alirudi hima upande ulipo mlango ili amuamshe mzee Baluguza pia amtoe ndani mke wake,lakini kabla hajafanya jambo lolote,moto ulifunika nyumba nzima kwani muda ule kulikuwa na upepo mkali uliofanya moto kutambaa kwa kasi zaidi. Mwenyekiti akajikuta anashindwa afanye nini, alibaki amesimama huku mikono akiwa ameweka kichwani pia akilia kilio cha mtu mzima akilitaja jina la mkewe aliyepoteza maisha kwa ajari hiyo ya moto. Baada ya lisaalimoja mwanakijiji mmoja mmoja alijitokeza kwa Mwenyekiti kuja kushuhudia kitu gani kimetokea,walimkuta Mwenyekiti wao akiwa mnyonge asijue cha kuwaambia. Hakika walichoka sana kila moja aliona hakuna haja ya kuendelea kuishi katika hicho kijiji cha mauaji ya kinyama,na hivyo baadhi za familia zilianza kufanya mikakati ya kukikimbia kijiji hicho. Alfajiri mapema mbiyu ililia kwa mara nyingine,mbiyu hiyo ilitangaza maafa yalitokea kwa Mwenyekiti huku mtoa taarifa aliwajuza wanakijiji kuwa Mwenyekiti kafiwa na mke wake usiku wa jana,alienda mbali zaidi na kusema si mke wake bali na mzee Baluguza. Hapo wanakijiji walizidi kuchanganyikiwa kwa taarifa ile "Mmh sio bure huyu mtu atakuwa anakisasi na kijiji hiki ", alisema mzee mmoja mlemavu akiwa ndani ya nyumba yake ya matete asubuhi hiyo baada kusikia hiyo taarifa. Na wakati mpiga mbiyu anaendelea kutangaza taarifa hapo kijiji,mara ghafla akafika eneo lile walilo fanyia mkutano siku iliyopita. Punde alistua mpiga mbiyu huyo baada kuona damu chini ya mti huo ambao waliutumia kumwona mtukutu Zabroni akichoma nyumba ya mzee Ngurumo. Mpiga mbiyu akajiuliza "Damu hii kakamatwa nguruwe pori ama?..", akiwa na wasi wasi alijiuliza hilo swali,tonya la damu likamdondokea kutoka juu ya mti huo. Aliinua uso wake kutazama juu akauona mwili wa mzee Baluguza ukiwa unaning'inia huku damu zikivujia kwenye shingo. Alichinjwa kikatiri mtaalamu Baluguza. Mpiga mbiyu alistuka,mwili ulimsisimka huku akitetemeka kwa hofu, muda huo huo ilisikika sauti ikijirudia mara mbili mbili, ilikuwa sauti ya Zabroni Sauti ya ilisema "Zabroni! Zabroni " sauti hiyo ilimaliza kwa kicheko kizito.

