Mkuu kucha za vidole vya miguu ziling'ookaje? ulikuwa umevaa kandambili au? manake kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ni lazima ufanye preparation ya vitu vifuatavyo:
1.Viatu vigumu (Boots) lakini viwe vyepesi ili kukusaidia kutembea bila kuchoka.
2.Soksi pair 4 ndefu safi na nzito.
3.Mycotta powder.
4 Gloves safi zenye sufi ndani.
5.Jacket au pullover zito.
6.Boshori lile kofia la sweta linalofunika kichwa na kuacha sehemu ya macho tu.
7.Miwani nyeusi kupunguza mng'ao wa theluji.
7.Climbing stick
8.Kibuyu au chupa ya maji.
9.Back pack kwa ajili ya kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama glucose,biscuits,juice n.k.
Hayo ndio mahitajio ya msingi unayotakiwa kuconsider kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima.
Sent using
Jamii Forums mobile app