USIKOSE MUENDELEZO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA TISA-09

Mpiga mbiyu alipo sikia sauti hiyo alitimua mbio huku akipiga kelele,watu waliokuwa wanaishi jirani na eneo hilo walikurupuka na kutoka nje ili kuja kushuhudia nini hasa kilicho mkuta mpiga mbiyu huyo. Walipigwa na butwaa baada kuuona mwili ukining'inia juu kwenye mti huku damu zikivujia kwenye shingo, walipo mtazama vizuri waligundua kuwa mtu yule ni mzee Baluguza. Walichoka sana,pumzi walishusha,hofu nayo ikiendelea kutanda mioyoni mwao ilihali upande wa pili mpiga mbiyu wa kijiji alikuwa akiendelea kukimbia kuelekea kwa Mwenyekiti,alipo fika akasema "Mwenyekiti,kama kijiji kuchafuka basi hiki kijiji tayari kimechafuka haswaa. Unahabari kama mzee Baluguza kanyongwa kwenye mti ule tunapo fanyia mkutano?.." alisema mpiga mbiyu huku akihema mithiri ya faru aliyekuwa akiukimbia mtutu wa bunduki ili usimzuru. Mwenyekiti pamoja na watu wengine ambao tayari walikuwa wamefika nyumbani hapo kwake kila mmoja alipigwa na butwaa kiaina yake,bila kupoteza muda walinyanyuka wakaenda kushuhudia.
Upande mwingine,asubuhi hiyo na mapema mama Tina ambaye ndio mke wa mzee Fungafunga alimuita binti yake ili aseme naye jambo kabla hajaelekea msibani. "Tina mwanangu"
"Abee mama" Tina aliitikia huku akijikusanya vizuri kutoka kitandani ili aweze kumsikiliza mama yake. Mama Tina aliongeza kusema "Umeamkaje?.."
"Nimeamka salama,shikamoo"
"Malakhabaaa,Tina leo mimi nataka kusema na wewe. Nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa unamchumba hapa kijijini, na mchumba mwenyewe ni yule kijana mtukutuku. Si ndio? Hivi Tina,uzuri wako huo unaweza kuolewa na yule kijana ambaye hana hata chembe ya huruma? Tazama mauaji anayo yafanya kwa kuchoma nyumba za watu,wakubwa kwa wadogo wanakufa. Kiukweli mimi kama mama yako sitaki yule kijana awe mkwe wangu ", aliongea mama Tina wakati huo Tina alikuwa amejiinamia. Tina alikaa kimya ila mwishowe akajibu "Sawa mama nimekuelewa lakini tatizo sio mimi bali ni moyo,moyo wangu umempenda Zabroni mama nitafanyaje mimi", jibu la Tina, halikumfurahisha mama yake, ghafla akakunja uso na kisha akamuuliza kwa sauti kali "Kati ya mimi na Zabloni ni nani bora?..", kabla Tina hajamjibu mama yake,Ghafla mlango uligongwa kisha ikasikika sauti ya mzee Fungafunga ikisema "Mama Tina na mwanao hebu njooni hapa mara moja" Tina akavaa nguo haraka haraka akatii wito. "Jamani mnahabari lakini? Mzee Baluguza kauwawa", "We unasema kweli?..", mama Tina pamoja na binti walistuka kusikia taarifa hiyo,punde si punde akamtazama mwanaye kisha akamwambia "Unaona? Haya sasa nambie sisi wazazi wako tunaweza kuwa na mkwe muuwaji kama yule? Loh! Yule sio ameingiliwa na shetani, Zabroni ni shetani"
"Tina..Tina...Tina. yani nikikufuma upo na yule mtu? Hiyo pua kama kinu nitaing'oa pumbafu toka mbele yangu mwanahidhaya mkubwa wewe", alidakia mzee mzee Fungafunga, aliongea kwa sauti kali juu ya suala la binti yake kuwa na mahusiano na kijana Zabroni. Haraka sana Tina akarudi chumbani kwake huku akilia,aliona wazazi wake wanamkosesha amani ya moyo maana kupenda sio mchezo.
Wakati hayo yanajili nyumbani kwa mzee Fungafunga, kwingineko vijana wa kijiji wenye hasira kali walishika siraha mbali mbali kisha wakaelekea nyumbani anapoishi Zabroni,kwa dhumuni la kumuuwa kabisa. Ukweli vijana hao walijitoa muhanga kwani ni rahisi sana mwanamke kuruka tikitaka kuliko kumuuwa mtukutu Zabroni, ila walipofika hawakumkuta zaidi walichoma nyumba huku wakijizatiti kwamba lazima na wao walipe kisasi kwani wamechoka kuwa wanyonge. Jioni Zabroni aliporudi kutoka shamba alistaajabu kuona nyumba yake ikiwa imeteketezwa na moto. Hapo sasa hasira zikampanda zaidi ya! Ilihari baadhi ya wanakijiji walipo gundua kwamba Zabroni kachomewa nyumba haraka sana walihama kijiji kwani waliamini kijana huyo hatomuacha mtu salama abadani. Na wale wasio kuwa na pa kwenda waliomba Mungu tu ili kijana huyo asifanye kitu chochote kibaya,ukweli kijiweni sasa pakawa hapakaliki. Watu waliogopa kulala majumbani mwao,walilala nje kama mateja wa Kariakoo. Yote hayo kuogopa kufia ndani na familia zao,ukweli Zabroni alitishia maisha ya watu yote hayo akifanya ikiwa kama kulipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wake waliokufa kwa pamoja wakiuliwa na mzee Fungafunga aliyechoma nyumba huku msibani napo wakijitokeza wanakijiji wachache,wengi hawakujitokeza kwa madai kwamba wazazi wake hawana utu wala ushirikiano na wanakijiji wenzake. Uzushi huo ulitokea baada mmoja wa mwanakijiji kunyimwa kibarua cha kulima na mzee Ndalo. Baba yake Zabroni. Kwani marehemu mzee Ndalo alikuwa na mashamba mengi ila ilikuwa nadra kutoa vibarua kwa walima kwa mikono,aliingiza Trekta lakini baada mkewe kuugua ugonjwa wa kupooza alijikuta akifirisika kila leo,akihangaika huku na kule kutafuta tiba. Mwishowe aliishiwa kabisa,na ndipo ilimbidi akope fedha ambayo mwishowe ilimghalimu.
"Mmmh", siku moja aliguna Zabroni, ilikuwa yapata usiku wa saa mbili muda huo alikuwa katika matembezi yake huku akitafuta nyumba ya kuchoma usiku huo,ghafla alisikia bwana mmoja akijinasibu kwa mkewe kwamba yeye ndio shujaa aliyefyatua njiti ya kibiriti kuunguza nyumba ya Zabroni.
"Huwezi amini mke wangu, karibia wote waliogopa ila mimi nikasema hebu nipeni kibiriti hapa. Wakanikabidhi, nami upesi sikutaka kupepesa macho. Nikakiwasha", aliongeza kujisemea maneno hayo tena kwa mbwembwe zote mbele ya mkewe.
"Mmh lakini wewe jiangalie isije kuwa balaa bwana", alijibu mke wa huyo jamaa. Jamaa akajitutumua halafu akaongeza kusema "Hakuna balaa hapa mke wangu,ila naomba kesho uende kwa shangazi nilisha andaa kila kitu,tutaishi huko utajifungua salama kabisa bila hofu yoyote"
"Anhaa sawa! Na namuomba Mungu nizae mtoto wa kike sitaki wa kiume asije akawa kama hili jitu linalo uwa watu hovyo hivyo", alisema mke wa jamaa huy. Jamaa alicheka kidogo kisha akajibu "Haya bwana,kwahiyo kesho asubuhi mapema anza safari. Mimi nitakuja jioni kwa sababu kuna shamba nitaenda kuliuza ili tupate Fedha za kutumia siku mbili tatu hizi"
"Sawa mume wangu nimekuelewa", walipo kwisha kusema hayo mke na mume walirudi ndani kulala,wasijue kuwa ni kosa kubwa walilofanya hawakujua kwamba Zabroni yote waliyoongea alikuwa akiyasikia. Na punde si punde alikatiza eneo hilo huku Moyoni akijisemea "Naam! ukila tambua ipo siku zote na wewe utaliwa.. Ngoja nitakukomesha", kwisha kusema hayo ajabu macho yake yaliwaka kama macho ya simba kisha akapotea ikasalia sauti ya mtoto mchanga akilia ambayo nayo haikudumu ikatoweka. Usiku huo hakuchoma nyumba hata moja,waliolala ndani walifurahi sana kusikia jogoo anawika kwani waliamini tayari pamekucha salama. Alfajiri hiyo mapema mke wa yule jamaa aliyekuwa anajinadi kwa mkewe juu ya kuchoma nyumba ya Zabroni, alianza safari pole pole kwenda kijiji jirani kama walivyopanga yeye na mumewe usiku wa jana ikiwa njia ya kuyakimbia maafa yanayo endelea. Akiwa njiani kwenye giza totoro lililo jichanganya na ukungu kwa mbaali, mwanamke huyo mwenye ujauzito alizipiga hatua pole pole huku akihofia kukutana njiani na mtukutu Zabroni. Katika ya kijiji hicho ambacho Zabroni anafanya mabalaa na kijiji jirani palikuwa na msitu mkubwa ila sio sana,huo msitu kwa mwendo wa miguu inakubidi utatembea saa moja na dakika kumi na tano kuumaliza msitu huo wenye miti mirefu na mifupi, uoto wa asiri nao ukiunakshi vema. Mwanamke huyo alijawa na hofu,alikazana huku kimoyomoyo akimuomba Mungu afike salama. Lakini wakati anatembea,ghafla mbele yake alimuona mtu ni baada kuondoka ungungu ule uliokuwa umetanda,mwanamke huyo alifurahi akakazana zaidi ili kumfikia yule mtu aliyeonekana amebeba kifurushi kidogo mgongoni. Mtu huyo alionekana mzee wa makamo, ndani ya nafsi yake akaamini kuwa ndio wale wale wanao kikimbia kijiji. Upesi akaongeza mwendo ili wawe sambamba katika safari hiyo isiyokuwa na matumaini. Alipo mfikia alimsalimia kisha akasema "Afadhali hapa naweza kuwa na amani"
"Amani gani tena mwanangu?.. ", alihoji mzee huyo huku wakiendelea kutembea.
"Mmh hujui kama kuna muuwaji anakitikisa kijiji?.." Mzee huyo alikaa kimya kidogo kisha akaongeza kusema "Nasikia hivyo ila sijawahi kumuona katika uso macho yangu, we vipi ukimuona utajua kweli? .."
"Ndio kwanini nisimjue? Yani ni kijana mdogo sana huwezi amini lakini mambo yake ni makubwa mno" alijibu.
"Doh! Ila nasikia analipa kisasi, sasa sijui ni kweli? Na hata hivyo jana nimepata habari kwamba amechomewa nyumba.."
"Ni kweli"
"Mmh waliochoma kweli ningewajua basi ningewapa mzizi wa kumtia hatiani yule kijana maana nasikia anatumia dawa na ndio maana hakamati", alisema mzee huyo,yule mwanamke aliposikia maneno hayo alihamaki kisha akasema "Kweli? Basi nadhani ningekuwa nipo na mume wangu ungempatia ili amkomeshe. Naye jana alishiriki,tena yeye ndio aliyefyatua njiti kuichoma nyumba yake. Lakini bahati mbaya nimemuacha kijijini kuna mambo anayeweka sawa" Mzee huyo aliposikia maneno hayo alisimama kisha akasema "Basi mimi ndio mhangwa. Naitwa Zabroni Zabroni ", sauti ilijirudia mara mbili mbili,Ghafla alibadilika akageuka Zabroni mwenyewe mtukutu kutoka kwenye hali ya uzee. Yule mwanamke alistuka akaanza kupiga mayowe akiomba masaada,lakini Zabroni hakujali kelele hizo. Macho yake yakabadirika, yakawa kama macho ya nyoka upesi alichomoa kisu kisha akampiga ngumi nzito mwanamke yule, naye hakuteteleka zaidi aliangua chini, akashuka naye akamtumbua tumbo mwanamke huyo mjamzito, akavitoa vijusi mapacha viwili ndani ya tumbo la huyo mwanamke kisha akavitumbua style ya mshikaki,akavining'iniza juu kwenye mti ambao kila mpita njia akipita lazima avione vijusi hivyo,ambavyo ndio kwanza vilikuwa vikikaribia kuwa katika hali ya kuitwa mtoto.. Zabroni baada kufanya kitendo hicho cha kutisha akapotea kwa kishindo kikubwa ambacho kilimpelekea nyasi mbichi kukauka!

Je, nani wa KUMFUNGA ATAMKAMATA MTUKUTU? USIKOSE SEHEMU IJAYO

Itaendelea jumanne uck

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi :Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA SIBA-07

Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.
Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.
Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. "Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"
"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.
"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. "Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.

ITAKUAJE HAPO tukutane sehemu ijayo!

Sent using Jamii Forums mobile app
hii hadithi mtunzi umeipangilia kiufundi haswa.
.Big up sana kaka
 
Back
Top Bottom